Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

MBARONI kwa Kukutwa na Fuvu la Binadamu..!!!

0
0

Jeshi la Polisi mkoani Pwani linawashikilia watu wawili wakazi wa Kibiti kwa tuhuma za kukutwa na fuvu la kichwa cha  binadamu.

Akithibithisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani,  Onesmo Lyanga amesema watu hao walikamatwa  mwishoni mwa wiki iliyopita wakati polisi wakiwa kwenye doria katika kijiji ya Jaribu.

Lyanga amesema watuhumiwa hao waliokuwa wakitoka Mkuranga kuelekea Kibiti kwa kwa kutumia pikipiki  walikuwa wameficha fuvu hilo kwenye begi.

Amesema baada ya kufika katika kijiji hicho wakiwa kwenye pikipiki  walisimamishwa na polisi waliokuwa doria eneo hilo na baada kuwakagua ndipo walipokuta fuvu hilo ndani ya begi.

Amesema uchunguzi unaendelea ili kubaini mahali lilipotoka fuvu hilo.

MBUNGE Amwaga Chozi Bungeni..Kisa Ni..!!!

0
0

Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) Faida Bakari amemwaga chozi bungeni akielezea udhalilishaji unaofanywa kwa watoto nchini.

Faida akichangia bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni leo mjini Dodoma amesema watoto wanadhalilishwa kwa kufanyiwa vitendo vibaya na watu wazima. Ameiomba Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wanaobainika kufanya hivyo.

“Watoto wanaharibiwa mheshimiwa waziri, naomba mchukue hatua kali za kisheria kwa watu hawa. Nilienda Pemba nililia watoto wanaharibiwa maumbo. Mheshimiwa nasema kwa uchungu,” anasema huku akilia na kuvuta pumzi ndefu kabla ya kuendelea kuzungumza.

Anasema walimu wamekuwa wakiwadhalilisha watoto huko Pemba na kumuomba waziri ashughulikie suala hilo.

“Tumrudie Mungu, unakuta mibaba mizima inawapa mimba watoto na madevu yao mengi wanawatia watoto wenzao mimba,” anasema.

Faida pia amesema wazee wamekuwa wakinyanyaswa katika jamii na kuwataka Watanzania kuwatunza kwa sababu ipo siku nao watakuwa wazee. “Ukiona nyumba zao unalia naomba  mheshimiwa uangalie katika eneo hili la wazee.”

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Suzan Lyimo yeye alisema wazee wametelekezwa katika kambi za kuwahudumia na kuitaka Serikali kuwaangalia.

“Mwaka jana mlisema mtaleta Sheria ya Wazee lakini mwaka huu haikuzungumzwa, hakuna sheria ya wazazi ndiyo maana wazee bado wanauawa,” alisema.

CHAKULA cha Msaada cha CCM Chazua Maswali..!!!!

0
0

Kitendo cha Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kuahidi kutoa tani 500 za mahindi wilayani Longido kimetafsiriwa vingine na Mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga.

Ahadi hiyo ya chakula, imetolewa jana  na Polepole wakati akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Longido na viongozi wa chama hicho ngazi ya kata na matawi.

Katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaban Mdoe, Polepole amenukuliwa akisema chakula hicho, kitaanza kusambazwa kuanzia Jumatatu na kitauzwa  kwa Sh500 hadi 600 kwa kilo.

Hata hivyo, Kalanga alionyesha wasiwasi na kuhoji ni kwa nini chakula hicho kinatolewa Longido?  Na kwa nini ni wakati huu?

“Kuna wilaya za Ngorongoro na Monduli zote hizi zina uhaba wa chakula mbona wanapeleka huko pekee?

“Hii ni aina fulani ya ushawishi wa CCM kutaka wakazi wa Longido kuwapa kura, kwa sababu kuna tetesi huenda uchaguzi jimbo hilo ukarudiwa tena,” alisema Kalanga.

Jimbo la Longido awali lilikuwa likiongozwa na Onesmo Ole Nangole (Chadema) lakini uchaguzi ulifutwa.

MAALIM Seif; Nitaendelea Kugombea Urais Zanzibar..!!!

0
0

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema ataacha kugombea urais visiwani Zanzibar iwapo tu wananchi wataamua asigombee.

Maalim Seif tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1990 amegombea urais wa Zanzibar mara tano kupitia CUF na mara zote amekuwa akishindwa ingawa amekuwa akisisitiza kuwa anashinda lakini anaporwa ushindi.

“Inapofika wakati wa uchaguzi mkuu napata shinikizo kubwa la wananchi visiwani Zanzibara na bara wakitaka nigombee urais na wengine wanaamua kutoa pesa zao kunichukulia fomu ya urais,”alisema.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano na kituo kimoja cha luninga, alisema mipango ya uchaguzi mkuu wa 2020 itaanza ndani ya chama baada ya kumalizika kwa kesi iliyopo mahakamani inayohusiana na mgogoro unaoendelea katika chama.

Maalim Seif amesema pamoja na kuwepo kwa mgogoro huo, hata hivyo hakuna mgawanyiko wowote wa wanachama uliojitokeza kiasi cha kufanya kuwa na makundi mawili kwa maana ya CUF Maalim Seif na Cuf Lipumba bali ipo CUF moja ambayo ni ya wanachama.

Kuhusu utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano, alisema yapo mambo mazuri yanayofanywa na Rais John Magufuli na yapo mengine yenye kasoro.

JINAMIZI la Clouds Lamrudia Makonda..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo Tarehe 4/5/2017..!!!

UKWELI Mchungu...Vyeti Feki Havikubaliki, Tusioneane Huruma..!!!

0
0

Wiki iliyopita ilikuwa ya simanzi kwa baadhi ya watu ambao waliorodheshwa kama watumishi wa umma waliokuwa wanatumia vyeti feki, huku wengine ambao wana vyeti vyao wakilalamika kukuta majina yao katika orodha hiyo.

Ninawapa pole wote ambao wameorodheshwa kimakosa, haki yao bado ipo na watasikilizwa kwa kuwa wana ushahidi wa elimu yao. Hamna haja ya kuwa na wasiwasi kama unajua una sifa na vyeti vyako.

Jambo ambalo halikubaliki ni kwa hawa wengine ambao ama hawana vyeti au wametumia vyeti vya watu wengine kupata ajira katika utumishi wa umma. Orodha ya watu 9,932 iliyotolewa ni kubwa na inaonyesha uozo katika utumishi wa umma.

Baadhi ya watu wamekuwa wakiwaonea huruma watu hao kwa madai kwamba wana watu wanaowategemea. Ni kweli wana wategemezi wao lakini wanasahau kwamba kuna maelfu ya watu wengine ambao wamekosa ajira licha ya kuwa na sifa na elimu ya kutosha.

Hao nao wana ndoto nyingi za maisha na wengine tayari wana familia. Suala la vyeti feki siyo la kuoneana huruma, huu ni wakati wa kurudi kwenye misingi ya utumishi wa umma kwa kuwa na watu wenye uwezo wa kufanya kazi kulingana na elimu.

Kila nafasi ya kazi inakuwa na kiwango cha elimu ambacho mtumishi anatakiwa kuwa nacho ili kutimiza majukumu hayo. Kuweka mtu asiye na sifa ni kukiuka misingi hiyo ambayo inatuelekeza kufuata weledi katika utendaji kazi.

Huenda tumefika hapa kutokana na kuwa na watendaji ambao hawana sifa na uwezo wa kusimamia masuala ya msingi. Hii ni fursa ya pekee ya kutengeneza mfumo wa utumishi wa umma unaowajibika kwa wananchi na siyo genge la watu wanaotafuta “kula”.

Katika utendaji wa serikali, watumishi ndiyo mashine inaoongoza nchi. Wanasiasa ni kama madereva tu lakini mashine yenyewe ni watumishi wa umma. Kama taifa linakuwa na watumishi wasio na weledi basi hata utendaji kazi utakuwa chini au mbovu.

Tujisahihishe! Ninampongeza Rais Magufuli kwa hatua aliyoichukua kwa sababu inalenga kuimarisha utumishi wa umma nchini. Kila mtu atekeleze majukumu yaliyo ndani ya uwezo wake kulingana na sifa za elimu yake.

Nitakuwa mtu wa mwisho kuwaonea huruma watu hawa eti kwa sababu wana wategemezi. Lazima uamuzi mgumu ufanyike sasa kwa ajili ya manufaa ya badaye ya taifa hili. Na katika uamuzi huo ambao tayari umefanyika, lazima baadhi ya watu wataumia.

Ninaamini mlango mmoja ukufungwa, mwingine utafunguka. Siyo mwisho wa maisha kwa watumishi walioondolewa kwenye utumishi wa umma, zipo shughuli nyingi ambazo wanaweza kuzifanya ili kujiongezea kipato mathalani ujasiriamali.

Ombi langu kwa Rais Magufuli ni kufanya mabadiliko ya Katiba ili na viongozi wa kisiasa na wateule wake wachaguliwe kwa kuzingatia elimu yao na siyo tu kujua kusoma na kuandika. Kwa mfano, mtu awe na sifa ya kugombea ubunge akiwa na angalau shahada moja.

Mfumo huo utaongeza uwajibikaji bungeni na kuwafanya wabunge kuwa na upeo mkubwa wa kuhoji mambo bila kuburuzwa na serikali au chama chao. Huo utakuwa ni mwanzo mzuri wa ukombozi wa taifa hili, tayari Kenya wamefanya hivyo.

Tunaamini kwamba wabunge ndiyo watunga sheria, kazi hiyo haiwezi kukamilika kama wabunge hao hawatakuwa na elimu inayowawezesha kuchambua miswada ya sheria, ripoti za ukaguzi wa fedha na bajeti.

Taifa lolote lenye maendeleo linaongozwa na watu wenye elimu. Ukiona kuna ombwe katika uongozi basi chunguza mfumo wa elimu ya nchi hiyo, utabaini kuna kasoro nyingi ambazo zimesababisha mkwamo huo.

Sasa ni wakati kwa serikali kuangalia mfumo wa utoaji elimu ili uwe ambao unamjengea uwezo mwanafunzi. Pia, serikali iweke mazingira magumu kwa watu wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya wengine.

Kadhalika, serikali iwe na mfumo imara wa kusimamia mchakato wa kuajiri wafanyakazi ili watu wasio na sifa wasipate nafasi ya kuingia kwenye utumishi wa umma. Hii ndiyo misingi itakayoweza kututoa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

KAMA Kweli Unampenda Mpenzi Wako Kwanini Umfanyie Unyama Huu

0
0

Pamoja na uwepo wa manjonjo mengi katika ulimwengu wa mapenzi, kizazi hiki kisichotabirika kimeanza kugeuza tendo kuwa kama uwanja wa vita badala ya starehe inayoweza kumhamisha mtu kifikra mpaka katika ulimwengu wa kusadikika.

Vijana wengi wamekua busy kutafuta dawa za kuwafanya wawe na nguvu kupitiliza kanakwamba wanaenda vitani. Wengine wanatamba kwamba akikukamata ni mpaka kivimbe ndo akuachie. Kwani lengo ni kuumizana?

Mchezo ule hauhitaji hasira ila upole, utaratibu maalum na hisia kali zitakazo kuhamisha katika ulimwengu uliopo. Inashangaza kuona mtu ana-pump kama anazibua chemba iloziba mwaka mzima na kumsababishia kero na maumivu makali mwenza wake.

Ukifanikiwa kukaa jirani na eneo ambalo zoezi hilo huendelea unaweza kusikia kelele nyingi utadhani mtu anapigwa mangumi ila ukiuliza utaambiwa ni wapenzi wanagegedana.

Hebu tujaribu kufanya romantic love na sio vita na utaona matokeo yake, upendo utazidi kuliko awali.

Nini maoni yako ? Share na Washkaji Pia.

MANARA - Tunahitaji Dakika 9 Tu Kuichapa Mbao FC ..!!!

0
0

Msemaji wa Klabu ya Simba SC, Haji Manara ameanza majigambo yake mapya kwa kuwaambia Mbao FC watatumia dakika tisa tu kuwaangamiza katika fainali za Kombe la FA, zinazotarajiwa kuchezwa Mei 28, katika uwanjwa wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Manara amebainisha hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kujigamba kuwa Simba wanawajua vizuri Mbao FC, na kusema walishawahi kuwafunga hapo awali katika uwanja wao wa nyumbani CCM Kirumba ndani ya dakika tisa tu.

“Kama Simba ili wachukua dakika tisa kuwafunga wababe wa Gongowazi (Yanga) pale kwao Kirumba, unadhani itatuchukua dakika ngapi katika mji wenye ‘Fans’ wengi zaidi wa Simba kumgalagaza ‘Ngariba’ wao, tutashinda kokote InshaAllah”. Aliandika Manara kupitia Instagram yake.

Kwa upande mwingine, timu itakayoweza kuibuka kidedea kwa ushindi dhidi ya mwenzake itaweza kupatiwa kitita cha Milioni 50 fedha taslimu za kitanzania kutoka kwa wadhamini wa mashindano hayo pamoja na kuiwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika linalosimamiwa na CAF.

AHUKUMIWA Kifungo cha Maisha Jela kwa Kuchoma Nyumba..!!!

0
0

MKAZI wa kijiji cha Kabita wilayani Busega mkoani Simiyu, Hezroni Mahila (28) amehukumiwa kutumikia kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuchoma nyumba na kusababisha hasara ya Sh. 6,000,000.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa Simiyu, John Nkwabi, baada ya mtuhumiwa kukubali kutenda kosa hilo.

Awali kabla ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Moses Mfuru, alieleza mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Februari 24, mwaka jana, saa 8:00 usiku kwa kuchoma nyumba mali ya Kapeji Sostenes.

Baada ya kusomewa shtaka lake, mshtakiwa alikiri kutenda kosa hilo na kuomba kupunguziwa adhabu kwa madai kuwa hakuisumbua mahakama lakini hakimu alimhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha.

AFYA ya Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria Bado Kitendawili..!!!

0
0

Hali ya Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari, inazidi kua kitendawili kwa wananchi wa nchini humo baada ya rais huyo kutoonekana kuweza kuyamudu na kuyatekeleza majukumu yake kama mkuu wa nchi.

Rais Buhari, alikua kwenye matibabu nchini Uingereza mapema mwaka huu, ambapo alikaa kwa takriban wiki sita akiuguza maradhi ambayo bado hayajawekwa wazi na Serikali yake. Hata hivyo, siku ya jana, wanaharakati kutoka katika Asasi za Kiraia wametoa tamko wakimtaka Rais Muhammadu Buhari achukue likizo ya matibabu kutokana na afya yake kutetereka.

Rais Buhari hajahudhuria vikao viwili vya Baraza la Mawaziri hali iliyozua taharuki juu ya afya ya kiongozi huyo.

Mke wa Rais huyo, Aisha Buhari leo amekanusha tetesi za Rais huyo kuugulia maradhi makali kupitia mtandao w twitter na kusema mume wake haumwi kiasi hicho ambacho watu wanahisi. Wananchi wa Nigeria wameanzisha kampeni katika mitandao ya kijamii kwa kiunganishi cha #WhereIsBuhari (Yuko Wapi Rais Buhari).

MFAHAMU John Stephen Akhwari; Mtanzania Maarufu Ulimwenguni Kuliko Hapa Bongo..!!!

0
0

John Steven Akhwari ni mwanariadha mstaafu. Alizaliwa mwaka 1938 kule Mbulu- Mkoani Manyara. Aliiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Olimpic mwaka 1968 nchini Mexico, katika mashindano ya riadha ya kilomita 42. Washiriki walikuwa 75, lakini waliomaliza shindano ni 57 pekee, huku John Steven Akhwari akimaliza wa mwisho kabisa.

Kwa nini alimaliza wa mwisho? Baada ya mbio kuanza, walipofika kilomita ya 19, mshiriki mojawapo alimparamia, kumsukuma na kuanguka vibaya mno. Aliumia begani, na goti la mguu wa kulia lilitenguka. Gari la huduma ya kwanza lilimfikia na kumpa matibabu, akaweza kusimama tena na kuendelea na riadha.

Umaarufu wake duniani. Watu waliomhudumia walimlazimisha kuaihirisha shindano na apande kwenye gari lakini alikataa katakata. Aliendelea na riadha huku akichechemea. Alifanikiwa kumaliza kilomita zote 42, jioni ya saa 1 kwa saa za Mexico. Watu wachache waliokuwa wamebakia uwanjani walimshangilia sana.

Mwishoni kabisa, waandishi wa habari walimuuliza, Kwa nini aliendela kukimbia ili hali ameumia kiasi hicho? Aliwaambia Nchi yangu Tanzania haikunituma maili 5000 kuja Mexico kuanza hili shindano bali walinituma kumaliza shindano.

Katika mashindano ya Olimpic na mpaka hivi leo Bwana John Stephen Akhwari anatambulika kama 'The Greatest Last- Place Finish Ever'. Japo hakushinda tuzo yoyote lakini ameonyesha uvumilivu, ujasiri na wenzetu wamekuwa wakimtumia kufundishia watoto na vijana wao kwamba they must struggle to finish the race, not just to start it.

Kwa bahati mbaya sana, watanzania walio wengi hawamjui. Huyu ni mfano wa kuigwa, ilistahili kauli yake hiyo ingekuwa nukuu muhimu kwa vijana wetu. 

Lipumba amwagia sifa Jecha kufuta matokeo Zanzibar

0
0

Mwenyekiti wa CUF Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, amesema ni afadhali  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar(ZEC), Jecha Salim Jecha aliyefuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar  kuliko Maalim Seif aliyejitangazia matokeo.


 Lipumba amesema, Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF alifanya kosa kubwa  kujitangazia matokeo.


Lipumba anaendelea na mahojiano ya moja kwa moja yanayorushwa na televisheni ya Clouds.

Sakata la Makonda kuivamia Clouds laibuliwa upya

0
0

SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds liliibuliwa upya na wadau wa habari jana baada ya kulilaani.


Wadau hao wa habari walilaani tukio hilo jana ikiwa ni siku maalum ya Uhuru wa Habari iadhimishwayo Mei 3 kila mwaka.


Akizungumza kama mgeni rasmi katika siku hiyo jijini, Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), mkoa wa Dar es Salaam, Salma Mwasa alisema si jambo jema viongozi wa umma kuonekana wanakuwa mstari wa mbele kuminya uhuru wa habari.


Alisema kitendo alichokifanya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ni cha kulaaniwa na kitaendelea kulaaniwa na kila mpenda amani na mpenda ustawi wa vyombo vya habari, na anayetambua umuhimu wake katika nchi.


“Viongozi wa umma na watunga sera, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda vyombo hivi vya habari na kuhakikisha vinafanya kazi yao kwa uhuru," alisema Mwasa.


"(Viongozi wa umma) wanapogeuka na kuonyesha wa kwanza kuviminya (vyombo vya habari) inaonyesha sifa mbaya na hawapeleki ujumbe mzuri kwa hawa wengine wanaowategemea, wanaowasikiliza na kuwaamini.


“Kiukweli kile kitendo kinatakiwa kulaaniwa na kitaendelea kulaaniwa, kwa sababu pasipo kufanya hivi, vitendo hivi vinaweza kuendelea kufanyika na huko tunakoenda hali ya uhuru wa vyombo hivyo inaweza ukawa mgumu zaidi.”


Tukio hilo la staili ya utekaji wa vituo vya habari wakati wa mapinduzi ya kijeshi, lilifanywa na mkuu huyo Machi 17 saa 5 usiku.


Mkuu huyo alionekana katika video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na askari wasielekea kuwa polisi, waliokuwa na bunduki.


Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya waziri iliyochunguza sakata hilo, mkuu huyo alivamia kituo hicho usiku huku vipindi vikiwa vinaendelea na kwamba aliwatisha na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kuonyesha taarifa yake.


Taarifa hiyo ya upande mmoja, ilikuwa ikimtuhumu Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuwa amezaa na muumini wake.


Gwajima ambaye alikanusha vikali madai hayo kanisani kwake, alianzisha tuhuma za mkuu huyo kutumia cheti feki kujiunga na elimu ya juu na kwamba jina lake halisi ni Daud Bashite.


Mwasa alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyosonga na kwamba licha ya changamoto wanazokutana nazo, waandishi wa habari hawapaswi kukata tamaa.


“Tumeshuhudia baadhi ya waandishi wanapigwa na wengine hata kujeruhiwa wanapokuwa wanafanya kazi zao," alisema Mwasa. "Nataka kuwaomba wasikate tamaa."


"Watanzania wanawategemea, wakumbuke kuwa hakuna ukombozi bila mateso, tunajua wako katika wakati mgumu lakini tunaomba hali hiyo isiwakatishe tamaa.”


Alisema wao kama wawakilishi wa wananchi, wataendelea kupambana kuhakikisha uhuru huo unalindwa hata ikiwezekana kujenga hoja bungeni ili Sheria ya Vyombo vya Habari iliyopitishwa hivi karibuni irudishwe bungeni ili baadhi ya vipengele ambavyo vilionekana kuwa vina mtego kwa waandishi hao, virekebishwe.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Siasa (Taporea), George Maziku alisema ripoti ya hali ya uhuru wa waandishi wa habari iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka inaonyesha kuwa katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi 800 kutoka mataifa mbalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza majukumu yao.


Akizungumzia Sakata la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni, alisema ni jambo la kusikitisha kuona mpaka sasa hakuna hatua yoyote ambayo mkuu huyo amechukuliwa.

EDWARD Lowassa ni Mzigo...Lipumba Atoa ya Moyoni

0
0

Profesa Ibrahim Lipumba amesema aliamua kurudi CUF  kwa sababu ya sintofahamu iliyokuwapo kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi(Ukawa) baada ya kumtangaza Edward Lowassa kuwa mgombea urais wa chama hicho.


 Profesa Lipumba amesema hayo leo asubuhi wakati akihojiwa na  Televisheni ya Clouds katika kipindi cha 360.


 Amesema  alidhani Dk Wilbroad Slaa ndiye atakuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Ukawa na aliafiki hilo lakini akadai hakupenda Lowassa kuwania nafasi hiyo kwa sababu ni mzigo mzito kumnadi.

WAZIRI Mwenye Umri Mdogo zaidi Somalia Auawa

0
0

Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu. 
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 ameuawa karibia na ikulu ya Rais. 

Abas Abdullahi Sheikh Siraji hakuwa waziri wa kawaida nchini Somalia. 
Alipata umaarufu mkubwa baada ya kushinda kiti cha ubunge na kuiwakilisha Jubbaland. 

Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu. 

Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi huku watu wengi wakimtaja kama mtu machachari sana miongoni mwa mawaziri. 

Saa chache kabla ya kuuawa kwake alizindua mradi wa ujenzi wa jengo kwa ajili ya watumishi wa umma. 

Waziri wa habari wa Somalia amesema kuwa washukiwa wa mauaji hayo wamekamatwa.

PATA Tiba ya Asili Kutoka Kwa Mtabibu wa Nyota Maalim Hussein...Una Shida na Mapenzi Au Pesa Hazikai?

0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza, Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba, MIGUU Kufa GANZI, Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA, Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI, Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi 

ZaidiWhatsapp +255 674 835107  Au Piga +255746757102

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Bongo Movies Kumshitaki DJ Mark (Anayetafsiri Movies za nje)

0
0
Mtafsiri wa Movies akifanya yake , sio Dj Mark
Akiongea kwenye E-News ya East Africa Yusuph Mlela amesema Bongo Movies wameanza taratibu za kumshitaki jamaa maarufu anaetafsiri movies za nje maarufu kama Dj Mark na wengine wote wanaotafsiri movies za nje na kuwaharibia soko la Bongo Movies.

Mlela, "Tumeanza taratibu za kumshtaki jamaa sisi tunataka movies za nje zifuate taratibu kama sisi tunavyofuata ili kuwe sawa" Msikilize Hapa:

LIPUMBA " Mimi Sikusaliti Chama, Waliosaliti ni Wale Waliomkaribisha Lowassa"

0
0

Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa yeye bado ni Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ni Katibu Mkuu ila tatizo hafiki ofisini ilimpangie majukumu yake.

Pia amesema kuwa yeye na Dkt. Slaa hawakusaliti vyama vyao, walisimamia misingi halisi ya vyama. Waliowasaliti ni wale waliomkaribisha Lowassa.

Maalim Seif anatumia ubabe kuwadhibiti Wabunge ambao wananiunga mkono wapo Wabunge 42 wenye msimamo ni wawili tu.

Aidha Prof. Lipumba amekiri kuwahi kuwa mwanachama wa CCM lakini hakuwahi kuwa mwanachama kindakindaki alikuwa mwanachama wa kawaida tu.

JINAMIZI Clouds Lamrudia Makonda..!!!

0
0

SAKATA la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni cha Clouds liliibuliwa upya na wadau wa habari jana baada ya kulilaani.

Wadau hao wa habari walilaani tukio hilo jana ikiwa ni siku maalum ya Uhuru wa Habari iadhimishwayo Mei 3 kila mwaka.

Akizungumza kama mgeni rasmi katika siku hiyo jijini, Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Wananchi (CUF), mkoa wa Dar es Salaam, Salma Mwasa alisema si jambo jema viongozi wa umma kuonekana wanakuwa mstari wa mbele kuminya uhuru wa habari.

Alisema kitendo alichokifanya mkuu huyo wa mkoa wa Dar es Salaam ni cha kulaaniwa na kitaendelea kulaaniwa na kila mpenda amani na mpenda ustawi wa vyombo vya habari, na anayetambua umuhimu wake katika nchi.

“Viongozi wa umma na watunga sera, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kulinda vyombo hivi vya habari na kuhakikisha vinafanya kazi yao kwa uhuru," alisema Mwasa.

"(Viongozi wa umma) wanapogeuka na kuonyesha wa kwanza kuviminya (vyombo vya habari) inaonyesha sifa mbaya na hawapeleki ujumbe mzuri kwa hawa wengine wanaowategemea, wanaowasikiliza na kuwaamini.

“Kiukweli kile kitendo kinatakiwa kulaaniwa na kitaendelea kulaaniwa, kwa sababu pasipo kufanya hivi, vitendo hivi vinaweza kuendelea kufanyika na huko tunakoenda hali ya uhuru wa vyombo hivyo inaweza ukawa mgumu zaidi.”

Tukio hilo la staili ya utekaji wa vituo vya habari wakati wa mapinduzi ya kijeshi, lilifanywa na mkuu huyo Machi 17 saa 5 usiku.

Mkuu huyo alionekana katika video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na askari wasielekea kuwa polisi, waliokuwa na bunduki.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati ya waziri iliyochunguza sakata hilo, mkuu huyo alivamia kituo hicho usiku huku vipindi vikiwa vinaendelea na kwamba aliwatisha na kuwalazimisha watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kuonyesha taarifa yake.

Taarifa hiyo ya upande mmoja, ilikuwa ikimtuhumu Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kuwa amezaa na muumini wake.

Gwajima ambaye alikanusha vikali madai hayo kanisani kwake, alianzisha tuhuma za mkuu huyo kutumia cheti feki kujiunga na elimu ya juu na kwamba jina lake halisi ni Daud Bashite.

Mwasa alisema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyosonga na kwamba licha ya changamoto wanazokutana nazo, waandishi wa habari hawapaswi kukata tamaa.

“Tumeshuhudia baadhi ya waandishi wanapigwa na wengine hata kujeruhiwa wanapokuwa wanafanya kazi zao," alisema Mwasa. "Nataka kuwaomba wasikate tamaa."

"Watanzania wanawategemea, wakumbuke kuwa hakuna ukombozi bila mateso, tunajua wako katika wakati mgumu lakini tunaomba hali hiyo isiwakatishe tamaa.”

Alisema wao kama wawakilishi wa wananchi, wataendelea kupambana kuhakikisha uhuru huo unalindwa hata ikiwezekana kujenga hoja bungeni ili Sheria ya Vyombo vya Habari iliyopitishwa hivi karibuni irudishwe bungeni ili baadhi ya vipengele ambavyo vilionekana kuwa vina mtego kwa waandishi hao, virekebishwe.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Siasa (Taporea), George Maziku alisema ripoti ya hali ya uhuru wa waandishi wa habari iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka inaonyesha kuwa katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi 800 kutoka mataifa mbalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza majukumu yao.

Akizungumzia Sakata la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kuvamia kituo cha televisheni, alisema ni jambo la kusikitisha kuona mpaka sasa hakuna hatua yoyote ambayo mkuu huyo amechukuliwa.

RAIS wa Korea Kaskazini Atoa Agizo Wakulima Walime Bangi kwa Wingi..!!!

0
0

Rais wa Korea Kaskazini Kim Un Jong amewaamuru wakulima wa nchi hiyo kulima bangi kwa wingi. Serikali ya Korea Kaskazini inatumia mafuta ya bangi kwa ajili ya kurusha ndege zisizokuwa na rubani (Drones).

Nchi hiyo inakabiliwa na upungufu wa mafuta kutokana na vikwazo vya uchumi.
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images