Mimi na watanzania wenzangu tunasikitishwa sana na kauli za kujirudia rudia za Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akitumbukiza Tanzania katika LAANA. Mara hii Membe ananukuliwa na Vyombo vya Habari akilaani ISRAELI kwa mauaji yanayoendelea huko Gaza.
Mimi binafsi nimefuatilia vyanzo vingi vya Habari kuhusu yanayoendela Gaza, na haya ndiyo mambo 6 niliyojifunza:
Hamas inayoongoza Gaza ndio walianzisha misuguano hii kwa kuwateka vijana watatu wa Israeli na kasha kuwaua. Kitendo hiki kilipongezwa sana na Hamas huko Gaza, kuashiria palikuwa na mahusiano ya moja kwa moja kati ya watekaji na chama hiki cha Hamass.
Hamas walikuwa wakirusha roketi kuelekea miji ya Israeli bila kujali yatawaua raia au la, kitendo ambacho ni cha uchokozi.
Israeli inatumia teknolojia kubwa sana kuyaharibu maroketi hayaya Hamas kwa kutumia IRON DOME SYSTEM kabla hayajaleta madhara yoyote. Ndiyo maana hadi sasa, hakuna muisraeli hata mmoja ameuliwa na roketi hizi zaidi ya 1,000 zilizorushwa na Hamas hadi sasa.
Hamas haitambui uwepo wa Israeli. Kwa maana nyingine, Hamas katika ILANI yao, wameapa kuwafurukusha Israel wasiwepo kabisa eneo lote la Mashariki ya Kati.
Hamas wanahamasisha raia wa Gaza wasiondoke maeneo yale hatarishi ili watumike kama ngao ya kibinadamu (human shield) wakidhani Israeli itawaacha warushe tu roketi,
Israeli inatumia njia za kisayansi kuwatumia watu wa Gaza meseji kwenye simu zao kuwatahadharisha wasiende maeneo yanayotarajiwa kupigwa mabomu. Hili ni jambo la kistaarabu sana, huwezi kulitarajia wakati wa vita. Ubishi wa tahadhari kama hizi ndio umepeleka raia wa Gaza kudhuriwa na mashambulizi ya Israeli.
Baada ya maelezo hapo juu, tujiulize kama Taifa, Je, Membe alitaka Israeli wakirushiwa maroketi na Hamas wakae kimya wasiyajibu? Membe ukiwa Waziri wa Mambo ya Nje, upo tayari kuona miji ya Dar es Salaam au Dodoma ikirushiwa maroketi na nchi jirani, na Tanzania tukaae kimya tu kwa sababu Tanzania ikijibu inaweza kuua raia wa hiyo nchi ya jirani chokozi?
Waziri Membe umeonesha udhaifu mkubwa ulio nao katika tasnia ya diplomasia za kimataifa na mambo ya nje kwa kutojua historia ya mgogoro huu, na kitendo chako cha kuegemea upande mmoja ni cha aibu na fedheha kwa wizara unayoongoza. Miaka ya nyuma uliwahi pia kunukuliwa ukilaani Israeli pale ulipoalikwa kama mgeni wa siku ya Palestina katika Ubalozi wao hapa Dar es Salaam.
Waziri Membe tunakuhakikishia kuwa, kiitendo chako cha kuilaani Israeli hakiwezi kupita kimya bila kupingwa na Watanzania. Umelaani Israeli lakini laana yako ikurudie wewe mwenyewe na familia yako. Ni aibu kubwa kwa mtu kama wewe unayetamani kuongoza ofisi kubwa kuliko zote hapa Tanzania (IKULU) unatamka maneno ya laana hata kabla hujapewa ofisi.
Imeandikwa, HESABU 23: 8 “Nimlaanije, yeye ambaye Mungu hakumlaani? Nimshutumuje, yeye ambaye Bwana hakumshutumu?” , Ni wazi kuwa Anayelaani ISRAELI naye ANALAANIWA. Anayebariki ISRAELI naye ANABARIKIWA. Tunamshukuru Mungu kwa kutuonesha Moyo ulio nao ili waakati wako wa kugombea urais ukifika tukuweke kwenye jalala la milele. Waziri Membe Umetegwa kwa maneno ya kinywa chako mwenyewe.
By proisra via JF
Quote of the Day
You are always a student, never a master. You have to keep moving forward.