Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104415 articles
Browse latest View live

SHILOLE - JLo Alinizingua Kolabo, Ila Nitamtafuta Nick Minaj..!!!

0
0

Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ametoa ufafanuzi wa kushindikana kufanya kolabo yake na Jennifer Lopez(JLo) ambayo msanii huyo alitangaza kufanya nae.

Shilole amesema kuwa alisha onana na meneja wa msanii huyo kutokea Marekani na kuongea nae kuhusu mpango wake wa kufanya kolabao, lakini baadae ilishindikana hivyo naye ameshindwa kwenda tena Marekani kutokana na kuwa busy.

“Nilishindwa kurudi tena Marekani kutokana na mambo niliokuwa nayo ikiwemo ya kifamilia na pia Jlo nae alikwa busy busy na nyimbo yake ya “Ain’t your mama” nikaona basi tusisumbuane sana mwache aendelee na mambo yake, ila nitamfuta Nick Minaj.

STEVE Nyerere - Kuna Wasanii Wanajifanya ‘Mungu Watu’ ..!!!

0
0

Msanii wa filamu, Steve Nyerere, amedai wasanii wa filamu wanashindwa kufanikiwa kutokana na kukosa ushirikiano huku akidai kuna baadhi yao wanajifanya wao ni mungu watu.

Muigizaji huyo amedai hakuna mtu wa nje ambaye ataweza kuja kuikomboa tasnia yao ya filamu isipokuwa wao wenyewe.

“Leo hatupo katika umoja, kwanza ili tuweze kufanikiwa mafanikio hayapo ya mmoja mmoja, mafanikio yote duniani yalipita kwa watu ndiyo wewe ukafanikiwa kwa hiyo lazima tukubaliane, tupendane na nyoyo zetu ziwe zimefunguka kwa kufanya vitu vizuri,” Steve alikiambia kipindi cha Enewz cha EATV.

Aliongeza, “Kuna ma-director wazuri zaidi lakini leo wote hawapo, wanachokikosa ni ushirikiano, tunao ma-director wazuri tu, wanaweza wakafanya kitu kizuri tu ‘site’ lakini ushirikiano hawana, kuna watu wanakuwa Mungu watu haiwezekani, haiwezekani kuwa Mungu mtu jamani Mungu ni mmoja tu,”

Muigizaji huyo amekuwa akipingana na wasanii wenzake wa filamu walioandamana mwezi mmoja uliopita wakiishinikiza serikali kuzifungia filamu za nje ambazo hazilipi kodi kwa madai zinawaharibia soko lao la filamu za ndani.

WANAFUNZI Wa Kike 82 Waliotekwa Na Boko Haram Waachiwa Huru..!!!

0
0

Ofisi kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa 2014, wameachiwa huru.

Maafisa wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi hiyo.

Wasichana hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wasichana hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi habari wa BBC Stephanie Hegarty kutoka Lagos.

HIMID Mao Atisha Majaribioni Denmark...!!!

0
0

Nahodha Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, anaendelea na majaribio yake kwenye kikosi cha Randers FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Denmark. 
Himid tayari ameshafanya mazoezi mara kadaa mpaka sasa toka awasili ndani ya kikosi hiko cha Randers.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, umeeleza kuwa kiungo huyo nyota mkabaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, 24, yuko tayari kwa mara ya kwanza kucheza soka la kulipwa na kulipa kisogo soka la nyumbani kwa kuhakikisha anapata mkataba wa kusajiliwa na Randers.

Nyota huyo ambaye atafanya majaribio ndani ya timu hiyo kwa siku 10, aliondoka nchini Jumatatu iliyopita baada ya pande zote mbili za timu hizo kufanya makubaliano kuhusu mchezaji huyo,

Mara baada ya kumaliza zoezi hilo atarejea mara moja Azam FC kabla ya taratibu nyingine kufuata kama watakuwa wamevutiwa na huduma yake.

Habari njema ni kuwa mbali na kufanya mazoezi na Randers, pia anatarajia kucheza mchezo mmoja akiwa na kikosi cha wachezaji wa akiba wa Randers kitakachocheza na AC Horsens Jumanne ijayo kwenye Ligi ya Wachezaji wa Akiba ndani ya Ligi Kuu ya Taifa hilo ‘Danish Superliga’.

FAHAMU Faida 9 za Kushangaza Utakazozipata kwa Kutumia Chai Yenye Mchaichai..!!!

0
0

Mchaichai ni mmea ambao unatambulika hapa nchini pamoja na Afrika kwa ujumla wake, lakini hapa nchini wengi huutambua mmea huu kama kiungo katika chai na husaidia kinywaji hicho kuwa na harufu mwanana zaidi na kuwavutia watumiaji.

Miongoni mwa faida za mchaichai ni pamoja na hizi zifuatazo:-

1. Kuzuia kutapika

2. Kutuliza maumivu ya tumbo

3. Kupunguza makali ya homa.
4. Msaada kwa wenye tatizo la  baridi yabisi,

5. Husaidia  kusafisha figo

6. Huzuia tatizo la tumbo kuunguruma 

7. Husaidia uyeyushaji wa chakula

8. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini.

9. Husaidia kupunguza maumivu kwa kinamama wakati wa hedhi 

MWANANGU ni Biashara, Msinipangie Cha Kufanya- Skyner Ally

0
0
Mzazi mwenzake Nay wa Mitego, Skyner Ally  amewatolea povu watumiaji wa mtandao wa kijamii wa Instagram wanaomnenea mabaya mtoto wake kuwa atakuwa jike dume kutokana na mavazi anayomvalisha yatawarudia wao na kwamba yeye anaendelea kutengeneza pesa.

Skyner ameamua kutoa povu hilo baada ya watu kum-'diss' namna anavyomvalisha mtoto wake wa kike huku wengine wakidai mtoto ataharibikiwa na kuwa jike dume kutokana na mavazi kitu ambacho kimemfanya Skyner kuweka wazi na kudai mtoto wake anamtumia kibiashara katika kuuza nguo zake na si vinginevyo.
"Wazazi na walimu wa instagram ifike pahala mniachie mwanangu, msiniingilie wala  kunipangia na hayo mnayomuombea mwanangu sijui atakuja kuwa jike dume Inshallah itawarudia nyie na vizazi vyenu  ifike pahala mnielewe nipo Instagram kibiashara sipo kwa ya ajili ya show off hapana"- aliandika Skyner.
Aidha Skyner ameongeza kuwa hawezi kutumia watoto wa watu wengine  katika kutangaza biashara yake wakati ana mtoto wa kufanya kazi hiyo pasipo kumlipia huku akidai mtoto wake ni wa kike japo kafanana na baba yake.

Huu ndiyo ujumbe aliouandika Skyner

"Huyu ni model wangu, Model wa biashara yangu. Nimchukue mtoto wa nani sasa anitangazie biashara yangu najua kuzaaa nimezaa na kulea pia nalea, lakini sura kachukua kwingne so sad. Nahitaji support yenu sana kwenye biashara yangu jamani namkubali tu kwamba huyu ndo Model wa biashara yangu atavaaa code zote ziwe za kike au za kiume kwa ajili ya biashara zetu mie na mwanangu niachieni mwanangu" - Skyner aliongeza



Skyner ambaye ni mama mzazi wa mtoto 'Munie' aliyezaa na mwanamuziki Nay wa Mitego amekuwa akimtumia binti yake katika kutangaza biashara zake zanguo katika mitandao ya kijamii kitu ambacho kimewafanya watumiaji wa mtandao huo kumjia juu kwamba anamuharibu mtoto kisaikolojia kutokana na aina ya mavazi anayomvalisha.

RAIS Magufuli Awapa Tumaini Jipya Wafanya Biashara

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 06 Mei, 2017 alizindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa 10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baraza hili ni la tatu na mkutano huu ni wa kwanza kuongozwa na Mhe. Rais Magufuli tangu aingie madarakani ambapo tofauti na mikutano mingine, Mhe. Rais Magufuli aliendesha majadiliano ya pamoja ambapo wajumbe wa baraza na wawakilishi wengine kutoka sekta binafsi walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo na dukuduku, kisha kupatiwa majibu kutoka kwa Mawaziri, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Mhe. Rais.

Miongoni mwa yaliyojitokeza ni kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika upangaji na utekelezaji wa mipango, sera na sheria mbalimbali za uwekezaji na biashara, kuendelea kuondoa vikwazo na urasimu ambao unachangia kupunguza ufanisi katika biashara na uwekezaji, kuongeza vivutio vya uwekezaji na kuendelea kushirikisha sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi, utalii na viwanda.

Aidha, wawakilishi wa sekta binafsi waliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi kubwa inazozifanya kujenga miundombinu muhimu kwa uwekezajina biashara kama vile ujenzi wa reli, barabara, meli na ununuzi wa ndege, kukabiliana na rushwa, kusimamia mpango wa ujenzi wa viwanda, kujenga nidhamu na uwajibikaji wa watumishi wa umma na kujenga uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali duniani.

Pamoja na majibu yaliyotolewa na Mawaziri ambao ni wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaahidi wawakilishi wa sekta binafsi waliohudhuria mkutano huo kuwa Serikali itahakikisha maoni yao yote yanafanyiwa kazi ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali zake na kusonga mbele kimaendeleo.

“Naomba niwahakikishie kuwa hisia zenu tumezipata, maoni yenu tutayazingatia na tutahakikisha tunayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kwa pamoja tufanye kazi ya kuijenga nchi yetu” alisema Mhe. Majaliwa.

Mhe. Rais Magufuli aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara pamoja na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Reginald Mengi kwa juhudi kubwa zinafanywa kuendeleza biashara na uwekezaji nchini na amewaahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwathamini na kushirikiana na wawekezaji na wafanyabiashara kwa manufaa ya Taifa.

Mhe. Rais Magufuli alielezea kufurahishwa na maoni, mapendekezo na dukuduku alizozipata kutoka kwenye mkutano huo na amewakikishia kuwa Serikali anayoiongoza itafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa ikiwemo kuondoa usumbufu unaosababishwa na uwingi wa taasisi zinazomhudumia na kumtoza mfanyabiashara na mwekezaji, kuongeza vivutio, kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa kodi mbalimbali na kuishirikisha sekta binafsi katika mipango na utekelezaji wa miradi.

Kuhusu tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini Mhe. Rais Magufuli aliagiza kuanzia Jumatatu tarehe 08 Mei, 2017 taasisi zote zinazotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ziungane na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoa huduma kwa muda wote wa saa 24.

“Kama alivyosema Waziri Mkuu, tunataka kufanyia kazi maoni yenu mara moja, kuanzia Jumatatu nataka taasisi zote za pale bandarini zitoe huduma saa 24, haiwezekani bandarini kwetu mizigo ichukue siku 13 kuitoa bandarini wakati bandari za wenzetu majirani inatoka baada ya siku 3, tutashindana vipi?” alihoji Mhe. Rais Magufuli.

Hata hivyo Mhe. Dkt. Magufuli aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wajirekebisha kwa kasoro ambazo baadhi yao wanazo ikiwemo ukwepaji wa kodi, kupandisha viwango vya bei kwa huduma wanazotoa Serikalini, kujihusisha na rushwa, kutaka faida kubwa isiyostahili bila kuwajali wananchi na kutochangamkia fursa za uwekezaji za ndani na nje ya nchi licha ya juhudi zake za kuwaleta viongozi na wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.

“Nataka mjiulize amekuja Waziri Mkuu wa India, amekuja Rais wa Vietnam, amekuja Rais wa Uturuki, amekuja Rais wa Kongo (DRC), amekuja Rais wa Zambia, amekuja Rais wa Uganda, amekujaMfalme wa Morocco na wengine wengi, tumenufaikaje? Mbona wao wanakuja kuwekeza hapa nyie kwa nini hamuendi kwao?” alihoji Mhe. Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

PSG Yamtengea Dau Nono Pierre - Emerick Aubameyang..!!!

0
0

Matajiri wa Ufaransa, Klabu ya soka ya Paris Saint-Germain yaweka mezani dau la Euro Milioni 70  kwa klabu ya  Borussia Dortmund ili wapate saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.

Taarifa kutoka ndani ya PSG zinakanusha habari hizo zilizoandikwa na gazeti la Bild la nchini Ujerumani kwamba mzaliwa huyo wa Ufaransa, ambaye amefunga jumla ya mabao 35 msimu huu, tayari amekutana na Mkurugenzi wa Soka wa PSG, Patrick Kluivert mjini Paris.

Aubameyang, mwenye umri wa miaka 27, kama dili hilo litafanikiwa,  atakuwa anaingiza kitita cha Euro Milioni 14 kwa msimu akitua PSG, pato ambalo ni mara mbili ya mshahara wake wa sasa.

Taarifa zinasema kuwa Dortmund inajipanga kupokea ofa ya PSG msimu utakapomalizika baada ya fainali ya Kombe la Ujerumani Mei 27 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kwa upande wa mchezaji huyo mara kwa mara amesikika akisema kuwa anataka kujiunga na kikosi cha Mfaransa, Zinedine Yazid Zidane,”Zizou” , kocha wa klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania.

RUPESH Kumar Kijana wa Miaka 21 Aliyezeeka Kabla ya Wakati..Matajiri Wajitokeza Kutaka Kumnunu Kama Kinyago..!!!

0
0

WAKATI mtu mwenye maradhi kama yake Ontlametse Ntlami Phalatse aliyefariki dunia nchini Afrika Kusini akiwa na umri wa miaka 18 ni kipenzi cha wengi nchini mwake, hali ni tofauti kwa Rupesh Kumar wa India.

Phlatse, ambaye tulitoa makala yake mara baada ya kifo chake hicho katika gazeti hili, hakuwa kiongozi, mpigania uhuru, msanii au mwanamichezo nyota bali mtu wa kawaida lakini mwenye maradhi  nadra, yasiyo na tiba ya Progeria, ambayo husababisha mtu kuzeeka haraka.

Phlatse licha ya maradhi yake hayo aliweza kujijengea sifa ya moyo wa kijasiri, kutokata tamaa, ucheshi, ukubwa wa upeo na akili katika kuelewa na kuchanganua mambo licha ya hali yake hiyo.

Lakini kwa ‘kijana mzee’ Kumar, kutoka Hanumanganj, nchini India badala ya heshima, anachukuliwa kuwa kituko, kikaragosi au kibwengo anayepaswa kutumika majukwaani kufurahisha watu kwa mwonekano wake.

Kumar amekuwa akizeeka kwa kasi ya mara nane kuliko kawaida kutokana na maradhi haya ya nadra ya kuzeeka.

Hali inayomkabili inayojulikana kwa kitaalamu kama Hutchinson-Gilford progeria, huathiri mmoja kwa kila watu milioni nane.

Kumar ndiye anayejulikana kama mtu aliyeishi miaka mingi zaidi (21) kutokana na maradhi haya akiwa na uzito wa kilo 19 tu.   

Kama ilivyo kawaida kwa maradhi hayo ya nadra, Kumar alianza kuonesha dalili hizo mbaya katika umri mdogo. 

Baba yake Ramapati Kumar (45), mfanyakazi wa shambani, anasema: “Ilianza kwa maumivu ya mara kwa mara ya kichwa na tumbo, wakati alipokuwa mdogo.

“Tulimpeleka kwa madaktari kadhaa, lakini hakuna aliyeweza kubaini maradhi yanayomkabili.

“Walituandikia dawa chache za kuua maumivu na kuturuhusu kuondoka.” 

Wakati Rupesh alipokua, wazazi wake waliona mabadiliko yasiyo ya kawaida katika mwili na mwonekano wake.

Baba yake anasema: “Kwa kipindi fulani, alikuwa akikua kwa hali isiyo ya kawaida na alianza kushuka uzito kwa kasi mno.”

Miaka mitano iliyopita, mara kadhaa watu wachache walikuja katika kijiji chao wakijifanya kuwa na lengo la kumsaidia Rupesh.

Anasema; “nilidhani walikuwa watu wazuri waliotaka kutusaidia na matibabu ya mwanangu.

“Lakini nilishtushwa nilipobaini lengo lao lisilo la kawaida. Ni pale waliposema walitaka kumnunua mwanangu na kumtumia katika maonesho yao kama kikaragosi.

“Hakika nilifedheheka mno kusikia hivyo, yaani mwanangu awe kichekesho majukwaani kisha kujiingizia fedha ninazoamini zitakuwa haramu?

“Walitoa ofa ya Rupia za India (Rs) 300,000 (sawa na karibu Sh milioni 12). Licha ya hasira, ghadhabu na kujisikia vibaya kwa nia yao, nilijikaza na kuwaambia kwa upole waondoke mara moja.”

Anasema tangu aneshe msimamo wake huo, wakaogopa na hawakurudi licha ya uroho wao mwovu kwa mtoto wake. Anasema asingeweza kumtoa mwanawe hata kama wangetoa Rs 10,000,000 sawa Sh milioni 350.

Mama wa Rupesh, Shanti Devi ambaye amekuwa mwangalizi wake mkuu anasema: “Hawa wana utu kweli? Wanawezaje kuthubutu kutoa ofa hiyo isiyo ya kibinadamu?”

Bahati mbaya maradhi ya Hutchinson-Gilford progeria hayatibiki, lakini bado Rupesh ameweza kuishi hadi miaka ya 20 kinyume ya matarajio ya wengi.

Daktari wake Dk. Yugantar Pandey, anasema mtoto huyo anaugua maradhi ya progeria ambayo hayana tiba.



“Watu wengi wanaougua progeria hufa wakati wafikishapo umri wa miaka 13-15, lakini katika baadhi ya kesi, kama Rupesh huishi hadi umri wa miaka 21.

Dalili za progeria kwa mara ya kwanza zilionwa katika mwili wa Rupesh akiwa na umri wa miaka miwili.

Kwa sababu ya maradhi hayo, ukuaji wa mwili wake ukakoma, nywele zikaanza kunyonyoka na ngozi na meno kudhoofu.

Anasema misuli ya wagonjwa hupoteza nguvu. Kama ilivyo kwa kesi nyingine za progeria, macho ya Rupesh yamezama ndani na ngozi kuwa angavu.

Daktari huyo anasema: “Hili ni tatizo la kinasaba, ambalo hutokea kutokana na mabadiliko ya vinasaba.”  

Wazazi wa Kumar' wanasaka msaada na wameenda mbali hadi kumwandikia barua Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi kwa ajili ya msaada ambapo sasa wanasubiri jibu kutoka serikalini.

Kwa wakati fulani asasi isiyo ya kiserikali Memorial Trust, inasaidia kuhakikisha Rupesh anapata tiba hasa. 


Hutchinson-Gilford Progeria ni nini?

Maradhi ya Hutchinson-Gilford Progeria ni ya nadra yakiwa hali mbaya ya kinasaba inayoshuhudia mwonekano wa kuzeeka miongoni mwa watoto.  

Inasababishwa na mabadiliko ya kinasaba kiitwacho LMNA, ambazo hutengeneza protini inayozishikilia seli pamoja.

Kukosekana kwa utulivu wa seli hizo huonekana kusababisha kuzeeka kabla ya wakati.

Waathirika kwa kawaida huonesha dalili wakiwa na umri wa miezi 18-24.

Dalili hizo ni pamoja na kushindikana kwa ukuaji, kupoteza mafuta mwilini na nywele, ngozi kuzeeka, matatizo ya viungo. 

Wagonjwa kwa kawaida hufa kwa maradhi ya moyo wakiwa na umri wa miaka 14.

10 Phylosophy of Life. Hebu Jaribu Kuzifuata Hizi kwa Usalama Wako..!!!!

0
0

FALSAFA BORA YA MAISHA YAKO!
1-Uckubali kuzoeana na mtu usiyemjua
2-Unapoitwa ghafla usigeuke,puuza kama husikii ili kupima sauti ni ya nani?
3-ucpendelee kutumia njia moja,badilisha njia nyingine ili usiwe maarufu kwa njia fulani
4-popote utakapo kwenda fuata shida yako iliyokupeleka
5-Epuka kuchunguza na kufuatilia kitu kisichokuhusu na epuka kulaumu hadharani
6-jitahid kumjua mtu tabia yake
7-mjali mwenzako tunza siri na jitahid kutimiza ahadi
8-Ukiaminiwa basi na wewe jiaminishe.
9-Usiwe na tabia ya kudharau wenzio
10-Ridhika na ulichonacho kwa MUNGU useme ahsante...
ongezea na ww falsafa yako!!

MWALIMU Asimulia Safari Iliyoua Wanafunzi 32..!!

0
0

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya Lucky Vicent Academy waliyokuwa wanasoma wanafunzi 32 waliofariki dunia kwa ajali jana, Longino Vicent amesema ndiye aliyesimamia safari iliyosababisha vifo vya watoto hao na wafanyakazi watatu.

Vicent amesema wanafunzi hao na walimu wawili pamoja na dereva waliofariki, walianza safari yao saa 12:30 asubuhi kuelekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.

“Mimi ndiye niliyesimamia safari hiyo na niliwasafirisha waliondoka hapa saa 12; 30 asubuhi, sikufikiri kama yatatokea haya. Kila kitu kilikuwa salama tu,” alisema akisimulia walivyoanza safari watoto hao kabla ya gari walilopanda aina ya Toyota Costa lenye namba za usajili T 871 BYS kupinduka korongoni na kusababisha vifo hivyo.

Mwalimu Longino alisema shule hizo mbili zimekuwa na tabia ya kufanya mitihani ya ujirani mwema na kuwa hiyo ni mara ya tatu.

“Huu ni mwaka wa tatu, hata shule ya Tumaini huwa inakuja Arusha,” alisema.

Mwalimu huyo alisema shule hiyo ilikuwa ya kwanza kimkoa mwaka 2004 na ya 20 kimkoa katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Wanafunzi hao waliofariki dunia walikuwa wakisoma shule hiyo ya bweni ambayo kwa mujibu wa wakazi wa Arusha ni miongoni mwa shule bora na iliyotoa mwanafunzi bora katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga alisema eneo la ajali lina kona nyingi na mteremko mkali na kwamba, kuna maeneo ambayo yamekuwa yakisababisha ajali kutokana na miundombinu yake ilivyokaa.

Aliyataja eneo jingine kuwa lipo barabara ya Morogoro kwenda Dodoma linaloitwa Makunganya lina utelezi mwingi na kuwasihi madereva kuwa makini sana wakati wa mvua. Wanafunzi waliofariki ni wa darasa la saba.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro alisema miili ya wanafunzi hao itaagwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid leo.

SAKATA la Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Laibuka Bungeni...Ni baada ya Godbless Kulianzisha Huku Akidai Amefichwa..!!!

0
0

Kauli aliyoitoa bungeni juzi usiku mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amefichwa ilisababisha mawaziri wawili wa sasa na mmoja wa zamani wamkomalie kuifuta.

Bunge lilikuwa likijadili Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Awali, Lema alisema ameona kwenye mitandao juu ya Kinana kufichwa na kupaza sauti akitaka kumtetea akiwa kama Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani.

Hata hivyo, kauli hiyo ilimsimamisha Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene akitumia kanuni ya 64 (2) ambayo alisema inatoa nafasi kukumbusha Bunge kwamba kuna kanuni inayovunjwa.

“Mbunge anayezungumza anasema jambo ambalo hana uhakika nalo, linatia mashaka, sidhani kama ana uhakika kwamba Kinana amefichwa. Alithibitishie Bunge hili na kama hawezi kuthibitisha, kupitia kanuni ya 72 (2) nakuomba Mwenyekiti umtake afute maneno hayo,” alisema Simbachawene.

Ufafanuzi huo ulimuinua kitini Tundu Lissu na kusema Simbachawene hajui atendalo, Mungu amsamehe.

“Kanuni ya 72 (2) inasema mbunge atakayekiuka utaratibu uliowekwa na kanuni hizi anaweza kutakiwa na Spika hapohapo afuate utaratibu au mbunge atasimama kwa kutumia utaratibu huo na kutaja kanuni iliyokiukwa,” alisema Lissu.

Baada ya maelezo hayo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenister Mhagama ambaye ni mnadhimu mkuu wa Serikali aliweka msisitizo kwenye kanuni ya 64 (1) (a) ambayo inakataza mbunge kutotoa taarifa ambazo hazina ukweli.

“Naomba nimthibitishie mheshimiwa Lema kwamba Kinana tumezungumza naye wakati wa maadhimisho ya Muungano, wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi. Kinana ametoka kwenye matibabu na sasa anapumzika nyumbani kwake.

Alipomaliza kuzungumza Jenister aliinuka Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika ambaye aliwahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali katika Serikali ya Awamu ya Nne na kuomba mwongozo wa mwenyekiti kuwa tangu Lema aanze kuchangia hakuwa anazungumzia jambo lililoko mezani, yaani bajeti ya wizara ya habari.

“Mheshimiwa Lema tangu ameanza hakuzungumza habari zozote kuhusu wizara. Mimi kwa umri huu hata ukinizomea siachi kuzungumza. Mheshimiwa Mwenyekiti naomba muongozo wako kuhusu kanuni ya 64 (b) inayosema mbunge hatazungumzia jambo nje ya mjadala.

Akitoa mwongozo wake Mwenyekiti wa Bunge, Azzan Zungu alisema kwa mujibu wa kanuni hizi 68 (10) Spika ndiye mwenye uamuzi wa mwisho kuhusu masuala yote ya kanuni, kwa hiyo akamtaka Lema afute maneno hayo na Lema aliyafuta akisema anafanya hivyo kwa kuwa waziri amemhakikisha kwamba Kinana hajatekwa.

Rais Kenyatta wa Kenya Akiwaombea Wanafunzi 33 wa Tanzania Waliofariki Jana

0
0
Rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Kenya amewaongoza raia wa nchi hiyo jana katika kuomboleza vifo vya wanafunzi 33 vilivyotokea Wilayani Karatu, Mkoa wa Arusha nchini Tanzania.

Kenyatta ambaye ni mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya muungano wa Jubilee, aliwaomba raia wa Kenya kusimama kwa dakika moja kuomboleza na kuwaombea wanafunzi 33, walimu 2 na dereva waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jana saa tatu asubuhi.

Rais Uhuru alitoa heshima hiyo alipokuwa katika moja ya mikutano yake ya hadhara nchini humo ambapo anatetea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.

Kuolewa sio bahati, USIBAHATISHE

0
0

“KUOLEWA NI BAHATI!!” hii kauli ina ukweli kiasi gani kwako?! Unaamini kuolewa ni bahati??
Kuna wanaume na wanawake ambao wanaamini  kwamba mwanamke anapoolewa tu basi amebahatika sana bila ya kujali kaolewa na mtu wa aina gani na kwasababu zipi. Ambapo ni sawa na kusema kwa kuolewa, mwanamke anakua amefanyiwaFAVOUR, AMESAIDIWA au AMEPEWA ZAWADI kwa kuolewa kana kwamba mwanamke pekee ndie anaefaidika na ndoa. Na hiyo bahati yenyewe inayotokana na kuolewa huko sio kupata mume ambae anastahili kuitwa mume bali ni kupata mahali pa kulala, chakula na mavazi. Wengine hua wanafika mbali kiasi cha kuwauliza wenzi wao  moja kwa moja “unalalamika nini wakati unakula, unalala na unavaa vizuri?” 

pale mwanamke anapoonyesha kutoridhisha na namna mahusiano yao ndani ndoa yanavyoenda mf. mume kutokua mwaminifu,  kutokuwepo nyumbani muda wa kutosha,  kulewa sana, kumdharau mkewe n.k .

Je, ina maana wanawake wanaolewa ili wale, walale na wavae? Walipokua kwa wazazi wao au wakijitegemea waliishi bila kula, kuvaa na kulala ndani ya nyumba?
Kinachosikitisha zaidi ni kuwa baadhi ya wanawake wanaunga  mkono mawazo haya. Wanakubali kuchukuliwa kama watu wanaopewa msaada kwa kuolewa.

Ladies, wahenga waliposema “Majuto ni mjukuu.” hawakukosea hata kidogo. Siku zote majuto huja baadae. Usikimbilie ndoa kwa minajili ya kukamatia‘BAHATI’ chini alafu baadae ukashangaa wewe ndo umekamatiwa chini na ndoa ambayo kila ukilala, kila ukiamka unajiuliza ilikuwaje ukakubali kuolewa na uliyeolewa nae. Usishinikizwe na mtu ama jambo lolote lile kuingia ndoani bila kuwa na uhakika huyo unaeingia nae ndio mtu sahihi kwako. Tumia muda wa kutosha kufanya tathmini kabla ya kufanya maamuzi.
Kuna mambo kadhaa ambayo naamini yanaweza kusaidia sana katika kufanya tathmini…
Mnapokuwa mmetofautiana/mmegombana huwa unajuta kumfahamu ama kuwa kwenye mahusiano nae?Jiulize, utakuwa wapi miaka 5 ijayo? Unajiona ukiwa na unayetarajia kuolewa nae?Mvue / mnyang’anye mtarajiwa wako mali na cheo alichonacho alafu uangalie je, bado unajiona ukiolewa nae? Yani kesho na kesho kutwa mwenzio kibarua kimeota nyasi, hela hana utamkimbia au utaendelea kuwa nae na kum-support?Mungu aepushie mbali mtarajiwa wako amepata ajali na kupoteza kiuongo cha mwili wake/mwili wake unaacha kufanya kazi vizuri ama anapata ugonjwa ambao unamuondolea uwezo wa kujitegemea na kujihudumia hata kwa mambo madogo madogo tu, UTABAKI NAE?Na je, ikitokea kwamba wewe ndio umepatwa na matatizo (umefulia, huna kazi, mgonjwa hujiwezi, umepata ukilema n.k) UNAAMINI kwamba mtarajiwa wako atakuwa na wewe bega kwa bega bila ya kukudharau na kukusimanga? Maana siku zote majibu yote huwa tunayapata mwanzo kabisa wa mahusiano (mf. mtu ni mbinafsi sana, mnyanyasaji, sio mwaminifun.k) ila huwa tunachagua kupuuza na kukomaa na mahusiano ambayo hayakuwa mazuri tangu mwanzo. (hii mada tutaizungumzia siku nyingine).

BAHATI ya kweli ipo kwenye kumpata mtu ambae anaelewa nini maana ya ndoa na kuiheshimu ndoa yake,  anaempenda mwenzi wake, anaemheshimu mwenzi wake pamoja na mawazo yake,  anaemsikiliza mwenzake,  anaejielewa na kujitahidi kumwelewa mwenzake, aliye tayari kujitoa kwa mwenzake, anaejua na kutimiza majukumu yake, anaejitahidi kumfurahisha mwenzake kwa maneno na matendo. Vivo hivyo kwa wanaume. . . .wenye bahati sio waliooa bali ni waliooa wanawake wenye sifa nilizotanguliza hapo juu. Mtu ambae hata ndani ya moyo wako unajua kabisa ni wako kwa 100% na sio mtu unaeishi nae kwa wasiwasi ama kwa kujilazimisha.
Kuolewa (hata kuoa) sio bahati hivyo usibahatishe.

EXCLUSIVE VIDEO: Mume mpya wa Flora afunguka

0
0
Daud Kusekwa ndio jina la Mume mpya wa Mwimbaji wa nyimbo za Injili Madame Flora (zamani Flora Mbasha) ambapo ndoa yao wameifunga mwishoni mwa April 2017.

Baada ya Daud kuona mitandao inavyosema na watu wanavyokosoa muungano mpya wa wawili hao, amekaa kwenye AyoTV na millardayo.com na kuzungumza ya moyoni EXCLUSIVE, bonyeza play kumtazama hapa chini

UINGEREZA Yatengeneza Nyambizi Hatari Zaidi Duniani

0
0
Astute ni nyambizi mpya kabisa zinazotarajiwa kuanza kazi kwenye jeshi la majini la Uingereza kuanzia mwaka 2018.

Nyambizi hyo inaendeshwa kwa nguvu za nyuklia pia inatajwa kua ni nyambizi kimya sana kuliko zote jambo linalofanya kua ngumu kujulikana ama kuonekana na adui.

Inaarifiwa kwamba nyambizi hii ina uwezo wa kukaa ndani ya maji hadi miaka 25 bila ya kutokeza juu labda kwa ajili ya kuongeza hifadhi ya chakula au mahitaji mengine kwa wafanyakazi wake.Japo ina uwezo wa kukaa ndani ya maji kwa hadi miaka 25 lakin mahitaji ya chakula hufanya kukaa kwa hadi miezi mitatu tu kwa ajili ya kuongezea hifadhi ya chakula kwa wahusika. Pia ina uwezo wa kubeba wanajeshi maalum(special forces) kuwapeleka sehem husika na kutoka ndani ya nyambizi hiyo bila kulazimika kuja juu ya maji.

Japokua nyambizi hii inaendeshwa kwa nguvu za nyuklia lakini silaha zake hazihusiani kabisa na ubebaji au mashambulizi ya nyuklia(hazibebi makombora ya nyuklia) bali katika mashambulizi ya kawaida kama kuwinda na kuzilipua nyambizi nyingine. Silaha zake inajumuisha makombora ya kulipua meli,mashambulizi ya makombora ya cruise(Tomahawk), nk.

Nyambizi hii inayotarajiwa kuanza kazi mwakani bado taarifa zake nyingi zimefichwa(siri) ikiwemo ni umbali gani inaweza kuzama chini ya maji japo kwenye majaribio iliweza kwenda chini umbali zaidi ya mita 300(300m).

NAHISI Nina Pepo la Ngono...Nagegeda Wanawake Wanne Kwa Siku Plus Mke Wangu

0
0
Habari wana Jambi
Kiukwel siku ya Jana kama ingekuwa Olympic nngetwaa medal ya gold.
Picha linaanza asubuh ofisini mfanya usafi Monica ananipa utamuuu bila hiyana mezan pale ofisini ka nusu saa ivi kakojoa Mara mbili na kusquirt juu

kwa kuwa Jana j mos kazin kutoka mapema naenda carnival mabibo pale nakutana na Malaya flani ivi nlipiga kitambo duuh kanona kwl nkachukua chumba fasta nkampga viwil vya adabu pia na kuishia nkimwacha na smile kwa mapenz yale
jioni nko kwa gari naenda home Aisha jiran yangu anasema npitie kwake anaumwa nimsalimie duuh nayeye akaishia anataka mchezoo nkapgaaa mtoto wa kiume kimoja huku akilia nimuowee
Nkiwa nmechoka hatari mke wanguuu na yeye full kujiliza ana minyege nkampa kimoja fasta akalala
Nmeamka morng nmechokaaaa wife kaenda church Niko na beki tatu mtanga huyo kanjia na kanga moja na kamvua haka na yeye nmemlaaa bila uogaaa kachafua mashukaa naenda kufuuaaa
Nahis nmevunja record ndugu zanguuuu au nina pepo la ngono?

By Tajiri/JF

RAILA Odinga Kumtumia Rais Magufuli Kwen ye Kampeni Zake za Urais Kenya ni Kosa Kubwa..!!!

0
0

hebu tujadili UBAYA na UZURI wa kumtumia Magufuli katika kampeni za jirani zetu Kenya.

Katika mkutano wao wa KUMUIDHINISHA rasmi mgombeaji wa upinzani wa ODM dhidi ya rais Kenyatta. Mh. Raila odinga alitumia video ya kushangaza sana iliyomwonyesha Rais wetu John Pombe Magufuli kama vile ANASAPOTI kampeni ya RAILAOdinga.

Mimi binafsi naona ni kama strategists wa NASA wamefanya MAKSUDI ili KUTUGOGANISHAU kati yetu na jirani zetu wazuri Kenya.
Urafiki wao wawili walipokuwa MAWAZIRI hauhusiani HATA KIDOGO na maswala ya USALAMA wa nchi yetu.

Nina maana Magufuli sasa is AN INTERNATIONAL FIGURE/Mtu wa KIMATAIFA. Hivyo kumweka kwenye VIDEO ya KUOMBA URAIS Kenya HAIMHUSU hata kidogo na NIKUTUCHONGANISHA!

Kwanza yeye ni Mwenyekiti wa EAC na haitajiki kuwa na upendeleo wowote. Kampuni za Kenya hapa Tanzania zimeajiri watu 50 elfu na zaidi.

Ni vizuri IKULU ama MSEMAJI wa serikali atoe KAULI rasmi, kuwa Tanzania haipendelei MGOMBEAJI yeyote yule nchini Kenya na maamuzi ya Wakenya ndo yatakubalika katika Jumuia ya Africa Mashariki.

Hii itatusaidia Raila Odinga ASIITUIINGIZE katika mizozano isiyo na tija kati yetu na Kenya maana HATUJUI nani atakuwa RAIS wa KENYA baada ya UCHAGUZI..

CONFIRMED: Ni Kweli Tanzania Imenunua Ndege ya Boeing 787-8 Yenye Line Number 719..!!!

0
0

Kumekuwepo na uvumi kuwa eti Tanzania imenunua ndege mbovu aina ya boeing 787-8 Dreamliner ambayo ni Terrible Teen line number 19 yenye serial number 35508.

Uvumi huo na uchochezi huo ulienezwa na kukolezwa zaidi na mbunge wa Kigoma mjini mh. ZK kwenye mitandao yake ya kijamii zikiwemo akaunti zake za facebook na twitter kuwa eti serikali imenunua ndege TT liyokatataliwa na Rwanda na Moroko yenye line #19 kwa bei ya ndege mpya na ZK kupata uungwaji mkono wa watanzania wengi.

Mh. ZK amekuwa akitoa ushahidi kutoka vyanzo visivyo na uhakika kama b787register.com, chanzo ambacho kimeweka taarifa kuwa ndege hiyo itakuwa delivered kwa Air Tanzania mwezi Agosti 2017 kitu ambacho ni uongo.

Ikumbukwe kuwa baada ya mazungumzo kati ya Rais wa Tanzania na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya ndege ya Boeing Bw. Jim Deboo, Rais wa Tanzania alisema kuwa ndege inayonunuliwa na Tanzania itawasili mwezi juni mwaka 2018.

Katika majibu yake bungeni kwa swali lililoulizwa na mh.ZZK , waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Mbarawa alikanusha uvumi kuwa Tanzania imenunua ndege ambayo ni Terrible Teen yenye line#19 na kubainisha wazi kuwa taarifa hizo ni za uongo na ukweli ni kwamba ndege ya boeing 787-8 iliyonunuliwa na Tanzania ni mpya kabisa na ina line #719 .

Sijui kwa kutafuta kick zaidi, mh ZK akazidi kutweet kuwa eti Mh Waziri amedanganya bunge anaficha ukweli na hata mh mbunge huyo kutweet akiwauliza Boeing kuhusu TT line #19 kuuzwa kwa Tanzania kwa bei ya mpya, uzuri Boeing hawakumjibu.

Sasa imekuja kudhihirika kuwa maneno ya Waziri ni sahihi kuwa Tanzania imenunua ndege mpya ya Boeing 787-8 yenye line #719. Ndege 787-8 TT yenye line #19 imechukuliwa na kampuni nyingine

Woodys AeroImages na 787blogger kupitia akaunti zao za twitter wamethibitisha kuwa ndegeiliyonunuliwa na Tanzania kutoka Boeing ni yenye line #719

My Take: Nawashauri wanasiasa wasiingize siasa katika mambo ya msingi ya maendeleo ya Taifa kwa ajili ya manufaa yao kisiasa, hiyo inaweza kuwaharibia na wakati mwingine kupoteza imani kwa wananchi

WAZIRI Muhongo: Mikataba Yote ya Umeme Nchini ni Mibaya..!!!

0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo amewataka watanzania kukubaliana na ukweli kuwa mikataba yote ya umeme iliyopo hapa nchini ni mibaya. Waziri Muhongo ameyasema hayo alipokuwa akijibu changamoto zilizoelekezwa katika Wizara yake katika Mkutano wa Baraza la Taifa la Biashahara, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Hatahivyo,Waziri Muhongo hakufafanua kuhusu wahusika wa mikataba hiyo;mikataba husika na namna ya kuifanya iwe mizuri. Mtakubaliana nami kuwa mikataba ya umeme kati ya TANESCO na Makampuni ya kuzalisha umeme imekuwa ikizalisha kashfa za kifisadi pamoja na kesi mbalimbali za jinai na madai kwa miaka mingi sasa.

Viewing all 104415 articles
Browse latest View live




Latest Images