Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

FIFA yaipiga marufuku Nigeria kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa

$
0
0
Shirikisho la soka duniani (FIFA ) limeipiga marufuku Nigeria kushiriki mashindano yeyote ya kandanda yanayoandaliwa na shirikisho la soka duniani FIFA.

Hatua hii imeafikiwa baada ya maafisa wa serikali kuwaondoa wasimamizi wa shirikisho la soka nchini Nigeria NFF afisini.
Marufuku hii inamaanisha hakuna klabu yeyoye ya soka nchini Nigeria inaweza kushiriki mashindano yeyote ya Kimataifa.

FIFA ilikuwa imeionya Nigeria kuwa ingeichukulia hatua ifikiapo Jumanne kama Shirikisho la NFF halijarejeshewa madaraka yao lakini Serikali ikapuuza makataa hayo.

Mwishoni mwa juma Serikali ya Nigeria ilikuwa imemteua afisa mshikilizi kuongoza shirikisho hilo hadi uchaguzi wa huru na wa haki utakapofanyika kulingana na taarifa ya wizara ya michezo.

FIFA katika taarifa imeonya kuwa marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo maafisa waliochaguliwa watarejeshwa mamlakani.
Marufuku hiyo itaathiri timu ya taifa ya Super Eaglets ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 ambayo inapaswa kushiriki mchuano wa kombe la dunia iwapo marufuku hiyo haitaondolewa ifikapo juma lijalo.(Julai15)

Msemaji wa serikali hata hivyo alisema kuwa hatua iliyochukuliwa dhidi ya NFF ilifuata kanuni kwani hata kiongozi wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari alikamatwa na polisi punde baada ya kurejea nyumbani kutoka Brazil.

Mahakama ya Nigeria ilikuwa imeamua kuwa Maigiri hakuwa anastahili kuendelea kuiongoza NFF haswa baada ya matokeo duni huko Brazil.

Wajumbe wa NFF waliafiki kauli ya mahakama ya kumn’goa mwenyekiti huo madarakani lakini lakini kwa sasa erikali ya Nigeria inasubiri mawasiliano kutoka FIFA baada ya kutuma ithibati ya mkutano maalum uliofanyika na wajumbe wa shirikisho la soka la NFF

Source:BBC

Diamond atoa sababu za kuwatumia wazungu kwenye video ya ‘Mdogo mdogo’

$
0
0
Kumekuwa na maoni tofauti kuhusiana na video ya ‘Mdogo mdogo’ ya Diamond Platnumz iliyotoka Jumatatu ya wiki hii. Wapo ambao wamefurahishwa na story iliyoko kwenye video hiyo na wengine ambao hawajaiunga mkono moja kwa moja kutokana na kila mmoja kuwa na sababu tofauti hali ambayo imeleta mabishano mengi katika comments za youtube na kwingine.

Lakini inawezekana wengi ama wote hatujui maana halisi ya story iliyoko kwenye video hiyo na sababu za Diamond na timu yake kuamua kuifanya hivyo ilivyo.

Diamond amefunguka jinsi story ya video hiyo ilivyozaliwa na script kuandikwa:

Ujumbe ulikuwa kwamba mapenzi yanakuwa hayachagui rangi wala kabila na kuutoa ubaguzi kama mtoto flani labda muhindi hawezi kuolewa na mswahili au mzungu, mswahili hawezi kumuoa muhindi au mzungu au mchina no no no…haya ni mapenzi na wote mkiridhiana yaendane yakubalike tu. So hiyo ilikuwa message, lakini pia nikaamua kuifanya kisehemu mbili tofauti tofauti ili pia kutokupoteza culture halisi ya kitanzania. Ndio maana utaona kuna character moja ndo naigiza mimi kijijini kabisa kama Tarzan yaani kama mtu wa kijijini kabisa halafu yule ndio mtoto wa mfalme ambaye ndio ananipenda mimi hapa.” Amesema Diamond kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM.

Diamond pia amemtaja director maarufu wa bongo movie marehemu Adam Kuambiana kuwa ndiye mtu aliyeleta wazo la script iliyotumika kwenye video hiyo na baadae kuongezewa chachandu na mpenzi wake Wema Sepetu.

“Script wakati inaanza kwanza nilikuwa sasa mimi nataka kufanya kitu flani lakini nilikuwa sijui nakianzaje…so nakumbuka that time Adam Kuambiana alikuwa anadirect movie ya kina baby nilikua naenda kambini nakutana naye, na baby aliniambia ni mzuri sana, nikamfata nikamwambia bana na wimbo wangu nataka uniandikie story …akasema basi itakua vizuri nikifika studio na nuiisikilize….akaskiliza ngoma akawa ananipa namna story inavyotakiwa kuanza kwenda. So naweza kusema mwanzoni wakati story inavyoanza picha hata ya kuipata story ni Kuambiana ndo alinipaso baada ya hapo mi nikaenda nikakaa nayo nyumbani mi na baby tukakaa baby nikamwambia Kuambiana katoa wazo kama hili unaona tulifanyeje, so tukakaa unajua baby nae master katika maswala ya movie movie, so akakaa akawa anaiandika hapa iwe hivi aah isiwe hivi hapa iwe hivi, baada ya kumaliza kuiandika akaichora katika lugha ngeni tukaituma kwa director akaitazama na akaipitisha.”


Platnumz ameongeza kuwa video hiyo imemgharimu dola elfu 32 pamoja na gharama za kusafiri yeye na timu yake hadi Afrika Kusini.

Wema Afunika Instagram Aweka Picha Akiwa na Mama Mkwe Wake na Kuandika Maneno ya Choko Choko

$
0
0
 Siku ya Birthday ya Mama Diamond Wema Alikuwa na Kazi ya Kupost Picha tu Insta Akiwa na Mama Mkwe Wake ambapo alipost Picha zaidi ya 20...Hongera Wema kwa Kumpenda Mama Mke ila Isije ikawa ya Muda Mfupi kesho tukasikia Mengine...Maana Tumeambiwa Movie Bado linaendelea

Mchekeshaji Mpoki Atoa Wimbo Mpya Akimshirikisha Ben Pol ..Sikiliza Hapa

$
0
0
Mchekeshaji Maaarufu Mpoki ameachia ngoma Mpya akimshirikisha Ben Pol ngoma inaitwa “Umiza Kichwa” Poroducer ni Lamar

Quote of The Day: I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Baba Kanumba Afunguka 'Mama Kanumba Tafadhali Acha Njaa'

$
0
0
BABA wa aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Bongo, marehemu Steven Kanumba, Charles Kanumba ameibuka na kumtaka mama Kanumba, Flora Mtegoa kuacha tabia ya kuombaomba michango mbalimbali.

Akipiga stori na paparazi wetu, Baba Kanumba alisema anashangazwa na tabia ya mama Kanumba kuombaomba ambapo hivi karibuni alimuona mjini Shinyanga ambako alikuwa akiomba rambirambi kwenye kumbi za starehe.

“Namshangaa mama Kanumba ni njaa gani hiyo, naomba aache kudhalilisha ukoo wa Kanumba kwani anatumia jina hilo kuombaomba, anahangaika bila sababu za msingi wakati sisi tuko vizuri,” alisema Baba Kanumba.

Akijibu tuhuma hizo, mama Kanumba alisema kama ana malalamiko yoyote aende mahakamani maana yeye si mume wake. “Aache kunifuatafuata kwani mimi si mkewe na Shinyanga nilialikwa kwenye Miss Shinyanga siyo kwamba nilijiendea tu,” alisema.

Quote of The Day:
I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Amanda Mwigizaji wa Bongo Movies Afunguka Sababu za yeye Kutokuzaa Mpaka Sasa

$
0
0
Na Gladness Mallya
STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona mwanaume wa kuwa baba watoto wake.
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila anashukuru kwa sasa amempata.

“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.

Quote of The Day:
I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.


Flora Lymo'Wafanyakazi wa Ubalozi UK ni Wanafiki Wanafanya Kazi Viongozi Wakija UK Tu' Atoa Ombi

$
0
0
Ndugu zangu Watazania wenzangu ''kwanza Huu ni Mwezi mtukufu wa Ramadan kwa wale wenzetu Waislam '' napenda kuwatakieni Ramadan Njema''
Mimi hapa ninayo machache ''juu ya huu mualiko wa kukutana na Waziri wetu Mkuu Mh.Pinda'' Nadhani wengi wenu mnanifaham vizuri sana hasa kwangu Mimi kuipenda Nchi yangu na kujihusisha kwenye Mikutano au chochote kinachoihusu Nchi yangu au niseme Watanzania wenzangu''
Lakini Tangu Habari zangu kutangazwa wazi na gazeti moja maafuru kule Nyumbani Tanzania kuhusu Mimi kubakwa na Godbless Lema Mbunge wa Arusha '' Wengi wenu mlianza kunitenga ,kunidharau ,kutokunishirikisha kwenye Shughuli zenu za Watanzania na Vile vile kunizuia hata ninapokuja kama Watanzania wengine kuhudhuria mikutano yenu kama huu wa sasa hivi wakukutana na Waziri wetu Mkuu 'Ubalozini ''
Yani Wanaofanya kazi mle au niseme pia Viongozi hao Wanakuwa na chuki zao juu yangu na maisha yangu 'mbali na kilichotukutanisha pale na vile vile kazi yao waliyo pewa''
MNAMO MWEZI WA NANE MWAKA 2013
Waziri mkuu Mh.Pinda akiambatana na Mkewe walikuwepo hapa jijini London na kulikuwa na mkutano Ubalozini wa Watanzania waishio UK kukutana nae'' Mimi sikuwa na habari hizo '' Ila Dula langu kwa bahati nzuri lipo karibu na Ubalozi wa Tanzania UK House''
Na nilipomaliza kazi nikawa najiendea zangu kukutana na Rafiki yangu ambae nae alikuwa in Town '' Nikakuta watu wengi wengi wamesimama Nnje ya Ubalozini ''Ndipo nikapitia kuuliza kuna nini ? Yani huwa siyo kawaida kuona Watu wengi pale ''Mimi hupapita Kila siku'' Nikauliza na nikaambiwa ni Waziri wetu Mkuu yupo hapa leo '' Basi nikampigia Rafiki yangu sim nikamuambia anisubiri nataka na mimi nimuone Waziri wangu Mkuu labda anaweza kunisaidi matatizo yangu '' Basi nikaingia ndani na kukuta ndiyo wapo karibu kumaliza'' Nikakaa pale na kusikiliza vya mwisho mwisho ''Wakamaliza na kuanza kwenda kupiga Picha za Pamoja'' Lakini Kwa sababu nilichelewa basi nikaona isiwe Tabu wacha niongee na Mama Penda'' Nilipotaka kuongea na Mama Pinda nilianza kuburutwa naanza kuambiwa yani hata kupiga Picha ya pamoja sikubaliwi ? kwanini ? Hata sikuelezwa sababu hizo ''Lakini kwli Ninavyojikubali hasa pale Mtu ananinyima haki yangu ''walahii pale nilipawasha moto ''mliokuwepo I think mnakumbuka what happen on last time'' Hizo Picha hapo Chini mtaona Mimi na Waziri Mkuu na Mke wake  kwenye Picha ya Pamoja ''ni baada ya kukataliwa kupiga Picha ya pamoja nikiwa nao kule ndani Ubalozini kama Wenzangu '' Basi nikajua Tatizo lao lilikuwa ni kunikataza nisiseme kwa Waziri kwamba nilibakwa na Godbless Lema'' Wajua nini ? I was this is it'' na mwambia wazi hapa hapa mbele zenu wote'' wakaanza kunivuta na kusema muda umekwisha'' Basi nikamshikilia waziri mkuu'' Kwa Heshima yako Baba yangu ''Mheshimiwa Waziri wangu naomba unisikilize ''Mimi nilibakwa na Godbless Lema 'Na hakuna Mtu anaetaka kunisikiliza na ndiyo sababu unaona wananikataza hata nisipige picha ya pamoja na wewe'' Yani unajua maana ya Kimnya'' Basi watu wote walikaa kimnya na kushangaa''Huku Waziri mkuu akinisikiliza na hakuenda tena Popote 'Yani wale waliokuwa wanamkimbiza kwamba Muda umekwisha''walitamani kujitia vitanzi'' Thats is Maana ya Kiongozi anae faa'' MHESHIMIWA WAZIRI PINDA'' MWINGINE HAKUNA'' YANI ALINISIKILIZA NA AKATOA AMRI KWAMBA'' KESI CHANGU ANAKIKABIDHI AMOS MSANJILA'' WA UBALOZINI ANISIKILIZE NA AMPE MAELEZO YOTE KUHUSU KESI CHANGU ''YEYE ATAKWENDA TANZANIA KUFUATILIA ZAIDI''
 Basi Mheshimiwa akaondoka na Mkewe na wakaniachia Hope wakaniacha na furaha hata hiyo picha unaona tunacheka sana ni baada ya kumaliza kumuelezea kuhusu kwangu Mimi kubakwa na watu wote unaowaona Pichani hapo na wengine wenggi hawapo pichani walisikia kila kitu ''na Mariam Mungula nae ndipo akaja kuniambia Pole pale adharani like hajawahi kusikia na wao ni Watu wa CCM tena Viongozi ambao Godbless Lema anadai ndio walionituma mimi kwenye Mkutano wake wa Chadema in London mnamo mwezi wa nane mwaka 2012'' na ADHABU YAKE NI KUNI BAKA'' Ndiyo maana nasema hivi''

WATANZANIA WALIOKO UBALOZINI NA VIONOZI WOTE WA VYAMA VYOTE NI WANAFIKI NA UKIWA NA MATATIZO HAWAKUSAIDII NA HATA WAKIAMBIWA WAKUSAIDIE WATAITIKA NA VIONGOZI WETU WAKISHA RUDI TANZNAIA NI BASI ''UTAZUNGUSHWA MPAKA UTAMANI KUJITIA KITANZI'' ALAFU BILA AIBU VIONGOZI WANAPOKUJA WANA ANZA KUWAITA WATANZANIA WAISHIO UK ''LIKE WANAWAJUA '' YANI HAKUNA ANAE KUJUA KAMA WEWE NI MTANZANIA UNAE ISHI HAPA UK ''
KWA SHIDA AU HATA KWA RAHA''
 UNAFANYA KABIASHARA CHAKO HUWEZI KUSIKIA HATA MTU AKINYANYUA HIYO SIM KAMA KIONGOZI NA MTANZANIA MWENYE KUTAKA MAENDELEO YA WATANZANIA WENZAKE ''KUKUPIGA SIM HATA KUKUPONGEZA'' AU BASI TUSEME WAFANYE MIKUTANO YA WATANZANIA WAISHI UK TUKUTANE KWA KUJUANA NA KAMA MTU ANA SHIDA TUJUE TUMSIKIZE NA TUTAMSAIDIA VIPI 'KWANINI MSIFANYE HIYO MIKUTANO YA KUWAJUA WATANZANIA WAISHIO UK NA SHIDA ZAO MBALI MBALI '' WENGINE TUNATAKA KUWASAIDIA NA WENZETU KULE NYUMBANI LAKINI TUNASHINDWA KWA UTARATIBU ULIOPO TANZANIA KWA BIDHAA ZINAZOTOKA UK '' NASEMA UK KWA SABABU Mimi MWENYEWE NATUMA BIDHAA KUTOKA UK KWENDA TANZANIA NA USHURU UTAKAO TOZWA BANDARINI NI NOMAA'''
 KWANINI ZANZIBAR HAWANA MATATIZO NA BIDHAA ZINAZOTOKA UK ? YANI MIMI SASA NAANZA KUHAMIA ZANZIBAR '' IKIWA TUNA PATA HUDUMA ZISIZO NA RUSHWA  SIONI KWANINI WATU TUSIANZE KUHAMIA ZANZIBAR ''SIYO BURE HATA HAWA VIONGOZI WETU HAWANA HABARI NA HIVI VITU NA NDIYO  MAANA WANAPO KUJA HAPA UK 'KUKUTANA NA WATANZANIA WAKAWAIDA WAISHIO HAPA UK ''WATU TUNANYIMWA KUTOA DUKU DUKU ZETU'' NA NDIYO MAANA MIMI HAWATANIONA TENA KWENYE MIKUTANO YAO '' NA WALA HAWANISAIDII KWA CHOCHOTE NA HATA MIMI SIJAWAONA WAKIWASAIDIA WATANZANIA WENZAO KWA CHOCHOTE'' WE NEED KUJIPANGA UPYA ''KWA MIKUTANO YETU KABLA YA KUWASHIRIKISHA VIONGOZI WETU '' HII MNAFANYA KUJIFUNIKA ILI VIAONGOZI WETU WAJUE MNAFANYA KAZI ZENU VYEMA WAKATI HAMFANYI ''TENA WENGI WENU MMECHEPUKA HATARI NA KWENYE BLOG YA FLORA LYIMO MMEIFANYA OFISI ZENU'' KAMA HUJAIFANYA OFISI ''ULIZIPENDAJE PICHA ZANGU ZA CHUPI NA KUANZA KUNIULIZA NI SHILINGI NGAPI ? NAOMBA UNIJIBU AMOS MSANJILA'' NA PILI NAOMBA UNIJIBU TANGU MHESHIMIWA ALIPOKUPA KAZI YAKUNISIKILIZA KESI CHANGU NA GODBLESS LEMA ''UMEFANYA NINI MPAKA SASA HIVI ? NA NI KWANINI MIMI NIKUULIZE IKIWA UMESHASIKIA CHOCHOTE KUTOKA KWA WAZIRI ''ALAFU UNANIPIGA CHINI NA KUNIAMBIA NIANZA KUMTAFUTA MIMI MWENYEWE? SI WEWE ULIPEWA HIYO KAZI TENA LIVE WATU WAKIWA WANASIKIA ? SASA LEO UNATAKA NIJE TENA HAPO UBALOZINI NIANZE KUBURUTANA NA NYIE? SASA NAKUAMBIA SITAKUJA NA WAZIRI MKUU NITAMSUBIRIA APO MLANGONI ''MBUTA NANGA'' MNANISIKIA TU'' MIMI NAISHI KWA SASA HIVI NIKIWA NA HASIRA SANA ''NI VILE HAMJUI LAKINI SIKU ZIKILIPUKA ZA KICHAGGA 100% NDIO WALE MNAO NIITA CHIZI MTAONA UCHIZI WANGU'' JAMANI NI HAYO TU'' MIMI NA HASIRA ZANGU HAPA NA NA SEMA HIVI''
MSIENDE HUU UKUTANO NI WAKUFUNIKA BOVU''SASA WEWE KAMA NI TEAM FUNUA BOVU aka TEAM FLORA LYIMO MAENDELEO '' USIENDE'' WAACHE WAKAE NA WAZIRI MKUU WENYEWE WAMUELEZEE NI KWANINI WATANZANIA HAWAJAENDA? ?? I THINK HAPO WAZIRI MKUU MH.PINDA ATAPATA PICHA KAMILI '' HAWASIKILIZI WATANZANIA NA MATATIZO YAO '' WAKATI HAMPO MHESHIMIWA WAZIRI NA MHESHIMIWA RAIS WETU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA'' WE NEED YOUR HELP '' BAADHI YA VIONGOZI MNAOWATEUA NI MICHEPUKO ,WASHINDA MITANDAONI (BLOGS SEXY ) KAMA ZA FLORA LYIMO FASHION POLICE BLOG, NA WANAFIKI WAKUBWA''
NIMEMALIZA MWENYESHIDA ANIPIGIE SIM '07787471024 AU WHATSAPP +44 7787471024 EMAIL :flo1974@btinternet.com
PIA NAOMBA KUSEMA HIVII'' SAY NO TO RAPE NA UNYANYASAJI '' KWA WANAWAKE NA HATA WANAUME ''
FLORA LYIMO ''

Source:Flora Lyimo Blog

Quote of The Day:
I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Mabinti Msio Ndani ya Ndoa, Ndoa Nyingi za Matajiri ni Utata Mtupu Msihadaike!

$
0
0
Mabinti walio wengi hutamani sana kupata wenzi wao wa maishay aani waume wenye uwezo mkubwa kifedha,yaani mume ambaye ana nyumba nzuri tayari,gari la kutembelea na mazagazaga mengine kibao yanayoonyehsha maisha ya kifahari na starehe. 

Lakini nyuma ya pazia kuna mambo wasiyoyajua yanayowapata wake wa matajiri ambao kwa nje wanaonekana wenye furaha wanaishi vizuri na wanafurahia maisha wala hawana shida yeyote. 

Inaweza ikawa hivyo kwa nje lakini kihalisi kuna mambo ambayo walio wengi hawafahamu hutokea kwenye ndoa za matajiri na hivyo mabinti wengi kuwa na ndoto za kuishi kitajiri na kufanya bidii kupata mume wa ainahiyo na kisha kuvunjika moyo mara baada ya kukutana na hali halisi:je wajua kuwa:

1.Wake wengi wa matajiri wana magari mengi ndani ya nyumbalakini huenda hajui hata ndani yake panafananaje zaidi ya kuyashika kwa nje tuau kuyaona tu yale pale yamepakiwa?

2.Maneno ya kumsimanga mtu kama vile unajua gahrama ya hivivitu wewe,?au ulivionea wapi hivi vitu wewe,unayajulia wapi haya mambo,vyakula hivi,kwenu uliviona ?na mengine mengi ni ya kugusa?

3.Wake wengi wa matajiri hawana nafasi ya kuhoji mumeanashinda wapi na nani,majibu yanayotolewa hapo,:unafikiri haya maisha unayoishi hapa yanakuja tu hivihivi,unafikir tukikaa kuangaliana sura utaviona vyote hivi?

4.Wanaume wengi matajiri hawaishi masimango kama vile unishukurumimi bila mimi usingekuwa hapo ulipo wala watu wasingekutambua,ulikuwa na ninicha maana,nimekutoa ukiwa huna mbele wala nyuma(hata kama kwa kweli alikukutaunajiweza kwa kiasi Fulani)

5.Wanaume wengi matajiri hawana nafasi ya kuonyeshaupendo,kukaa na kuwajali wake zao,mara nyingi wako bize na shuhguli zao na hatamke akiomba walau apate nafasi ya kukaa na mume waongee mawili matatu,mumeanajibu huli,huvai unalala chini?hayo ndo majibu.

6.Mara nyingi wake za matajiri hawashirikishwi kikamili auhata kidogo kwenye shughuli zinazowaingizia waume zao utajiri huowalionao,pengine hata kama mume ana kazi basi mke kamwe hawezi jua mapato yamume wake kwa mwezi yakoje.
Jamani mabinti hayo ni machache tu yaliyo nyuma ya pazia kwenyenyumba za matajiri walio wengi.

Kwa hiyo tahadhari kwa mabinti usitamani sana kumpata mumetajiri kwa kujua kuwa ndo furaha ya maisha, japo sio vibaya kupata mume anayejiweza, tena ni vizuri zaidi kuolewa na mume mwenye uchungu wa maisha na malengo yabaadaye ya maisha yenu na watoto wenu. 

Mbaya ni hii tamaa waliyonayo mabinti wengi ya kutaka kuolewa na mume tajiri sio ndoto nzuri sana,mengiyamejificha na kwa kuwa kuta haziongei ndo basi tena mume na mke matajiriwakitoka wameshikana mikono,tabasamu pana unadhani wameyamaliza maisha kumbeni ni siri ya kuta za nyumba zao.

Quote of The Day:

I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Maamuzi Gani Nichukue Dhidi ya Ndoa Yangu?

$
0
0
Mimi ni mama wa watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita, mwanzo kabisa maisha yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo, first of all niliwahi kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya hapo niliishi maisha ya tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza kujitambua.

Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na mwanaume niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndio atakayenifuta machozi na huzuni zangu.

Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya mahusiano yetu alienda oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata mawasiliano kabisa. Nilibaki na kovu na maumivu niliyokosa tiba. Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua kumove on na maisha yangu,ingawa ilikuwa ni ngumu sana.

Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye sikujua kama ni kweli nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa namuwaza X wangu aliyeniacha bila kusema neno lolote.

Mwanaume huyu mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na mkorofi kwa watu dakika mbili alishabadirika haeleweki kama kinyonga ,police kwake ilikuwa ni kama nyumbani.

Nyimbo zake mara nyingi zilikuwa ni za kina Tupac ,Snopy D na wale aina ya magang star Ingawa alikuwa msomi na kazi nzuri,na maisha yake mpaka sasa bado miziki yake ndio hiyo ,starehe kwake hataki kuacha wala kupunguza.

Niliamini atabadilika ingawa nilikuwa nakwazika sana kuwa nae alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa mnywaji mzuri na ili niwe nae Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio nakuwa huru na hayo ndio yakawa maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano ya muda mrefu hatimaye nilianza kumzoealakini si kumpenda ,

Tukiwa tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana kuanza kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi lakini kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwa akiniacha na kurudi usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku hadi siku.

Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baada ya kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua kabisa mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa najiuliza kwanini nafunga ndoa? 

Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama najifosi kufanya. Tulifunga ndoa takatifu nakuanza kuishi kama mke na mme ,na mungu akatujaalia kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini system yangu ni mpaka ninywe ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme wangu.

Ndani ya ndoa yangu nimekuwa nikiishi kwa kujifanya nampenda mme wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa nikilia na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake of my kids ndio napata faraja kidogo.

Kila siku zinavyoenda nazidi kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi mpaka lini nifanye nini ili nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa usingizi usiku kucha.
Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu unazidi kuwa mnyonge 

Nisaidieni juu ya hili 
By Ndoa Yangu JF

Quote of The Day:

I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

FLora Lyimo Aendelea Kumuanika Le mutuz "Mwanaume Mzima Unashindana na Wanawake Mutandaoni"

$
0
0
SASA WACHA NIKUFUE NA NIKUANIKE NNJE NA 360 NA OLE WAKO USIPOKAUKA,MAANA NITAENDELEA KUKUANIKA MPAKA UTAKAPO KAUKA MBWA WA SOKONI USOJIJUA'' WEWE APO KULIA PICHANI 'LEMUTZ aka LEMUTUMBAZ'
NI HIVI''' Kwa hiyo hapo umeamka na ulikuwa umelala na hilo kama dira vile'' kweli lijizeeshoga huwezi kukosa kulijua'' hapa huwezi danganya Wanaume wenye kuamcha mashine zao na kukobolea wanawake bidhaa zao kila siku 'yani uwadanganye wale mashoga wenzako ambao mashine zao zimeshalegea kama hiyo ya kwako ilolegea kama mlenda ulokosa maji''Yani mwanaume mzima unashindana na wanawake mitandaoni hadi kujipiga picha za uongo eti umeamka hivi na kupiga picha hii kwa hiyo na wao waamke asubuhi kujipiga picha waweke mitandaoni kama wewe ? una ona kweli hilo ni jambo la kuwaelimisha wanawake au wanaume wenzako ? yani badala waamke na kwenda kazini kuwahi dala dala na pia ofisini au sokoni kuuza bidhaa zao wao waje kuuza sura mitandaoni tena sura za kujificha ujinsia wao ?Yani hapa ndiyo umeonyesha jamii wazi how stupid idiot you are na hizo degree zako za uongo ''pumbavu na omba Mungu nimepata huu muda wakukujibu hapa Leo ''maana Instagram inakutosha mpaka utahama huko na hii Dunia kwa ujumla'''wewe shindana na Flora Lyimo the top in town ''alafu tuone'' sasa nasubiria picha zako kama hizi za kwangu ''ukiwa umevaa UNDERPANTS'' YANI UKIWA UMEVAA HIZO CHUPI ZANGU KUBWA ZA KIUME'' MAANA HATA FASHION HUJUI ''ETI HIZI CHUPI NILIZO VAA HAPA NI ZA KIUME''MBUTA NANGA!!

Quote of The Day:
I hope everyone that is reading this is having a really good day. And if you are not, just know that in every new minute that passes you have an opportunity to change that.

Mwanamke Aliyemng’ata Hausigeli na kumchoma Pasi Aachiwa

$
0
0
Mtuhumiwa wa kesi ya kujeruhi kwa kumng’ata sehemu mbalimbali za mwili  mfanyakazi wa ndani, inayomkabili Amina Maige (42) amepatiwa dhamana jana baada  ya mahakama kuthibitisha kuwa hasira kutoka kwa wananchi zimepungua.

Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Yohana Yongolo alisema ameridhishwa na ufafanuzi uliotolewa na Mwendesha mashitaka wa Serikali pamoja na Wakili wa mshitakiwa kuwa haki ya dhamana itolewe kwa kufuata masharti na kwamba hakuna uhalifu wowote utakaofanyika dhidi ya mshitakiwa huyo.

Hakimu  Yongolo alitoa masharti ya dhamana ambayo yalimtaka Maige kutoondoka nje ya Dar es salaam bila ya ruhusa ya mahakama hiyo.


Pia alitoa masharti ya kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa kutoka taasisi inayotambulika hapa nchini ambapo mdhamini huyo anaweza kuwa mwajiriwa, mfanya biashara na mkulima.

Alisema wadhamini hao watatakiwa kusaini hati ya makubaliano kwa kila mmoja kulipa Sh milioni tatu.

Aliongeza kuwa kesi hiyo itasikilizwa Julai 22 mwaka huu.

Maige alidaiwa Januari mwaka jana hadi Juni mwaka huu, alimng’ata na kumchoma na  pasi  sehemu mbalimbali za mwili wa  mfanyakazi waje wa ndani Yusta Kashinde (20) na kumsababishia maumivu mwilini.

Hatimaye Penny Aliyekuwa Mchumba wa Diamond Avalishwa Pete ya Uchumba

$
0
0


Mtangazaji maarufu nchini VJ Penny ambaye alikuwa mpenzi wa Diamond Platnumz amechumbiwa.  Kupitia Instagram Penny ameweka picha akiwa amevaa pete ya uchumba  na  kuandika  ujumbe  huu: “Road trip ….site her we come…cc @halimakimwana1.”

Pia juzi  tulisikia   kuwa Penny amechumbiwa ingawa hatukupata habari kwa kina mpaka Penny mwenyewe alipoweka picha Instagram  akiwa  amevaa  pete  ya  Uchumba.
VJ Penny ambaye  inadaiwa alikuwa chaguo la kwanza la mama Diamond Platinumz ameweka picha hiyo siku moja baada ya Wema Sepetu kupost picha nyingi kwenye Instagram akiwa na mama Diamond kwenye sherehe ya siku yake ya kuzaliwa na kuzipa caption mbalimbali huku nyingine zikiwa na vijembe.

Rose Ndauka Amkimbia Mumewe

$
0
0
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.

Akipiga stori na mwanahabari wetu, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.

“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

VANESSA MDEE azungumzia nia yake ya kushiriki BIG BROTHER

$
0
0
LEO July 11  ndo siku ambayo usaili wa kuwatafuta washiriki watakaoiwakilisha Tanzania katika reality show ya Big Brother nchini Afrika Kusini utaanza kufanyika.

Mara nyingi zinapokaribia siku za usaili mashabiki mbalimbali huweka ubashiri wao wa mastaa ambao wanadhani wanafaa kwenda kutuwakilisha.

Vanessa Mdee ni miongoni mwa mastaa mabao walitajwa na baadhi ya watu kuwa anaweza kufaa kama atawania nafasi hiyo mwaka huu.

Hiki ndicho alichojibu Vanessa kama yuko tayari kuwaridhisha mashabiki wanaotamani achukue fomu na kushiriki kwenye usaili wa kupata nafasi hiyo.

“Nasikitika kuwaambia wale wote ambao wangependa kuniona katika nyumba ya Big Brother kwamba haitakaa itokee” Amesema Vee Money na kutaja sababu, “character yangu haiendani na kukaa kwenye nyumba na watu wengi hivyo, yaani I will be so defeated yaani ntatoka siku ya tatu afu ntawa disappoint wale waliokuwa wanapenda niwe pale”.

Licha ya yeye kutokuwa na wazo la kushiriki ila amemtaja mtu anayedhani anaweza kufaa kwa nafasi hiyo.

“I think Rahim should Try, Rahim da Prince. Rahim I think he understands a lot about the world halafu pia ana personality he is very outgoing so nadhani angeweza kufanya vizuri pale”.

Lakini pia amemtaja mtu ambaye hastahili na asiyetakiwa hata kujaribu kuchukua fomu:

“Nadhani mpoki asiende”.LOL!

Usaili wa kuwatafuta wawakilishi wa Tanzania kwenye Big Brother utafanyika kwa siku mbili kuanzia leo July 11 na July 12 katika hotel ya New Afrika jijini Dar.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Chid Benz Amshushia Kipigo Ray C, Amfuata Nyumbani usiku wa Manane

$
0
0
Na Musa Mateja
Uonevu! Rapa mwenye ‘swagger’ za Ja-Rule Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, anadaiwa kukwaa kisanga kingine kibaya baada ya kukurupuka kutoka nyumbani kwake na kwenda kumvamia staa mwenzake, Rehema Chalamila ‘Ray C’ nyumbani kwake anapoishi na kumtwanga makonde ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo apate msala mwigine wa aina hiyo.

TUJIUNGE NYUMBANI KWA RAY C
Ilidaiwa kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita nyumbani kwa Ray C, Changanyikeni jijini Dar es Salaam ambapo ilisemekana kwamba Chid Benz alimvamia mishale ya saa 4:00 usiku kwa gia ya kumsaka mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina moja la Mariam.


CHID BENZ ATAKA KUMUONA MWANAYE
Ilidaiwa kwamba Chid Benz alisema kuwa alizungumza na mpenziye huyo kwamba alitaka kwenda kumuona mwanaye ambapo Mariam alimjibu kwamba kwa muda huo alikuwa nyumbani kwa Ray C  Changanyikeni.

UNGA WATAJWA
Sosi wetu alidai kwamba baada ya kujibiwa hivyo, Chid Benz alianza kulalama na kumwambia anamfuata palepale kwa nini usiku ule alale kwa Ray C, wakati ana uwezo wa kwenda nyumbani au amekwenda kwa staa huyo ili kunywa dawa zao za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’, jambo ambalo jamaa huyo siku zote huwa hataki hata kulisikia masikioni mwake.


CHID BENZ AWAVAMIA
“Huwezi kuamini baada ya muda kama wa saa moja, Ray C na Mariam wakiwa ndani wakitazama TV, ghafla mlango ulisukumwa kwa nguvu kisha akaingia Chid Benz na kumdaka Mariam na kuanza kumshushia kipigo.“Yaani huo mshtuko walioupata walidhani wamevamiwa na Al-Shabaab.

KIBAO CHAMGEUKIA RAY C
“Mungu mkubwa kwa sababu Mariam alifanikiwa kuchoropoka na kukimbilia chumbani ndipo kibao kikamgeukia Ray C.

“Ray C akiwa anashangaa ghafla naye alipokea kipigo kikali kutoka kwa Chid na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini.

RAY C AKIMBILIA KWA MAJIRANI
“Baada ya kuona maji yanazidi unga, Ray C alitafuta upenyo na kukimbilia kwa majirani huku akipiga kelele za kuvamiwa, mara moja majirani waliambatana naye mpaka nyumbani kwake.
“Walipofika Chid Benz alikuwa ametumia staili za kininja kwa kuruka geti na kutokomea kusikojulikana huku akiwaacha Ray C na Mariam wakiangua vilio kwa kipigo kikali walichopokea.

RAY C AVUJA DAMU
“Ray C aliumia mkono na mguu ambao ulionekana ukivuja damu. Mariam alikuwa akililia mbavu zake kuchakazwa kwa makonde mazito na upande mwingine baadhi ya vyombo vya ndani vikionekana kuvunjwa na vingine kusambaratishwa kufuatia tafrani iliyozuka muda mfupi baada ya Chid Benz kutia maguu nyumbani hapo,” chanzo kilishusha madai hayo mazito.

RAY C ATIRIRIKA SAKATA LILIVYOKUWA
Akizungumzia na gazeti hili Alhamisi iliyopita juu ya sakata hilo, Ray C alisimulia mkasa mzima: “Kweli Chid Benz alikuja nyumbani kwangu na kunivamia.

“Alinipiga vibaya sana na kuvunja baadhi ya vitu vya ndani kwangu, jambo ambalo lilinishangaza zaidi ni namna alivyopafahamu nyumbani kwangu hadi kuja kunifanyia fujo nikiwa na mzazi mwenzake, Mariam ambaye nilitoka naye ofisini kwangu.

“Ujue jana (Jumatano) tulikuwa na kazi sana ofisini kwangu mimi na Mariam, sasa kutokana na kubanwa na kazi kweli muda ulienda sana hivyo nikamwambia Mariam akalale kwangu.
“Kwa kuwa muda ule ilikuwa ngumu kwenda kwao Mbezi Beach, Mariam alikubali na tulikwenda wote nyumbani kwangu.

“Huko nyuma Mariam alikuwa mwathirika wa madawa ya kulevya lakini baada ya kusikia mimi nimeacha, naye aliachana nayo na kuanza kutumia dawa za kuondoa sumu.

“Tumeendelea kutumia naye dawa na sasa ameshapona kabisa hivyo kuna baadhi ya kazi nimekuwa nikimshirikisha kunisaidia kwenye ofisi yangu. Pia alishawahi kumshawishi Chid Benz ili aje kutumia dawa lakini jamaa alikataa na kumfanyia vurugu sana huku akimkataza kuwa na mimi kwa madai mimi ndiyo namfanya amwambie kuachana na utumiaji dawa za kulevya.

“Sasa jana alipojua hivyo nadhani Chid Benz alikuja kutimiza dhamira yake ambayo siku nyingi alikuwa akiahidi kunipiga.”

SOO LIPO POLISI
Ray C alisema baada ya tukio hilo alikwenda kuripoti kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Kinondoni na kufunguliwa jalada la kesi ambapo Chid Benz anasakwa na polisi.

Juhudi za kumpata Chid Benz hazikuzaa matunda kwani simu yake haikuwa hewani hivyo jitihada zinaendelea na kama ana ufafanuzi au utetezi anaweza kutupigia.

CHID BENZ NI TATIZO?
Chid Benz anadaiwa kuwa ni tatizo kwani tukio hilo la Ray C amelifanya wakati akiwa na tukio la pili kwa wanawake kwani kwenye Mahakama ya Mwanzo, Ilala ana kesi mbichi aliyoshitakiwa kwa kosa la kumpiga mrembo aitwaye Mwanaisha.

Mbali matukio hayo pia Chid Benz ana rekodi ya kukorofishana na wasanii wenzake kama Kalapina na marehemu Ngwea.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Kajala 'Wema ni Mnafiki Kabisa. Upatanisho Wetu ni wa Uongo'

$
0
0
Musa Mateja na Shakoor Jongo
STAA wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni baada ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.


Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”

Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe wa shosti wake huyo.

Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.

“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.

“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema Kajala.

Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili) usiku tu,” alisema Wema.
GPL

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

RIYAMA: 'Ukinitokea' Sina Hiyana. Nakukalisha Chini Tuzungumze

$
0
0
STAA wa filamu Bongo, Riyama Ally amesema katika maisha yake hajawahi kumtukana mwanaume pindi anaponitokea hata kama hamuhitaji, anamjibu kwa busara.

Akipiga stori na paparazi wetu, Riyama alisema yeye yupo tofauti na wasichana wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuwatukana wanaume pindi wanapowasilisha hisia zao za kimapenzi kwa sababu tu hawavutiwi kuwa nao.

“Hata kama mtu akinitongoza na nikawa simuhitaji kamwe siwezi kumtukana wala kumuonyesha dharau , kimaadili sisi sote ni binadamu na kila mtu ana hisia zake na maamuzi yake, namjibu tu kistaarabu kwamba mimi nina mtu wangu, kumjibu mwanaume vibaya Mungu hapendi,” alisema Riyama.

Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Daktari Mwingine Feki Akamatwa Hospitalini

$
0
0
Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi
WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.

Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.


Quote of The Day:
“Each day means a new twenty-four hours. Each day means everything's possible again. You live in the moment, you take it all one day at a time, You try to walk in the light” 

Maskini:Aliyedhani Kupona Ukimwi Augua Tena

$
0
0
Mtoto mmoja nchini Marekani ambaye alidhaniwa kuwa mtu wa kwanza nchini humo kutibiwa virusi vya HIV akiwa mtoto, amepatikana tena kuwa na virusi hivyo.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka minne kutoka jimbo la Mississipi amekuwa bila ya virusi hivyo kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kupata matibabu maalum akiwa bado mtoto mdogo.
Taarifa zinazohusiana
Marekani
Kisa chake kiliibua matumaini makubwa ya tiba ya ugonjwa wa ukimwi.
Madaktari wanasema kuwa kuibuka tena kwa virusi hivyo kumewasikitisha sana.
Madaktari walimpima mtoto huyo na kugundua kuwa angali ameambukizwa virusi vya HIV.
Mwezi Machi mtoto huyo alipopimwa hakupatikana na virusi ikizingatiwa kuwa hakuwa anapokea matibabu kwa karibu miaka miwili.
Bila shaka taarifa hii ni pigo kwa matumaini ya matibabu kutoweza kumaliza virusi vya HIV mwilini kabisa.

Ukweli Kuhusu Kuzikwa Kwa Balali 'Kabari Lake Laonekana'

$
0
0
Mkazi wa Kijiji la Luganga, Wilaya ya Mufindi, Iringa, alikozaliwa Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali analazimika kutumia saa 32 kufika katika kaburi la kiongozi huyo lililopo eneo la Silver Spring, Maryland nchini Marekani.

Ndugu wa Ballali (pichani) wanaweza kutaka kwenda kuona kaburi la ndugu yao, kutokana na ukweli kwamba wengi wao hawakuwahi kupata fursa ya kumzika Gavana huyo ambaye alikuwa kiongozi wa juu kabisa wa taasisi kubwa inayosimamia masuala ya fedha na uchumi wa nchi.

Mwandishi wa gazeti hili alisafiri kwa saa 24 kutoka Dar es Salaam hadi Washington, Marekani ambako alithibitisha pasi na shaka kwamba Ballali alizikwa Mei 21, 2008 katika makaburi ya Gate of Heaven, baada ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake Maryland, Mei 16, mwaka huo.

Safari hiyo ya siku kumi, ilianza Alhamisi Juni 26, 2014 hadi Jumapili, Julai 6. Mwandishi wa habari hizi aliligundua kaburi hilo baada ya kwenda makaburi ya Gate of Heaven kwa siku tatu mfululizo.

Siku ya kwanza, mwenyeji wa mwandishi ambaye jina lake tunalihifadhi kwa sasa alimfikisha katika makaburi hayo, lakini kaburi la Ballali halikuonekana na hata mwandishi alipokwenda siku ya pili peke yake, kaburi hilo pia halikuonekana kwa kutokana na ukubwa wa eneo hilo.

Siku ya tatu, Mwandishi wa Mwananchi alilazimika kuomba msaada wa Ofisi ya Makaburi ya Gate of Heaven, ambayo ilimsadia kuonyesha eneo lilipo kaburi hilo, hivyo kuwezesha kupata picha zake.

Kaburi lake liko katika msitari wa mwisho kabisa na Ukanda wa Kijani wa miti iliyozunguka makaburi ya Gate of Heaven, likiwa limeandikwa jina la kiongozi huyo, pamoja na maneno ya Kiingereza yanayosomeka “When the heart weep for what it has lost, the soul rejoices for what it has found”.

Maana ya maneno hayo ni kwamba “wakati moyo ukiomboleza kwa kile kilichopotea, roho hufurahi kwa kile kilichopatikana”. Kaburi hili limezungukwa na makaburi mengine kadhaa ambayo si ya Watanzania, kwani kwa haraka kutokana na mazingira yalivyokuwa, Mwandishi wa Mwananchi hakuweza kuona kaburi jingine lenye majina yenye asili au kuwa na mwelekeo wa asili ya Tanzania.

Uthibitisho huu ni tofauti na hekaya za miaka nenda rudi zilizogubika kifo cha kiongozi huyo, ambaye tangu alipoondoka nchini kwenda Marekani Agosti 2007, hakuwahi kurejea na badala yake zilisikika taarifa za kuugua kwake, kifo chake na baadaye mazishi yake yaliyokuwa ya siri kubwa yakiwahusisha ndugu wa karibu pekee.

Kutokana na mazingira hayo, kumekuwapo na uvumi kwamba Ballali hakufa na pengine amefichwa kusikojulikana, madai yanayochagizwa na mtu aliyejitokeza katika mitandao wa kijamii ya Twitter na facebook, akidai kwamba yeye ni Ballali na kwamba hajafa, huku akisisitiza kuwa wakati ukiwadia ukweli utafahamika.

Mtu huyo asiyefahamika hadi sasa alianza kujitokeza Twitter, Oktoba Mosi, 2012 pale aliposema “Nitakutana na Rais Kikwete (Jakaya) na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani”. Mtu huyo alidai kwamba alikuja nchini Tanzania na kukaa karibu na Hoteli ya Hyatt Kempinski Kilimanjaro na baadaye kuondoka ghafla kwa kile alichokiita sababu za kiusalama.

Novemba 13 mwaka huo alituma ujumbe akisema:“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” akimaanisha kwamba niko Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, najisikia vizuri kuwa karibu na ofisi yangu ya zamani BoT.

Mtu huyo ambaye sasa tunaweza kuthibitisha kuwa ni feki amekuwa akiendelea kutuma ujumbe akijitambulisha kwa jina hilo la Ballali.

Ballali alifariki dunia kama ilivyotagazwa, lakini ilikuwaje akaenda safarini Washington, ugonjwa wake na hata kifo chake kilikuwaje? Je ndugu zake wanasemaje, safari

Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images