Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Dawa ya Kurekebisha Mzunguko wa Hedhi Kwa Mwanamke Mwenye Tatizo Hilo

$
0
0
Hili ni tatizo linalowatokea karibu wanawake katika safari yao ya kuishi hapa chini ya jua.

Tatizo la kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi huanza ghafla au polepole ambapo mwanzo mwanamke alikuwa akipata siku zake katika utaratibu unaoeleweka lakini mara haelewi au hajielewi namna mzunguko wake unavyoenda.

Kuvurugika kwa hedhi ni kitendo cha mwanamke kuanza kuona siku zake bila tarehe au mzunguko maalumu na matokeo yake ni kuwa mwanamke atashindwa kutimiza malengo yake kwa kutumia mzunguko huo sababu ni haueleweki.

Unaweza kutokewa ghafla tu unapata hedhi mahali usipotarajia jambo linakufanya ubaki na woga na huelewi nini cha kufanya kwani hukuwa umejiandaa kwa tukio hilo kama matokeo ya siku zako kutokuwa mzunguko maalumu.

Wakati mwingine unaweza kupitiliza mwezi hata miezi kadhaa bila kuona kabisa siku zako na hata ukipima ujauzito unakutwa huna ujauzito wala dalili huna.

Madhara ya kuvurugika kwa mzunguko ni pamoja na;  kushindwa kupata ujauzito, maambukizi katika kizazi na kuziba kwa mirija ya uzazi.

Kwanini unahitaji mzunguko wa hedhi ulio sawa?

Faida za kuwa na mzunguko wa hedhi ulio sawa:

Utakusaidia kupata ujaouzito ulioupangilia
Utakuepusha kupata ujauzito ambao hukuupangilia
Utaweza kuamua jinsia ya mtoto unayemtaka
Nini husababisha kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi

Ni rahisi kugundua kama mzunguko wako umevurugika ikiwa tu unauafahamu vizuri mzunguko wako ulio sahihi.

Kufahamu mzunguko unahitaji uifahamu siku ambayo ulianza kuona damu hadi siku utakapoona tena katika mzunguko unaofuata. Karibu kila mwanamke huwa na mzunguko wake usiofanana na wa mwingine.

Tatizo linaweza kuanza kwa kurukaruka siku, mwanamke pia anaweza kupoteza siku yaani mwezi mwingine anaona na mwezi mwingine haoni, au anaingia mara mbili kwa mwezi au anaona damu ya hedhi kwa siku nyingi hata zaidi ya siku arobaini mfululizo.

Damu yake inaweza kutokea kidogo kidogo kila siku au nyingi huku ikiambatana na mabongemabonge na maumivu pia. Maumivu haya ya wakati wa hedhi huenea chini ya tumbo mpaka miguuni na kiunoni.

Kuvurugika kwa hedhi kunaweza kutokea kutokana na sababu zifuatazo:

Mabadiliko ya mazingira ambayo hupelekea mfumo wa mwili hubadilika pia hasa mwanamke akitoka sehemu ya joto kwenda mikoa ya baridi au toka mikoa ya baridi kwenda mikoa ya joto.
Msongo wa mawazo (stress)
Hofu
Woga
Mabadiliko ya kisikolojia
Uvimbe kwenye kizazi
Matatizo kwenye mfumo wa homoni
Matatizo kwenye vifuko vya mayai
Mimba kuharibika
Maambukizi sugu ya kizazi pia ni mojawapo ya sababu.
Maumivu ya tumbo chini ya kitovu ya mara kwa mara na kila ukipima unaambiwa ni ugonjwa wa U.T.I kumbe siyo yutiai
Kutokwa na uchafu ukeni
Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
Dawa ya kurekebisha mzunguko wa hedhi



Kabla ya yote unapopatwa na tatizo hili kwa muda mrefu ni vizuri ukaonana na daktari uweze kupata uchunguzi wa kutosha kubaini nini hasa inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Zifuatazo ni dawa mbadala 6 unazoweza kuzitumia ukiwa nyumbani ili kurekebisha tatizo hili

1. Papai



Papai ni moja ya dawa nzuri sana katika kutibu tatizo la kuvurugika kwa hedhi. Ina viinilishe mhimu kama carotene, chuma ( iron), Kalsiamu (calcium) na vitamini A na C ambavyo husaidia kulainisha na kunywea kirahisi kwa kuta za mji wa uzazi.

Siku 2 au 3 kabla ya kuanza kula papai kila siku nusu papai papai zima kutegemea na ukubwa wake au uwezo wako.

Kwa mtu mwelevu sababu ameshagundua papai laweza kumsaidia hivyo basi atalifanya papai kuwa sehemu ya chakula chake kila siku na si mpaka aumwe tu.

2. Mdalasini

mdalasini

Mdalasini unayo sifa ya kuondoa tatizo la damu kuganda sifa inayoweza kusaidia kuondoa tatizo la maumivu wakati wa hedhi.

Mdalasini ni chanzo kizuri cha nyuzinyuzi (fiber), kalsiamu (calcium), chuma (iron) manganizi (manganese).

• Tengeneza chai ya tangawizi kwa kutumia kijiko kidogo cha mdalasini ya unga na maji kikombe kimoja (robo lita), ipua na uache ipowe kidogo, ongeza asali kijiko kikubwa kimoja ndani yake na unywe. Fanya zoezi hili mara 2 mpaka mara tatu siku 2 au 3 kabla ya kuanza siku zako.

• Au changanya kijiko kidogo kimoja cha mdalasini ya unga na kijiko kidogo kimoja cha asali katika glasi moja ya maji ya uvuguvugu na unywe kutwa mara 2 siku za mwanzoni unapoanza au kukaribia kuingia katika siku zako.

3. Tangawizi



Tangawizi ni dawa ya asili yenye maajabu katika kutibu tatizo la mvurugiko wa hedhi. Tangawizi hufanya kazi mhimu kabisa katika kushusha kiwango cha homoni inayosababisha maumivu ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘prostaglandins’.

Tangawizi husaidia pia katika kupigana na uchovu uletwao na mzunguko wa hedhi katika siku zile za mwanzo au siku 2 hivi kabla ya kuanza siku zako na huweza pia kufanya mzunguko usio sawa wa hedhi kuwa sawa

• Tengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi mbichi, kunywa kikombe kimoja kutwa mara 3 wakati wa siku zako au siku yoyote tu kama kinga. Kamulia ndimu kidogo ndani yake na utumie asali kupata radha badala ya sukari.

• Unaweza pia kuongeza tangawizi kwenye vyakula na mboga mboga nyingi unazopika kila siku.

4. KOTIMIRI (Parsley):



Tengeneza juisi ya kotimiri, viazi pori (Beet Root), karoti au matango. Tumia asali mbichi ukitengeneza juisi hii. Hii kotimiri inapatikana kirahisi Dar na Zanzibar ni mboga mboga inayotumika zaidi kwenye mahoteli ya kitalii.

Mboga hii inacho kitu mhimu sana kijulikanacho kama ‘Apiol’ amabcho kazi yake kuu ni kurekebisha na kuweka sawa homoni za kike.

Changanya kwa ujazo sawa yaani kama juisi ya kotimiri ni kikombe kimoja basi ya kiazi pori nayo kikombe kimoja kadharika kwa matango.

Juisi hii ni dawa tosha ya maumivu wakati wa siku za hedhi, hurekebisha mzunguko wa hedhi na imethibitika kuwa bora kuliko dawa nyingi za kizungu.

Kunywa glasi moja ya juisi hii kutwa mara 2.

5. MREHANI



Mrehani au Basil kwa Kiingereza ni mmea mwingine mzuri sana katika kuondoa maumivu wakati wa hedhi na kurekebisha mzunguko wa hedhi kwa ujumla.

Mmea huu unatumika sana jikoni kwenye mahotel ya kitalii Dar na Zanzibar. Unao sifa kuu ya kuzuia au kuondoa maumivu mwilini.

• Ongeza kijiko kikubwa kimoja cha majani freshi ya mrehani yaliyokatwakatwa na kisu (chop) kwenye kikombe kimoja cha maji ya moto, funika vizuri na usubiri ipowe. Kunywa yote ikishapoa na ufanye zoezi hili kutwa mara 3 kwa wiki 3 mpaka 4 au mpaka tatizo lako limeisha.

• Au tengeneza juisi ya majani haya. Yatwange kwenye kinu au kwenye blenda ya umee kupata majimaji yake kisha chota vijiko vya chai viwili uweke ndani ya kikombe kimoja cha maji ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hili kutwa mara 3.

• Unaweza pia kuongeza majani freshi ya mrehani kwenye vyakula vingi unavyokula kila siku.

6. MAJI YA KUNYWA


Matatizo karibu yote mwilini chanzo chake ni mwili kutokuwa na maji ya kutosha. Maji ni uhai. Unachohitaji hapa ni kutokusubiri kiu. Kiu ni ishara ya mwili iliyochelewa kuhitaji maji.

Matatizo mengi ya kiafya tumeyaona kwa watu wasiopenda kunywa maji ya kutosha kila siku.

Jitahidi hata iweje iwe unaumwa au huumwi chochote unywe maji lita mbili mpaka tatu kila siku iendayo kwa Mungu na utaniletea mrejesho hapa hapa.

Madhara ya Chai na Kahawa Kiafya

$
0
0
Pamoja na faida kadhaa hapo juu za matumizi ya kahawa na chai bado kuna hasara kadhaa za kutumia vinywaji hivi. Kwenye chai na kahawa kuna kitu kinaitwa kafeina.

Kafeina ni nini?:

1. Kafeina ni madawa ya kulevya katika kundi la madawa yanayoamsha mwili

Hii ndiyo sababu kwa mtu aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma, ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.

Kafeina ni kiungo mhimu karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi; Coca-cola, Pepsi, Sayona nyeusi, Azam cola na kadharika. Kafeina huongezwa pia katika Red bull, Malta na katika baadhi ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.

Kwahiyo Kafeina ambayo hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.

2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).

Kafeina ni dawa ya kukufanya ukojowe. Ukinywa kikombe kimoja cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda kukojoa vikombe viwili.

Kwa sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au soda.

Madhara yake ni nini?

Moja, Kama unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili.

Pili, Kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili, hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.

3. Kafeina husababisha KANSA.

Seli ndani ya mwili lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka 7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0 ni asidi na juu ya 7.0 ni alkalini.

Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi asidi.

Jarida moja la afya la Uingereza, ‘The British Medical Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.

4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamini mhimu mwilini.

Kafeina ambayo ni kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.

5. Uchovu sugu.

Wapenzi wengi wa chai ya rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa au chai.

Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.

Utolewaji wa sukari iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa dharura wa mwili.

Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo. Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.

Kwa sababu ya biashara kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno, kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya matumizi yake ya dharura.

Hakuna nguvu iliyomo kwenye kafeina au ginseng.

Kaffeina itaisisimua tezi ya adreno na kusababisha ini kuitoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa au hata kuitengeneza toka tishu za mwili wenyewe ‘(gluconeogenesis)’.

Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri unakilishaji wa kinasaba (DNA), namna ambavyo seli mpya hutengenezwa.

Kafeina inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi C, zinki, potasiamu na madini mengine.

Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye utumbo mdogo.

Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.

Kafeina siyo kwamba tu huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.

Kituo cha Sayansi kwa maslahi ya umma (Center for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.

Madhara ya chai ya rangi na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha inakuwa haiishi.

Namna ya kuepuka kaffeina kwenye kahawa na chai:

Kwa upande wa kahawa ikiwa una tatizo lolote la kiafya na ungehitaji kupata uponyaji wa haraka basi ningekushauri uamuwe tu kuacha kutumia kwanza kahawa.

Au ikiwa umeanza kuonyesha dalili za matatizo haya nimeyaainisha kama matokeo ya kutumia kahawa basi ni vema ukachukuwa uamuzi wa kuacha kuitumia. Wakati mwingine inaweza isiwe kazi rahisi sababu ina kawaida ya kukupa uteja wa kuitumia kila siku lakini penye nia pana njia na hakuna lisilowezekana.

Kwa upande wa chai ya rangi kama unapenda kunywa chai asubuhi, badala ya kutumia majani hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako; unaweza kutumia tangawizi na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.

Kwahiyo unapoinywa chai ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa mengine mengi mwilini.

Unaweza pia kuweka mdalasini, mchaichai, kukamulia ndimu, pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea).

Mwanamke Makalio Bwana Sura Hata Panya Anayo...

$
0
0
Kama kichwa cha habari kinavyosemeka hapo juu

Unakikuta kisichina chembamba kweli hakina hata tako alafu kinaringa kweli kisa tu kana sura nzur

Ngoja tu niwachane ukweli sisi wanaume tunapenda sana makalio siyo sura zenu ndo maana huwez kuta mwanaume anageuka kutazama sura lakin mwanaume hugeuka kutazama wethere sura haka kungun wanazo

Hiyo sura yako kamuoneshe kaka yako nyumban ambaye haish kukuchunga chunga

Kutana na Mtabibu wa Magonjwa Sharifu Seif Mohamed Kutoka Mombasa Kenya Sasa Yupo Tanza

$
0
0
KUTANA NA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA MOMBASA KENYA sasa yupo TANZANIA, pia atayatembelea maeneo mbali mbali ndani ya nchi popote pale atakapo hitajika,

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOPIGA SIMU ZA SHUKRANI NA KUTOA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,

(RUDISHA MAHUSIANO YAKO NDANI YA MASAA 72 TU)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, anatumia kitabu cha Qur'an, dawa za kiarabu, njiwa, juju za mombasa, na majini kwa kumtuliza mke, mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, Anazo dawa za napenzi, nguvu za kiume, chango, ngiri maji, miguu kuwaka moto na kuvimba na n.k, Je? Umezunguka bila mafanikio na unahitaji Pete ya bahati iliyo ambatanishwa na jini mali? Kusafisha nyota , mafanikio ya maisha bila mashart, mvuto wa  biashara, zindiko la nyumba na mashamba, umaarufu, kupata kazi  kulingana na elimu yako, kupandishwa cheo kazini, na mengine mengi ya siri, Je  umehangaika kupata mtoto bila mafanikio? Wasiliana na mtaalam huyu  kwani yeye ufaulu pale wote  walipo shindwa, pia humaliza kazi  zilizo shindikana kumalizwa na wataalamu wengine ndani ya masaa 24 tu, Pia anatibu kwa njia ya simu popote pale ndani au nje ya nchi, Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi:

Mobile + imo  +255 654-836970
Mobile + WhatsApp +255 756-033670

NB: kama unahitaji msaada ni  bora kupiga simu kuliko kutuma sms ili upate  msaada kwa haraka.

Polisi Wasaka Fulana za Tundu Lissu...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 18

$
0
0
Polisi Wasaka Fulana za Tundu Lissu...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 18
Advertisement

Mahojiano ya Msigwa na Lema KTN: Serikali iongeze Msisitizo Kwenye Somo la Kiingereza

$
0
0
Mahojiano ya Lema na Msigwa ndani ya KTN, nadhani Lema na Msigwa walikuwa wana mambo mengi ya kuiambia dunia lakini ukosefu wa maneno kadhaa ya kiiengereza kumewaficha sana.

Mfano neno dictator uchwara ukiliongea kwa kiingereza linapoteza uzito.

Lema kaongea 'actually' mara 83 kwnye interview ya dk 24.

Tunapotaka kuongelea kiingereza cha Rais inabidi tuangalie kwanza wapi tumekanyaga. VIDEO:

Prof. Lipumba: Sitawafukuza Wabunge wa Majimbo, ila Wakimsikiliza Maalim Seif Nitawaondoa wote

$
0
0
Jana Prof Lipumba alikuwa na sherehe ya kuwapokea wabunge wa viti maalumu katika ofisi za chama Buguruni.Mkusanyiko huo ulioruhisiwa na polisi ulihudhuriwa na wanachama wengi wa CUF wa upande wa Prof Lipimba.

Katika sherehe hiyo,Prof Lipumba amenukuliwa akisema "Sina nia ya kufukuza wabunge wa majimbo,lakini kama watakuwa na kiburi cha kumsikiliza Maalim Seif,basi wembe ni uleule."

Lipumba anasema ana vijana wake aliowafundisha siasa toka akiwa mwalimu Chuo Kikuu,akimtolea mfano mbunge wa Malindi-Zanzibar,Mh.Ally Salehe.

Prof.Lipumba anasema wabunge wa majimbo,wasimsikilize Maalim Seif,akiwaita kwenye kamati ya Maadili ya chama,wafike haraka na sio kumsikiliza Maalim Seif ambaye atawaponza na wao wapitiwe na wembe kama wa wale wabunge wa kuteuliwa ambao saizi wanajuta kwa kumsikiliza Maalim Seif,na sasa wameonja ubunge wa miaka miwili,huku wakiwa na madeni tele waliyokopa kwa kudhani watakaa bungeni miaka mitano.

Baadhi ya wabunge wa kuteuliwa,wamesema wanaingia kazini,ili kuhakikisha CUF kinarudi kuwa chama kikuu cha upinzani,na katika maeneo watakayokuwepo,hakutakuwa na CHADEMA wala chama kingine cha upinzani kuibuka.

Lipumba amewaasa wabunga hao kuwa watii kwa viongozi wa chama,na watambue ofisi yao ipo Buguruni na sio sehemu nyingine.

Watano Wadakwa na Polisi Kwenye Doria ya Kuzuia Maombezi ya Tundu Lissu

$
0
0
Watu watano wanaosadikika kuwa ni wanachama wa CHADEMA wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa mahojiano zaidi kujua kama walikuwa na mpango wa maombezi ya Mhe. Tundu Lissu uliopangwa kufanyika katika uwanja wa Tip -Sinza, wilayani Ubungo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne aliyekuwa uwanjani hapo na kikosi cha askari wapatao 25 amesema watu hao walikamatwa saa 3 asubuhi wakiwa katika eneo hilo.

Tunawashikilia na tutawahoji kama wana uhusiano na kile kilichopangwa kufanyika hapa kwa sababu kilishapigwa marufuku. Kama hawana uhusiano tutawaachia,” amesema Kamanda Jumanne kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi huku akiwaonya Wananchi waliopanga kufanya maombi hayo.

Atakayetaka kujaribu aje ila cha moto atakiona kwa sababu jitihada za kuzuia watu wema wasikanyage hapa zimeshafanyika sasa wanakuja kufuata nini.”

Baadhi ya polisi wameonekana wakiwa na mabomu ya kutoa machozi na walifika uwanjani hapo wakiwa kwenye magari aina ya Toyota Land Cruiser.


Doria hiyo inakuja baada ya Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha) jana Jumamosi kutoa taarifa kuwa leo litaungana na viongozi wa kiroho kufanya maombi maalumu kumwombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeendelea na matibabu Nairobi, nchini Kenya baada ya kusha

Video: Lissu ni shabiki wa ‘Seduce Me’, Mungu amponye haraka – Alikiba

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka RockStar4000, Alikiba amesema hakutegemea mtu kama Mh Tundu Lissu angeweza kuweka hadharani hisia zake juu ya wimbo wake, Seduce Me. Muimbaji huyo amemuomba mwenyezi Mungu ampe siha njema mbunge huyo machachari wa CHADEMA ambaye amelazwa nchini Kenya baada ya kipigwa risasi na watu wasiojilikana. Wiki chache zilizopita mbunge huyo alidaiwa kupost kitu mtandaoni akiuzungumzia wimbo huo huku akiushindanisha na zilipendwa wa Diamond.

Picha za Hamisa Mobetto na Diamond Platnumz kitandani Zazua Maswali

$
0
0
Baada ya video ya wimbo wa Salome kutoka kulikuwa na romours kwamba muimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz, anatoka kimapenzi na mwanamitindo Hamissa Mobetto ambaye alikuwa moja kati ya warembo waliyotokea katika video ya Salome kama video Vixen.

Sio Hamisa wala Diamond Platnumz aliyewahi kukubali  kuhusiana na stori hizo, lakini romours zilizidi kusambaa mtandaoni zikidai wao ni wapenzi, usiku wa September 17 2017 on social networks imesambaa picha inayodaiwa ya Diamond na Hamisa wakiwa kitandani wamelala pamoja. 
VIDEO:

Familia ya Tundu Lissu Yafunguka Kuhusu Dereva Wake

$
0
0
Familia ya Tundu Lissu Yafunguka Kuhusu Dereva Wake
Siku 10 baada ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi, familia yake imezungumzia tukio hilo na namna inavyomfahamu dereva wake kwa zaidi ya miaka 20.

Tangu kutokea kwa tukio hilo mchana wa Septemba 7 huko Dodoma, dereva wa mbunge huyo, Simon Mohamed Bakari amekuwa akitajwa kama mtu muhimu anayeweza kusimulia tukio hilo na hata kusaidia kuwabaini wahalifu.

Hata polisi imekuwa ikimtaka ili imhoji ikisema ni shahidi muhimu katika tukio hilo. Hata hivyo, kijana huyo yupo Nairobi akimuuguza bosi huku mjadala juu yake ukiendelea nchini.

Katika mahojiano na Mwananchi, familia ya mbunge huyo imeonyesha kuwa na imani kubwa na dereva hiyo ikibainisha inavyomfahamu kwa miongo miwili.

Akizungumza katika mahojiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa baba wa mbunge huyo, Lissu Mughwai katika Kijiji cha Mahambe, Kata ya Unyahati wilayani Ikungi, Singida, Muro Lissu ambaye ni kaka yake alisema hawana wasiwasi na dereva huyo kwa kuwa ni kijana aliyelelewa na mwanasheria huyo mkuu wa Chadema tangu akiwa na umri wa miaka 15.

“Yule kijana alienda kwa Lissu akiwa mdogo kama kijana wa kazi za nyumbani. Alimchukua katika Kijiji cha Sefuka kilichopo Magharibi mwa Singida. Tangu wakati huo alimfunza kazi zote akiwa pale nyumbani kwake. Amemlea, amekulia kwake,” alisema Muro.

Alisema dereva huyo alifundishwa mambo mengi akiwa mmoja wa wana familia ikiwamo kupelekwa kujifunza udereva.

Muro alisema Lissu alipoanza harakati za kuwania ubunge mwaka 2007 alikuwa na kijana huyo.

“Amekuwa dereva wake tangu alipoanza kuhangaikia jimbo mpaka amechukua ubunge mwaka 2010 akawania tena 2015. Wana miaka mingi na yule kijana zaidi ya miaka 20 amemlea,” alisema Muro.

Alisema licha ya Lissu kutozungumza chochote kuhusu vitisho alivyokuwa akipewa na kufuatiliwa na watu wasiojulikana, dereva wake alikuwa akiitaarifu familia kuhusu matukio hayo kila yalipotokea, hivyo walijua kinachoendelea kupitia kwake.

Katibu wa Chadema Wilaya ya Ikungi, Jihala Ibrahim aliyekuwapo pamoja na wanafamilia katika mahojiano hayo alisema licha ya kuchanganyikiwa, dereva huyoalielezea tukio zima lilivyokuwa baada ya wao kuwasili hospitalini Dodoma wakitokea Ikungi.

“Nilikutana na dereva wake Dodoma baada ya tukio, kwa kweli yule kijana alikuwa amechanganyikiwa na mpaka anaondoka siku ya pili kwenda Nairobi alikuwa ameathirika kisaikolojia,” alisema.

Ibrahim anaamini kuwa kama asingekuwa dereva huyo, Lissu asingepona kirahisi, “Dereva wake anasema tangu wanatoka bungeni, magari mawili yalikuwa yakiwafuatilia na kila alipojaribu kuegesha gari pembeni na wao walifanya hivyo hivyo aliamua kwenda moja kwa moja nyumbani na walipofika getini gari moja lilibaki nje na lingine liliingia ndani.”

Ibrahim alisema dereva huyo aliwaeleza kuwa kabla ya watu hao kutekeleza azma yao, Lissu alikuwa tayari kushuka lakini alimzuia licha ya kutaka kushuka kwa nguvu.

“Dereva alisema baada ya kimya kifupi, gari hilo liligeuza tayari kwa kuondoka hapo alishuka mmoja wa watu hao akiwa ameficha uso wake kwa kofia na miwani myeusi, alitoa silaha na kuanza kushambulia gari la Lissu. Dereva alimwinamisha Lissu kwa nguvu kupitia nafasi iliyopo kati ya kiti chake na yeye na alifungua mlango na kujificha chini ya uvungu wa gari nyingine iliyokuwa pembeni,” alisimulia Ibrahim.

Alisema kutokana na hali ambayo alikuwa nayo kijana huyo, walilazimika kumwondoa hospitalini hapo na kumhifadhi.

“Siku ya pili baada ya Lissu kupelekwa Nairobi, dereva wake aliletwa sababu siku ya tukio makamanda wa Chadema Dodoma walimhifadhi na baadaye tulimpeleka Nairobi kupata matibabu ya kisaikolojia kwa kuwa alikuwa mtu wa kwanza kushuhudia damu ya Lissu ikimwagika,” alisema.

Kauli kwa familia

Muro alisema mdogo wake hakuwa mwepesi wa kuzungumza yanayomkabili, lakini kuna siku alizungumza kauli yenye utata ambayo amekuwa akiifikiria.

Alisema akikariri maneno ya Lissu, “Kuna wakati nafikiria tupo kwenye tanuru la moto wa mkaa wa tofali kama unaweza kutokea huku na huku tanuru linawaka ni kazi ngumu mbele yangu, kama nakanyaga tanuru nitokee upande wa pili.”

Muro alisema hakumjibu lakini alishangaa ni kwa nini alitoa kauli hiyo.

Alisema japokuwa familia ilikuwa inaona anachokifanya ni kizuri, lakini yeye Muro kuna wakati alikuwa akiwaza.

Muro alisema wiki mbili kabla ya tukio hilo, Lissu alikutana na familia yake alipohudhuria mazishi ya kaka yao na kwa kipindi chote walichokaa naye hakusema lolote.

“Baada ya kukutana, tumekaa, tumezika mpaka tukafanya kikao jioni cha ukoo kwa kweli hakuzungumza lolote na tangu alipotoka huku hatujawasiliana naye,” alisema.

Shambulio la risasi

Muro alisema tukio la Lissu kushambuliwa lilimshtua kila mwanafamilia na mpaka sasa hawajui cha kufanya na zaidi ya kusubiri taarifa kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama.

“Mimi nafanya kazi pale Ikungi, siku hiyo nilikuwa nimepumzika saa saba hivi watoto wakaja mbio wakaniambia baba; baba mdogo kapigwa risasi niliruka sababu nilikuwa usingizini, sentensi ya kwanza ilikuwa amekufa? Walinijibu subiri kidogo,” alisema.

Muro alisema alipoambiwa kuwa amepelekwa hospitali Dodoma alipumzika kwa nusu saa baadaye akaamua kuelekea huko.

“Nilipofika Manyoni nilipigiwa simu kuambiwa nirudi maana hata ningefika nisingeweza kumuona kwa kuwa wanafanya utaratibu wa kwenda Nairobi, Nilirudia hapo. Familia tumepigwa na mshangao na mpaka sasa japokuwa tunasikia kwamba hali yake ni nafuu lakini tumelipokea suala hili kwa mshtuko mkubwa ,” alisema.

Alisema baba yake mdogo, shangazi zake, mama zake wadogo, binamu zake na hata wapigakura wake wa Ikungi na wananchi kwa jumla walipigwa na bumbuazi.

Muro alisema familia imewatuma ndugu akiwamo kaka yake Alute ambaye ni mwanasheria jijini Arusha, mjomba wao na dada yao anayeishi Songea kwenda Nairobi kufuatilia hali yake.

“Kule kuna dereva wake ambaye yupo karibu na sisi, mke wake na watu wengine ambao ni viongozi wa chama wapo kule. Kuna dada yetu anayekaa Songea na kesho anaondoka mdogo wetu anaitwa Vincent, ni muda mfupi hatujafikiria tufanye nini,” alisema.

Muro alisema mwishoni mwa mwezi huu watafanya kikao Dar es Salaam wajue nini cha kufanya.

Baba mdogo wa Lissu, Muro Sawa (79), alisema kitu ambacho wazazi wangefurahia ni kumwona kijana wao akirudi nyumbani akiwa mzima.

“Familia tutakaa kikao kushauriana ili tujue suala hili tunalitatua vipi, lakini niiombe Serikali kumzidishia ulinzi kijana wangu. Sisi familia tuna uchungu mkubwa kuhusu hili,” alisema Sawa.

Shangazi wa Lissu, Ninaa Sawa Muro (83) alisema, “Tunakula chakula hakishuki, matonge yanakaba shingoni, maungo yote yanauma kwa sababu ya mtoto wetu, tangu siku ile niliposikia nilikuwa kwenye kiti ghafla nikaanguka na kuanza kutetemeka.”

Alisema alijisikia vibaya baada ya kuambiwa na mtoto wake taarifa hizo, “Aliniuliza umesikia kwamba Tundu Lissu amepigwa risasi? Nikanyamaza, nikaona joto. Kwa jinsi shangazi yangu anavyonipenda hata anikute Manyoni hata Dar es Salaam ananiita jina langu la kikwetu anakuja ananikumbatia iliniuma sana.”

“Alifanywa hivyo kwa nini? Kama tunavyojiona wote roho moja tumfikirie huyo Tundu Lissu,” alisema shangazi huyo ambaye baada ya baba yake Lissu kuzaliwa ndiye aliyemfuata.

Mama mdogo wa Lissu, Bula Muro, alisema baada ya kupata taarifa alianguka chini na kuanza kulia hakufikiria kama amepona.

Mitandao ilivyoiliza familia

Mmoja wa wanafamilia, Msengi Ntandu Mughwai alisema walipata shida siku hiyo ya tukio, “Tulipanga kwenda Dodoma wakasema turudi anaendelea na matibabu, tulihisi wanatudanganya sababu mtandaoni wanasema hali mbaya na kwa kuwa walikuwa ni wanafamilia waliotushauri, tuliamua kurudi usiku kwa kweli kesho yake kulikuwa na habari za ajabu kwenye mitandao yaani zilituumiza sana,” alisema.

Msengi alisema walikuwa wakipigiwa simu na kupewa taarifa zenye utata na wakiingia mitandaoni wanaona habari za ajabuajabu na kwamba hali kwao ilikuwa mbaya.

“Kwa kweli tulipata shida, wazazi wetu walikuwa wanakuja mara kwa mara tunawajibu kwamba anaendelea vizuri lakini wazee wetu walikuwa wanapata taarifa mbaya kwingine kutokana na mitandao ya kijamii,” alisema.



Serikali ya Brazili Imeisamehe Tanzania Deni la Bilioni 445

$
0
0
Serikali ya Brazili Imeisamehe Tanzania Deni la Bilioni 445
Serikali ya Brazil imeisamehe serikali ya Tanzania deni lenye thamani ya bilioni 445 za kitanzania, ililokuwa inadaiwa na nchi hiyo.

Tarifa hiyo imetolewa leo na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas kwenye ukurasa wake wa twitter, na kufafanua kwamba deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma, mwaka 1979 pamoja riba yake.

"Serikali ya Brazil imesamehe Tanzania deni la jumla ya dola za Kimarekani mil. 203 ambazo ni sawa na tsh bil. 445,deni hilo lilitokana na mkopo uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Morogoro-Dodoma mwaka 1979 pamoja riba," ameandika Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbas
Msemaji wa serikali ameendelea kwa kusema kwamba kitendo hicho kimefungua milango iliyokuwa imefungwa kutokana na deni hilo, ambapo sasa makampuni ya Brazil yataweza kuja nchini na kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo.

Pia serikali imeshukuru Brazil kwa kitendo hicho na kuunga mkono jitihada za Rais John Pombe Magufuli za kuleta maendeleo ya nchi.


Hizi Hapa Sababu za Jeshi la Polisi Mkoani Geita Kumshikiria Mbunge Msukuma

$
0
0
Hizi Hapa Sababu za Jeshi la Polisi Mkoani Geita Kumshikiria Mbunge Msukuma
JESHI la Polisi mkoani Geita linamshikilia Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku ‘Musukuma’ kutokana na vurugu zilizotokea eneo la Mgodi wa GGM Septemba 14 mwaka huu.
Mbunge Msukuma na madiwani wa wilaya ya Geita walifunga barabara zinazoingia kwenye mgodi wa GGM wakishinikiza kulipwa dola 12 milion zinazotokana na kodi ya huduma.

Kamanda wa polisi mkoani hapa Mponjoli Mwabulambo jana alithibitishwa kukamatwa kwa Msukuma na kusema askari walimkamata katika eneo la CCM mjini Geita. Kamanda amesema kukamatwa kwa Musukuma ni mwendelezo wa Polisi  kuwakamata watu wote waliohusika katika vurugu zilizotokea Septemba 14.

Amesema tayari wamekamata madiwani wengine wawili na wananchi  watano na kwamba jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi na msako wa kuwakamata wote walioshiriki.
“Bado tunaendelea na msako na hawa ni wahalifu kama wahalifu wengine na sheria lazima ichukue mkondo wake na  Musukuma tumemkamata sio kwamba amekuja mwenyewe ”amesema

Lipstiki za Wema Sepetu Zapigwa Stop Bongo, Mzigo Wake Wazuiwa Kuingia Nchini

$
0
0
Lipstiki za Wema Sepetu Zapigwa Stop Bongo, Mzigo Wake  Wazuiwa Kuingizwa
KAMA ilivyo ada ya ubuyu kutoka visiwani Zanzibar, huwa haumuachi mtu salama kutokana na namna unavyoandaliwa! Ndivyo ulivyo ubuyu wa wa motomoto uliotufikia kunako meza ya kujilamba kuwa, staa mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bongo, Wema Isaac Sepetu anadaiwa kupata pigo baada ya mzigo wake mkubwa wa zile lipstick zake za Kiss kuzuiwa kuingizwa Bongo na taasisi moja serikalini.

UNAKUMBUKA ZILE LIPSTICK ZA WEMA?
Kwa mujibu wa mnyetishaji wetu wa ubuyu, badaa ya lipstick alizozitoa mwanzoni kugombewa kama njugu na wasambazaji mbalimbali wa urembo wa jumla na rejareja Bongo, inasemekana kuwa, mlimbwende huyo alinogewa na mambo ya fedha hivyo akaagiza mzigo mwingine kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendeleza biashara hiyo.
Hata hivyo, chanzo hicho kilimwaga ubuyu kuwa, kutokana na namna bidhaa hiyo ilivyokubalika na kupendwa na wanawake wa rika mbalimbali, Wema alipata shauku kubwa na kuagiza mzigo mkubwa zaidi.

“Unajua ule mzigo wa kwanza wa Wema, watu waliupenda sana na kuugombea sana hivyo aliamua kuagiza mwingine tena kwa ajili ya kuendelea na biashara yake kwa kuwa mzigo haukukaa sana,” kilinyetisha chanzo hicho.
Mtoa habari huyo alizidi kutiririka kuwa, baada ya Wema, kuagiza mzigo huo, ulifika Bongo, lakini kisheria lazima upitie kwenye taasisi moja serikalini ili kuthibitisha kama zina ubora.

ZADAIWA KUPIGWA ‘STOP’
Ilidaiwa kuwa, katika hatua hiyo ndipo zilipogundulika kuwa hazina kiwango au ubora kwa afya ya binadamu hivyo kupigwa ‘stop’ kusambazwa Bongo.
“Wale jamaa walisema hauna kiwango sahihi kwa ajili ya kuwauzia watu hivyo ukazuiliwa na hakuweza tena kuusambaza na kuamua kukata tamaa,” kilizidi kufunguka chanzo hicho.

KADINDA ASAKWA
Baada ya Ijumaa Wikienda kumwagiwa ubuyu huo lilianza kusaka njia za kuthibitisha madai hayo ambapo lilianzia kwa mmoja wa mameneja wa Wema, Martin Kadinda.
Kadinda alipobanwa juu ya ubuyu huo alisema kuwa, anachokijua ni kwamba Wema alitoa zile lipstick za mwanzo hivyo kama kuna zilizopigwa stop, zitakuwa ni za mtu mwingine ambaye alitaka kuziingiza nchini kwa kutumia jina la bosi wake huyo.

“Ninachojua ni kwamba Wema alitoa zile za kwanza tu, kama kuna za pili, sina uhakika maana kama zilitoka mimi ningejua.
“Inawezekana kabisa katika mazingira tuliyo nayo, kuna mtu anaweza akawa anatumia jina lake (Wema), lakini siyo yeye kabisa,” alisema Kadinda.
Jitihada za kuzungumza na Wema hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kupigwa mara kadhaa lakini haikupokelewa. Hata alipotumiwa ujumbe mfupi na chatting kwa njia ya WhatsApp hakujibu.

NENO LA MHARIRI
Kazi ya Ubuyu Ulionyooka ni kuupokea ubuyu kutoka kwa chanzo kisha kuutafutia ladha maridhawa na kuufikisha kwako ili uumung’unye kwa raha zako na hicho ndicho tulichokifanya.
Baada ya Bongo Muvi Kufa, Yafufuka Kupitia BARAZANI

Marekani Yatathmini Kufunga Ubalozi Wake Cuba

$
0
0
Marekani Yatathmini Kufunga Ubalozi Wake Cuba
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Washington inathamini iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.
Sasa zaidi ya wafanyakazi 20 wa ubalozi wa Marekani wameripotiwa kuwa na matatizo ya kupoteza uwezo wa kusikia au kupatwa na mfadhaiko kutokana na sauti hiyo.
Cuba na Matumaini Mapya
Trump atishia kufuta sera za Obama kuhusu Cuba
Trump kufufua vikwazo dhidi ya Cuba
Marekani imeiambia Cuba kuwa ina jukumu la kuwalinda wafanyakazi wote wakigeni wakiwemo .
Cuba imekana kuhusika na swala hilo huku uchunguzi zaidi ukiendelea .kujua chanzo cha watu hao kukumbwa na matatizo hayo ya kiafya wanayoyauzungumzia. .

Polisi Yafunguka Mabomu ya Arusha Yaliyosababisha Vifo

$
0
0
Polisi Yafunguka Mabomu ya Arusha Yaliyosababisha Vifo
Kamanda wa polisi Arusha Charles Mkumbo amewataka viongozi waliopo karibu na kambi za mazoezi ya kijeshi kuweka utaratibu wa kuwakumbusha wananchi kutoa taarifa pindi wanapoona vitu wasivyovijua hasa vyenye asili ya chuma ili kuepusha madhara.

Kamanda Mkumbo ametoa hadhari hiyo alipokuwa akizungumzia tukio la vifo vya watoto watatu wakazi wa kata ya Loksale wilayani Monduli vilivyosababishwa na mlipuko wa bomu waliookota wakati wanachunga mifugo na kuanza kulichezea kama mpira ambalo lililipuka na kuwajeruhi vibaya miguuni.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda Mkumbo amesema licha ya kuwa tukio hilo ni la bahati mbaya lakini lingeweza kuepukika kama watoto hao wangeweza kutoa taarifa ya kitu walichokiona.
Kamanda Mkumbo amesema kuwa watoto hao  wangeweza kufanya hivyo kama wangekuwa wanakumbushwa na wazazi wao mara kwa mara wanapokwenda machungani.
Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Monduli Bw. Iddy Kimanta aliyezungumza na ITV kwa njia ya Simu amesema watoto hao wote ni wanafunzi wa shule ya msingi Nafko na wawili akiwemo Landisi Setabau miaka 12 na Samweli Nyandusi miaka 9 walikuwa wanasoma darasa la kwanza wakati mwingine aliyetajwa kwa jina la Seuri Losila miaka alikuwa darasa la tatu.
Viongozi wa eneo lililopotokea tukio hilo wamesema kimsingi tukio hilo ni bahati mbaya kwani kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakielimishwa juu ya kufuata maelekezo na mara nyingi wamekuwa wakitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja kutoa taarifa wanapoona mabaki ya vyuma.
Kwa mujibu wa viongozi hao katika maeneo mengi ya wafugaji wakati wa likizo watoto huwasaidia wazazi wao kuchunga mifugo na pia wakati wote wamekuwa wakitoa taarifa wanapokutana na vitu kama hivyo na wahusika wamekuwa wakifika mara moja na kuvichukua

Sitamani Kuolewa na Ray Tena Ila Nimeamua Kumpa Zawadi ya Mtoto- Chuchu

$
0
0
Sitamani Kuolewa na Ray Tena Ila Nimeamua Kumpa Zawadi ya Mtoto- Chuchu
CHUCHU Hans ni mmoja wa mastaa wa filamu ambao wanafanya vizuri kupitia tasnia hiyo na kama ukibahatika kuangalia moja ya kazi zake, utakiri niyasemayo.
Pia si msanii tu wa filamu bali yupo vizuri kwenye kuigiza hata kucheza muziki mbalimbali na ndiyo maana akiwa katika mashindano ya urembo wa Miss Tanzania miaka hiyo, aliibuka mrembo mwenye kipaji cha kucheza muziki (dancing talent).
Staa huyu ambaye miezi nane aliyopita alibahatika kupata mtoto wa kiume aliyempa jina la Brian aliyezaa na mwigizaji nguli wa kiume Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameweka wazi maisha yake ya sasa hivi pamoja na kazi zake;
Swali: Vipi maisha ya ulezi maana umepumzika kwa muda mrefu?
Chuchu: Naendelea vizuri na ninayafurahia maisha haya kwa sababu kuna vitu vingi ninajifunza hasa kuwa jasiri kama mama.
Swali: Mnaendeleaje na maisha ya kimapenzi wewe na mzazi mwenzio Ray?
Chuchu: Tupo vizuri, Ray anasimama kama baba na mimi ninasimama kama mama kwa mtoto wetu.
Swali: Kulikuwa na tetesi za kufunga ndoa kabla hata ya kujifungua, vipi ishu hiyo bado ipo?
Chuchu: Hakuna ishu kama hiyo tena.

Wakiwa wamepozi.
Swali: Ni kwa nini au nini kimetokea?
Chuchu: Hakuna lililotokea ila tu sitamani kuolewa naye (Ray) tena, nafikiri ni kwa sababu tumejuana sana na kila mtu amemzoea mwenzake.
Swali: Mbona kuna tetesi kuwa mnaishi pamoja?
Chuchu: Hapana, wala haijawahi kutokea, yeye anaishi kwao na mimi ninaishi kwangu.
Swali: Ulijisikiaje kwa mara ya kwanza, Ray alipokuanika kama mpenzi wake na huko nyuma hakuwahi kuweka wazi uhusiano wake wa kimapenzi?
Chuchu: Najisikia furaha na ndiyo maana niliamua kumpa zawadi ya mtoto kwa kuwa umri wake niliona unaenda na watu walishaanza kumsema tofauti maana kumzalia mtoto mimi ni kumpa zawadi yeye.
Swali: Huna mpango wa kuongeza naye mtoto mwingine?
Chuchu: Hapana, zamani nilifikiria hivyo, lakini hilo wazo hakuna tena.
Swali: Kwa nini umeamua kuahirisha mpango huo?
Chuchu: Sina hata sababu maalum, nimebadili tu mawazo.
Swali: Kutokana na kazi zenu na baba watoto wako ni moja na unajua mambo mastaa, vipi hujisikii wivu na yeye?
Chuchu: Hapana, sina wivu kabisa, roho yangu ni ya Kizungu.
Swali: Mara nyingi mastaa watoto wao wakifikisha arobaini ndiyo huwa wanawatoa nje, lakini kwa nini mpaka leo, miezi nane hujamuonesha mtoto wenu?
Chuchu: Huo ni uamuzi wa baba yake maana kila kitu nimemuachia baba yake.
Swali: Kuna kipindi mlianzisha kampuni yenu ya CHURA (Chuchu na Ray), vipi imeishia wapi?
Chuchu: Ipo, ninaiendesha mimi.
Swali: Baada ya kujifungua tayari umesharudi kazini?
Chuchu: Ndiyo, nimeanza kufanya kazi hata za watu, wakiniita ninafanya na pia sasa hivi napika vyakula, ninasambaza kwenye ofisi mbalimbali
Swali: Najua Ray amekukuta na watoto wako wengine wawili, je, anawachukuliaje?
Chuchu: Anawachukulia kama watoto wake kabisa.
Swali: Vipi kwa upande wa wakwe zako, umepokelewa vizuri?
Chuchu: Sana na wananipenda mno.
Swali: Kulikuwa na tetesi kuwa ulikuwa na bifu na msanii Johari, vipi limeisha?
Chuchu: Sijawahi kuwa na mgogoro naye na tupo vizuri tu.
Swali: Nakushukuru sana Chuchu kwa ushirikiano wako.
Chu-chu: Asante na karibu tena.
   

Ushahidi Huu Hapa wa Hamisa Mobetto Kulala Kitandani Kwa Zari Akiwa na Diamond Platnumz Usiku wa Leo

$
0
0


Wadau huku Instagram wanaendelea kurusha picha za ushahidi wa Penzi la Diamond na Hamissa Mobetto na kuwa usiku wa leo wamelala wote nyumbani kwa Diamond tena kitanda kile kile alichokuwa analala na Zari....


Mdau mmoja kaandika hivi:

"Hivi Mpaka sasa kuna mtu bado hakubali🤣🤣Mnaosema ni PhotoShop hii ni Real jamani kama hamuamini mkawaulize wafanyakazi wa madale😂 na mama dangote anajua vizuri tu"

Zitto Kabwe Afunguka 'Baada ya Kumuona Tundu Lissu Alivyoumizwa Nimerudi Tanzania Nikiwa Mnyenyekevu'

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alionyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

 Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook asubuhi ya leo na kusema japo Lissu ameumizwa sana lakini hakuacha kumuonyesha ucheshi licha ya kuwa na maumivu makali aliyokuwa nayo katika mwili wake.

"Siku mbili hizi nilizoenda kumuona Lissu zimeniacha nikiwa mawazo sana, nimerudi nchini nikiwa kwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu amenionesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali. Siyo mara nyingi hapa nchini kusikia tukiongelea ujasiri lakini namfikiria lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi, najua hivyo ndivyo alivyo", ameandika Zitto.
Pamoja na hayo, Zitto ameendelea kwa kusema "waliomshambulia wamemuumiza kweli na bado wakati tuliokuwa naye amenionesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri, alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu siyo kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha niumie moyo kama asingesema maneno haya kwangu kuwa  'tumeshinda. Tumeshashinda", amesisitiza Zitto.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.

Full video: Nyumbani Kwa mtoto wa Bakhresa ni Maajabu matupu, huwezi Amini

$
0
0
Hii video chini inaonesha maisha halisi ya Yusuph Salim Bakhresa , Na Mali anazomiliki ndani.

Magari ya kifahari zaidi ya 20 ndani, Na mengine jionee VIDEO:
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images