Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Huyu Mwanamke Ndio wa Kuoa ila Sijui Kama Anapatikana Tanzania.......

$
0
0

1. Mpenzi wako akija kwako na akakakuta unakula ugali na kachumbari na akaamua kula nawe..huyo muoe....

2.ukienda nae hotelini akaamua kuagiza ugali dagaa na maji tu...muoe anajua uchumi.

3.Mdada ambaye akimuona mkaka mwingine anaendesha Land cruiser na wewe una vitz yako Number A lakini akaamua kuja kwako...usimuache...

4.Mwanamke akikutembelea kwako akakuta nguo zako chafu akafua zote mpaka za wadogo zako, huyo mke usimuache!

5. Mwanamke unampa sh elfu tano akafanye shopping sokoni anakurudishia chenchi..huyo usimuache...anajua kubana bajeti na muaminifu.

6. Ukimpata mwanamke ambaye anakupigia simu na kukuuliza kama anaweza kukutumia credit au hela ya lunch, au anakupa pocket money saa nyingine, huyo tangaza ndoa fastaaa!

7.Mwanamke ambae anakupa password ya benki,laptop, simu na emails zake, huyo ni zaidi ya malaika.oa haraka..watamgombania wenzako!

8.Ukipata mwanamke ambaye mkipanda daldala analipa nauli au mkitoka out analipia bill ya chakula na vinywaji...huyo usimuache! anajua wajibu wa wana ndoa!

9.Ukimpata mwanamke ambae mnapokula, yeye anachagua mifupa tu na minofu anakuachia wewe, huyo usimuache...oa fastaaa... anajali afya yako!

10. Ukipata mwanamke ambae kila ukimuuliza angependa umletee nini ukirudi toka kazini, lakini yeye anakwambia hahitaji kitu ila anataka urudi salama, huyo ndio mke...sio kila siku unatumwa chips na kuku!

Fiza Ally Anataka Aanze Kupiga Picha za Utupu...Ataka Mil 100 tu

$
0
0
Mtangazaji wa kipindi cha familia Faiza Ally amesema yupo tayari kupiga picha za utupu endapo mtu anayemtaka kupiga picha hizo atafikia dau analolitaka kama Mil 100
Aliyaongea hayo alipokuwa akihojiwa na kipindi cha Shilawadu Clouds FM kuwa atapewa milioni 6 ili apige picha hizo

SIKILIZA HAPA:

Video: RC Makonda Aeleza Namna Atavyojenga Majengo 402 ya Shule za Dar

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda Jumanne hii  ameelezea dhamira yake ya kuhakikisha ujenzi wa ofisi za kisasa 402 za walimu pamoja na vyoo kwa shule za msingi na sekondari zilizobainika kuwa upungufu wa huduma hizo.

Ofisi hizo za kisasa zitakuwa na sehemu ya chumba cha mwalimu Mkuu,Chumba cha Muhasibu, Chumba cha Katibu Muktasi pamoja na ofisi za Msaidizi wa Mwalimmu mkuu na walimu wote huku zikiwa na Vyoo vya kisasa pamoja na Bafu.

“Siwezi kuwa na amani kama walimu wangu hawana ofisi wala vyoo katika shule 402, ni haibu na fedhea kwa walimu kugombania choo na mwanafunzi au kutumia vyoo vya majirani au Bar, hii sio heshima ya mwalimuwa Mkoa wangu,ndio maana nimeamua kuanza kufanyia kazi changamoto hizi,” Alisema Makonda.

Kutokana na gharama za ujenzi kuwa kubwa Mheshimiwa Makonda ameviomba vyombo vya Ulinzi na usalama vya Mkoa wa Dar es Salaam kumpatia mafundi wa ujenzi kama sehemu ya kuunga mkono jitiada alizoanzisha za ujenzi wa Ofisi hizo ambapo vyombo hivyo vimeridhia kumuunga mkono.

“Kipekee napenda kuvipongeza vyombo vyote ya Ulinzi vilivyoamua kuniunga mkono vikiongozwa na Mkuu wa JKT kwa utayari wa kunipa vijana watakaofanya ujenzi huo, na niwaeleze kuwa ujenzi utaanza baada ya wiki mbili zijazo” Aliongeza Makonda.

Ujenzi wa Ofisi hizo unategemea zaidi jitiada za wadau wa maendeleo ikiwemo wamiliki wa kampuni pamoja na Wananchi wenye dhamira ya kuona Walimu wanafanya kazi katika mazingira Mazuri.

Tayari jitiada za Mheshimiwa Makonda zimeanza kuzaa matunda baada ya kufanikiwa kupata Mabati 11,000 na mifuko ya Saruji 1,000 ambapo Mahitaji ni Mabati 50,000, Mbao zaidi ya Million mbili  pamoja na vifaa vingine vya ujenzi.

Makonda amesema ataanza kutembelea viwanda vinavyojihusisha na uzalishaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemoMabati, Saruji, Nondo na vinginevyo kuona namna wanavyoweza kuunga mkono ujenzi huo ili kuhakikisha walimu wanafanya katika mazingira rafiki.

TAZAMA VIDEO:

Tazama Wimbo Mpya wa Goodluck Gozbert – Shukurani

$
0
0
Goodluck Gozbert ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Shukurani’. Wimbo huo ameutayarisha yeye mwenyewe kupitia studio za Mpo Africa wakati video imeongozwa na Destro kutoka Wanene Entertainment.

VIDEO:

SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo

$
0
0

KUTANA na Mtaalam wa Tiba za Asili Toka Komoro Maalim Fadhili..Anatibu Magonjwa Mbali Mbali na Kusafisha Nyota

$
0
0
KUTANA NA MAALIM FADHIL RASHID KUTOKA KOMORO NI MTAALAM WA TIBA ZA ASILI

UNASHIDA NA MCHUMBA UNATATIZO PESA HAIKAI KURUDISHA MUME AU MKE KWA MUDA MFUPI MVUTO WA MAPENZI

MVUTO WA BIASHARA KUMSHIKA MUME AU MKE ASIKUSUMBUE

DAWA YA ( LIMBWATA )KUMTAWALA MPENZI WAKO KWA SABABU MAALUM KUSAFISHA NYOTA ILI UWE NA MUONEKANO

NA PIA ANATOA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA MASHARTI

NA KUMILIKI MALI DAWA YA KUONGEZA UUME SAIZ UIPENDAYO

DAWA YA NGUVU ZA KIUME INAPATIKANA PIA ANAYO DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEP KUA NA UMBO BOMBA UMEIBIWA AU KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALI YAKO NDANI YA MASAA 24 ANAFUNGA KESI NA KUPATA HAKI YAKO DAWA YA MVUTO WA BIASHARA KUUZA MALI YAKO KWA HARAKA KUZUIA CHUMA ULETE

NA KUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHA KUTESEKA ACHA KUHANGAIKA MAALIM FADHIL RASHID

YUPO TANZANIA KWA AJIALI YAKO. CALL...+255719362806/
+255763276239/

WhatsApp IMO +255785786436/

Historia ya Sanamu ya Askari, Dar es Salaam

$
0
0
Sanamu ya Askari au Askari Monument ni sanamu iliyopo kwenye kitovu cha jiji la Daressalaam kwenye mahali ambapo mitaa ya Samora na Azikiwe (zamani: Maktaba) zinakutana.

Sanamu inamwonyesha askari Mwafrika katika sare ya kijeshi ya wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia (1914-1918) akishika bunduki yenye kisu cha kando na kutazama upande wa bahari.

Iliwekwa hapa 1927 na Waingereza kama kumbukumbu ya askari na wapagazi Waafrika waliopigania vita hii katika Afrika ya Mashariki hasa kati ya Uingereza na Ujerumani ambao wengi wao walikufa.

Kuna maandishi ya kumbukumbu kwa Kiingereza na Kiswahili kilichondikwa kwa herufi za Kiarabu na herufi za Kilatini pia. Maneno yake kwa Kiswahili ni kama yafuatayo:

"Huu ni ukumbusho wa askari Waafrika wenyeji waliopigana katika Vita Kuu na ni ukumbusho pia kwa wapagazi ambao walikuwa miguu na mikono ya majeshi. Ni ukumbusho pia kwa watu wote waliotumika wakafa kwa ajili ya mfalme na nchi yao katika Afrika ya Mashariki kwenye Vita Kkuu toka mwaka 1914 mpaka 1918 . Ukipigania nchi yako ujapo umekufa watoto wako watalikumbuka jina lako."


Mahali pa sanamu hii iliwahi kuwa na sanamu ya meja Hermann von Wissmann aliyekuwa gavana wa kwanza wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani na sanamu hii ilibomolewa na Waingereza walipoteka mji katika mwaka 1916

Msemaji wa Jeshi Aliyedaiwa Kutoweka Ajitokeza Kenya

$
0
0
Wizara ya ulinzi nchini Kenya imeshutumu taarifa zilizokuwa zimeenezwa kwamba msemaji wa jeshi la Kenya Kanali Joseph Owuoth alikuwa ametoweka.

Waziri Raychelle Omamo, akihutubia wanahabari, amesema taarifa kama hizo zinatishia usalama na kuzua wasiwasi miongoni mwa maafisa wa jeshi na familia zao.

"Kanali J. M. Owuoth hajatoweka na yuko nasi hapa, akiwa hai na mzima wa afya," alisema Bi Omamo.

Kanali Owuoth aligonga vichwa vya habari baada ya kuthibitisha kwamba nyaraka zilizokuwa zimetumiwa na muungano wa upinzani nchini humo Nasa kudai kwamba serikali inapanga kutumia jeshi kutekeleza 'mapinduzi' ili kuendelea kusalia madarakani zilikuwa halisi.

Msemaji huyo hata hivyo alisema nyaraka hizo zilinukuliwa na kufasiriwa visivyo.
Bi Omamo, kwenye kikao hicho, alisema baada ya uchunguzi, imebainika kwamba nyaraka hizo zilizotumiwa na muungano wa Nasa zilikuwa ghushi.

Taarifa za kudaiwa kutoweka kwa Kanali Owuoth zilikuwa zimezua wasiwasi mkubwa kwani zilijiri siku moja baada ya mwili wa meneja wa teknolojia katika Tume ya Uchaguzi Kenya (IEBC) Chris Msando, aliyetoweka Ijumaa usiku, kupatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City jijini Nairobi pamoja na mwili wa mwanamke mwingine.

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati aliambia wanahabari kwamba hakukuwa na shaka kwamba Bw Msando aliteswa kabla ya kuuawa na kuwataka polisi wafanye uchunguzi wa kina kufumbua kitendawili kuhusu kuuawa kwake.


Mkojo wa Wema Sepetu Watikisa Mahakamani Baada ya Kukutwa na Chembe Chembe za Bangi

$
0
0
KESI inayomkabili staa wa Bongo Muvi, Wema Sepetu, jana ilichukua sura mpya baada ya mawakili wa pande mbili, ule wa utetezi na Jamhuri kuchuana kuhusu mkojo wa msanii huyo uliochukuliwa na kupimwa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali wakati wa upelelezi wa polisi kuhusiana na mwanadada huyo kudaiwa kutumia madawa ya kulevya.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba, shahidi wa kwanza wa upande wa Jamhuri aliyefahamika kwa jina la Elias Mulima kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali akisoma ripoti ya uchunguzi alisema mahakamani hapo kuwa, mkojo wa Wema baada ya kupimwa ulikutwa na chembechembe za bangi.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Peter Kibatala, alisema ripoti hiyo iliyosomwa na Mulima ina upungufu mwingi wa kisheria. Baada ya kutokea malumbano hayo Hakimu Mkazi Simba aliwaomba mawakili wa pande zote mbili kuridhia apate muda wa kuipitia taarifa hiyo ya Ofisi ya Mkemia Mkuu ili itakapoendelea aweze kuitolea ufafanuzi. Awali, kesi hiyo iliahirishwa kusikilizwa kwa muda mahakamani hapo kutokana na wakili wa Wema kutokuwepo hivyo ikaanza kusikilizwa saa 6:30. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 4, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, Wema anatuhumiwa kukutwa na msokoto mmoja wa bangi na vipande viwili vidogo vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08. Mbali na Wema washitakiwa wengine ni wafanyakazi wake wa ndani Angelina Msigwa (21) na Matrida Abbas (16), ambapo wote wanashtakiwa kwa kosa moja la kukutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya. Msanii huyo na wenzake hao wako nje kwa dhamana ya wadhamini wawili waliosaini Sh. 5,000,000 kila mmoja. Inadaiwa kuwa Wema na wenzake walitenda kosa hilo Februari 4, mwaka huu, nyumbani kwake Ununio, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

VIDEO: Maskini Jini Kabula..Adaiwa Kupatwa Uchizi.....Adai yeye ni Mmarekani na Rihanna ni Dada yake....

$
0
0
Ikiwa ni takriban miezi miwili na siku kadhaa tangu kuzagaa kwa ishu za kuugua ugonjwa wa afya ya akili ukiambatana na kuchanganyikiwa kwa mwigizaji wa sinema za Kibongo, hasa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, hatimaye ameibuka na kunena mambo mazito yenye kuumiza juu ya sakata hilo.
Miongoni mwa mambo anayodai kutendewa, Kabula alisema kuwa, alilazimishwa kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi ‘ngoma’ kisha akaanzishiwa dozi ambayo hakuwa anajua kinachoendelea.

MACHOZI KABLA YA SIMULIZI
Muda wote Kabula alikuwa akitiririkwa na machozi yaliyobeba hisia na kila tafsiri ya uchungu huku akitamka maneno mengi makali kwa mfululizo (busara imetumika kutoyaanika).
MKASA WENYE KUUMIZA
“Ninakumbuka siku hiyo nilitoka kanisani, wakati huo nikiishi kwa dada aitwaye Angel. Nilipofi ka nyumbani nilishangaa kukuta watu wengi, nikashtuka kwa kudhani kuna msiba, lakini ghafl a nilikamatwa kwa nguvu na kufungwa kamba.

“Niliuliza kuna nini, lakini hakuna aliyenijibu, zaidi ya baadhi yao kuanza kulia. “Nilikuwa na nguvu sana, maana ndugu zangu wa Marekani akiwemo pacha wangu, Mwanamuziki Rihanna wa Marekani (hapa stori inaanza kuwa mchelemchele) walikuwa wameshatuma makombora kuja kuniokoa mimi malaika niliyezaliwa Tanzania kwa bahati mbaya ili kuja kuikomboa nchi hii.
“Wakanipakiza kwenye lori na kunipeleka Muhimbili (hospitalini). Nilikuwa ninalia sana huku
nikipambana nao kwa nguvu zote, kiukweli nilichoka sana jamani (machozi). “Nimeteswa na kuumizwa sana, eti mimi ninaitwa kichaa, kweli eti (jina la mwandishi), mimi ninaweza kuwa
kichaa kwa unavyonifahamu supastaa mkubwa Bongo? Aah! Hii dunia ni katili sana, lakini Mungu hashindwi na jambo,” ndivyo alivyoanza kusimulia Kabula na kuendelea:


SIMULIZI INAKOLEA SASA
“Wakanipeleka Muhimbili. Lakini kabla ya hapo walishanichoma sindano yenye dawa kali na kunilegeza mwili huku wakinilazimisha kumeza dawa, Mungu anajua (kilio).

“Hapo nikapitiwa na usingizi. Nilipozinduka nilijikuta hospitalini, lakini sasa Wamarekani walikuwa wamekizunguka kitanda changu huku wakirekodi matukio yote (picha limeanza mchelemchele tena). “Basi wakaniuliza kama ninalifahamu eneo hilo, nikawajibu ni Ocean Road (Hospitali ya Saratani), wakaitikia ni kweli japokuwa baadaye nilikuja kujua kwamba ni Muhimbili, yaani walinifanya kama zuzu au mdoli mdogo.”

AFUNGIWA WODI YA VICHAA
Kabula aliendelea kusimulia; “Eti cha ajabu nikafungiwa kwenye wodi ya vichaa. Huko nilikutana na giza la ajabu (kimya, kilio na kigugumizi cha hasira). Kulikuwa na wachawi wakiwa uchi wa mnyama, wakijisaidia karibu kabisa na nilipoweka uso wangu. “Ilikuwa kama nipo kuzimu, lakini hata hivyo, nilijitambua kuwa mimi si Mtanzania ila ni Raia wa Marekani na hata Rihanna ambaye ni pacha wangu nilishamwambia, akasema atakuja kurusha makombora ya ajabu nchi nzima iteketee (mchelemchele tena).  “Nikafungwa kwa minyororo, hebu ona nilivyoumia jamani (akifunua gauni na kuonesha alama za kufungwa eneo la mapajani na makovu sehemu mbalimbali mwilini).

ALIFANYIWA HAYA PIA
“Eti nilipimwa damu na kuambiwa nina Virusi Vya Ukimwi, nikapewa vidonge vya kumeza na mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kupokea ili niwafurahishe lakini ukweli sina Ukimwi. Kwa kweli sijawahi kupitia kwenye kipindi kigumu kama hiki, wananionea wivu tu kwa kuwa mimi ni mzuri na mrembo kuliko mama yao yule ambaye walimvisha matambara meusi mbele ya moto mkubwa (mchelemchele tena).


HAJAWAHI KUSINZIA
“Unajua sijawahi kusinzia hata kidogo, walinichoma madawa ambayo yamenikosesha usingizi kwa zaidi ya miezi miwili sasa, yaani usingizi hauji kabisa, si unaona nilivyokondeana jamani, nimechakaa kama chokoraa, sijui hatima yangu, lakini ninamuachia Mungu.”

Kabula aliendelea kusimulia kuwa, baadaye alitolewa wodini na kupelekwa maeneo ya Mbagala jijini Dar, lakini kwa kile alichokiita manyanyaso na masimango alitoroka na kukimbilia kwa rafi ki yake kipenzi ambaye ni msanii wa fi lamu za Kibongo, Esha Buheti ambaye alimkuta akijiandaa kwenda Mbezi-Beach ukweni kwake kwa maandalizi ya kujifungua (ana mimba ya miezi tisa na wiki mbili sasa), ambaye alimshauri aende kwa rafi ki yake mwingine aitwaye Naima maeneo ya Magomeni. Alisema kuwa, huko kwa Naima alikaa siku moja kabla ya kutoroka na kufika Ofisi za Global na kusimulia mkasa mzima.

ETI AMETENGWA
Kabula alisema kuwa, watu wengi wamemtenga na wamekuwa wa kwanza kumsema vibaya na wakati mwingine kumcheka kwa jambo ambalo halijui kwani anajiona mzima wa afya. “Watu wengi ni wanafi ki, sina hata mpango nao na sitaki hata kuwasikia kwa kweli,” alisema Kabula.

APELEKWA KITUO CHA POLISI
Baada ya mahojiano maalum ‘yaliyotafuna’ zaidi ya saa tatu, Kabula alisema kuwa, hana pa kwenda na Global ndiyo msaada wake wa mwisho, ambapo viongozi walimkirimia chochote kwa chakula na nauli ambapo walishauriana kumpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay huku ndugu zake wakitafutwa.


ESHA BUHETI ATINGA POLISI
Baada ya mwandishi wetu kumfikisha Kabula kituoni hapo, aliendelea kuwatafuta ndugu zake na rafiki yake, Naima kasha msanii Esha Buheti ambaye ndiye alifi ka pekee usiku wa manane licha ya kuwa mjamzito wa kujifungua wakati wowote ambapo alishauriana na askari na kukubaliana wamuache hapo hadi kesho yake (Alhamisi) kwa utaratibu mwingine.

NDUGU ANENA YA KUSHANAGAZA
Mwandishi wetu alimtafuta dada wa Kabula ajulikanaye kwa jina la Angel ambaye alisisitiza kuwa, suala la Kabula kulala polisi hadi kesho yake lakini alisema imefi ka hatua wamemshindwa kwani anaumwa kwa kiwango kinachokatisha tamaa. “Kabula anaumwa mno jamani, tunacho hadi kibali cha mahakama ili hata akimdhuru mtu asichukuliwe hatua yoyote.

Kinachoshangaza ni kwamba ana kumbukumbu ya matukio yote na asilimia kubwa ya yale aliyokueleza (baada ya kupewa madai ya Kabula), ni kweli kabisa hapa tulipo tunajiandaa kumpeleka nyumbani Mwanza kwa utaratibu mwingine,” alisema ndugu huyo.



ASUBUHI ALIAMSHA DUDE
Alfajiri ya Alhamsi, mwandishi wetu alikuwepo Kituo cha Polisi cha Oyster bay ambapo alimkuta Kabula akiwatolea ‘mbofumbofu’ askari kwa kuwaporomoshea maneno makali yasiyoandikika, jambo lililowashangaza wengi.

NENO LAKE KWA WATANZANIA
“Watanzania wajue mimi siyo kichaa, lakini huu ni mchezo ninaofanyiwa na watu ambao ni wabaya wangu, nimekonda na kuwa siyo Kabula mnayemjua.

“Naombeni mjue kuwa nina matatizo makubwa sana. Nina mateso kama kufungiwa ndani, nisaidieni jamani, simu yangu imezuiwa, nimetengwa na watu wananikimbia, sijui mwanangu yupo katika hali gani, baba yake (Tuesday Kihangala ‘Chuzi’) hana mawasiliano na mimi. “Nimedhalilishwa sana, ila ninakwenda Marekani kushitaki kwa Obama na Magufuli (mchelemchele unaingia tena), nisaidieni,” alisema Kabula.

KUTOKA GLOBAL TV
Kwa mtazamo ambao gazeti hili limeushuhudia kwa Kabula, kuna kila dalili ya kuwepo kwa tatizo kubwa kwani mazungumzo yake hayana mpangilio sahihi hivyo watu wake wa karibu waungane naye katika kipindi kigumu anachopita kwa kuangalia namna ya kumsaidia.

TAZAMA VIDEO:




MWANDISHI : BRIGHTON MASANU | GLOBAL TV ONLINE

Jack Wolper "Nitaendelea Kubadili Wanaume Nnavyotaka"

$
0
0

WAKATI mashabiki wakiwa bado wanamshangaa staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Massawe‘Wolper’ juu ya tabia yake ya kubadili wanaume kila kukicha, katika hali ya kushangaza, ameibuka na kudai kuwa ataendelea kubadili wapenzi, muda wowote atakapogundua kuwa aliyenaye, hana vigezo.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Wolper alisema hawezi kuogopa maneno ya watu wanayosema juu yake kwa vile hawaelewi anachokumbana nacho katika mapenzi, kwani hawezi kung’ang’ania kukaa kwenye uhusiano ambao haendani nao au unampa shida. “Unajua unapokuwa na mpenzi huwezi kujua kuna tabia utakumbana nazo ambazo haziendani na wewe, lakini pindi unapogundua ni bora kuondoka kuliko kukaa sehemu ambayo huna furaha nayo,” alisema Wolper.
Staa huyo aliongeza kuwa hata mtu aliyenaye hivi sasa endapo atagundua kama tabia hazirandani, ataangalia ustaarabu mwingine kwani haogopi kusemwa kuhusu kubadilisha wapenzi.

GPL

Bibi Harusi Ajaribu Kumuua Mumewe Baada ya ndoa

$
0
0

Bibi harusi katika jimbo la Tennessee nchini Marekani ametiwa nguvuni baada ya polisi kusema kuwa alitoa bunduki kwenye gauni lake la harusi na kumtishia mumewe saa chache tu baada ya kufunga ndoa.

Kate Elizabeth Prichard, mwenye umri wamiaka 25, alikuwa bado amevalia gauni la harusi wakati alipokamatwa katika hoteli moja katika mji wa Murfreesboro.

Alidaiwa kuchukua bunduki aina ya pistol, na kuiweka kwenye kichwa cha mumewe na kufyatua.

Bunduki haikuwa na risasi ,lakini baadae alidaiwa kuijaza risasi na kufyatua angani, jambo
lililowafanya waliokuwa wakishuhudia tukio hilo kukimbia.

Walioshuhudia tukio hilo waliandikisha taarifa kwa polisi ndipo polisi walipowasili eneo la tukio.
Walisema wawili hao walikuwa wakinywa pombe nje ya hoteli.

Sajenti polisi katika mji wa Murfreesboro Kyle Evans alisema kuwa maharusi hao wote wawili hawakushirikiana na mamlaka.

"Alivuta pistol kutoka kwenye gauni lake la harusi," Sajenti Evans aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo.

"akaielekeza kwenye kichwa cha mume wake na kufyatua.

" Maafisa walimfahamisha mumewe afahamu kwamba fungate imeisha na mkewe mpya anakwenda jela ." aliongeza Sajenti Evans

Sajenti Evans alisema kuwa bibi harusi alijaribu kuficha silaha bafuni katika hoteli walimokuwa.

Pendeza na Markson, Ongeza Hips, Makalio, Kuwa Mweupe na Ongeza Nguvu za Kiume

$
0
0
PENDEZA NA MARKSON. ONGEZA HIPS, MAKALIO NA MAPAJA, KUWA MWEUPE NA SOFTI, ONGEZA MAUMBILE YA KIUME, NGUVU NA HAMU YA TENDO N.K @markson_beauty_pr Tunakuletea bidhaa bora zenye matokeo ya uhakika na haraka zisizo na kemikali wala madhara. Zimetengenezwa kwa mimea na matunda na kudhibitishwa kiafya. NB.

 Matokeo ni uhakika na garantii na risiti

 BIDHAA ZETU:-

1.Kurefusha nywele na kuzuia kukatika ovyo @130000@130,000/=
2.Kuongeza shepu (hips, makalio na mapaja) kwa:-
(a)BOTCHO MULT-PLUS 10× @200000@200,000/=
(b)Vidonge @180000@180,000/=
(c)BOTCHO 10× ya kupaka @150000@150,000/=
3.Kuwa mweupe na softi mwili mzima kwa:- (1)Mafuta @130000@130,000/=
(11)Vidonge @150000@150,000/=
4. Kupunguza unene na manyama uzembe @150000@150,000/=
5.Kuongeza uume pamoja na nguvu za kiume kwa:-
(a)SHARK POWER gely ya kupaka (Inaongeza inch 6-7) @150000@150,000/= (b)Vidonge kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150000@150,000/= (C)HANDSOME UP ORIGINAL- kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo @250000@250,000/=
6.Kuondoa mvi milele zisiludi tena @150000@150,000/=
7.Kuongeza unene wa mwili mzima na uzito pamoja na hamu ya kula @130000@130,000/=
8.Kupunguza tumbo (kitambi) na nyama za pembeni kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @130000@130,000/= (b)Mkanda wa kawaida @100000@100,000/= (c)Micro-computer belt wa umeme @200000@200,000/=
9.Kupunguza maziwa na kuyasimamisha hata kwa walionyonyesha @130000@130,000/=
10.Kushepu miguu (CHUPA YA BIA) na kuondoa vigimbi @130000@130,000/=
11.Kuondoa mipasuko mwilini (michirizi) @120000@120,000/=
12.Kurudisha usichana (bikra) @120000@120,000/=

Wasiliana nasi :- (+255) 0767447444 au. 0714335378

 TAHADHARI: Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako. 👉🏻Ili kuona bidhaa zaidi na shuhuda za waliotumia bidhaa zetu

Ndege Jasusi Aina ya Tai wa Israel Auawa Nchini Syria

$
0
0
Upinzani nchini Syria watangaza kumuua ndege aliyetumiwa na Israel kufanya shughuli za kijasusi nchini Syria

Upinzani nchini Syria umetangaza kumpiga risasi  ndege aina ya Tai aliyekuwa anatumiwa na Israel kufanya ujasusi katika kanda hiyo .

Ndege huyo anasemekana kuonekana maeneo ya Idlib karibu na mpaka wa Uturuki.

Vikosi vya upinzani vilimuua ndege huyo kwa risasi baada ya kugundua kuwa alikuwa anapaa na kuzunguka  eneo moja katika kanda hiyo .

Ndege huyo alikuwa amewekwa kamera na vifaa vya uchuguzi katika mwili wake .

Syria imekuwa ikikumbwa na vita kwaa miaka 6 sasa .

Simba si Lolote Simba Yachapwa 1- 0 na Orlando Pirates Huku South Afrika

$
0
0
Simba imechapwa kwa bao 1-0 katika mechi yake ya kwanza ya kirafiki baada ya maandalizi ya msimu wa 2017-18.

Simba imelala kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wake Orlando Pirates katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Mganda Emmanuel Okwi na John Bocco ndiyo walioongoza mashambulizi na walifanya kila juhudi kutaka kusawazisha bao hilo lililofungwa katika kipindi cha kwanza lakini hawakufua dafu dhidi ya vigogo hao wa Afrika Kusini.


Huduma za Kuhamisha Fedha Kwa Simu zaipaisha Tanzania kimataifa

$
0
0
HUDUMA ya M Pesa inayotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imetajwa kuwa chachu ya hatua kubwa iliyopigwa na Tanzania katika kuhakikisha watu wake wengi wanafikiwa na huduma za kifedha, imefahamika.


Kwa mujibu ripoti mpya ya Benki ya Dunia (WB) iliyopewa kichwa cha habari “Tanzania Economic Update: Money Within Reach, Extending Financial Inclusion” wakati M Pesa ikianza mwaka 2008, asilimia 16 tu ya Watanzania ndiyo ilikuwa na uhakika wa kupata huduma za kifedha lakini sasa asilimia 86 wanapata huduma hiyo.


“ Kulinganisha na nchi nyingine katika bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Tanzania imewaacha wenzake kwa mbali sana. Kutoka asilimia 16 hadi 86 katika kipindi cha chini ya muongo mmoja, hiyo ni hatua kubwa sana,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.


Kwa mujibu wa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndullu, Vodacom kupitia M Pesa inashikilia asilimia 54 ya soko la huduma za kibenki kwa kupitia mawasiliano ya simu na kampuni nyingine ndiyo zinagawana asilimia iliyobaki.


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Ndullu Tanzania inatakiwa izishukuru sana kampuni za simu kwa hatua hii ambayo imefikiwa, kwa sababu huduma za kawaida za kibenki zilishindwa kukidhi mahitaji ya wengi.


“ Katika mambo ambayo mimi kama Gavana wa Benki Kuu nilisema nitayasimamia kwa dhati lilikuwa ni hili la kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanapata huduma za kifedha kuliko hali ilivyokuwa. Leo nashukuru hali ni nzuri,” alisema.


Akizungumzia matokeo ya ripoti hiyo, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom, Rosalynn Mworia, alisema Vodacom imetiwa nguvu na ukweli kwamba mapinduzi iliyoyaleta katika sekta ya mawasiliano nchini yameanza kuleta matunda.


“Tangu Vodacom imeingia hapa nchini mwaka 2000, imekuwa na kawaida ya kuwa ya kwanza kubuni vitu ambavyo baadaye vimekuwa vikiigwa na wengine. Mfano mmoja wapo wa ubunifu wa Vodacom ni huduma hii ya M Pesa.


“ Hivi sasa hakuna mtu ambaye utakutana naye njiani na umuulize M Pesa ni nini na asijue. Vodacom tunatamka kwa fahari kabisa kwamba sasa tuna wateja zaidi ya milioni tisa ambao wanatumia huduma hii. Hii ni idadi iliyo sawa na taifa kamili katika nchi nyingi duniani,” alisema Mworia.


Kupitia huduma ya M Pesa, wateja wa Vodacom wanaweza kupokea na kutuma fedha kupitia simu zao za mkononi na pia wanaweza kutoa fedha na kuweka katika akaunti zao za benki za kawaida, wakiwa mahali popote ambapo huduma za Vodacom zinapatikana.


Ripoti hiyo ya WB, pamoja na mambo mengine, imeweka bayana mchango mkubwa wa kampuni za simu katika uchumi wa nchi za Afrika, huku ikitamka kwamba kiasi cha fedha kinachozunguka kwa mwaka kupitia huduma kama M Pesa hapa Tanzania kwa sasa ni sawa na asilimia 47 ya Pato la Taifa.


“ Matumizi na imani ya wananchi kwa kampuni za simu imekua sana katika miaka ya karibuni kiasi kwamba watu sasa wanahifadhi zaidi fedha zao katika simu zao za mkononi wakati idadi ya wanaoweka benki fedha zao ikishuka,” ripoti hiyo imebaini.


Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya kundi la kampuni za Vodacom lenye makazi yake nchini Afrika Kusini. Kampuni hiyo ya Afrika Kusini nayo ni sehemu ya kundi la kampuni za Vodafone lenye makao yake makuu nchini Uingereza.

Chanzo: Swahili Times

Clouds TV na Radio Kinara wa TV na Radio Zinazosikilizwa Zaidi Tanzania...Zingine Zafuata

$
0
0
Taasisi ya Utafiti ya GeoPoll imetoa list ya top 10 ya vituo vya Radio ambazo zimesikilizwa zaidi Tanzania kwa Q2 2017, ikitumia data za kila siku zilizokusanywa kupitia Media Measurement Service ambapo kituo cha Radio ya Clouds FM kimeongoza.

Clouds FM imeongoza kwa mara nyingine kwenye list hiyo ikifuatiwa na Radio Free Afrika wakati TBC Taifa ikikamata nafasi ya tatu.

Aidha Taasisi hiyo pia imeitaja Clouds TV kuwa kituo kinachotazamwa zaidi Tanzania katika top ten list ya Television zinazotazamwa zaidi Tanzania ikifuatiwa na ITV na East Africa TV.

Radio zinazosikilizwa zaidi Tanzania


 Television zilizotazamwa zaidi Tanzania


Haji Manara wa Simba Aanza Vijembe Kwa Yanga...."Tutachezesha Wachezaji Tisa Dhidi ya Yanga"

$
0
0
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Sports Club, Haji Sunday Manara aiomba Shirikisho la soka nchini (TFF) iwaruhusu kuchezesha wachezaji tisa uwanjani badala ya 11 katika mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao Yanga SC.



Manara ameyasemahayo huku akitanabaisha kuwa kipigo chao kwa Yanga hakiepukiki.

“Mchezo wa Yanga na Simba natamani uwekesho kwa sababu inasaidia kupunguza kelele mtaani na maneno ya kuzuazua”.

“Tunawaomba TFF kama wataweza waturuhusu tuanze na wachezaji tisa hivi kama wataturuhusu na kanuni zinaruhusu tutawaandikia barua rasmi ikiwezekana tuanze tisa tutawafunga tu Yanga”

Afisa huyo aliyetoka kifungoni hivi karibuni kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ameongeza kuwa ameyapokea kwa mikono miwili maamuzi ya Kocha Mkuu wa Simba Omog juu ya kumvua unahodha, Jonas Mkude

“Mimi ukiniambia, kwangu nimefurahia hili kwa sababu ukiwa nahodha unakuwa unabeba vichwa vya wachezaji kumi sasa kutolewa katika unahodha itamsaidia kumrudisha katika kiwango chake zaidi”.
VIDEO:

Young Dee ashindwa Kuwa Karibu na Mtoto Wake Kisa… (Video)

$
0
0
Msanii wa muziki wa hip hop, Young Dee amedai kwa sasa anashindwa kuwa karibu zaidi na mtoto wake kutokana na kubanwa na shughuli nyingi za muziki. Rapa huyo amekanusha kumtelekeza mtoto wake huyo pamoja na mama yake kama baadhi ya vyombo vya habari vinavyoripoti. VIDEO:

Mambo Manane Kutikisa Kikao Cha Makinikia

$
0
0
Dar es Salaam. Baada ya siku 160 tangu usafirishaji wa mchanga wa madini ulipozuiwa na baadaye kuundwa kwa kamati mbili na Rais John Magufuli kuchunguza biashara hiyo nchini, hatimaye mazungumzo kati ya pande mbili yameanza.

Mazungumzo kati ya Serikali na kampuni ya Barrick Gold yameanza huku Watanzania wakisubiri kwa hamu kujua hatima yake.

Licha ya kwamba hakuna upande ambao umesema kitakachojadiliwa, kuna hoja muhimu nane ambazo zinaweza kuibuka na kuchukua nafasi kubwa katika mazungumzo hayo.

Ripoti za kamati

Tangu ripoti zote mbili zilipowasilishwa kwa Rais mwishoni mwa Mei na mwanzoni mwa Juni, taarifa zake zilipingwa na Acacia ambayo ilienda mbali zaidi na kusema haikupewa nakala kuona kilichomo.

Madai yote yaliyobainishwa ikiwamo kiwango kikubwa na aina nyingi za madini yaliyomo kwenye makinikia kwenye makontena 277 yaliyozuiliwa Bandari ya Dar es Salaam pamoja na kodi inayokadiriwa kufika Sh108 trilioni, yalipingwa na kampuni hiyo iliyosisitiza kwamba wakati wote imekuwa ikitoa taarifa sahihi.

Acacia ilifika mbali na kusema endapo ingekuwa inafanya udanganyifu wa kiwango na wingi wa madini ndani ya makinikia kama ilivyoripotiwa na kamati za Rais, basi migodi yake miwili ingeongoza kwa uzalishaji wa dhahabu duniani.

Mkaguzi huru

Kutokana na kutoridhishwa na ripoti za kamati, Acacia ilisisitiza kuhitaji kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi kuhusu suala hilo jambo ambalo halikuungwa mkono na Serikali. Pia, Rais Magufuli alitoa msimamo akiwa kwenye ziara ya kikazi kanda ya magharibi kwamba endapo kampuni hiyo itachelewa kuja kufanya mazungumzo, atafuta leseni yake.

Wengi wanaamini kuwa suala la mkaguzi huru litachukua nafasi katika majadiliano hayo wakati timu za watalaamu wa Tanzania na wale wa kampuni ya Barrick Gold wanapotafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

Kodi ya Sh424 trilioni

Hivi karibuni, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ilikadiria kiasi cha Dola 40 bilioni za Marekani (zaidi ya Sh89 trilioni) ikiwa ni kodi iliyokwepwa pamoja na faini na riba yake, Dola 150 bilioni (zaidi ya Sh335 trilioni).

Kutokana na utata uliopo hapa, kipengele hicho nacho kinatarajiwa kuwa na mvutano kabla muafaka haujapatikana. Wapo waliosema malipo ya Sh424 trilioni kutokana na ukokotozi wa TRA hayawezekani, lakini endapo itakuwa kinyume chake, Tanzania itakuwa nchi ya kipato cha kati.

Usafirishaji makinikia

Hili ni suala nyeti lililosababisha kutumbuliwa kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, mabadiliko ya sheria ya madini iliyopunguza madaraka ya waziri kwenye eneo hilo, kuvunjwa kwa Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kuanzishwa kwa kamisheni ya madini.

Kuhakikisha suala hili linakuwa endelevu, Serikali imeagiza kujengwa kwa mtambo wa kuchenjulia mchanga huo nchini. Hoja kadhaa za kupinga uwezekano huo ziliibuliwa na wadau, lakini Serikali imeendelea na msimamo huo na kukazia imeliweka kwenye sheria mpya.

Acacia yenyewe inasema mkataba unairuhusu kufanya hivyo na kuuza mchanga huo popote duniani ambako mteja atapatikana. Serikali ikishinda kipengele hiki huenda ombi la Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche kwamba mtambo huo ujengwe inakochimbwa dhahabu litatimia.

Mikataba ya madini

Kwenye Bunge la Bajeti lililomalizika hivi karibuni, Serikali iliwasilisha kwa hati ya dharura miswada miwili ya sheria mpya za rasilimali. Serikali pia iliwasilisha mswada wa mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ambayo yaliigusa mikataba ya utafutaji, uchimbaji na biashara ya sekta hiyo kwa ujumla.

Miongoni mwa matakwa yaliyomo kwenye sheria hizo mpya ni kuwapo kwa majadiliano kwenye mikataba iliyopo ili kuondoa vipengele vyote vinavyoinyonya Serikali na kuwanufaisha wachimbaji.

Licha ya sheria hizo mpya zilioweka asilimia moja ya ada ya ukaguzi kwa madini yanayosafirishwa kwenda nje ya nchi, Sheria ya Fedha ya mwaka 2017 imeongeza mrabaha kwa asilimia moja kutoka nne zilizokuwapo kwenye mikataba mingi ya madini inayotumika hivi sasa. Sheria hizo mpya pia zimeleta mabadiliko makubwa ambapo sasa wawekezaji hawataruhusiwa kupeleka malalamiko yao yanayoruhusu rasilimali za Tanzania nje ya nchi kwenye mahakama za usuluhishi wa migogoro ya biashara za kimataifa. Wakati hayo yakitokea, tayari Acacia imekwenda kwa msuluhishi wa kimataifa kama inavyoelekezwa na mikataba ya madini kati ya mwekezaji na Serikali. Hili nalo huenda likachukua nafasi kubwa katika mazungumzo yanayoendelea.

Mikataba ya kimataifa

Miongoni mwa mambo yaliyoibua mjadala mkubwa bungeni wakati wa kujadili miswada mitatu ya mabadiliko ya sheria ya madini ni hatua zilizochukuliwa na Serikali kuzuia makontena 277 ya kutosafirishwa nje ya nchi wakati mikataba inaruhusu hilo.

Waliotahadharisha walisema kilichofanywa ni kinyume na mikataba ya kimataifa ya uwekezaji ambayo Tanzania imeiridhia.

Suala hilo nalo linaweza kuwa sehemu ya majadiliano na endapo hakutakuwa na muafaka, shauri hilo linaweza kupelekwa kwenye mahakama za kimataifa za usuluhishi wa migogoro ambako tayari Acacia imefungua kesi ingawa ina matumaini makubwa kwamba suluhu itapatikana.

Masilahi ya pande zote

Ingawa Barrick na Acacia zipo kwenye mataifa mengi duniani ambako zinaendesha shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini, kiasi kikubwa cha madini yake kwa sasa kinatoka nchini na kuifanya iwe kampuni kubwa ya usafirishaji wa dhahabu Afrika.

Kampuni hizo zitakuwa na wakati mgumu kufunga migodi yake nchini na ndio maana suala hilo la masilahi ya pande zote mbili linaweza kuchukua nafasi yake katika majadiliano hayo.

Ugumu huo unatokana na ukweli kwamba Acacia wakiondoka, watalazimika kuwa na kipindi cha mpito cha kutokuwa na bidhaa sokoni kutokana na kutokuwa na uzalishaji sehemmu nyingine yoyote duniani, ingawa inaendelea na utafiti kwenye mataifa kadhaa.

Lakini, muafaka ukipatikana utaiwezesha Tanzania kutimiza ndoto yake ya kukuza mapato yatokanayo na sekta ya madini hasa dhahabu, kujengwa kwa mtambo wa kuchenjua makinikia pamoja na maghala ya kuhifadhi madini bila kusahau Benki Kuu (BoT) kuanza kutunza dhahabu kama akiba za Serikali.

Nafasi ya Acacia

Kitakachokubaliwa katika majadiliano kati ya Barrick na Serikali kitapelekwa kwenye uongozi wa Acacia ambayo ina uamuzi wa ama kukubali au kukikataa.

Hata hivyo, Barrick ina hisa nyingi Acacia hivyo kuwa na nafasi kubwa ya kutoa uamuzi.

Maoni ya wadau

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPASF), Godfrey Simbeye alibainisha kutotambulishwa kwa timu ya wataalamu wanaoiwakilisha Serikali kwenye mazungumzo hayo na akasema huenda Serikali imewatafuta baadhi kutoka nje ya nchi.

Alisema pamoja na kitakachoamriwa kwenye majadiliano hayo Tanzania itakuwa na jukumu la kujisafisha kimataifa.

“Tanzania itakuwa na jukumu la kujisafisha kimataifa juu ya mazingira yake ya uwekezaji. Tumechafuka huko nje. Suala muhimu sio amani iliyopo, bali uhakika wa kuwa na uwekezaji endelevu ndiyo maana wawekezaji wanaenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo licha ya mapigano yanayoendelea.”

Akitambua umuhimu wa ripoti za kamati za Rais, alisema kama kilichobainishwa ni sahihi basi kuna haja ya kujiuliza kwa nini Serikali imewafikisha hapa Watanzania kwani ina kila kitu kuchunguza na kuzuia udanganyifu wa namna hiyo kutokea.

“Sheria inayotoa uhuru wa kupitiwa na kubadilishwa kwa mikataba ni mbaya zaidi kwa uwekezaji,” alitahadharisha.

Profesa Haji Semboja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alikuwa na mtazamo tofauti kidogo kuhusu faida za majadiliano hayo.

Alisema endapo tuhuma zilizopo zitamalizika dunia itaelewa zaidi.

“Acacia watapata heshima kwa uwezo wa kushughulikia migogoro inayoweza kujitokeza dhidi yake vivyo hivyo kwa serikali,” alisema msomi huyo.

Hata wakibainika walikwepa kodi kama kamati ilivyobainisha, alisema itahitaji kujichunguza kuhusu mifumo yake ya ndani. “Inawezekana ni watumishi wachache waliokuwa wanafanya hivyo,” alieleza Profesa Semboja.

Mbunge wa Kinondoni (CUF), Maulid Mtulia alisema busara kubwa itatumika kurekebisha kasoro zote zilizopo kabla ya kuupata muafaka.

“Wawekezaji wasiwe na wasiwasi wa kufutiwa mikataba yao itakapoanza kutekelezwa sheria mpya inayoagiza kufikishwa bungeni kwa makubaliano yoyote yaliyoridhiwa na Serikali kuhusu uvunaji wa rasilimali za taifa,” alisema.  

Source: Mwananchi
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images