Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live

Jinsi ya Kupunguza Mwili, Kupunguza Tumbo na Kuufanya Mwili Uwe na Shepu...!!!

0
0

kila mtu huwa anajiuliza ni jinsi gani ya kuondoa mafuta tumboni, iwe tumbo ni la kati au ni kitambi kimejitokeza. Kwa mwili mnene wenye mafuta mengi ni vigumu kuona matokeo mazuri ya kuridhisha kwa kufanya mazoezi pekee, maana asilimia hamsini ya mafuta mwilini huifadhiwa chini ya ngozi, na kiasi kingine kilicho baki huwa ndani ya misuli. Kufanya mazoezi ya mwili pekee hakuwezi kuondoa mafuta hayo mwilini.

Mtu mnene akifanya mazoezi ya kuvuta tumbo hawezi kuona matokeo, hata kama akirudia mazoezi hayo mara mamia kwa siku, kitakachotokea ni kweli ataimalisha misuli yake ya tumbo ila  hatoweza kuona matokeo hayo kwa sababu tumbo bado litakuwa limezungukwa na mafuta.

JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA

Kuna usemi unaosema, kwa matokeo ya mazoezi unahitaji.. “ASILIMIA 70 DAYATI, ASILIMIA 30 ZOEZI!”. Kwa matokeo mazuri na ya haraka njia hii hutoa matokeo mazuri Zaidi tofauti na kupiga mazoezi pekee ambapo ni kweli unaweza kuwa unaumguza mafuta mwilini ila hauwezi kuunguza mafuta yakutosheleza kwa siku kuweza kuonyesha matokeo mazuri ya mazoezi unayopiga.

Ila kwa njia ambayo itakupa matokeo ya muda mrefu maara nyingi huwa ni ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu, na matokeo haya nayaita ya muda mrefu maana mazoezi hayo yatakufanya uwe na adabu ya kubadilisha mwenendo wa maisha yako na kuutunza mwili wako kwa heshima.

Njia ya 70 kwa 30 inatoa matokeo mazuri maana asilimia 70 ya upunguaji wa mafuta mwilini hufanywa na dayati ya kuangalia nini cha kula na kipi cha kuondoa kabisa kwenye mlo wako wa kila siku. Hata hivyo kwa kuangalia dayati pekee haiwezi kukupa matokeo mazuri, maana tafiti mbali mbali za kisayansi juu ya kupunguza mafuta mwilini zimeonyesha huwezi kupunguza mafuta mwilini kwa dayati pekee na kupata mwili wa kuvutia pasipo kufanya aina yeyote ya mazoezi ya mwili, ukitaka mwili uliopungua kwa mpangilio na mvuto lazima uhusishe pia mazoezi ya mwili.

Njia kuu ya kupunguza mafuta kwa njia ya dayati ni kupangilia milo yako ya siku, iwapo ukitaka kujua ni chakula gani kitakachokupa matokeo mazuri

Lazima ujue mlo wako utaupangilia katika hali gani, kwa mfano badala ya kula ovyo hovyo, unatakiwa upangilie milo yako kwa kula kiasi, kama umezoea kujaza tumbo wakati wa kula, jaribu kushusha mlo wako uwe unakula kwa kuondoa njaa kwa kuupa mwili vile virutubisho unavyovihitaji tu, na unaweza kula milo mitatu mpaka mitano kwa siku na usizidishe zaidi ya hapo.

Hakikisha unakula mlo kamili ila kwa kuhakikisha huli vyakula vilivyotengenezwa kwa sukari, na zingatia kuachana na milo inayotayarishwa kwa haraka, (fast sood) kama chipsi, vitafunwa na vinginevyo vinavyohusiana na hivyo, zingatia kula vyakula vyenye protini na milo yako iwe kamili na hasa pendelea kula mboga mboga.

Kwa kuzingatia dayati na kwa kufanya mazoezi yanayohusisha kuchemsha mwili wako kwa kuongeza mapigo ya moyo zaidi utafanya mwili wako ubadilike na kupata matokeo unayo yahitaji, maana kwa kadri mwili wako unavyochemka ndivyo unavyozidi kuchoma mafuta mwilini, na kwa jinsi mwili wako unavyopunguza mafuta utafanya ngozi yako kukakamaa na kufanya mwili wako kupata shepu, kwa hiyo kitu cha kufanya ni kukazania mazoezi yanayoongeza mapigo ya moyo na kusababisha upumuaji wa haraka, fanya mazoezi hayo mara tano kwa wiki

Mazoezi yote unayofanya hakikisha yanahusisha sehemu zote za mwili kuanzia misuli ya mikono, nyonga, mgongo, mapaja, misuli ya chini ya miguu na sehemu zote za mwili kwa ujumla.

Breaking News: Simba Washinda Rufaa Dhidi ya Kagare Sugar

0
0

Simba wameshinda rufaa yao dhidi ya Kagera Sugar na wamepewa point tatu baada ya kuibainika mchezaji wa kagera Sugar Mohammed Fakhi alicheza mechi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano katika michezo dhidi ya Mbeya City, Majimaji, African Lyon hizo ndio mechi ambazo amepata kadi za njano😄😄

Polisi Wadaiwa Kuuawa kwa Risasi Kibiti..!!!

0
0

Polisi saba waliokuwa doria katika Kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, wanadaiwa kuuawa usiku huu kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo, lakini akasema taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Pwani.

Taarifa za uhakika zilizolifikia Mwananchi Digital zimeeleza kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Ukubali Ukatae...Ukweli wa Aliyoyasema Rais JPM Jana; Hili ni Mojawapo..!!!

0
0

Kuna kitu ambacho Rais amekuwa akikisema mara kwa mara na ninaamini kuna ukweli wake. Kwamba, siyo wote wanaolalamikia utawala wake wanafanya hivyo kwa sababu wanataka afanikiwe. Ni kweli pia kuwa wapo wanaolalamika kwa sababu wanafikiri kuna labda namna bora ya kufanya mambo fulani fulani. Lakini, kuna masuala ambayo anayafanya ambayo bila ya shaka Watanzania wako nyuma yake.

"Tulionewa sana
Tumechezewa sana
Tumedharauliwa mno"

Siku ya Krismasi ya mwaka juzi gari langu dogo la Nissan Maxima lilizimika kwenye eneo la kuegeshea magari hapo hapo kanisani. Bahati nzuri nyumba yangu ni dakika kumi tu kutembea kutoka kanisani. Kila namna ya kuliwasha tena haikuwezekana. Nilipowaita mafundi wakaniambia tu kuwa injini imekufa! Hakukuwa na jinsi isipokuwa kuweka injini nyingine!

Kuna ukweli kwamba wakati mwingine hata gari zuri kiasi gani inabidi ulipeleke kufanyiwa matengenezo ya kawaida. Lakini, kuna wakati gari linahitaji matengenezo makubwa. Katika kufanya matengezo makubwa gari linaweza kukongolewa kabisa, injini kushushwa, vilivyochakaa kutolewa, n.k Mtu yeyote atakayeliona gari likiwa kwenye matengenezo makubwa anaweza kudhania ndio mwisho wake; kwamba limeharibiwa. Lakini likiunganishwa tena na kuanza kazi linakuwa katika ubora zaidi kuliko wa awali. Sasa watu wakilalamika tu kusema kuwa gari limeharibiwa wanaweza kuwa sahihi kwa sababu wanaweka mkazo katika mwonekano likiwa kwenye matengenezo!

Kazi kubwa kwa Magufuli ni kuwafanya watu waamini kuwa analitengeneza gari hilo na kuwa matengenezo haya ni kwa ajili ya ubora wa baadaye. Na kwamba katika kufanya hili hatoonea huruma kuondoa visivyo faa na hata ikibidi kuishusha injini na kuweka injini nyingine. Katika matengenezo ambayo anaendelea kuyafanya Tanzania ambayo sisi wengine tuliyaita "mabadiliko ya kweli" na sasa naomba kupendekeza yaitwe pia "mabadiliko sahihi"kuna vitu ambayo anatakiwa kuendelea navyo na kuvifanya vizuri zaidi lakini kuna vingine ni lazima avifanye kama hivyo vingine vinatakiwa kufanikiwa.

Kufumua Idara ya Usalama wa Taifa ni moja ya mambo muhimu sana ya kuweza kufanikisha maeneo mengine yote. Mgonjwa wa moyo hata kama ana matatizo mengine ya mguu na meno; au hata kama ana matatizo ya tumbo; anaweza kuyashughulikia hayo mengine yote lakini bila kushughulikia tatizo kubwa la moyo mengine yanaweza kushughulikiwa lakini mwisho wa siku ni moyo utakaoamua kama hayo mengine yana nafasi ya kufanikiwa! Usalama wa Taifa ni moyo wa taifa! Hautakiwi hata kwa siku moja uonekane unapiga kwa matatizo, au una matatizo mengine...

Inshallah, wiki ijayo nitaendeleza hoja hii ya mabadiliko makubwa ya Idara. Tusisubiri watu wa nje watushunikishe kufanya mabadiliko. Baba wa Taifa alikuwa na msemo ambao wengi labda wameusahau (hii ilikuwa mara baada ya uhuru) kuwa "Tanzania ni ya Watanzania na Watanzania ni Wote - Tanzania is for Tanzanians and Tanzanians are All". Msemo huu ulikuwa unasisitiza tu kuwa hakuna mwenye Utanzania zaidi ya Watanzania wengine. Kila Mtanzania - haijalishi kabila, dini, rangi, uwezo, hadhi, mahali, hali au umbali - ana haki sawa na Mtanzania mwingine yeyote. Hakuna Mtanzania wa juu zaidi!

Kisa cha Mbuzi Wanaojichunga Wenyewe Dar, Mzee Anayewamiliki Asema Ukiiwaiba Utawarudisha Tu..!!

0
0

Kama wewe ni mtembezi mzuri wa jiji la Dar es Salaam, bila shaka umewahi kukutana na kundi la mbuzi wanaokatiza barabarani wao wenyewe bila mtu anayewachunga. 

Mbuzi hawa ni maarufu, huja mjini na kurudi wanakokaa bila kudhurika. Hakuna anayediriki kuwaiba wala kuwadhuru – waguse uone.

Mwandishi wa BBC Swahili, Humphrey Mgonja aliamua kuwafuatilia ili kubaini ukweli wa maisha yao, na aliyoyabaini, yatakuacha mdomo wazi.

“Wakifika barabarani hapo wanasimama kama vile binadamu, wanaangalia huku na huku wakiona gari hamna wanavuka, wana akili kuliko binadamu,” anasema mkazi mmoja wa Dar es Salaam.

“Wanavuka katikati ya zebra, mbuzi gani wa kuvuka katikati ya zebra kama binadamu?” Anahoji mwingine.

Kwa aliyewahi kutaka kuwafanyia hila mbuzi hao, cha moto alikiona.

“Aliwachukua Shoppers akawapeleka Vingunguti machinjioni, lakini kule hakufanikiwa hata kushika mbuzi mmoja, alichofanya ni kurudisha mbuzi hadi hapa Shoppers akainua gari lake, mbuzi wakaruka akaachana nao yeye akaamua kuondoka zake,” anasema Pascal Mshau aliyewahi kumshuhudia nduguye aliyejaribu kuwachukua.

Mwandishi Humphrey Mgonja aliwafuatilia mbuzi hao hadi usiku wa saa mbili walipoelekea kwenye makaburi ya Kinondoni ambako ndiko yalipo makazi yao. Mmiliki wa mbuzi hao, Mzee Omari amemwelezesha mwandishi huyo kuwa mbuzi wake hawaibiki.

“Hawa mbuzi huwa siwachungi, na wala huwa siwafungi, huwa nawaacha wanaenda kula wenyewe malishoni huko baada ya muda wanarudi wenyewe hapa nyumbani,” anasema mzee huyo.

“Sijawahi kuibiwa, na hata kama ataiba mtu, yeye mwenyewe atanirudishia tu, atarudisha mwenyewe,” anaongea kwa kujiamini.

Ukweli Mchungu..Anayewachukia Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar Afikirie Mara Mbili..!!!

0
0

Tokea dunia iumbwe na hata katika kufanya tafiti zangu kadhaa maeneo mbalimbali hasa zinazohusu viongozi wa kiafrika na tawala zao leo naomba tu niseme ukweli kuwa sijawahi kuona na kuvutiwa na aina ya uongozi mzuri kabisa wa hawa wawili Rais Dkt. Magufuli na Mkuu wake wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul C. Makonda.

Nadhani ifike muda sasa watanzania tuache kusikiliza maneno ya kimajungu, unafiki na uwongo tunayoaminishwa juu yao na ifike muda sasa kila mmoja wetu aonyeshe mapenzi yake ya dhati kabisa kwa Rais JPM na Mkuu wa Mkoa Makonda.

Kamwe chuki zetu ambazo zinaratibiwa kwa kiasi kikubwa sana na maadui wa nchi hii waliopo ndani na nje zisitufanye tukawachukia kiasi hiki hadi kufikia hatua ya kuwasema, kuwadhihaki na kuwahisi vibaya wakati pengine hata huo ushahidi labda hatuna.

Hivi kwa nchi kama yetu ya Tanzania iliyobarikiwa kabisa na Mwenyezi Mungu hadi akatupa hawa Viongozi wawili Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda na jinsi wanavyofanya kazi zao vizuri kabisa na kiueledi tukisema wewe au nyie ambao mnawadhihaki na kuwachukia kuwa pengine mna matatizo ya akili na mnahitaji kwenda kupimwa akili tutakuwa tunakosea?

Katika maisha yangu yote hadi sasa sijawahi kumpenda na kumkubali mtu hasa kiongozi halafu asiwe ni mzuri au anayefaa hivyo basi kupitia huu uzi wangu naomba kuanzia leo nyote mnaowaona akina Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda ni wabaya au hawafai basi badilisheni upesi hayo mawazo yenu kabla hamjamuudhi Mwenyezi Mungu kisha akawaondoa na nchi yenu ikawa kwa watu wengine wasiokuwa na hata chembe ya uchungu na Tanzania yetu.

Ewe Rais Magufuli na Mkuu wa Mkoa Makonda msiogope, fanyeni kazi na Mungu atawalinda na kuwabariki.

Waziri Nchemba Awasili Eneo Yalipotokea Mauaji ya Polisi Wanane..!!!

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewasili eneo yalipotokea mauaji ya askari wanane katika kijiji cha Jaribu, Wilayani Kibiti.

Waziri Nchemba ameambatana na naibu wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.

Nchemba atatembelea kambi za askari polisi wa kanda ya Pwani na katika kata ya Bungu wilayani Kibiti.

Alichokisema Rais Magufuli Baada ya Askari Nane Kuuawa Mkoani Pwani..!!!

0
0

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo. 

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu. 

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Kimenukaa..Jeshi la Polisi Latangaza Vita ..Lajiandaa Kuvamia Mkoa wa Pwani kijeshi Kupambana na Majambazi Walioua Askari..!!!

0
0

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi, Nsato Marijani ameongea na waandishi wa habari mchana huu na kutolea ufafanuzi tukio la mauaji ya Askari Polisi 8 lililotokea jana jioni huko Kibiti, Pwani.

CP Marijani ameeleza kuwa tukio hilo sio la kigaidi kama ambavyo imekuwa ikivumishwa, bali ni tukio la kawaida la ujambazi ambalo halililazimu Jeshi la Polisi kuunda Kanda Maalumu ya Kipolisi kwa Mkoa wa Pwani.

Aidha, amesisitiza kuwa, hilo ni tukio la kawaida na wala sio tukio la kutisha na kuzua hofu bali imetokea tu bahati mbaya mapolisi kuuawa na wao kama Jeshi Imara watazidisha mapambano na kudumisha ulinzi.

Mpaka sasa, wameshajibu mashambulizi yaliyowalaza chini majambazi 4 na idadi yao itaongeza kwa kuwa imeundwa operesheni maalumu ambayo haitokuwa na mzaha wala msamaha.

Nikimnukuu CP Nsato Marijani

"Ninasema wazi kwamba hiki ni kitendo ambacho hakikubaliki, mpaka sasa nimekwishapoteza askari zaidi ya kumi. Ninaamini wanatosha.

Kuanzia sasa jeshi linakwenda kwenye operesheni maalumu, hatutokuwa na mzaha wala msamaha, tutafanya kile ambacho Jeshi linapaswa kufanya.

Tutawafuata popote walipo, tutawashughulikia kikamilifu na hakuna ambaye atakayebaki. Na mapambano haya hayana mwisho, yaani huu ni mwanzo hayana mwisho. Askari 10 ni wengi sana.

Wananchi mtuwie radhi, mtuunge mkono. Katika hili mtaona sura halisi ya Jeshi la Polisi

Dawa ya moto ni moto, tuna uhakika tutawakamata, sasa hivi ni nane kwa nne lakini magoli yetu yatakuwa mengi kuliko wao.

Wale wote ambao walikuwa wanafikiria kufanya ujambazi wa aina hii wa kutumia silaha wajue kwamba dawa ya moto ni moto."

Majina ya Nyimbo Yamfikisha Msanii Polisi..!!!

0
0

Msanii kutoka Arusha chini ya Weusi kampuni, Bonta Maarifa amedai kuwa mara nyingi majina ya nyimbo zake huwa yanampa matatizo kutokana na kuwa na utata

Bonta amebainisha kuwa jina la wimbo 'Nauza kura yangu' ilimfanya akapelekwa kituo cha polisi kipindi akiwa mwanafunzi wa chuo cha Mzumbe.

Leo akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio wakati akitambulisha ngoma yake mpya ‘Zero', Bonta amesema kuwa majina ya nyimbo zake huwa yanaendana na matukio yanayoendelea kwenye jamii kitu ambacho alipotoa ‘Nauza kura yangu' ilionekana kama anashawishi wanafunzi wenzake kuuza kura kinyume na maadili ya uchaguzi.

“Watu huwa hawanielewi sana wanaposikia majina ya ngoma zangu mpaka wasikilize nyimbo na kuzielewa, Nakumbuka hili swali ambalo naulizwa leo kuna tukio liliwahi kutokea miaka ya nyuma nilipotoa Nauza kura yangu, maaskari walikuja kunikamata wakanipeleka polisi kwa kosa la uhamasisha wanafunzi Mzumbe wauze kura zao kumbe sivyo nilivyomaanisha mpaka baadaye kuna baadhi ya viongozi walikuwa wanaelewa kitu nachokifanya ndipo wakaja kunitolea dhamana” Alisema Bonta.

Hata hivyo Bonta ameongeza kuwa wimbo wake mpya unaitwa 'Zero, kwa kuwa unahamasisha serikali iboreshe miundombinu ya elimu ili kupunguza idadi ya wanafunzi  wanaofeli mashuleni na siyo tu kung’ang’ania madawati wakati waalimu wanafundisha wakiwa hawana ari.

"Unajua wanafunzi wanaofanya vizuri wanakimbilia udaktari na kazi zingine za heshima anayepata daraja dhaifu ndiyo anaenda kuwa mwalimu, lakini wakati huo hata ualimu wenyewe umlipe vizuri hakuna kitu kama hicho kwa mfumo wa elimu wa hapa nyumbani tusitegemee Zero zikawa chache kuliko Division 1 hivyo mimi nimeikumbusha serikali ikazie macho suala la elimu na siyo vinginevyo" Bonta.

Zitto Aandika Haya Kuhusiana Na Mauaji Ya Askari Saba..!!!

Korea Kaskazini Yasema Iko Tayari kwa Vita na Marekani..Wadai Watatumia Silaha Zao Zote Kali za Nyuklia na Makombora ya Masaafa Marefu..!!!

0
0

Hayo ni maneno ya uongozi wa Korea Kaskazini katika joto la wababe hawa linaloendelea kupanda kila kukicha.

"Tumejiandaa vizuri kwa chochote kitakachotoka kwa Marekani."

Haya yanatokea wakati Korea Kaskazini inajiandaa na tukio kubwa wanaloliita "day of the sun" na huenda na siku hiyo wakafanya majaribio ya silaha zao za nuclear. 

Baada ya Kudai Kuwa Anapokea Vitisho Vingi Juu ya Miasha Yake.Nay Ageukia Ufugaji wa Kuku!.

0
0

KUFUATIA mambo mengi kumtokea Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ tangu aachie wimbo wake wa Wapo, jamaa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Utakumbuka hivi karibuni NaY alielezea vitisho vya kuuawa anavyovipata kutoka kwa watu wasiojulikana ambao wanaonesha kutofurahishwa na tamko la Rais Dk. John Magufuli la kutaka aachiwe licha ya wimbo wake kuonekana una ukakasi.

Hata hivyo, kufuatia tukio hilo, dizaini kama jamaa ameamua kutojichanganya sana kitaa, badala yake inadaiwa na watu wake wa karibu kuwa, amekuwa akitulia nyumbani kwake akifanya shughuli za hapa na pale ikiwa ni pamoja na kufuga kuku wake wa kienyeji.

Kusikia hivyo, mapaparazi wetuwakamfungia safari hadi nyumbani kwake, Kimara Mwisho jijini Dar ambapo katika hali ya kushangaza, palikuwa pametawaliwa na ukimya ndipo baadaye ikabainika kuwa, watu aliokuwa anaishi nao akiwemo mama yake, wameondoka kwa hofu ya kufanyiziwa.

HUYU HAPA NAY Baada ya kubisha hodi kwa muda mrefu, alifi ka getini kijana mmoja ambaye kabla ya kufungua aliuliza maswali kibao ndipo alipokwenda kumuita baba mwenye nyumba (Nay).

Alipokuja Nay na kuona ni waandishi anaowafahamu akafungua. Akizungumzia maisha yake kwa sasa, msanii huyo alisema:

“Ni kweli hali yangu ya usalama haipo vizuri, sasa ili kujiepusha na mambo mengine inanilazimu kukaa nyumbani muda mwingi na kufanya shughuli kama hizi za kulisha kuku wangu, kuhudumia garden na shughuli nyingie ndogondogo.

“Kwa kifupi mimi ni mfugaji mzuri sana wa kuku wa kienyeji, ninao wengi na wamenizoea kwa kuwa ni wa kienyeji lakini nawalisha kizungu kama unavyoona.”

MAJAMBAZI Wanne Walioua Askari 8 Kibiti Wauawa, Msako Waendelea

0
0
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.


Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

“Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati,” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

WAZIRI Nchemba Awasili Eneo yalipotokea Mauaji ya Polisi Wanane

0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amewasili eneo yalipotokea mauaji ya askari wanane katika kijiji cha Jaribu, Wilayani Kibiti.

Waziri Nchemba ameambatana na naibu wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.

Nchemba atatembelea kambi za askari polisi wa kanda ya Pwani na katika kata ya Bungu wilayani Kibiti.
   

TRA Yabadili Mfumo Matumizi za EFDs

0
0
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanya mabadiliko katika mfumo wa usimamizi wa matumizi ya Mashine za kielektroniki za Utoaji risiti (EFDMS) ili kudhibiti uwezekano wa kughushi risiti.

Aidha, mfumo huo una usalama wa hali ya juu, kwani miamala na risiti zote zitakuwa na saini ya kielektroniki na “QR Code”, hivyo kupunguza uwezekano wa kughushi risiti kutoka kwenye mashine za kielektroniki ambazo hazijasajiliwa na mfumo wa mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kufungua semina ya Walipakodi Wakubwa, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA, Neema Mrema alisema mfumo huo ni wa kiintelijensia kwani una uwezo wa kutambua hati ya mauzo kwa mkopo, marejesho ya mauzo, risiti halali na durufu.

“Mfumo umezingatia kupunguza gharama, kwani mfumo huu ni wa Tehama ambao utaipunguzia gharama serikali kununua mashine halisi kwa kuwa umeunganishwa na seva ya TRA,” alisema Neema.

Alisema mfumo huo pia una ufanisi mkubwa na ni rafiki kwani unaweza kuunganishwa na mifumo mingine kama mifumo ya ankara, mauzo na stakabadhi mbalimbali kwa kufanya mabadiliko machache, pia unaruhusu matumizi ya fedha mbalimbali.

Semina hiyo ya siku moja imewakutanisha walipakodi wakubwa kwa ajili ya kupata elimu juu ya Sheria ya fedha ya mwaka 2016 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014.

Mada zingine zilizowasilishwa ni kodi ya zuio katika bidhaa na huduma, mfumo wa ukusanyaji wa maduhuli kwa kutumia mashine za kielektroniki za utoaji risiti (vitual EFD).

Akizungumzia kodi ya zuio, Neema alisema utekelezaji wa Kodi ya zuio iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2013 umekuwa na changamoto mbalimbali kwa idara na taasisi za serikali.

WANAUME Kiumbe Kilichokuwa Adimu Kinaelekea Kutoweka Duniani

0
0

Habari zenu Kuna Jambo linakera saana kutoka kwa wanaume wa siku hizi wamekuwa ni watu wasiojiongeza hata kidogo, Kuna mkaka alikuwa ananitaka kimapenzi ana kazi kubwa tuu ya kuheshimika sasa amekuwa ni mtu wa kupenda kubebwa kila ofa nimtoe, hajiongezi yaani yupo kama chuma ulete sijui ni ubahili au kutokujiongeza kiukweli naona kiumbe hiki adimu kinazidi kutoweka siku hadi siku Kuna haja ya serikali kukiweka makumbusho ya taifa, nakumbuka zamani mzazi akipata mtoto wa kiume anasema nimepata mkombozi, mrithi, jembe lkn siku hizi ni tofauti kabisaa wanaume wamekuwa wa mizinga, kupenda kulelewa mi nikikuona tuu najua Kuna hasara kichwani na huwezi kuiendesha familia kama baba...

Wanaume Suruali Siwataki..

By Queen of the Jungle

AJALI Mbaya Imetokea Maeneo ya Mbwewe na Manga Tanga..

0
0

Kuna ajali ya Gari imetokea kati ya Mbwewe na Manga Tanga kuhusisha RAV 4 no T 455 CLA ya kugongana na lori. Taarifa za awali zinasema kuna waliofariki na kujeruhiwa.. Mungu awalaze mahali pema Marehemu na kuwapa uponaji majeruhi.
Taarifa kamili itawajia baadae

Vitu 4 Ambavyo Vitakufanya upewe Mapenzi Zaidi na Mpenzi wako Wikiendi Hii....!!!

0
0

Watu wengi siku hizi huwa wanaanza kuiwaza wikiendi pale tu jua la jumatano linapokuwa linaanza kuzama.

Usije kuwalaunu watu hawa maana huwa ni kawaida.

Ni kawaida maana wikiendi ni siku ambazo watu wengi huweza kukutana na wawapendao bila kuwa na mashaka au mawazo mengine ya kiofisi au shughuli yoyote nyingine.

Mihangaiko na jinsi mambo yanavyokuwa bize kipindi hiki cha kiutandawazi na maendeleo ni vigumu mtu kuwaza mapenzi hasa katikati ya wiki.

Na huwa inatokea na ni mara nyingi wikiendi inafika ila unajikuta haupati mapenzi ya kutosha kama vile moyo wako unavyokuwa unatamani itokee, kwa wale ambao wangependa mambo mazuri ya kubomoa chaga za vitanda yatokee wikiendi hi, hizi hapa ni njia za kufata ili ufanikishe unayoyawaza.

1. Mnunulie mpenzi wako zawadi. Zawadi ni njia moja nzuri na inayoweza kukufanikishia mambo yako yakaenda utakavyo na kuvunja buyu la asali, tafuta zawadi nzuri ambayo unajua atapendezwa nayo, iwe gauni zuri au mkoba mzuri na mapenzi yaliyozidi kipimo yatakuwa yako mwisho wa wiki hii.

2. Mtoe mtoko sehemu nzuri. Wikiendi hii inaweza kuwa wakati mzuri wa kumtoa kwenye mtoko msichana wako, jaribu kutafuta sehemu nyingine tofauti na chumbani kwako na utaona mafanikio ambayo yatajitokeza, mkitumia siku mbili kwenye hoteli flani, mapenzi yatakuwa mengi kama vile mpo kwenye hanimuni, maana itakuwa kula, kunywa na mambo yetu yakifuata katika kipimo ukipendacho wewe kwa wikiendi nzima.

3. Umtaarishavyo vizuri kimahaba ndivyo utakavyo pewa mapenzi mengi na mazito zaidi. Je wewe ni kati ya wale wanaohisi mapenzi ni kitendo cha uume kuingia sehemu ya kike tu? Hapana, kitu cha kwanza unatakiwa umtengenezee hakshi ya mahaba, mpeti peti umfanye apate hamu kwa kumtaarisha kwa hali nzuri na kwa mitekenyo inayohitajika, mtayarishe bila haraka, mbusu mabusu ya hisia, mashavuni, kwenye midomo yake telemka taratibu mpaka apate raha duniani na mpe maneno matamu ya kumchanganya zaidi. Mambo yote haya ukiyafanya vizuri na ukamfanya apagawe hakika lazima na yeye atataka zaidi na wewe utapata yakutosha pia.

4. Mwachie Aongoze Mambo. Ukweli ni kwamba wanaume wengi huwa hujiangalia wao tu, hawataki kusikiliza japo hata kumuuliza mwenza wao naye angependelea nini, wanawake wanapenda sana akipewa nafasi ya kuamua ni spidi gani itumike mkiwa kitandani, kwa hio badala ya wewe kufanya bila kumuuliza mwenzio anataka nini na mfanye mapenzi kwa staili gani, mwachie nae aamue, mwambie hii siku ni ya kwake yeye, wewe kwake ni mtumwa tu, atatakacho upo kwa ajili ya kumtimizi, muulize umshike wapi na umfanye nini maruhani yake yapande, muulize angependelea kasi gani ya ufanyaji wa mapenzi, mnongoneze maneno matamu ya kumpagawisha. Kama akitaka yeye ndo awe juu, na wewe uwe chini mwache dada wa watu afanye yake, ajifikishe mwenyewe apendako na kama ni kileleni, haya! jinsi atapokuwa anasikia raha na kufurahi ndipo atakapo hitaji zaidi na wewe mwisho wa siku kupewa zaidi.

Na hapo mpaka wikiendi iishe lazima uwe mwepesi kama bendera

Njia 10 za kumfanya mwanamke akufukuzie na kukutaka baada ya kumuonyesha hisia...!!!

0
0

Huwa tunatumia mda mwingi sana hapa tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, na kadhalika.. Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea huwa ni kama theruji kwenye mlima kilimanjaro, ila volukano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia kumi za kuwa mkufunzi wa kiumeni na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.



Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.

Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.

Kitu kimoja wanaume wengi wanacho kiharibu na kupoteza nafasi yeyote ya kuwafanya mwanawake aanze kumfuatilia kwa kuharibu mambo tokea mwanzoni, ni pale mwanaume unapopata nafasi na kuanza 'aaahaa' na 'eeehee, si unajua.. aahaa', na kuonyesha tabia ya kutojiamini na kuwa na wasiwasi, tabia ambayo humfanya mwanamke asivutike tena na wewe, ukimuuliza mwanamke yeyote ni kitu gani anachovutiwa kwa mwanaume, cha kwanza atakuambia anapenda mwanaume anayejiamini.

Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa kutongoza toka moyoni bila hata kufikilia utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, "Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba", mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.

Namba 2. Muonyeshe changamoto.

Hili kiumeni tumeshaliongelea, mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha hana la kufanya zaidi ya kumlamba miguu, kama waswahili wasemavyo "Ukimwonyesha mwanamke unampenda sana, lazima atakusumbua", wanawake hawavutiki na mwanaume fala, mwanaume ambae anaweza kumpelekesha jinsi yeye anavyotaka, sasa atawezaje kukufatilia wakati havutiki na aina hio ya wanaume, tofauti na hapo anajua tu lazima mwenyewe utajipeleka.

Tokea binadamu kuumbwa, mwanamke huwa anapenda kitu ambacho hawezi kukipata, na hata kama akikipata na akajua kakipata lazima hamu ya kuwa nacho imwishie na kukitaka kingine ambacho hana uwezo nacho, ndivyo fikra na akili ya mwanamke ilivyo, umenielewa hapo jamaa?

Onyesha changamoto, mwonyeshe hutawaliwi na tamaa na huendeshwi na mapenzi, unamambo mengi ya kufanya, na kama una marafiki wa kike hakikisha anawajua, ili ajue kumpenda yeye ni uamuzi na sio lazima maana wapo wengi, muonyeshe wewe ni kati ya wale wanaume wachache kupatikana, mwanaume lijali ambaye wanawake wote wameumbwa kutoka kwenye ubavu wake mmoja tu kati ya mbavu nyingi alizonazo. Hivi haujawahi kuona mwanamke anampenda sana mwanaume halafu mwanaume hana hisia na huyo msichana, unajua msichana huwa anakuwaje?

Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.

Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika mkubwa ataendelea kukufikilia kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahio ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia.. huyo mwanamke ataanza kukufikilia kuwa utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huwo ndo utakuwa mwisho wako.

Kwahiyo ni vizuri ukaondoa kabisa maswali ya kuonyesha kama wewe ni mtu ambaye hujiamini, maswali kama "Kwa hio ni aina gani ya wanaume unaowapenda?", au "Vipi, hivi mie naendana na wewe?" baya zaidi ni "Hivi unamvulana?" Hivi unauliza anamvulana ili iweje, kama umevutika naye fanya yako kwanza, uhusiano ukiwa umejenga muhimili mwenyewe atajua sheria zinasemaje, tafadhali usijaribu maswali ya namna hii.

Namba 4. Usimfatilie sana.

Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubili na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja, uhusiano wa wewe kuumia na mawazo na kujipendekeza kwake kwa kumramba miguu na kumfanya yeye asikujali. Iwapo akiwa anakutarajia kuwa utafanya hivi hapo kutakuwa tena hakuna kipaumbele kwa upande wake, hakuna ile hali ya kumfanya akufatilie wewe na kukutaka, tofauti na hapo kumfata fata kunampa maana nyingine mwanamke ambae ndo kwanza ameanza kupata hisia kwako, kunampa maana kuwa amekutana tena na Fala mwingine.

Ukimwonyesha tabia ya kumuhitaji sana lazima atakuona wa kawaida usio na uzito wowote kwake, ila ukijionyesha wewe ni kiumbe ambae haupatikani kirahisi, kiumbe wa nadra ambae akikukosa maishani mwake lazima atakuja kujutia nafasi, kutamfanya akutake na kuanza kukufatilia kwa ukaribu maana tayari anakuwa ameshagundua anakuhitaji wewe na wewe ndie yule mwanaume lijari aliyekuwa anamsubiria, maana upo tofauti na wanaume wengine anaowapuuzia.

Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani.

Habari ya Mjini: Wanawake wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo haziitajiki, kumnunulia zawadi bila sababu, kwa hio acha kumnunulia zawadi bila sababu na kumpa sifa pale ambapo haziitajiki, sio kwamba kidogo tu kabadili pozi, tayari na wewe umeshamsifia, kabla siku haijaisha tayari umeshamsifia mara 100. Mwisho wa siku atakuona unamsifia sifia tu kumshika masikio bila kumaanisha chochote kile ukiongeacho, na juu ya zawadi atakuona unampa mpa zawadi ili kununua upendo wake na wala hauna mapenzi yeyote ya dhati kwake.

Badala yake mwambie ulikuwa unamfikilia leo au mwambie umemuota jana, ili ajuwe yupo akilini mwako unamfikilia badala ya kumpa sifa mpaka azione za kawaida, unavyomsifia mara chache ndo husuda yake ya kutaka kusifiwa na wewe inavyokuwa kubwa, ndivyo atakavyokuwa na tamaa ya kusikia maneno kutoka kwako.

Namba 6. Mwingie kwenye kichwa chake.

Kumfanya mwanamke awe anakufukuzia, inakubidi umfanye mwanamke awe anakufikilia badala ya wewe kuwa ndie unayemfikilia, na njia moja ya kufanya jambo hilo lifanikiwe kwa urahisi ni: Kataa au zipuuzie mialiko au vitendo unavyovipokea tokea kwa mwanamke, ukitaka ufanikiwe kwa uzuri zaidi fanya uonekane upo bize na sio mtu wa kupatikana kwa wepesi. Mwambie, "Aah, unataka tutoke ijumaa hii? Sijui. Kuna ishu nyingine inatokea siku hio na sidhani kama huyu msichana ataniruhusu nisifike".

 Fanya hivyi kwa usahihi na hatoweza kukutoa akilini mwake.

Namba 7. Mringishie

Hii hatua ina umuhimu wake, kumfanya mwanamke aanze kukufatilia lazima ugeuze baadhi ya mambo, hii nikimaanisha lazima ujiweke wewe uwe kama mchaguzi, na mwanamke anatakiwa ajionyeshe kuwa anafaa kuwa na wewe.

Ila inabidi ufanye hii hatua kwa kuzingatia usije ukaonekana kama unajiona, tafuta staili ya kuifanya, fanya maongezi ya kirahisi kama kumuuliza "Hivi ni nini kinachokutofautisha wewe na wasichana wengine niliokwisha kuwa nao kimahusiano?" au "Ni vitu gani vitatu ambavyo unauhakika mwanaume atavipenda kwako, na tafadhari usiniambie uzuri", Muulize hivi ukiwa kama vile unafanya maongezi ya kutania na huyo mwanamke ataanza kuvutiwa na wewe kwenye maongezi, na hii haina uchawi.

Na pia unaweza kuwa umemwahidi kitu ambacho unajua anakipenda ila ukatumia pia kumcheleweshea kumpa, ukawa unamtamanisha kwa maneno mazuri, hali hii inaongeza mvuto zaidi wa kukitaka hicho kitu na kuongeza mvuto zaidi juu yako ila kuwa mwangalifu asigunduwe unamringishia. 

Namba 8. Mfurahishe na Mchekeshe.

Kicheko ni kitu kilicho na nguvu sana kuuteka moyo wa msichana, na inabeba sababu ya kisayansi. Kumfanya mwanamke afurahie kuwa na wewe ni njia kuu ya kumfanya awe anafikiria kutumia muda wake na wewe na kukufikiria wewe pia.

Kwahiyo mfanye mwanamke achekelee na hata kama akiwa na msimamo kiasi gani, kibaiolojia atajikuta anavutika na wewe kwa sababu ya hisia nzuri anavyojisikia akiwa na wewe, hiyo hisia hawezi kuipuuzia zaidi ya kuendelea kukuwaza na kutaka kufahamu ulipo ili akufuatilie umpe tabasamu jingine.

Namba 9. Usionyeshe karata zako zote.

Hii njia ndio nayoipenda kupita njia zote ndani ya kiumeni.com kwa sababu ni njia rahisi na nzuri zaidi na inamfanya mwanamke afanye kazi zote, unachotakiwa kufanya ukikutana na mwanamke kwa siku ya kwanza usiwe kama redio, unatangaza matangazo yako yote, unaweza kuanza kufanya hivi kwa kutojitambulisha jina mpaka hapo atakapokuuliza jina lako, au kwa kumuwekea kichwani fikra ya "Labda." Mwambie "Sikia, natakiwa nirudi nikawape kampani rafiki zangu, labda ntaweza kukuona baadae."

Kwa njia hii kunamfanya asikutambue na akilini anabaki na labda, Labda ananitaka? labda kavutika nami? na siku zote mashaka na kutokujua ni njia moja nzuri sana ya kutengeneza mvuto. Ukimfanya apate zile hisia za kukutaka kukujua, zile hisia za mvuto wa kutaka kukufahamu, kutamfanya aanze kukufuatilia bila yeye kutokujua anafanya hivyo.

Namba 10. Acha kumfatilia.

Kama kila saa unashindwa kujizuia kumfatilia msichana, kutaka kujua anafanya nini, yupo wapi, kwa njia hiyo huwezi kufuzu kuwa na uwezo wa kumfanya msichana aanze kukufatilia wewe.

Kwa hiyo njia ya mwisho ni kuacha kumfatilia. Na hapo ndipo hiyo tabia ya kumfata fata mwanamke kama katoto kanyonyacho kinavyomlilia mama akiwa hayupo itakavyoisha. Utakuwa tofauti na wanaume wengine wanavyokuwa, wanawake watakuona mtu unaejiamini na kijua kile utakacho kutoka kwenye maisha yako mwenyewe na watavutika na wewe kwa mvuto wa mafanikio sio mvuto wa kupewa ahadi hewa. Anza kutengeneza tabia ambazo zinawavutia wanawake, tabia ambazo zitakuweka juu na kukufanya uwe kile mwanamke anachotamani kuwa nacho, tabia ambayo inampa mwanamke hamu ya kukutaka kukujua zaidi, kutaka kukufahamu, kutaka kukaa karibu yako, kutaka kukupa vitamu alivyonavyo ili mradi tu awe na wewe.
Viewing all 104432 articles
Browse latest View live




Latest Images