Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

“Chiti na Msichana Mkali, Mpaka Ukifumaniwa Aombwe Kupiga Picha” Nikk wa Pili

$
0
0

Leo March 16,2018 kwenye upande wa burudani story ambayo imechukua headlines kwenye mitandao ya kijamii ni kutoka kwa staa wa muziki wa Hipo Hop Nikk Wa Pilianayeunda kundi la weusi ambapo caption yake katika instagram yake imezua gumzo mitandaoni.

Kupitia instagram account ya Nikk Wa Piliameandika ujumbe ambao mashabiki wameutafsiri tofauti kutokana na maneno aliyoyaadika

“Chiti na demu mkaliiii mpaka demu wako akikufumania nae, badala ya kumpiga mangumi ana mwomba kupiga nae picha, nakumuuliza anatumia mafuta gani, amewezaje kuwa na ngozi nzuri hivyo na namna alivyo tunza shepu na kutokua na tumbo kabisa” -Nikk wa Pili

“So akiondoka haondoki na machozi anaondoka na notes alafu akukubali kuwa wewe mbaya, yani ye mwenyewe kabahatisha kuwa na wewe ha ha ha naangalia comedi hapa usije ukachukulia serious” -Nikk wa Pili

Hali ya Hewa ya Misri Pasua Kichwa kwa Simba

$
0
0
Hali ya Hewa ya Misri Pasua Kichwa kwa Simba 

KUNA dalili hali ya hewa ya hapa itaipa ugumu Simba kati­ka mechi yake ya keshokutwa Jumamosi dhidi ya Al Masry.

Simba iko mjini hapa kuivaa Al Masry ka­tika mechi ya Kombe la Shirikisho lakini hali ya baridi na hasa jioni inaweza kuwa tatizo kwa Simba.


Hali ya nyuzi joto 17 wakati wakiwa wame­toka jijini Dar es Salaam ambako kuna nyuzi joto hadi 33.
Hata hivyo, inaonekana kufika mapema mjini hapa inaweza ikawa faida zaidi kwao kwa kuwa watafanya mazoezi zaidi ya mara mbili.


Simba walionekana wakiwa na uchovu wa safari tangu mara tu baada ya kuwasili mjini hapa na Kocha Mfaransa, Pierre Lechantre alitoa nafasi ya wachezaji wake kupumzika kwanza kabla ya kuanza maandalizi tena.

Hali ya hewa ya baridi kali si nzuri kwa wachezaji wa Simba ingawa wenyeji wa­naona baridi ni kama vile imeisha na si kali ambako hufikia wakati mwingine hadi nyuzi joto 5.

Ndoto ya Diamond Yazidi Kung'aa Sasa Apata Nafasi Billboard

$
0
0
Ndoto ya Diamond Yazidi Kung'aa Sasa Apata Nafasi BillboardMoja ya ndoto nyingi za mastaa kibao wa muziki ni kupata nafasi Billboard. Diamond Platnumz amepata bahati hiyo baada ya kuandikwa kwenye makala ya mtandao wa Billboard.
 

Katika picha ambayo imewekwa kwenye makala hiyo, Diamond amewekwa pamoja na wasanii wengine wanne kutoka Afrika Magaribi akiwemo Wizkid, Davido na Tiwa Savage.
Kwenye makala hiyo ambayo imewaonyesha wasanii hao inazungumzia juu ya lebo kubwa za muziki duniani zinavyoangazia Afrika kumpata staa ajaye wa Pop duniani.

Hilo limekuja ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kampuni ya Universal Music Group ambayo pia inasimaamia kazi za Diamond, kupitia tawi lake la nchini Uholanzi ilitangaza kununua hisa asilimia 70 za lebo ya AI Records ya nchini Kenya.

UMG watakuwa wanafanya kazi za kusambaza kazi za wasanii wa Al Records duniani kote ikiwemo kwenye mitandao mikubwa tofauti tofauti ya muziki.

Mafuriko Yasababisha Ofisi za Mwendokasi Kuhamishwa

$
0
0
Mafuriko Yasababisha Ofisi za Mwendokasi Kuhamishwa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka (Udart) umeamua kuhamisha ofisi zake kwa muda ili kuepusha uharibifu unaoweza kujitokeza kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Udart, Deus Bugaywa amesema wamehamisha ofisi hizo ili shughuli zinazofanywa na mradi huo zisiweze kutetereka kutokana na mvua zinazoendelea.

"Maji yalianza kujaa saa nane usiku, tulianza kuhamisha magari yetu yote na kuyapeleka katika vituo vikubwa vya mabasi yetu, licha ya mabasi pia tumehamisha vitu vingi vya ofisi kwa sasa hatutaitumia kwa muda," amesema Bugaywa.

Amesema wameamua kusitisha huduma za usafiri wa mwendokasi leo, kutokana na maji kujaa eneo la jangwani na hivyo barabara hiyo ilifungwa tangu saa kumi alfajiri na imefunguliwa saa tatu asubuhi baada ya trafiki kujiridhisha kwamba inafaa kupitika.

Imewekwa wazi kuwa ofisi zilizopo eneo la Jangwani kwa sasa hazitatumika na mabasi yote yaendayo haraka yatalazwa katika vituo vikuu vya mabasi hayo.

Mbowe Atinga Kituo cha Polisi Dar Apangiwa Tarehe Nyingine

$
0
0

Mbowe Atinga Kituo cha Polisi Dar
Leo March 16, 2018 Mwenyekiti waChama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA  Taifa, Freeman Aikael Mbowe, amefika katika kituo kikuu cha Polisi akiwa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu ambae alikuwa mgombea katika jimbo la Kinondoni.

Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliagiza kukamatwa kwa viongozi saba waandamizi wa CHADEMA, akiwamo Mbowe, Katibu Mkuu Vincent Mashinji na Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika.

Wastara Atoboa Siri Aloishi Nayo Zaidi ya Miaka Tisa

$
0
0

Wastara Atoboa Siri Aloishi Nayo Zaidi ya Miaka Tisa
Msanii wa filamu nchini Wastara Juma ambaye sasa amepata shavu la ubalozi wa moja ya taasisi za kusaidia watu nchini Sweden amefunguka na kutoa siri ambayo ameishi nayo kwa zaidi ya miaka tisa bila kumweleza mtu.
Wastara akiwa kwenye kipindi cha KIKAANGONI ambacho kinafanyika kila siku ya Jumatano kupitia ukurasa wa facebook wa EATV amesema kuwa kipindi ambacho alikuwa akimuuguza mumewe marehemu Sajuki ndiyo kipindi ambacho alipatwa na majanga ya kupasua mguu wake wa bandia wakati akimfuatia mumewe chakula nje ya hospitali.

"Watu hawajui mimi wakati nampeleka Sajuki hospitali nilianguka barabarani na mguu niliokuwa nao ulinipasukia barabarani India wakati nashuka chini kwenda kumchukulia chakula Sajuki kwa siri maana alikataa chakula cha hospitali, nilikuwa sijawahi kushuka chini kwenye zile barabara maana sizijui wala sijui fujo zao kwani barabara za India zinafujo sana watu wanapiga sana honi utafikiri wanaenda harusini kwa hiyo zile kelele zilinichanganya akili nikaanguka katikati ya barabara na mguu ukanidondoka na kupasuliwa hapo hapo bahati nzuri nilikuwa na shemeji yangu akanibeba kama vile kanyakua kifaranga"alisema Wastara

Wastara amedaikuwa wakati yupo hospitali watu walikuja palepale hospitali na kumpima mguu kisha wakamtengenezea mguu mwingine kwa fedha ambazo alitumiwa na ndugu zake ambao wapo Omani Muscat kwani huko ndipo aliomba msaada.

"Hili jambo watu hawalijui na wala sijawahi kulisema sehemu kwani hapa ndiyo mara ya kwanza nalisema kwa hiyo kama mguu wangu naufanya ni mradi ningesema na kupiga picha ili mwisho wa siku watu wanichangie lakini sikusema sehemu kwa kuwa sifanya tatizo langu kama mradi"alisisitiza Wastara

Albamu ya Diamond Yamuibua Harmorapa ''Albamu Mbaya Kama Sura Yangu''

$
0
0
Albamu ya Diamond Yamuibua Harmorapa ''Albamu Mbaya Kama Sura Yangu''

Msanii wa Rap Bongo,Harmorapa ameibuka na kuiponda Albamu ya Diamond ‘A boy from Tandale’ na kudai ni mbaya kama ilivyo sura yake.



Harmorapa ambaye amejipatia umaarufu kwa kudaiwa kupenda kiki ameiponda Albamu hiyo iliyofanyiwa uzinduzi rasmi nchini Kenya hivi karibuni.

“Bro #chibu nae kelele nyingi za album miez saba mwisho wa siku anatutolea Album mbovu kama sura yangu sokwecha kukushaur simba kama mkataba wako wa karanga umeisha kaa dukani kwa Dada yako #Esma umsaidie kuuza vitenge –




Dunia Kwa sasa inasubili ulbum yangu ya #uThigawePathi na ulubamu ya #kingkiba_for_life,“ ameandika Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Mke wa Mwana wa Trump Aomba Talaka Marekani

$
0
0
Mke wa Mwana wa Trump Aomba Talaka Marekani 

Mke wa Donald Trump Jr, mwana wa kiume wa kwanza wa Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha ombi la kutaka kumpa talaka mumewe, vyombo vya habari Marekani zimeripoti.
Taarifa zinasema Vanessa Trump anataka talaka isiyo na mvutano kwa mujibu wa ombi alilowasilisha katika mahakama moja New York.

"Baada ya miaka 12 kwenye ndoa, tumeamua kila mtu aende njia yake," wawili hao walinukuliwa wakisema kwenye jarida la habari mtandaoni la Page Sit.
"Tunaomba haki yetu ya kuishi maisha ya faragha iheshimiwe."

Talaka isiyo na mvutano ina maana kwamba wawili hao hawatazozana kuhusu kugawana mali yao na kuhusu nani atabaki na watoto wakati wa kusikilizwa kwa ombi lao la talaka.
Mapema mwaka huu, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba wawili hao walikuwa wanakabiliwa na matatizo kwenye ndoa yao.

Walisema chanzo cha matatizo hayo ni safari za mara kwa mara za Bw Trump Jr na hatua yake ya kupenda sana kutumia mitandao ya kijamii.

Trump Jr ndiye mwana wa kwanza wa kiume wa Donald Trump na mke wake wa kwanza Ivana Trump.

Kwa sasa ni makamu wa rais mtendaji wa shirika la The Trump Organization.
Alimuoa Vanessa Haydon baada ya wawili hao kukutanishwa katika hafla ya maonyesho ya mitindo na babake.

Upendo wake, na nduguye Eric, wa kuwinda wanyama wakubwa ulikosolewa baada ya picha kutolewa zikiwaonesha wakipigwa picha na wanyama waliouawa, wakiwemo chui na mamba. Donald Jr alikuwa pia ameshika mkia wa ndovu uliokuwa umenyofolewa kutoka kwa ndovu.

Munalove Akomalia Kufuta Tatoo Zake Kutumia Milioni Tano Kufuta

$
0
0



Niki wa Pili Awapa Funzo Wanaume “Chiti na Demu Mkaliiii Ukifumaniwa Aombe Kupiga Picha''

$
0
0


Niki wa Pili Awapa Funzo Wanaume “Chiti na Demu Mkaliiii Ukifumaniwa Aombe Kupiga Picha''
Leo March 16,2018 kwenye upande wa burudani story ambayo imechukua headlines kwenye mitandao ya kijamii ni kutoka kwa staa wa muziki wa Hipo Hop Nikk Wa Pilianayeunda kundi la weusi ambapo caption yake katika instagram yake imezua gumzo mitandaoni 
Kupitia instagram account yaNikk Wa Pili ameandika ujumbe ambao mashabiki wameutafsiri tofauti kutokana na maneno aliyoyaadika

“Chiti na demu mkaliiii mpaka demu wako akikufumania nae, badala ya kumpiga mangumi ana mwomba kupiga nae picha, nakumuuliza anatumia mafuta gani, amewezaje kuwa na ngozi nzuri hivyo na namna alivyo tunza shepu na kutokua na tumbo kabisa” -Nikk wa Pili

“So akiondoka haondoki na machozi anaondoka na notes alafu akukubali kuwa wewe mbaya, yani ye mwenyewe kabahatisha kuwa na wewe ha ha ha naangalia comedi hapa usije ukachukulia serious” -Nikk wa Pili

Dogo Janja Afunguka Kwanini Amepangiwa Ratiba ya 'Utamu' na Uwoya

$
0
0
Dogo Janja Afunguka Kwanini Amepangiwa Ratiba ya 'Utamu' na UwoyaMsanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo Janja ambaye ni mume halali wa muigizaji wa filamu bongo Irene Pancras Uwoya, ameweka wazi sababu za kupangiwa ratiba na mke wake huyo, jambo ambalo lilizua kizaa zaa baada ya kuiweka kwenye mtandao.

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema alishtuka baada ya kuona ratiba hiyo imebandikwa ukutani alipoamka, na kueleza sababu zake.

“Nilikuwa nimelala nimeamka nikakutana na ratiba kwenye ukuta, nikaangalia duh!! nikaipost insta. Unajua yule ni mshkaji wangu sana alikuwa ananitania, na yeye ndiye alianza kuipost, na kimvua hiki uniambie ratiba!!? Atadondoka mtu”, amesema Dogo Janja

Wawili hao walifunga ndoa ya kimya kimya jambo ambao wengi hawaamni mpaka leo kuwa ni wanandoa, na pia kutokana na tofauti ambazo wanaonekana wanazo za kiumri.

Sikuwahi Kuwaza Kuwa ‘Single Mother’ – Faiza Ally

$
0
0
Sikuwahi Kuwaza Kuwa ‘Single Mother’ – Faiza Ally
Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Faiza Ally amefunguka kuwa wakati anakua hakuwahi kuwaza kuja kuwa ‘single mother’.


Faiza ameendelea kufunguka kuwa baada ya kuwa mama akawa anajiuliza ni kwasasababu ya wanaume ndio aishi maisha asiyoyataka? alihoji.
 
Faiza kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika hivi “Wakati nakua sikuwahi kuwaza kuwa single mom, lkn kutokana na misimimo yangu wanaume wajinga hawakunielewa nikajikita ktk kujitegemea, baada kuwa mama nikawa najiuliza ni kwa sababu tu ya mwanaume au baba mtoto ndio niishi maisha nisiyo yataka , nikaondoka nikiwa nauchungu mwingi mno lkn nikasema maisha yangu ni bora kuliko kuwa mke! Nikapitia mengi sana haikua rahisi lkn

 Leo nimesimama imara kwa sababu niliamua kuchagua maisha ninayo ishi kwa hiari ! Nilipita wapi na nikavuka vikwazo vyote ????? Njoo nita share stori yangu na wewe kuwa single mom sio mwisho wako ! Kuna maisha zaidi ya kukaa usipo stahili ! JUA THAMANI YA UANAMKE WAKO BILA KUJALI WANAO BWEKA NJIANI“.

Shilole Afunguka Kuhusu Kuvunjika kwa Ndoa Yake na Uchebe

$
0
0

Msanii wa muziki bongo ambaye kwa sasa mjasiriamali anayehakikisha matumbo ya watu yanapata afya, Shilole au Shishi Trump, hatimaye amefunguka kuhusu kuvunjika kwa ndoa yake na mume wake Uchebe.
Akizungumza na mwandishi wa habari, Shilole amesema hajaachana na mume wake na wala hawafikirii kuachana.
Kwa upande wa mume wake Shilole Bwana Uchebe amesema sio kweli kwamba ameachana na mkewe, na kwamba kuna wanafiki wanapenda wasikie wameachana.

Akifunguka kuhusu kupost kwa ua jeusi na caption yenye utata, Uchebe amesema kuna mtu alihack acount yake na kupost hivyo, lakini hawajaachana namkewe na wala sio kiki.

“Sio kweli sijaachana na mke wangu na wala hatufikirii kuachana, kuna watu wanafiki wanapenda kusikia tumeachana, kuhusu ile post kuna mtu alifanikiwa kuhack acount yangu na kupost vile lakini sijamuacha mke wangu, na wala hatuna ugomvi, na niwaambie tu kuwa hatuachani leo hata kiama”, amesema Uchebe.

Tetesi za wawili hao kuachana zimekuja baada ya kupostiwa kwa ua jeusi kwenye ukurasa wa instagram wa Uchebe na caption ambayo ilikuwa na utata, na watu kuhisi labda wawili hao hawako pamoja tena.

Hizi Ndio Kauli 10 za Mtu Asiye na Malengo wala Uthubutu.

$
0
0

Kauli 10 za mtu asiye na malengo wala uthubutu.

1. Sina mtaji
2. Sina Connection
3. Nitaanza rasmi kesho
4. Mimi ni wa hivihivi tu
5. Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma
6. Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo
7. Kupata ni majaliwa
8. Usilazimishe mambo
9. Kuna watu special siyo mimi.
10. Sina bahati

Mbinu Bora Ya Kuishi Ndani Ya Bajeti Yako

$
0
0

Hivi falsafa juu ya matumizi ya  bajeti ambayo ipo  ndani ya uwezo wako ikoje? Hili ni swali la muhimu sana ambalo kila mmoja wetu anatakiwa kujiuliza kataka maisha yake ya kila siku.

Nasema hivi kwa sababu moja kati ya tabia ya watu wengi huwa wanaishi nje ya bajeti ambayo wanakuwa wamepanga.

Yote hii hutoka na sababu kubwa moja, sababu hiyo ni pale mtu ambapo amepata fedha nyingi kwa wakati mmoja. Kitendo hicho ndicho ambacho humfanya mtu kuweza kuishi nje ya bajeti yake ya kila siku.

Kwa mfano mtu akipokea mshahara hawezi kuishi maisha ambayo alikuwa ameyazoea ukifananisha na alipokuwa hana pesa, unakuta matumizi yanakuwa mengi kuliko pesa aliyonayo. Wapo wengine mara baada ya kutumia pesa yote hujikuta wanaingia kwenye madeni yasiyo ya msingi.

Achilia mbali madeni, wapo baadhi ya watu pindi wapatapo pesa utakuta wananua vitu vingi hata ambavyo hawakupanga kununua, tatizo hili lipo kwa watu wengi sana, siwezi ita tu ni tatizo bali ni ugonjwa wa matumizi ya pesa.

Niliwahi soma kitabu kimoja cha kanuni ya pesa, ndani ya kitabu hicho mwandishi anasema ya kwamba ukimpa mtu maskini pesa basi ndani ya sekunde kadhaa basi jiandae kujua tabia za mtu huyo, hii ni kwasababu ni mtu ambaye mara zote huongozwa na pesa, basi kila kilichopo mbele yake anataka kukimiliki yeye.

Lakini pesa hiyo ukimpa mtu ambaye anaelewa ni nini maana ya pesa,  basi  pesa hiyo huweza kufanya kitendo cha uwekezaji, ili pesa hiyo iweze kujizalisha yenyewe hapo baadae. Kwa nukta hiyo jaribu kutafakari  hivi pesa ambayo huwa unaipata mikononi mwako   unajiona upo kundi gani kati ya hayo niliyoyaeleza?

Kama utaona ya kwamba upo kundi ambalo umekuwa ni mtumiaji mzuri kuliko kuwa mwekezaji basi tambua lipo tatizo kubwa ndani yako, ambalo linakufanya uishi nje ya mstari wa bajeti yako, Hivyo unatakiwa kujua ni kwa namna gani unatakiwa kuishi ndani mstari bajeti yako kwa kuzingatia jambo hili.

Jambo Kwanza kabisa hakikisha pesa isikupelekeshe hasa pale unapoipata ila wewe ndiyo unatakiwa kuipelekesha pesa, kwa kuzingatia ya kwamba pindi utakapo ipa nafasi pesa ikuendeshe  basi tambua fika lolote linaweza kutokea ndani yako.

Lakini pia kwa  kuwa wanasema pesa ina makelele sana hasa pale unapoipata hivyo hakikisha pale unapoipata pesa unaishi kwenye pajeti yako ambayo umeizoa, kwani pindi utapopandisha bajeti yako eti kwa sababu umeipata pesa basi tambua ya kwamba  utaunganaa na wale wanaosema vyuma vimekaza.

Hivyo  pesa isiongeze matumizi yako ya kila siku eti kwa sababu umepata pesa, hivyo kila wakati jifunze kuishi ndani ya bajeti yako.


Hizi Ndio Sababu Kubwa za Ugumba kwa Wanawake

$
0
0


Ugumba ni nini? 
Hii ni hali ya wapenzi au mke na mume kutopata ujauzito. Ugumba unaweza kua primary infertility yaani mtu hajawahi kubeba mimba kabisa   tangu azaliwe au secondary infertility yaani mtu ambaye amewahi kuzaa lakini kwa sasa ameshindwa kubeba ujauzito. utafiti uanonyesha katika kila ndoa tano au mahusiano matano ya kimapenzi basi uhusiano mmoja una matatizo ya uzazi ya kushindwa kuzaa.

hali hii imekua ikiongezeka kadri miaka inavyosonga mbele kwa sababu mbalimbali kama mionzi ya mawasiliano yaani wi-fi , magonjwa mapya ya binadamu na kadhalika. Kwa wanawake utafiti mpya unasema uwezo wao wa kubeba mimba unaanza kupungua baada ya miaka 30 ya umri kutokana na kuanza kuishiwa nguvu kwa viungo vya uzazi. Ugumba una vyanzo vingi sana ambavyo vingine havifahamiki mpaka leo  lakini hebu tuone vyanzo muhimu vya ugumba.

• Utoaji wa mimba.
Huenda hichi ndio kitakua chanzo kikuu cha ugumba miaka ijayo kwani siku hizi kila karibia kila mwanamke ana sababu za kutoa mimba, utoaji wa mimba una hatari nyingi ambazo huweza kuleta ugumba kama kuoza au kuharibika kwa kizazi baada ya kushambuliwa na bakteria, makovu yanayoletwa na vifaa vinavyotumika kutoa mimba kwenye mfuko wa uzazi na mlango wa uzazi huweza kusababisha ugumba usiotibika.

• Matatizo ya vizaalishaji vya mayai [ovari].
Ovari ni kiungo ambacho kinatoa yai moja kila mwezi ili liweze kurutubishwa na mbegu ya mwanaume lakini kuna magonjwa ambayo yanaweza kusababisha ovari hiyo ikaugua na kushindwa kutoa mayai, mwanamke ana ovari mbili lakini moja ikiuugua tu na nyingine haifanyi kazi mfano ugonjwa wa ovarian cyst.

• Matatizo ya mirija ya uzazi.
Ovari zimeunganishwa kwenye  mirija ambayo hupitisha mayai kwenda kwenye mfuko wa uzazi..wakati mwingine mirija hiyo huziba kwa sababu mbalimbali hivyo mayai hushindwa kupita na kusababisha ugumba.mfano ugonjwa wa endometriosis, upasuaji na peritonitis.

• Matatizo ya kizazi.
Kizazi ndio sehemu kuu ambayo mtoto hutunzwa na kuishi kwa miezi yote tisa, tatizo lolote linaloshambulia kizazi huleta ugumba. mfano, makovu ndani ya kizazi, uvimbe ndani ya kizazi, kugeuka kwa kizazi na magonjwa ya zinaa kama kaswende na kadhalika.

Kansa ya kizazi.
Kansa ya kizazi huzuia yai la mama lililorutubishwa kushindwa kujiweka kwenye kizazi ili kukua, hivyo huchangia sana mimba kuharibika au kutotungwa kabisa.

• Matatizo ya mlango wa uzazi.
Oparesheni za kizazi, utoaji wa mimba na magonjwa ya zinaa huweza kusababisha kuziba kwa mlango wa uzazi hivyo mbegu za kiume kushindwa kabisa kupita kwenye mlango wa uzazi na kusababisha ugumba.

• Magonjwa mengine ya mwili.
Magonjwa yeyote ya binadamu  ambayo huingilia mfumo wa homoni za uzazi huleta ugumba mfano magonjwa ya ini,kisukari, hyperthyrodism, na kadhalika.

• Matumizi ya sigara na pombe.
Uunywaji wa pombe sana na uvutaji wa bangi huzuia yai kutoka kwenye ovari, lakini pia uvutaji wa sigara hupunguza uwezo wa yai kutembea kutoka kwenye ovari kwenda kwenye mfuko wa uzazi na wakati mwingine husababisha mimba kutunga nje ya kizazi.

Msongo mkubwa wa mawazo.
Ukiwa unatafuta mtoto tayari ukiwa umepaniki kwamba huenda usimpate husababisha inasababisha mwili kutoa homoni kitaalamu kama cortisol ambazo huzuia kazi za homoni za uzazi kitaalamu kama gonadotrophin releasing hormone hivyo hali huzidi kua mbaya.

Uzito uliopitiliza.
mwili mkubwa unaingilia mfumo wa utengenezaji homoni za uzazi hivyo huweza kuleta ugumba katika umri mdogo sana, hivyo kupunguza uzito ni moja ya njia bora kabisa ya kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuzuia ugumba.

Kumbuka; kabla hujaanza kuzunguka kwa waganga wa kienyeji na mahospitalini ni bora kujichunguza kama uko kwenye hatari zilizotajwa hapo juu. hakuna dawa moja ambayo ina uwezo wa kutibu ugumba kwa watu wote bila kutibu chanzo chake kwanza.... hivyo naweza kusema kila mtu ana dawa yake ya ugumba kulingana na historia ya maisha yake na chanzo cha tatizo lake.

Ugumba unaweza kupona kabisa kulingana na chanzo cha tatizo na hali ya ugonjwa ilivyo na unaweza usipone kabisa kama ugonjwa umeshapea sana, ndio maana kuna watu wenye uwezo mkubwa sana wa kifedha, wasanii na wafanyabishara wakubwa lakini wameshindwa kupata watoto pamoja na kwenda mpaka nje ya nchi na kuonana na madaktari bingwa kwenye hospitali za kisasa kabisa.makala ijayo ntaongelea  matibabu ya ugumba kwa kina, usikae mbali.


Ijue Misingi ya Kuwa Mbunifu

$
0
0

Katika maisha yako yote ambayo utaishi hapa dunia basi tambua ya kwamba bila kuwa mbunifu basi  utaendelea kuungua na jua maisha yako yote, nasema hivyo nikiwa na maana ya kwamba asilimia 99.99 ili uweze kupiga hatua za kimafanikio kila wakati  katika maisdha yako ni lazima uwe mbunifu.

Ubunifu ndio nguzo nambari moja ambayo itakufanya wewe kuweza kufanikiwa, ikiwa hautajenga misingi ya ubunifu katika jambo lolote ambalo unalifanya basi ni kwamba utaendelea kuishi maisha ya kawaida na matokeo ambayo utayapata nayo tayakuwa ni ya kawaida tu.

Kwa sababu  katika karne hii kwa asilimia kubwa kitu ambacho  unakifanya wewe kwa asilimia kubwa ni lazima kitafanana na mtu mwingine, kama ndivyo hivyo basi ikiwa mfanano wa vitu unazidi kuongeze swali la msingi ambalo unatakiwa kujiuliza ni, hivi natajitautishaje na wenzangu?

Majibu ya swali hilo ni kwamba ili kujitofautisha kivingine unachotakiwa kufanya ni kuhahahakikisha ubunifu unahusika kwa asilimia kubwa. Mtu mwingine anaweza kuja kifua mbele akaniuliza sasa afisa mipango huo ubunifu ni nini? Pasipo kuona haya endapo niutaulizwa swali kama hilo jibu ambalo nitampa nitamwambia, ubunifu ni kuongeza thamani kwa kitu ambacho unakifanya, aidha kama  utashindwa kuongeza thamani basi utakiwa kuunda kitu kipya.

Katika swala kuunda kitu kipya hapa ndipo pamekuwapo na tatizo fulani kwa sababu watu wengi wanapenda sana ganda la ndizi kuleteleza, kwa maneno mengine tunaweza kusema akili zao zimeganda hasa katika suala la kufikiria wao wamekuwa wanapenda sana kufanya copy & paste. Kufanya hivyo ni kujipoteza mwenyewe hivyo unachotakiwa kufanya ni kwamba lazima uwe na misingi ya kubuni kitu cha kwako.

Pasipo kupoteza kusudio la mada yangu ya siku ya leo, niliona ni vyema niianze na utangulizi huo ili uelewe maana ya ubunifu. Mara baada ya kufahamua maaana ya ubunifu basi naomba japo kwa dakika chache tuangalie misingi ya ubunifu  kama ifuatavyo.

1.    Ukitaka kuwa mbunifu katika eneo lolote lile , kwanza ni lazima uhakikishe unafanya kitu ambacho unakipenda. Ukifanya kitu ambacho unakipenda kwa asilimia zote, upo uhakika wa asilimia zote kwamba ni lazima utakuwa mbunifu ili kuwashinda washindani wako wanakuzunguka.

2.     Ili uweze kuwa mbunifu katika jambo ambalo unalifanya jambo jingine ambalo unatakiwa kulizingatia ni kwamba ipo haja kubwa sana ya kuwekeza muda mwingi katika kuliwaza na kulitenda jambo hilo. Hivyo kwa kuwa umeamua kuyasaka mafanikio kwa udi na uvumba huku ukiamini ya kwamba ubunifu ndiyo ambao utakusaidia kuwa hivyo basi hakikisha ya kwamba unajipanga kikamilifu kuweza kujitoka kwa kuwekeza muda wako mwingi ili kuweza kulitimiza jambo hilo.

3.     Jambo jingine ambalo litakufanya wewe uweze kuwa mbunifu ni kwamba ni lazima uhakiishe ya kwamba kila wakati huchoki kujifunza vitu vipya ambavyo vinaendana na jambo hilo. Samabamba na hilo kwa kuwa binadamu kwa asilimia kubwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kile alichojifunza kuweza kusahau, hivyo kwa kile ambacho unajifunza ni lazima uhakikishe ya kwamba unakiandika na uwe unakipitia mara kwa mara ili usikishau.

4.     Jambo la mwisho kati ya mengi yahusuyo somo hili ni kwamba kila wakati ni lazima uwe ni mtu wa kujiuliza maswali ya mara kwa mara. Moja kati ya swali muhimu ambalo unapaswa kujiuliza wewe katika misingi hii ya ubunifu ni, Je hivi nikifanya jambo hili nitapata faida gani?

Njia 5 Kali za Kupata Mtoto wa Kiume

$
0
0

Uzazi wa mpango una mambo mengi sana.. sio kuzuia mimba tu ndio uzazi wa mpango ila hata kupanga idadi na jinsia za watoto ni moja ya njia za uzazi wa mpango..

Watu wengi wamekua wakitamani jinsia flani za watoto ili wazae watoto wachache ila kukosa kwa jinsia waliyoipanga hujikuta wakizaa watoto wengi wakati wakitafuta jinsia husika, mpaka familia hugombana na kutengana kwa sababu hizi.

Mara nyingi wazazi wa kiume hufikia hatua ya kuvunja ndoa kabisa hasa wanapokosa watoto wa kiume.

Leo ntamaliza kitendawili hiki kwa kutoa njia ambazo zinaweza kufanya mtu kupata mtoto wa kiume kwa asilimia nyingi…

Kitaalamu mbegu  zinazotoa mtoto wa kiume XY huenda kwa mwendo mkali sana kwenda kwenye mfuko wa uzazi lakini hufa haraka. lakini mbegu zinazotoa mtoto wa kike XX husafiri taratibu na huchelewa kufika na kufa  ndani ya mfuko wa uzazi kwani mbegu hizi huweza kuvumilia hali mbaya ya kimazingira ndani ya mfuko wa uzazi wa mwanamke, hivyo njia pekee ya kupata mtoto wa kiume ni kuhakikisha mbegu hizo za kiumeXY zinakutana na mayai ya kike kwenye mfuko wa uzazi haraka kabla ya kufa..

Zifuatazo ni njia hizo tano kali…
1. Hakikisha unashiriki tendo la ndoa siku mayai ya mwanamke yanapokua yameshuka{ovulation}
Ukishiriki tendo la ndoa siku hii ambayo yai linakua limeshuka    mbegu za kiume huweza kufika mapema na kujiunga na mayai ya kike  na kutengeneza mtoto{fertilization}hii ni siku ya 14 KABLA YA KUONA DAMU YA MWEZI UNAOFUATA SIO BAADA YA KUONA SIKU ZAKO..

Kama wewe mwanamke hujui siku yako ya ovulation fanya hivi.
Pima joto lako la mwili: nunua kipima joto[thermometer} na kisha pima joto lako kila asubuhi , siku ukiona joto lako limeongezeka kidogo ujue umeanza ovulation na hiyo ndio siku muhimu ya kutafuta mtoto..

Angalia maji maji ya uke: kawaida maji ya uke hua mazito na kuvutika kama maji ya mayai mabichi wakati mwanamke anapoanza ovulation..

2. Wewe mwanaume ongeza idadi ya mbegu zako..{sperm count}
Mwanaume anatakiwa aongeze wingi wa mbegu zake hasa kwa kukaa siku mbili mpaka tano bila kushiriki tendo la ndoa wakati akisubiri mwanamke wake aanze ovulation.

Njia zingine za kuongeza mbegu ni weka korodani kwenye hali ya ubaridi:
kawaida korodani hutengeneza mbegu nyingi wakati wa hali ya ubaridi kuliko joto  hivyo mwanaume anatakiwa kuepuka kuvaa nguo zilizobana sana, na  kuwekalaptop kwenye mapaja acha kuvuta sigara na kunywa pombe:wanaume wanaokunywa pombe na kuvuta sigara hua na mbegu kidogo sawasawa na wavutaji wa bangi.. matumizi ya dawa za cancer pia husababisha uzalishaji wa mbegu kidogo sana.

3. Tumia style za ngono ambazo zinahamasisha muingilio mkubwa{deep penetration}
Hii huzipa faida mbegu za mtoto wa kiume{XY} kufika haraka na kufanya fertilization na upande mwingine, muingiliano mdogo{shallow penetration}husababisha mbegu kumwagwa mbali na mlango wa mfuko wa uzazi hivyo mbegu huweza kukutana na hali ya tindikali kwenye uke hivyo mbegu za mtoto wa kiume  kufa haraka na kuziacha mbegu zinazotoa mtoto wa kike.{XX}.

4. Hakikisha mwanamke anafika kileleni:
Mwanamke anapofika kileleni hutoa maji mengi ukeni ambayo hupunguza wingi wa tindikali ambayo ni adui wa mbegu  zote hasa mbegu za mtoto wa kiume XY ambazo hua haziwezi kuvumilia hali ngumu ya kimazingira.

5. Usifanye tendo la ndoa kabla na baada ya ovulation;
Kabla ya ovulation mbegu za mtoto wa kiume XY hufika haraka kwenye mfuko wa uzazi  kama kawaida na kukuta mayai ya mwanamke hayajafika na kufa vivo hivyo baada ya ovulation..

Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Apagawe na Wewe

$
0
0

Kuna vitu vingi ambavyo unaweza kutumia kwa manufaa yako ili kufanya wanawake wakuone unavutia. Amini usiamini, hivi vitu si lazima uwe tajiri wala uwe na urembo wowote. Mwanzo kati ya vitu hivyo vingi ni rahisi kuvitumia kwa urahisi. Hii hapa ni orodha ya mambo ambayo ukiyazingatia yatakufanya wewe uwe na mnato kwa mwanamke yeyote yule.

1. Uwezo wako wa nishati
Nishati inaweza kuwa na mkusanyiko wa vitu kadhaa, kama vile kuhisi kwa vipepeo ndani ya tumbo, kusuka, wasiwasi ama vitu tofauti kabisa. Kwa mtizamo wa moja kwa moja, nishati inahusiana na yote yale ambayo yanamfanya mwanamke kujiskia raha wakati anapokuona ama kutaka kuutumia muda wake mwingi akiwa na wewe. Nishati inacheza nafasi kubwa katika mapenzi kama wataka kumtongoza mwanamke na ufaulu kwa urahisi. Ili kupeana nishati zaidi kila wakati unapokuwa na mwanamke, hakikisha kile kikuu unachohitaji kufanya ni kumchekesha, kumsapraiz, umguse kwa bahati mbaya mara kwa mara, kuwa mwenye michezo nk. Zote hizo zitamfanya kukufikiria wewe mara 24/7.

2. Mbinu utakayoitumia kumsifu
Kulingana na utafiti kutoka NBC unadai ya kwamba wanawake wengi hawajiskii huru kupewa ama kupokea sifa kutoka kwa wanaume. Lakini usikatwe na tamaa! Vile ambavyo utampongeza mwanamke inaweza kucheza pakubwa kufaulu kumpata mwanamke unayempendae baada ya muda. Afterall ukimsifu kitofauti tofauti anaweza kukubali ama kukuona kama wewe ni mzaha kwake. So kuhepa aibu kama hizi ndogo ndogo, unafaa umsifu mwanamke kwa jambo ambalo ni la kwake pekee, yaani kitu ambacho utamsifu nacho hakipatikani kwa mwingine. Mfano waweza kumakinika kwa kitu ambacho anafanya wakati flani na utumie ujuzi wako wa kiume kumsifia na jambo hilo. Mfano unaweza kumsifu kwa uwezo wake wa kuimba, kuchora, mtindo wake wa kutembea nk. [Soma: Mbinu ya kutongoza kwa wale wanaojifunza]

3. Upambo wako
Si lazima uwe mwanamume wa kuvutia ili umvutie mwanamke. Utafiti umebainisha kuwa wanawake hawavutiwi na urembo wa mwanamume, nywele zake wala ngozi yake. Mwanzo kuwa mrembo kama mwanamume kuna ubaya wake mwingi ikizingatiwa kuwa unaweza kuonekana kama pleya ambaye unapendwa na wanawake wengi.

Kile ambacho unachohitajika hapa ni uhakikishe kuwa uwe nadhifu kimwili na mavazi yako. Kufanya hivi kutakusaidia wewe kuonekana mtu timamu halikadhalika inakufanya wewe kuwa na confidence ya kapproach demu yeyote yule.

4. Ujuzi wako wa kutangamana 
Lazima atleast uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kuweza kutangamana na wengine. Kama mwanamume lazima uwe na ujuzi ambao utakusaidia wewe kutangamana na wengine kwa urahisi. Hii inamaanisha kuwa lazima uwe na ujuzi flani wa kuongea na wanawake ndipo utakapojua jinsi ya kumfanya apagawe na wewe.

5. Kiwango chako cha kujiamini
Kitu cha mwisho ambacho ni muhimu kwako kuwa nacho ni kujiamini. Kujiamini ni njia moja wapo ya lazima uwe nayo ili uweze kuiteka hisia ya mwanamke yeyote yule.[Soma: Njia za kuwa na confidence kama mwanaume]

KUMBUKA: Vitu vyote tulivyoeleza hapo juu havitakuwa na manufaa yeyote yale iwapo kama hutaweza kujiamini kama mwanamume. Hivyo ni lazima kwako kuhakikisha kuwa mwanzo unajijenga kwa kuwa na confidence. Hii ni kuanzia kujitambua wewe mwenyewe bila kujishuku, kuongea bila woga wowote wala kutoingiwa na wasiwasi wakati wowote ukiwa karibu na mwanamke.

Mambo Yatakayokusaidia Kudumisha Mahusiano ya Mapenzi

$
0
0

Kuna nukuu inayosema “Uhusiano mzuri hautokei tu peke yake bali huchukua muda, uvumilivu, na watu wawili ambao kikweli wanataka kuwa pamoja.”

Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi.

Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea, yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana.

1. Uaminifu
Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote. Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako.

Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano. Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli mara zote. Ongeeni juu ya mipango na mawazo yenu bila kufichana.

Watambulishe kwa mpenzi wako ndugu ,jamaa na marafiki wakaribu ili kumpa mwenza wako amani.

2. Weka muda kwajili ya Mwenza wako
Mahusiano mazuri kati ya wapenzi yanahitaji muda wa wapenzi hao kukaa pamoja. Wapenzi wasio na muda wa kukaa wana hatari ya kupoteza mvuto wa mahusiano yao na hivyo kuhatarisha uhai wa mapenzi kati yao.

Kama wapenzi wapo mbali mbali basi wanahitaji kuweka muda wa kuongea kila inapowezekana. Tafuta muda wa kutoka pamoja, hata kama mtaenda mgahawani kunywa chai au juisi tu inatosha sana na inawaweka karibu zaidi.

3. Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu sana baina ya wapenzi. Hata kama umebanwa na kazi pata dakika chache za kuongea na mpezi wako na kumtaka hali. Andika hata ujumbe wa maneno au barua pepe. Mwambie mpenzi wako ulipo kila mara inapobidi ili kumjengea imani na wewe na kumpa amani moyoni. Tuma ramani ya mahali ulipo kama unatumia simu ya “Smart” (Tuma location kwenye whatsapp)
Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha upendo.

Wakati kuwasiliana na mpendwa wako, kumbuka kwamba upendo ni muhimu. Ongea toka moyoni na si kwa ajili ya kutimiza wajibu tu, kwani mpezi wako atajua tu kama hakuna mahaba katika mawasiliano yenu hivyo kutoleta faida ile inayotegemewa.

Mawasiliano mengine ni yale ya kuelezana yaliyo moyoni. Mweleze mwenza wako linalokusibu ili kupata ufumbuzi wa pamoja. Wapenzi wanaoongea kwa utulivu siku zote watakuwa pamoja.

4. Zawadi
Tafuta kitu cha kumpa mpenzi wako. Si lazima kiwe na thamani kubwa. Inaweza ikawa pipi au matunda tu. Mnunulie zawadi kila inapowezekana hasa unaposafiri au katika siku yake ya kuzaliwa.

5. Onyesha Upendo Wako 
Kila mtu anajinsi yake tofauti ya kuonyesha upendo, lakini vyovyote itavyokuwa ni jambo la muhimu sana kuonyesha hisia zako kwa mpenzi wako. Mara nyingi wapenzi wa muda mrefu wanasahau juu ya hili.

Maneno kama “Nakupenda”au majina ya mahaba kama “Mpenzi” au ”La-azizi” yanachangia sana kuonyesha mapenzi na kumfanya mwenza wako kujisikia vizuri. Maneno haya yanaposemwa kwa hisia halisi na toka moyoni yana mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano.

Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images