Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live

FAHAMU Ukweli Juu ya Vita vya Karansebes Ambavyo Zaidi ya Wanajeshi 10000 wa Jeshi la Australia Waliuana Wenyewe kwa Wenyewe Bila Kujua..!!!

$
0
0

Unaweza kudhani ni hadithi ya kutunga lakini hii kweli ilitokea! Vita ya Karansebes, ni miongoni mwa matukio yaliyoushangaza sana ulimwengu baada ya wanajeshi wa jeshi moja la Austria, kushambuliana wenyewe kwa wenyewe na kusababisha wanajeshi zaidi ya 10,000 kupoteza maisha.

Ilikuwaje? Usiku wa Septemba 17, 1788, wanajeshi zaidi ya 100,000 wa Jeshi la Austria lililokuwa linaundwa na makabila mbalimbali, walikuwa wameweka kambi katika Mji wa Karansebes (Romania ya sasa) wakijiandaa kuvamia Himaya ya Ottoman (Uturuki ya sasa).
Ili kurahisisha uvamizi, wanajeshi waligawana katika makundi, wengine wakaenda upande mmoja na wengine upande mwingine. Wakati wakijiandaa kufanya shambulio, kukatokea kutoelewana kati yao, wakaanza kushambuliana wenyewe kwa wenyewe kimakosa wakidhani wanawapiga wanajeshi wa Ottoman.

CHANZO CHAKE KINASHANGAZA
Inaelezwa kuwa kundi moja kati ya yale mawili, lilivuka Mto Timis na kuingia Mji wa Hussar uliokuwa ngome ya wanajeshi washirika, Wahussar waliokuwa wakisaidiana kuwapiga Waturuki. Baada ya kuingia, wanajeshi wa Austria waliomba hifadhi kwa wenyeji wao ambao waliwakarimu kwa pombe na chakula wakati maandalizi ya vita yakiendelea.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa wanajeshi hao, pombe iliisha wakati wanajeshi wakiwa bado wanaihitaji, wakaanza kuwashinikiza wenyeji wao wawaongeze, jambo lililosababisha kutokea kwa hali ya kutoelewana na kurushiana maneno. Mmoja kati ya wanajeshi wa Austria, ambaye tayari alishaanza kulewa, kwa hasira alifyatua risasi juu akishinikiza waongezwe pombe.
Mlio wa risasi ulisababisha taharuki kubwa eneo hilo, wenyeji wakahisi wamevamiwa na wanajeshi wa Ottoman (Waturuki), wakawa wanakimbia huku na kule wakitamka neno ‘Turci! Turci!’ (Waturuki! Waturuki).

Mkanyagano ulipozidi kuwa mkubwa, ilibidi viongozi wa jeshi la Austria waingilie kati na kuanza kuwatuliza wanajeshi wao ambao nao walishachanganyikiwa wakidhani kweli wamevamiwa na Waturuki! Viongozi hao wakawa wanatumia neno Halt! Halt! Ambalo kijeshi hutumika kuwaamuru wanajeshi kuacha kila wanachokifanya na kutulia mara moja.

Kwa kuwa kabila la wenyeji, Wahussar hawakuwa wakijua Kiingereza wala Kijerumani, waliposikia neno hilo walilifananisha na ‘Allah! Allah!’ ambalo lilikuwa likitumiwa na wanajeshi wa Uturuki wanapokuwa vitani.

Wakaamini walikuwa wamevamiwa na Waturuki, wakaanza kuwashambulia, mapigano makali yakatokea kati yao. Kundi la pili lililokuwa upande wa pili wa mto, liliposikia mapigano yamekolea, nalo lilivuka mto na kwenda uwanja wa vita. Kwa kuwa tayari giza lilikuwa limeingia, wakaanza kuwashambulia wenzao ambao nao walijibu mapigo, vita ikazidi kupamba moto, kila mmoja akiamini anapigana na Waturuki.

Mpaka kunapambazuka, wanajeshi 10,000 walikuwa wamekufa huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa. Kila mmoja aliyepona akawa anashangaa iweje katika wote waliokufa, wawe ni wa upande mmoja wa wanajeshi wa Austria na washirika wao wa Hussar, hapo ndipo ukweli ulipofahamika kwamba kumbe walikuwa wakipigana wenyewe kwa wenyewe.

Waturuki waliposikia taarifa hizo, walifika haraka eneo hilo na kufanikiwa kuuteka mji wa Hussar na mingine hivyo kushinda vita hiyo kiulaini.

HIVI Hapa Vyakula Nane vya Kuongeza Nguvu za Kiume Haraka..!!!

$
0
0

Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.

Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.

Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’. Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.

1. Kitunguu swaumu

Chukuwa punje 8 mpaka 10 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja. Pia hakikisha kila chakula unachopika basi kitunguu swaumu lazima kiwemo kama moja ya viungo na ukiweke mwishoni mwishoni kwamba kisiive sana katika moto wakati unapika hicho chakula.

2. Tikiti maji

Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.

3. Ugali wa dona

Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.


4. Chumvi ya mawe

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

5. Maji ya kunywa

Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

6. Mbegu za maboga

Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 100 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Ukitafuna meza vyote, hakuna cha kutemwa hapo. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako.

7. Asali na Mdalasini

Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

8. Chai ya TANGAWIZI

Tangawizi ni chakula ambacho husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini, na tangawizi zinajulikana sana kwa kusukuma damu kwenda sehemu za viungo vya uzazi yaani uke na uume. Inaweza kuliwa mbichi, au kupikwa au kuanikwa na kuwa kama unga.

Ulaji wa tangawizi mbichi nusu saa kabla ya tendo la ndoa husaidia katika kuongeza hamu na nguvu ya tendo la ndoa. Unaweza ukanywa chai ya tangawizi tu nusu saa kabla ya kuanza tendo au unaweza ukatafuna kipande cha tangawizi mbichi kwa ukubwa wa dole gumba la mtu mzima nusu saa kabla ya tendo.

Kunywa chai ya tangawizi mbichi kila siku, katika chai hiyo unayopika ndani yake weka tu maji na Tangawizi mbichi uliyosagia ndani yake (usiongeze majani ya chai humo), kumbuka tangawizi inaoshwa tu na maji na uisagie ndani ya sufuria pamoja na ganda lake la nje. Sasa badala ya kutumia sukari wewe tumia asali kwenye hii chai yako ya tangawizi na ukiitumia hivi kila siku hutachelewa kuona faida zake. Tangawizi peke yake ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!

HIVI Ndivyo Jinsi Unavyopanga Kuwa Maskini kwa Hiari Yako Mwenyewe Bila Kujijua..!!!

$
0
0

Katika hali ya kawaida, kila binadamu anaishi kwa kupanga vitu vya kufanya. Katika zoezi zima la mpango, kuna makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza ni watu waliopanga kutokuwa na mpango wowote wa maisha yao na kundi la pili ni watu waliopanga kuwa na mpango wa maisha yao.

Kundi la watu waliopanga kutokuwa na mpango, maisha yao yanategemea zaidi imani na matumaini. Kwa kawaida watu hawa wanaamini mambo yote yanapangwa na Mungu, na kwa hiyo, wao ni kufanya yale tu yanayowajia vichwani mwao kila waamkapo asubuhi.

Imekuwa ni kitu cha kawaida kusikia wengi wa kundi hili wakinena “Hata ufanyeje, Mungu kama hajapanga unajisumbua bure! huwezi kufanikiwa”. Kauli za namna hii ni za kukata tamaa ya maisha na pia yule anayeambiwa anakatishwa tamaa pia—anza kukaa mbali na wenye kutoa kauli hizi ni hatari kwa mafanikio yako.

Tabia hii ya kutokupanga aina ya matokeo unayoyataka ndiyo inayopelekea watu kuishi maisha ya kufuata upepo kama siyo mkumbo. Pia ni tabia hii inayowafanya watu kuwa na mipango ya muda mfupi na kupenda matokeo ya haraka.

Kwanini tunasema ni lazima kuwa na mpango? Kwasababu kuna vitu vikubwa viwili ambavyo vina nguvu sana katika maisha yako; navyo ni MUDA na MABADILIKO. Muda una nguvu kwasababu, utake usitake lazima muda uende na mabadiliko ni hivyo hivyo, lazima yaje utake usitake .

Njia pekee ya kuweza kuwa na mamlaka juu ya muda na mabadiliko ni wewe kuwa na mpango. Binadamu wote tumepewa uwezo wa kuweza kupanga nini cha kufanya hata kama hakijatokea.

Tofauti na wanyama wengine, wao huweza kuishi kwa kufuata matukio au hali ya wakati huo. Wanyama hawana kabisa mpango unaoweza kuwaongoza kwenda kwenye mwelekeo wa maisha wanayoyataka.

Ikitokea malisho yameisha wao uhamia sehemu nyingine na hiyo sehemu nyingine wakikuta wanyama wanaowawinda watarudi huko ambako walihama mwanzoni.

Ajabu na kweli ni kwamba watu wengi wanaishi kwa kufuata mabadiliko yanayojitokeza kwenye mazingira yao. Kikubwa hapa ni wewe kubadilika na siyo kubadilishwa na mabadiliko. Ukisubili kubadilishwa na mabadiliko maana yake mabadiliko yatakubadilisha jinsi yanavyotaka.

Yawezekana wewe unajiona uko sawa na mambo yako yanaenda vizuri, lakini ujue kuwa ukiwa na maisha ambayo huna mpango ulio katika maadishi, hapo ujue kuwa lazima ufuate kile ambacho mabadiliko yatakuletea na siyo wewe unavyotaka mabadiliko yawe. Ndiyo maana tunaambiwa kwamba ufunguo pekee wa mtu kuweza kudhibiti MUDA na MABADILIKO ni kuandika “mpango”.

Mpango maana yake ni kwamba wewe mwenyewe unapanga aina ya mafanikio unayoyataka kabla ya kuanza kuyatafuta. Mafanikio yoyote makubwa lazima upange kuyapata. Kwahiyo, tuseme kuwa mafanikio yako yapo tayari, kinachosubiliwa sasa hivi ni mpango kazi wako. Kama umepanga kutokuwa na mpango—tambua kuwa “Usipopanga kupata mafanikio, basi ujue unapanga kimya kimya kuwa masikini”.

Mpango ndio unakupa mwelekeo mzuri wa unakotakiwa kwenda. Kama wewe ndiye unayeshika upinde na mshale basi “Mpango” ndio unasaidia kuelekeza wapi mshale uende—wewe unachagua upande gani mshale upige. Athari za kutokuwa na mpango ambao unatuongoza juu ya nini cha kufanya ni pale tunapojikuta tunadhibitiwa na maisha badala ya sisi kuyadhibiti maisha.

Mpango unakupa nguvu na uwezo wa kuuamrisha muda ukufanyie nini. Ikiwa umepanga kutokuwa na mpango, basi ujue muda ndio utakupangia nini cha kufanya. Inafika kipindi fulani muda wenyewe unakulazimisha kufanya vitu ambavyo hupendi kuvifanya. Ulikuwa na nafasi ya kuamrisha muda, lakini hukuitumia, sasa ni zamu ya muda wenyewe kukuamrisha cha kufanya.

Ukiwa huna mpango unakuwa ni mtu wa kuishi kwa matumaini. Lakini kumbuka kuwa watu wengi wanaoishi kwa matumaini mara nyingi ni maskini. Kwahiyo, unahitaji mpango ambao ndio utakujengea imani ya kufanikiwa.

“Imani ni bora zaidi kuliko matumaini” jitahidi kuwa na imani juu ya mpango wako, huku ukizidi kuutekeleza kwa nguvu zako zote—hakika mafanikio uliyolenga kupata lazima yatokee tu!

Habari njema ni kwamba Mungu yupo anasubiri mpango wako ili aubariki. Mafanikio yako makubwa yapo, lakini utayapata tu endapo utaandika leo mpango wako. Ukishindwa kupanga unapanga kuwa maskini—habari ndio hiyo!.

BAADA ya Kushindwa Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki..Masha Afunguka Haya Mazito ya Moyoni..!!!!

$
0
0

Kada wa Chadema, Lawrence Masha amesema hana kinyongo na wawakilishi waliochaguliwa na Bunge kuwa wabunge wa Afrika Mashariki kupitia chama hicho kwa kuwa wote wanatoka chama kimoja na Kamati Kuu ndiyo iliyowapendekeza.

Masha amesema hayo baada ya kuulizwa maoni yake kuhusiana na uchaguzi uliofanywa na Bunge la Jamhuri ya Muungano ambao uliwachagua wanawake wawili; Josephine Lemayan na Pamela Massay kuwa miongoni mwa wabunge tisa wataoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (Eala).

“Katika chaguzi kama zile itikadi za vyama hazihitajiki. Kilichonichekesha mara ya kwanza waliturudisha kisa tuliopendekezwa na chama ni wanaume tupu, awamu ya pili walioteuliwa ni wanawake tu,” alisema Masha.

Mwanasiasa huyo alisema Watanzania walishuhudia kilichotokea na watafanya tathmini na hata kama kuna uhasama wa kisiasa katika uchaguzi ule hapakuwa wakati wake.

“Ninasisitiza sina kinyongo na kina Pamela na Josephine bali nina furaha. Nina imani nao watawakilisha vyema Eala,” alisema Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Masha ambaye aliwahi Mbunge wa Nyamagama (Mwanza) alidai kuwa CCM walicheza michezo ya kisiasa kwa kuamua kuwachagua wagombea saa chache kabla ya uchaguzi bila kusikiliza sera zao.

Akizungumzia uchaguzi huo,Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Juliana Shonza alisema ulikuwa wa huru na wa haki na watu walichaguliwa kulingana na walivyojinadi sera zao.

“Hakuna mtu aliyepangiwa kumchagua fulani.Kila mtu alipiga kura kwa mgombea anayemtaka kwa uhuru bila kushurutishwa,”

RASMI..TRA Washusha Rungu la Kodi kwa Wamachinga..Yawataka Kuanza Kulipa Kodi..!!!

$
0
0

MAMLAKA ya MapatoTanzania (TRA) imetangaza mkakati wa kuanza kuwasajili wafanyabiashara wadogo maarufu wamachinga ili waweze kutambulika na kurasimishwa rasmi.

Mkurugenzi wa Elimu Kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo, akizungumza katika semina ya waandishi wa habari jana amesema wamachinga baada ya kutambuliwa watawekewa utaratibu mzuri wa kufanya biashara zao na kuchangia mapato Kwa serikali.

Kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), amesema TRA haitozi Kodi Kwa mizigo inayosafirishwa kwenda nje ya nchi badala yake mizigo hiyo inatozwa Kwa huduma zinazofanyika nchini.

Mada zilizojadiliwa ktk semina hiyo ni Kodi ya Majengo na elimu ya Kodi Kwa anayeanza biashara.

WAKENYA, Wasomalia Wafukuzwa Tena Marekani....!!!

$
0
0

Serikali ya Marekani, wiki hii imewarudisha makwao raia watano wa Kenya na raia 67 wa Somalia kwa kukosa vigezo vya uhamiaji.

Shirika la habari la BBC limemnukuu afisa mmoja wa Serikali ya Kenya akieleza kuwa watu hao wemewasili leo katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.

Hatua hiyo ya kutimuliwa kwa raia wa nchi hizo mbili ni matokeo ya oparesheni maalum ya Marekani iliyoasisiwa na Rais Donald Trump kuwashughulikia raia wote wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria na taratibu za uhamiaji.

Hili ni kundi la pili la raia wa nchi hizo kutimuliwa kutoka Marekani. Januari 2017, raia wawili wa Kenya na raia 90 wa Somalia walitimuliwa kutoka Marekani kwa sababu za uhamiaji.

Rais wa Marekani, Trump alianza na kupigilia msumari kwa sekta ya uhamiaji nchini humo huku akitangaza marufuku ya siku 90 kwa raia wa Iran, Iraq, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen kuingia nchini humo.

UGONJWA wa Ebola Wazuka Upya Congo DRC..Tayari Watu Watatu Wameripotiwa Kufariki..!!!

$
0
0

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa ugonjwa wa Ebola umezuka katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Eugene Kabambie ni msemaji wa WHO nchini humo amesema kuwa shirika hilo limeanza kuchukua hatua baada ya watu watatu kufariki wakihisiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Pia WHO imesema mlipuko huo unaathiri maeneo ya msituni ya Aketi, katika mkoa wa Bas-Uele karibu na mpaka wa nchi hiyo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Waziri wa Afya wa DR Congo, Oly Kalenga kupitia barua, amesema kuwa watu tisa kutoka eneo la kiafya la Likati, Aketi waliohofiwa kuwa na Ebola.Watano kati yao walipimwa na mmoja wao akathibitishwa kuwa na virusi hivyo na watatu walifariki.

Mwaka 2014, mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamuhuri ya demokrasia ya Congo ulidhibitiwa kwa haraka ingawa watu 49 walifariki. Na watu waptao watu zaidi ya 11,000 walifariki kutokana na mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi 2014-2015, sana nchini Guinea, Sierra Leone na Liberia katika mlipuko wa Ebola ulioatajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kutokea duniani.

Mlipuko huo wa sasa ni wa nane kutokea nchini DR Congo tangu mwaka 1976.

STEVE Nyerere - Ukaguzi wa Vyeti Feki Upite na Bongo Movie..!!!

$
0
0

Muigizaji Steve Nyerere ameeleza kuwa, iwapo zoezi la ukaguzi wa vyeti feki lingegusa tasania ya uigiza yeye angecheka sana.

Kupitia mtandao wa instagram, ameandika ujumbe huu, “Sidhani kama hili zoezi la vyeti feki limeisha, lingekuja mpaka huku kwetu ningecheka sana, maana huku kuna makundi 2 wasaniii feki (2) na vilaza wasio jitambua hawa wote ni mzigo kwa TAIFA,”

HASIRA Tano za Lowassa kwa Serikali ya Magufuli..Habari Vichwa vya Magazetti ya Leo 14/5/2017..!!!

Shamsa Ford Awajibu Wanaodai Amemfilisi Mumewe Chid Mapenzi Baada ya Kuolewa

$
0
0

By @shamsaford

Nikiwa kama binadamu ni vibaya kuishi na kinyongo kwasababu natembea na umauti na sijui ni lini Mungu atanichukua. kiukweli mmenisononesha sana binadamu..ila kubwa kuliko vyote nimegundua kwamba watu wengi hawaitakii ndoa yangu mema. Nilipoanzana uhusiano na mume wangu wakasema tutachezeana na kuachana.Tulipooana wakasema hatutofikisha mwezi tutaachana, mitihani mingi iliyotutokea binadamu hawahawa walikuwa wanacheka.. Leo hii mnatusimanga na hayo mambo mnayopost..Nyie Binadamu mnataka nini jamani..Ni wa kwangu Mimi hata aweje ni wa kwangu mimi.Mnalotaka litutokee inshaallah kwa kudra za Mwenyezi Mungu halitatokea. Pale mnapowaza mabaya yatutokee kwenye maisha yetu na Mungu naye anapanga kutuepusha na hayo mabalaa....

Michelle Obama akosoa utawala wa Trump

$
0
0

Michelle Obama ametetea vikali mipango ya kuwapatia wanafunzi vyakula bora vyenye afya alivyopigania akiwa m,ke wa rais. 

Katika kongamano la afya mjini Washington ,aliushutumu uongozi wa rais Trump kwa kufutilia mbali viwango vya lishe bora inayolenga kuwafanya wanafunzi kuwa wenye afya nzuri. 

''Sijui kwa nini mtu anapendelea watoto kula vyakula visivyo bora'' ,alisema. 

Mmoja kati ya watoto watano nchini Marekani wanaugua ugonjwa wa kunenepa kupita kiasi, kulingana na takwimu za serikali. 

Akikosoa sera za utawala wa rais Trump, bi Obama aliwaambia waliohudhuria kongamano hilo: Hapa ndipo unafaa kuangazia kuhusu malengo ya mtu. 

Lazima ujiulize kwa nini hutaki watoto wetu kula vyakula vyenye lishe bora katika shule? Na ni kwa nini hilo liwe tatizo, kwa nini hilo liingiziwe siasa? Kunaendelea nini jamani?Aliongezea: Musinishirikishe mahala popote: nipende usinipende, fikiria kwa nini mtu anapendelea mtoto wako kula chakula kibaya. 

Kwa nini usherehekee, Kwa nini ufurahie kitu kama hicho? Kwa sababu hii hapa siri: Iwapo mtu anafanya hivyo hawatilii maanani watoto wenu.

Tatizo la Kunuka Kikwapa, Tiba Hii Hapa

$
0
0

Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa. 
Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako. 

Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo 
Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbayaVaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbayaOga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbayaKunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa.Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated soaps)Punguza kula chakula chenye viungo vingi hasa vitunguuKumbuka kutumia pafyume na Spray zitasaidia kuondoa harufu mbaya kwa muda na sio kutibu tatizo moja kwa moja.Baada ya kuoga jifute kwa taulo au kitambaa safi na usiache unyevu unyevu ambao uwavutia bakteria kukua katika eneo ili.Jitahidi kunyoa nywele za sehemu hii mara kwa mara.Epuka kukaa sehemu zenye joto kupita kiasi kwa muda mrefu.

Kisa Cha Mama Mkwe Wa Mwendo Kasi

$
0
0

“Mpaka sasa hivi bado anaendelea kukupiga?” Mama John alimuuliza mkwe wake.” Ndiyo mama tena amezidi, yaani kila siku nimekuwa kama ngoma, nimechoka Mama nibora nirudi kwetu, kwetu sijaua Mama..” Anna alaiongea huku akitokwa na machaozi. Mama mkwe wake alimuangalia kwa huruma, kisha akamuambia.

“Usiondoke mwanangu, nitaongea naye…”

“Haitasaidia chochote Mama, mara ngapi tumekaa vikao kuongea naye lakini habadiliki. Wanangu wameshakuwa wakubwa naondoka, sitaki kuendelea kuteseka…”

“Hapana usiondoke mwanangu, sasa hivi nilazima akusikilize…”. Anna alikuwa amekata tama, miaka nane ya ndoa yake ilikuwa ya mateso sana na mara kadhaa alishamlalamikia mama mkwe wake kuhusu tabia ya mumewe kumpiga lakini haikusaidia.

Kila mara mumewe alisema atajirekebisha anapokuwa mbele ya wazazi wake lakini akifika nyumbani huanza upya akimpiga  hata kwa kushitaki. Anna alishafanya mamauzi ya kuachana na mumewe, tayari alishapata chumba chake na alienda kumpa tu taarifa Mama mkwe wake ambaye walikuwa wakipatana sana.

“Wewe nenda nyumbani nitakuja huko huko kuongea naya, safari hii atanisikiliza, si bado mnafuga Kuku?” Mama mkwe wake alimuuliza swali ambalo hakuelewa kuwa lilikuwa linahusiana na nini na kupigwa kwake, lakini alijibu. “Ndiyo Mama bado tunafuga…”

Alijibu na Mama mkwe wake alimuambia kwenda nyumbani kwake na kesho yake angeenda kuwatembelea. Anna aliondoka akiwa na wasiwasi, wazo la kumuacha mumewe lilikuwa palepale, hakuwaza ni kitu gani ambacho angefanya ambacho kingemfanya kubadilisha mawazo yake.

*

Jioni ya siku iliyofuata Mama John alifika nyumbani kwa mwanae, John alikua bado hajatoka kazini na Anna alikuwa akijiandaa kupika chakula cha usiku, Mama John alimuambia mkwe wake siku hiyo anataka kupika yeye. Ingawa Anna hakutaka lakini alilazimishia mpaka akawa hana namna, aliingia jikoni na kuanza kupika akiwaambia watu wote kukaa sebuleni kuangalia TV.

John aliporejea alimkuta mkewe na watoto wakiangalia TV aliambiwa Mama yake yupo na yuko jikoni anapika, alitaka kufoka kwanini mkewe anamufanyisha kazi Mama yake ambaye alikuwa mzee lakini Mama yake alitokea na kumuambia yeye ndiyo kaamua kupika.

John alikuwa ampole kwani pamoja na ukali wake kwa mkewe lakini bado alimpenda na kumuogopa Mama yake kama mtoto. Alikaa kistaarabu sebuleni kama mkewe, Mama yake alimaliza kupika na kutenga chakula mezani, Anna na Mfanyakazi wa ndani walipotaka kumsaidia alikataa na kusema atafanya kila kitu mwenyewe.

Alitenga chakula mezani na kumpakulia kila mtu kwenye sahani kisha akawakaribisha. Ingawa haukua utaratibu kwa maana kila alikuwa akipakua chakula chake mwenyewe lakini hakuna aliyeongea, wote walifurahia chakula cha Mama.

Wakiwa wamekaa mezani baada ya sala, John alichukua kijiko na kuchota chakula, alipandisha mkono wake kukiweka mdomoni lakini kabla hajafika mdomoni Mama yake ambaye alikaa pembeni yake akimuangalia alikipiga kile kijiko chakula kikamwagika.

“Acha kula hicho chakula, chukua hiki?” Mama John aliongea huku akichukua sahani iliyokuwa na chakula cha John na kumsogezea ile ya kwake. Watu wote walishangaa kwa kile kitendo lakini Mama John hakujali, aliichukua ile sahani na kijiko alichotumia John akarudi jikoni kisha baada ya muda akarudi na sahani nyingine ambayo alikula yeye.

John aliuliza nini kinaendelea lakini Mama yake alifoka “Kula, hakuna kuongea wakati unakula! Unakuwa kama sikukufundisha nidhamu?” Mama yake alimjibu kwa sauti ya juu. Waliendelea kula  kimya kimya, hakuna aliyetaka kuongea.

*

Baada ya kumaliza kula, Mama John hakutaka mtu aguse vyombo, aliondoa vyombo mwenyewe na kuvipeleka jikoni. Kila kitu kilikuwa chakushangaza hawakujua kwanini kaamua kufanya hivyo. Baada ya kuondoa vyombo na watoto wenda kulala, ulikuwa ni wakati wa wakubwa nao kulala.

Kabla ya kwenda kulala Mama John alirudi jikoni na kuchukua sahani ya chakula, ilikuwa ni ile ambayo alimkataza mwanae kula. “Naomba mnisindikize nnje..” Aliwaambia na wao bila kujua kuwa alikua anataka kufanya nini walinyanyuka na kuongozana naye, “Uje na funguo za banda la Kuku”. Aliamrisha na Anna alienda kuchukua funguo la banda la Kuku.

Walifika katika banda la Kuku, kulikuwa na mabanda matatu, Mama John aliwaambia kufungua moja ambapo alimwaga kile chakula kwenye lile banda la Kuku ambao walianza kukimbizana, alifunga banda na kuwaambia waende wakalale. Bila kujua sababu zake za kufanya hivyo waliingia ndani kulala kila mmoja akiwa na mawazo yake.

*

Siku iliyofuata ilikua ni Alhamisi hivyo Anna na Mumewe walitakiwa kwenda kazini. Waliamka mapema na kukuta Mama mkwe kashaamka zamani na kashaandaa chai, ulikua ni mshangao kwani mara kadhaa alikuja kukaa pale na hakuwa akifanya hivyo. Aliwaandalia chai mezani na kwa mara nyingine John alipotaka kunywa alimzuia na kubadilisha kikombe.

Walimuuliza kwnaini anafanya hivyo lakini alikataa kuwajibu akiwaambia wanywe chai kwanza. Walikunywa chai na baada ya kumaliza wakati wakitaka kuondoka, aliwaambia waende kwanza kwenye banda la Kuku. Walifika na baada ya kuangalia, katika mabanda mawili hakukuwa na kitu, Kuku walikuwa salama.

Lakini katika banda lile ambalo alikua wamemwagia chakula ambalo lilikua na kuku zaidi ya kumi, wote walikuwa wamelala chini wamekufa. John na mkewe walistuka na kushangaa nini kimetokea, Mama yake aliwaangalia akiwa maetulia kwa muda kisha akasema.

“Unaona mwanangu, hicho ndiyo chakula nilichokutengea mezani jana. Nilikuwa nimeweka sumu kama ambavyo nimeweka katika chai asubuhi, kijiko kimoja tu au funda moja la chai vilitosha kukufanya kuwa kama hao Kuku hapo!” Aliongea huku akiwaangalia namna walivyokuwa wanashangaa midomo mizito hata kufunguka.

“Jana niliokoa maisha yako, lakini ningeweza kukuacha ule na subuhi ukaamka kama hao Kuku nikawaambia majirani umekufa kwa presha kama ambavyo naweza sema hawa Kuku wamekufa na kideri…

Mkeo kila siku analalamika unampiga, kila siku nakusihi acha kumpiga mkeo lakini husikii. Jana alikuja kwangu na kuniambia kuwa kachoka na anataka kuondoka, huyu ni mke mwema, wengine wanapochoka hawaondoki bali wanakuondoa wewe.

Nikuulize kitu kimoja wakati una miaka mingapi?” John alilisikia swali lakini hakuweza hata kujibu bado alikuwa ameshikwa na butwaa. “Huwezi kujibueee… mimi nakumbuka miaka 35, hembu niambie wakati unakua kuna Babu yako hata mmoja ambaye ulimuona…?

“Hapana, hata siwakumbuki…” John alijibu kinyonge kabisa.

 “Na Bibi zako…”

“Wote wapo mpaka sasa…”

“Nadhani sasa umepata jibu… chezea kila kitu lakini si mwanamke anayekupikia chakula! Usifikiri kila mwanaume anayekufa ni Mungu kapanga, wengine ni wake zao wamechoka tu kupigwa na kunyanyasika. Mke wako anaondoka kwakuwa ana kazi anajua anaweza kujihudumia, hembu jiulize kama angechoka halafu hana kazi anajua ukimuacha anaenda kuwa ombaomba…

Mimi ni Mama yako nimeona mengi, acha kujifanya mwanaume kuliko wanaume wengine, mwanaume kamili hampigi mke wake anenda kupigana na wanaume wenzake. Mimi naondoka, sitegemei kusikia umempiga mkeo tena…

Kama unataka kuendelea kumpiga basi anza kupika mwenye…” Mama John alimaliza kuongea kisha akarudi ndani akiwaacha wote wameduwaa, alichukua mfuko wake aliokuja nao na kutoka nnje kuondoka. Alirudi na kumuona mwanaea amepiga magoti akimuomba mkewe msamaha…”

Anna alikubalia kumsamehe mume wake ambaye aliahidi kutokurudia tena. John aliahidi kubadilika na kweli alibadilika, alianza kuwahi kurejea nyumbani na kurudisha mapenzi yote kama kipindi cha uchumba, hakumpiga tena mkewe na sasa ndoa yao ina miaka kumi na tano bila ugomvi wowote.

MWISHO

MREMBO Jambazi Anaswa, Auawa kwa Risas Kenyai..!!!

$
0
0

MWANAMKE aliyekuwa akidhaniwa kwamba ndiye jambazi mrembo kuliko wote katika jiji la Nairobi, Kenya, aliuawa baada ya majibizano ya risasi na Polisi katika eneo la Kayole, mchana wa jua kali katikati ya wiki.

Ilidaiwa kabla ya kuuawa, mrembo huyo alikuwa na majambazi wenzake watatu wa kiume waliokuwa wakiwapora mali wakazi wa eneo hilo.

Awali, Polisi walijulishwa na raia wema kuhusiana na mahala walipokuwa majambazi hao kabla ya kuwavamia, wakiwataka kujisalimisha.

Badala yake, majambazi hao waliwarushia risasi risasi polisi, ambao nao walilazimika kujibu mapigo, hivyo kuwauwa watuhumiwa wawili waliokuwa wakijaribu kukimbia.

Bastola iliokotwa katika eneo la tukio, ikiwa na risasi sita za mduara wa milimita 9 kila moja na miili ya wafu ilibebwa na kupelekwa katika mochwari ya jiji la Nairobi kwa uchunguzi zaidi.Ilielezwa kuwa kundi hilo hatari la majambazi halikuwa likifahamika kwa urahisi na kwamba polisi walijulishwa kupitia kundi mojawapo la kuchati la mtandao wa kijamii wa Whatsapp.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kayole, Joseph Gichangi, polisi walikuwa bado wakiwatafuta majambazi wengine wawili waliofanikiwa kukimbia na kwamba, mrembo jambazi ambaye hakumtaja jina, alikuwa ni mke wa mmoja wa watuhumiwa hao.

Ilidaiwa violevile kuwa mrembo huyo jambazi alishitukiwa na mmoja wa watumiaji wa mtandao wa kijamii, jina limehifadhiwa, kama mke wa mmoja wa majamabzi hatari katika eneo la Kayole.
(The Standard)

TANESCO Waeleza Chanzo Kukatika Umeme Mara kwa Mara..!!!

$
0
0

MVUA zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeathiri huduma za utoaji wa umeme ikiwa ni pamoja na kusababisha kukatika kwake katika maeneo ya Tabata, Tandika, Kariakoo na Mbagala jijini Dar es Salaam.

Aidha, kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara, mafundi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), walishindwa kufika kwa wakati katika maeneo yenye matatizo na hivyo kusababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, alisema katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kumekuwapo na tatizo la kukatika kwa umeme kwa  sababu hizo.

Alisema tatizo halipo katika miundombinu ya Tanesco bali ni tatizo la miundombinu kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha kushindwa kufikika kwa urahisi.

"Kumekuwapo na tatizo katika baadhi ya maeneo kukosa umeme na changamoto ya kuchelewa kurudisha huduma hiyo kwa wakati inatokana na maeneo mbalimbali kuharibiwa vibaya na mvua. Ni vyema wananchi wakatoa taarifa haraka wanapoona tatizo badala ya kuanza kulitafutia ufumbuzi wenyewe… ingawa si rahisi kufika kwa wakati kutokana na hali ya hizi mvua," alisema Dk. Mwinuka.

Meneja Utekelezaji, Simon Kihiyo, alisema wakati huu wa mvua wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari kwa kutosogelea au kushika nyaya na nguzo zilizoanguka kwa sababu zinaweza kuleta madhara zaidi.

Pia aliwataka wananchi kutoa taarifa mara tu wanapoona tatizo kwenye miundombinu ya Tanesco; kutotatua tatizo kwa njia ya mkato na kuwa makini na mifumo ya ndani ya nyumba zao.

Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji, alisema kuharibika kwa miundombinu ya maeneo ya tukio ndiko huathiri kufika kwa wakati katika maeneo yenye kuathirika.

"Kama tulikuwa tukifika eneo la tukio baada ya nusu saa basi kwa sasa tuna chukua muda mrefu kwa sababu ya hizi mvua, mafundi wanatakiwa kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara zaidi," alisema.

ADAIWA Kumuua Mumewe Baada ya Kuoa Mke wa Pili..!!!

$
0
0

MKAZI wa Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadija Mbarouk (44), anashikiliwa na polisi kwa madai ya kumuua mumewe kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. 

Mtuhumiwa huyo inadaiwa alimchoma kisu mumewake baada ya kugundua ameoa mke mwingine. 

Inadaiwa baada ya kugundua mume wake, Tani Ali Tani (41), ameoa mke mwingine, alimchoma kisu akiwa nyumbani kwa mke mdogo na kufariki dunia. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya 2:30 usiku, katika eneo la Kizimbani, Wete Pemba. 

Alisema, mwnaume huyo alijeruhiwa baada ya kuchomwa kisu na mkewe katika mguu na kutokwa na damu nyingi na kusababisha kifo chake. 

"Khadija alikwenda nyumbani kwa mke mwenziwe (mke mdogo) na kutaka kuzungumza nae na katika mazungumzo yao walianza kugombana na ndipo mwanamke huyo alipochukua hatua ya kumchoma kisu mumewe," alisema. 

Alisema kuwa, mara baada ya kujeruhiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Wete na ilipofika saa 9:00 usiku alifariki dunia, wakati akipatiwa matibabu. 
Alisema mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi na upelelezi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili. 

Aidha alisema katika tukio jengine la mauaji, polisi katika mkoa huo, inawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mtoto mchanga akiwamo mama na baba mzazi wa mtoto huyo akiwamo bibi wa mtoto huyo. 

Aliwataja wanaotuhumiwa kuwa ni Riziki Juma (19), mama mzazi wa mtoto, Khamis Hamad Ali (25), baba mazazi na Chumu Matari (bibi wa mtoto). 

Kamanda Haji alisema, tukio hilo lilitokea saa 2.00 usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya kudaiwa kumuua mtoto huyo kumtupa katika msitu wa mjini Wingwi, Wilaya ya Micheweni Pemba. Inadaiwa watuhumiwa walitumia kitu chenye ncha kali kumuua mtoto huyo mara baada ya kuzaliwa. 

Alisema polisi ilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema na kuchukua hatua za kuwatia mbaroni. 

Aidha, inadaiwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa lengo la kuficha aibu, kwa madai mama wa mtoto huyo alijifungua ndani ya wiki baada ya kuolewa mwezi uliopita, mwaka huu. 

MULUGO, Mbatia Waichana Serikali Bungeni..!!!

$
0
0

Mbunge wa Songwe (CCM), Philipo Mulugo amesema kitendo cha Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi kuchapisha vitabu vyenye makosa kinaitia doa Serikali na kutaka watalaamu waliopo katika Taasisi ya Elimu (TIE) waangaliwe.

Akichangia bajeti ya wizara hiyo, alisema uchunguzi wake umebaini madudu mengi.

“Suala la vitabu unaweza ukalia, nimefanya uchunguzi wa vitabu ni hatari na aibu ya dunia,” alisema naibu waziri huyo wa elimu wa zamani na kuongeza:

“Kuna mambo mengine lazima tuseme Serikali ni ya kwangu, nchi ya kwangu, hatuwezi kufumbia macho.”

Naye Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia alisema Serikali ni lazima ichukue hatua dhidi ya watu ambao wanataka kuangusha elimu nchini, kwani bila vitabu bora ni vigumu kufikia malengo ya kuondoa ujinga nchini.

“Tatizo kubwa la elimu nchi hii linaanzia bungeni, tusitumie wingi wa itikadi zetu kuliua Taifa hili. Inatia uchungu kila Waziri anayeingia kwenye Wizara hiyo yeye ndio sera, mitaala na kila kitu,”alisema.

Aliongeza kuwa kama Bunge haliwezi kuisimamia Serikali ipasavyo, taifa haliwezi kufanya vizuri kielimu.

“Mwaka jana tulizungumza kuhusu vitabu, udhibiti wa vitabu ukapelekwa Taasisi ya Elimu, leo hii Serikali ya Awamu ya Tano inaandika kitabu cha Kiingereza darasa la tatu hapa juu penyewe tu pameandikwa ‘I learn English Language’ ndiyo kodi tunazopitisha zinaandika vitabu hivi?” alihoji.




BAADA ya Kitwanga Kudai Kuwa Ataenda Kuharibu Mitambo ya Maji..Waziri wa Maji Amemjibu Haya..!!!

$
0
0

Kauli ya Mbunge wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga kuwa kama Serikali haitashughulikia kilio cha maji jimboni kwake atahamasisha wananchi kubomoa mashine ya Ihelele, imejibiwa.

Aliyetoa majibu hayo ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Gerson Lwenge aliyeanza kwa kuhoji iwapo alichosema Kitwanga alitumwa na wapigakura wake.

“Sasa nataka nimuulize Kitwanga kama yupo hapa kwamba hayo ni maneno yake au ya wananchi? Kama ni ya wananchi nitawaambia nini kimefanyika Misungwi kwani hata juzi tumesaini mikataba ya maji na mwenyekiti wa halmashauri alikuwepo ya kupeleka maji Misungwi kutoka Ziwa Victoria kwa fedha nyingi zaidi ya Sh38 bilioni,” alisema.

Lwenge akasema haoni sababu za Kitwanga kushupalia kuharibu miundombinu ya maji kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano imemfanyia mambo makubwa jimboni kwake.

Katika mchango wake, Kitwanga alihoji Serikali kutoshughulikia ipasavyo kilio cha maji kwa wananchi wake na kwamba, fedha ilizotenga kwa ajili ya miradi ya maji ni chache.

“Kwa hiyo, nitakachokifanya safari hii sitatoa shilingi kwenye bajeti, bali nitakwenda kuwahamasisha wananchi wa Misungwi wapatao 10,000, twende tukazime mtambo katika kile chanzo cha maji ili wote tukose,” alisema mbunge huyo.

Pia, Kitwanga alishutumu kuwa kuna mpango wa kumuandaa Bashite kuwa mbunge wa Misungwi.


KUTANA na Mtabibu Ostadhi Khamisi Kutoka Mombasa Kenya Kwasasa Yupo Tanzania Kwa Ajili yako

$
0
0
Kutana na ostadhi khamisi kutoka mombasa Kenya kwa sasa yupo Tanzania ni mtabibu na mtafiti Wadawa za asili anatibia kama vile:
Miguu kuuma
Miguu kufagazi
Miguu kuwakamoto
Chango lauzazi kwakina mama
Dawa ya uzazi wakina mama inapatikana
Kusafisha nyota ili uwe namuonekano kwa kila mtu
Kumrudisha mpenzi wako na liekukimbia ndani yasiku 3 bila yapingamizi yoyote
Kumshika mume au mke asitoke nnje ya ndoa
Pata pete ya Bahati inayo endana na nyota yako
Kurudisha mali ilipotea au kudhurumiwa ndani yasiku 3
Pata utajili usiokuwa namashaliti yoyote
Dawa za nguvu za kiume
Dawa ya biashara inapatikana
Dawa ya kuzuia chuma ulete kwenye biashara inapatikana
 Zindiko la nyumba au shamba
 Anatuliza familia zinazogombana DUWA pamoja navisomo vya ufunguzi wa mwili wako njoo ufunguliwe vifungo ulivyo fungwa kutana na ostadhi khamisi utimiziwe ahadi ulizo hadiwa acha kuteseka acha kuhangaika ostadh khamisi yupupo tanzania kwajili yako...

Call +255718746825 +255754765246 kwa what'sapp +255783708487

KIMENUKA Simba...MO Dewji Ataka Kurudishiwa Mamilioni ya Pesa Aliyowapa

$
0
0
Ikiwa ni siku mbili tu zimepita baada ya Simba kutiliana saini kandarasi ya udhamini na kampuni ya SportPesa, mdau wa klabu hiyo Mohammed ‘MO’ Dewji amekuja juu na kutaka kurejeshewa fedha zake TZS 1.4 bilioni baada ya klabu hiyo kuvunja makubaliano waliyokuwa wameafiki.

MO amesema kuwa anataka kulipwa fedha hizo ambazo alizitumia kuwalipa mishahara wachezaji wa Simba tangu mwaka jana.

Uamuzi huu ameutoa baada ya klabu hiyo kuingia makubalino ya udhamini na kampuni ya SportPesa pasi na kumshirikisha yeye ikiwa ni kinyume na makubaliano.



Mei 12, 2017, uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva, ulisaini kandarasi ya udhamini wa miaka mitano na Kampuni ya SportPesa yenye thamani ya Sh. 4.9 bilioni.

Katiba barua aliyoandika MO, amesema kuwa Simba wamekiuka makubaliano waliyokuwa wamefikia kwamba, atoe fedha kwa makubaliaono ya kuingia kwenye mfumo wa hisa, na ikitokea kampuni inataka kuidhamini Simba, inabidi wakae meza moja viongozi na yeye na hiyo kampuni ili hiyo kampuni itambue mwelekeo wa Simba. Lakini katika kandarasi ya SportPesa, MO amesema hakushirikishwa.

Simba tayari ilishaanza mchakato wa marekebisho ya katiba yao ili kuruhusu kipengele cha uwekezaji kwa mfumo wa hisa kama lilivyokua ombi la MO kuwekeza katika klabu hiyo kwa asilimia 51 za hisa huku wanachama wakibaki na hasilimia 49.
Viewing all 104776 articles
Browse latest View live




Latest Images