Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Watu Waliomkufuru Mungu Wakafariki Dunia Saa Chache Tu Baada ya Kumkufuru..!!!...

$
0
0

1. Mtengenazaji meli ya titanic.
Baada ya kutengeneza meli ya TITANIC, mwandishi wa habari alimuuliza ni kiasi gani ilikuwa salama, nae akajibu " Ni salama sana na haiwezi kuzama na hata mungu hawezi kuizamisha". 
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu TITANIC

2.AZUZA (mwanamuziki brazil)
Alipokuwa kwenye show yake ndani ya jiji la Rio dejeneiro , alichukua sigara akaanza kuvuta, akachukua nyingine kisha akairusha juu na kusema " Mungu na hiyo yako , chukua na wewe uvute. Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu, ambayo iliharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote.

3.Christina hewt (mwandishi)
Huyu alikaririwa akisema " Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya kama biblia, siku chache baada ya kusema maneno hay, mwili wake ulikutwa umeunguzwa moto ambao haijajulikana hadi Leo umesababishwa na nini.

4. John Lennon (muimbaji)
Wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari la gazeti la america alinukuliwa akisema " ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwas na hilo kwa kuwa Nina uhakika nalo. Huyu naye baada ya mda alikutwa amekufa nyumbani kwake

5. Tancredo neves (rais wa brazil)
Alisema kwamba endapo angeshinda kura laki tano katika uchaguzi mkuu Brazil na kuwa rais , hata mungu asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa akapata kura zaidi ya laki tano akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa akafariki dunia.

Kimenukaaa..Lipumba Aibuka na Lundo la Tuhuma Dhidi ya Maalim Seif na Chadema..!!!!

$
0
0

Sarakasi zimeendelea ndani ya Chama cha CUF baada ya mwenyekiti wake anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba kumshutumu Maalim Seif Sharif kwa madai ya kutaka kukiua chama hicho.

Lipumba alitoa tuhuma hizo jana, wakati wa kongamano la Jumuiya ya Vijana wa CUF (Juvicuf), lililofanyika kwenye ofisi za chama hicho Buguruni.

Akihutubia kongamano hilo alimtuhumu Maalim Seif kwa madai ya kubadili utaratibu wa vikao vya ushauri kwa kuzungumza na mkurugenzi mmoja mmoja badala ya kuwaweka pamoja.

Alisema kitendo hicho ni cha kumdhalilisha Naibu Katibu mkuu wa chama hicho Bara, Magdalena Sakaya.

“Sakaya amefanya kazi kubwa sana kukijenga chama hiki. Lakini leo katibu mkuu (Maalim Seif) anamsimamisha uanachama Sakaya ili afukuzwe ubunge. Hivi tunajenga chama kweli hapa,” alihoji Lipumba na kujibiwa na wanachama wenzake kuwa chama kinabomoka.

Alisema huu ni wakati wa kukijenga chama na hakuna mwanasiasa bara aliyefanya kazi kubwa kuwatetea Wazanzibari kama yeye (Lipumba).

“Nasikia Maalim Seif anasema kutatokea machafuko endapo Rita wakifanya mambo yao. Maalim…hivi kukiwapo maandamano, kweli utakuwa mstari wa mbele, lini kulitokea ukawapo? Wakati maandamano yakifanyika unakimbilia Ulaya na habari unazipata huko huko,” alisema Lipumba.

Hata hivyo, Lipumba alisema amemsamehe Maalim Seif na yupo tayari kukaa naye meza moja ili kukijenga chama hicho ikiwamo kujenga uchumi utakaoleta manufaa kwa wananchi.

“Wakati wowote Maalim Seif njoo tuzungumze na turekebishe mambo,” alisema Lipumba.

Pia, Lipumba alikishutumu Chama cha Chadema kwamba kinamhadaa Maalim Seif na kinaweza ‘kumuuza’ kama kilivyofanya kwa Dk Wilbrod Slaa na kwamba hakina demokrasia kama kinavyotamba.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim alisema chama hicho kinamtakia kila la kheri Lipumba na alimtaka akiache chama hicho kama kilivyo.

“Hata kama …hatuna demokrasia atuache kama tulivyo. Lakini tunachojua hatumtambui yeye kama mwenyekiti wa CUF,” alisema Mwalim.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema Lipumba bado anaendelea kutapatapa na asitarajie yeye au Maalim Seif kufanya naye kazi pamoja.

“Umeniambia Profesa Lipumba amemsamehe Maalim Seif kwa kosa lipi? Hivi kati yake na Maalim nani kafanya kosa. Profesa Lipumba ndiyo anatakiwa kuomba msamaha Watanzania,” alisema.

Alisema chama hicho kinafuata taratibu na hatua ya kumsimamisha uanachama Sakaya ilifuata kanuni kwa mujibu wa chama hicho.

Profesa Lipumba aliingia katika mgogoro na chama chake baada ya kuandika barua ya kujivua uenyekiti lakini baada ya mwaka mmoja wa nje ya uongozi alitengua kujiuzulu kwake.

Mkutano mkuu wa chama hicho ulikubali barua ya Lipumba ya kujiuzulu uongozi, lakini baadaye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini iliandika barua ya kumtambua Lipumba kuwa ndiye mwenyekiti halali wa CUF, hali iliyokipasua chama hicho hadi sasa.

Inasikitisha Sanaaa..Mtoto wa Miaka 12 Abakwa..Apewa Mimba na Kujifungua Mtoto..Stori Kamili Hii Hapa..!!!

$
0
0

Binti mwenye umri wa miaka 12 amejikuta akipoteza haki yake ya kuwa mtoto baada ya kubakwa, kupewa ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume.

Ni sawa na kusema mtoto amejifungua mtoto.

Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 inamuelezea mtoto kuwa ni yule aliye na umri chini ya miaka 18 na kimaadili gazeti hili linahifadhi jina lake.

Mwananchi ilienda maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam kumshuhudia mtoto huyo akiwa amempakata mwanae huku akimbembeleza anyonye kwa kuwa alikuwa akilia.

Uso wake uligubikwa na machozi wakati wote wa mazungumzo na gazeti, na unyonge ulizidi pale mtoto wake alipolia. Kilio cha kichanga huyo mwenye umri wa miezi minne, kilitokana na njaa kwa kuwa maziwa ya mama yake yalikuwa hayatoki.

Bibi yake, Elizabeth Mahundi alisema mjukuu wake, alijifungua kwa njia ya kawaida Novemba 28, 2016 katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

“Ni kweli kwamba mjukuu wangu ni mtoto wa miaka 12, hakuna aliyeamini kama angeweza kujifungua salama lakini, kwa uwezo wa Mungu, imekuwa. Inahuzunisha, inaumiza naomba Serikali isikae kimya inisaidie,” alisema na kuongeza:

“Akili yake haipo sawa japo alikuwa akisoma darasa la nne Shule ya Msingi Pera, ni mtoto asiyeweza kumhudumia mwanaye. Kila kitu nafanya mimi, na kibaya zaidi sina uwezo kabisa.”

Mtoto huyo alisimulia kinagaubaga alivyofanyiwa ukatili na mwanaume (Jina linahifadhiwa), ambaye anadai ni mtoto wa shangazi yake.

Simulizi ya mtoto

Mtoto huyo alisema, ilikuwa mchana wakati anatoka shule alipokutana na mwanaume huyo ambaye alimvutia kwenye pagale (nyumba mbovu). “Nilikuwa natoka shuleni nikakutana na..., aliniita nikaitika, akanivutia kwenye pagale,” alisema. Alisema mwanaume huyo alimtaka avue nguo lakini kwa sababu hakujua kinachotaka kufanyika, aligoma na kuomba arudi nyumbani.

“Alinikamata akanivua nguo zote na akanifanyia kitu kibaya. Nililia lakini alisema nisimwambie mtu kwani nikifanya hivyo atanifanyia kitu kibaya tena,”alisema.

Mtoto huyo alisema kuwa alirudi nyumbani kwa bibi yake mzaa baba, aliyekuwa akimlea katika kijiji cha Pera, Chalinze, Bagamoyo Mkoa wa Pwani na hakusema kitu akihofia kuumizwa na mbakaji huyo.

“Niliendelea kukaa nikashangaa kila siku nimeshiba, tumbo kubwa ndio wakaniweka kikao nikawaambia ni... alinifanyia kitu kibaya. Wakasema nisiseme kwa mtu,” alisema mtoto huyo na kuangua kilio zaidi.

Mtoto huyo anashindwa kuzungumza kutokana na kilio hicho. Wakati huo mtoto wake aliyekuwa akibembelezwa na bibi alikuwa amelala na hivyo kulazwa kitandani, kwenye chumba kimoja wanamoishi.

Alisema anaomba aendelee na masomo yake kwani anaamini anaweza kumaliza shule.

“Naomba msaada wa maziwa ya mtoto hayatoki na naomba nisome,” alisema.

Hali niliyoikuta nyumbani

Mwananchi lilifika nyumbani kwa familia hiyo na kumkuta akimbembeleza mtoto na ilikuwa kama sinema ya mtoto anayecheza na mdoli wake, akiigiza kumnyonyesha. Lakini hili lilikuwa ni tukio halisi la binti wa miaka 12 akimnyonyesha mtoto wa miezi minne.

“Nyamaza, nyamaza unyonye” ilikuwa sauti ya mtoto huyo akimbembeleza mwanaye.

Bibi Mahundi alisema, mtoto huyo analia njaa. Hata siku Mwananchi linafika katika familia hiyo, inaelezwa kuwa walishindia uji na hali hiyo inasababisha mzazi mtoto akose maziwa.

Hatukuweza kuanza mazungumzo, hivyo ikabidi yatafutwe maziwa kwa ajili ya mtoto.

“Maisha yangu magumu, sina kazi na kama unavyoona. Sina namna inabidi nijitahidi kumlea mjukuu wangu ambaye hajiwezi. Hawezi hata kumfulia mwanae nguo, ama kweli dunia ngumu,”aliongea bibi ambaye alibubujikwa na machozi.

Bibi Mahundi alisema siku hiyo hakukuwa na hata tone la unga.

Afya mtoto huyo imezorota na ngozi yake inaonyesha anakosa lishe bora kutokana na hali ngumu ya maisha inayomkabili bibi yake.

Midomo imebadilika rangi kwa kukosa chakula, ni ukweli usiopingika, anahitaji msaada.

Ilikuwaje

Bibi Mahundi anasema ilikuwa saa sita usiku aliposikia mlango unagongwa. Alifungua na kukutana na mtoto huyo akiwa analia huku akishindwa kuongea.

“Nilishangaa kuona mtoto wangu analia, wakaniambia wameniletea mtoto nimuangalie hali yake, nilichungulia nje na kumkuta akiwa na tumbo kubwa, jasho linamtoka na amechoka sana. Niliishiwa nguvu kwa kweli,” alisema.

Aliwaambia waingie ndani ndipo wakamwambia kuwa mtoto aliyekuwa akiishi Pera, Chalinze kwa bibi yake mzaa baba ameletwa akiwa mjamzito licha ya umri wa miaka 12, alionao.

“Nilimpokea mjukuu wangu, nikalala naye hadi asubuhi. Kulipokucha mama yake alienda kijijini alikokuwa anaishi lakini aliambulia kutukanwa,”alisema na kuongeza:

“Aliambiwa kwanza mtoto si wa kwao kwa sababu kule ni kwa bibi mzaa baba. Na wakajigamba kwamba hakuna sheria inayoweza kuwafanya chochote, kwa unyonge alirudi, nikamsihi atulie tumtunze mtoto tukimuombea uzima.”

Siku ya kujifungua

Baada ya wiki mbili tangu mtoto huyo awasili Dar es Salaam, alipata uchungu. Bibi yake alisema walihangaika kutafuta usafiri hadi Mwananyamala na baada ya muda mfupi, alijifungua kwa njia ya kawaida.

“Nilimshukuru Mungu, sikuamini kama mtoto wa miaka 12 anaweza kujifungua kawaida. Alikaa hospitali siku saba, kisha tukaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na afya njema,”alisema.

Mama yake mdogo, Rose John alisema jambo hilo limeiumiza familia nzima. “Kila nikimuangalia huyo mtoto naishia kulia, natamani kumsaidia lakini hata mie zaidi ya kufanya kazi za ndani sina msaada wowote. Hakika naomba Serikali isikae kimya, huu ni ukatili,”alisema.

Waziri atoa tamko

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema wamepokea kwa masikitiko taarifa hiyo na jitihada zinafanywa kumkamata mwanaume aliyehusika kwenye tukio hilo. “Tutahakikisha kijana aliyempa ujauzito binti huyu anakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola,” alisema.

Alisema Serikali haiwezi kuvumilia kuona watoto wadogo wa kike wanadhalilishwa na kupewa ujauzito wakiwa na umri mdogo na hivyo kuacha masomo.

“Hivi kweli tutafikia Tanzania ya viwanda wakati asilimia 27 ya watoto wa kike wanabakwa na kupewa mimba hivyo? Hakika mimba za utotoni na ukatili ni kikwazo,” alisema Ummy. Alisema tayari kikosi kazi kimeanza kufuatilia suala hilo na kuahidi kuwa Serikali itatoa taarifa zaidi ya kitakachoendelea.

Wanaharakati wazungumza

Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania, Lilian Liundi alisema lazima ukimya uvunjwe ili hatua za kisheria kwa aliyehusika kumdhalisha mtoto huyo kukamatwa.

“Haijalishi ni binamu, mjomba wala nani anapaswa kukamatwa ili hatua zichukuliwe. Haya masuala ya ndugu ndiyo yaliyotufikisha hapa tulipo kwa watoto wengi kubakwa, kupewa mimba na kuzalishwa kwenye umri mdogo,”alisema.

Mama mzazi azungumza

Mama mzazi wa mtoto huyo (jina linahifadhiwa) alisema hana la kuzungumza zaidi ya kuomba msaada kwa ajili ya mwanae.

Kwa atakayeweza kuisaidia chakula anaweza kutuma fedha kwa simu 0787 672117

Ukweli Mchungu..Roma na Wenzako, Msithubutu Kuwasariti Wapiga Yowe Wenu..!!!!

$
0
0

Kitendo chenu cha kuficha ukweli wa mambo ulivyo, eti kwa sababu ya mapatano na watekaji; 

Mosi.
Huku kutakuwa ni kuwasariti wale walioshinikiza kuachiwa kwenu, na ni dhambi mbaya sana!

Pili.
Kitendo cha kuficha ukweli wa mambo ulivyo;
Huko kutakuwa ni kuridhia ndugu zenu na jamaa zenu waendelee kutendewa kama ninyi au zaidi yenu, yaani kupotezwa kabisa kama Ben.

Tatu.
Kitendo cha kuficha ukweli wa yale yaliyowakuta;
Huko kutakuwa ni kuiridhia dhambi ya watekaji.

Nne. kitendo cha kudanganya ili kuficha dhamira ya watekaji;
Huko kutakuwa ni kumkosea Mungu aliyewatoa katika makucha ya simba wenye uchu wa nyama zenu.

Mwisho.

Roma mkatoriki, mnamkumbuka Dr. Ulimboka?

Nani ajuae huenda angeweka ukweli wa mambo yaliyomkuta wazi leo msingekuwa wahanga wa haya!

Narudia. 
Semeni ukweli ili kuwatia moyo watetezi wenu kusudi waendelee kuwapambania wengine.
Semeni ukweli maana wasema kweli ni wapenzi wa Mungu.

Noma Sana..Watanzania Wageukia Lugha ya Kichina..Wanajifunza Kama Mchwa...!!!

$
0
0

Kutokana na ushirikiano uliopo kati ya nchi ya Tanzania na China, lugha ya Kichina imeelezwa kuwa ni fursa ya ajira kwa Watanzania hivyo inatakiwa kufundishwa hasa katika vyuo.

Hayo yalibainishwa jana na Naibu Mkuu wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA), Dk Thomas Ndaluka wakati wa warsha ya utamaduni wa China iliyofanyika kwenye chuo hicho.

“China na Tanzania ni marafiki hivyo ni muhimu kujua utamaduni wa kila mmoja, lakini Watanzania wanapojifunza Kichina wanapanua wigo wa kuweza kuajirika kwenye kampuni za China,” alisema.

Aidha, alisema lengo hilo linaenda sambamba na kuhamasisha ufundishaji wa Kiswahili kwa Wachina.

“Sisi kama Tanzania tunafanya juhudi za kufundisha Kiswahili kwa wageni kupitia kozi zetu na hata Watanzania wanaokwenda nchini China kwa masomo au kikazi wana nafasi kubwa ya kuendeleza Kiswahili,”alisema.

Mratibu wa Kozi ya Kichina wa Chuo hicho, Dk Phillip Daninga alisema uhitaji wa kujifunza lugha hiyo umeongezeka kutokana na fursa zilizopo kupitia lugha hiyo.

“Hadi sasa kuna Watanzania zaidi ya 600 wanaojifunza Kichina. Pia, takribani wahitimu 5,000 wa lugha hiyo wameajiriwa na kampuni za China hapa nchini,” alisema Dk Daninga.

Dk Daninga alisema kuwa chuo hicho kipo mbioni kuanzisha kozi ya Kichina kwa ngazi ya diploma na shahada mara baada ya kupata kibali cha Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (Nacte).

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza Kichina iliyopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Liu Yan alisema kuwa Taifa hilo linatambua uhusiano uliopo na umuhimu wa kujua utamaduni kuwa ni suala la msingi.

“Ni muhimu kutambuana kila mmoja, walimu kutoka China wanajifunza Kiswahili na sisi tunahamasisha Watanzania wajue Kichina,”alisema Profesa huyo.

TAZAMA LIVE Mahubiri ya Gwajima Leo....Alipoahidi Kumfanyia Kazi Diamond

$
0
0

TAZAMA LIVE Mahubiri ya Gwajima Leo....Alipoahidi Kumfanyia Kazi Diamond

Bonyeza Play:

NAFASI ya Kazi USAID na Zingine Nyingi Zilizotangazwa Magazetini na Mitandaoni

$
0
0

ASKOFU Gwajima Atangaza Kumsamehe Diamond Platnumz..Ila Ampa Onyo Hili

$
0
0
Askofu Gwajima leo alikuwa ameahidi kuweka wazi mambo ya Diamond Platnumz kujiunga kwake na Freemason , Lakini amedai kuwa Jana Diamond kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram Alimuomba Msamaha Kwa Mchungaji huyo,

Watu wengi leo walifurika katika kanisa hilo na wengine kutazama live kupitia Youtube wakitarajia kuwa anafunguka makubwa kuhusu Diamond lakini Karibia na Mwisho wa Mahubiri yake alidai Bibilia inasema mtu akiomba Msamaha Hupashwa Kusamehewa hivyo Hata ameamua Kumsamehe na kumsitiri , lakini ametoa onyo kuwa akiendelea kumchokoza wiki ijayo atafunguka....

Gwajima na Diamond wameingia katika vita baada ya Diamond Kumuimba askofu huyo katika wimbo wake uitwao Niache nikae Kimya

MBUNGE Halima Mdee Katika Kumi na Nane za Gwajima...Amtaka Akamuombe Msamaha

$
0
0
Leo Askofu Gwajima amemuongelea Halima Mdee katika Mahubiri yake na amemtaka Mbunge huyo kuacha mara moja kumtukana Spika akiwa Bungeni maana ni moja ya Mhimili wa Dola.

Amesema kuwa Halima Mdee asipoomba msamaha kwa tukio la kumuita fala Spika basi Jumapili ijayo atamchapa ipasavyo.


Diamond Afurahia Kiki za Gwajima...Amshauri Shetta Kumuoa Mange

$
0
0


By @diamondplatnumz
@officialshetta ndugu yangu, Najua unanionea gere mwenzako toka juzi insta imehamia Madale....na wewe unataka kuingia kwenye huu upepo wa #Mzikisiasa ...we usijiulize ingia tu😁...maana mjini sasa hivi vingoma vya Mapenzi Vigumu...ikiwezekana jifanye hata unataka kumtolea Mahali Mange Umuoe...Kesho mji wote wako.....ila kuna mawili: Sentro au Matusi😅😅😅😅 - #SimbaMason
.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

A -Z ya Kilichomuua Kiongozi wa Freemason Tanzania..Familia Yake Yaibuka na Kufunguka Haya Mazito...!!!!

$
0
0

MWILI wa aliyekuwa Kiongozi wa Jumuiya ya Freemason Tanzania na Afrika Mashariki, Sir Jayantilal Keshavji Chande (89) ‘Andy’ Chande, umewasili juzi kutoka jijini Nairobi nchini Kenya alipokuwa akipatiwa matibabu.

Akizungumza na MTANZANIA mmoja wa wafanyakazi wa Sir Chande ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini, alisema kiongozi huyo aliyefariki juzi alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya tumbo.

“Mwili wake umeshawasili tangu jana (juzi) saa 2:30 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) na wamerudi wote pamoja na familia yake yaani mkewe na watoto watatu waliokuwa wakimuuguza,” alisema mtoa taarifa huyo.

Alisema kwa sasa mwili huo umehifadhiwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, ukisubiri maziko yatakayofanyika Jumanne ijayo.

Mbali na hilo pia alishangazwa na kusambaa kwa taarifa za kifo hicho kwa haraka juzi kwa kuwa familia hadi jana mchana ilikuwa haijapata taarifa rasmi.

“Mzee ni mtu mkubwa si Tanzania tu hata India, Marekani wote wameandika habari zake baada ya kusikia katika mitandao, lakini bado watu hawajaanza kuja kutoa pole, wengi wanapiga simu kuuliza tu kama ni kweli sisi tumeshangaa taarifa hizi mmezitoa wapi wakati hakukuwa na mtu aliyetoa habari  kutoka katika familia jana,” alisema mfanyakazi huyo.

Alisema Sir Chande ambaye anatarajiwa kuchomwa Jumanne katika eneo la Makumbusho, aliugua tumbo kwa kipindi cha wiki moja wakati ugonjwa wake mkubwa uliokuwa ukimsumbua ulidaiwa kuwa ni shinikizo la damu.

Alisema vikao vya familia bado vinaendelea na kwamba wageni kutoka nchi mbalimbali wanatarajiwa kuingia kuanzia Jumapili kuhudhuria mazishi hayo.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana jioni na msemaji wa familia ya Sir Chande ambaye ni mtoto wake, maziko ya kiongozi huyo yatafanyika Jumanne saa nne asubuhi katika makaburi ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

“Taratibu za kuaga mwili wa Sir Chande zitafanya siku hiyo hiyo kuanzia saa 2.30 asubuhi nyumbani kwake,” ilieleza taarifa hiyo.

FAMILIA YAMWELEZEA


Katika taarifa, familia yake pia ilimwelezea Kiongozi huyo kama mtu aliyekuwa na hekima ambapo mara nyingi alikuwa anaisaidia Serikali na Watanzania na watu wengine duniani kote kwa kujihusisha na shughuli za kijamii, uchumi na misaada ya kibinadamu.


“Katika kutambua hilo, Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza alimtunuku medali ya heshima ya kuwa Commander of the Civil Division of the Most Excellent Order of the British Empire (KBE),” ilieleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, wakati akitoa maoni ya tuzo hiyo alisema anashangilia kushuhudia Mtanzania aliyestahili kutunukiwa ‘Order of Knighthood in the British Empire’.

Familia yake pia imesema Chande aliwahi kupewa tuzo ya heshima ya Pravasi Bharatiya Samman kutoka kwa Rais wa India ambayo inatambulika kwa kiasi kikubwa nchini India kama mwanachama wa Diaspora.

Mwaka 2004, Chande alichapisha hotuba zake pamoja na mafundisho na habari kuhusu Freemason katika kitabu kinachoitwa Whither Directing Your Course na mwaka 2011 alichapisha kitabu kingine cha Transitions of a Life na kingine  ‘A Knight in Africa: Journey From Bukene.

Vitabu vyake viligusa maeneo mbalimbali ikiwemo historia, biashara, mazingira, elimu na mambo ya kijamii.

Taarifa hiyo ya familia pia imeelezea namna Sir Chande alivyoshiriki katika harakati za ukombozi na uhuru nchini.

Inaelezwa uzalendo wa Sir Chande katika taifa kwa mara ya kwanza ulijitokeza mwaka 1967 katika harakati za maazimio ya Arusha wakati wa biashara ya familia yake, kiwanda cha Chande Industries Limited kilitaifishwa kwa Serikali Februari 7, 1967.

Hayati Mwalimu Nyerere alimwalika Chande kusaidia kuanzishwa kwa Shirikisho la viwanda vya kusaga na kuchakata (National Milling companies).

Alikubali kwa uaminifu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa National Milling Corporation kwa miaka mitano, baada ya kustaafu alitumikia kama mshauri wa Bodi ya Wakurugenzi.

Kati ya mwaka 1958 hadi 1961 kabla ya uhuru wa Tanzania, Sir Chande inaelezwa alitumikia katika nafasi ya mwanachama wa Legislative Council (LEGICO ).

Mwaka 1959, alipata nafasi ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Katibu Mkuu wa Serikali ya Uingereza, Ian McLeod, kuhusiana na mapendekezo ya Uingereza kutoa uhuru wa kujitawala kwa Tanganyika.

Baada ya uhuru, Chande inaelezwa alishiriki katika shughuli mbalimbali nchini hasa za kijamii na kiuchumi.

Kwa nyakati tofauti aliwahi kuwa Mwenyekiti au kama mwanachama wa Bodi ya Wakurugenzi wa makampuni kadhaa ya umma na binafsi ikiwa ni pamoja na Benki ya Barclays Tanzania na Uganda na pia mashirika mbalimbali ya Serikali ikiwa ni pamoja na Shirika la Reli la Afrika Mashariki na East African Harbors Corporation.

Kufuatia kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, Sir Chande, aliteuliwa kuwa mwanzilishi na Mwenyekiti wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na baadaye Mwenyekiti wa Mamlaka ya Bandari Tanzania na wa Tanzania Railways Corporation.

Inaelezwa pia Chande alikuwa anajishughulisha na masuala ya kisiasa na kidiplomasia, wakati mmoja aliwahi kuwa mshauri wa Wizara ya Kamati ya Umoja wa Afrika ambayo inashughulikia masuala ya migogoro ya mafuta nchi za Waarabu.

Nyumbani kwake Masaki

Mazingira ya nyumbani kwa Sir Chande,  Masaki hayaonyeshi eneo hilo kama kuna tukio lolote kubwa kutokana na ukimya uliokuwepo jana.

Mwandishi wa gazeti hili ambaye alifika nyumbani hapo mchana, alishuhudia wana ndugu wachache pamoja na watoto waliokuwa ndani.

Ndani ya nyumba hiyo kulikuwa na waombolezaji wapatao watano waliokuwa wakionekana sebuleni huku baadhi ya wana ndugu wakitajwa kuwa eneo la juu la nyumba hiyo wakiendelea na kikao cha kupanga taratibu za mazishi.

Sir Chande alizaliwa Mei 7, mwaka 1928 nchini Mombasa, Kenya ameacha mjane Jayalaxmi na watoto watatu.



Hatua kwa hatua atakavyochomwa

Baada ya mwili wa marehemu kuingia ndani ya jengo lakuchomea maiti, Wahindi huvunja nazi tatu katika kaburi lililo karibu kabisa na lango kuu.

Baada ya hapo mwili huletwa katika tanuru lenyewe na hupangwa kuni juu ya tanuru hilo ambalo limeundwa mithili ya kitanda cha chuma.

Kuni hupangwa kwa ustadi mkubwa na zile za ukubwa kiasi hupangwa katika umbile la reli na magogo makubwa manne hupangwa kushoto, kulia Magharibi na Mashariki ya tanuru hilo ambapo kuni zinakuwa nyingi.

Kabla ya kuchoma maiti


Kabla ya kuuweka mwili katika tanuru huuzungusha mara nne kulizunguka tanuru hilo.

Baada ya hapo, mwili wa marehemu ukiwa na sanda huwekwa katikati ya kuni hizo, kichwa kikielekezwa Magharibi.

Kabla ya uchomaji wenyewe kuanza, mila za Wahindu hutaka kuhakikisha iwapo kweli ndugu yao amefariki. 

Ndugu mmoja wa marehemu hutakiwa kuhakiki kwa kuchukua kipande kidogo cha kuni chembamba kilichoshika moto, kisha humchoma marehemu katika unyayo mara nne huku akilizunguka tanuru.

Hatua inayofuata ni kuchukua moto kwa kutumia makoleo maalumu, kisha kuuchanganya moto huo na mafuta ya samli.

Mwili wa marehemu hupakwa mafuta ya samli kuanzia usoni mpaka miguuni kabla ya kuwasha moto, baada ya hapo moto huwashwa na unakuwa moto mkali zaidi ya gesi.

Mafuta ya samli pamoja na mafuta ya marehemu mwenyewe husaidia moto kuwa mkali kuliko kawaida.


Wakati moto unaendelea kuwaka kwa kasi, mbegu za ufuta hurushwa juu ya mwili unaoendelea kuungua na ndugu za marehemu ambao wanakuwa wamelizunguka tanuru.

Uchomaji mwili kawaida kuchukuwa saa mbili au mbili na nusu kumalizika au kuteketea kabisa.

Baada ya mwili kuungua na kwisha kabisa, kinachotakiwa kubaki ni vipande vya mifupa, lakini wakati mwingine moto huweza kwisha kabisa na wakati huo mwili bado haujamalizika.

Baada ya mwili kuchomwa na kwisha, ndugu mmoja wa marehemu huchukua chungu maalumu kilichojazwa maji na kukiweka katikati ya miguu, kisha anatakiwa kutazama Magharibi akiyapa kisogo mabaki ya mwili huo wakati huo waombolezaji wote wanageuka pia.

Anachofanya ndugu huyo wa marehemu akiwa amesimama ni kuchukua jiwe na kukipiga chungu hicho kwa nguvu hadi kivunjike na maji yamwagike kuelekea lilipo tanuru.

Baada ya tukio hilo yeye pamoja na umati wote wa waombolezaji hutakiwa kuondoka bila kugeuka nyuma.

Kwa upande mwingine baada ya mwili kuchomwa na moto kumalizika kabisa, mabaki ya mwili hutolewa kama vipande vya mifupa ya mwili na fuvu, vilivyochanganyika na majivu na mkaa kutoka tanuruni.

Mifupa hiyo huwekwa katika mifuko maalumu na hatua ya mwisho ni ndugu kwenda kuyatupa baharini.

Ukweli Mchungu..Ununuzi wa Ndege Nyingine Mpya: Serikali Iwe Wazi Vinginevyo Tunaweza Kulia na Kurudia Yale ya Richmond...!!!

$
0
0

Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia na mashaka ya aina hii yataendelea kujitokeza kila siku.

----
Patriote said,
Kuna taarifa mitandaoni kuwa ndege tajwa hapo juu ambayo tanzania ineshajicommit kuinunua inaweza kununulika kwa bei ya chini tofauti na ilivyoeleza. Katika taarifa ya ununuzi wa ndege hiyo, Tulielezwa kuwa ndege tunayonunua ina thamani ya USD 224.6 Mil sawa na TZS (482.89bn/-) kulingana na rate ya dollar ya wakati huo wakati Serikali inaseal deal na Boeing.

Ukiangalia kwenye mtandao wa Boeing (Boeing: 787 Dreamliner to become part of Air Tanzania fleet). Hela tunayolipia kunnua ndege hiyo haipo wazi sana mana imesema Tanzania inanunua ndege hiyo ambayo thamani yake kwenye price lists za Boeing inaonyesha ni USD 224.6 Mil. It says "Boeing and the United Republic of Tanzania have confirmed an order for one 787-8 Dreamliner, valued at $224.6 million at list prices". 

Naimani watu wa Boeing wanajua sana English, sijaelewa kwanini wameshindwa kuelezea bayana kabisa kuwa Tanzania imenunua ndege hiyo kwa bei fulani. Ieleweke pia kuoneshwa kwa bei fulani kwenye pricelist ya supplier haimaanishi ndio final proce utayonunulia bidhaa hiyo mana kwenye biashara kuna kuburgain/kuombe upewe discount. Na kwenye ununuzi wa kitu kama ndege ndio kuna mambo mengi zaidi mana unaweza hata kuicustomize ndege unatotaka kununua ikawa tofauti na nyingine kwa either kuwa more luxurious or kuwa more economic/basic au ukaburgain kununua bei iliyododa kwa bei rahisi kama walivyofanya wenzetu.

Wakati hali ikiwa hivyo toka Boeing's website, taarifa nyingine zinaeleza kuwa Kampuni hiyo ilikuwa ina ndege aina hiyo hiyo Boeing 787-8 Dreamliner ambazo zilikuwa zimedoda (Zilikosa wanunuzi kwa miaka kadhaa kutokana na kuwa nzito zaidi ya kawaida). Ndege hizo zilizododa zinatambulika kama "Terrible Teens" na kwenye pricelists ya Boeing hao hao inaonyesha ni around USD 224. Mil, ila kwa kuwa zimedoda taarifa kutoka vyanzo vingine zinasema kuwa ndege hizo zinauzwa kwa nusu bei yaani around USD 115 Mil. Nchi ya Ethiopia ni moja kati ya wateja waliokwisha kununua "Terrible Teens" kwa bei ya punguzo (half price). "Ethiopian Airlines is in advanced discussions to buy eight of the early-build 787s (Terrible Teens), said four people who asked not to be identified because they weren’t authorized to speak publicly".

Vilevile, taarifa zaidi zinasema kuwa Boeing inakiri kupata mteja atayenunua Terrible teen iliyobakia ila inakataa kuweka wazi taarifa na jina la mteja wa mwisho anayeinunua hiyo terrible teen ilobakia. Ilichofanya Boeing iliweka information za wadau wawili kuwa ndio watanunua hiyo ndege moja ilobakia.( http://www.bizjournals.com/seattle/news/2016/12/12/tanzania-orders-a-new-boeing-787-8-dreamliner-to.html).

Kulingana na maelezo yangu hapo juu maswali yafuatayo yanahitaji majibu.

1. Tanzania imeweka order ya kununua ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner . Je ndege tunayonunua ni moja kati ya Terrible Teens???

2. Kama tunanunua Boeing 787-8 Dreamliner ambayo ni moja kati ya Terrible Teens, Je tunanunua kwa USD ngapi??? Kwa taarifa zilizopo tumeambiwa thamani ya ndege hiyo ni USD 224.6 Mil. Nimepekua maeneo mengi haipowazi kwa kweli kama tutatoa hiyo hela kama ilivyo kwenye pricelist au na sisi tutanunua kwa bei ya punguzo au lah?? Hapa wabunge tunaomba mtueleze budget iliyotengwa kununua hii ndege ni USD ngapi

3. Kama tunanunu moja kati ya Terrible Teens, kwanini tumechagua kufufua shirika letu la ndege kwa kutumia ndege ambazo zimekuwa challenged na mashirika ya ndege yenye uzoefu mkubwa na yenye wataalam waliobobea wa kuassess ubora wa ndege?? Yaani motivation yetu ni nini katika kununua moja kati ya Terrible Teens?

4. Kwanini Shirika la Boeing limeshindwa kuweka wazi details za mteja anayenunua Terrible teen iliyobakia??? Je kuna connection kati ya kutoweka wazi jina la mteja huyo na Order ya Tanzania?? Ikumbukwe kwamba Boeing liliingiza order details za unidentied buyer katika kipindi hicho hicho ambacho wameingia mkataba wa Ununuzi na Tanzania. Check hii site (Magufuli holds talks with top Boeing official)

Toa maoni yako kulingana na hii mada. Unaweza kujiridhisha kwa kusoma taarifa kwenye mitandao mbalimbali mana hizi ndege zimeleta mijadala sana katika anga za kimataifa.

Kimenukaaa..Askofu Gwajima Kumshughulikia Halima Mdee..Ni Baada ya Kumtukana Spika..Mtaka Afanye Haya Ili Wayamalize..!!!

$
0
0

Askofu Gwajima katika Ibada ya Jumapili amezungumzia vitu/watu watatu nchi Tanzania. 

Amezungumza kuhusu Diamond kumshambulia katika wimbo wake, na amesema mtu wa Mungu huwa hashambuliwi na binadamu. Amedai kuwa atazungumzia kuhusu Diamond kujiunga Chama cha Freemason na alijiunga lini, wapi na kafara gani alitoa ili aweze kukubaliwa kujiunga. Mchungaji Gwajima alishusha pumzi na kusema hatamoiga Diamond baada ya Diamond kujirudi na kumuomba msamaha Askofu Gwajima. Mchungaji Gwajima ameinukuu Biblia na kusema inakataza kumchapa/kumpiga mtu aliyeomba msamaha.

Kuhusu Makonda, Askofu Gwajima amesema Bashite anahusika kwa utekaji wa Msanii Roma, amesema mtu huyo huyo aliyevamia kituo cha Habari Clouds Media ndiye huyo huyo mtekaji kwasababu ana mtu wa kumkingia kifua. Pia amemtaka Bashite akajifiche huko kwenye Balozi kama Congo na kwingineko ili akajiendeleze na Elimu ya QT au MEMKWA maana akibako hapa Tanzania watu watamgawana akiingia mtaani.

Askofu Gwajima kuhusu Halima Mdee kumtukana Spika wa Bunge la Jamhuri, amemtaka Mbunge Halima Mdee kuacha mara moja kumtukana Spika maana ni moja ya Mhimili wa Dola. Amesema kuwa Halima Mdee asipoomba msamaha basi Jumapili ijayo atamchapa ipasavyo.

Hatareee..Askofu Gwajima Afichua Jinsi Diamond Alivyojiunga na Freemason ,Ataja Aina ya Kafara Aliyoitoa Ili Afanikiwe..!!!

$
0
0

Askofu Gwajima katika Ibada ya Jumapili amezungumzia vitu/watu watatu nchi Tanzania. 

Amezungumza kuhusu Diamond kumshambulia katika wimbo wake, na amesema mtu wa Mungu huwa hashambuliwi na binadamu. Amedai kuwa atazungumzia kuhusu Diamond kujiunga Chama cha Freemason na alijiunga lini, wapi na kafara gani alitoa ili aweze kukubaliwa kujiunga. Mchungaji Gwajima alishusha pumzi na kusema hatamoiga Diamond baada ya Diamond kujirudi na kumuomba msamaha Askofu Gwajima. Mchungaji Gwajima ameinukuu Biblia na kusema inakataza kumchapa/kumpiga mtu aliyeomba msamaha.

Nape Nnauye: Sakata la Roma ni Picha la Kichina..!!!

$
0
0

Kupitia ukurasa wake twitter Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh Nape Nnauye ameweka wazi kuwa sakata zima la kutwekwa na kupatikana kwa Msanii maarufu wa nyimbo za kufoka foka Roma Mkatoliki ni picha la kichina ambalo limetengenezwa kwa makusudi maalum.

Ukijaribu kusoma Caption ya tweet hiyo unaweza kupata jibu la swali ambalo watu wengi wamekuwa wakijiuliza kutokana na kauli ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyosema kuwa "Roma atapatikana kabla ya siku fulani"


Hivi Jamani Mnamuelewa Huyu Diamond Kweli..Tazama Post Aliyopost Tena Leo..Kisha Dondosha Maoni Yako Hapo Chini..!!!

Rasmi..Maalim Seif Amvua Nguo Prof Lipumba Mchana Kweupeee..Aanika Madudu Anayoyafanya Akishirikiana na CCM..Atoa Tamko Hili..!!

$
0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama hicho kitaendelea kufanya mambo kiungwana kwa kuwa Tanzania ni nchi ya amani na kuwa hakuna CUF ya Maalim Seif wala CUF ya Lipumba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Maalim Seif alisema CUF inatimiza wajibu wa kutunza amani na iwapo kingetaka kuleta machafuko basi kingefanya hivyo tangu zamani.

“CUF ni moja. Ni kweli sisi tumekuwa wapole na waungwana, sisi si tunaambiwa hii nchi ya amani, sisi tunatimiza wajibu wetu wa kutunza amani. Hakuna chama kinachotunza amani kama CUF” alijibu mara baada ya kuulizwa na waandishi wa habari.

 “The struggle we continue, mtatia ndani Maalim Seif, mtatia ndani Mtatiro lakini there are so many Maalim Seif’s. Kuna Maalim wengine ni vichaa,” alisema

Wakati huhuo Maalim Seif aionyooshea kidole Rita

Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad amezungumza na waandishi wa habari leo na kusema  Wakala wa Usajili wa vizazi na vifo, (RITA) utakuwa umekiuka sheria iwapo utaisajili  na kuitambua bodi  ya wadhamini iliyoundwa na Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba.

 “Sisi tumekuwa wapole sana, tunaona katiba inavunjwa, lakini niseme kwamba, kama Rita wataisajili bodi ya Lipumba, watakuwa wamekiuka sheria yao wenyewe. Bodi ipo na imesajiliwa 1993 na tunacho cheti cha kusajiliwa” alisema

 Alisema ni utaratibu kuwa kila kipindi fulani marekebisho hufanywa lakini bodi haifi.

Alisema bodi ya CUF ipo na kama ofisa Mtendaji mkuu wa Rita ataisajili basi ajue anavunja sheria.

Breaking News...Panya Road Warudi Dar Kwa Kasi ya Kimbunga..Wateka Gari la Harusi na Kufanya Unyama wa Kutisha..!!!!

$
0
0

Kimenuka maeneo ya mzinga Kongowe jijini Dar es Salaam vijana wahuni almaruuf kama panya rod wanafanya yao wameteka gari ilokua na msafara wa harusi na kuwajeruhi baadhi ya watu waliomo...

Taarifa zaidi na picha znakuja mda si mrefu

JACK Wolper Amshukuru Mungu Kwa Kutuletea Paul Makonda na Mwakyembe

$
0
0

Pande mbili zaendelea kuvutana huko Bongo Movies huku wengine wakiongozwa na Wema Sepetu wakirusha madongo kwa wanao support harakati za RC kupiga marufuku filamu za nje Dar, Leo Jack Wolper amerudi tena na kuandika haya:

By @wolperstylish
"MUSA AKAULIZA AKASEMA U NANI WEWE? MUNGU AKAJIBU AKASEMA MIMI NI JEHOVA NIKO AMBAYE NIKO NAKUTUMA SASA NENDA KWA FARAO UKAMWAMBIE AWAACHIE WATU WANGU.HALIKUWA JAMBO RAHISI KWA MUSA MAANA ALIUJUA MOYO WA FARAO KWA ZAIDI YA MIAKA 40 THANKS GOD KWA KUTULETEA MSETO HUU WA MH.MAKONDA NA WAZIRI WETU MH.MWAKYEMBE TUNAAMINI UMEWATUMA KAMA ULIVYOMTUMA MUSA KWA FARAO TAJIRI MWENYE KIBURI MWENYE MOYO MGUMU NA MAMLAKA ZISIZOWEZEKANA LAKINI UKAWEKA NENO LAKO NDANI YA MUSA NA WANA WA ISRAEL WAKASHUHUDIA FARAO NA JESHI LAKE WAKIFA KATIKA BAHARI YA SHAMU HUKU WAO WAKIWA NG'AMBO YA PILI AMBAPO MUNGU ALIWAVUSHA. SISI BONGO MOVIE TUNAAMINI MH.MAKONDA NA MH.MWAKYEMBE WATATUVUSHA NG'AMBO YA PILI SALAMA." Wolper
.

TOA MAONI YAKO HAPA

Mambo 15 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda - Mtizamo Kutoka Kwa Wanawake

$
0
0

Hebu tuseme ukweli, kuna wakati mwingine ambao wanaume wanashindwa kuwaelewa wanawake. Unaweza ukamwaproach mwanamke huku ukijua wazi hutatoboa lakini unashangazwa mwanamke kama huyo anakukubali fasta.

Na wakati mwingine utaapproach mwanamke ambaye unaamini kuwa ni rahisi kabisa kumtongoza lakini ukirusha nyavu badala ya kushika samaki inanasa mawe (sitaki kusema kinachotokea wakati mwanamke anakuzima mbele ya hadhira)

...halafu sasa kuna wale marafiki zetu ambao kila wakati wao wakitongoza wanakataliwa. (inauma sana)

Well, usitie shaka tena coz hivi karibuni kama Nesi Mapenzi tumekuwa tukitafiti kwa kuuliza wanawake ni mambo gani ambayo yanawavutia sana kutoka kwa wanaume na mambo ambayo yanaweza kuwafanya wafall in love na wanaume na haya ndio mambo ambayo waliyazungumzia sana:

#1 Kuvalia nadhifu
Kulingana na wanawake ni kuwa mwanaume anapaswa kuvalia nadhifu kila wakati. Hii ni muhimu kwa mwanaume kwa kuwa huwezi kujua ni wapi au lini unaweza kukutana na mwanamke wa ndoto yako. Ni jambo muhimu la kuzingatia lakini masikitiko ni kuwa ni wanaume wachache ambao huwa wanaona umuhimu ikija katika hili swala. Ok. ni hivi, kuanzia sasa hadi milele hakikisha kuwa unavalia kisafi na kinadhifu wakati wote, jipulize marashi na utumie bidhaa zote za wanaume ambazo zitakupamba.

#2 Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La. Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe. Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.

#3 Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua kuzungumza maneno ya kunata. Upo? [Soma: Mbinu za kufuata uonyeshe kuwa una ushawishi]

#4 Mwili mzuri/shepu
Kama vile ambavyo ungependa mwanamke mwenye shepu na figa, pia wanawake wanapenda wanaume wenye shepu. So utafanyaje kama wewe una shepu la duara? Ingia gym, fanya mazoezi ya kukimbia angalau dakika 30 kila siku. Hii itakufanya uwe na toni nzuri kwa mwili wako. Si mimi ndio nimesema hivi, ni maneno kutoka vinywa vya wanawake. Anza mazoezi pindi utakapomaliza kusoma hii post.

#5 Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye. Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha. Usijilazimishe kama wewe si mcheshi. Mwanamke anaweza kucheka kwa mizaha ambayo hata haichekeshi kama umemsoma mambo anayoyapenda.

#6 Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti. Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa una haki ya kupaza sauti yako usikike  balada ya kukasirika ama kusinyaa.

#7 Kazi nzuri na hela ndefu
Ok. Haya si maoni yangu. Ni mambo ambayo yametamkwa kutoka kwa vinywa vya wanawake. Lakini ngoja tuseme ukweli...pesa ni muhimu ikija katika maswala ya mapenzi. Ni hivi! Wewe hupenda wanawake warembo zaidi kuliko wanawake wabovu. Kweli? Hivyo hivyo wanawake hupenda wanaume ambao ni matajiri zaidi kuwaliko wale maskini. Kuwa tajiri na kuendesha gari la kifahari ni advantage kwako (usitie wasiwasi, haya ni maoni ya wanawake tu. hapa Nesi Mapenzi tushalizungumzia tatizo hili mara kwa mara, pesa si muhimu katika kutongoza, ushapu wako ndio muhimu)

#8 Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila mtu. Tumeelewana?

#9 Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi yalivyo ulimwenguni. [Soma: Hatua za kujiamini]

#10 Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo  ni muhimu na yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa kumchumbia au la.

#11 Mwanaume anayejua kuzungumza
Kama tu vile kujua jinsi ya kutumia ucheshi katika mazungumzo yako, kujua jinsi ya kuzungumza na mwanamke kwa kutumia Sanaa ya Mazungumzo kama vile banta, miondoko ya mwili na kuchanganya Programu ya Isimu Ubongo ni muhimu zaidi kwa kuwa kutamfanya mwanamke kujiskia huru zaidi akiwa na wewe na ni mambo ambayo mwanamke anatamani kutoka kwa mwanaume yeyote. Sanaa zote hizi ziko kwa kitabu cha Kutongoza Mwanamke: Kuanzia Hadharani Hadi Kitandani

#12 Tabia ya kuheshimu
Kuwa na tabia ya kuheshimu wengine vile inavyotakikana. Wanawake wote wazuri hawawapendi wanaume ambao wanapenda kuwachukulia vibaya wengine. Usiwe mbaya kwa watu walioko chini yako bila ya kuwa na sababu yeyote. Ukiheshimu wengine nao pia watakuheshimu. Wanawake huwaona wanaume wenye tabia ya kuwaheshimu wengine kuwa wanaweza kuwa wazazi wazuri. So hakikisha kuwa unatabia nzuri wakati wote.

#13 Kuwa mwanaume alpha
Wanawake wazuri huwa kwa mikono mwa wanaume bora. Hakuna mwanamke atataka kuwa na mwanaume mwoga, asiyejiamini, asiyeheshimu wengine. Itakuwa ushawahi kugundua kitu flani, kwa kawaida huwa kuna mwanaume mmoja katika kikundi flani ambapo yeye anadeti wanawake warembo zaidi ilhali wenzake wanadeti wanawake wa kawaida. Wanaume kama hawa ndio huitwa alpha. [Soma: Hatua za kujijeuza Alpha]

#14 Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha, ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.

#15 Mwanaume mwenye usambamba/ compatibility
Ok. Tatizo kuu linajitokeza hapa. Mara nyingi mwanaume anaweza kumpendeza mwanamke kwa kila kitu lakini mwanamke anaweza asikubali mwitikio wako kwa kuwa hamna uwiano ulio sawa. Mwanamke anaweza kukukataa kwa sababu zake binafsi. Kama unataka kufanikiwa na hili basi hakikisha kuwa unakuwa mkweli, makinika na interests zake na usome mambo anayopenda na kuchukia. Kama ataona kuwa kuna uwiano ndani yenu, basi ni rahisi kwa yeye kukukubali.

Mwisho ni kuwa haya ni maoni ambayo yametoka kwa vinywa vya wanawake, hivyo kama kuna moja kati ya haya maoni 15 tuliyoyaorodhesha unayakosa, basi ni muhimu uanze kazi sasa hivi.

Mafanikio Kwako.
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images