Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumatatu


WOLPER: Kuna Mtu Anamuita Mpenzi wangu Mbeba Pochi, Ila Mpenzi Wangu ni wa Kimataifa

$
0
0
WOLPER: Kuna Mtu Anamuita Mpenzi wangu Mbeba Pochi, Ila  Mpenzi Wangu ni wa Kimataifa
Muigizaji na mfanyabiashara wa mavazi nchini, Jacqueline Wolper amefunguka na kudai hatamani kumuona mpenzi wake akiendelea kufanya kazi zake za kimitindo ndani ya nchi kwa maana ameshaanza jitihada za kumtafutia kazi za kimataifa.

Jacqueline WolperAkizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu Wolper amesema watu wanadai mpenzi wake ni mbeba pochi lakini anachojua ni wivu ndiyo unaowasumbua kwa sababu wanafahamu kazi anayofanya lakini kwa kuwa yeye anathamini kazi ya mpenzi wake huyo lazima atahakikisha anamvusha boda kwa kutumia mtandao alionao.
"Kuna mtu anamuita 'BFF' mbeba pochi, najua anafahamu ni kazi gani anafanya lakini kwa kuwa anaumia lazima amchafue. Mpenzi wangu ni 'model' ambaye ameshafanya kazi nyingi tu za kutembea majukwaani lakini si unajua sekta za mitindo hapa nyumbani?, hazijazingatiwa sana kwa hiyo mimi kwa kuwa tayari nina 'connection' nje nitampigania kuona anafanya kimataifa zaidi na siyo nyumbani" Wolper

Akizungumzia kuhusu mpenzi wake huyo kutumika kama mpendezeshaji video 'Video King'"Suala la kutumika kama 'video King' hapa nchini sitaki kabisa kusikia wala kuona kwa sababu hakuna maslahi, na mpaka sasa jiandaeni kuona 'suprise' kwani tayari kuna 'dea'l za kazi za South Afrika tumeshasaini mikataba kwa hiyo mambo ni mazuri upande wetu".
Mbali na hayo Wolper amesema haogopi kumsaidia mpenzi wake kwa hofu ya kuja kusalitiwa mbeleni kwani anaamini Mungu amempatia Brown kwa kuwa ana vigezo vyote anavyohitaji na hata ikitokea akamsaliti hatakuwa na shida kwani atakuwa daraja la mafanikio yake.

Tuliowakamata Jana kwa Kufanya Mkusanyiko Usio Rasmi Lazima Tuwashughulikie- Mambosasa

$
0
0
Tuliowakamata Jana kwa Kufanya Mkusanyiko Usio Rasmi Lazima Tuwashughulikie- Mambosasa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema watu waliokamatwa na polisi hapo jana kwa kufanya mkusanyiko usio rasmi, walishaonywa kutofanya hivyo lakini hawakujali hivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yao.

Kamanda Mambosasa amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, na kusema  kitendo cha kufanya mkusanyiko usio rasmi ni kuvunja sheria, hivyo lazima watafikishwa Mahakamani kujibu shtaka lao, huku akikanusha kuwakamata watu hao kwa kutokana na kuvaa  t-shirt zilizoandikwa 'pray for Tundu Lissu'.

"Kwanza ifahamike hatujawakamata kwa kosa la kuvaa tshirt, zile ni nguo kama nguo nyingine wanavyovaa mashabiki wa Simba na Yanga, hawa walichofanya mpaka wakamatwe ni kufanya mkusanyiko usio rasmi na kibaya zaidi tulishawaeleza, na wenyewe walipoona polisi wanakuja wakaanza kutukimbia kwamba walijua wamefanya nini", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameendelea kwa kusema  jeshi la polisi linaendelea kuwahoji watu hao na kisha kupelekwa Mahakamani kusomewa mashtaka yao ili sheria ifanye kazi yake.


Snapchat Yafunga Huduma za Al Jazeera Nchini Saudi Arabia

$
0
0
Snapchat Yafunga Huduma za Al Jazeera Nchini Saudi Arabia
Mtandao wa kijamii wa Snapchat umefunga huduma za kituo cha Al Jazeera nchini Saudf Arabia.
Snapchat ilisema kuwa mamlaka nchini Saudi Arabia ziliiomba ifunge huduma za Al Jazeea kwa kuwa ilikiuka sheria za nchi hiyo.

Qatar inaendelea na mzozo yake na Saudi Arabia, Bahrain, Misri na UAE.
Nchi hizo nne zilikata uhusiano na Qatar mapema mwaka huu na kuilaumu nchi hiyo kwa kuunga mkono Ugaidi.

Saudi Arabia ina moja ya sheria kali zaidi kwa vyombo vya habari, kwa mujibu wa makundi ya kutetea haki za binadamu.
Lakini kawaida Saudi Arabia haiipenda Al Jazera. Wakati mmoja waliitaka serikali Qatar ikifunge kituo hicho kama moja ya masharti 13 ili kuiondolea vikwazo.

Saudi Arabia ni moja na masoko makubwa zaiid ya mitandao ya kijamii eneo la mashariki ya kati itokanayo na matumizi makubwa ya simu za smart phone.

'Tumeshinda Tumeshinda' Ndio Ujumbe wa Tundu Lissu Kwa Zitto Kabwe

$
0
0
Tumeshinda Tumeshinda' Ndio Ujumbe wa Tundu Lissu Kwa Zitto Kabwe
sasa zimepita tangu Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kuvamiwa na watu wasiojulikana kisha kupigwa risasi September 7, 2017 Dodoma kisha kupelekwa Nairobi kwa ajili ya matibabu huku hali yake ikielezwa kuwa nzuri.

Watu mbalimbali na wanasiasa hasa wa CHADEMA wamekuwa wakimtembelea Hospitalini hapo kujua hali yake na mmoja kati ya waliomtembelea ni Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ambaye baada ya kuonana naye alimwambia maneno ambayo Zitto aliayaandika kupitia kupitia Facebook yake.

Ujasiri ni nini ?

Nimetumia wikiendi iliyopita kumsabahi ndugu Tundu Lissu jijini Nairobi. Nimerudi nikiwa mwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao kaka yangu ameuonyesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali.

Si mara nyingi hapa nchini utasikia tukiongelea ujasiri. Lakini namfikiria Lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi. Najua hivyo ndivyo alivyo. Waliomshambulia wamemuumiza. Wamemuumiza kweli. Na bado wakati tuliokuwa naye amenionyesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri.

Alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu sio kitu rahisi kwa mtu yoyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha nimeumia moyo Sana kama asingesema maneno haya kwangu “tumeshinda. Tumeshashinda”.

MAHAKAMA: Upelelezi wa Awali Kesi ya Aveva na Kaburu Umekamilika

$
0
0
MAHAKAMA: Upelelezi wa Awali Kesi ya Aveva na Kaburu Umekamilika
Upelelezi wa awali katika kesi ya utakatishaji fesha inayowakabili Rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa leo September 18, 2017 kuwa, upelelezi wa awali wa kesi hiyo umekamilika ambapo jalada la kesi limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ili alisome na kueleza kama anaona umekamilika au la.

Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi September 27, 2017

Inasikitisha Mjamzito Afariki kwa Kuchomwa Mkuki

$
0
0
Inasikitisha Mjamzito Afariki kwa Kuchomwa Mkuki
Watu watatu wameuawa kwenye Bonde la Yaeda Chini katika matukio tofauti, ikiwamo wawili kuteketezwa kwa moto, huku mjamzito akichomwa mkuki.

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga alisema jana kuwa matukio hayo yalitokea juzi kwenye vijiji vya Dumanga na Mongo wa mono vilivyopo katika Bonde la Yaeda Chini.

Mofuga alisema katika tukio la kwanza watu watatu waliodaiwa kuwa majambazi walipora pikipiki na wakati wanakimbia mmoja aliyejulikana kwa jina la Makafo Elia alishindwa kukimbia akakamatwa na wananchi baada ya mafuta ya pikipiki kwisha na wananchi hao kumuua kwa kumchoma moto na kuteketea hadi kuwa majivu.

Alisema katika tukio la pili Martin Boay (25) alimchoma mkuki mjamzito Elizabeth Elias (35) na kufariki dunia, lakini naye aliuawa na wananchi wenye hasira walioamua kumfunga mikono na miguu na kumtupa kwenye moto ambako aliungua hadi kubakia majivu. “Hadi hivi sasa bado polisi wanaendelea na uchunguzi wa matukio hayo matatu ili kuhakikisha mambo ya kujichukulia sheria mkononi yanakomeshwa,” alisema Mofuga.

Aliongeza kuwa kamati ya ulinzi na usalama imekemea tabia ya watu kujichukulia sheria mikononi. Pia, mkuu huyo wa wilaya amemuagiza mkuu wa polisi wa wilaya kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika ili iwe fundisho kwa wengine.

“Bonde la Yaeda Chini lina historia ya matukio ya uhalifu hasa mauaji, ujangili wa nyara za Serikali na wizi wa mifugo. Tunaanzisha harambee kwa kuhamasisha wananchi na wadau wengine ili kujenga kituo cha polisi katika bonde hilo,” alisema.

Mofuga aliongeza kuwa, ujenzi wa kituo na nyumba za familia 12 utagharimu Sh435 milioni na unatakiwa kuanza mara moja.

Alisema ameanza harakati za kuwaomba wadau, wananchi na Serikali kuchangia ujenzi huo ili kutafuta amani ya kudumu katika eneo hilo.




Lema Awapa Atoa Neno kwa Mwigulu na Kamishina Sirro

$
0
0
Lema Awapa Atoa Neno kwa Mwigulu na Kamishina Sirro
Mbunge wa Arusha Mjini ambaye sasa yupo nchini Kenya amewaomba Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP Sirro wawaachie watu ambao jana walikamatwa na jeshi la polisi wakiwa wamevaa Tshirt za Tundu Lissu na UKUTA na kusema kitendo hicho kinazidi kuleta chuki.

Lema amesema hayo kupitia mitandao yake ya kijamii na kudai kuwa watu ambao wameratibu maombi kwa ajili ya Tundu Lissu hawakupaswa kukamatwa bali walipaswa kulindwa na jeshi la polisi kwani wao wanaratibu watu waweze kumlilia Mungu wao kwa maombi na si vinginevyo.
"Hivi kweli hawa watu wangekuwa wanafanya mkusanyiko wa maombi kwa ajili ya Rais Magufuli au kiongozi mwingine yoyote yule hawa watu wangepata mateso makubwa kama ambavyo wale vijana wamepata, Mwigulu Nchemba wewe ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Kamanda Sirro tunakuomba sana waachie watu wote waliokamatwa wakiwa wamevaa Tshirt za UKUTA waachie kwa sababu hiki mnachokifanya kikiendelea kukomaa siku moja hamtawaona na Tshirt wala na kitu chochote wakiacha kuvaa Tshirt mioyo yao ikaendelea kuumia wakiacha kusali maana yake watakuwa wameelekea katika njia nyingine mbaya zaidi" alisisitiza Gobless Lema
Godbless Lema ametoa kauli hii siku moja baada ya jeshi la polisi kuzuia watu kufanya maombi ya kitaifa kwa Mbunge Tundu Lissu maombi ambayo yaliandaliwa na vijana wa CHADEMA (BAVICHA) ambayo yalipaswa kufanyika Septemba 17, 2017 katika viwanja vya TIP Sinza l Rights

Katibu wa Mbunge Ashangazwa na Kamatakamata ya Polisi

$
0
0
Katibu wa Mbunge Ashangazwa na Kamatakamata ya Polisi
Katibu wa Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche, Mrimi Zabloni amesema analishangaa Jeshi la Polisi nchini kwa kukamata watu wanaokusanyika kumuombea Tundu Lissu na kuruhusu matamasha yanayofanyika usiku kucha huku viongozi wa mikoa wakishiriki.

Mrimi amefunguka hayo wakati akizungumza kwa njia yasimu na Mwandishi wa EATV na kusema kwamba anasikitisha na vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi kukataza mikusanyiko ya wanachadema badala ya kuipa ulinzi.

"Kuna vitu hawa askari polisi wetu wanafanya vya kushangaza, kuna matamasha mengi yanafanyika usiku na viongozi wa mikoa wanashiriki lakini maombi ya Lissu yanayofanywa mchana kweupe wanayapinga, sijui tunaelekea wapi. Kati ya matamasha ya usiku na maombi yapi yanahatarisha amani? Wenzetu Kenya jana wamefika hadi hospitalini na kufanya ibada kwa ajili ya kumuombea Lissu kwa nini hatujifunzi kutoka huko? alisisitiza kwa njia ya kuhoji.
Aidha Mrimi amewataka watu kutohusisha tukio la Tundu Lissu kama mtaji wa siasa kwa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) na kwamba harakati zinazofanywa na vijana hao ni kuhakikisha wanatoa hisia zao juu ya matatizo aliyoyapata mwanasheria wao.
Amesema kuwa wanachokifanya Bavicha siyo siasa bali wanatumia uhuru wa Katiba na kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi nchini kwani wanaruhusiwa kuzungumza na hata kuandamana ili kutoa hisia zao kwa mambo yanayoendelea nchini.
"Wanaosema Bavicha wanamtumia Lissu kama mtaji wa kisiasa ni mtazamo wao tu, kwani naamini wanafanya kazi kwa mujibu wa heria na katiba hayo mengine ni hila tu. Naamini wamekumbwa na matatizo mengi viongozi kupotea, misukosuko ya viongozi wa chama lakini pia hata mauaji yaliyowahi kutokea kwa viongozi na shambulio la Lissu kwa hiyo ni haki yao kama vijana kupaza sauti kukemea" Mrimi aliongeza


Kutana na Mtatibu Wanyota za Binadamu Duniani Kote Maalim Fadhili Rashid Kutoka Comoro

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU WANYOYA ZA BINADAMU DUNIANI KOTE MAALIM FADHILI RASHIDI KUTOKA COMORO

KWA SASA YUPO TANZANIA MAALIM FADHILI RASHIDI ANA IWEZO WAKUJUWA JAMBOLAKO NAKULI TATUWA KWAMUDA MFUPI

MAALIM FADHILI RASHIDI ANAJUWA UMEHANGAIKA SANA LAKI HUJAFANIKIWA MUONE HARAKA AKUSAIDIE

MAALIM FADHILI RASHIDI NI BINGWA WAKUTIBU MARADHI SUGU KAMA VILE MIGUU KUUMA MIGUU KUWAKA MOTO

KISUKARI VIDONDA VYATUMBO PUMU TEZI NA UVIMBE TUMBONI PUMU ANA UWEZO WAKURUDISHA MTU ALIE POTEA KIMAZINGIRA

(MSUKURE) KUMFANYA MKE MUME MPENZI ASIKUSALITI DAWA YA (LIMBWATA) KUMTAWALA MPENZI WAKO UNAVYOTAKA

KUMUONA MBAYA WAKO LIVE KWASABABU MAALUM ANATOWA PETE YA BAHATI INAYO ENDANA NA NYOTA YAKO ITAKAYO KULETEA PESA BILA YA MASHARITI YEYOTE

NAKUMILIKI MALIZA MAJINI KWAYULE ANAE HITAJI DAWA YAKUONGEZA UUME ZAIZI UIPENDAYO DAWA YA NGUVU ZA KIUME ANAYO

DAWA YA KUONGEZA HIPSI SHEPU KUWA NA UMBO BOMBA KAMA UMEIBIWA AMA KUDHURUMIWA UTARUDISHIWA MALIYAKO NDANI YA MASA (24)

ANAFUNGA KESI NAKUPATA HAKIYAKO DAWA YAMVUTO WABISHARA KUUZA MALIYAKO KWA HARAKA KUZUIYA CHUMA ULETE

KUSAFISHA NYOTA NAKUONDOA MIKOSI NA KUPANDISHWA CHEO KAZINI ACHAKUTESEKA NJOO UWONE MIUJIZA YA MAALIM FADHILI RASHIDI

CALLING+255719362806/ +255763276239

KWA WHATSAPP IMO +255785786436

Watanzania 13 wa Familia Moja Wafariki Katika Ajali Nchini Uganda

$
0
0
Tangazo la Ajali ya Gari TZ 540 DLC

Gari tajwa hapo juu lilipata ajali karibu na mto Katonga, barabara ya Masaka kuamkia leo tarehe 18/09/2017.

Lilikuwa likiwarudisha Watanzania wa Familia ya Bw Gregory Teu ambao walikuja kwenye harusi tarehe 16/09/2017 hapa Kampala. Bibi harusi ni mtoto wa Bw na Bibi Gregory Teu wa Dar es salaam.

Jumla ya abiria waliokuwa kwenye gari ni abiria 19. Kati yao 13 wamefariki dunia na 6 wamelazwa Nsambya hospital.

Ubalozi unaendelea kufuatilia msiba huu pamoja na kupata majina yote ya waliokufa na kunusurika.

Naibu Balozi Mh. Maleko pamoja na Brigedia Generali S S Makona wameelekea Nsambya Hospital kuona Walio nusurika.

Asante sana

Ofisi ya Ubalozi

Faiza Ali Yamefika Hapaaa....Amshukia Vikali Baba wa Mtoto wake Sugu

$
0
0
Yule mwanadada machachari na ex wa Mbunge maarufu kutoka mkoa wa Mbeya, Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ameibuka na kuicharua shule maarufu ya watoto wa kishua kwa kumrudisha mtoto nyumbani kisa anadaiwa laki moja ilihali yeye mzazi ameshalipia kiasi cha milion mbili taslim.

Kama kawaida yake hasira zake akazimalizia kwa muheshiwa kwa kumshushia kichambo heavy ambaye mara nyingi ndiye victim wa stress zake.


G-Nako Awashirikisha Washindi wa Mwagika Challenge Kwenye VIDEO yake Mpya

$
0
0
Shindano la “Mwagika Challenge” lililoendeshwa na kampuni ya bia ya Tanzania Breweries Limited (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager hivi karibuni limefikia tamati ambapo Iddi Kidungwa, Michael Mwalembe na Nasma Msangi wakiibuka washindi. Washindi hao wanatarajiwa kuonekana kwenya video mpya ya msanii mkubwa wa bongo Fleva, G-Nako Warawara
‘Mwagika Challenge’ iliyokuwa na lengo la kuwapa fursa vijana kuonesha vipaji vyao pia liliungwa mkono na mastaa kama Shettah na Shilole waliokuwa mstari wa mbele kuhimiza mashabiki kushiriki shindano hilo pia ni miongoni mwa wasanii watakaonekana kwenye video hiyo.

Video hiyo inayotarajiwa kutoka 17.09.2017 itakuwa ya aina yake kutokana na vionjo mbalimbali vilivyotumika. Sitaki kukuchosha na stori nyingi, tizama teaser hapa chini na endelea kufuatilia mitandao ya kijamii ya Kilimanjaro kuona safari ya Mwagika challenge hadi kutengeneza video hii.

Kipanya Ameamua Kuishi Maisha Bila Mawasiliano ya Wasiwasi

$
0
0

Instagram Caption: Punguza ghasia zisizo na msingi linapokuja suala la mawasiliano, jiunge na #VodacomREDRLX  ufurahie mawasiliano bila wasi. Piga *149*01# na chagua RED

Pendeza na Kessy Products: Badili Muonekano Wako na Kuweka Mwili Wako Sawa Bila Madhara yoyote

$
0
0
PENDEZA NA KESSY PRODUCT: BADILI MUONEKANO WAKO NA KUWEKA MWILI WAKO SAW KWA PRODUCT ZA ASILI ZISIZO NA MADHARA YEYOTE WALA KEMIKALI, MATOKEO NI KWAARAKA


1) KUTOA MVI SUGU PIA ZA KUZALIWA NAZO _80,000/
2) KUREFUSH NYWELE  KUZIJAZA NA KUZUIAKUKATIKA 90,000/
3) TENGENEZA SHEPU YAKO KUWA NA UMBO ZURI (HIPS & BATKS)KUNADAWA AINA TATU (@)KUPAK (B) KUNYWA (C)VIDONGE_130,000/
  4)ONDOA NYAMA UZEMBE MIKONONI, KIUNONI KUPAK _90,000/
5)TOA  KITAMBI KABISA(@) KUPAK 10O,000/ (B)VIDONGE/SLIMING MAJAN 130,000/
6) PUNGUZA MWILI MZIMA KUANZIA KILO UNAZOITAJI WEWE
@) DAW YA MAJIN NA VIDONGE_130,000/
7)PUNGUZA MAZIWA NA YASIMAME KAMA MWANZO _80,000/
8) PIA UNA KUONGEZA MAZIWA SAIZI UNAYOHITAJI WEWE_80,000/
9)ONGEZA UNENE WA MWILI MZIMA_100,000/
10) ONDOA MICHIRIZI ILIYO SHINDIKANA_90,000/
11) TOA MAKOVU, CHUNUSI, WEUSI KWENY MAPAJA KIKWAPAN_90,000/
13) KUWA MWEUPE WAKUPENDEZA(@) VIDOGO(WHITE SOLUTION)_130,000/(B)MAFUTA YAKUPAK 100,000/
14)TOA NDEVU VINYWELEO MILINI _90,000/
15/ ONGEZA NGUVU ZA KIUME (@)JELI_80,000/(B)VIDONGE MAX MAN_ 100,000/
16) ENGEZA MAUMBIL YA KIUME
@) (HANDSOME UP) MASHINE _200,000/
@) JELI NA VIDONG VYA SHARK_120,000/
17) RUDISHA HAMU YA TENDO NA KUCHELEWA KUFIKA KILELE_90,000/
18) RUDISH(BIKRA) 100,000/
19)ONDOA MAFUTA USONI _90,000/
20) ONDOA MIKUNJO USON_70,000/
(21) ENGEZA  MGUU_80,000/

 TUNAPATIKAN DAR W SALAAM: NAKWA MIKOAN KOTE UTAPATA PIGA CM                     (+255) 0719955528
0756259180
0785371237
@dr_kessy_product
Delivery  POPOTE ULIPO

Lwandamina, Cannavaro Waamua Kumfuata Manji Mahakamani

$
0
0
Lwandamina, Cannavaro Waamua Kumfuata Manji Mahakamani
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amekwenda moja kwa moja hadi katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kuteta na bosi wake wa zamani, Yusuf Manji.

Lwandamina alikutana na Manji katika viwanja vya mahakama ya Kisutu akiwa ameongozana na wasaidizi wake kam Shadrack Nsajigwa akiwemo Kocha wa Makipa wa Yanga, Juma Pondamali 'Mensah' na Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh.

Naye nahodha wa Klabu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, leo  ameibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar na kupata nafasi ya kuzungumza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Yusuf Manji.

Baada ya kutinga mahakamani hapo, Cannavaro alimuwahi Manji na kusalimiana naye kisha kupiga kuzungumza mambo machache ambayo hata hivyo haijajulikana kama walikuwa wakijadili mambo ya soka kuhusu klabu hiyo au la!

Manji alikuwa mahakamani hapo kutokana na Kesi inayomkabiri Manji kuhusiana na kutumia madawa ya kulevya imeshindwa kusikilizwa leo katika mahakama ya Kisutu na kusogezwa mbele hadi Septemba 25.

Suala la kushindwa kusikilizwa ,limetokana na Manji kuchelewa kufika mahakamani, lakini naye alimueleza hakimu kuwa aliambiwa hakimu yuko katika kikao.

Kutokana na hali hiyo, imesogezwa mbele hadi Septemba 25, Manji atakapotakiwa kuleta mashahidi wake.

Manji anatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya, jambo ambalo amekuwa akilikanusha.

Miili ya Watoto Waliokufa Kwa Mlipuko wa Bomu Arusha Yaagwa

$
0
0
Miili ya Watoto Waliokufa Kwa Mlipuko wa Bomu Arusha Yaagwa
Miili ya watoto watatu waliofariki dunia kwa mlipuko wa bomu kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli imeagwa na kusafirishwa kwa maziko katika Kijiji cha Nafco.

Shughuli ya kuaga miili hiyo imefanyika leo Jumatatu katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.

Watoto hao walifariki dunia Ijumaa jioni katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale walipokuwa wakichunga ng'ombe.

Ilielezwa watoto hao walilipukiwa na bomu walipokuwa wakilichezea wakidhani ni mpira.

Watoto waliofariki dunia wametajwa kuwa ni Johnson Daniel, Lendisi Saitabau na Samweli Nyangusi.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kuaga miili ya watoto hao.

Serikali Yatoa Onyo kwa Gazeti la MwanaHalisi Yaitaka Kujieleza Kwanini Lisichukuliwe Hatua

$
0
0
Serikali Yatoa Onyo kwa  Gazeti la MwanaHalisi Yaitaka Kujieleza Kwanini Lisichukuliwe Hatua
Gazeti la Mwana halisi limetakiwa na Serikali kupitia idara ya Habari maelezo kujielesa kwanini gazeti hilo lisichukuliwe hatua zaidi kutokana na kukiuka  maadili na usiofuata weledi wa kitaaluma.

Mkurugenzi Mkuu wa idara ya habari maelezo na msemaji wa serikali Hassani Abbasi amesema gazeti hilo limekuwa likiandika habari ambazo zimekuwa zikikiuka misingi ya uandishi wa habari na kusema kuwa sheria za nchi na hata za kimataifa zinazohusu wajibu wa uhariri  kwa taaruma hii.

Gaze

Mfanyabiashara Avamiwa na Kuuwawa Kwa Kupigwa Risasi

$
0
0
Mfanyabiashara Avamiwa na Kuuwawa  Kwa Kupigwa Risasi
Mfanyabiashara wa Lupa Tingatinga wilayani Chunya, Nestory Kyando ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliovamia nyumbani na dukani kwake.

Katika tukio hilo lililotokea saa tatu usiku wa kuamkia jana Jumapili watu hao walipora Sh4 milioni.

Taarifa zinaeleza mfanyabiashara huyo aliyekuwa akiuza bidhaa kwa jumla alivamiwa nyumbani ambako waliomvamia walimnyang’anya ufunguo wa sefu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema watu wanne wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

Amesema baada ya mfanyabiashara huyo kunyang’anywa ufunguo, watu hao walienda dukani ambako aliwafuta kwa nyuma ndipo alipopigwa risasi.


Msigwa Aweka Wazi Namba Zake Za Simu Kwa Polisi Asema Ahitaji Kuviziwa

$
0
0
Msigwa Aweka Wazi Namba Zake Za Simu Kwa Polisi Asema Ahitaji Kuviziwa
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa amepata taarifa jeshi la polisi linamtafuta na kusema endapo jeshi la polisi litamwita kwa kufuata utaratibu basi na yeye ataitika wito huo ila si kuviziwa

Mbunge Peter Msigwa akiwa na Mbunge Godbless Lema jana walipokwenda kwenye maombi katika kanisa la Lutheran Highway Nairobi!

Mbunge Msigwa ametoa taarifa hii kufuatia kuwepo kwa taarifa toka jana kuwa kiongozi huyo naye anatafutwa na jeshi la polisi akidai kuwa ni moja kati ya watu waliokuwa wakiratibu mkusanyiko wa maombi ambao ulitakiwa kufanyika jana kumuombea Mbunge Tundu Lissu katika viwanja vya TIP Sinza jambo ambalo yeye mwenyewe alipinga na kusema bado yupo nchini Kenya.

"Nimepata taarifa Kuwa polisi wamenitafuta toka asubuhi (jana) maeneo ya sinza, Wakisisitiza kuwa nipo hotelini hapo , wakati mimi niko Nairobi, nitaitika wito wa polisi ukiletwa rasmi, sihitaji kuviziwa +255754360996 mnaweza kunipigia au kunitumia ujumbe mfupi Whatsaap" alisema Msigwa.

Mbunge Peter Msigwa bado yupo jijini Nairobi nchini Kenya kwenye matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa mjini Dodoma.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images