Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

TUNDU LISSU "ZITTO NA WENZAKE WATATU WAMEBAINIKA KUKIHUJUMU CHAMA"

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kimemvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama  kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni ambapo yeye, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba na mwingine mmoja Makao makuu wamepewa siku kumi na nne wajieleze kimaandishi kabla ya kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu ikiwemo kuvuliwa Uanachama.

UFAFANUZI WA CHADEMA KUHUSU MAAZIMIO YA KAMATI KUU

$
0
0
Live Updates: Ndugu Wanachama na Watanzania na wote muda si mrefu tutawaletea Mkutano na Waandishi wa Habari kuwajulisha Watanzania maazimio na maamuzi ya Kamati Kuu iliyokutana kwa siku mbili tarehe 20-21/11/2013 katika Hotel ya Blue Pearl Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam

================
UPDATES

- M/Kiti Mh. Freeman Mbowe ameshawasili na ameanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imemteua Mh. Tundu Lissu kuwa Mwanasheria Mkuu wa Chama na pia Kamati Kuu imefikia maamuzi ya kinidhamu kwa baadhi ya viongozi.

Anamkaribisha Mh. Tundu Lissu kwa ajili ya kutoa taarifa ya maazimio ya Kamati Kuu kwa niaba ya M/Kiti

- Tundu Lissu anaanza kwa kusema kuwa Kamati Kuu imenasa waraka wa mkakati wa siri wa kukipasua Chama vipande vipande unaohusisha watu wanne ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba na mtu mwingine ambaye hajajulikana.

- Anasema lugha iliyotumika katika waraka huo ni ya siri ambapo kuna mtu anaitwa MM ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr. Kitila Mkumbo, M2. Hajajulikana na Dr. Mkumbo alikana kumfahamu kabisa M2, na M3 ni Mwigamba.

Lissu anasema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini, majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.

Lissu anasema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa na masharti ya katiba yetu

- Anasema Kamati Kuu imeamua kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.

Pia kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake

Kamati Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.

- Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.

- Lissu anasema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata kidogo.

- Kamati Kuu pia imeazimia kuusambaza waraka huo kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili watanzania waone na kujua ukweli.

Lissu anamalizia kwa kuwaomba watanzania na Wanachama wote wa CHADEMA nchi nzima wasife moyo na waendelee kukijenga Chama na nchi yao.

- Kamati Kuu pia imemteua Wakili Msomi Mh. Peter Kibatara kuwa Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa Chama

- Mh. Mbowe anasema waraka wa siri za Zitto haukutengenezwa wala haukutoka Makao Makuu. Alikuwa akijibu swali la Mayage kuhusu zitakapopatikana fedha za kutekeleza mpango huo

Jamii Forums

WILLIAM MALECELA " CCM TUNAWAHITAJI SANA CHADEMA HII INAYOONGOZWA NA AKILI NDOGO-TUWASAIDIE WASISAMBARATIKE

$
0
0
- Ni muda mrefu sasa kumekuwa na mtafaruku mzito ndani ya Chadema ambao umekuwa ukikitafuna sana chama hicho, na pia kuna utabiri mzito sana ulitolewa na Waziri Wassira kwamba Chadema ipo katika siku zake za mwisho. Ninasema hivi kufa kwa Chadema kama dalili zinavyoonyesha sasa hivi sio the best Interest ya chama chetu CCM. Tunahitaji kuwasaidia sana waendelee kuwepo kwa sababu they have proven time and time kwamba ni paper tiger tu, wazuri kwenye makaratasi lakini hawana nguvu yoyote kisiasa.

- Kupitishwa kwa musawada wa Katiba mpya juzi bungeni ni mfano mzito sana ulio hai wa jinsi wasivyo na nguvu kabisa za kisasa za opposed na makelele yao ya kila siku na lile gazeti lao lenye makao makuu yake kwenye Club ya Disco ya Mwenyekiti wao. Ninawaomba sana CCM tunahitaji kuwa makini sana na matatizo ya chama hicho sasa hivi, tutumie nafasi hii kuwasaidia wasiambaratike maana Chadema ikisambaratika tutaanza kufukuzana na adui tusiyemjua, ni bora kushindana na huyu huyu adui tunayemjua, anayelia posho za wabunge ni kubwa na huku anazipokea, anayelia lia kwamba magari ya wabunge ni ya gharama sana na huku anayapokea hayo hayo. Anayelia lia safari za Rais huku wabunge wake wanasafiri kila siku nje kwa visingizo vya kamati za bunge.

- AGAIN KWA WANA-CCM WOTE NI KWAMBA TUNAWAHITAJI SANA CHADEMA HII INAYOONGOZWA NA AKILI NDOGO, MAANA OTHERWISE TUTAKUTANA NA WAPINZANI WENYE AKILI KUBWA WATATUSUMBUA, TUWASAIDIE WASISMBATRATIKE!! ha! ha! ha!

- KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!


LE Mutuz Big Shoow!!

BAADA YA ZITTO KUVULIWA UONGOZI CHADEMA..MAKAMU MWENYEKITI WA CHADEMA BARA NAE AJIUZULU LEO

$
0
0
Salaam,

Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. 

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.


Said A Arfi (mb)

WARAKA ULIOWAVUA VYEO ZITTO, DK KITILA NA MWIGAMBA HUU HAPA

$
0
0
MKAKATI WA MABADILIKO 2013
UTANGULIZI:
Taasisi tunayoizungumzia ilisajiliwa rasmi mwezi January 1993 na tokea wakati huo imeongozwa na wakuu wa taasisi wapatao wawili na aliyepo kwa sasa ni wa tatu. Wa kwanza aliongoza kwa miaka mitano tangu wakati huo 1993 hadi 1998 na kumwachia aliyefuata ambaye naye aliongoza kwa miaka mitano hadi mwanzoni mwa 2004 na kumwachia aliyepo sasa. Huyu aliyepo aliongoza kwa miaka mitano tangu mwaka 2004 hadi 2009 na kisha akachaguliwa tena mwaka 2009 kwa kipindi cha pili.
Tunapenda kwa hatua ya mwanzo kabisa kutambua juhudi za wakuu wetu wote waliopita walizozifanya katika kuhakikisha taasisi yetu inakua kwa kutumia uwezo wote waliokuwa nao na katika mazingira yaliyowakabili. Mwaka 1995 chini ya mkuu wa kwanza tulipata wawakilishi watatu kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi. Mwaka 2000 chini ya mkuu wa pili tukapata wawakilishi wanne pamoja na wa nyongeza mmoja na kufanya idadi kuwa watano. Mwaka 2005 chini ya mkuu wa tatu ambaye ndiye aliyepo hivi sasa, tulipata wawakilishi watano na wa nyongeza sita jumla wakawa 11. 2010 chini ya mkuu huyu huyu wawakilishi wakaongezeka na kuwa 23 na wa nyongeza 25 na kufanya idadi kuwa 48 kabla ya kupata mwingine mwaka jana na kufanya sasa wawe 49.
Dk. Kitila Mkumbo.
Tunapopongeza juhudi zao hizi tunahitaji pia kuwapongeza wakuu wetu wawili wa kwanza ambao kimsingi waliweka msingi mzuri sana wa kutong’ang’ania madaraka na badala yake kuachia mapema na kumwachia mwingine kidemokrasia bila vurugu. Hawakuwa madikteta na tunawapongeza sana. Walijitahidi sana kutokuwa wapenda madaraka na kimsingi walituwekea utamaduni ambao walitaka wote tuufuate na kujenga taasisi imara inayojali demokrasia na haki ya kila mwana taasisi. Ni kwa msingi huo waliamua kuandika kabisa katika mwongozo wetu kwamba kiongozi yeyote katika ngazi yoyote ya kuchaguliwa atakapogombea na kushinda ataongoza kwa kipindi kimoja cha miaka mitano na kisha ataweza kugombea na kuongoza kwa kipindi cha pili cha miaka mitano baada yapo hawezi kugombea tena katika nafasi ile ile aliyoitumikia kwa vipindi viwili. Ili kuonyesha kwamba walimaanisha kile walichokisema, wote wawili hawakuwahi kukaa madarakani kwa vipindi viwili vilivyoruhusiwa katika mwongozo bali wote wawili walikaa kipindi kimoja kimoja tu.
Samson Mwigamba.
Lakini kuna matatizo yameanza kujitokeza na tusipochukua hatua haraka huko mbele tunaweza kupata shida kubwa. Tunapenda kuainisha matatizo hayo kwa uchache kama ifuatavyo:

Wakati tukiufanyia mwongozo wetu mabadiliko mwaka 2006 hatukugusa kipengele kinachomzuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano. Lakini wakati mwongozo unachapwa chini ya uongozi uliopo, kipengele hicho kiliondolewa kinyemela. Mambo yanayotokea hivi leo yanaonyesha dhahiri kipengele hicho kiliondolewa kwa makusudi kwa maslahi na kwa faida ya viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Hiki kinaweza kuchukuliwa kama kitendo kidogo lakini kama viongozi wetu wanaweza kutokuwa waaminifu katika jambo kama hili, ni dhahiri hawawezi kuaminika na wanaweza kufanya mambo mengine makubwa na yenye athari zisizomithirika kwa taasisi yetu.

Ni dhahiri kwamba uongozi uliopo umeishiwa mbinu na kuakisi jambo la msingi sana ambalo waasisi wetu waliliona tangu mwanzo na kuamua kuweka kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye mwongozo wetu. Kuchoka kwa uongozi wetu kunaonekana dhahiri katika mipango na mikakati ya taasisi ya miaka kadhaa. Mfano mwaka 2008 uongozi ulianzisha mkakati wa operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara). Huo ulifanyiwa kazi katika mikoa kadhaa na hatimaye ikafa kimya kimya. Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kulianzishwa matembezi ya maandamano ambayo nayo yalikuwa yakipeleka ujumbe kwa watu na yalipangwa kufanyika mikoa yote na wilaya zote.

Kumbukumbu zetu zinaonyesha kwamba yalikuwa yakianzia makao makuu ya mkoa na kwenda kwenye wilaya zote. Lakini kumbukumbu hizo zinaonyesha kwamba yalifanyika Mwanza, Musoma, Shinyanga, Kagera na mikoa ya Nyanda za Juu kusini (Mbeya, Iringa, Njombe na Rukwa) kisha nayo yakafa kifo cha mende. Kisha mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko maarufu kama Movement for Change (M4C). Hiyo ilikuwa inakwenda kwenye mikoa na timu kama nne hivi ambazo kwa ujumla zilitathmini hali ya mtandao na uongozi wa taasisi, kuhamasisha umma kwa njia ya mikutano ya hadhara, kuingiza wanachama na kusimika uongozi na hatimaye kufanya mafunzo kwa viongozi. Hiyo ikafanyika Mtwara na Lindi, Morogoro na kisha ikaenda kufia Iringa. Mwaka huu viongozi wetu wamekuja na ugatuaji madaraka kutoka makao makuu ya taasisi na kupeleka madaraka kwenye kanda mbalimbali. Mkakati huu ulikufa kabla ya kuanza pale viongozi wakuu walipobadilisha maazimio ya kikao kikuu na kutekeleza matakwa yao ikiwa ni pamoja na kuleta suala la viongozi wa muda kwa muda mrefu badala ya kuajiri maofisa na wakahakikisha wanaweka watu wao kwenye uongozi wa muda. Kitendo hiki kwa peke yake, cha kufeli kwa kila mkakati unaoletwa na viongozi wetu katika hatua za utekelezaji unaofanywa na wao wenyewe waleta mkakati, ni kiashiria tosha kwamba uongozi uliopo umechoka.

Performance yetu kwenye chaguzi ndogo nayo ni ishara kwamba mabadiliko yanahitajika. Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika chaguzi ndogo 8 za wawakilishi kwenye chombo kikuu, kati ya hizo tumeshinda 2 tu sawa na asilimia 25. Aidha baada ya mwaka 2010 kumefanyika chaguzi kadhaa za wawakilishi kwenye halmashauri. Mwezi Oktoba 2011, mwezi wa4 2012, mwezi Septemba 2012 na mwezi Juni 2013. Kote performance yetu imekuwa poor kupindukia. Mfano mwezi wa Juni 2013 tumepata viti 6 kati ya 22 (27%) na mwezi Septemba 2012 tulipata viti 7 kati ya 29 (24%). Ni dhahiri mabadiliko yanahitajika kwa kuwa wakuu waliopo wanatumia mbinu zile zile na kupata matokeo yale yale. Tunahitaji mbinu mpya. Kwa kifupi, ushindi ambao tumekuwa tukiupata katika chaguzi ndogo haulingani na ukubwa wa hamasa kwa taasisi yetu iliyopo mitaani. Hii ni kwa sababu tumekuwa tukitumia mbinu hizohizo katika kila chaguzi. Aidha, tu wepesi mno wa kuridhika na kujisifu kwa mafanikio madogo badala ya kukaa chini na kutafakari kwa kina mahala tunapojikwaa.

Matumizi ya fedha za taasisi. Hakuna mtu anayejua hivi sasa fedha za chama zinatumikaje zaidi ya kakikundi ka watu watatu yaani mkuu kabisa, mtendaji mkuu na mkuu wa fedha kwenye taasisi yetu. Maamuzi ya vikao hayaheshimiki tena na mabwana hawa. Baada ya uchaguzi wa 2010 vikao halali vilielekeza kiasi na aina ya fedha ambazo hazitaguswa bali zitunzwe kwenye akaunti maalum kwa ajili ya uchaguzi wa 2015. Lakini leo si tu akaunti hiyo haina fedha bali hakuna akaunti yoyote yenye fedha. Watu watatu ndo wanaamua fedha zitumikeje. Mfano mwingine ni maamuzi ya kikao cha juu mno cha hivi karibuni kilichoamua kwamba kiasi cha fedha inayotoka serikalini kipelekwe kwenye mikoa na wilaya na kiasi kingine kipelekwe kwenye kanda. Leo ni mwezi wa tano maamuzi hayo hayajatekelezwa. Lakini kuna michango ya watu binafsi kama yule mtanzania mwenye asili ya kihindi, hizo nazo hazijulikani zimechukuliwa lini kwa mfumo gani, zikatunzwa wapi na hatimaye zimetumikaje. Hapo hatujataja fedha zinazopatikana kutoka kwenye fundraising events mbalimbali kama ile ya Dar es salaam na Mwanza. Hizo nazo hazijawahi kuonekana na walioendesha hizo fundraising, uaminifu wao kwenye masuala ya fedha ni questionable.

Taarifa za fedha. Tokea baada ya uchaguzi wa 2010 mpaka leo, hakuna kikao chochote kilichowahi kupokea na kujadili hadi mwisho ripoti ya mapato na matumizi ya fedha za taasisi. Kila kikao agenda hiyo inarushwa kiaina. Wanaojua mchezo huo ni watu watatu tu tuliowataja hapo juu na malengo ya kurusha hiyo agenda kila wakati na kukwepesha isijadiliwe pia wanayajua wao. Ni dhahiri tukiendelea na hawa watu tutafika 2015 tukiwa hatuna pesa hata ya kuweka mawakala kwenye vituo na tutapigwa tukiwa tumesimama. Kwa kiasi kikubwa mkuu aliyepo anatengeneza mazingira yaleyale ya mwaka 2005 na 2010 ya kutaka chama kiwe hakina hela ili ikifika wakati wa uchaguzi kimpigie magoti. Kisha atatoa pesa bila kumbukumbu zozote na mara baada ya uchaguzi anapeleka lundo la deni na kudai alipwe hela aliyekikopesha chama wakati wa uchaguzi. Alifanya hivyo katika chaguzi za 2005 na 2010. Wakati wote wa kampeni za mwaka 2010, kwa mfano, taasisi yetu ilihangaika sana kwa kukosa hata hela ya kununua maji kwa wajumbe wa ngome. Lakini ajabu ni kwamba baada ya uchaguzi mkuu wa taasisi na baadhi wa wapambe wake walilete deni kubwa la takribani shililingi milioni mia tano akiadi kuwa walikikopesha chama. Taasisi imewalipa pesa zote hizi kwa muda mwaka mmoja. Sasa anatengeneza mazingira hayohayo kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Mipango ya kukipatia chama mapato ya ziada kutoka nje ya chama. Wakuu waliopo hawana hata ndoto ya namna ya kupata fedha za ziada. Wanachokijua ni kukusanya ‘sadaka’ kwenye mikutano ya hadhara na kuwapatia kazi watu wanaoonekana kuwa matapeli eti waendeshe harambee za kuchangisha fedha kwa njia ya matukio. Mawazo mazuri kama lile la kuanzisha kampuni la uwekezaji la taasisi yetu litakalowekeza kwenye miradi mbalimbali, halijawahi kufanyiwa kazi, na hivyo uanzishaji wa miradi mbalimbali ya kuiingizia taasisi fedha imebaki ndoto ya mchana. Hatuwezi kufika hata siku moja bila fedha. Hata uchaguzi wa wenzetu wa hapa jirani juzi juzi wakuu wetu ingawa walishiriki lakini hawaonekani kama wamejifunza chochote.

Njia haramu za kubaki madarakani. Ili kuhakikisha wakuu wanabaki madarakani, wameanzisha vikundi vikundi ndani ya taasisi yetu. Siku hizi ni rahisi sana kuambiwa kwenye taasisi yetu eti huyu ni wa boss na huyu ni wa dogo. Na wale walio wa boss kwa kuwa boss ndo anashikilia raslimali za taasisi anatumia mfumo haramu kuwaneemesha watu wake kwa kutumia raslimali za taasisi na kuwakandamiza wote wanaoonekana wanapishana naye kimtazamo. Jambo hili limewaibua wachumia tumbo, wapenda madaraka, na vibaraka lukuki wanaokwenda kujipendekeza kwa wakuu wa taasisi kwa malengo ya kujinufaisha binafsi. Katika kufanya hivyo vibaraka hao wamekuwa wakiwaendea wakuu wa taasisi na kuwajaza maneno mabaya dhidi ya viongozi wenzao na kuzidi kuwafarakanisha viongozi wa juu.

Kuna mchezo umeanzishwa na wakuu wa taasisi unaitwa ulinzi wa chama uliogawanyika katika makundi mawili yaani visible na invisible. Visible ni ule unaoonekana ambao uko chini ya kikosi chetu chekundu ambacho kinajulikana kwa kila mtu lakini invisible wanajulikana kwa mkuu wa taasisi na mtendaji mkuu peke yake. Wanafanya kazi kwa maelekezo ya wakubwa hao wawili na hawajulikani kwa viongozi wengine wa juu. Ni hawa hawa ambao wanatumika vibaya pale wanapoleta taarifa za kiintelijensia ambazo zinawahusisha viongozi wasiopendwa na wakuu na usaliti dhidi ya taasisi. Hakuna kamati maalum inayowathibitisha maaintelijensia hao bali wakuu wenyewe wanawachukua wanaowataka. Ni katika mfumo huu wa kipuuzi mida eight amekuwa akitumika vibaya kwa kumshambulia mtendaji mkuu msaidizi hadharani kwa kutumia mitandao ya kijamii na wakuu wanafurahia na kumlipa pesa.

Udhaifu wa utendaji wa mtendaji mkuu. Mtendaji mkuu ni dhaifu mno na ni mara nyingi sana tumeshuhudia mkuu wa taasisi akifanya mambo ya kiutendaji kinyume na utaratibu kama vile yeye mwenyewe kuja kwenye kamati ya makatibu na wakurugenzi na kupangua mipango yao na ku-inject ya kwake na mtendaji mkuu kuadopt tu kana kwamba yeye hawezi kupanga mambo ya kiutendaji, hata tunapokuwa kwenye operesheni maalum tumeshuhudia mkuu wa taasisi ndo akipanga watendaji, posho zao na hata kusimamia matumizi ya pesa na shughuli mbalimbali za kiutendaji. Udhaifu wa mtendaji mkuu ni udhaifu wa mkuu wa taasisi kwa kuwa amemteua yeye mara mbili tena mara ya pili alileta jina moja mbele ya Baraza la juu kuonyesha kwamba aliridhika na utendaji wake kiasi cha kutotaka kumpambanisha na mwingine. Lakini baada ya kumpendekeza mara ya pili ndipo tumeshuhudia yeye kuingilia kati mara nyingi sana mambo ya kiutendaji kana kwamba anamfichia aibu mtendaji wake. Swali kwa nini alimteua tena? Jibu lake litakuwa rahisi tu kwamba ni kwa sababu mtendaji huyu ni passivekwa kila takwa la mkuu wake.

Matumizi mabaya ya madaraka yanayoweza kuhusishwa na ufisadi. Taasisi yetu inayo kamati ya tenda ambayo iko chini ya kamati ya makatibu na wakurugenzi. Lakini uzoefu unaonyesha kwamba kamati hii haifanyi kazi imezimwa kimya kimya na wajumbe wote wa kamati ya tenda kwa kuwa ni wachumia tumbo wanaojigonga kwa wakuu, wamekubali kuzimwa. Leo ikidaiwa kamati hiyo ilete nyaraka za mchakato wa manunuzi ya magari, pikipiki, vifaa vya kueneza taasisi, set ya televisheni iliyofungwa ofisini kwa mtendaji mkuu, hawana. Manunuzi haya yote yote yanafanywa na wakuu hasa hasa mkuu wa taasisi bila utaratibu wowote jambo ambalo ni hatari na linarahisisha matendo ya kifisadi. Bila aibu, mkuu wa taasisi ndio amekuwa mnunuzi wa vifaa vyote vya chama nje ya nchi kwa bei anayoijua mwenyewe na ambaye haihojiwi popote. Huu ni mfano wa wazi wa mgongano wa kimaslahi jambo ambalo ni hatari kwa kiongozi mkubwa wa taasisi kama yetu inayojitambulisha katika kupinga vitendo vya ufisadi na uvunjifu wa maadili ya uongozi kwa ujumla.

Makubaliano ya kifisadi na mtu binafsi anayeuza vifaa vya kueneza taasisi. Hakuna kikao chochote cha juu kilichojadili ama kilichowahi hata kupewa taarifa tu kwamba sasa kuna mtu binafsi kapewa tenda ya kuuza vifaa vya taasisi na taasisi inanufaika vipi na mauzo hayo na kwa nini vifaa muhimu vya taasisi vinauzwa. Jambo hili linajulikana kwa wakuu tu.

Mifumo ya uteuzi wa maofisa wa makao makuu ya taasisi imevurugwa na siku hizi wakuu wa taasisi hasa mtendaji mkuu anateua na kutimua ofisa anavyotaka na mara nyingi bila hata kamati ya makatibu na wakurugenzi kujua. Mambo haya yanafanyika mbele ya macho na masikio ya mkuu wa taasisi jambo ambalo linazidi kuthibitisha kwamba mkuu na mtendaji mkuu wanajuana na wanafanya kwa kulindana.

NANI TUMUUNGE MKONO KUCHUKUA NAFASI YA MKUU:
Baada ya utangulizi huo unaoonyesha kinagaubaga kwamba tunahitaji mabadiliko, hatua iliyofuata ilikuwa ni kuangalia nani anaweza kuleta mabadiliko tunayohitaji. Ni vema ikazingatiwa kwamba mtu ambaye tungemuunga mkono lazima awe ni mtu mwenye uwezo mkubwa kuliko tunayetaka kumtoa. Awe ana qualities za kiuongozi na zaidi sana awe na uwezo wa kupambana na mkuu aliyeko. Tukileta mtu asiyefahamika sana kwenye mifumo ya taasisi yetu hata kama angekuwa mzuri kiasi gani hatachagulika na mkuu aliyeko atarudi kwa urahisi na kuendelea kuididimiza taasisi.

Katika kuchunguza ndani ya taasisi tuliridhika kwamba mtendaji mkuu msaidizi ana sifa zote tulizozitaja hapo juu ingawa kila mwanadamu ana udhaifu wake. Ni dhahiri pia kwamba udhaifu wa mtendaji mkuu msaidizi unarekebika kuliko wa mkuu aliyepo. Kwa ujumla mtendaji mkuu:

Ni kiongozi anayeweza kuongoza taasisi bila kujenga makundi akijali zaidi kazi ya taasisi kuliko maslahi binafsi.
Ameonyesha kwa vitendo kwamba hana maslahi binafsi kwa kuwa tumeshuhudia akifanya kazi nyingi za taasisi bila kudai malipo kwa njia ya posho ama vinginevyo.

Anaheshimika na viongozi wa ndani na nje ya taasisi jambo ambalo ni la muhimu sana kwa ustawi wa taasisi na kwa yeye kuwa mkuu wa taasisi tunatarajia wakubwa wengi sana kutoka nje ya taasisi yetu kuiamini na hata kujiunga nasi katika kuhakikisha tunafanikisha lengo la taasisi.

Ni msomi wa kiwango cha juu na mwenye uwezo mkubwa katika kuchanganua mambo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii, kimichezo, nk jambo ambalo ni muhimu sana kwa kuwa ni hatari kuwa na kiongozi asiye na ujuzi wa kutosha kwenye masuala kama hayo.
Ndani ya taasisi anakubalika kwa makundi yote ya vijana, wazee na akina mama.

Uongozi wa sasa wa taasisi yetu umefanya tuonekana kwamba taasisi yetu ipo kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi. Yote hii ni kwa sababu tumekuwa hatuna mbinu mpya za mapambano zinabadilikabadilika zaidi ya maandamano ya kila mara. Kwa kuzingatia utamaduni wa watanzania wa kupenda amani, kuna haja ya kufuta hii taswira na njia rahisi ni kubadilisha uongozi wa taasisi haraka iwezekanavyo.

Uelewa wake wa mambo ya kiuchumi ni muhimu sana kwa taasisi kwa sasa. Tunahitaji kuja na vyanzo vipya vya mapato ikiwa tunahitaji kufanikiwa. Mkuu aliyepo si kwamba ameishiwa bali hana mbinu za maana za kuiimarisha taasisi kimapato kwa ajili ya malengo yake ya mbele.

Exposure kubwa na kukubalika katika siasa za kimataifa. Tunahitaji kiongozi ambaye anazifahamu siasa za kimataifa na anayeweza kuungwa mkono na viongozi wengi wa kimataifa. Ni hatari kutegemea utaweza kufanikisha malengo kama ya taasisi yetu bila mpango kabambe wa kuungwa mkono na jumuia ya kimataifa. Mpaka hivi sasa hakuna mpango wowote wala hata mchakato wa maana kuwa connected na jumuia ya kimataifa. Kiongozi wetu mkuu wa sasa yupo ‘too local’ na hana mawasiliano yeyote ya maana na viongozi wengine katika kanda na kimataifa. Ndio maana mkuu huyo na mtendaji wake mkuu wamekuwa hawaonekani katika matukio makubwa ya kimataifa. Hata katika kutoa maoni katika mambo makubwa ya kitaifa na kimataifa viongozi hawa hawapo. Kwa kifupi kwa sababu ya aina ya viongozi tulio nao, nafasi ya taasisi yetu katika nyanja za kimataifa haipo!

Aina na staili ya uongozi wa sasa wa taasisi yetu ni kina kwamba nchi hii haipo hadi taasisi yetu itakapochukua dola. Yaani tunafanya mambo kama kwamba tutaanza upya kabisa tukichukua dola. Ni kwa sababu tumegombana na kila mtu katika utawala wan chi, vikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama. Ukweli ni kwamba tutavihitaji vyombo hivi kabla na baada ya kuingia madarakani na ni ndoto kudhani kwamba tutakabidhiwa nchi kwa kugombana na kila mtu. Ni kwa sababu ya mtazamo kama huu ndio maana wakuu wetu wa sasa hawaonekani kabisa katika shughuli za kitaifa kama vile sherehe za uhuru wan chi, n.k.

Uwezo wa kuwaunganisha wasomi wa kada mbalimbali, wafanyabiashara wakubwa, watumishi wa umma na sekta binafsi, nk katika kupata muunganiko wa mawazo na kutoka na sera murua zinazogusa kila sekta. Hili la kuwashirikisha litaenda sambamba na kutoa elimu kwa wote waelewe na watuunge mkono. Tunasema hivi kwa kuwa watu wa kada mbalimbali hawajaelewa sera zetu juu ya mambo yanayowahusu mfano wafanyabiashara wakubwa, wawekezaji, wakulima, watumishi, wanafunzi,nk na hivyo hawajawa tayari kutuunga mkono. Kile kinachofanywa wakati wa uchaguzi kwa njia ya ilani ya uchaguzi na elimu kutolewa kwa njia ya kampeni majukwaani hakitoshi. Tunahitaji watu wajue tumeunda think tank kwa ajili hiyo na baadaye wajue nini kimetokana na think tank hiyo ili wajadili na kutoa maoni na hatimaye tutoke na kitu kinachokubalikwa na wananchi wote. Na tuna imani hilo tunayempendekeza ana uwezo nalo.

Kubwa zaidi ni kwamba alishaiangalia taasisi yetu na kuona mambo yanayohitaji mabadiliko na kujiangalia yeye na kuridhika kwamba ataweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji na ndipo mwaka 2009 aliamua kujitosa kuutafuta ukuu wa taasisi yetu kabla ya kuombwa kumwachia aliyepo.

SWOT ANALYSIS:
Kwa kutumia uchambuzi huu hapa chini wa uimara, udhaifu, fursa na vitisho ama vikwazo dhidi ya mtu tunayempendekeza, utaweza kutuonyesha kama tunayempendekeza ataweza kushinda vita iliyo mbele yetu. Kama SWOT inavyotaka, tutaangalia sifa njema alizonazo tunayemtaka ambao ndio uimara wake, tutaangalia pia udhaifu wake, tutaangalia fursa alizonazo na mwisho tutazingatia vitisho ama vikwazo vilivyopo. Ni muhimu tukaeleza kwamba katika SWOT analysis tunajikita kwa mambo yanayohusika moja kwa moja na uwezekano wa tunayemtaka, kuchaguliwa. Kwa hiyo kwa mfano utakuta kwamba katika sehemu hii hatutazungumzia sifa njema alizonazo tunayemtaka kama kiongozi lakini sifa hizo zikawa hazina ushawishi wa kuwafanya wajumbe wa kikao cha uchaguzi kumchagua.

Uimara wa tunayemtaka:
Ingawa si mmoja wa waasisi wa taasisi yetu, lakini ni mwana taasisi mkongwe akiwa amejiunga na taasisi yetu miaka miwili tu tangu ianzishwe na mwaka mmoja tangu isajiliwe rasmi na serikali.

Zaidi ya kuwa mwanataasisi mkongwe, hajawahi kujiunga na taasisi nyingine hapo kabla. Alijiunga na taasisi hii kabla hata haijajulikana kwa watu na alibaki kuwa mwana taasisi mwaminifu hata pale taasisi zingine zilipoonekana kuwa imara na maarufu zaidi ya hii.

Kutokana na vipengele ‘a’ na ‘b’ hapo juu, hakuna mtu hata mmoja anayeweza kusema mtu huyu alikuja kwenye taasisi yetu kwa ajili ya kutafuta maslahi kama vile uwakilishi kwenye chombo chetu kikuu cha uwakilishi hapa nchini.

Ni mvumilivu sana. Katika jitahada za wakuu waliopo kuhakikisha wanaendelea kukalia viti vyao, wamejitahidi sana kumpaka matope lakini amevumilia. Mahali ambapo wengine wangeshakata tamaa na kuhama taasisi, yeye alibaki kuvumilia mpaka imefikia wana taasisi wa ngazi za chini waliokuwa wanadanganywa kwamba mtu huyu ni msaliti, wameanza sasa kushtuka.
Ana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi.

Ana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Uwezo wake unachagizwa si tu na elimu yake ya darasani bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa.

Ni mzalendo wa hali ya juu anayeipenda nchi yake kwa moyo wa dhati. Amethibitisha hilo kwa namna anavyolitetea taifa letu katika medani za kimataifa na jinsi anavyolipigania ndani dhidi ya mafisadi na wasiolitakia mema taifa letu. Ni mwakilishi pekee aliyekuwa tayari kukosa mishahara ya miezi kadhaa kwa kuamua kusimamia ukweli kwamba kuna ufisadi ulifanyika mpaka akasimamishwa uwakilishi wake kwa mikutano kadhaa ya chombo chetu cha uwakilishi.

Katika kuzidi kuonyesha alivyo mzalendo tunaweza kusema hapa kwamba ni kiongozi pekee kutoka upande huu ambaye ameonekana sana kwenye mambo ya kitaifa kwa mfano kulipigania taifa letu katika mambo ya kimchezo, kutumia gharama zake kwenda nje ya nchi na kujifunza mambo mbalimbali yanayoweza kulisaidia taifa katika sekta nyeti kama mafuta, gesi na madini, nk bila kusahau kwamba amekuwa ndiye mwakilishi pekee aliyeongoza katika kuibua kashfa nyingi na nzito za ubadhirifu ndani ya serikali hata kufikia mawaziri kadhaa kufukuzwa kazi.

Mambo hayo tuliyoyataja kwenye vipengele ‘e’, ‘f’, ‘g’ na ‘h’ yamemfanya kuwa kiongozi wa kwanza kuwa maarufu sana katika taasisi yetu aliyewapiku hata viongozi wa serikali kwa umaarufu. Hii ya umaarufu ni sifa muhimu sana linapokuja suala la uchaguzi.

Uwezo wake wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi. Hata pale anapokuwa amepakwa sana matope na wenzake, anapopewa nafasi ya kujieleza huweza kuwashawishi watu wengi wanaomsikiliza. Hii itamsaidia sana siku ya kujieleza mbele ya kikao cha uchaguzi ambapo ataweza kupangua hoja zote dhaifu za kumpaka matope.

Ana uwezo wa kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama mwenzao, wanawake humwona kama mtetezi wao wakati wazee humwona kama kijana mwenye busara anayeweza kuelekeza kama kiongozi.

Ana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na ziara nyingi alizozifanya na kukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Mahusiano haya mazuri yanachagizwa na jinsi anavyotumia muda wa kuongea na viongozi wa ngazi za chini kuzungumza kwa lugha ya upole na kuelekeza viongozi wenzake bila kuwaonyesha dharau.

Si mtu wa kujipenda nafsi na katika kupambana umaskini wa watu badala ya umaskini wake, alifikia kuzikataa posho wanazolipwa wawakilishi wakati wakitekeleza majukumu ambayo kwayo wanalipwa na kuiomba ofisi ya chombo hicho kuzipeleka posho hizo kwa watu maskini.

Ana limu nzuri sana aliyoipata katika vyuo vinavyoeleweka kitaifa na kimataifa
Ni kijana na hii ni taswira njema kwa sababu taasisi yetu inaungwa mkono sana na vijana

Udhaifu wa tunayemtaka:
Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.

Kama ilivyo kwa maneno, kuna matendo pia ambayo mara nyingine huyafanya bila kuzingatia mazingira na wasikilizaji wake na hivyo kupunguza imani ya wana taasisi kwake.

Hali ya ndoa ya tunayemtaka kutoeleweka msimamo wake

Kuna wakati tunayemtaka hu-respondkwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka huonekana kufanya maamuzi kwaemotion zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kurespond.

Jambo lililoelezwa katika ‘d’ hapo juu humfanya tunayemtaka wakati mwingine kuonekana ana jazba sana kwa sababu akishataharuki na kuchukua maamuzi akingali kwenye taharuki huwa ni rahisi sana kuonekana anajibu mapigo kwa jazba sana.

Ustahimilivu: yaliyotajwa katika ‘d’ na ‘e’ hapo juu yanaashiria tunayemtaka si mstahimilivu sana sifa ambayo inahitajika sana kwa kiongozi.

Uwazi:
 Katika taasisi zetu hizi ni muhimu sana kuepuka kufanya mambo yote wazi wazi hata kama ni mema ama ni haki ya mhusika ama si makosa katika jamii tuliyomo. Kuna mambo ambayo ni haki ya mtu mfano mahusiano binafsi ya kimapenzi, kuwa na marafiki wa damu kutoka upande mwingine wa utawala, nk. Lakini mambo hayo ni muhimu wakati mwingine ama kwa kiwango fulani yakafanywa kwa siri kuepuka mitazamo potofu kwa unaowaongoza.

Fursa alizonazo tunayemtaka:
Utamaduni wa taasisi yetu wa kubadilisha wakuu wa taasisi kila baada ya vipindi vifupi ili kuleta maono mapya kwenye taasisi unampendelea tunayemtaka.

Udhaifu ulioonyeshwa na uongozi uliopo chini ya mpinzani wetu katika kutekeleza program mbalimbali za taasisi nyingi zikiwa zimebuniwa na wao wenyewe, pia ni fursa kwa tunayemtaka.

Udhaifu mkubwa ulioonyeshwa na uongozi uliopo kwenye ugawanyaji wa raslimali za taasisi kama vile fedha za ruzuku, michango mbalimbali ya wahisani na hata vifaa vya uenezi.

Kujitokeza kwa tunayemtaka kutaonekana kama fursa kwa wanataasisi kufanya mabadiliko makubwa na kuua kabisa ile propaganda ya kwamba taasisi yetu ni ya kabila fulani ama eneo fulani kwa kufanya reference kwa uongozi wa taasisi.

Hoja ya uongozi uliopo kushindwa kabisa kusoma taarifa za fedha tokea 2010 ikifahamika kwa wapiga kura inaweza kuwa machinjio kabisa ya uongozi uliopo na kumpa fursa kubwa tunayemtaka.

Imani ambayo wana taasisi wengi wanayo kwake. Utafiti mdogo unaonyesha kwamba bado jina la tunayemtaka linatamkika sana midomoni mwa wanataasisi pale wanapotajwa viongozi wa juu wa taasisi yetu. Hii inaonyesha bado wana taasisi wanayo imani kubwa kwake na kwa hiyo atakapopata fursa ya kupangua matope aliyopakwa atakuwa na nafasi kubwa ya kuchaguliwa.

Mpinzani wetu hana historia nzuri ya utendaji uliotukuka ndani na nje ya chombo cha uwakilishi. Hakuonyesha utendaji wowote wa pekee alipokuwepo kwenye chombo mwaka 2000 -2005 na hata alipopewa uongozi wa upande wetu ndani ya chombo tokea 2010 hadi leo 2013 hajafanya lolote la kutukuka ndani ya chombo hicho.

Mpinzani wetu hana uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi, jamii, utamaduni, michezo, nk. Si tuelimu yake ya darasani ni ya magumashi bali pia vipaji na akili ya kuzaliwa havijaonekana katika maisha yake.

Uzalendowampinzani wetu unatia shaka akiwa hajaonyesha lolote la maana katika kulitetea taifa letu kimataifa. Ingawa ameshapata nafasi lukuki ya kwenda nje ya nchi lakini mara zote akifika huko ni kuiponda tu nchi yake. Ingawa anayo majukwaa ya kufanya hivyo akiwa ameshakuwa mwakilishi mara mbili kwenye chombo chetu lakini hatujawahi kumsikia akiibua kashfa mahsusi ya ufisadi na kuisimamia zaidi ya yeye mwenyewe wakati fulani fulani kutuhumiwa kwa ufisadi mfano pale alipokopa kwenye shirika la umma na kugoma kulipa mkopo.

Katika kuzidi kuonyesha uzalendo hafifu wa mpinzani wetu tunaweza kuangalia jinsi ambavyo mpinzani haonekani kwenye mambo ya kitaifa. Hii ni fursa kwa tunayemtaka.

Mpinzani wetu si maarufu akilinganishwa na tunayemtaka na hivyo kumpa fursa zaidi tunayemtaka kumshindani mpinzani wetu kwenye uchaguzi.

Uwezo wa mpinzani wetu wa kujieleza kwa kujenga hoja pale anapopewa nafasi ni mdogo sana.

Mpinzani wetu hajazoea ushindani na changamoto. Ni mtu aliyezaliwa kwenye utajiri na anadhani pesa ni kila kitu. Ukimnyang’anya pesa ukamwambia ashindane kwa hoja hawezi na ndo maana anajaribu sana kuhakikisha anaingia mwenyewe ulingoni bila kupingwa.

Kutokana na tuliyoyasema hapo juu kwenye ‘m’ ni dhahiri kwambapale mpinzani wetu anaporushiwa kombora la kashfa anakuwa mzito kujieleza hata kama anapewa nafasi ya kufanya hivyo na hii ni fursa muhimu kwa tunayemtaka.

Mpinzani wetu ni mgumu sana katika kuchangamana na makundi yote ambapo vijana humwona kama si mwenzao kiumri na kifedha, wanawake humwona kama malaya anayependa kutumia miili yao kujistarehesha wakati wazee humwona kama mtu anayedhalilisha hata nafasi aliyopewa kwa kufanya uhuni waziwazi hata kuvunja ndoa si ya kwake tu bali hata za watu wengine.

Mpinzani wetu hana mahusiano mema na mazuri na viongozi wa ngazi za chini kutokana na dharau nyingi anazozionyesha pale anapokukutana na viongozi wa ngazi za chini akiwa katika kuijenga taasisi hii. Hutumia muda mwingi kuwaponda viongozi wenzake hata kufikia kutamka mara nyingi kwamba kama kiongozi hawezi kujigharamia nauli na malazi ya kutoka mahali fulani kwenda mahali fulani kwa siku kadhaa hafai kuwa kiongozi bila kujali kwamba kuna viongozi wetu wana moyo na taasisi hii na ndo wameifikisha hapa ilipo lakini hawana uwezo wa kifedha na hivyo kauli kama hizo za mkuu huyu huona kama anawadharau kwa kuwa yeye ni tajiri. Hii imemfanya kutopendwa na viongozi wengi wa ngazi ya chini hivi sasa na kutoa fursa ya pekee kwa tunayemtaka.
Mkuu aliyepo amekuwa na mkakati unaoitwa kuondoa watu wa zamani. Jambo hili linawaudhi sana viongozi wa ngazi za chini ambao wanaona kama baada ya kuifikisha taasisi mahali ilipo kwa sasa wanaonekana hawana maana tena. Wengi wamefikia kuapa kwamba kama mwendo ni wa kuwaondoa watu wa zamani basi na yeye ni wa zamani lazima aondoke.

Mpinzani wetu amejionyesha dhahiri kujipenda na kujijali nafsi bila kujali watu wa hali ya chini. Matukio mawili yanamwacha uchi katika hili pale alipolitangazia taifa kwamba wawakilishi wetu wote hawatachukua posho za vikao halafu yeye na wengine wote wanazichukua hadi leo na kumwacha mtendaji msaidizi peke yake. Na la pili linalofanana na hilo ni pale alipotangaza kutotumia gari la serikali ambalo ni la kifahari kisha akalirudia kimya kimya.

Kuwepo muhtasari wa kikao cha wazee ambacho mwaka 2009 kilimshauri tunayemtaka ajitoe na kumwachia mkuu aliyepo na kumtaka mkuu aliyepo kumwachia tunayemtaka katika uchaguzi ujao na wote wakasaini makubaliano hayo, nayo ni fursa muhimu sana kwa tunayemtaka.

Mkuu aliyepo anaamini kwamba ameshamsambaratisha tunayemtaka na hivyo kwa sasa amebweteka na hiyo inatupatia sisi fursa kuendelea kuimarisha mtandao wetu.

Kwa kuwa ni mwislamu. Hii ni fursa katika kupata kuungwa mkono na wanachama waislamu ambao wamekuwa na kigugumizi wakidhani waislamu hawatakiwi katika uongozi wa taasisi yetu.

Elimu ndogo na duni aliyenayo mpinzani wetu ambaye ndiye mkuu wa taasisi yetu kwa sasa. Kwa sasa ni kiongozi pekee katika nchi yetu anayeongoza taasisi kubwa asiye na elimu ya shahada huku taasisi yetu ikiwa inaongoza kwa kuwa na wasomi waliobobea katika kila nyanja. Hii ni kejeli hasa kwetu sisi ambao tumekuwa tukiwasema wenzetu kwamba ‘akili ndogo’ inaongoza akili kubwa. Kimsingi tumekuwa tukijisema kwa kukubali kuongozwa na mtu mwenye akili ndogo.

Mkuu wa sasa kutokuwa na msimamo thabiti katika mambo ya msingi. Rejea swala la maandamano ya kumshinikiza Kawambwa ajiuzulu na kujitoa katika mchakato wa katiba.

Vikwazo dhidi ya tunayemtaka:
Sisi wenyewe tunaoandaa mkakati huu hatuna uhakika kama tunayemtaka yuko tayari na yuko serious na business hii, na kwa hiyo huenda tusifanye kwa nguvu zetu zote ikiwa hatutapata nafasi mapema ya kukutana na mhusika na akatuhakikishia kwamba yuko serious.

Utayari wa mhusika mkuu kutekeleza yale tunayokubaliana. Inapotokea baada ya kukubaliana sisi na yeye akapata ushauri tofauti na ukauona uko more genuine, basi tuwasiliane kwamba nimeshawishika kufanya hivi badala ya vile tulivyokubaliana kwa sababu hizi ama zile. Hii haitatukatisha tamaa tofauti na kama tutakuwa tunapanga hivi halafu yeye anafanya vile bila maelezo yoyote
Kitendo cha mkuu aliyepo kung’ang’ania kuendelea nayo ni kikwazo kwa kuwa baada ya kuwa madarakani kwa miaka yote hiyo lazima amejipatia watu wanaomhusudu ama kumpenda ama kumkubali na kuwepo wengine wanaoogopa tu kwamba mkuu aliyepo akitoka taasisi itakufa hata kama hawana sababu yoyote.

Tunatazamia mkuu aliyepo atafanya vitendo vingi zaidi vya haramu katika kumdhibiti tunayemtaka pale tunapoelekea kwenye uchaguzi wenyewe.

Raslimali za taasisi kutumiwa na viongozi waliopo katika kumsaidia mkuu aliyepo wakati wa kwetu anatumia raslimali zake za mfukoni.

Propaganda chafu zilizokwishapigwa dhidi ya tunayemtaka zimepunguza imani ya wanataasisi kwa tunayemtaka kwa kiasi fulani
Baadhi ya mambo ambayo amekwishayasema ama kuyatenda nayo yameshawapunguzia imani kiasi fulani wanataasisi mbalimbali.
Kutoonekana sana kwenye operations za taasisi yetu pia kumewapa wasiwasi baadhi ya wanataasisi.

Muhtasari wa SWOT analysis unaonyesha kwamba strength na opportunities za tunayemtaka ni nyingi sana zikilinganishwa na weaknesses zake na threats dhidi yake. Aidha ukichambua zaidi utaona kwamba weaknesses za tunayemtaka nirepairable na vikwazo dhidi yake pia ni rahisi kuvikabili na kuvisambaratisha. Tukishamaliza maandalizi ya mkakati huu tukaonana na mhusika mkuu na kumpa ushauri akatulia na kufanya kazi, mkuu aliyepo hatafua dafu. Tunahitaji kutekeleza mkakati huu kwa siri kubwa ili mkuu aliyepo aendelee kubweteka na ndiyo maana hata lugha iliyotumika ni ndani hapa ni ya pekee. Tunahitaji tunayemtaka asionekane kama kuna kitu anafanya na tunafurahi kwamba kuna wakati alitangaza kwamba hana nia ya kugombea tena waliopo wanatosha. Ikitokea vyombo vya habari vikamuuliza tena hiyo ndiyo iwe kauli yake ili kuendelea kumfanya mkuu aliyepo asihangaike na hivyo kuja kummaliza kirahisi. Aidha katika utekelezaji wa mkakati kama tutakavyoeleza hapo baadaye, tunayemtaka atajitenga mbali asionekane hata kuwa karibu na sisi. Vikao vyetu na yeye vitafanyika mara chache sana na mahali pa faragha kupita kiasi ikiwezekana hata nchi jirani.

Mkakati huu hautatakiwa kupatikana kwenye komputa zaidi ya tatu yaani ya mchapaji ambaye ni M3, ya M3 na ya MK mwenyewe. Hata hivyo email zitakazotumika kusafirisha mkakati huu kutoka kwa M3 kwenda kwa M1 hadi kwa MK hazitakuwa zile za kawaida za hao watu bali mpya kabisa zilizofunguliwa kwa makusudi haya tu na kwa majina fictitious. Aidha kila atakayekuwa na mkakati huu kwenye computer yake anatakiwa kuliwekea file hilo password ili hata mtu wa karibu naye anayeweza kufungua computer yake asiweze kulifungua file hilo. Pia email address hazitatolewa kwa sms bali kwa kupiga na kuambiana spelling za address.

MTANDAO WA USHINDI:
Mtandao wa ushindi utakuwa kama ifuatavyo. Kwenye ngazi ya kitaifa tutakuwa na kamati yenye members watatu tu. M1 ndiye atakayekuwa anawasiliana na tunayemtaka ambaye ataitwa MM (Mhusika Mkuu). Tumepanga kwamba kusiwe na mawasiliano mengi kati ya kamati na mhusika mkuu kuepuka tracking ya wapinzani wetu. M1 ni mtu wa karibu na MM kwa hiyo mawasiliano yao hayataweza kutiliwa shaka na mtu yeyote hata wangewasiliana mara nyingi kiasi gani. Hata hivyo, linapokuja suala la mkakati huu tunasihi mawasiliano yawe kwa kuonana uso kwa uso ama kwa simu na si sms. M1 ndiye atakayewasilisha mambo yote yanayotoka kwenye kamati ya kitaifa na endapo kuna haja ya MM kukutana na kamati ya kitaifa, mipango yote ya kikao itafanywa na M1 kwa usiri mkubwa. M2 ni mtu ambaye yuko kwenye ofisi kuu za taasisi yetu wakati M3 ndiye mchapaji wa mkakati huu.

Kamati hii imefanywa kuwa na members wachache sana wenye uelewa mpana wa mambo na wenye elimu nzuri ili kuhakikisha kazi inafanyika kitaalam na kwa uhakika sana. Kamati ya kitaifa itapeleka mapendekezo yake kwaMM na yeye pia ataleta ushauri wake kwa kamati kama mishale inavyoonyesha. Chini ya kamati ya kitaifa kutakuwepo waratibu wa kanda zote kumi watakaojulikana kama MK1 – MK10. Hawa watatafutwa na kusimikwa na kamati ya kitaifa kwa kushauriana na MM kwa utaratibu utakaokubalika na pande zote yaani MM na kamati ya kitaifa. Chini ya waratibu wa kanda kutakuwapo waratibu wa mikoa yote 30 (MMK1 – MMK30) ambao watapatikana kwa utaratibu ule ule wa kuwapata waratibu wa kanda. Isipokuwa pale ambapo inakuwa ngumu, itabidi kamati ya taifa isaidiane na waratibu wa kanda kuwapata waratibu wa mikoa lakini kamati itashauriana na MM kabla ya kuwasimika rasmi hao waratibu wa mikoa.Mtandao utakuwa kama inavyoonyeshwa kwenye mchoro ufuatao:
NAMNA YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Kazi itagawanywa katika awamu tatu:
Awamu ya kwanza ni kuanzia sasa mpaka uchaguzi wa ngazi ya matawi utakapoanza. Katika awamu hii kazi ni kuhakikisha kwamba mtandao mzima umekamilika mpaka kwenye ngazi ya mkoa. Kazi nyingine itakayofanyika ni kwa waratibu wa mikoa kuendelea kuspot makada kwenye wilaya na mikoa ambao tayari wana mtazamo tulio nao ama ambao wanaweza kuingiziwa kirahisi mbegu hii ya mabadiliko na wakawa tayari na wana uwezo na sifa za kushinda uongozi kwenye wilaya na mikoa yao bila kusahau sifa ya kuwa waaminifu wenye uwezo wa kutunza siri. Kulingana na muda hii ni kazi inayotakiwa kufanyika sasa lakini kwa uangalifu mkubwa. Ni muhimu kukumbushana hapa kwamba katika awamu hii hakuna anayetakiwa kujua mpango mzima zaidi ya kamati ya kitaifa na MMili kuhakikisha uwezekano wa mkakati wetu mapema kwa wapinzani wetu unakuwa minimized to almost zero.

Awamu ya pili ni kipindi kuanzia uchaguzi wa matawi mpaka uchaguzi wa mikoa unapokamilika. Katika awamu hii tutasaidiana na waratibu wa kanda na mikoa kuhakikisha makada tuliowaspot kwenye wilaya wanapanga safu zao kwenye kata ili kuhakikisha watakaochaguliwa kwenye kata ni watu wao ili waje wawachague kwenye wilaya.Vivyo hivyo kwa makada tuliowaspot kwenye mikoa wahakikishe wanaochaguliwa kwenye wilaya ni wale makada wetu ili nao waje wawachague kwenye mikoa yao. Hapa ndipo kwenye kazi kubwa ya mkakati wetu na hapa ndipo tutakapohitaji kuingia gharama zaidi kwa ajili ya kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia angalau 80.

Awamu ya tatu ni kuanzia baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa mikoa hadi uchaguzi wa kitaifa utakapoitishwa. Katika kipindi hiki kwa ustadi mkubwa tutakuwa tukiwaandaa makada wetu waliochaguliwa tayari kuja kufanya mabadiliko makubwa kitaifa. Ni wakati huu ambapo tutawaingizia mkakati taratibu lakini kwa ustadi mkubwa tukijikita hasa kwenye kuonyesha kwa nini tunahitaji mabadiliko. Ni katika kipindi hiki ambapo kwa ustadi mkubwa tunaweza kuwaspot wale waliochaguliwa ambao hatukuwaandaa na kuwaingizia pia mbegu ya mabadiliko ili kuwawin na kuwarecruit kwenye mkakati.

Aidha katika awamu zote tatu kazi ya kuianalyze ofisi kuu itakuwa non stop kwa kuzingatia kwamba mabadiliko ya wakurugenzi na maofisa yatakuwa yanatokea na watu nao watakuwa wanabadilika kimtazamo. Analysis ya ofisi kuu ni kuhakikisha tunajua nani na nani wako na sisi na nani na nani wako against na pia nani na nani wanaweza kupandikiziwa mbegu kwa ustadi na wakaungana nasi.
MAHITAJI YA KUFANIKISHA MKAKATI:
Raslimali watu. Tunahitaji watu waaminifu watatu kwenye ngazi ya kitaifa ambao tayari wapo. Tunahitaji watu waaminifu kumi kwenye kanda ambao tutawatafuta na pia waaminifu wengine 30 kwenye mikoa yote thelathini.

Fedha. Tunahitaji fedha kwa ajili ya mawasiliano kati ya wanakamati na wale wa ngazi ya chini. Aidha tunahitaji fedha kwa ajili ya gharama za usafiri pale tutakapohitaji kwenda kwenye kanda na mikoa husika kwa ajili ya kusimika watu hao tunaowahitaji.

MAPENDEKEZO MAHSUSI NA HITIMISHO:
Katika kuhitimisha tunapendekeza mambo mahsusi yafuatayo:

Kuhusu Bajeti:
Tunapendekeza kwamba bajeti ya mkakati huu isipangwe hivi sasa. Ni muhimu tu sote kuelewa kwamba wakati wenzetu wanatumia raslimali za taasisi kujijenga na kutekeleza mkakati wao wa ushindi, sisi tunapaswa kuingia mifukoni. Kwa kila kila mmoja wetu atakuwa budget conscious ili kuepuka matumizi makubwa ya pesa. Hata hivyo, kwa kuzingatia kwamba lazima pesa inahitajika ni muhimu M1 na MM kujaribu kuangalia namna ya kuraise pesa na kushauri. Otherwise, tutakapokuwa tunahitaji kufanya hatua yoyote ama jambo lolote tutakuwa ndo tunapiga hesabu za funds tunazohitaji kwa jambo husika na kuingia katika utekelezaji.

Kuhusu mwenendo wa MM kuanzia sasa:
Ni maoni yetu pia kwamba kuanzia sasa MM aenende katika mwenendo ambao utarahisisha ushindi. Mfano tunapendekeza afanye yafuatayo kuanzia sasa:

Apunguze ukaribu na viongozi wa serikali na wa chama tawala na awe crical zaidi na utendaji wa serikali nje na ndani ya bunge.
Ashiriki kikamilifu katika shughuli za taasisi yetu zikiwamo vikao vyote vinavyomhusu, operesheni mbalimbali, chaguzi ndogo, nk.
Aendelee kushusha ‘nondo’ ndani ya chombo chetu cha uwakilishi na kuendelea kuwa juu ya wawakilishi wengine katika hoja mbalimbali zenye maslahi ya kitaifa.

Ajitahidi kudhibiti jazba hata pale anapokuwa amebambikiziwa tuhuma nzito namna gani. Atulie, ashauriane na wazee ili kuona namna nzuri ya kujibu tuhuma zinazomkera. Tukumbuke kwamba wakati mwingine kukaa kimya ni jibu zuri zaidi kuliko hoja nzito.
Sambamba na ‘iv’ hapo juu, adhibiti sana emotion ili kuhakikisha kila kitu kinachofanywa ama kuzungumzwa kinachomgusa asikimbilie kuongea na vyombo vya habari ama kwenye mitandao ya kijamii bali afuate kile tulichokizungumza kwenye kipengele cha ‘iv’ hapo juu.

Kuhusu mapambano ya kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii:
Katika hili sisi hatukuona haja ya kufanya hivyo kwa sababu mbili:
Imani yetu kwamba taasisi yetu ni kubwa kuliko watu kwa hiyo ni muhimu kuzingatia kwamba hatuiui taasisi katika mapambano haya. Tukiendekeza mashambulizi kwa njia ya mitandao ya kijamii hatutakuwa na ngao ya kuwakinga watu wa kawaida (wanataasisi na wasio wanataasisi) dhidi ya kujikuta wakiamini kwamba taasisi hii nayo haina jipya ni sawa tu na ile tunayotaka kuitoa.

Tutakuwa tumeiua taasisi na mkakati huu hautakuwa na maana sana kama lengo ni kufanya mabadiliko ya uongozi wa taasisi tu lakini malengo ya taasisi ya mwaka 2015 yasitimie!

Kujikita kwenye mashambulizi kupitia mitandao ni kuzidi kuwashtua wakuu waliopo kwamba bado tuko serious na mkakati wa kuwatoa na kuwafanya wafanye kazi zaidi huku wakiendelea kumpaka matope MM kwamba ndiye anayerusha makombora hayo kwenye mitandao kwa kusudi la kuhujumu taasisi maana hiyo ndo lugha yao. Hatukatai kwamba wakuu wanajua kabisa kwamba bado MM ana nia ya kumvaa mkuu aliyepo lakini tunajua kwamba kwa sasa wanaamini wamemdhoofisha na hana madhara tena. Ndiyo maana tunataka kutekeleza mkakati wetu kwa siri sana ili wafikiri MM amekata tamaa kumbe ndo anakuja na mkakati mzito zaidi.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbushana kwamba wenzetu hawatanyamaza kwa sababu eti sisi tumeacha kuwashambulia kwenye mitandao ya kijamii. Lazima wataendelea! Wataendelea kumchafua MM kwa kupitia wapuuzi kama yule kichaa wa ‘ars’ na kundi lake. Nini tutakuwa tunakifanya sasa? Tutahakikisha tuko busy kupost mambo mema na mazuri yatakayokuwa yakifanywa na MM kila wakati na kuzidi kusambaza sifa zake njema kila inapotokea nafasi. Atakayefanya kazi hiyo ni sisi wengine wala si yeye! Pia tutahakikisha kila post ya kumchafua inapatiwa majibu bila kutumia ID yake inayojulikana. Ni vema aidha akatupatia majibu na sisi kuyapost ama afungue ID mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwepo kwenye mitandao halafu ndo awe anazitumia kujibu lakini kwa kuzingatia tuliyokwishayazungumza hapo juu yaani kutofanya kwa emotion na kuepuka jazba lakini pia kushauriana na watu wa karibu kabla ya kutoa majibu kwa jambo lolote linalomhusu.

Kuhusu kamati ya kitaifa (hususan M2 & M3):
Tulikubaliana kwa kauli moja kwamba katika kutekeleza mkakati huu tunahitaji members hawa wawe wametulia kimaisha. Inakuwa vigumu kwa mfano kumtaka member aende mahali fulani kwa makusudi ya mkakati huu wakati hajui familia yake nyumbani anaiacha inakula nini. Tuliona kwamba M3 tayari hana kazi kwa sasa tena kwa kufanyiziwa na wakuu waliopo. Ni katika mwendelezo huo huo tunamwona M2 naye akiwa ukingoni kupigwa nje na kuachwa mtupu na wakuu waliopo katika kile wanachokiita wao reshuffle ya ofisi kuu. Kwa sababu hiyo tukapendekeza kwamba MM kwa kushirikiana na M1 kwa hatua ya kwanza wanaweza kutafuta kiasi cha sh. 2m kila mmoja tukijua kwamba kama members hawa wawili wakisaidiwa milioni mbili mbili wanaweza kuanzisha projects ambazo zitawasustain hata kama hawana ajira. Kwa hatua ya baadaye tutasaidiana kuona kama hawa members wanaweza kusecure good employments mahali, provided hazitawazuia kufanya siasa.

SIWEZI KUMVULIA DIAMOND CHUPI YANGU HANA HADHI YA KUTEMBEA NA MIMI-LULU

$
0
0
Msanii wa filamu bongo,na mwenye jina kubwa kuliko umri wake,Elizabeth Michael aka LULU, ameonesha msimamo mkali baada ya msanii wa bongo fleva mwenye jina la madini expensive Naseeb Mohamed au DIAMOND kufanya kila aina ya mbinu ikiwemo ile ya kutaka kumuagizia msanii huyo gari expensive aina ya nissan murrano yenye thamani ya shiling million zaidi ya 60,ambapo hata hivyo mbinu yake iyo imeonekana kugonga mwamba baaada ya Lulu kukataa kata kata kutoka na staa huyo anayetamba na ngoma ya my number one.

Kwa kumaanisha kuwa hataki kutoka na staa huyo, Lulu alilazimika kubadilisha namba ya simu yake ya mkononi ili kuepuka usumbufu kutoka kwa bwana mdogo huyo ambaye kila kukicha amekuwa akiwindwa na wasichana warembo ili tu waonje sukari yake. 

Pia inasemekana lengo la diamond kutaka kutoka na Lulu ni kutaka kukuza jina lake(kiki) kwa kuwa anaamini staa huyo ana jina kubwa na lenye mvuto hivyo kumfanya na yeye aogelee kwenye dimbwi la umaarufu na kuongelewa zaidi na watu,na kuwa ishu iyo ndo itakuwa habari ya mujini yaan yeye kutoka na lulu.

Baadhi ya watu wameonyesha kushangzwa sana na msimamo mkali wa binti huyo,kwa kuwa waliamini hakuna staa yeyote bongo mwenye ubavu wa kupindua kwa diamond,kama ilivyokuwa kwa Wema,Jokate,Aunt,Wolper na baadhi ya mastaa ambao dogo huyo aliwamega kiulaini. 

Watu wanahaha kumjua mwanaume anayempa jeuri Lulu hadi kufikia hatua ya kuchomoa kwa diamond..

HUYU NDIYE DIRECTOR ALIEFUKUZWA KAZI NA WEMA SEPETU BAADA YA KUGEUZA GARI YA WEMA CHUMBA CHA KUFANYIA NGONO.

$
0
0
Taarifa za sababu kubwa zilizopelekea Wema Sepetu kumtimua aliyekuwa director wake maarufu kwa jina la Chid ni ufuska uliokubuhu wa director huyo ambaye alikuwa akitumia magari ya Wema Sepetu kama gest ya kumaliza haja zake. 
Wema aliamua kuchukua maamuzi hayo magumu ili kunusuru kashfa kubwa ambayo ingeweza kuikumba kampuni yake 
Habari zaidi zinaarifu kuwa baada ya kupata taarifa hizo Wema aliamua kumtimua Chid kwenye kampuni yake ili kulinda heshima ya kampuni hiyo ambapo Chid na vijana wengine walikuwa wakitumia gari hiyo kung'olea watoto wakali na kuwachapa ndani ya gari hiyo. 

"Hii ilitokana na upendo wa mashabiki kwa Wema na wasichana wengi walikuwa wakiiona ile gari wanaingia wenyewe kwenye gari wakidhani ndani yuko Wema, hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwa Chid na wenzake kuwamaliza wasichana hao"

RIDHIWANI KIKWETE ALAANI SIASA ZA CHUKI ZA CHADEMA ZILIZOFANYA ZITTO NA WENZAKE KUVULIWA MADARAKA

$
0
0
Baadhi  ya watu maarufu  nchini akiwemo  mtoto wa Rais Kikwete, Ridhiwan wamezipokea taarifa za kuvuliwa wadhifa wa unaibu Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa Zitto Kabwe kwa mitazamo tofauti.

Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho.
   Haya  ni maoni  ya  Ridhiwani  Kikwete  aliyoiweka  katika ukurasa  wake  wa  facebook na  twitter kuhusiana  na  sakata  hilo:

Naendelea kujifunza matunda ya Siasa za Chuki na Ukanda zinavyoumiza siasa za Tanzania. Mungu anatuasa kupitia vitabu vitakatifu kuwa ” ili kuepusha balaa dogo kutokea, basi liwe balaa kubwa zaidi ya hilo.”. Imani kuwa aliloandika limetimia… 


Zitto Kabwe pamoja na Dk Kitila Mkumbo watakutana na wahariri na waandishi wa habari  kesho Jumapili  kuzungumzia hatua hiyo

MR.BLUE AGEUKA TAPELI..!! AKOMBA PESA ZA WATU NA SASA ANATAFUTWA NA POLISI HUKO NCHINI KENYA

$
0
0
Hitmaker wa ‘Mapozi’ Mr. Blue aka Kabayser anatafutwa na polisi wa Kenya kwa Utapeli.

Msanii huyo anatafutwa kwa shutuma za kushindwa kutokea kwenye show aliyokuwa amesaini mkataba huko Mombasa, Kenya. Mr. Blue alikuwa anatakiwa kutumbuiza kwenye maeneo ya Office Restaurant, Likoni na Mariakani Jubilant Hotel, November 16 na 17.
Mratibu wa show hiyo, Sammy Ondwar Onyango, aliamua kwenda kushtaki polisi sababu anadai alikuwa ameshamlipa msanii huyo sehemu ya malipo waliyokuwa wamekubaliana.
“Mr Blue si mtu mwaminifu kabisa. Aliwahi kuniangusha pia mwaka 2012 kwenye show ya Jet Bar, Likoni, baada ya kudai kuwa alikosa basi ya kwenda Mombasa na nililazimika kuingia zaidi mfukoni kumlipia basi jingine,” Onyango aliliambia gazeti la The Star.
Promota huyo amesema kwenye tukio la sasa, walikubaliana kumlipa shilingi 100,000 (za Kenya) ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.8  na tayari alikuwa ameshamlipa shilingi 40,000 kupitia M-Pesa.
Kesi hiyo imeripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Likoni.
Gazeti hilo limesema baada ya kuwasiliana na Mr Blue kwa simu, aliweza kujibu kwa ujumbe mfupi wa simu kwamba alikuwa akiendesha gari na simu haikupatikana tena

BABY MADAHA"UTUNDU KITANDANI NDIO SILAHA YANGU KUWAPAGAWISHA WANAUME NAYAJUA MAPISHI"

$
0
0

Wakati  kukiwa  na  madai  kuwa  msanii Baby  Madaha  anatumia  dawa  za  kienyeji  kuwateka  wanaume  kimapenzi, mrembo  huyo  ameibuka  na  kusema  kuwa  siri  ya  kuwateka  wanaume  ni  utundu  wake  kitandani....
Akiongea  na  mwandishi  wetu, Baby Madaha  amedai  kuwa  tuhuma  za  kutumia  dawa za  kienyeji  hata  yeye  amezisikia   tu, lakini  wote  wanaomtuhumu  hivyo ni  kwamba  hawamjui  yukoje  anapokuwa  kitandani...
Alisema  kuwa  utundu  wake  anapokuwa  kitandani  ndo  siri  ya  kuwateka  wanaume  kwani  huzingatia  sheria  na  kanuni  zote  za  maandalizi  ya  tendo  hilo  pindi  awapo  na  mteja  wake  kitandani....
Madaha  aliongeza  kuwa  hata  huyu  mkenya  aliye  naye  watu  wanasema  kamuwekea  dawa.Ukweli  ni  kwamba  yeye  hajatumia  dawa  yoyote  bali karidhika  na  mapishi  yake  ya  chumbani...
"Situmii  dawa  yoyote.Ni  ufundi  wangu  tu  ninapokuwa  kitandani  na  mwanaume. Nayajua  mapishi  na  najua  njia  zote  za  kumpagawisha  mwanaume  hata  awe  mgumu  kiasi  gani"...Alisema  baby Madaha

BLOGS ZINAVYO MKERA RAIS KIKWETE"TETEENI NCHI NA SI KUIPONDA KWENYE BLOGS"

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kukerwa na tabia ya baadhi ya watanzania wanaotmia muda wao mwingine kwenye mitandao ya kijamii Blogs kuiponda nchi yao, Akizungumza na Watanzania waishio nchini Pland alisema kwamba, "Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu", Rais Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania. Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa jana, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya, viongozi hawafai..mnapata faida 

gani. Mnazo nchi ngapi?”Rais Jakaya Kikwete akitafakari jambo juu ya utawala wake

Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba mtasukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu.

Fursa zilizoko hapa mnazijua wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?.

” Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. “Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi.”

Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya. “Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi nyumbani.

"Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu.”

Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao. 
 Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike. Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: “Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa.”

MAMA ZITTO AFUNGUKA "NILIKUWA NAOMBA KILA SIKU ZITTO AFUKUZWE CHADEMA"

$
0
0
Dar es Salaam. Siku moja baada ya Kamati Kuu ya Chadema kumvua uongozi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Taifa wa chama hicho, Zitto Kabwe, mama yake mzazi, Shida Salum ametoa ya moyoni akieleza kuwa kilichomkuta mwanaye kimefunika mabaya mengi yaliyopangwa afanyiwe.

“Kwa upande wangu naona kama ni ushindi kwa Zitto kutokana na jinsi ninavyojua hali ilivyo, mambo yalikuwa ni mengi mno na nikwambie tu, Zitto kuvuliwa uongozi kumefunika hayo yaliyokuwa yamekusudiwa kufanywa dhidi yake. Nilikuwa naomba Mungu  kila siku ili afukuzwe Chadema,” alisema mama huyo wakati akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake Tabata, Dar es Salaam.

Shida Salum alisema kuwa Mungu amemnusuru mwanaye na kusisitiza, “Watu walikaa na kutengeneza ripoti ya siri kuhusu Zitto na kuiweka kwenye mtandao kisha kuituma kwa wanachama wa Chadema wanaowafahamu. Mpaka wanafikia hatua hiyo maana yake ni kwamba wamejaribu njia zote za kummaliza, lakini wameshindwa.”

Alisema kutokana na hali ilivyo hivi sasa amemnyang’anya mwanaye kwa muda simu zake zote za mkononi, kompyuta mpakato (Laptop) pamoja na iPad ili asiwasiliane na watu, kwa maelezo kuwa wapo wenye nia mbaya wanaomsaka kumpa pole za kinafiki. “Kwa sasa nataka mwanangu atulize akili.”

Shida Salum, mbali na kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, pia ni  mwasisi wa  Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata) na Mwenyekiti wa Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Viungo (Chawata).

Zitto pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Dk Kitila Mkumbo juzi walivuliwa uongozi kutokana na uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kilichokutana kwa siku mbili, kuanzia Novemba 20 mwaka huu katika Ukumbi wa Blue Pearl jijini Dar es Salaam, wakituhumiwa  kukisaliti chama.

Mbali ya kuwavua uongozi Zitto, Dk Mkumbo pamoja na  aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Arusha, Samson Mwigamba, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama.

Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).

Katika ufafanuzi wake wa jana, Shida aliwataka wanachama wa Chadema kuwa watulivu kwa maelezo kuwa Zitto hajafukuzwa uanachama, “Siku nyingi walikuwa wanamwinda na hata hilo jambo ambalo Chadema wanasema amefanya, hawana uhakika nalo.”

Juzi wakati akisoma uamuzi wa Kamati Kuu,  mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema wamebaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.

Alisema kikundi hicho vinara wake wapo wanne,  Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne ambaye alieleza kuwa hajatambulika na anatumia jina la M2.

Mama Zitto ambaye wakati akizungumza na gazeti hili alikuwa amelala kutokana na kusumbuliwa na maradhi alisema, “Kutolewa katika uongozi ni jambo la kawaida.  Zitto hajafukuzwa chama ila anaweza akafukuzwa maana kapewa siku 14 tu za kujieleza.”

Alisema kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, kwamba chama hicho walimwondoa Aman Kabourou (aliwahi kuwa Mbunge wa Kigoma Mjini-Chadema)  itakuwa Zitto, inaonyesha jinsi watu walivyo na chuki na mwanaye.

“Hayo ni maneno ya chuki, maana hata Zitto naye ana watu wake ambao wanaweza kutengeneza aina fulani ya chuki kwa viongozi wa chama na wanaweza kupata wakati mgumu kufanya safari au mikutano yao mikoani,” alisema.

Alisema tangu siku nyingi ndani ya Chadema kulikuwa na mpango wa kumng’oa Zitto, akifafanua kuwa hata katika kikao cha Kamati Kuu iliibuliwa hoja ya ruzuku za vyama, huku wajumbe wakimshutumu Zitto kwamba kwa nafasi yake na Naibu Katibu Mkuu alitakiwa kuitetea Chadema kuhusu ruzuku.

Katika vikao vya Kamati ya PAC, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.

“Zitto alipoingia katika kikao cha Kamati Kuu alishikilia msimamo wake kwamba kama Chadema inachukia ufisadi, nacho lazima kihakikishe kinakaguliwa,” alisema na kuongeza;

“Wao wanaona ili waweze kusalimika katika suala hili la ruzuku ni lazima wamfukuze Zitto. Chadema hawako sawa, hesabu zao haziko sawa.”

Alisema kuwa tatizo lililopo ni kuwapo kwa mkakati wa watu fulani kuiyumbisha Chadema , hivyo kila juhudi zinafanywa ili kukitingisha chama hicho kipoteze mwelekeo.

“Siwezi kusema wamemwonea au hawajamwonea, wao wametumia waraka wa Mwigamba ambao Zitto amekiri katika Kamati Kuu kwamba hajawahi kuusikia wala kuuona, tofauti na Dk Kitila ambaye amesema amewahi kuuona,” alisema na kuongeza;

“Zitto anahusishwa na kitu ambacho Chadema hawana uhakika nacho, ukiusoma ule waraka katika aya ya mwisho umeandikwa hivi, ‘Huyu mtu tunayefikiria awe mwenyekiti hajaoa,

tumshauri aoe akikataa tutafute mtu mwingine’, maana yake ni kwamba waraka huo ulikuwa haujamfikia Zitto, kama ungekuwa umemfikia Zitto watu hao wasingemwomba Zitto agombee uenyekiti.” Alipoulizwa nafasi yake ndani ya Chadema kutokana na yaliyomkuta mwanaye alisema, “Mimi hawawezi kunitengenezea jambo. Hivi Zitto anaweza kuwa mbaya mimi nikawa mzuri.”

Mama huyo alieleza kuwa tangu alipovamiwa na majambazi nyumbani kwake, Aprili 19 mwaka huu hajawahi kuhudhuria kikao chochote cha Chadema. “Wale wanaodhani Zitto kaonewa wanatakiwa kuwa wavumilivu na wapole, wasubiri kwani kila kitu kinawezekana.”

Ushauri kwa mwanaye

Alisema kuwa mwanaye ana uamuzi wake na kwamba hata kama Chadema itamfukuza uanachama, haitaweza kumnyang’anya vyeti vyake vya elimu aliyoipata.

“Zitto anaweza kufanya kazi mahali popote duniani, lakini pia ni mwalimu anaweza kuamua kufundisha. Ubunge ni mgawanyo wa madaraka. Watu wote hatuwezi kuwa wabunge,” alisisitiza.

Alisema wakati Kikao cha Kamati Kuu kikifanyika Zitto alikuwa nje ya nchi na kwamba yeye alimshauri kuhakikisha kuwa anahudhuria kikao hicho.

“Alipotua tu na ndege aliniambia kuwa kuna foleni na alitaka kukodi pikipiki ili awahi kikao, aliniambia lazima aende ili kujua hatima yake.

Aliacha gari lake na kwenda na hata mimi nilimsisitizia kwamba ni lazima aende katika kikao,” alisema. Alisema kuwa Zitto alipofika katika kikao hicho aliweza kuzima hoja zote zilizomhusu ikiwamo ya ruzuku za vyama, kwamba baadhi ya wajumbe walipoona amebadili mwelekeo wa kikao, mjumbe mmoja (akamtaja kwa jina) aliibua waraka uliomng’oa Zitto katika wadhifa wake.

“Unajua Kamati Kuu ilijadili zaidi kuhusu ruzuku. Hata ule waraka uliongezwa maneno baada ya baadhi ya wanachama kumpora Mwigamba laptop yake alipokuwa mkoani Arusha katika kikao cha Chadema,” alisema.

Huku akiwataja wanachama wa Chadema walioongeza maneno katika waraka huo (wakiwamo wabunge wawili) na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, mama Zitto alisema kilichomkuta mwanaye ni ushindi mkubwa, kwamba alipangiwa kufanyiwa makubwa zaidi ya yaliyomkuta.

“Hakuna amani maana ukisikia kengele inagongwa hapa nyumbani unasema hao ndiyo wamekuja kumuua Zitto nini, hivi sasa mpaka walinzi wanaolinda hapa wakisikia unakuja nyumbani kwa Zitto lazima wakuandike jina na kukufuatilia,” alisema mama huyo.
-Mwananchi

LAPTOP ILICHANGIA MAUAJI YA RISASI ILALA BUNGONI

$
0
0
Yumkini wengi wanapotamka neno ‘penzi’ lenye herufi tano tu, hudhani ni dogo lisilo na uzito katika maisha ya binadamu.

Lakini kama umeshawahi kusikia kuwa mapenzi yanaua, basi uhalisia unaoonyesha  madhara, uzito na machungu ya mapenzi...ndiyo huu hapa.

Desemba mwaka jana ni wakati, Gabriel Munisi alipokutana na Christina Newa. Awali lilikuwa penzi, ambalo Christina aliamini litampa faraja, kicheko na kuyabadili maisha yake.

 Hata hivyo, ndoto yake hiyo ilibadilika muda mfupi tu wa penzi hilo baada ya mpenzi wake, Munisi, kuanza kuonyesha ukali uliopitiliza, wivu na maneno makali.

 “Gaby alikuwa anaishi kwa kasumba, hajiamini, mkorofi na aliyependa kunitishia kwa kutumia silaha mara kwa mara,” anasema Christina.

Ukali wa Munisi haukupungua licha ya Christina kujaribu kumbadili hata kumshauri aonane na daktari wa masuala ya saikolojia ambaye anaweza kumtibu.

 “Nilimwona si wa kawaida. Nilipomshauri kuhusu tiba, alikubali na akampigia simu daktari mmoja aliyekuwa hospitali ya Bugando ambaye alikubali kuwa, inawezekana Gaby ana matatizo ya kisaikolojia na wakakubaliana kuwa ataanza tiba,” anasema.

Christina baada ya kuona penzi lake na Munisi limekithiri kwa  misuguano, mifarakano na vitisho, alishauriana na familia yake, kisha wakaamua kuwa aende kusoma katika Visiwa vya Cypruss, ili kujiongezea maarifa lakini pia atakuwa mbali na Munisi ambaye alikuwa sasa anaonekana kuwa tishio. 

Munisi alionekana kuwa tishio mara baada ya kumtakia hadharani Christina kuwa endapo atamchezea ataisambaratisha familia yake akianzia na Goba, anakoishi mama yao, Ellen Eliezer, kisha Zanzibar anakoishi mdogo wake, Alpha Newa na kumalizia Ilala, inakoishi familia hiyo.

Kwa maelezo ya Christina, kosa kubwa ambalo lilionyesha kumuudhi zaidi Munisi, ni kitendo chake cha kuondoka nchini bila kumuaga. Hata hivyo Munisi hakukata tamaa bali alihakikisha anapata mawasiliano ya Christina akiwa huko visiwani Cypruss.

“Tuliwasiliana tukiwa kule na tukazungumza. Kwa sababu ilikuwa  ni kipindi cha likizo akaniambia atakuja kunipokea uwanja wa ndege. Nilidhani atakuwa amebadilika kwa kipindi hiki,” anasema.

Cha ajabu, Munisi baada ya kumpokea Christina, alimkataza kwenda nyumbani kwao na badala yake alimlazimisha waende, Mwanza, Kitangiri, anakoishi.

Alimchukua moja kwa moja na kumkataza hata kwenda kuisabahi familia yake, na siku ile ile safari ya kuelekea Mwanza ilianza. Lakini usiku wa manane wakiwa katikati ya safari, Munisi alifanya jambo la kushangaza.

“Alisimamisha gari maeneo ya Singida na kunitaka nishuke. Niliposhuka, alitoa bastola akaniambia kwa nini niliondoka bila kumuaga au nataka kumuacha?” anasema na kuongeza: “Kitendo kile kilinitisha kwa sababu sikutegemea kama angenishusha usiku ule porini namna ile na kutoa bastola.”

Laptop ilichagiza mgogoro

 Walipofika Mwanza, Munisi alimfungia ndani Christina, lakini alichukua simu zake zote mbili pamoja na laptop ambavyo ilivifanyia uchunguzi wa kina.

Christina anaeleza kuwa Munisi aliipeleka laptop kwa wataalamu wa teknolojia, ambao walimsaidia kuifungua (ilikuwa ikitumia namba ya siri) na alianza kupekua taarifa zote zilizomo. “

Alikuta baadhi ya picha zangu ambazo nilizituma ‘facebook’. Picha hizo ni za ufukweni ambazo nilipiga na wenzangu  huko Cypruss. Nilikuwa nimevaa nguo za kuogelea na ndiyo jambo lililomkera,” anasema.

 Anasema baada ya kuona picha hizo, alimgombeza na kumpiga kiasi cha kumuumiza kwenye magoti na ndipo alipozidisha ulinzi katika nyumba yake.

Inaelezwa kuwa Munisi alibaki na laptop ya Christina ambayo alikuwa akitembea nayo na kuwaonyesha watu picha za mpenzi wake huyo na kusema:

“Unajua mi nilitaka kumuoa huyu, lakini angalia picha anazopiga, ungekuwa wewe ungefanyaje?”

Lakini Christina alijitetea kuwa hilo si jambo la ajabu katika familia yao kwani hata akiwa nyumbani huvaa hivyo.

Anapanda dirishani kuomba msaada

Baada ya kuona anaendelea kufungiwa ndani bila mawasiliano ya aina yeyote, alichukua uamuzi wa kupanda dirishani na kuwaita wapita njia ili wamsaidie.
ama mwenye nyumba hiyo pamoja na watoto walimsaidia Christina kwa kuwapigia simu ndugu zake na kuwaeleza matatizo anayoyapata. “Mama mwenye nyumba aliniambia kuwa wanawake zaidi ya 30 walioishi na Munisi, walikuwa wakipitia matatizo kama hayo niliyopitia mimi,” anasema.

 Anaondoka Mwanza na ulinzi wa polisi

 Baada ya ndugu zake kupambana, ilibidi polisi watumie ujanja na kumdanganya Munisi kuwa aende kituo cha polisi kwani kuna biashara (dili) ya magari.

Hata hivyo, Munisi alitia shaka na akaamua kwenda na Christina huko polisi, ambaye alikuwa amevaa khanga na fulana tu.

 Ingawa Christina alimbembeleza Munisi aingie chumbani kuvaa, lakini hakuruhusiwa hata kidogo.

Walipofika polisi, simu ilipigwa na wazazi wa Christina wakamtuma ndugu yao ainayeishi  Mwanza,(alifahamika kwa jina moja la Mpangala) ambaye alisaidia kumrudisha Dar es Salaam.

Nyendo za Munisi

 Baada ya Christina kurudi Jijini, Munisi alianza nyendo za kushangaza ambazo pengine ndizo zilizosababisha maafa haya.  Munisi alipanga katika hoteli ya M.M. ambayo ipo karibu kabisa na nyumbani kwa Christina, Ilala Bungoni. Akiwa hapo alikuwa akifuatilia maisha ya wanafamilia hao.

“Nilijua anatufuatilia kwa sababu alikuwa akinitumia meseji kunieleza kila tulichokuwa tunafanya na ndugu zangu. Nahisi pia alikuwa na mtu anatupeleleza,” anasema

 Siku moja Christina akiwa kituo cha mabasi cha Amana, alihisi mtu amemshika bega, alipogeuka alishangaa kumwona Munisi.

“Nilitetemeka na kutamani kupiga kelele, lakini alinitoa hofu na kuniambia ananipenda, hivyo twende pembeni kuzungumza,” anasema.

 Walitafuta eneo wakaketi na kuanza mazungumzo ambapo hata hivyo Christina hakuwa na amani tena na mwanaume huyo.

Maafa yanatokea

Siku ya tukio, Christina, mama yake, mdogo wake, Alpha  pamoja na shemeji yake, mume wa dada yake, marehemu  Francis Shumila walikuwa katika gari wakielekea uwanja wa ndege. 

“Wakati gari linatoka getini, tulimwona Munisi akivuka barabara kwa kasi, akija upande wetu. Nilijua anakuja kufanya jambo baya,” anasema.

Shumila ambaye aliufahamu fika ugomvi huo, alishuka kwenye gari ili akamsihi Munisi asimdhuru Christina, lakini Munisi bila kuchelewa alimmiminia risasi zaidi ya tano kichwani.

“Risasi zilimuishia, akaweka nyingine kisha akaenda upande aliokaa Alpha na kumpiga za kifuani,

kisha akaanza kutumiminia mimi na mama,” anasema.Shumila, alifariki dunia siku moja baadaye, Alpha alikufa palepale, wakati Christina na mama yake walijeruhiwa.

Hata hivyo Caroline Newa, dada yake Christina, ambaye ndiye mke wa marehemu Shumila, anasema polisi walipewa taarifa za vitisho vya Munisi lakini hawakutilia maanani.

“Tulitoa taarifa zaidi ya mara nne, lakini polisi walitudhalilisha wakatuambia hayo ni mambo ya mapenzi tu,” anasema Caroline.

Walibembeleza angalau kupewa hati ya taarifa(RB) lakini polisi walikataa katakata.

Shumila alijitabiria kifo

Caroline, anasema, siku chache kabla ya tukio hilo, Shumila, ambaye ni mume wake, alimtoa hofu Christina na kumwambia kuwa atamlinda kwa gharama yeyote ile hata kama kupoteza maisha yake.

“Kwa kuwa alikuwa akijua historia yote ya mfarakano huu, alimwambia Christina asiwe na wasiwasi atamlinda na kweli ndivyo ilivyotokea” anasema Caroline.
Mwananchi

MTEI "TUTAENDELEA KUWAFUKUZA WALE WOTE AMBAO NI WASALITI CHADEMA"

$
0
0
Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edwin Mtei amesema kuwa chama hicho kitaendelea kuwafukuza wote wanaokihujumu huku akieleza kwamba, anaunga mkono kuvuliwa uongozi kwa Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, nyumbani kwake jana, Mtei aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu (BOT) na Waziri wa Fedha katika utawala wa awamu ya kwanza wa Mwalimu Julius Nyerere, aliweka wazi kuwa daima ataunga mkono dhamira ya kukisimamia chama hicho aliyoitaja kuwa ni safi.

 “Naunga mkono uamuzi wote wa Kamati Kuu, kuwasimamisha na kuwavua uongozi Naibu Katibu Mkuu wetu Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo. Na kwa sababu Chadema inataka kusonga mbele, lazima iwafukuze mafisadi na wezi wanaoshirikiana kukihujumu chama,” alisema Mtei.

Bila kufafanua zaidi au kutaja majina, mwenyekiti huyo wa kwanza wa Chadema alisema: “Hatuwezi kuendesha chama wakati viongozi wengine wanapokea pesa na kuzihifadhi kwenye akaunti za siri.” Alisisitiza kwamba kwa nafasi yake akiwa mwasisi wa Chadema ni lazima ahakikishe anaunga mkono dhamira safi ya kukisimamia chama.

Kuhusu Arfi kujiuzulu

Akizungumzia hatua ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Saidi Arfi kujiuzulu, Mtei alisema kuwa inafaa kiongozi huyo ajitazame upya na kujisahihisha badala ya kuwa mlalamikaji kila siku.

“Aache kulalamika kwa sababu, wakati alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti mimi nilisimamia uchaguzi. Kama alikuwa na ndoto kwamba siku moja atakuwa mwenyekiti wa Chadema taifa alipaswa kujichunguza kwanza,” alisema.

Mtei aliongeza kuwa iwapo kuna watu wanadhani Chadema itakufa hiyo ni dhana potovu, lakini kwa sasa chama hicho kimejipanga kuchukua dola na tayari wamejiimarisha kimkakati.

“Katika suala la kushughulikia watu wanaokihujumu chama  hakuna ‘compromise’ (mjadala),” alihitimisha Mtei.   Juzi Chadema ilitangza uamuzi wa Kamati Kuu yake kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila, huku Arfi akitangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tanzania Bara.

Mtei amewahi kumkemea na kumwonya Zitto katika mambo mbalimbali aliyofanya ndani ya Chadema, moja ikiwa Oktoba mwaka jana ambapo mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, alipotangaza kuwania urais mwaka 2015.

Alisema kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama,  huku akiongeza kwamba amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana-Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.

“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.

Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015, imekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema, akiweka wazi kuwa wakati ukifika chama hicho kitafanya uchaguzi sahihi.

“Siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza. Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.

Hata hivyo, Zitto alipinga kauli hiyo akisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja,  bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”

Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri, kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.

“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015.  Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.

Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”

DR KITILA MKUMBO ATOA KAULI KUHUSU KUVULIWA VYEO NDANI YA CHADEMA

$
0
0
Tunawashukuru watanzania kwa kufuatilia kinachoendelea ndani ya CHADEMA. Nawapa pole wote waliokwazwa na jambo hili, na ninawashukuru wote walionipa pole na kunitia moyo. Ninawashukuru pia walionilaumu na ni vizuri kunyosheana vidole na kuwekana sawa pale ambapo moja wetu anaonekana kukwamisha harakati za mabadiliko. 
Haya ni mawimbi katika harakati za mabadiliko na ninaamini yatapita na hayatayumbisha mchakato wa kusimika mfumo wa demokrasia hapa nchini kwetu. 

Ninashauri tuwe na subira katika kutoa hitimisho na hukumu katika jambo hili. Mpaka sasa tumekwisha kupata upande mmoja juu ya kilichotokea. Vuteni subira nasi tuseme ndipo mpitishe hukumu. Mungu akijalia tutakuwa na mkutano na waandishi wa habari wakati wowote kabla ya wiki ijayo na tutaeleza upande wetu, na hasa kutoa maoni yetu juu ya kile kilichotamkwa jana kwamba sisi ni wahaini na wahujumu ndani ya chama chetu. 
Kwa sasa tambueni tu kuwa mie binafsi bado nipo imara katika kuhakikisha kwamba siwi kikwazo na ninachangia kikamilifu nguvu zangu katika harakati takatifu za mabadiliko hapa nchini.

SAKATA LA UBAKAJI LAENDELEA, PROFESA JUMA KAPUYA ABURUZWA POLISI KWA TUHUMA ZA KUBAKA.

$
0
0
HATIMAYE binti anayedaiwa kubakwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Profesa Juma Kapuya (CCM), amefungua jalada Polisi dhidi ya mbunge huyo.

Habari za kipolisi ambazo Tanzania Dama limezipata, zinasema kuwa binti huyo ambaye anadai kubakwa na kisha kutishiwa kuuawa na Profesa Kapuya, amefungua jalada namba OB/RB/21124/13 katika Kituo cha Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam.

Harakati za kufungua jalada hilo zilianza juzi jioni na kuendelea hadi jana ambapo polisi walitumia zaidi ya saa 12 kumhoji binti huyo anayedaiwa kubakwa ili kupata ukweli wa sakata hilo.

Akiwa kituoni hapo, binti huyo alikutana na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi ya Oysterbay (OCD) na OC-CID wake na kutoa maelezo ya awali kabla ya viongozi hao kumruhusu ayaweke malalamiko yake katika maandishi kwa ajili ya kufunguliwa mashitaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius  Wambura, alikiri polisi kufungua jalada hilo na kuongeza kwamba hivi sasa wanafanya uchunguzi kubaini kama ujumbe ulio katika simu ya binti anayedai kubakwa na kutishiwa maisha unatoka katika simu ya  mbunge huyo.

“Tumefungua jalada, lipo kwa ajili ya uchunguzi na tukibaini kuwa ni nani anahusika na tuhuma hizo tutamsaka na kumkamata popote alipo,” alisema Wambura.

Habari zaidi zinasema polisi wamechukua namba ya Kapuya inayodaiwa kutumika mara kwa mara kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa binti huyo, akitishiwa kuuawa.

Simu hiyo namba 0784993930 inayodaiwa kumilikiwa na Profesa Kapuya, mbali ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno ya kutishia kuua, pia ndiyo inayodaiwa kutumika kutuma pesa kwa njia ya mtandao kwenda kwa binti huyo.

Moja ya ujumbe wa vitisho unaodaiwa kutumwa na Kapuya kupitia simu hiyo unasomeka hivi;  “Mkiuawa itakuwa vizuri…itawapunguzia gharama za kuishi, usitake kugombana na serikali mtoto mdogo kama wewe, sisi ndiyo wenye nchi yetu, mwenye hilo gazeti ni Mbowe sasa mwambieni nyumba ya kuishi si mmemuingizia hela leo? Mnatumika tu bure watu wanaingiza hela nyingi, ila mmenitibua lazima niwaue wiki hii haitaisha, nitapiga kambi kote, jana si wamekuficha tuone utalindwa milele maana washatengeneza hela, lazima mvae sanda tu hilo sio ombi ni wajibu wenu, mnajitia na nyie mafia watoto siyo, watoto wetu wanauza unga nani anawakamata? Nani atapingana nasi.”

Pia simu hiyo iliwahi kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaosomeka hivi; “Ni lazima nitakuua wewe na ndugu yako na atakaetaka kuwasaidia, huyo Sitta asijiingize kwenu, yaani nitakuua tena sijui leo mtalala wapi? We unadhani nani atakaenifunga, ndo nishakupa ukimwi, sasa nakutaka uache mara moja kuongea na mtu, nitakuwinda popote tuone.”

Mbali na kutishia kumuua binti huyo na ndugu yake na mtu mwingine yeyote atakayejitokeza kumsaidia, Tanzania Daima limenasa baadhi ya mawasilino ya simu za ujumbe mfupi wa kuhamisha fedha kutoka kwa Profesa Kapuya kwenda kwa binti huyo ambaye mbunge huyo alikana kumfahamu na kwamba hajawahi kukutana naye.

Tanzania Daima  pia lilinasa mawasiliano ya kutumiana fedha kutoka kwa Kapuya kwenda kwa binti huyo.

Baadhi ya mawasiliano hayo ni pamoja na yale yaliyofanyika Agosti 31 mwaka huu kupitia simu ya Kapuya ambapo alituma sh 300,000 kwenda kwa binti huyo kama sehemu ya makubaliano ya kutuma pesa kila mwezi kwa ajili ya matunzo.

Mawasiliano hayo ni kama ifuatavyo: U26UG365 Imethibitishwa Umepokea Tsh 300,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 31/8/13 saa 3:28 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 300,000

V04EU470 Imethibitishwa Umepokea Tsh 400,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 24/9/13 saa 2:38 PM Salio lako la M-PESA ni Tsh 400,040.

R93NY448 Imethibitishwa Umepokea Tsh 505,000 kutoka kwa JUMA KAPUYA Tarehe 21/6/13 saa 11:07 AM Salio lako la M-PESA ni Tsh 505,000.

Kutokana na mfululizo wa habari hiyo, Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake Yasin Memba, ametishia kuliburuza mahakamani Tanzania Daima endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.

Source: Tanzania Daima

TAARIFA YA ZITTO KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU KUPOKONYWA UONGOZI CHADEMA

$
0
0
1. Utangulizi Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. 

Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013.
 
 Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu . Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. 

Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.
  
Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika.  
Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA.  
Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho. 
  
2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. 
 Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. 
 
Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama. 
  
i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili: 
  • Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
  • Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
  • Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
  • Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.

 ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua. 
  
iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. 
 Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. 
 
Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho. 
  
iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. 
 Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko. 
  
v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae.  

Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo: 
  • Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
  • Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.

 vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili: 
  • Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
  • Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala lakimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
  • Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.

 3Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA.  
Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo: 
  1. Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
  2. Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.


 4. Hitimisho Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. 
 Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'.
 
 Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. 
 
Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.
  
Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.
  
Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.
  
 Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. 
  
Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia.  
Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.
  
Kabwe Zuberi Zitto, Mb Dar es Salaam. 24 Novemba, 2013

PETER WA P-SQUARE APAGAWISHWA NA BINTI WA KIBONGO AMVISHA PETE JUKWAANI

$
0
0





Jionee mwenyewe hapo ilikuwa jana usiku kwenye show yao hapa dar ...dada kwenye picha alipata bahati ya pekee ya kutukiwa upendo na Peter wa P-square na kupewa jina la Onyinyee...nakupewa Pete....mmmhh Kazi kweli kweli Nani zaidi hapo kati ya Lola mke wake na Huyu ...?

JE KUNA UKWELI WOWOTE HAPA: ETI WANAUME WAREFU NDIO UGONJWA MKUBWA WA WANAWAKE

$
0
0
Wakuu ktk pitapita zangu za kila siku nakutana na minong'ono kuwa wanaume warefu wana mvuto mkubwa kwa wanawake tofauti na wenzao wafupi. hii nimeisikia kwa baadhi ya wanaume wakikiri kuwa wanaume warefu wanakubalika kirahisi kwa wanawake, basi nikajaribu upande wa pili nisikie wenyewe wanachosema, wengi wamekiri kuwa wanaume warefu wana mvuto sana ila tatizo ni mila na desturi za kwetu haziruhusu mwanamke kumtongoza mwanaume, mwingine akaniambpga kuwa wanaume warefu wengi wao wana confidence na wanajikubali sana, wapo wengi tu wanaokubali kuwa wanaume warefu wanakuwa ni wend mvuto, sasa wanawake na nyie mnasemaje??

MBOWE "NITAENDELEA KUIONGOZA CHADEMA WANACHAMA WAKIAMUA"

$
0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Chadema endapo kama wanachama wataendelea kumhitaji.

Kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya chama chake amesema kamwe chama chake hakizuii watu kutamani uenyekiti lakini akatahadharisha zitumike njia za kidemokrasia na uwazi.Amesema katu Chadema hakitaruhusu watu kutumia njia za kihuni kinyume na Katiba.

Mwenyekiti huyo ambaye ni mhimili mkuu kwa chama chake ameshangaa watu kukimbilia madaraka kwa njia ovu na za kihuni.Amesema kuongoza upinzani si lelemama na wala si wa kukimbiliwa.Amesema kuongoza upinzani ni kukubali kufungwa,kupigwa mabomu na kuzushiwa kila kashfa kila uchao.

Kiongozi huyo amesema kwamba kamwe hawatakubali Chadema kusambaratishwa kwa njia yoyote.

Kuhusu Ukomo wa uongozi amesema Katiba ya Chadema haina kipengele hicho kwa ngazi yoyote na kama mtu anafaa wanachama wataendelea kumchagua bila kujali muda atakaokuwa ametumikia chama.

Source:Nipashe Jumamosi.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images