Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104743 articles
Browse latest View live

UPDATE ..Muda Wowote Kuanzia Sasa Vita ya Kinyuklia Kuanza Kurindima Kati ya Marekani na Korea Kaskazini...!!!

$
0
0

NI katika mkutano wa waandishi wa habari katika Umoja wa Mataifa ulioandaliwa na Korea Kaskazini, ndipo unapoweza kumsikia mwanadiplomasia akiwatakia wanahabari sikukuu njema ya mwisho wa wiki halafu kutoa onyo la vita ya kinyuklia.

Katika miongo ya karibuni Korea Kaskazini imekuwa ikitoa vitisho vya mara kwa mara juu ya kuzuka kwa vita baina yake na Marekani, lakini utawala wa Rais Donald Trump ulitangaza kumalizika kwa zama za sera ya uvumilivu dhidi ya Pyongyang. Balozi mdogo wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa, Kim In Ryong aliitisha mkutano wa haraka wa waandishi wa habari jijini New York.

Mkutano huo uliandaliwa masaa kadhaa baada ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence kutembelea eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi katika mpaka wa Korea Kaskazini na Kusini. Pence alionya kwamba Korea Kaskazini isitake kuijaribu nchi yake “au nguvu za majeshi yetu.”

Huko New York, Korea Kaskazini ilirusha moto wa maneno. Balozi huyo alilaani kuongezeka kwa uwepo wa majeshi ya Marekani katika bahari karibu na peninsula ya Korea, pamoja na shambulizi la kombora lililofanywa dhidi ya Syria.

Kim alisema, “Hii imeleta hali ya hatari ambayo inaweza kusababisha vita ya kinyuklia kuibuka muda wowote katika peninsula na inatishia kupotea kwa amani na usalama wa dunia.”

Wakati waandishi katika Umoja wa Mataifa wamewahi kusikia lugha kama hiyo kutoka kwa Korea Kaskazini, maneno yaliyotolewa juziJumatatu yalikuwa ni makali zaidi.

Akisoma taarifa iliyoandaliwa kwa ajili ya waandishi wa habari, alisema, “Marekani inataka kuharibu amani na ustawi wa dunia kwa kufanya mambo ya kihuni kama kufanya uvamizi wa taifa huru ni jambo jema ambalo lina lengo la kulinda ustawi wa ulimwengu na inajaribu kufanya hivyo katika peninsula ya Korea pia.”

Kim alisema kuwa nchi yake ipo tayari kuchukua hatua dhidi ya hali yoyote ya kivita kutoka kwa Marekani. Shambulizi lolote la makombora au nyuklia litakalofanywa na Marekani litajibiwa kwa nguvu ile ile,” alisema.

Ni wazi kwamba Umoja wa Mataifa una wasiwasi. Msemaji wake Stephane Durarric aliwaambia waandishi wa habari, “Tunasikitishwa na kuongezeka kwa hali ya wasiwasi ambayo tunaishuhudia katika peninsula ya Korea. Tunazitaka pande zote kutumia njia za kidiplomasia kumaliza tatizo hili.”

Korea Kaskazini ilifanya jaribio la kombora ambalo lilishindwa mwisho wa wiki hii. Dujarric alisema, “Nadhani jaribio la karibuni kabisa ambalo limefanyika mwisho wa wiki hii linatia wasiwasi. Tunaitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua zote muhimu ili kutuliza hali ya mambo na kurudi kwenye meza ya mazungumzo ya kuachana na mpango wake wa kutafuta silaha za kinyuklia.”

Korea Kaskazini imekasirishwa kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaitisha kikao baadae mwezi huu kuzungumzia suala hilo, kikao ambacho kitaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson.


Gonjwa la Ajabu Laua Mamia ya Watanzania..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 19/4/2017..!!!

Sakata la Point Tatu Walizopewa Simba Bado Kizungumkuti..Tff Washindwa Kutoa Jibu...!!!

$
0
0

Sakata la pointi tatu ambazo Simba SC ilipewa na Kamati ya Saa 72 kutokana na kile kinachodaiwa Kagera Sugar ilichezesha mchezaji Mohamed Fakhi akiwa na kadi za njano tatu kinyume na sheria za ligi kuu msimu 2016/17 limechukua sura nyingine baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania kusema bado ushahidi haujakamilika ipasavyo hivyo.

Akitangaza mbele ya waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine Mwesigwa amesema kikao cha jana kilikuwa maalumu kwa ajili ya kumaliza kazi ilianzwa na Kamati ya Saa 72 na sio kuiharibu maamuzi yake ambayo ilitoa.

“Mashahidi wengi hawajaweza kufika hivyo lazima usubiri mpaka waletwe ili kukamilisha kazi. Pia nyaraka muhimu haziletwa. Kamati ya Saa 72 haina nguvu ya kustafiri sheria hivyo kinachofanyika sisi (Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji) tunamalizia ilipoishia,” alisema Mwesigwa.

Mwesigwa ameongeza kuwa ni lazima kuliweka suala hili vizuri kwa maslahi ya siku za usoni hivyo wakienda nalo kwa pupa litakuwa na athari katika siku zijazo katika soka la Tanzania.

Kikao hicho kimeahirishwa hadi leo Aprili 19 mwaka huu.

Lulu Atokwa Povu Bethidei Yake Kubuma...!!!

$
0
0

Kweli utawala wa awamu ya tano kiboko! Tofauti na miaka iliyopita ambapo mastaa mbalimbali hufanya kufuru katika kusherehekea kumbukumbu ya siku zao za kuzaliwa, Jumapili iliyopita, ambayo ilikuwa ni bethidei ya staa wa filamu, Elizabeth Michael ‘Lulu’, lakini haikufanyika

Chanzo makini kilipolidokeza Risasi Mchanganyiko juu ya kutofanyika kwa shughuli hiyo, liliwasiliana na muigizaji huyo, lakini katika hali ya kushangaza, alitoa povu (kufoka) mno, akitaka watu kuachana na habari zake, kwa vile haziwahusu. Kwa miaka kadhaa iliyopita, Lulu alidhimisha bethidei yake katika hoteli kubwa au kumbi zenye ‘akili’ zikiambatana na mbwembwe nyingi za ulaji na manywaji, lakini mwaka huu imekuwa kimya.

“Mwaka huu Lulu hajafanya sherehe kama ilivyozoeleka miaka mingine iliyopita, hapo ndiyo unajua kiukweli mambo yamebana awamu hii, hakuna fedha, bethidei yake imebuma, hakuna cha ukumbini wala nini, hapana chezea utawala wa Rais Dkt. John Magufuli, kila mtu ana nidhamu ya fedha,” kilisema chanzo hicho.

Ili kuujua ukweli, Risasi Mchanganyiko lilimtafuta kwa njia ya simu Lulu ili kumsikia anazungumziaje kuhusu siku yake hiyo kubwa maishani mwake.

Risasi: Haloo Lulu, gazeti la Risasi hapa, hongera kwa kuongeza mwaka mwingine kwenye maisha yako.

Lulu: Asante sana.

Risasi: Je, bethidei yako ulifanyia wapi maana mashabiki wako wanapenda kujua ilikuwaje?

Lulu: Hilo haliwahusu.

Risasi: Kuna habari kwamba mwaka huu hujafanya sherehe kwa sababu ya ukata, hili likoje?

Lulu: Kama nimefanya au sijafanya linawahusu nini, kwanza kuanzia leo msinipigie simu tena, yaani sitaki kabisa simu zenu.

Risasi: Sisi tulitaka tu kuujua ukweli kuhusu suala la kwamba ukata ndiyo umesababisha sherehe isifanyike.

Lulu akakata simu.

Hata hivyo, wakati Lulu akishindwa kufanya sherehe hizo Jumapili, jana yake, msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Isabela Mpanda, alifanya bethidei yake katika Ukumbi wa Belinda uliopo Mbezi Beach.


Askari 17, Viongozi 18 Wameuawa Mkuranga, Kibiti

$
0
0

Idadi na watu, raia na askari polisi waliouawa kwa kupigwa risasi katika Wilaya za Rufiji, Kibiti na Mkuranga mkoani hapa imekuwa kubwa hivyo kutia wasiwasi kwamba, maisha katika eneo hilo ni ya roho mkononi, Uwazi limechimba na kuchimbua.

Uwazi limebaini hayo kufuatia Aprili 13, mwaka huu, askari polisi wanane wilayani Kibiti kuuawa kwa kupigwa risasi kisha kuporwa bunduki 7 na watu ambao jeshi hilo linasema ni majambazi.

Askari hao ni A/INCP Peter Kigugu, F.3451CPL Francis, F.6990PC Haruna,G.3447 PC Jackson, H.1872PC Zacharia, H.5503 PC Siwale, H.7629PC Maswi na H.7680PC Ayoub ambao wote wamezikwa Jumapili iliyopita.

KWA NINI MKURANGA, KIBITI NA RUFIJI?

Matukio ya askari kupigwa risasi wilayani humo si mageni lakini mbali na askari, pia viongozi wa vijiji wapatao 18 katika wilaya hizo nao wameuawa kwa kupigwa risasi. Inauma sana!

WANANCHI WA KIBITI

Wakizungumza na Uwazi baada ya mauaji ya askari hao, baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mkengeni Kibiti, walisema kuwa, Mkoa wa Pwani umekuwa si salama kwa maisha ya watu na mali zao kwani mpaka sasa, hesabu za haraka zinaonesha kuwa, unaongoza kwa mauaji ya risasi huku viongozi na askari wakiwa wanashika namba kubwa.

“Mimi kumbukumbu inaniambia, katika Mkoa wa Pwani na wilaya zake hizo, tayari askari kumi na saba (17) wameshauawa kwa kupigwa risasi na viongozi wa vijiji kama kumi na nane (18) nao pia wameuawa.

“Hii idadi ni kubwa sana, siamini kama kuna mkoa umefikia, labda Dar es Salaam kwa sababu ya ukubwa wake wa makazi, lakini nje ya hapo sidhani,” alisema mkazi mmoja wa aliyejitambulisha kwa jina la Masaidi Khalidi. Anaongeza:

“Jeshi la Polisi likitaka kumalizana na hii hali ni kuingiza ushirikiano na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waingie msituni na kufanya kazi kama wako vitani, naamini wahalifu wote watakamatwa na itajulikana nguvu yao ilipo.”

KUHUSU POLISI NI KWELI?

Kufuatia madai hayo, Uwazi lilichimba kwenye kumbukumbu za nyuma na kukuta kweli idadi ya askari waliopoteza maisha Pwani inatisha, lakini pia idadi ya viongozi wa vijiji ambao pia wameuawa kwa kupigwa risasi pia inatisha.

WALIANZA POLISI HAWA

Juni 11, 2014, watu wenye silaha za jadi walivamia Kituo cha Polisi cha Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga mkoani hapa na kumuua kwa kumshambulia kwa mapanga askari Joseph Ngonyani kisha kupora bunduki tatu aina ya SMG na risasi 50.

Mwaka 2015 nao ukaingia na balaa, matukio ya mauaji yaliendelea  kuukabili mkoa huu kufuatia askari wanne wa Kituo cha Polisi Ikwiriri kuvamiwa na kuuawa na watu ambao jeshi hilo lilisema ni majambazi. Askari hao ni Koplo Yahya Malima, Koplo Tito Mapunda,  Koplo Gaston Lupanga na Koplo Khatib Ame Pandu.

KIZUIZI CHA POLISI VIKINDU

Machi 30, 2015, saa 1:30 usiku wa kuelekea Sikukuu ya Pasaka, askari wawili waliuawa kwenye kizuizi cha barabarani katika Kijiji cha Kipara, maeneo ya Vikindu, Pwani. Waliouawa ni Sajenti Michael Aaron Tuheri na Koplo Francis Mkinga. Mauaji hayo yaliliacha jeshi la polisi nchini katika hali ya huzuni huku yakifananishwa na yale yaliyotokea katika vituo mbalimbali vya polisi nchini.

IKWIRIRI TENA

Januari 21, 2016, watu wasiojulikana walivamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani humu na kuwaua askari wawili, Koplo Edgar na WP Judith na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo.

KIJIJINI VIKINDU

Agosti 26, 2016, askari wa ngazi ya juu katika kikosi cha kupambana na majambazi nchini, SSP Thomas Njiku aliuawa kwenye Kijiji cha Vikindu, Mkuranga akiwa katika oparesheni ya kuwasaka watu waliodaiwa kufanya uhalifu maeneo na Mbande, Temeke jijini Dar es Salaam.

JARIBU MPAKANI

Februari 22, 2017, taarifa kutoka Kibiti zilisema, mpelelezi wa wilaya hiyo (OC-CID), SP Peter Kubezya aliuawa kwa kupigwa risasi ya tumboni na watu hao wanaosadikiwa kuwa ni wahalifu. Tukio hilo lilijiri usiku wa saa 1, ambapo watu sita wenye bunduki  zinazosadikiwa kuwa ni aina ya Sub Machine Gun (SMG) walivamia Kituo cha Kutoza Ushuru wa Mazao ya Kilimo na Misitu Kijiji cha Jaribu Mpakani na kumuua kwa kumpiga risasi afande huyo na raia wengine wawili.

KUHUSU VIONGOZI WA VIJIJI

Kwa upande wa viongozi wa vijiji si rahisi kuamini lakini ndiyo ukweli ulivyo kwamba, idadi yao ilifikia kumi na nane (18) wakiwa wameuawa kwa nyakati tofauti. Usiku wa Machi 28, mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Makondeko, Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini, Emmanuel Lukanga aliuawa kwa kupigwa risasi.

MUDA MCHACHE KABLA

Akizungumza na Uwazi, kwenye mazishi ya kiongozi huyo, Katibu Kata wa Ikwiriri Kaskazini, Sauda Mningi alisema saa chache kabla ya Lukanga kufikwa na mauti walikuwa kwenye kikao cha kujadili suala la ulinzi na usalama wa eneo hilo.

STAILI YAO YA KUUA

Staili ya watoa roho hao ni kuua kwa risasi wakitumia bunduki aina ya SMG bila kuchukua pesa wala mali yoyote kutoka kwa marehemu huku wakiwa wamevaa kininja na wakitumia bodaboda hali inayotafsirika kuwa, ni mauaji ya visasi. “Huku jamani sisi wananchi, giza linapoingia wasiwasi tupu. Tunakuwa hatujui nani atauawa. Hawa watu wameanza zamani, tangu mwaka 2015,” alisema kiongozi mmoja huku akiomba hifadhi ya jina lake.

VIONGOZI WALIPOKEA MESEJI

Ilielezwa kuwa, viongozi mbalimbali wakitimia 18 wa vijiji vya wilaya hizo walianza kupokea meseji za vitisho kutoka kwa kundi moja la wahalifu wakidai roho zao ziko mikononi mwao, watawaua mmoja baada ya mwingine.

MAUAJI YA KWANZA

Mapema mwaka 2015, kundi hilo lilidaiwa kumuua kwa kumchinja karani wa Mahakama ya Mwanzo Mkuranga aliyetajwa kwa jina moja la Pazi.

MACHI MOSI, 2016 Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao waliovamia nyumbani kwake. JULAI 17, 2016 Mwenyekiti wa Kijiji cha Kimanzichana, Ramadhani Mkagile naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao waliofika nyumbani kwake kwa njia ya bodaboda wakiwa wamevaa kininja.

AGOSTI 12, 2016 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mkuruwili wilayani Mkuranga,  Salum Kiswamba ambaye pia alikuwa imamu wa msikiti, naye aliuawa nje ya nyumba yake kwa kupigwa risasi.

OKTOBA 6, 2016 Katika Kijiji cha Kimanzichana, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Bakari Simkole akiwa ofisini, alipigwa risasi ya kifuani na kufariki dunia papohapo. OKTOBA 24, 2016 Kundi hilohilo lilimuua Mtendaji wa Kijiji cha Nyambunda, Ally Omar kwa kumpiga risasi akiwa nje ya nyumba yake.

DESEMBA 6, 2016 Mohammed Ally Thabiti ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyambunda, Kijiji cha Nyang’hundu naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu waliovaa kininja.

WAWILI WALIUAWA

Nyuma ya mauaji ya viongozi hao wa kijiji hicho, waliuawa viongozi wengine wawili ambao Uwazi halikupata majina yao wala tarehe. Kijiji kikabaki hakina viongozi. JANUARI, 2017 Mauaji ya viongozi hao hayakuishia hapo, Januari mwaka huu, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda Wilaya ya Kibiti mkoani hapa, Said Mkandambuli naye aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi hilo, nyumba yake imeota majani baada ya familia yake kukimbia.

JANUARI 19, 2017

Katibu Mtendaji wa Kijiji cha Nkwandala wilayani Kibiti (zamani kilikuwa katika Wilaya ya Mkuranga), Oswald Mrope naye aliuawa na wauaji hao ambao walimkuta akiwa amejipumzisha nje ya nyumba yake.

FEBRUARI 9, 2017 Saa 6 usiku, kundi hilo linaloaminika kuwa ndilo linalotoa roho za viongozi, lilimuua Kamanda wa Mgambo Kata ya Bupu, Mussa Koti na kuichoma moto nyumba yake.

SIKU HIYOHIYO

Wauaji hao siku hiyohiyo walimuua kwa risasi, Kamanda Msaidizi wa Mgambo, Mohammed Cheleu na kuzichoma moto nyumba zake mbili, ya mke mdogo na mke mkubwa na kuacha ujumbe kupitia vipeperushi kuwa, roho zaidi zitaendelea kutolewa.

FEBRUARI 21, 2017 Watu watatu walipoteza maisha (mmoja kati yao akiwa OC CID wa Kibiti) baada ya kuuawa na  kundi la watu wanaodhaniwa ni walewale wakiwa na silaha aina ya SMG/SAR. Mbali na OC-CID, wengine  ni Peter Kitundu aliyekuwa Mkaguzi wa Maliasili Kituo cha Jaribu  Mpakani na mgambo  aliyekuwa akifanya kazi za ulinzi kwenye kizuizi hicho, Athumani Ngambo.

MACHI 12, 2017

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kazamoyo, Hemed Njiwa naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu hao akiwa nyumbani kwake.

GAZETI LA UWAZI

Gazeti la Uwazi, mara kadhaa tangu mwaka 2015 limekuwa likiandika habari za watu waliopo kwenye baadhi ya misitu kwenye wilaya hizo kwamba, ndiyo wanaopanga mauaji ya kutisha ya polisi kwa lengo la kuchukua silaha kwa matumizi wanayoyajua wao, ikiwemo kuwaua viongozi.

KINACHOTOKEA

Hata hivyo, licha ya mambo kuwa wazi, bado Uwazi limewahi kuitwa na uongozi serikalini na kuhojiwa juu ya habari hizo, hasahasa habari iliyowahi kuandikwa Julai 17, jana kwenye gazeti ndugu na hili, Amani yenye kichwa cha habari;

WANAOJIITA AL QAEDA WAUA IMAMU WA MSIKITI.

Katika habari hiyo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mkuruwili Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, Salum Kiswamba ambaye pia alikuwa imamu wa msikiti wa eneo hilo, aliuawa nje ya nyumba yake kwa kupigwa risasi na watu waliovalia kininja waliokuwa kwenye bodaboda.

Katika kusema ukweli huu, baadhi ya viongozi serikalini hutaka kuamini kuwa, magazeti ya Global Publishers yanazua hofu huku ukweli ukiwa unaonekana.

UWAZI NA BARUA KWA MAGUFULI

Pia, Uwazi liliwahi kumwandikia barua Rais Dk. John Pombe Magufuli ikimweleza namna wananchi wa mkoa huo, hasa Mkuranga, Kibiti na Rufiji wanavyoishi kwa wasiwasi wakimwomba msaada wake kwa imani kwamba, anaweza kutuma jeshi maalum na kuwaangamiza wahalifu hao.

KAMANDA KOVA ALIWAHI KUSEMA HAYA

Kabla ya kustaafu kwake, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova aliwahi kusema kuwa kuna mtu anaitwa Hery, alihusika  katika kufadhili matukio ya mauaji huko Amboni (Tanga), Mkuranga (Pwani) na Stakishari (Dar) na mengineyo lakini aliongeza jeshi la polisi kwa  kutumia kikosi cha intelijensia kiliweza kubaini nyendo zake na kuinasa picha yake.

UWAZI LILISEMA HOFU YATANDA MKURANGA

Gazeti hilihili liliwahi kuandika mwaka 2015 kuwa, hofu kubwa imetanda wilayani Mkuranga hasa katika Kijiji cha Mamndi Mkongo kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa  kushirikiana na wale wa Mkoa wa Pwani kunasa silaha  za kivita zikiwa zimefukiwa kwenye shimo msituni. Tukio hilo  la unasaji wa silaha lilifanikiwa Agosti 29,  2015 katika msitu  mmoja uliopo  katika kijiji hicho  kilichopo umbali wa kilomita 23  kutoka mjini Mkuranga.

SILAHA ZILIZOKUTWA

Uwazi lilizungumza na kamati ya ulinzi na usalama kijijini hapo na kusema silaha zilizokutwa ni bunduki za kivita aina ya AK-47 (moja), SRA  (mbili), RPG (mbili) Greana (moja) na risasi 388, tambi za milipuko mikali, kitabu cha muongozo wa kijeshi, kemikali za kutengenezea mabomu ya kutupa kwa mkono na kitabu chenye maelekezo ya namna ya kujibadili mwanaume kuwa mwanamke au mwanamke kuwa mwanaume.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Uwazi, wamemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kufuatilia kwa kina matukio hayo kwani yanawatia hofu wananchi.

KUTOKA KWA MHARIRI

Ni vyema jeshi la polisi likaongeza nguvu ya ulinzi ili kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Tunalaani mauaji haya kwa nguvu kubwa tukiamini kwamba, waliouawa hawakuwa na hatia!

Credit - Uwazi/Globalpublishers

Ile Kesi ya Scorpion Mtoboa Macho Yafikia Hatua Hii..!!!

$
0
0

Kesi ya kujeruhi na unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili Salum Njwete ‘Scorpion’, anayedaiwa kumjeruhi kwa kumchoma visu na kumsababishia upofu Said Mrisho, jana imeshindwa kuendelea baada ya shahidi upande wa Jamhuri kushindwa kutokea mahakamani.

Katika viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kama kawaida umati uliokuwa ukitaka kusikiliza kesi hiyo ulifurika mapema asubuhi kutaka kujua kinachoendelea.

Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akitokea Gereza la Ukonga na kuhifadhiwa kwa muda kwenye mahabusu ya mahakama hiyo.

Majira ya saa nne kamili chumba cha mahakama kilikuwa tayari kimeandaliwa kwa ajili ya kesi hiyo ambapo Wakili wa Scorpion, Juma Nasoro, Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga, Hakimu anayeendesha kesi hiyo, Frola Haule na makarani wote walikuwa tayari kwenye chumba inapoendeshwa kesi hiyo wakimsubiri mtuhumiwa huyo apelekwe ili kesi iendelee.

Baadaye maafande wa magereza zaidi ya nane wengine wakiwa na silaha walimchomoa Scorpion na kumpeleka kwenye chumba cha mashitaka mbele ya hakimu, Frola Haule.

Scorpion akiwa kizimbani, Wakili Katuga aliiambia mahakama hiyo kuwa kesi hiyo ilifika mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa nane upande wa Jamhuri kutoa ushahidi wake.

 Wakili huyo alisema shahidi huyo alitoa udhuru mahakani hapo kuwa asingeweza kufika mahakamani hapo kwa kuwa anaumwa.

Baada ya ombi la wakili huyo, mahakama hiyo iliahirisha kesi hiyo mpaka Mei 2 mwaka huu ambapo Scorpion alirudishwa rumande.


Alichosema Zitto Kabwe Baada ya Mauaji ya Polisi 8, Kibiti..!!!

$
0
0

Baada ya vifo  vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha tarehe 13 Aprili, 2017 katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Jana Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe  kupitia akaunti yake ya Twitter amesema haya juu ya Polisi 8 waliouawa

Mkuranga, Kibiti na Rufiji ( #MKIRU ) ni eneo ambalo lazima kazi kubwa ya ujasusi wa kiusalama ifanyike. @mwigulunchemba1 simamia hili haswa
Nimetazama magazeti makuu Leo, English and Swahili, naona uzito wa usalama wa eneo la #MKIRU unakuwa mdogo. Makosa makubwa @mwigulunchemba1

Hii Imetokea ..BBC Wakosa Habari za Kutangaza..!!!!

$
0
0

BBC ni moja kati ya shirika kubwa ambalo hufaamika kwa kutoa taarifa za habari mbalimbali,lkn mnamo 18 April 1930 ikiwa ni miaka 87 imepita shirika hilo lilikosa habari ya kutangaza! ilipofika muda wa kutangaza habari mtangazaji alisema "hakuna habari" hivyo walitumia muda huo kurusha vipindi vyengine.moja kati ya sababu iliyosababisha kukosa habari ni teknolojia ya miaka hiyo!

Chanzo BBC wenyewe

Baada ya Dakika 90 Wachezaji wa Bayern Munich Wavamia Chumba cha Muamuzi, Polisi Waingilia

$
0
0

Katika kile kinachoonekana kutoridhishwa na maamuzi ya refa wa mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Bayern Munich Victor Kassai, baadhi ya wachezaji wakiongozwa na mshambuliaji wa timu hiyo Roberto Lewandoski walivamia vyumba vya kubadilishia nguo waamuzi baada ya mchezo huo.

Taarifa zinasema Artulo Vidal, Thiago Alcantara nao walikuwepo kwenye kikundi hicho cha wachezaji wa Bayern ambao waliingia katika vyumba hivyo vya kubadilishia nguo waamuzi kabla ya polisi kuitwa na kuwalazimisha kuondoka kwa nguvu katika vyumba hivyo.

Kipigo cha bao 4 kwa 2 katika uwanja wa Santiago Bernabeu kiliwafanya Bayern Muinch kufungasha kilicho chao katika michuano hiyo na kurudi kwao Ujerumani lakini kadi nyekundu aliyopata Artulo Vidal na goli lilioonekana la offside alilofunga Ronald liliwafanga Bayern Munich wakasirike sana.

Inasemekana wachezaji hao watatu wlivamia ofisi hizo na kuanza kumtukana muamuzi huyo huku Vidal akienda mbali zaidi kwa kumsogelea, wakati wakiendelea kufanya hivyo muamuzi aliwaomba waondoke chumba hicho lakini wachezaji hao walikataa na kuendelea kumtupia maneno yeye na wenzake.

Kitendo walichofanya nyota hao kinaweza kuwaingiza matatani kwani vhama cha soka barani humo UEFA kinaweza kuchunguza tukio hilo na ikibainika walitenda kosa baasi adhabu itawahusu.

Magonjwa Haya, Huathiri Nguvu za Kiume na Kuharibu Kizazi kwa Wote, Wake na Waume...!!!

$
0
0


KUNA magonjwa mengi tofauti ya zinaa, lakini yale ambayo yameenea sana ni kisonono, kaswende, klamdia, kankroidi, utando mweupe, Virusi Vya Ukimwi  na Ukimwi. Magonjwa mengi ya zinaa ni kwamba dalili zake hazionekani kwa urahisi na kama yasipotibiwa kikamilifu yanaweza kuleta madhara makubwa. Tuchambue kwa ufupi magonjwa hayo:

Kisonono:

Huchukua muda wa siku moja hadi 14 tangu kuambukizwa mpaka kuonyesha dalili za kuumwa. Kwa wanawake dalili za kisonono ni maumivu chini ya tumbo ambayo yanaweza kuambatana na homa na kutokwa uchafu ukeni. Wapo wanawake wengine ambao hawaoni dalili zozote. Athari yake kwa mwanamke ni kuziba mirija ya kupitisha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi, na vilevile ugumba.

Kwa mtoto aliye tumboni mwa mama mjamzito kisonono cha mama yake kinaweza kusababisha upofu. Kwa mwanaume athari yake ni kuziba mirija ya kupitisha mkojo. Kwa wanaume dalili ni kutokwa na usaha uumeni na kupata maumivu wakati wa kukojoa.

Kaswende:

Dalili ya kaswende kwa mwanamke ni vidonda sehemu za siri hasa kwenye mashavu ya uke na sehemu ya njia ya haja kubwa, pamoja na sundosundo sehemu ya siri. Kwa mwanaume dalili ni vidonda. Mara nyingi kimoja kwenye kichwa cha uume, kwenye kishina cha uume na kuzunguka njia ya haja kubwa.

Pia mwanaume anaweza kupata sundosundo sehemu za siri. Ugonjwa huu husababisha matatizo ya moyo na kuharibu ubongo na kuzaa watoto walemavu.

Klamdia:

Dalili yake kwa mwanamke mara nyingi siyo rahisi kuonekana. Kwa mwanaume dalili ni kupata maumivu wakati wa kukojoa, na kukojoa mara kwa mara. Athari kwa mwanamke ni kuziba kwa mirija ya kupitisha mayai na mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi. Mimba hizi kuhatarisha maisha ya mama na kuleta ugumba vinaweza kutokea.

UtasaKankroidi:

Dalili yake ni vidonda sehemu za siri vinavyokuwa na maumivu makali, maumivu wakati mkojo unapopita kwenye vidonda na kuvimba tezi sehemu za siri. Tezi huweza kupasuka na kutoa uchafu na maumivu makali. Utando mweupe: Dalili kwa mwanamke ni kutokwa na uchafu ukeni (kama maziwa yaliyoganda), kuwashwa na kuwa na michubuko sehemu za siri. Kwa mwanaume ni kuwashwa sehemu za siri na kusikia maumivu wakati wa kukojoa. Athari ni maumivu wakati wa kujamiiana.

Virusi Vya Ukimwi:

Katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa hakuna dalili maalum. Hatua hii inaweza kuchukua mpaka miaka kumi. Lakini mara mtu anapoanza kuugua Ukimwi dalili zinakuwa nyingi. Pamoja na kupungua kinga ya mwili, kupungua uzito na kuumwa mara kwa mara.

Jifunze Jinsi ya Kupika Kababu za Mayai na Nyama ya Kusaga..!!!

$
0
0

NI wiki nyingine tena mpenzi msomaji tunakutana tena katika safu hii ya Mapishi ya Leo ambapo tunajifunza jinsi ya kuandaa kababu za mayai na nyama ya kusaga, ungana nami.

MAHITAJI


  • Nyama ya kusaga (kiasi unachotaka)
  • Mayai 5
  • Vipande vya mikate
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga nusu kijiko cha chai
  • Pilipili nzima iliyosagwa nusu kijiko cha chai
  • Ndimu kipande
  • Mafuta ya kupikia
  • Mayai 2 ya kuchomea kababu
  • Bizari iliyosagwa
  • Vitunguu swaumu na tangawizi ya kusaga


JINSI YA KUPIKA
– Chemsha mayai mpaka yaive vizuri na uyamenye
– Chemsha nyama weka ndimu na chumvi.
-Ikikauka ichanganye na viungo vyote mpaka ichanganyike vizuri.
-Weka vipande vya mkate ambavyo unatakiwa uvivuruge kwa kuvishikia kwa maji kidogokidogo
-Vunja yai moja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa nyama.
-Fanya mviringo na uweke kishimo cha kuweka yai ulilochemsha.
-Lifunge ndani vizuri yai kwenye nyama lisionekane.
-Piga yai kwenye kibakuli na uchovye mviringo kisha anza kuzikaanga ndani ya mafuta ambayo tayari yana moto.
-Ikiiva itoe na uiweke kwenye chujio kuchuja mafuta na itakuwa tayari kwa kula.

Jinsi Ya Kuwa Na Deti Ya Kwanza Na Mwanamke Ambayo Itampendeza..!!!

$
0
0

Kusema ule ukweli, hakuna kitu kama formula ama mbinu ambayo inaweza kukufanya upate deti ambayo imeshamiri na bora zaidi. Mwanzo ukiplan kutumia ujanja na gemu katika deti yako ya kwanza, unaweza usifike popote katika deti hio. Lakini hii haimaanishi ya kuwa hakuna mbinu ambazo unaweza kuzitumia kuhakikisha ya kuwa unakuwa na deti muruwa kabisa. Hivyo basi tumekuja na baadhi ya mambo ya kufanya wakati ambapo utatoka deti kwa mara ya kwanza na mwanamke.

#1 Kuwa wewe mwenyewe
Inaweza kuwa na ukweli kiasi flani ya kwamba ni lazima uonyeshe mvuto kwa mara ya kwanza unapotoka deti na mwanamke, lakini hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kuingiwa na wasiwasi kutimiza jambo hilo. Mwanzo, kuwa wewe mwenyewe ni njia rahisi ambayo unaweza kuitumia kumteka mwanamke. Pia hii haimaanishi ya kuwa unapaswa kujifanya kuwa mtu ambaye hafanani na hulka yake. Kando na hayo yote, kama utaendelea kuiga tabia ambayo haifanani na wewe usiku mzima, utamfanya afall in love na mtu mwingine. Hivyo basi ni bora zaidi uwe wewe mwenyewe, na uendelee kuanzia hapo.

#2 Pumua
Haina haja ya wewe kujistress na deti yako ya kwanza ama kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa. Deti za kwanza kwa kawaida huwa si za kueleza kwa kina, bali ni kupata kujuana wewe na huyo mwanamke. So hata kama kuna jambo ambalo linaweza kufanyika usiku huo, wewe pumua na kuchulia kosa lolote ambalo linaweza kutendeka kama mwanzo wa gumzo lako ama unaweza kufanya mzaha jambo hilo wakati mwingine ambapo utakutana katika deti ya pili. Pia, usisahau kuonyesha confidence na uonyeshe kuwa wewe ni mwanaume alpha.

#3 Chagua sehemu bora
Kama tulivyotangulia kusema awali, deti za kwanza huwa lengo lake kuu huwa ni kujuana zaidi kati yako na huyo mpenzi wako. So, weka simu yako kando usiku huo, msikilize kwa makini mwanamke uliyetoka naye deti na uhakikishe ya kuwa umechagua sehemu ambayo nyote wawili mtaiona bora ili muweze kutangamana vizuri pamoja. Hii inamaanisha kuwa hupaswi kwenda deti ya kwanza na mwanamke katika sinema, concerts ama sehemu za michezo.

#4 Uliza maswali
Amini usiamini, kitu rahisi kama kuonyesha interest ya uhakika kwa mwanamke katika deti kunaweza kumfanya apendezwe na wewe kwa muda mfupi sana. Haijali kama utamuuliza swali tata au lisiloeleweka. Ilimradi tu uendeleze mazungumzo yenu wawili huku ukimsikiliza kwa umakini, utaonyesha idhibati kuwa wewe ni mwanaume anayejali. Njia hii unaweza kumjua zaidi mwanamke aina hii na pia kupata ujuzi wa kuongea na wanawake kwa ujumla, na kuwa na uunganisho wa haraka katika deti zako.

#5 Jienjoy
Hii inaenda sambamba na pointi tulioieleza awali. Wakati mwingi, wanaume wengi huingiwa na wasiwasi na kibaridi wanapotoka deti kwa mara ya kwanza kiasi cha kuwa wanasahau kujiachilia na kuenjoy deti hio ambayo inaendelea. Unapaswa kujua kuwa mwanamke anayetoka deti na wewe hatavutiwa kwako kama hutatabasamu wala kucheka na yeye hata kwa mara moja.Tofauti na kama utamwonyesha mwanamke kuwa unajienjoy na kuburudika na uwepo wake, basi naye pia ataenjoy company yako wakati wote. So, jaribu kufanya mizaha, mchekeshe na mwonyeshe ishara za mapenzi kadri uwezavyo. Usisahau kumwambia kupitia jumbe au simu kuwa ulienjoy kuwa naye katika deti hio.

Upo!

Mapenzi na Sababu Tisa za Kwa Nini Watu Hujikuta Wanapendana..!!!

$
0
0

Mapenzi ni nini? Kuuliza swali hili kwa mtu yeyote atakupa majibu yasiyokuwa na kikomo. Mapenzi ni dhana pana ambayo kila mtu anakuwa na mtizamo tofauti wa kueleza. 

Kiufupi mapenzi ni jambo lisiloeleweka, jambo lisilo na mwisho. Na kwa kuwa mpenzi wako anachangia pakubwa katika kuyaendeleza mahusiano yenu yawe marefu ya kufaana, furaha, na hata kukuwezesha kuwa na maisha bora, tumekuja na tafiti tulizilokusanya kukupa sababu za kisaikolojia ambazo zinachangia wapenzi wawili wapendane.

Ok, kabla ya kuorodhesha orodha nzima je  ulikuwa ukijua kuwa homoni zako, maslahi, na hata sura ya mzazi wako inachangia pakubwa kwa kumchagua yule ambaye atakuwa mpenzi wako?

Zama nami...

Sababu za kwa nini watu huangukia katika mapenzi


1. Kama mnafanana ile sana
Tafiti zinaonyesha ya kuwa ile dhana ya kuwa "watu tofauti huvutiana" haina msingi. Badala yake wale watu ambao wanagawa mambo mapana, kama vile hulka, wana urahisi wa kuhisi sawa katika maisha yao ya kila siku. Utafiti huu uliweza kuthibitishwa na Gian Gonzaga, mwandishi mkuu katika eHarmony. Utafiti huu ni wa uhakika kwani katika maisha ya kawaida  ya mapenzi, iwapo wapenzi wanagawa hulka, moja maisha yao ya kimapenzi huwa marefu na ya kufaana.

2. Kama unafanana kama mzazi wake
Kulingana na mwana saikolojia David Perrett kutoka chuo kikuu cha St. Andrews amegundua ya kuwa watu huvutiwa na jinsia ile nyingine ambayo wana nywele na rangi ya macho ambayo ni sawia na ya mzazi wake wa ile jinsia tofauti. Pia katika tafiti yake amegundua kuwa "wanawake ambao walizaliwa na wazazi ambao ni 30+ hawavutiwi sana na  wanaume vijana ila wale wakubwa, tofauti na wanawake waliozaliwa na wazazi wadogo." Katika wanaume, Perrett alikiri kuwa kuchagua mpenzi kisura kwa mwanaume kunachangiwa pakubwa na umri wa mzazi wake wa kile.

3. Kama unanukia ipasavyo
Katika mapenzi, chuo kikuu cha California kilifanya utafiti kikagundua ya kuwa mwanamke ambaye ameingia siku zake ya uzazi (ovulating) huwa wanapenda na kuvutiwa sana na harufu ya tsheti iliyovaliwa na mwanaume ambaye ana kiwango kikuu cha homoni za testosterone. Pia wanawake hao hao walikiri kupenda wanaume ambao wana taya ndefu.

4. Kama utawacha mikono yako na kifua chako wazi
Kuweka mikono yako ndani ya mifuko na kuyaweka mabega yako ndani unatoa ishara ya kuwa hujiskii kuongea. Lakini iwapo unaongea huku mikono yako umeiweka wazi na kusimama wima kifua mbele kunaonyesha ya kuwa ukotayari kwa lolote lile.

5. Kama mtaangaliana machoni kwa dakika mbili
Wakati mwanasaikolojia Joan Kellerman katika chuo kikuu cha Massachusetts alipowaagiza wanafunzi 72 wawili wawili waangaliane kwa dakika mbili mfululizo, waliripoti kuongezeka kwa hisia za upendo na mapenzi kwa huyo mwenzake. Hii ni idhibati tosha ya kuonyesha ya kuwa muda mrefu wa kuangaliana macho kunaweza kukakuunganisha na mtu na hata kuchangia hisia za mapenzi.

6. Kama unamiliki mbwa
Katika majaribio katika chuo kikuu cha Michigan, wanawake hupenda kusoma tabia za wanaume. Iwapo kuna habari ambayo inahusisha mwanaume ambaye anamiliki mbwa, wanawake wanampa kiwango cha juu cha uhusiano mrefu wa kuvutia. Hii ni kwa sababu watafiti walivumbua ya kuwa umiliki mifugo wa nyumbani inaweza kuwa ishara ya mtu ambaye ni mmakinifu na mwenye kuwa na hulka ya kupenda kujitweka majukumu katika mahusiano.

7. Kama unacheza mziki
Watafiti katika nchi ya Ufaransa wamegundua kuwa uhusisho wa mziki kunahusiana na uchaguzi wa mapenzi. Katika majaribio, mwanaume aliyebeba gita ama begi la mchezo aliuliza wanawake 300 namba zao za simu. Mwanaume aliyebeba gita aliweza kupewa namba nyingi zaidi kuliko alipobeba begi la mchezo.

8. Kama utavalia nguo nyekundu
Katika utafiti uliofanywa Slovakia, wanawake ambao walivalia nguo za rangi nyekundu walifanikiwa zaidi katika mchezo wa kufanya mapenzi. Hii ilichangiwa pakubwa na ishara ya kuwa nguo nyekundu wanawake wengi wanaitumia kama njia ya kuwavutia wanaume wenye uwezo. 

9. Kama una nywele flani katika uso wako
Katika utafiti wa mapenzi uliofanywa nchini Australia uligundua kuwa wanawake huvutiwa zaidi na wanaume ambao wana ndevu wastani katika uso wao. Waligundua kuwa mwanaume mwenye ndevu nyingi ama ambaye amenyoa uso mzima hawavutii kwao. Pia watafiti waligundua kuwa mwanaume mwenye nywele nyingi zaidi, huonekana na wanawake kuwa kiume zaidi.

Maiti za Wahamiaji Zaokotwa Baharini

$
0
0

Maiti za wahamiaji zimekutwa katika bahari ya Mediterania. 

Kwa mujibu wa habari,maiti za wahamiaji hao zilipatwa na mvuvi katika bahari hiyo. 

Kati ya maiti 28 nne zimetambulika kuwa ni za wanawake. 

Ripoti zinaonyesha kuwa wahamiaji hao walikuwa wanajaribu kuvuka bahari ya Mediterania kutoka Libya kuelekea Ulaya. 

Mtumbwi huo unasemekana kupinduka na kusababisha wahamiaji hao kupoteza maisha baada ya kuzama huku wengine walipoteza maisha kutokana na kukaa kwa njaa kwa wakati mrefu. 

Ni zaidi ya wahamiaji haramu 100 wameweza kupita katika bahari hiyo kuelekea Italia ndani ya miaka mitatu iliyopita. 

Vilevile ni zaidi ya wahamiaji mia saba wamepoteza maisha wakijaribu kuvuka bahari hiyo. 

Imebainika: Kumbe Marekani haikutuma meli za kivita Korea Kaskazini........Vilikuwa ni Vitisho Kwa Korea Kaskazini

$
0
0

Marekani na Korea Kaskazini zimeendelea kujibizana vikali, ambapo safari ya meli za kivita za Marekani ikiwemo meli yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita ya Carl Vinson imeibua hisia kubwa na uwezekano wa Marekani kufanya shambulio la mapema kujaribu kulemaza mfumo wa kijeshi wa Korea Kaskazini.


Wakati taarifa hizo zikienea, imebainika kwamba meli hizo za kivita za Marekani hazikuwa zinaelekea upande wa Korea Kaskazini kama ilivyoripotiwa awali, bali zilikuwa zinaelekea eneo tofauti.


Awali iliripotiwa kuwa, Jeshi la wanamaji la Marekani lilikuwa likielekea Korea kama hatua ya kuionya Korea Kaskazini, ambapo Rais Trump pia alitangaza kwamba kundi kubwa la meli za kivita lilikuwa likitumwa eneo hilo, hivyo imebainika kuwa si kweli.


Hadi kufikia mwishoni mwa wiki, meli hizo zilikuwa zimesafiri mbali sana na rasi ya Korea na zilikuwa zinapitia mlango wa bahari wa Sunda kuingia katika Bahari ya Hindi.

Wakuu wa jeshi la wanamaji la Marekani katika Bahari ya Pasifiki walisema Jumanne kwamba walikuwa wamefutilia mbali safari ya meli hizo katika bandari ya Perth.

Kundi hilo la meli sasa "linaelekea Magharibi mwa Pasiki kama lilivyoamrishwa".

Bado haijabainika iwapo kulitokea sintofahamu katika mawasiliano au labla Marekani ilipotosha watu makusudi kujaribu kumtia wasiwasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.


Aidha, Marekani imesema Korea Kaskazini ilipotekeleza jaribio la kombora ambalo lilifeli mwishoni mwa wiki ilikuwa na nia fulani ya kiuchokozi.


Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis amesema Marekani inafanya kazi kwa karibu na China kukabiliana na Korea Kaskazini. Amesema kuwa jaribio hilo lililofanywa na Korea Kaskazini lilikuwa la kutojali na ilifanya hivyo kwa kuichokoza Marekani.


Aidha, Korea Kaskazini wamesema kuwa itafanya majaribio ya makombora kila wiki na pia ikaonya kwamba kutatokea vita kamili iwapo Marekani itaichukulia hatua za kijeshi.


“Iwapo Marekani wanapanga kutushambulia, tutajibu kwa shambulio la nyuklia kwa mtindo na njia yetu wenyewe,” amesema Naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini, Han Song-ryol


Pande zote mbili zimekuwa zikijibizana vikali baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio hilo la makombora.


Bw Mattis alisema kwamba jaribio hilo la Jumapili halikuhusisha kombora linaloweza kuruka kutoka bara moja hadi jingine lakini bado lilikuwa ishara ya kutojali.


“Inadhihirisha ni kwa nini tunafanya kazi kwa karibu kwa sasa na Wachina…tunajaribu kudhibiti hali hii na lengo letu ni kumaliza silaha za nyuklia katika rasi ya Korea,” alisema.

Credit:BBC

Jinsi Ya Kunyoa Ndevu kwa Ufanisi na Kuepukana na Vipele ..!!!

$
0
0

Moja  ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa. Ndevu huwafanya wanaume wengi kuhisi kuwa ni tatizo kubwa sana kwao kwani wakati wa kuzinyoa huwa ni tatizo kubwa kutokana na wengine kuweza kupata matatizo wakati wa kunyoa ndevu.

Ili kuondoa matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka katika aina Fulani ya raha kubwa. Chagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi yako, kuna aina nyingi sana za mashine za kunyolea pamoja na nyembe zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa kuzingatia mahitaji yako hasa ya aina ya ndevu.

Weka uso safi na usio mchafu, Safisha kabla ya kunyoa, hii inakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.

Usisahau kuloweka kidevu chako vyema, hii inasaidia wenye kupita kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.

Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia sana kufungua vishimo vya vinyweleo, pia unaweza kupata masaji ya chapchap katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.

Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi yako na chagua linalostahili unalotaka,  jipake kiasi cha kutosha katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.

Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote,tumia moistrurizer baada ya kunyoa.

Steve Nyerere Ayasusia Maandamano ya Bongo Movie, Aanika Haya..!!!!

$
0
0

KUFUATIA maandamano ya wasanii wa Filamu nchini, Bongo Movie, ambao wameandamana jana katika mtaa wa Aggrey Kariakoo  wakipinga uingizwaji wa filamu za nje na urudufishwaji wa filamu za ndani huku wakiwataka wamachinga wanaouza filamu hizo waache mara moja, msanii wa tasnia hiyo Steve Mengele Nyerere amefunguka kuhusu kutoonekana kwenye tukio hilo.

Akifanya mazungumzo Steve ameeleza kuwa sababu ya yeye kutoungana na wasanii wenzake kuandamana ni kwa kuwa jambo hilo halioni kama lina tija kwake.

“Binafsi ninalipinga hili, wasanii tunataka kutumika ndivyo sivyo, siwezi tu kuambiwa kuwa kuna maandamano nikaenda.

“Tunavyosema filamu za nje zinazuia soko la ndani ni uongo, hizi filamu za nje tangu tunazaliwa zilikuwepo, tumewakuta akina Arnold Schweziniger na Rambo, filamu zao zilikuwa zinauzwa Kariakoo. Tulichukua majority yao tukatengeneza filamu zetu. Tuliwakuta Nigeria tukashindana nao tuaweza, hata za filamu za Kihindi tuliweza kushindana nazo.

“Hatujawahi kumzuia Yemi Alade afanye muziki hapa nchini ijapokuwa tuna wanamuziki wetu akina Diamond na Ali Kiba.

“Nachoweza kusema ni kwamba turudi tuangalie ni wapi tumeharibu, tuache kuingiza visingizio ambavyo havina mantiki. Wafanyabiashara Kariakoo wanauza filamu zinazouza na siyo uzalendo.

“Watanzania tumezoea kukaa mezzani na siyo maandamano. Utazuia Dar, je vipi kuhusu Arusha, Dodoma, Mwanza nk… hili janga sio la Dar es Salaam pekee ni la Tanzania nzima.

“Mpaka sasa msambazaji ni mmoja, kaelemewa mzigo, serikali iruhusu wasamazaji wengine waingine kwenye biashara hii.”

“Tumeshindwa kutengeneza radha ya Watanzania, tusiwaadhibu wafanyabiashara, tujiadhibu sisi wenyewe kwa kutengeneza filamu zisizouza.” Alisema Steve Nyerere.

Harmorapa Achafua Hali ya Hewa, ‘Adai Hamjui na Hajawahi Kumsikia Mtu Anaitwa Master J..!!!

$
0
0

Ni kweli nilichokisikia au ninaota? Eti Harmorapa hamfahamu Master J?

Rapper huyo ameonekana kuwashangaza mashabiki Jumatano hii wakati alipokuwa katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV kuwa hamfahamu mtayarishaji huyo mkongwe wa muziki nchini.

“Master J mbona simjui? Sidhani kama ni producer maana hakuna ngoma yake yoyote inayohit ambayo mimi naijua,” amesema Harmo.

Hitmaker huyo wa ‘Kiboko ya Mabishoo’ ameongeza kwa kusema kwamba ataachia wimbo wake mpya mwezi ujao ambao umetayarishwa na P-Funk huku video yake ikiongozwa na Karabani.

Kauli hiyo ya kejeli ya Harmorapa kwa Master J, imekuja baada ya hivi karibuni producer huyo wa muziki kudai kuwa Hamorapa siyo msanii direct bali ni mburudishaji kama wasanii wengine waliowahi kupita akiwemo marehemu John Walker.

Kutana na Kijana Anayetafuna Chupa na Misumari,,!!!!

$
0
0

KIJANA mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James John mkazi wa Mchikichini jijini Dar es Salaam ameonakana kuwashangaza watu wengi wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa kivutio kikubwa kwao alipoonekana  akitafuna vitu vya ajabu vikiwemo vipande vya chupa na misumari.

Mtandao huu ulipata fursa ya kuzungumza na kijana huyo ambaye alieleza kuwa yeye ni mzaliwa wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kogoma na alikuja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupanua uwezo wa kipaji chake cha sanaa.

Ameeleza kuwa katika sanaa yake anao uwezo mkubwa wa kufanya vitu vya ajabu vinavyoweza kushangaza watu kiasi cha  kutokuamini kile anachokifanya.  Miongoni mwa matukio yaliyoshuhudiwa na kamera yetu ni  kutafuna vipande vya chupa, kulalia kibao chenye misumari bila kumchoma na kutafuna misumari.

Mbali na hayo,  kijana huyo ameeleza kuwa pia anayo staili ya kubadilisha mkanda kuwa nyoka na kunywa maji lita 20 papohapo.

Katika kuonyesha shoo yake,  hutoza kiasi cha Sh. 100 na kuendelea kulingana na wananchi wanachomchangia.

Huu Ndio Ujumbe wa Diamond kwa Raymond na Fahyma..!!!

$
0
0

Diamond aibariki familia mpya ya msanii wa WCB,Rayvanny ambaye amepata mtoto wake wa kwanza wiki hii.

Ni furaha kuitwa baba au mama hasa katika kipindi ambacho ulichokuwa ukikisubiria kwa hamu. Wawili hao wamefanikiwa kupaa mtoto wa kiume ambaye wamempatia jina la Jayden.

Kupitia mtandao wa Instagram, amewapongeza Ray na Fahyma kwa kuandika, “Congrats @rayvanny & @Fahyma_ on your first Born!… Inshaallah, Mwenyez Mungu awape Baraka, awalindie na wajalie kila lenye kheri ili Mumkuze vyema @jaydanvanny ….🙏.”

Mpaka sasa wasanii wanne kutoka familia ya WCB wamefanikiwa kupata mtoto huku Harmonize akiwa bado.
Viewing all 104743 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>