Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104713 articles
Browse latest View live

BINTI wa Mugabe Kugombea Urais wa Zimbabwe..!!!

$
0
0

Makamu wa Rais wa zamani wa Zimbabwe Joice Mujuru alikuwa swahiba mkubwa sana wa kisiasa wa Rais Robert Mugabe. Alikuwa mstari wa mbele kabisa kumtetea rais huyo na sera zake.

Mujuru mwenye umri wa miaka 61 alipandishwa wadhifa kutoka uwaziri hadi kuwa Makamu wa Rais mwaka 2004. Alikuwa mtetezi mkubwa wa Mugabe wakati uchumi wa nchi hiyo ulipokuwa unadidimia, na amekuwa akimuunga mkono na kumfanyia kampeni kali katika chaguzi tatu, chaguzi ambazo wapinzani nchini humo na watazamaji wa kimataifa walisema hazikuwa huru na haki.

Mwaka 2007 Mujuru aliwahi kuliambia gazeti la Telegraph la Uingereza kwamba kwa namna walivyokuwa karibu na Mugabe, alikuwa anajihisi kama ‘binti’ yake tu.

Lakini miaka mitatu baada ya kujiondoa kutoka chama tawala cha Mugabe (ZANU-PF) kutokana na madai kwamba alikuwa anapanga njama za kumuua Mugabe, mawasiliano kati yake na rais huyo yakatoweka kabisa.

Anasema tangu ajitoe kutoka chama hicho mwaka 2014, hajapigiwa simu na Mugabe, naye pia hajampigia simu – yaani hawajaongea kabisa.

Akiwa London wiki iliyopita akihamasisha Wazimbabwe walioko nje ya nchi kumtosa Mugabe, Mujuru aliliambia jarida la Newsweek kwamba hana mawasiliano na Mugabe kabisa na kwamba hajutii uamuzi wake wa kujiondoa ZANU-PF kwani aligundua kuwa Mugabe alikuwa anataka kumtumia tu kisiasa.

Mwaka jana 2016 alianzisha chama chake cha siasa – National People’s Party (NPP) – ingawa wapinzani wenzie wana shaka naye hasa kutokana na baadhi ya kauli zake za kusifia sera fulani za Mugabe.

Aidha katika mkutano mmoja mkubwa uliojumuisha vyama vya upinzani mjini Harare mwezi uliopita Mujuru hakuwapo jukwaani ingawa wafuasi wake wengi walikuwepo – kitu ambacho kilianzisha minon’gono.

Hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema uswahiba wa muda mrefu wa kisiasa uliokuwapo baina yake na Mugabe umemsaidia Mujuru kwa kumemjenga hadi kuwa mwanasiasa mashuhuri zaidi nchini Zimbabwe.

Lakini sasa hivi Mujuru anavyojitayarisha kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018, uchaguzi ambao wengi wanaona utatoa fursa ya mabadiliko makubwa ya kisiasa nchini humo, mwanamama huyo anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuwaaminisha wananchi wake kwamba anaweza kuwaletea hali tofauti ya ile iliyopo chini ya ‘mlezi’ wake wa zamani – Mugabe.

Anasema katika uchaguzi ujao Wazimbabwe wataona uzoefu wake katika serikali ya Mugabe kama ni turufu ya kisiasa na siyo doa katika hadhi yake.

Anasema: “Wazimbabwe wamekuwa wananifahamu kwa muda mrefu, tangu nilipokuwa waziri mwenye umri mdogo, na wanafahamu vizuri jinsi nilivyokuwa natimiza wajibu wangu.”

Na sasa hivi Zimbabwe inakabiliwa na matatizo makubwa ya uchumi kwani haujatulia sawasawa baada ya mfumuko wa bei na kuanguka thamani ya sarafu yake (Dola ya Zimbabwe) mwaka 2008/2009. Wakati ule sarafu hiyo ilikuwa inaanguka thamani kwa asilimia bilioni 80 kila mwezi na mkate mmoja uligharimu Dola za Zimbabwe milioni 10.

Sasa hivi asilimia 63 ya Wazimbabwe wako chini ya mstari wa umasikini na robo ya wananchi wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na ukame.

Wachumi wengi wanasema nyingi ya changamoto hizo zinatokana na sera mbovu za kiuchumi za kiongozi huyo. Kati ya 2000 na 2008, Pato la Taifa (GDP) la Zimbabwe’s lilianguka kwa asilimia 50 kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.

KIMENUKAAA..Korea Kaskazini Watishia Kuizamisha Meli Vita ya Marekani Iliyoko Katika Rasi ya Korea..!!!

$
0
0

KOREA KASKAZINI jana imesema itaonesha uwezo wake mkubwa wa kijeshi kwa kuizamisha meli ya kubebea ndege za kivita ya Marekani iliyo njiani kuelekea rasi ya Korea.

Kauli hiyo imekuja baada ya meli mbili za japani kuungana na ya Marekani kwa mazoezi ya kivita magharibi mwa Bahari ya Pasifiki.

Rais wa Marekani, Donald Trump aliamuru meli hiyo USS Carl Vinson kuelekea katika rasi hiyo kufuatia majaribio ya makombora ya nyuklia ya Korea Kaskazini na tishio la shambulio dhidi ya Marekani na washirika wake wa Asia.

Marekani haijataja eneo hasa ambalo meli hiyo imefika, lakini Makamu wa Rais wa Marekani, Mike Pence alisema itawasili ndani ya siku chache bila kufafanua.

“Majeshi yetu ya mapinduzi yamejiandaa kuizamisha meli inayotumia nguvu za nyuklia ya Marekani kwa pigo moja,” Rodong Sinmun, gazeti la chama tawala cha Wafanyakazi nchini humo lilisema.

Gazeti hilo liliifananisha meli hiyo na ‘mnyama mchafu’ na kwamba pigo hilo litaonesha mfano halisi wa uwezo wa kijeshi wa Korea Kaskazini.

Katika kinachoonekana ongezeko la mgogoro baina ya pande hizo mbili, Korea Kaskazini imemkamata mtu mwenye asili ya Marekani na Korea na kufanya idadi ya Wamarekani wanaoshikiliwa mjini Pyongyang kufikia watatu.

Mtu huyo aliyejulikana kwa jina moja la Kim, amekuwa nchini humo kwa mwezi moja kwa shughuli za hisani, shirika la habari la Yonhap limesema.

Alikamatwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa Pyongyang wakati akijiandaa kuondoka humo.

Taifa hilo linatarajia kuadhimisha miaka 85 ya kuwekwa msingi wa jeshi lake la watu wa Korea kesho.

Huko nyuma maadhimisho muhimu kama hayo yamekuwa yakiendana na majaribio ya silaha.

Hukumu ya Babu Seya, Papii, Mapya Tena

$
0
0
Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro.

“Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana.

“Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?



“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.

“Sasa ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba, kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.

“Kingine kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).

“Kwa hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.

“Hili suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.


TUMEFIKAJE HAPA?

Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Januari 27, mwaka, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Nyaucho Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari, 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis Nguza.

Mali za Lugumi Mikononi Mwa TRA

$
0
0
Kampuni  ya udalali ya Yono, imefanikiwa kukamata mali za wafanyabiashara wanaodaiwa kodi ya serikali inayofikia zaidi ya Sh bilioni 68.1. Operesheni ya kukamata mali hizo kwenye maeneo mbalimbali ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam imefanywa ndani ya wiki moja.

Katika operesheni hizo maofisa wa Yono wamekuwa wakishirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato(TRA), ambayo ndiyo imeipa kampuni hiyo kazi ya kukusanya kodi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono, Scholastica Kevela, Yono imepewa kazi na TRA kukusanya madeni yake ya kodi kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Pwani Njombe, Mbeya, Iringa na Zanzibar.

Aliwataka watanzania kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuleta maendeleo kwa kulipa kodi bila shuruti ili zipatikane fedha za kujenga miundombinu kama barabara, reli, shule, madaraja, hospitali na zahanati.

Kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba hata baadhi ya mali za Kampuni ya Lugumi zimeshikiliwa, Mkurugenzi huyo alithibitisha kuwa habari hizo ni za kweli ambapo wanashikilia nyumba za kifahari za mfanyabiashara huyo.

“Mmeniuliza kwamba mmesikia nyumba za Lugumi zimefungiwa ni kweli, amefungiwa nyumba zake za kifahari na anadaiwa Sh bilioni 14, yupo mtu anaitwa Gm Dewji naye anadaiwa Sh bilioni 1.8, Kampuni ya ujenzi ya Mutluhan Construction anadaiwa Sh bilioni 45,” alisema.

Alisema wanaodaiwa wanapaswa kulipa madeni yao TRA ndani ya siku 14 na kwamba muda huo ukipita watapewa maelekezo na serikali kama ni kuuza mali hizo ili kufidia madeni yao.

Ofisa Mwandamizi wa TRA, ambaye hakupenda jina lake litajwe alithibitisha kwamba nyumba ya Lugumi iliyoko Upanga mtaa wa Mazengo inashikiliwa na mamlaka hiyo na ghorofa la kifahari lililoko Mbweni JKT, Dar es Salaam.

“Hakuna siri maana mkienda kwenye hizo nyumba mtakuta alama ambazo huwa Yono wanaweka kwa nyumba inayoshikiliwa, nendeni Upanga na kule Mbweni JKT mtakuta hizo nyumba tunazoshikilia,” alisema

RAY C Afunguka ya Moyoni Jinsi Anavyomtamani Chid Benzi..!!!

$
0
0

Msanii mkongwe ambaye kwa sasa anasikika na ngoma ya 'Unanimaliza' Rehema Chalamila 'Ray C' amekiri kutamani kufanya kazi nyingine na rapa Chid Benzi na anamuombea kwa Mungu ili aweze kutoka rasmi kwenye mtihani wa dawa za kulevya

Ray C amefunguka hayo hivi karibuni na kusema kuwa mbali na kuwa walisha fanya wimbo wa pamoja na Chid Benz kipindi cha nyuma wa ‘Nihurumie’ bado uwezo  mkubwa wa kimuziki alionao Chid ni sababu inayompa shahuku kubwa ya kutaka kufanya naye kazi kwa mara nyingine.

"Chid benzi ni bonge la msanii na kwa upande wa Hip hop nadhani ni 'one of the best artist' na kwa sasa hayupo pengo lake linaonekana. Nampenda sana Chid Benzi  na ninamuombea sana kwa Mungu aweze kutoka katika janga hilo la madawa na akirudi natamani kufanya nae kazi nyingine. Aweke nia naamini atatoka" alisema Ray C 

Pamoja na hao Ray C ametoa ushauri kwa watu wanaopitia matatizo haswa utumiaji wa madawa za kulevya na kusema kama ukitanguliza nia ya kuachana na mateso lazima utashinda mitihani.

"Binadamu wote lazima wapitie mitihani lakini tatizo mitihani hiyo lazima itakuwa inatofautiana. Haifurahishi kabisa kumuona mtu anateseka na matumizi ya dawa .Kama binadamu lazima uwe na nafasi ya kujifikiria kwa sababu hakuna mtu anayeweza kubebea ugonjwa au matatizo. Naamini Mungu aliyenisaidia mimi nikatoka kule atawasaidia wote siyo Chidi tuu bali wote wenye nia ya kuachana na yale mateso"- aliongeza Ray C.

CHADEMA Yakanusha Kupoke Barua ya Bunge Inayowataka Wapeleke Majina ya Wagombea Ubunge wa Afrika Mashariki (EALA)...!!!

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kuwa hakijapokea barua yeyote kutoka bungeni ikiwataka kupeleka majina ya wagombea ubunge wa Afrika Mashariki (EALA).

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya, amesema kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinasubiri barua ya maelekezo kutoka bungeni lakini mpaka sasa hakijapokea.

Uchaguzi wa wabunge wa EALA uliingia dosari baada ya wagombea wa Chadema, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje kupigiwa kura za hapana hivyo kukosa wawakilishi wa nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema kuwa mpaka sasa hawajapata barua kutoka kwa katibu wa bunge Dkt. Thomas Kashililah kuhusu hatua wanazopaswa kuchukua.

“Tangu umalizike uchaguzi wa awali hatujapata taarifa zozote kutoka Ofisi ya Bunge, tunasubiri barua kutoka kwa Katibu wa Bunge mchakato gani ufanyike ili suala hilo lifikie muafaka,”amesema Mrema.

Hata hivyo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa kama Chadema watapeleka wagombea waliokataliwa basi wategemee majibu yale yale na kwamba atalazimika kutumia utaratibu mwingine.

YANGA Yatoa Ufafanuzi Kuchezesha Timu B..!!!

$
0
0

Uongozi wa klabu ya Young Africas wamefunguka mazito baada ya mashabiki wa timu hiyo kulalamikia hatua ya uongozi huo kupeleka timu  B vijana chini miaka 20 kuchuana na Kombaini ya majeshi siku ya jana.

Katika taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga amesema kulikuwa na dosari kadhaa katika kufikia makubaliano ya ushiriki wa mechi hiyo ya kirafiki katika kilele cha sherehe za Muungano zilizofanyikia huko Mjini Dodoma hasa upande wa stahiki ya timu hiyo pamoja na ukaribu wa ratiba za michuano ya nusu fainali za FA.

"Uamuzi wa kutokupeleka kikosi cha kwanza ni kwa maslahi mapana ya Yanga katika kufanya vizuri mashindano tunayoshiriki lakini pia kulikuwa na dosari kadhaa katika makubaliano ya ushiriki wa mechi hiyo hasa upande wa stahiki ya Yanga, upana wa kikosi, ukaribu wa mechi ya FA na ligi kuu pia". Alisema Sanga

Pamoja na hayo, Sanga amewaomba radhi mashabiki wote waliosikitishwa na uamuzi huo kwa namna moja ama nyingine huku akiwasii waendelee kuungana na kushikamana ili waweze kutwaa makombe wanayoshiriki kwa sasa.

Kwa upande mwingine, timu ya Yanga U20 iliweza kutoka sare ya bao 1-1 ambapo goli hilo la Yanga lilifungwa na Yusuph Mhilu kwenye dakika 52 ya mchezo.

JE, Unajua Wakati Gani ni Sahihi Kunywa Maji..!!!

$
0
0

Naamini kuwa wengi wetu tunafahamu umuhimu wa kunywa maji na tumekuwa tukisikia kutoka kwa wataalam wa afya kuhusu faida zake kiafya.

Sasa leo napenda tufahamu muda gani au wakati gani si sahihi kunywa maji:-

1. Hupaswi kunywa maji punde tu unapomaliza kazi au kukimbia.

2. Unaporudi tu kutoka kwenye shughuli zako

3.Hupaswi kunywa maji mara tu umalizapo kupata kifungua kinywa (chai) au kula chakula.

4. Pia hutakiwa kunywa maji katikati ya kifungua kinywa (chai) mlo.

Je, ni wakati gani sahihi kwa kunywa maji ?
1. Wakati tumbo lako halina kitu na unajiandaa kupata chakula.

2. Angalau saa 1 kabla ya kula au baada ya kula

3. Mara tu unapoamka asubuhi.

UNAJUA Kuwa Kitunguu Swaumu & Tangawizi ni Msaada kwa Wenye Pumu..!!!?

$
0
0

Pumu ni tatizo la kupumua ambalo mara nyingi huwapata watoto na hata watu wazima kutokana na hitilafu mbalimbali katika mfumo wa kupumua. 

Pumu huweza kusababishwa na kuvimba kwa kingo za mirija ya kuvuta hewa, matatizo ya mzio (allergy), matatizo ya uyeyushaji wa chakula ndani ya tumbo pamoja na matatizo ya kisaikolojia. 

Tatizo hili la pumu likishughulikiwa vizuri kwa watoto wadogo huweza kuisha kabisa. 

Mara nyingi tiba ya pumu huwa hailengi katika kuponya kabisa bali husaidai kufifisha nguvu ya mashambulio ya pumu pale yanapotokea, pia kumbukuza kwa kiasi kikubwa idadi ya mashambulio ya pumu kwa mgonjwa. 

Moja ya njia inayoweza kutoa ahueni kwa mgonjwa wa pumu ni pamoja na hii ya kutumia tangawizi na kitunguu swaumu.

Unachopaswa kufanya ni kukatakata na kuponda punje tatu za kitunguu swaumu zilizochanganywa na kiasi kilicholingana na cha tangawizi. Kisha chemsha katika maji glasi moja na unywe kila jioni kabla ya kulala. Fanya hivyo mara mbili kwa siku asubuhi na jioni

FAHAMU Mambo 6 Yamsingi Yatakayokufanya Uwe na Afya Njema..!!!

$
0
0

Wengi wamekuwa wakituuliza mtindo bora wa maisha ni upi? Jibu ni kwamba mtindo bora wa maisha ni kuishi kwa kuzingatia kanuni za afya. 


Kimsingi mtindo bora wa maisha unahusisha haya yafuatayo:-


1. Kuzingatia ulaji bora 


2. Kufanya mazoezi ya mwili 


3. Kuepuka matumizi ya pombe 


4. Kuepuka matumizi ya sigara au bidhaa zitokanazo na tumbaku na madawa ya kulevya 


5. Kuepuka msongo wa mawazo

6. Kuzingatia kunywa maji yakutosha

FAHAMU Njia Sita za Asili za Kuongeza Nguvu za Kiume ..!!!

$
0
0

Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa watu wengi. Tatizo hili limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa.

Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo hili.

Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo kwani mwili unakuwa umechoka.

Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea.

Jitahidi kutumia vinywaji na vyakula visivyokuwa na sukari nyingi.

Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula  asili na nafaka ambayo haijakobolewa, kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na utakuwa imara katika tendo la ndoa.

Epuka unywaji wa Pombe.

Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.

Fanya mazoezi ya viungo.

Watu wengi wamelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya kutosha. 
Kufanya mazoezi hupunguza kuwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.

Rudisha Virutubisho ambavyo vimepotea mwilini mwako.

Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na matunda ya aina mbalimbali.

Kunywa maji ya kutosha kila siku.

Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu mbalimbali mwilini.

Epukana na msongo wa mawazo.

ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya kwenda faragha na mpenzi wako, unaituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha katika uume.

FAHAMU Mambo Muhimu Yanayokupasa Kuzingatia Ukiwa Kama Kijana..!!!

$
0
0

Matatizo mengi yanayowatokea binadamu husababishwa na mwanzo mbaya wa mipango ya maisha yake. Ni asilimia ndogo sana ya matatizo hutokea kwa bahati mbaya tu kutokana na sababu za hapa na pale.

Lakini mengi kati yao, husababishwa na kwenda ilimradi siku zinakwenda. Wale wanaopanga mambo yao mapema huwa hawana kitu kigeni kwenye maisha yao. Kila kitu kinachotokea huwa kwa sababu tayari walishajipanga kabla hakijatokea.

Binadamu makini mwenye mafaikio na afya njema, pamoja na mabo mengine husababishwa na umakini wake katika hatua na mapito ya maisha yake. Ukiweza hayo, maisha yako yatakuwa rahisi.
Hata hivyo kwa bahati mbaya au kwa kutokujua, wapo ambao hukosea sehemu za hatua za maisha jambo linalosababisha baadae waharibu kabisa maisha yao.

Kama kijana unapaswa kujua mambo muhimu zaidi ambayo unapaswa kuyafanya ili maisha yako yawe bora. Kwa hakika mambo haya , kama yakizingatiwa bila shaka kijana atakuwa amejenga msingi imara wa maisha yake na kwamba huko mbele atakuwa mjuzi wa mambo mengi, akiwa na maarifa chanya yatakayomjenga kimaisha.

Imarisha imani yako katika dini

Hofu ya Mungu ni kitu cha muhimu sana katika maisha. Lakini huwezi kuwa na hofu kama ukiwa huna imani. Inawezekana unayo imani yako kiasili, lakini usiwe mshirika mkamilifu wa imani hiyo, 
katika maisha ni kosa. Kuijua, kujifunza, kuifuata, kuitii na kuipenda imani yako itakusaidia sana maishani. Mtu mwenye kuifuata imani yake, bila shaka atakuwa mbali na vitu vibaya.

Ukimjua Mungu hutaiba, hutasema uongo, hutadhulumu wala kufanya mambo mengine yanayofanana na hayo ambayo kimsingi si ya kuwapendeza hata binadamu wenzako.

Msingi wa yote hayo ni kwamba utakuwa kioo kwenye maisha na hapo utapata marafiki wengi watakaokusaidia kutimiza ndoto za maisha yako.

Utii kwa wazazi

Hili ni jambo la msingi sana, uzuri ni kwamba jambo hili limeelekezwa hadi katika vitabu vya dini. Kwamba watoto wana wajibu wa kuwaheshimu na kuwapenda wazazi wao.Heshima kwa mzazi kuna faida nyingi, utakuwa na hakika ya kupata radhi zao, hivyo kuwa na uhakika wa kuishi maisha bora.
Kufungamana na jamii

Mafanikio ya maisha yana uhusiano mkubwa sana na namna unavyoishi na jamii inayokuzunguka. Ikiwa utaishi kipeke yako kwa kila kitu, jamii itakutenga. Mazoea haya huanzia katika kipindi cha ujana. Lazima kijana atengeneze wigo mpana wa kuwa mshirika mkubwa kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

Kufanya hivyo kutakusaidia sana kusaidika pale unapokuwa na matatizo. Shiriki kwenye shughuli za kijamii, mfano msiba, sherehe nk. Kujichanganya kwako kutakuweka karibu zaidi na jamii 
inayokuzunguka. Muhimu zaidi ni kwamba, utakuwa sehemu ya jamii na siku zote tunasema mtaji namba moja kwenye maisha ni watu. Ukiwa na watu hesabu maisha yako ni rahisi. Ni kweli vitu muhimu ni fedha, wazo na watu, lakini cha kwanza kati ya vyote ni watu.

Acha tabia ya  kupoteza muda wako sana.

Kuna wakati unaweza usifanikiwe sio kwa sababu huna malengo na mipango mizuri uliyojiwekea ila ni kwa sababu unapoteza muda mwingi katika mambo yasiyo ya msingi na  ya lazima katika upande wa maisha yetu. Na hili ndilo moja ya kosa kubwa wanalofanya vijana na linawazuia kufanikiwa.

Ni ukweli uliowazi ukiwa kijana umekuwa ukipoteza muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiangalia kwa makini hakuna unachokifanya huko kikubwa zaidi ya kupoteza muda wako wa thamani ambapo pengine ungeweza kuutumia kukuzalishia.

Kama unataka kugeuza maisha yako na kuwa ya mafanikio zaidi acha kuchezea muda wako kama unavyofanya sasa. Acha kujivunia ujana ulionao kwa kuamini unao muda wa kutosha. Mapinduzi makubwa juu ya maisha yako unatakiwa uyafanye ukiwa bado kijana. Sasa huwezi kuleta mabadiliko kama utakuwa ni mtu wa kupoteza muda sana. Pangilia muda wako vizuri kisha fuata malengo yako.

Acha kuishi na watu wasio sahihi kwako.

Maisha yako kwa sehemu kubwa umekuwa ukiyafanya kuwa magumu kutokana na kushikilia marafiki wengi ambao sio msaada kwako. Hebu jaribu kuchunguza wewe mwenyewe marafiki ulionao wanakusaidia vipi kukufikisha kule unakotaka kufika katika maisha yako.

Utakuja kugundua kuwa marafiki wengi ulionao ni walewale ambao hawana msaada sana kwako zaidi ya kukurudisha nyuma kimafanikio. Ukiwa katika hali hii upo kwenye hatari kubwa sana, kwani mara nyingi marafiki zako wana nguvu kubwa sana ya kubadili maisha yako kuliko unavyofikiri.

Ili kuweza kubadilisha maisha yako ni lazima kwako kubadili mwelekeo haraka sana na kuchagua marafiki watakaoweza kukusaidia kufanikisha malengo yako kwa sehemu kubwa. Ukiweza kufanya hivyo utakuwa umejiweka kwenye nafasi kubwa sana ya kuweza kufanikiwa.

Usiogope kuchekwa kwa kile unachotaka kufanya.

Mara nyingi umekuwa na fikra za kuogopa kuchekwa kila unapojifikiria kufanya kazi ya aina fulani. Na hili linasababishwa hasa kila unapoangalia elimu uliyonayo unakuwa unajihisi huwezi kufanya kazi fulani kwa sababu ni ya watu wa chini sana katika maisha.

Kwa kuhofia kwako kuchekwa hivyo ndivyo ambavyo umekuwa ukizidi kujichelewesha kufikia malengo yako. Kumbuka kazi ni kazi, kama utaendelea kuogopa watu katika maisha yako kuwa watakucheka kwa jambo unalotaka kulifanya utakuwa unajichelewesha mwenyewe kufanikiwa.

Tambua maisha yako ni maisha yako wewe, usimuogope mtu na kuhisi kuwa atakucheka eti kwa sababu unafanya kitu fulani. Hata ikitokea wamekucheka hiyo  haitasaidia kitu endelea na maisha yako. Kuwa na fikra chanya, achana na mawazo potofu ya vijana wenzako ya kuamini kuchekwa. Ukiendekeza ugonjwa huu wa kuogopa kuchekwa, hakika huwezi kufanikiwa.

RAY Kigosi Afunguka Mambo Mazito Kuhusu Marehemu Kanumba Kuhusika na na Uchawi wa Freemason..!!!

$
0
0

Msanii wa filamu nchini Ray Kigosi amefunguka na kusema kuwa baadhi wa Watanzania ni wanafiki na wamekuwa wakikatisha tamaa watu katika mambo yao kutokana na unafiki wao.

Ray Kigosi amesema hayo kupitia ukurasa wake wa Instgram na kusema kutokana na unafiki huo wa baadhi ya watu ulimfanya mpaka marehemu Kanumba kuvunjwa moyo katika kazi yake.

==>Ray Kigosi ameandika;
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na nguvu za giza!!

2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama Kanumba!

3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !….. HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani industry Ni Mtu sio system !

4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia ya mafanikio kuna watanzania, wasanii wenzake na hata baadhi ya wanahabari wanasema Ni Freemanson, wengine wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini na kina Wema.

Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa ! Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni sehemu ya Maisha.

5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo mganga wangu mkashindwa kumleta, akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema lolote Ni haki Yao.

Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na ubora uliovuka mipaka na viwango ambao hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni nyeusi kiwe nye.

KIMENUKAA..Ndesamburo Aibuka na Kufichua Yaliyojificha Sakata la Richmond..Amuumbua Dk Mwakyembe Livee..!!!

$
0
0

Moto aliouwasha Mwenyekiti wa Kamati teule ya Bunge iliyochunguza sakata la Richmond, Dk Harrison Mwakyembe, umemuibua mwanasiasa mkongwe nchini, Philemon Ndesamburo.

Ndesamburo ambaye ni miongoni mwa waasisi wa mageuzi nchini, alisema Dk Mwakyembe alificha baadhi ya taarifa za sakata hilo ili kuilinda Serikali na mhusika mkuu.

Kauli ya Ndesamburo aliitoa jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuhusu kauli ya Dk Mwakyembe aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, akitaka wanaohoji suala la Richmond walirudishe bungeni.

Bila kumtaja mhusika huyo mkuu, Ndesamburo alisema Dk Mwakyembe ni mtu asiyeeleweka, asiye na msimamo na mwenye ndimi mbili katika suala moja lenye mazingira yanayofanana. “Dk Mwakyembe alisoma ripoti yake bungeni ikiwa na maelezo ya upande mmoja pasipo kumhoji mtu aliyemtaja kama mhusika mkuu wakati anajua vizuri sheria. Natural justice (haki ya asili) inataka umpe nafasi mtu ya kusikilizwa kabla ya kufikia uamuzi, pamoja na kubobea katika sheria, Dk Mwakyembe hakumhoji Edward Lowassa.

Sakata la Richmond liliibuka upya Bungeni wiki iliyopita, baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kumtuhumu Dk Mwakyembe kwa kutomtendea haki Lowassa, aliyekuwa Waziri Mkuu na alijiuzulu kutokana na sakata hilo.

LEO Ndio Leo..Rais Magufuli Kutoa Hatima ya Makonda na Wenye Vyeti Feki..Majina Yao Kuanikwa Leo..!!!!

$
0
0

Rais John Magufuli, leo atapokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.

Kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba mwaka jana.

BABU Ambaka na Kumpatia Ujauzito Mjukuu Wake..!!!

$
0
0

Polisi mkoani Mwanza inamshikilia mkazi wa mtaa wa Nyasaka wilayani Ilemela mwenye miaka 66 kwa kumbaka na kumpata ujauzito mjukuu wake mwenye umri wa miaka 16.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo liligundulika Aprili 25.

Alisema mwanamume huyo alikuwa akiishi na mjukuu wake  (jina linahifadhiwa) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Nyasaka.

“Mtuhumiwa alikuwa akiishi na mjukuu wake tangu mwaka 2011 akitokea Musoma vijijini na alikuwa akimfanyia ukatili wa kingono kwa kumwingilia kimwili wakati  mkewe hayupo,” alisema Msangi.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa alikuwa akimtisha kuwa atamwachisha shule na kumrudisha kijijini kwao mjukuu wake endapo atatoa siri kwa mkewe au ndugu zake.

Msangi alisema kutokana na vitisho hivyo, binti huyo aliendelea kuvumilia hali hiyo pasipo kumwambia mtu na Aprili 25 walimu walitilia shaka hali ya afya yake na alipopelekwa hospitali kupima iligundulika ana ujauzito wa miezi minne.

“Walimu walimhoji aliyempa ujauzito na alidai ni babu yake. Walitoa taarifa kituo cha polisi ambapo walifanya ufuatiliaji na kumkamata mtuhumiwa,” alisema Msangi.

KUMBE! Rais Kim Jong-UN Anashabikia Ligi ya Italia ya Serie A tu..!!!

$
0
0

Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-UN amejibainisha kuwa ni shabiki mkubwa wa Ligi Kuu Italia ‘Serie A’.

Hayo yalibainika muda mfupi baada ya kinda wa miaka 18 Kwang-Song Han kufunga bao kwenye klabu yake ya Cagliari nchini Italia hivi karibuni.

Seneta wa Italia, Antonio Razzi hivi karibuni alipokutana na wawakilishi wa nchi za bara Asia, alielezwa kwamba siyo tu Rais Kim amekuwa akifuatilia maendeleo ya mshambuliajia Kwang-Son, pia ni shabiki mkubwa wa ligi hiyo kwa ujumla.

Rais huyo wa Korea yeye ni shabiki mkubwa wa timu za Italia na mara kwa mara hufuatilia mechi za timu hizo zinapocheza.

Kiongozi huyo anayeonekana kama dikteta, ilielezwa kwamba amekuwa akifuatilia kwa karibu ligi ya Seria A na maendeleo ya mchezaji wa nchi yake, Kwang-Son.

Pia amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka bara hilo kufunga bao kwenye Ligi ya Seria A.

Klabu ya Cagliari ilimsajili mchezaji huyo tangu Februari mwaka huu na mkataba wake utamalizika 2022.

Mchezaji mwingine wa Korea Kaskazini alisajiliwa klabu ya Fiorentina mwaka jana na amekuwa akicheza kwenye timu ya vijana kabla ya kutemwa mwishoni mwa mwaka 2016.


TRUMP Amtumia Rais Magufuli Salamu za Pongezi ya Muungano wa Tanzania..!!!

$
0
0

Rais Donald Trump wa Marekani ametuma salamu za pongezi Tanzania kwa kuadhimisha mwaka wa 53 wa Muungano.

Katika salamu zilizotolewa jana jioni na kuwekwa katika tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje, Trump ameeleza uhusiano baina ya Tanzania na Marekani na matumaini yake ya kuuendeleza.

“Kwa niaba ya Rais Trump na wananchi wa Marekani, nawapongeza wananchi wa Tanzania wakati mnaposherehekea mwaka wa 53 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” anasema Rex W. Tillerson, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.

“Tanzania na Marekani zina uhusiano mkubwa, unaoonyeshwa na juhudi za pamoja kufikia malengo yetu na ushirikiano wa karibu katika programu na jitihada mbalimbali, kuanzia katika afya na elimu, kuendeleza ukuaji uchumi na uongozi wa kidemokrasia na kukuza usalama wa kanda. Katika mwaka unaokuja, tunategemea kufanikisha malengo yetu ya pamoja kadri tunavyoendeleza juhudi zetu.

“Wakati Watanzania wakisherehekea Siku ya Muungano, naungana nao katika matumaini ya kuwa na amani, afya, na ufanisi.”

Hizi ni salamu za kwanza kwa Trump na Serikali yake kwa Tanzania tangu kiongozi huyo kutoka chama cha Republican asimikwe kuwa Rais wa taifa hilo kubwa duniani Januari 20 baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

JPM Kunguruma Kilimanjaro Sherehe za Mei Mosi..!!

$
0
0

Rais John Magufuli amethibitisha  kuwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho ya  siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo kitaifa zitafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwa niaba yake, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki amesema kuwa Rais atakuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,hivyo wananchi na wafanyakazi wajitokeze kushiriki na kusikiliza hotuba yake.

Sadiki amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na huduma za  upimaji wa afya zilizoandaliwa na taasisi za afya hivyo aliwataka wakazi wa mkoa huu na watakaofika kutumia fursa hiyo kupima afya zao.


POLEPOLE Afunguka Haya Mapya Kuhusu Katiba Mpya ya Warioba..!!!

$
0
0

Akiwa ni miongoni mwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema msimamo wake bado upo kwenye Rasimu ya Katiba hiyo.

Polepole aliipigia debe la nguvu rasimu hiyo ambayo miongoni mwa mapendekezo yake ni uwapo wa Serikali tatu; Shirikisho, Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza kwenye ofisi za gazeti hili wiki hii jijini Dar es Salaam, Polepole alisema msimamo wake bado uko kwenye Rasimu ya Jaji Warioba.

“Msimamo wangu ndivyo ulivyo muda wote tangu mwanzo hata sasa na CCM inaamini hivyo, kuheshimu maoni ya wananchi,” alisema Polepole na kuongeza:

“Hatuwezi kupuuza watu kwa namna yoyote, CCM haiko hapa kupuuza watu bali kuwasikiliza na ndiyo maana msingi wa mageuzi ya chama ni kuwa cha wanachama, unapokuwa na chama cha wanachama unakuwa daraja kati ya wananchi na Serikali.” 

Kuhusu utawala wa Rais John Magufuli kwa suala la Katiba, alisema kumekuwa na mageuzi yanayofanywa kabla ya kufikia kwenye mchakato wa Katiba.

Credit - Mwananchi
Viewing all 104713 articles
Browse latest View live




Latest Images