Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Ridhiwani Kikwete Ampongeza Fid Q

$
0
0
Ridhiwani  Kikwete Ampongeza Fid Q
Mbunge wa Chalinze  (CCM) Ridhiwani Kikwete amempongeza Fid Q baada ya kutii kauli ya Rais John Pombe Magufuli ambayo aliitoa Jumanne Disemba 12, 2017 kwenye Kamati Kuu ya CCM na kuwataka wasanii wa kike kuvaa vizuri kwenye video zao.


Ridhiwani Kikwete ametoa pongezi hizo baada ya kuiona video mpya ya Fid Q anayokwenda kwa jina la 'Fresh Remix' ambayo ndani yake mabinti wengi ambao wameonekana kwenye video hiyo walikuwa wamevalia magauni marefu ambayo yameonekana kuwasitili na kuwapendeza zaidi bila kuharibu muonekana wa video hiyo. 

"Hii inaitwa tii bila shuruti. Hongera sana mdogo wangu Diamond, Fid Q kwa kuonyesha usikivu. Mavazi mazuri ni yale yanayohifadhi utu na jinsi. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" aliandika Ridhiwani Kikwete

Rais Magufuli akiwa kwenye Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM mwaka jana Disemba 12 aliwataka Jumuiya ya Wazazi ya CCM kutokaa kimya pindi wanapoona mambo mabaya katika jamii na alisema kuwa amekuwa akikerwa na tabia ya baadhi ya wanawake kwenye video za wasanii wa bongo kuvaa vibaya na kuonyesha maumbile yao ya ndani kitu ambacho hakikubaliki.

Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli wasanii hawa wakubwa wamenza kuwa mfano kwa kuwavalisha wapambaji wa video yao nguo ndefu ambazo zimesaidia kuipamba video hiyo.











Kigogo Ashindwana Tabia na Kidoa Ampokonywa Gari

$
0
0
Kigogo Ashindwana Tabia na Kidoa  Ampokonywa Gari
MUUZA nyago machachari Bongo, Asha Salum ‘Kidoa’ anadaiwa kupokonywa gari aina ya Subaru na mwandani wake ambaye ni kigogo wa serikali baada ya kushindwana tabia.

Taarifa kutoka kwa chanzo kilicho karibu na mrembo huyo zimeeleza kuwa, bishosti huyo  licha ya kujitapa kwamba gari hilo alinunua mwenyewe, ukweli ni kwamba alipewa na bwana’ke ambaye alikuwa anaishi naye kinyumba maeneo ya Tabata jijini Dar.

“Ile gari Kidoa alipewa na huyo mwanaume wake, sasa kuna mambo walishindwana kwenye uhusiano wao  ikabidi kila mmoja asepe kivyake, ndipo yule jamaa akampokonya gari,”kilisema chanzo hicho.

Baada ya kuinyaka ishu hiyo, paparazi wetu alimtafuta waya Kidoa, akafunguka.

“Ni kweli sionekani na gari mjini, kuna siku nilipata ajali mbaya niligongana na basi, hivyo lipo gereji linaendelea na matengenezo, soon mtaliona.”

Kamati ya Nidhamu ya TFF Yampa Adhabu Meneja wa Prisons

$
0
0
Kamati ya Nidhamu ya TFF Yampa Adhabu Meneja wa Prisons
Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.



Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons, Meneja wa timu ya Tanzania Prisons Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba,kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba na hivyo imemfungia miezi miwili(2) na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya udhibiti wa viongozi.

Kamati pia ilipitia suala la golikipa wa Mbeya City, Owen Chaima kudaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam FC, Yahya Mohamed.

Chaima alikiri kumpiga, Yahya na Kamati kupitia kanuni ya 35(7b) ya udhibiti wa wachezaji imemfungia kucheza mechi 4 na faini.

Polepole Awatupia Dongo Upinzani " Ukitukana Tusi Moja Napokonya Kiongozi Mmoja"

$
0
0
Polepole Awatupia Dongo Upinzani " Ukitukana Tusi Moja Napokonya Kiongozi Mmoja"
January 4, 2018 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amewatahadharisha Chama cha Demokrasia na Maendelo (CHADEMA) ndani ya mkoa wa Dar es salaam kuwa atamng’oa kiongozi mmoja wa chama hicho.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Polepole amesema  baada ya madiwani wawili wa CHADEMA kuachia ngazi Mjini Iringa, ambapo ametoa sababu ya Madiwani hao kuhamia CCM kuwa ni kumuunga mkono President JPM.

“Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa. Nasikia wameambiwa “never outshine your master”. Mimi nilidhani “masta” ni wananchi kumbe ni “pasta”. Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM ” – Polepole


Humphrey Polepole
@hpolepole
Leo Madiwani wengine wawili wamehama na kujiunga na CCM. Ukiwasikiliza kilichowaondoa ni Uongozi Mbovu na Ubabe pale Iringa Mjini. Nasikia wameambiwa "never outshine your master". Mimi nilidhani "masta" ni wananchi kumbe ni "pasta". Ukitukana tusi moja Kiongozi mmoja nachomoa DSM

Mganga wa Kienyeji Aamua Kujiua Baada ya Kukosa Wateja

$
0
0
Mganga wa Kienyeji Ajiua Baada ya Kukosa Wateja
January 4, 2018 nikusogezee stori hii kuhusu wakazi wa eneo la Maili Saba katika Jimbo la Trans Nzoia wamepigwa na butwaa baada ya mganga Joshua Shalongo kujiua kwa sababu ya kukosa wateja na hali ngumu ya maisha.

Shalongo ambaye ni mganga maarufu katika eneo la Kitale nchini Kenya inasemekana suala la kukosa wateja lilimtatiza sana kiasi cha kuchukua uamuzi wa kujiua.

Mwili wake umepatikana ukining’inia kwenye paa la nyumba ukiwa umefungwa kamba taarifa hii imeripotiwa katika jarida la Citizen’s Edaily.

Chief wa eneo hilo Esther Waswa amethibitisha tukio la mganga huyo kujiua.

Trump Amshambulia Msaidizi Wake wa Zamani Steve Bannon

$
0
0
Trump Amshambulia Msaidizi Wake wa Zamani Steve Bannon
Rais Donald Trump amemshambulia msaidizi wake wa zamani wa Ikulu ya White house Steve Bannon,kwamba alipoteza akili zake mara tu alipopoteza ajira yake.Trump amefikia hatua hiyo kufuatia Bannon kunukuliwa na kitabu kipya kilichopishwa akiwa anaelezea jinsi mtoto wa rais Trump alivyokutana kwa siri na kundi la watu kutoka Urusi ili kupanga njama za uchaguzi.

Ndani ya kitabu hicho kilichoandikwa na mwandishi wa habari Michael Wolff,afisa huyo wa zamani wa ikulu ya Marekani,ameelezea namna ambavyo Donald Trump mtoto,mwanaye rais Trump alivyopewa taarifa na Urusi zilizolenga kummaliza kisiasa Bi Hillary Clinton ili yeye aweze kushinda.

Hata hivyo kutokana na shutuma hizo ndani ya kitabu hicho zilizopewa uzito na afisa huyo wa zamani wa ikulu ya white house,rais Donald Trump amesema kuwa lolote la kuweza kumuathiri yeye binafsi na urais wake pia,bali amesisitiza kuwa amegundua kuwa ofisa huyo hakupoteza kazi yake tu lakini alipoteza akili zake pia.

Trump: Kibonyezo changu cha nyuklia kina nguvu kuliko cha Kim
Trump adai Pakistan imeihadaa Marekani muda mrefu
Marekani yanuia kukata misaada kwa Palestina
''Steve alikuwa ofisa aliyekuwa akifanya kazi kwaajili yangu,mara baada ya mimi kuteuliwa kuwania urais baada ya kuwabwaga wagombea wengine 17,'' amesema Trump.

Amesema pia kuwa Steve anafanyayote hayo kwa maslahi binafsi,akifikiri kuwa suala la ushindi si rahisi kama ilivyokuwa katika ushindi wangu,hana lolote la kuweza kufanya kuhusiana na historia ya ushindi wetu ambao ulipatikana kwa kura za wanawake na wanaume waliokuwa wamesahaulika.

Steve Bannon, ni afisa wa zamani wa rais Trump nayetajwa kuwa mtu muhimu na alibuni kauli mbiu ya rais Trump Marekani kwanza yaani America first kabla kuacha kazi mwezi August mwaka jana.

Msemaji wa Serikali Afunguka Kuhusu Mwalimu Anayeidai Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu

$
0
0
Msemaji wa Serikali Afunguka Kuhusu Mwalimu Anayeidai Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu
Stori kuhusiana na ishu za Mikopo ya Elimu ya Juu zinaendelea kuchukua headlines nchini baada ya juzi Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi HESLB, Abdul Razaq Badru alitangaza kuwapata baadhi ya wadaiwa sugu na kuwakata fedha kwa ajili ya malipo ya mikopo yao.

Jana January 3, 2018 katika moja ya Gazeti nchini ilichapishwa taarifa ya Mwl. Ndyamukama akimuomba Waziri Mkuu amsaidie arejeshewe fedha alizokatwa kimakosa na Bodi ya Mikopo.

Leo January 4, 2018 Dr. Hassan Abbas kupitia ukurasa wa Twitter wa Msemaji wa Serikali ametoa taarifa juu walipofikia kuhusu suala hilo.

“Tumefuatilia malalamiko hayo na suala hilo limepatiwa ufumbuzi. Atarejeshewa fedha zake Jumanne ijayo.” – Dr Hassan Abbas

Chupa ya Vodka Inayotajwa Kuwa ya Gharama Kubwa Zaidi Duniani Yaibiwa

$
0
0
Chupa ya Vodka Inayotajwa Kuwa ya Gharama Kubwa Zaidi Duniani Yaibiwa
Chupa ya Vodka inayotajwa kuwa ya gharama kubwa zaidi duniani inayopatikana nchini Denmark imeripotiwa kuibiwa.

Inaelezwa kuwa chupa hiyo ambayo ni ya thamani ya Dola za Marekani Milioni 1.3 sawa na Tsh Bilioni 3.1 imetengenezwa kwa dhahabu na fedha na kifuniko chake ni cha madini ya almasi.

Chupa hiyo iliibiwa baada ya kukopeshwa baa moja huko Copenhagen nchini humo ambayo ilikuwa imekusanya chupa za mvinyo kwa ajili ya maonyesho. Polisi wanaendelea na uchunguzi kubaini waliohusika.


Mbaroni Kwa Kutapeli Milioni 15 za Raisi

$
0
0
Mbaroni Kwa Kutapeli Milioni 15 za Raisi
Kijana mmoja ambaye amefahamika kwa jina la Mohamedy Msangi (28) mkazi wa Kilakala Manispaa ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kughushi nyaraka na kujipatia mkopo wa milioni 15 katika taasisi ya mfuko wa Rais Kanda ya Morogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa jambo hilo na kusema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa na askari walifuatilia na kumkamata mtuhumiwa huyo ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kufanya kosa hilo kwa kuomba mkopo katika taasisi hiyo inayojihusisha na utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana. 

Matei amedai kuwa kijana huyo alipoomba mkopo huo aliorodhesha majina ya vijana wengine wanne akijifanya kuwa vijana hao wamejiunga kwenye kikundi hicho kisha kupatiwa mkopo huku hao vijana aliowaorodhesha wakiwa hana taarifa yoyote. 
Mbali na hilo Kamanda Matei alitoa rai kwa wananchi wa Morogoro na kuwataka wananchi kuacha wizi "Tuache huu wizi kwa kutumia vyombo vinavyotoa mikopo kwani mikopo hii imewekwa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa chini na hilo ndiyo lengo la Serikali kuwaondolea watu umasikini ili waweze kufungua viwanda vidogo vidogo na kujipatia kipato, lakini wapo watu wanatumia vibaya vikundi hivi" alisema  Matei

Watu 456 Wafariki Dunia Mbeya

$
0
0
Watu 456 Wafariki Dunia Mbeya
Jumla ya Watu 456, wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 700 wamejeruhiwa mkoani Mbeya kutokana na matukio ya ajali za barabarani katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2017.


Akizungumza hali ya usalama ya mkoa kwa mwaka 2017 mbele ya waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amebainisha kuwa jumla ya makosa 82,211 ya ukiukwaji wa sheria za barabarani yalipatikana katika kipindi cha mwaka 2017, wakati mwaka 2016 yalikuwa ni 66,172.

Kamanda Mpinga, alisema Mwaka jana jumla ya watu 170 walipoteza maisha kutokana na ajali za barababani wakati mwaka 2016, watu waliopoteza maisha ni 286 hivyo kuna upungufu wa asilimia 40.5 ya idadi ya vifo vilivyolipotiwa katika kipindi cha miaka miwili.

“Sababu za kutokea kwa matukio ya ajali ni kuongezeka kwa vyombo vya usafiri mkoani Mbeya hasa magari na pikipiki, baadhi ya madereva kutozingatia sheria za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na mwendokasi hasa usiku na ulevi licha ya jitihada za jeshi la polisi kwa kushirikiana na wadau kutoa elimu mara kwa mara” alisema.

Akizungumzia hali ya uhalifu, kamanda Mpinga alisema jumla ya makosa 26,009 yaliripotiwa kutokea katika mkoa wa Mbeya kwa kipindi cha mwaka jana ikilinganishwa na matukio 32,943 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2016.

Aidha Kamanda Mpinga amesema kwa mwaka 2018 jeshi la polisi limeandaa mikakati mbalimbali ya kukabiliana na wahalifu na uhalifu pamoja na kupunguza ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kubaini muelekeo wa uhalifu na maeneo tete ili kuelekeza nguvu katika maeneo hayo.

Prisons na JKT Zapewa Ushindi na TFF

$
0
0
Prisons na JKT Zapewa Ushindi na TFF
Kikao cha kamati ya Mashindano kilichokutana Desemba 29, 2017 kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kujadili mchezo namba 31 na 32 uliohusisha timu za Abajalo FC dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya na ule kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu katika Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) iliyokuwa ifanyike Desemba 20, 2017 kwenye Uwanja wa Uhuru na Chamazi.


Kamati ilikaa na kupitia taarifa mbalimbali za michezo hiyo.

Kamati kupitia kanuni ya 24 kifungu cha (1) katika mchezo kati ya Abajalo FC na Tanzania Prisons imeipa ushindi timu ya Tanzania Prisons baada ya kubaini Abajalo kukiuka kanuni hiyo.

Kwenye mchezo mwingine kati ya Mvuvumwa na JKT Ruvu Kamati baada ya kupitia na kujiridhisha imeipa ushindi timu ya JKT Ruvu baada ya Mvuvumwa pia kukiuka kanuni ya 24 kifungu (1).

Kwa maamuzi hayo timu za Tanzania Prisons na JKT Ruvu zinafuzu kwenda kwenye hatua ya tatu(3) ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Mnada wa Magari 140 Yalyo Telekezwa Bandarini Walalamiiwa

$
0
0
Mnada wa Magari 140 Yalyo Telekezwa Bandarini Walalamiiwa
 Mamlaka ya Mapato nchini kupitia kampuni ya Yono Aunction Mart imeendesha mnada wa magari 140 yaliyotelekezwa bandarini.

Licha ya watu wengi kujitokeza kwenye mnada huo uligubikwa na malalamiko huku wateja wakilalamikia utaratibu mbovu wa uendeshaji wa mnada.

Mwananchi ilishuhudia watu waliofika kwa wingi katika eneo hilo wakiondoka huku wengine wakiwa wamekaa chini kwa kukata tamaa.

Wananchi hao walidai kuwa matarajio yao yalikuwa tofauti kabisa na hali waliyoikuta kwenye mnada kwa kile walichodai kuwa bei zilishapangwa.

Mmoja wa wateja hao Posian Simon amesema alitegemea kuwa mnada huo ungekuwa huru na wanunuzi wangeshindana kwa bei lakini inaonekana kuwa bei zimepangwa.

“Nilijua kuwa mwenye pesa kubwa kuliko wenzake ndiye anayechukua gari sasa hapa mambo yako tofauti mnaweza kushindana na ikafika kiwango cha mwisho lakini wenyewe wakaamua gari haliuzwi kwa kuwa haijafikiwa bei wanayotaka,”

“Nimefunga safari kutoka Bukoba kuja kushiriki kwenye mnada huu ila naona nimepoteza muda wangu na kuja kuteseka na jua, nashauri siku nyingine uwekwe utaratibu mzuri”

Malalamiko kama hayo aliyatoa Diwani wa Tabata,Patrick Assenga ambaye pia alifika katika eneo hilo kwa ajili ya kununua gari.

“Kwa kweli kinachoendelea hapa ni kitu cha ajabu, nilijua mnada huu utafuata taratibu za minada mingine ambayo watu wanashindana na anayeshinda ndiye anapaswa kuchukua mali lakini hapa mtu anaweza fikia kiwango cha juu na bado wakaamua gari iwekwe pembeni,

“Kinachonishangaza zaidi ni hizi bei wanazozitaka wao yani ni sawa na mtu akaenda show room kuchukua gari au labda na wao wangebandika bei kwa kila gari maana hakuna haja ya kuwajaza watu kwenye jua hapa halafu wanafanya mambo tofauti na utaratibu,” amesema Assenga.

Akijibu kuhusu malalamiko hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Auction Mart, Scolastica Kevela amesema mnada huo unazingatia taratibu zote na watu wanashinda kwa bei kama inavyopaswa kuwa.

Kuhusu kusitisha uuzaji wa baadhi ya magari licha ya kuwa kuna kiwango cha bei kilichofikiwa Kevela amesema mauzo yoyote yanafikiwa kulingana na thamani ya gari husika.

“Hata kama Serikali inataka kukomboa kodi yake haiwezekani bei kuuzwa kwa bei ya kutupa, lazima tuzingatie thamani halisi ya gari. Kwa kifupi mambo yanakwenda vizuri kabisa,”

Abiria Kilimanjaro Wahaha kurejea Mijini

$
0
0
Abiria Kilimanjaro wahaha kurejea mijini
 Mamia ya abiria katika kituo kuu cha mabasi Moshi wamejikuta wakishindwa kusafiri kama walivyotarajia kutokana na uhaba wa mabasi unaotajwa kuchangiwa na wingi wa watu wanaorejea mikoa mbalimbali baada ya kumalizika kwa Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

Akizungumza leo Alhsmisi Januari 4, mwenyekiti wa wakala wa mabasi kituo cha Moshi, Wile Tuli amesema abiria wamekua wengi kwa kipindi hiki ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Amesema adha ya usafiri imetokana na watu wengi kuanza kurejea katika shughuli zao baada ya kumalizika kwa sikukuu za mwisho wa mwaka, baadhi kupeleka watoto shule.

“Wapo waliokuja Moshi kwa magari binfasi, ila inavyoonekana magari hayo yalirudi na sasa wanapanda mabasi,” amesema,

“Jana abiria walikua wengi kuliko leo kutokana na kunyesha mvua kubwa hapa na usafiri kutoka vijijini umekuwa shida.”

Mmoja wa wakata tiketi ya mabasi ya kampuni ya Machame, Manase Ndosi amesema magari ni machache kutokana na abiria kuwa wengi.

Amesema Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) inapaswa kuongeza mabasi ili kuweza kunusuru abiria waliokwama kutokana na uhaba huo wa mabasi.

“Wengi nauli wanazo shida yao ni usafiri tu. Mfano leo kama mtu ana Sh40,000 eti ndio nauli yake, anataka tiketi aende Dar es Salaam. Kwa kuwa mabasi hamna amejikuta akishindwa kusafiri,” amesema.

Mmoja wa abiria,  Dismas Mfoi  amesema, “Hali ya  usafiri hapa stendi ni ya shida, Sumatra ilitazame hili kwa kweli.”

Tanzia;Kingunge Apata Pigo Mkewe Afariki Dunia

$
0
0
Tanzia;Kingunge Apata Pigo Mkewe  Afariki Dunia
Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini kingunge Ngombale,Pelasi amefariki dunia katika hospitali ya taifa Muhimbili mtoto wa kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha kutokea kwa msiba wa mama yake.

Pata Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0

MHULI: Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.


Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na Nasi kwa Namba;0783140065  

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia

$
0
0

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

"Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling'atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka," amesema

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

Barakah Afunguka Alichozungumza na Tundu Lissu ‘Ni Mungu Alinisukuma’ (Video)

$
0
0
Baada ya kusambaa picha katika mitandao ya kijamii zikimuonyesha muimbaji, Baraka The Prince akiwa amemtembelea hospitali Mhe. Tundu Lissu nchini Kenya, Bongo5 ilimtafuta muimbaji huyo ambaye ni rais ya label ya Bana Music na kueleza alichozungumza na Lissu baada ya kumtembelea hospitali hapo.

CCM Yamsaka Diwani Wake Aliyeipa Ukawa Kura..Habari Zilizopo Katika Magazeti yya Leo Ijumaa ya January 5

$
0
0


CCM Yamsaka Diwani Wake Aliyeipa Ukawa Kura..Habari Zilizopo Katika Magazeti yya Leo Ijumaa ya January 5

Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Kigoma Akamatwa

$
0
0
Jeshi la polisi linamshikilia Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Mgalla Mashaka kwa tuhuma za kushindwa kukarabati Shule ya Sekondari Kigoma.

Meneja huyo alikamatwa akituhumiwa kushindwa kukarabati shule ya sekondari Kigoma kwa wakati licha ya kupewa zaidi ya shilingi milioni mia nne kati ya mia tisa tangu mwezi wa nane mwaka jana.

Mhandisi Mgalla amekamatwa baada ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, kufanya ukaguzi katika shule hiyo ambayo imeanza kupokea takribani wanafunzi elfu moja huku katika miezi mitano ya ukarabati hadi sasa ukarabati wa vyoo, mabweni, maabara na vyumba vya madarasa haujakamilika

Prof. Ndalichako amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TBA kufika Kigoma kutatua tatizo hilo ili kuepusha maafa yanayoweza kutokea. Kutokana na hali hiyo serikali imeamua kujenga vyoo vya muda ili wanafunzi waweze kuanza masomo wiki ijayo.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images