Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live

TCRA Yatoa Tahadhari Juu ya Tishio la Virusi wa Kwenye Kompyuta Wnaoshambulia Dunia Nzima..!!!

$
0
0

KUFUATIA tishio la kuwapo kwa ‘software’ yenye virusi aina ya WannaCry, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewatahadharisha watumiaji wa kompyuta kutofungua viambatanishi wasivyovijua kwenye barua pepe zao.

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba,  amesema kufuatia tishio hilo taasisi zianza kuchukua tahadhari kwa kutunza data (taarifa) nje ya mtandao ili kuepuka athari hizo kama kutatokea kompyuta kusambuliwa na virusi hivyo.

Kilaba amesema tishio la virusi WannaCry haliko kwenye kompyuta pekee bali pia kwenye simu za kisasa endapo utafungua kiambatanisho au link yenye virusi hivyo.

“Endapo mtumiaji au taasisi wanakumbwa na tatizo hilo basi watoe taarifa kwa Timu ya kitaifa ya dharura ya kompyuta (TZCERT),”

NDALICHAKO Awasimamisha Kazi Vigogo Wawili Sakata la Vitabu vya Kufundishia..!!!

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi vigogo wawili hadi uchunguzi wa sakata la vitabu vya kufundishia utakapokamilika.

Waliosimamishwa ni Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu (TIA) ambayo ndiyo imepewa idhini ya kusimamia ubora wa vitabu.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jana (Jumatatu) kutokana na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Esther Mmasi kutoa hoja ya kushika shilingi katika mshahara wa waziri akitaka uamuzi kuhusu suala hilo.

Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wa kambi zote bungeni wakiwamo, Philipo Mulugo (Songwe -CCM), Peter Serukamba (Kigoma Kaskazini -CCM), Suzan Lyimo (Viti Maalumu -Chadema) na Mwita Waitara (Ukonga -Chadema).

Profesa Ndalichako akijibu hoja hizo, amesema ameunda tume kuchunguza suala hilo na kuwahakikishia kuwa waliohusika hawako katika taasisi ya TIA.

“Nawahakikishia kuwa baada ya kukamilisha uchunguzi kila aliyehusika atabeba msalaba wake,” amesema.

ALIYEKUWA Mke wa Sugu Faiza Ally Akinukisha Tena Huko Instagram

$
0
0
Msanii wa filamu, Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka mengi kuhusu watu wanaomfuatilia kupitia mitandao ya kijamii.


Faiza Ally

Muigizaji huyo ambaye alikuwa mke wa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu, amedai anaumizwa sana na komenti hizo kutoka mitandaoni.

“Huna hizi komenti huwa nazichukia sana na huenda mkawa mnahisi labda zina nifurahisha, oh nilikua sikuelewi sasa nimekuelewa,  oh wakuseme kwa yote sio malezi, yote yapi unayo yajua wewe kuhusu maisha yangu?.  Oh siku hizi umetulia hivi unanijua mimi mpaka unasema as ni kama mtu anae nifahamu sana?.  Hivi mna jua maana hizi comment kweli?,”  Faiza Ally aliandika Instagram.

Aliongeza, “Nikikuuliza yapi mengine utajibu nini ? . Chupi au kipande cha tako? ni nini unacho kijua kwenye maisha yangu zaidi ya mavazi ?. Je hayo ndio yanayokupa nafasi ya kunijua mimi ni nani? Guys pls stop that stupid comment on my page I am more than that sawa????? First you all should know kuwa mama ni jukumu so haliingilini na chochote… nikikwambia sifa nilizo nazo kwangu kwenye familia yangu pengine no one of you mnazo au mnaweza kunifikia kwa hivyo nina jisikia vibaya vijitu vya insta visivyo jielewa just be coz vimeona picha za tako na chupi au vimebebwa na mabwana wenye hela au labda vimeolewa basi kujifanya vinaweza kunijaji! Ktk maisha yangu mm ni bora zaidi ya yoyote … sio mwenye digrii wala kiongozi wala mke wala yoyote ! Na to cut long story short sijaanza kumlea tu sasha nimeanza kulea familia in a very young age and i maneji kusomesha Watoto zaidi wa tatu na mmoja Leo yuko form four sawa ?? So I am not only a mom … ni shangazi,ni dada,na mama wa mama Yangu na baba Yangu mzazi… na sikukua na elimu wala sikua na jina la baba wala la yoyote na sijawahi kuwa mdananda kwa namna yoyote …. I AM WHO I AM TODAY BE COURSE OF ME …. nguvu zangu akili,zangu uwezo wangu ndio umenifanya niwe mm bila hata kutegemea ada ya nyumbani… na sibebwi na jibeba !!!! save ur stupid comment kwa wajinga wenzio i am not one them !!!! 😏,”

BAADA ya Ajali ya Lucky Vicent, Kamanda Mpinga Ameanzisha Operesheni hii

$
0
0
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga, amesema mara baada ya kusikia ajali iliyoua wanafunzi zaidi ya 30 wa Shule ya Lucky Vicent ya Mkoani Arusha, alichukua hatua kadhaa na sasa wanafanya operesheni ya nchi nzima.


Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Mohammed Mpinga.

Akizungumza na kipindi cha Super Mix cha East Afrika Radio, Kamanda Mpinga amesema alipata mshkuko mkubwa sana hasa alipoambiwa lile gari limetumbukia kwenye korongo likiwa na wanafunzi.

“Kitu cha kwanza nilichofanya, kwa vile mimi ni msaidizi wa Inspector General wa Jeshi la Polisi, ilibidi kumtaarifu, sambamba na hilo ni kumuelekeza  mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Arusha kufuatilia kwa ukaribu na kunipa taarifa mara kwa mara.

“Aidha vile vile nikaongea na RPC wa Mkoa wa Arusha kuhusu tukio lile na kutoa maelekezo ya kufuatilia kwa karibu ile kuweza  kujua nini hasa chanzo cha ajali,” amesema.

Katika hatua nyinge Kamanda Mpinga amesema kwa sasa wanafanya operesheni ya nchi nzima kwani ajili ile imewafanya waongeze nguvu zaidi.

“Sio kwamba huko nyuma tulikuwa hatufanyi lakini tukio hili sasa limeongeza umakini na kizuri ni kwamba tunaungwa mkono na wakuu wa shule, wamiliki, wananchi kwa ujumla, na wazazi kwamba ni zoezi ambalo tunafanya ni zuri.

“Uko nyuma walikuwa wakilalamika wanafunzi wetu wataendaje shule, lakini sasa tunaungwa mkono, kwa hiyo lazima tufanye kwa nguvu na kila mtu anaona umuhimu wa usalama wa mtoto wake anapokwenda shule na anaporudi,” amesema na kuongeza.

“Bodaboda si sahihi kubeba wanafunzi kwa kupeleka shule lakini tax ni sawa endapo itazingatiwa idadi inayotajwa kwa mujibu wa sheria, yaani nyuma wanafunzi watatu na mbele mmoja, hiyo ni sahii hakuna tatizo. Hata kwenye bajaji si sahihi, lakini mtoto chini ya umri wa miaka tisa huwezi kumpakia kwenye bajaji hadi awe na mtu mwingine mkubwa amekaa naye na si vinginevyo,” amesema Kamanda Mpinga.

Amesema kuwa ukaguzi ambao wanaofanya, kwanza ni uzima wa gari lenyewe, kujua kama linafaa kukaa barabarani, pia ukaguzi kuhakikisha nyaraka zote wanazo, idadi ya wanafunzi wanaopakia ipo sawa sawa na uwezo wa gari lenyewe, pia je wana leseni ya Sumatra ya kupakia wanafunzi, na kama ni gari la wanafunzi linatakiwa kupakwa rangi ya njano na ubavuni kuandikwa School Bus kila mtu ajue lile gari ni la wanafunzi.

“Kibaya ninachosikia hawa wamiliki wa mabasi wameyaficha magari, wanaogopa kuyaleta barabarani lakini tunachotaka kufanya tuende mpaka kwenye shule zenyewe tukute magari kule. Watu wanafikiri hadi kitu kitangazwe lakini huku chini chini vitu vinafanyika wao wasie na wasi wasi tunafanya kazi,” amemaliza kwa kusema.

By Peter Akaro

JACK Wolper “Kwenye Maisha Yangu Sijawahi Kuachwa, Sina Kabisa Record Hiyo"

$
0
0
Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kuizungumzia ishu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize.

Muigizaji huyo amedai hana msongo wa mawazo kutokana na tukio hilo huku akidai hajaachwa kama baadhi ya watu kwenye mitandao wanavyodai.

“Kuachwa ndio nini? kweli ulilolijua ni kama usiku wa giza,” Wolper alikiambia kipindi cha U Heard cha Clouds FM. “Kwenye maisha yangu sijawahi kuachwa, sina kabisa record hiyo sema sitakagi kufanywa mjinga. Yeye kama amezungumza ishu ya kuachana na mimi, mimi sitaki kulizungumzia kwa sababu na mambo yangu mengi ya umuhimu nafanya,”

Harmonize hivi karibuni alifunguka na kuweka wazi kwamba hayupo tena kwenye mahusiano ya mrembo huyo kutoka tasnia ya filamu huku akishindwa kueleza sababu.

MAHAKAMA Yaamuru Halotel Kulipa Faini ya Shilingi Milioni 700..!!!

$
0
0

MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Viettel Tanzania ‘Halotel’, Do Manh Hong na wenzake nane wamehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya milioni 700 baada ya kupatikana na hatia katika mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.

Hukumu hiyo, imetolewa baada upande wa mashtaka kuomba kufanyia marekebisho hati ya mashtaka kwa kuondoa mashtaka matatu Kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili.

Mashtaka mapya ni pamoja na kusimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutumia mitambo ambayo haijathibitishwa na kuitia hasara Serikali na TCRA ya milioni 459.

Akisoma Hukumu hiyo, Hakimu Wilbard Mashauri amesema amewatia hatiani washtakiwa mwenyewe baada ya kukiri kutenda makosa yao

Kabla ya kuwasomea hukumu, Hakimu aliwauliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote ambapo wakili, Johavenes Zacharias ameiomba mahakama kutoka adhabu stahiki kwa washtakiwa.

Naye Wakili wa utetezi, aliiomba mahakama kuwapa adhabu ndogo washtakiwa kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza na wanafamilia zinazowategemea.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mashauri amewahukumu washtakiwa kulipa faini ya jumla ya faini ya milioni 700. 

Akifafanua adhabu hiyo, hakimu Mashauri amesema kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya milioni tano kwa kila shtaka linalomkabili na pia walipe milioni 459 kwa TCRA kwa hasara waliyoisababisha.

Ameongeza kuwa, ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwao na kwa wafanyabiashara wengine wanaohujumu uchumi.Ameongeza kuwa, watuhumiwa wamekuja nchini kuwekeza kwenye biashara na siyo kuhujumu mitambo ya nchini.

"Washtakiwa hawa ni wafanyabiashara na wamekuja kwa ajili ya kuwekeza, hivyo ili kuonyesha Tanzania ipo makini kwenye masuala ya uwekezaji lazima wafate sheria" amesema Mashauri.

Mbali ya Hong, watuhumiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka na Viettel Tanzania Limited.

Katika mashtaka yao wamedaiwa, kuwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 Dar es Salaam walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.

Wanadaiwa kuwa katika kipindi hicho waliendesha hiyo mifumo ya kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila ya kuwa na leseni.Pia inadaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki bila ya kuwa na leseni. Pia katika tarehe isiyofahamika Novemba 2016 walisimika vifaa hivyo ikiwamo sim box yenye namba ya siri 1152000.8.n.t.n na Laptop mbili aina ya Dell bila ya kuwa na kibali cha TCRA.

Katika kipindi hicho, washtakiwa hao wanadaiwa kuunganisha vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.

Kwa upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la kusajili lakini za simu 1000.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA na serikali ya Tanzania ya milioni 459.

Mpaka mwandishi  anaondoka katika viunga vya Mahakama, ni mkurugenzi pekee ndiye aliyelipa faini, huku watuhumiwa wengine wakiendelea kusota lupango.Mkurugenzi huyo amelipa jumla ya milioni 479 ambazo ni faini yake ya milioni 20 ambapo ni kwake yeye na kampuni na Viettel Tanzania Ltd.

KAMANDA Sirro Ametoa Ufafanuzi Kuhusu Askari Aliyefyatua Risasi Hewani Mbele ya Waziri wa Zamani..!!!

$
0
0
'
Kamishna Sirro asema mzozo kati ya Polisi na Adam Malima ulisababishwa na kuegesha gari vibaya na alipotakiwa kulipeleka 'yard' alikataa.

Kamanda Sirro ametoa ufafanuzi kuhusu askari aliyefyatua risasi hewani mbele ya Waziri wa zamani Adam Malima, "Waziri alikataa kutoa gari"

"Kukosekana maelewano ndio kilichofanya askari kutumia nguvu ya ziada na kufyatua risasi tatu ili kuwatuliza wananchi"

Kamishna Sirro: Polisi alifyatua risasi hewani kuwatawanya watu na kufanikisha ukamataji wa mtuhumiwa. Ile ni mbinu ya kufanikisha ukamataji

Kamanda Sirro ametoa kauli muda mfupi uliopita wakati akiongea na waandishi wa habari leo.

Majibu haya yametokana na Mjala unaoendelea Mtandaoni kuhusu Adam Malima kutishiwa kwa Bunduki

BAADA ya Kuonyeshwa Bunduki Jana na Polisi..Waziri wa JK Apandishwa Kizimbani kwa Kosa la Shambulio..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Adam Malima amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la shambulio.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono alidai kuwa Mei 15,2017 katika eneo la Masaki kwa makusudi Malima alimzuia Ofisa wa polisi H.7818 PC ABDU kufanya kazi yake halali.

Malima ambaye alikuwa mbunge wa Mkuranga amedaiwa kumzuia Ofisa huyo kufanya kazi yake ya kumkamata Ramadhani Kigwande kwa kosa la kumshambulia Mwita Joseph.

Kwa upande wa mshtakiwa wa kwanza, Ramadhani Mohammed Kigwande naye anakabiliwa na shtaka la kushambulia Mwita Joseph.

Wakili Kombakono aliendelea kudai kuwa Mei 15,2017 kwenye eneo hilo la Masaki wilaya ya Kinondoni mshtakiwa huyo akiwa na nia ya kumzuia Mwita Joseph ambaye ni Ofisa oparesheni wa kampuni ya Priscane Business Enterprises  wakati alipokuwa akimkamata kwa kupaki vibaya gari namba T 587 DDL alimshambulia(Mwita) na kumsababishia maumivu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo,washtakiwa wote waliyakana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.

Hakimu Mkazi Mkuu,Respicius Mwijage alimtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja ambaye atasaini bondi ya Sh 5milioni.

Washtakiwa wamekamilisha masharti ya dhamana na kuachiwa huru.

 Washtakiwa wanatetewa na wakili Peter Kibatala ambaye amewasilisha pingamizi dhidi ya shtaka la pili kuwa shtaka halifanani na maelezo ya kosa.

Hakimu Mwijage ameiahirisha kesi hiyo namba 168 ya 2017 hadi Juni 15,2017 kwa ajili ya kutajwa ambapo pia pingamizi hilo litasikilizwa.



Siwezi Kumsamehe Mke Wangu, Ametembea na Mkurugenzi wa Ofisini Kwake

$
0
0

Baada ya kupoteza kazi yangu niliyumba sana, niliwaza nitaishije bila kazi hapa mjini, hata hivyo nilijipa moyo kwamba kwa kuwa wife ana kazi Basi mambo madogo madogo hayatasumbua wakati huo nami nitakua nakazana kutafuta kazi nyingine.


Kumbe nilikua nimekosea kuwaza hivyo, ilianza taratibu kama mzaha wife kuchelewa kurudi na kuja kuanzia saa tano usiku na kuendelea kwamba wamelazimika kufanya overtime.


Baada ya wiki kadhaa visingizio vikaisha akawa hana cha kusingizia tena, anakuja usiku ule ule mwingi bila kunisemesha chochote na kupitiliza chumbani kulala moja kwa moja bila kula wala kuoga.


Nikajiuliza, kwa biologia ya wanawake ilivyo na joto la Dar inawezekana wife akarudi na kulala tu bila kuoga? Na chakula je ina maana analala na njaa? Nikasema nitapata tu majibu ya maswali Haya, only time will tell.


Hadi napoteza kazi yangu sikua namiliki Gari wala wife hakua nalo, baada ya hizi harakati za kurudi usiku mwingi na kutoshinda home weekend nzima hatimaye wife """"" akanunua Gari""""" Toyota IST.


Nilikua naumia rohoni kwa suspicion but sikujua where and how to start investigation on that particular matter hadi siku moja tulienda pamoja na wife kwenye Gari lake na mdogo wake wa kike aliyekuja toka Jana yake.


Mimi niliomba nikae nyuma wao mbele, kabla hatujaondoka nashangaa kuiona chupi ya wife bikini pembeni ya miguu yangu ndani ya Gari, kwa kifupi ile safari ilikufa.


Nilimtoa ndani ya Gari kwa kipigo kikali sana nikitaka kujua kulikoni hiyo chupi kuwepo humo, hakawa hana cha kujitetea, nikamfungua chumbani na nikachukua simu zake zote nikawa nazo sebuleni, tangu kufunga ndoa sikuwahi kumpiga zaidi ya siku hiyo.


Hapo sebuleni nilipitia meseji zote kwenye simu zake, baada ya zoezi hilo nililidhika beyond reasonable doubt my wife was seeing someone else.


Na mtu huyo alikua ni mkurugenzi wake kazini, na hiyo kampuni anayofanya wife ni ya huyo bosi, nikamfungulia saa tatu usiku na kumpa simu zake nikaendelea na mambo mengine.


Sikupata usingizi siku hiyo, nilikaa kwenye TV nikibadilisha Chanel mbali mbali, saa nane usiku alinifuata sebuleni na kupiga magoti akaniomba msamaha kwa machozi kwamba hatorudia, haelewi kwa nini alifanya vile, sikumjibu nikamwambia arudi alale.


Nika conclude kwamba sina mke, nikaazimia kwamba nisilete fujo, kwa hali niliyonayo nijifanye -- tu huku moyoni nikijua sina mke, halaf niendelee ku fight nikifanikiwa niachane nae niendelee na maisha yangu.


Wife ali pretend kwamba ametubu na ameachana na yule jamaa, lakini kwa siri aliendelea nae, hakujua kama mimi najua yule mpenzi wake ndie bosi wake kazini, alikua amenidanganya kwamba ni mteja wa kampuni yao na kwamba hawaonani tena.


Kunipumbaza, kwa mara ya kwanza, ilikua ni Ijumaa, akaja na bahasha akanipa ilikua na million mbili za elfu kumi kumi, kaniambia amepata kazini baada ya kufanya deal, nikazipokea nikaziweka benki, Ili kuni fool kila siku mbili tatu au wiki alikua ananiletea pesa, laki tano na kuendelea nami nikawa natunza pesa nikikusanya mtaji.


Nikaanza kufanya shughuli zangu za kibiashara, kidogo kidogo mambo yangu yamekua mazuri kwa pesa hizo hizo za uzinzi wa wife, yeye kwa kipindi chote anaamini kwamba amenifanya --
, akienda kulala kwa hotels na huyo jama, wakati mwingine akiaga anakwenda safari kikazi kumbe yupo humu humu Dar, nami nikajifanya mjinga nikajiimarisha.


Kila jambo lina mwanzo na mwisho, mkurugenzi kapata msichana mpya kazini inaonekana mke wangu katemwa, yupo tu nyumbani namuacha hapo asubuhi naenda kwa business zangu narudi jioni, nikimuuliza kulikoni analia tu, yupo frustrated, ndipo nikapata chanzo kikanieleza yaliyotokea huko kazini kwao, mapenzi na bosi yamefikia mwisho.


Nimeishi kwa mateso rohoni kwa miaka 4, huku nikificha hasira yangu, nikishiriki tendo la ndoa, ili kumhadaa huyu mzinzi bila yeye kujua, sikuwahi kupata wazo la kufumania kwa kua nilikua nitaharibu mpango wangu.


Wiki hii najiandaa kuhamia kwangu ingawa ni vyumba viwili na sitting room but it is my home, naenda kuanza upya

Nasamehe mtoto pia, nitapata mwingine, kwanza sina imani kama ni wangu, nitaondoka na begi tu.


Yote Tisa, kumi nimepona rohoni, nasikia amani sana.


Kusamehe ni msamiati kwangu kwa sasa, hatua hii niliipanga miaka minne nyuma.


Ama kweli poteza kazi ndo utajua sura halisi ya mkeo

RAY - Kuyumba kwa Tasnia ya Filamu ni Kitu cha Kawaida..!!!

$
0
0

Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ amedai kuyumba kwa tasnia ya filamu ni hali ambayo inaweza kuikumba tasnia yoyote.

Muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri na filamu ‘Gate Keeper’ amedai hali hiyo itaondolewa na wasanii hao kwa kufanya kazi kwa bidii.

“Tasnia ya filamu haijafa kama baadhi ya watu wanavyodai bali imeyumba na kuyumba ni kitu cha kawaida kabisa kwa binadamu kwani anaweza kuanguka na akasimama tena,” Ray Kigosi aliimbia Bongo5.

Anasema kwa hali hiyo wao kama watayarishaji wakubwa wamekaa kimya wakijipanga na kuendeleza harakati ambazo zitainua tena soko lao na filamu kurudi katika ubora wao kama zamani pamoja na changamoto zinazojitokeza kwao ni kipindi cha mpito tu.

“Lazima tasnia itarudi kama awali, ni sawa tu na maisha ya mtu asiyekata tamaa katika kutafuta anapopata changamoto anajipanga na kurudi tena na sisi itakuwa hivyo tutarudi kama awali,” anasema.

Daaaaa, Hii kali: Binti Adaiwa Kunyonga Kichanga Chake cha Siku 3, Kisha Kukizika

$
0
0

KAGERA: Katika hali isiyokuwa ya kawaida Binti mmoja anayeishi mtaa wa Ntungamo Kata ya Buhembe, Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera, Latifa Vedasto anadaiwa kumnyonga mtoto wake aliyejifungua siku tatu zilizopita na kisha kumzika 

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi linamshikilia binti huyo mwenye umri wa miaka kumi na minane kwa uchunguzi zaidi baada ya kufukua shimo alilokuwa amezikwa kichanga huyo. 

Chanzo: TBC 1

GAMBO Afunguka Mengine Mapya Kuhusu Michango ya Rambirambi za Msiba wa Wanafunzi Arusha..!!!

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema anasikitishwa na baadhi ya  viongozi wa kisiasa ambao wamelichukulia suala la vifo vya wanafunzi 32 wa Lucky Vicent kisiasa.

 Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Gambo amesema  uongozi wa mkoa wa Arusha umeamua kutoa taarifa ya wazi kwa yumma kuhusu michango iliyotolewa na matumizi yake.

“Hili si tukio la kisiasa bali ni mtihani na changamotyo kubwa uliozikumba familia za wananchi wetu. Wakati serikali inahangaika na shida za watu tunasikitika kuona baadhi ya viongozi wa kisiasa wanahangika na mitandao ya kijamii,”imesema taarifa hiyo

 Taarifa hiyo iliyoambatana na jedwali lenye mchanganuo wa rambi rambi hizo inaonyesha kuwa jumla ya michango ya serikali na ya wadau ni Sh 261.3 milioni.

Michango ya  Serikali ni Sh 102.7milioni na ya wadau ni Sh 158.5milioni.

 Katika mchanganuo wa taarifa hiyo, Gambo amesema familia za  wafiwa hao zitapewa Sh 3,857,143 kwa kila familia. Kila familia ilipewa Sh1milioni siku ya kuaga miili uwanja wa Sheikh Amri  Abeid.

     

Jambazi aliyeuawa na Askari Dar alikuwa akisema "Allahu Akbar, Allahu Akbar"

$
0
0

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, , Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, jambazi aliyeuawa juzi katika eneo la Kurasini, Manispaa ya Temeke, na wenzake wawili kutoroka, alikuwa anataka kupora Sh. milioni 320 kutoka katika gari la kampuni ya G4S lililokuwa likizisambaza kwenye mashine za kutolea fedha (ATM) za CRDB.


Fedha hizo zilikuwa kwenye gari lenye namba za usajili T155 DCB aina ya Nissan mali ya kampuni ya ulinzi ya G4S huku likisindikizwa na askari wawili wa kikosi cha FFU.


Alisema wakati wahudumu wa G4S wakisambaza fedha, mmoja wa watu waliokuwa katika bodaboda hizo ghafla aliruka na kumvamia askari kwa lengo la kumpora silaha ili kufanikisha zoezi la uporaji wa fedha hizo. Alisema kuwa baada ya kitendo hicho jambazi huyo aliamriwa asimame lakini alikaidi na ndipo alipopigwa risasi iliyomjeruhi mguuni na nyingine tumboni kisha aliishiwa nguvu na kusika akitamka " Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar"

DOGO Janja Aingia Kwenye Bifu Zito na Davido wa Nigeria..Amchana Kuwa Hajui KuvaaKama Yeye..!!!

$
0
0

Rapa Dogo Janja amefunguka na kusema msanii kutoka Nigeria Davido licha ya kuwa na pesa nyingi lakini msanii huyo hajui kabisa kupendeza kwani mara nyingi hata nguo anazovaa ni kama zimetundikwa tu mwilini mwake.

Dogo Janja anasema wapo watu wengine wanapesa nyingi lakini suala la kuvaa kwao ni zero na kumtolea mfano Davido kuwa ni moja ya watu ambao wanapesa nyingi lakini hajui kuvaa na hata nguo akivaa zinakuwa hazimkai vizuri mwilini. 

Mbali na hilo Dogo Janja alikwenda mbali na kusema kwa bongo yeye ndiye anakamata nafasi ya kwanza kwa uvaaji kwa wasanii huku akisema msanii mwingine ambaye amekuwa akijitahidi tahidi kwa mitupio kuwa ni G Nako, Jux kwa mbali na Joh Makini.  

Janjaro aliendelea kusema kuwa wasanii wengi wa bongo wamekuwa wakivizia nguo za kutungua Kariako ndiyo maana hawawezi kushindana na yeye kwa kuwa yeye nguo zake anaagiza kutoka nje ndiyo maana anaonekana tofauti na wao katika uvaaji na kupendeza. 

IFAHAMU Kanda Maalum ya Ushirikina..!!!

$
0
0

kila kinachotokea kwenye ulimwengu wa macho ya kawaida ni replica ya ulimwengu wa roho! (Ushirikina ni mkusanyiko wa juju uchawi ulozi chumaulete kuwanga nk)

Tunapozungumzia kanda maalum ya kitu maana yake ni kwamba eneo hilo lina uhitaji wa ziada wa huduma fulani

..mfano Dar kwa sasa ni kanda maalum ya kipolisi kutokana na matukio ya ujambazi kushamiri! Kariakoo kwa sasa ni kanda maalum ya kodi za mamlaka ya mapato Tanzania kutokana na uhitaji wake!

Eneo lote la pwani ya Dar nenda mpaka bagamoyo msata wami pangani mbwewe mkata mpaka tanga mjini ni kanda maalum ya ushirikina 

Hapa ndio kuna vilinge vingi vya ushirikina kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania, hapa ndio kuna wachawi waganga na walozi(kwa ujumla wao washirikina wa kila aina)

Hapa ndo kuna kila aina ya matibabu kuanzia miti shamba tunguli kisomo mpaka uganga/uchawi wa kitabu

Unaweza kwenda mikoani na sehemu tofauti kama gambosh nk lakini ukashindwa kwa hakika kukutana na ushirikina halisi....huu ukanda hukosi 

Kwanini ukanda huu lakini? 

Mazingira na jiografia yanaruhusu, malighafi za baharini na nchi kavu vinapatikana kwa wepesi urahisi na kwa wingi! Taka viungo vya binadamu hupati shida! Taka makombe na mazao bahari mengine ni rahisi mno! Taka variaties ya mizizi miti magome na hata matunda na majani huku sio tatizo kabisa 

Lakini kwanini isiwe ndani ya Dar na ni nje ya Dar na maeneo ya karibu au mbali kidogo?
Ushirikina ni mambo ya kiroho zaidi yasiyo na ithibati za kisayansi! Yanahitaji ukimya utulivu upweke usiri uchache wa watu na kitu chochote kilichoendelezwa na binadamu kwenye ulimwengu wa teknolojia..teknolojia na usasa ni sumu kubwa kwenye ushirikina 

Unaposhuhudia misafara isiyokoma kwa waheshimiwa sana Unaposhuhudia ajali za kila siku! 

Unaposhuhudia upotevu wa watu wazima na watoto! Unaposhuhudia mambo ya ajabu ajabu usishangae sana bali jua kwamba uko karibu kabisa na

YANGA Mabingwa ...Waichapa Toto Africa , Haji Manara Akubali Kushindwa

$
0
0

Ushindi wa Yanga wa goli 1-0 dhidi ya Toto Africans unaifanya Yanga kuusogelea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kufikisha pointi 68 sawa na Simba lakini Yanga wanarejea kwenye nafasi ya kwanza kutokana na wastani wa magoli. 

Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya ligi kumalizika, Simba inahitaji kushinda mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa magoli mengi halafu Mbao nayo iifunge Yanga kwa idadi kubwa ya magoli ili Simba itwae taji la VPL kitu ambacho ni kigumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa. 

Haikua rahisi kwa Yanga kupata ushindi dhidi ya Toto kwa sababu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikua hazijafungana. Goli pekee kwenye mchezo huo limefungwa na Amis Tambwe dakika ya 81 ya mchezo.

KWA Taarifa Yako..Kukaa Muda Mrefu Kwenye Kiti Husababisha Kufa Mapema..!!!

$
0
0

Pengine tayari unafahamu kuwa kutokujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ni hatari kwa afya yako. Ndiyo hilo ni jambo ambalo kila mtu analijuwa (common sense). Vipi lakini ikiwa ni kweli unajitahidi kila siku kutimiza jukumu hilo la kufanya mazoezi dakika 30 hadi lisaa limoja na wakati huo huo unatumia masaa mengi ukiwa umekaa kwenye kiti, ukiangalia TV masaa mengi, masaa mengi umekaa na una kazi katika Kompyuta?.

Ndiyo wewe unadhani kwakuwa unaenda kufanya mazoezi kila siku basi hiyo inatosha, si ndiyo?. Ukweli ni kuwa hata kama wewe ni mtu wa kutembeatembea hapa na hapa lakini kama masaa mengine mengi yanatumika ukiwa umekaa kwenye kiti, mwili wako unakuwa karibu na magonjwa mengi bila mwenyewe kutambua.

Haya ndiyo madhara 7 ya kiafya utakayoyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa masaa mengi kwenye kiti au chini kila siku:

1. Kunakosesha kupata oksijeni ya kutosha

Mara nyingi ukiwa umekaa unapenda kuegemea mgongo na siyo kukaa wima umenyooka, matokeo ya mkao huu ni kuzuia oksijeni kutembea kwa uhuru wote ndani ya mwili na mapafuni kwa ujumla.

Kisayansi tunapumua kwa uhuru wote tukiwa tumesimama na siyo tukiwa tumekaa. Ukiwa umesimamaa ndipo mapafu hupata uwezo wa kujitanua mpaka mwisho na hivyo kuweza kutoa hewa chafu na kuingiza hewa safi ndani kiurahisi zaidi. Hali hii ya kukosa oksijeni ya kutosha mwilini hujulikana kwa kitaalamu kama ‘hypoxia’. Wanasema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6. Bila kupata oksijeni ya kutosha mwilini mwako kunapelekea magonjwa mengi mwilini bila idadi.

2. Unapata kirahisi kansa ya titi na kansa ya tumbo

Kansa ya titi na kansa ya utumbo mpana mara nyingi imeonekana kujitokeza kwa watu wa kula kulala yaani wale wasiopenda kujishughulisha na mazoezi ya viungo. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimesema maisha ya kula kulala yanaweza kukuweka kuwa karibu karibu na kansa kwa zaidi ya 40%. Hii ndiyo sababu wanawake wengi wanapatwa na kansa ya matiti miaka hivi karibuni sababu wengi wao ni watu wa kukaa tu nyumbani masaa mengi tofauti na wanaume ambao hutembea huku na huko kutafuta riziki ya kila siku. Kuepuka kansa ya matiti na kansa ya utumbo mpana epuka kukaa kwenye kiti masaa mengi.

3. Una uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na maradhi ya moyo

Matatizo katika mfumo wa upumuwaji ndiyo moja ya matokeo makubwa unaweza kuyapata ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi. Ni matokeo ya kutokupata oksijeni ya kutosha kama matokeo ya kukaa kwenye kiti masaa mengi. Kwenye utafiti mmoja uliohusisha watu 800,000, wale waliokuwa wakikaa kwenye kiti masaa 10 kila siku walikuwa na uwezekano mara 147 zaidi wa kupatwa na magonjwa ya moyo kuliko wale waliokaa kwenye kiti masaa machache au mara moja moja.

Kuna tafiti nyingi zinazokubaliana na nadharia hii na inatokana na ukweli kwamba ukiwa umekaa ni rahisi mafuta mengi kujilundika mwilini mwako kuliko ukiwa umesimama. Kadri unavyokaa masaa mengi kwenye kiti ndivyo vimeng’enya vinavyofanya kazi ya kuchoma mafuta mwilini vinavyokuwa na nguvu chache kuchoma hayo mafuta. Na tatizo la unene au uzito kupita kiasi lina uhusiano wa moja kwa moja na matatizo mbalimbali ya moyo.

4. Itakuwa vigumu kitambi na uzito kukuisha

Umewahi kujaribu kufanya mazoezi, kubadili chakula au hata kufunga na bado ukawa unasumbuliwa na kitambi au uzito kuwa mkubwa? Basi jibu la tatizo lako ni kukaa kwenye kiti masaa mengi. Utafiti unaonyesha kukaa tu kwenye kiti hata kama hauli chakula kingi bado utaendelea kuongezeka uzito.

Kwahiyo kama unataka kuondoa kitambi au tumbo au kupungua uzito kwa haraka acha kukaa masaa mengi kwenye kiti, hata kama kazi yako ni ya ofisini jaribu namna unaweza kupata meza ya kusimama huku unaendelea na kazi yako.

5. Ni rahisi kupatwa na ugonjwa wa Kisukari

Unataka kupona au kuepukana na Kisukari aina ya pili? Basi acha kukaa kwenye kiti muda mrefu. Moja ya hatari zaidi za kukaa kwenye kiti masaa mengi ni kuwa mwili unakuwa hauitiki vema kwa insulin jambo ambalo ni matokeo ya kukaa masaa mengi kwenye kiti na hii ni matokeo ya kuzalishwa kwa wingi kwa kongosho kupita inavyohitajika kama matokeo ya kukaa muda mrefu.

Wakati ukiwa umekaa tu kwenye kiti kongosho linaendelea kutengeneza insulin lakini katika mwili huo uliokaa tu, insulin inakuwa haitumiki vema na mwili jambo linalomaanisha kuwa damu sukari (glucose) haiondolewi kwenye mzunguko wa damu kwa haraka. Hivyo uwezekano wa kupata Kisukari unaongezeka kwa zaidi ya asilimia 14 kwa Yule mwenye tabia ya kukaa masaa mengi kwenye kiti kuliko mtu mwingine yoyote.

6. Utapatwa na maumivu ya nyuma ya mgongo

Ukiwa ni mtu wa kupenda kukaa kwenye kiti masaa mengi kuna uwezekano ukawa haukai hata mkao mzuri kiasi cha kuwa karibu na maumivu ya mgongo kila mara. Watu wa namna hii pia huwa na maumivu ya kwenye uti wa mgongo kila mara. Kwa mjibu wa utafiti wa Taasisi ya ‘DNA India’ wagonjwa wengi wenye matatizo ya uti wa mgongo ni wale wenye miaka 20 na 30 na wengi wao ni wale hufanya kazi wakiwa wamekaa kwenye kiti masaa mengi.

Miaka ya sasa ni rahisi kukutana na watu wanaolalamika kupatwa na maumivu ya mgongo na wengi wao ukiwachunguza ni wale wanaotumia masaa mengi kukaa kwenye kiti.

7. Utakufa ukiwa bado kijana

Shirika la afya duniani limesema mtindo wa kukaa masaa mengi kwenye kiti ndiyo unaohusika na kuongezeka kwa uzito na unene kupita kiasi katika nchi nyingi zilizoendelea. Na uzito kupita kiasi ni moja ya tatizo kubwa la afya kwa mtu mzima yoyote kuwa nalo ingawa wengi hawaelewi hilo, wengi hasa waAfrika wakiwa wanene au wenye uzito mkubwa ndiyo hudhani hiyo ni afya. Uzito na unene kupita kiasi huja na matatizo mengine makubwa ikiwa ni pamoja na matatizo katika mfumo wa upumuwaji, kisukari, stroke, kukosa usingizi nk na haya yote yanaweza kupelekea wewe kufa ukiwa bado kijana.

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Harvard mwaka 2014 ulitoa hitimisho kwamba kukaa kwenye kiti masaa mengi ni moja ya sababu ya vifo vya mapema kwa watu wengi. Mtandao wa Huffington ulienda mbali zaidi na kusema kukaa kwenye kiti masaa matatu tu kwa siku ni sawa na mtu aliyevuta sigara 6 na kuwa kukaa kwenye kiti masaa mengi kunaua watu wengi zaidi duniani kote kuliko hata UKIMWI.

Mara ya kwanza niliposoma habari hizi nilishikwa na mshangao wa ajabu maana mimi mwenyewe nimekuwa mtu wa kukaa kwenye kiti kwa miaka mingi sasa kwani kazi zangu nyingi huzifanya nikiwa kwenye computer. Yaani haikuchukuwa muda nikabadili mkao tayari ninafanya kazi zangu nikiwa nimesimama, na tayari nimeona mabadiliko makubwa kwenye afya yangu kwa ujumla.

Pamoja na kuwa kusimama ni bora zaidi kuliko kukaa, bado unatakiwa utumie muda fulani kukaa pia, usisimame masaa yote kutwa nzima, ukisimama masaa matatu tumia nusu saa nyingine kukaa hivyo hivyo mpaka siku yako inaisha.

Nini maoni yako? umekaa muda mrefu kwenye kiti na unapata mojawapo ya madhara yaliyoandikwa hapa? nipe uzoefu wako.

SABABU za Kukoroma Ukiwa Umelala na Jinsi ya Kuzuia Hali Hiyo...!!!

$
0
0

Kukoroma ni tatizo linalowapata watu wengi wakati wanapolala ambalo linaweza kuwatokea watu wa kila umri ingawa hutokea mara nyingi kwa wanaume au watu wanene. Kukoroma kwa kawaida sio tatizo kubwa na mara nyingi huleta tu karaha kwa mtu anayelala karibu na mkoromaji.

Mtu huwa anakoroma pale kunapokuwa na kitu au sababu yoyote itakayoziba kuingia au kutoka kwa hewa mdomoni na katika pua. Kuta za koo hutikisika wakati wa kupumua na matokeo yake ni sauti inayosikika ya kukoroma. Kuingia au kutoka kwa hewa huweza kuzuiwa na sababu mbalimbali kama vile.

Kuziba tundu za pua kusiko kamili ambako husababisha nguvu zaidi zitumike katika kupitisha hewa kwenye pua wakati mtu akiwa amelala. Kitendo hicho hupelekea nyama laini za pua na koo zijikusanye na kusababisha mkoromo. Kuna baadhi ya watu wanakoroma tu kipindi cha allergy (allergy season) au wanapatwa na matatizo ya sinus. Baadhi ya matatizo kama vile kupinda pua (deviated septum) au ukuta unaotenganisha tundu za pua na polyps za pua pia huweza kufanya pua zizibe na kusababisha kukoroma. Watu wengi wanaofanya operesheni za pua pia hupatwa na tatizo la kukoroma.

Kuwa na misuli dhaifu katika koo na ulimi. Misuli au nyama za koo na ulimi zinapokuwa dhaifu sana hulegea na kuanguka upande wa nyuma wa sehemu inayopita hewa. Suala hilo hutokea pale mtu anapolala fofofo au kuwa na usingizi mzito na kusababisha kukoroma.

Sababu nyinginezo zinazoweza kumsababishia mtu akorome anapolala ni kuwa na umri mkubwa au uzee, imeshuhudiwa kuwa watu wa makamo na wazee hukoroma, kwani misuli na nyama za koo huanza kuzeeka na kulegea kadri umri unayoongezeka.

Vilevile wanaume wanakoroma zaidi kuliko wanawake hii ni kutokana na wanaume kuwa na njia nyembamba zaidi ya hewa kuliko wanawake.

Kuondoka na hali hiyo mkoromaji yampasa kuzingatia mambo kama; kupunguza uzito, safisha njia ya koo ya hewa, Kuwa na pua iliyoziba hufanya kupumua kuwe kugumu na kusababisha kukoroma.

Unaweza kufanya hivyo kwa kutumia dawa za kusaidia kupumua kwa urahisi (nasal decongestants) zinazopatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa pia  kuaacha kuvuta sigara, kutokunywa pombe kabla ya kulala, au kutumia vinywaji au vyakula vyenye kafeini. Zingatia kulala mapema ili kupata muda wa kutosha kupumzisha mwili.

HASARA ya Kushauriwa Uamuzi Juu ya Mapenzi..!!!

$
0
0

Wengi wamekuwa wepesi sana kukimbilia kwa rafiki, ndugu zao ili kuomba msaada wa mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi katika jamii yetu ni kuwa ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.

Kwa mtazamo wa haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi. Unapokerwa na mpenzi unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.

Je, umeshawahi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki yako? Hebu ungana nami nikumegee kidogo hasara za ushauri ambao siku zote ndio unaona kimbilio kwako

UTAKUPOTOSHA

Ni wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.

Uchunguzi unaonesha kuwa, wapenzi wengi sana hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vema kuwa makini unaposhauriwa.

UTARAHISISHA MAMBO

Mara nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi kwao kupima vitu kwa juujuu tu na kushauri kirahisi. “Duuh kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana, unayeachana ni wewe anayekushauri.

“Mkubali tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.

UTAKUGEUZA

Ulimwenguni kuna aina zaidi ya 1,000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa staili zake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalam kuwa hazifanani hata kidogo. Uzoefu unaonesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini je, ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?

Jibu ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze aamue na apende kama staili yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi.

UTAKUONDOLEA UJASIRI

“Kwa maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”

Huu ni ushauri unaoweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumrekebisha.

Ushauri huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayeku-shauri atakapo-lipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi. Ikumbukwe kuwa anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha sana mumewe kaacha ulevi.”

Ukitambua hili, utafanya bidii ya kujenga uwezo binafsi wa kuchambua tatizo unalokumbana nalo.

SEHEMU 4 za Mwili Usizopaswa Kumshika Mkeo Nyakati Hizi 18+..!!!

$
0
0

Ingawa kuna mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa ukishamuoa mwanamke na mkawa mwili mmoja basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa.

Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au kuwakwaza wake zao.

Kama tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie sana anataka kukidhi haja yake.

Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa.

1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani

Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo.

2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga

Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa jasho.

3. Sehemu za siri kabla ya kuoga

Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga.

Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi.

4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba

Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe.

Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’.

Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe.
Viewing all 104775 articles
Browse latest View live




Latest Images