Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Habari za Udaku, Siasa, Mapenzi na Michezo

(Page 1) | 2 | 3 | .... | 2994 | newer

  0 0

  Mbunge Wa Kawe “Kwa Wajanja” Ammwagia Sifa Msanii Diamond Platinumz Kwa Kazi Zake …
  Mbunge wa kuchaguliwa jimbo la Kawe “Kwa Wajanja” katika bunge la Tanzania kupitia chama pinzani cha CHADEMA Halima James Mdee, leo amemmwagia sifa msanii mahiri wa
  Bongo Flava nchini Tanzania, Diamond Platinumz kutokana na uwezo anaouonyesha katika sanaa ya muziki nchini Tanzania.
  Kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter mheshimiwa Halima James Mdee amepost tweet za kumsifia Diamond kwa kusema, “Huyu dogo DIAMOND…..Mungu ambariki….ni mtoto wa kitaa…aliyeonyesha kwamba inawezekana..ktk sanaa yetu , kutoka 0-100%. BE BLESSED!”  0 0

  Taarifa za sababu kubwa zilizopelekea Wema Sepetu kumtimulia mbali aliyekuwa director wake aliyefahamika kwa jina moja la Chid kuwa ni ufuska uliokubuhu kwa director wake huyo huku akitumia magari yake kama gest ya kumalizia haja zake.

  Website hii inakupa mchongo mzima Habari za uhakika zilizotua mezani kwenye meza yetu ya habari zilisema kuwa Wema aliamua kuchukua maamuzi hayo magumu ili kunusuru kashfa kubwa ambayo ingeweza kuikumba kampuni yake"

   Kwa kweli Wema Sepetu alikuwa
  anampenda sana Chid kutokana na ubunifu wake kazini na alimpa uhuru wa kufanya kila kitu ikiwemo kumuachia magari ambayo yeye alikuwa kama kiongozi hivyo alikuwa na uhuru nayo sana na alikwenda kila mahali "

   Kilisema chanzo hicho ambacho ni ndugu na Wema aidha habari zaidi ziliendelea kusema baada ya kupata taarifa hizo aliamua kumtimua Chid kwenye kampuni yake ili kulinda heshima ya kampuni hiyo ambapo Chid na vijana walikuwa wakitumia gari hiyo kung'olea watoto wakali"

   Unajuwa Wema ana mashabiki sana hata ile gari wakati mwingine alikuwa anavunja hata sheria za barabarani bila kufanywa chochote hii ilitokana na upendo wa mashabiki kwa Wema na wasichana wengi walikuwa wakiiona ile gari basi wanaingia wenyewe kwenye gari wakidhani ndani yuko Wema hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Chid na wenzake kuwamaliza wasichana hao"

   Alisema dada huyo Aidha baada ya taarifa hizo tulivuta waya kwa kumcheki hewani Chid na Wema ili kuthibitisha madai hayo ama kuna jingine lililopelekea kutimuana kwa bahati mbaya watu hao hawakupatikana kuzungumzia hilo hadi habari hii inaruka hewani:
  Source:XDEEJAYZ

  0 0

  MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam jana amefariki dunia jana asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.

  Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu waliofariki katika tukio hilo kuwa watatu hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred Newa Mwanafunzi wa masuala ya
  Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar es Salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na Kablu ya wazee huku maziko

  0 0

  Mwanamziki mkongwe nchini Nguza Viking aka Babu Seya na mwanaye Papii Kocha, wataendelea na kifungo cha maisha jela baada ya mahakama ya rufani nchini kuitupilia mbali rufaa yao iliyosikilizwa leo

  Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela mwaka 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar ambapo wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini wakagonga mwamba. Hukumu hii ya rufaa ndiyo ya mwisho kusikilizwa.

  0 0

  MREMBO aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus Season 2, Jacqueline Dunstan ‘Jack wa Maisha Plus’ amezua jambo katika mtandao baada ya kutundika picha akiwa anabusiana na mwanamke mwenzake.

  Jack ambaye kwa sasa yupo nchini Dubai, aliweka picha hiyo katika mtandao wa Instagram hali ambayo iliwashangaza wadau wengi waliopo kwenye mtandao huo ambapo walimchana kuwa aache vitendo vya kisagaji lakini mwenyewe hakujibu.

  Jack baada ya kuweka picha hiyo aliandika maneno haya; ‘mwaaah’ ndipo wadau walipoanza kumshambulia na kumtaka aondoe picha hiyo chafu.

  0 0

  Mwanamziki aliyepata kutamba na Bendi ya FM Academia ya jijini Dar es Salaam, Rapa, Haristot Shungu ameuawa nchini China huku kifo chake kikitawaliwa na utata mkubwa. 

  Kwa mujibu wa chanzo  makini kilichopo nchini China, rapa huyo alikamatwa uwanja wa ndege baada ya kugundulika kuwa amebeba madawa ya kulevya akiwa ameambatana na rapa mwingine wa Bendi ya Akudo Impact, Kanal Top na wote wawili kuhifadhiwa mahabusu.

  “Tulijua kama Haristot alikamatwa pamoja na Kanal Top lakini ghafla juzi (Ijumaa) tukaambiwa kuwa amefariki dunia, hatujui kifo chake kimesababishwa na nini lakini mwili wake unaonekana kama vile aliungua na moto au mtu aliyechomwa sindano ya sumu,” kimesema chanzo hicho.

  Baada ya kupata taarifa hizo mwandishi wetu aliwasiliana  na Kiongozi wa FM Academia, Nyoshi El Saadat na kumuuliza kama alikuwa na taarifa zaidi za Haristot.

  Nyoshi alikiri kuwa marehemu alikuwa mwanamuziki wao na kudai kwamba kifo chake kimetawaliwa na utata mkubwa.

  “Haristot alikuwa mwanamuziki wetu, mara ya mwisho aliaga kuwa anakwenda Ulaya kwa mchumba wake, nimeshangaa kusikia ameuawa nchini China kiukweli hakuna anayejua ukweli wa kifo chake,” alisema Nyoshi.

  Credit: GPL

  0 0

  Na Waandishi Wetu
  Global Publishers Ltd ilipoamua kufuatilia sakata la denti anayedai kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Juma Athuman Kapuya, lilijua yapo mengi yatajitokeza, Amani lina jipya lingine.
  Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano
                                         Mbunge wa Urambo Magharibi (CCM), Profesa Juma Athuman Kapuya.
  Huu ni muendelezo wa utekelezaji wa ahadi ya Global, iliyotoa Jumamosi iliyopita kwenye Gazeti la Risasi kwamba waandishi wake watafuatilia kisha magazeti yake yataandika kila kitu. Katika Ijumaa Wikienda, Kapuya alifunguka, Uwazi liliandika utapeli mzima wa denti husika.
  Amani linalo jipya la denti huyo tapeli, Halima Hamad au Felista, aliyeamua kufunguka mbele ya waandishi wetu kwamba ni kweli yeye ni mama wa mtoto mmoja.
  Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano.
  Kuhusu kubakwa, Felista ambaye pia hutumia majina ya Leylat au Leila, alisema: “Kapuya hakunibaka ila nimezaa naye mtoto mmoja.”
                                                   Denti akiwa busy na simu yake wakati wa mahojiano na GPL..
  ILIKUWAJE AKAFUNGUKA?
  Timu ya waandishi wa habari wa Global Publishers hutekeleza majukumu yake kisayansi, baada ya kurukaruka sana, Felista akidai hahusiki na skandali hiyo na kwamba yeye ni shahidi tu wa mtu anayeitwa Leylat, hatimaye alibanwa kwa maswali magumu, akajikuta akisema ambayo hakuyapanga.
  MWANDISHI:  Hizi namba 0753 7…7…28 na 0713 7...20…0 (tarakimu mbilimbili zimefichwa), ni za nani?
  FELISTA: Ni namba zangu.
  MWANDISHI: Hizi namba ndizo ambazo Kapuya ametutumia  kwamba ndiyo za mtu ambaye huwasiliana naye na humtumia pesa, na ndiye anayejidai ni denti aliyebakwa na kuambukizwa naye Ukimwi.
  FELISTA: Siyo kweli, huyo Kapuya anatafuta njia za kujinasua kwenye hili tatizo lake. Anajua mimi namjua Leylat ambaye ndiye denti aliyebakwa.
  MWANDISHI: Wewe unaitwa nani?
  FELISTA: Naitwa Felista.
  MWANDISHI: Unamjua Halima Hamad?
  FELISTA: Halima Hamad simjui.
  MWANDISHI: Kapuya kasema denti anayedai kubakwa anaitwa Halima Hamad na ndiye mwenye hizo namba ambazo wewe unakiri ni zako.
  FELISTA: Nimesema simjui Halima, mimi naitwa Felista. Aliyebakwa ni Leylat, siyo mimi.
                                                                Denti akiwasikiliza wana GPL wakati wa mahojiano

  AKUMBUSHWA ALIYOSAHAU
  Miaka ya nyuma Felista akitumia mwavuli wa uyatima, aliwahi kuomba hifadhi kwa mmoja wa waandishi wetu wa kike, aliyeishi naye kwa muda mrefu kidogo nyumbani kwake kabla ya kumgundua kwamba ni tapeli, hivyo kuamua kuachana naye.
  MWANDISHI: Wewe Felista umesahau kwamba umeshawahi kukaa nyumbani kwangu na kipindi hicho chote, ulikuwa ukiniletea ripoti za shule zenye jina la Halima Humudy. Vilevile ulishawahi kutolewa kwenye gazeti moja la kila siku (halizalishwi na Global), ukiomba msaada kwamba wewe ni yatima, jina ulilotumia ni hilohilo la Halima Humudy.
  Hizohizo namba zako, usajili wake wa laini na katika Tigopesa zimesajiliwa kwa jina la Halima Hamad. Haya kataa mbele ya macho yangu!
  FELISTA: …. (kimya).
  MWANDISHI: Wewe siyo Halima, sema nikusikie.
  FELISTA: Ni kweli, Halima Hamad ni mimi, ila hilo jina silitumii sana.
  MWANDISHI: Haya sasa, baada ya kukiri Halima Hamad ni wewe, unaweza kutuambia ukweli kuwa wewe ndiye huyo Leylat au Leila unayemtaja.
  FELISTA: (Kwa sauti ya chini iliyopoteza ujasiri), ni kweli mimi ndiye mhusika.
  MWANDISHI: Sasa kwa nini ulikuwa unakataa?
  FELISTA: Nilikuwa sipendi ninyi Global mjue.
  MWANDISHI: Haya tuambie ukweli sasa kuhusu wewe na Kapuya.
  FELISTA: Nimezaa naye mtoto mmoja.
  MWANDISHI: Mbona unatubabaisha? Mara alikubaka, mara umezaa naye mtoto mmoja, ukweli ni upi?
  FELISTA: Ukweli ni kwamba yeye ndiye baba wa mtoto wangu.
  MWANDISHI: Wewe hujazaa na Kapuya, huu nao ni utapeli mwingine.
  FELISTA: Kama hamtaki basi.
  MWANDISHI: Kama ni kweli yule ni mzazi mwenzako, mbona unaamua kumchafua na unataka kumharibia maisha yake?
  FELISTA: Amekataa kunihudumia ndiyo maana namchafua.
  MWANDISHI: Unafikiri hii vita mwisho wake ni nini?
  FELISTA: Atakapoanza tena kunihudumia.
  MWANDISHI: Haya turudi kwenye pointi ya Ukimwi, kwa nini unamshushia madai mazito kiasi hicho?
  FELISTA: Ni kweli nina Ukimwi.
  MWANDISHI: Na mtoto wako naye ni mzima?
  FELISTA: Mtoto naye ni mgonjwa.
  MWANDISHI: Unatumia dawa?
  FELISTA: Bado sijaanza kutumia dawa, CD4 zangu bado zipo vizuri.
  MWANDISHI: Mbona ulisema mwanzoni kwamba unatumia dawa?
  FELISTA: Ni kweli natumia dawa.
  MWANDISHI: Mbona unatuchanganya? Mara hutumii dawa, mara unatumia dawa, sasa hivi umesema CD4 zako zipo vizuri.
  FELISTA: Nimekwambia natumia dawa. Hata kama CD4 zangu zipo vizuri, natumia dawa hivyohivyo.
  MWANDISHI:  Katika maisha yako yote umewahi kupata matatizo ya akili? Maana naona kama haupo sawa.
  FELISTA: Mimi ni mzima kabisa. Mtaniona kama ni mzima siku nitakaposimama na Kapuya mahakamani.
  MWANDISHI: Wewe Felista umewahi kudanganya unasoma Turiani Sekondari, Mugabe Sekondari na Jangwani Sekondari kumbe ni uongo mtupu.
  FELISTA: Nimesoma Turiani tu, sijawahi kusoma Mugabe wala Jangwani.
  MWANDISHI: Nimeshawahi kukuona umevaa sare za Jangwani, leo unabisha? Na uliniambia unasoma huko.
  FELISTA: Siyo kweli.
  MWANDISHI: Kwa nini uliwatapeli Dk. Kimei na Mama Salma Kikwete?
  FELISTA: Kuhusu Kimei ni uongo, Mama Salma ni watu walitaka kuniharibia, nikapelekwa Segerea lakini nilitoka.
  MWANDISHI: Ilikuwaje ukamtapeli Mama Salma kuwa wewe ni yatima?
  FELISTA: Nilitaka nipate nafasi ya kusoma Mkuranga, sasa ili nipate nafasi kule ilibidi nionekane nasoma Jangwani, kwa hiyo nilitengeneza nyaraka zinazoonesha nasoma Jangwani ndiyo baadaye ikaonekana nimefanya utapeli.
  MWANDISHI: Umeona sasa? Mwanzoni ulikataa kuhusu kujidai unasoma Jangwani, sasa hivi unakiri. Haya sasa twende tukapime Ukimwi.
  FELISTA: Sipimi.
  MWANDISHI: Sisi tunaamini hauna Ukimwi. Hata mwanzoni ulishatuthibitishia kuwa ulishapima na upo salama. Kama una uhakika wewe ni mwathirika basi twende tukapime.
  FELISTA: Sipimi nimesema.

  NI SKANDALI LA VIGOGO
  Katika mahojiano hayo, Amani limeweza kubaini kuwa wapo wanasiasa kadhaa ambao wapo nyuma ya Felista na ndiyo wanaompa kampani kwenye harakati zake za kumchafua Kapuya.
  Mmoja wa wabunge wa Mkoa wa Tabora (CCM), sauti yake imenaswa mara mbili kwenye simu ya Felista, ya kwanza akimuelekeza binti huyo: “Njoo Dodoma, nitakuitia waandishi wa habari, ufanye mkutano nao uwamwagie kila kitu.”
  Sauti nyingine ya mbunge huyo, inasikika ikihoji: “Nimesikia Kapuya anatangaza wewe una watoto wawili, ni kweli?” Felista anasikika akipinga na kusema hana mtoto hata mmoja.
  Wapo wanasiasa wengine ambao wamebainika kumuunga mkono Felista, hivyo kuzidi kulifanya ‘saga’ hilo lionekane la kisiasa zaidi.

  ENDELEA KUKAA CHONJO
  Magazeti ya Global Publishers, bado yapo kazini. Yanaendelea kuchimba na baadaye yataweka wazi majina ya wanasiasa hao ambao wanamsapoti Felista.
  Source:Global Publishers


  0 0

  "Tatizo watu mmezoa ku cram sana kwamba kila anaeenda katika harusi aende na suit, Nchi nyingine hawapo hivyo kama ukiona hao waliopo na Diamond hapo chini hakuna aliepigiliaa kihivyo yaani unatakiwa uwe simple but elegant,, besides ilikuwa ni ndoa ya kimila so kupigiliamo suit haihusu,,

  daah mnavyokosoa as if mnajua sana fashion, to me Diamond was on point na ameonekana mbunifu, maana hajatuendea na suit pale, me nadhani alisoma kwanza mazingira ndio akatupiamo kitu chake,,, its all about fashion sio mna cram

  wamaaa Diamond ulitokelezea na kuwa so different kwenye ukweli lazima nasimama na ukweli....." Sintah
  0 0


  Ni dhahiri kwamba huu ndio mwisho wa harakati za Mwanamuziki maarufu wa muziki wa dansi Tanzania mwenye asili ya Congo DRC Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza (Papii kocha) kujinasua kwenye kifungo cha maisha gerezani.
  Kwa mara nyingine tena harakati zao za kujitoa kwenye adhabu hiyo zimegonga mwamba baada ya Mahakama ya Rufani kupigia msumari wa mwisho uliozima harakati zao kujinasua baada ya kutupilia mbali maombi yao ya marejeo ya hukumu ya rufaa yake.
  hii ni mara ya tatu kwa wafungwa hawa kugonga mwamba baada ya Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam na Mahakama ya Rufani kutupilia mbali rufaa zao kupinga hukumu ya Mahakama ya hakimu mkazi  kisutu iliyowahukumu kifungo cha maisha.
  Wafungwa hawa kupitia kwa Wakili Mabere Marando walikua wakiiomba Mahakama ya Rufani ifanye marejeo ya hukumu yake ya February 11 2010 iliyothibitisha adhabu hiyo waliyohukumiwa na Mahakama ya chini na badala yake iwaachie huru lakini Mahakama ya Rufani katika uamuzi wake uliotolewa na Majaji watatu, Nathalia Kimaro, Salum Massati na Mbarouk Mbarouk ilitupilia mbali maombi hayo hivyo waendelee kutumikia kifungo cha maisha gerezani.
  Ni uamuzi ambao uliibua machungu sio tu kwa Wafungwa na ndugu zao lakini hata kwa Wakili wao mwingine Gabriel Mnyele aliesema ‘hakuna namna nyingine ya kuwachomoa kwenye adhabu hii isipokua miujiza’
  Ndugu na watu wengine waliohudhuria Mahakamani waliendelea kutokwa na machozi ya huzuni pale Wafungwa hawa walipokua wakipandishwa kwenye gari la Magereza kurudishwa kuendelea kutumikia adhabu yao.
  Kauli ya Mahakama baada ya kutupilia mbali maombi yao ni ‘Waomba Marejeo hao hawakuwa na hoja ya msingi kwa sababu hoja zilizotolewa sio tu hazikidhi kuifanya Mahakama irejee hukumu hiyo bali pia zilishatolewa wakati wa usikilizwaji wa rufaa na kutolewa uamuzi na kwamba waomba Marejeo hawakuweza kubainisha makosa waliyodai yalijitokeza kwenye hukumu iliyowatia hatiani na hawakuweza kueleza ni jinsi gani yalisababisha haki kutotendeka’
  Mahakama hiyo imesema ‘kuhusu upande wa mashtaka kushindwa kuwaita Mahakamani mashahidi wanaoonekana kuwa muhimu kuunga mkono ushahidi wa Watoto, tunasema hoja hiyo haina msingi…. suala la shahidi gani aitwe Mahakamani kuthibitisha kesi ya upande wa mashtaka liko mikononi mwa upande wa mashtaka, zaidi ya yote idadi ya Mashahidi sio hoja ya msingi bali kuaminika kwao’
  Wakili Mnyele amesema ‘huu ndio mwisho wa mchakato, kulinganisha na hukumu ilivyokua ni kwamba kunahitajika kuwepo na Mahakama ya juu zaidi ya hii, kungekuwepo na Supreme Court ingeweza kusikiliza na kufikia maamuzi ya haki’
  Kwa upande wake, Babu Seya wakati akipelekwa na askari kwenye gari la Magereza alitoa kauli ambayo hakuipa ufafanuzi wowote baada ya kuisema kwamba ‘kwa binadamu ni makosa lakini kwa Mungu hakuna makosa’
  Papii Kocha nae wakati anapelekwa kupanda gari arudishwe Magereza alisema ‘sasa tunamuachia tu Rais ndie anaweza kutoa uamuzi wa mwisho’
  Babu Seya na wanawe watatu walihukumiwa adhabu ya maisha gerezani na Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu June 25 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka na kuwalawiti watoto kumi wa kike wenye umri chini ya miaka 10.

  0 0

  Mi nimechoshwa na wasichana wa humu mtandaoni mana wa kwanza alikuwa mwizi, wa pili alikuwa malaya wa kutupwa ,wa tatu mpenda hela ka amezaliwa kwenye ATM wa mwisho ana majini ...Daah Mechoka Mie

  0 0

  d8
  Lilikuwa swali kwamba inakuaje video iliyotumia ya gharama kubwa zaidi ya msanii wa bongoflava haipati airtime kwenye vituo vya kimataifa wakati video nyingine za wasanii wa muziki huu huu wanafanikiwa kupata airtime.
  Jibu la swali hilo hatimaye limepatikana baada ya video ya My number one kuanza kuchezwa kwenye vituo maarufu duniani.
  Diamond kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii aliwajulisha mashabiki wake kwamba wanaweza pia kuiona video ya My number one kwenye channel ya Trace na Sound City.
  Kupitia Trace video hiyo imetambulishwa kama video mpya na kwenye Sound city imerushwa kwenye trending video request na hizi ni picha kutoka kwenye screen wakati video hiyo ikipata airtime kwa mara ya kwanza kwenye vituo hivi.
  d1
  d2
  d3
  d6
  d7  0 0
 • 11/21/13--22:06: FUMANIZI LA JB UTATA MTUPU
 • LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa utata.

  Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’. 
  Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa jina moja la Sarah.
  Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika hoteli hiyo usiku.
  Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo ukafunguliwa.
  Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu wa mume wa Sarah,  JB alipokea  kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo  waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
  Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
  Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
   “Mimi simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake sizielewi bora niachane  naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”

  HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA

  Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
  “Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu, akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku hiyo.
  “Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
  “Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango, akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
  “Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
  “Kule nje niliwaambia wenye hoteli, wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”
  Sarah alipopatikana hewani juzi  alisema hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.

  Credits: Global Publishers

  0 0

  Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.

  Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.
    Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.

  CHANZO: JAMII FORUM  

  0 0

  Admin hide my name , mimi ni kijana wa kitanzania nina mke na mtoto mmoja kwa muda wa miaka miliwili sasa nimekuwa nikisoma UK Deree yangu ya pili , kwa sasa nimemaliza nimerudi Tanzania , sasa cha ajabu ambacho sikielewi ni kuwa kila nikikutana na mke wangu anataka nimwingilie kinyume na maumbile..yaani sometimes anaipeleka mwenyewe huko sehemu kwa siku kama mbili nimekuwa nafanya bila kujua imeingia huko...sasa nimejua nimemkalisha kikao lakini haeleweka hajanipa jibu la maana paka sasa...nahisi wakati mimi nipo uk kuna mtu alikuwa anamchezea sasa imekuwa hawezi sikia raha mpaka afanye hivyo ..mimi ninajua madhara ya huo mchezo siwezi kabisa kufanya kwa mke wangu ...swali linakuja hapa sasa nisipomfanyia ina maana ataendelea na hao jamaa zake wanao mfanyia ...sasa sijui nifanyaje ..naomba ushauri wa kina hapa 


  0 0

  Kuna taarifa kuwa Watanzania wawili wamekamatwa na dawa za kulevya nchini India na kwamba mmoja wao amefariki dunia. Taarifa zinadai kuwa Watanzania hao, ambao walikuwa watatu, waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Chatrapati Shivaji juzi asubuhi na Ethiopian Airlines Flight 610.

  Baada ya kutua uwanjani hapo, maafisa kutoka uwanjani hapo waliwakamata Watanzania wawili kati ya watatu kwa mahojiano zaidi baada ya kutonywa (tip-off) kuwa walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Baada ya kuhojiwa kwa muda wa masaa matano, Watanzania hao walikataa katakata kuwa walikuwa "punda" wa dawa za kulevya. 

  Taarifa zinadai kuwa maafisa hao waliamua kuwapa Watanzania hao chakula na maji kama trick ya kujua kama walikuwa wamebeba dawa za kulevya. Kwa kawaida, mtu aliyemeza vidonge vya dawa za kulevya hali wa kunywa ili kuepukana na kifo. Hivyo basi, kama mtuhumiwa akipewa chakula na kukataa kula inaweza kuwa ni dalili kuwa amemeza vidonge vya dawa za kulevya. 

  Hivyo basi, baada ya kupewa chakula na maji, Mtanzania mmoja alikataa kula wala kunywa. Hata hivyo, Mtanzania wa pili alikubali kula chakula alichopewa. Baada ya hapo, Watanzania wote watatu walipelekwa mahakamani, lakini yule aliyekubali kula alikataa na kutaka kukukimbia. Baada ya purukushani katika eneo la mahakama, yule aliyekubali kula chakula alifariki baada ya kuzidiwa na vidonge vya cocaine kama 120 alivyokuwa amemeza. 

  Hali ya Mtanzania wa pili ilizidi kuwa mbaya na alipelekwa katika hospitali ya JJ. Baada ya kufanyiwa X-ray na CT-scan alikutwa amebeba vidonge vya cocaine kama 100 hivi. Kwa mujibu wa maelezo ya mkuu wa hosipitali hiyo, hali yake ni mbaya lakini hajapelekwa ICU. 

  Mtanzania wa tatu, ambaye ni mwanamke wa makamo, bado anahojiwa na vyombo husika. Mwanamke huyo hakukutwa na dawa zozote lakini alikuwa ameongozana na wanaume hao wawili. Upelelezi bado unaendelea kujua kama alikuwa mmiliki wa hizo dawa za kulevya.

  Habari kwa mujibu wa India Today, The Times of India, Daily News India

  0 0

  Wanamuziki wa kundi la P-Square Peter na Paul baada ya kutua jijini Dar usiku wa kuamkia leo. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkrulu ambao ndio wadhamini wakuu wa onesho lao ambalo limeratibiwa na East Africa Radio na EATV.
   
   Hapa wakifanya mahojiano na kituo cha East Africa TV ambao ndio wenyeji wao.
  Mahojiano na picha za hapa na pale zikiendelea.
  Vijana wakielekea kupumzika tayari kwa kazi ya kesho
  (Picha na Mdimuz Blog)

  0 0

  Imebainika kwamba sababu ya shambulizi la risasi lililotokea Ilala Bungoni, Dar es Salaam Jumanne iliyopita na kusababisha vifo vya watu watatu, ni wivu wa mapenzi uliopindukia.

  Akizungumza nyumbani kwao Ilala Bungoni jana, mmoja wa majeruhi ambaye ndiye aliyekuwa kiini cha shambulizi hilo, Christine Newa alisema si kweli kwamba sababu ya mchumba wake, Gabriel Munisi kuwashambulia na kuwajeruhi kwa risasi yeye na mama yake mzazi, Ellen Eliezer na kumuua mdogo wake wa kike, Alpha Newa ni kutokana na kusaliti uchumba wao.

  Awali, ilidaiwa kwamba sababu ya shambulizi hilo ni Christine kumkataa Munisi, (ambaye pia alijiua baada ya kufanya mauaji hayo) na kuchumbiwa na rubani wa ndege, marehemu Francis Shumila ambaye pia alifariki katika tukio hilo... “Kwanza Shumila hakuwa mchumba wangu kama ilivyoelezwa. Alikuwa shemeji yangu, mume wa dada yangu Caroline Newa. Pia hakuwa rubani wa ndege, bali nahodha wa meli.”

  Alisema amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Munisi katika kipindi kisichofikia mwaka mmoja lakini sehemu kubwa ya maisha yao ikitawaliwa na misuguano iliyowafikisha polisi mara kadhaa.

  Alisema katika kipindi cha uhusiano wao marehemu Munisi alikuwa akimpiga, akimkataza kufanya kazi, kusoma na alikuwa na wivu uliopindukia.

  Christine kuona hivyo, aliamua kufanya mipango ya kwenda kusoma katika Visiwa vya Cyprus kimyakimya pasi na kumuaga, jambo ambalo alisema lilimkera mchumba wake huyo na kuweka kisasi.

  “Nikiwa huko, Munisi alitafuta mawasiliano hadi akayapata na tukawasiliana na siku niliporejea alikuja kunipokea uwanja wa ndege lakini cha ajabu, alinikataza kwenda nyumbani na badala yake akanipeleka moja kwa moja hadi Mwanza eneo la Kitangiri,” alisema na kuongeza: “Tukiwa njiani kuelekea Mwanza, katika maeneo ya Singida, alisimamisha gari akaniambia nishuke, akatoa bastola na kuniuliza kwa nini niliondoka bila ya kumuaga. Je, nataka kumuacha?”

  Alisema alimwomba msamaha na kuendelea na safari yao. Anasimulia kwamba baada ya kufika Mwanza, alimpora simu zake zote na kumfungia ndani kwa zaidi ya wiki mbili hadi alipopanda kwenye dirisha na kuomba msaada kwa majirani na kuwapa namba za simu za ndugu zake ili wamsaidie kuwapa taarifa.

  Ndugu zake walianza mchakato wa kuwasiliana na polisi hatua iliyofanikisha msichana huyo kurudishwa Dar es Salaam... “Hata hivyo niliondoka na khanga na fulana tu. Vitu vyote niliviacha huko.”

  Baada ya kurudi Dar es Salaam, anasema Munisi naye aliamua kumfuata lakini safari hii alifikia katika Hoteli ya MM iliyotenganishwa na ukuta wa nyumba yao na akawa anafuatilia nyendo za familia hiyo.

  “Alikuwa ananitumia meseji kwamba amemuona dada Caro, mama na Alpha na wakati mwingine anasema ameniona mimi mpaka nguo tulizovaa, tukaanza kupata na wasiwasi,” alisema.

  Wasiwasi huo ulitokana na historia ya maisha yao ya Mwanza na pia tishio ambalo anadai kwamba Munisi aliwahi kulitoa kwamba atahakikisha anaiteketeza familia yote kuanzia Goba anakoishi mama yake (Ellen), Zanzibar anakoishi mdogo wake (marehemu Alpha) na hapo Ilala.

  Anasema walikwenda polisi lakini walielezwa kwamba hayo ni masuala madogo ya mapenzi na kwamba yatamalizwa kifamilia.

  Siku ya tukio Christine alikuwa akitoka kwenda uwanja wa ndege tayari kwa safari ya kurudi shuleni Cyprus ndipo Munisi alipotokea na kuanza kumrushia Shumila risasi na baadaye Alpha kisha mama na yeye kabla ya kujiua.

  Akizungumzia tukio hilo, Caroline alisema mumewe alitabiri kifo chake kabla kwani baada ya kusikia vitisho vya Munisi, alimtoa shaka Christine akimwambia kwamba atamlinda hata ikibidi kupoteza maisha yake, jambo ambalo lilidhihiri.

  Alisema mama yake amepata nafuu na ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa na mazishi ya mdogo wake, Alpha ambaye ameacha mtoto mwenye umri wa miezi minane, yamepangwa kufanyika Jumamosi Goba, Dar es Salaam.

  Alisema mipango ya mazishi ya mumewe inafanywa huku akidokeza kwamba huenda akasafirishwa kwenda Mombasa.

  0 0

  Vanessa Mdee, Gosby na Mabeste hawapo tena B’Hits Music Group. Kwa mujibu wa B’Hits Mabeste aliondolewa tangu miezi minne iliyopita japo hawakutangaza rasmi na Mabeste alipewa muda wa kujitetea kutokana na kwenda kinyume na mkataba wake ikiwa ni pamoja na kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi.
  Akiongea na Bongo5, Mabeste ambaye leo ametangaza kutokuwa chini ya label hiyo kupitia Facebook, amesema pamoja na label hiyo na kutengeneza hits nyingi, muziki wake haukuwa ukimpa kipato anachostahili na kusema kuwa tatizo lake na B’Hits ni katika kuufanya muziki wake uingize fedha zaidi pamoja na kuufanyia promotion.

  Amesema nyimbo zote alizowahi kutoa amekuwa akiachiwa yeye zaidi kuzifanyia promotion na kuzifikisha mahali kitu ambacho anaamini ilikuwa ni kazi ya label yake.

  “Sitaki kuonekana mzigo kwao. Haiwezekani kila siku wao wawe wanarekodi halafu wao hawaoni faida. Baada ya kutoona faida, wanarekodi nyimbo nyingine tena wananipa inaenda,” amesema Mabeste.

  Aliongeza kuwa anaumia kuona producer wake Pancho ambaye alimkutanisha na B’Hits miaka mitano iliyopita hapati faida ya muziki wake. Hata hivyo amekanusha madai ya kufanya show bila kutoa taarifa kwa uongozi na kudai kuwa katika dunia ya sasa si rahisi kufanya show kwa siri bila kujulikana.

  “Sasa mabadiliko ambayo yanatokea ndani ya haya maisha, wanahisi maybe mimi ninapata show siwaambii. Hivi hii Tanzania sasa hivi social networks ilivyotawala, kuna mahali unaweza kupiga show mtu asijue? Na nani atakuita show yake na aachie kuifanyia promotion kwa social network,” amehoji Mabeste.

  Mabeste amesema kutokana na maisha kubadilika na kwakuwa sasa amekuwa baba, kiasi alichokuwa anakipata akiwa B’Hits ni kidogo kuweza kukidhi mahitaji yake ya kila siku na hivyo kumfanya aishi na stress wakati ana uwezo mkubwa.

  Hata hivyo CEO wa B’Hits Music Group, Hermy B amesema anashangaa kumsikia Mabeste akilalamika hivyo wakati wao walimtoa mbali ambako alikuwa akiishi maisha ya chini na kuingia gharama nyingi za kumtunza ikiwa ni pamoja na kumlipia kodi ya nyumba, kumnunulia nguo pamoja na kumpa fedha ya kujikimu pale alipokuwa akihitaji.

  Hermy B amesema kama akiamua kujumlisha gharama alizotumia kwa Mabeste zinafika si chini ya shilingi milioni 30 na haoni kama Mabeste ana uwezo wa kuzirejesha.

  Ameongeza kuwa wote Mabeste, Gosby na Vanessa hawana shukrani kwa kile B’Hits imewafanyia.

  Ametoa mfano kuwa video ya Closer ya Vanessa Mdee aligharamikia fedha zake kutoka mfukoni ambazo ni takriban shilingi milioni 8 ambazo hazijawahi kurudi hadi sasa na pia alilipia kwa hela yake hata kazi alizofanya kwenye studio nje ya B’Hits.

  Naye Amani Joachim, ambaye ni mwanasheria na mmoja wa viongozi wa B’Hits, alisema Vanessa Mdee na Gosby waliondolewa B’Hits kutokana na kuingia mkataba wa kufanya show ya Fiesta Dar bila kuutaarifu uongozi. Amesema wawili hao walifikia hatua ya kwenda kufanya fujo B’Hits wakidai nyimbo zao kwaajili ya kutumbuiza kwenye show hiyo hali iliyokiuka masharti ya mkataba wao.

  Ameongeza kuwa ukimya wao umewafanya watu wengi waamini kuwa wasanii hao walijiondoa wenyewe wakati uongozi ndio ulifanya uamuzi wa kwanza wa kuwaondoa.

  Pamoja na hivyo, Hermy B amesema B’Hits itaziachia nyimbo zote za wasanii hao zichezwe redioni kwakuwa kuzifungia kutakuwa na hasara kwao kutokana na kutumia nguvu na akili nyingi kuziandaa.

  Hata hivyo amesema, wasanii hao hawatakuwa na haki ya kuzitumia popote kwakuwa ni mali halali ya kampuni. Hermy B amesema, uongozi wa B’Hits hauna ugomvi na wasanii hao na mwanzoni mwa mwaka ujao wanatarajia kutangaza wasanii wapya watakaokuwa chini ya label hiyo.
  -Bongo5.com

  0 0

  Wadau hapa nilipo nimechanganyikiwa na nisijue cha kufanya, naombeni ushauri wenu, nilikwenda field huko Tabora, nikamwacha mchumba wangu Tanga(ndiko kwetu) tulikuwa tukiwasiliana kama kawaida, na niliondoka nikiwa nimeshavishwa pete.

  Nilipigiwa simu baba yangu ni mgonjwa sana, watoto wake wote tulio mbali, tunatakiwa kurudi Tanga, basi nami nilirudi, na kukuta kweli hali ya baba si nzuri, nikampigia simu mchumba wangu kumuuliza yuko wapi, ili tukutane nae hospitali, akasema kwamba amesafiri kikazi gafla kwa siku moja tu then kesho yake angegeuza, nikamuuliza inakuwaje huniambii, akasema nimesafiri gafla, hata hivyo nilitaka nikujulishe maana nimeondoka leo.

  Niliumia sana kwa alichokifanya, sasa kuna rafiki yangu mmoja akaniambia, mbona mimi nimemuona jana super market? Akiwa na msichana? Nilijisikia huzuni sana ila nilijipa moyo

  nilikwenda moja kwa moja hadi kwake, nikamkuta mtoto wa mwenye nyumba, nikamuuliza kama kweli mchumba wangu amesafiri,(nikajua labda alikwenda supermarket kununua vitu vya safari) akasema mbona yupo? Na asubuhi nimemuona?, nikampigia simu kuwa nipo pale kwake, akasema atachelewa sana kurudi, hivyo nirudi nyumbani kesho ndio nije, nikamwambia namsubiri, ilifika saa sita mimi niko mlangoni nimekaa namsubiri, aliponikuta nimesinzia mlangoni alishtuka sna, na kuanza kunifokea kwanini nisingesubiri hadi kesho.

  Ile naingia tu! Ndani, nikakutana na sandols za kike, na kwenye mto kuna chupi ya kike, niliumia na kuanzisha ugomvi mkubwa,

  Kinachonishangaza eti anasema yeye mwenyewe hajui ni vya nani, itakuwa mama mwenye nyumba mchawi, maana alikuwa anamtaka, na bado anasisitiza eti ananipenda na anataka nifunge nae ndoa mwezo wa tisa.

  Sasa mimi hata sijui nifanyaje, naombeni ushauri wenu?

  0 0

  Muimbaji wa ‘Beautiful’ Q-Chilla amesema amesikitishwa na jinsi wasanii wenzake walivyokuwa kimya kwenye rufaa ya Babu Seya na Papii Kocha ambao rufaa yao imekataliwa leo na hivyo kuendelea na kifungo cha maisha jela.

  Q-Chilla amesema kama kungekuwepo na kauli za wasanii kuhusiana na rufaa hiyo huenda mambo yangekuwa tofauti.

  “Wameshindwa, wamekaa tu kufanya kazi zao za kujipromote wao, this is very stupid,” amesema Chilla.

  “Kauli yao tu ni faraja kwa hawa jamaa. Wangeona kuna watu kule nje hata kama hawana uwezo wa kututoa au kuiambia serikali itutoe, kwamba kuna watu kweli wako touched na hii issue. Always wanasubiri mtu afe au jambo hili litokee, ndio wajitokeza wazungumze. Nahisi kila mtu anaishi sababu anafanya kazi zake na afulfill dreams zake, but we are not there for other people who need hata kauli zetu. Ukizungumza unaonekana una stress. Ila Mungu ana sheria zake na serikali ina sheria zake. Nimekubaliana na hilo.”

(Page 1) | 2 | 3 | .... | 2994 | newer