Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live

BREAKING: ACT- Wazalendo wamtangaza Mrithi wa Kitila Mkumbo

$
0
0

Chama Cha ACT- Wazalendo kimemtangaza rasmi Mwanasheria Albert Msando kuwa mrithi wa Nafasi ya Mshauri Mkuu wa Chama hicho iliyoachwa awazi na Prof Kitila Mkumbo aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji 

Kwa Mujibu wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Doroth  Semu, Utuezi huo umeanza Mara tangu Mei 8, 2017. 

Kabla ya uteuzi huo ndani ya Chama hcho Msando alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria.

LEMA Afunguka Makubwa Kuhusu Unyanyasaji Unaofanyika Huko Magerezani..

$
0
0

Kambi ya rasmi ya upinzani bungeni imeitaka serikali kuhakikisha inalionya Jeshi la Magereza kuacha mara moja vitendo vya udhalilishaji kwa wafungwa unaofanywa na maaskari wakati wa ukaguzi pindi watuhumiwa wanapotoka mahakani.

Akisoma hotuba ya upinzani Waziri kivuli wa Mambo ya nje, Mh. Godbless Lema amesema kuwa ukosefu wa vifaa vya kisasa ndio chanzo cha udhalilishaji hivyo hali inayowafanya wafungwa kuvuliwa nguo hadharani na kukaguliwa kipindi wanapotoka mahakamani kitu ambacho ni udhalilishaji wa wa kibinadamu. "Wafungwa na mahabusu kuvuliwa nguo siyo vitendo vya kibinadamu ni utekelezaji wa mikakati ya kishetani. Kitendo hiki ni utekelezaji wa mikakati ya kishetani wazee na vijana kuvuliwa nguo na kukusanywa uchi na kukaguliwa hadharani, hata askari wanaofanya hivyo husababishiwa na huzuni bila sababu. Serikali inapaswa kununua vifaa vya ukaguzi maalumu ambavyo ni vya kisasa na haviwezi kuvunja utu. lakini pia kuna unyanyasaji ambao unatekelezwa na askari na kanuni mbovu za uendeshaji wa majeshi ya magereza"- Lema alifunguka.
Aidha katika hotuba hiyo iliyosomwa na Lema imeitaka serikali itimize vyema sheria ya Parole na kuwaachia huru wafungwa waliokaa magereza muda mrefu waachiliwe kwani hawawezi tena kufanya uhalifu. "Serikali iwaachie huru wafungwa waliokaa muda mrefu magereza wanautamani sana uhuru. ni vyema serikali ikaangalia jinsi ya kuwapa uhuru na kuachana na wale wafungwa wa vifungo vya muda mfupi. Kama mtu ana miaka 65 amekaa magereza miaka 25 akiachiliwa hawezi kwenda kufanya uhalifu tena. tunaiomba serikali iweze kuwaachia wafungwa wote waliofungwa toka awamu ya Nyerere mpaka awamu ya nne ya Mh. Kikwete kwa kuzingatia sheria ya Parole"- aliongeza Lema.
.
JE UNAMUUNGA MKONO LEMA AU UNAMPINGA????.

HIVI Ndivyo Utofauti Ulipo Kati Ya Mwanaume na Mwanamke Katika Hisia Za Kimapenzi

$
0
0

Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia inasadikika hakuna kitu ambacho kina nguvu sana kama mahusiano ya mapenzi, hata hivyo kutokana na nguvu hiyo ya mahusino, watu wengi hufikiri mwanaume ndio ambao wanaathiriwa kwa kiwango kikubwa na nguvu hiyo.

Watafiti wa masuala ya mahusiano wanazidi kusema ya kwamba, mwanaume kila baada ya dakika tano ni lazima awaze masuala ya kimapenzi, hii ni kutokana wanaume wengi hupenda zaidi jinsia ya kike kwa kuona kwa macho. Ndio maana ukichunguza kwa makini wanaume huwa wanakuwa wanazingatia zaidi katika kutazama jinsia hii ya kike mahali popote walipo.

Hivi hujawahi ona wanaume wamekaa mahali wanapiga stori ghafla akapite mwanamke mzuri mbele ya macho yao ghafla stori zile zikasimama kwa muda? Bila shaka umewahi kuona. Utawasikia wakisema kwa minong'ono aaah angalia kifaa hicho, wapo wengine utawasikia wakisema mcheki chura huyo. Hii ina maana ya kwamba macho ya mwanaume ndio chanzo kikubwa cha kuingia katika mahusiano kabla ya kumjua tabia aliyonayo mtu huyo.

Lakini ukweli ambao upo nyuma ya pazia ni kwamba wanaume wengi  huingia katika matamanio ya kimahusiono kwa kuona kwa macho zaidi tofauti na mwanamke. Hata hivyo mahusiano ya kimapenzi aliyonayo mwanaume ni matokeo ya macho yako. Kwa maneno mengine tunaweza kusema matamanio ya hisia za mwanaume yapo katika kuona zaidi kuliko kitu chochote.

Lakini ukienda upande wa pili wa shilingi, mwanamke huwa yupo tofauti sana ukilinganisha na mwanaume katika suala zima la kuingia katika mahusiano. Hisia za mwanamke huwa zipo zaidi katika maneno na mguso katoka kwa mwanaume. Hisia za mwanamke huwa hazipo katika kuona kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na mwanaume.

Mwanamke huamini sana katika maneno ambayo ataambiwa na mwanaume,  kwa mfano mwanamke akiambiwa anapendwa zaidi ya kitu chochote katika dunia hii mwanamke huamini hivyo,hivyo maneno ya mwanaume yana nafasi kubwa katika kuziteka hisia za mwanamke.

Lakini pia kama hiyo haitoshi mwanamke hupata hisia zaidi pale anapoguswa na mwanaume, hivyo ndio maana kama utakutana na msichana kwa mara ya kwanza ataka usimguse katika mwili wake, hii ina maana mguso wa mwanaume una nguvu sana katika kuamsha hisia mwili wa mwanamke.

Hivyo kama ndivyo hivyo basi hii ni utofauti mkubwa ulipo kati ya mwanaume na mwanamke katika kuamsha hisia za kimapenzi. Na kitu kikubwa ambacho huongoza hamasa na kudumu katika mahusiona ya kimapenzi ni "mawasiliano", mawasiliano ndiyo chachu kubwa katika mahusiano yenu. Hivyo kila wakati ili muweze kudumu katika mahusiano yenu hakikisha unakuwa na mawasilino bora kati yako na mwenzi wako.

Wachungaji 10 Matajiri Zaidi Duniani (Hawa Hapa)

$
0
0

Hii ndio top 10 ya Wachungaji (Watumishi wa Mungu) wenye utajiri mkubwa zaidi Duniani, ripoti hii ni ya mwaka 2016. 

1. Bishop David Oyedepo Net Worth 2016 – $150 Million (Nigeria) 

2. Bishop T.D. Jakes Net Worth 2016 – $147 Million (America) 

3. Chris Oyakhilome Net Worth 2016 – $50 Million (Nigeria) 

4. Benny Hinn Net Worth 2016 – $42 Million (America) 

5. E. A .Adeboye Net Worth 2016 – $39 Million (Nigeria) 

6. Creflo Dollar Net Worth 2016 – $27 Million (America) 

7. Kenneth Copeland Net Worth 2016 – $25 Million (America) 

8. Billy Graham Net Worth 2016 – $25 Million (America) 

 9. T.B. Joshua Net Worth 2016 – $10 Million (Nigeria) 

10. Joseph Prince Net Worth 2016 – $5 Million (Singapore) 

SERIKALI Yaeleza Hali Ya Sukari Nchini Kuelekea Mwezi Wa Mtukufu Wa Ramadhan..!!!

$
0
0

Serikali imesema kuwa iko macho kuhusiana na suala la sukari nchini na inafanya jitihada zote ili kupata mahitaji yote wakati mwezi Mtukufu wa Ramadhan ukikaribia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hayo Bungeni Mjini Dodoma na kudai kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 ambapo kwa hapa nchini tani 320,000 zinazalishwa na hivyo mwaka huu imeagiza sukari tani 80,000 na tayari tani 35,000 zimeshaingia nchini.

Majaliwa amewataka Watanzania kushirikiana katika kuwasihi wafanyabiashara kushusha bei ya sukari ambayo wameipandisha hivi sasa.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge, Jakuh Hashim Ayoub aliyemuuliza kuhusu mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kwamba kuna tatizo la sukari huku wananchi wakihiwa na uhitaji na kwamba hivi asa zipo tani 100,000 tu za sukari.

Mhe. Ayoub amesema kuwa sukari iliyoagizwa kwa watu waliopewa vibali vya sukari itakuwa imekwisha wakati mwezi mtukufu wa Ramadhan utakapoanza.

KIMENUKAA..Mbowe Aibua Upya Sakata la Escrow Bungeni..Amswalika Maswali Magumu Waziri Mkuu..!!!

$
0
0

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amemuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhusu kutokutekelezwa maazimio ya Bunge ikiwemo Escrow, Tokomeza na mabilioni ya Uswiss.

Akijibu swali hilo Majaliwa alimuhakikishia Mbowe kuwa Serikali inaheshimu muhimili wa Bunge na kuthamini maamuzi yake.

Amesema kunahitajika uchunguzi wa kina na yapo ambayo yana umuhimu wa kuletwa bungeni hivyo uchunguzi wa Serikali utakapokamilika yatawasilishwa bungeni.

KITWANGA Aibuka na Jipya Bungeni..Adai Atawahamasisha Watu wa Jimbo Lake Kuharibu Mitambo ya Maji..!!!

$
0
0

MBUNGE wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM), amewapiga mkwara mawaziri bungeni kuwa atahamasisha wananchi wa jimbo lake kwenda kuzima mtambo wa maji ulioko Ziwa Victoria.


Kitwanga ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa kwanza katika serikali ya awamu ya tano, alilieleza Bunge jana kuwa mtambo huo upo kwenye chanzo cha maji cha Iherere, kilichoko jimboni kwake Misungwi mkoani Mwanza.

Katika mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji bungeni mjini hapa jana mchana, mbunge huyo aliyekuwa wa kwanza kupewa nafasi ya kuchangia, alitoa onyo hilo kwa Waziri Gerson Lwenge na msaidizi wake, Mhandisi Isack Kamwele, kwamba yuko mbioni kuuzima mtambo huo ikiwa wananchi wake hawatakuwa sehemu ya mradi huo wa maji.

“Mheshimiwa Naibu Spika, jimboni kwangu hakuna maji ya uhakika na tangu mwaka 2008 wananchi wamekuwa wakiyasubiri bila mafanikio," Kitwanga alisema.

“Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii, sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose.

“Wanamchi wa Misungwi hawana maji na katika bajeti yenu leo (jana) mmesema Nyang’omango kuna maji wakati hakuna, sasa nawaambia, sitatoa shilingi 'nita-mobilize' (nitahamasisha) wananchi tukazime ule mtambo.

“World Bank' (Benki ya Dunia) walifika pale kijijini, wakasema hawa wananchi walioko kwenye kile chanzo wanatakiwa kupata maji, lakini nyie hamuoni, hivi nyie mkoje?

“Nakipenda chama changu (CCM), nampenda Rais wangu (John) Magufuli, lakini lazima tutendeane haki kwa sababu hii nchi ni yetu sote.

“Hamuwezi kupeleka maji sehemu nyingine kwa gharama ya Sh. bilioni 600 halafu mkashindwa kuwapa wananchi wangu hata mradi wa Sh. bilioni 10.

“Mshukuru kwamba nilipokuwa waziri, nilikuwa siwezi kusema kitu, lakini sasa nimetoka, tutapambana kwa sababu lazima tuwe na mipango mizuri ya kuwapelekea wananchi wetu maji kama inavyofanyika katika umeme kupitia REA (Wakala wa Umeme Vijijini).”

Kitwanga alitumbuliwa na Rais Magufuli Mei 20, mwaka jana kwa tuhuma za kuingia bungeni na kujibu swali linalohusu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Kitwanga pia alilalamikia kile alichokiita tabia ya baadhi ya viongozi wa wizara hiyo kukwamisha upatikanaji wa maji kupitia kwa marafiki zake kutoka nchini Austria.

“Rais alipokuja Misungwi, aliwaambia wananchi, kwamba nina marafiki zangu huko nje wanaoweza kunisaidia kupata maji," alisema. "Ule mradi ulipokuja, nikawekewa figisu wakasema mimi nina 'interest' (maslahi) nao.

"Ni kweli nina 'interest' nao kwa sababu wananchi wangu wa Kolomije wanahitaji maji, wananchi wa Bukumbi wanahitaji maji.

“Kwa hiyo, Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena, safari hii sitatoa shilingi, nitakwenda kuwahamasisha wananchi wangu tukazime ule mtambo wa maji ili wote tukose,” alisisiza Kitwanga.

Hata hivyo, muda mfupi kabla ya kusitisha shughuli za Bunge jana mchana, Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, alimtahadharisha Kitwanga kuwa, uamuzi wake huo huenda ukamsababishia matatizo kwa kuwa unakiuka sheria za nchi.

Dk. Tulia alisema kuwahamasisha wananchi ili wavunje sheria ni kosa la jinai, hivyo mbunge huyo anapaswa kuwa makini kwa kuwa anaweza kuchukuliwa hatua kabla hata hajawahamasisha wananchi wa maeneo ya Kolomije na jimbo zima la Misungwi.

BAJETI ISIPITE

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), ambaye alikuwa wa pili kuchangia mjadala huo baada ya Kitwanga, aliwashauri wabunge washirikiane kuhakikisha wanaikwamisha bajeti hiyo ili ikaandaliwe upya.

Zitto ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo, alisema bajeti hiyo haipaswi kupitishwa na Bunge ili serikali ikaiandae upya kwa kuwekwa mipango imara ya kukabiliana na uhaba wa maji nchini.

Alisema bajeti iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri Lwenge haina mambo mapya na kwamba haioneshi nia ya kutatua kero ya maji ambayo yamekuwa yakiwasumbua wananchi kwa miaka mingi.

“Rais alipokuja hapa bungeni, alieleza jinsi serikali yake ilivyojipanga kuwatua kina mama ndoo kichwani. Pia tumekuwa tukiona jinsi Makamu wa Rais (Samia Suluhu Hassan) ambavyo amekuwa akizunguka nchini kuhakikisha anawatua ndoo kichwani kina mama," alisema.

"Pamoja na jitihada hizo, nimeshangaa kuona katika bajeti ya waziri, fedha za maendeleo zimepungua kutoka Sh. bilioni 915 za mwaka uliopita hadi kufikia Sh. bilioni 623.

“Kwa hiyo, waheshimiwa wabunge, njia pekee ya kuifanya serikali iwe na mikakati ya kutatua kero ya maji, ni sisi hapa kuungana kwa kuikataa bajeti hii ili ikaandaliwe upya na kuja na majibu ya kutatua kero ya maji.

“Kama wewe mbunge una kero ya maji kijijini kwako, wilayani kwako, jimboni kwako na mkoani kwako, tuikatae bajeti hii ikaandaliwe upya iletwe nyingine."

Katika Bunge la Bajeti mwaka jana, bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji iliibua mjadala mkali baada ya wabunge karibu wote kuitaka serikali kuongeza fungu la Mfuko wa Maji.

Utekelezaji wake hata hivyo umefanyika kwa asilimia 19.8 tu ya Sh. bilioni 915 hizo hadi Machi mwaka huu.

GWAJIMA na Wasidizi Wake Kuhukumiwa Mwezi wa Saba..!!!

$
0
0

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wasaidizi wake watatu wanaotuhumiwa kushindwa kuhifadhi silaha na risasi wanatarajiwa kuhukumiwa Julai 31, mwaka huu.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, baada ya jana wakili wa utetezi, Peter Kibatala kueleza kuwa wamefunga ushahidi wao wa mashahidi sita.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mkeha alisema  anaahirisha kesi hiyo hadi Julai 31, mwaka huu kwa ajili ya kusoma hukumu.

Katika kesi hiyo, upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali, Shedrack Kimaro na Joseph Maugo.

WALIMU Mbaroni kwa Kuvujisha Mtihani Kidato cha Sita ..!!!

$
0
0

JESHI Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, linawashikilia walimu wawili na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Chang'ombe (Mazoezi) kwa tuhuma za kukutwa na mtihani wa Kemia wa kidato cha sita. Mitihani hiyo inaendelea kufanyika nchini.


Kamishna wa Kanda hiyo, Simon Sirro, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Musa Elius na Innocent Murutu ambao ni walimu wa shule hiyo. Mwanafunzi ni Ritha Mosha.

Kamishna Sirro alisema wiki iliyopita saa 1:00 usiku Jeshi la Polisi lilipokea taarifa kutoka kwa Ofisa wa Baraza la Mitihani, Aron Mweteni, aliyesema alimkuta kwenye shule hiyo mwalimu Elius na mtahiniwa Ritha wakiwa na karatasi yenye maswali na majibu ya somo la vitendo la kemia.

Alisema baada ya kuwatilia shaka na baadaye kuwatia mbaroni, walifanya ufuatiliaji wa awali kwa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) ambako ilibainika kuwa mtihani huo ni miongoni mwa ile ya kidato cha sita inayofanyika mwaka huu.

"Watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa polisi na upelelezi ukikamilika tutawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani," Sirro alisema.

Katika tukio lingine, Kamishna Sirro alisema mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam zimesababisha kifo cha mkazi wa Gulani Suka, Alice Genadi ambaye alitumbukia kwenye shimo la choo cha jirani yake ambacho kilikuwa kimejaa maji na hakikuwa kimefunikwa.

Kamanda Sirro alisema msichana huyo alikuwa akimfuata dada yake dukani.

Wakati huo huo, Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kukutwa na vipande sita vya meno ya tembo.

Pia kamanda Sirro alisema wanawashikilia watuhumiwa watatu waliodaiwa kukutwa na lita 36,000 za gongo yenye thamani ya Sh. milioni 72.

Job Opportunities at Tanzania Telecommunications Company Limited ( TTCL)

$
0
0

For more information please see the pic above

CHADEMA Watoa Tamko Hili Baada ya Uchaguzi wa Wabunge wa Afrika Mashariki Jana..!!!

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewapongeza wabunge wake wateule wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala).

Wabunge waliochaguliwa na Bunge la Tanzania kutoka kundi C ni Josephine Lamoyan na Pamela Maassay.

Chadema imesema ina imani kubwa kuwa wabunge hao wateule wa Eala watakuwa wawakilishi bora wa nchi kwenye Bunge hilo wakizingatia manufaa, masilahi na matakwa ya Watanzania na wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Taarifa ya pongezi ya Chadema inasema kupitia uwezo, uzoefu na u-tayari walionao wa kujifunza na kupokea maarifa mapya; Lemoyan na Maassay watabeba matumaini ya mabadiliko ya Watanzania, ambao wangependa kuona ushirikiano wa EAC unakuwa na nguvu za kiuchumi na kisiasa uliojengwa katika misingi ya kidemokrasia kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya wananchi.

“Chama kinawaahidi ushirikiano wakati wowote watakapohitaji ili waweze kutimiza wajibu na majukumu hayo kwenye uwakilishi wa Eala na EAC kwa jumla kwa niaba ya nchi yetu,” imesema taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano Chadema Tumaini Makene baada ya uchaguzi uliofanyika jana (Jumatano).

USAJILI Mpya Simba Wavuja..Hawa Hapa Ndio Wachezaji Watakao Ondoka na Watakaoingia..!!!

$
0
0

SIMBA imesikia kilio cha mashabiki wake ambao wamekuwa wakiukosoa udhaifu uliopo kwenye kikosi chao na sasa uongozi wa timu hiyo umeamua kufanya kweli, kwa kupanga mikakati ya usajili kimya kimya, ili kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Huku Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ikiendelea ukingoni, Simba imeanza kukitathmini kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi na michuano ya kimataifa kama watapata nafasi hiyo.

Habari za uhakika kutoka kwa mmoja ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, zimelieleza  kwamba, kwa sasa wanahitaji kujaza wachezaji wa kimataifa katika nafasi tatu muhimu, ambazo ni straika, beki wa kulia na kati.

Nafasi ya straika mpaka sasa wana uhakika wa kumsainisha straika wao wa zamani, Mganda Emmanuel Okwi, kuchukua nafasi ya Frederick Blagnon anayetemwa, huku utata ukibaki kwa beki Mcongo Janvier Bukungu.

Kwa mujibu wa mjumbe huyo, Bukungu ameibua mvutano baina ya viongozi, kwani kuna wanaotaka abaki, wengine wakitaka aachwe ili atafutwe beki wa kulia shupavu atakayeweza kuhimili michuano ya kimataifa.

Mwingine anayetajwa kutupiwa virago ni beki Method Mwanjali, ambaye umri mkubwa na majeraha ya mara kwa mara vinatajwa kutolishawishi benchi la ufundi kumbakisha kikosini.

Straika wa kimataifa Mrundi, Laudit Mavugo, amebakizwa kundini kutokana na mchango wake mkubwa, huku Mganda Jjuuko Murshid naye akisalia kwa vile bado ana mkataba na Simba.

Aidha, kipa Daniel Agyei amefanikiwa kufanya kile kinachotakiwa langoni, kwani ameonyesha uimara wa kutosha tangu ajiunge na timu hiyo katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

Alisema hata hivyo, kikosi hicho kinaweza kikapanguliwa zaidi kama watapata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, kwani timu hiyo ya sasa haiwezi kuhimili michuano ya kimataifa.

“Viongozi wengi wanasikilizia kwanza, kama Simba itapata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa, kikosi kitafumuliwa, utashangaa watabaki wachezaji wachache sana,” alisema mjumbe huyo.

WANAUME wa Dar es Salaam Acheni tu Wenzenu wa Mikoani Wawadharau kwa Aibu Kubwa Kama Hii..!!!

$
0
0

Tokea hali hii ya Hewa ya Mvua kubwa na hii baridi ianze kwa takribani kama wiki moja sasa nimekuwa nikipita kwa ' Washikaji ' zangu kuwatembelea lakini nilichokikuta huko Kwao kimesinikitisha mno na kinatia mno aibu.

Huko nyuma nilikuwa ' nachukia ' sana jinsi Wanaume waishio Mikoani walivyokuwa ' wakitudhihaki ' sisi Wanaume wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa ' lege lege ' huku tuki ' deka deka ' kama Watoto wa Kike kutokana na ' matendo ' yetu lakini kwa aina hii ya ' Upuuzi ' huu nilioushuhudia mwenyewe katika Wanaume kama saba ( 7 ) hivi na bahati nzuri wote hao kila uchao lazima waende ' gym ' kupasha ili ' kujikomaza ' lakini kumbe hamna lolote.

Jamani kwa haka ' kaubaridi ' tu ka uwongo na kweli ni halali kweli Wanaume wa Mkoa wa Dar es Salaam kuoga maji ya moto? Hivi kweli baridi hii iliyopo sasa jijini ni ya kuwafanya Wanaume wa huu Mkoa kusubiri maji yachemke jikoni kisha waweke katika Ndoo zao na wakaoge?

Wanaume wa Mikoani mlikuwa ' mkitudharau ' sisi Wanaume wa huu Mkoa wa Dar es Salaam nami leo naungana nanyi kwa 100% kuwa mnastahili ' kutudharau ' kwani hii ya sisi Kuoga maji ya moto kwa kisingizio cha baridi kali lililopo ni dalili mbaya mno na pengine ndiyo maana hata Wanawake wa Dar es Salaam wanatucheka na kutudhihaki mno.

Wanaume wa Dar es Salaam tubadilikeni upesi na tuoge maji ya baridi tu na tuache kujilegeza na kudekadeka kwa kuoga maji ya moto badala yake hayo maji ya moto tuwaachie Mama na Dada zetu kwani kiukweli ' tunajiaibisha ' mno.

UKWELI Mchungu..Siku Zinavyozidi Kwenda Inaonesha Kuna Uhaba Mkubwa wa Wanaume Nchini Serikali Iangalie Jambo Hil..!!!

$
0
0

kutokana na matukio kadhaa yanayoendelea ni wazi kuwa nchini kuna tatizo kubwa sana la upungufu wa wanaume(UWAWA) hasa Mafaru Dume. nimekuwa nikikaa na vijana sehemu mbalimbali na kuasikiliza maneno yao na kuangalia matendo yao siku za weekend kiukweli nimekatishwa tamaa sana. kuna mambo ambayo kama vijana kuna haja ya kukumbushana maisha haya dada zetu watakuja kukosa watu wa kuwaoa kabisa.

1. mtu unamkuta ana lalamika, anasononeka na kunung'unika kwa mambo ya kipuuzi kabisa hatafuti ufumbuzi yeye kila siku anasema maisha magumu na asilimia 70 ya maongezi yake ni kuhusiana na wanawake au wanaume .. nani anatoka na nani au nani ana beef na nani. hatukuwa na team x na team y.hayo mambo hayakuwepo.

2. unakuta mtu amevaa suruali au kaptula lakini maongezi yaliyomjaa ni kuponda wenzie wanavyofanya au wanavyokula na kuvaa. sisi zaman ilikuwa ukifanya hivyo kama ni kijiweni wanakufukuza haraka sana wanakwambia hiyo si sehemu yako

3. unakuta mtu kavaa suruali kabisa au kaptula na jina la kiume anasimulia alimtembelea mwenzie sehemu akakuta mwenzie analala chini au hana kitanda na pengine akasema jamaa anapikia jiko la mkaa au kila siku anakula mihogo. hii miaka yetu tunakua usingeweza isikia kabisa.

4. unakuta jamaa kavaa nguo za kiume amesimama au amekaa sehemu na kuna mwanamke ananyanyaswa au mtoto ananyanyaswa na huyu naye amesimama au kukaa sehemu hiyo kana kwamba yeye haimhusu. miaka yetu sisi tulikuwa tunapoona mwanamke au mtoto ananyanyaswa tuna chukua nafasi zetu za uanamue au ubaba haraka sana pasipo kusita.

5. unakuta kajikajana kamepishana na mwanamke kanapiga miruzi au makelele.sisi zaman hatukuwa tukifanya hivyo. ni mawili unamfuata kumsemesha na kumpa sifa zake au unakula kona kama vile hujamwona unamsifia kimoyo moyo

6. miaka ile ilikuwa ngumu kabisa kumwona mtu anaonesha chupi aliyovaa au boxer kwa kuvaa mlegezo . na mtu wa hivyo asingeruhusiwa kukaa na wanaume kijiweni maana wangedhan anajihusisha na mambo haramu.siku hizi eti ni fashion moja wapo

7. miaka yetu ilikuwa huwezi kaa kwenye daladala na kuna mwanamke mjamzito au mtu mzima amesimama wewe ukawa unachezea chezea simu au unasikiliza music. ilikuwa ngumu.wanaume tulikuwa makamanda na tuna kazi ya kuilinda jamii na kuisadia kila wakati.

8. hatukuruhusu ulalamishi na kulia lia kwa mtu ambaye tunadhani ni mwanaume. ilikuwa haitokei, watu tulikuwa tunakomaa na changamoto kwa hali na mali. ilikuwa huwezi sikia mtu anatukana badala ya kutoa hoja. ilikuwa uanaume ni kupambana na kusaidia jamii kwa ujumla. hatukuwa na ubinafsi. jamaa yako kama hajala ukinunua chakula mnakula wote.ilikuwa kama jamaa amekosa kitu flan unamsaidia apate. na kama mwanaume mwenzie amekosea jambo unamwambia na yanaishia huko huko huji kutangaza kwa wanaume wenzio. na ilikuwa ukiletea habari kuwa "flan ana....." ukamsema negatively sisi wanaume wengine tungekubalasa uondoke hufai kukaa na wanaume ukiwa unawasema wenzio vibaya.

9. ulaji wetu ulikuwa ni mzuri tunapiga msosi hasa sababu kila kazi ambayo ilikuwa inapaswa ifanywe nasi tuliifanya. ilikuwa ukifika wakati wa kula miaka ile tunakula chakula cha kutosha sana. na tukimaliza tunashushia maji mengi au maziwa. hatukuwa tukijivunga wakati wa kula.tofaut na sasa mtu anakula ugali mdogo,chips au sausage.

10. sisi tulikuwa na miili iliyojengeka vizuri sana ya ukakamavu. hatukuwa wazembe wa kujipodoa na kuwa lege lege. ilikuwa ni ngumu kusikia unamwita mwanaume mwenzio "we fala" au "ms**g* ugomvi wake ungekuwa mkubwa sana ingekuwa issue hasa. na haikuwezekana kabisa kwa mwanaume kumshika mwanaume mwenzie makalio. maana huyo uliyemshika angeweza kukupiga na kitu chochote kilicho karibu na hakuna ambaye angekutetea hata kama ungekufa au kujeruhiwa vibaya. maisha ya sasa yamebadilisha sana watu.

tunakoeleka nadhan mambo yatakuwa mabaya sana. kama nawe kuna mambo ambayo unayaona si ya ki uanaume kwa sasa yaweke tu hadharani ili tuliokoe taifa hili.

MBUNGE Ahoji: Bila Maji Huwezi Kulala na Mama, Je tutapataje Watoto..!!!

$
0
0

Ni mbunge wa Kilwa Suleiman Habib Ngala alipokuwa akisisitiza umuhimu wa maji, huku akisema serikali imekuwa ikitoa ahadi lukuki kuhusu maji lakini hadi leo kuna tatizo kubwa, na jimboni kwake upatikanaji wa maji ni 48.3% 




KANUSHO la Taarifa zinazosambazwa Facebook Kuhusu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Alichosema Miss TZ Diana baada ya kupewa gari lake miezi 6 baada ya fainali (+video)

$
0
0
Miss Tanzania 2-16 Diana Edward ameongea baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aliyoahidiwa kwenye mashindayo hayo yaliyofanyika October 2016.

Diana amesema hakukata tamaa kuhusu kuisubiria zawadi yake hata kama imechukua miezi 6 baada ya fainali yenyewe kufanyika na kwamba hata yeye hajui ilikuaje japo wakati wa shindano kuna gari lilionyeshwa kwamba ndio ilikua zawadi yenyewe.

‘Nilikua nategemea kupata gari dogo lakini sijui ni aina gani… na kuhusu kuchelewa kupata zawadi siwezi kulaumu sana kwasababu kila mtu anajua sasa hivi uchumi wa nchi umeshuka, namshukuru Mungu tu‘

Kutazama FULL VIDEO ya Diana akiongea bonyeza play hapa chini…

Zitto Kabwe: Nina Wasiwasi na Uwezo wa Wawakilishi wa ‘EALA’ Kutoka Chadema

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa amesikitishwa sana na matokeo ya uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) uliofanyika jana usiku bungeni mjini Dodoma kwa upande wa Chadema.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Zitto ameandika kuwa kuchagua watu bila kuangalia uwezo, uzoefu na uhusika wao kulingana na sehemu wanapotakiwa kuwepo ni kuliangamiza taifa, hasa ukizingatia changamoto zilizopo katika nchi hizo Afrika Masahriki.

Amesema kuwa nchi kama Rwanda, Burundi na Uganda zimepeleka wawakilishi mashuhuri na wenye uzoefu mkubwa katika bunge hilo kulingana na umuhimu wa shughuli zinazofanywa na bunge hilo.

“Jana usiku nilikuwa na hasira sana, kufuatia matokeo ya uchaguzi wa wawakilishi wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki (EALA) haiwezekani kuchagua wabunge ambao hawana uwezo wa kwenda kujenga hoja, huku tukitegemea kupambana na changamoto za muungano wa nchi hizi za Afrika Mashariki”ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Facebook.

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa World Vision, DTB Bank na KCB Bank

$
0
0

Mjukuu auwawa kwa kuchapwa viboko na Bibi

$
0
0

Mwanza. Licha ya vitendo vya ukatili kupigwa vita, bado vitendo hivyo vimeendelea kujitokeza baada ya mkazi wa Kijiji cha Mhungwe, Kata ya Mabuki wilayani Misungwi mkoani hapa, kutuhumiwa kumuua mjukuu wake mwenye umri wa miaka saba kwa kumchapa fimbo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema tukio hilo lilitokea Mei 10, saa moja jioni baada ya bibi  kumchapa viboko mjukuu wake akimtuhumu kuchelewa kurudi nyumbani alipoenda kucheza nyumba jirani. 

Msangi amesema mtoto huyo Balangi Mika aliporejea nyumbani bibi yake alimkamata na kumchapa fimbo maeneo mbalimbali ya mwili wake na kusababisha kifo chake. 

Amesema bibi huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi na utakapokamilika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu mashtaka.
Viewing all 104701 articles
Browse latest View live




Latest Images