Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Hii Hapa Kauli ya Jose Mourinho baada ya kupewa kazi Tottenham

$
0
0

Mara baada ya kukabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha  Tottenham inayoshiriki Ligi kuu ya Soka ya Uingereza (EPL), kocha Jose Mourinho afunguka.

Ikumbukwe Jose Mourinho amechukua nafasi ya Mauricio Pochettino aliyetimuliwa baada ya miaka mitano ya kuinoa Tottenham ndani ya White Hart Lane.

“Nina furaha ya kujiunga na club hii yenye historia nzuri na mashabiki wenye moyo na timu yao. Ubora wa kikosi na mfumo wa kukuza vipaji wa club hii unanifurahisha sana. Kwenda kufanya kazi na wachezaji ambao wananivutia inapa hamasa zaidi” amesema.

Mourinho ambaye mara ya mwisho alikuwa kocha wa Man United amepewa mkataba mpaka msimu wa 2022/2023.

Jose Mourinho anaongeza orodha ya timu ambazo amewahi kuzifundisha ambazo ni FC Porto, Inter Milan, Chelsea, Real Madrid, Manchester United na sasa ni Spurs.

Alichokisema Lema baada ya Meya wa CHADEMA Arusha kutimkia CCM

$
0
0

Baada ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kupokelewa na Ndg. Humphrey Polepole Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ametoa neno.

Lema amesema kuwa ni baraka kubwa kwa Chadema Meya huyo kuondoka kwenye CCM huku akidai kuwa bado rafiki yake mmoja.

"Wakati Yesu Kristo anataseka msalabani Wayahudi walikuwa wanapiga kelele wakisema amekwisha,amekwisha..lakini yeye alisema Imekwisha," ameandika Lema kwenye ukurasa wake wa Twitter.

"Wanafikiri tumekwisha na kumbe Imeisha. Ni baraka kubwa  kwa Chadema Mayor wa Arusha Mjini Kalist Lazaro kwenda CCM,bado rafiki yake mmoja."

Punyeto Husababisha Ukosefu wa Nguvu za Kiume na Uume Kuwa Mfupi zifuatazo ni Sababu Kuu

$
0
0


Punyeto husababisha ukosefu wa nguvu za kiume na uume kuwa mfupi zifuatazo ni sababu kuu

i🥕kudhoofisha na kuharibu mishipa ya uume ambayo hufanya uume kuwa na nguvu
ii🥕hudhofisha utendaji kazi wa mishipa ya ater ambayo ambayo ndio hutumika kama njia ya kusafirishia damu kupeleka kwenye misuli ya uume na ivyo kuufanya uume usimame
iii🥕punyeto hupelekea kuvuja kwa mishipa ya neva na hivyo kusababisha kufyonzwa kwa haraka Sana kila kila iingiapo ndani ya misuli ya uume na matokeo yake ni uume kusimama kwa mda mfupi Sana wakati wa tendo la ndoa
iv🥕punyeto huathiri mtiririko wa damu kwenda kwenye mishipa ya uume kwa sababu hudhoofisha misuli ya uume pamoja na mishipa ater ambayo ndio hutumika katika kusafirisha damu kwenda kwenye Hume
V🥕hujenga ukungu katika kiwanda cha uzalishaji manii  (mbegu za kiume)ambayo hudhoofisha manii na kusababisha joto la haraka pindi tu upatapo hisia ya mapenzi ndio unajikuta unakojoa haraka
DALILI ZA MTU ALIYE ATHIRIWA NA PUNYETO
i🌶uume kurudi ndani
ii🌶uume kusimama ukiwa legelege
iii🌶uume kusinyaa na kuwa kama wa Mtoto
iv🌶kufika kileleni haraka wakati wa tendo
v🌶kushindwa kurudia tendo round inayo inayofuata au kuchelewa kurudia ten do
vi🌶muda mwingini uume kusinyaa ndani ya uke wakati wa tendo la ndoa
vii🌶kutoa manii nyepesi zisizo na nguvu hata utokaji wake sio wa kuruka

Kwa ushauli zaidi zaidi piga simu 255783185060

Wagombea wote wa upinzani waliopitishwa kugombea Nachingwea wajitoa

$
0
0


Wanachama wa vyama vya upinzani ambao waliteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wilayani Nachingwea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 wamejitoa kushiriki katika uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea, Nnunduma Ali alipozungumza na Muungwana Blog, leo mjini Nachingwea.

Nnunduma alisema wagombea wa nafasi  mbalimbali walioteuliwa kutoka vyama vya CHADEMA na CUF wamejitoa wenyewe kwa kuandika barua, pia ngazi za vyama zilizowadhamini viliandika barua za kujitoa.

 ''Hadi kufikia tarehe 16.11.2016, jioni wagombea wote waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali  kupitia vyama vya CUF na CHADEMA walikuwa wamejitoa. Sisi kama wilaya tunaandaa fomu za matokeo zitakazotumika kuwatangaza viongozi hao, tutabandika kwenye mbao za matangazo siku ya tarehe 24.11.2019,'' alisema Nnunduma.

Msimamizi huyo wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea alisema awali Chama cha Mapinduzi asilimia 98 ya wanachama wake waligombea nafasi mbalimbali walipita bila kupingwa, kwahiyo baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa ni dhahiri kimeshinda kwa asilimia mia moja.

Nnunduma aliitaja idadi ya viti vilivyotarajiwa kugombewa ni vijiji 127, vitongoji 525, viti maalumu vyote 997 na viti mchanganyiko 1556. Wakati vyama vilivyosimamisha wagombea vilikuwa CUF, CHADEMA na CCM. Akivitaja vyama ambavyo wagombea wake walichukua fomu na kurejesha ni CUF, CHADEMA, ADC na CCM.

Ujenzi wa njia nne Dodoma – Morogoro waiva

$
0
0

Waziri wa Fedha na mipango Dkt. Philip Mpango amefanya mazungumzo na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) ili iweze kuipatia Tanzania mkopo nafuu kwa ajili ya kujenga barabara ya njia nne toka mkoani Morogoro hadi Jijini Dodoma kwa lengo la kuboresha usafirishaji wa abiria na mizigo.

Dkt. Mpango ametoa ombi hilo Jijini Dodoma wakati alipokutana na Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya wakurugenzi ya benki hiyo Amos Cheptoo anayewakilisha nchi nane za ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema ombi lake kwa Mkurugenzi huyo wa AfDB ni kuona namna gani wanaweza kuanza kuliweka jambo hilo kwenye miradi ambayo benki hiyo imekuwa ikiigharamia ili kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo ya njia nne itakayo kuwa na uwezo wa kupitisha magari mawili kwa njia ya kwenda na ya kurudi.

“Baada ya Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi tunahitaji usafirishaji kwa njia ya barabara uwe bora na haraka zaidi lakini pia tuweze kupunguza ajali maana kuna ajali nyingi kwa sababu magari yanayokwenda Dar es Salaam na yanayokuja Dodoma au kwenda Mwanza yanapishana kwenye njia moja,” amefafanua Dkt. Mpango.

Akijibu ombi la Waziri Dkt. Mpango Mkurugenzi mtendaji huyo wa Bodi ya wakurugenzi ya benki ya AfDB Amos Cheptoo amesema watahakikisha Tanzania inapata mikopo ya miradi yake ya kimkakati na ya kipaumbele ukiwemo wa ombi hilo la ujenzi wa barabara ya Morogoro hadi Dodoma kwa kiwango kinachokusudiwa.

Kuhusu uwezeshwaji kwa taasisi nyingine nchini Cheptoo amezitaka sekta binafsi kuchangamkia fursa za mikopo nafuu zilizopo katika benki hiyo kutokana na kuwa na nafasi nzuri ya upatikanaji wake ili ziweze kujikwamua kiuchumi na kutokomeza umasikini barani Afrika.

“Sekta binafsi za Tanzania hazijatumia vizuri dirisha la mikopo ya AfDB ikilinganishwa na chi nyingine za ukanda huu wa Afrika ninakuomba Waziri wa fedha uwahamasishe wakope fedha hizo ili kukuza mitaji yao na kuongeza ajira,” amedisitiza Cheptoo.

Katika hatua nyingine Cheptoo amesema benki ya AfDB ipo katika hatua za mwisho za kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa msalato jijini Dodoma na tayari benki hiyo imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini hapa pamoja na miradi mipya ya kuzalisha nishati ya umeme.

Aidha Mkurugenzi huyo pia amempongeza Rais John Magufuli kwa kuwa kiongozi mwenye maono ambaye amesaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kuzitaka nchi nyingine barani Afrika kujifunza kutoka Tanzania.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imefadhili miradi 23 nchini ikiwemo 21 ya umma na miwili ya sekta binafsi ikiwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 2.1 katika nyanja za nishati, miundombinu ya barabara, usafiri, kilimo, maji na usafi wa mazingira.

Msanii Davido akamatwa na Polisi

$
0
0
Msanii Kutoka Nigeria, ameingia matatani baada ya Ugomvi uliopelekea shabiki aliyekuwa akimsumbua kupigwa na chupa kichwani.

Tukio hilo la fujo lilitokea Dubai ambapo Davido alikuwa akifanya show kwenye Tamasha la ONE AFRICA MUSIC FESTIVAL.

Inasemekana kuwa baada ya show, Davido alishuka jukwaani ndipo akakutana na shabiki aliyekuwa akilazimisha akutane Naye. Baada ya shabiki huyo kuzuiliwa alikasirika na kuamua kumpiga shabiki Mwingine na chupa kichwani.

Baada ya tukio hilo Davido alijitahidi kutoweka hilo lakini askari walifanikiwa kumkamata na kumtia ndani kusubiri uchunguzi zaidi.

Makabila: Aslya ndiye aliyebadili maisha yangu!

$
0
0

MKALI wa Muziki wa Singeli anayetamba na ngoma yake mpya ya Motoni Kumedamshi, Abdallah Ahmed ‘Dulla Makabila’ amesema moja kati ya vitu ambavyo Watanzania wanapaswa kujivunia ni pamoja na muziki wa Singeli.  Mbali na hilo, katika makala haya, Dullah amefunguka mambo mengi kuhusu maisha yake ya muziki:

MWANDISHI: Kwanza tupe historia yako fupi na jinsi ulivyoanza kuimba?

DULLA: Mimi ni Myao wa Tunduru, historia yangu kiufupi ni kwamba mimi nilianza kuigiza kwa miaka sita lakini sikupata nafasi ya kutoka na kuwa mkubwa kama nilivyo sasa, hivyo nikaacha kuigiza. Nilikutana na Mkubwa Fella na kujiunga na Kundi la Mkubwa na Wanawe, nikaanza kuimba Bongo Fleva lakini baadaye nilibadilika na kuanza kuimba Singeli.

Ngoma yangu ya kwanza ni Yanga japo haikujulikana kama ni yangu kutokana na Msaga Sumu kuuimba mara kwa mara na pia yeye kujulikana sana. Sikuwa na la kufanya kwa sababu sikuwa na pesa, hivyo niliamua kupotezea japo nilikuwa nikiumia kwa sababu nilikuwa nikisikia wimbo wangu ukiimbwa na mtu mwingine kwenye matamasha makubwa. Baada ya hapo niliendelea kutoa ngoma nyingine kama Makabila, Hujaulamba na nyingine nyingi ambazo zimenifikisha hapa mpaka leo.

MWANDISHI: Ni wimbo gani uliokufanya ukajulikana kuwa wewe ndiye Dulla Makabila?

DULLA: Wimbo ulionitoa ni wa Makabila ambao pia ndiyo uliosababisha mimi kuitwa Dulla Makabila kwani watu walianza kuniita hivyo baada ya mimi kuachia ngoma hiyo

MWANDISHI: Ni nani aliyekushawishi wewe kutoka kwenye Bongo Fleva na kuhamia kwenye Singeli?

DULLA: Aliyenishauri mimi kuimba Singeli ni Aslay, nakumbuka siku moja tukiwa Mkubwa na Wanawe jioni, tulikaa sehemu moja ambapo kulikuwa na mama aliyekuwa anauza uji tukawa tunakunywa uji ambapo kaka yangu Aslay aliniambia kuwa niimbe Singeli kwa sababu sitakuwa na nafasi kubwa kwenye Bongo Fleva kama kwenye Singeli. Ninamshukuru sana kwa ushauri alionipa kwa sababu mpaka leo nafanya vizuri kwenye Singeli na ninapata hela.
MWANDISHI: Ni ugumu gani unaoupata kwenye muziki wa Singeli?

DULLA: Kiukweli ugumu upo kwenye maneno kwa sababu waimbaji wengi wa Singeli tunatakiwa kutumia maneno ambayo mashabiki wakisikia tu wapige kelele na hicho ni kitu kigumu sana.

MWANDISHI: Ni nani huwa anakutungia nyimbo zako?

DULLA: Mimi sijawahi kutungiwa nyimbo, huwa naandika mwenyewe, naimba mwenyewe, mdundo natafuta mwenyewe,

yaani kila kitu nafanya mwenyewe.

MWANDISHI: Huwa unatumia studio gani kurekodi nyimbo zako?

DULLA: Sina studio maalum kwa ajili ya kurekodi nyimbo zangu, naendaga studio tofautitofauti kwa sababu naamini kuwa kuna wimbo nikirekodi kwenye studio fulani utatoka vizuri zaidi, hivyo huwa nabadilishabadilisha studio.

MWANDISHI: Vipi kuhusu menejimenti, una meneja au unajisimamia mwenyewe?

DULLA: Mameneja wangu kwa sasa ni Mkubwa Fella na Faridi na ndio ninaofanya nao kazi.

MWANDISHI: Kuna mabifu mengi sana yanatokea kwenye Singeli, shida ni nini haswa?

DULLA: Tatizo ni kwamba kila mtu anataka kuwa mkubwa kuliko mwenzake, hivyo tunajikuta tunapotezeana heshima na hii tofauti na Bongo Fleva ambako wenzetu wanaheshimiana yaani unakuta wanajua kuwa mmoja wao kawazidi kila kitu kuanzia pesa mpaka umaarufu lakini kuheshimiana kuko palepale.

MWANDISHI: Uko karibu sana na Kundi la Wasafi na hata safari zote za Tamasha la Wasafi mikoani na Dar umeshiriki, je una mpango wowote wa kufanya kolabo na Diamond au msanii mwingine yeyote kutoka Wasafi?

DULLA: Kolabo zipo lakini ziliingiliwa kati na Tamasha la Wasafi na kwa kuwa tumeshamaliza tamasha hilo, mipango yote ya kufanya kolabo itaendelea. Mashabiki wakae mkao wa kula.

MWANDISHI: Muziki wa Singeli kwa sasa unabamba sana na tunaona wasanii wengi wanahamia huko akiwemo Diamond ambaye aliachia wimbo wa singeli unaojulikana kama Moto, wewe binafsi umejipangaje kufanya mapinduzi ya Singeli?

DULLA: Singeli ina nafasi kubwa sana kwani ukiaangalia hata kwenye matamasha ya Serikali inapigwa, msanii wa Bongo Fleva anaweza kulipwa pesa nyingi huku msanii wa Singeli akalipwa kidogo lakini bado msanii wa Singeli akateka mashabiki kuliko wasanii wengine. Kikubwa ni umoja kwa wasanii wote wa Singeli na kujitambua kuwa sisi tuna thamani ili tuhakikishe tunafanya mziki wetu unaenda kwa sababu yapo mengi yanayofanya muziki wetu uyumbe, natamani ningekuwa na umoja na wenzangu ili tupate sapoti kutoka kwa Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe tuzungumze kwani sio vyombo vyote vya habari vinavyosapoti Singeli, ukizingatia Singeli ndiyo muziki wa Watanzania tunaojivunia kuwa nao.

MWANDISHI: Moja kati ya nyimbo zako, kuna wimbo unaitwa Dua na ndani ya wimbo huo kuna kipande unasema unamuombea dua Steve Nyerere azidi kuumbuka na ROMA hajakoma atekwe tena, ulikuwa na maana gani?

DULLA: Roma alikuwa ametekwa na baada ya kuachiliwa alitoa wimbo wenye mstari unaosema kuwa kutekanatekana ni mambo ya kishamba hivyo nikaona hajakoma nikaamua kumuombea dua atekwe tena. Kuhusu Steve Nyerere niliamua tu kuweka kipande hicho ili kunogesha wimbo japo hakupenda jambo hilo lakini tuliongea na baada ya kumuomba msamaha akanielewa yakaisha.

MWANDISHI: Uliwahi kuwachanganya Tiko na Sajenti kwenye mahusiano na mpaka leo wawili hao wana bifu, unalizungumziaje hili?

DULLA: Shida iko kwao wenyewe kwani walishindwa kujiheshimu, baada ya kupata mashabiki walianza kusumbua na kujiona wameshakuwa mastaa na hiyo inanigharimu mimi. Mimi mwanamke wangu napenda tuwe sawa, asiniletee ustaa na ni kweli kwa sasa siko nao wote.

MWANDISHI: Umesema kuwa umeachana nao wote, kwa sasa uko katika mahusiano na nani?

DULLA: Kwa sasa nina mpenzi wangu mwenye asili ya Ugiriki na nimeshamtambulisha kwa wazazi wangu ambao wamempokea vizuri, kwa sasa tunaishi wote nyumbani.

MWANDISHI: Mbali na muziki, unajishughulisha na nini?

DULLA: Nina biashara zangu ndogondogo zinazoniweka mjini kwa sababu kwa maisha ya sasa hivi huwezi kutegemea chanzo kimoja cha pesa.

MWANDISHI: Neno la mwisho kwa mashabiki wako…

DULLA: Nawapenda sana na watembelee ukurasa wangu wa You Tube ili wazidi kuziona kazi zangu haswa wimbo mpya wa Motoni Kumedamshi na video nitawadondoshea hivi karibuni.

MWANDISHI: Asante sana kwa ushirikiano wako.

DULLA: Asante pia!

Kilimanjaro Queens Yaichapa Zanzibar Bila Huruma

$
0
0

 Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) imehitimisha hatua ya makundi kwa kutoa kipigo cha nguvu cha bao 7-0 kwa ndugu zao Zanzibar.

Japan: Wanawake Walazimika Kuvaa Viatu Virefu

$
0
0

Katika utafiti huko Japan, moja katika kila kampuni 10 nchini imeripoti kuwa wanawake wanalazimishwa kuvaa viatu virefu.

Asilimia 12 ya watu waliochunguzwa katika uchunguzi uliofanywa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyabiashara Japan imegundulika kuwa taratibu za mavazi sio sawa.

Asilimia 57 ya waliohojiwa walisema waliwekewa wazi kuwa mavazi yanapaswa kuwa hivyo, wakati asilimia 8 walisema kuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya urembo.

Kulingana na utafiti huo, imeoneana kuwa wanawake wanalazimika kuvaa viatu virefu katika moja ya kampuni 10 nchini humo.

Utafiti, asilimia 13 ya wanawake katika nafasi za juu nchini Japan walisisitizwa kuvaa viatu virefu. Utafiti huo pia umeonyesha kwamba asilimia 11 ya wafanyikazi wa kiume wanapaswa kuvaa suti.

"Kuweka sheria tofauti kwa wanaume na wanawake husababisha ubaguzi wa kijinsia," afisa mmoja kutoka kwa shirika hilo ameliambia gazeti la Japan Times.

Tangu Februari mwaka huu, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yamekuwa yakipanga kampeni kuhusu mipangilio ya mavazi ya wanawake nchini. Katika muktadha huu, zaidi ya watu elfu 31 walishiriki katika kampeni ya utiaji saini kuondoa sheria hiyo.

Wanawake wengine wamepingana na ukweli kwamba waajiri wengine wanalazimisha wanawake kuvaa viatu vyenye visigino vya juu,.

Waziri wa Afya na Kazi wa Japani, Takumi Nemoto, amesema kwamba ni sahihi na ni lazima kwa wanawake kuvaa viatu vyenye visigino vya juu.

Habari kwamba kampuni zingine nchini Japani huzuia wafanyikazi wa kike kutovaa miwani za macho pia ni suala lililosababisha mzozo nchini.

Profesa Aliyeandika Kitabu cha Uhujumu Uchumi Ashtakiwa Kwa Uhujumu Uchumi

$
0
0

Profesa wa Chuo kikuu ambaye ameandika kitabu kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya na jinsi uhalifu unavyopangwa ameshtakiwa na mamlaka za Marekani kwa kosa la uhujumu uchumi wa kiasi cha dola milioni 2.5 kutoka kwenye akaunti ya Venezuela.

Mwendesha mashtaka anadai kuwa Bruce Bagley alipokea fedha kutoka akaunti ya benki ya Switzerland na Umoja wa Falme za Kiarabu na kuhifadhi kiasi cha dola 250,000 kwa ajili yake mwenyewe .

Miaka minne iliyopita, Profesa huyo aliandika kitabu kuhusu usafirishaji wa madawa ya kulevya, jinsi uhalifu unavyopangwa na vurugu zilizopo nchini Marekani, ambacho sasa kinasemwa kuwa Uhujumu uchumi ni shughuli inayokua .

Akizungumza kupitia chombo cha habari cha CBS News, profesa wa masomo ya kimataifa katika chuo kikuu cha Miami amekanusha madai hayo dhidi yake na kusema: "Ninajihisi vizuri tu , sina hatia .Hivyo ndivyo ninavyojisikia. Wananishutumu uongo tu.''

Mamlaka za New York zimedai kuwa Bagley alifungua akaunti katika benki ya Florida kwa ajili ya kampuni ambayo ilimtaja yeye na mke wake kuwa afisa na mkurugenzi.

Mwezi Novemba 2017, akaunti hiyo ilipokea ufadhili kutoka nchi za falme za kiarabu kwa ajili ya kampuni ya chakula inayoendeshwa na raia wa Colombia.

Raia wa Colombia ambaye alikuwa na akaunti ughaibuni hajabainisha ufadhili ulitumikaje vibaya huko Venezuela.

Kitabu cha Bagley kinaelezea namna shughuli za uhujumu uchumi zinavyofuata mlolongo mkubwa.

Mwendesha mashtaka anadai kuwa akaunti hizo zilitumika kupokea au kutoa rushwa na kutumika kwa shughuli za ufisadi nchini Venezuela.

Kesi hii ni sehemu ya jitihada ambazo Marekani wameziweka kutekeleza sheria za kuwakamata wahujumu uchumi wanaovuruga mfumo wa uchumi wa Marekani kutokana na utajiri wa mafuta nchini Venezuela.

Bwana Bagley anashtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi, utakatishaji fedha kwa kuwa na akaunti mbili za fedha na kila kosa atahukumiwa miaka 20 gerezani.

Baada ya kufika mahakamani huko Miami, aliachiwa huru kwa dhamana ya kiasi cha dola za Marekani 300,000.

Pamoja na taaluma yake, profesa alikuwa na ushahidi mahakamani dhidi ya kesi yake kwa kuwa na mashahidi wenye taalumu walizungumza kumtetea.

Kutokana na kesi inayomkabili bwana Bagley, mkurugenzi msaidizi wa shirika la kijasusi FBI William Sweeney alisema: "Wahalifu huwa wanatumia kila mbinu za uhujumu uchumi katika uhalifu wao ili waweze kufanikiwa nia yao na kupata mwanya wa kuficha fedha zao."

Wakili wa profesa huyo Daniel Forman aliliambia gazeti la Miami Herald kuwa amejipanga vizuri kutetea kesi hiyo na kushinda .

Chuo kikuu cha Miami kinasema kuwa Bagley yuko likizo na kueleza kuwa kesi inayomkabili ni mambo yake binafsi.

Wagombea Wote wa Upinzani Waliopitishwa Kugombea Nachingwea wajitoa

$
0
0

Na Ahmad Mmow-Nachingwea

Wanachama wa vyama vya upinzani ambao waliteuliwa kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wilayani Nachingwea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 wamejitoa kushiriki katika uchaguzi huo.

Hayo yamebainishwa na msimamizi wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea, Nnunduma Ali alipozungumza na Muungwana Blog, leo mjini Nachingwea.

Nnunduma alisema wagombea wa nafasi  mbalimbali walioteuliwa kutoka vyama vya CHADEMA na CUF wamejitoa wenyewe kwa kuandika barua, pia ngazi za vyama zilizowadhamini viliandika barua za kujitoa.

 ''Hadi kufikia tarehe 16.11.2016, jioni wagombea wote waliopitishwa kugombea nafasi mbalimbali  kupitia vyama vya CUF na CHADEMA walikuwa wamejitoa. Sisi kama wilaya tunaandaa fomu za matokeo zitakazotumika kuwatangaza viongozi hao, tutabandika kwenye mbao za matangazo siku ya tarehe 24.11.2019,'' alisema Nnunduma.

Msimamizi huyo wa uchaguzi wa wilaya ya Nachingwea alisema awali Chama cha Mapinduzi asilimia 98 ya wanachama wake waligombea nafasi mbalimbali walipita bila kupingwa, kwahiyo baada ya wagombea wa vyama hivyo kujitoa ni dhahiri kimeshinda kwa asilimia mia moja.

Nnunduma aliitaja idadi ya viti vilivyotarajiwa kugombewa ni vijiji 127, vitongoji 525, viti maalumu vyote 997 na viti mchanganyiko 1556. Wakati vyama vilivyosimamisha wagombea vilikuwa CUF, CHADEMA na CCM. Akivitaja vyama ambavyo wagombea wake walichukua fomu na kurejesha ni CUF, CHADEMA, ADC na CCM.

Bastola ya Ushahidi Mahakamani Yamuua Mwendesha Mashtaka

$
0
0

Gumzo linaloendelea hivi sasa ni kuhusu kifo cha Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Afrika Kusini Addelaid Ferreira Watt (51).

Kama inavyoelezwa kwamba kifo hakina taarifa, basi kwa mujibu wa mitandao mbalimbali Afrika Kusini imeripoti kuhusu kifo cha Ferreira Watt aliefariki Duniani kwa kupigwa risasi baada ya bastola ya ushahidi kudondoka katika meza ya Mahakama.

Kwa mujibu wa mitandao huko Afrika Kusini imebainisha kuwa tukio hilo limetokea Novemba 18, 2019 katika Mahakama ya Mkoa Ixopo, Kwazulu-Natal.

Tukio hilo la kustaajabisha limetokea wakati Mwendesha Mashitaka huyo akisimamia kesi ya wizi wa kutumia silaha.

Mkurugenzi wa Mashitaka nchini humo, Elaine Zungu amesema kuwa Ferreira Watt alipigwa risasi katika nyonga akiwa ndani ya chumba cha mahakama akiendesha kesi ya Wizi wa kutumia silaha.

Ameeleza kuwa bastola ilidondoka yenyewe kutoka katika Meza ya mahakama kisha ikafyatuka na risasi zikatoka na kumjeruhi Mwendesha Mashitaka huyo Ferreira Watt katika nyonga.

Inaelezwa kuwa Bastola hiyo ilikuwa ni kielelezo cha ushahidi katika kesi ya Wizi wa Unyanganyi kwa kutumia silaha.

Baada ya kutokea kwa tukio hilo, Ferreira Watt alichukuliwa na kukimbizwa Hospitali ambapo madaktari wakathibitisha kwamba amejeruhiwa katika Nyonga ya Upande wa Kushoto.

Hata hivyo baadaye, ikatolewa taarifa nyingine siku hiyo ya Jumatatu, Novemba 18, 2019 kwamba mwendesha mashitaka huyo amefariki Dunia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi November 21

$
0
0













Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi November 21

Wakati ambapo unapitia MAGUMU kwenye maisha ni wakati MUHIMU Sana Kwako...

$
0
0
Wakati ambapo unapitia MAGUMU kwenye maisha ni wakati MUHIMU sana,sio kwa sababu ya USHINDI utakaoupata bali kwa sababu ya STAMINA unayojenga itakayokusaidia mbele ya safari.
.
Arnold Schwarzenegger aliwahi kusema “Nguvu haiji pale unaposhinda.Changamoto zinazokukabili zinakuimarisha.Unapopitia magumu na kuamua KUTOKATA TAMAA,hapo hasa ndio unajenga NGUVU za kufanikiwa.(Strength doesn’t come from winning.Your struggles develop your strengths.When you go through hardships and decide not to surrender,that is strength).

Jirani Athibitisha Kusah Kumshambulia Ruby Hadi Chumba Kutapakaa Damu "Kipigo Alikipata"

$
0
0
Jirani athibitisha Kusah kumshambulia Ruby hadi chumba kutapakaa damu, watupiwa vyombo nje baada ya Kusah kushindwa kulipa kodi !

“Ruby na Kusah wamekuwa ni watu wa kugombana kila kukicha kiasi ambacho watu walikuwa wakigombelezea, maana huyo mwanaume alikuwa akitoa kipigo kikali bila kujua kuwa wana mtoto mmoja,” jirani huyo ameliambia Ijumaa Wikienda -

Chanzo hicho kiliendelea kutiririka kuwa, siku ya tukio, Ruby alikuwa amelala ambapo Kusah aliingia na kuchukua simu ya msanii huyo ndipo akakutana na meseji ya msanii Jux. “Alichokifanya ni kumpiga ngumi ya shingo, kisha kumshushia kipigo kikali kilichomfanya Rubby akimbilie kwa rafiki yake akiwa pekupeku huku chumba chote kikitapakaa damu.

“Kama ni kipigo tu, basi Ruby amekipata. Lakini hiki cha hivi karibuni kilikuwa ni hatari, kibaya zaidi, wakati wanagombana walikuwa wanadaiwa kodi ya shilingi laki saba, hivyo baba mwenye nyumba akawatupia virago vyao nje,” kilisema chanzo hicho

Ruby alipotafutwa na Ijumaa wikienda amesema

“Nimejiuliza maswali mengi sana kwa nini nikubali kipigo na mimi bado ni mdogo? Nimeamua kuachana naye na simtaki kabisa. Ni kweli hivyo vitu vilitolewa nje kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha yote hayo, kwani ndiye aliyetakiwa kulipa, matokeo yake nimeambulia aibu na fedheha,” alisema Ruby huku akiomba wanasheria kuingilia kati kusaidia wanawake wanaopigwa na kunyanyaswa na wanaume. -

Kwa mujibu wa Ruby, aliamua kumsaidia baba mtoto wake huyo hasa kwenye eneo la kutoboa kimuziki kwa kumuunganisha na mastaa wakubwa kama Diamond na Jux, lakini mwisho wa siku jamaa huyo aliishia kumtusi na kumwambia kuwa anatembea nao, jambo ambalo siyo kweli kwani lengo lake lilikuwa kumsaidia mzazi mwenzie huyo nae afanikiwe Kwenye muziki

Baada ya Wazazi Wangu Kufariki Boyfriend Analazimisha Tufange Ndoa Harahara Bila ya Harusi...Naombeni Ushauri

$
0
0
ANAOMBA USHAURI : Mimi ni binti wa miaka 29, sijaolewa lakini nina mchumba wangu ambaye tumekaa kwenye mahusiano naye kwa miaka 7 sasa, yeye anafanya kazi ni mwanajeshi lakini ni wale watu ambao hawahudumii kabisa, mimi ni mwalimu na kipato changu ni kidogo kuliko yeye. Amekua ni mtu wa kunilalamikia kila siku, akija akinililia shida nikikataa kumsaidia basi hununa na kuacha kupokea simu zangu hata kwa wiki nzima, mimi hujitrahidi kumtafutia alichoniomba na kumpa, nimekua nikifanya hivyo kwa muda mrefu kila siku nikijariubu kumridhisha yeye tu.

Nimeshaizoea hiyo hali kwani nimeomba Mungu ataabdilika habaidliki. Sababu ya kuja kwenu nikuwa, aktika kipindi chote hicho sual la ndoa limekua gumu sana kwake, kila nikimuambia amekua mtu wa kubaidlika badilika, mara nne alishaniambia kuwa anatuma watu kwetu lakini hatumi, anasingizia sababu nyingine mara kazini hivi, mara nilikua na kile na mambo mengi, nmimekua nikimfumania na wanawake tofauti tofauti lakini namsamehe ingawa hata kuomba msamaha haombi, ananiambia kuwa yeye ni mwanaume hawezi kuwa na mwanamke mmoja.

Sababu ya kuja kwako nikuwa, wmezi uliopita nilifiwa na Mama yangu, kwetu tuko wawili na baada ya Baba kufariki dunia basi Mama ndiyo alikua anasimamia kila kitu. hata arubaini haijaisha mchumba wangu katuma watu eti anataka tufunge ndoa ya harakaharaka hata bila sherehe, mimi nimeshangaa sana kwani bado niko kwenye machungua nasema anataka kufunga ndoa na mimi ili kunifariji katika kipindi hiki kigumu. Nilikubali na kutaka kuongea na baadhi ya ndugu zangu kuwaambia.

Lakini kabla ya kufanya hivyo kuna mwanamke wake mmoja ambaye mara nyingi huwa tunagombana akanitumia meseji za matusi, akiniambia naringia kuolewa lakini sipendwi bali mwanaume anataka mali za urithi tu anampenda yeye. Tulitukanana sana lakini baadaye nimefikiria, kama tukigawana mali ni mimi na mdogo wangu nusu kwa nusu, Mama kaacha nyumba nne magari na vitu vingine vingi, je hivi ni kwelia anvitaka hivyo vitu au ananipenda, nimechanganyikiwa sijui nifenye nini,nawaza kumuuliza lakini naogopa kumuudhi akaacha kunioa, naomba ushauri wenu jamani.

Mbwana Samatta Afunguka Malalamiko ya Watu Kuhusu Kuonyesha Kiwango Kidogo Akiwa Timu ya Taifa

$
0
0

Mbwana Samatta akiri kuzipokea comments za Watanzania kuhusu kucheza chini ya Kiwango na aahidi kuzifanyia kazi ili kuhakikisha Anakuwa bora


Tunda Akinukisha Amwagia Povu Zito Casto.,.... Aanika meseji Zake Anazombembeleza Warudiane

$
0
0

Muuza nyago wa bongo fleva, Tunda Sebastian amwaga mapovu kwenye kurasa yake ya instagram, hii ni baada ya mpenzi wake wa zamani kumuwashia moto aachae kumchafua na kutumia jina lake kutafuta kiki.



Tunda ameshindwa kukaa kimya na kuamua kutoa siri zote za sms alizokuwa akimtumia na yeye kutomjibu.




“Mimi sio muongeaji na huwa siwezi uswahili kabisa lakini ukiona mpaka nachafua page yangu nakuweka ujue kuna vitu umeshindwa kujiheshimu!.



“Jamani huyu kaka sijawahi kuwa na tatizo nae, lakini kila kutwa naletewa maneno anayoyaongea kuhusu mimi shit wakati kwenye simu yangu halali siku ipite bila hajanipigia na kuniandikia ma-message, kutwa kupigia watu wangu wa karibu waongee na mimi.



“Una hali mbaya unataka kufa halafu ukiwa na wanao ofisini huko unaniongelea ujinga mwanamke wa starehe siwezi, sijui kuolewa, yani mambo ya kijinga!



“Yani mtu niliekutengeneza mwenyewe ujulikane leo hii nikuongelee kujibust🤣 unaakili wewe? Sema nakubust navoongea ivi sema sijali ndo nishakuambia sitaki simu zako sitaki message tulia kwenye mahusiano yako sahau kuhusu mimi mxieeew

Mwanamke Amchinja Mwanae Mwenye Ulemavu wa Viungona Kumla Nyama

$
0
0

MWANAMKE mmoja anaejulikana kwa jina la Christina Mlelwa (38) mkazi wa Kijiji cha Mavanga Kata ya Mavanga, Kitongoji Cha Mji Mwema, wilayani Ludewa, Mkoa wa Njombe anashikilikiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumchinja mwanae Joseph Gumbilo (4) mwenye ulemavu wa viungo na kumla nyama.



Awali akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Andrew Tsere amesema baada ya kufikishiwa taarifa za tukio hilo alilazimika kufika eneo la tukio na kumhoji mtuhumiwa ambaye alikiri kutekeleza mauaji ya mwanae na kisha kumkata viongo vyake na kumla huku viungo vingine kuvitupa porini na chooni.



Tukio hilo linaleta mshituko kwa kamati ya ulinzi na usalama mkoa na kumsukuma Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Olesendeka kufika katika kijiji hicho kuzungumza na wananchi na kisha kutoa agizo kwa wakuu wote wa wilaya za mkoa huo kukamata kijiji kizima na kuweka lockup endapo watagoma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuhusu matukio ya mauaji.



Katika hatua nyingine, Olesendeka ameliagiza Jeshi la Polisi kusaka ukweli wa tukio hilo haraka na wahusika kufikishwa mahakamani kama ambavyo katiba inalinda haki ya kuishi ya kila binadamu bila kujali ulemavu wake.



Katika mahojiano ya awali na Jeshi la Polisi, mama huyo ambaye anaonekana kuwa na matatizo ya akili amekiri kuua na kukata vipande vipande na kumla nyama huku masalia mengine ikiwemo fuvu la kichwa na miguu akiyatupa porini hatua ambayo ililazimu kamati ya ulinzi kuvamia pori na kukuta vitu hivyo.



Lakini Mume wake, Daniel Gumbilo anasema mke wake alisha wahi kufanya jaribio kama hilo miaka ya nyuma kwa mototo wao mwingine anaesoma ambapo majirani walinusuru maisha ya mototo wao.



Nae kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe, Hamisi Issa anasema jeshi linaendelea kuchunguza kwa kina zaidi kuhusiana na tukio hilo ili wahusika wapewe haki yao ya hukumu ya uovu wao.



Kwa upande wa mtendaji wa Kijiji cha Mavanga Fadhiri Tajiri alisema ni kweli tukio hilo limetokea na kwamba taarifa zaidi anasubiri muongozo kutoka kwa viongozi wake.



“Ni kweli Hilo tukio lipo lakini viongozi wangu wamesema wapo njiani wanakuja nasubiri muongozo wa kutoka kwao”alisema Tajiri

Boss Mkuu Simba Atoa Tamko Juu ya Patrick Aussumes

$
0
0
Patrick Aussems, kocha mkuu wa Simba ambaye kwa sasa yupo nchini Ubelgiji ametangaza hali ya hatari kwa wapinzani wa Simba ambao atakutana nao kwenye mchezo wao unaofuata wa ligi.

Aussems aliondoka nchini Tanzania Jumatatu ya wiki hii kimyakimya na kurejea nyumbani kwao Ubelgiji kwa kile alichokieleza kuwa ni kutokana na sababu zake binafsi na aliahidi kurejea jana akiwa na hasira za kupata pointi tatu za Ruvu Shooting iliyo nafasi ya nane na ina pointi 15. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Aussems amesema:”

"Niliondoka kwa sababu zangu binafsi mwenyewe kwa siku mbili nitarejea kesho (jana), kwa ajili ya maandalizi  ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting nazihitaji pointi tatu.

” Championi Jumatano, lilizungumza na Meneja wa  Simba, Patrick Rweyemamu ambaye alisema kuwa hawezi kuzungumzia suala la kocha kwa kuwa bosi wao ameshazungumza.

“Bosi amesema kuwa hajui alipo kocha sasa mimi nitazungumza nini hapo, zaidi ya kufuata kile ambacho amesema CEO? (Mkurugenzi Mtendaji) basi kwa kuwa mwajiri hajui alipo mfanyakazi wake hakuna nitakachoweza kuzungumza,” alisema Rweyemamu.

Simba inatarajiwa kushuka Uwanja wa Uhuru Novemba 24 kumenyana na Ruvu Shooting mchezo wao wa 10 kwenye ligi ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 9 na imejikusanyia pointi 22, imepoteza mchezo mmoja mbele ya Mwadui FC na imeshinda mechi saba na sare moja dhidi ya Prisons
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images