Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Asha Baraka Amjia Juu Alichoki "Sitaki Ali Choki Afie Kwangu''

$
0
0
Asha Baraka Amjia Juu Alichoki "Sitaki Ali Choki Afie Kwangu''
Baada ya msanii wa mziki wa Dance Ali Choki kupiga stori na eNEWZ wiki chache zilizopita na kusema mwaka 2018 atafanya kazi zake mwenyewe kama Mama Asha Baraka ataendelea kulala, kiongozi huyo wa Twanga Pepeta amemjibu Choki.


Mama Asha Baraka baada ya kusikia kauli hiyo  amesema anamshangaa sana Ali Choki kusema maneno hayo kwani tangu mwaka jana alishamruhusu akafanye kitu anachotaka hata kama ikiwa ni pamoja na kazi zake binafsi.

''Namshangaa sana Ali Choki mimi nishampa ruhusa afanye kazi nyingine yoyote bila kujali mkataba wetu unasemaje hivyo yeye aendelee na mambo yake wala asinifikirie'' amesema.

Asha Baraka pia amesema kuwa hataki Ali Choki afie Twanga Pepeta hivyo kama ana uwezo arudi akaifufue  Extra Band kwani alimpa uongozi ndani ya Twanga Pepeta akashindwa kuiongoza.

Ali Choki tayari ameshaonekana akiingia  studio na msanii Beka Flavour kuandaa kazi zake binafsi hivyo huenda akawa tayari ameshajiandaa na maisha bila ya Twanga Pepeta. Zaidi tazama eNEWZ ya EATV.


Bodi ya Filamu Wamaliza Beef na Kampuni ya Utaarishaji wa 'Filam Utu Wangu'

$
0
0
Bodi ya Filamu Wamaliza Beef na Kampuni ya Utaarishaji wa 'Filam Utu Wangu'
Bodi ya Filamu Tanzania (KBF) kupitia kwa Katibu Mtendaji wake Bibi. Joyce Fissoo, wamefanikiwa kumaliza tofauti zilizokuwepo kati ya Sikujua Mbwembe ambaye ni mtayarishaji wa filamu ya ‘Utu Wangu’ dhidi ya Kampuni ya Steps
Entertainment.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Dilesh Solanki
akibadilishani mihutasari ya kikao cha usuluhi wa madai ya msanii wa filamu Sikujua Mbwembwe

Sikujua alikuwa na tofauti na kampuni hiyo ya usambazaji wa filamu kutokana na kuidai fedha zake kutoka kwenye filamu hiyo ambapo kutokana na kikao hiko ameahidiwa kulipwa fedha zake hizo anazodai kuanzia February 5 ya mwaka huu.



Soma barua hiyo hapo chini.

Hatimaye Bodi ya Filamu nchini imerejesha furaha kwa msanii na mtayarishaji wa filamu ya Utu Wangu kufuatia kuongoza kikao cha usuluhishi kilichofikia muafaka kwa msanii huyo kulipwa stahiki zake.

Hayo yamejitokeza leo wakati wa kikao cha usuluhishi wa madai ya Msanii Sikujua Mbwembe mtayarishaji wa Filamu ya Utu Wangu dhidi ya Kampuni ya Steps Entertainment kilichofanyika katika ofisi za Bodi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

“Nitumie fursa hii kumshukuru Dilesh Mkurugenzi wa Steps kwa kukubali wito lakini pia kukiri kuwa msanii huyu hajalipwa stahiki zake na kuamua kumaliza suala hili kwa kumlipa kwa jasho lake Bibi. Sikujua” alisema Mama Fissoo.

Mama Fissoo ameishukuru Kampuni ya Steps kwa hatua ilizochukua na kusema kuwa huo ni muendelezo way ale ambayo walikubaliana huko awali ikiwemo kuwalipa wale wote wanaoidai Kampuni hiyo jambo ambalo wameanza kulitekeleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Steps Entertainment Dilesh Solanki amesema kuwa wao kama kampuni inayojihusisha na mambo mbalimbali ikiwemo usambazaji wa filamu hawafurahishi na kuona wana ingia migogoro na wasanii kwa hao ndio wateja wao muhimu.

Aidha amesema kuwa shida ambayo ilipelekea kutoka kwa tatizo la malipo kwa msanii huyo ni kitendo cha kuwepo kwa mtu wa kati ambaye kwa kiasi kikubwa bndiye amekuwa akifanya mawasiliano nao tofauti na mhusika mkuu.

Kwa upande wake Msanii Sikujua Mbwembwe ameishukuru Serikali kupitia Bodi ya Filamu kwa kusema kuwa ameamini kweli kwamba Awamu ya Tani ni Serikali ya kutetea wanyonge ndiyo maana leo hii haki yake anaenda kuipata kwani ameangahika kwa muda mrefu sana.

“Binafsi nipende kuchukua fursa hii kuishukuru sana Serikali kupitia Ofisi yetu ya Bodi ya Filamu Tanzania, nimeleta malalamiko yangu tumekaa vikao vitatu haki yangu imepatikana keli Mungu ni mwema sana” alisema Bi. Sikujua.

Sikujua Mbwembe ni msaani mwenye ulemavu wa miguu ambaye alitayarisha filamu yake ya Utu Wangu na kuingia mkataba na Kampuni ya Steps Entertainment na kukutana na misukosuko katika malipo yake hata hivyo hii inaonyesha alipita katika njia zisizo sahihi, pamoja na yote hayo baada ya kuwasilisha madai yake katika mamlaka husika suala lake limeshughulikiwa na sasa anataraji kulipwa fedha zake na kunufaika na jasho lake mwenyewe.

Kigwangalla Awataja Vigogo Watano Waliochukua Maeneo ya Hifadhi Akiwemo Lowassa na Sumaye

$
0
0
Kigwangalla Awataja Vigogo Watano Waliochukua Maeneo ya Hifadhi Awataja Lowassa na Sumaye
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema vigogo watano ni miongoni mwa wanaotajwa kuwa ni kati ya watu 83 waliochukua maeneo na kujenga nyumba katika kiwanja cha Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro (NCAA), wakiwamo mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.

Akizungumza na wajumbe wa bodi mpya ya NCAA aliyoizindua jana, Dk Kigwangalla alisema mwingine ni Daniel Ole Njoolay ambaye aliwahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Arusha, ambaye alisema ameshangazwa na madai hayo.

Aidha, Lowassa kupitia kwa mwanae, Fredrick ambaye ndiye msemaji wa familia amepangua tuhuma hizo huku Sumaye ambaye alikuwa waziri mkuu tangu mwaka 1995 hadi 2005, akisema atamburuza mahakamani Dk Kigwangalla kwa maelezo kuwa hana nyumba katika eneo hilo wala jijini Arusha.

“Nimewataja hawa baadhi, najua kuna wengine, sasa naipa jukumu bodi na menejimenti kuendelea kuwataja na hatua za kurejesha ardhi zianze,” alisema.

Waziri huyo alisema tayari ameshamueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi juu ya mgogoro huo.

Alisema anajua njama zilizotumika kugawa eneo hilo la ekari 20 kati ya 40 kwa kuwa jiji la Arusha lilikuwa halina uwezo wa kugawa eneo ambalo si lake.

“Jiji wamegawa eneo hili mwaka 1996 wakati likiwa chini ya umiliki wa Shirika la Taifa la Utalii lililobinafsishwa na NCAA walinunua hili eneo mwaka 2006,” alisema.

Lakini, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Juliana Peter alisema walipata viwanja hivyo baada ya jiji kutangaza kuvigawa wakifuata taratibu zote, “Mzazi wangu ndiye alinunua kiwanja na najua ana hati hivyo sisi si wavamizi.”

Majibu ya Sumaye, Lowassa, Njoolay

Akizungumzia tuhuma hizo Sumaye huku akicheka alisema, “...Nitampeleka mahakamani. Nyinyi cha kufanya andikeni hicho alichokisema vizuri ili nimpeleke mahakamani. Sina nyumba yoyote Arusha sasa kama anadhani yeye kazi yake ni kuwachafua watu acha aendelee, nampeleka mahakamani.”

Fredrick katika ujumbe wake alioutoa mara baada ya baba yake kutajwa alisema, “Nimesikia taarifa za Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha.”

Alisema amesikitishwa na matamshi hayo akisema hakutarajia kutolewa na mtu mwenye wadhifa wake.

Alisema Dk Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina wataalamu wenye uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

“Nikiwa kama msemaji wa familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa,” alisema, “Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Kigwangalla hayapo na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.”

Baadaye waziri huyo alimjibu mtoto huyo wa Lowassa akisema, “Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha.
Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa sababu kuna majina mengi makubwa yanasemwa... Hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa.”

Njoolay, ambaye pia amewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Mwanza na Rukwa alisema, “Nimesikitishwa sana na tamko la waziri. Niliwahi kuwa kiongozi serikalini, siwezi kuwa mvamizi kwa sababu Jiji lilitangaza viwanja na sisi tukaomba na kupatiwa kama wananchi wengine. Kigwangalla kama alitaka kupata ukweli angekutana na sisi kwanza. Akitaka kupata ukweli aunde kamati ndogo ambayo itabaini ukweli. Kusikiliza kabla ya kutuhumu ndio utawala bora. Tunajua Serikali haifanyi kazi kwa matamko kama suala hili lipo tunasubiri barua kutoka serikalini.”

Maagizo kwa bodi mpya

Mbali na kuitaka kufuatilia suala hilo la ardhi, Dk Kigwangalla ameitaka, “kusaidia kusimamia mali za NCAA lakini pia kuongeza siku za watalii kukaa Ngorongoro kutokana na kuongeza vivutio.”

“Pia mnapaswa kukaa na jamii kuboresha mahusiano ili ule mpango wa Ngorongoro wa miaka 10 ufanikiwe, hivyo mnapaswa kukaa na jamii kutafuta namna bora ya kujenga mahusiano kupitia miradi ya maendeleo,” alisema.

Agizo la Polisi palepale

Dk Kigwangalla alirejea agizo lake kwa Jeshi la Polisi kutaka liwakamate watuhumiwa wanne kwa madai ya kushiriki katika mtandao wa ujangili ndani ya siku saba.

Alitoa agizo hilo Januari 25 na kusisitiza kwamba jeshi hilo likishindwa kuwakamata, atalishtaki kwa Amiri Jeshi Mkuu ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk Kigwangalla alisema jana kwamba anasubiri siku saba zifike na kama hatua zitakuwa hazijachukuliwa atafikisha suala hilo kwa Rais John Magufuli.

“Uamuzi wangu niliotangaza Januari 25 upo palepale nilitoa siku saba hazijafika ila zikifika kama hakuna hatua nitampelekea Rais jambo hili,” alisema.

Alisema ana imani kubwa na Polisi kuwa itazifanyia kazi taarifa alizotoa.

Hata hivyo, siku moja baada ya kutoa agizo hilo, msemaji wa jeshi hilo, Barnabas Mwakalukwa alisema halifanyi kazi kwa matamko, bali kwa kufuata kanuni, taratibu na sheria za kuanzishwa kwake.

Mwananchi lilipomtafuta Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba kujua utekelezaji wa agizo la Waziri Kingwangalla alisema atafutwe Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro.

Hata hivyo, IGP Sirro alipopigiwa simu yake ya kiganjani hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kuhusu utekelezaji wa agizo hilo hakuujibu.   

Breaking News: Necta Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne

$
0
0
Breaking News: Necta Yatangaza Matokeo ya Kidato cha Nne
Matokeo ya kidato cha nne yametangazwa rasmi na Katibu Mkuu wa Necta,  Dk Charles Msonde na aliyengoza kitaifa ni Ferson Mdee kutoka Marian Boys.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Siku ya Leo Jumanne

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba, Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

$
0
0
Ni dawa ya nguvu za kiume inayorefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo (Inch 1-7) kwa muda wa siku 6 tu.Dozi hii itakufanya uchelewe kufika kileleni kwa muda wa dakika 30, utarudia tendo la ndoa zaidi ya mara 4 bila hamu kuisha bila kujali umri na garantee ni miaka 60 baada ya kutibu tatizo.

Pia tunatibu Busha bila kufanyiwa Oparesheni, korodani moja kuvimba, ngiri, tumbo kujaa gesi na kuunguruma, kutopata choo vizuri, miguu kuwaka moto na kufa ganzi, chango la wanawake, kisukari na kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa.

MIHAYO:
Inarudisha mke, mchumba, hawara na atakutimizia kila kitu unachotaka kutoka kwake ndani ya  saa 2 tu hata kama yupo mbali. atarudi na kumfunga asiwe na mwingine zaidi yako.

Umefukuzwa kazini? unataka kupandishwa cheo? Umepoteza pesa zako kwenye biashara bila kujua umepandikizwa chuma ulete? Njoo urudishe pesa zako. Unauza mali yako haiendi?


Wasiliana na mtaalam Challo kwa; 0714006521 

Wauza Nguo Mtandaoni Wamuingiza Mjini Shilole "Nikirudia Tena Labda Mimi Sio Da Mwajuma"

$
0
0
Wauza Nguo Utandaoni Wamuingiza Mjini Shilole


Mwanadada shilole amejikuta akiingizwa mjini na wafanyabiashara wa mtandaoni baada ya kuagiza nguo aliyoipenda na kuletewa nguo tofauti na hiyo iliyoonekana kutoipenda.


Shilole alishindwa kujizuia kuonyesha hisia zake na kuamua kuandika ujembe kwenye ukrasa wake wa istagramu.

Aliandika "Yaani kama ntaagiza nguo mimi mitandaoni tenaaaaaaaa walah labda mimi sio dada Mwajuma" akuishia hapo alipost picha yake aliyovaa nguo hiyo na kuandika "mwanamke mtindi babu weee"


Hofu Yatanda Kenya Mamia ya Watu Wafurika Kushuhudia Kuapishwa kwa Odinga

$
0
0
Hofu Yatanda Kenya Mamia ya Watu Wafurika Kushuhudia Kuapishwa kwa Odinga
Hofu ya kuzuka kwa vurugu nchini Kenya imezidi kutawala wakati mamia ya watu wakifurika katika viwanja vya Uhuru Park kushuhudia tukio la kuapishwa kwa kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, Raila Odinga.

NASA wamepanga kumuapisha Raila Odinga kama Rais wa Kenya huku wakidai kuwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta mwezi Oktoba 2017 haukuwa wa halali na wa haki hivyo kukataa matokeo hayo.

Hata hivyo, Serikali nchini humo imesema haitambui sherehe hizo za kuapishwa kwa Raila Odinga ingawaje imeuruhusu umoja huo kutumia viwanja vya Uhuru Park.








Lowassa, Njoolay Watupilia Mbali Tuhuma za Kigwabgalla ..... Sumaye Ahaidi Kumfikisha Mahakamani

$
0
0
Lowassa, Njoolay Watupilia Mbali Tuhuma za Kigwabgalla ..... Sumaye Ahaidi Kumfikisha Mahakamani
Familia ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Sumaye na  na Njoolay imetupilia mbali madai yaliyoelekezwa kwake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamis Kingwangalla, jana.

Katika madai yake aliyoyatoa wakati wa kuzindua Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Njiro mjini hapa, Dk. Kigwangalla alidai Lowassa ni sehemu ya watu waliojipatia eneo katika eneo la mamlaka hiyo.

Msemaji wa familia ya Lowassa, Fredrick Lowassa, alitupilia mbali madai yaliyotolewa na Dk. Kigwangalla huku akisema familia yao inatambua kumiliki eneo hilo kihalali.

Akizungumzia tuhuma hizo Sumaye huku akicheka alisema, “...Nitampeleka mahakamani. Nyinyi cha kufanya andikeni hicho alichokisema vizuri ili nimpeleke mahakamani. Sina nyumba yoyote Arusha sasa kama anadhani yeye kazi yake ni kuwachafua watu acha aendelee, nampeleka mahakamani.”

Fredrick katika ujumbe wake alioutoa mara baada ya baba yake(Lowassa) kutajwa alisema, “Nimesikia taarifa za Kigwangalla akitaja jina la Lowassa kama mmoja ya watu eti walioshiriki kupora ardhi Arusha.”

Alisema amesikitishwa na matamshi hayo akisema hakutarajia kutolewa na mtu mwenye wadhifa wake.

Alisema Dk Kigwangalla anatumia vibaya dhamana aliyopewa na Rais John Magufuli kwa mambo ambayo Wizara ya Ardhi ina wataalamu wenye uwezo wa kuchukua hatua stahiki kwenye mgogoro wowote.

“Nikiwa kama msemaji wa familia ninazo katika kiganja cha mikono yangu taarifa zote za umiliki wowote unaomgusa Lowassa,” alisema,

“Ninaweza kuuhakikishia umma kwamba yote aliyosema Kigwangalla hayapo na kama anayo basi sisi tuko tayari afanye lolote lililo chini ya mamlaka yake badala ya kurejea kule tulikopita ambako yeye na wenzake kadhaa walifanya bila mafanikio kuchafua heshima za wote anaowataja bila sababu.”

Baadaye waziri huyo alimjibu mtoto huyo wa Lowassa akisema, “Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha.

"Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa sababu kuna majina mengi makubwa yanasemwa... Hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa.”

Njoolay, ambaye pia amewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Mwanza na Rukwa alisema, “Nimesikitishwa sana na tamko la waziri. Niliwahi kuwa kiongozi serikalini, siwezi kuwa mvamizi kwa sababu Jiji lilitangaza viwanja na sisi tukaomba na kupatiwa kama wananchi wengine.

"Kigwangalla kama alitaka kupata ukweli angekutana na sisi kwanza. Akitaka kupata ukweli aunde kamati ndogo ambayo itabaini ukweli. Kusikiliza kabla ya kutuhumu ndio utawala bora. Tunajua Serikali haifanyi kazi kwa matamko kama suala hili lipo tunasubiri barua kutoka serikalini.”

Baada ya Kifungo Kumalizika Mdee, Bulaya Watinga Bungeni

$
0
0
Baada ya Kifungo Kumalizika Mdee, Bulaya Watinga Bungeni
Kifungo walichokuwa wakitumikia wabunge wa Chadema, Ester Bulaya (Bunda Mjini) na Halima Mdee (Kawe) cha kutohudhuria shughuli za Bunge  kimemelizika na leo Januari 30, mwaka 2018 wamehudhuria kikao cha kwanza kwa Bunge mjini Dodoma.

Wabunge hao waliingia katika ukumbi wa Bunge saa 3:28 asubuhi na kushangiliwa kwa makofi, mengi kutoka kwa wabunge wa upinzani huku wabunge wachache wa chama tawala wakitoa kauli za kuwatania.

Wabunge hao waliadhibiwa kwa azimio la Bunge Juni 5 mwaka jana kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge ambayo ni jumla ya siku 47, waliyokosa ukiondoa shughuli zote za mikutano ya kamati za Bunge.

Adhabu hiyo ilikwenda sanjari na kulipwa nusu mshahara na posho kwa kipindi chote walichotumikia adhabu hiyo wakituhumiwa kudharau kiti cha spika.

Mikutano mitatu waliyoikosa ni wa bajeti uliokuwa ukiendelea, wa saba uliofanyika kati ya Septemba 5 hadi 15 na mkutano wa tisa wa Novemba 7 hadi 17.

Vituo vya Habari Vyafungiwa Matangazo Nchini Kenya

$
0
0
Kituo cha Citizen TV,  Citizen Radio Vimezimwa na Serikali Nchini Kenya
Vituo vya Citizen TV na Citizen Radio vimezimwa na serikali nchini humo tukio ambalo limehusishwa moja kwa moja na kurushwa kwa matangazo ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Raila Odinga.

Citizen TV na Radio walikuwa wakirusha Live tukio la kuapishwa kwa Raila Odinga katika viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam.

Kupitia tovuti ya Citizen TV imeeleza kuwa tukio hilo limekuja siku moja baada ya Serikali kupitia Mamalaka ya Mawasiliano nchini humo (The Communications Authority of Kenya) kutoa onyo kwa vyombo vya habari vitakavyorusha matangazo ya kuapishwa kwa Odinga.

Kiwango cha Kufaulu Mtihani wa Kidato cha Nne Waongezeka kwa Asilimia Saba

$
0
0
Kiwango cha Kufaulu Mtihani wa Kidato cha Nne Waongezeka kwa Asilimia Saba
Baraza la Mitihani la Tanzania limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) leo Januari 30, 2018 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na mwaka jana 2016.


Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde ametangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam na kusema ufaulu kwa wanafunzi umeongezeka kwa asilimia 7 ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana.

"Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09%  kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7" alisema Msonde

Mbali na hilo Msonde aliweza kuweka wazi kuwa jumla ya wanafunzi 265 wamebainika kufanya udanganyifu mbalimbali katika mitihani hiyo ambayo ilianza kufanyika Oktoba 30, 2016 mpaka Novemba 17, 2016

"Afrika Yaazimia Kuzalisha Umeme"- Majaliwa

$
0
0
"Afrika Yaazimia Kuzalisha Umeme"- Majaliwa
Waziri Mkuu Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.

Waziri Majaliwa ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza baada ya mkutano wa viongozi wa wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli na kusema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.

Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

"Nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia mapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa ina mikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali", alisema Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita ambapo ni pamoja na tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.

"Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC", alisisitiza Majaliwa.

Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo  kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

Maelfu Waliodhulumiwa Wazidi Kumiminika Ofisini kwa RC Makonda

$
0
0
Maelfu Waliodhulumiwa Wazidi Kumiminika Ofisini  kwa RC Makonda
Zaidi ya wananchi 3000 Jumanne hii wamejitokeza kwa wingi ikiwa ni siku ya pili ya utatuzi wa malalamiko ya kisheria kwa wananchi waliodhulumiwa chini ya wanasheria magwiji 160 ikiwa ni Mkakati wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kusaidia wanyonge waliodhulumiwa mali zao kupata haki pasipo kuvunja sheria.

Wananchi hao wametaabika kwa muda mrefu baada ya kudhulumiwa Mali zao Walizochuma kwa Tabu na sasa kupitia huduma ya Masada wa kisheria uliotangazwa na RC Makonda wanaamni watarejeshewa haki yao.

RC Makonda amesema idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza leo inatoa picha kamili Kuwa wapo viongozi wasiotekeleza vyema majukumu yao ya kiofisi kwenye idara zao ambapo ameahidi kuwawajibisha.

Aidha RC Makonda amesema kilichomgusa kuandaa Wiki ya msaada wa kisheria ni baada kubaini uwepo wa wananchi wanaonyanyasiki na hata kufikia hatua ya kufa kwa presha au kupooza miili baada ya kudhulumiwa na watu wenye pesa au wanaotumia uelewa wa sheria kukandamiza wanyonge.


Kutokana na idadi kuwa kubwa wanaoendelea kujitokeza RC Makonda anaongeza wanasheria wengi zaidi ili kuhakikisha Kila anaefika na kupata namba anahudumiwa ipasavyo ambapo amewaomba wanasheria kuhakikisha wanawasikiliza wananchi kwa umakini na kuchambua nyaraka kwa ufasaha na wasitoe hukumu.

Makonda amesema katika zoezi hili limehusisha Wanasheria wabobezi, Wataalamu wa kutambua nyaraka zilizogushiwa, watendaji wa Ardhi na watumishi wa Mahakama ambao wapo kwaajili ya kuwahudumia Wananchi. RC Makonda amesema baada ya kupokea ripoti kamili ya kesi zote atasimama kuhakikisha Hakuna mnyonge anabaki akinyanyasika.



Zoezi la kusikiliza wananchi waliodhulumiwa Mali zao ikiwemo Nyumba, Viwanja, Magari, Mirathi na Kazi litaendelea hadi siku ya Ijumaa ya February 02.

Nao wananchi waliojitokeza wamemshukuru RC Makonda kwa kutambua Tabu wanazozipata baada ya kudhulumiwa na wajanja ambapo wengine wamesema wamepoteza Waume, Wake zao na wengine kupata magonjwa baada ya kudhulumiwa na wametaabika Muda mrefu kutafuta haki pasipo kufanikiwa lakini kupitia utendaji kazi makini wa RC Makonda wanaamni haki inapatikana.

Yanga Kibaruani Leo Dhidi ya Ihefu FC

$
0
0
Yanga Kibaruani Leo Dhidi ya Ihefu FC
Mabingwa wa kwanza wa Kombe la Shirikisho, klabu ya Yanga SC leo inashuka dimbani kuvaana na timu ya Ihefu FC ya Wilayani Mbarali  jijini Mbeya kwenye mchezo wa hatua ya 32 ya michuano hiyo.

Msimamo wa ligi kuu soka Tanzania Bara utaifanya Yanga itolee macho zaidi mechi ya leo ili iweze kusonga mbele kwaajili ya kuusaka ubingwa ili kujihakikishia uhakika wa michuano ya kimataifa mwakani. Hadi sasa Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa nyuma ya Simba na Azam FC.

Michuano hiyo ambayo bingwa wake huwa anapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa leo itashuhudiwa mechi saba zikichezwa katika viwanja tofauti.

Klabu ya Ihefu imetinga hatua hii ya 32 baada ya kuitoa Mbeya City katika hatua iliyopita hivyo mechi haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa kikosi hicho ambacho kitakuwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Sokoine jijini Mbeya.

Tayari bingwa mtetezi wa michuano hiyo Simba SC ameshaondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kukubali kichapo kutoka kwa timu ya Green Worriors ya Dar es salaam kwenye hatua iliyopita.

Ratiba kamili ya leo

Ihefu FC Vs Yanga SC
JKT Tanzania Vs Polisi Dar
Polisi Tanzania Vs Friends Rangers
Shupavu FC Vs Azam FC
Ndanda FC Vs Biashara
Kariakoo Lindi Vs Mbao FC
Kagera Sugar Vs Buseresere

Maskini..Elias Maguri Amekwama Usajili South Africa

$
0
0
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Elias Maguri bado yupo nchini licha ya awali kuripotiwa kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki ligi kuu South Africa.

Prisca Kishamba kupitia Sports Xtra ya Clouds FM amepiga story na Maguri ambaye ameelezea kinachomfanya aendelee kuonekana kwenye mitaa ya jiji la Dar es Salaam na sababu iliyopelekea ashindwe kujiunga na klabu ya Polokwane.

“Watu wengi wanategemea kwamba mimi nipo South Africa, lakini kuna sababu ambazo zimenifanya niendelee kuwepo hapa mjini. Awali ilikuwa nimehitajika Polokwane City na nilishasaini mkataba wa awali ambao tulikuwa tumekubaliana wakati nikiwa naenda kwenye mashindano ya Challenge Cup nchini Kenya.”

“Badae niliondoka kwa ajilki ya kwenda kumalizana na watu wa Polokwane nikaiacha timu (Taifa Stars) ikiwa bado kwenye mashindano, lakini kilichotokea kule (South Africa) ndio kinanifanya niendelee kuwa hapa mjini, nilipofika kule makubaliano tuliyokubaliana awali nikaambiwa inabidi kiwango cha fedha kishuke kitu ambacho mimi na wakala aliyenipeleka hatukukubaliana.”

“Kwa sababu klabu na mchezaji wakifikia hatua ya kusaini mkataba wa awali maana yake wameshakubaliana kila kitu lakini mabadiliko ya makubaliano yaliyokuwa yanatakiwa yafanyike baada ya kufika kule ndiyo kitu ambacho hatukukubaliana nacho kwa sababu ukiangalia pia nilikuwa natakiwa nilipe kodi tofauti na ilivyokuwa kule Uarabuni ambako hakukuwa na masuala ya kodi. Unaweza ukajikuta unarudi hapa hauna kitu kwa sababu kiasi kikubwa cha fedha kimetumika kwenye kulipa kodi.”

Maguri amesema kuna ofa kadhaa zipo licha kwamba dirisha la usajili limefungwa kwa hapa nyumbani lakini pia hatokaa tu nyumbani kusubiri hadi dirisha la usajili litakapofunguliwa.

“Ofa zipo licha kwamba tayari dirisha la usajili limeshafungwa kwa hapa nyumbani lakini kuna ofa nyingi ambazo zipo, kwa kuwa mimi ni mchezaji sitoweza kukaa tu nje kwa muda wote huo mpaka dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa, bado kuna michakato inaendelea hadi sasa na mambo yatakapokuwa yamekamilika nitaweka wazi wapi naelekea.”

“Sasa hivi ndiyo watu wanaweza kuwa wanapata habari kwamba nipo nyumbani kwa sababu wengi wanajua nipo south Africa kutokana na taarifa zilizokuwepo hapo mwanzo, kabla ya hapo kulikuwa na vilabu vingi vya hapa nyumbani ambavyo vilitaka nikafanye kazi kwao lakini baada ya kutoka taarifa kwamba naenda nje hata ule mtafutano ukaisha.”

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Madogo?

$
0
0

KWA NINI BAADHI YA WANAUME WA NA MAUMBILE MADOGO?

Matatizo haya yame kuwa yakiwaathiri watu wengi sana kisaikolijia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wenzao kwa kawaida mwanaume ana takiwa awe na uume kuanzia inch(6_8)vinginevyo mtu huyo atakuwa na matatizo.

Zipo sababu nyingi zinazo sababisha tatizo hilo baadhi ni upungufu wa vichocheo (Hormones za Getrogen) Ambazo mwanaume akisha balehe vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume, chango husababisha NEVA ambayo huathiri misuri ya uume. Ngiri ambayo Huleta maumivu ya tumbo kuunguruma na kujaa guess, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri , miguu kufa ganzi, maumivu ya kiuno,upigaji wa punyeto sababu hizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembaba na mara kwa mara hipelekea kupunguka kwa nguvu za kiume na ham ya tendo la ndoa hukosekana na kuisha kabisa

NSUMBU:__Ni dawa dawa inayo zalisha hormones za Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka mara dufu.

NZAGI :--Ni dawa bora ya kurudisha nguvu za kiume na kukupa hamu ya kurudia tendo la ndoa mara dufu utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara nne
(4)bila hamu kuisha (kuchoka) dawa hii ni tiba kamili kwa matatizo hayo. Dawa hii pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk(15_30)kwa tendo moja la ndoa dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji kuanzia miaka(18_90)wana ruhusiwa kuzitumia Pia tunatibu KISUKARI, PRESHA, PUMU, MALARIA SUGU, MIMBA KUHARIBIKA(Chango)

POWER :__Ni dawa ya mitishamba inaongeza hips, (makalio), miguu, ina punguza maziwa (chuchu). Ina toa harufu mbaya sehem za siri Nk.

Pia anazo dawa za mvuto wa mapenzi,biashara, kurudishwa kazini, kumuita aliye mbali kwa mda mfupi tu

OSTADH JUMA ANAPATIKANA MBANGALA ZAKHIEM SIMU: 0769-597778 au 0784-002216 au 0627457957 Wote mnakaribishwa

Raila Odinga Ajiapisha kwa Kushika Biblia

$
0
0
Raila Odinga Ajiapisha kwa Kushika Biblia
Raila Odinga amefika katika pamoja na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia.

Amewaambia kuwa mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.

Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo.

Bw Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.

Aslay Atamani Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph......... Amuomba Amuombee Dua

$
0
0
Aslay Atamani Kufuata Nyayo za Mzee Yusuph......... Amuomba Amuombee Dua
Msanii wa bongo fleva ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha 'Subalkheri mpenzi' alichoshirikiana na mwanadada Nandy, Aslay amemuomba Mzee Yusuph amuombee dua ili nae siku itakapofika basi arudi katika dini japo kwa sasa hajatizamia hilo.


Aslay ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo minong'ono ya chini kwa chini kwamba msanii huyo ameishiwa ubunifu katika kazi zake mpaka kufikia hatua ya kuiga uimbaji wa aliyekuwa muimbaji maarufu wa taarabu Alhaji mzee Yusuph ambae kwa sasa anafanya shughuli zake za kidini.

"Wengi wanafikilia hivyo lakini hata kama nimemuiga Mzee Yusuph sio mbaya maana ukisikiliza 'original' ya wimbo wa Subalkher ni vile vile kama nilivyo imba mimi. Wao walivyokuwa wanaimba ni 'melody' na njia zile zile ambazo sehemu nilizokuwa navuta nawao wanavuta", alisema Aslay.

Pamoja na hayo, Aslay amesema endapo Mzee Yusuph atamsikia basi yeye anamuombea dua katika harakati zake za kila siku.

"Mimi namuombea kwa Mwenyezi Mungu Alhaji Mzee Yusuph anaendeleea na dini na inshallah atuombee na sisi wengine endapo tutakapoona sasa hapa kuna haki ya kumrudia kwenye dini nasi twende. Siwezi sema chochote kwa sasa juu ya hilo suala kwa sababu bado sijajua nini nafanya kutokana na mimi kijana na nina vitu vingi vya kufanya",alisisitiza Aslay.

Kwa upande mwingine, Aslay amewaahidi mashabiki zake hatoweza kuwaangusha katika utendaji kazi wake kwa kuwa hao ndio anawategemea katika kazi zake za muziki.

David Beckham Afunguka Kuhusu Sanchez Kusajiliwa Man U

$
0
0
David Beckham Afunguka Kuhusu Sanchez Kusajiliwa Man U
Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya England, David Beckham amezungumzia usajili wa Alexis Sanchez kutua katika timu hiyo akitokea Arsenal.

Nahodha huyo wa zamani wa England amemzungumzia mchezaji huyo wakati wa uzinduzi wa klabu yake Miami huko nchini Marekani, “Mpaka sasa nashindwa kuamini kwa kile kilichotokea hakika,” amesema Beckham.

Beckham ameongeza “Wakati alipokuwa sehemu ya timu kubwa kama ya Arsenal na mara ghafla akaama kwa muda mchache tu na kuelekea kaskazini katika klabu kubwa ni ajabu kushuhudia hilo.”

“Sote tunamtakia mafanikio, mimi ni shabiki wa Manchester United hivyo ninafurahi kuona timu yangu imefanikiwa kumpata mchezaji mwenye uwezo na kipaji kama yeye,”

 Mshambuliaji huyo raia Chile mwenye umri wa miaka 29 ametua United mwanzoni mwa juma lililopita huku akifanikiwa kulipwa paundi 600,000 kwa wiki mshahara paundi 350,000, haki ya matangazo paundi 100,000 na paundi 144,000 kama nyongeza.
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images