Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104756 articles
Browse latest View live

UKWELI Mchungu..Hili ni Taifa la Wanung'unikao Mno: Tulideka, Tulidekezwa, au Tulidekeka..!!!?

$
0
0

Swali Korofishi: Hivi sisi kama taifa ni kuwa tulikuwa tumedekezwa, tumedeka au tumedekeka mno? Maana, kuna baadhi ya mambo yanapotokea hadi unashangaa tulikuwa ni watu wa aina gani? Sukari imebadilika bei kidogo, "mamaaa wee tunakufa sukari imepanda bei!" utadhani sukari inatakiwa iwe kwenye bei ile ile ya miaka kumi iliyopita! Mara upungufu kidogo wa chakula baadhi ya maeneo "Mamamaaa wewee tunakufa njaaa, watu wanakufa njaa"!

Kigogo kapigwa mkwara na imechomolewa bastola - wala hajalengwa mtu wala nini - "mama weweeeeee watu wanatumia bastola, n.k!" Hivi tulijenga taifa la namna gani? Yaani, tunaonekana kukereka na vitu vidogo na wakati mwingine vya kawaida sana (hata kama ni vikubwa) hadi inashangaza.

TUlizoea kuona vigogo wanaweza kufanya lolote au popote na kwa mtu yeyote, leo watu wanaoneshwa kuwa sheria haina macho watu tunaanza kushangaa "eeh wamemfanyia hivi na yule" wakati miaka yote tulitaka tuone sheria zinatumika sawasawa bila kujali nani ni nani. Mwisho watu wanasema "wataisoma namba". Si tulitaka tuone kuwa wana CCM nao wanatendewa vile vile wanavyotendewa wengine? Sasa leo wanatendewa tunashangaa? si ndio maana ya sheria?

Hivi tukianza kuona sheria inauma ikienda na kurudi tunashangaa?NI taifa la watu wasio taka kupata shida hata kidogo sisi? Hivi tungekuwa katika mazingira ya watu wa nchi nyingine ingekuwaje? Nakumbuka kuna watu walikuwa wanataka hata "jeshi lichukue" nchi! Hivi kweli walikuwa wanamaanisha au walidhani ikitokea itakuwa ni kusimama na kuimba "kumbaiya my Lord kumbaiya"?

Jamani, mabadiliko yoyote yale ni magumu. Lakini pia kama watu wanaona hivi sivyo wanavyotaka njia pekee ni kujipanga na kuanza kujiandaa kubadilisha mwelekeo wa nchi katika uchaguzi ujao. Na kama mambo ni magumu kweli basi ni jukumuu la watu kuanza kuamua sasa hivi wanataka iweje; si wameona yanayotokea Venezuela?

Maana imefikia watu wanatamana kurudi wakati wa Kikwete na Mkapa! Inashangaza sana!

MECK Sadiki Afunguka Mazito Yaliyopelekea Kujiuzulu Ukuu wa Mkoa..Adai Ameepuka Kumkwaza Rais Magufuli..!!!

$
0
0

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, amesema ameamua kuondoka Serikali baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki. 

Aidha Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dkt John Magufuli kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza Rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa. 

Uamuzi huu wa kupumzika nilimuomba rais muda mrefu sana, na nikirudi Kijijini nitaendelea na ufugaji wa samaki maana nilishaandaa bwawa la kufugia, nitaendelea nalo huku nikiwaza jambo lingine la kufanya," alisema. 

Sadiki alisema hayo jana wakati wa mahojiano maalumu na Habari leo kuhusu sababu zilizochangia kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro. 

"Namshukuru Rais kuridhia ombi langu, nimetumikia Serikali tangu mwaka 1999 nikiwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ninapoondoka mwenyewe..nimeona ni wakati muafaka kumweleza aliyeniteua kuwa nahitaji kupumzika nikiwa na akili timamu na afya njema", alisema. 

"Kama kiongozi muungwana lazima ifike mahali ukiri kwamba wapo vijana wenye uwezo mzuri na kasi ambayo inaendana na serikali ya awamu ya tano.. mimi nilishatekeleza wajibu wangu na mchango kwa serikali yangu, sasa inatosha, tupate mawazo na michango ya wengine", alisema. 

Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi kujitathimini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua.

SOMA Nafasi za Kazi Zilizotangazwa Leo

$
0
0

NIMEAMINI Binadamu ni Mnafiki na Anapenda Vita..Ukweli Mchungu Kuhusu Nia Njema ya Donald Trump

$
0
0

By Barbarosa

D.Trump anawasiliana na kushirikiana na Urusi anatukanwa mpaka wanaanza mpango wa kumshitaki, ikumbukwe kwamba Vita ikiibuka kati ya Urusi na Ulaya hakuna atakayepona, na cha ajabu zaidi Waafrika hawampendi Trump ingawaje ndiyo Raisi pekee wa USA ambaye ana sera rafiki kwa Afrika, Black Americans hawampendi Trump ingawaje ndiyo Raisi pekee anayewapigania!

Trump amesema
lets make peace" lkn Binadamu wanataka avamie Syria, Korea, Irani n.k.!

Trump anapigania Makampuni ya USA kujenga Viwanda USA na mnufaika mkubwa ni Black America kwani wao ndiyo wanaotegemea kazi za viwandani kwa kuwa wengi wao hawana University degrees, Trump anataka kuondoa violence ghetto America ambapo muathirika mkubwa ni Black Amerika, lkn bado hawaelewi, ...



[​IMG]

VIDEO: Gigy Money Adai Vyeti Kwa Bashite Kwa Style Hii

$
0
0
Gigy Money nae ameingia katika mkumbo wa watu wanaodai Bashite ajitokeze na kuonyesha vyeti vya Elimu yake ambapo kuna madai kuwa hana...

Ametumia staili ya kipekee angalia Video hapa chini:

HABARI Zetu Unaweza Kuzipata Kirahisi Kupitia Android Application Yetu..Download Hapa

$
0
0
Kama Huna Application hii Kwenye Smart Phone yako Basi Hujapitwa sana , Fanya Kubonyeza HAPA ili Kuidownload Kwenye Simu yako 

Au Click Udaku Special

WEMA Sepetu Ashtuka...Sasa Kwake Wanaume Maarufu Noo!!!

$
0
0

Malkia wa filamu bongo, Wema Issac Sepetu amefunguka na kuwataka mashabiki wamuombee apate mume bora atakayekuwa na heshima na wala asiwe mtu maarufu na siyo kumhusisha kila mara na uhusiano wa kimapenzi na msanii Diamond Platnumz..
.
.

Wema amefunguka hayo wakati akimjibu Shabiki katika kurasa wake wa Instagram, na kumtaka atambue Diamond ni baba wa watoto wa wili kwa sasa na ifike kipindi watu wanatakiwa wakubali kuwa hakuna kinachoendelea kati yake yeye na Diamond bali wamuombee na yeye apate mume wake ambaye siyo mtu maarufu. "Sasa baby aliokwambia namtaka Damond ni nani? Life has to go on, yule ni baba wa watoto wawili jamani. Its about time u guys accept that Me and Naseeb no more. Mnachotakiwa kuniombea ni nipate mwanaume bora na siyo bora mwanaume na mwenye heshima zake"- aliandika Wema Sepetu..
.
TOA MAONI YAKO HAPA

Jakaya Kikwete Ala Shavu la Cheo UN

$
0
0

Rais mstaafu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete amechaguliwa  kuwa mwenyekiti mwenza wa  Baraza la Kimataifa  la Wakimbizi.


Rais Kikwete amechaguliwa kushika wadhfa huo wakati akiwa bado ni Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High-Level Panel on Global Responses to Health Crises). Itakumbukwa kuwa mwaka juzi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alimteua  Rais Kikwete kushika wadhfa huo.


Na sasa amekuwa tena kiongozi wa ngazi ya juu wa baraza hilo la kimataifa, ambapo katika nafasi hiyo  atakuwa na wenyeviti  wenza ambao ni Hina Jilani kutoka Pakistan na Rita Sussmuth kutoka Germany.


Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza  baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1951 ni Lloyd Axworthy kutoka Canada.

KIMENUKA..Wazee Simba Wambwatukia Mo Dewji

$
0
0

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Wazee Wanachama wa Simba SC, Felix Makua amesema Kupitia kikao chao cha Mei 15, 2017 waliadhimia kwenda kumuona Rais Dkt.

John Pombe Magufuli ili wamueleze kuhusu baadhi ya viongozi wa Simba wakishirikiana na baadhi ya viongozi wa Serikali ambao wanataka kutumia mamlaka yao na pesa (rushwa) kuiuza klabu hiyo ambapo suala hilo kwa sasa lipo Takukuru na viongozi hao wameshaanza kuhojiwa.

Mzee Makua amezungumzia pia suala la Katiba ya Simba kutofanyiwa marekebisho huku wakielekeza kilio chao kwa Waziri mwenye dhamana, Dkt. Harrison Mwakyembe ili aweze kulishughulikia mapema kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo.

Aidha wazee hao wamesema kuwa anayebeza udhamini wa Kampuni ya Michezo ya Bahatinasbu, SportPesa kwa Simba basi mtu huyo hafai ndani ya klabu hiyo huku wakimuomba Rais Aveva aendelee na motto huo huo wa kufanikisha dhamini mbalimbali.

Akizungumzia suala la udhamini wa mfanyabaishara Mo Dewji ndani ya Simba, Mzee Makua amemtaka aiheshimu klabu hiyo huku akikanusha madai ya Mo kuidai Simba mabilioni ya pesa.

RAIS Magufuli Afanya Uteuzi uu leo

$
0
0

Dar es Salaam. Rais John Magufuli leo (Jumatano) amemteua Geoffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya uteuzi huo Mwambe alikuwa mkuu wa wilaya ya Manyoni. Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Clifford Tandari kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro.

Tandari anachukua nafasi ya Dk  John Ndunguru ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo  Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Uteuzi huo unaanza mara moja.

TETESI..Zinazodaiwa Kuwa ni Sababu za RC Meck Sadiki, Jaji Mujulizi na Jaji Upendo Msuya Kuacha Kazi..!!!

$
0
0

Hizi ni habari za uhakika za ndani kabisa kuhusu kuacha kazi kwa Majaji wawili na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

1. Ndg. Saidi Meck Sadiki - Aliyekuwa mkuu Wa Mkoa wa Kilimanjaro

Ukweli ni kuwa anakabiliwa na kesi mbaya sana ya hela hewa za usafi alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, imethibitika alifuja kiasi kikubwa takribani bilioni mbili za usafi ktk Jiji la Dsm na ilikuwa akamatwe na PCCB lakini kaamua kuachia ngazi nadhani atashughulikiwa.

2. Ndg. Aloysius Kibuuka Mujulizi - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Huyu ana makosa mawili makubwa, la kwanza ni lile la ESCROW Account alipokea fedha chafu za Rugemalira na kukosa sifa za kuwa Jaji mwaminifu, la pili huyu si raia wa Tanzania hivyo si mtanzania yeye ni Mganda habari za uhakika zimethibitisha hilo, Hivyo hana sifa ya kuwa Jaji huyu.

3. Ndg. Upendo Hillary Msuya - Aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Tanzania.

Huyu ndiye Jaji wa hovyo kabisa yeye ameshiriki kuwaachia watuhumiwa wa kesi za madawa ya kulevya na kupokea rushwa kitendo hicho kinamuondolea sifa ya kuwa Jaji mwaminifu.


EVERTON ya Uingereza Yaingia Mkataba na Mdhamini wa Simba Sc ya Tanzania..!!!

$
0
0

SIKU chache baada ya Kampuni ya SportPesa kutangaza kuidhamini klabu ya Simba kwa mkataba wa miaka mitano wenye thamani Sh. bilioni 4.9, kampuni hiyo imeimarisha uwapo wake katika soko barani Ulaya baada ya Jumatatu kukubali kuwa mshirika mkuu wa klabu ya Everton ya England.

Dili hilo kwa Everton ambayo imekuwa mshindi mara tisa (9) England, limeanza rasmi Jumatatu na jezi mpya zenye kuitangaza SportPesa zitaanza kutumika kuanzia msimu wa 2017/18.

Wakizungumza katika uzinduzi wa dili hilo kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Liverpool, Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Everton, Robert Elstone, alisifia makubaliano hayo ya kihistoria.

“Tunaikaribisha SportPesa kwenye familia ya Everton na tunatazamia kufanya kazi kwa ukaribu na kampuni hiyo ambayo inakua kwa kasi duniani.

Tangu kuanza kwa mazungumzo yetu, kwa pamoja tumekuwa tukivutiwa na mlingano wa maadili na malengo ya SportPesa ambayo yanawiana na yale ya klabu yetu.

Kwa miaka ijayo tutashirikiana kikamilifu katika kutimiza malengo yetu,” alisema.

Meneja masoko wa SportPesa Uingereza, Shaun Simmonds, alisisitiza uhusiano wao na Everton, kama moja ya taasisi zinazoheshimika katika ulimwengu wa soka kwani inaendana na mkakati wa kampuni katika kukuza michezo kwa kupanua wigo wake ndani ya Uingereza.

“Tunajisikia fahari, mafanikio ya SportPesa Uingereza na shughuli za SportPesa barani Ulaya kwa ujumla pamoja na ushirikiano ambao ushirika huu utaleta maendeleo katika shughuli zetu barani Afrika na ulimwenguni,” aliongeza Simmonds.

Kwa Tanzania, Kampuni ya SportPesa imeukaribisha ujio wa Everton katika udhamini ambao unaonesha dhamira ya kweli katika maendeleo ya mpira wa miguu.

“Ndiyo maana hapa Tanzania, Sportpesa imejiingiza katika udhamini kwa klabu za Tanzania, ikiwa ni kuungana na Sportpesa nchi nyingine kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu,” alisema Tarimba Abbas, Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania.

Kampuni ya SportPesa ilianza rasmi nchini Kenya mwaka 2014 na tangu hapo imekuwa ikikua kimataifa.

Kuongezeka kwa ushirika na klabu ya Everton ni hatua mpya katika kukuza orodha ya timu washirika ambapo timu hiyo kutoka Jiji la Liverpool itaungana na klabu za Hull City, Southampton, Arsenal [zote za England], Gor Mahia, AFC Leopards [Kenya] na Simba SC [Tanzania].

TAKUKURU Wanasa Mali Kufuru za Mhasibu Wao.. Ni Maghorofa 7, Nyumba 9 za Kifahari Zilizopo Mbweni, Kinondoni, Mwanza..!!

$
0
0

HATIMAYE Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanika mali za aliyekuwa Mhasibu Mkuu wake, Godfrey Gugai, ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa wa thamani ya Sh. bilioni 3.5.


Miongoni mwa mali zinazomweka mhasibu huyo katika kundi la matajiri katika nchi hii inayotambuliwa kimataifa kama mojawapo ya mataifa maskini, ni pamoja na viwanja 37, maghorofa saba, nyumba za kawaida tisa, magari matano na pikipiki.

Maghorofa, nyumba za kawaida na viwanja vya mhasibu huyo ambaye alishafukuzwa kazi tangu mwaka jana viko kwa mtawanyiko katika maeneo mbalimbali nchini yakiwamo ya ghali karibu na bahari, Kigamboni na Mbweni jijini Dar es Salaam na pia Bagamoyo mkoani Pwani. Kwingineko kuliko na mali hizo ni Kinondoni (Dar), Musoma, Nyegezi na Kiseke jijini Mwanza.

Hata hivyo, chanzo cha uhakika kimeiambia Nipashe kuwa hivi sasa mali hizo ziko chini ya himaya ya Takukuru, baada ya kuzinasa kufuatia idhini ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotokana na ombi la taasisi hiyo.

Mei 9, mwaka huu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa amri ya zuio la mali za Gugai ambaye anakabiliwa na tuhuma za kujilimbikizia mali kinyume cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa  Namba 11 ya mwaka 2007.

 Amri ya zuio la mali za Gugai ilitolewa na Mahakama hiyo kutokana na ombi la Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) chini ya kifungu namba 38(1)(a) na (b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007 katika shauri namba 13 la 2017.

Mali hizo ni nyumba saba za ghorofa moja moja zilizopo maeneo ya Wilaya ya Kikondoni jijini Dar es Salaam, nyumba nane, viwanja 37, magari matano na pikipiki moja.

Katika orodha ya mali hizo zinazoshikiliwa na Takukuru, na ambayo Nipashe imeona nakala yake, inaonyesha kuwa mali za mhasibu huyo wa zamani zilizowekewa zuio la Mahakama ni nyumba nne za ghorofa moja moja zilizoko kiwanja na 64 kitalu Ununio, Kinondoni, Nyumba tatu za ghorofa moja zilizoko kiwanja na 150 kitalu 8 Bunju na Kinondoni, nyumba nne zilizoko Kiwanja na 225 Kitalu 6, Mbweni JKT,  Kinondoni.

Nyingine ni nyumba zilizoko kwenye kiwanja namba 62 na 63 kitalu C, Kinondoni, nyumba iliyoko kiwanja namba 29 kitalu L, Majita,  Musoma, nyumba namba 713 PPF Kiseke, Mwanza na nyumba iliyoko kwenye kiwaja namba 438 bloku D, Nyegezi, Mwanza.

VIWANJA 37
Katika orodha ya viwanja ni pamoja na kiwanja namba 14 kitalu J, Bunju, Kinondoni, Kiwanja namba 47 kitalu B, Mwongozo, Kigamboni, kiwanja namba 184 kitalu B, Buyuni,Temeke, kiwanja namba 103 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo, kiwanja namba 104 Kitalu L, Kaole, Bagamoyo na kiwanja namba 209 kitalu B, Kibaha.

Vingine ni kiwanja namba 195 kitalu 3, Kihonda, Morogoro, kiwanja namba 993 kitalu L, Kiegeya,  Morogoro, kiwanja namba 868 Kitalu Q, Lukobe, Morogoro, kiwanja namba 34 kitalu K, Kisasa B, Dodoma, kiwanja namba 32 kitalu N, Itega, Dodoma, kiwanja namba 39 Kitalu M, Itega, Dodoma, kiwanja namba 24 kitalu B, Chidachi, Dodoma, kiwanja namba 64 Nzuguni, Dodoma, kiwanja namba 230 Kitalu B, Nyegezi, Mwanza na kiwanja namba 439 Kitalu D, Nyegezi, Mwanza.

Viwanja vingine ni kiwanja namba 275 Kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  277 kitalu 2 Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  296 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba  297 kitalu 2, Nyamhongolo, Mwanza, kiwanja namba 286 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 287 kitalu G, Nyamagana, Mwanza, kiwanja namba 90 kitalu 5, Bugarika, Mwanza, kiwanja namba 126 kitalu A, Makoko, Musoma, kiwanja namba 622 kitalu A, Gomba , Arusha, kiwanja namba 621 na 623, kitalu A, Gomba na Arusha, kiwanja namba 737 kitalu C, Mwambani, Tanga

Kiwanja namba 1,2 na 3 kitalu J, Mwambani,Tanga, kiwanja namba 4 kitalu J Mwambani, Tanga, kiwanja namba  5 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 18 kitalu J, Mwambani Tanga, kiwanja namba 7,9 kitalu J, Mwakidila, Tanga na kiwanja namba 11, 13 kitalu J, Mwakidila, Tanga

ORODHA YA MAGARI

Orodha ya magari ya mhasibu huyo wa zamani Takukuru inahusisha magari matano ambayo ni gari namba T 180 DBQ , Mitsubish Canter; gari namba T 581 BQU, Toyota Hillux; gari namba T 814  CSC Nissan Murrano; gari namba T 679 ASD Toyota RAV 4 na gari namba  T 913 DHE Suzuki. Pia inashikiliwa pikipiki yenye namba zz usajili MC 837BCL

Kutokana na maombi ya DPP mahakama imeamuru mali zilizotajwa za Gugai ziwe chini ya zuio la Mahakama.

Pia mawakala wake na watu wengine wote wanaomwakilisha wamezuiwa kuuza au kuhamisha umiliki au kuweka dhamana mali zote zilizowekewa zuio.
Aidha, Msajili wa hati ameagizwa kusajili zuio hilo kama kizuizi dhidi ya mali zote zilizotajwa.

 Pia Msajili Msaidizi wa magari ameagizwa asiruhusu uhamishaji wa umiliki wa vyombo vya moto vilivyowekewa zuio mpaka mahakama itakapoelekeza vinginevyo.

KIKWETE Apata Ulaji Mwingine Kimataifa..!!!

$
0
0

Rais mstaafu  Jakaya Kikwete amechaguliwa  kuwa mwenyekiti mwenza wa  Baraza la Kimataifa  la Wakimbizi.

Rais Kikwete amechaguliwa kushika wadhfa huo wakati akiwa bado ni Mwenyekiti wa jopo la ngazi ya juu kuhusu Mwitikio wa Kimataifa wa Majanga ya Afya (High-Level Panel on Global Responses to Health Crises).

Itakumbukwa kuwa mwaka juzi, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alimteua  Rais Kikwete kushika wadhfa huo.

Na sasa amekuwa tena kiongozi wa ngazi ya juu wa baraza hilo la kimataifa, ambapo katika nafasi hiyo  atakuwa na wenyeviti  wenza ambao ni Hina Jilani kutoka Pakistan na Rita Sussmuth kutoka Germany.

Mwenyekiti aliyechaguliwa kuongoza  baraza hilo lililoanzishwa mwaka 1951 ni Lloyd Axworthy kutoka Canada.

WAITARA Awekwa Mtu Kati Bungeni..Akubali Yaishe Baada ya kukosea Kuasilisha Hotuba..!!!

$
0
0

Bunge limembana Naibu Waziri Kivuli wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mwita Waitara na kulazimika kufuta baadhi ya maneno yaliyokuwa katika hotuba ya kambi rasmi ya upinzani bungeni kuhusu bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu amembana Waitara baada ya mwongozo ulioombwa na Waziri wa Nchi,  Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama mara baada ya bajeti ya wizara hiyo kupitishwa na Bunge.

Mambo yalianza kwenda kombo kwa Waitara wakati Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alipokuwa akihitimisha hoja yake kumtaka naibu waziri huyo afute kauli zake zinazodaiwa kuwa za uongo au azithibitishe kabla ya kuombewa mwongozo na Mhagama.

 “Kauli kama hizi zinasababisha kupandikiza mbegu za utomvu wa nidhamu jeshini. Narudia nimesikitishwa sana na maneno yenye lengo la uwagombanisha wanajeshi na Serikali yao na uongozi wao wa juu. Hii halipwaswi kuvumiliwa na ni vyema Bunge lako liangalie utaratibu wa kumtaka msemaji wa kambi hii ya upinzani athibitishe maneno yake,”amesema.

Hata hivyo, baada ya kubanwa sana na Zungu, Waitara alitamka kuwa ameyafuta maeneo hayo na maneno ya Dk Mwinyi ndio yachukuliwe kuwa ya ukweli.

“Kwa heshima na taadhima naomba kufuta maneno hayo, tuko pamoja,”amesema Waitara.

TANZIA: Msanii Dongo Mfaume Afariki Dunia

$
0
0

Msanii wa Bongo Fleva, Dogo Mfaume, anayekumbukwa zaidi kwa wimbo wake wa 'KAZI YA DUKANI' amefariki dunia leo hii.

Dogo Mfaume alikuwa anasumbuliwa na Matatizo ya kutumia madawa ya kulevya..

RIP

KLM Kugharamia Safari ya Kurudi ya Wanafunzi wa Lucky Vincent

$
0
0

Arusha. Wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent ya jijini hapa waliosafirishwa nchini Marekani kwa ajili ya matibabu, watarejea nchini pamoja na waliowasindikiza kwa usafiri wa bure uliotolewa na Shirika la Ndege la Uholanzi(KLM)

Wanafunzi waliosafirishwa ni Sadia Awadh,Wilson Tarimo na Doreen Elibarick kila mmoja akiwa na mama yake, muuguzi na daktari bingwa wa mifupa ambao waliondoka nchini tangu Mei 14, mwaka huu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyewezesha safari ya kwenda Marekani kupitia taasisi Stemm ambayo ni mwenyekiti mwenza, amesema kuwa usafiri huo uko tayari muda wowote matibabu ya wanafunzi hao yatakapokuwa yamekamilika.

"Napenda kuthibitishia kuwa usafiri wa kurudi upo jambo la muhimu Watanzania wote tumwombe Mungu wapate nafuu kwa haraka baada ya upasuaji waliofanyiwa ili waweze kuendelea na masomo yao,"amesema Nyalandu.


NAY wa Mitego Aumbuka Shamsa Ford Amkana

$
0
0
Baada ya minong'ono kuongezeka kwamba Muigizaji Shamsa Ford atamsindikiza aliyekuwa mpenzi wake Nay wa mitego kwenye tamasha la 'Wapo Tour' ya jijini Dar, Shamsa amekanusha kuhusu kushiriki katika show hiyo huku akidai hajui chochote

Shamsa amekanusha kuwepo katika show ya ‘Wapo Tour’ ya rapa Nay wa Mitego itayofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, May 20, ikiwa ni siku chache kufikia kufanyika kwa tamasha hilo kwa madai kuwa hana tarifa rasmi ya kuhusishwa bali anaona kwenye mitandao tu akitajwa kuwepo.

Aidha amedai kuwa hajui chochote kuhusiana na show hiyo “Kusema kweli sina show yoyote na mtu na wala sijazungumza na Nay wa Mitego kuhusu show ya Dar Live".

Aliongeza,”Hajaniambia chochote siwezi kudanganya, ndio kwanza hizo taarifa naziona katika mitandao ya kijamii. Kama kweli na mimi nitakuwepo ungeona hata nikipost. Kwahiyo sitakuwepo kwenye hiyo show kwa sababu sina taarifa yoyote"- alisema Shamsa Ford

Wiki iliyopita rapa Nay wa Mitego alidai licha ya kuachana na muigizaji huyo na kuolewa na mtu mwingine lakini wanashirikiana katika mambo mbalimbali huku akimtaja Shamsa atakuwa MC siku ya show yake Dar live.

Rais Magufuli Aufuata Ushauri wa Zitto Kabwe

$
0
0

Siku moja baada ya Rais Magufuli kuzuru kituo cha shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Nakuagiza kupitiwa upya mkataba wa uliongiwa baina ya shirika hilo na kampuni ya kichina ya Startimes, Basi Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook ameandika hivi...

 "Nasikia Rais kaagiza kuhusu Mkataba wa StarTimes na TBC. Mwaka 2011 tulipata kuazimia Hivi;

"7.2.10 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Mkataba baina ya Shirika la Utangazaji Tanzania ( TBC) na Star Times International Communication una mapungufu kadhaa ya kisheria na ambayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Hesabu wa TBC baada ya kuchambua Mkataba na Taarifa ya Hoja za Ukaguzi,na kwa kuwa mapungufu hayo yanaweza kuwa na athari katika utendaji wa TBC kwa siku zijazo , kwa hiyo basi Kamati inapendekeza kuwa, Serikali iupitie upya Mkataba huo ili kuainisha maeneo ya maboresho, aidha Serikali ifanye utaratibu wa kuangalia namna nzuri ya kutoa fedha kwa uendeshaji wa TBC ili kiwe chombo cha utangazaji wa Umma chenye kujiendesha kwa uhuru na kwa maslahi ya Umma."

HUKU Ndiko Alipokuwa Dogo Mfaume Kabla ya Mauti Kumkuta..!!!

$
0
0

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Dogo Mfaume ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama 'Kazi Yangu Ya Dukani' amefariki dunia leo 

Dogo Mfaume ambaye alitumbukia kwenye janga la madawa ya kulevya na baadaye kuanza kupata matibabu ya kuondokana na matumizi ya madawa hayo kupitia kituo cha Pilli Missana Foundation kilichopo Kigamboni.

Akiongea na EATV Pili Missana ambaye ni Mkurugenzi wa kituo hicho amethibitisha kufariki kwa msanii huyo.

Mungu amlaze mahali pema peponi Dogo Mfaume. Jikumbushe na moja ya kazi yake hapo chini 

Viewing all 104756 articles
Browse latest View live




Latest Images