Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

HITILAFU: Abiria 48 wa PrecisionAir Wanusurika

$
0
0


Ndege ya Shirika la PrecisionAir iliyokuwa imeruka kwa safari zake kutoka Mwanza kwenda Nairobi nchini Kenya kupitia Kilimanjaro jana, imelazimika kutua kwa dharura baada ya kupata hitilafu ikiwa angani.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege hiyo namba 5H-PWC ATR 72, zilieleza kuwa tayari walikuwa wameruka lakini baada ya muda mfupi waliambiwa hawawezi kuendelea na safari kutokana na ndege kupata hitilafu.

Baada ya kuruka, ndege ilitaka kukunja magurudumu kwa ndani ikashindikana hali iliyomlazimisha rubani kuzunguka eneo la uwanja huo, huku akijaribu kuyarudisha bila mafanikio na kuamua kutua kwa dharura.

Alisema abiria 48 waliokuwa kwenye ndege hiyo hadi jana saa 12:00 jioni walikuwa wanasubiri nyingine ili kuendelea na safari.

Akizungumza kwa simu Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, Ester Madale alisema hitilafu hiyo ilikuwa ya kawaida hivyo haikuwa na madhara.

Madale alisema iliruka saa 7:54 mchana kwenda Kilimanjaro, lakini baada ya kuruka magurudumu yalishindwa kujikunja kurudi ndani hivyo rubani alijaribu kuyarudisha ikashindikana, hivyo akalazimika kutua kwa dharura.

“Hitilafu hiyo ni ya kawaida, wahandisi wetu waliangalia hitilafu hiyo na saa 9:15 alasiri walifanya majaribio kuirusha na imetua, hivyo siyo tatizo kubwa la kawaida,” alisema Madale.

Matukio ya karibuni

Desemba 13, mwaka jana ndege ya PrecisionAir aina ya ATR 42-600 ilipasuka magurudumu  manne ya nyuma wakati ikitua uwanja wa KIA, miongoni mwa abiria waliokuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa.

Julai 24, 2012 ndege ya shirika la Precision Air magurudumu yalipasuka wakati ikitua Uwanja wa Ndege mkoani Kigoma.


Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Kinara wa Madawa ya Kulevya Zanzibar Akamatwa Uwanja wa Ndege na Kilo 5000 za Unga

$
0
0
Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata Ali Suleiman Rashid (34) akiwa na mikoba 14 ya wanawake aliyohifadhia dawa za kulevya zenye uzito wa kilo tano akitokea Oman katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume visiwani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Mkuu ya Polisi Ziwani mjini Zanzibar, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI ), Yussuf Ilembo alisema kuwa mtuhumiwa huyo raia wa Tanzania  amekamatwa muda mfupi baada ya kushuka kutoka Ndege ya Oman yenye namba za usajili .WY.717 iliyokuwa ikitokea Muscat.

Ilembo alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Julai 9,  saa 8 mchana akiwa amehifadhi mikoba hiyo katika sanduku kubwa lenye rangi nyeusi na maofisa wa upelelezi waligundua ndani yake kuwemo mikoba 14 iliyokuwa na dawa hizo ikiwa imeshonewa kwa vitu maalumu.

“Dawa hizo  za kulevya zina uzito wa kilo 5.605, zilihifadhiwa kwenye mikoba 14 inayotumiwa na wanawake. Upelelezi kukamilika, atafikishwa mahakamani mara moja,” alisema DCI Ilembo.

Alisema polisi inaendelea na uchunguzi wake ili kusaka mtandao wa watu wanaojishughulisha na vitendo hivyo kwa kuchunguza njia mbalimbali za mawasiliano za mtuhumiwa huyo aliyekamatwa.

Kwa mujibu wa polisi,  mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia hati ya kusafiria namba AB 363906 iliotolewa Desemba 29 mwaka 2009 Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji Dar es Salaam na tayari  ameshasafiri katika nchi za Brazil, China, Japan, Hong Kong, Afrika Kusini na Falme za Kiarabu.

Ilembo aliwataka wananchi kuchukua hatua kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kuwafichua kwa siri, wanaoingiza dawa za kulevya na wauzaji ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

‘Wakati wa kulindana, kuleana na kuoneana aibu umekwisha, kila mmoja ajione ana wajibu wa kulilinda taifa kwa maisha yake na vizazi vijavyo,”alisema DCI Ilembo.

Mapema mwaka huu polisi walikamata mabegi mawili yakiwa na dawa za kuelvya katika chumba cha kuondokea abiria, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light”

Uchaguzi wa washiriki wa Big Brother: Siri iliyofichuka nyuma ya story ya Dida na Mume wake

$
0
0
Nimeangalia video iliyowekwa mitandaoni inayomuonesha Yule aliekuwa mume wa Dida akihojiwa sababu za kuachana na mke wake.

Kuna hiki kitu amekitaja kimenivutia kdogo nidadisi
" Kwamba Mult choice walikuwa wanamuandaa Dida kuwa mshiriki wa mwaka huu? Tena kabla ya mchakato rasmi kuanza??

Je hivi ndivyo ina vyokuwaga au ??
Na Jee ile Interview ya Tarehe 11 Jul ni Kanya Boya? Mshindi Alishachaguliwa?

Mpoki atangaza vita na Shigongo & Joseph Shaluwa wa GPL

$
0
0
Katika wimbo wake mpya alio mshirikisha Ben Paul. Mpoki anasikika akisema maneno yafuatayo :


" WATU WA BONGO MOVIE, WALA MSILALAMIKE KUPOROMOKA KWA MAUZO YA KAZI ZENU, KWANI ANAYE WACHAFUA NI MSUKUMA WA BAMAGA NA NYIE MNAMJUA, NA NYIE HAO HAO NDIO MNAO MUENDEKEZA.

NA NDIO MAANA NILIWA AMBIA SISOMI MAGAZETI YA UDAKU MKANIONA CHIZI,
NA SASA HIVI UKINIAMBIA NIMTAJE MUANDISHI BORA WA KIKE, MI NTAMTAJA DADA SHALUWA "

TUSUBIRI SHIGONGO ATA RESPOND VIPI, BUT UZOEFU UNAONYESHA KUWA SHIGONGO HUWA HARSPOND BEEF ZA WASANII, MWAKA 2004 DUDUBAYA ALIMDISS VIBAYA SANA SHIGONGO KUPITIA CHANNEL TEN, 3 DAYS LATER DUDU ALIWEKWA NDANI KWA KOSA LA KUMPIGA MR. NICE, SHIGONGO HUYO HUYO AKAENDA KUMTOA, NA INASEMEKANA ALIKAA NAE KAMA MDOGO WAKE, WAKAYAMALIZA NA KUENDELEA NA MAISHA KAMA KAWAIDA.

Nifanyeje Mat'ako' Yasitingishike Nitembeapo?

$
0
0
Mimi ni Binti wa Miaka 21 kwa sasa , Naandika hili kuwaomba wadau ushauri..ombo langu kidogo lina utata hasa maeneo ya makalio ki ufupi nimejaliwa sana sijisifii ..Pamoja na Kujaliwa huko nimekuwa napata shida sana ninapokuwa naenda mahali kutembea ama chuoni kwani maungo yangu ya nyuma hutikisika sana kiasi kwamba huamsha hisia za wapita njia za zingine mpaka napigiwa miluzi njiani na kushangiliwa kitu ambacho sikipendi kwa sasa mpaka nimepunguza mizunguko kwa ajili hiyo ..Je nifanyanye ili yasitingishike nitembeapo ?

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Penzi ni Kikohozi Alifichiki...Huyo Ndio Mwanaume Mpya wa Jack Wolper

$
0
0
Mambo yametoka huko INSTAGRAM....Calisah ambaye ni Model aliewhi kushiriki shindano la Mr Tanzania (2013-2014)  na kushika nafasi ya 4...ameamua kuweka wazi uhusiano wake wakimapenzi na mwanadada  Wolper..japokuwa kwaupande wake Wolper hajasema chochote hadi sasa hivi.

He posted Wolper’s photo and captioned;

" words can't explain how much u mean to me, u the 1 I lv and am not gona let u go... thnx for keepin ma love alive,promis to lv u mo and take good care ov u, umenifanya nisitamani mwanamke yeyote mwingine cz I get evrythn from u, I lv uuu & wil keep lovin u #kamdoli kangu. #kichuna changu, #myHAPPINES. #maBLOOD. @wolpergambe"

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Dayna Nyange Aeleza Uamuzi Aliouchukua Baada ya Kukutana na Changamoto za Kujichubua

$
0
0
  Mwimbaji wa kike Dayna Nyange azungumzia jinsi alivyokutana na changamoto nyingi baada ya kuamua kubadili rangi ngozi yake na kuwa nyeupe.

Akiongea katika The Jump Off ya 100.5 Times Fm, Dayna ameeleza kuwa amekuwa akisolewa na watu wengi huku wengine wakitumia lugha mbaya dhidi yake lakini yeye ameipokea vizuri kwa kuwa anaamini ni watu wanaompenda.

“Ni sawa kwa sababu mimi naamini ni watu wangu wa karibu na ni watu ambao wananipenda ndio maana wanakuwa wanasema japo wengine wanatumia kauli mbaya. Lakini pia ni sawa kwa sababu mimi najua hao ni binadamu na kila binadamu anajua jinsi ya kupresent kwa mtu vile ambavyo anajisikia kwa hiyo ni mimi kutumia tu akili nakipokeaje.” Amesema Dayna Nyange.

Ameeleza kuwa yeye anaamini hakuna kitu ambacho aliwahi kukifanya kabla kikawa gumzo au tatizo kwa watu na ndio maana watu wanaamua kulichukulia hili kama tatizo kubwa.

Mwimbaji huyo alitangaza uamuzi aliouchukua kufuatia changamoto hizo alizokutana nazo ingawa anaamini kila mtu anauhuru wa kufanya maamuzi kama alivyoamua yeye.

“Kwa hiyo mimi naweza kusema ni sawa, inawezekana kweli nimekosa. Lakini mimi kama binadamu pia nina maamuzi yangu na nina sababu nyingi tu za kufanya kile ninachokifanya. Japo nimesikia maneno mengi sana mpaka Lol..’nimeacha.!

“Siwezi kusema kuwa nimeacha kabisa lakini nimetoka kule nilikokuwa, sasa hivi narudi kuwa Dayna yule ambaye mnataka awe. Japo pia binadamu pia mnakitu kimoja, sifieni kile kilicho bora kabla hakijakuwa sio.” Ameaongeza.


Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

Mama Diamond 'Wanawake Wengi Wanajitongozesha Kwa Diamond, Wanatuma Mpaka Picha za Uchi Kwenye Number ya Simu ya Biashara

$
0
0

Mama mzazi wa star anayeipeperusha vizuri bendera ya Tanzania kimataifa kwa sasa kupitia muziki, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz jana (July 11) alipata nafasi ya kuzungumza na Watanzania kupitia kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM, mambo mbalimbali yanayomhusu mwanaye.

Moja ya Swali aliloulizwa ni hili hapa:


Na hii tabia ya mara (msichana) huyu mara huyu wewe ukiwa kama mama kwako huo unaipokea vipi?


Jibu:
"Na hii tabia ya mara (msichana) huyu mara huyu wewe ukiwa kama mama kwako huo unaipokea vipi?
“ Siipokei vizuri laikini sasa nitafanya nini nay eye star, wengine wanajitongozesha bila kutongozwa..mi mwenyewe hapa kutwa napigiwa simu mpaka nazima, wananipigia simu wanafikiria Nasib wanajitongozesha mpaka nawatumia meseji mbona mnajitongozesha, hii sio namba ya Nasib hii namba katoa ya biashara ya Tshirt 0716186318 sio namba ya Diamond, namba yake mama yake.sitaki usumbufu..wananitumia mapicha ya uchi , mapicha ya nini sasa ni ustarabu gani huo”

Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.


Dr Dre ashitaki Makampuni ya kichina yaliyoingiza $ Billion 135 kwa kuuza headphones fake za 'Beatz By Dre'

$
0
0
Dr Dre na Jimmy Lovin ambao wanaendelea kushangilia kuwa mabilionea baada ya kuwauzia Apple kampuni yao ya Beatz Electronics kwa $ Billion 3 tu, wamepata mshituko baada ya kugundua kuwa Makampuni ya kichina yameingiza pesa hiyo zaidi ya mara 40 kwa kuuuza headphones fake za ‘Beatz By Dre’.

Kwa mujibu wa TMZ, makampuni mengi ya China yamegundulika kuwa yalikuwa yanatengeneza headphones zenye logo ya Beats na kuuza kwa bei nafuu dunia nzima kwa njia ya mtandao wakitumia tovuti mbalimbali.

Dr Dre amekasirishwa na hatua hiyo na amefungua mashtaka dhidi ya makampuni hayo na kitu cha kwanza alichoiomba mahakama ni kuhakikisha kwanza wanachukua majina ya ‘domain’ za tovuti zote zinazofanya biashara hiyo na pia kuhakikisha faida zote zinazopatikana kwenye mauzo hayo.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

Neymar Atokwa na Machozi Asema Amemsamehe Aliyemuumiza, Asema Ilibaki Kidogo Apate Kilema cha Maisha

$
0
0
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa timu ya taifa ya Brazil, Neymar da Silva Santos Júnior amejikuta akibugujikwa na machozi, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya hali yake mara baada ya kupata majeraha ya mgongo mwishoni mwa juma lililopita.

Neymar amekutana na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu aliporuhusiwa kutoka hospitalini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu ya kufuatia jeraha la mgongo ambalo liliwashtua mashabiki wengi wanaozifuatilia fainali za kombe la dunia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amesema alikuwa hatarini kupoza, kutokana na kubainika wazi kwamba endapo Juan Zuniga angemjeruhi sentimita chache kwenda chini angepata kilema cha maisha.

Mshambuliaji huyo aliyefunga mabao manne kabla ya kuumia wakati wa mchezo wa hatua ya robo fainali dhidi ya Colombia, pia amesema beki wa The Coffers, Juan Zuniga amempigia simu na kumuomba radhi kwa kumfanyia rafu mgongoni kwenye mchezo huo.

Wakati akizungumzia suala hilo Neymar akijikuta akibugujikwa na machozi

"Zuniga alinipigia simu siku chache baadaye kuniomba msamaha na kuniambia kwamba hakudhamiria kuniumiza," amesema Neymar. "Nimeukubali msamaha huu, lakini siwezi kulichukulia lile kama tukio la kawaida. Siwezi hata kusema lilikuwa tukio la makusudi, lakini kila mmoja anafahamu haikuwa kawaida. Namna alivyokuja, nyuma yangu, nisingeweza kujitetea.

"Namshukuru Mungu kanisaidia, kwa sababu kama pigo lile lingezama ndani kwa inch chache, ningeweza kupooza,"amesema Neymar huku akibubujikwa na machozi.

Neymar amesema hajui nini tatizo hadi Brazil ikafungwa 7-1 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali na Ujerumani.

"Kilichotokea hakikutarajiwa. Lakini hata walipokuwa nyuma kwa 6-0, 7-0, hawakukata tamaa, waliendelea kukimbia, kuendelea kujaribu.

Sioni aibu kuwa Mbrazil, sioni aibu kuwa sehemu ya timu hii.

Ninajivunia kila mmoja katika wachezaji wenzangu,"amesema.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

UKATILI! Wasichana 7 wafariki dunia baada ya kubakwa na kuchomekwa Chupa sehemu zao za Siri

$
0
0
Wasichana saba wamepoteza maisha wilayani Nachingwea mkoani Lindi baada ya kubakwa na kunyongwa kisha kuwekewa vijiti na chupa kwenye sehemu zao za siri.

Wasichana hao wamepoteza maisha kwa nyakati tofauti katika kipindi cha miezi minne iliyopita na wamekuwa wakipigiwa simu nyakati za usiku na kukutana na waliowapigia simu ambapo hubakwa na kunyongwa na kisha katika sehemu za siri kuwekewa vijiti au chupa.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila amebainisha aina hiyo ya mauaji  jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine.

Mwananzila alikuwa amekwenda hospitalini hapo kuwatazama majeruhi ambapo alifafanua kuwa mauaji hayo yanaendelea na juzi mtu mwingine aliuawa katika mazingira hayo.

Alisema, “serikali ya wilaya ilishatoa namba za simu kuwa unapopigiwa simu mtoto wa kike fanya juhudi kumjulisha mwenzako au piga simu kituo cha polisi ili kuweza kukabiliana na watu hao wanaotoa roho za watu”.

Mwananzila alisema kuwa binti mmoja aliweza kupigiwa simu na kundi hilo, aliamua kupiga simu kituo cha polisi na kuweka mtego baada yeye kutoka nje, polisi walikuwa wameshazingira maeneo hayo na wauaji wale walimfuata ndipo huyo binti alianza kuvutana nao na hatimaye Polisi  waliwatia mbaroni watu hao.

Mkuu huyo wa mkoa aliwaonya mabinti hao na kusema: “ni makosa kwa wasichana kutoka nje baada ya kupigiwa …

“kinachotakiwa kwanza mjulishe mwenzako, lakini unafanya siri madhara yataweza kukutokea, hususani watoto wa kike”.

Alisema mauaji hayo yana ishara ya imani ya kishirikina. Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika.

Alisema suala hilo liko ndani ya uchunguzi hivyo ni vizuri kufanyia kazi kwanza na kuwataka wananchi wawe na subira.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

UKATILI: Mtoto Afichwa Uvunguni kwa Miaka 6 Huko Morogoro

$
0
0
Wakati jamii ikiwa bado haijasahau mateso aliyoyapata mtoto Nasra Mvungi na kusababisha  kifo chake, tukio lingine la aina hiyo limetokea katika Kijiji cha Matongola, Tarafa ya Magole Wilaya ya Kilosa, baada ya kubainika mtoto wa miaka sita akiwa amefichwa uvunguni mwa kitanda na kufanyiwa vitendo vya kikatili na mama yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa za mateso ya mtoto huyo zilifikishwa Kituo cha Polisi wilayani Kilosa  saa za mchana jana, baada ya uongozi wa  kijiji na kata kutoa taarifa na tayari mwanamke huyo amekamatwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Mama aliyefanya ukatili huo anafahamika kwa jina la Sala Mazengo ambaye alimficha ndani mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Devota Malole na kumfanyia vitendo vya kikatili ikiwa pamoja na kutompa chakula, wala kumfanyia usafi.

Baada ya kufichuliwa kutoka alipofichwa, mtoto huyo alionekana kuwa dhaifu kiafya kutokana na kukosa lishe pamoja na mazingira aliyokuwa akiishi kutoridhisha, jambo ambalo ni kosa kisheria, pia ukiukwaji wa haki za watoto.

Inadaiwa kuwa tangu mwaka 2009 Sala amekuwa akimficha mtoto wake huyo ambaye sasa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa kwa ajili ya kupatiwa vipimo na matibabu.

Hata hivyo, mwanamke huyo alipoulizwa alidai kuwa afya ya mtoto wake ilikuwa mbaya tangu alipozaliwa kutokana na magonjwa ya mara kwa mara, pia hali ngumu ya maisha ilichangia kudhoofisha afya ya mtoto huyo.

Alidai kuwa ana watoto sita, pia alikiri kumlaza chini mtoto huyo kutokana na kuwa na kitanda kimoja, ambacho hakiwatoshi watoto hao.

Aliongeza kuwa hata chakula amekuwa akikipata kwa shida kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa kuwa ana mtoto mwingine mdogo.

Kamanda Paulo alisema kuwa  mwili wa mtoto huyo umedhoofu kutokana na kufichwa ndani kwa muda mrefu na bado mwanamke huyo hajaeleza sababu za kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto huyo.

“Siwezi kutoa taarifa ya kidaktari, lakini kutokana na afya ya mtoto yule na mazingira tuliyomkuta ni dhahiri alikuwa akipata mateso na kufanyiwa vitendo vya ukatili. Hata hivyo, uchunguzi zaidi tunaufanya na kwamba taratibu za kumfikisha mtuhumiwa huyo Kituo Kikuu cha Polisi mkoani hapa zinaendelea,” alisema Kamanda Paulo.

Alisema kuwa mpaka sasa bado haijafahamika kama mtoto Davota ni mlemavu au la na kwamba taarifa za afya ya mtoto huyo zitatolewa baada ya madaktari kumfanyia uchunguzi wa kina.

Quote of The Day:
Happiness is not something you postpone for the future; it is something you design for the present.

Kauli ya Mwisho ya Ballali Kabla ya Kifo Chake

$
0
0
Dar na Marekani. Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania BOT), Marehemu Daudi Ballali aliacha wasia unaotaka maiti yake isionyeshwe hadharani atakapofariki dunia na wala maiti yake isiletwe Tanzania kwa ajili ya maziko.

Ballali aliyefariki Mei 16, 2008 na kuzikwa Mei 23 mwaka huohuo katika makaburi ya Gate of Heaven, eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani alifahamu kuhusu kifo chake wiki mbili kabla, baada ya matibabu kushindikana.

Mwandishi wa Mwananchi aliyekuwa nchini Marekani kwa siku kumi kufuatilia suala hilo, alibaini kuwa kiongozi huyo alilazwa mara ya pili katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha George Washington, April 2008 na alirejea nyumbani kwake, Washington DC wiki mbili kabla ya kukutwa na mauti.

Habari kutoka ndani ya familia yake zinasema baada ya madaktari kushindwa kumtibu walimwambia kwamba asingeweza kuishi kwa zaidi ya wiki mbili, hivyo walimshauri ahamie kwenye ‘hospice’ ambayo ni nyumba maalumu ya kusubiri kifo kwa watu ambao magonjwa yao yameshindikana.

Hospice hutumika kwa ajili ya kuwaweka wagonjwa wanaohitaji faraja hasa kutoka na maumivu makali chini ya uangalizi wa washauri na wauguzi kwa lengo la kuwaongezea wagonjwa husika siku za kuishi.

Baadhi ya hospice hutoa huduma za kiroho, kijamii na kifedha na wakati mwingine huduma hizo hutolewa kwa wagonjwa ambao wanaugulia nyumbani. Hata hivyo, gazeti hili lilidokezwa kwamba Ballali alikataa kwenda kwenye nyumba hiyo na badala yake kutaka apelekwe nyumbani kwake.

“Alikataa kwenda kwenye hospice, aliwaambia madaktari kwamba yeye hawezi kwenda huko ijapokuwa kuna huduma nzuri na uangalizi wa nesi (muuguzi). Aliwaambia kwamba nitakwenda kufia nyumbani kwangu maana nina nyumbani kwangu,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Aliporejeshwa nyumbani, alikuwa anazungumza kama kawaida lakini kadri siku zilivyosogea hali ilikuwa ikibadilika na kama sikosei siku mbili au tatu za mwisho (za uhai wake) alikuwa anajitambua lakini alikata kauli, hakuwa akizungumza chochote”.

Uchunguzi wetu umebaini kuwa katika siku hizo za mwisho za uhai wake, Ballali aliacha maelekezo kwamba pindi atakapofariki dunia, mwili wake usiwekwe hadharani kwa maana ya kutazamwa na watu nje ya familia wala kusafirishwa kuja Tanzania kwa ajili ya maziko.

“He said, he doesn’t like to be turned into a laughing staff (alisema asingependa kugeuzwa kichekesho), sababu watu wasingekuja kutoa heshima za mwisho, bali wangekuja kumdhihaki kuangalia Ballali aliyetuhumiwa kwa ufisadi wa EPA na siyo Gavana,” kilisema chanzo hicho.

Sumaye: Nitagombea urais 2015

$
0
0
Hatimaye Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambaye kwa muda mrefu amekuwa akitajwa kuwania urais amethibitisha rasmi kuwa atagombea kwenye uchaguzi mkuu mwakani.

Kiongozi huyo aliweka wazi nia ya kuelekea Ikulu wakati alipokuwa akihojiwa na Radio Deutsche Welle (DW) ya Ujerumani jana mchana na hivyo kuwa kiongozi wa pili kutangaza nia kupitia vyombo vya habari vya kimataifa.

Julai 3, mwaka huu, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba alitangaza nia ya kuwania urais baada ya kuhojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) alipokuwa amekwenda huko kuhudhuria mkutano wa sekta ya mawasiliano.

Akifafanua kwa nini anataka kuwa rais, January alisema kuwa huu ni wakati wa fikra mpya kushika dola na kwamba anaamini muda wa wazee kukaa kando umefika.

Sumaye ambaye aliwahi kugusia suala hilo kwa kusema kuwa angeweza kugombea kwenye kinyang’anyiro kijacho kama wananchi wangetaka afanye hivyo sasa ametegua kitendawili kwa kusema kuwa yuko tayari kuwania nafasi hiyo.

“Maana siyo kila mtu anayejaza kutaka kwenda kugombea. Ni watu wamemtaka na wapo wengi tu ambao wanajaza kwa sababu wametaka wenyewe eeh! Kwa hiyo kama watu wakinitaka nitagombea kwa nini nisigombee, nitagombea na ninafikiria nitagombea,” alisema.

Hata hivyo, alionyesha kutishwa na kiwango cha rushwa katika mchakato wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu kwa kusema kuwa:

“Ukweli ni kwamba matumizi ya fedha ndiyo yamekuwa makubwa sana na kwa kiwango fulani Watanzania wanadhani, siwezi kuwamo. Watanzania ni wale ambao wana nafasi ya kuchagua na wanadhani kama hawajapata fedha basi huyo ambaye hajatoa fedha anaonekana kama hachaguliki.

“Ukweli ni kwamba ni jambo la hatari na lazima tulipige vita katika nchi yetu. Matumaini yangu ni kwamba viongozi wetu waliopo watajitahidi kupiga vita,” alisema Sumaye.

Pia kiongozi huyo alikosa baadhi ya watu wanaosema wakati wa kuwa na rais kijana umefika kwa kusema kuwa umri hauwezi kuwa kigezo pekee cha kumpata rais.

“Kama kuna kijana hata kama ana miaka 41 ambaye anadhani anafaa na umma unadhani anafaa si kwa sababu ni kijana hakuna tatizo, mradi asiwe anakwenda pale kwa kusema mimi ni kijana ninayefaa. Unaweza kusema kila kijana anafaa kuongoza hii nchi? Haiwezekani” alihoji.

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa Januari 1 mwaka huu alitangaza ‘kiaina’ kuwania nafasi ya urais kwa kusema kwamba anaanza safari ya matumaini.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Aibu Kubwa:Wabongo Wafumaniana China, Wazichapa Bara barani na Kuvuana Nguo

$
0
0
Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja

Ni aibu kubwa kwa taifa! Huku Waislamu wakiendelea na Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, warembo wawili, raia wa Tanzania (Wabongo), mmoja mkazi wa Sinza, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Glory na mwingine ambaye jina halikupatikana, wanadaiwa kufumaniana laivu nchini China na kugeuka kituko cha aina yake, Ijumaa Wikienda ndilo lenye uthubutu wa kuripoti tukio hilo.

Habari za awali zilidai kuwa Glory ndiye aliyemfuma mwenzake na bwana’ke, raia wa Nigeria kisha kumshushia kipigo kabla ya kutoana nje na kwenda kuchaniana nguo barabarani, mchana kweupe.

OFM KUTOKA GUANGZHOU, CHINA
Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mwakilishi wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers nchini China (jina kapuni), alisema kuwa akiwa katika pitapita zake za kukusanya matukio ili kuyatuma Bongo kuonesha jinsi gani Wabongo wanavyoidhalilisha nchi yao ughaibuni, wikiendi iliyopita alitembelea eneo la Guangzhou Rujing Lu Sky Coffee nchini humo ambalo Watanzania wengi hufanyia ‘biashara’ zao.

Mwakilishi huyo wa OFM alisema akiwa eneo hilo linalosifika kwa matukio na starehe za kichumbani ndipo alipokumbana na timbwili hilo ambalo linaichafua taswira ya Wabongo ambao wanakwenda China kuchukua biashara mbalimbali.

NI AIBU KUBWA
“Dah! Hii ni aibu kubwa ambayo sijawahi kutegemea kuwa nitakutana nayo, yaani Wabongo kwa Wabongo wanapigana, wanachaniana nguo na kuumizana kisa bwana wa Kinigeria, tena ughaibuni!” Alisema kwa masikitiko mwakilishi huyo wa OFM nchini China.

Akiendelea kufunguka, OFM alisema kwamba ilisemekana kuwa Mnigeria huyo aliwahi kuwa na uhusiano na Glory hivyo siku ya tukio, jamaa alimtosa Glory na ‘kuchepuka’ na mwenziye.

KIPIGO CHA MBWA MWIZI
Ilielezwa kwamba Glory hakukubali ndipo akamuanzishia timbwili mwezake na kumpa kipigo cha mbwa mwizi akimtuhumu kwa nini amemchukulia bwana’ke.

WASABABISHA FOLENI
Katika timbwili hilo, warembo hao walijikuta wakichaniana nguo na kubaki nusu utupu huku wakirushiana matusi ya nguoni (hayaandikiki gazetini kimaadili).
Wakati wakipigana waliingia barabarani na kusababisha bonge la foleni huku wakinusurika kukanyagwa na magari hasa walipoangushana katikati ya barabara.

POLISI WAITWA
Kuna wakati Glory alimkaba mwenzake hadi mashuhuda wa sinema hiyo ya bure wakahisi anamuua mwenzake hivyo kulazimika kuita polisi wa usalama barabarani ambaye alifika mara moja na kuwaamulia.
Ilisemekana kwamba, askari huyo alipoona hawaelewani lugha ndipo akawaachia huku kila mmoja akichukua hamsini zake.

GLORY ANASEMAJE?
Baada ya kupata taarifa hizo, Ijumaa Wikienda lilifanya jitihada za kumtafuta Glory kwa njia ya simu yake ya kiganjani lakini hakupokea na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kuhusiana na tukio hilo, licha ya kuonekana umemfikia (delivered) hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea.



YATOKANAYO
Kumekuwa na wimbi la warembo ambao huenda nchini China kwa kisingizio cha kwenda kuchukua biashara lakini ukweli ni kwamba huenda kufanya mambo mengine mabaya (hasa biashara haramu ya kuuza miili).

Mbali na ukahaba, wapo wanaodaiwa kufanywa punda wa kubeba madawa ya kulevya na matokeo yake ni kuishia kunyongwa mara wanapokamatwa.
Hata hivyo, baadhi ya Wabongo waliozungumza na gazeti hili kutoka China, waliziomba mamlaka husika kushughulikia suala hilo hasa wanapotoa vibali vya kutoka nje ya nchi wajue mhusika anakwenda kufanya nini.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Shilole Adaiwa Kukataliwa Ukwenu..Kisha Umri

$
0
0
Stori: Jamila Said na Emelder Tarimo

Haijakaa poa! Habari zinadai kwamba baadhi ya ndugu wa msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda ambao ni wakwe wa staa wa muziki na filamu za Kibongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ hawamtaki kwa madai kuwa ana umri mkubwa kuliko ndugu yao.

Wakizungumza na Ijumaa Wikienda kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanandugu hao (majina yanahifadhiwa) walisema umri wa Shilole siyo wa kuishi na ndugu yao, Mziwanda kwani hawaendani.
“Ukweli ni kwamba mapenzi hayaingiliwi lakini tunaumia kuona ndugu yetu katika penzi zito na Shilole ambaye hawaendani kiumri,” alidai mmoja wa ndugu hao.
GPL

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Aunt Ezekiel:Sina Gundu na Wanaume Mimi, Watu Wanaongea tu Bila Kujua ukweli

$
0
0
GUNDU? Baada ya kudaiwa kuwa na gundu kufuatia kila mwanaume anayeishi naye kuandamwa na majanga, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ameibuka na kukanusha madai hayo akisema hayana ukweli.

Baada ya maneno hayo kutua katika dawati la Ijumaa Wikienda, wanahabari wetu walimsaka Aunt ili kumsikia anazungumziaje taarifa hizo ambapo alitiririka:
“Sina gundu na wanaume jamani, uzuri ni kwamba kila niliyeishi naye kulikuwa na sababu za msingi za kuachana. Siyo Jack Pemba wala Hartmann (Mbilinyi).

“Watu wanazungumza tu bila kujua ukweli, hata kwa Sunday Demonte (mumewe wa sasa), yupo vizuri na hajafungwa kama wanavyosema,” alisema Aunt. 
Miongoni mwa wanaume walioogelea katika penzi la Aunt kisha kumwagana kwa sababu tofuati ni pamoja na Mwilu Mwilola ‘Silvanus’, Hartman na Jack Pemba.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Full time ya Ujerumani vs Argentina, Tuzo za Wanasoka Bora wa Michuano

$
0
0
Baada ya mwezi mmoja hatimae michuano ya kombe la dunia imemalizika nchini Brazil ambapo mechi ya fainali iliwakutanisha Ujerumani vs Argentina jijini Rio de Janeiro kwenye uwanja wa Maracana.
Ushindi ni wa Ujerumani wa goli moja tu lililofungwa ndani ya dakika 30 za nyongeza baada ya full time kuwa 0-0 na mfungaji alikua Mario Gotze aliesababisha Ujerumani kuchukua ubingwa wake wa nne wa dunia.
Unaambiwa pia hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Ulaya kuchukua ubingwa wa dunia kwenye ardhi ya Amerika ambapo pia kwenye sentensi nyingine, tuzo ya mchezaji bora wa mashindano imeenda kwa Lionel Messi, mfungaji bora James Rodriguez, kipa bora Manuel Neur na mwanasoka bora chipukizi wa mashindano amechukua Paul Pogba.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Sikuwahi Kufikiria Naweza Kufanya Mapenzi na Mtu Nisiye Mjua Tena kwenye Basi

$
0
0
Nilikuwa Siamini Ule msemo wa Wazungu unaosema Love at the First Sight , ila yaliyonikuta mwenzenu acheni tu..
Mimi ni Msichana wa Miaka 25 Ilikuwa Week iliyopita nikiwa Safarini naenda Mwanza kutokea Dar Kuripoti kazini Baada ya kupata kazi mpya huko, Nikiwa Kwenye basi pembeni yangu nilikaa na Kaka mtanashati na mchangamfu toka tumetoka Ubungo Terminal kaka wa watu alikuwa akinipigisha stories mbali mbali kiasi niliona kama safari fupi , ki ukweli nilipenda uchangamfu wake ,Mambo yalianza tulivyofika Shinganya muda kama wa saa tatu usiku tukiwa sasa tunaelekea Mwanza , Pale Shinyanga waliteremka watu wengi kidogo kiasi Kwenye Basi Upande wa Nyuma tuliokuwa tumekaa Sisi hapakuwa na watu bali mimi na huyu mkaka..Na Kigiza kile yule kaka alianza kunishika mkono wangu nilisisimka balaa mpaka sikumbuki ilikuwaje tukajikuta tunakiss na kuanza mambo mengine ya kikubwa humo humo kwenye basi ..Kwa vile ilikuwa giza hakuna aliyeshtukia , Ki ukweli nilienjoy sana..Sintasahau ...Yule kaka Baada ya Kufika Mwanza alinipa Namba ya Simu ila Nimejaribu sana Haipatikani ....Sijui nifanyaje Natamani kumuona Tena ...

UPDATE: Hali ya Mtoto Devota Malole aliyefichwa Uvunguni kwa Miaka 5 yazidi kuwa Mbaya

$
0
0
Mtoto Devota Malole aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa kufuatia mama yake kumtesa kwa kumfungia ndani na kumlaza chini kwa muda wa miaka mitano amehamishiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya afya yake kiafya kubadilika.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya kilosa Dr Shedrack Mponzi amesema wamelazimika kumuhamishia mtoto huyo katika hospital ya rufaa ya mkoa wa Morogoro baada ya hali yake kuwa mbaya na uchunguzi wa awali umebaini anamagonjwa mbalimbali ikiwemo utapia mlo kwa kukosa lishe ambapo katika hospitali ya mkoa wa morogoro waandishi wetu wameshuhudia madaktari wakifanya kila juhudi za vipimo na matibabu

Wasamaria wema wamejitokeza katika hospitali ya mkoa wa Morogoro kumjulia hali mtoto Devota ambapo mbunge wa jimbo la Morogoro Abdul Azizi Abood amewataka maafisa ustawi wa jamii kuacha kulala na badala yake watekeleze wajibu wao ipasavyo kuwasaidia watoto wanaoteseka .

Nae mfanyabiashara wa kampuni ya mabasi ya Alsaidi Omari Alsaidy ameahidi kugharamia matibabu ya mtoto huyo hata kama italazimika kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu ili kunusuru maisha yake.

Quote of The Day:
“You can't depend on your eyes when your imagination is out of focus.” 

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images