Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live

Baby Madaha Anusurika Kubakwa Baada ya Kupanda Jukwaani Akiwa na Kivazi Cha Nusu Uchi

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.

“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.


Irene Uwoya Chizi , Asema Apendi Vazi Linaloitwa Chupi aka Kufuli

$
0
0
Mrembo na staa wa filamu nchini Irene Uwoya amesema kuwa hakuna vazi asilolipenda kulivaa kama chupi a.k.a kufuli. Irene amesema hayo alipokuwa akizungumza na magazine maarufu ya burudani ya VIBE.

Alipoulizwa na mwandishi wa jarida hilo kuwa ni nguo gani ni vigumu kuikuta kwenye kabati lake,  “Chupi – sipendi kabisa hilo vazi” Alisema Irene uwoya. Hatari sana hii.

Dereva wa Basi la UDA Apewa Kibano Kizito na Trafiki

$
0
0
Devera wa Basi la Kampuni ya Usafiri Dar es Salaam (UDA) ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, amejikuta akipewa kibanokizito  na askari wa usalama barabarani ‘trafiki’ baada ya kuleta ubabe wakati alipotakiwa kutii sheria bila shuruti.

Tukio hilo la aina yake lililosababisha usumbufu kwa abiria wa basi hilo, lilitokea juzi Bamaga-Mwenge jijini Dar kufuatia dereva huyo kukataa kuegesha pembeni basi hilo lenye namba za usajili T 619 CVP lililokuwa limevunja sheria ya usalama barabarani.

Imedaiwa kuwa, basi hilo lilishusha abiria kinyume na sheria kwenye kituo kisicho rasmi maeneo ya Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Barabara ya Shekilango.

Chanzo makini kilichoshuhudia tukio hilo kimedai kuwa, kufuatia hali hiyo ndipo trafiki hao watatu walio makini na kazi yao, walilisimamisha basi hilo ili kumsomea mashitaka dereva huyo sambamba na kondakta wake lakini wakaleta ubishi na kutoa lugha chafu kitendo ambacho trafiki hao walishindwa kukivumilia.

Waliendelea kutoa lugha chafu, hawakuonesha kutii amri ili waambiwe walichokosea ndipo trafiki wakalazimika kuwadhibiti kwa kuwafunga pingu baada ya kukataa kutii sheria bila shuruti, tunawapongeza trafiki hawa kwa kuwataiti,” kilisema chanzo hicho.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kwamba, madereva wa mabasi ya Uda wamekuwa wakivunja sana sheria kama wao wako juu ya sheria kuliko madereva wengine.

Matokeo ya Manchester Utd vs Swansea City Haya Hapa

$
0
0
Ligi kuu ya Uingereza maarufu kama Barclays Premier League imeanza rasmi leo hii kwa mchezo wa ufunguzi kati ya Manchester United dhidi ya Swansea City.
Mchezo huo uliomalizika hivi punde katika dimba la Old Trafford, United imeendelea pale pale ilipoachia msimu uliopita kwa kupoteza mechi ya kwanza kwenye dimba la nyumbani kwa kipigo cha magoli 2-1.
Swansea ndio walikuwa wa kwanza kuona nyavu za United kwenye dakika ya 28 kipindi cha kwanza kupitia Ki Sung, kabla ya Wayne Rooney kusawazisha dakika 58.
Huku United wakiwa wanatafuta goli la pili, kinda Tylor Blackett akapoteza mpira kwa Wilfred Bony na kusababisha goli la pili lilofungwa na
Sigurdsson.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Swansea 2-1 Man uTD.
Hiki ndio kipigo cha kwanza kwa United katika mechi ya ufunguzi wa EPL tangu mwaka 1972.
Man Utd (3-4-1-2): De Gea; Jones, Smalling, Blackett; Lingard (Januzaj (24min), Fletcher, Herrera (Fellaini 67), Young; Mata; Hernandez (Nani 46), Rooney.
Subs: Kagawa, Michael Keane, Amos, James.
Goal: Rooney 53.
Booked: Blackett, Young.
Swansea (4-2-3-1): Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor (Tiendalli); Ki, Shelvey; Routledge, Sigurdsson; Dyer (Montero 67), Bony (Gomis 77).
Subs: Tiendalli, Montero, Tremmel, Bartley, Richards, Sheehan.
Booked: Dyer, Taylor, Shelvey.
Goals: Ki 28, Sigurdsson 72.
Referee: Mike Dean (Wirral)

Sentensi 5 za Meninah Kuhusu stori za Uhusiano Wake na Diamond Platnumz.

$
0
0
Mwanzoni mwa wiki hii kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kulisambazaa taarifa za Meninah kuhusishwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake ambae ni Diamond Platnumz ambapo kupitia Leo Tena ya Clouds Fm Meninah amekubali kuongelea hii.
Matano aliyoyasema Menina ni haya hapa chini…
1.Sina uhusiano wowote na Diamond Platnumz.
2.Mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa Dodoma kwenye uzinduzi wa video ya Miaka 50 ya Muungano.
3.Sijawahi kuwasiliana nae hata namba yake ya simu sina kwenye simu yangu.
4.Mimi napenda uhusiano wao kati yake na Wema Sepetu.
5.Nampenda Wema kama dada yangu na namkubali Diamond Platnumz kama msanii mwenzangu.

Mashabiki wa Diamond nao Waanza Kampeni Dhidi ya Wema, Wasema Aunt Ezekiel ndio Chanzo

$
0
0
Baada ya mashabiki wa Wema kuamua kuanzisha kampeni maalum dhidi ya Diamond wakimtaka amrudishe wema wao kwenye game walilomzoea #BringBackOurWema, mashabiki wa Diamond nao wameibuka na yao.

Katika Instagram imefunguliwa akaunti maalum ya watu wanaojiita TeamDiamondTz nao wameanzisha kampeni ya kumtetea Diamond huku wakimtaka Wema kuachana na starehe zisizo na faida kama alivyosema Diamond.

Masanja Naye Apigilia Msumari ndoa ya Diamond Platnumz na Wema Sepetu

$
0
0
Baada ya uhusiano wa Diamond na Wema kuingia katika misukosuko na Diamond kutoa ujumbe mzito kumhusu wema sepetu, mchekeshaj maarufu hapa bongo Masanja mkandami ameamua kufua ya moyoni kuhusiana na uhusiano wa wawili hawa.

Masanja alisema haya “Street Pastor Anasema.. HILI SWALA LA DIAMOND NA WEMA NADHANI MUNGU AMEMUHURUMIA MMOJA WAPO KATI YA HAO WAWILI. KAMA WANGEKUWA WATU WA KUOANA WANGESHA OANA UCHUMBA GANI MREFU KAMA WANASOMEA UDOKTA???? RAFIKI YANGU NASIB, KAMA KWELI MLIPENDANA KWA DHATI HIZO KASORO ZINAREKEBISHIKA, MAANA HAKUNA MWANADAMU ALIYE SAHIHI KWAN HATA WW NASIB UNAMAPUNGUFU YAKO. NA WEWE DADA YANGU WEMA LAZIMA UJUE MME NDIO KICHWA CHA NYUMBA KWA MAELEZO HAYO INAONYESHA HAUMSIKILIZAGI MWENZIO OMBA MSAMAHA TENAAA NA TENA NA UKUBALI KUBADILIKA. MI SIPENDI MKIWA MNAONGOZANA WOTE KWENYE MA SHOW YA USIKU MME KAFANYE KAZI MKE ABAKI HOME UKIRUDI MWILI UMEPOA HATA UJAUZITO UNAINGIAA!! SASA WOOTE STEJINI MKIRUDI MIILI YA MOTO SI MTAZAA POPOMPOO JAMANIII!! NITAFURAHI KUSIKIA TOFAUTI ZENU MMEZIMALIZA KWA AMANI ILI MASHABIKI WENU WASIJISIKIE VIBAYA.” - See more at: http://moro5.blogspot.com/2014/08/masanja-naye-apigilia-msumari-ndoa-ya.html#sthash.p3ZSjPaz.dpuf

Yamoto Band Wamtaja Anaewaandikia Nyimbo Kwa Asilimia 90

$
0
0
Yamoto Band inayoundwa na wasanii wenye umri mdogo inazidi kufanya vizuri kila kukicha na hivi sasa wanatamba na ngoma tatu zikiwa ni pamoja na Nibemende/Nitajuta, Niseme.

Akiongea kupitia kipindic ha The Chart ya 100.5 Times Fm kinachoongozwa na Jayree, Asley ambaye ni kiongozi wa bendi hiyo amesema kuwa Said Fella (boss wao) amekuwa msaaada mkubwa katika nyimbo zao zote.

“Mara nyingi sisi huwa tunafanya melodies yeye anatoa maneno…Producer alitengeneza beat akatuita studio tukaanza melodies na maneno kidogo yetu. Bahati nzuri Mkubwa alikuwa anatoka kwake anakuja studio tukampigia simu ‘mkubwa sisi tumepata melody kuna nyimbo tulikuwa tunafanya hapa studio ila bado tunaona maneno kama hayajakuwa mazuri. Kweli mkubwa alivyokuja kuyasikiliza akaanza kuyapasua neno maoja baada ya moja.”  Amesema Asley.

“Lakini maneno asilimia 90 ya nyimbo hiyo yote alitoa mkubwa. Na idea ya Nitajuta pia katupa baadhi ya maneno. Kama ukisikia sijui ‘mtu kunywakunywa milenda’ yote katoa yeye mkubwa Fella. Yaani mara nyingi yeye ndiye anatusaidia. Hii nyimbo ya mwisho yeye alitupa idea lakini maneno tulitoa wenyewe.” Amefafanua.

Wimbo wa Nitajuta wa Yamoto Band umeshika nafasi ya pili kwenye The Chart ya 100.5 Times Fm wiki hii.

Kipindi cha The Chart kinakuwa hewani kila Jumamosi kuanzia saa nne kamili asubuhi hadi saa sita kamili mchana. Unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii, bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.

Karrueche Tran atoa tamko rasmi kuhusu penzi lake na Chris Brown

$
0
0
Karrueche Tran ambaye amekuwa na mapenzi ya kimulimuli na Chris Brown kwa muda mrefu, ametoa tamko ambalo linaongeza hisia kuwa huenda tetesi za ukaribu wa Rihanna na Chris Brown zikawa za kweli.

Karruche ametoa tamko lake rasmi wakati akijibu swali la shabiki mmoja na kueleza kuwa Chris sio wake

Napenda Kuwa Maarufu Kama Kina Wema Sepetu, Mwili Mzuri Ninao Nifanyaje?

$
0
0
Admin , Mimi ni Msichana na miaka 19 , Napenda sana kuwa Maarufu ila sijui pa Kuanzia , Naomba uniweka katika blog nami nijulikana ntakutumia picha zaidi kwenye e-mail...naitwa Fatuma nipo Dar Kijitonyama, na Kama kuna msanii atapenda kunitumia kwenye video yake niko tayari 

Meninah Azua Jambo Asema yeye na Diamond Hawaendani Kuwa Wapenzi

$
0
0
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Meninah Abdulkareem ‘Meninah’ amefunguka juu ya tetesi zinazoeneo kuwa na uhusiano wa chinichini na Nasib Abdul ‘Diamond’ kwa kusema kuwa siyo levo yake

Akichonga na paparazi wetu, Meninah anayetamba na ngoma ya Pipi ya Kijiti alikanusha na kusema kuwa, wote ni mastaa lakini wametofautiana kwa kiasi kikubwa na kwamba hawezi kuwa naye katika mahusiano ya aina yoyote.

“Kwanza nilishawahi kukutana naye kwenye shoo tofauti na zote sikuwahi hata kuzungumza naye chochote, ni staa na mimi staa lakini tunatofautiana kuwa yeye yupo juu yangu,” alisema Meninah.

Napenda Kupiga Chabo, Mpaka Mke Wangu Mwenyewe Huwa Namchungulia

$
0
0
Wadau Sijui haka Katabia ni Ugonjwa ama Kawaida, Nimekuwa Mtu wa Kupiga chabo sana yaani kabla sijaoa nilikuwa nakaa uswahilini sasa kule mabafu yapo nusu nusu na mengine ni mabafu ya magunia tu, sasa nilikuwa nakatabia kakupiga chabo wadada ama wamama wakiwa wanaoga , kwa sasa nimeoa nina mke na mtoto mmoja ila kale katabia ka kupiga chabo bado kananisumbua mpaka nikuwa namvizia mke wangu akiwa anaoga au akiwa amekaa kihasara nampiga chabo bila yeye kujua hapo napata raha na moyo kusuuzika...Nataka niache haka katabia nifanyaje?

DIASPORA Yupi Aliyefanikiwa Kiuchumi, Kisiasa na Kijamii Awe wa Kupigiwa Mfano?

$
0
0
Huwa najiuliza na Kucheka nikiona Mijadala ya Watanzania waishio nje ya nchi jinsi wanavyojigamba na kujiona wa maana kuliko Watanzania waishio Bongo , Mijadala ya kujionesha kuwa wanazo mingi huwa kwenye blogs na kwenye mitandao ya kijamiii, William Malecela alishwahi kuwasema hawa jamaa na kuweka hali halisi ya maisha ya kuishi ulaya wakaja juu sana kumtukana vibaya kwa kuweka wazi jinsi maisha ya nje yalivyo magumu

Sasa Embu Niambieni nani ambae anaishi nje ambae amafanikiwa kiuchumi au kijamii kiivyo kiasi cha kuwa mfano mzuri kwa wanaotamani kwenda kuishi nje ya nchi ? 

Tutabanana hapa hapa Bongo

Utabiri wa Askofu Kakobe Unaendelea Kutimia: Ikulu na Mwanasheria wa Serikali watofautiana

$
0
0
Ni mazingaombwe yanayoweza kupatikana tanzania pekee duniani.

'ikulu inatoa tamko lao kuwa bunge litaendelea na katiba lazima ipatikakane bila hata ya kuwepo umoja wa katiba ya wananchi [ukawa].

Na wakati huo mwanasheria mkuu wa serikali anakuja na vituko vingine vya kuueleza umma wa watanzania kuwa bila [ukawa] katiba mpya haiwezi kupatikana.na tena anaenda mbali kwa kuwaomba kwa moyo mweupe na kiunyenyekevu wale aliowaita matumbili,ati tu kwa sababu wanapigania maslahi ya umma wa watanzania kuwa ame miss manjonjo yao ya kupigania ukombozi wa watanzania!

-hapa tukubali tukatae lazima kutakuwa na ombwe la uongozi nchini.

Na askofu zackari kakobe atashinda kwa unabii wa maneno yake kuwa c.c.m itasambaratika katika ramani ya dunia na hatutaiona wala kuisikia tena!

Ndoa Nyingi za Kizazi Hiki Zinavunjika Kwa Sababu za Kijinga, Nguvu ya Mwanamke Katika Ndoa

$
0
0
POWER OF A WOMAN IN MAKING THE MARRIAGE WORK!

1st Lesson SOMETIMES A WOMAN WINS BY LOOSING! Unaweza mwanamke ukajiona umepoteza kitu ila in reality umeshinda! Na unaweza kuona umeshinda ila in reality umepoteza. Usiendekeze hisia za moyo zinavokuongoza na wapambe! Tumia akili na busara zaidi! Mfano unapewa data mumeo yuko guest kafumanie, kuliko kwenda na kumuita shigongo kuvunja utu wako na wa mumeo na kutia doa maisha yenu shukuru tu taarifaa, mpe mumeo benefit of the doubt sali kwa Mungu wako. Kuchapiwa ni siri ya ndani indeed! Usimchunguze mumeo kama CIA au KGB sababu ukitafuta sanaa kitu utakipataaa! Manake wanawake kuna tabia unamfatilia una withold eveidence hiku unaikusanya hadi uhakikishe siku ukimsomea mashtaka hana pakutokea ushahidi unatosha kuconvict. Hahahaaaaaa!

2nd Lesson! BY NATURE MARRIAGE IS SELF DESTRUCTORY, LOOK FOR SOLN TO MAKE IT WORK! Yaani nature yenyewe mambo ya kumkinai mwenzio, kutamani vipya, ni natural tu, hayahitaki hata sababu, sasa baada ya kuwa mtu wa lawama, kulaani kwanini mambo kama hayo yawatokee, kumuona mwenzio hana shukrani, spend more time kudeal na situation kuliko mwenzio. Kama uzazi umekubongesha work out, acha kula hivo. Kuliko kudemand the impossible kuwa sababu umemzalia akupende hivo hivo kwenye jimwili jipya sio rahisi. Shirikiana kutafuta soln.

3rd Lesson USISAHAU HATA SIKU MOJA AT A POINT LIFE YOU WERE HIS NUMBER ONE NDO MAANA AKAKUOA! Hata kama anakunyanyasa saivi, heshima haipo, anachepuka, labda wewe upo number 100 saivi not even once dont let you forget once upon a time you were his number 1, he married you, yes you na mapungufu yote yako, not Lily the cutest, mima the big as.s, Rose the beauty queen etc, wote aliwaona yet still akakuona wewe ugly betty or whatever! Tatizo ni kujisahau, wakati anakuoa you might have been ugly still lakini una heshima, upo humble, etc sasa umo ndani ndo unajifanya king kong atakwambia nini si ushindani hamna! Ukiona mambo magumu rudi back in the days ujiulize ulimloga vipi wakati ule umloge tena!

4th Lesson UTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILE ILE! Unakuta mtu unamuacha mumeo kisa muhuni ana michepuko? Mwanaume gani asie na michepuko? Hahahaaa! Utamuacha wa kwanza utatafuta 2, wembe ule ule, utahangaika mpaka basi! Kabla hujamuacha mumeo kisa michepuko jiulize nani hachepuki utaempata? Au mimeo hela hana! Hata unaemkuta nazo zaweza kusiha vile vile. Tulia vumilia unyolewe. Wenzio wote wametulia wewe unajilegeza! Ifike mahala fumba macho uombe Mungu siku ziende maana hata ukisema uende kwingine mwendo ule ule! Unamuacha mumeo unaanza kuiba wa wenzio! Akili matope hayo?

5th Lesson KABLA HUJAPANIC KWA JAMBO MOJA KUMBUKA MEMA YAKE ELFU MOJA NDO UAMUE KUHUSU HIKO KIMOJA! Mtu kakuoa miaka 5, anakupa yote utakayo, anakiabudu malkia wake, hakuna unachokosa, shabash kateleza kidogo shetani kampitia sisi wote binadamu kakusoea kachepuka one time! Basi wewe. Unasahau mema yoooooote ya 5 years huko kumshika ndo unafunga mabegi na kutokomea! Khaaaaa! Au mmeishi vizuri miak 7, mwaka huu ndo kabadilika, japo uvumilie na kuomba atambue makosa na kujirudi miaka yote 7 watia kwenye dustbin, unashupalia matendo yake mwaka huu na kudai talaka! Sasa na mwanaume mda mwengine nae anakereka anaona kama wema wake wa miaka 7 sio issue basi nendaa tu! Power of love sio kufaidi goodtimes ni kuhimili mikimikiki! Wapambe nuksi kina lara 1 tunakutia ndimu ondoka bwanaa, kwanini afanye hivo, ndo unakole kweli kweli. Usiruhusu tendo moja la kijinga likupotezee 7 yrs of your life n hard work! Kwani ukisamehe hilo fumanizi utababuka? Vitakuuma vitapoa mnaanza upya! Hatoki mtu inaitwa! Atafanya visa wee akikuona mkomavu atachoka mwenyewe!

6th lesson! JIFUNZE KULET THINGS GO! Sio basi ukimfumania mara moja kila akikosea kidogo unamshikia kooni ile ugoni wa mwaka juzi. Kitu kidogo unaretrieve file! Au ulimsaidia mwaka juzi alipokwama, akikunyima hela kidogo unakumbushia, mwaka juzi fyoko fyoko! Daaah! Sio issue. Inatakiwa uwe mkomavu ukisema umesamehe kitu basi ndo unakizika kooni forever! Haukitaji tena! Unamuepusha shaitwani kukaa kati kati yenu kila wakati! Unavomsamehe mara nyingi inaondoa hata ile ladha ya kukusoea tena! Sababu anajua utamsamehe na wala hutomuuliza tenaaa! Mwenyewe anajistukia. Ananza kuona kweli huyu si binadamu wa kawaida, labda namtendea ndivo sivo.

7th lesson! MUME NAE BINADAMU LOLOTE LINAWEZEKANA! Usiwe na expectations kubwa sanaaaaaa! Ukamuona yule malaika labda hawezi kukosa. Aaaaah! Wapi! Jua tu yule binadamu kupitiwa inawezekana pia, na hata akipitiwa unajua umejipanga kusort hizo issue out kuendeleza libeneke! Ila kama ndo ulikuwa unamuona mungu mtu, siku akiteleza waweza kuga kwa pressure! Wakati cha ajabu hamnaa mbona! Kwani ye wa kwanza kufanya hivo? Au wa mwisho? Hamnaaaaa!

By Lara 1

Alikiba: Nawaomba watu Wasinikosanishe na Diamond, Sina Ugomvi Naye!

$
0
0
Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba.

“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.

Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha. Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

Bongo5

Gari lililobeba Maiti Kumi za Mafunzo Laua Wawili Mikese

$
0
0
Gari la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), lililokuwa likisafirisha maiti 10  za watu kwenda katika Hospitali ya Mtakatifu Francis Ifakara, wilayani Kilombero, limewagonga watu wawili waliofariki dunia papohapo, eneo la Mtego wa Simba, Mikese mkoani Morogoro.

Waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea saa 5:25 asubuhi jana ni dereva na abiria wa bodaboda.

Maiti hizo zilizokuwa zimehifadhiwa katika mifuko maalumu ya plastiki, zinaelezwa kuwa zilikuwa zikipelekwa katika Hospitali ya Mtakatifu Francis, ili zitumike kwa mafunzo.

Akizungumzia ajali hiyo katika eneo la tukio, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, Boniface Mbao alisema kuwa gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Pankrasi Pascal, mkazi wa Ifakara, wilayani Kilombero.

 Mbao  aliwataja waliokufa kuwa ni Shaaban Rajabu na Ally Benulo, wakazi wa Kijiji cha Mikese, waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki.

Tukio hilo limekuja siku kadhaa baada ya mabaki ya miili ya binadamu kugunduliwa ikiwa imetupwa katika dampo moja lililoko Bunju, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

Muonekano Mpya wa Lulu Michael, Kwa Mwendo Huu Sasa Anafaa Kuwa Mke wa Mtu

$
0
0


Haka Kabinti Katamu Kweli Kweli ...Kumbe Kakivaa Kiheshima pia kanapendeza , Endelea hivyo hivyo basi mamito soon utakuwa Mke wa Mtu ...Hahaha

Diamond Platnumz na Wema Sepetu Mwisho Umefika

$
0
0
Stori: Imelda Mtema na Gladness Mallya

Mwisho wa reli? Lile penzi lenye taito na mbwembwe nyingi Bongo kati ya sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ linadaiwa kufika mwisho baada ya jamaa huyo kumwandikia mwenziye waraka wa kumdhalilisha mtandaoni, Ijumaa Wikienda lina sarakasi nzima.

TUJIUNGE INSTAGRAM
Suala la Wema kukashifiwa liliibuka baada ya wadau mbalimbali ambao ni mashabiki wa Wema wanaojiita Team Wema kuhoji kwenye Mtandao wa Instagram kwamba ni kwa nini Diamond alimtumia Wema kwa kukata mauno jukwaani (hivi karibuni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza) badala ya kumfungulia biashara ya maana?

“Tujaribuni kumshauri Wema maana tunaona anatumiwa vibaya na huyu Diamond. Haiwezekani ampandishe kwenye majukwaa halafu amkatishe mauno namna ile kama kweli ana nia ya kumuoa,” aliandika mmoja wa wadau ambaye ni mfuasi wa Team Wema.
Team Wema walidaiwa kufungua mjadala huo wa kumshauri ‘msanii wao huyo wa ukweli’ kufuatia kusambaa kwa picha zinazomuonesha Wema akiwa na shosti wake, Aunt Ezekiel Grayson wakikata mauno jukwaani kupitia wimbo wa Diamond wa Mdogomdogo.

WATOA MIFANO YA WAREMBO
Wadau hao walimtaka Wema kuiga mifano ya warembo wenzake waliopita kama Nancy Sumari (2005), Hoyce Temu (1999), Faraja Kotta (2004) na wengine wengi kwa jinsi wanavyojishughulisha na shughuli mbalimbali na kuweza kuendesha maisha yao bila kudhalilishwa majukwaani.

WAKERWA WEMA KUWA MCHEZA SHOO WA DIAMOND
Team Wema walikwenda mbali zaidi kwa kusema kwamba, wanasikitishwa na Wema kutojulikana moja kwa moja anafanya kazi gani ya maana, zaidi ya kuwa na uhusiano na Diamond ambaye anamgeuza kama mcheza shoo wake wa kukata mauno.

DIAMOND AWAJIBU
Baada ya wadau hao kumshauri Wema huku wakihoji baadhi ya mambo ambayo walidai yanamdhalilisha, kupitia mtandao huohuo wa Instagram, Diamond alishindwa kuvumilia ushauri huo uliomgusa na kuamua kuandika waraka wake unaodaiwa kumdhalilisha Wema.
Katika waraka huo, Diamond alieleza kwamba yeye kama yeye huwa anamtimizia Wema mahitaji ya muhimu kama mpenzi wake na suala la kumpa mtaji wa kufanya biashara.

WARAKA WENYEWE:
“Nafikiri ningewaona kweli mna akili na mapenzi ya dhati kwa huyo msanii wenu (Wema) kama mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe zisizo na faida, huenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe, mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi. “Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka ng’ombe wake kwenye maji safi ila yeye ng’ombe mwenyewe ndiyo anatakiwa aamue kunywa maji!

“Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie miye? Nisiende studio nikae dukani nimuuzie miye? Ni juhudi zako kwanza! Leo hii hata ningepewa mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu, nisingefikia hapa nilipo! Kama nimekuchefua lamba ndimu usitapike.”

WAMGEUKIA DIAMOND
Baada ya waraka huo, mashabiki na wadau waliopo kwenye mtandao huo walimgeukia Diamond kwa kumlaumu kwamba anavyofanya siyo vizuri mbona amemfungulia dada yake Esma Platnumz duka la maana lakini Wema amekuwa akimtumia tu bila faida yoyote?

MARTIN AJIVUA UMENEJA
Kutokana na waraka huo, aliyekuwa meneja wa Wema, Martin Kadinda naye aliandika wa kwake na kutangaza kuachia ngazi ya umeneja kwa mwanadada huyo.

MAMA WEMA AFUNGUKA
Baada ya meneja huyo kubwanga manyanga, wanahabari wetu walimsaka mama mzazi wa Wema, Miriam Sepetu na kumuuliza juu ya mtazamo wake kuhusiana na penzi hilo la mwanaye ambapo alisema kwa sasa penzi hilo limemchosha hivyo anaacha ‘liserereke’.
Alisema kuwa anawaachia wenyewe waendelee kwani ni watu wazima sasa hadi pale atakapohitajika kutoa msaada kama mzazi.

“Jamani sitaki mniweke kwenye masuala ya Wema na Diamond, wao wazungushane wee mpaka watakakoamua wenyewe maana wao ni watu wazima.
“Siwezi kuwaingilia, acha liserereke tuone mwisho wake,” alisema mama Wema.
Jitihada za kumpata Wema zilishindikana baada ya simu yake kuita bila kupokelewa, achilia mbali kutojibu ujumbe aliotumiwa katika Mtandao wa WhatsApp huku mmoja wa marafiki zake akisema kuwa ishu hiyo imemchanganya.

TUJIKUMBUSHE
Penzi la Wema na Diamond limekuwa likigubikwa na sarakasi nyingi kila kukicha. Waliwahi kumwagana kipindi cha nyuma kabla ya kurudiana Oktoba, mwaka jana. Kabla ya kurudiana, kijiti cha penzi la Diamond kilikuwa kikishikiliwa na Mtangazaji Penniel Mungilwa ‘Penny’.
GPL

Mwanaume Aliye Jifanya Mwanamke na Kupewa Kazi ya House Girl Akamatwa

$
0
0
Mwanaume mmoja huko nchini Uganda Amekamatwa baada ya Kujifanya ni Mwanamke ili apate kazi ya House Girl, Zoezi lake hilo lilifanikiwa na kuweza kupata hiyo kazi lakini siku zilivyozidi kwenda Boss wake ambae ni Mama Mwenye Nyumba alishtukia mchezo na kugundua ni Mwanaume, Baada ya kugundulika jamaa alichukua kipigo kutoka kwa Majirani , alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo alijitetea akasema Maisha ni magumu na kupata kazi kama mwanaume ni ngumu...
Viewing all 104799 articles
Browse latest View live




Latest Images