Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Baba Ahukumiwa Miaka 50 Jela baada ya Kumuua Mwanaye Akimtoa Mapepo

$
0
0
Baba Ahukumiwa Miaka 50 Jela baada ya Kumuua Mwanaye Akimtoa Mapepo
Mwanaume mmoja nchini Ujerumani mwenye umri wa miaka 5o amehukumiwa kifungo cha miaka tisa jela baada ya kumuua binti yake aliyekuwa na matatizo ya akili kwa kumkanyaga hadi kufa.

Inaelezwa kuwa kutokana na matatizo ya akili ya binti huyo, baba huyo aliamini kuwa mwanaye ana mapepo hivyo kuamua amuombee kwa kumkanyaga ili yamtoke jambo lililosababisha binti huyo kupoteza maisha.

Mwanaume huyo pia alishutumiwa kujihusisha kimapenzi na mtoto wake huyo ambaye hakuwa sawa kiakili, pia akiamini itasaidia kumponya ‘mapepo’ hayo.

Kwenye kusikilizwa kesi hiyo, ilioneshwa video ambayo ilionesha baba huyo amesimama juu ya mwili wa mwanaye huyo wa miaka 26, akimkanyaga tumboni hadi binti huyo kufariki.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Tillerson Augua Ghafla Asitisha Shughuli Alizopanga Kufanya Kenya Leo

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Tillerson Augua Ghafla  Asitisha Shughuli Alizopanga Kufanya Kenya Leo
Waziri wa mambo nje wa Marekani, Rex Tillerson amesitisha shughuli alizokuwa anapaswa kufanya nchini Kenya kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa nzuri.

Hakuna ishara yeyote inayoainisha kuwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 anasumbuliwa na tatizo kubwa la kiafya.

Msemaji wake amesema,Tillerson amekuwa kwenye ratiba ngumu katika ziara yake ya Afrika wakati huo huo akitumia muda mwingi kwenye mazungumzo ya simu kufuatilia kazi nyingine nchini mwake kama vile suala la Korea Kaskazini.

Maasifa wamesema watahairisha baadhi ya ratiba ambazo bwana Tillerson alikuwa ameweka ikiwa ni pamoja na safari yake ya kwenda kuona eneo ambalo ubalozi wa Marekani ulikuwa umelipuliwa mwaka 1998.

Rex Tillerson amekuwa katika ziara ya mataifa matano ya Afrika tangu siku ya jumatano akiwa ameanzia Ethiopia na sasa yuko Kenya kwa siku ya pili.


Tanesco Waanika Chanzo cha Kukatika kwa Umeme

$
0
0
Tanesco Waanika Chanzo cha  Kukatika kwa Umeme
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema chanzo cha kukatika kwa umeme usiku wa kuamkia leo Machi 10, 2018 kumetokana na hitilafu katika mfumo wa gridi ya Taifa.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Machi 10, 2018 inaeleza kuwa hitilafu hiyo imesababisha  kukosekana kwa huduma ya umeme katika maeneo na mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi hiyo.

Inaeleza kuwa baada ya hitilafu hiyo kutokea, mafundi na wataalamu wamechukua hatua za haraka na bado wako kazini kuhakikisha kuwa umeme unarejea mapema kadri iwezekanavyo.

“Uongozi wa shirika unaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza. Tafadhali usishike wa kukanyaga waya ulioanguka au uliokatika, ukiuona toa taarifa,” inaeleza taarifa hiyo.

Radio ya Umoja wa Mataifa Yafungiwa

$
0
0
Radio ya Umoja wa Mataifa Yafungiwa
Taarifa kutoka nchini Sudan Kusini ni kwamba Mamlaka ya Vyombo vya Habari nchini humo jana March 9, 2018 imefunga radio inayomilikiwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo, radio hiyo iitwayo Radio Miraya imefungwa kutokana na kushindwa kufuata masharti na sheria za vyombo vya habari nchini humo.

Inaelezwa kuwa chombo hicho cha habari kimekuwa kikipokea vitisho vya kusitishiwa shughuli zake na mamlaka hiyo tangu mwaka 2016 na hatimaye jambo hilo limefanyika.

Akizungumzia suala hilo mbele ya vyombo vya habari, Mkuu wa Mamlaka hiyo Elijah Alier Kuai, ameeleza kuwa radio hiyo imeshindwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria zinazoongoza vyombo vya habari na hiyo ndio sababu kubwa ya kufungiwa.

‘Kuna kikundi kimetumia mtandao wa Telegram kuhamasisha maandamano’-Polisi Makao Makuu

Man U, Liverpool Kuonyeshana Ubabe Leo

$
0
0
LEO Jumamosi saa 9:30, kwe­nye Uwanja wa Old Trafford kutakuwa na mechi kali ya watani wa jadi wanaotoka katika miji tofauti, ndiyo ni North vaWest Derby inayozihusisha Man­chester United na Liverpool.

Hii ni mechi ya Ligi Kuu England maarufu kama Premier League, ambayo kwa msimu huu wa 2017/18, ambapo mshindi wa leo atatoa nafasi ya pili kwa yeyote yule.

North West Derby kwa mara ya kwanza ilichezwa Aprili 28, 1894, katika mechi ya kirafi­ki kuelekea msimu wa ligi wa 1893/94, ambapo Liverpool ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Man United ambayo wakati huo ilikuwa ikiitwa Newton Heath.




Timu hizi mbili ndizo ze­  nye rekodi ya kutwaa mataji mengi nda­ni na nje ya England kwani kwa pamoja zina mataji 38 ya ligi kuu (mengine kabla ya mfumo wa sasa), mataji nane ya Eu­ropa Cup, mataji manne ya Uefa, mataji manne ya Uefa Super Cup na mataji 19 ya Kombe la FA.

Mataji mengine ni 13 ya Kombe la Ligi, moja la Klabu la Fifa, moja la Inter­continental na 36 ya mataji ya Ngao ya Jamii.



MTU AKIPIGWA ANASHUKA

Kwa sasa katika ligi kuu, Man United ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 62 huku Liverpool ikiwa nafasi ya tatu na pointi 60. Man City wao wapo kileleni mwa ligi hiyo wakiwa na pointi 78. Timu zote zimecheza mechi 29.

Kama zikitoka sare, hali itabaki kama ilivyo lakini Man United ik­ishinda itajiimarisha katika nafasi yake ila ikitokea Liverpool ikashinda itaku­wa imepanda hadi nafasi ya pili kwani itafikisha pointi 63.



Liverpool akipoteza atajiweka kwe­nye nafasi ngumu kwani atabaki na pointi 60 huku Tottenham Hotspur mwenye pointi 58 kama akishinda atapanda nafasi ya tatu kutoka nafasi ya nne.


LIVERPOOL FOWADI KIWEMBE, BEKI NYANYA

Safu ya ushambuliaji ya Liverpool ina mabao 67 hadi sasa ambayo ni 11 zaidi ya yale ya Man United am­bayo

ni 56, hii ina maanisha kwamba safu yao ya ush­ambuliaji in­a y ­oongozwa na Mo­hamed Salah n i kali kuliko ya M a n United iliyo chini ya Romelu Lu­kaku.

Licha ya fowadi ya Liverpool kuoneka­na kuwa bora, beki yake ni nyanya kwani imeruhusu mabao 32 huku ile ya Man United ikiruhusu mabao 22 tu ambayo






ni kumi pungufu ya yale ya Liv­erpool. Hivyo, katika mchezo huu Liverpool inaweza ku­pata mabao hata mawili lakini nayo inaweza ku­ruhusu mabao kama hayo.

Man United nao safu yao ya ushambu­liaji haiaminiki sana ila inaweza kubadili ma­tokeo muda wowote ule kwani wachezaji kama Lukaku, Paul Pog­ba, Jesse Lingard, Anthony Martial na Marcus Rash­ford wapo vizuri.

Virgil van Dijk, De­jan Lovren na Nath­aniel Clyne wa­naonekana bado hawana uwele­wano mzuri katika beki ya Liverpool kama ilivyo kwa Vic­tor Lindelöf, Chris Smalling na Phil Jones wa Man United.



HAPA SALAH PALE LUKAKU

Licha ya Salah wa Liv­erpool kufikisha mabao 24 katika ligi kuu hadi sasa huku Lukaku akiwa na mabao 14, hiyo haiwezi kufanya Lukaku aonekane si lolote mbele ya Salah.

Wawili hawa watatazamwa zaidi kwa kila upande katika kuhakikisha ushindi un­apatikana h a s a u k i l i n ­g a n i ­s h a n a mechi z a o zilizopita.



Salah amecheza mechi 28 na kufunga ma­bao 24, akiwa amepata ushindi mara 16, kufungwa mara tatu, lakini ametoa asisti nane na amepiga pasi 758, huku akiwa ameten­geneza nafasi 10.

Amepiga krosi 64, na kati ya mabao 24 aliyofunga kwa kichwa amefunga mara moja, mguu wa kulia mara mbili na k u s h o t o mara 21 na mara moja kwa penalti.



Lukaku yeye, katika mabao yake 14, amecheza mechi 28 na kupata ushindi mara 18, kafungwa mara tano, ana asisti sita, amepiga pasi 618, ametengeneza nafasi saba huku akipiga krosi 28.

Kati ya mabao 14, Lukaku ame­funga matatu kwa kichwa, mawili kwa mguu wa kulia na tisa kwa mguu wa kushoto akiwa hana bao la penalti wala la faulo.



MOURINHO, KLOPP ANA KWA ANA

Wote ni makocha wenye ujuzi wa hali ya juu, lakini wamezidiana mbinu za kimchezo kwani Kocha wa Man United, Jose Mourinho ni mzuri katika kuzuia kwani akipaki basi ni ngumu kumfunga.



Wakati Mourinho ni mjuzi wa ulin­zi, katika ushambuliaji anaonekana si mzuri sana mbele ya Liverpool ndiyo maana ana mabao 56 wakati Liver­pool inayo 67.



Klopp yeye ni mzuri katika kush­ambulia lakini mbovu katika ulinzi ndiyo maana timu yake inapata ma­bao mengi pia inaruhusu mabao mengi, kwa hiyo mechi hii ni tamu kuitazama.



Mechi ni tamu sababu inazikutani­sha timu zenye makali katika mae­neo tofauti, Liverpool ushambuliaji, Man United ulinzi japokuwa wakati mwingine inakuwa nyanya.

MAN UNITED KIBOKO

Katika mechi 51 walizocheza hadi sasa katika mfumo wa sasa wa ligi kuu, Man United imeshinda mara 27 huku Liverpool ikishinda mara 13 na timu hizo zimetoka sare mara 11.



Kati ya ushindi wa mara 27 wa Man United, mara 15 imeshinda ny­umbani na 12 ugenini wakati Liver­pool mara nane imeshinda nyumba­ni na tano ugenini.

ACT Wazalendo Walila na Tatizo la Ajira kwa Vijana

$
0
0
ACT Wazalendo Walila na Tatizo la Ajira kwa Vijana
Ngome ya vijana ya Chama cha ACT Wazalendo imewataka mawaziri wenye dhamana ya kusimamia viwanda, ajira na fedha kukaa pamoja kutafakari tatizo la ajira kwa vijana na kuweka mazingira bora ya ufanyaji wa biashara ndogondogo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Machi 10, 2018, Katibu wa Sera na Tafiti wa Ngome ya vijana wa chama hicho,  Kitentya Luth amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kushuhudia wimbi la waajiri sekta binafsi na Serikali kupunguza wafanyakazi.

"Hata sekta ya elimu na viwanda ambazo awali zilikuwa zinatoa ajira nyingi nazo hali ni mbaya. Walimu hawajapata ajira kwa zaidi ya miaka mitatu, jambo hilo linasababisha mkwamo katika elimu lakini pia vijana hao wanashindwa kujikwamua kimaisha," amesema Luth.

TFF Kuzisaidia Simba, Yanga Michuano ya CAF

$
0
0
TFF Kuzisaidia Simba, Yanga Michuano ya CAF
UONGOZI wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umesema kuwa unajipanga kuhakikisha unazisaidia timu za Simba na Yanga ili zifanye vizuri katika mechi zake za marudiano za michuano ya kimataifa ambazo zitacheza Machi 17, mwaka huu.

Simba itapambana na Al Masry huko nchini Misri wakati Yanga itavaana na Township Rollers huko nchini Botswana.
Katika mechi hizo Simba ambayo ilitoka sare ya mabao 2-2 na Al Masry hapa nchini inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wakati Yanga ambayo ilifungwa mabao 2-1 na Township Rollers katika mchezo wake wa kwanza, yenyewe inashiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, alisema kuwa ili kuhakikisha timu hizo zinasonga mbele katika michuano hiyo wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanazisaidia ziweze kutimiza ndoto hiyo.


Kikosi cha timu ya Yanga.

“Tutahakikisha tunazipatia muda wa kutosha wa maandalizi lakini pia tutatuma wawakilishi wetu katika mechi hizo kwa ajili ya kwenda kuweka mambo sawa ili siku zitakapoenda huko zisikumbane na usumbufu.



“Michuano hii ni ya kimataifa na zikifanya vizuri sifa itakuwa siyo kwa klabu pekee bali kwa taifa zima la Tanzania, kwa hiyo inatubidi tushirikiane nazo kwa karibu kabisa ili kuhakikisha zinapata matokeo mazuri katika michezo yake,” alisema Kidao.



Kutokana na hali hiyo, timu hizo hazitacheza tena mechi zao za Ligi Kuu Bara ambazo zilitakiwa kucheza hivi karibuni mpaka hapo zitakapokuwa zimerudiana na timu hizo katika michuano hiyo ya kimataifa.

Rais Magufuli Aifumua Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali

$
0
0
Rais Magufuli Aifumua Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Rais John Magufuli ameifumua Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na kuanzisha ofisi mbili huru zitakazosimamia mashauri ya jinai na madai ambayo Serikali ina masilahi nayo.

Mabadiliko hayo ambayo yametangazwa hivi karibuni kupitia notisi za Serikali namba 48, 49 na 50, yameeleza muundo mpya wa ofisi hiyo kwa kuanzisha Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Jinai na ile ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Japokuwa ofisi hizo mpya zitakuwa chini ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, mamlaka yake katika kuteua, kuadhibu na kuwasimamia maofisa na wafanyakazi wanaofanya kazi chini ya ofisi hizo yameondolewa.

Chini ya muundo mpya, AG anabaki kuwa mshauri mkuu wa Serikali katika masuala ya kisheria na kiutawala, naibu AG atakuwa mkuu wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

Mabadiliko hayo ni hitimisho la mchakato wa miaka mingi wa mawazo ya wataalamu wa sheria waliopendekeza kutenganishwa kwa jukumu la kusimamia masuala ya madai na yale ya jinai kutoka kwenye usimamizi wa moja kwa moja wa AG.

Masuala hayo sasa yanawekwa chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa wakili mkuu wa Serikali na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya jinai.

Mabadiliko hayo pia yanayaweka mambo yote ya kisheria ambayo si ya kimahakama yanayohusiana na Katiba na haki za binadamu chini ya waziri mwenye dhamana ya katiba na masuala ya sheria.

Ibara ya 36 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inampa Rais mamlaka ya kuanzisha na kufuta nafasi za madaraka ya namna mbalimbali katika utumishi wa Serikali ya Muungano.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ndiye ataongoza Ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka ya jinai.

Ofisi yake itachukua na kuendesha kesi zote za jinai kwa niaba ya Serikali Kuu, idara zake zinazojitegemea, wakala Serikali na Serikali za Mitaa.

Pamoja na kuwasimamia maofisa wa sheria na mawakili wa Serikali walio chini yake, DPP ataratibu na kusimamia uchunguzi wa kesi za jinai na kuendesha mashtaka ya jinai mahakamani.

Kwa upande mwingine, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itakuwa huru na inayojitegemea mbali ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Ofisi hii imeundwa ili kuongeza uwezo wa Serikali katika kuendesha mashauri ya madai yakiwamo ya haki za binadamu na masuala ya kikatiba katika mahakama.

Kama ilivyo kwa DPP, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali itachukua na kusimamia mashauri ya jinai na upatanishi kwa niaba ya Serikali, hivyo kutoa maelekezo kwa maofisa wa sheria, mawakili wa Serikali wanaoendesha masuala ya jinai.

Mwanzoni mwa mwezi uliopita, Rais Magufuli alitoa kauli iliyoashiria mabadiliko makubwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na ile ya DPP baada ya kueleza kutoridhishwa ya utendaji wa ofisi hizo.

“Sitalalamika tena ninajua nitakavyofanya kwa sababu nimeshajifunza vya kutosha,” alisema Rais Magufuli alipohutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini.

Alianza kwa kuwapa pole majaji kwa changamoto wanazokumbana nazo pindi wanapo shughulikia mashtaka yanayopelekwa na Serikali na kuahidi kulifanyia kazi jambo hilo kabla ya Februari kuisha.

Rais Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP na AG ambalo wakati mwingine huwapa majaji changamoto kubwa.

“Najua mnapata shida sana mnapo-deal (mnaposhughulika) na mashtaka yanayoletwa na Serikali, mnauona kabisa ushahidi upo lakini watetezi hawajitokezi hadharani kuutetea.

“Mwaka jana nililalamika lakini mwaka huu nitalishughulikia vizuri. Sitalalamika tena ninajua nitakavyofanya kwa sababu nimeshajifunza vya kutosha na nimejua wapi kuna ‘weakness’ (udhaifu) na wala huu mwezi wa Februari hautoisha.”

Ajari Nyingine Mbaya Yatokea Eneo la Tabata Mwananchi Gari Lafunga Barabara

$
0
0
Ajari Nyingine Mbaya Yatokea Eneo la Tabata Mwananchi Gari Lafunga Barabara
Ajali imetokea leo karibu na Ofisi ya Mwananchi na kufunga barabara baada ya lori lilokuwa limebeba mbao kuacha njia na kugonga nyumba hali iliyosababisha mbao hizo kuanguka chini na kufunga barabara.


Liverpool Ikiifunga Manchester Nahama CCM Najiunga na Chama cha Hashim Rungwe– Haji Manara

$
0
0
Liverpool Ikiifunga Manchester Nahama CCM Najiunga na Chama cha  Hashim Rungwe– Haji Manara

Afisa habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa ikitokea majogoo wa Uingereza, timu ya Liverpool ikaifunga Manchester United katika mchezo wao wa leo hii wa ligi kuu ya EPL basi ataachana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) nakujiunga na Chama Cha Chauma kinachoongozwa na aliyekuwa mgombea Urais, Hashim Rungwe.



Manara ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.


Ikitokea Liverpool kuifunga Manchester nahama CCM najiunga na chama cha Hashim Rungwe ..hawatufungi hata kwa bahati mbaya

Kubenea Afunguka Mazito Baada ya Kufukuzwa Kwenye Ofisi Yake na Mkuu wa Wilaya

$
0
0
Mbunge wa Ubungo Saed kubenea amesema Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Hapi kumufukuza kwenye Ofisi yake ya ubunge iliyokuwa Katika manispaa ya Kinondoni ni kujitafutia ujiko kwa wakubwa wake wa kazi ili apandishwe cheo.

Kubenea ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kinondoni na kubainisha kuwa kwa sasa umezuka mtindo kwa watumishi umma kugomba na wabunge wa upinzani ili wapandishwe vyeo.

Ameongeza kuwa ni kweli amefukuzwa katika ofisi hizo na kwamba tayari  amekwishapata ofisi nyingine katika eneo la ubungo maeneo ya majengo ya urafiki.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ali Happi aliwafukuza katika ofisi zao wabunge wote walikuwa wakitumia jingo la mkuu wa wilaya kwa madai kuwa anataka kuzitumia ofisi hizo kwa matumizi ya serikali.

Tattoo Zamtesa Munalove "Zimekuwa Maumivu Makubwa Moyoni Mwangu"

$
0
0
Tattoo Zamtesa Munalove "Zimekuwa Maumivu Makubwa Moyoni Mwangu"
Msanii wa filamu tanzania (BONGO MOVIE), Munalove, amesema kuwa anaumia sana kuwa na tattoo mwilini mwake zimekuwa maumivu makubwa sana na kupelekea kutokuelewana kati yake n mwanae, hivyo anatafuta sehemu ya kuzifuta kwani nae ameshaokoka


Yanga: Hamtaamini Kitakachowatokea Township Rollers Kwao

$
0
0
Yanga: Hamtaamini Kitakachowatokea Township Rollers Kwao
KOCHA Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, amesema wengi hawataamini kitakachotokea kwani wamepanga kushangaza mashabiki wao kwa matokeo mazuri watakayopata katika mchezo wao wa marudiano dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Nsajigwa ametoa kauli hiyo baada ya mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyochezwa Jumanne iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo Yanga ilifungwa mabao 2-1.

Timu hizo zinarudiana Machi 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa uliopo Gaborone, Botswana ambapo moja kati ya viingilio vyake ni Pula 40, sawa na Sh 9,240.

Ili iweze kusonga mbele, Yanga inatakiwa kushinda kuanzia uwiano wa mabao 2-0 ambapo itakuwa imeingia moja kwa moja katika hatua ya makundi, kinyume na hapo itacheza mtoano na timu za Kombe la Shirikisho ili kufuzu hatua ya makundi.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Nsajigwa alisema benchi lao la ufundi chini ya Kocha Mkuu Mzambia, George Lwandamina wameona udhaifu wa wapinzani na wamepanga kuufanyia kazi ili kuhakikisha wanapata ushindi ugenini.

Nsajigwa alisema, Rollers ni wepesi na wanafungika kirahisi baada ya kuwaona katika mchezo uliopita na kikubwa kilichosababisha washindwe kupata ushindi nyumbani ni baadhi ya wachezaji kushindwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake.

“Rollers siyo wazuri wa kufikia hatua ya kukata tamaa ya kufanya vizuri katika mchezo ujao wa marudiano, nikuhakikishie kuwa kama wachezaji wetu watacheza kwa kufuata maelekezo yetu vizuri, niamini tunakwenda kuwatoa nyumbani kwao.

“Wanayanga wanatakiwa kuendelea kutupa sapoti ili katika mechi hiyo ya marudiano tupate ushindi mzuri utakaotupeleka katika makundi, mashabiki hawataamini kitakachotokea.

“Katika mchezo uliopita, tulishindwa kuwadhibiti katika kiungo na tukawaacha wakatawala na kusababisha kupiga pasi nyingi, kitu ambacho tumekiona na tunakifanyia kazi kisijirudie,” alisema Nsajigwa.

Akizungumzia mechi hiyo, beki wa pembeni Hassan Kessy alisema: “Kama wao walitufunga hapa nyumbani kwetu kwa nini sisi tushindwe kuwafunga kwao? Tunakwenda kuwafunga kwao kwani ni timu ya kawaida, kikubwa tunaomba sapoti ya mashabiki.”

Kwa upande wake, Gadiel Michael alisema: “Tulipoteza mechi ya hapa nyumbani kutokana na makosa madogo, tunafanya marekebisho tukawafunge kwao kwani baadhi ya majeruhi wamerudi.”


Kiungo Pappy Kabamba Tshishimbi yeye alisema: “Soka ni mchezo wa makosa ambayo tuliyafanya na wenzetu wakayatumia kutufunga, hivyo hatutaki kurudia makosa hayo badala yake tutapambana kwa nguvu ili tushinde.”

Ushirikiano Mbovu Kati ya Wabunge na Serikali Unakwamisha Maendeleo: Lema

$
0
0
Ushirikiano Mbovu Kati ya Wabunge na Serikali Unakwamisha Maendeleo: Lema
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema uhusiano usioridhisha kati ya wabunge na viongozi wa Serikali unakwamisha shughuli za maendeleo.

Mbunge huyo ameshauri itafutwe suluhu ili kurejesha mahusiano mazuri baina ya makundi hayo.

Akizungumza leo Machi 10, 2018 katika  kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Arusha, Lema amesema kama hakuna mahusiano mazuri kwa viongozi si rahisi kuwapatia wananchi maendeleo.

"Hili ni suala la utawala bora, leo hii kuna watendaji wa Serikali wanaogopa hata kupiga picha na wabunge, hasa wa upinzani. Jambo hili linapaswa kuondolewa kwani lina athari katika jamii,” amesema Lema.

Amesema wabunge wana nafasi ya kuchochea maendeleo ya wananchi na kuondoa kero zao, kwamba kuna wakati kiongozi wa serikali kutokana na sababu za kiitifaki hawezi kupeleka hoja moja kwa moja kwa viongozi wa juu lakini mbunge anaweza.

"Tufanye kazi pamoja, leo hii tunapitisha bajeti ya mkoa lakini kama hatuna mahusiano mazuri baina yetu, sisi kama viongozi sidhani kama tutafanikiwa,” amesema.



Akijibu hoja hiyo ya Lema Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Idd Kimanta amesema anaamini viongozi wa Serikali wanajua wajibu wao wa kufanya kazi na wadau mbalimbali.

"Utawala bora ni pamoja na kufanyakazi pamoja na nina imani hili linafanyika lakini kama kuna watu wanatengwa hilo ni jambo la watu binafsi,” amesema.

Hata hivyo, Kimanta ametaka viongozi kufanya kazi ya kutatua kero za wananchi na kuachana na mambo ya siasa kwani chaguzi tayari zimepita sasa ni wakati wa kufanyakazi.

Rais Magufuli Ampongeza Mkandarasi wa Barabara " Watu wa Chadema Watawahi Kwenda Kuandamana Mle"

$
0
0
Rais Magufuli Ampongeza Mkandarasi wa Barabara  " Watu wa Chadema Watawahi Kwenda Kuandamana Mle"
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kuwapongeza Wizara ya Ujenzi na mkandarasi aliyefanikisha ujenzi wa barabra ya Uyovu- Bwanga na kudai kuwa watu wa CHADEMA watawahi kwa ajili ya maandamano.


Magufuli amesema hayo leo Machi 10, 2018 akiwa kwenye ufunguzi wa barabara Uyovu - Bwanga, Bukombe mkoani Geita na kusema kuwa serikali imefanya maendeleo kwa ujenzi wa barabara na kudai hayo ndiyo mambo ambayo yeye anayahitaji kwenye serikali yake, aidha Rais Magufuli amedai kuwa kuna watu hawafurahii maendeleo ya Tanzania ndiyo maana wamekuwa wakijitahidi kufanya chokochoko.

"Nani afurahi nchii hii inayokaa kwa amani nyinyi pale mmekaa yupo wa ACT Wazalendo na wa CHADEMA yupo pale amekaa sawasawa kila mtu na kila mahali wote tunajiona ndugu kwa sababu maendeleo hayana chama. Tunajenga Hospitali ile huyu wa ACT atashindwa kwenda pale? Barabara hii wa CHADEMA si ndiyo wanawahi kwenda kuandamana mle hayo ndio maendeleo ninayotaka ya nchi yangu, hayo ndiyo maendeleo ya Watanzania na ndiyo maana nawapongeza sana Wizara ya ujenzi kwa kumaliza hii barabara" alisema Rais Magufuli

Mvua Zinazoendeea Kunyesha Zaleta Maafa Tanga Zaua Wawili

$
0
0
Mvua Zinazoendeea Kunyesha Zaleta Maafa Tanga Zaua Wawili
Watu wawili wamefariki dunia na nyumba sita zikiezuliwa na upepo wilayani Handeni mkoani Tanga kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Machi 9, jioni.



Akielezea tukio hilo Diwani wa kata ya Msasa wilayani hapa Hossein Omari amesema mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Mhando (32) amefariki baada ya kupigwa na radi wakati akitoka msikitini saa kumi jioni.

Amesema shuhuda wa tukio hilo, aliyekuwa akitoka na marehemu msikitini aliwaeleza kuwa mvua wakati inanyesha alisikia mlio wa radi na baadae kuona mwenzie anatoka moshi na kubaini amepigwa na radi.



“Ndugu wanasema mwili hauna jeraha lolote ila nguo ndio zimeungua na radi huku mwili kuonekana kuwa mweusi ila hana majeraha baada ya kupigwa na radi hiyo,”alisema Diwani Hossein.

Amesema wanaendelea kufuatilia kama kuna madhara zaidi na baadae watatoa taarifa kamili ya madhara yaliyotokea kwa vyombo husika.

Katika tukio jingine,mkazi wa kijiji cha Zavuza kata ya Kiva wilayani hapa Mwanahawa Ngoma(60) amefariki dunia baada ya kusombwa na maji wakati akitoka shambani kulima.



Akizungumzia madhara hayo Mtendaji wa kijiji hicho Rahma Bakari amesema walipata taarifa ya mtu kusombwa na maji na kutafutwa usiku mzima ila mwili ulionekana siku ya leo Machi 10.

Ameongeza pia nyumba sita katika kijiji hicho zimeezuliwa na upepo na kuwaacha wakazi wa eneo hilo bila makazi kutokana na kunyesha mvua iliyoambatana na upepo Ijumaa jioni.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Edward Bukombe amesema hana taarifa za matukio hayo  na akaahidi kufuatilia na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kutokana na mvua hizo.

Mtoto wa Miaka Mitano Ampeleka Baba Yake Polisi Kisa Shamba

$
0
0
Mtoto wa Miaka Mitano Ampeleka Baba Yake Polisi Kisa Shamba
MTOTO mmoja mwenye umri wa miaka mitano amemfikisha katika Kituo cha Polisi Ngara, mkoani Kagera baba yake mzazi baada ya kubaini kuwa baba yake anataka kuuza kinyemela shamba ambalo ni urithi wa watoto wake.

Akizungumza baada ya kufika kituoni hapo, mtoto huyo mwenye ujasiri mkubwa alikwenda kushitaki polisi kwa msaada wa dereva wa gari  aitwae Thabiti aliyempa msaada wa lifti ya gari na kuhoji iwapoi baba yake atauza shamba, wao kama familia wataishi wapi?

Kwa upande wa mtuhumiwa ambaye ni Baba, kukamatwa na polisi na kuhojiwa amekana kuhusu kutaka kuuza shamba hilo lakini mtoto amedai ni kweli baba yake alitaka kuuza shamba.

Alipoulizwa kama anafurahia baba yake kufungwa jela kwa kosa hilo alisema hafurahii baba yake kufungwa ikizingatiwa ana mzazi mmoja tu lakini alikuwa akipigania haki yake ya shamba kutokuuzwa kwani atakosa pa kwenda kuishi.

Kwa hakika mtoto huyu ni mfano wa kuigwa katika kupigania haki na usawa katika jamii.

Mechi ya Man U, Liverpool: Profesa Jay Apinga Kauli ya Steven Gerrard

$
0
0
Msanii mkongwe nchini ambaye hivi sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia CHADEMA Joseph Haule maarufu kama Profesa Jay amepingana na kauli ya nahodha wa zamani wa timu anayoishabikia ya Liverpool, Steven Gerrard.


Akiongea leo na East Africa Television Profesa Jay amesema kauli ya Gerrard aliyoitoa wiki hii kuwa nyota wa Liverpool Mohamed Salah ndiye mchezaji bora zaidi kutoka Africa kuwahi kucheza EPL hawezi kukubaliana nayo.

''Siwezi kuikubali moja kwa moja au kuipinga, lakini msimu huu Mo Salah amekuwa na msimu mzuri na msimu bora na tunatakiwa kujivunia kama mashabiki wa Liverpool, kikubwa nachoweza kusema Salah anaweza kuwa ni mchezaji aliyefanya vizuri zaidi katika msimu mmoja'', amesema.

Kwa upande mwingine Profesa Jay amesema kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ameitengeneza timu hiyo kuwa moja na kufanya vizuri hivyo anahitaji muda zaidi ndani ya timu hiyo ili aweze kuipatia mataji mengi.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0
DAWA BORA ZA NGUVU ZA KIUME NA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA
Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatinzo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurundia tendo kwa haraka Sasa inakuletea suluhisho juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za FULL POWER

Full Power dawa asili yenye vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu za kiume dawa hii inamchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hernone za gestro gen zikiwemo vitamin b6 na b1 vitamin e pamoja na madini aina ya zinc

Itakufanya kuwa na nguvu na mzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wakufanya tendo la ndoa zaidi hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20/30 ZAT 50

Inarundisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha nchi 3/7 na upana cm 3/4 standard.kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote pia anatibu matatizo mengine kama presha kisukari ngiri chango la tumbo kujaa gesi kutopata choo vizuri minguu kuwaka moto matatizo ya uzazi bawasili na magonjwa ya zinaa kama kisonono na kaswende

Tunapatikana Dar es Salaam  na mikoan wasiliana na DR Oshinda no 0755505099 au 0714126118  Karibuni kwa hunduma bora

Exclusive: Majibu ya Rosa Ree baada ya Stosh kumdiss kwenye Planet Bongo! Ampa Ushauri huu!

$
0
0
Exclusive: Majibu ya Rosa Ree baada ya Stosh kumdiss kwenye Planet Bongo! Ampa Ushauri huu!

VIDEO:

Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images