Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

VIDEO: Hamisa Mobetto Azungumzia Kukutana na Diamond Dubai “Diamond ni Mzazi Mwenzangu”

$
0
0
Mrembo Hamisa Mobetto amekaa kwenye Exclusive Interview ya AyoTV na millardayo.com na kueleza kuhusu taarifa zake za kukutana na Diamond Platnumz Dubai, ameongea kila kitu kwenye hii video hapa chini

 VIDEO:

KUTOKA IKULU: Kuhusu Taarifa za Uteuzi wa Katibu Mkuu Ndumbaro Kutenguliwa

$
0
0
Kumekua na Taarifa zilizosambaa kuanzia saa kadhaa zilizopita kwamba Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Dr. Laurian Ndumbaro.

IKULU imetoa taarifa jioni hii na kusema taarifa hizo sio za kweli vilevile Wananchi wazingatie kupokea taarifa sahihi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi vya serikali.

Sababu 6 Kwa Nini Hupaswi Kudeti Mwanamke Asiyependa Gharama

$
0
0
Kuwa na mwanamke asiyependa gharama ni ndoto ya kila mwanaume katika sanaa ya kudeti. Kwa kawaida wanawake aina hii hawana drama wala stress. Lakini je ni muhimu kweli kuwa nao?

Hebu jiweke katika hii hali: uko na mwanamke ambaye ukifika nyumbani tu ashakuandalia kila kitu, hakuulizi kwa nini umechelewa, hajibizani na wewe, hana time ya kukupa vikwazo kwa nini humpatii hela za kwenda kula bata wikendi wala pesa za kumnunulia viatu design latest ama kutaka kujua kila kitu unachofanya unapokuwa mbali na yeye. Yeye lake muhimu ni kukupa penzi ambalo huwezi kulisahau.

Raha ilioje hii?


Hii ndio aina ya wanawake ambao wanaume wengi wangetamani kuwa nao maishani. Uzuri ni kuwa wanawake hawa hupatikana katika dunia ya sasa, na ni wengi mno. Wanawake aina hii wanatoa mtizamo wa kuwa na maisha ya raha mstarehe lakini ukweli ni kuwa hawa wanawake ndio wabaya zaidi. Wanakata kwa sehemu mbili, mbele na nyuma. Wataua hisia zako za kimapenzi na pia wataua matamanio yako.

Je, aina hii ya wanawake ni ipi?


Mwanamke asiekuwa na gharama hujitambulisha kama mwanamke asiyekuwa na drama nyingi kama wale wengine. Unaweza kumtambua na hizi tabia.

#1 Kila kitu chake huwa sahala/simple. Katika kabati lake la nguo utaona zile nguo anazozivaa, na bathroom yake haijapangwa vipodozi vingi ambavyo wanawake wengi hupenda kupaka wakati wa kujiandaa kutoka out. Hii inamaanisha mwanamke huyu hachukui muda mwingi kujiandaa kutoka nje. Dakika 10 zatosha kwake.

#2 Ni mchumi. Ya nini kwenda kujivinjari katika mkahawa ambao utatumia pesa nyingi ilhali mnaweza kuweka deti yenu kwa nyumba mkiwa mumenunua vinywaji vyenu mkichangana na viumio mlivyoviandaa wenyewe? Mwanamke aina hii anajali vile anatumia pesa zake na vile unavyotumia pesa zako kwake. Ni mwanamke ambae hahitaji kutumbuizwa kila jioni ama kununuliwa nguo za gharama ili afurahie maisha.

#3 Anapenda mahusiano ambayo hayana drama. Si lazima umpeleke mkahawa wa pesa nyingi ili umfurahishe, yeye yuko sawa na penzi unalompa. Hutawahi kumskia akilalamika kuwa hukumpigia simu jioni umjulie hali, na si lazima umpangie saprize kubwa ama kumnunulia gift wakati wa happy birthday yake sababu hatajishughulisha. Yeye ni kama beste na girlfriend kuchanganya pamoja.

Matatizo ya mwanamke asiyependa gharama.


Ijapokuwa mwanamke aina hii anaweza kuonekana mwanamke bora wa kuoa, unawezakuwa umekosa kujua matatizo ambayo yanahusiana na mwanamke aina kama hii. Hebu zama nasi tukufafanulie.

#1. Anaweza kutarajia pia wewe uwe mwanaume usiyependa gharama. Mara itokezee kuwa yeye hapendezwi na maisha yako, ama umependa kuspendi sana mara moja au nyingine? Kama girlfriend wako anapenda mambo yawe rahisi, unaweza kujipata umeachwa kwa sababu ya kujifanya diva sanaa.

#2 Kuna nafasi ndogo ya romance na upendo. Moja wapo ya sababu ambazo hufanya watu kupendana ni romance. Huyu mwanamke wako asiyependa gharama anaweza kuwa mzuri kukaa mbele ya runinga, lakini nafasi ya kuwa romance ama kutoka deti kujifurahisha mara moja au nyingine iko wapi? Usijisumbue kufanya mambo ambayo wapenzi wa kawaaida hufanya kwa sababu hatakubaliana na wewe.

#3 Relationship yenu itaboa haraka. Kwa kuwa hakuna kelele, kupigana, kukasirikiana kuhusu mahusiano, unaweza jipata katika mzunguko usiokwa na mwisho. Hakutakuwa na sapraiz ambazo zitasisimua moyo wako, hakuna hisia kutoka kwake ambazo zinaweza kuchangamsha penzi lenu. Kama nyote wawili mumetosheka na vile penzi lenu liko, na hamuwezi kufikiria jambo ambalo litawasisimua, basi kilichobakia ni kutafuta mwingine.

#4. Uhusiano wenu unaweza kuleta majanga. Kumkimu mwanamke asiyekuwa na gharama ni rahisi kuliko mwanamke wa kawaida. Hii inamaanisha kuwa hautapitia zile shida za kawaida ambazo wachumba hupitia – na huku kukosa maarifa kunaweza changia kuwe na majanga katika relationship. Kupigana, kukosana, kusumbuana huwa kunajenga mahusiano yenu kuwa bora zaidi. Kama umeamua kumchagua mwanamke aina hii kwa kuwa ni rahisi kumuweka, basi fahamu kuwa pia ni rahisi kumpoteza.

#5 Mahusiano yenu yanaweza kuwa mafupi. Kuwa na mwanamke asiyekuwa na gharama huwa kunafurahisha mara ya kwanza, lakini itafikia mahali flani ambapo kila kitu kitafikia ukingoni na mambo kuanza kusambaratika. Kama hakuna mmoja kati yenu atajaribu kuyafufua maisha yenu na kuyafanya yawe na mnato, basi bila shaka itafikia mahali flani utajutia kwa nini umemchagua mwanamke aina hii.

#6 Unaweza kumchukulia hivi hivi. Wanawake wasiokuwa na gharama ni wazuri kutembea nao kwa kuwa hawana hasara. Hii itakufanya wewe uwachukulie tu kawaida. Lakini unapaswa kufahamu ya kuwa si eti kwa sababu haombi chochote kutoka kwako basi unapaswa kuyapuuza matakwa yake katika mahusiano. Tatizo hapa ni kuwa unachukulia kila kitu kiko sawa kwake. Umemiss birthday yake? Umevunja deti na yeye kwa kuwa ulienda kuangalia gemu ya Arsenal na Man U na marafiki zako? Ni sawa. Ijapokuwa anaweza kuvumilia haya yote, hakuna sababu yako wewe kumchukulia kama mtu asiyekuwa na thamani.

Anyway katika hii dunia hakuna kitu kilichokamilika. Kila kitu kina dosari. Kama umejikuta uko na mpenzi aina hii hupaswi kumwacha. Jaribu kuongea na yeye na umpatie sababu za kwanini anapaswa kubadilisha tabia yake ama vipi?

Mafanikio kwako.

Utajuaje Kama Girlfriend Wako Anakupenda? Dalili Na Ishara Zote Tunazo.

$
0
0
Unaweza kuwa na girlfriend kwa muda mrefu na usiweze kujua kama anakupenda au la. Wanawake wengine wanaweza kujifanya girlfriend wazuri kumbe wanakutumia. Na pia unaweza kuwa na girlfriend halisi ambaye anakupenda kuanzia juu mpaka chini.

Kama mwanaume, unapaswa kujua ishara zote ambazo zinaonyesha iwapo mwanamke anakupenda ama anakutenda. Hii ni muhimu kwa kuwa utakuwa unasoma vigezo vyake ili uweke uamuzi wa mwisho kama iwapo utakubali kuishi na yeye milele ama utaamua kumuacha katikati.

Hapa Nesi Mapenzi leo tumekuletea ishara zote ambazo zitakuonyesha iwapo mwanamke/girlfriend wako anakupenda au la. Zama nasi.

Ishara kuonyesha kama mwanamke/girlfriend wako anakupenda.


#1 Anakufanyia yale mambo madogo madogo kuyafanya maisha yako kuwa rahisi. Kama mwanamke anakupenda basi jambo la kwanza la kufanya ni kuonyesha upendo kwa anayempenda. Kama unamwona anakukunjia nguo zako, anakutembelea kuhakikisha nyumba yako iko safi ama kuhakikisha hausahau kununua kitu muhimu kwa nyumba yako basi ujue anakupenda.

#2 Anakuoshea nguo. Kama anakufanyia kitu nyumbani kwako ambacho yeye mwenyewe huwa hapendi kufanya kwake basi ni ishara nzuri. Anajaribu kuonyesha uanawake wake kinyumba. Katika DNA ya mwanamke ni kuwa ameumbwa kuwajali wale ambao anawapenda ili kuwarahisia maisha. Kama girlfriend wako anaonyesha hizi tabia basi ujue anakupenda.

#3 Kando na kuwa anajua chakula unachokipenda, anajaribu kukitengeneza. Anajua chakula nachokipenda? Ashawahi kukutengezea mara kwa mara? Huyo anakuonyesha kuwa anakupenda.

#4 Anaelewana na familia na marafiki zako hata kama hawamthamini. Kama girlfriend wako anatabasamu hata kama familia yako inachukiza, basi huo ni upendo. Kwa kawaida wanawake hawaelewani na familia ya mwanaume. Lakini ukiona anajaribu bila kulalamika, hio ni ishara ya upendo kwako.

#5 Anakatiza shughli zake kuja kukuona. Kama yuko tayari kuuza tiketi yake ya kwenda kwa concert ya Diamond ili aspend usiku na wewe, hio ni ishara ya kukuambia, "nakupenda."

#6 Anayaweka matakwa yako mbele. Ukiona yuko tayari kufunja sherehe na marafiki zake ili asherehekee na familia yako ama kwenda kula dinner na marafiki zako ni ishara ya mapenzi.

#7 Anakusifia pale ambapo inahitajika. Mwanamke ambaye anakupenda hataona tatizo kukusifia pale ambapo kunahitajika. Kuambia mtu kuwa unampenda kunaonyesha kuwa unamthamini.

#8 Ni mtu wa kwanza kukupigia iwapo ana furaha, huzuni ama hasira. Kitu chochote ambacho kitamtokea yeye atakuwa wa kwanza kukuambia. Hii inamaanisha anakupenda na anakuamini. Uwepo wako kwake anaudhamini na kuuzingatia.

#9 Atakwambia mambo ambayo hayapenda. Ashawahi kukuambia mambo yaliyomuaibisha, huzunisha ama kumfelisha? Ukiona anakwambia kila kitu hata siri zake za kuzimu basi fahamu kuwa anakupenda.

#10 Anaonyesha ukichaa wake. Hakuna mtu anaweza kufunguka asilimia 100 tabia zake kwa yeyote. Ukiona amekuwa huru na wewe kiasi cha kuwa anaweza kuachilia hewa, kukuonyesha sura za kiajabu, ama kufanya mambo ambayo hukutarajia, basi ni ishara ya kuwa penzi lake kwako ni la dhati.

#11 Anashikwa na wivu ukiongea kuhusu wanawake wengine, lakini si sana. Mwanamke anayekupenda huwa hapendi kuskia ukiwasifu wanawake wengine. Hio ni kawaida.

Hizi ni baadhi ya dalili kuonyesha kuwa mwanamke anakupenda. Je girlfriend wako anaonyesha hizi tabia ama ni mtofauti na tabia hizi tulizozitaja? Uamuzi ni wako sasa.

Peter: Sihusiki na Kundi la P-Square Kuvunjika

$
0
0
NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambaye alikuwa anaunda kundi la P-Square, Peter Okoye, ameweka wazi kuwa yeye si chanzo cha kundi hilo kuvunjika.

Kundi hilo kwa sasa limevunjika kwa madai kwamba kila mmoja alikuwa anafanya mambo kinyume na utaratibu na kila mmoja sasa anafanya kazi peke yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapacha hao walikuwa wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa, lakini kila mmoja alionesha kusherehekea kivyake japokuwa Paul aliposti picha yao ya utotoni.

Taarifa zilisambaa kwenye mitandao kwamba Peter ndio chanzo cha kuvunjika kwa kundi hilo, lakini ametumia ukurasa wake wa Instagram na kukanusha taarifa hiyo.

“Nashangaa kuonekana kuwa mimi ndio mwenye kosa, hakuna ukweli wowote nadhani kosa langu ni kuweka wazi tofauti zetu, ila mimi si chanzo kama watu wanavyosema kwenye mitandao ya kijamii, lakini nashukuru kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa,” aliandika Peter.

Tattoo za Mastaa zilizofutwa Baada ya Mapenzi Kuvunjika

$
0
0
MICHORO ya mwilini inayofahamika kama ‘Tattoo’ imekuwa ikitumiwa na watu mbalimbali katika kuhifadhi kumbukumbu ya vitu ambavyo mchorwaji anakuwa amavidhamiria kuviweka kwenye mwili wake.

Tattoo inaweza kuchorwa kama urembo, kumbukumbu au alama ya kitu fulani ambacho kinakuwa na umuhimu kwa mtu aliyechora ndiyo maana tunaona wapendanao wengi wakichorana michoro hiyo kama alama ya inayoonyesha upendo wao.

Bongo pia tumeendelea kushuhudia mastaa mbalimbali wakionyeshana ubabe wa kupendeza kwa kuchora tattoo zenye maana tofauti huku kapo kadhaa za mastaa nazo zikichorana michoro hiyo iliyoanza kuchworwa kitamaduni nchini Japani mnano karne ya 18.

Juma3tata leo tunakuletea orodha ya mastaa wa Bongo ambao walipagawa na mapenzi kiasi cha kuchora tattoo za wapenzi wao na baadaye kuzifuta baada ya kapo zao kuvunjika.

Amber Lulu & Young Dee

Julai 20 mwaka huu, ilifahamika kuwa Amber Lulu ameifuta tattoo yenye jina la Young Dee katika mkono wake na kubadilisha mchoro. Wawili hao wote wawili wamewahi kukanusha kuwa wapenzi japo kuwa Young Dee amewahi kunukuliwa akisema yeye na Amber Lulu waliwaahi kudondoka kitandani.

Shilole & Nuh Mziwanda

Shilole hivi sasa ameposwa na jamaa anayeitwa Asharafu Uchebe na ndoa yao inatarajia kutikisa nchi ifikapo Desemba 20 mwaka huu, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mrembo huyo.

Lakini Shilole enzi za ujana wake kwenye tasnia ya mapenzi aliwahi kuwa na uhusiano na msanii, Nuh Mziwanda, penzi lao lilikuwa maarufu mno kutokana na matukio waliyokuwa wanayafanya pamoja.

Desemba 30 mwaka 2015 ilifahamika kuwa Shilole aliifuta tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda aliyoichora katikati ya maziwa yake, aliibadili na ikawa kama ua fulani hivi nzuri nzuri.

Hali kadharika Februari 7 mwaka 2016, Nuh naye aliifuta tattoo ya Shilole iliyokuwa kwenye mkono wa kushoto ikisomeka Shishi Baby, alifanya hivyo baada ya penzi lao kuvunjika.

Nawal

Huyu ni mzazi mweza wa Nuh Mziwanda. Wawili hawa walifunga ndoa kamili ya Kiislamu, Novemba 10 mwaka jana na kufanikiwa kupata mtoto mmoja anayeitwa Anyagile.

Mwaka huu ndoa hiyo ilivunjika baada ya Nuh kurudi kwenye dini yake ya Kikristo ambapo enzi wapo pamoja, Nawal alijichora Tattoo yenye jina la Nuh Mziwanda ambayo hivi sasa ameibadilisha na imekuwa kama mchoro wa ua.

Fahamu

Kuwa hao ndiyo mastaa ambao walifuta Tattoo za wapenzi wao baada ya kapo zao kuvunjika lakini pia nikujuze kuwa msanii Harmonize naye aliwahi kufuta tattoo yenye sura ya bosi wake (Diamond Platnumz,) kisha kuichora tena nyingine nzuri kwenye mkono ikiwa chini ya tattoo nyingine yenye sura ya mama yake mzazi, hiyo ilikuwa mwaka jana mwezi Agosti.


Mtanzania

Miujiza ya Sharifu Seif Mohamed..JE Umeachwa na Mme/Mke au Mpenzi, Umesongwa na Mitihani ya Maisha..Piga Simu Upate Muujiza Wako

$
0
0
MIUJIZA YA SHARIFU SEIF MOHAMED KUTOKA BAGAMOYO.

SHARIFU SEIF MOHAMED ANAWASHUKURU WALE WOTE WANAOENDELEA KUPIGA SIMU, WENYE MATATIZO NA WALE WANAOTOA  SHUKRANI NA SHUHUDA JINSI TIBA ZAKE ZINAVYO WASAIDIA,
(Rudisha mahusiano yako ndani ya masaa 72 tu)

SHARIFU MOHAMED Ni  mtaalam na mnajimu maarufu wa nyota na kubashiri mambo yanayo watesa binadamu duniani kote na kupata ufumbuzi, Anatumia kitabu cha QUR'AN, Dawa za Asili, Dawa za Kiarabu na majini kwa kumtuliza mke/mme, mchumba au mpenzi ndani ya masaa 72 tu, na kutatua matatizo yote ya kimaisha,

Je Umeachwa na UMPENDAE awe Mme/Mke na bado unampenda? Je Umekimbiwa na Mmeo/ Mkeo n anaishi na mtu mwingine? Je Umejaribu sehemu nyingi bila mafanikio? Mpigie simu SHARIFU SEIF sasa hivi ujionee Muujiza wa Papo kwa Papo, Anauwezo wa hali ya juu wa kusambaratisha mahusiano yao na kumrejesha kwako haraka sana na Kumfanya Atimize Ahadi zote Ndani ya Muda Mfupi Endapo Utafwata Atakacho Kuelekeza

ANAZO DAWA ZA MAPENZI, NGUVU ZA KIUME, CHANGO NGIRI MAJI NA N.K, ZINDIKO LA NYUMBA NA BIASHARA, PETE ZA BAHATI, HUMALIZA KABISA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME NA KUREFUSHA UUME KWA SAIZI UNAYOTAKA, HUZUIA CHUMA ULETE KWENYE BIASHARA, HURUDISHA MALI ZILIZOPOTEA, MAGONJWA SUGU, MIGUU KUWAKA MOTO AU KUFA GANZI, HUTIBU BUSHA BILA KUPASUA, ANAO UWEZO WA KUMRUDISHA ALIE MBALI AU ALIECHUKULIWA MSUKULE, KUPANDISHA NYOTA NA KUSHINDA BAHATI NA SIBU, KASAFISHA NYOTA NA KUKUPA MVUTO WA AJABU, KUTOA NUKSI NA VIFUNGO MBALIMBALI,  MAFANIKIO YA MAISHA NA UTAJIRI BILA MASHARI, NA MENGINE MENGI YA SIRI,

Je UMAHANGAIKA KUPATA MTOTO BILA MAFANIKIO? WASILIANA NA MTAALAMU HUYU KWANI YEYE HUFAULU PALE WOTE WALIPOSHINDWA, PIA UMALIZA KAZI ZILIZO SHINDIKANA NA WATAALAM WENGINE NDANI YA MASAA 24 TU,

(NA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA NCHI YOYOTE AU MKOA WOWOTE ENDAPO UTAFWATA MAELEKEZO YAKE)

Kwa ushauri na mawasiliano  zaidi Piga SIMU No:
Mobile +255 654-836970
WhatsApp +255 756-033670

Sakata la Lissu Mwiba...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 21

$
0
0


Sakata la Lissu Mwiba...Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 21

Mugabe adaiwa kukubali kujiuzulu kwa masharti kuwa yeye na mkewe wapewe ulinzi wa kudumu.

$
0
0
Rais Robert Mugabe amekubali kung’atuka na kwamba ameshaandaa barua ya kujiuzulu, shirika la utangazaji la CNN limeambiwa na chanzo kilichokaribu na timu ya majadiliano upande mmoja wakiwemo majenerali waliotwaa madaraka wiki iliyopita.

Chanzo hicho kimedokeza kwamba majenerali wameridhia matakwa mengi ya Mugabe ikiwa ni pamoja na kupewa kinga ya kutoshtakiwa yeye na mkewe Grace, na abaki na mali zake.

CNN limeambiwa kwamba chini ya makubaliano hayo, Mugabe na Grace hawatashtakiwa. Pia, viongozi wawili waandamizi wa serikali ya Mugabe waliliambia shirika la habari la Reuters Jumapili kwamba Mugabe alikuwa amekubali kujiuzulu lakini hawakuwa wanajua yaliyomo katika mkataba wa kuondoka kwake.

Ili ionekane amejiuzulu rasmi, utaratibu ni kwamba barua lazima iandikwe kwenda kwa Spika wa Bunge, chanzo kingine kimeongeza.

Mugabe ambaye anakabiliwa na shinikizo la kujiuzulu kutoka kila kona aliwashangaza watu Jumapili alipokataa kufanya hivyo alipolihutubia taifa kwa njia ya televisheni akiwa ikulu.

Chama chake cha Zanu PF kimempa Mugabe, ambaye amekuwa katika kizuizi cha nyumbani na jeshi lililotwaa madaraka kilimpa hadi jana mchana  kuondoka vinginevyo atashtakiwa bungeni.

Kenya Yaiandikia Barua Tanzania ikitaka Ufafanuzi Sakata la Vifaranga Vilivyochomwa Moto

$
0
0
Serikali ya Kenya imeitumia barua serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikitaka ufafanuzi kuhusu suala la vifaranga vilivyoteketezwa hivi karibuni ambavyo vinadaiwa kuingizwa nchini kutokea Kenya.

Taarifa ya serikali kupitia wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imetibitisha kupokea barua hiyo huku serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiahidi kuijibu na kuitolea ufafanuzi kama ilivyofanya mwanzo.

“Vile vile serikali imepokea barua kutoka Serikali ya Kenya kuhusu masuala haya, na Serikali itaijibu barua hiyo kutoa ufafanuzi”, imeeleza sehemu ya taarifa ya wizara juu ya ufafauzi kuhusu suala la vifaranga pamoja na mifugo iliyoingizwa nchini bila kufuata sheria.

Aidha serikali ya Tanzania imesema itaendelea kuhakikisha inafuata sheria zote bila kuathiri uhusiano wake na nchi zingine, huku ikizitaka nchi zote duniani, ikiwemo Kenya, kufuata miongozo ya WTO na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani (OIE) kwa kutoa vibali (export permit) kwa mtu yeyote anayetaka kusafirisha mifugo nje ya nchi.

Kabla ya kuteketezwa kwa Vifaranga hivyo serikali imesema Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Tanzania alimpigia simu Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo wa Kenya kutaka kujua kama Mamlaka za Kenya zina habari kuhusu vifaranga hivyo ili virudishwe lakini alisema hana taarifa kuhusu vifaranga hivyo na kwamba Kenya haiko tayari kuruhusu vifaranga hivyo kurudishwa nchini mwao.

Wananchi Walalamikia Utaratibu Mbovu Meli ya Matibabu ya Bure Kutoka China

$
0
0
Wananchi wengi wajitokeza kupata matibabu bure katika meli ya madaktari kutoka China. Baadhi walalamikia utaratibu mbovu unachangia msongamano wa watu.

Raila Odinga Apinga Uhamuzi wa Mahakama wa Kuidhinisha Ushindi wa Kenyatta

$
0
0
Raila Odinga Apinga Uhamuzi wa Mahakama wa Kuidhinisha Ushindi wa Kenyatta
Kiongozi wa muungano wa upinzani (NASA) nchini Kenya, Raila Odinga amezungumzia uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu wa kuidhinisha uchaguzi wa Uhuru Kenyatta na kudai kwamba uamuzi huo umefanywa kwa shinikizo na kwamba wao hawatambui ushindi huo.

Taarifa iliyotolewa na mshauri wake Salim Lone, amesema kuwa serikali ya Jubilee sio halali na kuongeza kwamba  uamuzi huo wa mahakama ya juu ulifanywa kupitia shinikizo.
''Sisi watu wa Nasa tayari, tulikuwa tumeamua kabla ya uamuzi wa mahakama kwamba hatuitambui serikali ya Uhuru Kenyatta. Uamuzi huo haujabadilishwa na uamuzi wa mahakama ya juu ambao haukutushangaza. Ni uamuzi uliotolewa chini ya shinikizo kubwa, hatushutumu mahakama tunaihurumia''. Lone.
Aidha Lone amedai kwamba mahakama ilikutana chini ya shinikizo kubwa, baada ya kushindwa kukutana kutokana na wasiwasi mkubwa wa kiusalama kufuatia kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa dereva wa naibu jaji mkuu kabla ya kusikizwa kwa kesi ya uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba.
Mahakama ya juu leo imeidhinisha ushindi wa Kenyatta kutokana na kura zilizopigwa Oktoba 26. Uchaguzi wa kwanza uliofanyika Agosti 8 ulifutwa na mahakama hiyo kutokana na kudaiwa kuwa batili na siyo halali.

Hoja ya Kumnyang’anya Urais Mugabe Kuwasilishwa Bungeni Leo

$
0
0
Hoja ya Kumnyang’anya Urais Mugabe Kuwasilishwa Bungeni Leo
Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.
Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang’anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg’oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 “kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba”.

Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliye uhamishoni karibuni.

Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.
Jumapili, licha ya shinikizo kubwa Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuba yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.

Rose Ndauka Awapa Makavu Wanawake Wanaotoa Mimba

$
0
0
Rose Ndauka Awapa Makavu Wanawake Wanaotoa Mimba
MSANII wa Filamu Bongo, Rose Ndauka amewarushia dongo wasichana wa kizazi kipya ambao wengi wao wakipata mimba wanakimbilia kutoa badala ya kujifungua.
Ndauka ameiambia Full Shangwe, kuwa wanawake wengi wakipata ujauzito hutoa bila kujua kuwa mtoto ni faraja ya mwanamke na uhusiano kwa ujumla. “Nawashangaa wasichana wengi ambao wakipata mimba wanakimbilia kutoa.
I wish kama wangejua furaha, faraja na thamani ya mwanamke ni mtoto, wasingefanya hivyo,” alisema. Aliongeza: “Huwezi amini furaha ya kuwa na mtoto kwa mzazi ni zaidi ya changamoto.”

Baada ya Hukumu ya Miaka Miwili ya Lulu Mama Yake Mzazi Afunguka Mazito

$
0
0
IKU tano baada ya mwanaye ambaye ni staa wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mama yake mzazi, Lucresia Karugila, kwa mara ya kwanza amefunguka baada ya mtoto wake huyo kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kumuua bila kukusudia staa mwenzake, Steven Kanumba aliyekuwa pia mwandani wake.

Awali, kulienea lawama nyingi mitandaoni baada ya Lulu kuhukumiwa kuwa huenda kuna mahali wazazi walikosea malezi ndiyo sababu ya mtoto wao huyo kujihusisha na masuala ya kimapenzi akiwa na umri wa chini ya miaka 18 ambao hakubaliki.

Kufuatia hali hiyo, Ijumaa Wikienda lilimtafuta mama Lulu ili kujua mtazamo wake juu ya mwanaye kwenda jela na madai ya mitandaoni ndipo akafunguka mazito. Mama Lulu aliliambia gazeti hili kuwa, kwa sasa hapendi kuzungumza hovyo na watu na anahitaji muda mwingi wa kupumzika kwa kuwa hayuko vizuri. “Nafikiri kwa kipindi hiki nahitaji zaidi kupumzika kwa muda mwingi na sipendi kuzungumza hovyohovyo, siko vizuri kabisa,” alisema mama Lulu kwa sauti ya unyonge.

Akiendelea kuzungumza, mama huyo alisema kuwa, tangu apate majanga ya mtoto wake huyo hadi kwenda jela hayupo vizuri na wala hapendi kuongea kwa sababu hajisikii kufanya hivyo kwani anahisi anaiona dunia chungu. “Najua watu watanishangaa sana, lakini ndiyo nimeamua kuwa hivyo, siko sawa na sijisikii vizuri kabisa. “Sidhani kama kuna mzazi yeyote anaweza kupata usingizi wakati mwanaye yupo kwenye mateso kama ilivyokuwa zamani, kiukweli ninaumia sana,” alisema mama Lulu.
DAKTARI NAYE ANENA!
Naye daktari wa magonjwa ya binadamu, Dk Godfrey Chale, akizungumzia hali ya Lulu baada ya hukumu hiyo alisema kuwa, kuna magonjwa ambayo huweza kumpata mtu mwenye matatizo ya kimaisha ikiwemo kufungwa jela ikiwa ni pamoja na kuwa kichaa kutokana na msongo.

Dk Chale alisema mara nyingi watu ambao hupatwa na majanga makubwa kama la Lulu, huwa kwenye uwezekano mkubwa wa kukumbwa na msongo ambao husababisha mpangilio mbovu wa homoni kiutendaji na mhusika kuchanganyikiwa endapo atashindwa kukubaliana na mazingira ya tatizo.
Alisema kuchanganyikiwa kwa watu wenye matatizo kama ya Lulu, hutokana na kuzidiwa na huzuni na mgandamizo wa hisia (depression) hivyo kushindwa kabisa kuzuia mfumo wa kufikiri na kutafakari na ndiyo maana unakuta mtu anaongea peke yake au kufanya vitendo vya ajabu kama kuokota vitu mbalimbali kama sehemu ya kujifariji na hapo ndipo tatizo la kuchanganyikiwa huanzia.

Tatizo kubwa jingine ambalo linaweza kumpata Lulu ni kupoteza popularity momentum (nguvu ya umaarufu) na kushuka kwa uchumi atakapomaliza kifungo kwani kwa kipindi ambacho yuko jela atapoteza mikataba yake ya kikazi kama matangazo na uigizaji, vitega uchumi ambavyo vilikuwa vikimuingizia kipato cha kuyaendesha maisha yake
Chanzo : Global Publishers

Inasikitisha Mwanamke Amwagiwa Tindikali na Mumewe Kisa Kutafuta Ajira

$
0
0
Inasikitisha Mwanamke Amwagiwa Tindikali na Mumewe Kisa Kutafuta Ajira
Mwanamke mmoja kutoka katika wilaya ya Malwani, Mumbai nchini India amejikuta akipata kilema cha kudumu baada ya kumwagiwa tindikali usoni na mumewe siku mbili baada ya kupata ajira serikalini.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Zakira Ali Sheikh (26) amesema alikatazwa na mumewe ‘Roobab Ali Sheikh’ kutafuta kazi yoyote ya kuajiriwa na kuambiwa kuwa abaki tu nyumbani kwa ajili ya kulea familia na kazi ndogo ndogo.

Mwanamke huyo wakati anasimulia kisa hicho kwenye mahojiano yake na gazeti la Hindu Times la nchini India amesema mumewe alikuwa ni fundi magari na alikuwa haachi pesa ya matumizi nyumbani kitu ambacho kilikuwa kinamuumiza kichwa jinsi ya kuendesha familia yao yenye watoto wawili.

Bi. Zakira ambaye tayari jicho lake moja limeshapata upofu amesema alishindwa kuvumilia hali hiyo ndipo alipoamua kupeleka maombi ya kazi kwenye kiwanda cha Serikali cha Sabuni baada ya kuona matangazo ya kazi.



Anasema baada ya siku mbili aliona jina lake kwenye mtandao kuwa amechaguliwa kuanza kazi kwenye kiwanda hicho ndipo alifanya taratibu zote na kuanza kazi bila kumjuza mumewe.

Hata hivyo aliona sio vyema kukaa kimya ndipo siku ya tatu alipoamua kumwambia mumewe usiku na kuanza kuambulia kipigo na kisha kumwagiwa tindikali usoni.

“Nilipiga makelele usiku ule kwa muda wa dakika 10 lakini hakuna jirani aliyekuja kuniokoa hadi baadae kaka yangu alipokuja kuniokoa, niliumia sana nilijiona kama nakufa.“amesema Bi. Zakira .

Jeshi la polisi mjini Mumbai limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limesema tukio hilo limetokea tarehe 14 Novemba mwaka huu na tayari mtuhumiwa amekamatwa kwa mahojiano zaidi.

Kwa sasa mwanamke huyo anatibiwa katika hospitali ya Mumbai nchini humo na amewekewa mipira ya kupumulia ambapo anahitaji msaada wa Euro 29,090 sawa na Tsh milioni 76 ili aweze kukamilisha upasuaji.

Tayari mashirika binafsi yameshajitolea kumsaidia mwanamke huyo likiwemo shirika la ‘Make Love Not Scars’ kwa kumshangia dola $11,0000.

Simba, Yanga Kutumia Uwanja wa Azam Complex

$
0
0
Simba, Yanga Kutumia Uwanja wa Azam Complex
Mechi za wikiendi hii za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara zinazozihusu Simba na Yanga zitachezwa Uwanja wa Azam FC Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

Hiyo inafuatia uwanja wa Uhuru kuwa na matumizi mengine ya kijamii na wakati huo huo, Uwanja wa Taifa bado haujaruhusiwa kwa matumizi kufuatia ukarabati wa eneo la kuchezea.
Yanga watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya Jumamosi wakati Simba wataikaribisha Lipuli ya Iringa Jumapili katika michezo ya Ligi Kuu raundi ya 11.

Taarifa kutoka bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imesema kwamba kwa sababu hiyo mechi hizo zimepelekwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Baada ya mechi 10 za awali, Simba SC wapo kileleni kwa pointi 22, sawa na Azam FC wanaokaa nafasi ya pili kwa kuzidiwa wastani wa mabao, wakati mabingwa watetezi, Yanga SC wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 20.

Chadema Yaonya Msafara Nyalandu Kupigwa Mabomu

$
0
0
Chadema Yaonya Msafara Nyalandu Kupigwa Mabomu
SIKU moja baada ya msafara wa viongozi wake wakuu kupigwa mabomu na Jeshi la Polisi jijini Mwanza, Chadema kimeonya kuwa tabia hiyo ikiachwa iendelee bila kukemewa, itakuwa na athari kubwa kwa nchi.

Juzi, polisi jijini Mwanza walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliokuwa wanasindikiza msafara wa viongozi wakuu waliokuwa na mwanachama mpya Lazaro Nyalandu.

Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii kukabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa Chadema kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Mhandu wilayani Nyamagana jijini humo.

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana akiwa jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alisema chama chake kinasikitishwa na matukio ya viongozi na wafuasi wake kupigwa mabomu na Jeshi la Polisi bila sababu za msingi.

Alisema tabia hiyo inapaswa kukemewa kwa maslahi ya ustawi wa jamii na ukuaji wa demokrasia nchini.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, alisema wanasikitishwa na tabia hiyo inayoendelea kujengeka ya vyombo vya usalama kusababisha vurugu kwenye mikusanyiko ya Chadema.

Alidai viongozi wanapopita njiani na wananchi kuwasimamisha ili wawasalimie ni kitu cha kawaida kwa kuwa hata misafara ya viongozi wakuu wa nchi imekuwa ikisimamishwa na wananchi barabarani na wamezungumza nao na kusikiliza kero zao.

Alisema hali imekuwa tofauti kwenye mikusanyiko na misafara ya Chadema ambayo wananchi wamekuwa wakikumbana na kipigo hata kama hawajasababisha jambo lolote linalokiuka sheria na taratibu za nchi.

"Jana (juzi) Mwanza walipiga mabomu," Mbowe alisema, "wamepiga mabomu kwa Mheshimiwa (John) Mnyika (Kibamba, Dar es Salaam), wamepiga mabomu Momba (jimboni kwa David Silinde - Chadema).

"Wame-arrest' (wamekamata) vijana wetu, wamepiga vijana wetu, wanawaumiza bila sababu, wameharibu magari ya chama. Hili jambo si la kulifumbia macho. Ni tabia ambayo imezidi kujengeka miongoni mwa vyombo vya dola."

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro, alisema viongozi lazima waikatae kwa kuwa inaweza kuipeleka nchi kubaya.

"Sasa tunasema siasa zifanyike kistaarabu, unaposhangiliwa wewe na wenzako wanaweza kushangiliwa vilevile," Mbowe alisema na kueleza zaidi:

"Hali kadhalika, unapozomewa wewe, na wenzako wanaweza kuzomewa vilevile. Sasa haiwezekani Misafara ya CCM ikisimamishwa
na wananchi wakiwapongeza, polisi wanalinda lakini Chadema wakisimamishwa na wananchi kutaka kusalimiana na viongozi, wanapigwa mabomu bila sababu ya msingi.

"Unapiga mabomu wananchi ambao wamekusanyika kwenye mkutano, hawana ugomvi na mtu. Sasa kushangilia kwao vyama vya upinzani linakuwa tatizo?"

Mbowe alidai kuwa CCM wanapaswa kutambua kwamba hawawezi kubadili fikra na kugeuza mawazo ya wananchi ambao wameamua kuunga mkono Chadema na kuiamini kwa kuwapiga mabomu na kuwaumiza viongozi wake.

"Nawaambia tu CCM kwamba huu mchezo wa siasa wawaache wananchi waucheze, wawaache wananchi waamue, ndiyo maana ya 'freedom' (uhuru), ndiyo maana ya uhuru, ndiyo maana ya demokrasia," alisema.

"Serikali au CCM haviwezi kuanza kuwaona wananchi kama wabaya pale wanapoanza kuviunga mkono vyama vya upinzani.

"Jana (juzi) Mwanza polisi wametumia nguvu kubwa ambayo haikuwa na sababu, wamepiga wananchi mabomu, msafara wetu ulipigwa mabomu. Mimi mwenyewe nilikuwapo, Mheshimiwa Nyalandu nilikuwa naye gari moja na Mheshimiwa (Godbless) Lema
(Mbunge wa Arusha Mjini).

"Tulipigwa mabomu bila sababu ya msingi. Wananchi wakaanza kutawanywa, polisi wengine wakaanza kupiga virungu wananchi, jambo hili ni baya na litapelekea uhusiano mbaya na kujenga chuki katika jamii."

Mbowe alisema wanaendelea na kampeni za uchaguzi huo mdogo wakiwa na Nyalandu mkoani Arusha.

Kichuya Afunguka Kuhusu Mkataba Wake wa Simba

$
0
0
Kichuya Afunguka Kuhusu Mkataba Wake wa Simba
HUKU mkataba wake ukiwa unaelekea ukingoni, winga wa vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Shiza Kichuya, amesema bado hajafikia uamuzi wa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo kwa sababu ya kuangalia maslahi kwanza.

Simba inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, ilimsajili Kichuya Julai mwaka jana akitokea Mtibwa Sugar na kumpa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza na Nipashe jana, Kichuya, alisema bado yeye na meneja wake hawajafikia uamuzi wa kusaini klabu yoyote mpaka sasa kwa sababu wanataka kuona mkataba mpya unakuwa na maslahi bora kuliko alichokuwa anapata sasa.

Kichuya alisema yeye atakuwa tayari kusaini mkataba ambao utamridhisha bila kujali klabu itakayomvutia iwe ya ndani au nje ya Tanzania.

"Bado sijafanya uamuzi wowote kuhusu kusaini mkataba mpya, nitamsikiliza meneja wangu kile ambacho ataniamulia," alisema kwa kifupi nyota huyo anayevaa jezi namba 25 mgongoni.

Hata hivyo, Kichuya hakuwa tayari kueleza kama anajiona tayari ameiva na anafaa kwenda kupambana kucheza soka la kulipwa kama ilivyo ndoto ya wachezaji wengi wa Tanzania baada ya kung'ara kwenye ligi ya nyumbani.

"Siwezi kusema lolote juu ya ofa za nje, akili yangu ni kuendelea kupambana na kusubiri kile atakachoniamulia meneja wangu," alimaliza Kichuya.

Moja ya maslahi ambayo Kichuya anataka yaboreshwe ni mshahara.

"Anafanya kazi kubwa sana, ni lazima Simba imuangalie kwa jicho linalostahili, endapo watamboreshea maslahi yake, nina hakika atasaini mkataba mpya bila shaka na akipata "dili" la nje atakwenda," kilisema chanzo chetu.

Taarifa kutoka Simba zimeeleza kuwa zipo klabu mbili za Misri zinazomhitaji Kichuya na zinasubiri akikataa kusaini tena Msimbazi zimnase kirahisi akiwa mchezaji huru.


Breaking News:Jengo la Studio za Clouds Media Group Linaungua Moto

$
0
0
Sehemu ya jengo la kituo cha Chouds Media Group linaungua moto muda huu. Juhudi za kuuzima moto huo bado zinaendelea.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images