Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel Catalog


Channel Description:

Gossip News 24/7
  0 0


  Watu watatu wakazi wa Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwemo kuiba madini yenye thamani ya Sh. Mil 507,347,000.

  Washtakiwa hao ni Donald Njonjo (30) Mkazi wa Kigamboni, Gamba Muyemba (51) Mkazi wa Tandika na Kashif Mohamed (41) Mkazi wa Upanga jijini Dar es Salaam ambao wanadaiwa kuiba madini kwenye Tume ya Madini.

  Kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mwandamizi Mfawidhi, Kelvin Mhina kuwa kati ya Novemba 30, 2017 na Juni 29, mwaka huu katika Ofisi ya Tume ya Madini iliyopo Masaki wilayani Kinondoni, waliiba madini ya dhahabu yenye uzito wa Kilogramu 6.244 yenye thamani ya Sh.Mil 507,347,000 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, kesi imeahirishwa hadi Julai 29, 2019 kwa ajili kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kuwapatia dhamana.


  0 0


  Klabu ya Azam FC imesema kuwa kesho lazima wapambane mbele ya TP Mazembe ili kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kagame.

  Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa hakuna mchezo mwepesi ila wanapeleka timu uwanjani wakitafuta matokeo chanya.

  "Tupo vizuri tutakwenda uwanjani kutafuta matokeo chanya, tunashukuru Mungu tupo salama, tumeanza na tunaendelea kuimarika taratibu, timu inaimarika matarajio yetu kufanya vizuri.

  Idd Cheche ambaye ni Kocha Msaidizi amesema kuwa wana imani na kikosi chao kwa sasa ambacho kinazidi kuimarika.

  Ofisa habari wa Azam FC Jaffary Maganga amesema kuwa Kigali imechangamka na wengi wanauzungumzia mchezo wa kesho.

  0 0


  Facebook imeunda mfumo mpya unaowalenga watu wanaoweka matangazo ya uongo kwenye mtandao huo.

  Mfumo huo umekuja baada ya Martin Lewis, mwanzilishi wa tovuti ya Money Saving Expert, kushtakiwa baada ya jina na picha yake kutumika kwenye matangazo bandia kwenye ukurasa wa Facebook.

  Facebook iliamua kuchangia kiasi cha pauni milioni 3 kwa ajili ya kutengeneza programu ya kupambana na wadanganyifu nchini Uingereza.

  Taasisi ya kujitolea ya Citizens Advice imebuni laini ya simu ili iweze kuwasaidia watu wanapokutana na wadanganyigu mitandaoni-si tu kwa matangazo.

  Namna ya kuficha mawasiliano yako kwenye WhatsApp

  Mitandao ya kijamii yabadili muelekeo wa ushawishi

  Kadiri siku zinavyosonga mbele vitendo vya kitapeli vinazidi kuongezeka, hivyo taasisi hiyo inatarajia kuwasaidia watu 20,000 mwaka wa kwanza wa huduma watakayoitoa, na kutahadharisha kuwa mtu yeyote anaweza kuingia kwenye mtego huu.

  Citizens Advice imeainisha viashiria vitakavyojulisha kuwa matangazo ni bandia

  Tangazo lisilo na uhalisia-au bidhaa iliyo na gharama ya chini kuliko inavyotarajiwa.
  unapoambiwa ulipe haraka sana, au kwa njia isiyo ya kawaida-labda kwa huduma za kuhamisha fedha au kwa kutumia vocha.
  Mtu kuwasiliana na wewe bila kutarajia.
  kuulizwa kuhusu taarifa zako binafsi kama vile nywila (password) au pini.
  tangazo lenye picha za watu maarufu .
  Ndani ya Facebook, timu ya watu wenye ujuzi imeundwa kwa ajili ya kuchunguza matangazo yaliyoripotiwa kwa kutumia mfumo huu mpya.


  0 0

  Mawaziri wa mambo ya nje wa Ulaya, wanakutana hii leo mjini Brussels,  kujadili namna ya kuzishawishi Iran na Marekani kupunguza mvutano na kukaa katika meza ya mazungumzo.

  Japan Osaka | G20 Gipfel | Emmanuel und Angela Merkel (Reuters/J. Silva)

  Mgogoro kati ya Iran na Marekani umezidi kufukuta tangu Raisi wa Marekani Donald Trump alipoamua kujiondoa katika makubaliano hayo ambapo Iran ilikubali kupunguza shughuli za uundaji wa silaha za nyuklia, kwa sharti la kupunguziwa vikwazo vya kiuchumi na Marekani.

  Kutokana na Marekani kuiwekea tena vikwazo vikali, ambavyo vinaulenga moja kwa moja mfumo wa mapato wa nchi hiyo unaotokana na mafuta, Iran imeendeleza majukumu yake ya uzalishaji wa silaha za nyuklia kukiwa bado na makubaliano.

  Rouhani asema Marekani imefeli

  Kwa mujibu wa shirika la habari la DW, Akizungumzia mgogoro kati ya nchi yake na Marekani katika moja ya hotuba zake, Rais wa Iran Hassan Rouhani amesema kuwa kila jaribio ambalo Marekani imelifanya dhidi ya Iran ndani ya miezi hii 14, liwe kwa njia za kijamii, kisiasa ama kisheria limefeli halikufanikiwa.

  Katika Umoja wa Mataifa kwenye mikutano mbalimbali, na uwepo wao wiki iliyopita kwenye Shirika la kimataifa la nishati na Atomiki, ambalo lilionesha kuwa hakuna hata nchi moja duniani ambayo ingesikiliza tuhuma zao.  Kando ya Marekani na baadhi ya nchi, mataifa mengine yote yaliilinda Iran.


  Kutokana na msuguano huo, nchi zenye nguvu za Ulaya, Ufaransa Uingereza na Ujerumani, zimeionya Iran kuwa imeshindwa kuzingatia masharti ya makubaliano hayo.

  Mataifa hayo matatu, ambayo ni washirika katika makubaliano hayo  sambamba na Urusi, na China, yanatafuta namna ya kututatua mgogoro huo ambao umesababisha Marekani kuanzisha mpango unaolenga mashamblizi ya anga dhidi ya Iran, ambao Rais Trump aliusitisha katika dakika za mwisho.

  Raisi wa Ufaransa Emmanuel Macron, alimtuma mwanadiplomasia wake wa juu kwenda Iran wiki iliyopita ili kupendekeza namna ya kuituliza hali na kwamba alitaka kupitia upya maendeleo ya kidiplomasia ifikapo leo Julai 15.

  Siku ya Jumapili, Raisi Rouhani Rouhani alisisitiiza msimamo wake kuwa Iran iko tayari kufanya majadiliano na Marekani, iwapo Marekani itaviondoa vikwazo ilivyovirejesha kwa Iran kuhusiana na mpango wa nyuklia.

  Hata hivyo Trump, hajaonesha dalili yoyote ya ya kuondoa vikwazo hivyo licha ya kujadili na Raisi wa Ufaransa  na alisema wiki iliyopita kuwa ataongeza vikwazo zaidi.

  0 0  Staa wa Bongo Movie hapa nchini Tanzania Yusuph Mlela, leo ameeleza sababu ziliozofanya awe na tofauti na staa mwenzake wa Bongo Movie ambaye ni Hemed Suleiman "PHD".


  Yusuph Mlela amefunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya taarifa zilizokuwa zinaendelea kwamba wamegombana sababu ya mwanamke.

  "Hemed ni rafiki yangu sijawahi kugombana naye kabisa, hizo zilikuwa ni stori tu, hayo ni mambo tu yalitokea watu hawajui kiundani, ilikuwa ni kutoelewana kwa kawaida ila sasa hivi tupo vizuri, tunafanya kazi pamoja".

  Aidha msanii huyo amesema anapenda sana nywele zake kuliko kitu chochote, tangia ameanza kujitambua akiwa ana umri wa miaka 17 au 18 alikuwa anafuga nywele kwa mtindo wa Afro, kusuka au anaziachia anavyototaka.


  0 0
  0 0


  Pombe, maradhi na ulaji wa vyakula usiozingatia maoni ya wataalamu wa afya na tiba lishe ni baadhi ya mambo yanayotajwa kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.


  Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linatajwa kushika kasi na limesababisha baadhi ya wanaume kadhaa kuishi maisha ya uyonge yaliyojaa hofu hasa kuhusu hatima ya uhusiano wa ndoa zao.


  Kutokana na hali hiyo, baadhi ya waathirika hao wameendelea kuhangaika kurejesha heshima kwenye ndoa zao kwa kusaka tiba, wengine hospitali na wengine kwa waganga wa jadi.


  Kama unasumbuliwa na tatizo hilo Wasiliana Nami DR Justin Kwa Ushauri zaidi na Tiba ya Tatizo hilo Kwa Kutumia Dawa za Asili zisizo na madhara, Tupigie simu namba 0744040721 au 0683645920

  Au Fika Ofisini kwetu Mbagala Zakhemu Barabara ya Jeshini....

  0 0


  Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa vikao vya kuchunguza tuhuma za ufisadi dhidi yake, ni njama iliyopangwa dhidi yake.

  Zuma aliyasema hayo jana Jumatatu katika kikao cha uchunguzi wa faili la tuhuma za ufisadi wa fedha zinazomkabilia ambapo alikitaja kikao hicho kuwa ni njama dhidi yake.

   Aliongeza kwamba maadui wake hata walipanga njama ya kutaka kumuua, kwa kuwa walikuwa wanataka kutwaa madaraka na kumuweka kando.

  Mwanzoni mwa utetezi wake kwenye kikao hicho alisema kuwa tuhuma hizo zilikuwa na lengo la kumuondoa madarakani.

  Itakumbukuwa kuwa rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini aliondolewa madarakani mwezi Februari mwaka jana.

  Aidha Zuma anatuhumiwa kwamba katika kipindi cha miaka tisa ya uongozi wake, aliwapa fursa watu wake wa karibu kutumia mali ya umma kwa maslahi yao binafsi na pia kuwateua katika nafasi mbalimbali serikalini.

  Rais huyo wa zamani wa Afrika Kusini ametupilia mbali tuhuma hizo akizitaja kuwa ni za kisiasa tu.

  Katika hatua za kuendelea kumbana Jacob Zuma katikati ya mwezi Agosti mwaka jana Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini ilibatilisha uteuzi wa Mwendesha Mashtaka Mkuu ambaye alipewa kazi na Jacob Zuma baada ya kumpiga kalamu nyekundu afisa aliyekuwepo kabla yake.

  Kadhalika mahakama hiyo ilitoa amri kwamba, mwendesha mashtaka mkuu wa zamani arejeshwe kazini katika muda wa siku 90 kwa lengo la kufuatialia faili la tuhuma za ufisadi dhidi ya rais huyo wa zamani

  0 0


  Rais Magufuli amepongeza utendaji mzuri wa Jeshi la Polisi nchini, huku akieleza kuchukizwa na askari wake wachache wasio waadilifu.

  Amebainisha kuwa katika kipindi cha miezi sita iliyopita, askari polisi 157 wamechukuliwa hatua kwa kukiuka taratibu za kiutumishi. Kati yao, 54 wamefukuzwa jeshini.

  Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa nyumba 20 za askari polisi zilizojengwa kwenye Mtaa wa Magogo mjini Geita.

  Kutokana na kuwapo kwa changamoto hiyo, Rais Magufuli alimtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchni (IGP), Simon Sirro, kuwa mkali kwa wanaokiuka maadili na kuchafua sifa nzuri za jeshi hilo.

  Akifafanua zaidi kuhusu changamoto hiyo, Rais Magufuli alisema baadhi ya askari hao wamewajibishwa kutokana na makosa mbalimbali yakiwamo vitendo vya kushiriki katika kutenda uhalifu ukiwamo ujambazi na rushwa.

  Alimtaka IGP Sirro kutokubali wachache walioko katika jeshi hilo, kuchafua heshima na sifa ya jeshi hilo ambalo yeye analiamini na wananchi wanalikubali kwa utendaji wake mzuri.

  ''Ninapongeza kazi nzuri inayofanywa na Jeshi la Polisi kwani vitendo vya uhalifu ukiwamo ujambazi, hata mkoani Geita, vimepungua sana kama ambavyo pia wananchi wana imani na Jeshi la Polisi kwa uadilifu na utendaji wake," alisema.

  "Kuna askari wachache tu ambao wamekuwa wakichafua sifa na heshima ya jeshi, hao wasipewe nafasi. Sirro washughulikiwe hao wachache," Rais Magufuli aliagiza.

  Alisema wapo baadhi ya askari polisi wasio waadilifu, wanashirikiana na majambazi kufanya uhalifu, kubambikiza kesi wananchi wasio na makosa.

  Alisema askari wa aina hiyo lazima washughulikiwe ili kutochafua taswira ya Jeshi la Polisi na kulishusha hadhi mbele ya umma.


  0 0


  Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa  amefanya uteuzi wa Wakurugenzi Watendaji wa mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira Kahama na mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Tabora pamoja na kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya majisafi na usafi wamazingira Bukoba.

  0 0

  STAA wa Filamu Bongo, Irene Uwoya,  kupitia ukuarasa wake wa Instagram,  amewaomba radhi waandishi wa habari  kwa kitendo chake cha kuwarushia pesa wakiwa katika mkutano wa wanahabari na kusema kuwa hakufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa na  amesisitiza kuwa alifanya kwa moyo mzuri kutokana na juhudi za waandishi wa habari kwenye kusambaza taarifa.


  Uwoya alifanya hivyo akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza katika ukumbi wa Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam jana Julai 15, 2019 kwenye mkutano ulioitishwa na wasanii wa Bongo Muvi ukiwa na lengo la kuzungumzia uzinduzi wa Swahiliflix ambao ni mtandao wa kuuzia muvi, unaotarajiwa kufanyika tarehe 31, mwezi huu mwishoni.

  Alichokisema:- Ndugu zangu waandishi wa habari, leo katika press conference ya Swahili Inflix na ndugu zetu waandishi wa habari niliamua kutoa fedha kwa style ya kutunza.

  Baadhi yenu mmekwazika kwa kitendo hicho nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, binafsi nawapenda waandishi wa habari kwani nyie ni watu muhimu sana katika jamii.  Sikufanya hivyo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa.Kama binadamu moyo wangu ulijawa na upendo na furaha iliyopitiliza ndipo niliona niweze kushiriki nanyi furaha hiyo kwa aina ile ya kuwatunza pesa,sababu mara nyingi mmekuwa watu muhimu katika kazi na mambo yote yanayohusu sanaa yetu na jamii kwa ujumla.  Na baadhi ya waandishi ambao kwa bahati mbaya waliharibu vifaa vyao wakati wa kuokota shukrani yangu hiyo(pesa) naomba mniwie radhi na mnisamehe sana na poleni sana kwa changamoto.  Pia kuhusu ndugu zangu waandishi kuwaomba kuvaa suti ile nilikuwa na maana nzuri ya kwamba katika utanashati wenu wa kila siku sisi tulipendelea siku ya tar 31st August katika show yetu inayoandaliwa na Swahili Infilix itakayokuja kuleta mapinduzi makubwa na ukuaji mkubwa zaidi wa filamu zetu za hapa nyumbani tunatamani kuona wote mkiwa katika uniform ambayo itawatambulisha vyema kimavazi ambayo kwa wazo letu tuliweka suti na kiukweli mtapendeza sana na zaidi ya kawaida tulivyozoeana.Nawapenda sana maana hakuna mimi bila nyinyi nathamini na kuwashukuru sana sana.Na zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti.
  Asanteni sana.

  0 0

  NYOTA mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu.  Ajibu ambaye msimu uliopita wa 2018-19 alikuwa kinara wa asisti ndani ya ligi akiwa nazo 17 na pia alitupia mabao sita kwa sasa ni mali ya Simba ambapo amesaini kandarasi ya
  miaka miwili.  Akizungumza na Spoti Xtra, Ajibu alisema; “Bado msimu haujaanza na tunatarajia kuingia kambini muda wowote hivyo utakuwa muda mzuri kwetu kujipanga vema kwa ajili ya msimu ujao.  “Kila kitu kwa sasa kipo freshi, natambua ushindani ni mkubwa na kila mmoja anataka kuonyesha uwezo hilo sina tatizo nalo ninaamini kila kitu kitakuwa sawa na mashabiki watapenda wenyewe,” alisema Ajibu ambaye alikataa ofa ya TP Mazembe hivi karibuni.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli amemwagiza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kufuatilia malipo yote ya Wagonjwa wanoenda kutibiwa nje ya nchi ili kubaini ubadilifu unaofanywa na baadhi ya watu wasiowaaminifu.

  Rais Magufuli ameagiza hilo jana wakati akizindua miradi Saba ya huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa Bugando yenye thamani ya shilingi Bilion15, jambo litalosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma bora kwa ukaribu pamoja na kuokoa kiasi cha fedha miongoni mwa wanaohitaji huduma.

  “Na kwasababu Waziri wa Afya yupo hapa, akafuatilie malipo yote ambayo tunatakiwa kulipa, kule nje , akikuta kunamalipo yakulipa mtu ambae hakuwa mgonjwa aliyejihifadhi huko, akazilipe mwenyewe ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

  Rais Magufuli amesema kuwa baadhiya Watendaji waliona kupeleka Wagonjwa nje ya nchi kwaajili ya matibabu ni fursa yakujipatia kipato, jambo lililokuwa linapelekea hasara kubwa kwa nchi ya Tanzania kutokana na malipo kwa baadhiya watu wasiostaholi.

  ” Hata kupeleka kwa wagonjwa nje kwa Watanzania ilikuwa ni dili, ilikuwa ni fursa kwa Watendaji, wapo watu waliokuwa wanapewa vibali kwenda kutibiwa India lakini anaumwa mafua, ilikusudi apate safari na msindikizaji, bill zote zinaletwa kwa Serikali ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

  Dkt. Magufuli aliendelea kusema kuwa ni lazima tujenge nidhamu katika nchi, huku akisisitiza kuwa Serikali haijakataza kupeleka wagonjwa nje ya nchi, huku akisisitiza kuwa wagonjwa wanaostahili kupelekwa kwa matibabu nje ya nchi ni wale walioshindikana ndani ya nchi.

  Aidha, ameagiza kuboresha uzalishaji wa oksijeni ili kuhakikisha zinazalishwa kwa wingi jambo litalosaidia kuokoa kiwango kikubwa cha mapato kinachopotea kwa kuagiza nje ya nchi, pia itasaidia kuongeza ajira kwa wananchi wa Tanzania.

  “Ninawaomba ndugu zangu, tengenezeni oksijeni nyingi, panueni uzalishaji ili Wizara ya Afya iagize hapa hapa Bugando ili vijana wanaomaliza famasi hapa hapa Bugando wapate ajira hapa yakutengeneza Oksijeni ” alisema Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli


  0 0

  Winga wa kimataifa wa Tanzania Ramadhan Singano, ameweka wazi kuwa kabla ya kujiunga na klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, alifuatwa na Yanga.

  Singano amesema hayo kwenye mahojiano na East Africa Television leo Julai 5, 2019 ambapo amesema baada ya kumaliza mkataba na Azam FC, Yanga walimfuata lakini yeye alitaka kwenda nje.

  ''Mara nyingi nikimaliza mkataba nakwenda kujaribu soka la nje mpaka nikikosa ndio narudi hapa lakini mara hii nimepata TP Mazembe japo mwanzo klabu kama Yanga ilinihitaji lakini nilikuwa nataka kwenda nje'', amesema.

  Singano ambaye amewahi kuchezea Simba, amesaini mkataba wa miaka mitano kucheza TP Mazembe ya DR Congo baada ya mkataba wake na Azam FC kumalizika mwezi Juni mwaka huu.

  0 0  Tanzanian movie star, Jacqueline Wolper discloses she is in a relationship but chooses to keep it private.

  Speaking in a recent interview, the business woman revealed she is seeing someone though it is not for the public to know nor scrutinize.

  Unlike the past where her love life, would get spilt to the public, she is intimate about this one.

  Reason why masses are not aware of her lover.

  Adding that she has previously opened up about her relationships, which never ended well and does not want to be a victim of such again.  However, she bashes critics who believe she is busy going after fellow women´s husbands.

  Kwa sasa hivi najitahidi ku’keep secret mahusiano yangu
  japo me napenda nikiwa kwenye mahusiano kumpost mpenzi wangu
  hata kumuweka Profile picture
  kwani sina wakumuogopa sababu mimi sio mwizi wa mali za watu


  0 0


  I’m Linda 21 years, at the University and I stay with my Boyfriend…… I caught my bf with another girl, when I confronted him he denied it and said they are just friends. I got so angry that night and as I was preparing his supper, something bad came to mind and I felt I shud put my blood (Menses blood) into his meal.

  So I removed my pad, soaked it with some little water, then squeezed the blood into his food, put some other ingredient and gave him to eat. Now am worried coz he might get some complications or diseases….if he gets any diseases, should I tell him what I did so that he can go for medical checkup or I shud just remain quiet?? Am afraid coz he might beat me up to coma! Advice me on what to do please!

  0 0

  AMBER LULU Afunguka vilivyo "Siwezi kukaa wiki bila SEX, ndio starehe yangu, Harmonize ningempitia, Sarah ali-mind"...Mtazame hapa katika haya mahojiano na SNS kafunguka yote

  VIDEO:


  0 0


  Wasanii wa tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na Bongo Movie hapa nchini, Irene Uwoya pamoja na Amber Lulu wamekubali makosa yao na wameomba radhi kwa vitu ambavyo wamevifanya mbele za watu.


  Wawili hao wameomba radhi siku ya jana kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, baada ya Irene Uwoya kumwaga pesa mbele ya wanahabari hali iliyopelekea uharibifu wa vitendea kazi mbalimbali, huku Amber Lulu akidaiwa kutumia lugha chafu kwa Hamisa Mobetto, Dj pamoja na washindani wa Miss Kinondoni siku ya Jumamosi.

  “Ndugu zangu wahandishi wa habari, niliamua kutoa pesa kwa 'style' ya kutunza, nawaomba radhi sana sikuwa na nia mbaya juu yenu, sikufanya hivo kwa lengo la kuwadhalilisha kama ilivyotafsiriwa, Pia kuhusu kuwaomba kuvaa suti nilikua na maana nzuri katika utanashati wenu wa kila siku, kwa zaidi naomba radhi kwa yeyote aliyekwazika kwa namna moja au tofauti”, ameandika Uwoya.

  Aidha kwa upande wa msanii Amber Lulu yeye ameandika, “naomba radhi, sisi sote ni watu wenye mapungufu, kwa kusema hivyo naamini kila mtu anaweza kukosea, naomba radhi na kwa unyenyekevu naomba samahani kwa kile kilichotokea usiku wa Miss Kinondoni, na sikua katika hali maridhawa na tengamavu natambua nilipoteleza naomba radhi kwa yeyote niliemchukiza.”

  0 0


  Katibu wa baraza la ushauri la viongozi wastaafu CCM, Pius Msekwa amesema malalamiko ya makatibu wakuu wawili wa chama hicho atayapeleka ngazi za juu kwa hatua zaidi.

  Juzi, makatibu wakuu hao wawili wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana, walimwandikia barua Msekwa wakilalamika kudhalilishwa kwa mambo ya uongo na mtu anayejitambulisha kama mwanaharakati na mtetezi wa Serikali.

  Msekwa ambaye alisema barua hiyo ambayo ni ya kwanza kuwafikia wao kama Baraza la Wazee Wastaafu, kwa kawaida itapelekwa kwenye chama hicho ambacho ndicho kinachopaswa kuitisha vikao kushughulikia malalamiko yaliyotajwa.

  Amesema nakala nyingine za barua hiyo zimepelekwa kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Magufuli na Katibu Mkuu, Dk. Bashiru Ally.

  “Hii ni mara ya kwanza kupokea malalamiko ya aina hii, kwanza hakuna utaratibu wa kawaida, lakini tutafuata taratibu za chama, tutapeleka kwenye chama chenyewe." Amesema na kuongeza;

  “Barua hii nakala yake imeenda pia kwa Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu"


  0 0

  OFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba SC,  Crescentius Magori,  leo Julai 16, 2019,  amefunguka kwamba wameletewa barua ambayo inadhihirisha kuwa  Hamisi Kilomoni kavuliwa udhamini wa klabu Simba ya jijini Dar es Salaam.

  Magori ameyasema hayo akizungumza na vyombo vya habari alipoongeza kuwa mzee huyo anafanya makusudi ya kuichafua klabu hiyo na ndiyo maana uongozi umeamua kuliweka wazi jambo hilo wazi.

  “Alikoma udhamini wa Simba tangu Oktoba 2017, ambapo Novemba 8 alijulishwa kupitia wakili wake kuwa yeye siyo mdhamini wa Simba,” alisema Magori.

  Katika siku za hivi karibuni, baada ya klabu hiyo kuanza kujiendesha kibiashara kufuatia mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) kuwekeza katika klabu hiyo, kumekuweko na mgogoro wa chinichini baina ya uongozi wa klabu hiyo maarufu ya Dar es Salaam na mchezaji wa zamani wa klabu hiyo, mzee Hamisi Kilomoni.

  0 0


  Rais John Magufuli ametoa gunia 15 za mchele na ng'ombe watatu kwa wafungwa wa Gereza Kuu la
  Butimba mkoani Mwanza.

  Hii leo Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza na
  kusikiliza kero za Wafungwa.

  ‘’Kwa maaskari Magereza nimesikia kilio chenu ninyi hamna tofauti na majeshi mengine na hamuwezi mkawa mnafanya kazi kwa kulalamika, hakikisheni hawa wafungwa hawaingii na simu gerezani, nyembe, wanaofanya biashara na hawa wafungwa wasifanye.” amesema Rais Magufuli.


  0 0


  Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini Marc Batchelor amepigwa risasi na kufariki

  Picha za eneo la tukio zinaonyesha risasi zilipita kwenye dirisha la kioo cha gari lake na waliofanya tukio hilo inaelezwa walikuwa wamepanda pikipiki.

  Batchelor atakumbukwa sababu ni miongoni mwa wachezaji wachache waliocheza timu hasimu nchini Afrika kusini, Kaizer Chiefs na Orlando Pirates.

  0 0


  Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAf' limemtangaza mwamuzi, Bamlak Tessema Weyesa (39) kutoka Ethiopia kuchezesha mtanange wa fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kati ya Senegal  na  Algeria utakaopigwa Julai 19 Mwaka huu.

  Katika AFCON ya Mwaka huu, Bamlak Tessema amechezesha mchezo wa Nusu fainali Kati ya Senegal wakishinda dhidi ya Tunisia, Mechi nyingine Ni ya Robo fainali Algeria wakishinda kwa penati dhidi ya Ivory Coast na Mechi za hatua ya Makundi, Ghana wakitoka Suluhu dhidi ya Cameroon, Tunisia na Angola wakitoa Sare.

  Fainali hii inazikutanisha timu mbili ambazo zilipangwa katika kundi moja, Algeria na Senegal zote zinatokea kundi 'C' ambapo kulikuwa na timu ya Taifa Stars, Kenya, Senegal na Algeria Kenya na Taifa Stars zote zilitoka hatua ya awali kwenye kundi hilo.

  0 0


  Leo July 16, 2019 Rais Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika Gereza la Butimba Mkoani Mwanza kusikiliza kero za Wafungwa.

  Mmoja wa wafungwa anayetumikia kifungo cha miaka 30, Kalikenya Nyamboge, amemtuhumu Ofisa Usalama gerezani hapo kuwapa wafungwa simu halafu zikikamatwa wananyan’ganywa vitu vyao walivyo navyo lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote.

  “Mheshimiwa rais, huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakiwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru.

  “Sasa hivi Jenerali Kamishna ametuletea daktari msomi na alivyofika vifo ndiyo vimepungua maana walikua wakikuchoma sindano wanakuua.

  “Na si mara ya kwanza wao kuua mimi nilikuwa nimepanga nikitoka nije kukwambia na nikitoka nitakuletea mambo yote yanayotokea huku lakini huyu usimuache maana kwa Mwenyezi Mungu utakua umeandika maelezo ya mauji,” amesema Nyamboge.

  Naye mfungwa mwingine Kulwa Alphonce, alikamatwa mwaka 2017 akiwa na mafuta ya dizeli akapelekwa Kituo cha Nyegezi askari wakamuomba Sh milioni moja, akawaambia ana 200,000 tu ambayo walikataa kisha baadaye wakampeleka ‘central’ baada ya hapo akafunguliwa kesi ya mauaji.

  Aidha, mfungwa mwingine Shukrani Masegenya, alimuomba Rais Magufuli kuwapunguzia adhabu ya vifungo ili wakatumie ujuzi wao wanaofundishwa nje.

  Akizungumza baada ya kuwasikiliza wafungwa na askari magereza , Rais Magufuli amesema kufika kwake gerezani hapo kuna somo kubwa limemuingia na akwenda kulifanyia kazi.

  "Niliyoyasikia lazima nifanyie kazi, nimesikia changamoto za wafungwa na nimesikia pia changamoto za askari wangu.Niahidi nitayafanyia kazi yote ambayo nimeyasikia kwenu wote,"amesema Rais Magufuli na kuongeza hayuko tayari kuona askari magereza wanalalamika wakati yeye yupo.

  Rais Magufuli amefafanua kwenye gereza hilo la Butimba amegudua mambo mengi , amebaini kuna kuombwa rushwa wafungwa na mahabusu na uamuzi wake wa kufika hapo umetokana na kufahamu mambo mengi ambayo mengine wafungwa wameshindwa kueleza.

  Amewahakikishia wafungwa hao kwamba amewaelewa wafungwa na mahabusu hao na kuahidi kuwa amewasikia na yote ambayo ameleezwa yatafanyiwa kazi."Niahidi nimewasikia, nimewasikia na yote nitayafanyia kazi.Naomba muwe wavumilivu na niaminini."

  Rais Magufuli amesema hata walioko uraiani ni wafungwa au mahabusu wabadae na kwamba kufungwa au kuwa mahabusu haina maana ya kukosa haki za kibinadamu.


  0 0


  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza amesema kuwa wameamua kumuita msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya pamoja na Steve Nyerere, kufuatia kitendo alichokifanya Irene cha kuwarushia pesa waandishi wahabari katika mkutano wa wasanii, uliofanyika Julai 15, Dar

  Akizungumza leo Julai 17, Mngereza amesema kufuatia wito huo, wao kama Baraza hawajapanga kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.

  ''Wajibu wa baraza ni kukaa na wasanii, halafu kuzungumza nao, na  baraza linafanya kazi kwa mujibu wa sheria lililoziweka na kama uliona yale ni masuala ya fedha", amesema Mngereza.

  Aidha kwa upande wake Steve Nyerere amekiri kupokea taarifa hizo na kwamba yeye kama msanii na BASATA ni Serikali, hivyo atafika kama alivyotakiwa.

  Aidha Steve alipoulizwa kuhusu kitendo cha Irene Uwoya kuwatupia waandishi wa habari pesa, amejibu ''No Comment"