Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live

Yafahamu Mataifa Ambayo Hula Nyama ya Mbwa na Paka

$
0
0
Taiwan imepiga marufuku uuzaji na ulaji wa paka na mbwa kufuatia visa kadhaa vya ukatili dhidi ya wanyama na kuzua ghadhabu ya umma.

Sheria mpya ya kulinda wanyama imeweka adhabu ya faini pauni 6,500 kwa yule anayepatikana akiuza, kula au kununua nyama hiyo.Wanaopatikana wakiwadhulumu wanyama nao watapigwa faini ya Pauni 52,000 na miaka miwili gerezani.

Taiwan ndilo taifa la kwanza kuweka marufu hii Barani Asia.

Sheria mpya inanuia kukabili baadhi ya imani kuhusu ulaji mbwa. Kwa mfano kuna baadhi wanaamini kumla mbwa mweusi wakati wa msimu wa baridi kunamsaidia mtu kupata joto mwilini.

Sheria hii imeungwa mkono na Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen, ambaye ana mbwa watatu na paka wawili.

Ulaji wa paka na mbwa umeendelea kupungua wakati jamii ikibadilisha jinsi inavyoshughulikia wanyama wanaofugwa nyumbani. Shirika linalotetea mslahi ya wanyama ‘Humane Society International’, limetaja mataifa ambayo yana desturi ya kula mbwa na paka.

Haya ni pamoja,Thailand, Laos, Vietnam, Cambodia na jimbo la Nagaland nchini India. Aidha desturi hii iko katika nchi za China, Korea Kusini na Ufilipino.

CHINA

Licha ya kutokuwepo na takwimu rasmi, China inaaminika kuongoza duniani katika ulaji na uuzaji wa mbwa na paka. Kila mwaka karibu mbwa na paka milioni 10 wanaaminika kuchinjwa nchini China.

Shirika linalotetea maslahi ya wanyama linasema wanyama wengi wanaibwa wakati wakionekana barabarani bila wamiliki wao.

China inaongoza duniani kwa ilaji wa nyama ya Mbwa na PakaMteja akimkagua mbwa katika soko la Yulin China
Katika mji wa Yulin huko China mwezi Juni husherekea sherehe maalum ya mbwa na paka. Inakadiriwa mbwa na paka 10,000 huchinjwa mwezi huu kwa tamasha hiyo. Mwaka uliopita sherehe hizo zilikumbwa na maandamano kupinga kuwajicha mbwa na paka.

KOREA KUSINI

Nchini Korea Kusini, nyama ya mbwa ni maarufu sana kiasi cha kitoweo chake kupewa jina la ‘Gaegogi’. Inaaminika taifa hilo lina mashamba 17,000 yanayowafuga mbwa na kuuzwa kuwa chakula. Hata hivyo shinikizo za mashirika ya kutetea maslahi ya wanyama zimeanza kuzaa matunda.

Korea Kusini imefunga soko kubwa la kuuza mbwaMchuzi wa nyama ya Mbwa Korea Kusini
Hapo mwezi Februari, soko kubwa zaidi la mbwa lilifungwa katika eneo la Seongnam, kabla ya Korea Kusini kuandaa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi.

VIETNAM

Takriban mbwa milioni tano wanaaminika kuchinjwa na kufanywa kitoweo nchini Vietnam kila mwaka.

Ongezeko la wateja wa nyama hii limepelekea kuwepo na biashara ya magendo ya nyama ya mbwa katika nchi jirani za Thailand, Cambodia na Laos.

Mataifa ya Asia yameanza sheria kuthibiti ulaji wa nyama ya Mbwa na Paka
Mbwa wa Thailand ambao wanauzwa soko la Vietnam
Shirika linalotetea haki za wanyama la ‘Asia Canine Protection Alliance’, limeshinikiza serikali kujaribu kumaliza biashara ya nyama ya mbwa.

Shirika hilo limesema lina ushahidi kwamba nyama ya mbwa ni hatari kwa afya ya binadamu,na huenda ikasabaisha ugonjwa wa kichaa cha mbwa miongoni mwa watu wanaokula nyama yake.

Limetaka biashara hiyo kumalizwa katika mataifa ya Thailand, Laos na Vietnam.

Chanzo: bbcswahili

VIDEO: Afanya Maamuzi ya Ajabu Baada ya Kuachwa na Mpenzi wake

$
0
0
Moja kati ya habari ambazo zimekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii hivi karibuni ni stori kumhusu Stevie Stephens  ambaye alitumia ukurasa wake wa Facebook kurusha LIVE tukio la mauaji wakati anamuua mtu mmoja kutoka Cleveland, Marekani aliyefahamika kama Robert Godwin (74)

Stevie Roberts amedai kufanya mauaji ya watu 13 akisisitiza kuwa anaendelea ambapo Polisi mjini Cleveland wanafanya jitihada za kumpata huku mtandao wa TMZ.com ukiripoti kuwa inasemekana chanzo cha kufanya mauaji hayo ni kuachwa na mpenzi wake.

Nimekuwekea video hapa chini ambayo inamuonyesha Stevie Roberts  akitaja majina yake kamili na idadi ya watu aliowapotezea maisha pamoja na mipango yake ya kuendelea kufanya mauaji…

PATA Tiba ya Asili Kutoka Kwa Mtabibu wa Nyota Maalim Hussein...Una Shida na Mapenzi Au Pesa Hazikai?

$
0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza, Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba, MIGUU Kufa GANZI, Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA, Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI, Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi 

ZaidiWhatsapp +255 674 835107  Au Piga +255746757102

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Maajabu:Mwanamke Mwenye Sehemu Mbili za Uke Apata Ujauzito

$
0
0
Mwanadada Krista Schwab mwenye umri wa miaka 32 ameenda kinyume na utabiri wa madaktari waliomwambia hana uwezo wa kuzaa kwa sababu ya kuwa na sehemu mbili za uke.

Mwanamke huyo aliyezaliwa akiwa na sehemu mbili za uke, sehemu mbili za mifuko ya uzazi pamoja na matumbo mawili ya uzazi sasa anatarajia kupata mtoto wa kiume baada ya muda mrefu wa kuhangaika pamoja na mumewe kutafuta mtoto.

Krista anayeishi Washington huko Marekani aligundulika kuwa na hali hiyo ya kipekee inayojulikana kitaalamu kama ‘uterus didelphys’ alipokuwa na umri wa miaka 12.

Mwanamke huyo alitambua kuwa ana mifuko miwili ya uzazi alipokuwa na umri wa miaka 12 lakini hakutambua kama ana sehemu mbili za uke mpaka alipofikia umri wa miaka 30.

Madaktari walimwambia kuwa hawezi kupata ujauzito kutokana na hali yake. Alihangaika sana na aliwahi kubeba mimba mara mbili ambazo ziliharibika jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kukosa matumaini ya kupata mtoto.

Krista sasa ana ujauzito wa miezi mitano na yeye na Mume wake sasa wanatarajia kupata mtoto wa kiume.

“Kwa muda wa miaka mingi mimi na mume wangu tumekuwa tukilia, tukiomba na kuwa na ndoto za kupata mtoto. Tumemtafuta kwa hali na mali kwani tulitaka mtoto kwa hali na mali.” Alisema Krista.

Baada ya miaka mingi ya kuwa na ndoto ya kupata mtoto wa miujiza, Krista alinunua kipimo cha ujauzito pasipokuwa na matumaini yoyote.

“Baada ya kupima ujauzito kwa mara zaidi ya 1000 nilikata tamaa kabisa ya kupata ujauzito. Mwezi wa disemba niliamua kujaribu tena na nilinunua kipimo cha bei ghali, ambacho mimi na mume wangu tulidhani ni upotevu tu wa pesa” Alisema

Alisema kuwa amekuwa akiomba na kujipa matumaini huku akisubiri, lakini baada ya muda mrefu alikata tamaa kabisa, lakini kipimo kiliwashtua wote kwa kuleta matokeo ambayo hawakuwa wanayatarajia.

“Nilipoona kipimo kimetoa matokeo chanya, nilianguka chini kwa kilio. Tulishtuka na kufurahi  sana, hasa mume wangu” Alisema Krista

Aliongeza kuwa tokea alipokutana na mume wake alimwambia kuwa hana uwezo wa kupata ujauzito hivyo mara zote walipofanya mapenzi hawakutumia kinga.

Tatizo hilo la ‘uterus didelphys’ huusishwa mioja kwa moja na kutokuwa na uwezo wa kupata ujauzito. Lakini kwa Krista imekuwa muujiza kwani mtoto yupo katika mfukoo wa uzazi ambao hauwezi kutoa mbegu za uzazi.

Alisema kuwa mayai pekee ya uzazi yaliyokuwa yakifanya kazi ni yale yaliyo katika mfuko wa uzazi wa kulia. Na kutokana na kuwapo kwa uwazi kidogo sana kati ya mifuko hiyo miwili ya uzazi, ni vigumu kwa yai kutoka mfuko wa kulia kwenda mfuko wa kushoto.

“Ni ajabu sana kwa kuwa madaktari bado hawaelewi. Ukweli wa kuwa mjamzito katika tumbo la kushoto ambalo ni vigumu kwa mbegu za uzazi kufika humo. Ingawa ninaifurahia ndoa yangu siku zote” Alisema Krista aliyeonekana kuwa na furaha iliyochangiwa na hali ya yeye kuwa mjamzito.

VIDEO: Maajabu Mengine ya Jiji la Dar, mwanamke Adaiwa Kufa Kisha Kufufuka

$
0
0
Asubuhi ya April 18, 2017 kulisambaa taarifa za kufufuka kwa mwanamke ambaye alidaiwa kufa baada ya kugongwa na gari usiku wa kuamkia leo na kuthibitshwa kifo chake.

Mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Anna mkazi wa Tanki Bovu jijini Dar es Salaam anadaiwa kugongwa na gari usiku wa April 17, 2017 siku ya Pasaka kisha kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa kweli amefariki, lakini taarifa za kifo hicho ziliposambaa ndipo zikaibuka taarifa nyingine kuwa angali hai.

Katika hali ya kustaajabisha, vijana wawili waishio mtaa mmoja na mwanamke huyo walijitokeza na kudai kuwa mwanamke huyo hakufa bali yupo hai amechukuliwa kimazingara.

AyoTV na millardayo.com imewapata vijana hao ambao wamefanikisha kurudishwa kwa mwanamke huyo na hapa wanasimulia mlolongo mzima…

Bonyeza play kutazama…

Vita Kuu ya Tatu ya Dunia Yanukia (WW3)

$
0
0
Baada ya Wazee wa vita kuanza kufanya maandalizi ya Kuichapa Korea Kaskazini na baada ya wazee hao wa vita kufanya majalibio ya MOAB, Dalili zinaonyesha wazi kabisa nchi kumi zenye mabomu ys nuclea zimeanza kujiandaa kuingia vitani,

Hii vita ya tatu ya Dunia ya safari hii itakua ni balaa. Sasa na huu ugumu wa maisha tulionao nahisi tujiandae kula nyasi.

Baada ya Ushindi wa Jana..Wenger Aaanza Kuchonga..Atoa Kejeli Hili kwa Maashabiki wa Man United,Liver na Man City..!!!

$
0
0

.Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ameibuka na kuanza tambo baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Middlesbrough juzi.

Mabao kutoka kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil yalitosha kuwapa pointi tatu Gunners katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Riverside. Pia, kipindi cha pili Alvaro Negredo aliipatia timu yake bao.

Ushindi huo umewapa nguvu mpya kwenye mbio za kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu England inayoelekea ukingoni.

Timu hiyo imebakiza pointi saba ili kuipiku Manchester City inayoshika nafasi ya nne. Hata hivyo kikosi hicho cha Guardiola kina michezo mingi ukilinganisha na Arsenal yenye mchezo mmoja mkononi.

Kocha huyo raia wa Ufaransa amekiri,  awali walianza kupoteza mwelekeo baada ya kupokea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Crystal Palace wiki iliyopita.

“Nilihisi kwamba tulikuwa na mipango. Kama mlivyoona hatukucheza kwa kujiamini lakini kiuhalisia tulihitaji ushindi,” alizungumza Wenger wakati akihojiwa na Sky Sport.

Msanii wa Injili Amuomba Magufuli Amteue Kuwa Mbunge..!!!

$
0
0

Mwanamuziki wa injili, Upendo Nkone amesema yuko tayari kutumikia nafasi ya ubunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania endapo  Rais Magufuli atamteua.

Akiwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV, Upendo alisema, anaamini ametumwa na Mungu kufikisha ujumbe wake kupitia uimbaji, lakini pia yuko tayari kuitumikia jamii kupitia nafasi ya ubunge, na kuweka wazi kuwa si kwa ubunge wa kugombea jimboni.

"Sina mpango wa kuwa mwanasiasa, kwahiyo hata ubunge wa kugombea siwezi, lakini kama Rais wangu Magufuli akilala akiota kwamba anipe ubunge viti maalum, kwakweli napokea.... Mh. Magufuli nimeambiwa nigombee ubunge, basi unikumbuke baba" Amesema Upendo

Amesema aliwahi kushauriwa kugombea ubunge katika jimbo fulani lakini hakuwa tayari kwa kuwa hapendi kugombea.

Akieleza sababu kuu ya kutopenda ubunge wa kugombea, amesema masharti ya kugombea ni lazima uwe kwenye vyama vya siasa jambo ambalo halipendi.

Jambo lingine amesema mchakato wa kupata ubunge wa kugombea ni mgumu una mambo mengi ikiwa ni pamoja na gharama, jambo ambalo haliwezi na hivyo kusisitiza kuwa Rais Magufuli anapaswa kumkumbuka katika nafasi zake za kutea

Kifahamu Kikosi Hatari Duniani cha Marekani cha U.S.A Navy 'Seal' Ambacho Tayari Rasmi Kimeshatua Ndani ya Ardhi ya Korea Kaskazini kwa Ajili ya Kuanza Vita..!!!

$
0
0

Yumkini jaribio la mzee wa kiduku limeshtua sana Marekani ambapo sasa ni rasmi Kikosi hatari cha Makomandoo wa Kimarekani ambacho ndicho "The Most Feared Force" katika ulimwengu huu cha US NAVY SEAL inasemekana tayari kiko katika Peninsula ya Korea tangu Jana usiku kikitokea jimbo la Florida nchini Marekani. 

Hiki ni kikosi hatari zaidi duniani ambacho kazi yake ni kufanya operations ambazo ni hatari zaidi mno na za mwisho. US Navy Seal ni mjumuisho wa makomandoo hatari zaidi wanaotumia ujuzi wa hali ya juu na wenye mafunzo ya kitaalamu zaidi kuliko makomandoo wengine wa majeshi yote ya kimarekani. 

Makomandoo hawa ni wale tu wenye uzoefu wa hali ya juu wa kupambana popote pale iwe angani, ardhini au majini, na katika hali yoyote ile iwe barafu, mvua au jua. Na ndio maana ya neno SEAL ambayo kirefu chake ni Sea, Air and Land. 

Ni Mara chache sana kutumika. Hawa ni tofauti na majeshi mengine kama US Army Rangers, US Delta Force na mengine. Katika utawala wa Obama, ametoa ruhusa MARA MOJA tu kwa US Navy Seal kutumika. Mara ya mwisho kilitumika usiku wa manane kwa takribani dakika 45 tu kumuangamiza Osama na ni askari mmoja tu alijeruhiwa kwa ajali ya helkopta zisizotoa sauti ambayo ilikosewa ikagonga ukuta wakati makomandoo wakidrop kwenye makazi ya Osama. 

Na baada ya Operation Makomandoo hao waliilipua haraka helicopter yao iliyopata hitilafu ili maadui wasigundue teknolojia iliyotumika kutengenezea helicopter hiyo na baada ya kuilipua wakaondoka. Makomandoo wa Navy Seal waliotumika katika Operation hiyo ni 11 tu na Marubani Watatu ambao nao ni kutoka Navy Seal. Na ikumbukwe kuwa Operation hii ilikuwa ikitazamwa live (mubashara) kutoka White House ambapo Obama alikuwa akifuatilia (nilirusha tukio hili), kofia za makomandoo hawa zilikuwa na kamera mbele ambazo zilitumika kurekodi kila kitu kinachoonekana mbele na kurusha kwenye satelaiti had White House. Mkakati huu ulisimamiwa na Mwanamke hatari zaidi anayejulikana kama Alfreda Frances Bikosky ambaye ni Afisa mwandamizi wa CIA na jasusi aliyebobea na pia ni komandoo lakini si memba wa Navy Seal. Bibi Alfreda anajulikana zaidi katika jeshi la Marekani kama MALKIA WA MATESO. Serikali ya Marekani inajitahidi kudhibiti mitandao ya kijamii na google isisambaze picha za mama huyu hatari. 

Kikosi hiki cha US Navy Seal hutumika baada ya makomandoo wengine wa majeshi tofauti ya marekani kusoma Jiografia ya sehem husika, ramani ya ngome za adui na silaha zake then Raisi wa Marekani hutoa ruhusa ya NAVY SEAL kutumika kumalizia Operation. Baadhi ya majukumu/kazi za Navy Seal ni Direct Operations (kama wanavyotaka kumfanyia North Korea), Strategic Special Missions (kama walivyofanya kwa Osama), Hostage Rescue (kama walivyofanya miaka ya nyuma kuwaokoa Ma-Intelligensia wa Kimarekani waliotekwa Iran) na Foreign Internal Defence. 

Mpaka sasa Navy Seal ina jumla ya Makomandoo 8985 ambao ni hatari mno na wenye roho za kinyama. Makomandoo hawa huwa wapo kwenye mazoezi makali ya special operations na trainings ngumu muda wote huko Virginia, Marekani. Mara chache sana Navy Seal huwa Recruited kwenda CIA kufanya kazi za Kiintelligensia wanapotakiwa. Makamu wa Rais wa Marekani Bwana Pence yuko Korea Kusini na inasadikika ujio wake umeambatana na NAVY SEAL waliojichimbia katika Nyambizi zisizoonekana katika pwani ya Korea..

Klopp - Nitafia Liverpool..Mniache Tafadhali..!!!

$
0
0

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hafikirii kufundisha klabu nyingine hivyo atastaafu soka akiwa na miamba hiyo.

Kocha huyo mwenye miaka 49 alianza kufundisha soka klabu ya Mainz na alifanya kazi hiyo kwa miaka saba  dimba la Opel Arena kabla ya ujiunga na Borussia Dortmund mwaka 2008.

Pia aliwahi  kuifundisha BVR misimu saba, huku akitwaa mataji mawili ya Bundesliga kabla ya kuachana nao msimu wa mwaka 2014-15.

Klopp alisema hana nafasi ya kuanza kuzungumzia katika kipindi hiki kifupi kilichobaki kutokana na klabu mbalimbali kujitokeza kuomba huduma yake.

Wakati Watanzania Wakilia Katiba Mbovu..Waturuki Waiiga Katiba ya Tanzania na Kuipitisha Ili Kuitumia ..Trump Awatumia Salamu hizi..!!!

$
0
0

Wananchi wa nchi ya Uturuki wamemaliza kupiga kura ya maoni ambayo ilikuwa iamue kama Katiba ya nchi hiyo ibadilishwe na kumpa Raisi wa nchi madaraka makubwa kama ya Raisi wa JMTZ au ibakie kama ilivyo na madaraka madogo ambayo yako limited!

Sasa matokeo ya kura ya maoni yameonyesha kwamba wengi wao wanapendelea kuwa na Kiongozi mwenye madaraka makubwa yaani strongman dhidi ya Katiba ambayo madaraka ya Raisi yamevunjwa vunjwa kama waliyo nayo leo hii, matokeao ni 51.39% Ndiyo, na waliobakia Hapana!

Na tayari Raisi wa USA Donald Trump amempigia simu Raisi Tayyip Erdogan na kumpongeza kwa ushindi huo, sasa Uturuki inaongozwa na Katiba ambayo inampa Raisi madaraka makubwa sana!

Raisi Tayyip Erdogan sasa ni strongman wa nchi ya Uturuki!

Mwanamke Usafi Bibieh..Jifunze Jinsi ya Kuondoa Weusi Kwapani iIli Uwe Huru..!!!

$
0
0

Najua wengi wana tatizo la makwapa kuwa meusi tii hadi wanaogopa kuvaaa vijiguo wazi maana lol. Sasa hapa nakupa some tips zakuondoa huo weusi katika makwapa. Hapa ni njia 3 za kukusaidia; tumia ile iliyo karibu zaidi na wewe.

Baking Soda

Changanya baking soda na maji.
Weka au paka hapo kwenye kwapa jeusi
Acha kwa dakika 10 – 15
Osha na maji ya vugu vugu

Uwe ukifanya hivyo mara kadhaa katika wiki utaona tatizo lako linakwisha

Apple Cider Vinegar

Pakaa hiyo apple cider vineger
Baada ya dakika 5 futa na kitambaa cha cotton – usioshe na maji

Viazi ulaya

Kiponde ponde
Kisha pakaa uji wake katika kwapa
Acha kwa dakika 30 kisha osha vizuri

Haya nimekupa hizo tiba tatu tofauti kuondokana na kwapa jeusi please.

Kuwa Makini Sana Na Mambo Haya Yanaweza Kukuzia Kufanikiwa Kwako.

$
0
0

Kuna wakati unaweza ukawa unashangaa kwa nini ndoto zako hazitimii?  Utakuta umejiwekea malengo yako vizuri, lakini unashangaa ni malengo machache sana yanayotimia au wakati mwingine hakuna kabisa.

Sina shaka yoyote umeshawahi kukutana na hali kama hii wakati fulani katika maisha yako. Kiuhalisia, yapo mambo mawili ambayo kitaalamu hupelekea ndoto zako kushindwa kutimia ikiwa hutayajua vizuri.

Jambo la kwanza, ni kutokujua kile unachokitaka vizuri. Hili ni jambo ambalo hupelekea wengi kushindwa kufanikisha ndoto zao kabisa. Kama hujui kile unachokitaka vizuri, suala la kufanikisha ndoto zako litakuwa gumu kidogo.

Katika akili yako ili uweze kufanikisha ndoto yako au jambo unalolitaka kwa urahisi, ni lazima kile kitu unachokitaka uweze kukijua vizuri. Tambua njia utakazotumia hadi kukipata kitu hicho pia tambua kitu hicho changamoto zake ni zipi.

Acha kufanya kosa la kuuchanganya ubongo wako kwa kuupa vitu vingi. Kuwa maalumu kwa kujua vizuri kile unachokitaka. Usipojua kile unachokitaka kwa uhakika na kukifanyia kazi, ni wazi hutaweza kufanikiwa na hilo halina ubishi.

Jambo la pili, ni kukosa hamasa ya kutosha kwa kitu hicho unachokitaka. Hamasa ni kitu cha muhimu sana ili kufikia ndoto zako. Ukishakijua kitu hicho vizuri, hamasa itakusaidia kufanya kila jitihada hata kama umechoka.

Wengi ni watu wa kutaka kufikia lengo fulani katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hujikuta ni watu wa kukosa hamasa ya kuwasukuma kuweza kukamilisha malengo yao.

Ili kufanikiwa, fanya kila ufanyalo kuhakikisha una hamasa ya kufanya hicho unachotaka kukifanya katika maisha yako. Inapotokea hamasa hiyo umeikosa acha kusimama eti kwa sababu ya kukosa hamasa.

Maisha hayasimami eti kwa sababu wewe hujisikii kufanya kitu fulani au umekosa hamasa. Endelea kusonga mbele, huku ukitafuta hamasa ya kufanikiwa kwako kila siku. Ukifanya hivyo utafika mbali kimafanikio.

Katika hali ya kawaida, kama kila wakati unakosa mambo haya mawili suala la kufanikiwa kwako linakuwa ni gumu sana. Hivyo, ni lazima sana kwako kujua vizuri kile unachokitaka na kuwa na hamasa kubwa yaani ‘burning desire’ ya kuhakikisha kitu hicho ni lazima unaweza kukipata.
Ukichunguza watu wengi ambao hawajafanikiwa wanashindwa kufanikiwa kwa sababu hizi mbili tu na si vinginevyo. Kama unafikiri natania anza kufatilia, huku lakini ukianza na wewe.

Kama unajiona hujafanikiwa vya kutosha jiulize binafsi je, unakijua vizuri kile unachokitaka na huna tamaa ya kutaka  hiki mara kile na mwisho wa siku kuwa na malengo mengi yasiyotekelezwa?

Usiishie hapo tu, tena kama unaona hujafanikiwa vya kutosha jiulize, je, una hamasa kubwa ya kuona ndoto zako zinatumia? Je, unakosa usingizi na kuamua kujituma usiku na mchana hadi kufanikiwa?

Ukipata majibu ya maswali hayo yatakusaidia sana kuweza kufanikiwa na kuwa mtu mwingine tofauti na hatimaye kuweza kufanikisha zoezi zima la kutimiza ndoto zako. Jitoe kikamilifu kuona ndoto zako zinatimia kwa kuyajua mambo hayo mawili.
Ni wako rafiki katika mafanikio,

Hizi Hapa Sababu 10 za Mama Anayenyonyesha Kukaukiwa Maziwa au Kuisha Kabisa..!!!

$
0
0

Nimekuwa nikipata malalamiko mengi kwa akina mama wanaojifungua kwamba matiti yao yanatoa maziwa kidogo au hayatoi kabisa. hii imewafanya kushindwa kunyonyesha au kuingia gharama kubwa kuwanunulia maziwa ya lactogen fomula dukani au kutumia maziwa ya ngombe.

lakini pia tukumbuke kwamba maziwa ya mama hua hayana mbadala kabisa yaani virutubisho vinavyopatikana kwenye maziwa yale havipatikani popote hivyo kama una shida ya kutoa maziwa basi tumia maziwa mbadala huku ukitafuta suluhisho la maziwa yako.vifuatavyo ni vyanzo vya vya kushindwa kutoa maziwa.

1. Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango; wanawake wengi hutumia njia hizi baada ya kujifungua bila shida yeyote lakini kuna baadhi yao njia hizi huingilia mfumo wao wa  kutoa maziwa hasa zikitumika kabla mtoto hajafikisha miezi sita. hii husababishwa na kuongezeka kwa homoni za uzazi yaani progesterone na oestrogen ambazo hushusha homoni ya kutoa maziwa yaani prolactin hormone.kama umekumbwa na hali hii basi acha mara moja njia hiyo na utumie njia zingine kama kondom,kalenda au njia nyingine isiyotumia dawa.

2. Matatizo ya kimaumbile; baadhi ya wanawake matiti yao hayakukamilika wakati wamakua yaani yanakua na upungufu wa vitu muhimu vinavyohifadhi maziwa kwenye matiti kitaalamu kama grandular tissues hii hufanya maziwa yatoke kwa shida sana.mama anashauriwa akamue maziwa wakati wa kunyonyesha na mara nyingi mtoto wa pili mpaka watatu wakizaliwa matiti haya yanakua yameshazoea hivyo hayasumbui tena kutoa maziwa.

3. Upasuaji wa matiti; kama mama ameshawahi kupasuliwa matiti yake kwa shida yeyote labda majipu, ajari, upasuaji wa kuongeza au kupunguza matiti basi kwa namna moja au nyingine hii inaweza kuharibu mfumo wake wa matiti kupitisha maziwa na kujikuta hatoi maziwa ya kutosha.ukiwa na shida hii utahitaji kutumia maziwa mbadala kwa mtoto.

4. Matumizi ya dawa; wakati wa kunyonyesha mama anaweza kuugua na  kutumia dawa fulani fulani ili apone ugonjwa alionao lakini kuna  baadhi ya dawa ni hatari kwani hushusha kiwango cha maziwa. mfano dawa za kama bromocriptine,methergine,pseudoephredine.

5. Matatizo ya homoni za uzazi; matatizo ya homoni kua juu sana au kua chini sana yanaweza kusababishwa na magonjwa ya ovari, kisukari na kadhalika. pia magonjwa yeyote ya homoni yanayochelewesha mtu kupata mimba huweza kuzuia maziwa pia. ni vizuri ukaonana na daktari kupima kiwango cha homoni na kupata matibabu.

6. Kutonyonyesha usiku; wakati wa usiku homoni inayohusika na kutengeneza maziwa yaani prolactin hutengenezwa kwa kiwango cha juu sana lakini pia ili mtoto alale usiku mzima bila kusumbua lazima anyonye vizuri usiku.kutonyonyesha usiku hupunguza homoni hii na kumfanya mama atoe maziwa kidogo sana siku inayofuata.

7. Kutonyonyesha vya kutosha; kawaida mama anatakiwa anyonyeshe angalau mara kumi ndani ya masaa 24, sasa mwili hutengeneza maziwa unapohisi matiti hayana kitu na kama mwili ukihisi matiti yana maziwa muda mwingi basi unajua maziwa hayahitajiki sana na kuanza kupunguza kiasi cha kutoa maziwa.

8. Kutokula vizuri; maziwa anayotoa mama yanatengenezwa na chakula anachokula wala sio miujiza fulani hivyo kipindi hiki mama anatakiwa ale mlo kamili yaani matunda, protini ya kutosha, wanga, mboga za majan na maji mengi i na ikiwezekana atumie virutubisho vinavyotengenezwa maalumu kwa ajili ya kuongeza maziwa.

9. Matumizi ya vyakula mbadala; miezi sita baada ya kuzaliwa mtoto anatakiwa anyonye tu bila kupewa kitu chochote, kuna watu hua wanawapa maji wakidai eti watoto walisikia kiu sio kweli.sasa kuanza kumchanganyia maziwa ya ngombe na yale ya dukani kutamfanya anyonye kidogo kwako na mwili utapunguza kiasi cha maziwa yako...hivyo siku ukikosa mbadala utajikuta huna maziwa kabisa.

10. Mtoto kushindwa kunyonya; kama nilivyosema hapo mwanzo kwamba maziwa yakitoka mengi na mwili unatengeneza mengi zaidi na kama mtoto hanyonyi vizuri basi na maziwa hutoka kidogo zaidi.hali hii inaweza kusababishwa na dawa ya usingizi ambayo alipewa mama wakati wa kupasuliwa ambayo huamuathiri mtoto pia, au matatizo ya kuzaliwa nayo kama tongue tie[ulimi kushikwa chini ya mdomo, hii inaweza kurekebishwa na daktari] au mtoto kuugua.

Usipuuzie..Mara Uonapo Dalili Hizi 8 Wahi Haraka Hospitali ..!!!

$
0
0

Kuna wakati unaweza kujikuta hauko vizuri kila siku na ukashindwa kujua nini tatizo.

Sasa leo napenda tujuzane hizi dalili ambazo ikiwa utaziona basi huenda ukawa na matatizo kiafya:-


1. Kupungua uzito ghafla.
Kuna baadhi ya watu huweza kujikuta ghafla tu wamepoteza kilo kadhaa bila kuwepo na sababu za msingi, hivyo wataalam wa afya wanashauri inapotokea hali hiyo ni vyema kufanya uchunguzi zaidi ili kubaini sababu za msingi za hali hiyo kutokea.

2. Mabadiliko ya ngozi.
Ngozi ni alama tosha ambayo huashiria uwepo wa afya bora kwa binadamu hivyo basi ikiwa utaona ngozi yako imeanza kupoteza uhalisia wake basi ujue huenda tayari kunatatizo la kiafya linakunyemelea hivyo unaweza kuwaona wataalam kwa ushauri zaidi.

3. Mabadiliko ya haja ndogo
Unapoona kuanza mabadiliko ya haja ndogo au haja kubwa basi huenda nayo ikawa dalili ya tatizo, hivyo ni vyema kuwa mchunguzaji wa haja zako ili kung'amua baadhi ya matatizo ya kiafya kwa haraka na kuyatafutia ufumbuzi kwa wataalam.

4. Matatizo ya kukosa usingizi.
Hii nayo huweza kuwa ni kiashiria cha tatizo mwilini mwako hivyo unapoona mabadiliko yanahusu usingizi pia unaweza kujichunguza vizuri na unapoona huelewi basi waone wataalam kwa ufafanuzi zaidi.

5. Midomo kukauka.
Unapoona midomo inakauka au kupasuka nayo huweza kuwa dalili mbaya kiafya hivyo unaweza kufanya maamuzi ya kwenda kufanya uchunguzi wa kiafya ili kujua tatizo zaidi.

6. Mabadiliko ya joto la mwili
Iwapo mwili unakuwa na joto mara kwa mara nayo huweza kuwa ni moja ya kiashiria cha tatizo kiafya, hivyo ni vyema kuwaona wataalam kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya.

7. Unapokosa hamu ya kula kabisa
Nayo ni moja ya dalili kuwa mwili wako unashida hivyo ni muhimu kufika kwenye kituo cha afya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

8. Uchovu wa mwili
Mwili unapojihisi umekuwa mzito nayo huwa dalili ya tatizo ndani ya mwili wako nayo si vizuri kuipuuza na badala yake ni vyema kufanya uchunguzi zaidi.

Jinsi Ya Kupangilia Chumba Cha Kupumzika au Kulala..!!!

$
0
0

Nyumba ni urembo, nyumba ni mapambo, ili nyumba iweze kuvutia inahitaji mazingira yenye hadhi ambayo yanaweza kumvutia mtu kwa muonekano wake wa nje na ndani pia inaweza kumvutia mtu kutokana na rangi za chumba.

Watu wengi huweka mazingira safi jikoni, sebuleni na kusahau kuwa chumba cha kulala pia kinatakiwa kuwa safi muda wote kwani ni sehemu ambayo inatumiwa kwa mapumziko.

Ili kuweze kupumzika vizuri baada ya mizunguko ya kutwa nzima ni vizuri chumba kikawa katika muonekano mzuri ambapo sambamba na hilo uwepo mpangilio mzuri wa nguo na fenicha.

Chumba cha kulala hakitakiwi kuwa na vitu vingi, kinahitaki kuwa na hewa ya kutosha ili kumuwezesha mtumiaji kuweza kupata hewa safi pia inamsaidia mtumiaji kuweza kufanya usafi sehemu zote kutokana kuwepo kwa nafasi ya kutosha.

Epuka kujaza vitu vingi chumbani kama computer, meza viti, kapu la nguo chafu, kwani vitu hivyo vinaweza kuwekwa sehemu nyingine ya nyumba na chumba kubaki mahali pa kupumzika tu.

Prof Kitila Mkumbo Aanza Kazi kwa Kuishushia Mkwara Mzito Dawasco..!!!!

$
0
0

Katibu mkuu wa wizara ya maji Prof: Kitila Mkumbo amelitaka shirika la maji safi na taka nchini DAWASCO kuhakikisha wanawekeza sana kwenye usambazaji wa maji kwani ni aibu kwa jiji la Dar es salaam kuwa na maeneo ambayo hayana maji.

Prof: Kitila Mkumbo ametoa maagizo hayo jana jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara katika shirika hilo na kukutana na watendaji wakuu wa DAWASCO pamoja na watendaji wakuu kutoka Mamlaka ya maji safi na taka jijini Dar es salaam DAWASA.

“Pamoja na kazi nzuri mnayofanya ya kuhakikisha upatikanaji wa maji hakikisheni mnaongeza kasi ya usambazaji wa huduma hii muhimu kwa wananchi kwa kufanya hivyo mtakuwa mnatendea haki dhana ya kuwa mnaongoza kwa mapato lakini pia mnatoa huduma stahiki kwa wananchi”. Alisema Prof. Kitila

 Pamoja na hayo amewasii wateja wote wa DAWASCO kutii agizo la Mhe. Rais kwa kulipia huduma wanazozipatiwa ili kuziwesha mamlaka hizo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.

Prof: Mkumbo pia amelitaka shirika hilo kukamilisha miradi ya maji katika maeneo ambayo mpaka sasa inaonekana haijakamilika kwa lengo la wananchi kupata maji.

Duh Noma Sana..Eti Mchungaji Anamfananisha Rais Magufuli na Nabii Musa..!!!

$
0
0

MCHUNGAJI David Mabushi wa Kanisa la IEACT lililopo katika Manispaa ya Shinyanga, amesema kanisa linamuunga mkono Rais John Magufuli kwa yale anayoyatekeleza kulinda rasilimali za umma, huku akimfananisha kiongozi mkuu huyo wa nchi na Nabii Musa, aliyekuja kuwakomboa wana wa Israel.

Mchungaji Mabushi alisema hayo juzi ofisini kwake wakati akizungumza na gazeti hili baada ya kumalizika kwa ibada ya Sikukuu ya Pasaka, huku akieleza kuwa Rais Magufuli amedhamiria kuyafanya aliyokuwa akiahidi katika kipindi cha kampeni wakati wa Uchanguzi Mkuu mwaka 2015 hata Watanzania wakamwamini na kumchagua kuliongoza taifa.

Mabushi alisema kanisa lake linamuunga mkono Rais Magufuli kwa juhudi na kazi zote, anazozifanya kulinda rasilimali za nchi hii zisizidi kuwanufaisha Watanzania wachache. Kiongozi huyo wa dini, alisema utekelezaji wa ahadi alizotoa Rais Magufuli wakati akigombea wadhifa huo pamoja na hatua anazochukua kiutendaji ni mambo yanayoleta tija na ukombozi kwa Watanzania, kama Nabii Musa alivyokuja kuwakomboa wana wa Israel.

Alisema miongoni mwa masuala yaliyokuwa yakilalamikiwa na Watanzania wengi ni pamoja na kuwepo kwa mikataba mibovu ya migodi na mchanga, kusombwa kupelekwa nje ya nchi ukiwa na rasilimali nyingi. Hivyo, alisema kitendo cha kuzuia usafirishaji wa mchanga huo na kuunda tume mbili za kuchunguza ili kujiridhisha kuhusu vilivyomo katika mchanga huo ni cha kijasiri, kwani kimelenga kujiridhisha na hali halisi, na kuondoa manung’uniko kwa kuwa ukweli utakuwa wazi.

“Lakini ninashangazwa na baadhi ya Watanzania wamekuwa kama anachokifanya Rais kukemea uovu, ubadhirifu ufisadi na rushwa sio walichokuwa wakikisema kipindi cha nyuma…Wengi hawataki kupaza sauti kumuunga mkono na sasa sisi tunamuombea kwa Mungu huku tukimshauri amuachie Mungu kila jambo kwa kuwa ameamua kuwatumikia wananchi wanaonyonywa rasilimali zao,” alisema Mchungaji Mabushi.

Waziri Mkuu wa Israel Afunguka Haya Mazito Kuhusu Serikali ya JPM na Tanzania kwa Ujumla..!!!

$
0
0

WAZIRI Mkuu wa zamani wa Israel, Ehud Barak ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jinsi inavyovitunza vivutio vyake vya utalii. Barak anayeongoza kundi la watalii zaidi ya 100 kutoka Israel ikiwamo familia yake, aliwasili nchini mapema wiki iliyopita kwa ajili ya utalii.

Walitembelea Makumbusho ya Olduvai Gorge na kueleza kufurahishwa kwake na jinsi Serikali inavyofanya katika kuhifadhi maeneo ya kihistoria kama Olduvai Gorge. Aidha, walitembelea Hifadhi za Taifa za Ngorongoro na Serengeti zilizoko katika Urithi wa Dunia, unaotambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete, alisema Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Israel alizuru pia Olduvai Gorge akiwa njiani kwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti alikopokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani. Akiwa Olduvai Gorge ambayo ni moja ya eneo maarufu la masuala la kale katika Afrika Mashariki na linalotembelewa kwa kiasi kikubwa na watalii wakienda katika hifadhi za taifa za Ngorongoro na Serengeti, Barak alisema eneo hilo ni muhimu kutokana na uhusiano wake na binadamu wa kizazi cha sasa.

Akiwa na msafara wake waliwasili nchini Jumanne iliyopita wakitumia ndege ya Shirika la Ndege la Israel, na kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) walipokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe. Mapema mwezi huu, Balozi wa Israel nchini, Yahel Vilan alimtembelea Rais John Magufuli na kumueleza kuwa watalii wapatao 200 walikuwa wanatarajiwa kuitembelea nchi mwezi huu.

Tanzania na Israel zimeapa kudumisha uhusiano wake na ulipata nguvu zaidi baada ya uamuzi wa Tanzania kufungua ubalozi wake nchini Israel na kufunguliwa kwa kituo cha Israel cha utoaji viza jijini Dar es Salaam, Novemba mwaka jana. Sekta ya utalii itanufaika kutokana na hatua hizi. Kulingana na taarifa za kuaminika kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), idadi ya watalii kutoka Israel imeongezeka kutoka 3,007 mwaka 2011 hadi 14,754 mwaka 2015.

Tenaaa..Kenya Waiga Mwendokasi wa Tanzania..!!

$
0
0

Mara nyingi watanzania wamekuwa wanataja mafanikio ya nchi nyingine wakilinganisha na mazingira hafifu ya hapa nchini katika masuala ya Maendeleo.

Lakini  orodha ya mazuri yanayoigwa na nchi nyingine kutoka Tanzania itakuwa imeongezeka kwa jambo moja lingine ambalo ni Mabasi ya mwendo kasi.

Aidha, Mamlaka ya usafiri jiji la Nairobi imefufua mpango kupunguza foleni za magari kwa  kuanzisha usafiri wa Mabasi ya Mwendokasi kama yanayotumika kwa sasa nchini Tanzania.

Kwa mujibu wa Katibu wa Masuala ya usafirishaji Mwangi Mariga alisema ujenzi wa  mradi huo wa Mabasi ya  Mwendokasi  utahusisha miji mitano.

Naye  Katibu wa Baraza la Mawaziri James Macharia alishauri   mwaka jana kwamba mapendekezo maalum ya mfumo wa Mabasi ya  usafiri yalikuwa na changamoto kutokana na miundombinu iliyopo ya  barabara  kwa mabasi kuwa na msongamano.

Mradi wa Mabasi ya Mwendokasi   umebuniwa kufuatia idadi ya watu wa Nairobi kuongezeka hadi milioni 3.3 kutoka 350,000 mwaka 1963 na idadi ya magari inakadiriwa kufikia 300,000 bila ongezeko sawa katika mtandao wa barabara.
Viewing all 104684 articles
Browse latest View live




Latest Images