Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live

UNATAKA Kuwa Mwanaume wa Shoka Siku Zote..Epuka Mazoea ya Kula Vyakula Hivi Katika Maisha Yako..!!!

$
0
0

Katika post hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi kula ili kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila mwenyewe kujuwa.

1. Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele

Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala). Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku.  Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya kwenye maboksi.

Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha ‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.

Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.

2. Punguza kunywa pombe au acha kabisa kuzuia kuota matiti

Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.

Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.

Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama wanawake.

3. Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume

Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama. Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu wakahimizwa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe na saratani ya tezi dume.  Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya  canola na mafuta ya corn na mengine yote yenye omega 6.

4. Popcorn

Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’ kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.

Ni vizuri kuacha kula popcorn

5. Mkate mweupe

Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.

Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.

Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

6. Chumvi ya mezani

Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi kwa afya ya mwanaume.

FAHAMU Siri Iliyopo Kati ya Nguvu za Kiume na Asali Mbichi Pamoja na Mdalisini..!!!

$
0
0

Asali ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi zilizopita duniani kote. Vitabu vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa mbalimbali kutokana na asali.

Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbalimbali.

Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za mashariki za dunia. Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo mdalasini.

-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.

Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala kwa mwezi mmoja.

UNASUMBULIWA na Fangasi za Sehemu za Siri...? Usijali Zingatia Haya Kujitibu Bila Gharama Yeyote Ile..!!!

$
0
0

Ugonjwa wa fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea vijulikanavyo kwa kitaalamu kama ‘Candida albicans’. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote lakini hushambulia zaidi wanawake sababu ya maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachopelekea wao kuathiriwa zaidi kuliko wanaume.

Watu karibu wote tunaishi na vimelea hivi katika miili yetu kwa kiwango kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria wazuri wa mwili ndiyo kupambana na vimelea hivi hata unaona huuguwi ila kinga ya mwili ikiyumba kidogo na bakateria wabaya kuongezeka ndipo hapo unapokutana na ugonjwa kamili.

Tatizo la kuwashwa sehemu za siri ni tatizo kwa watu wengi miaka ya sasa na linawapata watu wa jinsia na rika zote yaani watoto, vijana hata wazee.

Fangasi siyo sababu pekee ya kuwashwa sehemu za siri, kuna sababu na magonjwa mengine yanahusika na tatizo hili na kupona au kuondoka kwa sababu hizo ndiyo kupona kwa huo muwasho.

Sababu za muwasho sehemu za siri za mwanaume
Sababu zifuatazo zinaweza kuhusika na muwasho sehemu za siri kwa mwanaume:

Mzio au aleji
Maradhi ya fangasi
Ugonjwa wa upele
Chawa
Maambukizi ya bakteria
Magonjwa ya zinaa
Lishe duni
Baadhi ya dawa kutibu bakteria
Kushuka kwa kinga ya mwili
Kuambukizana toka mtu mmoja hadi mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa
Hali ya hewa nayo yaweza kuwa chanzo hasa mazingira yenye joto sana
Sababu hizi ndizo hupelekea muwasho pia sehemu nyingine za mwili.

Dawa za asili zinazotibu fangasi kwa wanaume
Kumbuka kumuona daktari kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote, ni mhimu kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi ikiwemo kubaini chanzo hasa cha fangasi yako.

1. Mafuta ya habbat soda

Maambukizi ya fangasi yanatokea wakati bakteria wanapozidi juu ya ngozi yako na kupelekea kutokea kwa magonjwa mengi ikiwemo miwasho, upele na ukurutu. Tafiti zinaonyesha mafuta ya habbat soda ni mazuri kwa tiba karibu kwa kila aina ya fangasi kitu kinachopelekea wanasayansi wengi kuamini kuwa habbat soda ni dawa ya asili na mbadala mhimu zaidi kwa kila mtu kuwa nayo nyumbani.

Matumizi: Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai cha mafuta ya habbat soda kutwa mara 1 kwa mwezi mmoja. Mengine pakaa kama mafuta yako ya kupakaa sehemu yenye muwasho kutwa mara 3 hadi 3

2. Mafuta ya nazi

Siyo sehemu za ndani tu ya mwili zinazofaidika na mafuta haya ya nazi kama yanavyofanya mafuta mengine ya asili, kama unataka kuwa na ngozi nzuri yenye mng’aro na yenye afya na yenye muonekano wa asili basi paka mafuta ya nazi kila siku kwenye ngozi yako, mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa katika kuua bakteria, virusi, na vijidudu vya aina yeyote vinavyoweza kuidhuru ngozi, haya ni mafuta kwa mwili mzima yaani pakaa kwenye ngozi yote usoni, mwilini, kwenye nywele na kwenye kucha.

3. Mu-aloe vera (mshubiri)

Ngozi hupenda sana Vitamini C na E ambazo zote zinapatikana katika aloe vera na kusaidia kuboresha unene wa ngozi na kuiacha katika hali ya umajimaji. Ikiwa utachanganya jeli ya aloe-vera na mafuta ya asili ya nazi utapata krimu nzuri ya kuongezea viinilishe, mafuta mhimu na unyevunyevu katika ngozi.

Jeli ya Aloe Vera hupenyeza katika ngozi kwa haraka mara nne zaidi ya maji ya kawaida na sifa yake ya kulainisha ngozi husaidia ngozi kubaki na unyevunyevu muda wote.

Mhimu: Pamoja na hizi dawa pia unahitaji kitu kitakachoimarisha kinga yako ya mwili kwa ujumla na kwa sababu hii napendekeza utumie ama unga wa majani ya mlonge au mbegu za maboga kila siku wakati ukiendelea na hizi dawa za fangasi.

Pia hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku, jiweke msafi kila mara na usishirikiane na wengine vitu kama taulo na vifaa vingine vya kuogea.

Epuka vyakula vyenye sukari nyingi na hata sukari yenyewe ikibidi utumie asali badala ya sukari kwenye kila unachohitaji sukari. Epuka pia vyakula vya wanga.

Kama una ugonjwa wa kisukari jitibie kwanza kisukari.

MAMBO Manne (4) Ya Kimafanikio Ya Kumfundisha Mtoto Wako Mapema...!!!

$
0
0

Msingi mkubwa wa mafanikio ya mtu yeyote kitabia unatokana na malezi bora aliyopata hasa akiwa mtoto kuanzia mwaka mmoja hadi miaka kumi na mbili. Katika kipindi cha mwaka 1 hadi 12 ndio kipindi muhimu sana cha malezi.

Tabia nyingi ambazo zinatengenezwa au kufundishwa katika kipindi hiki, huwa kuna uwezekano mkubwa wa kudumu maishani mwako kote. Hapa hii inatokea bila kujali tabia hiyo ni nzuri kwako au mbaya.

Kwa mfano, kama ulikuwa unaendekeza uvivu au kama ulikuwa mtu wa kuchapa kazi sana na kujiona huo ndio kama utamaduni katika kipindi cha mwaka 1 hadi 12, ni rahisi tu tabia hizo kuendelea hadi ukubwani.

Kwa mantiki hiyo ndiyo maana ni muhimu sana kumfundisha mtoto wako mambo ya kimafanikio yatakayomsaidia  kwa baadae kwenye maisha yake. Mambo hayo ni yepi? Karibu na twende pamoja tujifunze.   

1. Mfundishe, njia bora ya kufikiri.

Ikiwa hupendi sana maisha yako yalivyokuwa mwanzoni yaendelee kwa kizazi chako, sasa ni wakati wa kumfundisha mtoto wako namna bora ya kufikiri. Hapa ni lazima umfanye mtoto wako aweze kufikiri chanya.

Unaweza kumfanya moto wako afikiri chanya kwa kumpa vitabu vizuri chanya kama uwezo wa kusoma anao au kwa maneno maneno unayomwambia. Hiyo haitoshi pia unaweza ukamtafutia marafiki wazuri wenye mtazamo chanya.

Kama mtoto wako unamlea kwa mtazamo chanya, kufikiri kwa njia bora itakuwa kwake ni jambo ambalo halikwepeki. Anza leo kuweka mikakati yakumjengea mwanao njia bora ya kufikiri itakayomsaidia hata kumjengea mtazamo chanya pia.

2. Mfundishe, kujitegemee mapema.

Kati ya kitu kitakachofanya ujenge msingi imara kwa watoto wako kwa baadae ni kule kufanya wajitegemee mapema. Hapa inatakiwa umfundishe mtoto wako kufanya baadhi ya mambo mwenyewe.

Kwa mfano, anapokuwa mkubwa kidogo kama ni kufua mwache afue mwenyewe. Kama ni kusaidia kazi fulani acha aifanye. Njia hii inakuwa bora kwa kujua kwamba kuna vitu fulani anatakiwa awajibike.

Lakini kama utakuwa ni mtu wa kumlea mtoto wako kwa kutaka kila kitu  afanyiwe basi wewe ndiye utakuwa mtu wa kwanza kumharibu mtoto wako. Mfanye mtoto wako ajitegemee mapema, 
itamsaidia sana kwa baadae katika makuzi yake.

3. Mfundishe, ajifunze kuchukua hatua mapema.

Siku zote vitendo ni bora sana kuliko kusema. Kwa kuwa unajua umuhimu wa hili anza kumfundisha mtoto wako juu ya umuhimu wa kuchukua hatua mapema katika maisha yake hata kwa vitu vidogo ambavyo anavyofanya.

Kwa kumfundisha hivi unakuwa unajenga utamaduni imara ambao utamfanya mtoto wako hata atakapokuwa mkubwa atakuwa anajua na kutambua umuhimu wa kuchukua hatua mapema pia kwenye maisha yake.

Ili hili lifanikiwe, mfundishe kitu fulani halafu anza kufatilia utekelezaji. Unaweza ukamwacha hata maswali kama kazi ya nyumbani, halafu uone atamaliza baada ya muda gani? Utakuwa unafanya hivyo mara kwa mara ili kumfanya achukue hatua mapema zaidi.

4. Mfundishe ajue mambo yote huwa hayaendi kama yalivyopangwa.

Katika kumfundisha atambue kwamba mambo kuna wakati hayaendi kama yanavyopangwa, subiri kipindi ambapo anataka kitu fulani tena kwa hamu kubwa. Inapofika katika hicho kipindi kwa makusudi mnyime.

Najua kama ilivyo kwa watoto walio wengi tabia zao atalia. Mwache alie halafu tafuta siku ama muda akitulia, kama kile kitu kilikuwa cjha kununua, mnunulie na mpe somo mapema atambue kuna wakati mambo hayaendi moja kwa moja kama uliyopanga.

Fanya hivi kwa mtoto ambae ameshaanza kujitambua ikiwezekana kuanzia angalau darasa la tano. Rudia tena na tena zoezi hili, mpaka ifike mahali ajue kwamba mategemeo na uhalisia ni vitu viwili tofauti.

Yapo mambo mengi unayoweza kumfundisha mwanao ya kumweka juu kimafanikio kwa baadae. Unaweza kumfundisha mwanao pia jinsi ya kuishi na watu sahihi, uaminifu katika maisha, misingi bora ya kuishi maisha ya kiroho napengine hata faida ya kujiamini.

Fanyia kazi haya machache kwa leo na chukua hatua katika kuweza kufikia mafanikio yako makubwa.

Ni wako rafiki katika mafanikio,
Imani Ngwangwalu,
0713 04 80 35,

KAMA Kweli Unataka Kufanikiwa Wekeza Akili Yako katika Jambo Hili....!!!

$
0
0

Kuna wakati mwingine watu hushindwa kulitekeleza jambo fulani sio kwa sababu hawajui jambo hilo au eti kwa sababu hawana uzoefu wa jambo hilo, la hasha huo si kweli watu wengi wanashindwa katika kulifanya jambo fulani kwa sababu wanakosa"umakini" juu ya kulitenda jambo hilo.

Na umakini ni ile hali ambayo ambayo mtu anakuwa nayo kutoka nafsini mwake katika kulitenda jambo fulani, lakini kulitenda jambo hilo bila kufikiri ni sawa na bure, hivyo kila wakati unahitaji kujenga umakini kwa kuwekeza nguvu na akili katika kufikiri na kutenda jambo hilo.

Kamwe hutoweza kufanikiwa kama utaendelea ile tabia ya kutofanya vitu kwa umaikini.  Kwani siri kubwa ya kushindwa kufanikiwa kwako ipo katika jambo hilo. Nasisitiza swala hili la kutenda mambo kwa umakini kwani pindi mtu anaamua kuwa makini humsaidia mtu huyo kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa jambo husika na mara nyingine kutenda jambo kwa umakini huumfanya mtendaji wa jambo hilo kuepuka kurudia makosa katika kulitenda jambo hilo.

Hivyo umakini katika kila nyanya na masuala mbalimbali ya maendeleo yako binafsi na ya jamii kwa ujumla yanahitajika kwa kiasi kikubwa, hivyo kama unataka kufanikiwa kwa kiwango kikubwa unatakiwa kuwa makini kwa kila jambo.

Mwisho jitahidi kuwa makini  juu ya mambo haya;

1. Kuwa makini katika kuchagua mawazo ya mambo ambayo unataka kuyatenda.

2. Kuwa makini katika kubeba mawazo na ushauri wa watu mbalimbali ambao wanakuzunguka. Au kwa maneno mengine tunaeza kusema kuwa makini na wewe mwenyewe na watu wengine.

3. Jitahidi kadri uwezavyo kuwa makini katika katika kufanya upembuzi yakinifu ni wapi ambapo umetoka ni wapi ambao unaelekea.

4. Kuwa makini katika katika kuchagua marafiki wenye tija kwako kila wakati.

5. Kuwa makini katika kuwekeza mambo ambayo unajifunza mara kwa mara. Jiulize yana tija gani kwako.

6. Kuwa makini katika kutambua thamani ya muda na pesa.

Hayo ni baadhi ya maeneo machache kati ya mengi ambayo unatakiwa kuwekeza fikra katika kulitenda jambo fulani.

UJUMBE wa Diamond Kwenda Kwa Baby Mama Wake Zari Hassan leo

$
0
0

By @diamondplatnumz
Kupata mtu wa kuzaa nae inaweza isiwe tabu sana ila kupata Mwanamke atae kubali kuacha stareh zote za dunia na kukulelea watoto ipaswavyo sio kitu rahisi.... kazi yangu imejawa na vishawishi vigi sana, wakati mwingine napatia wakati mwingine nakukosea lakini siku zote umekuwa mwenye kunielekeza nikoseapo na sio kunihukumu...na ndiomaana siku zote chochote ukitakacho nikiwa nacho lazma nikupe pengine itanisaidia kukuelezea ni kias gani nakupenda na kukuthamini.... Happy Mother's Day @zarithebosslady
.
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Wanawake: Hizi ni dalili 9 kuwa wewe si ‘main chick’ bali ni mchepuko wake tu !

$
0
0

Wanaume wengi ni wataalam wa kuwa na uhusiano na wanawake wengi kwa wakati mmoja. Sasa kwa msichana unayesoma makala hii, hizi ni dalili 9 kuwa huenda wewe si ‘baby number one’ wake bali ni mchepuko tu.
1. Mazungumzo mengi naye yanahusisha kufanya mapenzi tu

2. Hawezi kukualika kwenye mkusanyiko wa familia yake.

3. Hapendi surprises – hapendi uende kwake bila kumwambia

4. Ni mkali sana kwenye simu yake, hawezi kukuruhusu uishike

5. Ni mgumu kukuonesha mahaba ukiwa naye hadharani

6. Anahofia kupiga selfie na wewe

7. Anapigiwa simu za ajabu ajabu

8. Hakuiti wewe kama girlfriend wake. Akiwa na marafiki au
ndugu zake anakutambulisha kwa jina lako.

9. Haongelei kuhusu mipango yenu ya baadaye.

WIKI Moja Baada ya Ajali ya Wanafunzi Arusha..Hiki Ndicho Kinachofuata kwa Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vicent Kuanzia Leo..!!!

$
0
0

Wakati wanafunzi  watatu majeruhi katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent  wakienda kwa matibabu nchini Marekani wanafunzi waliobaki shuleni leo wataendelea na masomo huku kukiwa na ukimya shuleni hapo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Ephraim Jackson alisema jana kuwa shule hiyo inatarajiwa kufunguliwa leo baada ya kufungwa kwa wiki moja.

Amesema ratiba masomo pia itapangwa leo ikiwepo siku za kuanza mitihani ya muhula.

Hata hivyo tofauti na siku nyingine jana  katika shule hiyo kilikuwa kimya hakukuwa na mwanafunzi.

Baadhi ya wafanyakazi eneo la usafi wa madarasa na magari walikuwa wakiendelea na usafi.

ALICHOKISEMA Zitto Kabwe Kuhusu Bei ya Sembe Kuwa Juu Mara Dufu..!!!

$
0
0

Mbunge wa Kigoma mjini kupitia tiketi ya ACT Wazalendo Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa bei ya unga wa ugali kwa sasa ipo juu kuliko hata bei ya mafuta ya magari jambo ambalo linafanya wananchi kuumia zaidi na ugumu wa maisha.

Zito Kabwe amesema kwa sasa Bei ya Unga wa Sembe 1kg ni  Shilingi 2,300/= huku Mafuta ya Petroli lita moja ikiuzwa kwa Shilingi 2,060/= huku akishangaa kuwa ni mara yake ya kwanza kuona Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari.

“Bei ya Unga wa Sembe 1kg TZS 2,300/= ( wastani ). Bei ya Mafuta ya Petroli 1lita TZS 2,060/= ( wastani). Kwa mara ya kwanza Ugali umekuwa ghali kuliko mafuta ya gari“Ameandika Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook huku akiendelea kuhoji ukimya wa Serikali juu ya mfumko huo wa Bei

“Gharama hizi za maisha Kwa wananchi ni kubwa mno, hazistahmiliki na zinaingiza raia wengi kwenye umasikini. Serikali ipo kimya kana kwamba kila kitu kipo sawa“Ameandika Zitto Kabwe.

KAMA Wewe ni Mzazi Ujumbe Huu wa Ray C Lazima Ukutoe Machozi..!!!

$
0
0

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva,Ray C ametumia vizuri siku ya jana ya akina Mama Duniani kwa kuwakumbuka Wazazi wa watoto watatu walionusurika kwenye ajali ya Gari huko Karatu mkoani Arusha kwa kuwapa ujumbe wa faraja wenye maneno ya kutia Moyo.

Ray C amesema Mungu yupo mbele ya watoto hao na kwavile wameondoka wakiwa wanahema basi watarudi wakiwa wanahema na wenye Afya.

“Mtapona kwa nguvu ya Mungu kupitia madaktari….na mtarudi salama…Ya Mungu ni mengi na tayari kashawaonyesha kupitia mliyopitia na bado mnahema“Ameandika Ray C .

Ray C pia aliwapa moyo akina mama wa watoto hao watatu ukizingatia jana ni siku ya Akina Mama duniani kwa kusema waendelee kuomba na kumuamini Mungu kwani yeye ndiye ngao pekee iliyobakia kwenye maisha yao.

“Happy Mother’s day kwa wamama wote Wa hawa watoto,Mungu azidi kuwaonyesha uwepo wake kwenu muda wote na mzidi kumuamini kuwa yeye ndio ngao ya Maisha yenu“Ameandika Ray C kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Wazazi wa watoto hao watatu majeruhi wa ajali ya Basi ya Karatu iliyoua watu 35, wameondoka jana asubuhi hapa nchini kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya Matibabu zaidi .

TOYOTA Watia Mkono Kwenye Utengenezaji wa Gari Inayopaa..!!!!

$
0
0

Kampuni ya kuunda magari ya Toyota kutoka Japan imetangaza kuunga mkono kundi la waandisi ambalo linaunda gari linaloruka kwa kufadhili.

Toyota imetoa kiasi cha Dola 300k za Kimarekani kwa kundi hilo ambalo huendesha shughuli zake nje ya mji wa Toyota nchini Japan.

Kundi hilo limekuwa likipata michango kugharamia kuundwa kwa gari hilo linalotumia teknolojia ya ndege zisizokuwa na rubani na linatajwa kuwa gari dogo zaidi linaloruka kuwahi kuundwa.

Uharaka wa kuundwa kwa Gari hilo linalopaa unavaliwa njuga na makampuni mengi nchini Japan kwani matarajio ya kundi hilo la wataalamu wanataka magari hayo yatumike kwenye tukio la kuwasha Mwenge wa Michuano ya olimpiki mwaka 2020 mjini Tokyo,Japan .

KOREA Kaskazini Yafanya Jariio Jingine la Kombora la Masafa Marefu..!!!

$
0
0

Korea Kaskazini imefanya jaribio jingine la kombora ikiwa ni siku chache tu, tangu Rais wa Korea Kusini kusema yupo tayari kwa mazungumzo.

Kumekuwa na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hiyo ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio yake zana za nuklia

Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imeachwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.

Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi.

Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan.

Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama.

Jaribio lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba wiki mbili zilizopita.

Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo na kufanya majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za nuklia.

Chanzo: BBC

FEDHA za Rambi Rambi za Msiba wa Wanafunzi Arusha Zamweka Pabaya Gambo..Habari Vicha vya Magazeti ya Leo 15/5/2017..!!!

MAPACHA Walioungana Wahitimu Kidato cha Sita..!!!

$
0
0

HATIMAYE Pacha walioungana wilayani Kilolo Mkoani Iringa wamehitimu elimu yao ya sekondari ya Kidato cha sita huku wakiiomba serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo kuwasaidia mitaji ya biashara ambao itawasaidia kujiendeleza na kujikwamua kimaisha.

Pacha hao Maria na Consolata waliwasilisha ombi hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asiah Abdalah alipowatembelea kwa lengo la kuwaaga.

“Tumehitimu elimu yetu ya sekondari ya kidato cha sita, lakini tunaomba wasamaria wema watusaidie mtaji wa biashara wakati tukisubiri matokeo ya kuendelea na elimu ya chuo kikuu, sisi wenyewe tunavipaji tunaweza kufuma,kuchora na kudarizi na tukipata mitaji hiyo itatusaidia hata kujiendeleza kwa mambo mengine,’walisema.

Naye Mkuu wa Wilaya Asiah aliwaasa wanafunzi waliohitimu elimu yao kupiga vita rushwa inaangamiza taifa, inadhulumu haki hivyo watu wote wanatakiwa kupinga rushwa, na dawa za kulevya.

RASMI..Kitwanga Atakiwa Ahame CCM..Ni Baada ya Kusema Kuwa Ataenda Kuharibu Mitambo ya Maji ya Ziwa Victoria Bungeni..!!

$
0
0

SIKU chache baada ya Charles Kitwanga kutishia kuzima mtambo wa kusukuma maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mikoa ya Shiyanga na Tabora, serikali imemjibu waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kumtaka ahame kwenye chama tawala, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kama anaona hatendewi haki.

Akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji bungeni mjini hapa Jumatano, Kitwanga alitishia kuhamasisha zaidi ya wananchi 10,000 kwenda kuzima mtambo wa maji ulioko kwenye chanzo cha maji cha Iherere jimboni kwake Misungwi, mkoani Mwanza, ikiwa hawatapatiwa maji yatokanayo na mradi huo.

Hata hivyo, Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge, akihitimisha mjadala wa makadirio hayo juzi. alimjibu mbunge huyo kwa kumtaka aihame CCM kama anaona hakitendi haki dhidi yake.

"Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie suala la mchango wa Mheshimiwa Kitwanga. Amechangia hapa kwa hisia kubwa kuonyesha kuwa serikali ya CCM haijafanya chochote kwenye Wilaya ya Misungwi," alisema.

"Sasa nataka nimuulize Kitwanga kama yupo hapa kwamba hayo ni maneno yake au ya wananchi? Kama ni ya wananchi nitawaambia ni nini kimefanyika Misungwi kwani hata juzi tumetia saini mikataba ya maji na Mwenyekiti wa Halmashauri alikuwapo, ya kupeleka maji Misungwi kutoka Ziwa Victoria kwa fedha nyingi zaidi ya Sh. bilioni 38.

"Sasa anaposema anakwenda kuhamasisha wananchi wakabomoe mtambo wa Iherere, maana yake analeta uasi au hathamini kazi iliyofanywa na chama chake, sasa ajitoe kwenye chama kwa sababu serikali imepeleka fedha na maendeleo yaliyofanyika ni lazima tuwahamasishe wananchi kutunza miundombinu iliyopo badala ya kwenda kuibomoa.

"Hata kwenye umeme huwa tunaona wanaweka kwenye kijiji kimoja na kuruka hadi kijiji cha nne, lakini hatujawahi kuona wanang'oa nguzo. Sasa nataka nimwambie serikali inaendelea kuboresha maji katika maeneo mbalimbali ikiwamo Misungwi na Usagara."

HISTORIA :Hivi Ndivyo Nyerere Alivyomtetea Karume Mbele ya Viongozi wa Afrika Nchini Ghana..!!!

$
0
0

Na  AHMED RAJAB

KATIKA mwezi wa Machi hali ya hewa jijini Accra, Ghana, huwa inaudhi bila ya kiasi kwa joto linavyokuwa kali. Jioni ndipo huzidi kushtadi.  Nadra mvua kunyesha.  

Siku moja Machi 1958, saa za Magharibi, wakombozi wawili wa Kiafrika walikaa, glasi mkononi, wakipunga upepo kwenye baraza ya hoteli ya Avenada, iliyokuwa ikimilikiwa na Mgiriki.

Upande mmoja alikuwa Sheikh Ali Muhsin Barwani kutoka Zanzibar na aliyemkabili alikuwa Mwalimu Julius Nyerere kutoka Tanganyika.  Nyerere alikuwa rais wa chama kikuu cha Tanganyika cha kupigania uhuru, Tanganyika African National Union (TANU) na Barwani, akitambulika kuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (maarufu Hizbu) ingawa hakuwa na wadhifa maalum katika chama hicho. 

Rais wa Hizbu alikuwa Sheikh Vuai Kitoweo, mzawa wa Jambiani, kwenye mwambao wa kusini mashariki mwa Unguja. Kitoweo alishikilia wadhifa huo tangu alipochaguliwa 1955 hadi mapinduzi ya 1964.  Hata hivyo, Barwani ndiye aliyekuwa akionekana kiongozi wa Hizbu hata akapewa lakabu ya “zaimu”, inayotokana na neno la Kiarabu “zaim” lenye maana ya kiongozi.  

Wakati huo, Hizbu kilikuwa chama pekee kilichokuwa kikipigania uhuru wa Zanzibar. Chama kingine kikuu, cha Afro-Shirazi Party (ASP), kilikuwa kikipinga Zanzibar isipewe uhuru.  Ilifika hadi hata Waingereza walipokubali pafanywe uchaguzi Zanzibar, chama cha ASP kilipinga.  Uchaguzi huo ulikuwa wa  mwanzo katika Afrika ya Mashariki, ya Kati na kusini mwa Afrika, 

Sheikh Shaaban Soud Mponda, Mwafrika aliyekuwa mjumbe wa kuteuliwa katika Baraza la Kutunga Sheria (Legico) alihuzunika na kusema: “Hii ni siku ya giza kwa Waafrika wa nchi hii.”  Mponda akiunga mkono ASP. 

Mwafrika mwengine kwenye Baraza hilo, Sheikh Rashid Hamadi alimpinga akisema: “Sifahamu vipi katika karne hii ya maendeleo kuwa bado wapo watu wasiotaka uhuru. Haki ya mtu kumchagua mwakilishi wake ni hatua ya mwanzo ya kufikia uhuru.”  Hamadi, aliyetoka Ole, Pemba, alikuwa Hizbu.

Siku hizo kaulimbiu ya ASP ilikuwa: “zuwiya”, ikimaanisha uhuru wa Zanzibar uzuiwe.  Hoja ya ASP ilikuwa kwamba uhuru ukipatikana utawafaidia Waarabu waliokuwa wamepata elimu zaidi ya Waafrika.  

Chama cha ZNP (Hizbu) kiliundwa 1955 na miaka miwili baadaye Februari 5, 1957 Nyerere alisaidia kuasisiwa kwa ASP kwa kuziunganisha African Association na Shirazi Association, jumuiya ya Waafrika na ile ya Washirazi.  Chama hicho kilizaliwa kutoka tumbo la ukabila na hata ukunga wake ulikuwa wa kikabila. 

Mikono ya wakoloni wa Kiingereza pia ilionekana katika uzalishaji wa ASP. Hilo halikuwa jambo la kushangaza.  Waingereza walikwishazoea kufanya mambo kama hayo.  Hata Tanganyika mapema 1951, kabla ya TANU kuundwa, wakoloni walimwendea Abdulwahid Sykes na viongozi wenzake wa Tanganyika African Association (TAA), ambayo Nyerere alikuwa mwanachama wake, wakawaambia waunde chama cha siasa kitachokuwa na watu wa makabila mbalimbali.  

Sykes na wenzake walikataa kuwa vibaraka wa Waingereza. Waingereza wakamtomeza V.M. Nazerali, Mtanganyika mwenye asili ya Kihindi, na aliyekuwa mjumbe wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika (Legico) amwandikie barua Dossa Aziz na kumshauri aunde chama cha aina hiyo. Aziz naye alikataa.

Viongozi kadha wa kadha, wakiwa pamoja na Watanganyika wenye asili ya Kihindi, waliendewa na Waingereza waunde chama wakitakacho wao lakini Waingereza waliondokea patupu. 

Kama miaka mitatu baadaye, baadhi ya viongozi hao waliigeuza TAA iwe TANU, chama cha ukombozi. Waliokata uamuzi huo muhimu walikuwa Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, John Rupia, Dossa Aziz na Julius Nyerere. Mwandishi Mohamed Said ameandika kwa urefu kuhusu historia hii na jinsi Nyerere alivyowapiku wenzake.

Walipokuwa kwenye baraza ya Hoteli Avenada, Barwani na Nyerere walikuwa wakinywa huku wakizungumzia mustakbali wa nchi zao.  

Barwani akinywa maji ya nanasi na Nyerere akipiga vitu vikali kidogo.  Barwani alimwambia Nyerere kwamba shida kubwa aliyokabiliana nayo ilikuwa uhaba wa skuli.

“Hatuna skuli za sekondari za kutosha na baada ya sekondari hatuna kitu,” alisema Barwani.

Kwa mujibu wa Barwani,  Nyerere alimjibu hivi: 

“Miye sihitaji elimu, si kwa sasa. Bahati yangu sina watu wengi waliosoma, kwani ni hao wachache (waliosoma) wanaonipa taabu. Watu kama Fundikira, Lugusha, Marealle, ndio wenye kunipinga. Sitaki wengine zaidi ya hao kwa sasa. Elimu itakuja baada ya uhuru.

“Ninachotaka ni magari ya aina ya Land Rover. Nchi yetu ni kubwa, kubwa sana. Ili tushinde uchaguzi ujao, itatubidi tufanye kampeni nchi nzima.  Nitafurahi sana nikipata nchi itayotupa magari ya Land Rover.”

Fundikira aliyemkusudia Nyerere alikuwa Abdallah Said Fundikira aliyekuwa Chifu wa Wanyamwezi wa Itetemya, Tabora.  Lugusha alikuwa Chifu Haroun Msabila Lugusha wa Wanyamwezi wa Sikonge, Tabora, na Marealle alikuwa Chifu Thomas Lenana Marealle, aliyekuwa Chifu Mkuu (au Mangi) wa Wachagga wa Marangu, Moshi. 

Tunaweza kuandika mengi kuhusu kila mmoja wa waungwana hawa waliokuwa wazalendo lakini tukifanya hivyo tunaweza tukapotea njia na tukatoka kwenye mada yetu.

Mazungumzo hayo baina ya Ali Muhsin Barwani na Julius Nyerere ameyadhukuru Barwani kwenye kitabu cha kumbukumbu zake kiitwacho “Conflicts and Harmony in Zanzibar”. 

Barwani na Nyerere walikuwa Accra wakihudhuria sherehe za kuadhimisha mwaka mmoja tangu  Ghana iwe huru.  Walikuwa wageni wa Nkrumah. Waalikwa wengine walikuwa pamoja na Mallam Aminu Kano (Nigeria), Joseph Murumbi na Tom Mboya (Kenya), Rashidi Kawawa na Paul Bomani (Tanganyika), Kanyama Chiume (Malawi) na Eliradi Mulira (Uganda).  

Baada ya kumalizika shamrashamra za maadhimisho hayo, Nkrumah aliwaalika wageni wake nyumbani kwake.

Walipofika, Nkrumah aliwaambia kwamba alikuwa na siri aliyotaka kuwapa. Aliwaeleza kwamba aliwaalika katika sherehe za maadhimisho ya uhuru kama kisingizio kwa sababu akihofia ya kwamba angeliwaambia na mapema sababu hasa ya kuwaalika Ghana, pengine watawala wa kikoloni wangeliwazuia wasisafiri kwenda Accra.

Nkrumah alikuwa na George Padmore, mzawa wa Trinidad, mwandishi na mwanamajumui wa Kiafrika (Pan Africanist) aliyekuwa mshauri wake mkuu wa mambo ya Afrika. Aliwaambia wageni wake kwamba sababu hasa iliyomfanya awaalike Accra ni kuwataka wajadiliane uwezekano wa kuratibu harakati za kuikomboa kila ardhi ya Afrika iliyokuwa chini ya wakoloni.

Nkrumah na Padmore wakawaelezea mpango waliokuwa nao wa kuandaa mkutano mwishoni mwa mwaka huo wa 1958 hukohuko Accra kujadili utumizi wa mbinu za amani, kama zile za Mahatma Gandhi wa India, ili Afrika ijikomboe.

Murumbi, mpiganiaji uhuru kutoka Kenya ambaye siku hizo akiishi Uingereza kwa sababu wakoloni hawakumruhusu aishi Kenya, alisikiliza kwa makini.

Angekuwa Murumbi anaishi Zanzibar ya leo angeingizwa katika kaumu ya wanaoitwa “machotara” na  wabaguzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM). Angetiwa katika kundi hilo kwa sababu baba yake alikuwa Goa, kutoka India, na mamake alikuwa Mmasai. 

Kwa muda mrefu Murumbi alikuwa akisafiria paspoti ya Morocco aliyopewa na babu yake Mfalme Mohamed wa sasa. Alipokuwa London, Murumbi alifanya kazi kubwa ya kuueleza ulimwengu kuhusu madhila yaliyokuwa yakifanywa na wakoloni nchini Kenya.

Siku hiyo alipokuwa Accra nyumbani kwa Nkrumah akimsikiliza kiongozi huyo wa Ghana na mshauri wake Padmore, Murumbi alikuwa na swali lililokuwa likimhangaisha.

Aliuliza: “Tuwaalike viongozi wote, au wale tu tunaowajua kuwa ni wazalendo? Kwani kuna baadhi ya viongozi kama vile wale wa Afro-Shirazi wa Zanzibar wenye kukipinga chama cha Ali Muhsin, na wanajulikana kuwa ni vibaraka wa Waingereza. Tuwaalike nao pia?”

Nkrumah, aliyekuwa amekaa kitini, nusura aruke. Alifoka: “Hapana! Hatuwezi kuwa nao vibaraka!”

Nyerere aliingilia kati kumsaidia rafiki yake kiongozi wa ASP, chama ambacho yeye mwenyewe alisaidia kukiunda.

Alisema: “Nadhani itakuwa jambo la busara zaidi kuwaalika. Watu kama hao si vibaraka kwa imani. Hawajui (mambo). Wakija hapa na kuwa nasi watashajiika kuwa na msimamo wa kizalendo, na hivyo wataiimarisha dhamira yetu badala ya kuidhoifisha.”

Nyerere aliitoa hoja yake kwa ulimi wa asali. Na ilikuwa vigumu wenzake kumpinga. Padmore akatoa rai ya namna ya kulitanzua tatizo hilo.

“Tutauandika mwaliko kwa namna ambayo wakikubali kuja, mabwana zao wa kikoloni hawatokuwa tena na imani nao, na watajikuta peke yao,” alisema Padmore.

Taarifa ya mwaliko wa mkutano huo wa mwisho wa mwaka wa 1958 iliulaani vikali ukabila.  Kwa vile ukabila ulikuwa moja ya nguzo za ASP, kama ilivyotazamiwa Karume aliupinga mkutano wa Accra.

Alipopelekewa mwaliko alifanya mkutano mkuu wa hadhara Miembeni, Unguja, na akasema: “Uhuru wetu hautotoka Accra, wala hautotoka Cairo. Utapokuja, utatoka London. Wenye kudai uhuru sasa ni wapumbavu. Hatuwezi hata kutengeneza sindano.  Bado tuna miaka mingi ya kujifunza kutoka kwa Waingereza. Tutapokuwa tumekwishajifunza ndipo tutapowaambia waalimu wetu ‘Goodbye’. Sendi popote kutafuta uhuru.”

Karume aligoma.  Hakutaka kwenda Accra kuhudhuria Mkutano wa Mwanzo wa Waafrika Wote (All African People’s Conference).  

Vuguvugu la Umajumui wa Kiafrika la Afrika ya Mashariki na ya Kati (PAFMECA) liliwatuma Francis Khamisi kutoka Kenya na Kanyama Chiume kutoka Malawi kwenda Zanzibar kusema naye Karume.  Baada ya kumbembeleza kwa muda mrefu, hatimaye Karume akakubali kwenda Accra akifuatana na Barwani pamoja na Abdulrahman Babu aliyekuwa katibu mkuu wa Hizbu.

Hatujui pangetokea nini Nyerere angelishindwa kumtetea Karume mbele ya Nkrumah.  Gurudumu la historia likishapitia njia fulani huwa muhali, haiwezekani kabisa, kulirejesha nyuma na kulifanya lipite njia nyingine. Likishapita ndo limekwishapita. 

Lile la historia ya Zanzibar tangu mwongo wa 1950, kwa kiwango kikubwa, limekuwa likisukumwa na Nyerere.  

Tangu aanze kuziingilia siasa za Zanzibar 1957, Nyerere ndiye aliyekuwa akilisukuma gurudumu hilo .  Alifanya hivyo kwanza kwa kuzishawishi siasa za ASP na baada ya Aprili 1964 kwa kuidhibiti Zanzibar nzima.  Gurudumu alilolisukuma ndilo lililoifikisha Zanzibar hapa ilipo.a

LIFAHAMU Kundi la Lazarus.. Kundi Tishio Duniani kwa Kuingilia na Kudukua Mifumo ya Kompyuta...!!!

$
0
0

Kundi la Lazarus ndilo kundi lenye kuheshimiwa zaidi kwa sasa duniani kwa kuwa na uwezo wa hali ya juu kabisa wa kuingilia mitandao mbalimbali na nyeti na kisha kudukua taarifa mbalimbali.

Pia kundi hilo la Lazarus linasadikiwa kuhusika na uingiliaji mitandao ya kibenki, usafiri na habari na kisha kuvuruga taratibu za uendeshaji mifumo hiyo.

Kundi la Lazarus wanajulikana kwa kutumia mtindo wao uitwao “Shadowy Hacking Collective” ambapo wanatumia msimbo au “codes” maalum kuingilia mifumo ya kompyuta.

Mwaka 2014 Lazarus waliingilia mifumo ya kampuni ya Sony ambayo inatumia programs za windows na kusababisha kutotolewa kwa filamu ya kichekesho iitwyo INTERVIEW ambayo ilikusudia kumwonyesha kiongozi wa Korea Kaskazini .

Wakitumia jina lingine la Guardians of Peace kundi hili walianza kutoa hadharani taarifa za barua pepe, taarifa binafsi na taarifa mbalimbali za ndani.

Wakitoa sababu za kuingilia studio za kampuni ya Sony zilizoko mjini Hollywood, kundi la Guardian of Peace walidai kwamba walifanya hivyo ili kulipa kisasi kutokana na matengenezo ya filamu hiyo ya INTERVIEW.

Hata hivyo baadae raisi wa Marekani wakati huo Barak Obama akaomba radhi wapenzi wa filamu kwa kuwaambia kwamba kulikuwa na makosa fulani ya kiufundi na kuonekana kuwatumia lawama nchi ya Korea Kaskazini ambayo nayo ilikanusha kuhusika na udukuzi huo na kusema kwamba ni CIA na washirika wao ndiyo walikuwa wakipanga njama za kumuua kiongozi wa taifa hilo.

Kundi la Lazarus halikuishia hapo katika kampeni zake za kuangamiza mifumo ambayo haina ulinzi wa kutosha dhidi ya mitandao. Mwezi February mwaka 2016 kundi la Lazarus waliingilia mifumo ya kibenki nchini Bangladesh na kuchukua fedha kiasi cha dola milioni 100.

Kitendo hicho kiliendelezwa hadi katika nchi za Vietnam na Phillipenes ambapo misimbo au “codes” za Lazarus za Trojan.Banswift zilitumika na na program hasidi au “malware” ilojulikana kwa jina la Backdoor.Contopee iligundulika kuwa ilitumiwa na Lazarus.

Kampuni kubwa ya Symantec ya Marekani ikitumia watafiti wake na wachunguzi mbalimbali, walitoa taarifa kadhaa kuonyesha jinsi msimbo inavyotumiwa ambapo ilionekana inatokea sehemu moja.

Pia kuthibitisha hayo mtafiti na muanzilishi wa Anti-Virus software ya MacAfee bwana John MacAfee nae amethibitsha kwamba kundi hilo lipo na limegawanyika sehemu mbalimbali duniani.

Baada ya shambulizi la siku ya Ijumaa, serikali nyingi duniani, taasisi na makampuni mbalimbali zimetahadharishwa juu ya uwezekano wa kuwepo kwa mashambulizi zaidi katika mifumo na mitandao ambayo haiko salama.

Kwa mujibu wa taasisi ya usalama wa mitandao NCSC na ile ya ulinzi wa taifa ya Marekani ya NSA wadukuzi wamepanga kushambulia vifaa vya kiteknolojia ambavyo huunganishwa katika mitandao ya internet kama simu ya mkononi au smartphones, televisheni au Smart TV, kompyuta mpakato, tablets na saa za mikononi zenye simu au smartwatch.

Vifaa vingine na mitambo ni kama vile webcam, taa za kuongozea magari yaani traffic lights, mitambo ya kufua umeme, taa za barabarani, majokofu ya Samsung ambayo yana tumia teknolojia maalum ya kuyaongoza, mifumo ya camera za ulinzi ya CCTV na hata kamera maalum za kuwaangalia watoto wachanga au Video baby monitors vifaa ambavyo zinaunganishwa katika mitandao ya internet.

Mashambulizi ya kutumia ransomware katika vifaa tajwa hapo juu yatasababisha matatizo makubwa kwa watengenezaji hali itakayopelekea ugumu wa idara za usaidizi au support katika kutoa msaada kwa wateja kujaribu kufungua vifaa hivyo endapo vitadhurika na kirusi cha Ransomware.

Serikali mbalimbali duniani zimechukua hatua kadhaa ikiwa ni pamoja na kufanya vikao vya dharura na pia kuchukua hatua za tahadhari kulinda miundombinu muhimu.

Kwani kundi la Lazarus halijulikani na pia hakuna anaefahamu kundi hili linejipanga vipi kwa sasa.

WATOTO Walionusurika Kwenye Ajali ya Basi la Shule Wamefika U.S.A..!!!

$
0
0

Samaritan’s Purse has brought three severely injured Tanzanian children, the only survivors of a bus accident that killed 35 people and recently made world news, to the United States. They will be receiving specialized trauma care at a hospital in Sioux City, Iowa.

On Friday, May 12, Samaritan’s Purse sent our DC-8 airplane to Tanzania to pick up the children—Wilson, a 12-year-old boy; Sadhia, a 12-year-old girl; and Doreen, a 13-year-old girl. Their mothers have accompanied them on the journey, along with a Tanzanian doctor and nurse, as well as Ed Morrow, director of World Medical Mission, the medical arm of Samaritan’s Purse. They all arrived in Charlotte late Sunday night, May 14, and were quickly transferred to a specially equipped Phoenix Air plane that transported them to Sioux City.

“When I heard about the tragic bus accident in Tanzania and the three children who survived, I knew Samaritan’s Purse had to do everything we could to help,” President Franklin Graham said.

Thirty-two of the children’s primary school classmates and three adults—two teachers and the driver—were killed in the May 6 crash when their bus plunged off a gravel road into a steep ravine in remote northern Tanzania. They were on the way to another school to take an exam when the accident occurred. Tanzania President John Magufuli called the accident a national tragedy.

MBUNGE Lema Ampongeza Lazaro Nyalando Ajali ya Watoto Arusha

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Goodbless Lema amemshukuru Mbunge Lazaro Nyalandu kwa kufanikisha safari ya Marekani ya watoto watatu ambao walinusurika kifo katika ajali ya basi la shule ya Lucky Vicent iliyotokea Karatu na kusababisha vifo vya watu 35.

Mh. Nyalandu alikuwa bega kwa bega na kufuatilia kila hatua kuhakikisha watoto hao pamoja na wazazi wao na daktari wanasafiri kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kupata matibabu zaidi. .
. "Mh Lazaro Nyalando , Mungu akubariki sana kwa kazi nzuri ya kusaidia watoto waliopatwa na ajali hapa Arusha, jitihada zako Mungu atakulipa" alisema Godbless Lema
Katika hatua nyingine Mhn Lazalo Nyalandu ameomba pesa zitakazo endelea kuchangwa na Watanzania na watu wengine duniani kwa ajili ya watoto hao zitumike kujenga ICU katika hospitali ya Mount Meru. .
.
TOA MAONI YAKO HAPA

SIMBA Kumenuka...Wengine Watatu Kujiuzulu

$
0
0

Leo Mei 14, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Simba, Zacharia Hans Poppe ameachia ngazi.


Habari za uhakika zimeeleza kuwa Hans Poppe ameandika barua ya kuachia ngazi baada ya kuona mambo yanaendeshwa ndivyo sivyo katika klabu hiyo.  


Hata hivyo baada ya taarifa hiyo, Wengine wanaotajwa kuwa huenda wakajiuzulu nyadhifa zao kwenye kamati ya Utendaji ni Kassim Dewji, Abdallah na Nassoro 
Viewing all 104785 articles
Browse latest View live




Latest Images