Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live

MZIMU wa Live’ Waibuka Bungeni..!!!

0
0

Sakata la Serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni limeibuka upya, safari hii ukielekezwa kwa Rais John Magufuli.

Hata hivyo, shughuli nyingi zinazomshirikisha Rais zimekuwa zikirushwa moja kwa moja jambo lililomfanya Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Aida Khenani kuhoji sababu za kuzuia shughuli za Bunge kuonekana moja kwa moja.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Khenani alisema Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linatumia kodi za wananchi lakini vikao vya wabunge waliowachagua havionyeshwi moja kwa moja kuwawezesha kufuatilia wanachozungumza wawakilishi wao.

“Hapo kuna tatizo,” alisema Khemani.

Alihoji kama tatizo ni gharama kama Serikali ilivyoeleza, inakuwaje pale Rais anapozungumza gharama zinapungua na Bunge linaporushwa moja kwa moja ndiyo zinakuwa kubwa.

Khenani aliungwa mkono na mbunge mwenzake wa Viti Maalumu (Chadema), Mariam Msabaha aliyehoji sababu za Bunge kuwa na hofu ya vikao vyake kuonekana moja kwa moja.

Wabunge hao waliungana na mtangazaji wa zamani wa shirika hilo, Juma Nkamia (Chemba-CCM) aliyesema mwishoni mwa wiki kuwa shirika hilo limefika mahali pabaya hadi kuazima mitambo kwa watu binafsi kwa ajili ya kurusha matangazo ya ziara ya Rais Magufuli mkoani Mtwara.

Nkamia amesema hata studio inayotumika TBC ni ile iliyokuwapo tangu enzi za TVT na kwamba shirika hilo lina usikivu mbovu wa matangazo na pale wanaporusha moja kwa moja ni aibu.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura amesema ni kweli mitambo ya TBC imekuwa chakavu, lakini Serikali inaifanyia kazi na imeongeza bajeti ya shirika hilo kutoka Sh1 bilioni hadi Sh3 bilioni.

Akijibu hoja hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe alisema hoja ya Bunge Live amekuwa akiijibu na anachoweza kusema ni kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Mawasiliano Tanzania (TCRA) imelikabidhi Bunge leseni na sasa litaweza kuamua lolote.

Pia alijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na wabunge kuhusu bajeti ya wizara yake. Juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii, akisema ni hatari na isipoangaliwa inaweza kuingiza nchi katika matatizo, hivyo lazima sheria zichukuliwe dhidi ya wanaokiuka matumizi yake.

MWANAMKE Ameza Mamilioni ya Pesa Baada ya Kugunduwa Mumewe Ana Mchepuko...!!!

0
0

Raia wa Colombia, Sandar Milena (30) ametafuna na kumeza Yuro 7,000 sawa na Sh17 milioni alizokuwa ameweka akiba baada ya kugunduwa mumewe ana mchepuko.

Imeelezwa kuwa Milena amefanya hivyo kwa makusudi ili mumewe asizitumie na mchepuko wake.

Hata hivyo baada ya kutafuna na kumeza noti moja baada ya nyingine, Milena aliumwa na tumbo na kukimbizwa hospitali.

Kwa mujibu wa shirika ya utangazaji la BBC ni kuwa Milena alifikishwa hospitalini na kufanyiwa upasuaji.

Mkurugenzi wa upasuaji katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Santander, Juan Serrano amesema Milena alifanyiwa upasuaji na fedha hizo zikatolewa.

“Alifanya hivyo kutokana na tatizo lililomkabili ila tumefanikiwa kutoa baadhi noti zikiwa nzima  katika utumbo mkubwa lakini  nyingine zimeharibika,”amesema.

Mkurugenzi huyo amesema Milena anaendelea vizuri na afya yake inatarajiwa kuimarika zaidi.


BEI ya Sukari Dar Haishikiki..!!!

0
0

BEI ya sukari katika jiji la Dar es Salaam imeendelea kupaa, huku baadhi ya maeneo ikianza kuadimika.

Uchunguzi uliofanywa umebaini kupanda kwa bidhaa hiyo kutoka Sh 2,300 hadi 2,800 kwa kilo moja.

Gazeti hili lilifika kwa Wakala Mkuu, Haroun Zacharia na kukuta mfuko wa sukari wenye uzito wa kilo 50 umepanda kutoka Sh 104,000 hadi 116,000.

Mfuko wa kilo 25 unauzwa Sh 58,000 badala ya Sh 52,000, huku ule wa kilo 20 ukipanda kutoka Sh 42,000 na sasa unauzwa kwa Sh 46,000.

Kwa Wakala Mkuu mwingine, Mohamedi Enterprises, mfuko wa kilo 50 umeuzwa kwa Sh 118,000 hadi 120,000, mfuko wa kilo 25 unauzwa Sh 58,000 na wa kilo 20 umeuzwa kwa Sh 47,000.

Mmoja wa wafanyabiashara wa jumla, Lucas Tarimo, alisema kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo kunatokana na viwanda vya sukari kufungwa ili kufanyiwa usafi.

Alisema sukari imeanza kuadimika na kusababisha baadhi ya wafanyabiashara rejareja kupandisha bei na kuzusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

“Mara nyingi viwanda hufungwa katika miezi hii ili kufanya usafi na hivyo kusababisha upungufu wa sukari,” alisema Tarimo.

Credit =

LEMA Alihamishia Sakata Lake la Kunyimwa Kutoa Salamu za Pole kwa Wafiwa Jana Bungeni..!!!

0
0

Wabunge wawili wa Chadema, Peter Msigwa wa Iringa Mjini na Godbless Lema wa Arusha Mjini wameomba mwongozo wa Spika kuhusu ubaguzi wa kisiasa uliotokea kwenye msiba mjini Arusha Jumatatu.

Jana Jumatatu jijini Arusha ilikuwa inaagwa  miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vincent waliopoteza maisha katika ajali ya gari.

Wa kwanza kusimana alikuwa Msigwa ambaye amehoji kama ni haki kutowapa fursa Meya wa Arusha, Calist Lazaro na Mbunge wa jimbo hilo, Lema kutoa salamu za rambirambi.

Lema kwa upande wake amesema hata magari mawili ya kubeba wagonjwa yaliyotolewa na yeye na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari yaliondolewa kwa sababu yana majina yao.

Amesema ni kwa sababu walimheshimu makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, vinginevyo mambo kama hayo huwa hayatokei mbele yao.

SAMSUNG Watangaza Kuingia Kwenye Biashara ya Kutengeneza Magari Yanayojiendesha Yenyewe..!!!

0
0

Ni mwezi mmoja umepita baada ya Kampuni ya Apple kutangaza kuwa watajikita katika utengenezaji wa magari yanayojiendesha yenyewe, tayari mshindani wake kibiashara kampuni ya Samsung nao wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo.

Samsung wamepata kibali cha kutengeneza magari hayo kutoka kwa Serikali ya Korea Kusini ambako ndiyo makao makuu ya kampuni hiyo yaliko, huku wakijinadi kuwa wamefikia uamuzi wa kutengeneza magari hayo kuendana na teknolojia.

Taarifa kutoka mtandao wa Thenextweb zimeeleza kuwa Samsung wataanza kwanza majaribio yao na Kampuni ya magari ya Hyundai na baadae kutengeneza magari yao wenyewe.

“Lengo kubwa la Kampuni yetu ni kuhakikisha dunia inakuwa salama zaidi sio tu kwa mazingira bali hata viumbe hai ndiyo maana kila kukicha tunajitahidi kuleta vitu vipya,Teknolojia hii (Magari yanayojiendesha yenyewe) itasaidia kupunguza msongamano,Kupunguza ajali na kulinda mazingira“Alisema Afisa mipango wa Kampuni ya Samsung Bw. Young Sohn.

Mwishoni mwa mwaka jana Samsung walinunua kampuni ya HARMAN inayojihusisha na utengenezaji wa vifaa vya ndani vya magari kwa Dola Bilioni 8 za kimarekani hivyo huenda ilikuwa ni njia ya kujiwekea urahisi kwa kampuni hiyo kuingia kwenye teknolojia ya magari yanayojiendesha hivyo tutarajie kuona magari ya kampuni hiyo yenye nguvu zaidi duniani.

Kwa sasa bei ya magari hayo haijatajwa, kutokana na sababu za kibiashara .

Kampuni ya Samsung itaungana na makampuni mengine makubwa Duniani kama Tesla, Apple,Google na mengine kibao kwenye ushindani wa soko la magari yanayojiendesha yenyewe.

BAADA ya Askari Nane Kuuawa Pwani..Serikali Yaanzisha Mkoa Mpya wa Kipolisi Rufiji..!!!

0
0

Serikali imetangaza kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi katika wilaya za Mkuranga, Kibiti,  Rufiji na Mafia ili kuimarisha usalama katika maeneo hayo.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amelieleza Bunge leo (Jumanne) katika hotuba yake ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2017/18.

Nchemba amesema mkoa huo utaitwa Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

Kibiti kumekuwa na matukio mbambali ya mauaji ambayo yamegharimu maisha ya baadhi ya wananchi.

Yanga yaitandika Kagera Sugar 2 - 1

0
0

Mabingwa watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans, wamerudi kileleni rasmi baada ya kuwachakaza wapinzani wao Kagera Sugar bao 2-1 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

Timu ya Yanga iliweza kujiandikia bao lake la kwanza kupitia mchezaji wake Saimoni Msuva katika dakika 38 za mchezo katika kipindi cha kwanza na kuisababisha Kagera Sugar kuanza upya mashambulizi yake na hatimaye yaliweza kuzaa matunda kwa kuweza kusawazisha bao hilo ndani ya dakika  45 (+2) za nyongeza kabla kipindi cha kwanza kuisha kwa kupitia mchezaji wake Mbaraka Yusufu. 

Mara tu timu hizo ziliporejea kutoka mapumziko, hali ya mchezo ilionekana ya tofauti kutokana timu zote zikishambuliana kwa nguvu nyingi ili kuhakikisha kupata ushindi lakini bahati ikaangukia kwa Yanga katika dakika 53 za mchezo waliweza kuona nyavu za wapinzani wao kwa mara ya pili kwa kupitia krosi matata kutoka kwa Haruna Niyonzima na kumaliziwa golini na Obrey Chirwa. 

Kwa ushindi huo timu ya Yanga kwa sasa ndiyo imekuwa inaongoza ligi kuu kwa pointi 62

Bosi wa shule ya Lucky Vincent kufikishwa mahakamani

0
0

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha ( RPC ), Charles Mkumbo amesema wanamshikilia mmiliki wa basi dogo aina ya Coaster ambayo ilipata ajali na kusababisha vifo kwa wanafunzi, walimu na dereva siku ya Jumamosi huko Karatu, Arusha. 

RPC Mkumbo amedai wanamshikilia mmiliki wa shule hiyo kwa kuruhusu gari yake hiyo kubeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wa gari 
"Siku ya tukio walikuwepo abiria 38 kwenye gari katika uchunguzi baada ya kubaini hilo tumeshachukua hatua kwa mtu aliyewezesha gari hilo kupakia hao watu, tumeshamkamata mmiliki wa gari ambaye ndiye mwenye shule hii, sasa hivi tunaendelea na uchunguzi na utakapokamilika atafikishwa mahakamani" alisema RPC wa Arusha 

Kwa mujibu wa Mkumbo anasema gari hiyo ilikuwa na kibali cha kubeba watu 30 lakini gari hiyo siku ya ajali ilikuwa na watu zaidi ya 30.

Julius Mtatiro Akana Kuvamiwa na Kufukuzwa Tanga

0
0

"Kuna taarifa zinasambazwa kuwa mimi na viongozi waandamizi wa chama eti tulivamiwa na wanachama na kufukuzwa Tanga Mjini kwenye Ziara.


Ukweli ni kuwa ziara ile ya juzi Jumapili ilizuiliwa na Polisi siku hiyo hiyo kama mwendelezo wa hujuma ambazo tunafanyiwa na Wasaliti (Lipumba na Wenzake) wakishirikiana na Vyombo vya Dola.


Mapokezi niliyopewa Tanga yalikuwa makubwa mno na tulifanikiwa kufanya kikao kimoja cha ndani (Na Kamati ya Utendaji ya Wilaya, Madiwani na Wabunge) - Wakati kikao kinaendelea magari ya Polisi yalikuja kuzingira Ofisi ya Wilaya na kututaka tusitishe kikao hicho.


Niliwasihi viongozi wakubaliane na amri hiyo ya Polisi ili kuepusha shari na mapambano yasiyo na tija wala faida kwa chama na kwa usalama wa kila mmoja.


Nje ya Ofisi ya Wilaya kulijaa mamia ya wanachama wa CUF ambao nao walitaka niwahutubie, nilishindwa kupata wasaa huo kwa sababu Polisi walisema tutekeleze amri yao.


Siku moja kabla ya mimi kufika Tanga Polisi walitoa barua ya kuruhusu ziara yangu, ila siku ya ziara yenyewe walipokea maelekezo kutoka ngazi za juu kuwa waisitishe kwa hiyo wakakabidhi barua ya sitisho muda uleule wakati vikao vikiendelea (siku ya ziara).


Na mwisho, Tanga iko shwari sana. Kijikundi cha Lipumba kimejichimbia Buguruni tu, huko mikoani kuko shwari sana na hawawezi kukanyaga wala kutisha watu. Dar Es Salaam kwenyewe kikundi hicho kina ngome kwenye maeneo machache sana ambayo pia yanazidi kumomonyoka.


Hata hivyo, kama kungekuwa na kijikundi kimekuja kutuvamia Tanga, ningeliamrisha mamia ya wanachama wa CUF waliokuwepo wakishughulikie na tayari tumeshawaelekeza wanachama wetu hasa mkoani Dar Es Salaam, wakivamiwa na vikundi vya wahuni (kwa mfano ule wa Hotel ya Vina - Mabibo) basi wajilinde kwa nguvu zote, wavidhibiti vikundi hivyo na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola."


Mtatiro J,

Zitto aibua 'ufisadi' wa Bilioni 120 Ununuzi ndege ya JPM

0
0

Nimesoma ripoti maalum ya Gazeti wiki la Jamhuri la Leo Jumanne, Mei 9, 2017 yenye kichwa cha habari 'Zitto Anyukwa' inayohusu uchunguzi wa gazeti hilo juu ya ununuzi wa ndege ya Dreamliner kutoka shirika la ndege la Beoing, ununuzi ambao binafsi kwa nafasi yangu ya ubunge unaonipa mamlaka ya kuisimamia serikali, nimeutilia mashaka na kuomba maelezo zaidi ya serikali bungeni juu ya ununuzi huo.


Nawapongeza sana Waandishi na Wahariri wa Gazeti hili Kwa kufanya uchunguzi kuhusu suala la manunuzi ya ndege Hii ya Boeing 787-8 Dreamliner. Magazeti ya habari za uchunguzi ni taasisi imara na muhimu mno katika kujenga utamaduni wa uwazi, uwajibikaji na uadilifu nchini, utamaduni ambao Chama chetu cha ACT Wazalendo kinapigania kuusimika nchini. Gazeti la Jamhuri limethubutu kufanya vile wengine wameshindwa kufanya.


Gazeti la Jamhuri limeibua masuala mawili muhimu sana katika ripoti yao hii maalum, mosi limeeleza kuwa ndege inayonunuliwa ni mpya kabisa, ambayo bei yake kwa mujibu wa taarifa rasmi za Shirika la ndege la Beoing ni Dola za Kimarekani milioni 224.6 (zaidi ya shilingi bilioni 450), pili jamhuri wameeleza kuwa pamoja na kununua ndege mpya kabisa (ambayo bei yake ni zaidi ya shilingi bilioni 450) bado tumeuziwa ndege hiyo 'mpya kabisa' kwa bei ya dola milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330).


Baada ya kusoma ripoti husika, nimepata maswali muhimu yafuatayo yanayopaswa kujibiwa na Serikali (na naamini Jamhuri watatusaidia kuyauliza):


1. Jamhuri wanasema bei ya 'ndege mpya' ambayo si 'terrible teen' (zile zenye matatizo ambazo wenzetu duniani wameuziwa kwa bei ya chini), kwa mujibu wa mkataba waliouona Kampuni ya Boeing na Serikali ni dola za Kimarekani milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330) na si dola milioni 224.6 (zaidi ya bilioni 450) inayosemwa na Serikali. Bei sahihi ya 'ndege mpya' ni ipi kati ya hizo mbili?


2. Kwa mujibu ya Randama ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mawasilisho ya Bajeti ya mwaka 2017/18, ambayo iliwasilishwa kama Taarifa ya Waziri wa Wizara husika, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Serikali ilieleza kuwa imeilipa Kampuni ya Beoing kiasi cha dola milioni 67 (zaidi ya shilingi bilioni 134) ambazo ni 30% ya bei ya dola milioni 224.6 ambayo ndiyo bei ya ndege mpya kwa mujibu wa Boeing wenyewe (na kwa mujibu wa Serikali yenyewe Bungeni). Je Serikali mpaka sasa imelipa 30% ya $224.6m ambayo ni $67 (kama ilivyosema yenyewe) au imelipa 30% ya $150m ambayo haiwezi kuwa hiyo $67m.


Binafsi nimeomba Mkataba husika kwa mujibu wa sheria na taratibu za kibunge. Tukipata tutawajulisha. Lengo letu la kuhoji ni kupata ukweli, kujiridhisha na kusimamia matumizi sahihi ya fedha na rasilimali za umma kwa mamlaka tuliyopewa nanyi wananchi.


Hatuna nia mbaya Kabisa na mchakato wa kuboresha Shirika letu la Ndege la Taifa. Uboreshaji huu ulikuwa ni msimamo wa Chama chetu kwenye ilani yetu ya uchaguzi. Tunao wajibu wa kuhakikisha unafanyika kwa usahihi.


Kabwe Z. Ruyagwa Zitto 

Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo 

Mei 9, 2017

Dodoma

Agness Masogange Ajisalimisha Kisutu

0
0

Dar es Salaam.  Msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Kabla ya Masogange kujisalimisha mahakama ilitoa hati ya kumkamata baada ya kushindwa kuhudhuria mara mbili kwenye kesi hiyo inayomkabili.


Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange  ilikuja baada ya upande wa mashtaka  kuomba mahakama  kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshtakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.


Hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata Masogange.


Hata hivyo, Masogange leo (Jumanne) amefika mahakamani hapo mapema.


Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Kumteka Mwanamke Mwenye Mapenzi ya Kweli ni Rahisi

0
0

NINA afya njema kwasababu yupo anayepigania afya na uzima wangu, lazima nikubali kuwa uwezo wa kuandika makala haya si akili wala nguvu zangu, ni Mungu mwenyewe ndiye anayesimamia haya yote. 
Hii ni sababu inayonifanya kila wakati nimshukuru Yeye, maana ni mwema na fadhili zake ni za milele. 
Ndugu zangu, ninapozungumza juu ya mapenzi ya dhati  namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Hapa mapenzi ya ulaghai hayahusiki, namaanisha mapenzi ya dhati kutoka katikati ya moyo wa mtu kwenda kwa mwingine. 
Mapenzi hayo hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye hakupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi! 
Kama ndivyo, kwanini uwe mtumwa? Msomaji wangu huna sababu ya kuingia katika uhusiano tata, ambao mwisho wa siku utaishia kulia huku wa kukubebembeza akikosekana. 
Hebu sasa tugeukie hatua muhimu nilizoandaa kwa ajili ya kukuweka sawa katika mada hii muhimu katika uhusiano wa kimapenzi. 
  
NI KWELI UMEMPENDA?
Suala la mapenzi huhusisha moyo zaidi, moyo wako ndiyo mwamuzi wa mwisho katika hilo, hata siku moja usikubali kulazimisha moyo wako kwa mtu ambaye hujaridhia. Achana na imani kwamba ukimkataa kijana fulani basi bahati inaweza kukupita, nani amekudanganya? 
Suala la kuolewa halina bahati, Mungu mwenyewe ndiye mpangaji wa hili, unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi. 
Mapenzi ni nguzo katika maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako. 
Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe. Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? 
Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini ujilazimishe? 
Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi. Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu. 
Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. 
Hii inamaana kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha! 
  
HUWEZI KUJIFUNZA KUPENDA
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. 
Hufanya hivyo akijidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa. 
Wataalamu wa uhusiano huita ndoa hizo ‘Ndoa za kichwa-kichwa’,  usikubali kuingia katika ndoa ya aina hii hata siku moja. Mwisho wa siku utajikuta ukilia. Kamwe huwezi kujifunza kupenda. 
  
MADHARA YA KULAZIMISHA PENZI
Yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndiyo msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote. 
Hayo ndiyo mapenzi ya kweli bwana, siku zote hujisikia mwepesi na huru kwa mwenzako. Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea? 
Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza kukua, kumuua aliyekufumania naye au kujiua yeye mwenyewe kukwepa fedheha. 
Hapo utauficha wapi uso wako? Fikiria kwa makini… 
  
FIKIA MAAMUZI
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaloweza kukusababisha ukajuta kuzaliwa. 
Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo. Fanya maamuzi sahihi juu ya maisha yako.

Kuvumilia Mateso Kwasababu Ya Pesa Hakukufanyi Kuwa Mke Bora Bali Kahaba Anayeteswa

0
0

Najua ni maneno makali lakini nilazima yasemwe, kuna idadi kubwa ya wanawake ambao wapo kwenye ndoa, si kwasababu ya upendo bali kwasababu ya pesa. Hilo si jambo baya kwani maisha yenyewe mafupi, umezunguka hakuna wakukuoa au yupo na haeleweki poteli ya mbali kula hela utampenda mbeleni.

Lakini kama mwanaume uliyeko naye anakupiga, anakunyanyasa anakusaliti kila si na huna furaha halafu unajidanganya kuwa ndoa ni uvumilivu, wakati hata humpendi huyo mwanaume upo naye kwasababu ya pesa zake basi hata kama una ndoa inakufanya kuw akahaba anayeteswa

Labda ili unielewe kabla ya kutoa mapovu na kunilaumu kuwa nimetukana nichambue maana ya neno “Kahaba” tafsiri hii nimeitoa kutokana na neno la kizungu Prostitute ambayo humaanisha “…a person, typically a woman, who engages in sexual activity for payment”.

Hapa wanamaanisha kuwa ni mtu (hata mwanaume anaweza kuwa kahaba) hasa mwanamke ambaye hujishughulisha na masuala ya kimapenzi kwaajili ya malipo. Kwamba unafanya mapenzi kwaajili ya pesa, hapa hawajataja idadi ya wanaume ambao unapaswa kujishughulisha nao au kama mko kwenye ndoa au la.

Kwa manaa hiyo basi kama wewe ni mwanamke umeolewa na mwanaume ambaye humpendi na unapenda pesa zake, kwa maana kuwa uko kwake kwasababu anakupa hela, anakununulia chakula mavazi na kila kitu basi wewe ni kahaba.

Hivyo hivyo kwa mwanaume kama umeoa mwanamke kwasababu ya pesa na humpendi bali unafanya mapenzi ili upate pesa zake basi wewe ni kahaba. Lakini kama nilivyosema sijambo baya, nijambo baya kama unapigwa au unayanyasika hapo ndipo unageuka na kuwa kahaba anayepigwa.

Wakati kahaba wa mtaani yeye husimama au hukutana na mwanaume wakafanya mapenzi akalipwa na kila mtu kwenda kivyake. Wewe unakua na mwanaume, anafanya mapenzi na wewe mnaendelea kuwa pamoja mkiishi kwenye nyumba moja, lakini ukimuudhi anakupiga na kwakua unahitaji hela zake unavumilia na upo tayari kuvumilia kipigo ili uishi tu kwenye nyumba nzuri.

Kuna wanawake wanaovumilia vipigo kwakuwa wanapenda, yaani hawajali hata kuhusu pesa, ingawa sikushauri kuvumilia lakini wewe hauko kwenye kundi hili. Hapa nazungumzia wale ambao wanapigwa wanakasirika lakini mume akirudi anamnunulia nguo au mkufu anamsamehe, hasamehi kwasababu anafurahia kupigwa bali kwa sababu ya ule mkufu au nguo.

Lakini kuna wale ambao anamfumania mumewe kila siku na wanawake tofauti, lakini kwakuwa anapewa pesa basi huvumilia. Huyu hana tofauti na wale wanaojiuza, kwani wanaojiuza hutembea na wanaume tofauti tofauti na kulipwa nao, lakini yeye hutembea na mwanaume mmoja ambaye ana wanawake tofauti tofauti na kulipwa na huyo mwanaume mmoja huku akiwa sawa na ametembea na wanawake wote wanaotembea na yule mwanaume.


Hapoa nikimaanisha kuwa, ingawa unatembea na mume wako tu ambaye unajua ana vimada 20 lakini kama wale vimada ishirini kila mmoja akiwa na gonjwa lake yatakusanywa kwa mumeo na utapewa yote wewe. Hii ni sawa na yule kahaba wa mtaani aliyekusanya magonjwa ya wanaume ishirini.

Najua kwamba kama uko kwenye hali hii ushaanza kutukana na kuniona nimeandika vitu vya uongo, unajipa moyo kuwa unavumilia ndoa kwakuwa mna watoto, lakini ukweli nikuwa kama humpendi huyo mwanaume na hufurahii mnapofanya mapenzi acha kuwasingizia watoto, unavumilia kwasababu ya pesa.

Kwa mwanaume kufanya mapenzi na mwanamke ambaye hakuvutii na humpendi wala si shida kwakuwa hisia zetu si za kuunga unga zipo tu. Lakini kwa mwanamke kufanya mapenzi na mwanaume ambaye anakutia kichefu chefu ni kazi yaani hata hafurahii kwakuwa hisia zao ni za kuunga unga.

Hivyo kama unavumilia kufanya mapenzi na mwanaume kwa miaka kumi ambaye humpendi kwasababu tu ya pesa, hongera, lakini kama umevumilia na kipigo, manyanyaso basi pole na amka. Acha uvivu jishughulishe na tafuta cha kwako.

Vumilia ndoa kwasababu unampenda mtu, unafurahia kuwa naye hapo hata ukimuomba Mungu atakuelewa na kukubariki, anaweza kumbadilisha. Lakini kama unavumilia kwaajili ya pesa hata Mungu harakusikiliza kwakuwa hata wewe si msafi.

Unapoomba ushauri kwa mwanamke mwenzako akakuambia kuwa ndoa ni uvumilivu hata nayeye anavumilia hembu muulize sababu za yeye kuvumilia kwake ili usije kuwa unashauriwa na mtu ambaye amekubali mwili wake kutumika kwa mapenzi na kipigo kwaajili ya pesa!

Kwamba upo na mtu ambaye anavumilia kupigwa ili aendelee kuendesha gari zuri na kuringishia mtaani. Mtu ambaye anakubali kuipigwa kwasabu ya iPhone 6, mtu ambaye anakubali kupigwa kwasababu ya Brazilian hairs. Huyo atakuwa anajipa moyo tu kuwa ni mke wa mtu lakini ukweli ni mfanyakzi wa mtu.

Huna ulemavu wowote, una akili timamu halafu bado unajiuliza “Sasa nitafanyaje…nitaenda wapi?”. Acha kumkufuru Mungu aliyekupa nguvu na akili, siku huyo mwanaume akikuambukiza magonjwa, siku akikutoboa macho, akikuvunja miguu na kuw a mlemavu ndiyo utakosa kweli pakwenda.

Lakini pia huyo mwanaume anajua uko kwake kwaajili ya pesa ndiyo maana anakufanyia anachotaka. Mwanaume akijua unampenda kweli ni rahisi kubadilika kama unamvumilia lakini akijua unapenda pesa zake hana sababu ya kubadilika kwani ashajua unachotaka hivyo atahakikisha unakuwa nacho kila wakati.

Anajua akikupiga, ukimfumania akakuletea mkufu wa dhahabu unasahau, anajua akikupiga na kukupa ada ya ndugu zako unafurahi, sasa ana sababu gani ya kubadilika zaidi ya kuendelea kutafuta pesa tu ili kukuridhisha. usidhani nayeye ni mjinga hajui nini unapenda zaidi kwake pesa au yeye?

SAKATA la Ndege: Uchambuzi na Maswali ya Zitto Juu ya Ripoti Maalumu ya Gazeti la Jamuhuri...!!!

0
0

Nimesoma ripoti maalum ya Gazeti wiki la Jamhuri la Leo Jumanne, Mei 9, 2017 yenye kichwa cha habari 'Zitto Anyukwa' inayohusu uchunguzi wa gazeti hilo juu ya ununuzi wa ndege ya Dreamliner kutoka shirika la ndege la Beoing, ununuzi ambao binafsi kwa nafasi yangu ya ubunge unaonipa mamlaka ya kuisimamia serikali, nimeutulia mashaka na kuomba maelezo zaidi ya serikali bungeni juu ya ununuzi huo.

Nawapongeza sana Waandishi na Wahariri wa Gazeti hili Kwa kufanya uchunguzi kuhusu suala la manunuzi ya ndege Hii ya Boeing 787-8 Dreamliner. Magazeti ya habari za uchunguzi ni taasisi imara na muhimu mno katika kujenga utamaduni wa uwazi, uwajibikaji na uadilifu nchini, utamaduni ambao Chama chetu cha ACT Wazalendo kinapigania kuusimika nchini. Gazeti la Jamhuri limethubutu kufanya vile wengine wameshindwa kufanya.

Gazeti la Jamhuri limeibua masuala mawili muhimu sana katika ripoti yao hii maalum, mosi limeeleza kuwa ndege inayonunuliwa ni mpya kabisa, ambayo bei yake kwa mujibu wa taarifa rasmi za Shirika la ndege la Beoing ni Dola za Kimarekani milioni 224.6 (zaidi ya shilingi bilioni 450), pili jamhuri wameeleza kuwa pamoja na kununua ndege mpya kabisa (ambayo bei yake ni zaidi ya shilingi bilioni 450) bado tumeuziwa ndege hiyo 'mpya kabisa' kwa bei ya dola milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330).

Baada ya kusoma ripoti husika, nimepata maswali muhimu yafuatayo yanayopaswa kujibiwa na Serikali (na naamini Jamhuri watatusaidia kuyauliza):

1. Jamhuri wanasema bei ya 'ndege mpya' ambayo si 'terrible teen' (zile zenye matatizo ambazo wenzetu duniani wameuziwa kwa bei ya chini), kwa mujibu wa mkataba waliouona Kampuni ya Boeing na Serikali ni dola za Kimarekani milioni 150 (zaidi ya shilingi bilioni 330) na si dola milioni 224.6 (zaidi ya bilioni 450) inayosemwa na Serikali. Bei sahihi ya 'ndege mpya' ni ipi kati ya hizo mbili?

2. Kwa mujibu ya Randama ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika mawasilisho ya Bajeti ya mwaka 2017/18, ambayo iliwasilishwa kama Taarifa ya Waziri wa Wizara husika, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Serikali ilieleza kuwa imeilipa Kampuni ya Beoing kiasi cha dola milioni 67 (zaidi ya shilingi bilioni 134) ambazo ni 30% ya bei ya dola milioni 224.6 ambayo ndiyo bei ya ndege mpya kwa mujibu wa Boeing wenyewe (na kwa mujibu wa Serikali yenyewe Bungeni). Je Serikali mpaka sasa imelipa 30% ya $224.6m ambayo ni $67 (kama ilivyosema yenyewe) au imelipa 30% ya $150m ambayo haiwezi kuwa hiyo $67m.

Binafsi nimeomba Mkataba husika kwa mujibu wa sheria na taratibu za kibunge. Tukipata tutawajulisha. Lengo letu la kuhoji ni kupata ukweli, kujiridhisha na kusimamia matumizi sahihi ya fedha na rasilimali za umma kwa mamlaka tuliyopewa nanyi wananchi.

Hatuna nia mbaya Kabisa na mchakato wa kuboresha Shirika letu la Ndege la Taifa. Uboreshaji huu ulikuwa ni msimamo wa Chama chetu kwenye ilani yetu ya uchaguzi. Tunao wajibu wa kuhakikisha unafanyika kwa usahihi.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge, Kigoma Mjini - ACT Wazalendo
Mei 9, 2017
Dodoma

114 Wakutwa na Vyeti Feki Muhimbili..!!!

0
0

Wafanyakazi 114 wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wabainika kuwa na vyeti feki na kutakiwa kufuata agizo la Rais Magufuli kuachia nafasi hizo kwani hawana sifa tena za kuendelea kuwa watumishi wa Umma

Katika taarifa aliyotolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru imesema kuwa kwa mfanyakazi yoyote ambaye hajaridhika na uamuzi huo kuhusiana uhalali wa vyeti vyao wakate rufaa kwa Katibu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi ya Umma na Utawala bora kabla au ifikapo tarehe 15 Mei, 2017.

MAREKANI Yasitisha Msaada Kenya..!!!

0
0

Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na serikali ya Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje, limesitisha ufadhili wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.

Taarifa kutoka shirika hilo limesema kuwa kusitishwa kwa misaada yote yanayohusu masuala ya wizara ya afya na ni kutokana na Kenya kutotimiza masharti ambayo waliwapatia.

Hatua hiyo ya Marekani kusitisha misaada kunatarajiwa kuathiri shughuli mbali mbali za kiserikali ikiwemo ya mapambano dhidi ya malaria, kifua kikuu na Ukimwi pamoja na miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa waja wazito na watoto.

Mnamo mwaka jana Desemba madaktari wakenye waligoma kwa siku 100, pia mkaguzi mkuu wa hesabu nchini humo alisema jumla ya dola milioni 50 hazikutumika katika wizara ya afya kama ilivyo tarajiwa.

Hata hivyo maafisa katika wizara ya afya pamoja na baadhi ya viongozi nchini humo walidaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo, lakini Wizara ya nchi hiyo ilijitetea kwa kukanusha habari hizo.

PROF Jay Awakilisha Kilio cha Wasanii Bungeni..Aichoma Mkuki wa Moyoni CCM ..!!!

0
0

Mbunge wa jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii kama makarai ya kujengea.

Prof Jay alisema hayo  Bungeni wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Habari kwa mwaka 2017/ 2018 

"Wasanii wa Tanzania wamekuwa katika mazingira magumu sana na wamekuwa katika umasikini mkubwa licha ya mara nyingi kutumiwa katika kampeni mbambali na hata katika chaguzi zilizopita mmeona jinsi wasanii walivyokuwa wakitumika, mmewatumia kama makarai na baada ya hapo mmeyaweka uvunguni, tunajua makarai huwa yanatumika kwenye kujenga maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikikamilika yanawekwa uvunguni hayatakiwa kuonekana hata kwa wageni" alisema Prof Jay 

Mbali na hilo Prof Jay amesema wasanii wengi wa Tanzania wanakuwa masikini sana sababu wakishatumika huwa hawathaminiwa tena na kuachwa mpaka wakati mwingine wa uchaguzi au kampeni 

PROF. Muhongo Aahidi Neema kwa Wachimbaji Wadogo Wadogo wa Madini..!!!

0
0

Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeahidi kutimiza ahadi ilizozitoa wakati wa kampeni kwa wachimbaji wadogo wadogo wa madini na kusema kuwa muda wa kula matunda ya kazi hiyo umewadia.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo la kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora, amesema kuwa sasa ni vyema kuhakikisha wachimbaji hao wanatoa ajira kwa wingi kwa wanachi waliopo katika eneo hilo.

Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi wakati ikiomba kura kwa wananchi kuwashika mkono wachimbaji wadogo wadogo na kwa kuwa neema hiyo sasa imepatikana hapo ni vema vijana wengi wa eneo hilo wenye nia ya kushiriki katika uchimbaji wa madini wakanufaika na ajira.

“Kila mgodi uwe na majina ya watu wanaotaka kuwaajiri na orodha hiyo ifike kwa Mkuu wa Mkoa , Maafisa wa Madini wa Kanda ikiwa imeonyesha jina la kila moja na  idadi yao, hatuwezi kuwacha vijana hawa wote bila ajira,”amesema Muhongo.

Aidha, hatua hiyo imelenga kuondoa tabia ya baadhi ya wachimbaji hao kuvamia maeneo ya wengine na hivyo kuhatarisha maisha yao naya wengine.

Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda Kati Magharibi Salim Salim amesema kuwa ili kuhakikisha maafa mengine hayatokei, kabla ya kuanza tena uchimbaji katika eneo hilo Ofisi ya Kanda kwa kushirikiana na Afisa Mkazi wa Madini wameshaanza kusimamia zoezi la kuhakikisha mashimo ya uchimbaji wa dhahabu yanakuwa  kuanzia mita 15 toka moja kwenda jingine.

WAZIRI a Magufuli Atajwa kwenye Sakata la Vyeti Feki..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 10/5/2017...!!!

WATU Watano Wafariki Dunia Mkoani Arusha Baada ya Kuangukiwa na Mti

0
0
Watu watano wamefariki dunia katika kijiji cha Ngiresi wilaya ya Arumeru mkoani Arusha  baada ya mti mkubwa kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kuanguka kwa mti huo kumetokana na athari za mvua zinazoendela kunyesha.

Amesema kuwa waliofariki dunia ni watoto watatu ambao walikuwa wanafunzi na vijana wa wiwili. Kamanda huyo amesema taarifa zaidi atatoa hapo baadae.
Viewing all 104416 articles
Browse latest View live




Latest Images