Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live

BASHITE Awatesa Mawaziri Bungeni..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 23/4/2017..!!!


SIRI ya Vifo vya Askari Pwani Yafichuka..Kumbe Al Shabaab Wanahusika..Huwachukua Vijana wa Kitanzania na Kuwapeleka Somalia kwa Mafunzo Maalumu..Hivi Ndivyo Ilivyokuwa A - Z ...!!!

$
0
0

Matukio ya ujambazi wa kutumia silaha, mauaji ya polisi na viongozi wa vijiji katika wilaya za Mkuranga, Kibit na Rufiji mkoani Pwani, yanahusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia, JAMHURI limefahamishwa.

Kwa miaka minne hadi mitano iliyopita, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, amesema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

“Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi linavyokuwa gumu,” amesema.

Chanzo chetu kingine kimemtaja mtu ambaye jina lake tunalifupisha kwa kifupi kama S.B., kuwa ndiye hufanya kazi ya udalali wa kuwapeleka vijana hao nchini Somalia, huku wazazi wa watoto hao wakiambiwa kuna kazi wanakwenda kuifanya huko.

Chanzo hicho kimesema hata baada ya baadhi ya wenyeviti wa vijiji kupeleka taarifa za uhusika wa S.B. kilichofuata ni mauaji.

“S.B. alipotea hapa Ikwiriri kwa takribani miaka mitatu, hata baada ya kurejea amekuwa na mali nyingi. Mali ambazo si za kurithi na haziendani na utafutaji wa halali katika kipindi hicho kifupi. Yamekuwa yanasemwa mengi, lakini ukimgusa andaa sanda kabisa,” kimesema chanzo chetu.

Chanzo chetu kimeliambia JAMHURI kuwa vijana zaidi ya 27 kutoka maeneo mbalimbali wilayani Rufiji, wamechukuliwa kwenda kujiunga na al-Shabaab, chini ya udalali wa Bwana S.B.

Chanzo hicho kimesema mmoja na vijana ambaye alichukuliwa alishindwa aina ya kazi na akarudi.

Habari ambazo JAMHURI, limezipata zinaonesha kwamba kikundi hicho cha wauaji kimekuwa kikimtumia mtoto mdogo mwenye umri chini ya miaka 18, kuwapelekea chakula huko msituni eneo la Mparange wilayani Rufiji. Jina la mtoto huyo tunahifadhiwa kwa sababu za kitaaluma.

“Kijana huyo mdogo amekuwa akitumiwa na hao wauaji kuwapelekea chakula. Mtoto huyo amekuwa akiwahudumia pasipokuwa na simu. Akikamatwa huyo anaweza kusaidia sana upelelezi wa polisi… hapa kila mtu amejaa hofu kuhusu usalama,” kimesema chanzo chetu.

Ushauri

Baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama waliozungumza na JAMHURI wametoa ushauri kwa Serikali wa namna ya kukabiliana na wimbi la mauaji ya viongozi na polisi yanayoendelea Mkuranga, Kibiti na Rufuji mkoani Pwani.

Serikali inashauri wa kuwahusisha viongozi wa dini na wataalam wa saikolojia katika kutatua vitendo hivyo.

Akizungumza na JAMHURI, mchambuzi wa masuala ya usalama mwenye makazi yake Johannesburg, Afrika Kusini, ambaye kwa maudhui ya kiusalama tunamtambulisha kwa jina moja la Alexandre, anasema sehemu kubwa ya Afrika Mashariki inakabiliwa na matatizo ya usalama, hivyo njia pekee ya kukabiliana na tatizo hilo ni kuzihusisha pande zote.

Alexandre, anasema kumekuwapo tatizo linalohusishwa na vitendo vya ujambazi (ugaidi) katika Pwani ya Bahari ya Hindi, ukanda wa Mombasa, Tanga, Zanzibar, Mtwara, Lindi na Dar es Salaam.

“Ninashauri kwamba mamlaka; hasa vyombo vya usalama visifikirie kuhusu ‘confrontation’ na vikundi hivyo…Polisi wanapowaua, hao ‘majambazi’ nao wanahakikisha wanalipa kisasi. Katika mambo kama hayo ni busara wanasaikolojia pamoja na viongozi wa dini wakaingilia kati.

“Wanasaikolojia wanatakiwa kufanya utafiti, kwanini matukio kama hayo yamekuwa yanajirudia katika eneo hilo hilo katika siku za hivi karibuni? Hapo inawezakana kukawa na jambo kubwa zaidi…” amesema.
Hali ilivyo Mkuranga, Kibiti na Rufiji

Hali ya usalama katika maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji imezidi kuwa ya wasiwasi, huku vyombo vya usalama vikiweka zuio katika maeneo hayo.

Baadhi ya mazuio hayo ni marufuku ya kuendesha pikipiki kuanzia saa 12:00 jioni, wananchi hasa maeneo ya Ikwiriri wilayani Rufiji wamekuwa wakitakiwa kulala mapema.

Akizungumza na JAMHURI, Mbunge wa Jimbo la Kibiti, Ally Ungando, anasema hali si nzuri kutokana na ukweli kwamba wananchi hata yeye mwenyewe wako katika sintofahamu ya kiusalama.
JAMHURI: Mheshimiwa Pole kwa yanayotokea jimboni kwako
UNGANDO: Asante sana kaka, nimeshapoa!
JAMHURI: Unaweza kuzungumzia kuhusu hali ya usalama jimboni kwako?
UNGANDO: Yaani katika hili, naomba nisiwe mzungumzaji maana mwenyewe niko katika ‘danger zone’ viongozi wangu wa vijiji wanauawa, huoni kwamba anayefuata hapo ni mimi? Nisingependa kulizungumzia hata kidogo, unanitafutia balaa, sitaki kuongea kwenye vyombo vya habari, maana nikiongea utaandika kwenye magazeti, na hao wenzetu (wauaji) wanasoma. Hapa mimi nasubiri hatma yangu kaka!
JAMHURI: Umeshapata ujumbe wowote kutoka kwa wauaji?
UNGANDO: Hata kama nimepata ujumbe siwezi kusema maana hali ya usalama imekuwa tishio kwangu na wananchi wenzangu. Jitihada za pamoja zinahitajika katika kutatua tatizo hili, si kazi ya mbunge pekee.

Wakati Mbunge wa Kibiti, akizungumza na JAMHURI, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, yeye amesema hawezi kuzungumzia jambo hilo, badala yake anasubiri uchunguzi wa vyombo vya dola ukamilike.

Tukio la Kibiti

Tukio la wiki iliyopita, limechukua uhai wa polisi wanane. Nao ni Inspekta Peter Kigugu, F.3451 Koplo Francis, F.6990 PC Haruna, G.3247 PC Jackson, H.5503 PC Siwale, H.1872 PC Zacharia, H.7629 PC Maswi na H.7680 PC Ayoub.

Mauaji hayo ni mwendelezo wa matukio mengine saba ya aina hiyo yaliyotokea katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja mkoani Pwani.

Tukio la kuuawa kwa askari wanane limetokea ikiwa ni siku chache baada ya askari wa Jeshi la Polisi kuwaua kwa risasi wanaume watatu waliokuwa wamevalia baibui.

Wanaume hao ambao walikuwa na pikipiki mbili, walikuwa wakijaribu kukwepa vizuizi vya polisi vilivyokuwa vimewekwa katika Daraja la Mkapa.

Februari mwaka huu, watu watatu akiwamo Ofisa Upelelezi wa Wilaya (OC CID) ya Kibiti mkoani Pwani, Mrakibu wa Polisi, Peter Kubezya, waliuawa kwa risasi

Wengine waliouawa ni Ofisa wa Misitu ambaye alikuwa Mkaguzi wa Kituo cha Ukusanyaji Mapato ya Ushuru katika Kijiji cha Jaribu, Peter Kitundu na Rashid Mgamba ambaye ni mlinzi/mgambo ambao walipigwa risasi na walikufa papo hapo eneo la tukio.

Mei, mwaka jana Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyambunda, Said Mbwana, aliuawa kwa risasi.

Oktoba, mwaka jana Ofisa Mtendaji wa kijiji hicho hicho, Ally Milandu, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wanne. Novemba, mwaka huo huo wenyeviti wawili wa vitongoji wa kijiji hicho waliuawa kwa kupigwa risasi.

Januari, mwaka huu watu ambao Jeshi la Polisi hadi sasa halijawafahamu walimuua mfanyabiashara Oswald Mrope kwa kumpiga risasi mbele ya familia yake.

Februari 3, mwaka huu watu wasiojulikana walivamia nyumba ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Jaribu, Bakari Msanga na kuichoma moto huku yeye mwenyewe akifanikiwa kutoroka.

Matukio ya aina hii yanayotia shaka ustawi wa amani ya Tanzania, kwa mwaka 2013 yalitokea wilayani Kilindi mkoani Tanga ambako msikiti wa Madina ulibainika katikati ya pori kati ya Tanga na Bagamoyo.

Kama hiyo haitoshi, mwaka 2014 vijana waliokuwa wakipewa mafunzo ya kigaidi walikamatwa mkoani Mtwara wakiwa wanapewa mafunzo tayari kujiunga na al-Shabab.

Kenya kwa muda mrefu sasa imekuwa katika mapambano yasiyokwisha na kundi la al-Shabaab wanaoaminika kuwa wanatetea imani na Waislam nchini Somalia.

Ni kwa mantiki the0, matukio ya mauaji kwa mikoa ya Pwani, Mtwara na Lindi wachambuzi wa masuala ya kiusalama wameishauri ĺ kutumia zaidi diplomasia kuliko nguvu.

Copyright ©2017. Gazeti la Jamhuri

RAIS Magufuli Aitisha Kikao cha Wabunge wa CCM..Wabunge Hawajui Wanachoitiwa..!!!

$
0
0

Ikiwa ni takriban siku 40 baada ya kikao kizito kilichofanyika Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma, wabunge wa CCM watakuwa na mkutano mwingine keshokutwa ulioitishwa na mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli.

Hata hivyo, wabunge hawajaelezwa mahali wala muda utakaofanyika mkutano huo, kwa ahadi kuwa watataarifiwa baadaye.

Pia , wabunge hao hawajaelezwa ajenda za kikao hicho ambacho kwa kawaida huwa cha siri na ambacho hutumika kuweka misimamo ya chama katika masuala yanayojadiliwa au yanayotarajiwa kujadiliwa bungeni.

Katibu wa wabunge hao, Jasson Rweikiza ndiye aliyetuma ujumbe huo mfupi wa simu kwa wabunge ambao baadhi yao wameithibitishia Mwananchi suala hilo.

Ujumbe huo umemtaka kila mbunge awepo na hata wale waliosafiri, wajitahidi kurudi Dodoma kuhudhuria kikao hicho.

Alipohojiwa na gazeti hili jana, Rweikiza alisema Rais anaruhusiwa kuzungumza na wabunge wake muda wowote kwa hiyo hilo lisiwe nongwa linapotokea kwa CCM.

“Kwani (mwenyekiti wa Chadema, Freeman) Mbowe akiwataka wabunge wake inakuwa nongwa? Yeye ni mwenyekiti. Wabunge ni watu anaofanya nao kazi pamoja, hivyo kuwaita ili kuteta nao kujadili kazi isiwe nongwa,” alisema Rweikiza.

Rweikiza alisema Magufuli kama mwenyekiti wa CCM anaruhusiwa kuwaita wabunge na kukaa nao, kuongea au kuteta jambo lolote linalohusu mustakabali wa chama hicho.

“Mkumbuke yeye ni mwenyekiti wa chama tawala,” alisema.

Viongozi wa juu wa CCM na Serikali wanatarajiwa kuwepo katika kikao hicho, hasa kutokana na ukweli kuwa siku inayofuata itakuwa ni sherehe za Muungano ambazo mwaka huu zinafanyika mjini hapa.

Kwa maana hiyo, Rais Magufuli, Dk Ali Mohamed Shein (Rais wa Zanzibar), Samia Suluhu Hassan (Makamu wa Rais) na Phillip Mangula (makamu mwenyekiti CCM) na Abdulrahman Kinana (katibu mkuu wa CCM) wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho.

Vigogo hao wataungana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye yupo mjini hapa kuongoza shughuli za Serikali bungeni.

Vikao hivyo huwa vinaongozwa na Waziri Mkuu katika siku za kawaida za mikutano ya Bunge kwa kuwa mtendaji huyo mkuu wa Serikali huwa Dodoma kwa ajili ya mikutano ya Bunge.

Mara ya mwisho kikao baina ya Rais na wabunge hapo kilifanyika Machi 12, mwaka huu na Rais alitumia muda mwingi wa hotuba yake kuwaelekeza wabunge jinsi ya kuenenda, ikiwa ni pamoja na kuwaonya wasimpinge Waziri Mkuu.

Maelekezo ya Rais

Katika kikao hicho ambacho pia kilihudhuriwa na Kinana na Mangula, kiongozi huyo wa nchi aliweka bayana kuwa iwapo wabunge watampigia kura ya kutokuwa na imani naye (Waziri Mkuu Majaliwa), atamrudisha kwenye chombo hicho na iwapo watamkataa tena, atalivunja Bunge.

Rais aliwaambia watunga sheria hao kutoka CCM kuwa amepata taarifa kwamba wapo baadhi yao wanaotishia kuanzisha hoja ya kutaka Majaliwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kuwaambia wenye lengo hilo hawatafanikiwa kwa kuwa wakithubutu kufanya hivyo, atapeleka tena jina lake na wakirudia, atalivunja Bunge ili wote warudi katika uchaguzi.

Mbali ya kumkingia kifua Majaliwa, mwenyekiti huyo wa CCM pia aliwaonya wabunge dhidi ya vitendo vya kushirikiana na wapinzani kuishambulia Serikali, akitoa mfano wa mbunge wa chama tawala aliyemgawia muda wake wa kuchangia hoja mbunge wa upinzani.

Kwa kauli hiyo, alikuwa akirejea kitendo cha mbunge wa CCM, Boniface Getere kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba wakati wa kuchangia taarifa ya Kamati za Bunge za Ardhi, Maliasili, Kilimo na Utalii.

Pia alieleza kukerwa na wabunge wa CCM wanaofifisha vita dhidi ya dawa za kulevya na mmoja akimtuhumu kutoa siri za chama kwa upinzani.

Rais Magufuli pia alieleza kuwa yeye ndiye aliyeamua kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya televisheni kwa baadhi ya shughuli za Bunge.

Pia, mwenyekiti huyo wa CCM alionya kitendo cha baadhi ya wabunge wa chama hicho waliotaka kumtembelea gerezani Arusha, mbunge wa Chadema, Godlbess Lema kwa madai kuwa kitendo hicho ilikuwa ni sawa na usaliti kwa chama.

Katika kikao hicho, wabunge pia walimweleza Rais kuhusu uhusiano wao na baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya, wakisema si mzuri na bado suala hilo limeendelea kujitokeza katika mijadala ya Bunge la Bajeti.

Baada ya kuwasikiliza, Rais Magufuli alianza kuwapa taarifa za mafanikio ya Serikali yake pamoja na mipango kabambe katika kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, akiwataka waiunge mkono Serikali katika maeneo yao huku suala la ujenzi wa reli pana, ambao tayari umezinduliwa, likipewa kipaumbele zaidi.

Kikao moto cha Bunge

Kikao cha keshokutwa kinakuja wakati Bunge likiwa limetawaliwa na mijadala inayoonyesha Serikali haijafanya kazi yake vizuri baada ya hotuba tatu za bajeti kusomwa.

Bajeti hizo ni ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ilitawaliwa na majadiliano kuhusu vitendo vya utekaji, uvamizi na kuihusisha Idara ya Usalama wa Taifa na matukio hayo.

Suala la kutekwa kwa msanii Roma Mkatoliki, kitendo cha mteule wa Rais kuvamia studio za televisheni za Clouds Media, kutishiwa bastola kwa mbunge wa Mtama, Nape Nnauye na kutoweka kwa kada wa Chadema, Ben Saanane yalitawala mijadala ya hotuba hiyo.

Bajeti nyingine ni za Ofisi ya Rais (Tamisemi) na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, zilizojadiliwa kwa pamoja na kutawaliwa pia na hoja za utekaji na pia vitendo vya unyanyasaji unaofanywa na wakuu wa wilaya na mikoa.

Mawaziri pekee watetea

Tofauti na inavyokuwa wakati wa bajeti hizo, ni wabunge wachache wa CCM waliosimama au kuomba mwongozo wakati wapinzani walipokuwa wakiishambulia Serikali.

Badala yake, mawaziri watatu; George Simbachawene (Tamisemi), Angela Kairuki (Utawala Bora) na Jenista Mhagama (Bunge) ndio waliosimama mara kwa mara kutoa taarifa au kuomba mwongozo.

Hoja dhidi ya Serikali zinazotolewa na wabunge wa upinzani pamoja na wa CCM zinaweza kuchukua nafasi kubwa katika kikao cha keshokutwa, hasa ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi za maendeleo hazikupata fedha za kutosha kama ilivyopangwa katika bajeti iliyopita.

Hadi wiki mbili zilizopita, miradi ya maendeleo ilikuwa imepewa asilimia zisizozidi 40 ya fedha zilizotengwa. Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga asilimia 40 ya fedha zake kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Bajeti hiyo ya mwaka 2016/17 ilikuwa ya Sh29.5 trilioni na Sh11.8 trilioni zilitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Wabunge wamekuwa wakiilalamikia Serikali kuwa fedha zinazotolewa kwa ajili ya shughuli mbalimbali haziendani na kiwango kilichoidhinishwa na Bunge hilo na kusababisha nakisi ya zaidi ya asilimia 50 katika miradi ya maendeleo.

Hali ya uchumi inaweza kuibua mijadala mikali katika hotuba za bajeti za wizara zinazofuata, kutokana na malalamiko kuzidi kuongezeka, hasa sekta binafsi ambayo wadau wanadai kuwa mazingira ya biashara hayajakuwa rafiki.

Suala jingine ambalo limekuwa linazungumzwa na wabunge kutoka vyama vyote ni uhakiki wa vyeti vya mteule mmoja wa rais anayedaiwa kufeli kidato cha nne na kutumia vyeti vya mtu mwingine ambavyo vimeghushiwa jina ili vilingane na jina lake la sasa.

Suala hilo pia lilihojiwa na wabunge wa CCM katika kikao chao cha kwanza cha ndaniokabla ya mkutano wa bajeti kilichoongozwa na Waziri Mkuu.

Vilevile, zimekuwapo taarifa za wabunge kutaka masilahi yao yaongezwe, lakini hoja zao zimekuwa zikigonga mwamba na taarifa za ndani zinasema safari hii huenda kilio chao kikaongezeka.

Bunge, ambalo mwaka jana lilirejesha salio la Sh6.5 bilioni, mwaka huu limejikuta na nakisi ya Sh8.5 bilioni ambazo wabunge wameeleza hofu kama zitaweza kukifikia chombo hicho kabla ya kumaliza shughuli zake za bajeti.

MWALIMU wa Shule ya Msingi Amuua Mwanaye kwa Kipigo..!!!

$
0
0

Polisi mkoani Mwanza inamshikilia mwalimu wa Shule ya Msingi Mwamakoye wilayani Kwimba kwa tuhuma za kumchapa mtoto wake na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilitokea Aprili 21 mwaka huu, saa kumi jioni na kumtaja marehemu kuwa ni Sifael Emmanuel (8) mwanafunzi wa shule hiyo.

Msangi alisema taarifa zilizopatikana zinasema kuwa, mtoto huyo alikuwa na tabia ya kuchelewa kurudi nyumbani pindi anapoagizwa dukani na mama yake.

“Kutokana na tabia hiyo mama yake alikuwa akimpatia adhabu, lakini hakukoma na kwamba juzi mtoto huyo aliagizwa tena dukani na kuendelea na tabia yake ileile,” alisema.

Kamanda alieleza zaidi kuwa mtoto huyo aliporejea kutoka dukani, baba yake alimshika na kuanza kumshushia kipigo kwa muda mrefu.

“Wakati anaendelea kumpiga, mtoto alikuwa akilia na akaishiwa nguvu na baada ya muda mfupi akapoteza maisha,” alisema Msangi

Kutokana na tukio hilo, wananchi walioshuhudia walitoa taarifa kituo cha polisi na baadaye mwalimu huyo alikamatwa na kupelekwa kituoni.

Aliongeza kuwa kwa sasa baba wa mtoto huyo anahojiwa na polisi hadi uchunguzi utakapokamilika na atafikishwa mahakamani.

Pia, Msangi alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba kwa ajili ya uchunguzi na kwamba, utakapokamilika utakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Kamanda huyo aliwaonya baadhi ya wazazi wanaowafundisha watoto wao kwa kuwachapa na fimbo huku akiwataka kutumia namna nyingine ya kuwaelekeza wanao.

Vilevile, alishauri kuwa ni vyema zaidi kuwaonya watoto kwa maneno ya hekima au vitabu vya dini ili kuepuka adhabu zinazoweza kuleta madhara.

Akizungumzia tabia ya baadhi ya wazazi kuwaadhibu watoto wao kwa kuwachapa fimbo, mkazi wa Nyamanoro, Amina Lusheshu alisema ni vyema adhabu ikatolewa kwa kuzingatia umri.

MHE Mwigulu Hata Hili Nalo Utanyamaza..!!?

$
0
0

Wewe ndio kiongozi unayesimamia usalama wa RAIA na Mali zao ndani ya mipaka ya nchi. Sina mashaka na uwezo wako kiutendaji ila mashaka yangu ni jinsi ulivyo geuka bubu tokea upewe wizara hii na hasa unapo paswa kutolea kauli matukio yenye harufu za uhusika wa serikali.

Nikuulize tuu, jee na hili la uvamizi mkutano wa ndani wa CUF na watu kwenye silaha mbalimbali ikiwemo bastola nalo utanyamaza?

Anatajwa Lipumba kuhusika jee utahakikisha polisi wako wanamuondolea "kinga" ya kutokamatwa?

Tunajua pengine kuna uthibiti umefanywa dhidi yako ndio maana hufurukuti, lakini wewe bado kijana na una future katika siasa, mbona unakubali kuififisha? Hujui kimya chako (au woga) unakujengea picha kuwa wewe ni dhaifu na legelege asiye weza madaraka?

Ni katika kipindi chako tuu ndio tumeona silaha zinatolewa kweupe mchana na hakuna anaye chukuliwa hatua huku mamlaka zikihusishwa.

Fanya jambo Mwigulu na heshima yako itasimama juu bila kujali kwa sasa mteuzi atakufanyaje.

MLINGA Amjibu Mh Mbowe Kuhusu CCM Kutumia Miujiza..!!!

$
0
0

Mbunge wa Ulanga Mh.Mlinga amemjibu Mbowe kuwa CCM haitumii miujiza kutawala bali inatumia mpango mkakati kutekeleza ilani yake.

Vile vile ameeleza kuwa ni Mbowe ndiye mwenye kutumia miujiza kuongoza chama kwani amepata division sifuri form six lakini anatawala wafuasi wenye elimu za juu wakiwamo madaktari na maprofesa

Beef ya Yusuph Mlela na Nay wa Mitego Yafika Pabaya

$
0
0

Wawili hao waliingia kwenye bifu hilo baada ya Nay wa Mitego, kuwaita wasanii wa filamu ‘mataahira’ kisa kuandamana kupinga biashara ya filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi.

Rapa huyo amedai hawezi kupigana na muigizaji huyo huku akimkejeli kwa kumuita Mlela ni mwanamke.

“Nasikia kuna mwanaume/mwanamke yupo Bongo Movie anataka kupigana na mimi, bahati mbaya mimi sipigani na mwanamke hata baba yangu aliniambia mwanamke hapigwi,” alisema Nay kupitia video iliyosambaa mtandaoni.

Aliongeza,”Naona kuna watu wanashadadia hili suala kwamba tupigane, mimi siwezi kupigana naye labda nitafutiwe mwanaume mwenzangu ili tutengeneze hela lakini kunipiganisha na mwanamke ambaye wamepoteza marinda hapana. Baada ya kutangaza anataka kupigana na mimi Bongo Movie wenzake walinipigia simu wakaniambia achana na huyo mtu ni mwanamke mwenzao alishapoteza marinda,”

Baada ya maneno hayo ya kejeli, Mlela amerudi upya na kusisitiza bado anahitaji pambano na rapa huyo ili amshikishe adabu.

“Nay wa Mitego mimi nimelelewa vizuri na familia yangu ndio maana mambo ya matusi sijazoea, ingawa nina uwezo mkubwa niliopewa na mungu baba wa kupambana na matamshi hayo. Kikubwa acha woga, kama shida yako ni pesa huyu aliyepoteza marinda si ndio itakuwa rahisi tu?. Kwangu mimi PESA SiO KILA KITU MUNGU NDIO KILA KITU. Nikuchape au nikuchape (uwezi) PESA ZOTE UTACHUKUA WEWE MIMI SIITAJI ATA SHILINGI MIA. Nay APA RINDA LIPO tena LA ZIGIZAGA uliza vizuri sio Kwa niliowatumia kama dustbin kupitisha siku….sitobishana na wewe tena coz akili yako ya kutaka sifa ni fupi.. eti unakataa movie wakati wewe mwenyewe unafanya movie au ujui kama izo video zako ni movie na TAIFA likiwa na utaratibu mzuri wa kazi za wasanii pia utafaidika…Acha maneno NJOO kwenye stage ili tuheshimiane…samahani Kwa mashabiki zangu ninaowakwaza Kwa hili. #LINDALIPO TENA LA ZIGZAG HAHAHA HAHAHA ,” aliandika Mlela Instagram.

MTANZANIA Ashika Nafasi ya Tano Mbio za Nyika Uingereza..Akomba Mamilioni ya Pesa..

$
0
0

Wakati Mkenya Daniel Wanjiru ameshinda mbio za London Marathon, Mtanzania Alphonce Simbu ameshika nafasi ya tano.

Wanjiru aria wa Kenya ameshinda kwa muda wa saa 2, dakika 5 na sekunde 48 na Simbu ametumia saa 2, dakika 9 na sekunde 9 na kushika nafasi hiyo ya tano.

Inaonyesha anayeshika nafasi ya tano katika mashindano hayo anaibuka na kitita cha dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 22).

Hata hivyo, Simbu ambaye alianza vibaya alilazimika kubadili gia mwishoni na kuwashinda zaidi ya Wakenya sita na Waethiopia wawili, Mganda mmoja ili kushika nafasi hiyo ya tano.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Kenenisa Bekele wa Ethiopia ambaye mwishoni alichuana vikali na Wanjiru aliyeonekana kuwa katika kiwango bora.

IMEFICHUKA...Kumbe Waliivamia Mkutano wa Maalim Seif Jana ni Walinzi wa Prof Lipumba..Tazama Picha Zao Wakiwa na Lipumba Wakimlinda ..!!!!

$
0
0
Hapa Akiwa na Prof Lipumba Katika Moja ya kazi zake za Ulinzi



Hapa Akiwa Amekamatwa na Kushushiwa Kipigo na Wafuasi wa Maalim Seif

MAMBO ya Kuzingatia Katika Kupiga Hatua Kimaisha..!!!

$
0
0

Je ni hatua gani umepiga katika maisha yako ?

Usijibu kwa sababu mshahara ni mdogo, au kazi imebana, hapa nataka ujipe jibu halisi, kwa nini umeshindwa kupiga hatua? Kwa sababu nina imani kuna ambao wanafanya kazi kama yako, na wanalipwa kama unavyolipwa wewe ila wao inawezekana wamepiga hatua kuliko wewe. Hivyo hapa njoo na sababu za upande wako, achana kufikiria sababu za mwajiri wako kwa muda.

Inawezekana hujaweza kujitengenezea nidhamu ya fedha, kwamba ukipata mshahara unautumia wote mpaka unaisha halafu unaanza kukopa. Na hapa mara nyingi itakuwa imeanzia kwenye kushindwa kudhibiti matumizi yako na hatimaye yanakuwa yamezidi kipato.

Inawezekana pia una wategemezi wengi wa moja kwa moja na hivyo kipato chako kugawanywa mara nyingi na kukufanya ushindwe kupiga hatua.

Na pia inawezekana una matumizi mengi yasiyo ya msingi, labda umekuwa unanunua vitu kwa kusukumwa na hisia tu. Vitu kama nguo, au kutembelea maeneo ya starehe na kadhalika.Hapo nimetoa tu maeneo ambapo matatizo yako ya fedha yanaweza kuwa yanachochewa zaidi, ila wewe ndiye unayejua kwa upande wako ukweli uko wapi.

Kwa nini ni muhimu sana kujiuliza na kujijibu swali hilo?

Ni muhimu sana ujiulize na kujipa majibu ya swali hilo la kuhusu mchango wako wewe kwenye hali yako ya kipato kuwa ngumu. Hii ni kwa sababu hata kama utaacha kazi na kwenda kwenye ujasiriamali, sio kwamba tabia zako zitabadilika pale pale. Unaweza kwenda nazo kwenye ujasiriamali na mambo yako yakazidi kuwa magumu kuliko hata yalivyokuwa mwanzo.

Ni vyema ukajua ni wapi unapochangia ili uweze kujirekebisha kabla hujaingia kwenye ujasiriamali

UNATAKA Kumjua Mchawi Wako Kazini? Soma Hapa..!!!

$
0
0

Unakumbuka wiki ya kwanza ulipoianza kazi unayoifanya? Unakumbuka ulipoipata kazi hiyo uliwaambia watu wangapi na namna ulivyokuwa na furaha? Ilikuwa sherehe moyoni mwako. Kila kitu kilikuwa vizuri, ilikuwa habari njema na baraka kubwa kwako.

Mapokezi uliyopewa na muajiri wako mpya muda mfupi baada ya kusaini mkataba wako na maneno ya faraja yalikufanya ujione umeingia kwenye njia ya mafanikio haswa. Naipata picha nzima ya siku ulipokuwa unatambulishwa kwa kila mwajiri uliyemkuta ofisini.

Huenda Boss wako alikuwa mtu mwema sana, alikukaribisha vizuri na kuanza kukuelekeza kazi na hata ulipokosea alikuwa muungwana sana kwako na kukuelekeza taratibu hadi alipohakikisha umeelewa kweli.

Lakini sasa kila kitu kimebadilika, unaichukia kwa nguvu zote ile ofisi… Boss wako anakuandama kila wakati, kila unachofanya kwake hakifai. Muda mwingine anatumia maneno makali yanayokukwaza. Kile kipato ulichokifurahia wakati unaanza kazi sasa hakitoshi kabisa. Hii inakufanya uzidishe chuki yako na unatamani uondoke punde tu ukipata pa kukimbilia.

Unahesabu saa za kazi, sasa unaziona nyingi. Unatamani muda ufike ukimbie kutoka ofisini ukapumzike kwa sababu ni chanzo kikubwa cha msongo wa mawazo ulionayo.

Sio bure, kuna uchawi katika kazi unayofanya. Ndio, uchawi unaoufahamu ila hujatambua chanzo chake.

Ngoja nikuelekeze alipo mchawi wa kazi yako:

Watu wengi wanapokuwa kwenye matatizo kama haya ofisini, huanza kufikiria mbali sana. Kila aina ya sababu itatafutwa ikiwa ni pamoja na ushirikina. Lakini kufanya hivyo ni sawa na kwenda kwa jirani kumtafuta kunguni anayekung’ata kitandani kwako. Kunguni huyo yuko ndani mwako, utapoteza muda kumsaka kwa jirani.

Jipime kama una dalili hizi:

    1. Majigambo

Katika hali ya kawaida inawezekana kweli wewe ndiye unayefanya kazi kwa bidii na unajua vitu vingi kuliko wenzako, sasa zaidi hata ya wale uliowakuta kazini. Kwakuwa unafahamu hilo, ullianza kujigamba bila taratibu. Ulitaka wote wafahamu kuwa wewe ndiye kiungo muhimu katika ofisi hiyo na hata Boss wako anakutegemea zaidi wewe.

 2. Kutangaza umeichoka kazi yako/huipendi

Unapokuwa ofisini, kuna wakati unaona wafanyakazi wenzako kama wote ni rafiki zako hususan pale mnapokuwa mnapiga polojo mida ya ‘lunch’, na ndipo unapojikuta unatoa lawama kwa Watawala au muajiri. Kueleza kuwa huipendi tena kazi hiyo. Habari hizi hufika mbali na muajiri huanza kukuona kama kikwazo kwenye timu yake.

  3. Kujihusisha na umbea

Umbea una tabia mbili. Unapojihusisha na umbea, tambua kuwa yule mnaemsema leo hatasemwa tena kesho. Habari zako zitasemwa na uliyoyasema yataripotiwa. Huenda ulikuwa unaonekana mkamilifu ulipokuwa unaingia, lakini habari anazopata Boss wako ambazo ni mazao ya umbea mliopiga kwenye ‘kolido za ofisi’, zimembadili.

 4. Uko ‘emotional’ na unaonesha

Unapotofautiana na Boss wako, unaonesha hisia zako kwa kiwango cha juu. Kulia, kukasirika hadi kushindwa kufanya kazi za siku huku ukigonga baadhi ya vitu kuonesha hasira yako. Kuongea kwa hasira mbele ya wafanyakazi wenzako kuhusu Boss alivyokukwaza na hata kumwabia. Kugoma kula au kugoma kupokea simu za ofisini kwa sababu umekasirishwa sana. Hili ni tatizo kubwa kwenye ajira yako.

  5. Unadanganya

Wewe uligeuka kuwa bingwa wa kumpanga Boss wako, unajua nini ukimpiga ‘fix’ ataelewa. Bahati mbaya, Boss wako aliwahi kuwa kwenye nafasi yako kwahiyo anajua. Kubaini kuwa unamdanganya kunamuondolea uaminifu aliokuwa nao juu yako.

 6. Muda unaougusa mlango wa ofisi

Unaingia kazini umechelewa angalau dakika 15 na zaidi. Of Course kama uko Dar es Salaam unakuwa na jibu lako umelitenga kabisa, “Boss samahani nilikwama kwenye foleni.” Boss wako akikupigia simu ya ofisini angalau dakika 5 tu baada ya muda wa kazi hakupati kwa sababu ulishaondoka kwa kuwa ulianza kufungasha vyako dakika 15 zilizopita. Unawahi Foleni.

  7. Unajua sana

Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, sasa wewe ndiye mtaalam unaefahamu zaidi na kweli una akili nyingi sana. Unamuonesha Boss wako kiwango chako cha kujua na kukosoa. Kumbuka Kikombe kilichojaa maji hakiongezwi maji..!

 8. Unafanya kazi kwa bidii, kama jana kama mwaka jana (Haukui)

Unaamini unafanya kazi kwa bidii. Kama jana, kama mwaka jana. Na ukijipima na wenzako unaona unafanya kazi kama wao tu lakini unaandamwa wewe. Unapaswa kutambua kuwa haukui, hauna ubunifu na hauongezi uzalishaji. Kwa ufupi biddi yako imedumaa. Unafanya kama jana, kama mwaka jana kwa bidii. Kila mwajiri anahitaji zaidi ya bidii.. anahitaji mtu anayekua.

 9. Unabeba Kazi na Sifa za Timu kuwa zako

Unaweza kuwa unajiweka wewe kwenye kazi ambazo hukufanya peke yako na kutaka ionekane kama wewe ndiye uliyefanya zaidi. Kweli, inawezekana kuwa ulifanya wewe zaidi. Kiongozi mzuri ataona wewe unataka kuua vipaji vya wengine na kutaka usifiwe wewe kwanza.

10. Umepoteza uwezo wa kusikiliza

Kwa sababu unaamini unafahamu vitu vingi, umepoteza uwezo wa kusikiliza maelekezo kama awali. Hivi sasa wewe una uwezo mkubwa zadi wa kueleza. Unaamini unajua mengi na unataka usikilizwe wewe. Wenye uwezo wa kusikiliza zaidi ya kuzumgumza huongeza zaidi ufahamu.

Kama dalili hizi zinakuhusu… naamini tayari umeshamjua mchawi wako kazini. Mchawi wako kazini ni ‘Wewe’. Hivyo, unapaswa kubadilika haraka sana kuinusuru ajira yako iwe ya furaha.

Simba Majanga Matupu...Wapokonywa Point 3 Walizozipata Mezani...

$
0
0

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imebatilisha uamuzi ya Kamati ya saa 72 kwa kuipa simba pointi tatu na kuzirudisha Kagera Sugar. 

Akitangaza uamuzi huo Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa amesema Kamati ya sheria imebaini mapungufu kadhaa katika maamuzi ya Kamati ya saa 72 kwa kwanza rufaa ya Simba kukatwa nje ya wakati lakini pia haikulipiwa ada ya sh 300000. 

Mbali na hivyo Mwesigwa amesema Kamati ya saa 72 ilipokutana iliruhusu watu wasiokuwa wajumbe wa Kamati kushiriki kufanya uamuzi kitu ambacho ni kosa. 

Mbali na uamuzi huo Kamati imeitaka TFF kuwachukulia hatua baadhi ya watendaji wa bodi kwa kuipotosha Kamati ya saa 72

MY True Story: Alichonifanya Huyu Mrembo Kwenye Daladala Kinaniuguza..!!!

$
0
0

Na Edward Lucas

Ukiona ndege ametua kwenye ulimbo, kanasa lakini hana wasiwasi, anachambua tu mbawa zake mithili ya mrembo aliye mbele ya dressing table, basi fahamu kuwa ndege huyo amegundua amenasa kwenye ulimbo uliotegwa bahati mbaya na ‘Rasta Man’ asiyekula nyama. Vinginevyo yatakuwa ‘mang’ana’.

Hebu fuatilia kilichonikuta, cha ajabu na cha kushangaza kilichoniuguza… ni mapenzi gani haya au uchawi, au ni wizi gani huu!!!

Juzi nilikuwa katika mizunguko yangu ya kila siku, ila ilipofika majira ya saa mbili usiku hivi ilibidi nielekee kituo cha daladala ili nirejee kwenye kiota changu. Nilikuwa na uchovu mwingi hata honi za daladala nilihisi zinanipigia kelele.

Kama unavyojua jiji la Dar es Salaam, adha ya usafiri ni kubwa. Licha ya kuwa na rundo la daladala, bado abiria wanafunika wingi wa daladala hizo. Kwahiyo panahitaji msuri wa maana kupata gari hasa majira ya jioni.

Bahat nzuri siku hiyo nimefika pale Mawasiliano (Simu 2000), daladala nayo ndo ikawa inaingia kwahiyo ikabidi niwahi haraka ili nipate seat, japo kwa uelekeo wetu watu sio wengi sana ila kwa kiasi fulani kulikuwa na kambanano kidogo. Lakini kwa muda huo upande wetu gari ilikuwa wazi kidogo, so nilifika nikapata seat nikakaa.

Nikiwa hata sijatulia vizuri alikuja dada fulani akiwa kasi sana kama alikuwa anawahi seat wakati gari bado ilikuwa na seat za kutosha! Alikuja hadi pale nilipokuwa nimekaa akanambia, “samaha ni sogea kidogo tukae wote”.  “Bila samahani dada, pita ukae upande wa dirishani,” nilimjibu kwa sababu ilikuwa seat ya watu wawili. Nilimpisha akakaa upande wa dirishani mkono wa kulia ule upande wa dereva

Lakini muda mfupi tu gari likiwa ndo linaanza kuondoka. Ghafla, nilimuona anatapatapa kuangalia kwenye mkoba. Mara ajikague kama anatafuta kitu. Baadae, nikamsikia anajisemesha kwa huruma, “mmmm simu yangu jamani” huku zoezi la kujipekuapekua likiendelea.

Mimi nilikuwa nimechoka, natamani hata kusinzia, nikaanza kuwaza, “sasa huu msala wa simu tena..”

Akiwa anafanya hayo nilikuwa nimetulia kama simuoni hivi wala simsikii… Sikuonesha ushirikiano wala kumsikiliza. Alishindwa kutulia, mara akanigeukia na kuniambia, “kaka samahani, unaweza kunibipia simu yangu hapo mara moja”. Basi mtoto wa watu hata sikuuliza kitu nilishika simu na akanitajia namba zake kisha nikapiga simu kwa ile namba.

Punde simu ilianza kuita ikiwa kwenye mkoba wake…, ni uleule mkoba aliokuwa anausachi. Hapo hapo akasema “heee afadhali kumbe iko humu!!!! nilikuwa nimeshaogopa… asante sana kaka.” 
Sikuwa na maneno mengi nikamjibu, “usijali.” Safari yetu ikaendelea huku yowe la konda la vituo likiendelea. Niliifuta ile namba palepale, najua fujo za mpenzi wangu akiishika simu yangu huko nyumbani halafu aone namba mpya ambayo sina maelezo yake.

Lakini kupitia hiyo “oparesheni saka simu”  nilipata nafasi ya kumuangalia vizuri usoni. Nilimuona binti mrembo halafu kama wa kishua sana. Nilihisi alipaki gari lake sehemu akapanda daladala. 
Lakini kwa udadisi wa jicho langu niliona kama tayari ameshazaa. Si ujaua tena jicho linatuma taarifa nyingi kwenye ubongo.

Pua zangu zilisia harufu nzuri ya marashi. Yaani ile seat ilikuwa na hali nzuri muda ule. Sio marashi makali, ni laini ila yanavutia, nikaanza kuhisi raha kwa mbali. Sio rahisi kuisikia ile harufu uswahilini kwetu.

Lakini cha ajabu kipindi kondakta anatangaza kituo kinachofuata yule dada aliomba ashushwe pale…nilishtuka kidogo maana ni karibu sana na pale tulipopandia yaani hata mtu akisamama anaweza kumuita mtu wa kituo cha pili. Kama unavyojua vituo vya town. Nikasema kimoyomoyo kikwetu, “bhono mbosari bhwa sihera”. Yaani huu ni uharibifu mkubwa wa fedha.

Aliposimama, kwa kweli jicho lilimuangalia kidogo… eeh, alikuwa amejaliwa, mwembamba hivi ila nyuma alikuwa na minofu. Basi, niliishia kumuangalia hadi mlangoni. Basi nikaendelea na mambo yangu. Nikawa nafikiria kwa mbali..”huyu vipi!?”

Baada ya kuwa ameshuka na safari imeendelea kondakta alianza kukusanya nauli na alianzia kwangu lakini baada ya kunipa chenji aliniuliza “huyo dada mnafahamiana?” “Dada yupi?” nikamuuiliza Konda. “Huyo aliyeshuka hapo” nikamwambia, “hapana!” Yule konda akaguna kama mtu anayetahadhalisha jambo.

Konda akaniuliza “kwani unashukia wapi” nikamwambia mwisho wa daladala, basi akasema ngoja achukue kwanza nauli kwa abiria kisha tuongee..Yale maneno yake yalinishtua kidogo ikabidi nianze kujikagua labda kuna kitu nimepoteza lakini sikuwa na kitu chochote nilichopoteza so ikabidi nimsubiri kwa hamu na maswali mengi sana kichwani.

Nikiwa nasubiri konda amalize kukusanya nauli ili anambie nini kinaendelea, mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio kidogo nikijiuliza mambo mengi kuhusu huyo mtu. Kubwa likiwa nini nimepoteza. So niliendelea kujikaguakagua kwa kila nilichokuwa nafikiria lakini kwa kadIri nilivyojitathimini nilijiridhisha kuwa sijapoteza chochote hivyo ikabidi nisubiri maneno toka kwa kondakta.

Basi kondakta baada ya kumaliza kuchukua nauli alirudi kukaa kwenye kiti kilichokuwa mlangoni nami nilivyoona hivyo ikabidi nisogee siti ya mbele kidogo ili niwe karibu naye wakati huo baadhi ya siti zilikuwa wazi maana abiria wengi walikuwa wameshuka..kwahiyo nikakaa upande ule wa dereva yaani kulia mwa gari huku konda akiwa upande wa kushoto kule mlangoni.

Nilinyoosha mkono nikamgusa kondakta begani alipogeuka nikamwambia “hebu nambie mkuu, kuna nini?” Jamaa aligeuka na aliponiona ni mimi akasema “aaaaah!! nilikuwa nishasahau boss.”
Basi akaweka sarafu na noti zake vizuri kwenye koti na akaanza kunisimulia.

Kama unavyojua konda na mlango…so jamaa akanambia kipindi gari linafika katika kituo akiwa pale mlangoni , alimuona huyo dada akiwa na wenzake wawili wakiwa wamesimama miongoni mwa kundi kubwa la abiria. Waliokuwa pale kituoni ambapo licha ya baadhi ya abiria kukimbia kuja katika daladala hiyo wao walibakia wamesimama..jambo ambalo ni la kawaida tu. Akahisi sio gari walilokuwa wanasubiri.

Lakini ghafla mimi nikiwa nakimbia kuelekea katika hilo gari, Konda anasema aliwaona wanaoneshea kidole yaani mmoja kati yao alikuwa ananisontea kidole ishara ya kuwaonesha wenzie (nadhani hapo nitakuwa nimeeleweka vizuri) na hasa aliyekuwa anaelekezwa ni huyu aliyekuja kwenye gari.

Katika zoezi hilo ilionekana wale wengine wawili wanamshinikiza yule dada anifuate ambapo naye alionekana kusitasita. Nikiwa ndo ile naingia tu kwenye daladala hatimaye alipochomoka mbio kuja katika ile gari.

Hii movie yote kumbe yule kondakta aliiona….alianza kujiuliza kuwa pengine tunafahamiana lakini pia mawazo yake yalimtuma labda kuna jambo wanataka kulifanya kwangu. Kwahiyo, kwa kiasi fulani alianza kuweka kuangalia kwa makini hasa kwa yule mtu hata pale gari alipokuwa linaondoka.

Kumbe hata katika zile harakati za “oparesheni saka simu” kondakta alikuwa anatupimia tu ki-wiziwizi ili kama kutatokea shida yoyote basi aweze kubanana naye. Kumbe hata kile kitendo cha yule dada kushuka mapema ndo kilimshtua zaidi, akahisi kuna tukio lishafanyika tayari. Kwahiyo pale nje alimcheleweshea chenji kidogo ili kama kutasikika mtu analalamika humo ndani ya daladala basi aweze kumdandia lakini ilikuwa haina namna alimpa chenji na tukaendelea na safari.

Ndo maana aliporudi ndani ya gari tu akaanzia kwangu na kuniuliza kama nafahamiana naye. So, kondakta baada ya kunisimulia haya yote mwishoni tena alirudia kuniuliza swali lile lile “vipi wewe humfahamu kabisa?”

Nikamjibu, “hapana mzee wala sijawahi kumuona hata mara moja, ndo hivi leo tu”. Basi konda aliniuliza tena “vipi vitu vyako vyote viko sawa?” “Naona kila kitu kiko sawa.”

Basi aliyafunga mazungumzo yetu lakini maneno aliyomaliza nayo ndo yalinishtua sana, aliguna kisha akasema “inabidi uje ujichunguze vizuri maana huo ujio wake sio wa kawaida halafu siku hizi kuna vimambo vya ajabu ajabu huku, basi tu.” Basia akaendelea na kazi yake.

Daaaah!!!! Kusikia hili neno akili ilianza kufikiria maneno mengine mazito kidogo…yaani mbali na akili ya kupoteza kitu nilianza kujichunguza labda kuna kitu kisicho cha kawaida nimeachiwa au hata kupakwa. Lakini yule msichana mbona anaonekana wa kishua..!

Nilijitazama sana upande wa kulia maana alikuwa amekaa kulia kwangu. Lakini kila nilipotaza sikugundua kitu akili ikanituma nigeuke nyuma nitazame pale kwenye siti tulipokuwa tumekaa naye.

Lakini niliposimama tu kutazama kule kwenye siti..moyo ukashtuka mithili ya mvunjiko wa ‘bawaba’. Nikakumbuka wakati anatafuta simu yake aliniomba nimbeep…na baada ya kumbeep simu yake aliipata katika mkoba wake hivyo akili ikanituma haraka haraka labda shida kubwa ilikuwa ni mawasiliano yangu na ile njia ya kuvunga kapoteza simu ilikuwa ni gia tu ya kupata namba yangu.

Kweli nilijidharau kwa muda nikajiona mimi bata kweli..yaani mtoto wa kike kanizidi ujanja kiulaini namna hiyo!!. Basi nikaona haina shida nisubiri hicho kitakachojili na kama sio hivyo nilivyofikiri basi liwalo na liwe..kwa muda huo sikushtuka kuangalia namba yake katika simu yangu maana baada ya kuipata simu yake tu, namba yake niliifuta.

Baada ya daladala kufika kituoni nilishuka na kuanza kutembea mdogo mdogo kuelekea home huku njiani nikiwa natafakari nini dhima ya yule dada. Lakini nilipofika nyumbani wakati wa kuvua viatu na soksi ndo “nilistajabu ya Musa kabla sijaona ya Filauni”

Mwanzoni nilipoitazama niliona kama suluali yangu imedondokewa na vitu vyeupe mithili ya unga au poda katika mguu wa kulia karibu na viatu….ambapo nilitumia dekio la mlangoni kufuta uchafu huo na ukatoka kawaida lakini nilipokuwa najifuta, nilikuta suluali yangu imekatwa ka-kipande kadogo kiasi usawa wa pindo la suluali chini kabisa katika mguu wa kulia.

Nilianza kujiuliza ni wapi nilipopita hadi suluali yangu kuchafuka namna hiyo sikupata jibu lakini nilipo iona ile sehemu iliyochanwa na kuondolewa kabisa sehemu ya kipande cha suluali nilipatwa na hofu sana na akili ikanituma moja kwa moja kuwa hiyo ni kazi ya yule dada aliyekuwa katika daladala.

Ndipo nilipokumbuka muda flani nikiwa mle kwenye daladala muda mfupi baada ya kupata simu yake nilimuona akifungua mkoba na kutoa kitana, kioo na vitu vingine ambavyo sikuvichunguza vizuri kisha akainama kidogo katika seati akawa kama anaseti nywele si unajua tena mambo ya wanawake wa town.

Lakini katika harakati ile nilimsikia kama kadondosha kitu, halafu akainama chini kwenye siti kukiokota ambapo aliinamana kwa sekunde kadha kisha akainuka na kuchukua vitu vingine na kuvirejesha katika mkoba….mimi kwa wakati huo nilikuwa simzingatii sana tena nilikuwa namwangalia kiwiziwizi.

Ndipo nilipopata jibu kwamba muda huo ndo aliutumia kufanya kitendo hicho..lakini swali linabaki “nini haswa kusudi la kitendo hiki?” Na je, mimi nitaathilika kwa namna gani kuhusu hilo?.  “kwanini mimi?”. Maana ilionekana walisonteana kidole kisha mmoja akaniwahi katika gari…haya yote yanaendelea kunichanganya sana.

Lakini kila napofikiria na kusubiri kuona hicho kitakachotokea nikijiuliza nini tena matumizi ya namba yangu ambayo aliipata kiujanja ujanja.. “kweli sipati jibu”, kwa bahati mbaya mimi yake niliifuta ningeweza kumtafuta lakini pia kwa upande mwingine najipa matumaini kwamba kama alichukua namba basi atanitafuta….japo kwa nafasi hii nahisi labda ni kwa matumizi yake.

Nafikiria mambo mengi sana lakini sipati jibu kuwa ni ushirikiana wa kunidhuru, ni ushirikina wa kuweka mambo yake sawa? Au ndo nalogwa nidate kwenye mapenzi mazito ya mtoto wa kishua? 
Lakini kakosa nini hadi mimi.. tena kwenye daladala, hajawahi kuniona hata siku moja? Nguo yangu inahusikaje? Nimebaki na maswali sipati jibu, najuta kuifuta ile namba bora ningempigia mapema nimuulize.

Hapa sina jinsi zaidi ya kusubiri kitakachonikuta… ila hofu yenyewe inanikondesha kila kukicha na namuogopa kila ninaekaa naye kwenye daladala.. Nasubiri na bado sina jibu! Kilichobaki ni maombi tu.

Jerry Muro Aandika Haya Baada ya Haji Manara wa Simba Kufungiwa na TFF

$
0
0

Basra ya shirikisho la soka Tanzania OFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFF kutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu. 

Afisa habari wa zamani wa Yanga ambaye nae alifungiwa mwaka mmoja Jerry Muro ametumia ukurasa wake wa instagram kuandika

“Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara“ 

KWA Utajiri Huu wa Ridhiwani Kikwete,,Bill Gates Haoni Ndani..!!!!

$
0
0

Ukipanda daladala huwa hakuna mfumo unaoeleweka, siku nyingine utakutana na kelele kama sokoni, wale wanaongea yao, hawa wanabishana hivi, hapa napo kuna ubishi wa soka.

Siku nyingine ndani ya daladala kama mnasindikiza msiba, kimya kinatawala. Wakati mwingine kuanzia mwanzo wa kitu mpaka mwisho ni ugomvi tu kati ya kondakta na abiria. Kimsingi daladala huwa haina utaratibu maalum.

Nikipanda daladala huwa napenda kukaa siti ya mbele au karibu na dereva ili nijifunze jinsi ya kuendesha. Si unajua tena, wanasema ukiwa karibu na mahakama lazima utajua vifungu vya sheria. Matunda ya ujirani hayo.

Nikiwa namtolea macho dereva jinsi anavyobadili gia kwa mbwembwe, abiria aliyekuwa amekaa pembeni yangu akanifinya, nilipogeuka akanipa ishara nitazame mlangoni. Kulikuwa na mrembo anaingia.

Yule abiria jirani yangu alimfuatilia yule mrembo mpaka alipokwenda kuketi, kisha akanigeukia na kuniambia: “Kaka umeona mambo ya Ridhiwani Kikwete?”

Nikawa sijamuelewa, nikamuuliza: “Ridhiwani Kikwete amefanya nini hapo?”

Akasema: “Kaka si unaona mwenyewe mwanamke alivyo mzuri, ameumbika. Yule siyo wa kawaida.”

Nikamuuliza tena: “Sasa kuumbika kwa huyo mwanamke kunahusiana nini na Ridhiwani?”

Akanijibu: “Kumbe wewe ndugu yangu umechelewa mjini, nilivyokuona nilidhani mchangamfu mwenzangu wa jiji. Kwa taarifa yako misemo yetu sisi watoto wa mjini ni kwamba vitu vizuri tunaita mambo ya Ridhiwani.

“Magari yote mazuri mjini ni Ridhiwani, vituo vya mafuta vikubwa vyote Ridhiwani, maghorofa makubwa ni Ridhiwani, ndiyo maana na wanawake wazuri wote mjini tunasema ni mambo ya Ridhiwani.”

Aliposema hivyo, alinikumbusha kitu. Ikabidi niingie kazini kufanya mahojiano, maana habari za Ridhiwani na utajiri wake ni nzito na zimekuwa zikizungumzwa kwa kitambo kirefu sasa.
Nikamuuliza yule abiria: “Lakini ndugu yangu wewe si una mke? Ni mzuri au mbaya?”

Akajibu: “Wewe unaniona mimi wa kuja? Siwezi kuoa mwanamke mbaya. Mke wangu chuma, kisu kikali, mrembo hasa, tena niliwahi kugombana na Hashim Lundenga alipotaka kumchukua kumuingiza kwenye mashindano ya Miss Tanzania.”

Hapahapo ndipo nilikuwa napataka, nikamuuliza: “Wewe mkeo akiitwa wa Ridhiwani utafurahi?”
Haraka sana alijibu: “Thubutu, patachimbika siku hiyo.”

Uzuri alikuwa anajileta mwenyewe, nikampiga swali lingine: “Sasa mbona wewe unaona sawa kusema wake wa wenzako kuwa ni mali ya Ridhiwani?”

Safari hii kwa utulivu akasema: “Umeniuliza swali lenye maana kubwa, unajua mjini watu wanakuza sana maneno. Kuna kipindi nilikuwa nikisikia jina la Ridhiwani nilikuwa naogopa, siku nilipomuona nikashangaa, kumbe mtu mwenyewe ana umbo dogo tu, tena wa kawaida.”

Aliposema hivyo, siti ya nyuma yetu alikuwepo mtu ambaye alikuwa anafuatilia mazungumzo yetu, akauliza: “Samahani kaka, kama sijakosea nimekusikia ukisema Ridhiwani ana umbo la kawaida, tena dogodogo, hivi ni kweli?”

Abiria pembeni yangu akajibu: “Wa kawaida ndiyo, kwani ulifikiriaje?”

Abiria wa siti ya nyuma akasema: “Jamani hii dunia kumbe unaweza kumuogopa mtu mdogo ambaye unaweza hata kumzaa. Mwenzenu kwa jinsi stori za Ridhiwani zilivyo na jinsi anavyozungumzwa, mimi nilifikiri ni jitu kubwa la miraba minne mara 10.

“Tena niseme ukweli, mimi nilikuwa nafikiri Ridhiwani ni mkubwa kama zimwi, yale madude ya kutisha ya kwenye hadithi za kale. Nashangaa leo unaniambia kumbe Ridhiwani wa kawaida tu. Kusema ule ukweli leo nimestaajabu.”

Abiria mwingine naye akachangia, sasa mada ilikuwa imeshakua na kupanuka ndani ya daladala. Huyu alikuwa mzee. alisema: “Nyie vijana, mimi mwenyewe nilikuwa nasikia sana habari za Ridhiwani kuwa anamiliki mali nyingi, na nikawa naamini kweli na nikawa natangaza.

“Juzi hapa nikashangaa kuna nyumba yangu ghorofa moja nilijenga wakati mambo yangu yakiwa mazuri, nimeshindwa kuimaliza kwa sababu fedha zimekata, ghafla nakuta watu wanaijadili kuwa ile nyumba yangu ni ya Ridhiwani ameisahau ndiyo maana hajaimaliza.

“Tena wale watu walikuwa wanasema Ridhiwani ana nyumba nyingi mpaka nyingine anazisahau. Niliwaambia ile nyumba ni yangu, hakuna aliyenielewa, tena waliniambia nimetumwa.”

Sauti ya kike kutoka nyuma ikasikika: “Kila kitu wanasema cha Ridhiwani, magari, majumba, makontena, migodi, bado kidogo wataanza kutangaza na wake zao ni mali ya Ridhiwani. Ikifika kipindi hicho tukumbushane.”

Mwanamke mwingine akadakia: “Bado kidogo wapi? Mwenzenu usiku leo nimepokea mkong’oto wa maana kutoka kwa mume wangu, kanipiga kweli. Hatukuwa na ugomvi wowote, kafika ananiuliza kama namfahamu Ridhiwani, nikamjibu ndiyo. Hapo ndiyo ikawa chanzo cha ugomvi.

“Akaniuliza tena namfahamu kivipi, nikamjibu kupitia kumsoma kwenye magazeti na kumuona katika televisheni. Mume wangu hakuamini, akasema hana imani na mimi kwa sababu anasikia wanawake wote wazuri ni wa Ridhiwani. Nikamwambia aache wivu wa kijinga, hapo ndipo nilianza kupokea mkong’oto. Mwili wote unauma hapa nilipo.”

Gari lilikuwa limefika Posta, nilipokuwa nashuka nikapata wazo la kuendelea na usaili wangu. Nikamuuliza mpigadebe mmoja: “Unamfahamu Ridhiwani Kikwete?”

Akanijibu: “Namfahamu sana Ridhiwani, yule ni kibosile. Kwanza ni mwili nyumba, bajeti ya serikali yote inamtegemea yeye. Hapahapa mjini ana majumba kibao.”

Mpigadebe akaanza kunionyesha nyumba za Ridhiwani, akasema: “Unaona hii hapa? Mwenyewe ni Ridhiwani. Ila unajua Ridhiwani huwa hapendi sifa za kujulikana kama ana utajiri mkubwa, ndiyo maana hii hapa imeandikwa Benjamin William Mkapa Pension Tower. Huyu Benjamin amewekwa kama geresha tu. Mwenye mali Ridhiwani.”

Akanizungusha, akasema: “Unaona hii?” Ni jengo la PPF Tower, akasema: “Huyu PPF Tower naye amewekwa tu kama geresha, hili ghorofa la Ridhiwani.”

Tukasogea mbele, tukakutana na jengo la Golden Jubilee Tower, akasema: “Kaka umeona Ridhiwani alivyo mjanja, yaani majengo yake yote ameyapa majina tofauti. Huyu Golden Jubilee Tower naye kawekwa tu hapa, mwenye mali ni Ridhiwani.”

Tukiwa tumesimama nje ya jengo la Golden Jubilee, mpigadebe akanionesha jengo la Viva Tower, akasema: “Lile pia la Ridhiwani. Viva Tower naye kama wenzake, amewekwa tu. Nimeshakwambia Ridhiwani hapendi sifa.”

Tukiwa tunatembea kwa miguu kunionesha mali za Ridhiwani ambazo mpigadebe huyo anazijua, alisema: “Ila ukitaka kujua kama Ridhiwani ni mjanja, majengo yake yote jina la mwisho ameita tower ili wasimuibie. Tower ni jina la mtoto wake.”

Tukajikuta tumesimama nje ya majengo pacha ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT), mpigadebe akaniambia: “Kaka nimekwambia kuna watu wana fedha hapa nchini, unaona haya maghorofa mawili mbele yetu yanayofanana? Yote haya ni ya Ridhiwani.”

Hapo nikaguna, nikamuuliza: “Mbona haya majengo ni ya BOT?”

Naye akaniuliza: “BOT ndiyo nini?”

Nikamjibu: “BOT maana yake ni Benki Kuu.”

Huku akitabasamu, akasema: “Unaona sasa, bila shaka utakuwa umeamini haya majengo ni ya Ridhiwani kwa sababu hata hiyo Benki Kuu unayoisema ni ya Ridhiwani.”

Mpigadebe akanipeleka kwenye majengo pacha marefu kuliko yote Afrika Mashariki na Kati, PSPF Commercial Twin Tower, tukaenda Rita Tower, Uhuru Heights, Umoja wa Vijana Complex na mengine mengi, kote huko alisema: “Mambo ya Ridhiwani kaka, huyu mtu ni kiboko.”
Kwa kutumia simu yangu, ‘niligugo’ na kupata picha ya Ridhwani, nikamuonesha yule mpigadebe kisha nikamuuliza kama anamfahamu, akanijibu ni sura ngeni, hamtambui kabisa.

Nikamwambia huyo ndiye Ridhiwani, yule mpigadebe nusura anichape makofi, akasema: “Toa ujinga wewe, huyo mtoto mdogo anawezaje kuwa Ridhiwani? Ridhiwani ni jitu lenye mwili wake, kwanza haonekani hovyohovyo.”

Alipoona nimekaa kimya, akaniambia: “Huyu alikuwa rais wetu, Jakaya Kikwete si unamjua?” Nikamjibu ndiyo, akasema: “Kwa taarifa yako Ridhiwani ndiye baba wa Kikwete, ndiye amemfanya Kikwete awe rais, ana hela Ridhiwani mpaka yeye mwenyewe zinampa homa.”

Nilipoachana na yule mpigadebe, moja kwa moja nilikwenda Kariakoo, nikakutana na mtu amejiinamia, nilipomuuliza kama anamfahamu Ridhiwani, akanijibu harakaharaka: “Umenitajia hilo jina nahisi kama nakaribia kuuaga umaskini.”

Nikamuuliza: “Kivipi?”

Jawabu lake lilikuwa hili: “Natamani kukutana naye anipe kazi, si unajua anamiliki miradi mingi? Hesabu Daraja la Kigamboni, Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi, ana mabasi na malori mpaka idadi haitambui, majumba na viwanja. Jumlisha Uwanja wa Taifa na ule wa Uhuru baada ya kuununua, sasa hivi yupo anaufanyia marekebisho ili uwe wa kisasa.”

Nilimaliza usaili wangu nikiwa nimechoka kabisa. Niliporudi nyumbani jioni, nilimuuliza mtoto wangu, Captain Nyambo: “Captain unamjua Ridhiwani?”

Captain Nyambo alijibu: “Unamzungumzia Ridhiwani mbunge wa Chalinze, mtoto wa Dk. Jakaya Kikwete?”

Sikuona sababu ya kumjibu swali lake, maana aliniuliza kwa mtindo wa majigambo kuwa anamfahamu sana, nikamuuliza lingine: “Vipi kuhusu utajiri wa Ridhiwani?”

Akanijibu kwa kuniuliza: “Ukitaka stori za Ridhiwani kama changamsha genge, unaweza ukashangaa hata mimi mtoto wako mpendwa naambiwa ni wa Ridhiwani, kwa sababu kila kitu kizuri kimekuwa cha Anko Rizi.”

Nikamwangalia Captain Nyambo, mwenyewe wala hakutetereka, akasema: “Captain Mkuu si mwenyewe huwa unaona mambo yangu ya shuleni? Wabongo hawashindwi kusema Captain Nyambo ana akili sana, atakuwa mtoto wa Ridhiwani.”

Alipoona sifurahishwi na maneno yake, Captain Nyambo aliniambia: “Wewe ndiye baba yangu, Ridhiwani hana ubavu wa kunipata, Mungu amenifanya wewe ndiye uwe baba yangu, ndiyo maana nakupenda halafu tunaelewana sana.”

“Captain Mkuu eeeh,” Captain Nyambo aliniita, nilipoitika alisema: “Tuache hizo stori za Ridhiwani, hazina tija kwetu. Ila kiukweli baba Tanzania ni ya ajabu sana, yaani kama kila kinachosemwa ni cha Ridhiwani kingekuwa kweli, basi huyu mtu angekuwa tajiri kuliko tajiri namba moja ulimwenguni, Bill Gates.”

By Luqman Maloto
+255 713 355 717

UNAJUA Kwanini Mapenzi ya Mbali Hayadumu? Hizi Hapa Sababu 5..!!!

$
0
0

Wengi wetu hujiuliza kwanini  maisha ya mapenzi ya mbali huwa  hayafiki mbali na kubaki wa kijiuliza tatizo ni nini? Wakati mwingine watu huanza kuulizanaa mchawi ni nani katika mapenzi yao. Laa hasha!! Huenda mchawi wa mapenzi yako ni wewe mwenyewe lakini hujui kwa sababu hakuna mtu ambaye ameshawahi kukueleza jambo hili na lile ndio tatizo

Hata hivyo hakuna kumbukumbu ambazo zinaonesha ni kwa asilimia ngapi ambazo wapenzi wanapenda kuwa mbali mbali japo mazingira mara nyingi ndo huwa chanzo

Katika tafiti mbali mbali zinaonesha kwamba umbali humaliza kabisa mapenzi ambayo  wapenzi wengi wenye malengo ya kufika mbali huwakuta.

Lakini zipo sababu mbalimbali ambazo ukizichanganua utajua kwa nini mapenzi mengi ya mbali huw hayadumu

Wivu.

Wivu huwa ni chachu ya kupima upendo lakini ukizidi pia huwa tatizo. Wivu wa mapenzi  ukizidi husababisha kutokuaminiana  kwani kila mmoja kwa wakati wake tofauti huhisi mwenzake anamsaliti, mara nyingi hali kama hii humfanya mmoja wapo kati ya wapenzi hao wawili kuona kama mwenzake ameshamchoka na anamtafutia sababu. Ni vyema kuwa na wivu kiasi kwa mpenzi wako

Mawasiliano

Mawasiliano huimarisha mapenzi na hufanya wahusika kujihisi wapo pamoja. Inapotokea kuwa na ufinyu wa mawasiliano ndipo hali ya mapenzi ya upande mmoja hupungua na kuhisi kwamba tayari mwanamke/mwanaume tayari ameshapata mwingine wakumfanya asifanye mawasiliano ya mara kwa mara.

Ugomvi

Magomvi ya mara kwa mara hufanya mmoja wenu ahisi kuchoka na mahusiano. Inapotokea sababu za  ugomvi ambao unahisi unaweza kuwa chanzo cha kuvunja mahusiano yenu ni afadhali ukazizuia na kutafuta siku nyingine ya kutatua tatizo hilo.

Kutojali

Hii mara nyingi imetajwa sana kuwa ni chanzo cha mapenzi ya mbali kuvunjika kwa sababu  tofauti mfano mpenzi wako alipokuwa karibu ulikuwa ukimpatia huduma mbalimbali kama zawadi nk, lakini anapokuwa mbali unajisahau hali hii humfanya mpenzi wako ajiulize kulikoni?

Usikivu

Nayo ni sababu ambayo ukiwauliza wengi wao ambao walikuwa na uhisiano wa mbali ukavunjika lazima atakulalamikia kwamba alikuwa hanisikilizi nachomwambia. Mfano alitaka kutoka kwenda ‘OUT’ na wenzake nikamyima lakini hajanisikiza hivyo hanifai.

Hizi huenda zikawa ni baadhi ya sababu ambazo wapenzi wengi ambao mapenzi yao hayajafanikiwa kama jinsi walivyo hitaji wamekumbana nazo.

Ili kuepuka changamoto za kutengana  na mtu ambaye unamuhitaji katika maisha yako ni vyema ukaanza kujifunza pole pole kutoka kwake ili siku ukiwa mbali naye ujue kipi mwenzako anapenda na kipi hakipendi mnapokuwa mbali.

GWAJIMA Aingia Anga za Rais Magufuli..Anena Haya Kuhusu Ujenzi wa Reli ya Kisasa Nchini..!!!

$
0
0

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme  baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli  ya kisasa(standard gauge).

Gwajima ameyasema hayo jana katika ibada ya Jumapili  huku akimsifu Rais Magufuli kwa kuchukua hatua hiyo.

Alisema licha yeye ni mchungaji wa Taifa na anaamini ipo siku Dar es Salaam yote itakwenda kanisani kwake kusali.

Nay Achezea Kichambo cha Haja Kutoka kwa Mzazi Mwenzake..!!!

$
0
0

Msanii wa hip hop, Nay wa mitego amechezea kichambo kutoka kwa mzazi mwenzake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Skyner Ally kuwa ameshindwa kuwa baba bora kwa binti yake.

Kwenye ukurasa wake wa instagram Skyner amefunguka maneno hayo akiwa anamtakia heri ya kuzaliwa mtoto wake ambaye amefikisha miaka mitano na kudai kuwa alikuwa na dukuduku kutoka moyoni ndani ya miaka mitano na baada ya kuongea tayari limetoka.

"Thats face you make when you see your 'daddy jina' anakufanyia promotions na kudanganya watanzania kama Oooh my Twin sijui nanunua pisto, hata chupi unayovaa hajui thamani yake maskini. nimevumilia sana It's 5 Years now nimejiskia kutapika na nimetapikaa.  Am done Mungu wa mbinguni nakuomba unijaalie maisha marefu uwezo nizidishie riziki..... uzima wa afya nikuleee mwanangu aje akuone baadae Inshallah umekuja kuwa Waziri wa nchi & Raisi wa nchi then alete pua yake" aliandika Skyner.
"Aidha skyner ameendelea kufunguka kuwa "Endelea na drama zako ila please shobo na mwanangu sitaki...Please unapost picha za mtoto wangu za nini...shobo dundo zanini? Sitaki shobo na mwanangu koma kama ulivyo komaaa...Je, Wababa anaojisifu kama wanapenda watoto wao then hata hawajui mtoto anakula nini anasoma wapi anavaaa nini Wapooooooo? Drama nyingi sana mtandaoni halafu i love You Nyingi Hana Analofanya Wapooooooooo ??? Am done"- Aliongeza Skyner.

Skyner hakuishia hapo  aliendelea kutoa husia kwa binti yake kwa kuonyesha jinsi alivyo na umuhimu katika maisha ya binti yake "Hakuna anayejua thamani yako zaidi yangu hata huyo anayejita baba'ko hana analolijua kuhusu wewe, si shule, malazi wala chakula kutwa kucha kukupost na kuongopea jamii kama anakujali, ninayehangaika nimie nakuhakikishia na kumuomba Mola wangu anijaalie uhai nguvu uwezo riziki nizidi kukulea kwa nguvu zangu Inshallah nakuonea gere sana umepata mama bora na sio bora mama uko mikono salama mwanangu wa uchungu. Happy Birthday My Happiness"- Skyner alimaza 

Maneno hayo makali kwa Skyner yalikuja muda mfupi baada ya Nay kuweka picha ya binti yake na kumtakia heri ya kuzaliwa na kudai kuwa amenunua bastola kwa ajili ya kumlinda.

BABA Levo - CCM Kikwazo cha Maendeleo..!!!

$
0
0

Diwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma kwa tiketi ya ACT Wazalendo, Baba Levo amesema wakati anakabidhiwa Zahanati ya kati hiyo ambayo ilikuwa chini ya CCM toka Tanzania inapata uhuru, ilikuwa na uwezo wa kupima Malaria na kupima uzito tu.

Akiongea kwenye kipindi cha East Africa Breakafast Baba Levo amesema kata hiyo ilikuwa haina maendeleo kutokana na kuwa chini ya CCM kwa muda mrefu lakini toka kata hiyo imechukuliwa na upinzani chini yake saizi imepiga hatua ndani ya muda mfupi.

"Kata ya Kigoma Kaskazini ilikuwa inaitwa Butiama kwa sababu toka nchi hii imezaliwa ilikuwa inaongozwa na CCM sasa shida moja iliyoikuta ile kata unakuta kiongozi anayeongoza ile kata ni CCM lakini Kigoma Mjini yenyewe mara nyingi ilikuwa inaongozwa na madiwani wa upinzani, kwa hiyo unajikuta ile Kata uwezo wa kupata maendeleo ni ngumu" alisema Baba Levo 

Mbali na hilo Baba Levo anasema wakati anakabidhiwa Zahanati hiyo na CCM ilikuwa na uwezo wa kutibu Malaria tu na kupimisha uzito kwa watoto.

"Sasa hivi kata ya Mwanga Kaskazini imekuwa ndiyo bora kwa mkoa wa Kigoma, imekuwa bora kwa sababu diwani wao nimetimiza ahadi zangu maana mimi niliahidi ahadi saba tu, na kwa mwaka wangu wa fedha wa 2016/2017 nimetimiza ahadi tatu kwa hiyo katika miaka mingine iliyobakia natakiwa kutumiza ahadi nne ambazo ni rahisi tu. Mimi wakati naipokea ile kata nilikuta ina zahanati lakini zahanati ile ilikuwa inatibu Malaria peke yake, kumbuka Zahanati ina kiwango cha magonjwa ambayo inatakiwa itibu yakizidi mgonjwa aende hospitali kubwa lakini zahanati hiyo ilikuwa inatibu Malaria peke yake na kupima uzito watoto kama kliniki sasa nikajiuliza kama hii inahudumua watoto peke yake hii ni zahanati au Chekechea ya watoto? alihoja Bab Levo 

Baba Levo anasema toka amekuwa diwani saizi hiyo zahanati imekuwa ikitoa huduma zote na kusema amezidi kuiboresha, kwa kuingiza maji, kufunga umeme, pamoja na kujenga vyoo vizuri.

JULIAS Mtatiro: Baada ya Kujua Njama Zote Hizi Chama Chetu Kinajizatiti Kuchukua Hatua Hizi..!!!

$
0
0

OCD na OCCID wa Magomeni, wameelekezwa na mamlaka za juu (zisizotajwa) ati wawaite viongozi wa CUF (waliovamiwa jana na kundi la Mungiki la Lipumba), pamoja na Wavamizi (Lipumba na wenzake) ati OCD na OCCID wawapatanishe viongozi wa makundi hayo.

Baada ya maelekezo hayo, OCCID amewasiliana na viongozi waliovamiwa jana na MUNGIKI kuwaomba eti wakutanishwe na wavamiaji ili waombane radhi!

Yaani, wale wavamizi waliokuwa na bastola, mapanga, nondo na waya za umeme waliovamia mkutano wa jana na kuwapiga viongozi wa CUF na Waandishi wa Habari, eti majambazi hayo yapatanishwe na upande uliovamiwa (chama). Na wapatanishi ni POLISI.

This is so low and very stupid. Watu wamevamia mkutano halali kabisa wa chama, baada ya kuumiza watu na kuwatisha, wakakimbilia kwenye magari na kutokomea, eti watu hao sasa ni lulu na polisi inawalinda kweli kweli, hawagusiki!

Sasa mimi nawaambia POLISI, hebu wawasake wale Majambazi walioua POLISI wetu wasio na hatia kule Kibiti, wakishawapata majambazi hao, wapatane nao. I mean kwamba, POLISI wakapatane kwanza na wale majambazi waliotuulia vijana nane, ndipo waje kupatanisha haya majambazi ya jana VS Viongozi waliovamiwa/Waandishi wa Habari!

POLISI wameelekezwa wasimpeleke mahakamani Jambazi huyo alokamatwa na wameelekezwa wapotezee ile BASTOLA iliyooneshwa na yule Usalama wa Taifa aliyetumwa kuungana na MUNGIKI kufanya shambulio la jana.

Baada ya kujua njama zote hizi chama chetu kinajizatiti kuchukua hatua. Tunataka kuona Majambazi haya wanafikishwa mahakamani haraka na yaeleze ile Bastola ilikuwa ya nani? Hatuwezi kuwa na mazungumzo na watu wanaovaa kininja, wakipiga na kuumiza raia wasio na hatia.

Kama POLISI hawachukui hatua wanachofanya ni kuacha mambo haya yaendelee ili watu waanze kuuana, vifo vikishatokea eti ndiyo watasema kuna JINAI zimetokea. Sisi tunatimiza wajibu wetu. Shameful indeed!

JSM.
Viewing all 104689 articles
Browse latest View live




Latest Images