Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

BEI ya Sembe Yapanda Juu Mara 12 ya Bei ya Saruji..!!!

$
0
0

WAKATI bei ya unga wa sembe ikipanda mpaka kufikia kuuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500 kwa kilo, ile ya mfuko wa saruji wenye uzito wa kilo 50 imeshuka hadi sh. 9,000, sawa na Sh. 180 kwa kilo.


Katika masoko na maduka mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ambayo Nipashe ilitembelea jana, bei ya sembe ilikuwa ikiuzwa kwa kiasi hicho kwa rejareja huku wauzaji wa jumla wakiuza kiroba cha kilo 50 kwa kati ya sh.100,000 na sh.98,000.

Ibrahim Omary, mfanyabiashara wa Kariakoo alisema anauza unga wa sembe kwa Sh. 2,400 kwa kuwa hununua kwa bei kubwa kutoka kwa wazalishaji.

Alisema kampuni inayojulikana kwa jina la Mkulima huwauzia unga huo kwa Sh. 98,000 na Mama Neema huwauzia kwa sh. 100,000 kwa kiroba cha kilo 50.

Kwenye baadhi ya maduka ya kula ya Kinondoni, unga umekuwa ukiuzwa kati ya Sh. 2,200 na Sh. 2,500. Tandika bei ya wastani ni Sh. 2,200, Mwenge Sh. 2,400, Kimara sh. 2,500 na Yombo Vituka sh. 2,200.

Nipashe ilitembelea mashine zinazozalisha sembe katika eneo la Tandale ambako bei ya jumla kwa mfuko wa kilo 50 ni kati ya Sh. 92,000 na Sh. 94,000 huku kilo ya mahindi ikiuzwa kati ya sh. 1,300 na 1,500.

Baadhi ya wateja walikuwa wakilalamika gharama hizo za unga huku wakieleza kuwa kwa sasa wamepunguza matumizi ya unga wa sembe na kuamua kutumia mchele.

Janeth Masawe, mkazi wa Mwenge alisema kwa sasa wamekuwa hawanunui unga wa sembe mara kwa mara kama ilivyokuwa zamani kwa kuwa sembe inazidi gharama ya mchele.

“Bora ninunue mchele... maana naweza kupata mchele kwa sh. 1,800 kwa kilo lakini unga wa sembe ni mpaka niwe na sh. 2,400,” alisema.

Kupanda kwa bei ya unga kumetokana na kupanda kwa bei ya mahindi kulikosababishwa na uhaba wa chakula hicho kutokana na ukame ambao ulikumba maeneo mengi ya nchi kabla ya mvua za masika zilizoanza mwezi uliopita.

Gunia moja la mahindi linauzwa kwa bei ya wastani wa Sh. 112,000 kwa sasa katika maeneo ambayo ni chanzo kikuu cha zao hilo, uchunguzi wa Nipashe umeonyesha.

TWIGA JENGA

Tangazo kwa wafanyakazi wote lililotolewa na kiwanda cha saruji cha Twiga Jumatano wiki hii, lilibainisha kuwa mauzo ya mfuko mmoja wa Twiga Jenga kuwa sh. 9,000, Twiga Extra sh. 9,500 na sh. 10,000 kwa Twiga Plus.

Tagazo hilo lililoandikwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Jesse Shuma, lilitaka kuwaarifu wafanyakazi hao kuwa saruji "inauzwa kiurahisi na kwa bei nafuu katika eneo letu la maegesho ya magari lililoko Kizuga, nje ya kiwanda."

"Tafadhali mjulishe mfanyakazi mwenzako, rafiki, ndugu na jamaa.

"Wote mnakaribishwa."

Kuporomoka kwa bei ya saruji ambayo miaka miwili iliyopita ilikuwa ikiuzwa sh. 15,000 kwa mfuko wa kilo 50, kwa kiasi kikubwa kumetokana na ufunguzi wa Kiwanda cha Dangote mkoani Mtwara.

Kwa mujibu wa tovuti ya serikali ya mkoa wa Mtwara, "kiwanda hiki ni kikubwa kuliko vyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati" na kina uwezo wa kuzalisha tani milioni tatu za saruji kwa mwaka.

Kilianza uzalishaji rasmi Septemba, mwaka jana, baada ya uwekezaji wa dola za Marekani milioni 500 (sawa na Sh. trilioni 1.1).

Credit - Nipashe

RAIS wa CAF Akataa Kupokea Mshahara...!!!

$
0
0

Rais mpya wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amekataa kupokea mshahara wake kutoka kwa shirikisho hilo.

Akitoa sababu za kukataa kupokea mshahara huo, Ahmad alisema kuwa shirikisho hilo haliheshimu uongozi au utawala bora na haki za wafanyakazi.

“Nimekataa mshahara wa CAF kwa sababu rahisi, haiheshimu utawala bora. Mishahara ya waajiriwa wote wa CAF, kuanzia ngazi ya uongozi hadi kwenye Kamati na rais mwenyewe, kote inapaswa kuwe na uwazi,” Ahmad ameiambia BBC.

Ahmad ambaye ni raia wa Madagascar ameweka wazi msimamo wake kuhusu mshahara, wakati ambapo anafanya mkutano wake wa kwanza leo na viongozi waandamizi wa CAF kabla ya kushiriki mkutano wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), utakaofanyika Alhamisi ya juma hili.

Ajenda kubwa ya mkutano wa leo ni namna ya kufanya mageuzi ya kiutawala katika shirikisho hilo.

Ahmad aliingia madarakani mwezi Machi kupitia uchaguzi, baada ya kumwaga Issa Hayatou’s aliyeongoza kwa takribani miongo mitatu.

DOGO Janja Amwagia Sifa Harmorapa..!!!

$
0
0

Msanii wa bongo fleva mwenye 'hit song' ya 'Kidebe' Dogo Janja amefunguka kwa kusema anamkubali rapa chipukizi Harmorapa kwa kuonesha uthubutu wake katika muziki licha ya watu kumkatisha tamaa kwa kumwambia hajui kitu lakini hakurudi nyuma.

Dogo Janja amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kwa kudai kilichomfanya amkubali msanii huyo ni kutokana na kumuona ana moyo wa ujasiri wa kupambana muda wote katika kufikia mafanikio yake ya kimuziki bila ya kujali watu wanasema kitu juu yake.

"Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi kama mimi ....Ni mtu ambaye amejaribu kuonesha uthubutu..Stape ambayo ameenda ndiyo imenifanya mimi nimkubali zaidi, alianza wimbo wa kwanza watu wakamtisha tamaa, vunja moyo lakini hakuvunjika moyo. 'Dude' la pili akajaribu halafu likawa kali mimi nikasema huyu anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka kwa kuwa anaonekana na moyo wa uthubutu na anapenda kujifunza zaidi". Alisema Dogo Janja

Pamoja na hayo Dogo Janja amesema siyo kweli kwamba Harmorapa anabebwa na 'kiki' kuliko muziki wake ila watu wenyewe ndiyo wanamfanya kituko ili azidi kuonekana 'kiki.'

RAY C Afungukia A -Z Kuhusu Kutoka na Mbunge..111

$
0
0

Sexy lady mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi mbunge yoyote nchini kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakieneza ubuyu.

Ray C aliliambia Wikienda kuwa, mbali na kufahamiana na wabunge mbalimbali nchini, lakini hata siku moja hajawahi kujiingiza kwenye uhusiano na mheshimiwa yeyote kama inavyovumishwa.

“Kwanza kwa sasa mambo ya mapenzi nimeyaweka kando, niko bize na muziki wangu, akili na hisia zangu zote nimezielekezea kwenye kazi. Muziki ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Ray C.

MADAKTARI Watalii Kutoka Marekani Wajitolea Bure Matibabu ya Watoto Watatu Walionusurika Katika Ajali ya Basi..!!!

$
0
0

Madaktari watalii waliotoa msaada wa awali baada ya ajali iliyowaua wanafunzi na waalimu wa Lucky Vicent Academy wameahidi kuwapatia msaada majeruhi watatu waliobaki hospitalini hata kuwapeleka nje ya nchi kama itahitajika.

Akiwaongoza wakazi wa Arusha kuomboleza msiba katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu amesema kwamba Madaktari hao walikuwa watalii na gari lao lilikuwa mbele ya 'bus' la wanafunzi na hata baada ya ajali kutokea wao ndio walikuwa watu wa kwanza kutoa msaada wa kitaalamu.

Katika hotuba yake Makamu wa rais amesema kuwa hata baada ya kutoa msaada watalii hao  kutoka shirika la afya nchini Marekani wameahidi kujitolea kuwapatia matibabu wanafunzi watatu ambao ni majeruhi wa ajali hiyo na hata msaada kutoka nje ya nchi  wapo tayari kututoa.

KUTANA na Mtabibu Ostadhi Khamisi Kutoka Mombasa Kenya Kwasasa Yupo Tanzania Kwa Ajili yako

$
0
0
Kutana na ostadhi khamisi kutoka mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania ni mtabibu na mtafiti Wadawa za asili anatibia kama vile:
Miguu kuuma
Miguu kufagazi
Miguu kuwakamoto
Chango lauzazi kwakina mama
Dawa ya uzazi wakina mama inapatikana
Kusafisha nyota ili uwe namuonekano kwa kila mtu
Kumrudisha mpenzi wako na liekukimbia ndani yasiku 3 bila yapingamizi yoyote
Kumshika mume au mke asitoke nnje ya ndoa
Pata pete ya Bahati inayo endana na nyota yako
Kurudisha mali ilipotea au kudhurumiwa ndani yasiku 3
Pata utajili usiokuwa namashaliti yoyote
Dawa za nguvu za kiume
Dawa ya biashara inapatikana
Dawa ya kuzuia chuma ulete kwenye biashara inapatikana
 Zindiko la nyumba au shamba
 Anatuliza familia zinazogombana DUWA pamoja navisomo vya ufunguzi wa mwili wako njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa kutana na ostadhi khamisi utimiziwe ahadi ulizo hadiwa acha kuteseka acha kuhangaika ostadh khamisi yupupo tanzania kwajili yako...

Call +255718746825 +255754765246 kwa what'sapp +255783708487

WANAFUNZI wa Lucky Vicent Wafunguka Haya Mazito Baada ya Wenzao 33 Kufariki Katika Ajali ya Basi Juzi..!!!

$
0
0

Baada ya Shule ya Msingi ya Lucky Vicent kupoteza wanafunzi 32, walimu wawili na dereva katika ajali ya gari iliyotokea wilayani Karatu, wanafunzi wengine wamesema wamebaki nusu ya wanafunzi bwenini.

Kila mwanafunzi ameonekana mwenye hisia katika hafla maalumu ya kuaga miili ya wenzao kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa na msiba huu unaonekana utaendelea kuwa katika vichwa vya wanafunzi waliobaki kwa muda mrefu.

Ndiyo maana imemlazimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Eva Maria Semakafu kutoa ushauri wa uongozi wa elimu jijini Arusha, kuwatafutia mwalimu wa saikolojia ili awawezeshe kukabiliana na hali hiyo.

Noreen Josia, mwanafunzi wa shule hiyo anayesoma darasa la sita, anasema hatasahau msiba huo.

Anasema alishtushwa na taarifa kuwa gari lao la shule limepata ajali kutokana na simu ambazo zilikuwa zinapigwa na pia taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Nilirudi shuleni kuuliza kama ni kweli, nikaambiwa ni kweli. Tangu wakati huo hadi sasa, sijisikii vizuri, nahisi kuumwa kwa kuwa bwenini kwetu karibu nusu ya wanafunzi sijawaona. Nadhani wamefariki,” amesema huku akitokwa na machozi.

Noreen, ambaye muda mwingi, alikuwa ameshikiliwa na watoa huduma wa Msalaba Mwekundu, alisema: “Siwezi kusahau kwa kuwa tulikuwa nao bwenini wakati wakijiandaa kwenda kwenye mitihani ya majaribio Karatu na tuliagana. Sasa kuambiwa hawapo tena ni jambo ambalo siwezi kusahau,” anasema.

Noreen anawakilisha idadi kubwa ya wanafunzi wa shule hiyo ambao wameathiriwa na msiba huo mkubwa wa aina yake na ambao wamepewa siku saba za mapumziko kwa majili ya kutuliza akili.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ephraim Jackson anasema, wanafunzi 96 wa darasa la saba ndio walisafiri kati ya wanafunzi 106 wa darasa hilo.

KINANA Aibukia Arusha, Ateta na Lowassa, Mbowe..!!!

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana jana alionekana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva wa Shule ya Msingi ya Lucky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Aprili 6.

Na kilichovuta macho ya wengi ni kuonekana akizungumza na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa.

Kinana hajaonekana hadharani tangu kumalizika kwa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika Machi 12 mjini Dodoma.

Na maswali yalipoanza kuhusu kutoonekana kwake, Rais John Magufuli alisema “amemtuma India kwenda kutibiwa.

Jana, Kinana, ambaye amewahi kuwa mbunge wa Arusha na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki, alionekana mjini hapa na alitumia muda mwingi kusalimiana na watu waliokuwa wakimfuata.

Kinana alifika uwanjani akiwa kwenye gari la ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Arusha na alipanda moja kwa moja jukwaa kuu na baadaye alipata muda wa kusalimia mamia ya watu waliokuwa wamefurika katika uwanja huo.

Wakati shughuli za kuaga miili ikiendelea, Kinana aliteta kwa dakika chache na Lowassa aliyekuwa ameongozana naye.

Lowassa alisikika akimuuliza Kinana kuhusu afya yake na alijibiwa na katibu mkuu huyo wa CCM kuwa anaendelea vizuri. Wawili hao waliendelea na mazungumzo, huku wakipigwa picha.

Baadaye Kinana alizungumza na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia alimpa pole.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi jana kuhusu hilo, alisema: “Nitafute tutazungumza.”

Wakati huohuo, zaidi ya waombolezaji 100 walizimia wakati wa ibada ya kuaga miili hiyo.

Mmoja wa madaktari wa taasisi ya Msalaba Mwekundu ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema wamepokea watu watatu waliokuwa na hali mbaya akiwamo mtu huyo ambaye awali alidhaniwa kufa na baadaye akazinduka.

ATCL Yaanza Safari za Tabora—Dar..!!!

$
0
0

KAMPUNI ya Ndege ya Tanzania (ATCL), imeanzisha safari za kutoka Tabora kwenda mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam ikiwa na lengo la kurahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo kwa mikoa hiyo na ile ya jirani.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alisema katika uzinduzi wa huduma hiyo kuwa kuanzishwa kwa safari hizo kutaongeza wigo wa biashara na kukuza uchumi kupitia sekta  mbalimbali ikiwemo utalii na kilimo.

“Naamini wakazi wa mkoa wa Tabora na mikoa ya jirani, sasa mtanufaika kwa ujio wa ndege hii, matumaini yangu kwamba mtatumia usafiri huu kurahisisha shughuli zenu za kibiashara na kijamii,”alisema.

Ngonyani aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kutumia fursa ya ujio wa ndege hiyo kama chachu ya kuleta maendeleo katika mkoa huo.

Sambamba na hilo, Ngonyani alisema katika kuhakikisha usafiri wa anga unaimarika nchini, Serikali itaongeza ndege nyingine tatu katika mwaka wa fedha 2017/18 ambapo hadi kufikia mwezi Julai mwakani ndege hizo zitakuwa zimewasili.

Katika hatua nyingine, Ngonyani amewaagiza wafanyakazi wa ATCL kufanya kazi kwa juhudi, uadilifu na weledi ili kuijengea sifa kampuni hiyo na kuvutia wateja ili kujiimarisha katika soko la ushindani.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dk. Leonard Chamuriho aliwataka wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya kupata usafiri wenye gharama nafuu na wa muda mfupi.

Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri aliwataka wananchi wa mkoa huo na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kutumia huduma za usafiri huo waliokuwa wakiusubiri muda mrefu.

MBUNGE Mpya Chadema Aiga 'Swaga' Salma Kikwete Bungeni..!!!

$
0
0

MBUNGE wa Viti Maalum (Chadema), Catherine Ruge, jana aliuliza swali muda mfupi baada ya kuapishwa, akifuata nyayo za Salma Kikwete, mke wa Rais mstaafu ambaye ni Mbunge wa kuteuliwa.

Baada ya kuapishwa katika siku ya kwanza ya Bunge hili la bajeti Aprili 5, mke wa Rais wa Nne, Jakaya Kikwete, Salma hakupoteza muda kutaka kujua mpango mahususi wa serikali wa kuongeza usambazaji wa huduma ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini(TASAF) kwa watu maskini mkoani Lindi.

Si kawaida kwa wabunge wanaoapishwa siku hiyo kuuliza maswali, lakini muda mfupi baadaye jana, Ruge alihoji mkakati wa serikali wa kukuza utalii kwa upande wa magharibi wa mbuga ya Serengeti iliyopo mkoani Mara; ambao umeonekana kusahaulika.

Ruge aliuliza swali hilo la nyongeza kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, muda mfupi baada ya kuapishwa na Spika Job Ndugai.

Mbunge huyo alisema upande huo unaonekana umesahaulika, lakini una vivutio vingi vya utalii na hasa Ziwa Victoria, lakini pia kuna visiwa.

“Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa iliyobarikiwa kuwa na vivutio vya utalii vikubwa ikiwamo mbuga ya Serengeti kwa upande wa mashariki,” alisema Ruge.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri, Ramo Makani, alisema eneo linalopakana na Serengeti kwa upande wa magharibi ni kati ya maeneo ambayo serikali imeshaweka mipango thabiti ya kuboresha.

“Serengeti ipo milango ya kuingia ambayo mingi inatokea mkoa wa Arusha, lakini tumeshaangalia hili sasa kutakuwapo ya kutokea mkoa wa Mara, na Shinyanga tutaboresha mageti ili watalii waingie kwenye kona zote ili kuruhusu idadi kubwa ya watalii kuingia,” alisema Makani.

Alisema serikali ipo mbioni kuboresha maeneo hayo na kumkaribisha wizarani kutoa maoni ya kuboresha eneo hilo.

Ruge aliapishwa jana kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Dk. Elly Macha, ambaye alifariki dunia nchini Uingereza mwezi mmoja uliopita.

MKAGUZI Vyeti Feki Naye Atajwa Katika Orodha ya Wenye Vyeti Feki..!!!

$
0
0

Muosha huoshwa. Ndivyo ilivyo kwa mmoja wa wahakiki wa vyeti vya elimu katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Mkaguzi huyo naye ametajwa  katika orodha ya watumishi wanaotuhumiwa kuwa na vyeti vya kughushi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kumaliza kwa mafanikio kazi ya kuhakiki wafanyakazi wengine iliyomsababishia lawama na sasa ni mmoja wa wanaotakiwa kuondoka kazini kabla ya Mei 15.

Mkaguzi huyo aliyetajwa kwa jina la Adolph Shayo, jina lake ni namba 1,023 katika orodha ya watumishi 9,932 iliyokabidhiwa kwa Rais John Magufuli Aprili 28.

Baada ya kupokea majina hayo kutoka kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Rais Magufuli aliagiza wote waliotajwa waondoke vituo vyao vya kazi kabla ya Mei 15 na watakaokaidi wafikishwe mahakamani, ambako wanaweza kukumbana na kifungo cha miaka saba.

Pengine sio ajabu kutajwa kwenye orodha hiyo kwa kuwa ukaguzi wa vyeti haukuacha mtu au cheo, lakini kugundulika kwake kunaibua maswali zaidi katika uhakiki huo ambao tayari umeshaonyesha dosari kama ya kutaja baadhi kuwa wana vyeti vya kughushi vya elimu ya sekondari wakati hawakuviwasilisha kwenye uhakiki uliofanyika.

Kutajwa kwa Shayo kunaweza kuibua utata mwingine wa usafi wa uhakiki kutokana na ukweli kuwa utakuwa umefanywa na mtu ambaye hakustahili kuhakiki wengine.

Shayo alijipatia sifa ya kuwa  mkali na msumbufu wakati wa uhakiki, akidaiwa kuwataka mara kwa mara watumishi wenzake kumpelekea vyeti.

Mmoja wa waliokaguliwa na Shayo, ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema walimu walipata shida wakati wa uhakiki kwa sababu walikuwa chini ya mhakiki huyo.

Alisema alishangazwa kusikia amekuwa mmoja wa watu waliotajwa kuwa na vyeti vya kughushi wakati yeye pia alihusika kuhakiki.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Nassib Mmbaga alisema baada ya ukaguzi kufanyika ilibainika kuwa vyeti vyake vilikuwa na matatizo (ambayo hakuyataja) na wakamtaka kuthibitisha, lakini hakufanya hivyo.

“Ni kweli alikuwa mtumishi katika idara ya elimu na msaidizi katika kitengo cha bohari ya manispaa, lakini lilipokuja suala la ukaguzi wa vyeti ilibidi afanye kazi kama msaidizi,” alisema.

“Hata kama ni mkaguzi ni lazima akaguliwe. Hata mimi (mkurugenzi) nilikaguliwa. Lakini tulivyokagua vyeti vyake (Shayo) tuligundua vina shida,” alisema.

Alisema pamoja na kupewa nafasi ya kuthibitisha uhalali wa vyeti vyake, alishindwa kufanya hivyo hadi majina yalipotangazwa.

Mkurugenzi huyo alisema hadi sasa amepokea zaidi ya barua 60 za rufaa, lakini hajaona jina la Shayo.

Sakata la vyeti feki limezidi kuchukua sura mpya baada ya baadhi ya waliotajwa kuamua kwenda vyama vya wafanyakazi kudai wameonewa.

Mmoja wa waliochukua hatua hiyo ni mratibu wa elimu wa Wilaya ya Chamwino, ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM, Charles Ulanga ambaye hajawahi kusoma elimu ya sekondari.

Ulanga anadai kuwa hakuwahi kuwasilisha vyeti vya sekondari wakati wa ukaguzi na hivyo anataka kujua wahakiki walivitoa wapi.

Katika Manispaa ya Temeke, jumla ya watumishi walioghushi vyeti ni 270, kati yao 120 wakitoka idara ya afya huku Hospitali ya Rufaa ya Temeke ikiongoza kwa kuwa na watumishi 53.

Pia, Shule ya Msingi ya Mbagala imetoa walimu saba.

Kuhusu athari za matokeo ya uhakiki huo, Mmbaga alisema zinazidi kujitokeza kutokana na kupunguza idadi ya watumishi katika hospitali na shule. “Tunajaribu kujaza nafasi za watoa huduma kutoka katika zahanati ambazo hazihudumii watu wengi ili huduma zisisimame,” alisema.

BREAKING NEWS..Ajali Nyingine Yatokea Arusha na Kuua Watu Watano..Chanzo ni Nyumba Kuangukiwa na Mti Mkubwa..!!

$
0
0

MKOA wa Arusha Umeendelea Kukumbwa na baa la Ajali ,ambapo ikiwa haijakatika hata wiki toka ajali ya basi la shule kuua wanafunzi 36,leo hii kumetokea ajali nyingine ya nyumba kuangushwa na mti uliokuwa unasombwa na maji mengi,hali iliyopelekea vifo vya watu 5 na wawili kujeruhiwa.

Taarifa zilizotufiki hivi punde kutoka Jijini Arusha ,Zinasema kuwa mti huo uliseleleshwa na maji kwa umbali wa mita mia kabla ya kufikia nyumba hiyo na kusababisha watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo kupata ajali hiyo.

Taarifa zaidi ziwawajia kadri tutakavyozipokea kutoka Jijini Arusha..

VIDEO: Kali Nyingine ya Kagera, Mchungaji Aoa Mke wa Muumini

$
0
0
Wilaya ya Karagwe Kagera imeingia tena kwenye headlines kwa mkasa uliotokea katika kata ya Ndama baada ya Mchungaji wa kanisa katika huduma ya kristu {H.K.K} Japhes Josephat kumuoa Mke wa muumini wake kwa madai ameoteshwa na Mungu….

TAZAMA KILA KITU KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI

Breaking News: Basi la Ally's na basi la Isanzu Yagongana Uso Kwa Uso

$
0
0
Basi la Ally's lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Tabora limegongana na basi la Isanzu uso kwa uso lililokuwa linaelekea Mwanza kutoka Kahama

Ajali imetokea saa mbili asubuhi eneo la Samuye barabara barabara ya Shinyanga.Hali ya dereva wa basi la Isanzu si nzuri.

Watu kadhaa wamejeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya rufaa Shinyanga,hakuna mtu aliyepoteza uhai kwenye ajali hii.

MBUNGE Godbless Lema alaani ubaguzi aliofanyiwa msibani Arusha

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Godbless Lema ametoa masikitiko yake na kuonyesha kuumizwa na kitendo alichofanyiwa  jana wakati wa kuaga miili ya wanafunzi, walimu na dereva waliofariki katika ajali ya basi.

Lema anasema kitendo cha yeye kama Mbunge wa Arusha mjini pamoja na Meya wa jiji kunyimwa nafasi japo ya kutoa pole kwa familia na wafiwa wakati wa kuaga miili hiyo ni ubaguzi mkubwa.

==>Huu ni Ujumbe wa Godbless Lema

Leo(jana) katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki ktk ajali . Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .

Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais asingeweza kukubaliana na ujinga huu.

Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambirambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika na ilionekana dhahiri kuwa sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo, alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.

Wabunge wa CCM waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa, nitaeleza madhara yake kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto mara nyingi huwa wanafuata walichofundishwa na wazazi , pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais. Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama nchi na Syria ni wakati.

Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha, Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu hadhiakiwi apandacho mtu ndicho avunacho

LEMA

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Siku ya Leo

ALIYENUSURIKA Asimulia Wenzake 35 Walivyokufa..Aeleza Namna Basi Lilivyokuwa Likiviringika Huku Wakipiga Kelele Kuomba Msaada ..!!!

$
0
0

KUFELI kwa breki la basi la shule ya msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucy Vicent na udereva usio na uzoefu, vinahofiwa kuwa sababu ya ajali ya basi hilo iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa basi hilo.

Akizungumza jana , mmoja kati ya wanafunzi wasiozidi watatu walionusurika kwenye ajali hiyo, Urusula Godfrey, alisema mvua kubwa ilikuwa ikiyesha kabla ya ajali hiyo kutokea.

Kwa mujibu wa Urusula, ghafla aliona gari limeruka ambapo yeye wanafunzi wenzake wakiwemo waliokufa katika ajali hiyo, walibaini si mruko wa kawaida na mara moja walianza kupiga kelele za kuomba msaada.

Wakati wakipiga kelele hizo bila msaada, Urusula alisema alishuudia basi hilo likianza kuserereka mpaka mtoni (Mto Marera), ambako lilipinduka na kuanza kuviringika.

Baada ya hapo Urusula alisema hakutambua kilichoendelea zaidi ya kujikuta tu yupo hospitalini, alisema na kushindwa kuendelea kusimulia mkasa huo na kuanza kububujikwa na machozi kwa uchungu.

MAALIM Seif Afunguka Mapya Kuhusu Sakata la Jecha Kufuta Matokeo ya Uchaguzi Mkuu Znz

$
0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema alikasirika sana baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa 2015.

Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi huo Oktoba 28, 2015 akidai kulikuwa na ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi na miezi miwili baadaye aliitangaza Machi 20, 2016 kuwa terehe mpya ya kupiga kura.

Hatahivyo, CUF ilisusia uchaguzi huo wa marudio ambao Dk Ali Mohamed Shein alishinda kiti hicho kwa kishindo.

Uchaguzi huo ulifutwa siku ambayo mshindi wa kiti cha urais alitakiwa atangazwe huku matokeo ya majimbo 31 yakiwa yameshatangazwa na kura za majimbo tisa zikiwa zimeshahesabiwa pia nafasi za uwakilishi na udiwani zilishatangazwa na kutolewa hati za ushindi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu , Maalim Seif amesema, “Kama binadamu nilikasirika baada ya Jecha kufuta matokeo yale. Lakini mimi ni mtu mzima niliweza kujidhibiti mwenyewe hisia zangu, pia niliweza kutoa wito kwa watu kuwa wavumilivu, lakini kiukweli nilikasirika sana.”

Amesema kitendo cha Jecha cha kutangaza matokeo aliita cha kihuni kwa sababu ukishakubali mfumo wa vyama vingi ambao unawapa nafasi wananchi kufanya uamuzi kuhusu Serikali wanayoihitaji iwaongoze, lazima ukubali na matokeo.

Credit - Mwananchi


UJENZI wa Kituo Mbezi-Luis Kugharimu Sh Bil 28.7 Dar..!!!

$
0
0

GHARAMA za ujenzi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Mbezi Luis, Jijini Dar es Salaam zinakadiriwa kuwa Sh bilioni 28.71 zitakazotolewa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa Serikai za Mitaa(LAPF), Serikali imesema.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema). Kubenea alitaka kujua mradi wa kuhamisha kituo cha mabasi unatarajiwa kutumia kiasi gani cha fedha kutokana na ahadi ya serikali ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Ubungo kukipelekea eneo la Mbezi.

Akijibu swali hilo, Jafo alisema hadi tayari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na LAPF imeanzisha kampuni ya ubia ya Mzizima Properties Limited itakayohusika na usimamizi na uendeshaji wa shughuli za kituo za kila siku. “Kazi inayoendelea ni kumtafuta mtaalam mshauri kwa ajili ya kuthibitisha usanifu wa mwisho wa kina wa mradi ili kumpata mkandarasi wa ujenzi wa mradi,” alisema.

Hata hivyo alisema, gharama halisi zitajulikana baada ya usanifu wa kina utakaofanywa na mtaalamu mshauri. Naye Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema), katika swali la nyongeza alitaka kujua ni lini kituo hicho kitakamilika ili kuondoa msongamano katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo akisema kipo kwenye hali mbaya. “Kituo hiki kinajengwa pembeni ya barabara ya Morogoro na siku chache zilizopita Wakala wa Barabara (Tanroads) umetoa notisi kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara hiyo mita 121 kwa upande zote mbili kubomoa majengo yao ndani ya siku 28, ni kwanini serikali isitengue agizo hili ili majadiliano kwanza yafanyike,” alihoji.

Akijibu maswali hayo ya nyongeza, Waziri Jafo alikiri kuwa muda wa utekelezaji wa mradi huo umepita na kwamba, kuna ushauri umetolewa na Kamati ya Bunge ya Serikali za Mitaa kuhusu mradi huo. “Pia Jambo hili ni suala linalohitaji fedha nyingi na wastani wa Sh bilioni 28 siyo jambo dogo kuna makubaliano yalifanyika kati ya Jiji na LAPF, na Mfuko umewahakikishia kuwa utatengeneza kituo ambacho kwa Dar es Salaam ni kikubwa na kitakuwa na uwezo wa kuchukua magari mengi,” alisema. Alifafanua kuwa kuhusu utekelezaji asiwe na wasiwasi utatekelezwa na kuhusu uvunjaji serikali itaangalia nini kifanyike kwa mstakabali wa wananchi hao.

LITA 50,000 za Mkojo Zatumika Kutengeneza Pombe..!!!

$
0
0

Kiwanda kimoja cha pombe nchini Denmak kimetengeneza bia mpya kwa kuchanganya ngano na lita 50,000 za mkojo.

Hata hivyo bia hiyo haitakuwa na mkojo wa binadamu.

Mkojo huo ulikusanywa  kwa watu waliokuwa kwenye  hafla moja kubwa zaidi ya muziki barani ulaya miaka miwili iliyopita

"Wakati habari ziliposambaa kuwa tulikuwa tumeanza kutengeneza pombe, watu walidhani kuwa tulikuwa tukiweka mkojo huo moja kwa moja  kwenye pombe," alisema Mkurugenzi wa kampuni ya Norrebro Bryghus inayotengeneza pombe hizo.

“Kama ingekuwa na ladha ya mkojo ningeachana nayo, lakini hata huwezi ukahisi," alisema mtu moja ambaye alihudhuria warsha hiyo ya muziki mwaka 2015.

Lita hizo 50,000 zilizokusanywa kutoka kwa warsha hiyo ya muziki zilitosha kuunda chupa 60,000 za bia.

Mashine iliyotengenezwa na kundi la wanasayansi katika chuo kimoja nchini Ubelgiji, inabadili mkojo wa binadamu na kuwa maji ya kunywa pamoja   kwa kutumia nguvu za miale ya jua.

 Chanzo BBC.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images