Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104755 articles
Browse latest View live

TAJIRI NUMBER MOJA TANZANIA ROSTAM AZIZ AZIDI KUWA TAJIRI

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) party stalwart Rostam Aziz has earned USD 240 million (about Tsh. 384,000,000,000/-) from selling part of his stake in Tanzania’s largest mobile phone company, Vodacom Tanzania.
Rostam Aziz has made the fortune by selling 17.2% of his 35% shares in Vodacom Tanzania, the business magazine Forbes has reported.

Rostam owns part of Vodacom through the company Cavalry Holdings, a Jersey island-registered private investment company wholly controlled by the Tanzanian politician.In an article carrying the headline “Tanzania’s Richest Man Concludes Sale Of Vodacom Stake”, Forbes has published the following report:Vodacom Group Ltd, the African subsidiary of British telecoms giant Vodafone announced on Tuesday that it has finally concluded its acquisition of an additional indirect 17.2% interest in Vodacom Tanzania previously owned by Tanzania’s richest man, Rostam Azizi.

In a press release statement, the company said it had fulfilled all requirements as mandated by the Tanzanian regulatory authorities and that the transaction was now unconditional.“As all the conditions precedent to the transaction have been fulfilled, the transaction is now unconditional and closing is expected to take place today, 29 April 2014,” the company said.

Last November, Vodacom announced it would spend up to R2.5 billion ($240 million) to acquire a 17.2% stake in Vodacom Tanzania from Cavalry Holdings, a Jersey island-registered private investment company wholly controlled by Rostam Azizi. Cavalry previously held a 35% in Vodacom Tanzania.

With this acquisition, Cavalry’s holding the company is now reduced to 17.8%, while Vodacom Group, a Johannesburg Stock Exchange-listed entity that previously owned a 65% stake in the company will now own 82.2%. Vodacom Tanzania, which has more than 10 million active subscribers, is the country’s largest mobile phone company, and Vodacom Group’s second most successful operation in Africa, after its South African unit that boasts more than 23 million subscribers.

Azizi, 49, is Tanzania’s first billionaire with a fortune estimated at $1 billion, derived from stakes in contract mining firm Caspian Mining, a Port in Dar es Salaam, extensive real estate in Tanzania and the Middle East and, of course, cash coming from the sale of his stake in Vodacom Tanzania.

HUSBAND MATERIAL SIKU HIZI NI WACHACHE SANA

$
0
0
Habari kamiliiiiiiiii na ya uhakika
kwa masikitiko makubwa sana naona ongezeko kubwa la wanaume ambao wanakosa sifa za kua wame bora ndani ya familia zao kwa sababu ya kutoyatambua majukum yao kama baba wa familia, wengi wa wanaume wana ndoto za kufanikiwa maisha kupitia kazi au mishahara ya wake zao na ikifikia hapa jua wewe haufai kuishi na mwanamke, jitahidini kujipanga , acheni uvivu, vumbua fursa za kiuchumi na uwe na mipango endelevu hapo utakua ni husband material.

MAN U YAPEWA KICHAPO KITAKATIFU CHINI YA RYAN GIGS...DAVID MOYES ANACHEKA TU I GUESS

$
0
0

Ni game ambayo pia ilikua inasubiriwa sana na mashabiki mbalimbali wakiwemo wa Manchester United kuona game ya pili toka Giggs aachiwe timu kwa muda.
Full Time ni Manchester United wamefungwa 1-0 na Sunderland goli lililoingia kwenye dakika ya 30

POLISI KENYA WAONGEA KUHUSU GARI LA MBOWE LILILOKAMATWA KENYA

$
0
0
Kwenye magazeti ya April 30 2014 Tanzania miongoni mwa stori kubwa ilikua ni hii ya kukamatwa kwa gari la kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni ambae pia ni mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe ambapo baadhi ya vichwa vya habari vilisema ni kutokana na kuhisiwa kutumika kwa ugaidi.

Msemaji wa Polisi nchini Kenya Gatiri Mboroki anaethibitisha kwamba ni kweli gari la Mbowe lilikamatwa tarehe 25 April 2014 ambapo gari hilo baada ya kuvuka mpaka kuingia Kenya likitokea Tanzania lilibadilishwa namba.
Anasema ‘kutokana na visa vya ugaidi nchini Kenya baada ya Wananchi kuona gari imebadilishwa namba na kupaki kwenye hoteli wakaripoti Polisi, Polisi walikwenda na kumkuta dereva peke yake aliewaambia kwamba kiongozi wa chama ambae ni Freeman mwenye gari amekwenda Nairobi kwa ndege, hiyo ilileta utata kidogo kwa kujiuliza amekwenda Nairobi kwa ndege iweje aache gari?’

TAKWIMU ZA NGOMA (UKIMWI) HIZI HAPA, MIKOA INAYO ONGOZA TANZANIA

$
0
0
Cha ajabu mkoa wa Tanga ambao watu wanadai wapo vizuri kweye swala zima la mapenzi maambukizi yapo chini! Do they play safely? Manyara pia! Pemba na Zanzibar ambako watu wanadai kuna mapinduzi ya mapenzi nako maambukizi yapo chini! How this is possible?

MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.

Alisema Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.

Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).

Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).

Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.

Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.

Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo.

Visababishi vya Ukimwi:

Miongoni mwa vipengele muhimu ni pamoja na vifuatavyo:


Uasherati
Matumizi madogo na yasiyo endelevu ya kondomu
Ngono za marika yanayotofautiana sana
Kuwa na wapenzi wengi.
Ukosefu wa elimu ya maambukizo ya UKIMWI
Kuwepo kwa maradhi mengi ya ngono kama vile tutuko, homa,
Jando kwa wanaume


Sababu za mahali husika, za kushamiri kwa janga nchini ni:


Umaskini na biashara ya ngono pamoja na ongezeko la wafanyabiashara wa ngono
Tabia mbaya za ngono za wanaume kutokana na kuruhusiwa kimila kuwa na nguvu
Kukosekana usawa wa kijamii, kiuchumi, kisiasa na kijinsia pamoja na unyanyaswaji wa wanawake na wasichana walio ndani na nje ya mahusiano.
Matumizi ya pombe na dawa za kulevya.
Tabia za kimila (kama vile utakasaji wajane na jando na unyago)
Safari za aina zote zinazosababisha kuwa mbali kwa wanandoa na ongezeko la mahawara
Kutokutahiriwa

LE MUTUZ" KAJALA JIRUDI MY SISTER MUOMBE MUNGU WAKO AKUSAIDIE UELEWANE NA WEMA"

$
0
0


@ LE MUTUZ SYSTEM LIVE STRAIGHT TALK!!:-
LEO I HAVE TO SAY SOMETHING KUHUSU VITA YA MY TWO SUPER FRIENDS SUPER STAR KAJALA NA WEMA SEPETU.

MIMI NI BAHARIA KWENYE UBAHARIA TUNA RULE NAMBA MOJA NAYO NI WE DO NOT BETRAY OUR FRIENDS NA HASA KAMA AMEKUSAIDIA UKIWA NA MATATIZO, NA BINADAM YOYOTE ULIYEMSAIDIA AKIWA KWENYE MATATIZO MAKUBWA AKAKUGEUKA AKIWA HANA SHIDA TENA SIO MTU WACHANA NAYE NI MSHENZI NA NI MNYAMA, NINASEMA HIVI REGARDLESS YA CHANZO CHA BIFU LAO, I HOLD KAJALA RESPONSIBLE KWA KUENDELEA KWA THIS CHILDISH BIFU DUNIA NZIMA INAJUA KUWA KAMA WEMA SEPETU HAKUMTOLEA ZILE MILLIONI 13 ANGEOZA JELA MPAKA LEO, MIMI NILIFIKIRI KILA KAJALA AKIKUMBUKA THAT ATAMUHESHIMU WEMA NA MAPUNGUFU YAKE HATA YAWE VIPI NA KAMA YAMEZIDI KIPIMO SI UNAMKWEPA TU LAKINI YOU REMAIN FRIENDS!!

- I MEAN THIS ONGOING FEUD INANISIKITISHA SANA KWA SABABU INAKUTOA UTU KAJALA NA KWA SABABU MBILI MUHIMU KWANZA WEWE NI MKUWBA KIUMRI KULIKO WEMA NA PILI AMEKUSAIDIA MAHALI AMBAPO HAKUNA MTU MWINGINE ANGEWEZA KUKUSAIDIA HAO UNAOWARINGIA SASA WALIKUWA WAPI SIKU ILE PALE MAHAKAMANI? I WAS THERE MACHO YALIKUWA YAMEKUTOKA MEKUNDU MACHOZI YANAKUMWAGIKA KAMA MVUA, AKAJA WEMA KUKUOKOA NA SASA NI YALE YALE SHUKRANI YAKO YA PUNDA!! JIRUDI MY SISTER MUOMBE MUNGU WAKO AKUSAIDIE UELEWANE NA WEMA HATA KAMA HAMUWEZI KUWA MARAFIKI LAKINI KUWEPO NA AMANI KATI YENU, MIMI SIMZIMIKII MTU YOYOTE ASIYE NA SHUKRANI NA KWENYE HILI NI WEWE HUNA SHUKRANI, SO BACK OFF!!,
JAMANI JIONI NJEMA!! -LE MUTUZ

DIAMOND PLATNUMZ AJISOMBEA TUZO 7 ZA KILL MUSIC AWARDS...MWEE

$
0
0
Msanii wa kizazi kipya, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz leo May 3, 2014 amedhihirisha kuwa yeye ni msanii mkali kwa kuchukua tuzo saba katika Tuzo za Kilimanjaro 2014 (KTMA).

Diamond amejinyakulia tuzo:

Msanii Bora wa Kiume,
Video Bora ya Mwaka.
Mtumbuizaji bora wa Muziki wa Kiume.
Wimbo Bora wa Afro Pop.
Wimbo Bora wa Mwaka.
Mtunzi Bora wa mwaka Kizazi Kipya.
Wimbo Bora wa Kushirikisha/Kushirikiana.

Hakika Diamond ameonyesha ukali wake, na kuonyesha kuwa yeye ni bora zaidi na anapendwa na watu.

WASHINDI WA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC NI HAWA

$
0
0
1. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA TANZANIA - Bora Mchawi, Dar Bongo Massive

2. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKA - Young Killer Msanii Bora Chipukizi Anayeibuka, Young Killer akiwashukuru mashabiki baada ya kutwaa tuzo.

3. WIMBO BORA WA ZOUK - Yahaya, Lady Jaydee

4. WIMBO BORA WA AFRO POP - Number One, Diamond Platnumz

5. WIMBO BORA WA RAGGA / DANCEHALL - Nishai Chibwa Ft Juru

6. WIMBO BORA WA RAGGAE - Niwe na wewe, Dabo

7.WIMBO BORA WA TAARAB - Wasiwasi wako, Mzee Yusuf

8. KIKUNDI CHA MWAKA CHA TAARAB - Jahazi Modern Taarab

9. MWIMBAJI BORA WA KIKE  TAARAB - Isha Ramadhani

10. MWIMBAJI BORA WA KIUME TAARAB - Mzee Yusuf

11. WIMBO BORA WA KISWAHILI BENDI - Ushamba mzigo, Mashujaa Band

12. MWIMBAJI BORA WA KIKE BENDI - Luiza Mbutu

13. MWIMBAJI BORA WA KIUME BENDI - Jose Mara

14. RAPA BORA WA MWAKA BENDI - Furguson

15. BENDI YA MWAKA - Mashujaa Band

16. MWIMBAJI BORA WA KIKE, KIZAZI KIPYA - Lady Jaydee

17. MWIMBAJI BORA WA KIUME, KIZAZI KIPYA - Diamond

18. KIKUNDI CHA MWAKA CHA KIZAZI KIPYA - Weusi

19. WIMBO BORA WA RNB - Closer, Vanessa Mdee

20. WIMBO BORA WA HIP HOP - Nje ya Box, Nick wa Pili Ft Joh Makini & Gnako

21. MSANII BORA WA HIP HOP - Fid Q

22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKISHA / KUSHIRIKIANA - Muziki Gani, Nay wa Mitego ft Diamond

23. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI - Tubonge, Jose Chameleone

24. MTUNZI BORA WA MWAKA TAARAB - Mzee Yusuf

25. MTUNZI BORA WA MWAKA BENDI - Christian Bella

26. MTUNZI BORA WA MWAKA KIZAZI KIPYA - Diamond

27. MTUNZI BORA WA MWAKA HIP HOP - Fid Q

28. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, TAARAB - Enrico

29. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, BENDI - Amoroso

30. MTAYARISHAJI BORA WA NYIMBO WA MWAKA, KIZAZI KIPYA - Man Water, Combination Sound

31. HALL OF FAME, INDIVIDUAL - Hassan BItchuka

32. HALL OF FAME, INSTITUTION - Masoud Masoud

33. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA - Number One, Diamond

34.WIMBO WA MWAKA - Number One. Diamond

35. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI - Isha Ramadhani


36. MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME WA MUZIKI - Diamond

WEMA APAGAWA NA TUZO 7 ZA DIAMOND,SOMA ALICHOKISEMA BAADA YA DIAMOND KUTWAA TUZO HIZO

$
0
0
Kila msichana hivi sasa anandoto za kuwa kama WemaSepetu hivi sasa, kwa kuweza kujivunia mafanikio ya mpenzi wake Diamond Platnumz, baada ya kuandika historia katika Game hili la muziki wa Bongo Fleva, kwa kuchukua tuzo zote katika kila kitengo alichokuwa anawania, baada ya ishu nzima kuisha, haya ndio maneno ya Wema ya kwanza kuandika , Wema Sepetu aliandika kupitia Account yake ya instagram;


Yaani mpaka hadi kuzipanga unashindwa unaanzaje kupanga… He managed to snatch dem all…. My champion…. We hav an award for erday…. Monday to Sunday baby…. Yaaaani #tikaTika….. Im a proud girl…. Sooooo proud… Salute to U Champion… .dpuf

DK. KIGWANGALA AUTAMANI URAIS 2015

$
0
0
Na John Dotto
MBUNGE wa jimbo la Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala, ametanabaisha kuwa anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao kupitia chama cha mapinduzi CCM.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala mara kwa mara inayomshawishi kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema anatafakari jambo hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika atayazingatia maoni ya wananchi.

Akizungumzia maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk. Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.

Hivi karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la kumshawishi Dk. Kigwangala kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2015.

Mijadala hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu ujao.

Baadhi ya vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani, wakijenga hoja kuwa amekuwa na misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.

Dk Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.

TAASISI KONGWE BADO ZINATUMIA JINA LA TANGANYIKA..HII INAKUWAJE?

$
0
0
Kuna taasisi kongwe na muhimu sana zinaendelea kutumia jina la Tanganyika na pia huduma zake kimipaka ni "Tanzania bara''

1.Medical Council of Tanganyika aka MCT

2.Tanganyika law society aka TLS

3.Tanganyika Farmers Association
aka TFA

4.International School of Tanganyika
aka IST

5.Tanganyika Arms ltd.


hizi ni baadhi ya taasisi/jumuiya zinazotambulika kiserikali zinazoendelea kutumia jina la Tanganyika.

Nyuma ya taasisi/jumuiya hizi kuna madaktari,wanasheria,wanafunzi na wakulima.

Hebu ongeza list ya taasisi zinazotumia jina la TANGANYIKA!

DIAMOND ATINGA NA SKETI KILL MUSIC AWARDS

$
0
0
Wajameni mimi sijui mshamba au ndo kupitwa na mambo , hivi hii staili ya kuvaa sketi kwa wanaume ndio fashion sasahivi ama? Jana Diamond aliingia na sketi hiyo hapo juu ....nikabaki midomo wazi......Je ni sawa?

MAPENZI "NAKUJA CHUMBANI KWAKO ILA SITAKI UKOROFI WAKO"

$
0
0
Jamani Mapenzi kitu cha ajabu.

Ila Watu nao wapo wa ajabu vilevile.

Fikiria;
Ni muda sasa mmekuwa mnatongozana, 
Baada ya sitaki nataka nyiingi mwishoe Mtoto wa kike anakupa ile 'No inayomaanisha Yes' 
Huku akiangalia chini kwa sauti ya puani nahuku akionekana kukuonea soni,
"Basi nitakuja chumbani kwako iIa, Sitaki ukorofi"

Mkware hapo hapo unajua tayari keshajiingiza.

Binti kweli hatimae anakuja room kwako, 
Kajikwatua hasa; Yupo Msafi, Kapendeza, Ananukia na ukimuangalia yupo katika Mood ya majamboz kwa 100%.

Sasa mpo kwenye Sofa sebuleni kwako.
Stori mbili-tatu, Mvinyo wa kuwasindikiza kwa pembeni na kila mmoja yupo na Glass yake,
Kila mmoja apendapo mara kadhaa hajipendelei peke yake, anamnywesha mwenzake pia kupitia glass yake
(Sio Uchafu kwa wapendanao mara mojamoja) 

Maongezi yananoga...

Unamuomba mhamie room, 
Binti Kwa sauti ya puani anakupa si nilishakuambia? "Unaanza ukorofi wako", 
Unamvuta kwa kutumia mkono lakini unaona (Mbuzi yake kamba)
Habishi, Kimoyomoyo unajisemea Yess! -Tembo kwa Ubua, -mzee unang'oa leo. 

Fasta unabadilisha zoezi,
Unamua kumbeba kabisa unaona kama unachelewa kula Tunda, Vooom mpo kwa room. 
Mzee usha taarisha Chumba kwa ajili ya Tukio rasmi la game siku hiyo, 

Chumba Kinanukia roses, Huku nako Ipo chupa iliyojaa pomoni mvinyo ule ule mnaoutumia na glass zake tupu pia,
Well ventilated na kuna ukimya na faragha ya kutosha, Upepo wa ki-Feni kwa mbaaali, Sio sana.
Sub-Woofer yako nayo haipo nyuma,
Inachombeza pembeni kwa muziki muororo na laini lakini ni instrumental tu na umeiset non-stop mode.

Unaanza kumbusu mashavu ana tabasamu na anakupa ushirikiano,
Unaendelea, Unalamba Shingo huku unatomasa hapa na pale aili mradi kuamsha mshawasha, 
Alhamdulilah unapewa ushirikiano wa kutosha pia.

Alaa!! kumbe ushapewa kibali cha kutali katika mwili wa binti huyu?
Dunia ya nani tena kama si yako wewe pekeyako?

Unaanza kujisaulisha viwalo, Hee binti nae anawajibika kusaula vya kwake, 
Unajisemea kimoyomoyo mambo si ndio haya!,
Romance inaendelea na mwishowe wote mko kama mlivyozaliwa;Mataarisho yanaendelea,
shika hapa shika pale, nyonya hapa nyonya pale, tomasa huku.. ...

Mnaingia kwenye main event.

Mambo Si haba Kila kitu kipo kama ulivyotegemea,
Binti mzuri,mtamu na mjuzi pia.

Ila sasa,
Anaufunika uso wake kwa Viganja vya mikono yake almost muda wote wa majamboz .
Eti, Anakuonea aibu.

WAT IZ ZIS??

MENEJA WA WEMA SEPETU WATUPIANA VIJEMBE NA MPOKI JANA KWENYE TUZO KILI

$
0
0
Meneja wa Muigizaji maarufu wa Bongo Movie Wema sepetu amewaacha midomo wazi watu waliokuwa wamehudhuria Tuzo ya Muziki ya Kilimanjaro katika ukumbi wa mlimani City jana baada ya kupaniki na kujikuta anajibu mapigo kwa Mc wa sherehe hiyo Silvery Mjuni anayefahamika zaidi kwa jina la Mpoki.

Meneja wa Wema aitwae Martin Kadinda amejikuta ameshindwa kuzuia hisia zake kutokana na masihara ya mpoki pale alipowaambia kuwa timu Diamond ni kikundi kinachoongoza kupost picha hata zisizo na msingi kwenye mitandao ya kijamii hususani Instagram,

Mpoki aliwaambia  Diamond na wafuasi wake akiwemo wema,martin kadinda,Rommy Johnson kuwa  wanapost kila wakati kwa mfano wakiwawanakula,wamelala ndipo Martin kadinda alipomwambia mpoki kuwa atafute namna nyingine ya kutafutia pesa.


Kauli ya Kadinda iliwashangaza wengi kwani licha ya kuwa mpoki alikuwa anazungumza kimasihara lakini jambo lake linaukweli kwa kiasi kikubwa japo Kadinda alikuwa mwepesi kupanik na kushindwa kukubaliana na ukweli huo.

UCHUNGUZI: MAKALIO MAKUBWA KUNA VINGI NDANI YAKE

$
0
0
Uchunguzi uliofanywa nchini Uingereza umeendelea kulipandisha chati umbo la kibantu, kwa kusema kwamba, kuwa na unene zaidi eneo la mapajani, katika makalio na katika mahips ni vizuri kiafya, na humzuia mtu asipate matatizo ya kiafya.
Wataalamu wanasema kuwa, mafuta yanayopatikana katika mahips, huondoa fati asidi mbaya kiafya ambazo huwa na mada za kuzuia uvimbe ambazo huifanya mishipa ya damu isizibe. Timu hiyo ya wachunguzi imesema kuwa, makalio makubwa ni bora kuliko mafuta ya zaida yanayojilundika katika mzunguko wa kiuno, ambayo hayasaidii chochote.

Wachunguzi hao wamesema katika Jarida la Kimataifa la Obesiti kwamba, sayansi inapaswa kuangalia jinsi ya kuongeza mafuta katika eneo la mahips na pengine katika siku zijazo madaktari watatakiwa kuangalia njia za kuyahamisha mafuta mwilini na kuyapalekea katika sehemu za mahips ili kulinda afya za watu kutokana na magonjwa ya mishipa ya moyo na magonjwa mengineyo kama kisukari. 

Watafiti hao wameeleza kwamba, kuwa na mafuta kidogo katika hips kunaweza kupelekea matatizo makubwa ya umetaboli.
Wataalamu hao wameendelea kusema kwamba, ushahidi unaonyesha kwamba, mafuta yanayozunguka mapaja na sehemu za nyuma ni vigumu kuyeyuka kuliko yale yaliyo katika kiuno. 

Ingawa suala hilo linaonekama kana kama ni kinyume, lakini ni kweli kwamba kutoyeyuka huko kuna faida kwani, wakati mafuta yanapoyeyuka kwa urahisi hutoa mada inayoitwa cytokines ambayo huleta uvimbe katika mwili.Mada za cytokines zinahusiana moja kwa moja na magonjwa ya moyo na kisukari. Kuyeyuka taratibu kwa mafuta katika mapaja pia husababisha homoni ya adiponectin izalishwe kwa wingi na husaidia kudhibiti sukari katika damu na jinsi mafuta yanavyochomeka. 

Dakta Konstantinos Manolopoulos aliyeongoza utafiti huo kutoka chuo kikuu cha Oxford amesema kuwa, la muhimu ni umbo na wapi mafuta yanakusanyika, na kwamba unene wa mahips na mapaja ni mzuri kuliko unene wa tumbo.

TAIFA STARS KUSAFISHA NYOTA LEO ?

$
0
0
Taifa Stars inahitaji kusafisha nyota leo mbele ya mashabiki wa soka mkoani Mbeya na Tanzania kwa ujumla kwa kuitandika Malawi ‘The Flame’ katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa.

Wapenzi wa soka mkoani Mbeya walianza jana kupeperusha bendera ya Taifa kila kona huku gari la matangazo likizunguka mitaani kuwahimiza wajitokeze kwa wingi kujionea mchezo huo kwa kiingilio cha Sh5,000.

Hata hivyo, mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali kutokana na ukweli kwamba timu zote zitataka kufuta machozi ya kufungwa katika mechi za kirafiki zilizochezwa wiki mbili zilizopita, ambapo Stars ilinyukwa mabao 3-1 na Burundi wakati Flame ilitandikwa 4-1 na Zimbabwe, ambao wana mchezo na Stars mwishoni mwa mwezi huu.

MVUTANO MKALI WATOKEA KATI YA SERIKALI NA BUNGE...CHANZO NI VIGOGO MALI ASILI

$
0
0
Sasa ni dhahiri kwamba kuna msuguano wa wazi kati ya mihimili miwili ya dola, Bunge na Serikali, kuhusiana na hatua ya Serikali kuchelewa kutekeleza maazimio ya Bunge.

Msuguano huo umeshika kasi wiki hii baada ya Serikali kuwarudisha kwenye nyadhifa zao vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao hivi karibuni waliondolewa na Waziri Lazaro Nyalandu, huku wabunge wakiapa kuibana Serikali kuwang’oa viongozi hao.

Vigogo hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi, Jaffar Kidegesho kwa madai ya kutowajibika ipasavyo katika vita dhidi ya ujangili nchini.

Mbali na sababu hiyo, lakini Nyalandu alikaririwa akisema alichukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mazimio 16 ya Bunge, yaliyotolewa baada ya taarifa ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

PENNY APATA KAZI KITUO KIPYA CHA REDIO EFM 93.7

$
0
0


Kukufanya uelewe zaidi ni kuwa Penny ameshamove on… So wakati Weimond wakila bata Mtwara, Penny amekuwa akijiandaa kwenda hewani kama mtangazaji wa kituo kipya cha redio cha Dar es Salaam, EFM

“EFM 93.7 Dar es salaam… Wazungu wanasema??!!’ Coming soon,” ameandika Penny kwenye picha anayoonekana akiwa ndani ya studio za kituo hicho cha redio.

BREAKING NEWS:MABASI MAWILI YALIPULIWA NA MABOMU KENYA

$
0
0
One person dead and several others injured after two  explosions hit two buses along Thika road. The explosions occurred in different buses that had left town heading to Githurai. The first explosion happened outside Homeland Inn and the second at Thika Road Mall roundabout.

Kocha Mholanzi Awapiga Chini Wachezaji wa TFF Timu ya Taifa

$
0
0
KOCHA mpya wa Taifa Stars, Mart Nooij jana Jumapili ameanza kuiongoza timu hiyo na kutoka suluhu na Malawi katika mchezo wa kirafiki maalumu kwa maandalizi ya mechi za kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Afrika 2015 dhidi ya Zimbabwe.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sokoine mjini hapa, Nooij raia wa Uholanzi alianzisha kikosi kilichosheheni nyota wa timu za Ligi Kuu Bara huku akiwaweka benchi wachezaji wawili tu wa timu ya maboresho waliocheza dhidi ya Burundi hivi karibuni.

Baada ya mchezo huo, Nooij aliliambia Mwanaspoti kuwa: “Nimekaa na timu wiki moja tu, nimeridhika na kiwango walichoonyesha haya ni maandalizi mazuri dhidi ya Zimbabwe. Tutarekebisha makosa niliyoona leo ili tuifunge Zimbabwe.”

Kocha wa zamani wa Yanga ambaye sasa ni Kocha Msaidizi wa Malawi, Jack Chamangwana, alisema Taifa Stars imecheza vizuri na kama ikikomaa inaweza kufika mbali katika kufuzu Kombe la Afrika.

Kipindi cha kwanza Taifa Stars ilifanya mashambulizi kadhaa ikiwemo dakika ya 11 beki Aggrey Moris alipopiga kichwa kilichoshindwa kulenga lango na straika John Bocco dakika 36 alipiga shuti lililotoka nje kidogo ya lango la Malawi.

Kipindi cha pili dakika ya 52 kidogo Malawi ipate bao baada ya Rodrick Gonani kuwazidi maarifa mabeki wa Taifa Stars, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Moris na kupiga shuti kali lililopanguliwa na kipa Deo Munishi ‘Dida’. Taifa Stars itacheza na Zimbabwe kati ya 16 na 18 Mei mwaka huu jijini Dar es Salaam kabla ya kurudiana baada ya wiki mbili.
Viewing all 104755 articles
Browse latest View live




Latest Images