Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104667 articles
Browse latest View live

RAMA Dee: 'Lowasa Anapaswa Apumzike Awaachie Watu Wafanye Kazi'

$
0
0
Msanii wa rnb Rama Dee wakati akihojiwa kwenye kikaangoni eatv, ametoa ushauri kwa Lowassa juu ya uhusikaji wake kwenye siasa,

"Lowasa anapaswa apumzike awaachie watu wafanye Nazi, kwa kawaida wazee wetu wakifika miaka 55 au 60 ni umri wa kupumzika"

Je Mdau Wangu wewe Unaonaje..Apumzika au Bado?

KIJANA Aliyemuua Mpenzi Wake na Kumchoma Moto Akamatwa South Africa

$
0
0
Polisi wa nchini Afrika ya kusini wamethibitisha kumshikilia kijana wa miaka 27  na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya mpenzi wake Karabo Mokoena mwenye umri wa miaka 22 aliyeripotiwa kupotea wiki mbili zilizopita.

Mwili wa binti huyo ulikuwa ukiwa umechomwa na ilikuwa vigumu kuutambua.

Wanawake wengi wa nchini humo kupitia mitandao ya kijamii walionyesha kukasirishwa na kitendo hicho na kulaumu vitendo vya uonevu dhidi ya wanawake.

Nchi ya Afrika Kusini imeripotiwa kuwa na matukio mengi ya udhalilishaji na vitendo vya uonevu kwa wanawake ikiwamo ubakaji kwa muda mrefu sasa.

Huyu Ndio Kijana Aliyemuaa Mpenzi wake 


VIDEO: Roma Atoa Free Style Baada ya Kukaa Kimya Muda Mrefu Baada ya Kutekwa

$
0
0
Roma ! Wimbo mpya atakaoutoa ni balaa! Aongelea alivyopigwa na kutiwa kilema
Sikiliza Kionjo chake Hapa Chini mtu wangu:

HIVI Ndivyo Nilivyomuelewa Rais Magufuli, Siyo Huu Upotoshaji Wa Makusudi Kuhusu Ujenzi Wa Reli

$
0
0
IJUMAA Njema Wakuu
Kuna upotoshaji mkubwa unatembea mitandaoni tangu kuhusu pesa za ujenzi wa reli ya kisasa ya Standard gauge. Upotoshaji huu umefuatia ombi la rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumuomba rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma kuzishawishi nchi zinazounda umoja wa BRICS(Brazil-Russia-India-China-South Africa) kutoakana na mikopo yao kuwa ya masharti nafuu kukubali kuipa tanzania mkopo utakaowezesha ukamilishaji wa miradi yake ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya Standard Gauge kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

UPOTOSHAJI unaotembea mitandaoni ni pamoja na:
1. Kwamba rais alishasema reli hiyo itajengwa kwa pesa za ndani
2. Kwamba rais amemwangukia rais Zuma baada ya kukataliwa mkopo na nchi za China, Uturuki, Morocco, Marekani na marekani

Sote ni mashahidi na sote tunafuatilia hotuba za rais Magufuli na ukweli wa alichokisema rais ni huu.

1. Pesa za ndani zitatumika kujenga reli kwa awamu ya kwanza ambapo itaishia Morogoro, rais hajasema reli yote kutoka Dar hadi mwanza itajengwa kwa pesa za ndani. Hii maana yake ni kwamba zitahitajika pesa nje ya zile za ndani kukamilisha ujenzi huo.

2. Tanzania ilikataa mkopo kutoka china kutokana na masharti walioyatoa ya kutaka wakandarasi wa ujenzi huo watoke china na kwamba mkopo huo ni lazima upitie Benki ya EXIM ambayo ni ya china. Hakuna sehemu yoyoye ile ilipotolewa taarifa rasmi ya serikali kwamba nchi za Morocco, Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya zimeombwa mkopo na kukataa.

Myatake: Upotoshaji unaosambazwa na baadhi ya watu kwenye mitandao ya kijamii ina lengo gani? Nani yuko nyuma yake? Tunapaswa kuwa wafuatiji wazuri wa mambo ya nchi ili kujiridhisha na ukweli wa mambo. Upotoshaji wa ama makusudi ama kwa sababu ya kutokuwa na uelewa mzuri wa jambo lenyewe ni hatari kwa maendeleo na ustawi wa nchi yetu.

Snura Adaiwa Kutumia Dawa za Kutengeza Msabwanda (Shepu)

$
0
0

Mwanamziki wa kike wa  Bongofleva Snura amefunguka kwa kuweka wazi kuhusu madai yanayosambaa kwenye mitandao kuwa anatumia dawa za kutengeneza shepu akisema hajawahi kutumia dawa hizo bali shepu yake ni ya asili.

Akizungumza  kwenye kipindi cha  'Leo Tena' ya Clouds FM Snura amesisitiza kuwa familia yao imejaaliwa kuwa na shepu ambayo ni asili yao akiamini kuwa Mwenyezi Mungu amewaumba watu kwa utashi wake.

“Kuhusu suala la mimi kutumia Mchina, natamani sana siku moja nije na familia yangu muione. Hii ni asili yetu. Kwetu sote tumejaaliwa na mimi kama Muislamu naapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa sijawahi kutumia dawa kuongeza makalio.

“Kama nimewahi, Mwenyezi Mungu anilaani na aondoe Baraka kwenye familia yangu. Sitoweza kupita nyumba hadi nyumba kuwaaminisha watu juu ya hili, ila nikinenepa kila kitu kwenye mwili wangu kinaongezeka.

“Mimi naamini kwamba, kila binadamu ameumbwa kutokana na majaaliwa ya Mwenyezi Mungu pasipokuangalia makabila. Ndio maana wapo Wachaga wenye shepu zao.” – Snura

Aidha, Snura amesema anatamani kuolewa na mwanaume mwenye hofu ya Mwenyezi Mungu akiamini itakuwa rahisi kumfanya naye kuwa kwenye misingi ya Dini ambaye pia atajali familia yake: “Mimi sijawahi kuolewa, nimezaa tu. Nahitaji mwanaume mwenye Imani atakayeijali familia yangu.” – Snura.

Idriss Sultan na Miss Tanzania Hapatoshi Baada ya Kuliponda Gari Alilokabidhiwa Jana

$
0
0
Baada ya Idrisaa Sultani kumpiga vijembe  Miss Tanzania 2o16 Diana Edward kukabidhiwa zawadi ya gari lenye mabango la lisilo na hadhi  miss huyo amesema kuwa hawezi kumzuia kusema.

Miss Diana alipewa gari aliloahidiwa kufuatia ushindi kwenye shindano lililofanyika October 2016, gari hilo limekuwa gumzo mitandaoni kutokana na mabango yaliyowekwa kwenye gari hilo.

Kupitia Leo Tena ya Clouds FM leo May 12, 2017 Miss Tanzania 2016, Diana Edward amesema anatoa shukrani na anawaunga mkono waandaaji na hawezi kuwazuia watu kusema kwa kuwa hawafahamu namna gani wamepambana kulipata gari hilo.

“Mabango yatatolewa siku hizi mbili na nimefundishwa kushukuru. Kwa hiyo, nilichopewa nimeshukuru. Nitaliendesha gari, sina kipingamizi. Maneno, watu watayaongea, hiyo ipo. Hakuna binadamu anayekubali kitu. Ndio uwezo wao ulipofikia wa kunipa hiyo zawadi.

“Siwezi kuwapinga – ninawaunga mkono. Mimi ni binadamu pia, kwa hiyo, nimepewa zawadi na nimepokea kwa shukrani, na nawashukuru Kamati na wadhamini na watu wote walioshiriki mpaka nikapata gari.

“Sijui wanachokiongea, ila hali halisi ndio hiyo. Niliitwa nikaambiwa gari lako ndio hili. Nikalipokea kwa shukrani. Mimi sijali watu wanasema nini, maana maneno yapo. Wao wamenipa walichokiweza kwa sababu wamehangaika kweli kulitafuta hilo gari. Watu hawawezi kujua kwa sababu wapo kwenye social media, lakini wangekuwepo tangu watu wanahangaika kulipata hilo gari tangu mwezi wa 6 mpaka leo hii wmaepata.” – Diana Edward.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma afariki dunia leo

$
0
0
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu amefariki dunia leo saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)

Mdogo wa marehemu, Shaibu Mwambungu amesema kaka yake alifariki dunia leo asubuhi baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa hospitalini hapo.

Shaib amesema taratibu za mazishi zitatolewa baadaye ambapo kwa sasa anajiandaa kusafiri kutoka Songea kuja jijini Dar es salam kwa ajili ya mazishi.

Msukuma Awageuzia Kibao Nape Nnauye na Charles Kitwanga...Adai Hakuna Rais Aliyewahi Tekeleza Ilani Ndani ya Mwaka Mmoja

$
0
0
Wabunge wawili waliokuwa mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Tano, Nape Nnauye (Mtama) na Charles Kitwanga (Misungwi) jana waligeuziwa kibao, wakidaiwa kukiuka maadili ya uongozi baada ya kuzungumza kwa hisia dhidi ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Nape alikuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri, wakati uteuzi wa Kitwanga ulitenguliwa baada ya kuingia bungeni akiwa amelewa.

Wawili hao juzi walizungumza kwa hisia kuhusu kiwango kidogo cha fedha kilichowekwa wakisema hakiwezi kutatua tatizo la maji katika maeneo yao; Kitwanga akisema yuko tayari kuhamasisha wananchi wake 10,000 kwenda kufunga bomba la maji linalopita eneo lake.

Nape , ambaye pia alionekana kuwa na hisia kali, alisema sera ya Tanzania ya viwanda haitawezekana kama suala la maji halitapewa kipaumbele na kutengewa fedha za kutosha.

Jana, mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, alisema wakati akichangia hoja ya bajeti hiyo kuwa kauli za wawili hao zinaonyesha kuwa kuna haja ya kazi ya uhakiki wa vyeti kufanyika pia kwa mawaziri.

“Kazi zilizoahidiwa katika Ilani ni nyingi si moja. Hizi hela ni nyingi tuunge mkono na wala tusiwasumbue kwa kuzikataa. Tuwape nafasi ili wakafanye kazi,” alisema Msukuma.

“Lakini suala langu, nataka kuwazungumzia wana-CCM wenzangu ambao jana nilisikiliza mchango wa mmoja, Kitwanga analalamika anasema atawamobilize (atawashawishi) wananchi 10,000 wakazime mashine ya maji Iherere.

“Nataka niwaulize nyinyi mawaziri wa Magufuli hivi vile viapo mnavyokula mnajua maana yake? Kama hamvijui basi sina hakika kama mko sawasawa na kama hamko sawasawa, (Waziri wa Elimu, Joyce) Ndalichako hebu pitisha operesheni ya vyeti feki, huenda hapa penyewe kuna feki za kutosha.”

Alihoji sababu za mtu aliyekuwa waziri kusimama bungeni na kusema kuwa alivyokuwa waziri alibanwa kuzungumza.

“Kwahiyo sisi mambo (ambayo) hatuzungumzi kwa kuwasaidia nyinyi tumebanwa na nani? Mnasimama mnasema sasa nazungumza na nakwenda kuwahamsisha wananchi 10,000 wakazime mtambo?” alihoji.

“Hebu ngoja niwakumbushe tukio la mwaka 2014. Wakati Mheshimiwa Kitwanga akiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, alikuja Geita . Mimi kama mwenyekiti wa CCM wa mkoa nikawaambia wananchi wasitoke mpaka walipwe na mzungu, yeye akaja akamwambia mkuu wa mkoa hata kama kuna mwenyekiti wapigwe mabomu na kweli kesho yake tulipigwa mabomu.

“Kwa hiyo nataka nimwambie Waziri wa Mambo ya Ndani siku akienda kuunganisha wananchi palepale Misungwi naye apigwe mabomu aonje joto ya jiwe. Haiwezekani waziri uliyekula kiapo, ukitimuliwa unakuja humu kutuchanganya, wakati hatujui mambo mliyokuwa mnazungumza kwenye cabinet (baraza la mawaziri).”

Baadaye alimgeukia Nape.

“Nape ambaye alikuwa mwenezi wangu wa (CCM) Taifa, jana (juzi) alizungumza mambo mazuri lakini kuna moja alisema ‘tusipowatekelezea suala la maji wananchi hawataturudisha tena madarakani’.”

Alisema hilo haliwezekani kwa sababu wananchi wanawategemea kwa mambo mengi na si maji pekee yake na wamewafanyia vizuri.

Alisema ilani hazijaanza kuandikwa katika Serikali ya Awamu ya Tano na suala si kumaliza ahadi zote.

Awali alimpongeza Rais John Magufuli na wizara hiyo kwa kazi aliyoiita kuwa nzuri, akisema ameona mabadiliko makubwa.

“Mimi niko tofauti kidogo na wabunge wenzangu wanaosema tusipitishe bajeti kwa sababu hela ni ndogo. Binafsi naona hizi hela ni nyingi sana, tatizo ni zitoke zote tofauti na bajeti ya mwaka jana.” 


Jambazi Mwanamke Mrembo Auawa na Polisi Nairobi

$
0
0
Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi.

Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa kayole.

Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wane wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole.

Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa.

Taarifa katika gazeti la Daily Nation inasema polisi waliwaandama baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wenzao kupitia WhatsApp kwamba majambazi hao walikuwa wamekwepa mtego waliokuwa wamewekewa.



Polisi walijiandaa na kisha wakawakabili katika mtaa wa Lower Chokaa.
Mkuu wa polisi wa mtaa wa Kayole Joseph Gichangi amenukuliwa na gazeti la Daily Nation akisema: "Kwa mujibu wa wadokezi wetu, mwanamke huyo alikuwa mke wa mshukiwa wa ujambazi ambaye anafahamika vyema, ambaye bado anasakwa na polisi."

Alisema visa vya wanawake kujihusisha na magenge yanayotekeleza wizi wa kutumia mabavu vinaongezeka.

Wakenya mtandaoni wamekuwa wakisambaza picha za Mwaniki na kumjadili sana mtandaoni.
Katika Facebook, mwanamke huyo anajitambulisha kama mwanafunzi wa zamani wa chuo kikuu cha Nairobi na mtu anayependa kufurahia maisha.

Kuna wakati alipakia picha yake, ya mwanamume na mtoto, na kuongeza kwamba hiyo ni "familia".
Mkuu wa polisi Nairobi Japheth Koome anasema magenge mengi ya wahalifu huwa na wanawake.

"Wanawake hutumiwa kusafirisha silaha, kukusanya habari na hata kushiriki katika ujambazi," Bw Koome alisema.

Aliongeza kuwa wakati mwingine hutumiwa na majambazi wa kiume kuwapelekea chakula mafichoni.

Shirika la Ndege la Marekani Laguswa na vifo vya Wananfuzi 32, Wajitolea Kuwasafirsha Majeruhi

$
0
0
Shirika la ndegeSamaritAn Purse la Marekani, limetoa ndege aina ya DC 8, kwa ajili ya kuwasafirisha watoto walionusurika katika ajali ya basi iliyoua wanafunzi 32, walimu na dereva wilayani  Karatu.

Watoto hao ambao hali zao si nzuri ni Doreen, Saidia na Wilson na watakwenda Marekani kwa ajili ya matibabu pamoja na wazazi wao.

Nyalandu amesema ndege hiyo inaondoka jioni ya leo kutoka mji Mkuu Charlotte, Jimbo la North Carolina nchini Marekani na inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa Kilimanjaro majira ya jioni, Jumamosi, Mei 13.

“Endapo upatikanaji wa hati ya kusafiria (visa) utafanikiwa hapo kesho kama tunavyotarajia, wasafiri wataondoka asubuhi ya Jumapili, Mei 14 kuelekea Marekani.”

“Ndege hii aina ya DC 8 itatarajiwa kutua Mjini Charlotte, NC, na wagonjwa pamoja na waliowasindikiza wataingia katika ndege nyingine maalumu ya kubeba wagonjwa (Air Ambulance) hadi mji wa Sioux City, Iowa ambako.” amesema Nyalandu 

BREAKING: Mmiliki wa Shule ya Arusha Kafikishwa Mahakamani Kwa Makosa Matano

$
0
0
Mmiliki wa shule ya Lucky Vicent Arusha Innocent Moshi na Makamu Mkuu wa shule Longino Vicent Nkana wamefikishwa Mahakamani na kusomewa makosa matano.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Rose Sule amesema mnamo May 6 Mmiliki huyo wa shule aliruhusu Dereva kuendesha gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji, kutumia gari bila kuwa na BIMA pamoja na kushindwa kuingia mkataba na Mwajiriwa.



Makosa mengine ni kuzidisha abiria 13 kwenye gari pamoja kaimu mkuu wa chuo kuratibu safari pamoja na kuruhusu gari kuzidisha abiria.

Watuhumiwa wote wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kuwa na watu wawili kwa bondi ya milioni 15 kila mmoja na huku washtakiwa kutoruhusiwa kuondoka ndani ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuwasilisha hati zao zakusafiria.

Hakimu wa Mahakama ya hakimu mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Desdery Kamugisha ameahirisha kesi hiyo mpaka 8 mwezi wa 6 kutokana na upelelezi kutokamilika.

VIDEO: Historia ya Eneo Walikopata Ajali Wanafunzi, Arusha

$
0
0
Wakati Tanzania ikiomboleza vifo vya watu 35 wakiwemo wanafunzi 32 kutoka shule ya Lucky Vicent kwenye ajali ya gari iliyotokea Karatu, Arusha May 6, 2017. Ayo TV na millardayo.com imefika eneo ilipotokea ajali hiyo ambalo linatajwa kutokuwa na historia ya ajali.

Unaweza kulitazama hapa chini kwenye hii video…

Wenye Amana Benki FBME Kulipwa Milioni 1.5/-

$
0
0
WATEJA wenye amana katika Benki ya FBME iliyofilisiwa na Benki Kuu, wanaweza kuanza kulipwa amana zao wiki ijayo, lakini fedha watakazolipwa hazitazidi Sh milioni 1.5.

Mkurugenzi wa Bodi ya Amana, Emmanuel Boaz aliliambia gazeti hili jana kuwa wateja ambao wana kiwango cha fedha kinachozidi kiasi hicho, watalazimika kusubiri hadi mchakato wa kuifilisi benki hiyo utakapokamilika ndipo watalipwa salio litakalobaki.

Boazi alisema bodi yake italipa kiasi hicho cha fedha kwa kila mteja na wanafanya hivyo kwa mujibu sheria ya bima ya majanga inayokatwa na benki dhidi ya wateja walio na amana katika benki husika. “Naomba wateja wa FBME wavute subira, tunawahakikishia kuwa watalipwa baadhi ya fedha zao, hawawezi kupoteza fedha zote,” alisema Boaz.

Alifafanua kuwa kwa sasa wanaendelea na uhakiki ambao alisema uko katika hatua nzuri na wiki ijayo mwishoni wanaweza kuanza kuwalipa wateja wa benki hiyo. Alisema katika uhakiki huo wanachofanya ni kuhakiki idadi ya wateja waliopo, wateja wanaodaiwa na benki hiyo, mali zinazomilikiwa na FBME pamoja na wateja wanaoidai benki hiyo.

Alisema uhakiki huo ni muhimu kufanywa na bodi ya amana. Alisema baada ya hatua hiyo bodi ya amana itateua benki mojawapo nchini ambayo italipa fedha za wateja wenye amana. Alisema wanaendelea na mazungumzo na benki moja ambayo ina matawi katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Zanzibar na Mbeya ambako FBME walikuwa na matawi.

Alisema kwa kila akaunti sheria inaruhusu kumlipa mteja Sh milioni 1.5 tu na wale ambao wana akaunti zaidi ya moja wataziunganisha na kuwalipa stahiki yao. Hata hivyo, alisema anaamini baadhi ya wateja wana salio dogo jambo ambalo litasaidia kufanya kazi hiyo ya uhakiki kwa haraka.

Alisema baada ya kukamilisha ulipaji wa amana za wateja, ndipo mfilisi ataendelea na mchakato wa kuifilisi benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuuza baadhi ya mali za wadaiwa wa benki hiyo.

Alisema mali hizo zitauzwa ili zipatikane fedha za kuweza kuwalipa watu wanaoidai benki hiyo wakiwemo wateja wenye amana kubwa. Boaz aliongeza kuwa ni katika kipindi hicho mteja wa FBME ambaye alikuwa na deni, wataangalia dhamana iliyowekwa na kama ni nyumba, bodi hiyo ya amani italazimika kuuza nyumba hiyo au kama mteja kabakiza kiasi kidogo watakubaliana namna ya kuweza kumalizia kiasi kilichobaki

Mwanafunzi Udom Akutwa na Misokoto 826 ya Bangi

$
0
0
 Jeshi la polisi mkoani Dodoma linawashikilia watu wawili kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi akiwamo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) Nelson Matee (24) ambaye ni mwanafunzi wa kozi ya uuguzi mwaka wa nne.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake leo asubuhi, kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kuwa mwanafunzi huyo alikamatwa Mei 9 mwaka huu kufuatia msako mkali uliofanywa na jeshi hilo chuoni hapo ambapo mtuhumiwa alikutwa na jumla ya misokoto 826 ya bangi yenye uzito wa kilo 2.8 akiwa ameiweka kwenye mifuko ya nailoni chumbani kwake.

Mambosasa amesema kuwa mtuhumiwa alipohojiwa alisema kuwa amekuwa akifanya biashara hiyo ya kuuza bangi kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga na chuo hicho na kwamba alikuwa akiwauzia wanafunzi wenzake.

Mvua yaua 7 Tanga, mamia ya magari yakwama

$
0
0
IDADI ya wakazi waliokufa kutokana na athari za mvua ya masika inayoendelea kunyesha kwenye maeneo mbalimbali wilayani Korogwe Mkoa wa Tanga, imefikia saba sasa wakiwemo wanawake watano, wanaume wawili pamoja na majeruhi 10, huku barabara ya Segera – Mkumbara ikifungwa kwa muda.

Vifo hivyo vyote vimetokana na maporomoko ya maji, mawe, miti na mchanga kutoka katika Milima ya Usambara Magharibi ambavyo vimeendelea kuvamia kwa kasi baadhi ya nyumba zilizo mabondeni katika kata za Mkumbara, Chekereni, Makuyuni, Kwagunda, Kerenge na Ngombezi.

Pia Imebainika kwamba hali ya usalama kwa baadhi ya wananchi imekuwa tete hasa wale wanaokaidi agizo la serikali linalowataka kuhama badala yake wanaendelea kung’ang’ania kuishi ndani ya nyumba zao zilizoko bondeni jirani na kingo za Mto Pangani kwa kuwa tayari wanyama wakali akiwemo mamba wameanza kutumia mafuriko hayo kuvamia nyumba hizo ili kutafuta malisho.

Akizungumza jana jioni katika mahojiano kwa njia ya simu, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Robert Gabriel alisema hali ya uslama kwa wakazi wa maeneo hayo haijatengemaa hivyo jamii inapaswa kufanya kila linalowezekana ili kuokoa maisha.

“Kuna tukio la kusikitisha sana la jana huko Kata ya Ngombezi ambako ni jirani na mto Pangani kuna mama mmoja amenusurika kuliwa na Mamba wakati alipokuwa akisafisha kifaa cha kudekia nyumba kwa kutumia maji hayo ya mafuriko,” alisema mkuu wa wilaya na kuongeza: “Ilikuwa tu baada ya kumaliza usafi akaamua kwenda kusuuza dekio bila kujua kwamba kumbe mamba alikuwa mawindoni ametoka huko mtoni na kujichanganya kwenye hayo mafuriko jirani na nyumba wakati mama akiendelea kusafisha ndipo mamba akavamia hilo dekio na kuondoka nalo na mama akanusurika.

Hii ni hatari nawahimiza watii agizo la serikali ili tuokoe maisha kwa kukubali kuhamia maeneo makavu ya juu milimani.” Alisema kitendo cha mama kuvamiwa na mamba kutokana na mafuriko kuendelea kuzingira nyumba ni kiashiria tosha kwamba maji yanapoingia ndani na mamba nao wanahamia katika makazi ya wananchi hivyo ni muhimu kwa kila mwananchi kuchukua tahadhari.

Aidha, alitaja athari nyingine zilizopatikana ni kufungwa mara kwa mara kwa baadhi ya barabara kuu na kusababisha baadhi ya magari na watumiaji wengine kusubiri kwa muda wakati maporomoko ya maji na mawe yanapokatiza kwenye maeneo hayo.

Alisema mpaka sasa tathmini halisi ya hasara iliyosababishwa na maafa hayo bado haijapatikana kwa kuwa kamati ya wilaya inatarajia kukutana kesho. Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) mkoani Tanga, Alfred Ndumbaro akizungumzia madhara yaliyotokea katika baadhi ya barabara kuu kutokana na mafuriko hayo, alisema wao wamefanikiwa kuondoa vikwazo barabarani ili gari ziendelee kupitika.

“Kikosi kazi chetu kinashughulikia maeneo ya Mazinde na Mkumbara katika barabara kuu ya Segera - Mkumbara ili kuhakikisha miundombinu hiyo inarejea katika matumizi yake ya kawaida,” alieleza Ndumbaro baada ya magari kukwama kwa muda eneo la Mazinde.

Hata hivyo, alitaja maeneo mengine ambayo yanaendelea kushughulikiwa ni katika barabara kuu ya Mombo - Lushoto ambako vifusi vya udongo vilianguka kutoka juu milimani na kuziba njia katika baadhi maeneo.

Kuhusu barabara kuu ya Tanga – Pangani, alisema Tanroads inafanya juhudi za haraka za kuchepusha barabara katika maeneo yaliyoharibika ikiwemo karibu na daraja la Neema ili kuwezesha watumiaji kuendelea kupata huduma wakati serikali ikiangalia njia ya muda mrefu ya kutengeneza eneo hilo.

Mmoja wa wasafiri waliokuwa wakitoka Moshi, Jacob Tesha alieleza kuwa walikwama Mazinde tangu saa tano asubuhi, na walipewa taarifa na Polisi wa Mazinde kuwa Mombo barabara imeharibika na magari yamezuiliwa na wao walizuiliwa Mazinde. Alisema foleni ilikuwa ya mamia ya magari.

Alisema njia ilianza kufunguliwa saa 11 jioni, na akaeleza kuwa makalavati ya eneo la Mombo ni madogo, hivyo maji yamefurika na kuharibu njia. Wakati huo huo watu watano wamejeruhiwa na kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto baada ya magari matano waliyokuwa wakisafiria kati ya miji ya Soni na Lushoto mkoani Tanga kuangukiwa na kifusi cha udongo na mawe.

Magari hayo ambayo namba zake za usajili hazikuweza kupatikana mara moja ni mabasi mawili aina ya Costa, Toyota Carina moja, Noah moja pamoja na Hilux moja ambayo inamilikiwa na shirika La umeme Tanesco wilayani Lushoto.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba amethibitisha tukio na kuongeza usiku huu jana askari wa jeshi la Polisi wilayani Korogwe wamelazimika kufunga baadhi ya maeneo ya barabara kuu ikiwemo ya Mombo - Mkumbara - Mazinde wilayani Korogwe ili kuepusha madhara kutokana na ongezeko la maporomoko ya maji, tope, na miti kufuatia mvua nyingi zinazoendelea kunyesha.

Bibi Harusi Apewatalaka Saa Chache Baada ya Ndoa kwa Kuchat Usiku Mzima

$
0
0
Matumizi ya simu za mkononi hupelekea mtu unayekuwa karibu naye kimwili kuwa  mbali nawe kiakili na mawazo ambayo ameyaelekeza kwa mtu anayewasiliana naye muda huo. Balaa zaidi ni ‘kuchat’ ambapo mtumiaji wa simu hupelekea hisia zake zote kwenye vidole vinavyoandika huku akimuacha aliyenaye akiwa mpweke.

Hii imemgharimu bibi harusi aliyekesha akipokea salamu za pongezi kwenye simu na kumsahau mumewe. Fuatilia kisa hiki…!

Mwanaume mmoja ameamua kumtalakisha mkewe saa chache baada ya kufunga ndoa, kwasababu mkewe huyo mpya alitumia usiku wao wote wa ‘fungate’ kuchat na rafiki zake.

Kwa mujibu wa gazeti la Al Watan la Saudi Arabia, bibi harusi huyo alikuwa busy akipokea salamu za pongezi kutoka kwa rafiki yake akimsahau mumewe aliyenaye chumbani muda huo.

“Bwana harusi alijaribu kusogea karibu naye na kimahusiano, lakini alishitushwa kuona mkewe anampotezea, hajibu anachoulizwa au hata kuonesha vitendo,” ndugu wa Bwana harusi aliiambia Al Watan.

“Mwanaume alipomuuliza kama rafiki zake ni muhimu kuliko yeye, alimjibu ndio,” walisimulia mkasa walioelezwa na bwana harusi.

Mahakama ya mwanzo katika eneo hilo imejaribu kuwasuluhisha ili waendelee na ndoa yao, lakini mwanaume ameendelea kushikilia msimamo wake wa talaka.

Mambo 7 yanayowaumiza Wanaume Kwenye Mahusiano

$
0
0
Kupitia safu yetu ya mahusiano, leo nimekuletea makala maalum hasa kwa wanawake kutokana na malalamiko ya wanawake wengi kuwapoteza waume zao. Kilio chao kikubwa ni kukimbiwa na wanaume au kuachwa.

Leo anakuwa na mwanaume huyu, baada ya muda mfupi kunatokea chokochoko, mwanaume anatimka zake.

Jamaa anamkimbia na kwenda kuanzisha uhusiano mwingine. Baada ya kukimbiwa, mwanamke hakati tamaa. Anaanzisha uhusiano mwingine, ndani ya muda mfupi tu, anaambulia maumivu tena. Anabaki kujilaumu. Hajui chanzo cha yeye
kukimbiwa.

Matokeo ya hili, mwanamke anapoteza uelekeo. Kila mwanaume anayekutana naye anamkimbia. Mwisho wa siku anajikuta umri umeenda. Kuolewa inakuwa ni ndoto. Anaanza kulazimisha kusaka mtoto ili angalau na yeye aitwe mama.

Wanaume wengi hujikuta wakiwaacha wapenzi wao kwa sababu ya tabia fulani ambazo wakati mwingine huanza taratibu na baadaye huwa kikwazo kikubwa.

Ili kuweza kuepukana na tatizo hili ni vyema tukaangalia vitu ambavyo wanaume wamekuwa hawavipendi kutoka kwa wanawake ili kuweza kujua nini cha kufanya kuhakikisha unamweka mwanaume karibu, asikuache.

1. Chokochoko/Maneno Maneno
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. Kutoridhika
Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.
Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

Bahati mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi. Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.

Kwake kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake hamtimizii.

Mwanaume akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.

3. Kulinganisha
Hii nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo kubwa.

Mwanaume anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata yule anayemvutia.

Wanawake wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye bora kuliko wanaume wote duniani.

4. Kuwa Tegemezi
Wakati mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa mwanaume.
Hata kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi kipimo inageuka kuwa kero.

Yani kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.

Mwanaume akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.

5. Kutokuwa Muelewa
Mwanaume anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi. Anatamani kuwa na mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.

6. Kujigamba/Maringo
Hakuna mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.

Isikupite hii: Mambo matano '5' yatakayo kuongezea thamani katika maisha yako

Anatumia fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia watashindwana katika suala la kumtawala.

7. Kuwa bize sana
Wanaume wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata akose muda na mwenzi wake.

Unachotakiwa kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke mwingine ambaye hayupo bize

Hii Ndiyo Faida Ya Kupanda Mbegu Bora Kwa Wasaidizi Wako Wa Kazi Katika Familia Yako.

$
0
0
Kumekuwa na matukio mbalimbali yanatokea yakihusu wafanyakazi au wasaidizi wa kazi za ndani. Matatizo mengi yanatokea katika familia nyingi hayaji tu kama radi lazima kuna sababu zinazopelekea kutokea kwa matatizo hayo. Huwezi kupanda mahindi shambani halafu ukategemea kuvuna mbaazi.

Hivyo siku zote utavuna kile ulichopanda. Kama ukipanda mbegu bora ya upendo katika familia yako tegemea kuvuna mbegu bora ya upendo. Vivyo hivyo, kama ukipanda chuki katika familia yako tegemea kuvuna mauti. Hii ni sheria ya asili unapokea kile unachotoa.

Kwa tafiti zisizo rasmi, ukitembelea nyumba kumi kati ya nyumba hizo kumi moja tu ndio wanaishi vema na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Nyumba nyingi ni matatizo sana je matatizo haya yote yanasababishwa na nani? Lazima tuchunguze nini kiini cha kosa au tatizo kwanza. Huwezi kutatua tatizo bila kuchunguza kiini cha kosa.

Visa vimekuwa vikitawala ndani ya nyumba nyingi kwa wale wanaoishi na wasaidizi wao wa kazi za ndani. Wasaidizi wa kazi za ndani wanafanyiwa ukatili na waliowaajiri ndio maana nao wanalipa visasi kwa watoto wao. Wasaidizi wa kazi za ndani wanarusha visasi wanavyofanyiwa na waajiri wao kwa watoto.

Watoto wanakua wahanga wa matatizo mengi wanaumizwa na kuteswa na kuona dunia ni chungu na siyo sehemu salama ya kuishi kutokana tu na kuishi maisha yaliyokosa upendo ndani yake. Waajiri wa kazi za ndani wanapandikiza chuki kwa wafanyakazi wao wa ndani na wasaidizi wao wanaona sehemu sahihi ya kulipiza kisasi ni kwa watoto.

Hivyo wasaidizi wa kazi za ndani nao wanatoa kile walichopokea na siku zote chuki huzaa mauti. Ndio maana kuna faida kubwa sana kwa waajiri kupanda mbegu ya upendo ambayo itakwenda kuota kwa kila mwanafamilia na hatimaye watakuja kuvuna upendo.

Mpendwa msomaji, jaribu kuvuta picha ni matukio mangapi umeyasikia au kuyaona kwa macho yako yanayosababishwa na wafanyakazi wa ndani. Na je wahanga wakubwa wa matatizo hayo katika familia ni kina nani? Kama sio watoto? Wafanyakazi wa ndani ndio wanaonekana wana makosa au wakosa kama hujachunguza kiini cha tatizo au kosa kwanza.

Wanawake wengi walio na waume zao wanawaachia wadada wa ndani kila kitu wafanye hata zile kazi ambazo hawapaswi kufanya, kazi ambazo angetakiwa kufanya na mama au mwanamke aliyeolewa ambaye yeye ndio mlinzi wa familia. Wanawake wengi wanawatengenezea mazingira mabaya wao wenyewe na unakuta nafasi ya mke sasa anachukua dada wa kazi. Kwa kisingizio kua yuko bize na kazi mpaka anasahau wajibu wake kama mke au mama wa familia.

Lazima muwe na mipaka ya kazi na wasaidizi wenu wa kazi siyo kumuachia akufanyie kila kitu katika nyumba yako unayoishi. Wasaidizi wa kazi za ndani unakuta wanajua vitu vingi kuliko mama wa familia ndani ya nyumba sasa hii ni hatari sana.

Kutokana na mwanamke katika familia yake kushindwa kuwa mlinzi wa familia yake matokeo yake hata wale wanaume wasiokua waaminifu katika ndoa zao wanatembea na wasaidizi wao wa kazi kwa sababu mazingira hayo wanayasababisha wao wenyewe. Unampatia msaidizi wako wa kazi kufua nguo za muwe wako hata za ndani na kumwandalia kila kitu mume wako unafikiri unategemea nini?

Hujaolewa kwenda kuwa mtalii wa nyumba bali mwanamke aliyeolewa anakwenda kuwa mlinzi wa nyumba yake na baba kuwa kichwa cha familia yake. Na kazi hizo wamepewa na Mungu. Ndio jukumu la mke na mume wakishindwa kutimiza wajibu wao kila mmoja kinachofuata ni machozi tu.

Ukiwa ni mama wa kutoa agizo dada naomba nenda kamtandikie baba anataka kulala, au kamuandalie maji ya kuoga, chakula, mwangalie mtoto kama amekula, kama anaumwa, waangalie watoto kama wameenda shule nk na wewe umekaa sebuleni unaangalia tv na kubadilisha chaneli utakuja kupata hasara tu.

Kama wewe ni mwanamke ndani ya nyumba usikwepe majukumu yako na kumwachia dada wa kazi na wewe kama ni baba wa familia simama kama kiongozi kweli na mwanamke linda nyumba yako.

Mpendwa msomaji, unajua ni kwa nini matatizo yanatokea kwa wasaidizi wa kazi za ndani?

Sasa karibu ujionee viini vya matatizo hayo.

1. Kukosa upendo;
wasaidizi wa ndani wanakosa upendo badala yake wanapewa chuki ambayo ndio inakuja kuzaa matatizo mengi katika nyumba nyingi. Hakuna kitu kama upendo wewe lisikie tu neno hili upendo lina maana kubwa sana kwa binadamu.

Kama vile wewe unahitaji kupewa upendo na watu wengine mpatie na msaidizi wako wa kazi naye anakurudishia upendo. Mpende kama unavyojipenda wewe, kama unavyoipenda familia yako na mfanye awe sehemu ya familia yako. Vaa viatu vyake halafu utaona kama utavuna ubaya kutoka kwake.

2. Kukosa kuthaminiwa;
mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, hitaji la kwanza la binadamu ni kuthaminiwa. Anza leo kumthamini mfanyakazi wako uone naye atakavyokuwa anakuthamini. Unatoa kile unachopokea katika maisha yako.

Binadamu akihisi anakosa kuthaminiwa anakua amekufa kisaikolojia kabisa. Ni nani ambaye hahitaji kuthaminiwa? Kila mtu anataka kuthaminiwa katika hii dunia. Hakuna mtu aliyezaliwa kuja kupata mateso duniani mwache kila mtu afurahie na kuonja thamani yake hapa duniani.

3. Kukosa uhuru;
kukosa uhuru ni utumwa katika maisha. Ndio maana watu wanapelekwa gerezani kufungwa ili wakose ule uhuru wao. Kila mtu anahitaji uhuru. Sasa hawa wasaidizi wa ndani hawapewi fursa ya uhuru. Ukimbana sana mtu na kukosa uhuru na ni mtu mzima lazima atatafuta uhuru. Naye ni binadamu anahitaji uhuru kama wewe, uhuru wa kufanya mambo yake na usimtawale kama vile mtoto mdogo.

4. Kudharauliwa, kutengwa na kuchukuliwa kama siyo sehemu ya familia;
wasaidizi wa ndani wanachukuliwa kama watu wenye shida sana, siyo wa umuhimu na hafai kuwa sehemu ya familia. Wanalala sehemu isiyostahili kulala, wanavaa mavazi yasiyo nadhifu yaani ukienda nyumba nyingine unatamani hata kutokwa na machozi watoto wa familia wamevaa nguo nadhifu ukimuona yeye kachoka kabisa anachukuliwa siyo mtu muhimu.

Mtu anayekupikia, kukuangalizia watoto na nyumba yako halafu unamdharau ndio maana hata wengine wanawekewa sumu kwa sababu ya mateso wanayofanyiwa na wanafamilia. Wakati wa kula chakula dada wa kazi anakula jikoni peke yake wanafamilia wamekaa mezani wanakula hivi wewe ungekuwa unafanyiwa hivi ungejisikiaje? Wakati mwingine hata chakula wanapewa masalia wanafamilia kwanza. Ishi na msaidizi wako kwa upendo.

5. Kutukanwa, kupigwa na kudharauliwa;
baadhi ya wasaidizi wengine wanateswa na wanatukanwa matusi ya kila aina yaani wamegeuzwa kama jalala la matusi. Mwisho wa siku dada wa kazi anakua anapata majeraha ya moyo. Wengine wanapigwa na kuteswa na kunyimwa hata chakula. Halafu ukifanyiwa jambo baya utasikia wafanyakazi wa ndani sio watu siku hizi.

Kabla ya kulalamika chunguza kiini cha kosa ni nani msababishi wa yote haya? Wanafamilia wanatendea vibaya wadada wa kazi ndio maana nao wanawatendea mabaya. Ndio maana dawa ya chuki huzaa mauti, unamfanyia mwenzako mabaya halafu unategemea mazuri? Sahau kuhusu hilo.

6. Kusemwa maneno makali;
wanasemwa maneno makali yenye chuki ambayo yanakwenda kutengeneza majeraha katika moyo. Maneno ni mabaya kwani yanakwenda kutengeneza chuki ndani ya moyo. Acha kuwasema sana maneno mabaya bali mtie moyo na hamasa ya kufanya kazi na kushirikiana naye hata kama unamlipa. Kuwa kiongozi mzuri katika familia yako.

7. Kutopewa nafasi ya kujieleza na kushindwa kumpata mtu wa kumuelezea matatizo yake; nguvu ya pesa wakati mwingine huwa inatumika kwa kuwakandamiza wadada wa ndani. Ananyimwa mahitaji ya msingi anaingiwa na tamaa ya kuiba halafu akiiba nguvu ya pesa inatumika anakamatwa na kupelekwa polisi bila hata kupewa nafasi ya kujieleza.

Na kukichunguza kiini cha kosa utagundua mwajiri wake ndiye msababishi. Unakuta wakati ana shida anakosa mtu wa kumwambia watu wote ndani ya familia wamegeuka kuwa miiba hivyo anaendelea kubaki na uchungu ulioumbika na matokeo yake wanafanya matukio ya ajabu.

8. Kupewa ujira mdogo na kucheleweshewa ujira wao; dhahiri kwamba wafanyakazi wengi wa ndani wanalipa ujira mdogo na wanafanya kazi nyingi zaidi ya masaa 12 bila mapumziko. Kama anakufanyia kazi zako mpe stahiki yake hata kama ni kidogo.

Kama humpatii mahitaji yake binafsi lazima umpatie hela ili aweze kujitegemea. Kuna wengine hawapewi kabisa wanaambulia maneno kama haya unakula bure tu, kulala hapa na kujaza choo hapa. Mambo kama haya unakuwa unamuumiza msaidizi wako.

Mwisho, ndugu msomaji, panda mbegu bora ya upendo kwa manufaa yako na kwa jamii nzima. Mpe malazi mazuri na chakula bora. Mtendee mwenzako kama vile unavyotaka wewe kutendewa na vaa viatu vya mwenzako. Kuwa mfano sahihi kama unamwambia msaidizi wa kazi kuamka saa 11 au 12 na wewe onesha mfano. Siyo wewe unatoa agizo halafu unaamka saa 2 jihukumu kwanza wewe mwenyewe kabla ya kumhukumu mwenzako.

MMILIKI wa Lucky Vicent na Makamu Mkuu wa Shule Ambayo Wanafunzi Wake 33 Walikufa Ajalini Arusha Waachiwa kwa Dhamana..!!!

$
0
0

Mmiliki wa shule ya msingi Lucky Vincent,Innocent Mosha amefikishwa mahakamani jana  mjini hapa kujibu makosa manne  yaliyosababishwa na  ajali ya basi lake lililouwa watu 35 wakiwamo wanafunzi 32.

Pia makamu Mkuu wa shule hiyo,Logino Vicenti amepandishwa kizimbani kujibu shitaka moja la kuongeza abiria 13 kwenye gari lililopata ajali.

Mwendesha mashitaka Rose Sulle  ameiambia mahakama mbele ya hakimu mkazi Desderi Kamugisha kuwa  upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Watuhumiwa  wamepata dhamana kila mmoja yenye thamani ya Sh 15 milioni. Kesi itatajwa tena Juni 8 mwaka huu.

TRUMP Aibua Sintofahamu Mpya Kuhusu FBI na Sakata la Kumchunguza...Afunguka Haya Makali..!!!!

$
0
0

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hachunguzwi  na mtu yeyote wala shirika la ujasusi la FBI halimchunguzi. Hiyo ni baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la FBI.

Akizungumza na chombo cha habari cha NBC jana, Trump alisema  kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.

Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya maofisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.

Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliyopingwa na mrithi wa Comey.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo, Trump aliiambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza Comey iwapo alikuwa akimchunguza.

“Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia, huchunguzwi.” alisema Trump

 Chanzo BBC.
Viewing all 104667 articles
Browse latest View live




Latest Images