Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO WAGANDA WALIVYOTAKA 'KUMUUA' ANKO NGASSA LEO MOMBASSA

$
0
0
Mfungaji wa mabao mawili ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars katika sare ya 2-2 na Uganda, The Cranes kwenye Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge, Mrisho Ngassa akiwa ameketi benchi Uwanja wa Manispaa, Mombasa, Kenya baada ya kutoka dakika ya 80 alipoumizwa na wachezaji wa Uganda. Hata hivyo, Stars ilishinda kwa penalti 3-2 baada ya sare hiyo ya 2-2 ndani ya dakika 90. Picha zinazofuatia ni namna Ngassa alivyoumizwa kidevuni kwa kiwiko na kwanga la mguu lililomuumiza kifundo cha mguu. Na picha nyingine ni wakati anaumizwa uwanjani.






GOLKIPA IVO MAPUNDA AWA LULU YANGA NA SIMBA ZAMMEZEA MATE BAADA YA KUIBUKA SHUJAA JANA

$
0
0
Golkipa mkongwe wa hapa Tanzania Ivo Mapunda Ambae Anaichezea Team ya Gor Mahiya ya Kenya kama mchezaji wa kulipwa Jana kwa sasa ni kama Lulu Kwa Team Kongwe za Yanga na Simba ...Jana Aliziirishia Tanzania Kuwa Yeye bado yumo Baada ya Kudaka Penati Tatu na Kuiwezesha Tanzania Kutinga Nusu Fainali za Kombe La Challenge Huko Kenya ...Ivo Mapunda anakaribia Kumaliza Mkataba wake na Gori Mahiya, Japo Gori wameonyesha nia ya kumuongezea mkataba lakini Simba na Yanga nao Wanamdondoshea Mate ..

SALUTI: MOURINHO AIKUBALI ARSENAL...ILA PIA AIONYA

$
0
0
Kocha machachari na mwenye majigambo Mourinho wa Chelsea amejitokeza na kuipongeza team ya Arsenal ambayo inaonekana ni mwiba katika ligi hiyo ya England ..Amesema Arsenal kwa sasa Wamejipanga na wanastahili kushika number moja katika msimamo huo wa ligi ....Ili pia ametoa onyo na kusema Ubingwa wa Ligi huwa ni Mwezi May na sii December so wasijione ndio wameshashinda.

BOB JUNIOR ADAIWA KUVAA NGUO ZA MKOPO

$
0
0
Msanii wa Music ambae pia ni Producer wa Muziki na Mmiliki wa Studio ya Sharobaro Records Bob Junior ameingia katika Aibu Ingine baada ya Duka Moja la nguo Kujitokeza na Kudai Linamdai Msanii huyo Kiasi cha Shilingi 180,000 za Kitanzania ..Muuzaji wa Duka hilo Amesema  Bob Huwa anaenda hapo kuchukua nguo ambazo huwa tunamkopesha mpaka sasa deni limefikia kiasi hicho na tukimtafuta anapiga chenga kulipa..
Gazeti moja la hapa bongo limejaribu kumtafuta Bob kumuuliza kuhusu hiyo issue akasema yeye huwa anachukua nguo hizo kwa ajili ya kulitangaza hilo duka so hadaiwi na mtu....

KOCHA MANCHESTER UNITED AKALIA KUTI KAVU-ASISITIZA NI LAZIMA ASAJILI WACHEZAJI WAPYA

$
0
0
Nchini England mabingwa watetezi wa Ligi ya nchi Hiyo Manchester United wameendelea na mwanzo mbaya wa ligi hiyo baada ya hii leo kukubali kipigo cha bao moja bila toka kwa Newcastle United .
Bao pekee lililoacha simanzi kwa mashabiki wa United lilifungwa na kiungo Mfaransa Yohan Cabaye. Matokeo haya yanaiacha United kwenye nafasi ya tisa wakiwa wameachwa na vinara wa ligi hiyo kwa pointi 12.
Hii ni mara ya kwanza kwa United kupoteza mechi mbili mfululizo kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu mwaka 2002 huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Newcastle United kushinda mchezo kwenye uwanja wa Old Trafford kwa miaka 41.

Kocha wa Team Hiyo Ambae kwa sasa ni kama amekalia kuti kavu amesisitiza kuwa ni lazima asajili wachezaji wapya wakati wa majira ya Baridi ..ili kuokoa jahazi...

KANYE WEST AZINGUANA NA RAIS OBAMA WA MAREKANI

$
0
0
Rapper Kanye West amemtolea Uvivu Rais Barack Obama wa Marekani kwa kumzuia kutaja jina lake popote na wala la Mpenzi wake Kim Kardashian...Hii inakuja kama ni kujibu mapigo baada ya raisi wa marekani kumuita Kanye kuwa ni "Jack Ass" yaani mtu mjinga ama Chizi hivi ...

Mwaka 2009 kwa mara ya kwanza Obama alimwita Kanye Jack Ass baada ya Kanye Kupinga ushindi wa Taylor Swift kushinda tuzo ya Best Female Video MTV ..Kanye West alivamia jukwaa na kupinga uteuzi huo....
Juzi Tena katika Mahojiona fulani na TV moja Huko Marekani Obama Aliulizwa Jay z na Kanye Yupi Unamchagua Ombana Akajibu Jay z, na Obama akaulizwa kama bado anamchukulia Kanye kama Jack Ass ..na akajibu hivi:
He is a jackass,” Obama said. “But he’s talented.” 

MBUNGE AMSHAURI RAIS KIKWETE KUMG'OA WAZIRI MKUU PINDA ADAI HAWAJIBIKI NI MPOLE MNO

$
0
0
Dodoma. Rais Jakaya Kikwete, ameshauriwa kumng’oa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ikielezwa sababu kuwa ndiye kikwazo katika utendaji wa Serikali na kwamba akiachwa ataipeleka pabaya Serikali na CCM

Kikwete pia ameshauriwa kumfukuza kazi Waziri wa Tamisemi, Hawa Ghasia, kwa kushindwa kukabiliana na matatizo ya ubadhirifu katika halmashauri nchini.

“Kama (Rais) unaitakia mema nchi na CCM kuchukua hatua za kuwafukuza kazi Pinda na Waziri Ghasia,” alisema Mbunge wa Mwibara, Khangi Lugola (CCM), juzi alipochangia taarifa za Kamati za Bunge kuhusu hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30 mwaka jana.

“Kwa nini Watanzania wafe kwa kunyimwa misaada na wafadhili kwa sababu ya mtu mmoja tu Pinda, kwa ajili ya Ghasia ameiendesha Tamisemi kama Saccos ama Vikoba?” alihoji.

 “Mchawi wetu ... ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekuwa mpole mno hawajibiki,” alisema Mh. Lugola na kuongeza, “Kuanzia jana (juzi) Waziri Mkuu anahudhuria mahafali.”

Wakati Lugola akizungumza mawaziri waliokuwepo bungeni ni wanne, manaibu mawaziri wawiliwawili, wakati  mawaziri wote 53.

SINTASAHAU HUYU MDADA NIMEMVULIA KOFIA

$
0
0
Mambo niaje wakuu..sijui hata nianzie wapi?...hawa wanawake...!! basi tu!!basi bwana nmekua nikimdate dada mmoja mwenyeji wa iringa .sio siri kwa haraka haraka nlijua huyu ananipenda kwa dhati, mie kiukweli nlimpenda sana.Tumedate kwa almost mwaka na nusu,kwa mda wote huo sharti ilikua ni hakuna kugegendana mpaka tufunge ndoa.Kidume nlijipa moyo nkajikaza kwani mama nilihus namjua sana ni mlokole haswaa mpka watu uwa wananishangaa nlimptaje coz mie cnaga swaga za kilokole,aliku kesha nihakikishia kua yeye ni bikira na ajawai ku do.Kwa mda wote wa mapenzi yetu nmekua nikijaribu kuomba mchezo ila ilishndkana.juzi kati ulizuka ugomvi mkubwa sana kati yangu na yeye kisa kikiwa ni hicho hicho kugegenda,Mimi nkiwanataka yeye ataki,tumekaa bila kuongeleshana kwa almost wiki nzima,jana ijumamosi ndo aliamua kuvunja ukimya na kuniita niende kwake ili tusort out ili tatizo.Tuliongea mengi ila dada bado alikua kashikilia msimamo wake ila akaniomba nimpe mda kidogo afikilie jinsi ya kulifanya hilo,nlimkubalia,basi ile kuangana kwa hugs na kisses tukajikuta kitandani bahati nzuri ni kama she was 50/50 kufanya,na mie sikutaka kua ---- nikatoa dudu fasta nikijua leo ndo naifumua zawadi yngu ya chrsmas...mmmh..nlichokikuta huko staki kuamini mpka sa hvi..nahisi mie nlikua mwanaume wa 20 kuzamisha. Hata gori nlishdwa kupiga kwa sababu ya mawazo nlokua nayo,nlivaa surua yangu taratibu. nkimwacha demu analia sana uku akiniomba msamaha daa wanawake siwatamani tena..

SIKU MANCHESTER UNITED ILIPOSHUSHWA DARAJA

$
0
0
Ni mashabiki wachache wa Manchester United wanaikumbuka siku ile ambayo timu yao ilishushwa daraja. Ilikuwa msimu wa 1973/74 na mechi ya mwisho ya ligi ilikuwa tarehe 27 Aprili 1974. Kwa mashabiki wa Manchester United wataikumbuka tarehe 27 April 1974 kama "the worst day in the history of football". Kwa wasioipenda Manchester United, wanaikumbuka hiyo tarehe kama "the best day in the history of football." Kwa mara ya kwanza Manchester United ilishushwa daraja baada ya kucheza kwenye ligi daraja la kwanza kwa miaka 36.

Lakini huwezi kuongelea tarehe 27 April 1974, siku ambayo Manchester United ilishishuka daraja, bila kumwongelea Denis Law. Denis Law ni legend Old Trafford. Alijiunga na Manchester United mwaka 1962 akitokea Manchester City. Aliichezea Manchester United kwa muda wa miaka 11, ambapo alifunga magoli 237 kwenye mechi 404 alizocheza. Mashabiki wa Manchester United walimwita “The King” na “The Lawman”.

Itakumbukwa pia kuwa Manchester United ilikuwa ikisuasua kwenye ligi baada ya timu kupata ajali ya ndege Munich Ujerumani mwaka 1958 ambapo abiria 20 kati ya 44 walipoteza maisha. Kati ya abiria 20 waliofariki, saba walikuwa wachezaji wa Manchester United. Kwa hiyo, baada ya ajali hiyo, Manchester United ilikuwa wanapambana mara nyingi kuepuka kushuka daraja.

Baada ya kuichezea Manchester United kwa miaka 12, Denis Law alihamia Manchester City msimu wa 1973/74 bila ada (free transfer). Manchester United walikuwa hawamhitaji tena maana kiwango chake cha mpira kilikuwa kimeshashuka na umri pia ulikuwa umesogea. Pia George Best na Bob Chalton walikuwa wameshaondoka.

Katika mechi ya mwisho ya ligi msimu wa 1973/74, Manchester United ilicheza na Manchester City Old Trafford. Manchester United ilitakiwa kushinda ile mechi ili isishuke daraja. David Law alicheza lakini tokea mwanzo alionekana kutokuwa na raha maana kama timu yake kipenzi (Manchester United) ingefungwa basi ingeshushwa daraja.

Mpaka dakika ya 80 mechi ilikuwa bila bila. Mnamo dakika ya 81, Denis Law aliifungia Machester City goli kwa kisigino. Lilikuwa goli zuri na tamu lakini siyo kwa mshabiki yoyote wa Manchester United. Denis Law mwenyewe hakushangilia kwa kufikiri kuwa goli lake la kisigino lingeishusha daraja Manchester United. Mara tuu baada ya kufunga like goli, alibadiliswa huku akitoka uwanjani akiwa ameinamisha kichwa chini kwa masikitiko makubwa ya kuishusha daraja Manchester United.

Baada ya Denis Law kutoka uwanjani, mashabiki wa Manchester United walivamia uwanja na kumlazimisha refa kumaliza mechi katika dakika ya 85. Siku chache baadae, chama cha mpira kilifanya mapitio ya mechi ile na kusimama na matokeo ya mechi. Kwa hiyo, Manchester City ikawa imeshinda bao moja lililofungwa na Denis Law kwa kisigino na Manchester United kushushwa daraja.

Hata hivyo, ilikuja kugundulika baada ya mechi kuwa bado Manchester United ingeshuka daraja bila kutokana na matokeo ya ile mechi. Hii ilitokana na matokeo ya kwenye mechi nyingine za mwisho zilizochezwa siku ile. Lakini Denis Law aliamini kabisa kuwa goli lake la kisigino limeishusha daraja Manchester United.

Msimu uliofuata (1974/75) Manchster United ilicheza kwenye ligi ya daraja la pili na kufanikiwa kurudi tena ligi ya daraja la kwanza katika msimu wa 1975/76.

Watch Video:

MAJANGA:WACHINA WAWEKEZA HADI KWENYE BIASHARA YA KUGAWA URODA (UCHANGUDOA)

$
0
0

Amini Usiamini Wachina sasa Wameamua kuwekeza mpaka kwenye Ukahaba , Kama unataka kushuhudia hilo basi tembelea hotel za hapa dar zilizopo katika fukwe za bahari ya hindi ukajionee wadada wa kichana wana vyouza mapenzi kama karanga...Bei zao ni kuanzia 20,000 mpaka 60,000 .....Dahhhh

KUJIUA NA KUUA KWA BASTOLA KWA WAPENZI KUNAANZIAGA HAPA

$
0
0
Mapenzi ni kitu kingine kabisa chali yangu usisikia mtu kaji Ufosaroo aka kujiua na Bastola ukadhani ni uchizi tu ..hiyo tunaita ni dhuluma ya penzi...Inauma sana jamani..
Unakuta upo mapenzini na Binti unampenda kupindukia na yeye unaona anakupenda unamfanyia kila kitu unamtoa katika hali fulani na kumpeleka katika daraja fulani kwa mfano unamsomesha mpaka anapata degree ukitegemea labda akimaliza mtaoana na kusaidiana maisha lakini pindi anapomaliza tu na kupata kazi nzuri anaanza kukuonyesha madharau na kuanza kutoka na watu wengine ,,wewe unakuwa Fala tu tena Boyaaa la kutupwa ....Embu niambie hapo utachukua hatua gani?

MSAANI MAARUFU "KELLY ROWLAND " KUTOKA MAREKANI AKIWA KATIKA MITAA YA UWANJA WA FISI MANZENSE JIJINI DAR-ES-SALAAM

$
0
0

Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland, ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jana jioni baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya Uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying AliveFoundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini.

TAZAMA PICHA ZA MKE MTARAJIWA WA MBWANA SAMATA ANAECHEZA MPIRA KATIKA KLABU YA TP MAZEMBE

$
0
0



Huyo Ndio Shemeji yetu kwa Mbwana Samatta ..She is Cute No Doubt

MASKINI MTOTO SULEMANI RAJAB ALIYE KUWA ANASUMBULIWA NA UVIMBE WA MIGUU AFARIKI

$
0
0
Yule mtoto Suleiman Rajab aliyeteseka muda mrefu akisumbuliwa na uvimbe mkubwa mguuni huku mamia ya Watanzania wakijitolea kuchanga fedha kwa ajili ya matibabu nchini India amefariki dunia ghafla nyumbani kwao Ukonga-Kivule, Dar.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa baada ya kifo hicho, baba mzazi wa marehemu, Rajab Upinde alisema kwamba mtoto wake huyo hakuwa anasumbuliwa na kitu chochote zaidi ya uvimbe uliokuwa mguuni lakini alishikwa na ugonjwa wa ghafla na kufariki dunia.
Baba huyo alisema kwamba Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na Hoyce Temu kupitia kipindi chake cha Mimi na Tanzania kwenye Runinga ya Chanel Ten walifanya jitihada kubwa za kukusanya michango ambayo ilifanikisha maandalizi ya safari ya matibabu India.
“Naumia sana kwa vile kila kitu kilikuwa tayari. Tulikuwa tunasubiri siku ya kuondoka tu. Global Publishers na Hoyce wamefanya kazi kubwa kukamilisha safari ya India lakini ndiyo hivyo Mungu kampenda zaidi kiumbe wake,” alisema baba huyo kwa uchungu.
Akizungumzia kifo cha mtoto wake, baba huyo alisema kuwa siku ya tukio Sele aliamka akilalamika kichwa kinamuuma ambapo walimpa dawa za kutuliza maumivu.
Alisema aliporejea kutoka kazini mkewe alimwambia kuwa Sele alikuwa akilalama kuwa miguu inawaka moto ambapo alimfuata mwanaye chumbani ambaye aliomba aitiwe shehe.
Shehe alipofika alimuombea na baada ya muda aliwaita wadogo zake na kuwaambia yeye anakufa kwani anajisikia vibaya mno.
Baba huyo aliendelea kusema kuwa akiwa amekaa nje alisikia mwanaye mwingine akimuita aingie ndani kwani hali ya Sele ilikuwa imebadilika na alipoingia alimkuta mwili wote umelegea ambapo aliita majirani ili wamsaidie, walipoingia ndani walimkuta ameshafariki dunia.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
“ Ki ukweli sikuweza kuamini macho yangu kama mwanangu ndio ameniaga kwani nilikuwa na ndoto nyingi za kumuona akipona tena na kuwa mzima  kama walivyo watoto wengine” alisema baba huyo.
Kampuni ya Global Publishers kwa kushirikiana na kipindi cha Mimi na Tanzania kinachorushwa kupitia Televisheni ya Channel Ten na mwanadada Hoyce Temu, na kwa watanzania wote walio nje ya nchi kwa kujitahidi kutoa michango yao Mungu awabariki sana.
chanzo:globalpublishers.

ZITTO "SHILINGI 2 BILLION HUTOROSHWA NA KUPELEKWA NJE YA NCHI KWA KUKWEPA KODI"

$
0
0
Bunge limeelezwa zaidi ya Dola za Marekani 1.25 bilioni sawa na Sh2 trilioni hutoroshwa na kupelekwa nje ya nchi kila mwaka kwa lengo la kukwepa kodi. 
Taarifa hiyo imetolewa wakati wingu zito likiwa limegubika uwasilishaji wa ripoti ya kikosi kazi cha Serikali kilichochunguza sakata la Sh315 bilioni zilizofichwa na Watanzania katika mabenki nchini Uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza kila mwaka mapato hayo ambayo ni sawa na asilimia tano ya Pato la Taifa kupitia uhamishaji huo haramu.
“Uhamishaji huu haramu wa fedha kupelekwa nje ya nchi hufanywa kwa lengo la kukwepa kulipa kodi au wahusika kuepuka kukamatwa na fedha walizopata kwa kupokea rushwa,” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza Bunge kutunga sheria itakayodhibiti uhamishaji haramu au ufichaji wa fedha nje ya kwa lengo la kuogopa kukamatwa na rushwa, kufanya ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa 10 wa Jumuiya ya Kamati za Hesabu za Serikali za Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).
Alisema katika mkutano huo uliofanyika Septemba 2 hadi 7, mwaka huu Jijini Arusha, wajumbe waliazimia kuhamasisha mabunge ya nchi zao kutunga sheria kudhibiti uhamishaji huo wa fedha.

Wiki iliyopita, mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alikaririwa akisema bungeni ‘hapatatosha’ kama ripoti ya mabilioni ya Uswisi haitawasilishwa katika Bunge hili.
Mpina alisema yeye ni miongoni mwa wabunge waliohojiwa baada ya kutamka bungeni kuwa zaidi ya Sh11.9 trilioni zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 na mwaka 2008.
“Nilipolisema hilo jambo niliikabidhi Serikali kupitia Bunge taarifa za tafiti mbalimbali ili ifuatilie. Baadaye Zitto akaja na hoja ya bilioni 314… tunataka taarifa hatutanii,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe Bunge la Aprili lakini Serikali ikaomba muda zaidi na kuahidi kuiwasilisha katika Mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea Mjini Dodoma.

----Mwananchi

MAANDALIZI YA MAZISHI YA RAIS WA ZAMANI WA AFRIKA YA KUSINI NELSON MANDERA YANAENDELEA

$
0
0

Hili ni Banda linaloendelea kujengwa katika eneo la makazi ya Hayati Nelson Mandera kwa ajili ya maandalizi ya shughuli za maziko yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii, ambapo zaidi ya viongozi 70 wa mataifa makubwa, kutoka pande zote za dunia wanatarajia kuhudhuria maziko hayo

WANAUME WAWILI MASHOGA WAPATA VYEO VIKUBWA SEREKALINI...MMOJA NI WAZIRI MKUU MWINGINE MSAIDIZI

$
0
0
Hii itakua ya kwanza duniani kwa wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja kupata vyeo vikubwa kwenye serikali kuu ya nchi.
Makundi mengi yenye maoni tofauti yamekuwa yakipinga mapenzi ya jinsia moja na makundi mengine yakitetea, huko Luxemburg mwanaume anayejulikana kwa jina Xavier Bettel ambaye ameweka wazi kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja amekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo.
Hapo hapo mwanaume mwingine Etienne Schneider ambaye pia aliweka wazi kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moja amepewa umakamo waziri mkuu akimsaidia kazi Xavier Bettel .
Baada ya wawili hawa kupata vyeo hivi vya juu imefanya nchi ya Luxemburg kuwa nchi ya kwanza duniani kuwa na viongozi wa juu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja waziwazi.

MSANII MKUBWA WA HIP HOP TOKA MAREKANI AJICHORA TATTOO KUBWA YA NELSON MANDELA

$
0
0
Hakuna mtu yoyote ambaye hajaguswa na kifo cha Mzee Nelson Mandela kutokana na historia ya pekee aliyoiacha kiongozi huyu wa Afrika Kusini.
Kuanzia mataifa ya Asia,Ulaya,Marekani, wanamichezo,waigizaji hadi watu wa kawaida wameonyesha masikitiko yao kwa kumpoteza mfano mzuri kwenye uongozi.
Headline mpya inamhusisha msanii nguli wa hiphop The Game ambaye ni mpenzi mkubwa wa tatoo. Hivi sasa amechora tatoo kubwa za sura za wanae,Barack Obama, Trayvon Martin na Nelson Mandela akiangalia nje ya gereza.
The game ali-share picha akionyesha tatoo hiyo kubwa na kuandika ,“The finished ‘Nelson Mandela’ lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid,”.

HIVI DOCTOR ULIMBOKA YUPO WAPI? KAAMUA KUNYAMAZA AMA KANYAMAZISHWA?

$
0
0
Naomba kupata updates za Dr. Ulimboka:
1. Je, bado ndie mwenyekiti wa madktari Tz?
2. Je, yupo nchini?
3. Vijana walopoteza kazi kwa misimamo yake inakuaje?
4. Je, kaamua kunyamaza au kunyamazishwa?

Mwenye dondoo atuwekee plz!

MAKALI YA KILIMANJARO STARS YAIPA TEAM YA KENYA MCHECHETO-LAZIMA WAKAE

$
0
0
KENYA imeingia mchecheto na makali ya Kilimanjaro Stars na sasa imebainika kwamba Kocha Adel Amrouche ndiye aliyesisitiza mechi ikachezwe Machakos badala ya Mombasa.

Kenya itacheza na Stars kesho Jumanne kwenye mechi ya nusu fainali ya Chalenji kwenye Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Awali nusu fainali hiyo ilikuwa ichezwe hapa Mombasa, lakini kutokana na hali ya joto ambayo inaibeba Tanzania na kukaa vibaya kwa wachezaji wa Kenya wanaoishi Nairobi kwenye baridi ndio maana mechi hiyo imeahirishwa.

Baada ya mechi dhidi ya Rwanda ambapo Kenya ilishinda bao 1-0, Adel alikiri kwamba; “Hali ya hewa ya Mombasa si nzuri kwetu ni joto kiasi na wachezaji wangu hawajazoea.”

Habari za ndani zinadai baada ya Uwanja wa Kisumu kushindikana kumalizika kwa wakati waandaji walipanga mechi za nusu fainali zichezwe Mombasa na fainali ikachezwe Nyayo mjini Nairobi lakini kwa hali waliyoiona katika mechi za juzi Jumamosi wenyeji wakaamua kupeleka mechi ya Stars Machakos. Mechi nyingine ya nusu fainali itachezwa mjini Mombasa.

Habari za ndani zinadai kwamba Adel amewaambia viongozi wake kwamba endapo Kenya ikicheza na Stars mjini Mombasa itakuwa kwenye wakati mgumu kutokana na Tanzania kuzoea hali ya joto na vilevile ina sapoti kubwa Mombasa kwavile ni jirani na Tanga.

Kenya iko kwenye presha ya kufuzu fainali kwani siku ya fainali nchi hiyo itakuwa ikisherehekea Jubilee ya miaka 50 ya uhuru wake.

Wakati huohuo, Zambia iliitoa Burundi kwa penalti 4-3 katika mchezo wa robo fainali uliofanyika jana Jumapili hivyo kutinga nusu fainali.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images