Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live

Hizi Hapa Shule 10 Bora Zilizoongoza Matokeo ya Kidato cha Nne

$
0
0
Hizi Hapa Shule 10 Bora Zilizoongoza Matokeo ya Kidato cha Nne
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani ambao ulifanyika October 2017 ambapo Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.

TOP 10 YA SHULE BORA.

1. St. Francis Girls ya Mbeya

2. Feza Boys ya Dar es salaam

3. Kemebos ya Kagera

4. Bethel Sabs Girls ya Iringa

5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro

6. Marian Girls Pwani

7. Canossa ya Dar es salaam

8. Feza Girls ya Dar es salaam

9. Marian Boys ya Pwani

10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam

TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA
10. Mtule ya Kusini Unguja

9. Nyeburu ya Dar es salaam

8. Chokocho ya Kusini Pemba

7. Kabugaro ya Kagera

6. Mbesa ya Ruvuma

5. Furaha ya Dar es salaam

4. Langoni ya Mjini Magharibi

3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi

2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja

1. Kusini ya Kusini Unguja


Maskini!.... Kichanga cha Miezi Nane Amebakwa

$
0
0
Maskini!.... Kichanga cha Miezi Nane Amebakwa
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 28 anashikiliwa na polisi nchini India kwa kumbaka mtoto wa miezi 8 ambaye ni binamu yake, na kumsababishia majeraha makali yanayohatarisha usalama wake huko Shakurbasti kaskazini Magharibi mwa mji wa Delhi.


Taarifa kutoka nchini India zinasema kwamba mama wa mtoto huyo alikuwa ameenda kazini na kumuacha na wifi yake ambaye ndiye alitakiwa kumuangalia, lakini alichukuliwa na binamu yake aliyesema anakwenda naye chumbani kucheza naye, na kisha kumfanyia kitendo hiko cha kikatili.

Baada ya kurudi kazini mama wa mtoto huyo alimkuta mtoto wake ana damu mwilini huku akilia na sehemuzake za siri kuonekana zimevimba, ndipo alipoamua kumkimbiza hospitali, na baada ya vipimo mtoto huyo alionekana amebakwa na kujeruhiwa.

Kijana anayehusika na tukio hilo ambaye ni ndugu yao wanayeishi naye nyumba moja alikimbia, lakini polisi walifanikiwa kumkamata na kukiri kufanya tukio hilo.

Mtoto huyo bado yuko katika hospitali ya Kalawati Saran anakoendelea kupatiwa matibabu, huku madaktari wakisema kwamba hali yake bado ingawa yuko salama

Aunt Ezekieli Afunguka Ugomvi Wake na Mose Iyobo "Hata Vikombe Vinagongana ila hata Iweje Siwezi Kumuacha"

$
0
0
Aunt Ezekieli Afunguka Ugomvi Wake na Mose Iyobo "Hata Vikombe Vinagongana ila hata Iweje Siwezi Kumuacha"
Muigizaji Aunty Ezekiel amefunguka na kusema kuwa yeye na Mose Iyobo walipishana ambapo Mose alimjibu yeye vibaya ndipo akachukua maamuzi ya kuandika vile katika ukurasa wa instagram lakini pamoja na hayo Aunty Ezekiel amesema kuwa hawezi kuachana na Mose hata iweje licha ya kwamba amemzidi umri.

Aunty Ezekiel ameyazungumza hayo kwenye Exclusive interview wakati wa utambulisho wa msanii mpya wa WCB ambaye ni Maromboso ndipo Aunty akasema kuwa..>>>“Waswahili wanasema hata vikombe vinagongana mimi na Mose ni binadamu tupo karibu miaka minne so kitu hakiwezi pita bila kugombana, Huwa na muweka chini naongea naye mchana kweupe ila mimi na mose hatuwezi kuachana”

Odinga: Tunachokifanya si Mapinduzi ya Serikali

$
0
0
Odinga: Tunachokifanya si Mapinduzi ya Serikali
Bw Raila Odinga amezungumza na kituo cha habari cha KTN kwa njia ya simu ambapo amesisitiza kwamba Rais Uhuru Kenyatta hakuchaguliwa kwa njia halali.

Alipoulizwa anni atamwapisha, amesema: "Ngoja uone” na akasisitiza kwamba wanachokifanya leo kina msingi wake katika sheria na si mapinduzi.

“Hatutambui uchaguzi wa Oktoba 26 (uchaguzi wa marudio ambao Odinga alisusia), zaidi ya asilimia 86 ya Wakenya hawakushiriki. Tuna serikali ambayo si halali ambao inajidai kuwa mamlakani,” amesema.

Kuhusu taarifa kwamba amepokonywa walinzi, amesema: "Walinzi wangu waliondolewa muda mrefu sana uliopita. Najihisi kuwa hatarini ndio lakini watu raia ndio usalama wangu.”

Bw Odinga ameitaka serikali kutotumia nguvu kuusambaratisha mkutano wa leo.

"Wafuasi wangu wamo safarini kuelekea Canaan. Safari yetu ni halisi na haiwezi kuzuiwa.

Article share tools
Sambaza habari hii FacebookSambaza habari hii Twitter

Chenge Awachukiza Upinzani...... Wasusia Kusoma Maoni Yao Bungeni

$
0
0
Chenge Awachukiza Upinzani......  Wasusia Kusoma Maoni Yao Bungeni
Msemaji wa upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria, Ally Salehe amesusa kusoma maoni ya upinzani ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kukataa kusomwa kwa baadhi ya maneno yaliyomo katika maoni hayo.

Salehe alikuwa akisoma maoni hayo leo Januari 30 mwaka 2018 kwa niaba ya msemaji wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu aliyeko nchini Ubelgiji kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi Novemba 7 mwaka jana.

Maneno yaliyozuiwa na Chenge kusomwa na upinzani ni kuhusu matukio ya uhalifu nchini, likiwemo la kushambuliwa kwa Lissu.

Salehe alianza kusoma maneno hayo lakini alipofika aya ya nne alikatizwa na Chenge akimtaka asubiri, baadaye kumueleza kuwa lugha iliyotumika katika ukurasa kwa kwanza na pili wa hotuba hiyo si ya kibunge.

Baada ya kauli hiyo, Salehe amesema upinzani unaiamini na unaisimamia hotuba hiyo kwa kuwa wabunge wote wanayo nakala yake, akaomba kuiwasilisha na kurejea kuketi.

Serikali Yakubali Maoni ya Wabunge..... Yafuta Mamlaka ya Waziri, Umri wa Kustaafu

$
0
0
Serikali Yakubali Maoni ya Wabunge..... Yafuta Mamlaka ya Waziri, Umri wa Kustaafu
Serikali imekubali maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria ya kukifuta kifungu kilichokuwa kikimpa mamlaka Waziri wa Utumishi na Rais kubadili umri wa kustaafu kwa mtumishi wa umma.

Muswada wa Sheria Mbalimbali Namba 5 wa Mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria ya utumishi kwa lengo la kubadili umri wa kustaafu kwa baadhi ya kada za utumishi wa umma.

Kada zinazopendekezwa kuongozewa umri wa kustaafu kutoka miaka 55 hadi 60 kwa hiari na 60 hadi 65 kwa lazima ni maprofesa, madaktari bingwa na wahadhiri waandamizi  wa vyuo vikuu vya umma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju amesema bungeni leo Jumanne Januari 30,2018 kuwa kifungu kipya cha 25B ambacho kilikuwa kinapendekeza umri wa kustaafu kimefutwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohamed Mchengerwa amesema kamati haikuona haja ya kuwa na kifungu hicho kipya kwa sababu kinaweza kutumika vibaya kwa sababu mfanyakazi husika hapewi nafasi ya kushirikishwa katika uamuzi.

Zitto Ataja List ya Viongozi Ambao Atawateua Ikitokea Amekuwa Rais wa TZ

$
0
0
Zitto Ataja List ya Viongozi Ambao Atawateua Ikitokea Amekuwa Rais wa TZ
Mchana wa leo January 30, 2018 kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika watu ambao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali za serikali kama atakuwa Rais wa Tanzania.

Ameandika kuwa atamchagua Mwanaharakati Maria Tsehai Sarungi kuwa Balozi wa Umoja wa Taifa huku Kaimu wake akiwa Mwanzilishi wa Nyama Choma Festival Carol Ndosi.

Amewataja pia Mbunge wa  Arumeru Mashariki Joshua Nassari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu kuwa atawachagua kuwa Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ulinzi wa Jamii na Biashara za Umma).

Zitto pia amewataja Mbunge wa Tarime Esther Matiko kuwa Waziri wa TAMISEMI, na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) mkoa wa Geita Upendo Peneza kushika nafasi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hata hivyo Zitto ameongeza kuwa ambaye atamteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hamtaji jina lakini yeye mwenyewe anajijua.

Raila Odinga Apuuza Kauli ya Serikali...Adai Kuapishwa Kwake ni Alali

$
0
0

Kiongozi wa Muungano wa Upinzani (NASA), Raila Odinga amejitokeza katika viwanja vya Uhuru na kuapishwa kama Rais wa Watu wa Kenya.
-
Viongozi wengine wa Muungano huo, wakiwemo Kalonzo Musyoka, amabye ndiye alitarajiwa kuapa kama Makamu wake, Musalia Mudavadi na Moses Wetang'ula hawakuepo katika tukio hilo lililochukua chini ya dakika 10.
-
Kiongozi huyo alipuuza madai sherehe hizo za kuapishwa ni jaribio la kuipindua serikali na kuongeza upinzani utauonyesha Ulimwengu kuwa kuapishwa huko ni sahihi kisheria

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam

Watuhumiwa Waliovua Nguo Mahakamani Wafungwa Miezi Sita

$
0
0
Watuhumiwa Waliovua Nguo Mahakamani Wafungwa Miezi Sita
Watuhumiwa 24 kati ya 61 wanaokabiliwa na kesi za ugaidi jijini hapa wamehukumiwa kifungo cha miezi sita jela  kwa kosa la kuvua nguo na kisha kugoma kuingia ndani ya chumba cha mahakama kusikiliza kesi zinazowakabili.

Hukumu hiyo imetolewa leo Januari 30   katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Nestory Baro ambapo amesema kwamba watu hao wamehukumiwa kwa mujibu wa kifungu nambari 114 (a) cha mwongozo wa mashtaka ya jinai.

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo baadhi ya watuhumiwa  wamevua  nguo zao na kubakisha  nguo zao za ndani wakati wakipandishwa kwenye karandinga  wakati wakirejeshwa katika gereza kuu la mkoa wa Arusha.

Awali kabla ya kusoma hukumu hiyo mwendesha mashtaka wa Serikali ,Augustino Kombe ameiomba mahakama hiyo iwachukulie hatua kali na kutoa adhabu kwa watuhumiwa wa kesi hizo wanaogoma mahakamani.

Mara baada ya kauli hiyo ndipo Hakimu Baro akasema kwamba anatoa kifungo cha miezi sita kwa watuhumiwa hao  ili iwe fundisho kwa wengine watakaoonyesha vitendo hivyo ambavyo amesema sio vya kistaarabu.

“Kugoma sio ustaarabu kabisa halafu tuone mwisho wake hili ni fundisho kwa wote watakaogoma tena sasa muende jela miezi sita halafu mrudi na zile nguo za magereza” amesema Baro

Waliohukumiwa ni Rajabu Yakubu, Swalehe Hassan, Anwar Mashali, Jafari Lema, Abdul Hamid, Mgaya Mgaya, Abdallah Rabia, Hassan Said, Abdallah Juma, Maka Gewa, Sudi Nassib na Swalehe Hamis.

Wengine ni pamoja na Hamad Issa,Yassin Mohammed, Hamad Yahya, Juma Nguli, Khalid Makame, Shaban Wawa, Yassin Sanga, Ally Hamis, Ibrahim Lend, Rajab Hemed, Shaban Masu sanjari na Mohammed Nuru.

Mara baada ya kutoa hukumu hiyo Hakimu Baro aliahirisha kesi inayowakabili watuhumiwa hao hadi Februari  13 mwaka huu kwa madai kwamba upelelezi juu ya shauri lao bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao 61 wanakabiliwa na kesi ya kujihusisha na vitendo mbalimbali vya kigaidi ambapo kati ya hao watuhumiwa 23 wanatuhumiwa kwa kesi ya ugaidi nyumbani kwa Sheikh Sudy Ally Sudi julai 13 mwaka 2014.

Watuhumiwa hao wanatuhumiwa kufanya njama ya kufanya vitendo vya kigaidi nyumbani kwa Sheikh Sudi Julai 3, 2014 wakituhumiwa kurusha bomu la mkono na kumjeruhi kiongozi huyo huku baadhi yao wakituhumiwa kutoa msaada wa fedha kufadhili mpango huo.

Watuhumiwa wengine 13 wanatuhumiwa kufanya mauaji na kujaribu kuua ambapo kati ya mwaka 2014 watuhumiwa hao waliwaua Judith Mushi, Ramadhan Juma ,Fahad Jamal na Amir Daffa katika uwanja wa Soweto jijini Arusha.

Watuhumiwa 10  wanatuhumiwa kukusanya zana, kukutwa na zana na kusambaza zana yakiwemo mabomu mawili kati ya Julai 22 na 23 mwaka 2015 kwa lengo la kufanya ugaidi.

Watuhumiwa wanne kati ya 61 wanatuhumiwa kwa kosa la ugaidi ambapo kati ya Julai 2009 na Julai 2013 katika eneo la msikiti mkuu wa Arusha wanadaiwa kumwagia tindikali Mustapha Kiago na kumsababishia majeraha mwilini.

Watuhumiwa wengine wanne wanatuhumiwa kufanya vitendo vya ugaidi kati ya oktoba mosi na 25 mwaka 2012 nyumbani kwa Sheikh Abdulkarim Njonjo ambapo wanatuhumiwa kutupa bomu la kienyeji lililomjeruhi Sheikh Njonjo na kumsababishia majereha mwilini.

Watuhumiwa wengine watatu katika kesi hizo wanatuhumiwa kati ya machi 8 na julai 14 mwaka 2014 waliwashawishi vijana kujiunga na kikundi cha kigaidi cha Al-Shabaab.

Hapa Ndipo Ilipofikia Hali ya Msanii Radio.... Kufanyiwa Maombi Maalum Kwaajili ya Kuokoa Uhai Wake

$
0
0
Hapa Ndipo Ilipofikia Hali ya Msanii Radio.... Kufanyiwa Maombi Maalum Kwaajili ya Kuokoa Uhai Wake
Wadau wa burudani na mashabiki wa mwanamuziki Radio wanatarajia kufanya maombi maalum kumuombea msanii wa Mowzey Radio, ambaye amelazwa hospitali akiwa kwenye comma.


Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv  kwa njia ya ujumbe mfupi wa WhatsApp , msemaji wa kundi la Goodlyfe, amesema maombi hayo yanatarajiwa kufanyika Jumapili ya Januari4, katika kanisa la Light the World.

“Maombi yameandaliwa kufanyika kwenye kanisa la Light the World lililopo Nansana, ambalo linaongozwa na Wilson Bugembe, kwa ajili ya kumuombea kaka yetu Radio, na wote wanakaribishwa kuhudhuria”, amesema msemaji huyo.

Radio alikimbizwa hospitali wiki iliyopita baada ya kupata comma kutokana na kupigwa vibaya sehemu ya kichwani kwenye ugomvi, akitokea kwenye hoteli moja nchini Uganda, na mpaka sasa bado anaendelea kupigania maisha yake, ambapo hapo jana amefanyiwa upasuaji kwa mara ya pili.

Serikali: Hatuna Mpango Kurejesha Fedha za Sarafu

$
0
0
Serikali: Hatuna Mpango Kurejesha Fedha za Sarafu
Serikali ya Tanzania imesema haina mpango wa kurejesha fedha za sarafu ndogo kuanzia senti tano hadi shilingi 20 katika mzunguko wa fedha kutokana na ubebaji wake kuwa mgumu.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, leo Bungeni mjini Dodoma (Jumanne) katika mkutano wa 10 wa Bunge kwenye kikao chake cha kwanza wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Mhe. Salma Kikwete ambaye alitaka kujua ni kwa nini serikali haioni kuwa ni wakati muafaka kurudisha sarafu hizo katika mzunguko wa matumizi kutokana na kuwapo na bei za shilingi zinazohitajika kuwapo na senti.

"Benki kuu ya Tanzania imepewa kisheria jukumu la kuzalisha fedha za noti sarafu kulingana na mahitaji pamoja na mazingira ya kiuchumi yaliyopo. Mambo muhimu ambayo yanazingatiwa wakati wa kuondoa na kuingiza katika soko noti na sarafu ya thamani ndogo na kubwa ni mfumuko wa bei wa bidhaa za huduma, kulinda thamani na wepesi wa sarafu kubebeka", alisema Dkt. Ashantu Kijaji.

Pamoja na hayo, Dkt. Ashantu Kijaji aliendelea kwa kusema "kwa kuwa hatuna sera ya kupanga bei za bidhaa na huduma kwa sasa ni vigumu kurejesha sarafu hizo katika mzunguko wa fedha kwa njia iliyopendekezwa na Mbunge Salma Kikwete"

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango amesema sarafu hizo zitaweza kurudi katika mzunguko wa fedha kwa urahisi endapo pale teknolojia ya kufanya miamala ya fedha kwa njia ya mitandao itasambaa nchini kote na jamii kuwa tayari kufanya miamala hiyo kwa njia ya mitandao.

Shilole Afunguka Kuhusu Yaliyomkuta Kwenye Nguo Aliyoagiza Mtandaoni

$
0
0
Shilole Afunguka Kuhusu Yaliyomkuta Kwenye Nguo Aliyoagiza Mtandaoni
Msanii wa muziki bongo asiyeisha vituko, Zuwena Mohamedi maarufu kama Shilole, ameweka wazi janga lililomkuta kwenye nguo aliyovaa ambayo imeonekana kuwaacha watu midomo wazi huku wakimcheka.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Shilole amesema nguo hiyo aliagiza mtandaoni, lakini matokeo yake ilikuja kumbadilikia baada ya kuvaa.

“Kwaweli haya mambo ya kununua vitu mitandaoni yamenicost, nguo mimi nimeiona nikaagiza ikaja, nikajaribu siku ya kwanza ikanikaa vizuri tu, siku ya sherehe nikasema nivae leo ile gauni, nikavaa na ikanikaa vizuri tu, sasa balaa likaja kadri ninavoenda na yenyewe inashuka, nikasema hili sasa balaa na nishafika kwenye sherehe, ndio hivyo”, amesema Shilole.

Kufuatia tukio hilo Shilole amepost kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa hatokuja kurudia kuagiza nguo za mitandaoni, kuepuka lililotokea.

Wanaonizungumzia Mabaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio Anajua- Wastara

$
0
0
Wanaonizungumzia Mabaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio  Anajua- Wastara
Msanii wa filamu nchini Wastara Juma Sajuki ambaye sasa anasumbuliwa na maumivu ya mguu na mgongo amefunguka na kusema kuwa watu ambao wanazungumza mabaya juu yake hawezi kuwachukia ila yeye amemwachia Mungu ndiye ajuaye yote.

Wastara amesema hayo wakati akiongea na www.eatv.tv na kusema anawashukuru sana Watanzania na Rais Magufuli kwa moyo wao wa upendo na kujali matatizo yake kwani licha ya watu kumzungumzia kwa mabaya lakini bado wanaendelea kujitoa kwa msaada na kwenda kumuona jambo ambalo linazidi kumpa faraja.

"Nawashukuru na wao kwa changamoto wanayotoa kwa upande wangu nimeweza kujifunza kitu wakati wewe una tatizo lolote kuna watu hakuamini, inawezekana watu hao unaishi nao, unatembea nao au unawachukulia ni watu wema lakini mwisho wa siku wamevaa ngozi tu ya kondoo ndani yake wana mioyo ya chui. Kwa sababu mtu kusema anaumwa anaweza kuangaliwa na jamii nzima hivyo mtu yoyote anaweza kunitembelea na kunishuhudia sasa kivipi unaweza kuidanganya jamii.

Wastara aliongeza kuwa "Niseme tu wao waendelee kutoa changamoto kama ambavyo wameamua lakini wajue kwenye matatizo Mungu pia anahusika, anaweza kutoa mitihani, anaweza kukupima imani hivyo huwa hayaji kwa mtu mmoja leo yapo kwangu mimi lakini kesho yanaweza kumkuta mtu anayempenda yeye au yakamgusa huyo huyo mzungumzaji sijui atakuwa na wakati gani? Ila mimi namuachia Mungu yeye ndiye atajua atahukumu nini kwa watu ambao wanaongea 'negative' ila mimi siwezi kuwachukia ila naamini Mungu anajua fungu lao ni lipi" alisisitiza Wastara

Aidha Wastara amesema kuwa kwa sasa maandalizi yake ya safari kwenda kwenye matibabu yanaendelea vizuri na kama mambo yatakamilika huenda Jumapili ya tarehe 4 Februari 2018 ataanza safari kuelekea India kwa matibabu.

NECTA Watangaza Matokeo ya Kidato Cha Nne 2017....Bofya Hapa Kuyatazama

$
0
0
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.


==>Yatazame Matokeo hapo chini


Shule 10 BORA na Shule 10 za Mwisho Matokeo ya Kidato cha Nne 2017

$
0
0
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani ambao ulifanyika October 2017 ambapo Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.

TOP 10 YA SHULE BORA.

1. St. Francis Girls ya Mbeya

2. Feza Boys ya Dar es salaam

3. Kemebos ya Kagera

4. Bethel Sabs Girls ya Iringa

5. Anwarite Girls ya Kilimanjaro

6. Marian Girls Pwani

7. Canossa ya Dar es salaam

8. Feza Girls ya Dar es salaam

9. Marian Boys ya Pwani

10. Shamsiye Boys ya Dar es salaam

TOP 10 YA SHULE ZA MWISHO KITAIFA

10. Mtule ya Kusini Unguja

9. Nyeburu ya Dar es salaam

8. Chokocho ya Kusini Pemba

7. Kabugaro ya Kagera

6. Mbesa ya Ruvuma

5. Furaha ya Dar es salaam

4. Langoni ya Mjini Magharibi

3. Mwenge S.M.Z ya Mjini Magharibi

2. Pwani Mchangani ya Kaskazini Unguja

1. Kusini ya Kusini Unguja

Matokeo Kidato cha Nne 2017: Wanafunzi 10 BORA waliofanya vizuri na shule wanazotoka

$
0
0
Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne kwenye mtihani ambao ulifanyika October 2017.

==>Watahiniwa 10 waliofanya vizuri na shule wanazotoka ni kama ifuatavyo;

1.Felison Mdee -Marian boys
2.Elizabeth Mango -Marian girls
3.Anna Benjamin Mshana - Marian girls
4.Emanuel Lameck Makoye -Ilboru
5.Lukelo Thadeo Luoga-Ilboru
6.Fuadi Padic -Feza Boys
7.Godfrey Mwakatage -Uwata
8.Baraka Mohammed -Angels
9.Lilian Moses Katabaro -Marian girls
10.Everlyn Moses Mlowe -St. Fransis Mbeya

JE, Unaupungufu wa Nguvu za Kiume, Hamu ya Tendo la Ndoa au Maumbile Madogo ya Uume?

$
0
0

JE, UNA UPUNGUVU WA NGUVU ZA KIUME, HAMU YA TENDO LA NDOA AU MAUMBILE MADOGO YA UUME?
SOMA HAPA👇👇.
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa limezidi kuongezeka kwa kasi duniani kote na limekuwa chanzo kikubwa cha ndoa nyingi na mahusiano kukosa uaminifu kutokana na wengi kutoka nje ya ndoa ili kupata mtu atakayemtosheleza na kumfikisha kileleni. Pia udogo wa maumbile ni tatizo kubwa na limekuwa likiwakosesha wanaume wengi uwezo wa kujiamini katika tendo na kusababisha tendo hilo kutokufanyika kwa usahihi. Hili pia huchangia kwa kiasi kikubwa wanawake wengi kwenda nje ya ndoa ( MAHUSIANO) kutafuta mbadala wake.

BAADHI YA DALILI ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI KAMA:-
☆Kukosa hamu ya tendo la ndoa
☆Uume kusimama kwa ulegevu
☆Kuwahi kufika kileleni
☆Uume kusinyaa katikati ya tendo
☆Kushindwa kurudia tendo kwa wakati
☆Kuchoka sana baada ya round ya kwanza na hata kukinai kabisa.

Kwa kutumia mimea na matunda bila kemikali 🍇🍍🍓🌿🍉🍒🍎🍑 @markson_beauty_pr Tunakuletea suluhisho la matatizo hayo hata kwa wenye "KISUKARI NA PRESSURE" kwa:-
1.HANDSOME UP ORIGINAL:- kifaa chenye uwezo wa 99% kuongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @250,000/=
2.SHARK POWER ni gely ya kupaka inayoongeza uume kwa wastani wa inch 5.5 hadi 6 @150,000/=
3.VigRX CREAM:- ni gely iliyoboreshwa mahususi kwa ajili ya kuongeza maumbile kwa wastani wa inch 6.5 hadi 8 na kuimarisha misuli ya uume iliyolegea @200,000/=
4.Vidonge maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu na hamu ya tendo la ndoa hata kwa wenye kisukari @150,000/=
5.Spray ya kuchelewesha kufika kileleni na kuweza kurudia tendo ×3. @150,000/=
BIDHAA HIZI HAZINA MADHARA KIAFYA NA ZIMETHIBITISHWA
NA SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO).
KWA BIDHAA HIZI NA NYINGINE NYINGI TEMBELEA UKURASA WETU WA INSTAGRAM :-
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
@markson_beauty_pr
WEB:www.markbeauty.org
Wasiliana nasi Popote
ulipo duniani kwa (+255)
0767447444 na
0714335378
UTAPATA HUDUMA
NB:Matokeo ni uhakika na garantii na hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa MARKSON CO pamoja na garantii ili kukuhakikishia kufanikiwa kwako.

Shamsa Ford Apigwa Marufuku Kutumia Mitandao na Mumewe Baada ya Kuambulia Matusi

$
0
0
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford anadaiwa kupigwa stop kutumia mitandao ya kijamii na mumewe, Chid Mapenzi na kwa muda sasa haonekani hasa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram ambako aliwaaga kabisa mashabiki zake.

 Chanzo kilieleza kwamba Chid Mapenzi alimpiga marufuku mkewe Shamsa kutumia mitandao ya kijamii kwa kuwa muda mwingi alikuwa akiutumia kwenye mitandao hiyo huku wakati mwingine akiambulia matusi kutoka kwa mashabiki zake jambo ambalo lilimchefua mumewe huyo na kuamua kumkataza.

Alipoulizwa Shamsa kuhusiana na suala hilo alikiri kwamba ni kweli mumewe alimtaka atoke kwenye mitandao ya kijamii kwa muda mpaka atakapomruhusu tena na hajui sababu za kukatazwa.

 “Kwa sasa naishi kwa amani sana maana nimepumzika na matusi ya mitandaoni siyaoni tena, sijui mume wangu aliona nini ila aliniambia nitoke mpaka atakaponiruhusu tena ndiyo nitarudi,” alisema Shamsa.

Umri wa Kustaafu Kwa Madaktari Bingwa, Wahadhiri Waandamizi na Maprofesa Sasa miaka 65

$
0
0
Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298  (The Public Service Act) itakayowezesha muda wa kustaafu kwa  Wahadhiri waandamizi, Maprofesa na Madaktari Bingwa kuwa miaka 60 kwa hiari na lazima miaka 65.

Akizungumza wakati akiwasilisha muswaada huo  Mwanasheria  Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju amesema kuwa marekebisho katika jedwali yanapendekeza kuongezwa kwa kifungu kipya cha 25A ambacho kinaainisha kuhusu umri wa kustaafu ambapo kwa sasa sheria ilivyo  haina masharti hayo isipokuwa umri wa kustaafu umetajwa katika sheria zinazoanzisha mifuko ya hifadhi za jamii.

Aliongeza kuwa, uzoefu umeonyesha kuwamba Maprofesa na Wahadhiri waandamizi wa vyuo  Vikuu  vya Umma pamoja na madaktari Bingwa wa Binadamu wa Hospitali za Umma wamekuwa wakihitajika kuendelea kutoa huduma, utaalamu na uzoefu wao licha yakufikisha umri wa miaka 60 kwa sasa ya kustaafu na hivyo kulazimika kuajiriwa na Serikali kwa mikataba.

Hatua yakuwaajiri wataalamu hao kwa mikataba baada ya kustaafu imetajwa kuongeza gharama kubwa kwa Serikali ambapo muswaada ulipitishwa  unawezesha Serikali kuokoa Kiwango kikubwa cha fedha zilizokuwa zikitumika katika kuwalipa wataalamu wao mara baada ya kustaafu ili waweze kufanya kazi kwa mikataba.

Kwa upande wake Waziri  wa Elimu Sayansi na Teknplojia mhe. Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa anaunga mkono hoja  yakuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 60 kwa lazima hadi 65 na kutoka miaka 55 kwa hiari hadi miaka 60.

Aliongeza kuwa Serikali inayo mikakati ya makusudi yakuwaendeleza wataalamu wa kada zenye uhaba  wataalamu wabobezi ili kuziba pengo  lililopo.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wake wa 10 kikao cha 1 limepitisha muswaada wa marekebisho ya sheria mbalimbali nne ambazo ni Sheria ya Ufilisi, sura ya 25, Sheria ya Bajeti, sura ya 439, Sheria ya Ardhi, sura ya 113 na Sheria ya Utumishi wa Umma, sura ya 238.
Viewing all 104793 articles
Browse latest View live




Latest Images