Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live

MAMBO ya Msingi Unayopaswa Kuyafahamu Kuhusu Zabibu...!!!

$
0
0

Zabibu hujulikana kama chanzo kizuri cha divai, lakini pia huweza kuliwa kama tunda na tunda hili hukuwa katika kichana chenye zabibu 6 hadi 300.

Matunda haya inaelezwa kwamba yalianza kulimwa huko nchini Uturuki, lakini kwa hapa kwetu nchini yanapatikana sana mkoani Dodoma.

Matunda haya huwa na rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza , njano, kijani na hata pinki, licha ya kwamba hapa kwetu Tanzania wengi tumezoea yale ya rangi nyeusi.

Zabibu ni moja ya tunda lenye sifa nyingi na nzuri zaidi kutokana na uwezo wake wa kuupa mwili nguvu na kuimarisha afya ya mishipa ya damu hususani ile inayosambaza damu kwenye nyama ya moyo.

Pia zabibu husaidia damu kuwa nyepesi na kuifanya isigande ndani ya mishipa ya damu, hivyo mtumiaji wa zabibu hupunguza hatari ya kupata kiharusi (stroke)

Tunda hili pia husifika kwa kutibu tatizo la upungufu wa damu, hususani kwa wale wanaotumia mara kwa mara tunda hili huwasaidia kuepukana na ugonjwa wa bawasili pia.

Hali kadhalika zabibu pia husaidia katika tiba na kinga dhidi ya magonjwa ya ini kutokana na uwezo wake wa kuliongezea ini uwezo wa kuondosha sumu mwilini na kuzalisha nyongo kwa wingi.

Mbali na faida hizo, pia zabibu kutokana na kuwa na sukari yake ya asili hivyo huweza kumsaidia mtu katika kupunguza uchovu wa mwili na kutibu maumivu yasiyokuwa na sababu za moja kwa moja.

Sambamba na hayo, juisi ya zabibu (divai) husaidia tumbo na utumbo kufanya kazi kwa ufasaha zaidi na kuzuia ukavu wa haja kubwa , lakini pia divai huimarisha afya ya mishipa ya damu katika mfumo wa kumeng’enya, kusaga na kusharabu chakula na viini lishe.

Lakini pia kutokana na madini yaliyomo ndani ya zabibu huifanya divai kuwa ni dawa nzuri inayopunguza maumivu ya tumbo yanayotokana na kujiminya kwa misuli ya kuta za matumbo (antispasmodic effect)

Hizo ndio baadhi ya faida za zabibu ambazo mtumiaji huweza kuzipata pale anapotumia tunda hili mara kwa mara.


Waziri Mwakyembe: Mitandao ya jamii ni tatizo

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amesema watumiaji wa mitandao ya kijamii Tanzania ni wengi sana hivyo mitandao hiyo kama haitadhibitiwa mapema huenda ikaleta matatizo katika nchi. 

"Watanzania ambao wapo kwenye mitandao ni mamilioni kwa sasa, lakini tunachosema tatizo hapa ni matumizi mabaya ya hiyo mitandao, mwanasiasa maarufu wa Marekani nafikiri Clinton alisema mwaka jana kuwa matumizi mabaya ya mitandao ni ugonjwa hatari unaoweza kuteketeza dunia, kwa kweli mitandao ya jamii kama hatujaiangalia vizuri au kuithibiti inaweza kutuingiza katika matatizo makubwa sana" alisisitiza  Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe

IPATE Hii Orodha ya Vinywaji & Vyakula Vitakavyoongeza Kinga Zako za Mwili..!!!

$
0
0

Mara nyingi tumekuwa tukipokea maswali kuhusu maana ya kinga ya mwili wengi wakihitaji kujua kinga hizo ni kitu gani na zinaweza kuimarishwa vipi.

Kimsingi kinga za mwili huweza kupanda au kushuka kutokana na chakula unachokula au vinywaji unavyokunywa, lakini pia hata mazingira mazima ya maisha kwa ujumla

Mwili ulibuniwa na Mungu uweze kujitibu wenyewe bila kuhitaji dawa yoyote isipokuwa mwili unaweza kupambana na matatizo kutokana na vyakula unavyokula na kunywa. Shida ni kuwa watu wengi hatujuwi tule nini kwa ajili ya nini, mara nyingi tunakula ili tushibe.

Fanya chakula kiwe ndiyo dawa zako na si dawa kuwa chakula kwako. Kinga yako inapokuwa na nguvu ya kutosha huwezi kuugua ugonjwa wowote kirahisirahisi.

Vifuatavyo ni vyakula 14 vinavyoweza kukusaidia kuongeza kinga za mwili.

Matunda
Katika mlo wako wowote jitahidi usiache kujumuisha angalau tunda la aina moja. Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, mtu asiyekula matunda ana hatari kubwa zaidi ya kupata magonjwa zaidi ya mlaji wa matunda.

Asali
Asali halisi husaidia kuimarisha pia kinga za mwili, lamba kijiko kimoja cha chakula kila siku kutwa mara tatu kwa mwezi mmoja itasaidia kuimarishakinga zako za mwili.

Juisi ya ubuyu
Pata kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku kwani juisi hiyo inawingi wa vitami C nyingi ambazo husaidia pia kuimarisha kinga za mwili.

NaziMatumizi ya nazi huweza kusaidia kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na mafuta yaitwayo ‘medium chain fatty acids’ ambayo husaidia kuimarisha kinga ya mwili na hivyo kuupa mwili uwezo wa kuyashinda maradhi mbalimbali.

Tangawizi
Ni moja ya kiungo ambacho kinaingia kwenye orodha hii ya kuimarisha kinga za mwili pia.

Mtaalam Mandai anaeleza kuwa ukiona umeshindwa kabisa unaweza kuwasiliana naye ili akupatie moja ya kirutubisho murua ambacho huweza kusaidia kuongeza kinga za mwili (kipo hapo chini kwenye picha)

Salum Mwalimu amtumia Rais Magufuli, Majaliwa na Mbowe kujinadi uchaguzi Eala

$
0
0

Mgombea wa uwakilishi wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala) kwa upande wa Chadema, Salum Mwalimu ametumia jina la Rais John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kujinadi. 

Wakati akihitimisha maombi yake ya kura baada ya kuulizwa maswali matatu na wabunge, Mwalimu amesema atakapovuka mpaka wa Tanzania kuiwakilisha katika mataifa mengine kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki endapo atachaguliwa atakuwa mwakilishi wa Taifa na si chama. 

Mwalimu amesema hata akivuka mpaka Rais ni (John) Magufuli, Waziri Mkuu ni(Kassim) Majaliwa na (Freeman) Mbowe atabaki kuwa mwenyekiti wa chama, hivyo kuwahimiza wabunge kumchagua bila kujali itikadi za chama. 

Wagombea wengine wa nafasi hiyo kwa Chadema ni Profesa Abdallah Safari, Pamela Massay,  Ezekia Wenje, Lawrence Masha  na  Josephine Lemoyan

Gwajima aununua Mgogoro wa CUF

$
0
0

"Ni rafiki yangu amenieleza masikitiko yake kuhusu  mgogoro uliokuwepo CUF nitalifanyia kazi  suala hilo nitatoa majibu" 

Ni kauli ya Mchungaji wa Kanisa Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima baada ya mazungumzo yake na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalimu Seif Sharifu Ahmadi. 

Maalimu Sief alifika Ofisini Kwa Mchungaji Gwajima saa 10 kasoro, na kuanza mazungumzo yao yaliyochukua takribani saa moja. 

walipomaliza mazungmzo hayo waandishi wa Habari walipotaka kujua undani wa mazungmoz hayo wote (Maalimu Seif na Gwajima) waligoma kueleza walichozungumza. 

Maalimu Seif amesema kuwa yeye na Gwajima ni marafiki wa muda mrefu hivyo amezungumza na rafiki yake masuala mbalimbali yanayohusu taifa.

 


  

FAHAMU Siri Nzito Iliyoko Katika French Romance(+18)...Maalumu kwa Wakubwa Tu..!!!

$
0
0

Kama unadhani busu linalohusisha ndimi na mate ni kitu kidogo na cha kawaida basi fikiria mara mbili, yamkini unatenda tendo hili lakini hujui undani wake. Mtaalam mmoja alisema “In the mating game, a kiss is more than a kiss, it is a taste test”.

Mate ya binadamu yanahusisha chembechembe “molecules” kutoka maeneo mbalimbali ya mwili wako, mara ndimi zenu zinapokutana “molecules” hizi hutuma ujumbe katika ubongo wa mwanaume na mwanamke. 

Watafiti wamegundua kwamba kuna wingi wa “bioactive testosterone” katika mate ya mwanaume kuliko kwa mwanamke, hali hii huyapa mate ya mwanaume uwezo mkubwa wa kuamsha ndani ya ubongo wa mwanamke hamu na hisia kubwa za kufanya tendo la ndoa.

KAULI ya Msanii Diamond baada ya Profesa Jay Kusimama Bungeni na Kumtetea Kuhusu Kudaiwa Kodi ya Milioni 400 na TRA

$
0
0

Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni.

Kwenye video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘

"Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika; "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"

STEVEN Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya........Rufaa Yake Itasikilizwa Leo..!!!

$
0
0

Mahakama ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Bunda leo

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne wa jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa sababu  ya makosa yaliyofanyika kwa vile Wakili wa Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya kuitwa mahakamani.

Jopo la majaji linaloongozwa na  Jaji Mbarouk Mbarouk liliahirisha usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo yasirudiwe tena kwa kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.

Warufani wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na Mawakili wa serikali, Obadia Kamea na Angela Msagala.

Wakili wa mjibu rufani wa kwanza wa Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo  mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi iahirishwe kwa muda mfupi kutokana na umuhimu wake.

Jopo hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na ombi hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.

“Inasikitisha, haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda wakati tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi tulikuwa tayari kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,” alisema Jaji Mbarouk.

Wakata rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani dhidi ya Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wakili Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani  kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa sheria za uchaguzi na kanuni.

Alidai tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana na viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha kura na taarifa ya mwisho ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.


SERIKALI Kumwaga Ajira 4,339 Za Polisi na Magereza..!!!

$
0
0

Serikali inatarajia kuajiri watumishi 4,339 katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake kwa mwaka huo wa fedha.

“Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ujumla wake, inatarajia kuwapandisha vyeo jumla ya watumishi 7,317.

“Kati yao, watumishi 105 ni wa makao makuu ya wizara, askari 5,772 wa Jeshi la Polisi na askari 1,440 wa Idara ya Uhamiaji.

“Katika mwaka huo pia, wizara inatarajia kuajiri jumla ya watumishi 4,339 ambapo katika makao makuu ya wizara wataajiriwa watumishi 26, Jeshi la Polisi wataajiriwa 2,573, Jeshi la Magereza 500, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji 600, Idara ya Uhamiaji 600 na Nida wataajiriwa watumishi 40.

“Pamoja na hayo, wizara itaendelea kuwapandisha vyeo watumishi na askari wake kadiri watakavyopata sifa kulingana na miundo yao ya kiutumishi,” alisema Nchemba.

Wakati huo huo, Nchemba alisema Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi Rufiji ili kukabiliana na uhalifu katika maeneo hayo.

“Kutokana na ongezeko la matukio makubwa ya uharifu katika Wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji, katika mwaka 2017/18, Serikali inatarajia kuanzisha mkoa mpya wa kipolisi Rufiji.

“Lengo la kufanya hivyo ni kusogeza huduma ya polisi karibu zaidi na wananchi na kurejesha amani na utulivu katika maeneo hayo. Pindi mkoa huo utakapoanzishwa, Wilaya ya Mafia nayo itakuwa ndani ya mkoa huo mpya,” alisema Nchemba.

Akizungumzia uhakiki wa silaha ambazo baadhi zimekuwa zikitumika katika uhalifu, waziri huyo alisema hadi kufikia Machi mwaka huu, asilimia 63.2 ya silaha hizo zilikuwa zimehakikiwa.

“Katika uhakiki huo jumla ya silaha 486 zilisalimishwa kutokana na kutomilikiwa kihalali. Miongoni mwa silaha hizo ni bastola 16, rifle 18, shotgun 161, SMG 24, G3 moja  pamoja na magobore 266,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Adadi Rajabu, alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo, aliitaka Serikali iimarishe ulinzi katika wilaya za mkuranga, Kibiti na Rufiji ili wananchi wa maeneo hauo waweze kuishi kwa amani.

MATOKEO ya Uchaguzi Kwa Wagombea Ubunge wa EALA, Chadema..!!!

$
0
0

Matokeo ya uchaguzi kwa wagombea nafasi za ubunge wa Afrika Mashariki EALA kutoka Chadema.
1. Profesa Abdalla Safarikura 35.
2. Wenje kura 34
3. Lawrence Masha kura 44
4. Salim Mwalimu kura 54
5. Josephine Lemoyan kura 219
6. Pamela Maasay kura 200.
Washindi waliochaguliwa na wabunge.

1. Josephine Lemoyan
2. Pamela Maasay

Wabunge: 9
Wanaume: 4
Wanawake 5

DARASSA, Mbona Umekopi na Kupesti..!!!!?

$
0
0

NIANZE kwa kutoa pole kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wa familia za wanafunzi wa Shule ya Msingi Lucky Vincent, ya jijini Arusha, ambao wamepoteza maisha yao katika ajali mbaya kabisa ya gari, iliyoua watu 36.

Huu ni msiba wa taifa zima na kwa kweli wiki hii bendera zilipaswa kupepea nusu mlingoti.

Baada ya pole hizo, sasa nirejee kwenye mada yangu ya leo, ambayo ni barua yangu kwa msanii mkubwa wa Hip Hop nchini, Shariff Thabeet, ambaye wengi tunamtambua vizuri zaidi kwa jina la Darassa.

Ingawa alianza kufanya muziki siku nyingi, lakini wengi wamekuja kutambua uwezo wake baada ya kutoa kibao ambacho kiligeuka kuwa wimbo wa taifa, Muziki.

Wimbo uliomfanya hata nchi za jirani kumpa shoo, huku Watanzania walioko ng’ambo wakiufaidi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Darassa wewe ni mkali, ila ufundi wako wa kwenye Wimbo wa Muziki ulikufanya utambulike vyema. Nimeusikiliza na kuangalia video ya kazi yako mpya, Hasara Roho, dah!

Video ni nzuri lakini mtazamo wa mashabiki wengi ni kuhusu kukopi na kupesti mtindo uleule ulioimba kwenye Muziki. Umewaangusha sana kaka.

Swali langu kwako, Darassa umekosa ubunifu, umekosa usimamizi, washauri wazuri wa biashara ya muziki au ni haraka zako za kutaka kuachia ngoma mpya?

Kila shabiki alikuwa anasubiri ujio wako mpya, kwa sababu wengi waliamini Muziki ulibahatisha, isipokuwa wachache, nikiwemo mimi, ambaye nautambua uwezo wako tangu zamani.

Wimbo huu mpya kwa kweli umekur-udisha nyuma badala ya kwenda mbele kama ambavyo tulitegemea, yaani ulichofanya ni kuondoa maneno ya Muziki na kuweka ya Hasara Roho.

Kama msanii mkubwa, nilitegemea ungekuja na kitu tofauti kabisa, ambacho kingedh-ihirisha kuwa wewe ni mkali, lakini kitendo cha kukopi na kupesti, kimeonyesha udhaifu mkubwa.

Binafsi nilikutahadharisha kupitia ukurasa wangu wa Instagram kuwa baada ya Wimbo wa Muziki, ulikuwa na kibarua kikubwa sana cha kufanya wimbo mkali na mkubwa kuliko huo ili uendelea kusimama kwenye gemu, lakini pia kupanda levo za kimataifa.

Nilisema hivyo kwa sababu suala siyo kuimba, ishu ni kuimba vizuri na kuweza kusimama sehemu ulipo. Hata kama angekuwa ni msanii mwingine, kile nilichokisema kwako ndicho ningemwambia.

Darassa ulipaswa kuwa na muda mzuri wa kutafakari nini Watanzania wanakihitaji baada ya Muziki, ilikuwa ni muda wa kufanya utafiti ni wimbo wa mtindo upi ukiutoa utaweza kukuvusha hapo ulipo na kuufikisha muziki wako kimataifa.

Nilichojifunza wasanii wetu wana pupa, mna haraka ya kutaka kuonekana mmeachia kazi mpya mara kwa mara bila kuangalia nini kitafuata kwenye kazi hiyo kama haitafanya vizuri au lah.

Nimeamua kukuambia kwa sababu mimi pia nawasilisha maoni na ushauri wa mashabiki wako ambao hawawezi kukufikia kwa njia ya barua. Lakini pia nimeandika ujumbe huu ili kukukumbusha kuwa kila kitu ni mipango ya muda mfupi na mrefu.

KITWANGA Aitwanga Serikali Bungeni..Habari Vichwa vya Magazeti ya Leo 11/5/2017..!!!

Mwalimu Mkuu wa Lucky Vincent Afunguka Mazito Kuhusu Safari Iliyoua Wanafunzi

$
0
0

MWALIMU Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi ya mchepuo wa Kiingereza ya Lucky Vincent ya jijini Arusha, Loningo Vincent amesema kabla ya kuanza safari ya kwenda Karatu ambayo iliibua ajali iliyoua wanafunzi 33, walimu wawili na dereva, alitafakari kwa saa mbili waende huko au Njiro jijini humo kwa ajili ya mtihani wa kujipima. 

Wanafunzi hao 33, walimu wao wawili na dereva walikufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Mitsubishi Rosa kupinduka na kutumbukia korongoni eneo la Mlima Rhotia Marera wilayani Karatu wakati wakienda katika mtihani wa ujirani mwema wa kujipima na wenzao wa Tumaini Junior. 

Akizungumza wakati wa maziko ya mwanafunzi Irene Godson jana, Mwalimu Vincent aliomba samahani kwa wazazi na walezi kutokana na ajali iliyotokea ambayo si tu imeacha simanzi kubwa kwa familia husika, bali Taifa kwa ujumla. 

Alisema kabla ya kuondoka shuleni hapo, alitafakari sana ndani ya saa mbili watoto hao waende Njiro jijini Arusha au Karatu kufanya mtihani wao wa kujipima. “Kabla ya watoto hawa kuondoka, nilitafakari saa mbili kama waende Karatu au Njiro hapa hapa mjini, lakini sikuwa najua kama wanakwenda kufa, wazazi mtusamehe maana hakuna aliyejua mbele kuna nini kitatokea,” alisema Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Lucky Vincent. 

“Naomba nikabidhi kitabu hiki cha nyimbo za dini ambacho Irene alikuwa nacho kwenye begi Lake na walipopata ajali Irene alijitaja mara tatu kwa jina lake Irene, Irene, Irene. Kweli alikuwa akipenda sana dini kwa sababu pia ndani ya begi lake alikuwa na mafuta ya mzeituni yaliyowamwagikia wenzake wakati kila mmoja akiwa kwenye harakati za kujiokoa,” aliongeza mwalimu huyo. 

Awali kabla ya kuanza ibada, Mwalimu Vincent alikabidhi Biblia kwa wazazi kwani Irene alikuwa ni mcha Mungu na kila mara alikuwa na Biblia yake na hata eneo la ajali, walimu waliokota biblia hiyo. 

“Irene alikuwa ni mcha Mungu na sehemu aliyopata ajali alikuwa na Biblia yake na alikuwa akimtumaini mungu kwa kila jambo, hivyo kama walimu tunaikabidhi Biblia hii kwa familia yake,” alieleza mwalimu huyo. 

Mamia ya watu walijitokeza nyumbani kwa wafiwa Kwamrombo Murriet kwa ajili ya kumuaga Irene ambaye mwili wake ulipowasili nyumbani kwa bibi na babu yake saa 6.15 mchana vilio, huzuni na simanzi vilitawala, huku bibi yake akilia zaidi kutokana na jinsi alivyokaa naye tangu akiwa na miaka miwili hadi juzi mauti ilipomfika. 

Akiongoza Ibada ya mazishi, Mchungaji kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Asisisa Moshi kutoka Ushirika wa Olkerian alitoa pole kwa familia. Naye Askofu Solomon Masangwa wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini alitoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliokumbwa na msiba huo na kuwasihi wazazi kumwachia Mungu kwani hayo ni mapenzi yake Irene alizaliwa Mei 5, 2004, alisoma Shule ya Lucky Vincent na alipata ajali Mei 6, 2017 eneo la Rothia. 

Juzi miili ya watoto hao iliagwa kwa pamoja huku mengine ikisafirishwa na mengine ikienda kuzikwa maeneo mbalimbali ya Jiji la Arusha, ambapo Hospitali ya Selian miili iliyobaki ikisubiri taratibu za mazishi ikiwa ni miwili ambayo ni mwili wa Iyan Tarimo na Irene Kishari. 

Mjini Dodoma, Mwandishi Wetu, Maulid Ahmed anaripoti kuwa Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi nchi nzima kuanzia sasa kukagua magari yote yanayosomeka kuwa ni ya wanafunzi. Sambamba na hilo, Polisi wamegizwa kukagua madereva wote wanaoendesha magari ya wanafunzi kuhakikisha magari hayo ni salama ili kuwalinda watoto. 

Akijibu hoja za wabunge, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni alisema serikali imechukua uamuzi huo kutokana na ajali iliyotokea Arusha na kuua wanafunzi wasio na hatia. 

PROF Jay - Simba Waachieni Ubingwa Yanga .. Jipangeni na Kombe la Shirikisho Tu..!!!

$
0
0

Legendari wa Muziki wa kizazi kipya nchini na Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule , “Professa Jay” ameitaka timu yake ya Simba kuweka nguvu zaidi katika fainali ya kombe la shirikisho kuliku kombe la ligi.

Simba SC ipo katika nafasi ya pili katika ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa na alama 62 sawa na klabu ya Yanga inayoongoza kwa tofauti ya Mabao, pia ikiwa na michezo mitatu mkononi.

Professa Jay licha ya kuiombea timu yake kutwaa Ubingwa wa ligi kuu, amesema Simba ina nafasi ya kuutwaa Ubingwa wa kombe la shirikisho watakapocheza fainali dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja Wa Jamhuri mjini Dodoma  May  28.

Professa Jay ambaye ni Mbunge wa Chadema kupitia jimbo la Mikumi, alisema ubingwa wa Ligi Kuu kwa Simba utatagemeana na mechi za Yanga, kama watashinda mechi zao 3 zilizobaki watajihakikishia ubingwa huo tofauti na Simba yenye mechi mbili itakuwa ni kazi bure hivyo ni vyema zaidi kujipanga kwa fainali ya FA.

Furaha yangu ni kuona Simba Sc inachukua ubingwa wa ligi kuu bara na ubingwa wa shirikisho, kutokana na ubora wa kikosi cha timu yetu hivyo tutashinda mechi zilizobaki na kutwaa ubingwa, japo imani yangu kubwa zaidi ipo kwenye kombe la shirikisho. “alisema Professa Jay”.

GWAJIMA Apanga Kuanika Madudu ya Lipumba Cuf..Maalim Seif Amoa Ubuyu Wote Kuhusu Yaliyotokea..!!!

$
0
0

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima amemuweka kiporo Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba na kuhoji kwa nini mwenyekiti huyo anaruhusiwa kukivuruga chama hicho.

Askofu Gwajima ameyahoji hayo baada ya kupokea malalamiko ya mgogoro uliopo ndani ya CUF kutoka kwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad alipokwenda kumtembelea ofisini kwake, leo Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Katika mazungumzo yetu nilitaka kujua Lipumba anafanyaje kuvuruga chama chako ili nami nijue cha kufanya, si unajua tena. Kwa nini unamruhusu kukivuruga chama?” amehoji Gwajima.

Baada ya kuhoji hayo, Gwajima amesema atayatafakari mazungumzo hayo na kwamba baada ya kutafakari atajua cha kufanya sambamba na kuueleza umma kile atakacho kuwa nacho.

“Kwa vile ameniambia mgogoro jinsi ulivyo basi nami najua cha kufanya, na nitakacho kuwa nacho nitasema baadae, ngoja nitafakari kwanza,” amesema.

'Mimi huyu ni rafiki yangu kwa hiyo nilitaka kujua Professa Lipumba anafanya nini kuvuruga CUF, hivyo nilitaka kujua Lipumba amepatwa na nini mpaka amevuruga chama chako na kiukweli mimi nilikuwa siufahamu vizuri huu mgogoro ila saizi Seif ameniambia kwa hiyo na mimi nataka nitafakari alichoniambia rafiki yangu ni 'digest' baada ya hapo nitajua nafanya nini" alisema Gwajima

Nilikuwa siufahamu vizuri mgogoro wa CUF ila sasa Seif ameniambia. Natafakari alichoniambia ni 'digest' halafu nitajua nafanya nini - Gwajima

Kwa upande wake Maalim Seif ambaye alizuru kwa Gwajima kwa ajili ya kumjulia hali na kuzungumza naye masuala mbalimbali ya nchi, amesema anamuunga mkono mchungaji huyo kwa chochote atakacho kufanya.

“Namuunga mkono aliyoyasema, sisi ni marafiki wa muda mrefu nimekuja kumjulia hali na kuzungumza naye mambo mbalimbali na kila mmoja kayaeleza yake,” amesema Maalim Seif.


HAJI Manara Aibukia Facebook, Aitaka TCRA Kumshughulikia Shabiki Wa Yanga..!!!

$
0
0

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara ameiomba mamamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA, imchukulie hatua shabiki wa Young Africans, Pascal Lameck aliyeposti kwenye mtandao wa kijamii wa facebook taarifa ya uongo kuwa basi la wachezaji wa Simba limepata ajali na wachezaji wote wamevunjika mguu, huku kocha wao, Joseph Omog akiwa hajulikani alipo.

Kupitia posti aliyoitoa kwenye mtandao wa facebook, Manara amehoji uhalali wa shabiki huyo kuendelea kuwepo uraiani akitazamwa bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria na mamlaka ya mawasiliano ya TCRA.

“Always huwa najiuliza mashabiki wa aina hii tunawaacha kwa nini?  Na TCRA ichukue hatua, tusingoje hadi watukanwe wakubwa tu, hatuwezi kusamehe kila kitu,” ameandika Manara kwenye posti yake aliyoiambatanisha na posti ya shabiki huyo.

WATOTO Watatu Waliobaki Katika Ajali ya Gari la Shule ya Luck Vicent ya Arusha Kupelekwa Marekani kwa Matibabu..!!!

$
0
0

Jopo la madaktari bingwa wa Shirika la Stemm la Marekani kwa kushirikiana na Serikali, limeamua kuwapeleka  Marekani kwa matibabu majeruhi watatu  wa ajali ya wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva.

Majeruhi hao ambao wamelazwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru ni Jofrey Tarimo, Doreen Mshana na Sadia Awadh wanatarajiwa kusafirishwa kwenda Marekani wakiambatana na wazazi wao,  daktari na muuguzi wa hospitali ya mkoa wa Arusha.

Matibabu hayo  yatatolewa kwa  ufadhili wa madaktari hao kutoka Marekani ambao walikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuwasidia wanafunzi hao kutoka kwenye gari lililo pata ajali, wakiwa njiani kuelekea Ngorongoro na Serengeti kutalii.

Daktari mkuu wa hospitali Mount Meru,  Wonanji  Thimos  amesema kuwa Serikali kwa kushirikiana na madaktari hao imeshaanza taratibu za kuwasafirisha majeruhi hao kwa ajili ya matibabu zaidi.

Dk Thimos amesema taratibu za safari zikikamilika majeruhi hao watasafirishwa kwenda Marekani wakati wowote kuanzia sasa.

HIVI Ndivyo Magufuli Anavyong'aa Ulaya..Wazungu Wamwagia Misifa Kedekede..!!!!

$
0
0

Nimekaa Mahali Fulani Hapa Mtaa wa Poznańska Street Katika Mji wa Warsaw Poland, Yani Wazungu Fulani Nikawaskia Wanazungumzia Tanzania Kwamba Hivi Sasa Ina Rais Mzuri Ambaye Anasimamia Vizuri Uwajibikaji Katika Masuala ya Fedha za Umma na Kuanzisha Elimu Bure. 

Nikapata Hamu ya Kuwasogelea na Kuwauliza Iweje Wanaizungumzia Tanzania Hivyo, Wanaijua? Nikajibiwa Kwamba Wao (wako 9 wamekaa meza moja) wana kikundi chao walifika TZ mwezi April kwa ajili ya utalii na kwamba walipata fursa ya kuitembelea TZ na pia kutengeneza urafiki na baadhi ya watu na kwamba walifurahi kuona TZ inapiga hatua. 

Kumbuka hawa hawakutembelea TZ nzima ila wanasema walienda Zenji, Kilimanjaro, Arusha na Serengeti. Kiukweli wanaisifu sana Tanzania pamoja na Rais JPM. Nimefurahi kuona Nchi yangu inazungumzwa vizuri na baadhi ya watu hapa Poland.


KAULI ya Msanii Diamond Baada ya Profesa Jay Kusimama Bungeni na Kumtetea Kuhusu Kudaiwa Kodi ya Milioni 400 na TRA

$
0
0

Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni.

Kwenye video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘

"Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu"

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika;
 "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"

STEVEN Wasira Arudi Kortini Kumng’ang’ania Bulaya........Rufaa Yake Itasikilizwa Kesho

$
0
0
Mahakama ya Rufaa Tanzania imepanga kusikiliza rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Bunda kesho.

Mahakama hiyo ilitoa uamuzi huo jana katika rufaa iliyokatwa na wapigakura wanne wa jimbo hilo baada jopo la majaji watatu kukwama kuanza kusikiliza kwa sababu  ya makosa yaliyofanyika kwa vile Wakili wa Mbunge wa Jimbo hilo, Ester Bulaya, Tundu Lissu hakuipata notisi ya kuitwa mahakamani.

Jopo la majaji linaloongozwa na  Jaji Mbarouk Mbarouk liliahirisha usikilizwaji huo hadi kesho na kuamuru makosa hayo yasirudiwe tena kwa kuwa yamewapotezea muda na wana mambo mengi ya kufanya.

Warufani wanawakilishwa na mawakili Yassin Member na Constantine Mutalemwa huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiwakilishwa na Mawakili wa serikali, Obadia Kamea na Angela Msagala.

Wakili wa mjibu rufani wa kwanza wa Bulaya, Lissu hakuwapo mahakamani hivyo  mawakili wa wakata rufaa waliomba kesi iahirishwe kwa muda mfupi kutokana na umuhimu wake.

Jopo hilo, Jaji Mbarouk, Augustino Mwarija na Rehema Mkuye, lilikubaliana na ombi hilo, hivyo kuamua kuahirisha usikilizwaji huo hadi kesho.

“Inasikitisha, haipendezi mnaopeleka notisi muwe makini kwa sababu mnatupotezea muda wakati tuna mambo mengi ya kufanya, hili kosa lisijirudie tena, sisi tulikuwa tayari kusikiliza na tulipanga kesi moja tu,” alisema Jaji Mbarouk.

Wakata rufaa katika kesi hiyo ya uchaguzi Jimbo la Bunda ni Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na Ascetic Malagila ambao walikata rufani dhidi ya Bulaya, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Wakili Mutalemwa alitaja sababu za kukata rufani  kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki kutokana na ukiukwaji wa wazi wa sheria za uchaguzi na kanuni.

Alidai tafsiri isiyo sahihi ya kanuni za uendeshaji kesi za uchaguzi kuhusiana na viapo na kutofuatwa kwa taratibu za uchaguzi kwa kutomtaarifu mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mahali na tarehe ya kujumuisha kura na taarifa ya mwisho ya matokeo kuwa na idadi kubwa ya waliojiandikisha kupiga kura tofauti na Tume ya Uchaguzi ya Taifa.
Viewing all 104698 articles
Browse latest View live




Latest Images