Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi Nyingi za Kazi Zilizotangazwa Wiki Hiii

$
0
0

FAIZA Ally Akumbushia Enzi za Mapenzi ya Mbunge Sugu

$
0
0
Mwigizaji Faiza Ally ameleza jinsi mahusaino ya kimapenzi yalivyokuwa yanamsumbua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita hali iliyopelekea yeye kuugua mara kwa mara.

Kupitia instagram Faiza amepost picha akiwa kitandani na kuandika, ‘‘Kuna mambo sasa hivi nikiangalia nacheka sana … haya mapenzi jamani, hapo ni miaka mitatu iliyopita nilikuaga namlilia Baba Sasha mpaka natundikiwa drip halafu narusha Facebook picha ili anione labda atanihurumia au tu ataniuliza unaendeleaje nimsikie tu lakini wapi inakua holaaaaa.


Picha aliyopost

“Pamoja na yote sijawahigi kujuta kumpenda na sijawahi kuacha kumpenda #throwback about 3 years ago…. asante facebook kwa kumbukumbu ambazo kwa wakati huo ilikua ni uchungu lakini kwa sasa imekuwa nikichekesho kwangu, simcheki mtu akililia mapenzi yake maana najua vile ana feel … mapenzi ya kweli hayafi,” aliandika Faiza.

UONGOZI Mpya wa Young Dee Wadai Yound Dee Hatumii Madawa ya Kulevya

$
0
0
Baada ya uongozi wa zamani wa Young Dee ‘MDB’, kudai waliachana na rapa huyo baada ya kurudia kutumia dawa ya kulevya, uongozi mpya wa msanii huyo, King Cash umedai umemchunguza rapa huyo kwa miezi 5 na kugundua hatumii dawa hizo hatari kama baadhi ya watu wanavyodai.


Akiongea na Bongo5 Jumamosi hii msemaji wa label hiyo, King Maarifa, amedai wao hawawezi kumchukua mtu ambaye anatumia dawa za kulevya na kufanya naye kazi.

“Tumezisikia hizo tuhuma juu ya msanii wetu na sisi tumezipokea kwa namna mbili, moja sisi kama sisi tunajua Young Dee aliacha kutumia dawa za kulevya na baada ya sisi kuhitaji kufanya naye kazi tulimchunguza vizuri kwa kipindi cha miezi 5 na tumejiridhisha hatumii tena. Sisi tunachokijua Young Dee na uongozi wake uliopita walishindwa kuhafikiana baadhi ya mambo, hayo mambo ya dawa za kulevya ndio kwanza tunayasikia kwake,”


Aliongeza,
“Sisi tumeingia kwenye hii biashara kwa miguu miwili. Kwa hiyo tunavyomsikia mtu akiizungumzia vibaya brand yetu kamwe hatuwezi kukaa kimya, tunaomba aachane na hayo mambo, hatutaki kufikishana mbali zaidi kwa sababu tayari ameshatoka kwake. Pia sisi mwanzo tulijua kwamba baada ya kusikia tumesaini naye atakuja kutoa mikataba kueleza kwamba ana mkataba na Young Dee, sasa tunaposikia hizo tuhuma tunaanza kupata shaka sana juu ya hizo kauli zake,”

Hapo awali Young Dee akizungumza na Clouds FM, alidai aliondoka katika uongozi huo baada ya meneja wake huyo kutembea na mpenzi wake aitwae Tunda.

Hata hivyo meneja wa label hiyo, Max Rioba alikanusha taarifa hizo nakudai aliachana na rapa huyo baada ya kurudia kutumia dawa za kulevya.

Mwaka uliopita rapa Young Dee mbele ya waandishi wa habari alitangaza kuacha kutumia dawa za kulevya baada ya kutumia kwa kipindi cha miaka 2.

Mke adaiwa Kumuua Mumewe Baada ya Kuoa Mke wa Pili

$
0
0

MKAZI wa Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Khadija Mbarouk (44), anashikiliwa na polisi kwa madai ya kumuua mumewe kwa sababu zilizoelezwa kuwa ni wivu wa kimapenzi. 

Mtuhumiwa huyo inadaiwa alimchoma kisu mumewake baada ya kugundua ameoa mke mwingine. 

Inadaiwa baada ya kugundua mume wake, Tani Ali Tani (41), ameoa mke mwingine, alimchoma kisu akiwa nyumbani kwa mke mdogo na kufariki dunia. 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema tukio hilo limetokea juzi majira ya 2:30 usiku, katika eneo la Kizimbani, Wete Pemba. 

Alisema, mwnaume huyo alijeruhiwa baada ya kuchomwa kisu na mkewe katika mguu na kutokwa na damu nyingi na kusababisha kifo chake. 

"Khadija alikwenda nyumbani kwa mke mwenziwe (mke mdogo) na kutaka kuzungumza nae na katika mazungumzo yao walianza kugombana na ndipo mwanamke huyo alipochukua hatua ya kumchoma kisu mumewe," alisema. 

Alisema kuwa, mara baada ya kujeruhiwa alikimbizwa katika Hospitali ya Wete na ilipofika saa 9:00 usiku alifariki dunia, wakati akipatiwa matibabu. 
Alisema mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi na upelelezi utakapokamilika, atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili. 

Aidha alisema katika tukio jengine la mauaji, polisi katika mkoa huo, inawashikilia watu watatu wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mtoto mchanga akiwamo mama na baba mzazi wa mtoto huyo akiwamo bibi wa mtoto huyo. 

Aliwataja wanaotuhumiwa kuwa ni Riziki Juma (19), mama mzazi wa mtoto, Khamis Hamad Ali (25), baba mazazi na Chumu Matari (bibi wa mtoto). 

Kamanda Haji alisema, tukio hilo lilitokea saa 2.00 usiku wa kuamkia Ijumaa baada ya kudaiwa kumuua mtoto huyo kumtupa katika msitu wa mjini Wingwi, Wilaya ya Micheweni Pemba. Inadaiwa watuhumiwa walitumia kitu chenye ncha kali kumuua mtoto huyo mara baada ya kuzaliwa. 

Alisema polisi ilipata taarifa hizo kutoka kwa raia wema na kuchukua hatua za kuwatia mbaroni. 

Aidha, inadaiwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa lengo la kuficha aibu, kwa madai mama wa mtoto huyo alijifungua ndani ya wiki baada ya kuolewa mwezi uliopita, mwaka huu.

Kabla Ya Kuamua Kumchunguza Mwenza Wako Hakikisha Una Ubavu Wa Kumuacha

$
0
0

Kuna watu utakuta mume au mke akiweka simu tu chini wanaanza kuchunguza, kuangalia sms, wakikosa waaangalia simu zilizopigwa na wakiokosa huanza kuchambua majina ya jinsia tofauti yaliyopo katika simu za wapenzi wao.

Lakini hawaishii hapo, wakimuona tu mwenza na mtu wa jinsia tofauti hunza kupaniki na kutafuta namna ya kumfumania. Wewe endelea tu kutafuta na kumfuatilia, utapata unachokitaka, lakini swali linakuja ukishapata?

Unapomfumania mwenza wako unakuwa umejithibitishia kua hauko peke yako, utataka kuombwa msamaha na kutaka mwenza wako abadilike? Lakini hembu kabla hujaanza kumchunguza jiulize, hivi ukamfumania, akakataa kuomba msamaha au akaomba lakini akagoma kumuacha huyo anayechepuka naye utafanyaje?

Je upo tayari kuondoka na kumuacha? Kama jibu ni ndiyo endelea kumfuatilia lakini kama jibu ni hapana basi acha kabisa. Utajiumiza bure na kwakuwa utakuwa ushamfumania na kumsamehe bila hata kuombwa msamaha basi utakuwa umempa tiketi ya kuendelea naye.

Iko hivi mwanzoni alikuwa akichepuka kistaarabu, akijificha kwakuwa hujui. Lakini ukishamfumania akakuambia hayuko tayari kumuacha na wewe ukakomaa naye basi nisawa na umemruhusu, kwani hataogopa tena kufumaniwa mara ya pili.

Kwa maana hiyo wewe utaendelea kuumia na kila mara akitoka utajua yuko kwa fulani. Kama huna ubavu wa kumuacha hembu acha kumfuatilia maana utajiumiza bure, mfuatilie mtu kama unataka kumuacha zaidi utakuwa unahalalisha mke au mume mwenza tu.

MAPYA Yafichuka Ajali Iliyoua Wanafunzi 33 Arusha..!!!

$
0
0

SIRI mpya ya ajali iliyotokea wiki iliyopita na kusababisha vifo vya wanafunzi 33 wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Lucky Vincent, walimu wao wawili na dereva mmoja wa basi, imefichuka baada ya mmiliki wake, Innocent Mushi, kufikishwa mahakamani.

Mushi alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana na kutuhumiwa kutenda makosa manne ya usalama barabarani, yanayodaiwa kusababisha ajali hiyo iliyotokea Mei 6, mwaka huu, baada ya basi walilopanda wanafunzi na walimu wao kutumbukia kwenye korongo lililopo Marera, eneo la Rotia, Wilaya ya Karatu, mkoani Arusha.

Mushi na mtuhumiwa mwenzake, ambaye ni Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule hiyo, Longino Nkana, walifunguliwa kesi na 78 ya mwaka huu na wanatuhumiwa kwa makosa hayo, likiwamo la kusafirisha watoto bila kuwa na vibali muhimu.

Akiwasomea mashitaka yao mjini hapa mbele ya Hakimu Mkazi Desdery Kamugisha, Wakili wa Serikali, Rose Sule, alidai Mushi, ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza, anakabiliwa na makosa manne, wakati Nkana akituhumiwa kwa kosa moja.

Sule alidai kwamba, Mushi akiwa mkurugenzi wa shule hiyo anatuhumiwa kumiliki gari la abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji.

Alidai kuwa Mei 6, mwaka huu, katika eneo la Kwamrombo, wilayani Arusha, mtuhumiwa huyo alifanya shughuli ya usafirishaji wa abiria akiwa anamiliki gari aina ya Mitsubishi Rossa, lenye namba za usajili T871 BYS.

Aliendelea kudai mahakamani hapo kuwa kosa la pili linalomkabili ni la kuruhusu kuendeshwa kwa gari bila kuwa na bima (road license) ambapo Mei 6, mwaka huu, aliruhusu gari hilo kuendeshwa huku akijua halina bima.

“Kosa la tatu ni kushindwa kuingia mkataba na mwajiri wake, ambapo Mei 6, mwaka huu, ukiwa mmiliki wa gari hilo ulishindwa kuingia mkataba wa ajira na dereva wako, Dismas Gasper, ambaye kwa sasa ni marehemu,” alidai Sule, alipokuwa akisoma mashitaka na kuongeza:

“Mtuhumiwa unakabiliwa na kosa la nne ambalo ni la kubeba abiria waliozidi zaidi ya 13 ambapo Mei 6, mwaka huu ukiwa mkurugenzi, ofisa msafirishaji na mmiliki wa Lucky Vincent, ulibeba na kusafirisha abiria zaidi ya 13, kinyume cha sheria.”

Akisoma mashitaka kwa mtuhumiwa wa pili, Sule alidai mahakamani hapo kuwa, Nkana anadaiwa kuandaa safari iliyozidi abiria 13, huku akijua ni kinyume cha sheria.

Alidai kuwa Mei 6, mwaka huu, mtuhumiwa huyo akiwa na nafasi ya mwalimu mkuu msaidizi wa shule hiyo na mwandaaji wa safari aliruhusu kupakia abiria zaidi ya 13 katika gari lililosababisha vifo vya watu.

Kwa upande wake, Wakili Method Kimomogolo, anayewawakilisha watuhumiwa mahakamani hapo, aliiomba mahakama hiyo kuwapa dhamana wateja wake na Sule hakuwa na pingamizi dhidi ya ombi hilo.

Akitoa masharti baada ya kuzisikiliza pande zote mbili, Hakimu Kamugisha alisema washtakiwa hao watatakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaotakiwa kutimiza masharti.

“Mnatakiwa kuwa na wadhamini wawili kila mmoja watakaosaini dhamana ya shilingi milioni 15. Watuhumiwa mtatakiwa kuwasilisha hati zenu za kusafiria, lakini pia hamtakiwi kuondoka nchini na ndani ya mkoa bila ruhusa ya mahakama,” alisema Kamugisha.

Watuhumiwa wote wawili walifanikiwa kutimiza masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo na kesi hiyo sasa itatajwa Juni 8, mwaka huu.

UKWELI Mchungu..Linna Acha Kuigeuza Bongo Kuwa Marekani..!!!

$
0
0

Na JOSEPH SHALUWA

NAMFAHAMU Linna Sanga, mmoja wa wasanii mwenye uwezo mkubwa kwenye Bongo Fleva. Linna yumo kwenye listi yangu ya wasanii wa kike wanaojua wanachokifanya wakishika kipaza sauti.

Sina shaka hata kidogo na namna anavyoweza kucheza na sauti yake awapo jukwaani. Anaijua sauti yake ya dhahabu ilivyo, hivyo anaitumia vyema.

Ni miongoni mwa wasanii wachache wa rika lake, waliotoka pamoja na wakaendelea kuwepo kileleni hadi leo. Huwezi kusema amechuja! Utapigwa mawe. Ni msanii mkali, anayejua kujiongeza.

Kwa sasa msanii huyu mwenye figa bomba na kiuno chepesi awapo jukwaani, anapiga mzigo chini ya Kampuni ya Drops Up Entertainment ya jijini Dar es Salaam.

Singo yake ‘Raha Jipe Mwenyewe’ inadhihirisha namna anavyozidi kukua na kuujua muziki vizuri zaidi. Kwa maneno mengine, Linna anathibitisha ni kwa namna gani wasanii waliopitia THT walivyo bora na wanaojua muziki.

Niseme tu kwa kifupi na kwa lugha iliyonyooka, Linna ni msanii mzuri, mwenye kujua kipaji chake na kukitumia sawasawa. Vijana wa sasa tunasema, anakitendea haki.



SIDE B YAKE SASA

Side B ya Linna inaanza kuharibu heshima yake kwa jamii. Linna mwenye sifa zote nilizotaja, ameondoa utu wake na kufanya jambo la kipuuzi, akiigia Wazungu ambao tamaduni zetu na zao ni tofauti.

Sitaki kuzungumzia sana kuhusu historia yake ya mahusiano, lakini naweza kusema kuwa hana sifa mbaya inayoweza kumuweka kwenye kundi la wasichana wasiojielewa.

Amekuwa akijiheshimu na kutulia na anayekuwa naye kwenye uhusiano, tena kwa uwazi kabisa. Siyo msichana waluwalu kwenye uhusiano. Kwa sasa anatoka na mkurugenzi wa Drops Up Entertainment, inayosimamia kazi zake.

Tatizo ni baada ya uhusiano wake wa sasa kuzaa kitu cha tofauti na uhusiano mwingine aliopitia huko nyuma. Linna ni mjamzito.

Aliwahi kusema kuwa anajisikia fahari kupata ujauzito na kwamba ni kitu alichokuwa akikisubiria kwa muda mrefu – swadakta kabisa!

Lakini tatizo ni pale alipoanza kusambaza picha zinazomwonyesha baadhi ya sehemu za siri za mwili wake. Upuuzi huu nani alimshauri?

Namfahamu Linna, nimewahi kukutana naye mara kadhaa kikazi na hata kirafiki. Siyo jambo la ajabu kwa kazi yangu, lakini kwa hili sina haja ya kukupesa macho, namweleza kwa uwazi kabisa amebugi!

Kuacha tumbo nje, kuvaa kanguo ka ndani tu na kutundika picha kwenye mitandao ni kujidhalilisha. Ni kuwavunjia heshima wazazi wake na ndugu zake.

Ni kuwakebehi mashabiki wake. Ni ujumbe mbaya kwa jamii. Linna mwenye historia nzuri hata ya makuzi yake kiimani, anawezaje kufanya ujinga wa namna hii?

Tangu lini Watanzania tukawa hivyo? Mwili wa mwanamke wa Kiafrika husitiriwa. Mwanamke wa Kitanzania asili yake ni kujihifadhi, siyo kuonyesha sehemu zake za kujihifadhi hadharani.

Katika hili Linna amepotoka na anastahili kuomba radhi kwa wadau wake ambao kwa muda mrefu wamemuheshimu na kumuunga mkono kwenye shughuli zake za muziki.



ANANGWA MITANDAONI

Wadau walipoona picha za staa huyo, wakamnyoosha! Wakamkumbusha kuwa siyo sahihi kwa kueleza maoni yao. Wengi wameonyesha hasira zao, kwamba alichofanya siyo sahihi.

Tatizo ni namna alivyopokea. Akiwajibu mashabiki wake, Linna alisema eti alichofanya ni jambo la kawaida na kwamba yeye si wa kwanza kufanya hivyo.

Eti kwa Linna, kuanika tumbo na kutokea akiwa na nguo ya ndani nje ni Uafrika! Eti kwa sababu picha zenyewe zina mwonekano wa weusi zaidi ni jambo linalomwakilisha Mwafrika.

Maajabu haya! Mwafrika anakaa utupu? Leo hii Linna anataka kuturudisha nyuma, eti anasema asili ya Mwafrika ni kuvaa majani au ngozi sehemu ya mbele tu! Anakwenda mbali zaidi akidai kuwa eti kufunika mwili mzima ni utamaduni wa Wazungu.

Amesisitiza aachwe kwa sababu alichokifanya ni maisha yake na maamuzi yake binafsi. Namwambia wazi kuwa, hajafanya sawasawa na kama anadhani ni maisha yake binafsi basi aachane na muziki.

Kwa taarifa yake, yeye ni mali ya jamii nzima, ni kioo. Jamii inajifunza na kumwangalia yeye. Akikosea lazima aambiwe ukweli.

Kama ni akili yake, ajue alikengeuka na kama alishauriwa basi mshauri wake hakuwa sahihi. Kubwa zaidi na la muhimu kwake, afahamu kuwa mstaarabu akikosea huomba msamaha.

Ustaa siyo kujiachia hovyo. Si kila wanachofanya akina Kim Kardashian na wasanii wetu wa Bongo mfanye. Vingine angalia, kisha endelea na maisha yako ya kibongobongo.

Ni ngumu kuifananisha Bongo na Marekani. Kila kitu tupo tofauti. Nasema kila kitu. Ni kama walivyo tofauti Linna Sanga na Selena Gomez.

Linna badili mtazamo mdogo wangu, vinginevyo mashabiki  waliokupandisha, haohao wanaweza kukushusha wakati wowote. Kazi kwako.

KAULI ya Rais Mstaafu Benjamin Mkapa Kuhusu Serikali ya Awamu ya Tano Kubana Uhuru wa Habari..!!!

$
0
0

Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mzee Benjamin Mkapa amevikosoa vyombo vya habari barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahari kwa kile alichosema vingi vimejikita katika kuripoti habari za kisiasa na matukio ya nani kafanya nini au kawa nani, badala ya kuripoti habari za uchumi za kuwasaidia wananchi.

Mzee Mkapa aliyasema hayo alipokuwa akifanya mahijiano na na Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle (DW) ya nchini Ujerumani ambapo alisema kwenye vyombo vya habari vya Afrika kuna upungufu mkubwa wa wa habari za uchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina.

“Tatizo moja kubwa la vyombo vya habari vya nchi za Afrika hasa hasa Kusini mwa Jangwa la Sahara ni kwamba habari nyingi zinazopewa kipaumbele ni zile za kisiasa na zinazohusu nani ni nani na kafanya nini.”

“Kuna upungufu mkubwa wa habari za kiuchumi na maendeleo zilizofanyiwa utafiti wa kina na zinazochochea maendeleo. Kuna habari kidogo sana za utetezi wa kimaendeleo na kujipanga ili tupige hatua.”

Kufuatia hali hiyo, Mzee Mkapa alisema kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaodaiwa kuwa umebanwa, unahusu vyombo vya habari ambavyo havina mchango kwenye maendeleo ya uchumi wetu zaidi ya kuzungumzia matokeo badala ya uchambuzi.

“Kwa hiyo, huo uhuru wa vyombo vya habari unaosema unabanwa unahusu kundi la vyombo vya habari ambavyo havina mchango wowote katika uchambuzi wa masuala ya uchumi utetezi wa maendeleo wala kwenye kujipanga kujitafutia maendeleo. Nasi ni taifa masikini linalohitaji kuendelea. Nadhani ni uamuzi sahihi.”  alisema Mzee Mkapa.

Kauli hii ya Mzee Mkapa ilikuja baada ya kuulizwa kuhusu madai ya kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inabana uhuru wa vyombo vya habari hali ambayo haikuwapo miaka ya nyuma.

TRA Yafafanua Kuhusu Msanii Diamond Kudaiwa Kodi ya Milioni 400..!!!

$
0
0

Mkurugenzi wa  Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.

Hayo ameyasema jana Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi anayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahati nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. 

VYAKULA Vinne vya Kuongeza Hamu ya Tendo la Ndoa kwa Wanawake..!!!

$
0
0

Wanawake wengi wanaokaribia ukomo wa hedhi au waliokoma hedhi tayari(menopause) hukosa hamu ya tendo la ndoa.

Wataalamu wa afya wameshauri vyakula vinavyoweza kuwapa wanawake hamu  ya tendo la ndoa.

Mtaalamu wa Saikolojia wa Uingereza, Cassie Bjork, anasema badala ya kutumia dawa (Viagra) vya kuongeza hamu ya tendo la ndoa kuna vyakula maalum.

Spinachi

Wataalamu hao wanasema mboga ya majani aina ya spinachi ina wingi wa madini ya magnesium ambayo husaidia kusambaza damu kwenye mirija. Damu inaposambaa vyema mwilini hata hamu ya tendo la ndoa huongezeka.

Bjork anasema kula kwa wingi mboga hizo kunamsaidia mwanamke hata kufikia kilele.

Chai ya Kijani (Green tea)

Chai ya kijani ina kompaundi iitwayo catechins. Hii inaelezwa kuwa inasaidia kuyeyusha mafuta mwilini. Lakini pia inalisaidia ini  kuchuja sumu na kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri. Damu ikitembea vyema mwilini, ni rahisi kwa mwanamke kujisikia hamu ya tendo.

 Mafuta ya samaki

 Zipo aina nyingi za mafuta ya samaki. Lakini mafuta ya samaki wenye asidi ya Omega-3 yana virutubisho ambavyo huongeza kiwango cha ‘dopamine’ kwenye ubongo.

 Dopamine ni eneo la ubongo linalofanya kazi ya kudhibiti faraja na hisia.  Kama dopamine itaongezeka basi mwanamke hujisikia kuridhika anapokuwa na mwenza wake.

Chokoleti

 Pamoja na utamu wake, lakini ‘chocolate’ ina virutubisho na madini ya magnesium ambayo humfanya mwanamke kuridhika. Pia huufanya ubongo wa mwanamke kutulia kwa kuondoa msongo wa mawazo. Msongo wa mawazo ukiisha ni rahisi kwa mwanamke kupata hamu ya tendo la ndoa.

Mambo matano yanayompa hasira Lowasa kwa Serikali

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomkasirisha ambayo yanafanywa na Serikali huku akiionya CCM kuwa ipo siku upinzani utatawala. 

Lowassa aliyataja mambo yanayomkera kuwa ni pamoja na kuzuiwa kwa kongamano la kujadili demokrasia ambalo lilipangwa kufanyika jana, sakata la vyeti feki na Serikali kukaa kimya kuhusu mafuriko. 

Mengine ni kupaa kwa bei za vyakula na Rais John Magufuli kutohudhuria tukio la kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali ya Karatu, Arusha. 

Waziri Mkuu huyo wa zamani, alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni wilayani Kinondoni. 

Juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Demokrasia lililoandaliwa na Chadema, Makongoro Mahanga alitangaza kuwa lingefanyika jana katika Ukumbi wa Arnatouglou, Ilala na wanasiasa wakiwamo viongozi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali wangeshiriki. 

Hata hivyo, siku hiyohiyo jioni, CCM ilitoa taarifa ya kukanusha viongozi wake kualikwa katika kongamano hilo. 

Sinema iliendelea jana asubuhi wakati Chadema walipotoa taarifa kwa vyombo vya habari wakieleza kuwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam umewazuia kutumia ukumbi huo uliopo Mnazi Mmoja. 

Akizungumzia zuio hilo, Lowassa alisema amesikitishwa na kitendo hicho alichodai kimefanywa na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam. 

“Tunalaani kitendo hiki kwa lugha inayowezekana, hatua hii ni ya kuminya demokrasia. Nia yetu ilikuwa njema ya kuzungumzia demokrasia. 

“Waandaaji wa kongamano hili waliweka picha yangu na ya Kinana (Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM) tukionekana tumepeana vichwa lakini tuki- smile (tukitabasamu) jambo ambalo ni very important (muhimu),” alisema Lowassa. 

Picha iliyotumika katika tangazo hilo la kuhamasisha kongamano ni ya Kinana na Lowassa wakionekana kuzungumza kwa kunong’ona walipokutana katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mei 8 katika tukio la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva waliofariki dunia katika ajali ya basi Mei 6. 

Lowassa alisema Tanzania ni moja na watu ni walewale hivyo hakuna tofauti kwa watu wa CCM na Chadema na kwamba kila mmoja kuwa na maoni tofauti hakuna dhambi. 

Hata hivyo, Lowassa aliwataka CCM kutambua kuwa ipo siku nchi ya Tanzania itatawaliwa na watu (chama) wengine na siyo wao. 

“Kama watashindwa kuondoka wakati wetu, wataondoka wakati wa wajukuu wetu,” alisema. 

Alieleza kuwa vyama vya ukombozi duniani vimebaki vichache na katika Afrika anadhani vipo ANC cha Afrika Kusini na CCM, hivyo huo ni ujumbe tosha kwamba ipo siku wataondoka madarakani. Alisema kitendo cha kuwanyanyasa watu kwa sababu wapo upinzani siyo jambo zuri na ni kuminya demokrasia na kushangaa kwa nini halikemewi. 

“Waasisi wa Taifa hili wanapaswa kukemea, ndiyo maana tulialika kila mtu katika kongamano lile ili watuambie kwenye demokrasia Chadema mnakosea moja hadi tatu ili tujirekebishe. CCM inakosea hivi na mwisho mnakubaliana cha kufanya,” alisema Lowassa, “Ninalaani kwa nguvu zote kitendo kilichofanywa na Serikali ya Dar es Salaam tusifikishane hapa.” 

Kuhusu mafuriko, 

Lowassa aliitaja kero nyingine kuwa ni kutoshughulikiwa ipasavyo kwa athari ya mafuriko yanayoyakumba maeneo mbalimbali nchini. 

Alieleza masikitiko yake kuwa haoni mkono wa Serikali katika mafuriko hayo ikiwamo kuwapa matumaini wananchi au kiongozi yeyote wa Serikali kuonekana akiwafariji waliofikwa na adha hiyo. 

“Nawasifu na kuwapongeza wabunge jana (juzi) waliosimama na kutaka hoja hii ijadiliwe. Nadhani ni muhimu kujadiliwa na kuelezana ili Serikali ijue inafanya nini,” alisema Lowassa. 

Bei za vyakula 
Mbali na hilo, Lowassa alisema bei za vyakula zimezidi kupanda na wananchi wanapata tabu na kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, mahindi yapo juu kuliko mchele. 

“Everything (kila kitu) bei juu. That is problem (hili ni tatizo ) Serikali itaenda kufanya nini katika hili?” alihoji Lowassa. 

Alisema binadamu anaishi kwa matumaini, hivyo alitaka kujua wananchi wa vijijini wanapewa matumaini gani kutokana na hali hiyo. Aliiomba Serikali kutangaza na kuchukua hatua za kusaidia upatikanaji wa chakula na mambo mengine ili kuwasaidia Watanzania. 

Sakata la vyeti 
Kadhalika, Lowassa alizungumzia sakata la watumishi 9,932 wa umma wenye vyeti feki kwamba ubinadamu haujatumika katika kuwafukuza kwa wakati mmoja. 

“Siwatetei, lakini wananyimwa mishahara na mafao, wapo waliotumikia kwa miaka 30 au 20. Nakubali kama wamekosea tena sana… Lakini mafao ya mtu, sasa hawa wataenda wapi, mtu ana familia. 

“Hata kama walifanya makosa, moyo wa huruma ulihitajika. Sawa amekosa mimi sitetei kosa lao, bali natetea ubinadamu wake, hivi ingenifika mimi leo ungejisikiaje,” alisema. 

Alisema anatoa pongezi kwa mambo mengi mazuri yaliyofanywa, lakini katika sakata la vyeti feki, wahusika inabidi wafikiriwe na kwamba shule nyingi zitakosa walimu sanjari na kukosekana kwa wakunga. Alisisitiza kuwa pamoja na nia njema ya Serikali, lakini watumishi hao inabidi waangaliwe kwa sura ya huruma. 

Ajali ya Karatu 
Akiendelea kuorodhesha kero zake, Lowassa alizungumzia uwakilishi wa Rais Magufuli katika tukio la kuwaaga wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vicent ya Arusha waliofariki katika ajali ya basi Karatu. 

Alisema yeye binafsi na wakazi wa Arusha walisikitishwa na kitendo cha Rais kutohudhuriatukio hilo lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Mei 8 badala yake alimtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumwakilisha. 

“Sina mgogoro na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Lakini nasema kuna shughuli hatumwi mtoto, hii haikuwa shughuli ya kutuma mtoto. 

“Amiri Jeshi Mkuu, ndiyo mfariji mkuu. Watu wa Arusha walijisikia wanyonge kutomwona Rais katika tukio lile,” alisema Lowassa. 

Aliongeza kuwa kitendo cha Rais kutohudhuria kiliwasononesha, kuwahuzunisha na kuwasikitisha wakazi wa Arusha na kwamba anapaswa kwenda kutoa pole kwa wahusika. 

Pia alishangwaza na kauli ya Rais Magufuli aliyosema amewasamehe wakazi wa Moshi akiwa katika ziara yake ya kikazi hivi karibuni. 

“Unawasamehe kwa kosa gani, kutuunga mkono? Watu milioni sita walisema no (hapana) katika uchaguzi uliopita. Na wana haki, unasema umewasemehe hao,” alihoji Lowassa ambaye mwaka 2015 aligombea urais kwa tiketi ya Chadema na kupata kura milioni 6.03. 

“Wewe unawasamehe mimi natafuta nafasi ya kwenda kuwashukuru nanyimwa. Lakini ipo ruksa kwa Rais kuzunguka nchi nzima kwa gari na ndege za Serikali kuwashukuru wapigakura wake, lakini ni dhambi kwa Edward Lowassa,” alihoji. 

Lowassa alitumia nafasi hiyo kueleza furaha yake kuhusu ukuaji wa mitandao ya kijamii ambayo alisema inafanya kazi nzuri na akaitaka kuongeza juhudi katika kazi yao na wasikubali kuminywa. 

Wakati huohuo, wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wameitaka Serikali itoe taarifa ya kina kuhusu maafa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini. 

Akizungumza bungeni jana, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema maafa hayo yamejitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, lakini Serikali imekuwa kimya kuhusiana na suala hilo. 

Alisema wabunge wengi wamerudi majimboni mwao kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwasaidia wapiga kura wao. 

“Pemba zaidi ya nyumba 600 hazifai kabisa zimesombwa na maji na Unguja zaidi ya nyumba 200 na shule zote za Zanzibar zimefungwa miundombinu yake ipo hoi, Tanga maeneo ya Lushoto pia kuna athari kubwa miundombinu ya barabara, shule, taasisi za dini mawasiliano yamekatika,” alisema. 

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya NCCR Mageuzi aliitaja mikoa mingine iliyokumbwa na mafuriko kuwa ni Morogoro, Kagera na Kilimanjaro. 

Mbatia ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya majanga alisema Tanzania bado haijajiandaa vya kutosha kukabiliana na masuala hayo, jambo ambalo limekuwa likiwakosesha wananchi taarifa sahihi juu ya majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza na pia kujikinga. 

Mbunge wa Malindi, (CUF), Ally Saleh alisema maeneo ya Unguja na Pemba hali ni mbaya na kwamba wanashangaa kwa nini Serikali imekaa kimya kuhusu maafa hayo. 

“Jana Serikali imeagizwa ilete taarifa bungeni kuhusu maafa hayo lakini haijaleta, sisi tumefadhaishwa na ukimya huu,” alisema.

Farid Musa aanza kung'ara Hispania

$
0
0

Mtanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Hispania Farid Musa, ameendelea kufanya vizuri kwenye klabu yake ya Tenerife B inayocheza ligi ya vijana. 

Farid amefunga magoli matano (5) katika mechi 12 alizoichezea timu hiyo huku akiwa amepiga pasi za mwisho ‘assists’ sita (6). 

Nyota huyu ambaye anaichezea pia Taifa Stars alisajiliwa na Tenerife akitokea Azam FC lakini alipelekwa kwenye kikosi cha vijana ili kujifunza aina ya soka pamoja na mifumo mbalimbali inayotumiwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kucheza kwenye kikosi cha wakubwa. 

“Nimeanza kupata nafasi kwenye kikosi B lengo likiwa ni kufundishwa aina ya soka lao na mifumo wanayoitumia ili nikianza kucheza kwenye timu ya wakubwa kusiwe na kazi kubwa ya kuelekezwa nini natakiwa kufanya,” alisema Farid alipoitwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Botswana na Burundi. 

Shaffihdauda.co.tz inaungana na wadau wengine wa soka kumtakia kila la heri kijana Farid Musa katika kuipeperusha bendera ya Tanzania nchini Hispania.

MAMA Aliyezimia kwa Saa Nane Asimulia Jinsi Mwanae Alivyomuaga Kabla ya Kufariki Kwenye Ajali ya Gari la Wanafunzi Arusha..!!!

$
0
0

 Leo ni siku ya mama duniani. Kila mzazi anatarajia kupata salamu za shukrani na za upendo kutoka kwa mtoto wake.

Lakini kwa Jenita Japhet, wingu zito la simanzi limeusonga moyo wake baada ya kumpoteza mtoto wake Kelvin Amos (13).

Kelvin, ni miongoni mwa wanafunzi 32 wa Shule ya Msingi Lucky Vicent waliofariki katika ajali ya basi iliyotokea Karatu, Arusha, Mei 6. Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni walimu wawili na dereva.

Wanafunzi wengine watatu walijeruhiwa na wanatarajia kwenda Marekani kwa matibabu leo.

Baada ya kupata taarifa za kifo cha mtoto wake, Jenita alizimia kwa saa nane. Alizimia saa tano asubuhi alipopata taarifa za msiba, hadi saa mbili usiku alipozinduka akiwa wodini katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas katikati ya jiji la Arusha.

Kwa mujibu wa wazazi wake, Kelvin alikuwa ni mwanafunzi mwenye juhudi darasani kwani tangu aanze darasa la kwanza amekuwa akishika nafasi tano bora.

Katika mtihani wake wa darasa la saba mwaka huu, alishika nafasi ya tatu kati ya wanafunzi zaidi ya 100.

Mwandishi wetu alifika nyumbani kwake, eneo la Field Force na kumkuta Jenita bado akiwa amegubikwa na simanzi kiasi cha kushindwa kuzungumza vizuri na mumewe, Augustine Amos ndiye aliyekuwa akimsaidia mara kwa mara.

Jenita anakumbuka neno la mwisho aliloambiwa na Kelvin wakati akiingia kwenye basi hilo: “Kwaheri Mama”

Lakini Mungu ameficha siri kubwa katika mauti, Jenita hakujua kuwa kwaheri ile ilikuwa ni ya milele.

Akizungumzia safari iliyochukua uhai wa Kelvin, Jenita alisema mtoto wake alimpa taarifa za safari ya Karatu, Mei 5 saa tatu usiku.

Kelvin aliyekuwa na ndoto ya kuwa daktari, alimweleza kuwa kesho asubuhi (Mei 6) anatarajia kwenda Karatu kwa ajili ya mtihani.

Jenita alisema kutokana na baba yake Kelvin, kuwa Babati kikazi, alimwambia ampigie simu kumpa taarifa lakini Kelvin aliomba yeye (Jenita) ampigie huku akiendelea na maandalizi ya mtihani.

“Nakumbuka alfajiri kama saa 10 hivi, Kelvin aliamka na kuanza kujiandaa mimi, nilishtuka akiwa tayari ameshajiandaa na anataka kuondoka,” alisema.

Alisema alipoamka alimkuta getini anatoka ndipo alipoanza kumfuata nyuma kwani wanaishi jirani na shule.

“Nilimkuta anagonga geti la nyumba nyingine ya jirani, nikamuuliza unafuata nini hapo, akanieleza anampitia mwenzake,” alisema.

Alisema Kelvin akiwa na mwenzake ambaye amesalimika katika ajali hiyo, kwa kuwa alipanda gari jingine, walimwambia arudi nyumbani kwani wapo wawili na watafika shuleni.

“Sikurudi niliamua kuwafuata nyuma hadi shuleni, aliponiona aliniaga ‘kwa heri mama’ na wakapanda kwenye magari mimi nikarudi nyumbani,” alisema.

Alipopata taarifa za ajali, alikwenda shuleni na alipothibitishiwa kuwa Kelvin amefariki alizimia.

“Siwezi kuzungumza zaidi, kazi ya Mungu haina makosa,” alisema.

Baba yake Kelvin

Baba wa Kelvin, Amos ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya Posta Babati (TPB Bank PLC), alisema siku ya tukio alikuwa kazini.

Alisema wakati akiendelea na kazi zake, alipigiwa simu na jirani yake saa nne asubuhi akimweleza kuwa gari la shule ya Lucky Vicent limepata ajali.

Hata hivyo, alisema alimweleza jirani huyo, kuwa hadhani kama mtoto wake, ambaye anasoma kutwa alikuwa safarini kwani alikuwa hana taarifa kuwa angekwenda Karatu.

“Ilipofika saa tano hivi, nilianza kuona picha kwenye mitandao watoto wa shule miili yao ikiwa imepangwa kwenye ajali, nilipatwa na hofu nikampigia Mwalimu Onetto,” alisema.

Alisema baada ya kumpigia Mwalimu Onetto alimuulizia Kelvin, kama alikuwa kwenye safari, akaniambia wapo safarini wamepata ajali eneo la Karatu anaweza kuwafuata.

Amos alisema baada ya kupata taarifa hiyo, aliondoka kazini na kuanza safari ya kwenda Karatu.

Alisema akiwa njiani, alipata simu kwa mzazi mwingine mwenye mtoto katika shule hiyo akimwambia kuwa hana sababu ya kwenda eneo la ajali kwani tayari miili imechukuliwa kupelekwa Hospitali ya Mkoa Mount Meru.

“Niliamua kwenda hospitali na baada ya kufika kulikuwa na watu wengi sana hivyo ilikuwa ni vigumu kuingia ndani,” alisema

Hata hivyo, alisema kwa kuwa alikuwa anafahamiana na baadhi ya askari, aliwaeleza yeye ni mzazi na anataka kushuhudia majeruhi na waliofariki kwani kuna mtoto wake.

“Wale askari walinipa ruhusa kuingia ndani na baadaye miili ilifika ambapo nilitambua mwili wa mtoto wangu Kelvin,” alisema

Alisema Kelvin alikuwa ni mtoto wake wa sita na kuna watoto wawili wanaosoma katika shule hiyo; Gladness anayesoma darasa la pili na Glory wa darasa la nne.

Alisema anamkabidhi Mungu yote yaliyotokea kwani kama mtoto wake alipangiwa kufariki katika ajali hiyo hakuna jinsi angeweza kukwepa.

Mwalimu Mkuu azungumza

Alipoulizwa kuhusu ajali hiyo, mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ephraim Jackson alisema taarifa nyingi zinazozungumwa sasa hazina ukweli.

“Nawaomba waandishi muwe makini na taarifa hizi, kwani mambo mengi sana yanaongewa lakini ukweli unajulikana naomba tuyaache hayo,” alisema

Alisema shule hiyo itafunguliwa kesho na akawaomba wazazi kuwapeleka watoto, ili taratibu za masomo ziendelee.

“Huu ni msiba mkubwa ambao umetupata na bado tuna masikitiko makubwa. Ambacho naweza kukuambia sasa ni kuwa shule itafunguliwa Jumatatu,” alisema.

Majeruhi kwenda Marekani

Katika hatua nyingine, wanafunzi watatu ambao walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo wanatarajiwa kupelekwa Marekani kwa ajili ya matibabu leo chini ya ufadhili wa shirika la Stemm la nchi hiyo.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa tayari hati za kusafiria za wasafiri wote wanane, wakiwamo majeruhi hao watatu, daktari, wazazi wao na muuguzi mmoja zimepatikana.

LOWASSA Arusha Makombora Mazito kwa Rais Magufuli na Serikali Yake..Amshangaa kwa Kutokwenda Kuwafariji Wazazi Waliofiwa na Watoto Wao Arusha..!!!

$
0
0

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ametaja mambo matano yanayomkasirisha ambayo yanafanywa na Serikali huku akiionya CCM kuwa ipo siku upinzani utatawala.

Lowassa aliyataja mambo yanayomkera kuwa ni pamoja na kuzuiwa kwa kongamano la kujadili demokrasia ambalo lilipangwa kufanyika jana, sakata la vyeti feki na Serikali kukaa kimya kuhusu mafuriko.

Mengine ni kupaa kwa bei za vyakula na Rais John Magufuli kutohudhuria tukio la kuaga miili ya wanafunzi waliopata ajali ya Karatu, Arusha.

Waziri Mkuu huyo wa zamani, alisema hayo jana wakati akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mikocheni wilayani Kinondoni.

Juzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la Demokrasia lililoandaliwa na Chadema, Makongoro Mahanga alitangaza kuwa lingefanyika jana katika Ukumbi wa Arnatouglou, Ilala na wanasiasa wakiwamo viongozi wa CCM na wananchi wa kada mbalimbali wangeshiriki.

Hata hivyo, siku hiyohiyo jioni, CCM ilitoa taarifa ya kukanusha viongozi wake kualikwa katika kongamano hilo.

Sinema iliendelea jana asubuhi wakati Chadema walipotoa taarifa kwa vyombo vya habari wakieleza kuwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam umewazuia kutumia ukumbi huo uliopo Mnazi Mmoja.

Akizungumzia zuio hilo, Lowassa alisema amesikitishwa na kitendo hicho alichodai kimefanywa na Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam.

“Tunalaani kitendo hiki kwa lugha inayowezekana, hatua hii ni ya kuminya demokrasia. Nia yetu ilikuwa njema ya kuzungumzia demokrasia.

“Waandaaji wa kongamano hili waliweka picha yangu na ya Kinana (Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM) tukionekana tumepeana vichwa lakini tuki- smile (tukitabasamu) jambo ambalo ni very important (muhimu),” alisema Lowassa.

Picha iliyotumika katika tangazo hilo la kuhamasisha kongamano ni ya Kinana na Lowassa wakionekana kuzungumza kwa kunong’ona walipokutana katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mei 8 katika tukio la kuaga miili ya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva waliofariki dunia katika ajali ya basi Mei 6.

Lowassa alisema Tanzania ni moja na watu ni walewale hivyo hakuna tofauti kwa watu wa CCM na Chadema na kwamba kila mmoja kuwa na maoni tofauti hakuna dhambi.

Hata hivyo, Lowassa aliwataka CCM kutambua kuwa ipo siku nchi ya Tanzania itatawaliwa na watu (chama) wengine na siyo wao.

“Kama watashindwa kuondoka wakati wetu, wataondoka wakati wa wajukuu wetu,” alisema.

Alieleza kuwa vyama vya ukombozi duniani vimebaki vichache na katika Afrika anadhani vipo ANC cha Afrika Kusini na CCM, hivyo huo ni ujumbe tosha kwamba ipo siku wataondoka madarakani. Alisema kitendo cha kuwanyanyasa watu kwa sababu wapo upinzani siyo jambo zuri na ni kuminya demokrasia na kushangaa kwa nini halikemewi.

“Waasisi wa Taifa hili wanapaswa kukemea, ndiyo maana tulialika kila mtu katika kongamano lile ili watuambie kwenye demokrasia Chadema mnakosea moja hadi tatu ili tujirekebishe. CCM inakosea hivi na mwisho mnakubaliana cha kufanya,” alisema Lowassa, “Ninalaani kwa nguvu zote kitendo kilichofanywa na Serikali ya Dar es Salaam tusifikishane hapa.”

Kuhusu mafuriko,

Lowassa aliitaja kero nyingine kuwa ni kutoshughulikiwa ipasavyo kwa athari ya mafuriko yanayoyakumba maeneo mbalimbali nchini.

Alieleza masikitiko yake kuwa haoni mkono wa Serikali katika mafuriko hayo ikiwamo kuwapa matumaini wananchi au kiongozi yeyote wa Serikali kuonekana akiwafariji waliofikwa na adha hiyo.

“Nawasifu na kuwapongeza wabunge jana (juzi) waliosimama na kutaka hoja hii ijadiliwe. Nadhani ni muhimu kujadiliwa na kuelezana ili Serikali ijue inafanya nini,” alisema Lowassa.

Bei za vyakula

Mbali na hilo, Lowassa alisema bei za vyakula zimezidi kupanda na wananchi wanapata tabu na kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, mahindi yapo juu kuliko mchele.

“Everything (kila kitu) bei juu. That is problem (hili ni tatizo ) Serikali itaenda kufanya nini katika hili?” alihoji Lowassa.

Alisema binadamu anaishi kwa matumaini, hivyo alitaka kujua wananchi wa vijijini wanapewa matumaini gani kutokana na hali hiyo. Aliiomba Serikali kutangaza na kuchukua hatua za kusaidia upatikanaji wa chakula na mambo mengine ili kuwasaidia Watanzania.

Sakata la vyeti

Kadhalika, Lowassa alizungumzia sakata la watumishi 9,932 wa umma wenye vyeti feki kwamba ubinadamu haujatumika katika kuwafukuza kwa wakati mmoja.

“Siwatetei, lakini wananyimwa mishahara na mafao, wapo waliotumikia kwa miaka 30 au 20. Nakubali kama wamekosea tena sana… Lakini mafao ya mtu, sasa hawa wataenda wapi, mtu ana familia.

“Hata kama walifanya makosa, moyo wa huruma ulihitajika. Sawa amekosa mimi sitetei kosa lao, bali natetea ubinadamu wake, hivi ingenifika mimi leo ungejisikiaje,” alisema.

Alisema anatoa pongezi kwa mambo mengi mazuri yaliyofanywa, lakini katika sakata la vyeti feki, wahusika inabidi wafikiriwe na kwamba shule nyingi zitakosa walimu sanjari na kukosekana kwa wakunga. Alisisitiza kuwa pamoja na nia njema ya Serikali, lakini watumishi hao inabidi waangaliwe kwa sura ya huruma.

Ajali ya Karatu

Akiendelea kuorodhesha kero zake, Lowassa alizungumzia uwakilishi wa Rais Magufuli katika tukio la kuwaaga wanafunzi 32, walimu wawili na dereva wa Shule ya Lucky Vicent ya Arusha waliofariki katika ajali ya basi Karatu.

Alisema yeye binafsi na wakazi wa Arusha walisikitishwa na kitendo cha Rais kutohudhuriatukio hilo lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha, Mei 8 badala yake alimtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumwakilisha.

“Sina mgogoro na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Lakini nasema kuna shughuli hatumwi mtoto, hii haikuwa shughuli ya kutuma mtoto.

“Amiri Jeshi Mkuu, ndiyo mfariji mkuu. Watu wa Arusha walijisikia wanyonge kutomwona Rais katika tukio lile,” alisema Lowassa.

Aliongeza kuwa kitendo cha Rais kutohudhuria kiliwasononesha, kuwahuzunisha na kuwasikitisha wakazi wa Arusha na kwamba anapaswa kwenda kutoa pole kwa wahusika.

Pia alishangwaza na kauli ya Rais Magufuli aliyosema amewasamehe wakazi wa Moshi akiwa katika ziara yake ya kikazi hivi karibuni.

“Unawasamehe kwa kosa gani, kutuunga mkono? Watu milioni sita walisema no (hapana) katika uchaguzi uliopita. Na wana haki, unasema umewasemehe hao,” alihoji Lowassa ambaye mwaka 2015 aligombea urais kwa tiketi ya Chadema na kupata kura milioni 6.03.

“Wewe unawasamehe mimi natafuta nafasi ya kwenda kuwashukuru nanyimwa. Lakini ipo ruksa kwa Rais kuzunguka nchi nzima kwa gari na ndege za Serikali kuwashukuru wapigakura wake, lakini ni dhambi kwa Edward Lowassa,” alihoji.

Lowassa alitumia nafasi hiyo kueleza furaha yake kuhusu ukuaji wa mitandao ya kijamii ambayo alisema inafanya kazi nzuri na akaitaka kuongeza juhudi katika kazi yao na wasikubali kuminywa.

Wakati huohuo, wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wameitaka Serikali itoe taarifa ya kina kuhusu maafa yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza bungeni jana, Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia alisema maafa hayo yamejitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, lakini Serikali imekuwa kimya kuhusiana na suala hilo.

Alisema wabunge wengi wamerudi majimboni mwao kwa ajili ya kuangalia namna ya kuwasaidia wapiga kura wao.

“Pemba zaidi ya nyumba 600 hazifai kabisa zimesombwa na maji na Unguja zaidi ya nyumba 200 na shule zote za Zanzibar zimefungwa miundombinu yake ipo hoi, Tanga maeneo ya Lushoto pia kuna athari kubwa miundombinu ya barabara, shule, taasisi za dini mawasiliano yamekatika,” alisema.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya NCCR Mageuzi aliitaja mikoa mingine iliyokumbwa na mafuriko kuwa ni Morogoro, Kagera na Kilimanjaro.

Mbatia ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya majanga alisema Tanzania bado haijajiandaa vya kutosha kukabiliana na masuala hayo, jambo ambalo limekuwa likiwakosesha wananchi taarifa sahihi juu ya majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza na pia kujikinga.

Mbunge wa Malindi, (CUF), Ally Saleh alisema maeneo ya Unguja na Pemba hali ni mbaya na kwamba wanashangaa kwa nini Serikali imekaa kimya kuhusu maafa hayo.

“Jana Serikali imeagizwa ilete taarifa bungeni kuhusu maafa hayo lakini haijaleta, sisi tumefadhaishwa na ukimya huu,” alisema.

WABUNGE Wafichua Mazingaombwe Kwenye Vitabu vya Shule za Msingi..!!!!

$
0
0

Wabunge ‘wamewaka’ kuhusu makosa yaliyopo kwenye vitabu vya kujifunzia na kushauri kuzuia matumizi ya vitabu hivyo ili kuepuka kuendelea kuwaharibu wanafunzi shuleni.

Makosa yaliyobainika katika vitabu hivyo ni ya kisarufi, mpangilio wa kurasa, tafsiri sisisi na kimantiki.

Wakichangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2017/18 bungeni mjini Dodoma jana, walisema vitabu hivyo vina makosa mengi ya lugha ya Kiswahili na Kingereza jambo ambalo linaua elimu nchini.

Akisoma maoni ya kambi Rasmi ya Upinzani bungeni, Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema pia makosa hayo yamekithiri katika herufi kubwa na ndogo na matumizi ya nukta pacha. “Matatizo hayo yamo kwenye vitabu vyote hasa kujifunza kusoma, kuandika, kuhesabu, afya na mazingira, michezo na sanaa,” alisema.

Alitoa mfano wa Kitabu cha Najifunza Kusoma, darasa la Kwanza, ukurasa wa 99 kinataja kucha kikimaanisha ukucha. Pia kitabu hicho kinaeleza kumjulisha bila kubadili kwa wima (baada ya kumjumulisha kwa wima bila kubadili) ukurasa 93 na 94 maneno chupa/ chupa ya chai (yakichanganywa).

Lyimo alisema kitabu cha I Learn English Language, kina matatizo ya matumizi ya herufi kubwa na ndogo mengi mno karibuni kila ukurasa.

“Inaelekea pia mwandishi hana uwezo wa kutosha wa lugha yenyewe kwani kuna makosa mengi.”

Alitoa mfano wa sentensi ambazo zimekosewa kuwa ni These are my parent, which is long between a pen and ruler? The driver is taken the police station, a boy is on bed at hospital na which is the big city of Tanzania (meaning Capital City).

“Vitabu vya darasa la kwanza vilichelewa kuchapishwa na kuwasilishwa shuleni. Hata hivyo, baada ya hekaheka nyingi za kuchoma nakala zilizokuwa na makosa ya mchapishaji, baadhi ya vitabu vya darasa la kwanza vilitoka Juni, 2016 na baadhi ya Januari mwaka 2017,” alisema.

Alisema kitabu kimoja tu cha darasa la pili kimetoka mwaka huu wa 2017 na kingine cha Kingereza darasa la tatu, I learn English Language.

“Kwa hali hiyo ya utoaji wa vitabu vipya na ucheleweshaji, walimu na wanafunzi watapata shida kubwa kuutumia mtaala mpya,” alisema.

Lyimo aliitaka Serikali kuzuia matumizi ya vitabu hivyo vyenye makosa shuleni na pia kuiagiza taasisi elimu kufanya marekebisho ya makosa yaliyopo kwenye vitabu hivyo na kuvichapisha upya.

Aidha, aliitaka Serikali kufanya uhakiki wa taaluma na weledi wa watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ili kujiridhisha kama wana sifa stahiki, uwezo na weledi katika kufanya kazi utunzi wa vitabu.

Awali, katika hotuba yake ya bajeti Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema, “Uchambuzi wa kina unafanyika kwa vitabu vyote vilivyochapishwa mwaka 2016/17 ili kubaini endapo kuna dosari zilizobainika...”

Alisema mchakato wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa mujibu wa taratibu za utumishi umekwishaanza kwa watumishi ambao vitabu walivyoidhinisha vimebainika kuwa na makosa.

“Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wahusika ili kukomesha tabia ya uzembe kwenye kazi muhimu za Taifa,” alisema.

Alisema baada ya uchambuzi wa vitabu vyote vilivyochapwa kukamilika, wizara itaamua hatua za kuchukua dhidi ya vile ambavyo vitabainika kuwa na dosari.

“Nawahakikishia wabunge kuwa wazembe wote waliokuwa sio makini katika hili kuangalia vitabu hivi tutawaadhibu. Nawahakikishia tutasafisha taasisi hii (Taasisi ya Elimu Tanzania - TIE),” alisema.

Alisema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17, wabunge walishika shilingi katika mshahara wake kutokana na makosa katika vitabu vya kujifunzia.

SERIKALI Yatoa Tamko Kuhusu Ugonjwa wa Ebola Kuingia Tanzania..!!!

$
0
0

Siku moja baada ya kutangazwa kuzuka kwa ugonjwa wa ebola katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk Mpoki Ulisubisya amewatoa hofu Watanzania akisema imechukua tahadhari kuhakikisha hauingii nchini.

Dk Ulisubisya alisema jana kuwa hadi sasa hakuna taarifa za kuwapo kwa mgonjwa yeyote wa ebola nchini na uangalizi wa uhakika umewekwa mipakani kuzuia mtu aliyeathirika kuingia.

“Mara zote tumekuwa tukichukua hatua stahiki kwa magonjwa ya mlipuko kama haya, maandalizi ya kutosha yamefanyika kuhakikisha tunakabiliana nao kama utafika na tahadhari pia zinaendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa matangazo,” alisema Dk Ulisubisya.

Alisema eneo lililotajwa kuwa na mlipuko wa ugonjwa huo ni la Kaskazini mwa DRC ambalo ni nadra kufikiwa na wafanyabiashara na madereva wa malori kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa mtandao wa Aljazeera, eneo hilo ni Likati ambalo lipo kilomita 1,300 kutoka mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

Juzi, Waziri wa Afya wa DRC, Oly Ilunga Kalenga alitangaza kuwapo kwa ugonjwa huo na kwamba umesababisha vifo vya watu watatu tangu ulipoanza mwishoni mwa mwezi uliopita.

Waziri huyo alieleza kuwa licha ya ugonjwa huo kuwa janga la kitaifa, hakuna sababu ya watu kupata taharuki.

“Si mara ya kwanza kwa nchi yetu kupata janga hili, hatuna sababu ya kushtuka sana, wizara ya afya inachukua hatua za haraka kukabiliana nalo,” alisema Kalenga wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ugonjwa huo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu tisa walipimwa na kukutwa na homa kali iliyoambatana na viashiria vya ugonjwa huo. Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Christian Lindmeier aliiambia Aljazeera kuwa kati ya watu hao tisa, watatu wamefariki na mmoja amethibitika kuwa na ebola.

“Tunatakiwa kuchukua hatua stahiki na za haraka zaidi kuhakikisha tunawafikia watu walioathirika na kupunguza uwezekano wa ugonjwa huo kusambaa. Kwa kuwa si mara ya kwanza kwa DRC kufikwa na ugonjwa huu, ni matumaini yangu kuwa mfumo wa afya wa nchi husika unafahamu kwa kina, namna ya kukabiliana na janga hilo,” alisema.

Mwakilishi wa WHO huko DRC, Dk Allarangar Yokouide amesema tayari hatua za awali zimeanza kuchukuliwa na timu ya kwanza ya wataalamu wa afya imewasili eneo la Likati ambalo ugonjwa huo umeanzia.

Hii ni mara ya nane kwa DRC kukumbwa na ebola, mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2014 na kusababisha vifo vya watu 49.

Tangu mwaka 2013 ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu 11,300 na kuathiri wengine 28,600. Afrika Magharibi, hususan nchi za Guinea, Sierra Leone na Liberia ndiyo upande uliothiriwa zaidi na ugonjwa huu.

Hadi sasa ugonjwa huo hauna tiba lakini mwishoni mwa mwaka jana, chanjo ya rVSV-ZEBOV ndiyo iliyoonekana kuwa kinga thabiti ya ebola.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi na kuchapishwa kwenye jarida la Lancet ulionyesha kuwa majaribio ya chanjo hiyo yalikuwa na matokeo chanya kwa asilimia 100.

Majaribio yalifanyika Guinea, moja ya nchi iliyoathiriwa kwa asilimia kubwa na ebola na chanjo hiyo ni ya kwanza kutoa kinga.

ZIMBABWE, Mchungaji Aliwa na Mamba Watatu Akijaribu Kutembea Juu ya Maji Kama YESU..!!!

$
0
0

Mchungaji wa kijiji kimoja huko zimbabwe Pastor Jonathan Mthethwa ametafunwa vizuri na mamba watatu alipokuwa akijitutumua kutembea juu ya maji Kama yesu katika mto MPUMALANGA
au kwa jina maarufu MTO MAMBA kutokana na wingi wa mamba katika mto huo.

Alikuwa anafanya majaribio ya imani(DEMO) aliyowafundisha waumini wake kanisani....
Shemasi aliyehojiwa anashangaa kwa nini aliliwa maana kabla alifunga na kuomba wiki nzima...
Mashuhuda wanasema alitembea ndani ya maji kama mita 30, alipotaka kuanza kupanda ili aanze kutembea juu ya uso wa maji ndipo yalitokea mamamba makubwa matatu na kumtafuta na kumkatata vipande huku mwili wote ukiishia kwenye matumbo ya watafunaji hao...

Waumini Muwe makini na Wachungaji wenu, Leo kaenda yeye kesho anaweza kuibuka mwingine TZ akawaambia kanisa zima litembee juu ya mto ruvu ile sehemu yenye mamba na viboko wengi kama mazoezi ya Imani. Au kama mafunzo ya vitendo baada ya kufundishwa Theory/Nadharia za kiimani kanisani...

Imani na Akili lazima ziende sanjari na Vyote viwe mubashara Muda wote ukikoswa kimoja utaishia kuliwa kama sio wewe basi pesa zako...

Askofu Gwajima awajia juu wanaoizungumzia nchi vibaya

$
0
0

Dar es Salaam.Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amewaonya baadhi ya watu wanaoiongelea vibaya nchi akiwataka waache mara moja kwa kuwa wanachochea uvunjifu wa amani. 

Askofu Gwajima amesema kinachotakiwa watu waizungumzie nchi vizuri kwa kuwa amani itakuwepo na uchumi wa nchi utaendelea kukua. 

"Namkemea yule mtu ambaye anaiongelea vibaya nchi yetu huwezi ukawa unatoa kinywa kinachoashiria uvunjifu wa amani," 

"Huwezi kila siku unalaani kwa kuiongelea vibaya nchi yetu lazima nikemee ili nchi yetu iweze kuendelea kuwa na amani,"amesema Gwajima katika mahibiri kanisani kwake leo.

BREAKING: Hans Poppe wa Simba Sc abwaga manyanga

$
0
0

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.


Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi kwa madai kuwa anaona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo.


Chanzo chetu cha kuaminika kinaeleza kuwa "Hans Poppe ameachia ngazi kwa kuwa hakufurahishwa na mlolongo ulivyokuwa hadi Simba kuingia mkataba wa SportPesa,” kilieleza chanzo.


"Hans Poppe ameandika barua kujiuzulu kwenye kamati ya utendaji, maana yake anaondoka moja kwa moja katika nafasi ya mwenyekiti wa kamati ya usajili.


"Kilichomchukiza, anasema kuna kundi lililoongozwa na Rais Evans Aveva na makamu Geofrey Nyange Kaburu, lilifanya mambo kimya kimya na Hans Poppe amesema hata Mo Dewji aliyeisaidia Simba mishahara naye hakushirikishwa hata kiungwana tu, hivyo amepinga hilo."

Ajali ya Karatu sio ishu ya kisiasa- RC Mrisho Gambo

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, amesema kuna watu wanatumia mitandao ya kijamii wakiwa na lengo kuu lakutaka kuyumbisha lengo la serikali la kuwahudumia majeruhi wa ajali ya gari ya shule ya Lucky Vicent ambao leo wamesafirishwa kwenda Marekani kwa matibabu.


Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo


Mrisho Gambo akiongea uwanja wa ndege wa KIA amewataka watu wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kuendelea kuungana na kuwa wamoja katika lengo hilo ili kuhakikisha watoto hao wanapata huduma nzuri huko waendako na kurudi nchini salama ili baadaye waje kutumikia taifa lao la Tanzania. 


"Tunauhakika huko wanakokwenda watatibiwa vizuri na kurudi salama Tanzania ili kulitumia nchi yao, hili tukio siyo tukio la kisiasa tusikubali mtu yoyote kwa sababu yoyote atutoe kwenye lengo la msingi la kutoa huduma kwa watu wetu, wakati sisi tunahangaika kwenda kuzika watu, tunahangaika na kuhakikisha watu wanasafiri kwenda kutibiwa kuna watu wengine wanatumia mitandao ya jamii kutaka kupoteza focus ya serikali na watu wengine kuhakikisha kwamba wahusika wetu wanapata matibabu bora na wanabaki salama kwa hiyo nitumie nafasi hiii kuwaomba watu wa Arusha na watanzania wote tuendelee kuungana na kuwa wamoja kuhakikisha kwamba tunaikamilisha kazi hii ya Mungu" alisema Gambo  
Viewing all 104709 articles
Browse latest View live




Latest Images