Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Maofisa wa Wanyamapori Wapandishwa Kizimbani kwa Kusababishia Serikali Hasara ya Mil 78

$
0
0
Maofisa wa Wanyamapori Wapandishwa Kizimbani kwa Kusababishia Serikali Hasara ya Mil 78
Maofisa watatu wa Kitengo cha Matumizi ya Wanyamapori wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Dola za Marekani 32,599 takriban Tshs Mil 78.

Maofisa hao ambao ni waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii ni Rajab Hochi, Mohammed Madehele na Isaac Maji wamesomewa makosa yao na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Swai alidai washtakiwa wanakabiliwa na makosa sita mojawapo likiwa ni matumizi mabaya ya madaraka ambalo walilitenda kati ya October 12 na December 31, 2008.

Inadaiwa kosa hilo walilitenda katika Makao Makuu ya Wizara hiyo iliyopo Temeke Dar ea Salaam ambapo wakiwa kama Maofisa wanaowajibika katika kitengo cha Matumizi ya Wanyama pori wakiwa na jukumu la kukusanya mapato yatokanayo na uwindaji walitumia mamlaka yao vibaya kwa kushindwa kukusanya kiasi cha USD 250 kutoka Kampuni ya Uwindaji ya Northern Hunting Enterprises.

Baada ya kusomewa makosa yote sita, washtakiwa walikana, ambapo Wakili Wankyo alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo, washtakiwa hao waliepuka kwenda rumande baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na walidhaminiwa wawili waliosaini bondi ya Sh.milioni 50, huku wakitakiwa kutosafiri nje ya Dar es Salaam, ambapo kesi imeahirishwa hadi January 31, 2018.

Uingereza Yamteuwa Waziri wa Upweke

$
0
0
Uingereza Yamteuwa Waziri wa Upweke
Uingereza imemchagua waziri wa upweke ili kukabiliana na kile ambacho waziri mkuu wa Uingereza amedai ni uhalisia wa masikitiko kuhusu maisha ya sasa yanayoathiri mamilioni ya watu.

Tracey Crouch, ambaye ni naibu waziri wa michezo na wanaharakati atachukua wadhfa huo ikiwa ni miongoni mwa malengo ya kukabiliana na upweke unaowakabili watu wazima, wale waliopoteza wapendwa wao, wale wasio na watu wa kuzungumza nao ama hata kugawana mafikra na uzoefu, waziri huyo aliongezea.

Zaidi ya watu milioni tisa wanasema kuwa huwa pweke kati ya milioni 65.6 kulingana na shirika la msalaba mwekundu.

Shirika hilo limetaja upweke na kutengwa kuwa janga lililojificha miongoni mwa watu wenye miaka tofauti katika maisha yao kama vile waliostaafu , waliofiliwa ama waliotengwa.


Uanzilishi wa wizara hiyo unafuatia mapendekezo kutoka kwa kamati ya kumbukumbu za Jo Cox , mbunge wa chama cha upinzani cha leba ambaye aliuawa na watu wenye itikadi kali wa mrengo wa kulia.

Jo alikuwa na alishuhudia upweke katika kipindi chote cha maisha yake akiwa mwanafunzi mpya katika chuo kikuu cha cambridge na alijitenga na dadake Kim, kwa mara ya kwanza , wakfu wa Jo Cox uliandika katika mtandao wa twitter.

Angefurahishwa na kazi mpya ya Tracey Crouch kama waziri wa upweke na angesema twende kazi, wakfu huo uliongezea.

Mtu Mmoja Afariki Dunia Baada ya Kuigonga Ndege ya Fastjet

$
0
0
Mtu Mmoja Afariki Dunia Baada ya Kuigonga Ndege ya Fastjet
Mkazi mmoja wa mkoa wa Mwanza amefariki dunia baada ya kuigonga ndege ya Fastjet iliyokuwa ikiruka katika Uwanja wa Ndege Mwanza kuelelea jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi leo Januari 18, 2018 Kaimu MKurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela amesema tukio hilo la aina yake limetokea jana usiku.

Amesema ndege hiyo ilikuwa njia moja kuelekea jijini Dar es Salaam, kubainisha kuwa mtu huyo ndiye aliyeigonga ndege hiyo.

“Ingawa ndege ndio ilimgonga mtu huyo ambaye jina lake hatulifahamu, kisheria mtu au kitu chochote kinachokuwa kwenye njia ya kurukia  na kutua ndege ndiyo kinahesabiwa kuigonga ndege. Ni kama ilivyo kwa treni,” amesema Mayongela.

Amesema kabla ya ndege hiyo kuruka,  taratibu zote za kiusalama zilifuatwa ikiwemo kukagua njia kujiridhisha hakuna kitu chochote.

“Haijulikani mtu huyo alitokea wapi. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo eneo la tukio kuchunguza tukio hilo kwa kina na tutatoa taarifa kamili uchunguzi utakapokamilika,” amesema kaimu mkurugenzi huyo.

Amesema kitendo cha mtu huyo kuwepo katika njia ya kurukia ndege licha ya ukaguzi kufanyika kinawaumiza vichwa viongozi na wataalam wa usalama uwanjani hapo.

 “Pengine tatizo la muda mrefu la kukosa uzio tunaloanza kukabiliana nalo kwa ujenzi na upanuzi wa uwanja linaweza kuwa chanzo cha mtu huyo kuingia katika njia ya kurukia ndege,” amesema.

Ili kukabiliana na matukio ya aina hiyo, amesema wataimarisha mifumo ya usalama kwenye viwanja vya ndege nchini.

Zari Aendelea Kuteswa na Mapenzi Aamuuliza Diamond “Madale State Lodge au Guest house?

$
0
0
Baada ya tetesi kuzidi kuenea katika mitandao ya kijamii na watu kuzidi kusema kuwa inawezekenaTunda ana mahusiano ya kimapenzi na Diamond Platnumz kutokana tu na ukaribu walionao wawili hao.

Zari the boss lady ambaye ni mzazi mwenzakeDiamond Platnumz ameonekana kupata taarifa hizo kuhusiana na tetesi zinazoendelea katika mitandao ya kijamii na kuamua kuandika ujumbe kwa Diamond Platnumz kupitia mtandao wa snapchat.

Diamond Ameyasikia Aliyosema Zari Kuhusu Madale Kuitwa Gesti House....Ajibu Hivi

$
0
0
Diamond Platnumz azidi kuchukua headlines katika mitandao ya kijamii baada ya maneno yanayoendelea katika mitandao ya kijamii ya kudaiwa kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na Tunda. Maneno hayo yameonekana kumfikia Diamond Platnumz.


EXCLUSIVE: ‘Kufanya Ukahaba sio Kosa Kisheria’ -Wakili Juma

$
0
0
Biashara ya Ukahaba ni miongoni mwa biashara zinazopigwa vita duniani, ambapo leo January 18, 2018 wakili wa kujitegemea Juma Nassoro amesema kisheria ni kosa kufanya Ukahaba kwa ajili ya kujipatia kipato.

 Akizungumza na AyoTV, Wakili Nassoro amesema kuwa kisheria kufanya Ukahaba si kosa, isipokuwa kufanya Ukahaba kwa lengo la kibiashara ni kosa.

“Kidini ukahaba ni makosa lakini kwa sheria za nchi yetu mtu kuwa na mahusiano na watu tofauti tofauti sio kosa, isipokuwa litakuwa kosa la kijinai ni kufanya kazi hiyo kwa kujiingizia kipato na endapo akitiwa hatiani adhabu yake ni kifungo ama faini,”.– Wakili Juma Nassoro

VIDEO:

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0

Ni Dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?

Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521

VIDEO: Mwenyekiti Bavicha Amvaa Magufuli

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema Patrick Ole Sosopi amesema kitendo cha Rais John Pombe Magufuli Kumuita Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa Ikulu na Kumshawishi kujiunga na CCM sio kitendo ambacho kinafaa kufumbiwa macho. VIDEO:

Simba imetangaza Kocha Mpya Kutoka Ufaransa

$
0
0
Club ya wekundu wa Msimbazi Simba leo Alhamisi ya January 18 2018 imetangaza kufanikiwa kumpata mrithi wa kocha Josep Omog aliyefutwa kazi wiki kadhaa zilizopita kwa kushindwa kuuridhisha uongozi katika suala zima la mwenendo wa timu.

Simba Sports Club
Dar es salaam
18/01/2018. TAARIFA KWA UMMA
Klabu ya Simba inayo furaha kubwa kuwajulisha Wanachama na washabiki wake kwamba imempata kocha wake mkuu mpya,Mfaransa Pierre Lechantre.

Kocha huyo mzoefu ataanza kazi mara moja na atasaidiwa na kocha msaidizi wa sasa Masoud Djuma ambae alikuwa akikaimu nafasi hiyo, Kocha Lichantre keshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroun kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Kocha huyo pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na pia barani Asia mwaka 2012, Lechantre amekuja pia na kocha wa viungo Mmorocco Mohammed Aymen Hbibi

Leo jioni kocha Lechantre ataishuhudia Simba ikicheza na Singida United kwenye Uwanja wa Taifa.

IMETOLEWA NA
HAJI S MANARA

MKUU WA HABARI SIMBA SC

Wizkid Ashangazwa na bei ya Midoli ya Kufanyia Ngono ‘S3x Dolls’

$
0
0
Msanii wa muziki kutoka Nigeria, Wizkid ameshangazwa na bei ya midoli ya ngono ‘Sex Dolls’ ambapo amesema kuwa bei ya midoli hiyo ni kubwa kulikuwa hata gharama ya kununua wanawake wanaojiuza yaani makahaba.

Wizkid amesema makampuni yanayotengeneza midoli hiyo hayajui jinsi ya kupanga bei kuendana na mazingira kwani haamini kuwa mtu anaweza kutumia mamilioni ya pesa kununua midoli hiyo ile hali anaweza kulipia gharama ndogo kununua kahaba na kujiridhisha kingono.

“Najiuliza watu wanaotengeneza midoli ya ngono, hivi hawajui bei ya makahaba mtaani,“ameandika Wizkid kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Kauli nhiyo imekuja baada ya wiki iliyopita duka kubwa la midoli ya ngono ya kampuni ya eSex Dolls kufunguliwa nchini humo ambapo bei ya chini ya midoli hiyo ni tsh milioni 5 huku bei ya juu ikiwa hadi milioni 10 kitu ambacho watu wengi wa Nigeria wameshangazwa na bei hiyo.

Mwanamke Mjamzito Atolewa Kopo la Mafuta Sehemu za Siri

$
0
0
Veronica Paschal (29) mkazi wa Kishili jijini Mwanza ametolewa kopo la mafuta ya kujipaka mwilini katika sehemu za siri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwaeleza ndugu zake kuwa anataka kujifungua kopo.

Licha ya kutolewa kopo hilo, daktari aliyekuwa zamu katika kituo cha afya Igoma jijini hapa, Zaitun Lionge amelieleza Mwananchi leo Januari 18, 2018 kuwa mimba ya miezi sita ya mwanamke huyo ipo salama.

Tukio hilo la aina yake limetokea jana Januari 17, 2018 baada ya Veronica kufikishwa katika kituo hicho cha afya na ndugu zake waliomtoa kwenye zahanati binafsi.

“Mwanzoni hawakuonyesha ushirikiano ndio tukawambia tutafanyaje. Wakasema kuna kopo kwamba ndugu yao anataka kujifungua kopo, tukauliza kopo linazaliwaje? Amehoji na kuongeza,

“Tukawambia hilo kopo halijaingia lenyewe mtakuwa mmeliweka wenyewe. Kopo lilikuwa halionekani lakini anavyojaribu kusukuma likatokezea.”

Amesema walipomchunguza kwenye vipimo ndipo walipolibaini kopo hilo la mafuta ya kujipaka mwilini, kwamba baada ya kulitoa waliita Polisi kuchukua maelezo ya mhusika na ndugu zake.

Amesema ujauzito wa mwanamke huyo uko salama kutokana na njia kutofunguka baada ya kuondolewa kopo hilo.

UFAFANUZI: Mama Aliyesemekana Amejifungua KOPO Mwanza.

$
0
0


Kutoka Kituo cha Afya Igoma Mwanza, Mama mwenye umri wa miaka 29, ambaye ana ujauzito wa miezi 6, amekwenda kituo cha Afya kuomba ajifungue Kopo ambalo anadai aliota usiku amewekewa.

 AyoTv tumefika katika kituo cha Afya na tumezungumza na wahusika ili kuweza kufahamu ukweli, Zaithuni Lihonge ndiye alikuwa Daktari wa zamu katika kituo hicho cha afya ambaye alishughulika na zoezi zima la kumhudumia mama huyo, Bonyeza PLAY kumtazama akielezea hali halisi.

VIDEO:

Simba Yaonyesha Ubabe Wake Mbele ya Kocha Mpya Yaiadhibu Singida United Bila Huruma

$
0
0
Simba Yaonyesha Ubabe Wake Mbele ya Kocha Mpya Yaiadhibu Singida United Bila Huruma
Klabu ya Simba leo imepiga klabu ya Singida United bao 4- 0 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara ambao umechezwa katika uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na kocha Mkuu mpya wa Simba Mfaransa Pierre Lechantre.


Katika kipindi cha kwanza cha mchezo mshambuliaji mahiri Kichuya aliweza kuwaamsha mashabiki wa Simba ndani ya dakika ya tatu ya mchezo kwa goli la kwanza la kuongoza ambalo aliweza kulifunga kwa mtindo wa sarakasi na kumpoteza goli kipa wa Singida United Manyika Jr.

Mchezo uliendelea kuwa wa kasi na Simba kuonekana kutawala mchezo na kupelekea kuongeza furaha ya mashabiki wa klabu hiyo baada ya Beki wa Simba Asante Kwasi kuifunga goli la pili Singida United katika dakika ya 23 ya mchezo.

Mpaka wanakwenda mapumziko Simba tayari walikuwa wametangulia kwa goli 2-0 dhidi ya Singida United, katika kipindi cha pili cha mchezo Simba walionyesha uhai na nguvu zaidi ya mashambulizi na kupelekea mshambuliaji wa Kimataifa Emmanuel Okwi kuitandika goli ya tatu Singida United katika dakika ya 75.

Okwi aliongeza goli lake la pili katika mchezo huo katika dakika ya 82 ya mchezo na kupelekea klabu yake kuibuka na ushindi wa bao 4-0 dhidi ya Singida United

Alikiba Ashambuliwa na Mashabiki Kisa Lulu

$
0
0
Alikiba Ashambuliwa na Mashabiki Kisa  Lulu
KATIKA kile kilichoonekana kwamba amemkumbuka aliyewahi kuwa mpenzi wake zamani  ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani, Elizabeth Michael ‘Lulu’, staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba hivi karibuni alishindwakuficha hisia zake na kuweka picha ya mrembo huyo ambapo baadhi ya mashabiki walimshambulia huku wengine wakimpongeza.

Kiba aliweka picha hiyo ya Lulu kwenye ukurasa wake wa Instagram bila kuandika kitu chochote na kupata mashabiki wengi ambao walianza kuchangia huku wengine wakimnanga kwamba huenda anatafuta kiki na wengine wao wakionesha kusikitishwa na Lulu kuwa gerezani. “Sisi tunataka kazi mpya hatutaki mambo haya, au ni kiki! Kama ni Lulu basi tunaomba mtuletee picha mpya za alivyo sasa huko gerezani jamani,” yalisomeka baadhi ya maoni.


Lulu Diva Afunguka Kuhusu Kufunga Ndoa

$
0
0
Lulu Diva Afunguka Kuhusu Kufunga Ndoa
BAADA ya staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kufunga ndoa na Uchebe, msanii anayekimbiza na Ngoma ya Give It To Me, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefungukia upande wa maisha yake kwamba acha waoane wao lakini kwake noo!

Akizungumza na Showbiz, Lulu aliyewahi kuwa muuza nyago kwenye video za Kibongo alisema kuwa, hafikirii maisha ya ndoa wala kuwa na uhusiano na staa Bongo kwani atapata presha tu.

“Kama kuoana acha waoane wao lakini kwangu noo! Nimeingia kwenye muziki kwa hiyo focus yangu yote ipo hapo, sijawahi kufikiria hata kuwa na mpenzi msanii,” alisema Lulu Diva.

Hans Poppe Amzawadia Gari Said Ndemla

$
0
0
Hans Poppe Amzawadia Gari Said Ndemla
Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla.
Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, leo.
Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi.
Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla.
“Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema.
“Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.”
Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba. Alianza na Hussein Zimbwe aliyempa gari aina ya Toyota Raum. Lakini akaonyesha gari aina ya Toyota Lactic na kusema atapewa mchezaji atakayefanya vizuri.
Kuhusiana na aina, leo amesema: “Aina utaijua baadaye ila gari haiko mbali. Hivyo tutaangalia siku yenye nafasi atakabidhiwa.”

Waziri Mkuu wa New Zealand Afunguka Kuwa Mjamzito

$
0
0
Waziri Mkuu wa New Zealand  Afunguka Kuwa Mjamzito
Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern amefichua kwamba yeye ni mjamzito.

Bi Ardern alisema kwamba yeye na mpenzi wake Clarker Gayford walikuwa wakitarajia mwana wao mwezi Juni ambapo baadaye atachukua likizo ya wiki sita.

''Na tulidhani kwamba mwaka 2017 ni mwaka mkuu'', aliandika katika mtandao wake wa Instagram.

Bi Ardern mwenye umri wa miaka 37 alikuwa waziri mkuu mwenye umri mdogo nchini New Zealand tangu 1856 akiungwa mkono wakati alipotangaza kuhusu hali yake mpya siku ya Ijumaa.

Chama cha leba cha Bi Ardern kilikuwa cha pili katika uchaguzi wa mwezi Septemba ambapo hakuna chama kilichofanikiwa kupata wingi wa kura.

Aliunda serikali kupitia usaidizi wa Winston Peters ambaye ni kiongozi wa chama kidogo cha New Zealand.

''Nitakapokuwa ugenini Bwana Peters atakuwa kaimu waziri mkuu, akifanya kazi na ofisi yangu mbali na kuwasiliana nami'', alisema bi Ardern katika taarifa ilioripotiwa na gazeti la New Zealand Herald siku ya Ijumaa.

''Nitawasiliana na kupatikana katika kipindi hicho cha wiki sita wakati nitakapohitajika''.

Bi Ardern alisema kuwa aligundua kwamba ni mjamzito siku sita kabla ya kujua kwamba atakuwa waziri mkuu , na lilikuwa swala la kushangaza.

''Mimi sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi mbili.Sio mwanamke wa kwanza kufanya kazi huku nikihudumia mwanangu, kuna wanawake wengi ambao wamekuwa katika hali kama hii awali'', alisema.

''Bwana Gayford atakuwa baba ambaye atakuwa akisalia nyumbani'', aliongezea.

Mawaziri 2 wakuu wa zamani nchini humo walikuwa watu wa kwanza kutoa pongezi zao.

Mtoto wa Miaka 11 Ajiua Baada ya Ombi Lake Kukataliwa

$
0
0
Mtoto wa Miaka 11 Ajiua Baada ya Ombi Lake Kukataliwa
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 11 ameamua kujiua baada ya ombi lake la kuhamishwa shule kukataliwa huko nchini Kenya.


Taarifa zinasema kuwa mtoto huyo kutoka kijiji cha Ongata Rongai amechukua uamuzi huo mgumu baada ya mama yake kumuambia hana uwezo wa kumpeleka shule binafsi anayotaka, na kumtoa kwenye shule ya umma aliyokuwa akisoma.

Baada ya mama yake kutoka kwenda dukani moto huyo ambaye ni wa kwanza kuzaliwa kwenye familia ya watoto watatu, alichukua kamba na kujinynga sebuleni kwao, na mama mtu kukuta mwili wa mtoto wake ukining'inia.

Kwa mujibu wa mama wa mtoto huyo hakukuwa na ugomvi wowote baina yao zaidi ya kushindwa kutekeleza ombi lake, na jeshi la polisi kuanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo, kwani wanashindwa kuelewa kwa nini mtoto huyo hakwenda shule na kuamua kubaki nyumbani,  wakati shule zimeshafunguliwa.

Iren Uwoya, Dogo Janja Wamfariji Johari Kwenye Msiba wa Mama Yake

$
0
0
Iren Uwoya, Dogo Janja Wamfariji Johari Kwenye Msiba wa Mama Yake
SO SAD! Kufuatia kifo cha mama mzazi wa Staa wa Bongo Movies, Blandina William Wilbert Chagula ‘Johari’, Bi. Asha Chagula, maeneo ya Mburahati, jijini Dar wasanii wenzake Dogo Janja na mkewe Irene Uwoya jana walipata fursa ya kumtia moyo na kumpa nguvu ambapo walimtaka asikate tamaa na achukulie ni hali ya kawaida inayoweza kumtokea binadamu yeyote, wakati wowote.

Baada ya mazishi hayo jana Alhamisi katika Makaburi ya Kisutu, Dogo Janja alisema;

“Taarifa tulizipata mapema alfajiri mimi na mke wangu, na tangu msiba utokee tumekuwa karibu nafamilia tukifarijiana. Anachokihitaji Johari kwa sasa ni faraja, tutaendelea kumfariji hadi pale atakaporudi kwenye hali yake ya kawaida.


Kamati ya Bunge Yahoji Mwekezaji wa Mlimani City Kuja na Mtaji wa Sh 150,000

$
0
0
Kamati ya Bunge Yahoji Mwekezaji wa Mlimani City Kuja na Mtaji wa Sh 150,00
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeutaka uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurekebisha mkataba kati yake na kampuni ya Mlimani Holding Ltd kutokana na upungufu uliojitokeza, huku ikihoji sababu ya mwekezaji huyo kuja na mtaji wa Sh150,000 tu.

Wakizungumza katika kikao cha kamati hiyo kilichoketi eneo la Mlimani City jijinj Dar es Salaam leo Januari 18 wajumbe wa PAC walikosoa pia gawio la asilimia 10 la mapato yote kwa mwaka ambapo Mlimani  City wamekuwa wakikata gharama zao kabla ya kulipa.

Jambo la tatu lililolalamikiwa ni umri wa mkataba ambapo UDSM imetaka upunguzwe kutoka miaka 50 hadi miaka 35.

Mbunge wa Magomeni (CCM) Zanzibar, Jamal Kassim amehoji sababu za chuo hicho kumpokea mwekezaji akiwa na mtaji wa Sh150,000.

"Ukisoma mkataba huu utaona mtaji wa mwekezaji ni Sh150,000 yaani Dola 75. Maana yake mwekezaji hakuja na pesa bali alichukua pesa za upangishaji na kuzifanya kuwa mkopo na anajilipa riba ya mabilioni ya fedha," amesema Kassim.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Naghenjwa Kaboyoka amehoji: "Je, Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilimkubalije mwekezaji mwenye mtaji wa Dola 75 tu? Dhamana ilikuwa nini?"

Hoja hiyo ilimwibua Mbunge wa CCM (Vijana)  , Khadija Naasir akihoji sababu ya mwekezaji huyo kutuma barua pepe kila anapotakiwa kutoa maelezo na UDSM.

Mbunge wa Ulanga Magharibi Dk Haji Mponda amesema mkataba huo ni mbovu kwa sababu umeshindwa kuna ardhi iliyopangishwa bila kutumika kwa muda mrefu.

Baada ya hoja za wabunge hao, Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Hilal Aeshi ameitaka kamati kuwaita watumishi wa UDSM walioshiriki kusaini mkataba huo ili wahojiwe na kuchukulia hatua.

"Kwa kuwa waliotia saini mkataba huo wapo, tuwaite Dodoma, wajieleze ili wachukuliwe hatua na Rais. Mimi nilikuwa mjumbe wa kamati ya madini ya Spika, tuliwaita waliohusika wakajieleza," amesema Aeshi.

Hata hivyo baadhi ya wabunge walitaka viongozi wa sasa wa UDSM  wajieleze kabla ya kuwaita wa zamani.

Tofauti na mtazamo wa wabunge hao, Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho anayeshughulikia utawala, Profesa David Mfinanga amekiri kuwa mkataba huo una mapungufu na kwamba wana mgogoro na Mlimani Holding.

Mwanasheria wa Chuo hicho, Profesa Bonaventure Rutinwa amesema tangu alipoteuliwa alianza kuupitia mkataba huo.

"Tangu nilipoteuliwa mwaka jana nilifika ofisini kwa Profesa Rwekaza Mukandala nikamuomba vipaumbele vitano vya kisheria, mojawapo akaniambia ni kuupitia mkataba wa Mlimani," amesema Profesa Rutinwa.

Akifafanua zaidi, Kaimu Katibu wa Baraza la Chuo hicho, Dr Saudin Mwakaje alikiri kuwepo tatizo la mtaji na kwamba walishaiambia kamati hiyo.

Awali Mkurugenzi wa mipango na maendeleo wa chuo hicho, Pancras Pujuru amesema Mlimani Holding iliingia mkataba huo mwaka 2004 ukiwa katika sehemu mbili ambapo sehemu ya kwanza ulihusu kati yake na UDSM na sehemu ya pili ilikuwa kati yake na Serikali kupitia kituo cha
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images