Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Roma Mkatoliki: Nikikutana na Rais Magufuli ntamuomba msaada huu

$
0
0

Rapa Roma Mkatoliki ameweka wazi akipata nafasi ya kukutana ana kwa ana na Rais John Pombe Magufuli, atakachofanya ni kumweleza tu shida zake binafsi ili asaidiwe kutimiza ndoto zake.

Roma Mkatoliki alisema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema unapokutana na Rais kwa dakika chache ni fursa kubwa hivyo lazima uitumie vizuri kwani ukisema uanze kueleza matatizo ya wananchi unaweza kukosa nafasi ya kueleza mambo yako kutokana na kukosa muda.

Kamati ya Utendaji TFF Kukutana Tena Kwa Dharura

$
0
0

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, itakutana tena kwa dharura siku ya Jumanne Julai 04, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam ambako pamoja na ajenda nyingine, itatathmini mwenendo wa kazi za Kamati ya Uchaguzi ya shirikisho.


Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Salum Madadi amesema kwamba kamati hiyo ya utendaji inakutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1) ya Katiba ya TFF inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6).


Kamati hiyo inakutana baada ya barua ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Wakili Revocatus Kuuli kudai kwamba kuna mitazamo tofauti inayosababisha kutokamilisha majukumu yao kwa asilimia 100 kutoka hatua moja hadi nyingine wakati huu wa mchakato wa uchaguzi.


Kutokana na tofauti hizo, Wakili Kuuli kwa kutumia nafasi ya kofia ya uenyekiti, amesitisha kwa muda mchakato wa uchaguzi hadi hapo hali ya mambo itakapowekwa sawa na Kamati ya Utendaji inayotarajiwa kukutana Jumanne wiki inayoanza kesho.


Hii ni mara ya pili kwa kamati kukutana ndani ya wiki moja kwani Jumamosi Julai 01, 2017 kamati hiyo ya utendaji ilikutana na kufanya uamuzi wa kumpitisha Wallace Karia kuwa Kaimu Rais wa shirikisho.


Kadhalika, Kamati hiyo ya Utendaji ya TFF, ilimpitisha Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.


Viongozi hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakavyoamua kuhusu kesi zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa Selestine. 

JPM Aagiza kukamatwa wanaongea ongea ovyo kuhusu Kibiti

$
0
0

Rais Magufuli amewaonya baadhi ya wanasiasa na kuwataka kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake, Rais Magufuli amesema hayo leo wakati anazindua upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.


Rais Magufuli amewataka wanasiasa kuzungumza mambo wanayoyajua lakini si kuongea ongea tu vitu ambavyo hawavifahamu na kusisitiza kuwa baadhi ya watu ambao serikali inawashikilia katika vyombo vya usalama wanahusika na mauaji ambayo yanatokea mkoani Pwani.


"Lakini niwaombe pia na wanasiasa ambao wameshindwa ku 'contol' midomo yao na muda mwingine wanazungumza hata vitu wasivyovijua, unakuta mwanasiasa anasema watu wamekaa sana rumande anashindwa kuelewa Marekani wale watu wabaya walikaa Guantanamo miaka na miaka, lakini kwetu wanaposhikwa watu ambao wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi kuna watu wanaongea ongea. Pwani kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35 askari zaidi ya 15 na wanaohusika na vifo hivyo ni pamoja na hao waliopo rumande lakini mtu anatoka anasema watu wamekaa mno, unaweza kuona huyo mtu naye anahusika kwa namna moja au nyingine, wasitufanye tukafika hapo sababu wataumia, wajifunze kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake" alisisitiza Rais Magufuli. 


Rais Magufuli anasema kumekuwa na mzaha kwa baadhi ya watu kutokana na kuhongwa pesa ndiyo maana wao kazi yao ni kupinga kila kitu. 


"Mimi nimetuma ujumbe huu ili uwafikie Watanzania na waelewe, tuna mambo makubwa tunashughulikia katika nchi hii, lakini kumekuwa na mzaha mzaha tu, unakuta muda mwingine mnashughulikia rasilimali za watanzania zinavyoibiwa , lakini unakuta mtu mwingine anapinga hadharani kwa sababu amepewa vijisenti, ninawaomba watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao tutangulize masilahi ya nchi mbele, hujasimama hata siku moja kulaani mauaji yanayotokea huko halafu unaibuka unataka sifa za kisiasa eti hawa watu waachiwe, na bahati mbaya watu wanaokufa ni wa chama kimoja tu, nataka polisi mfanye kazi yenu."alisema Rais Magufuli 


Mbali na hilo Rais Magufuli amewataka polisi kuwakamata watu wote ambao wanaongea ongea juu ya mambo hayo ili walisaidie jeshi la polisi katika upelelezi, bila kuwaogopa kwa sura, wala mwendo wao. 

Rais Magufuli Amshukia Lowassa...Magazeti ya Leo Jumatatu

$
0
0


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu Ya July 3

Rais Magufuli Amekosea Sana- Zitto

$
0
0
"Rais anakosea Sana kuhusisha suala la Masheikh waliopo ndani na mauaji ya MKIRU. Amewapa maadui silaha. Acha tumalize kwanza suala la miswada ya Madini kwani ni jambo linalotuunganisha. Tukimaliza tutarudi kuzungumza kuhusu Hii kauli ya Rais.

Umoja na Mshikamano ni silaha ya ushindi." Ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook

Taifa Stars Yainyuka South Africa 1-0, Yatinga Nusu Fainali

$
0
0
Taifa Stars imetinga nusu fainali ya michuano ya Cosafa baada ya kuwatwanga wenyeji Afrika Kusini kwa bao 1-0.

Shuja wa mechi hiyo ambaye ameibuka nyota wa mchezo huo amekuwa ni Elius Maguri ambaye amefunga bao hilo pekee katika kipindi cha kwanza.

Kipa Aishi Manula mara kadhaa alilazimika kuokoa michomo mikali ya washambuliaji wa Afrika Kusini.

Safu ya ulinzi iliyoongozwa na Erasto Nyoni na Salim Mbonde ilionekana kukaa imara tokea kipindi cha kwanza lakini Muzamiru Yassin na Raphael Alpha wakaonekana kufanya vizuri zaidi katika.

Simon Msuva aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Thomas Ulimwengu na kusaidia kuongeza nguvu ya kupandisha presha kwenye lango la Afrika Kusini.

Figisu Figisu Zasababisha TFF Kuhairisha Uchaguzi....

$
0
0
Figisu Figisu Zasababisha TFF Kuhairisha Uchaguzi....
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetangaza kuwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo umesimamishwa hadi Kamati ya Utendaji itakapokutana Juni 4, mwaka huu.
Tamko hilo limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari leo Jumapili mchana kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya wajumbe wa kamati ya uchaguzi kukiuka taratibu.


Tayari zoezi la usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali ikiwemo urais lilikamilika jana Jumamosi tangu lilipoanza Alhamisi iliyopita huku wagombea wawili wakikosekana akiwemo Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambaye anatetea nafasi yake ya urais na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ anayewania nafasi ya Makamu Rais wa TFF kutokana na wahusika hao kuwa rumande.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kudaiwa kufanya juhudi ili Malinzi afanyiwe usaili licha ya kuwa mahabusu wakati ambapo inaelezwa Kaburu aliandika barua ya kujiondoa kwenye mchakato wa uchaguzi.

Chuchu Hans "Mimi na Ray Hakuna Anayewaza Ndoa..Tunaishi Kisela tu"

$
0
0
STAA wa kitambo wa Bongo Movies, Chuchu Hans amefunguka kuwa, baada kupata mtoto aitwaye Jaden na staa mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, kwa sasa hakuna anayewazia ndoa kati yao, badala yake kila mmoja anafikiria kuhusu malezi ya uzao wao huo.

Chuchu aliliambia Wikienda kuwa, yeye na Ray hawajakaa na kulizungumzia suala la ndoa lakini anaamini kuwa siku ikifika mambo yatakuwa bambam.

“Hakuna hata mmoja kati yetu anayeiwazia ndoa. Sasa hivi kila mtu jicho lake lipo kwa mtoto na naamini siku ikifika Ray mwenyewe atazungumza kwa kuwa jambo hili halitaki kulazimishwa hata siku moja,” alisema Chuchu.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Ulisikia Wema Sepetu Ameingia Kwenye Bongo Flava? Basi Huu Ndio Wimbo Aliyoshirikishwa Wema Sepetu

$
0
0
MSANII wa kike anayepanda kwa kasi kwenye gemu la Muziki wa Bongo Fleva Bongo, Haitham Ghazal Seif ‘Haitham’ ambaye pia yuko chini ya Lebo ya MJ Records jana ameachia ngoma mpya aliyomshirikisha Staa wa Bongo Wema Sepetu yenye jina la Play Boy.
 VIDEO:

Wanasiasa Ambao Wameshindwa ku ‘Contol’ Midomo Wanyamaze – Rais Magufuli

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaonya baadhi ya wanasiasa kwa kuwataka kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake. Rais Magufuli amesema hayo leo wakati anazindua upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.


Rais Magufuli amesema hayo leo mapema wakati wa uzinduzi wa upanuzi wa bandari ya Dar es salaam kwa kuwataka wanasiasa kuacha kuzungumza mambo wasiyoyajua na si kuongea vitu ambavyo hawavifahamu na kusisitiza kuwa baadhi ya watu ambao serikali inawashikilia katika vyombo vya usalama wanahusika na mauaji ambayo yanatokea mkoani Pwani.


“Lakini niwaombe pia na wanasiasa ambao wameshindwa ku ‘contol’ midomo yao na muda mwingine wanazungumza hata vitu wasivyovijua, unakuta mwanasiasa anasema watu wamekaa sana rumande anashindwa kuelewa Marekani wale watu wabaya walikaa Guantanamo miaka na miaka, lakini kwetu wanaposhikwa watu ambao wanahusika na mambo ya ajabu katika nchi kuna watu wanaongea ongea.“amesema Rais Magufuli huku akigusia mauaji yanayoendelea Kibiti.

“Pwani kuna watu wamekufa kule zaidi ya 35 askari zaidi ya 15 na wanaohusika na vifo hivyo ni pamoja na hao waliopo rumande lakini mtu anatoka anasema watu wamekaa mno, unaweza kuona huyo mtu naye anahusika kwa namna moja au nyingine, wasitufanye tukafika hapo sababu wataumia, wajifunze kufunga midomo yao wakati serikali inafanya kazi yake,”

Rais Magufuli anasema kumekuwa na mzaha kwa baadhi ya watu kutokana na kuhongwa pesa ndiyo maana wao kazi yao ni kupinga kila kitu.

“Mimi nimetuma ujumbe huu ili uwafikie Watanzania na waelewe, tuna mambo makubwa tunashughulikia katika nchi hii, lakini kumekuwa na mzaha mzaha tu, unakuta muda mwingine mnashughulikia rasilimali za watanzania zinavyoibiwa , lakini unakuta mtu mwingine anapinga hadharani kwa sababu amepewa vijisenti, ninawaomba watanzania wote bila kujali itikadi za vyama vyao tutangulize masilahi ya nchi mbele, hujasimama hata siku moja kulaani mauaji yanayotokea huko halafu unaibuka unataka sifa za kisiasa eti hawa watu waachiwe, na bahati mbaya watu wanaokufa ni wa chama kimoja tu, nataka polisi mfanye kazi yenu.”amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewataka polisi kuwakamata watu wote ambao wanaongea ongea juu ya ili walisaidie jeshi la polisi katika upelelezi, bila kuwaogopa kwa sura, wala mwendo wao.

Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa

$
0
0
Kutana  na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH CHIEF SULTAN MAKATA Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika

Anatibu kwa Njia ya Simu Ukiwa Nchi Yoyote / Mkoa wowote


..JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na  Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Chief Sultan Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU(LIMBWATA). Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine?Una Mpenzi wako ana Pesa na Unataka kumkamata? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.

Chief Sultan Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..
Anatibu kwa Kutumia  Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA,Hutoa  PETE ZA BAHATI inayoendana na NYOTA YAKO. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.HUZUIA CHUMA ULETE NA KUKUPA DAWA YA KUONGEZA FAIDA KWENYE BIASHARA. HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA AU KUDHULUMIWA.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI.Humaliza Kabisa Tatizo la Nguvu za KIUME na Kurefusha Uume kwa Saizi Unayotaka,HUMALIZA KESI YA AINA YOYOTE NDANI YA SIKU 14. na mengi zaidi

Whatsapp/Calls +255 710 279 458 +255 710 279 458

Tiba ni kwa Watu wenye Imani na Dini zote

VIDEO: Sababu iliyofanya uchaguzi Mkuu wa TFF kusitishwa leo

$
0
0
Wakati headlines za hatma ya Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake Selestine Mwesigwa zikiendelea kutawala wakiwa chini ya mikono ya sheria kwa tuhuma mbalimbali, headlines mpya zimeibuka kuhusiana uchaguzi Mkuu wa shirikisho hilo.

Uchaguzi Mkuu wa TFF ulipangwa kufanyika August 12 2017 lakini mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Revocatus Kuuli ameamua kuahirisha kutokana na sababu kuu ikitajwa kuwa uwepo wa mgawanyiko ndani ya kamati hiyo, hivyo leo July 2 Kaimu Katibu Mkuu wa TFF Salum Madadi amepokea taarifa za kuahirishwa kwa uchaguzi Mkuu.



Tuna neno moja tu ambalo tunataka liwafikie wadau wetu wa mpira hapa nchini, kumejitokeza mgawanyiko kwenye kamati yetu ya uchaguzi katika kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi na tumepokea barua ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi tumeshauriana nae na tumesitisha zoezi la mchakato wa uchaguzi” >>> Salum Madadi

Miongoni mwa vitu vinavyodaiwa kuleta tofauti ni kukosekana wakati wa usaili kwa mmoja kati ya wagombea wa nafasi ya Urais Jamal Malinzi anayetetea nafasi yake na Geofrey Nyange Kaburu anayegombea nafasi ya Makamu wa Rais, Kaburu na Malinzi wote wapo rumande kwa tuhuma tofauti. VIDEO:

Beyonce na Jay-Z wampa jina la kiislamu mtoto wao

$
0
0

Baada ya kujifungua mapacha wiki kadhaa zilizopita sasa,Beyonce na mume wake Jay-Z wabainisha majina ya wanao wawili .


 Mapacha wa magwiji wa sanaa ya Muziki kutoka Marekani wamepewa majina ya Rumi na Sir .


Rumi ni jina la mwanafalsafa wa kiislamu aliyeishi katika karne ya 13 ambaye hadi wa leo anakumbukwa kwa kazi yake ya mashairi na maneno yaliyopendekeza upendo ,furaha na uvumilivu .


Wasanii hao nyota wamesemekana kuwakilisha haki ya miliki kwa majina ya wanao kama Rumi Carter na Sir Carter ili kuhakikisha kwamba hamna mtu mwengine atakayefaidi kutokana na majina hayo .

KIMENUKA..Viongozi Sita wa America Kusini Wanadai Walipandikizwa Ugonjwa wa Cancer Na Marekani

$
0
0
Viongozi sita wa America ya Kusini inadaiwa waliuugua ugonjwa wa cancer kwa nyakati tofauti, inadaiwa viongozi wa nchi hizi za walipinga vikali sera za Marekani katika masuala ya kiuchumi na siasa. Aliyekuwa Rais wa Venezuela hayati Hugo Chaves aliwahi kutamka hadharani kuwa yeye binafsi alikuwa miongoni mwa viongozi waliopandikiziwa ugonjwa wa Cancer kupitia shirika la ujasusi la CIA Rais huyo alifariki kwa ugonjwa huo. Marehemu Hugo Chaves alidai alishawahi kuonywa na aliyekuwa Rais wa Cuba Fidel Castro kuwa ajihadhari sana kwani hawa Wamerekani walikuwa na teknologia ambayo ilikuwa rahisi kupandikizia mtu ugonjwa wa Cancer. Kuna viongozi wa kiafrika ambao nao walikufa vifo vya kutatanisha baada ya kuwa na msimamo dhidi nchi za magharibi kama aliyekuwa Waziri mkuu wa Ethiopia Menas Zenawi wa Ethiopia na Bingwa Mutharika wa Malawi na Rais Satta wa Zambia,. Aliyekuwa Rais wa palestina Yasser Arafat naye baada ya maiti kufanyiwa uchunguzi iligundulika naye alifariki kwa cancer ya kupandikizwa.

sources: Pravda News

DUNIA Inakwisha...Kanisa Katoliki Labariki Ushoga na Usagaji.....

$
0
0
Jamaa akiwa na mke wake huko Malta.

Kanisa katoliki nchini Malta labariki ndoa za jinsia moja au maarufu kama ushoga. Askofu Charles Scicluna aliliambia kanisa moja nchini humo kua kanisa halipingani na ushoga na halina nia ya kupingana na ushoga kama watu wengi walivyodhani.

Nchi hiyo pia imetunga sheria za kuruhusu ndoa za jinsia moja kama ilivyo kwa nchi nyingi za ulaya.

KUMEKUCHA: Wanaume Wengi wa Siku Hizi Wana Tabia za Umama Umama / Ukike Kike!!!

$
0
0
Zifuatazo ni sababu kadhaa ambazo ' Watafiti ' hawa wameziorodhesha ambazo zinaashiria tabia za Wanaume na Vijana wa siku hizi ambazo zimeondoa ule Uanamume / Ubaba / Ujana wao kiasi cha hata ' kuwasikitisha' Wanawake / Mabinti wengi:

  • Kutukuka kwa ' umbea ' na kukubali ' Kutawaliwa ' na Wapenzi wao nyumbani
  • Kutukuka kwa kupiga ' selfies ' sana
  • Kutukuka kwa Kuvaa Suruali zao halafu wanatuachia wazi ' makalio ' yao
  • Kutukuka kwa kupenda ' Kujiremba ' kuliko Dada / Mama / Wake / Mademu zetu
  • Kutukuka kwa kutokuwa ' Wasiri ' hasa kwa mambo yetu ya ' Faragha '
  • Kutukuka kwa kula Chips, mikate ya Siagi na Jam, Mayai ya Kukaanga na ' Soseji '
  • Kutukuka kwa kutoweza kuwafikisha ' Vileleni ' Wapenzi wao
  • Kutukuka kwa wengi wao kupenda kubana sauti pale wanapokuwa wanaongea
  • Kutukuka Kwao kwa kupenda Kuvaa mavazi ' yanayobana ' wanaita ' Vimodo '.
  • Kutukuka kwa Kuvaa ' hereni ' masikioni na ' Kusuka ' nywele zao
  • Kutukuka kwa kupenda Kukaa muda mrefu na Watoto wa Kike kuliko wa Kiume

Hizi ni baadhi tu ila ' yamesemwa ' mengi na hawa ' Watafiti ' hivyo ili ' usinichoshe ' au ' tusichoshane ' sana tafadhali kama unataka ' Kujijua ' kama Wewe mwana JF ( Mwanaume ) una tabia za Kimama mama / Kike Kike au upo kama akina sisi ( GENTAMYCINE ) wenye tabia za Kibaba Baba / Kiume Ume basi tafuta ' Kopi ' yako ya MWANANCHI au ingia zako tu MWANANCHI online uweze kusoma kila kitu.

Nawasilisha.

SUMAYE Afunguka Ukweli Mchungu "Katiba Mpya Imewekwa Pembeni..Watawala hawataki Madaraka yao Yadhibitiwe na Katiba"

$
0
0
Waziri  Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, amesema Katiba mpya imewekwa pembeni, kwani watawala hawataki madaraka yao yadhibitiwe na Katiba.

Sumaye, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, kwenye mahafali ya vijana wa chuo kikuu wa chama hicho (Chaso).

Alisema Katiba inayopendekezwa ni ya wananchi na ilipitishwa na Bunge, lakini inaonekana si jambo la kipaumbele na wala haitashughulikiwa tena kwa sababu itawadhibiti watawala.

“Mchakato wa Katiba mpya umeigharimu nchi fedha nyingi za walipa kodi na kuitupa ni “makanikia” nyingine, najua Rais John Magufuli  amekwishasema yeye haambiwi la kufanya, lakini sisi tutaendelea kumkumbusha yale ambayo tunadhani ni muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.

“Si jambo la kupuuzwa. Kama ni la kupuuzwa basi awakamate wote waliohusika na uamuzi huo, maana ni ubadhirifu unaofanana na ule wa makanikia,” alisema.

Mwenyekiti huyo alisema chama hicho pamoja na washirika wake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wataendelea kudai Katiba mpya hadi itakapopatikana.

Alisema licha ya watawala kueleza kwamba Tanzania ina mfumo wa vyama vingi, hata hivyo si kweli, bali ina mfumo ‘bandia’ wa siasa za vyama vingi.

“Tuna mfumo ‘bandia’ wa siasa ya vyama vingi, mfumo wa chama kimoja kilichovaa ngozi ya vyama vingi, mfumo wa vyama vingi vya siasa ni lazima ufuate utawala wa sheria na unaolinda, unaoheshimu na kuitetea Katiba ya nchi ambayo watawala wameapa nayo wakati wa kukabidhiwa madaraka.

“Ukiona katika nchi watawala hawatii sheria wala katiba ya nchi, basi hakuna utawala wa kweli wa vyama vingi vya siasa, bali kuna utawala wa imla uliovaa ngozi ya demokrasia ya vyama vingi vya siasa.

“Tanzania leo hakuna uhuru wa watu kutoa na kupokea habari kama Katiba yetu inavyotaka. Ibara ya 18 ambayo inazungumzia “Haki na Uhuru wa Mawazo,” alisema.

Alisema mfumo au demokrasia ya vyama vingi haurusu ubabe katika utawala na uongozi wa nchi.

“Kama kiongozi anatawala kwa ubabe na vitisho, lazima tukubali kuwa ama Katiba tuliyonayo siyo sahihi au mfumo uliopo siyo wa demokrasia ya vyama vingi kivitendo,” alisisitiza.

JAHAZI la James Rugemalila na Seth Lazidi Kuzama..Waongezewa Mashtaka Mapya

$
0
0

Jamhuri imeongoza mashatka mapya sita kwa watuhumiwa wa kesi ya Escrow James Rugemalila na Harbinder Sethi
Mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakili  Shedrack Kimario amewasomea Mashtaka Mapya watuhumiwa hao pamoja na Uhujumu uchumi.

Awali watuhumiwa walishtakiwa kwa mashtaka sita na sasa yameongezwa sita mengine na kufikia 12.

Kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 14 Julia 2017

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo....!!!

MBUNGE Chadema Amuunga Mkono Magufuli

$
0
0
MBUNGE wa Same Mashariki (Chadema), Naghenjwa Kaboyoka amesema mradi wa ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme katika bonde la Mto Rufiji ambao Rais John Magufuli amesema ni lazima ufanyike lije jua au mvua, utaokoa fedha ambazo serikali imekuwa ikigharamia umeme wa mafuta.

Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalumu juzi, Kaboyoka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), alisema nchi inapotaka kwenda kwenye uchumi wa viwanda, umeme wa dizeli au petroli, kwa kuwa ni wa gharama kubwa, hufifisha mkakati huo.

Akizungumza jijini juzi, Rais Magufuli alisema ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji (Stiegler’s Gorge) mkoani Pwani lazima ufanyike.

Rais alikuwa akizungumza katika ufunguzi wa Maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba), Manispaa ya Temeke.

Aliwaeleza wawekezaji kuwa changamoto ya umeme wa uhakika itakwisha kupitia bwawa hilo, kwani nchi itakuwa na umeme wa jumla ya megawati mpaka 5,000 utakapokamilika mradi huo.

“Inyeshe mvua, liwake jua Stiegler’s Gorge itajengwa," alisema Rais Magufuli kwa sababu "tumeamua kuchukua juhudi za makusudi kuifufua na ninawahakikishia wawekezaji tunaifufua...

"Na tunaanza kwa fedha yetu.”

GHARAMA NAFUU
Mama Kaboyoka alisema umeme wa maji ndiyo wa gharama nafuu zaidi duniani na kwamba nchi itanufaika zaidi kwa kuwa mradi huo utatoa umeme mwingi kwa gharama nafuu.

“Ingekuwa ni kuchimba madini hapo ningesema kutakuwa na uharibifu, lakini kutegeshea kujenga mitambo ya maji na mazingira mtu yeyote ukitengeneza maji utalinda na mazingira yako kwa kuweka miti,”alisema Kaboyoka akizungumzia maoni ya wanaharakati kuwa ujenzi huo utaharibu mazingira.

Aliuliza bwawa la Kidatu mkoani Tanga lenye uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 200, kwa mfano, limeharibu mazingira gani?

Alisema ni vyema kuangalia maoni ya wanaharakati huwa ni kwa faida ya nani, hasa baada ya mradi huo kuwa 'kizobo' cha mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma kupitia mikataba ya ununuzi wa umeme wa dharura.

“Kinachotakiwa ni kuwachukulia hatua kwanza hawa waliotuingiza kwenye mikataba mibovu," alisema zaidi Kaboyoka.

"Huwezi kununua umeme kutoka IPTL kwa zaidi ya Sh. 520 halafu wewe ukauze kwa bei nafuu... yaani unakwenda sokoni kununua mahindi debe moja kwa Sh. 5,000 halafu unakwenda kuuza kwa Sh.2,000. Hivi kweli ni akili hiyo?”

Ujenzi wa bwawa hilo katika Mto Rufiji unatarajiwa kufanywa na wataalamu kutoka Ethopia.

“Miaka 10 ijayo umeme utakaotokana na maji hayo utakuwa mkubwa sana, ina maana nchi yetu itaweza kupata nishati ya kutosha kwa viwanda vyake."
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images