Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live

RASMI...Mzee Mkapa Afunguka Haya ya Moyoni Kuhusu Serikali ya JPM..Anyooshea Kidole Sakata la Kufukuza Wenye Vyeti Feki..!!!

0
0

Rais mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa kwa mara ya kwanza amezungumzia utawala wa Rais Dkt John Pombe Magufuli huku akimpongeza utendaji kazi wake unavyokwenda.

Rais Mkapa alimpongeza kwa kufanikisha zoezi la kuondoa wafanyakazi hewa na wenye vyeti vya kughushi vya taaluma na kazi, na akasema anasikitika tu kwamba kwa nini yeye hakufanya hivyo wakati wa utawala wake.

Mzee Mkapa aliyesema hayo alipokuwa akifanya mazungumzo yake na Shirika la Habari la Ujerumani (DW) ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumzia ni utawala wa Rais Magufuli, uhuru wa vyombo vya habari, masuala ya uchumi.

Alisema Mkapa kuwa, wenye vyeti feki au watumishi hewa walikuwa wakiingizia serikali hasara wengine wakiendelea kukaa madarakani bila ya kustaafu, hivyo lilikuwa ni jambo la lazima kufanyika ni kwa manufaa ya taifa.

“Masikitiko yangu pekee ni kwamba kwa nini sikufanya uhakiki huu wakati nikiwa madarakani. Labda nilikuwa na mambo mengine makubwa zaidi niliyotakiwa kuyafanya lakini kwa hili alilofanya Magufuli namuunga mkono kabisa,” alisema Mkapa.

Kauli hii ya Rais Mkapa imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt Magufuli kuwaamuru watumishi wa umma 9,932 waondoke kwenye utumishi wao baada ya kubainika kughushi vyati vyao.

Mabeste Afunguka Makubwa Kuhusu Mkewe...Wasanii Wengine Inabidi Wasikie

0
0
Muandishi na Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mabeste amedai kuwa hajawahi kuwa na urafiki na wasanii wenzake kwa kuwa hapati mawazo mapya na kufunguka rafiki yake mkubwa ni mke wake.

Mabeste Mke wake na Mtoto wake
Mbele ya kamera za eNEWZ ya EATV, Mabeste amefunguka hayo kwa kusema kuwa wasanii wengi anaonekana nao wanakutana kikazi na siyo kirafiki kwani hawampi mawazo mapya ya kumfanya ajiongeze katika kazi zake.

Msanii huyo ameendelea kufunguka kwamba na tofauti na mke wake marafiki zake wengine ni watu waliopo nje ya muziki kwa kuwa wao ndio wanaona kipi kinafanyika katika tasnia na ndio washauri wa kumuelekeza kipi cha kufanya na kipi cha kuacha

"Ukiacha kuwa  kwa wasanii kuna unafki mimi mke wangu ndiyo rafiki yangu. Huwezi kunikuta katika sehemu za starehe kwa sababu sina hao marafiki wa kutoka nao. Mimi na wasanii wenzangu tukikutana ni kwa ajili ya kazi tuu. Unajua mkiwa uwanjani hamuoni mnayoyafanya, ila  waliopo nje ndo wanajua. Hata nikisema wasanii wenzangu ndio wa kushauriana nao basi itafika sehemu mawazo yatafika ukomo kwa sababu tunawaza wote sawa. Kitu kingine naweza kusema marafiki wa Mabeste ni wa Mabeste peke wala siyo wa William ndio maana nasema marafiki zangu ni watu wa kawaida siyo ma - star" - Mabeste

WAKOLONI Wamechangia Umaskini Afrika - Kikwete Afunguka

0
0
Aliyekuwa rais wa Tanzania awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete,amesema koloni za mataifa ya Afrika yamechangia kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ikiwemo kuwanyima elimu waafrika wengi katika maeneo waliyoyatawala.

Dkt Kikwete amesema hayo katika Mkutano wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa Afrika mjini Durban Afrika Kusini, lengo hasa likiwa kutafuta namna za kukuza uchumi wa Afrika.
Rais huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika zimechukua hatua katika kuboresha elimu katika mataifa yao kuanzia shule za chekechea,msingi na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma na kuandika katika kujiletea maendeleo

Ameongeza kuwa nchi zinapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu nchi nyingi zilianzia chini sana na uwekezaji wote huu uliopo sasa katika bara la Afrika umefanyika baada ya nchi hizi kupata uhuru.

SHILOLE Adai Ana Mzuka wa Kuolewa ...Huwezi Amini Sifa za Mwanaume Amtakae

0
0
Zuwena Mohamed ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na  kunyanyasia wanawake zao.

Shilole akiwa kikaangoni EATV
Akiwa Kikaangoni kwenye ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima, upole na ukarimu.

"Natamani sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi, napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake zao"- Shilole alifunguka.

Shilole hajaishia hapo ameendelea kufunguka kuhusu suala la muonekao "mimi siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na anayejituma kwenye utafutaji"- aliongeza Shilole.

SWALI la Kishushi...Wanawake Huwa Tunatamani Nini Kwa Wanaume?

0
0
Wanaume wengi wao japo siyo wote hupenda kuangalia/kushangaa wadada wenye makalio makubwaa .....wengine wanashangaa yansishia hapo hapo wengine wanatamanii kuwa na na mwanamke wa hivyooo n.k....... Kila mtu kaumbiwa matamanio..... Je kwaupande wetu sisi Madada huwa tunamtamani/ kushangaa mwanamme wa aje kila mtu anakitu chake anachopenda mwenza wake awe nachoo je sisi wadada huwa tunatamani non???.

Nianze na mimi......
....Huwa napenda sana mwanamme mwenye kifua kipana kilicho jengeka vizuuuri na kama nikibahatika kuongea nae angalao sauti iwe nzitooo......

PATA Tiba ya Asili Kutoka Kwa Mtabibu wa Nyota Maalim Hussein...Una Shida na Mapenzi Au Pesa Hazikai?

0
0

Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH Maalim HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Maalim Hussein Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. 

Anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU. 

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza, Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Maalim Hussein Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba, MIGUU Kufa GANZI, Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA, Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI, Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..na mengi 

ZaidiWhatsapp +255 674 835107  Au Piga +255746757102

NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

JINGINE Jipya :Serikali Yakanusha Uzushi Kuhusu DR Mwakyembe

0
0
Kupitia mitandao ya kijamii zilienea uzushi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua zuio la Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliyevitaka vituo vya redio na televisheni kutokuzisoma habari nzima katika dondoo za magazeti. Wizara hiyo imekanusha uvumi huo kama ifuatavyo:

Tarehe 03 Mei, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ulienezwa uzushi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametengua zuio la Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliyevitaka vituo vya redio na televisheni kutosoma habari nzima katika dondoo za magazeti.

Tunapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na uzushi uliotungwa kwa dhamira ovu kwani Mhe. Rais hajatoa tamko, maagizo wala maelekezo yoyote kuhusu maelekezo yenye nia njema yaliyotolewa na Mhe. Dkt. Mwakyembe.

Umma unakumbushwa kuwa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mitandaoni, 2015 kinakataza na kutoa adhabu kali ikiwemo kifungo jela kwa wanaoeneza taarifa za uongo. Katika uzushi huu hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Kama ilivyokuwa kaulimbiu ya Siku ya Uhuru wa Habari iliyoadhimishwa jana, na pia alivyosisitiza Waziri Mwakyembe kwa wadau jijini Mwanza, moja ya nguzo kuu ya uhuru wa habari na uhuru wa kujieleza ni ukweli. Tuitumie mitandao ya kijamii kwa faida na si kutangaza uongo na uzushi.

Siku ya maadhimisho ya sherehe ya vyombo vya habari, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo alipiga marufuku vituo vya redio na runinga kusoma habari nzima katika magazeti na kuamuru kusoma kichwa tu cha habari

PROF. Lipumba: Niko Tayari Kuondoka CUF kwa Sharti Hili Tu..!!!

0
0

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amesema yuko tayari kuondoka katika chama hicho ili kukiepusha na migogoro ikiwa tu mkutano mkuu utaamua, kama katiba yake inavyosema.

Mwenyekiti wa chama, kwa mujibu wa katiba ya CUF, alisema Lipumba anaweza kuondolewa madarakani kama wajumbe wengi wa mkutano mkuu wataridhia.

Prof. Lipumba alitoa kauli hiyo jana ikiwa ni siku moja baada ya Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad kusema hayuko tayari kupatanishwa naye kwa kuwa anatumiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuivuruga CUF.

Prof. Lipumba alisema endapo itathibitika kuwa uhai wa CUF unategemea yeye kuondoka, yupo tayari kufanya hivyo ila kwa mujibu wa katiba ya chama.

“Katiba ya CUF ipo wazi kuwa mwenyekiti wa CUF akitaka kufukuzwa, lazima theluthi mbili ya wajumbe wa Bara na theluthi mbili ya (wanaotoka) Zanzibar wampigie kura ya kukubali aondolewe," alisema msomi huyo wa uchumi.

Kumekuwa na mgogoro wa pande mbili CUF baada ya Profesa kujiuzulu uenyekiti kwa hiari yake Agosti, 2015 lakini akarudi miezi 10 baadaye, akidai hakuna kikao halali kilichopitisha uamuzi wake wa awali wa kujiengua kwenye nafasi hiyo.

“Huwezi kunifukuza uanachama," alisema Prof. Lipumba ambaye amefukuzwa uanachama na Baraza Kuu la CUF lakini akatambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

"Kwanza kadi ninayo nyumbani, lakini Katiba yetu ipo wazi.

"Ukitaka kumfukuza mwenyekiti lazima uitishe mkutano mkuu na wajumbe wapige kura, na theluthi mbili Bara na Zanzibar wakubali.”

Alisema baada ya kuandika barua ya kutengua kujiuzulu na kumkabidhi Maalim Seif, naye alimshauri asianze kazi kama alivyoeleza katika barua ili aweze kushauriana na wanasheria wa chama, kitendo ambacho alikikubali.

Alisema Maalim Seif aliitisha mkutano mkuu ambao yeye hakuitwa na wakati ukiendelea baadhi wajumbe walimpigia simu kuwa barua yake inasomwa na kumtaka aende, ambapo alifanya hivyo.

Alisema ndani ya mkutano alikuta mjadala ambao wajumbe baadhi walimtaka mwenyekiti wa mkutano, Julius Mtatiro, aridhie Prof. Lipumba aitwe; ahojiwe lakini kiongozi huyo wa muda alikataa.

Alisema mkutano huo ulivunjika baada ya kutangazwa kura za kumkataa yeye, alisema Lipumba, "kura ambazo hazikupigwa".

KUVAMIA MIKUTANO
Mwezi uliopita watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Prof. Lipumba walivamia na kufanya fujo katika mkutano wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye yupo upande wa Maalim Seif.

Lakini Prof. Lipumba alisema hawana utaratibu wa kwenda kuvamia mikutano hiyo bali wapo wanachama wanaokaa katika maeneo husika wakiona chama chao kitaadhirika huenda kuhoji.

“Tukio lile la Kigogo (mwezi uliopita) lilinisikitisha," alisema Prof. Lipumba. "Sihusiki wala sikutoa maagizo watu wakavamie na kuwapiga waandishi wa habari kwenye mkutano wa CUF.”

Akizungumzia kesi iliyofunguliwa na upande wa Maalim dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na yeye, Prof. Lipumba amependekeza maamuzi yatakayofanyika pande zote mbili ziyazingatie.

Aidha, alimtaka Maalim Seif aelewe kuwa maridhiano lazima yawepo.

Pia alisema endapo Maalim Seif angeacha usultani na kuheshimu Katiba ya chama kusingekuwa na tatizo la msingi.

“Usultani wake niliandika barua ya kujiuzulu na kuandika barua ya kurudi katika nafasi yangu ambayo yeye alikuwa nazo lakini Maalim Seif aliitisha mkutano mkuu wa chama wakati barua ya kujiuzulu nimeshaitengua,” alisema.

UPINZANI Waja Juu Madaktari 'Kenya' Kuajiriwa Nchini..!!!

0
0

KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni imekosoa uamuzi wa serikali kuwaajiri madaktari 258 waliokuwa wameomba kwenda kufanya kazi Kenya na kuwaacha mamia ya madaktari ambao hawakuomba na badala yake kusubiri ajira nchini.

Ester Bulaya, akiwasilisha hotuba bungeni mjini hapa jana kwa niaba ya Waziri Kivuli wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel, kuhusu utekelezaji bajeti ya wizara hiyo, alisema wameshangazwa na uamuzi wa serikali kutaka kupeleka madaktari Kenya ilhali kuna uhaba mkubwa wa wataalam hao nchini.

Alisema licha ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kupinga uamuzi wa serikali kupeleka madaktari 500 Kenya, serikali ilipuuza maoni ya chama hicho mpaka pale serikali ya Kenya ilipositisha ombi la uhitaji wa madaktari.

Alisema kitendo kilichofanywa na serikali cha kuipigia debe Kenya huku ikijua dhahiri Tanzania inakabiliwa na uhaba wa wataalamu hao, pengine kuliko Kenya, si cha kizalendo na kimedhihirisha nia mbaya ya serikali kwa wananchi wake wanaoteseka kwa kukosa huduma za afya.

Bulaya ambaye pia Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), alisema pamoja na jambo hilo kukosa uzalendo, mwezi uliopita Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alitangaza kuwa Rais ameamuru madaktari 258 walioomba kufanya kazi Kenya waajiriwe nchini mara moja.

“Uamuzi huo si tu umewashangaza Watanzania, bali ulimwengu kwa ujumla. Serikali hii imefanya uamuzi wa ajabu ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii tangu uhuru.

Kitendo cha serikali kuwaajiri madaktari walioomba ajira nje ya nchi na kuwatupia kapuni mamia ya madaktari ambao walionyesha uzalendo wa kutamani kuitumia nchi yao ni kitendo cha kibaguzi na kikatili sana kwa wazalendo wa nchi hii," alisema.

Aliongeza kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani inapata wasiwasi juu ya uwezo wa serikali katika kuratibu na kupambanua vipaumbele vyake kwa kuwa imeshindwa kujua kama nchi hii ina huduma duni za afya na inakabiliwa na uhaba wa watendaji katika sekta ya afya kuliko Kenya.

Akinukuu ripoti ya Benki ya Dunia (WB) ya Mei, 2016 ya 'Tanzania Service Delivery Indicators', Bulaya alisema inaonyesha utendaji wa sekta ya afya na maendeleo ya sekta hii katika nchi mbalimbali ikiwamo Tanzania na Kenya si mzuri.

WAGONJWA Waacha Vitanda na Kuomba Kupiga Picha na Mhe. Mbowe..!!

0
0

Wagonjwa waacha vitanda na kuomba kupiga picha na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Hai Mhe.Freeman Mbowe

Mhe.Mbowe jana alitembelea Hospitali ya Wilaya ya Hai pamoja na kuwasalimia wagonjwa waliopo hospitalini hapo ndipo gumzo lilipotkea baada ya sauti za wagonjwa kusikika zikisema "KAKA ,KAKA" kumbe walikua wakimuita Mhe.Mbowe wakihitaji angalau kumshika mkono nakupiga picha pamoja nae.

Mhe.Mbowe aliongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai Mhe.Helga Mchomvu pamoja na Katibu wake Irene Lema
Mhe.Mbowe alitembelea Maabara ya hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Mhe.Mbowe alitembelea shule za sekondari katika kata ya Machame Kaskazini,Masama kusini na kata ya Boma yang'ombe

Takribani siku kadhaa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa Jimbo la Hai Mhe.Freeman Mbowe alikiwepo Jimboni kwake na alikua na ziara mbali mbali.

MEYA wa Moshi Baada ya Kuzuiwa Kuingia Kikao cha JPM Amefunguka Haya Mazito..!!!

0
0

Meya wa Manispaa ya Moshi Raymond Mboya amesema kuwa haelewi lilikotoka agizo la kuzuiwa kwake kuingia kwenye kikao cha Rais Magufuli licha ya kuambiwa alihitajika kuhudhuria kikao hicho baada ya kualikwa na Mkurugenzi.

Meya Raymond Mboya na Mbunge wa Moshi Mjini Japhary Michael walizuiwa kuhudhuria kwenye kikao cha JPM na viongozi wa dini alichokifanya mjini Moshi wakati wa ziara ya siku 3 katika Mkoa wa Kilimanjaro

ALI Kiba Aendelea Kupoteza Mashabiki...Shilole Nae Amkana Live Amweka Mbele Diamond Platnumz

0
0
Msanii wa muziki, Zuwena Mohammed aka ‘Shilole’, amedai yeye ni shabiki wa damu wa Diamond na sio Alikiba.

Akiongea katika Kikaango cha EATV Jumatano hii, Shilole amedai anampenda Diamond kutokana na vile alivyo pamoja na vitu anavyofanya.

“Mimi namkubali zaidi Diamond Platnumz kuliko Alikiba,” alisema Shilole. “Nampenda Diamond kutokana na mambo yake na vile alivyo, kwa hiyo kila mtu ana watu anaowakubali na kuwapenda,”

Katika hatua nyingine Shilole amedai yeye alishtuka mapema na kuchomoka kwenye tasnia ya Bongo Movie maana kama aliona kuwa mbele itakuja kuyumba.

Alisema yeye ameridhika na muziki kwani muziki unamlipa na umempa mafanikio makubwa ambayo kama angekuwa kwenye filamu huenda asingeyapata.

MSIDANGANYIKE Zimbabwe ni Tajiri wa Pili Afrika Nzima -Robert Mugabe Ajigamba

0
0
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kuwa nchi yake ya Zimbabwe ndio taifa lililoendelea zaidi katika bara Afrika baada ya Afrika kusini.

‘Tuna takriban vyuo vikuu 14 na asilimia 90 ya watu wamekwenda shule, ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi barani Afrika’ huku akiongezea kwamba uchumi wao unaendelea kuimarika.

Hata hivyo Rais Mugabe amekana madai kwamba taifa hilo lina hali tete.

Zimbabwe imekuwa ikishindwa kuwalipa wafanyikazi wa serikali na huku ikiwekwa katika nafasi ya 24 kulingana na ripoti ya shirika la umoja wa mataifa UNDP, ya maendeleo barani Afrika.

Soma Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo

0
0

SAMAKI wa Magufuli Wazuia Kizaa zaa Bungeni....!!!

0
0

MBUNGE wa Nungwi (CUF), Yussuf Haji Khamis, ameibua Bungeni samaki waliokamatwa mwaka 2009 katika Bahari ya Hindi, maarufu kama ‘Samaki wa Magufuli’.

Katika kuibua suala hilo, mbunge huyo alihoji jana ni lini serikali itarudisha zaidi ya Sh. bilioni mbili ambazo ni thamani ya samaki tani 296.3 waliokamatwa wakati huo.

Akiuliza swali jana bungeni, mbunge huyo alisema mwaka 2009 serikali ilikamata meli ya uvuvi MFV Tawariq, Nahodha wake Tsu Chin Tai na watu wengine 36 na hatimaye kushtakiwa mahakamani.

“Kwa amri ya mahakama, samaki tani 296.3 wenye thamani ya Sh. 2,074,000,000 waligawiwa bure na meli hiyo ilizama ikiwa inashikiliwa. Watuhumiwa wawili walihukumiwa kifungo, walikata rufani Mahakama ya Rufani na mwaka 2014 waliachiwa huru,” alisema.

Akijibu swali hilo, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angella Kairuki, alisema Machi, 2009 kikosi kazi kilichokuwa kikifanya doria katika ukanda wa kiuchumi wa bahari hiyo kilikamata meli hiyo.

Alisema meli hiyo yenye namba za usajili 68 BU YOUNG ilikamatwa ikivua katika bahari hiyo bila kibali na ilikuwa ikitumia jina la Tawariq 1 na Tawariq 2 ili kuficha jina halisi na kuendelea kufanya uvuvi haramu.

“Nahodha wa meli hiyo na wenzake walishtakiwa Mahakama Kuu, kesi ya jinai ambayo nahodha na Zhao Hanquing aliyekuwa wakala wa meli hiyo walitiwa hatiani, walikata rufani na mahakama ilibatilisha na kufuta mwenendo mzima wa kesi,” alisema Kairuki.

Alibainisha kuwa mwenendo mzima wa kesi ulifutwa kutokana na kasoro katika taratibu za kuwafungulia mashtaka, hivyo hawakuwahi kushinda kesi na Mahakama ya Rufani haikuwahi kuwaambia wako huru kwa sababu hawana hatia.

Kairuki alisema baada ya uamuzi huo wa Mahakama ya Rufani, Mkurugenzi wa Mashtaka alifungua mashtaka upya katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na baadaye kuondoa mashtaka dhidi yao mwaka 2014.

Hata hivyo, alisema baada ya mwama jana Wakili Ibrahim Bendera alifungua maombi katika Mahakama Kuu akimwakilisha Said Ali Mohamed ambaye hakuwa mmoja wa washitakiwa katika kesi ya msingi, akiomba apewe meli au Dola za Marekani milioni 2.3 (zaidi ya Sh. bilioni 4.6) kama thamani ya meli na Sh. bilioni 2.074 kama thamani ya samaki.

Kadhalika, alisema Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili, ilikubali hoja ya Jamhuri na kutupilia mbali maombi hayo kwa kuwa hayakustahili. “Kutokana na mwenendo wa kesi hii, hili ni suala la kisheria na wahusika wanaweza kuendelea kulishughulikia kupitia mahakamani,” alisema Kairuki.

LISSU - Watanzania Msahau Bunge Kuonyeshwa Live' kwa Sasa..!!!

0
0

Mwanasheria wa CHADEMA, Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS) na mbunge Tundu Lissu amesema kuwa Bunge Live tusahau kwa sasa mpaka CCM itoke madarakani! 

Katika mahojiano  Lissu ameeleza pia kuwa yeye kama Rais wa TLS anaona kuwa kuna umuhimu wa kuhakikisha kuwa kikatiba juhudi zinafanywa kupunguza madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kuhakikisha viongozi wanafuata katiba na siyo kufikiri matamko yao ndiyo sheria.

TENA..Watu Wawili Wauawa Kinyama Mkoani Pwani..Walipigwa Risasi Mbele ya Familia Zao.!!!

0
0

Mtu mmoja Aitwae Amri Chanjale (55), mkazi wa kitongji cha Makaravati katika Kijiji cha Umwe Kusini wilayani Rufiji ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake.

Tukio hilo limetokea jana saa 1.30 usiku baada ya watu wasiojulikana kufika kwake na kutekeleza shambulio hilo.

Marehemu huyo ambaye pia ni mwanachama wa CCM ameuawa ikiwa ni baada ya siku tano kuuawa kwa  Mohammed Malinda ambaye nae alikuwa ni mwanachama wa chama hicho.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM wilayani Rufiji, Musa Nyeresa amethibitisha kuuawa kwa mwanachama huyo kwa kupigwa risasi.

LOWASSA Ampa Mbinu za UKAWA Uhuru Kenyatta Ili Ashinde Uchaguzi wa Kenya..!!!

0
0

Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amemuonya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya dhidi ya muungano wa vyama vya upinzani wa Nasa, akisema utakisumbua chama tawala cha Jubilee katika Uchaguzi Mkuu wa Agosti.

Akizungumza kwenye mahojiano na Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC) juzi, licha ya kusisitiza msimamo wake wa kumuunga mkono Kenyatta kuwania urais kwa awamu ya pili, Lowassa alisema Nasa ni umoja ambao pia una nguvu.

“Nawapongeza Nasa kwa muungano wao. Namshauri rafiki yangu Kenyatta asipuuze muungano ule kwa sababu una nguvu, na una watu wengi. Naamini hatapuuza,” alisema Lowassa, ambaye pia aligombea urais nchini akiungwa mkono na vyama vinne vya Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Lowassa alisema wakati mwingine chama kinapokuwa kimoja kura hazitoshi ndiyo maana vingine huungana kuwa kitu kimoja.

“Inawezekana mnapokuwa chama kimoja kura hazitoshi kwa hiyo mnajiunga na vyama vingine mnatengeneza ‘coalition’ na kama imejitengeneza vizuri mnachukua madaraka,” alisema Lowassa na kuongeza:

“Niko upinzani kwa sababu maalumu ya kuing’oa CCM madarakani.”

Alipoulizwa kama Nasa wana nguvu ya kutosha ya kumng’oa Rais Kenyatta, alisema hana uhakika lakini nguvu ya muungano ni kubwa.

“Wapinzani wengi tutajifunza kutoka kwao kutokana na muungano huo hasa kama watafanikiwa.”

Licha ya kubashiri kuwepo kwa ushindani mkubwa, Lowassa aliwashauri Wakenya kuzingatia amani.

“Watangulize amani na umoja mbele wakati na baada ya uchaguzi,” alisema.

Kuhusu kumuunga mkono Kenyatta, Lowassa alisema: “Kwanza ni wakati wenyewe wa kura za maoni za vyama, pili namuamini mtu mwenyewe, na tatu nataka kauli yangu isikike. Jana (juzi) nilikuwa na wanawake wa Kenya na walifurahi sana kusikia namuunga mkono,” alisema Lowassa.

Lowassa alisema Rais Kenyatta amekuwa mmoja wa viongozi wanaoonekana kupenda na kuilinda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

“Tunataka viongozi wanaojali watu. Wakati EAC inaanzishwa tulikiri kwamba ni jumuiya ya watu na huyu ameonyesha kwamba hii ni jumuiya ya watu,” alisema.

Mbali na kumsifia, Lowassa pia alisema kwa kipindi ambacho Rais Kenyatta amekuwa madarakani, amefanya kazi nzuri na ameonyesha ana uwezo, anapenda amani na maendeleo .

Lowassa alishika nafasi ya pili katika mbio za urais Tanzania akiwa amepata kura milioni 6.07 huku Rais John Magufuli akipata milioni 8.8.     

MASWALI Tata Yenye Majibu Tata Kutoka kwa Profesa Lipumba..!!!

0
0

Profesa Ibrahim Lipumba, ambaye ana mgogoro na chama chake cha CUF, jana alitinga studio za Clouds TV kujibu mapigo ya hasimu wake, Maalim Seif Sharif Hamad katika kipindi cha 360 na mambo matatu yalijitokeza.

Alichukua hatua hiyo baada ya kipindi hicho cha 360 kumuhoji Maalim Seif juzi na kumsukumia lawama Profesa Lipumba kuwa ndiye anayesababisha mgogoro katika chama hicho, akisaidiwa na Serikali.

Maalim Seif, ambaye alimtuhumu Lipumba kuwa msaliti, alisema ni bora kukaa meza moja na CCM kuliko mwanasiasa huyo msomi wa uchumi kwa kuwa chama hicho tawala kinajulikana kuwa adui wa CUF hivyo ni rahisi kuchukua tahadhari.

CUF ipo katika mgogoro baada ya Profesa Lipumba kuandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake Agosti 2015 kwa kile alichoeleza kuwa nafsi inamsuta na mwaka mmoja baadaye aliandika barua ya kubatilisha uamuzi huo.

Hata hivyo Mkutano Mkuu wa CUF, uliofanyika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam, haukukubali Profesa Lipumba kurejea madarakani, badala yake ukakubaliana na barua yake ya kujivua nyadhifa zote, hali iliyoanzisha mgogoro na viongozi wenzake.

Katika mahojiano hayo ya jana, Profesa Lipumba alizungumza na kujibu mambo mbalimbali lakini kati ya hayo, masuala matatu yalikuwa na utata zaidi.

Jambo la kwanza ni pale Profesa Lipumba alipoulizwa na watangazaji wa kipindi hicho sababu za kwenda kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CUF uliofanyika Agosti 21, 2016 wakati hakuwa mjumbe.

Lipumba alijibu kuwa aliitwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo ambao alisema walimtumia ujumbe mfupi wa simu na baadhi kumpigia simu.

“Nilipigiwa simu na wajumbe 12 wakiniambia ‘hapa kwenye mkutano mkuu, barua yako (ya kujiuzulu) inasomwa. Sisi wajumbe tunataka uje uthibitishe hii barua ndiyo yenyewe uliyoandika?” alisema Lipumba.

“Nilipata simu kama kumi au kumi na mbili. Nikaamua kwenda kwenye eneo la Mkutano Mkuu.Niliondoka nyumbani mimi na dereva mpaka kwenye Mkutano Mkuu.”

Maelezo hayo yalimfanya mtangazaji aulize sababu za kwenda kwenye Mkutano Mkuu wakati hajaalikwa na si mjumbe wa mkutano huo.

“Ah! Mimi nimeitwa na wajumbe kwamba hapa unahitajika kuja kuthibitisha,” alisema na kupandishiwa swali jingine.

“Hiyo imekaaje kikanuni. Unapotakiwa kuja kuthibitisha, kikanuni imekaaje. Unaalikwa kwa kutumiwa barua?” aliulizwa.

“Hapana nilitumiwa ujumbe wa simu. Katika taratibu zetu sisi ujumbe wa simu, barua ni utaratibu halali kumualika mtu kuhudhuria kikao,” alisema.

“Sasa sikujua nani ana-chair (mwenyekiti) nani katibu wa kikao kile, lakini nimekwenda kwenye mkutano mkuu. Nimefika eneo la mkutano nimekuta vijana, walinzi wa chama, blue guard, Nimeshuka wamenipokea, wakaniingiza ndani ya ukumbi wa Mkutano Mkuu. Wakanipeleka mahali nikaenda kukaa.”

Alisema alikuta mjadala kuhusu aitwe kujieleza, lakini mwenyekiti (Julius Mtatiro) alikataa na baada ya mapumziko, walipiga kura na kutangaza matokeo kuwa waliokuwa wanamtaka Lipumba ni wajumbe 14 na waliomkataa ni 476.

“Hiki ndicho chanzo cha sokomoko kutokea na kusababisha wajumbe kuimba ‘ni heri ya Jecha (Salim Jecha) aliyefuta matokeo kuliko Maalim Seif kutangaza matokeo wakati kura hazikupigwa’,” alisema Profesa Lipumba.

Jecha ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Mahojiano hayo pia yalijikita katika sababu za uamuzi wa Lipumba kujiuzulu.

Katika mahojiano hayo, Lipumba alisema aliamua kujiuzulu kwa sababu aliona si sahihi kwa Edward Lowassa kuingia ndani ya Ukawa na kugombea urais na kwamba hakuwa kinara wa kumshawishi Lowassa kujiunga upinzani.

“Ni uongo na mimi nilipata taarifa kutoka kwa (mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James) Mbatia kuwa Lowassa anahitaji kuzungumza na mimi na hata siku moja sikuwahi kuomba niunganishwe naye,” alisema.

Aliongeza kuwa hata siku moja hakuwahi kuomba namba ya Lowassa.

Alipotafutwa jana, Mbatia alisema hawezi kuzungumza chochote kwa sasa kuhusu kinachoendelea ndani ya CUF.

Juzi, Maalim Seif alisema ana ushahidi kuwa Profesa Lipumba alikwenda kumtafuta Lowassa ajiunge na Ukawa na alimuomba Mbatia amuunganishe naye.

Wakati akimkaribisha Lowassa ndani ya Ukawa Julai 2015, Profesa Lipumba alisema suala la ufisadi ni mfumo na si la mtu mmoja mmoja.

“Sisi tunaponda ufisadi na mfumo wa kifisadi na chanzo kikubwa cha ufisadi ni mfumo ndani ya CCM, kwanza tuing’oe CCM, hapo ndipo tutakapoweza kuondoa ufisadi,” alisema Lipumba wakati wa kumtambulisha Lowassa wakati huo.

“Lowassa alikumbwa na tuhuma za ufisadi mwaka 2008, leo ni 2015 lakini ufisadi umeongezeka au umepungua? Lowassa hayupo serikalini? Tatizo ni mfumo na jambo la kwanza ni kuing’oa CCM.”

Lakini jana, Lipumba alisema kuwa hakusema Lowassa ndiye awe kamanda wa kuongoza vita dhidi ya ufisadi.

Hata hivyo, katika mahojiano hayo Profesa Lipumba alikiri kwenda nyumbani kwa Lowassa na kufanya mazungumzo kuhusu watu wanaomuunga mkono kujiunga na Ukawa.

Alieleza kuwa mipango yote ilisukwa na Chadema na kitendo cha yeye kuhusishwa katika mchakato wa kumshawishi Lowassa ulikuwa ni propaganda.

Alisema hatua yake ya kumlaumu Maalim Seif imetokana na katibu huyo mkuu huyo kufanya vikao na Chadema bila kumshirikisha yeye.

Kuhusu nguvu yake ndani ya CUF, Profesa Lipumba alisema baadhi ya wanachama walimfuata kumshawishi ashiriki kampeni kwa kuwa walimtambua kama bado mwenyekiti.

“Walikuja kina mbunge wa Temeke, Abdallah) Mtolea na (mbunge wa Kinondoni, Maulid) Mtulia kuniomba nishiriki kampeni zao, nikawaeleza siwezi kutokana na hali ilivyo kwa kuwa nitaharibu uhusiano kati yao na Chadema,” alisema

Akizungumzia suala hilo jana, Mtolea alithibitisha kuwa alienda kwa Lipumba kumuomba ahudhurie uzinduzi wa kampeni kama mwanachama wa kawaida.

“Nilimuomba akanikatila kwa sababu ya Lowassa. Nikamweleza mkutano ni wangu mimi siyo wa Lowassa akakataa pia,” alisema Mtolea.

Kuhusu kuwa msaliti, Lipumba alisema “waliosaliti ni wale waliofanya utaratibu wa kumleta Lowassa”.

Sababu za kujiuzulu,

Akizungumzia sababu za kujizulu, Profesa Lipumba alisema ni ukosefu wa umoja ndani ya CUF, hasa baada ya Ukawa kuundwa.

Alisema wakati mwingine, vikao vilifanyika bila yeye kupewa taarifa. “Nikajikuta nina wakati mgumu kulinda maslahi ya umoja na maslahi ya chama na ukosefu huu ulitumiwa na Chadema kuwadhalilisha wagombea wa CUF Bara,” alisema.

Alisema Chadema walisema CUF haina fedha za kusimamisha mgombea na taarifa hizo walipewa na Maalim Seif.

Kuingia ofisini

Profesa Lipumba alisema baada ya Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa kumtambua kama Mwenyekiti alikwenda moja kwa moja hadi ofisi ya makao ya chama hicho, Buguruni na kukanusha kuwa hakuvamia.

Alisema anamtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu, lakini alishangaa kwa nini hafiki ofisini.

Alisema tayari ameshamwandikia barua ya kuitisha kikao cha kamati tendaji kisha Baraza Kuu la Uongozi.

Aliongeza kuwa hakuanza kutofautiana na Maalim Seif baada ya kujiuzulu bali wakati wa mchakato wa maoni ya Rasimu ya Katiba mpya.

Alisema Maalim Seif alitaka muungano wa mkataba wakati msimamo wa chama ilikuwa ni Serikali tatu.

CUF ina wabunge 42, na kati ya hao ni wawili tu wanaomuunga mkono Profesa Lipumba.  

BWANA Harusi Atiwa Mbaroni Kwa Kujaza Ndugu Feki Ukumbini

0
0
BWANA harusi mchina, amekamatwa na polisi na sasa yuko rumande, baada ya kuhadaa wakwe zake kuwa amealika wageni 200, kumbe ni uongo watu hao wote ni wasanii wa kulipwa ukumbini.

Alipatwa na msukosuko huo baada ya familia ya mkewe kugundua kuwa watu aliokuwa anadai ni marafiki na ndugu zake, aliwapa ‘mshiko’ ili kuhudhuria harusi.

Kwa mujibu wa gazeti moja la jimbo la Kaskazini, nchini China, Polisi walimkamata Liu Wang., wakati ulipotokea mjadala kwenye mgogoro uliozuka baina yake na wageni ambao ilibainika ni marafiki tu, ingawa haikuwekwa wazi uhusiano wake nao.

Sherehe zilipoanza, hakukuwepo dalili za wazazi wa Liu kuwepo na ndipo joto la msuguano likaanza kupanda.

Mmoja wa wageni hao waalikwa wanaolipwa, aliiambia televisheni moja ya Shaanxi kwenye kipindi kiitwacho ‘guests’ kwamba walilipwa Yuan 80 ambazo ni sawa na Dola za Marekani 12 au sawa na Shilingi 25,000 au Pauni tisa, ambayo ni sawa na Shilingi 28,000 kutoka kwa bwana harusi - Wang.

Walisema walilipwa kwa kila siku waliyotumika ili wajifanye kama wanandugu zake .

Pia inadaiwa kuwa watu hao ni pamoja na madereva wa teksi, wanafunzi na maswahiba wengine wa bwana harusi huyo, kupitia mtandao wa kijamii wa jukwaa la ‘WeChat walijadiliana naye gharama za malipo kwa ushiriki wao kwenye harusi.

Bibi harusi alisema kuwa, amemfahamu mumewe huyo kwa zaidi ya miaka mitatu, ingawa hakufahamu chochote kuhusu utapeli wake.
Bado haijafahamika kile Liu anachokificha, licha ya kwamba hakuvunja sheria za nchi.

Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kuwa, muoaji huyo alikuwa anatoka katika jamii maskini na katika kuficha uhalisia wake, aliamua kutosema ukweli kwa jamaa zake walioko vijijini, wasifike kwenye harusi, akihisi angeaibika.

Televisheni ya Kanda inayomilikiwa na serikali Xibu Online, imesema kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi.
Viewing all 104417 articles
Browse latest View live




Latest Images