Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live

Mwakyembe Apokea kwa Mshituko Mkubwa Kifo cha Msanii wa bendi ya Mzee King Kiki

$
0
0
Mwakyembe Apokea kwa Mshituko Mkubwa Kifo cha Msanii wa bendi ya Mzee King Kiki
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha aliyekuwa mwanamuziki wa dansi, Kalambay Bisongo aliyekua akifanya kazi kwenye bendi ya Wazeee Sugu ya Mzee King Kiki.



Bisongo alifariki April 18 ya mwaka huukatika Hospitali ya Mloganzila iliyopo maeneo ya Kibamba jijini Dra es Salaam. Msanii huyo amewahi kufanya kazi kwenye bendi tofauti tofauti ikiwemo Tanzania One, Achingo na baadae bendi ya King Kiki.

Soma taarifa hiyo ya Mhe. Mwakyembe hapa chini:

Waombolezaju Tumieni Picha za Masogange Zenye Staha Ili Tumpunguzie Adhabu ya Kabri- Roma

$
0
0
Waombolezaju Tumieni Picha za Masogange Zenye Staha Ili Tumpunguzie Adhabu ya Kabri- Roma
Wakati tasnia ya burudani Bongo ikiendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa video vixen, Agness Gerald ‘Masogange’, msanii wa muziki wa hip hop, Roma ametoa ushauri kwa waombolezaji kuhusu picha zinazosambaa kwa kasi mtandaoni za mrembo huyo.

Roma ameeleza wakati watu wakiendelea kuomboleza kifo cha mrembo huyo ni vema wakatumia picha zake zenye staha tofauti na ambazo zimekuwa zikitumika na baadhi ya watu. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Roma ameandika;

“Wazo langu, ni vema tuonyeshe hisia zetu kwa kupost picha zake zenye staha, ili tumpunguzie adhabu ya kaburi,” amesema Roma.

Roma ameendelea na kuongeza kuwa, “A soldier Die, A soldier Born, Chill Easy Baby, Aggy Gerry,”.

Agness alipata umaarufu mkubwa pindi alipotokea katika video ya msanii Belle 9 ambayo ilikwenda kwa jina la Masongange ndipo na yeye kuanza kutumia jina hilo. Masogange amefariki jana April 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, Dar es Salaam.

Sakata la Matibabu Lissu Amvaa Spika Ndugai "Bunge Linavunja Sheria Linaendeshwa kwa Chuki na Upendeleo wa Kisiasa"

$
0
0
Sakata la Matibabu Lissu Amvaa Spika Ndugai "Bunge Linavunja Sheria Linaendeshwa  kwa Chuki na Upendeleo wa Kisiasa"
Mbunge Tundu Lissu amefunguka na kudai sheria ya uendeshaji wa Bunge halijaweka masharti yeyote ya kupatiwa fedha za matibabu kama alivyo tangaza Spika wa Bunge Job Ndugai hivi karibuni na wala hakuna kifungu chochote kinachozungumzia kibali cha Hospitali ya Muhimbili au cha Rais Magufuli.


Lissu amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo kupitia ukurasa wa kijamii zikiwa zimepita takribani siku tatu tokea Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Mbunge huyo kuwa Bunge haliwezi kuidhinisha fedha kwa ajili ya matibabu yake kwa kuwa halijapata vibali vitatu ambavyo vingemuwezesha kupata fedha za matibabu kutoka Bungeni.

"Ukweli ni kwamba kauli ya Spika Ndugai inathibitisha jinsi ambavyo Bunge limepoteza mamlaka na hadhi yake chini ya uongozi wake dhaifu. Hata masuala ambayo Sheria haijampa Rais mamlaka, Spika Ndugai ameyakabidhi. Kauli hiyo ni uthibitisho pia wa jinsi ambavyo Bunge linaendeshwa bila kufuata sheria, kwa chuki na upendeleo wa kisiasa", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "yeye amekwenda India mara nyingi kutibiwa kabla na baada ya kuwa Spika kwa gharama za Bunge. Mimi mbaya wao niliyepigwa risasi nikiwa nahudhuria vikao vya Bunge ninakataliwa matibabu kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote. Sio kweli kwamba sikufuata utaratibu, kama maana ya neno hilo ni utaratibu uliowekwa na sheria".

Lissu ameendelea kusema..

"Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi.
Katika mazingira ya jaribio la mauaji dhidi yangu, utaratibu pekee uliokuwa unawezekana ulikuwa ni kunihamisha nchini kwa dharura. Nilikuwa nimeumizwa vibaya, mifupa imevunjwa kila mahali, nimepoteza damu nyingi na risasi zimejaa tumboni. Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi".

Aidha, Lissu amedai uamuzi wa yeye kupelekwa Nairobi nchini Kenya umetokana na makubaliano ya kikao kilichofanyika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Spika Ndugai na Naibu wake walikuwepo kwenye kikao hicho pamoja na viongozi wengine wa nchi akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dkt. Ulisubisya Mpoki na Mwenyekiti Mbowe na wabunge kadhaa walihudhuria pia.

"Baada ya kukubaliana kwamba napelekwa Nairobi, ndege ililetwa Dodoma saa sita za usiku. Uwanja wa Ndege wa Dodoma hauruhusu ndege kuruka au kutua baada ya saa 12 jioni. Nani aliyeruhusu ndege iliyonichukua kutua na kuruka saa sita usiku kama hakukuwa na kibali cha Bunge?", amehoji Lissu.

Meli Iliyokamatwa ni ya Serikali na Ilikua Ipo Kwenye Doria- Polisi

$
0
0
Meli Iliyokamatwa ni ya Serikali na Ilikua Ipo Kwenye Doria- Polisi
Jeshi la Polisi mkoani hapa limesema, meli inayodaiwa kuteka mashua na kisha ‘kutelekeza’ abiria Tanga, ni ya Serikali na ilikuwa ikifanya doria katika Bahari ya Hindi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe alisema hayo jana wakati akifafanua tukio la abiria 54 kutelekezwa nje ya jengo la kikosi cha majini cha Jeshi la Polisi.

Alisema meli hiyo haikuwateka bali iliwakamata abiria hao kwa kuwa mashua waliyokuwa wakisafiria, haikusajiliwa kubeba abiria na ilikuwa imejaza kuliko uwezo wake.

Mashua hiyo inayodaiwa kutekwa ilikuwa na hao abiria wakitokea Shimoni, Mombasa, kuelekea Pemba.

“Maofisa waliokuwa ndani ya meli ya doria ya vyombo vya ulinzi na usalama waliamua kuizuia mashua iliyokuwa ikiwasafirisha abiria hao baada ya kubaini kuwa haikusajiliwa kuchukua abiria na ilijaza kupita kiasi ndipo wakaamua kuwaleta sehemu salama,” alisema Kamanda Bukombe.

Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali imewaandalia basi maalumu litakalowasafirisha hadi jijini Dar es Salaam ambako watapanda boti ya abiria kuwapeleka kisiwani Pemba kupitia Unguja.

Wakizungumza na Mwananchi jana, abiria hao walisema baada ya kufikishwa nje ya Jengo la Polisi Marine, maofisa wa idara ya uhamiaji walichukua pasipoti zao za kusafiria kwa ajili ya uchunguzi na baadaye waliwarejeshea.

“Maofisa wa idara ya uhamiaji walikuja kuchukua paspoti zetu wakaenda nazo ofisini kwao lakini baadaye wakuatwambia hatuna matatizo,” alisema Time Bakari.

Abiria hao walilalamika kwamba maofisa wa meli hiyo ya Serikali waliwanyang’anya majaketi ya kujiokolea majini na hawakuwarejeshea.

Walisema viongozi wa Serikali walifika kituoni kuwaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kwamba tukio hilo limefanyika ikiwa ni jitihada za vyombo vya dola kuhakikisha Bahari ya Hindi eneo la Tanzania inakuwa salama.Polisi:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan aAutwa Kazi

$
0
0
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan afutwa kazi
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan Ibrahim Ghandur amefutwa kazi.

Katika taarifa iliyotolewa ni kwamba rais Omer al-Bashir amemfuta kazi waziri wake wa mambo ya nje Ibrahim Ghandur.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna maelezo kamili ya sababu kuu ya kufutwa kazi kwa waziri huyo.

Mchopanga: Nina siri Nzito ya Masogange Nitausema Siku ya Mazishi

$
0
0
Mchopanga: Nina siri Nzito ya Masogange Nitausema Siku ya Mazishi
Msanii wa filamu Juma Chikoka maarufu kama 'Chopa wa Mchopanga' anayedai ameshuhudia dakika za mwisho za kupigania uhai wake msanii wa muziki ‘Video Queen’, Agnes Gerald, maarufu Masogange' amesema mrembo huyo amemuachia ujumbe mzito ambao atausema siku ya mazishi.

Chopa ameyasema hayo jana wakati wa kikao cha dharura cha wasanii kuhusu maandalizi ya mazishi yake yanayotarajiwa kufanyika Jumatatu Jijini Mbeya ingawa ataagwa kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam kesho.

Msanii huyo ambaye ni mmoja wa marafiki wa karibu  wa Masogange, amesema dakika chache kabla hajafariki alikuwa kalala mapajani kwake na walizungumza vitu vingi ikiwemo kumpa ujumbe wa kuwaeleza Watanzania.

“Tuliongea mengi lakini kuna makubwa mawili ambayo aliniagiza niwaambie Watanzania, ila hilo nitalifanya kwa kuongea na vyombo vya habari na kuona namna sahihi ya kusaidiana kama vijana, hatupaswi kuingizana katika matatizo.

“Kwa sasa siwezi kusema alichoniambia, embu ngoja tumalize shughuli ya kumhifadhi halafu nitayaweka wazi aliyoniambia, kwani kwa sasa haitaleta picha nzuri na watu wanaweza kutafsiri ndivyo sivyo,”amesema.

Chopa amesoma alikuwa akimtembelea Masogange, tangu alazwe katika Hospitali ya Mama Ngoma. Amesema alilazwa hospitali kwa siku nne.

“Ugonjwa uliokuwa unamsumbua mbali na pumu, pia kupungukiwa damu, jana (juzi) nilikuwa nimejipanga kwa ajili ya kumtolea damu lakini ndio hivyo hakuweza kumaliza siku,” amesema.

Msanii huyo anasema amefahamiana na Masogange wakati akiwa Agnes Gerald na si Masogange, urafiki ambao umedumu hadi mauti yanamfika.

Kajala Arudi Mazima Kwa P Funk Amng'oa Mke wa P Funk

$
0
0
Kajala Arudi Mazima Kwa P Funk Amng'oa Mke wa P Funk
Muigizaji wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja amedaiwa kusababisha mke wa prodyuza mahiri Bongo, Paul Matthysse, Samira afungashe virago vyake tayari kwa kurudi kwao.



Mke huyo wa P Funk amedaiwa kufikia uamuzi huo baada ya mwanaume huyo kuonekana kurudisha majeshi kiaina kwa Kajala aliyewahi kuwa mchumba’ke zamani huku picha na video mbalimbali za kimalovee zikivuja.



Mtu wa karibu na mke wa P Funk alivujisha kuwa, Samira amefikia hatua hiyo baada ya kushuhudia matukio mbalimbali ya P Funk na Kajala na kukosa majibu yaliyonyooka. “Unajua P Funk kila alipokuwa akielezwa kuhusu Kajala alikuwa hanyooshi maelezo ingawa machoni alionesha kumpenda Kajala.


“Mkewe ambaye kwa sasa ni mjamzito, ameishi kwenye kipindi kigumu sana. Anashindwa kumuelewa P Funk kwani watu kibao wanampigia na kumuambia wamemuona mumewe akiwa na Kajala,” alidai mtu huyo wa karibu. Akizidi kushusha data, mtu huyo wa karibu na Samira alidai kuwa, mara kadhaa P Funk amekuwa akielezwa kuhusu …usaliti wake kwa Kajala lakini alikuwa akijitetea kwa kutumia kigezo cha kumlea mtoto aliyezaa na Kajala (Paula).



“Yani Samira alikuwa akimbana P Funk lakini mara kadhaa P (P Funk) alikuwa anasema hakuna lolote zaidi ya yeye kwenda kumcheki mtoto hususan anapokuwa shuleni,” alisema mtu huyo. Akizungumzia picha zilizovuja, rafiki huyo wa Samira alisema shosti wake alivumilia zile picha za awali zilizomuonesha P Funk akiwa supermarket na Kajala lakini zilivyokuja kuvuja video wiki hii, ameona isiwe tabu afungashe virago vyake.



“Hii video ya wiki hii ni balaa, anaonekana kabisa Kajala akiwa mbele ya gari, P Funk akiwa nyuma ya gari, anainuka na kumbusu Kajala huku mtoto wao Paula akishuhudia, yani pale ni live bila  chenga,” alisema rafiki huyo wa Samira na kuongeza: “Anaondoka nafikiri itakuwa Jumamosi au Jumapili ya wiki hii lakini tayari ameshafungasha kila kilicho chake kwenda kwao Arusha.”


Risasi Jumamosi lilivutia waya Samira ambapo alipopatikana na kuulizwa kuhusu suala la yeye kufungasha virago, alijibu kwa kifupi kwa hasira. “Ndio…na nyinyi nikiondoka inawahusu nini? Niacheni nimechoka jamani.”



Kajala na P Funk ambao walikuwa wapenzi kabla ya P Funk hajamuoa Samira, hawakupatikana walipotafutwa juzi lakini hata hivyo, kwa nyakati tofauti Kajala amekuwa akikanusha kuwa hajarudiana na P Funk na kumtaka Samira asijishtukie. Samira na P Funk wamedumu kwenye ndoa kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kupata watoto wawili.

Unitukane leo, kesho nife uandike R.I.P?, Mungu atupe mwisho mwema- Shamsa Ford

$
0
0
Msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford ameonyeshwa kukerwa na utamaduni wa baadhi ya vijana kupendelea kutumia lugha ya matusi mtandaoni.

Muigizaji huyo amesema badala ya vijana kufanya hivyo ni vema wakatafuta nafasi za kubadilisha maisha yao kwani bado zipo, pia kuacha kutumia muda mwingi kufanya vitu ambavyo havina faida na maisha yao.

“Tusiishi kwa kudharauliana, kutukanana, kujiona wewe bora kuliko mwingine, hizi team pia za mitandaoni ziache kutukana jamanii. Utajisikiaje unitukane leo kwenye page yako halafu kesho nife mbele yako uje uandike R.I.P?,” amesema Shamsa.

“Tutumie mitandao yetu vizuri, mbele ya Mwenyezi Mungu hakuna star, tajiri, masikini, kilema, mzuri, mbaya,..Inshaallah Mwenyezi Mungu atupe mwisho mwema,” amesisitiza.

Kwa sasa katika tasnia ya burudani Bongo kumetanda wigu jeusi kufuatia kifo cha aliyekuwa video vixen na muigizaji, Agness Gerald ‘Masogange’ ambaye alifariki jana April 20, 2018.

Mara kadhaa Shamsa Ford amekuwa akitoa nasaha mbali mbali kwa vijana. Hivi karibuni katika mahojiano na Bongo5 alisema hakuna mwanaume anayeweza kumfanya mwanamke chombo cha starehe ila inategemea mwanameke husika anajiweka vipi.

“Mwanaume hawezi akakufanya chombo cha starehe inategemea wewe na akili yako, kama unataka kuchezewa?, utachezewa basi, kama unataka uwe mwanamke wa maisha yake utakuwa kwa hiyo inategemea,” Shamsa Ford ameimbia Bongo5.

Download Hapa Application Mpya ya Udaku Special Uweze Soma Vimbwanga na Udaku Mtaani Kila Siku

$
0
0
Mpendwa msomaji wetu, tunakukumbusha Kuidownload Upya Application yetu ya UDAKU SPECIAL Maana ile ya Zamani Tutaifuta.

Kuna Marekebisho Makubwa tumeyafanya ikiwa na tatizo la Notification kutatuliwa

NB: App mpya ina Icon Nyekundu

 Bonyeza Hapa Chini

==>>Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Zari Afunguka Mapenzi Aliyokuwa nayo ‘Masogange’ kwa Watoto Wake

$
0
0
Zari Afunguka Mapenzi Aliyokuwa nayo ‘Masogange’ kwa Watoto Wake
Siku ya April 20,2018 story ambayo ilichukua headlines kwenye vyombo vya habari ni kuhusiana na kifo cha muigizaji na video vixen maarufu nchini Marehemu Agnes Gerald Masogange ambaye umauti ulimkuta katika hospitali ya Mama Ngoma Mwenge Dar Es Salaam

Zari the bosslady ni miongoni mwa mastaa walionyesha kuguswa na kifo cha video vixen huyo ambapo ametumia insta story take na  kuandika ujumbe kwa Marehemu Agnes Masogange.

>>>“Hatukuwa marafiki sana lakini tangu upate namba yangu umekua ukinitumia meseji kila mwezi na hakuna mwezi uliopita haujauliza kuhusiana na watoto wanaendeleaje pumzika kwa amani dada”

Manesi Waliofukuzwa Kazi Watoa Huduma Bure Mbele ya Viwanja vya Bunge

$
0
0
Manesi Waliofukuzwa Kazi Watoa Huduma Bure Mbele ya Viwanja vya Bunge
Manesi takriban elfu 16 waliofukuzwa kazi kwa mgomo nchini Zimbabwe wametoa huduma bure kwa watu mbele ya viwanja vya bunge la nchi hiyo, kupinga kitendo chao cha kufukuzwa kazi.


Akizungumza na waandishi wa habari nchini humo mmoja wa manesi hao Pretty Mugudza, wamesema wameona ni vyema kufanya hivyo ili kuonyesha kuwa wanajali uhai na afya za watu, lakini kugoma kwao walichokuwa wakitaka ni kuboreshewa mazingira ya kazi, kwani wanashindwa kuvumilia kuona wagonjwa wakifa kwa kushindwa kuwapa huduma kutokana na kukosa nyenzo.

“Tunafanya hivi kuonyesha tupo kwa ajili ya watu, tunachoomba sisi ni mazingira mazuri ya kufanya kazi, hatuwezi kuangalia wagonjwa wakifa hospitali kwa sababu hatuna nyenzo, tunataka kufanya kazi lakini tumezuiwa kuingia kwenye vituo vyetu vya kazi”, amesikika nesi Pretty Mugudza,.

Waziri wa Afya wa Zimbabwe  David Parirenyatwa amesema kwamba hawawzi kuwarudisha manesi hao, lakini kama wanataka kufanya kazi watume tena maombi ya kazi.

Shirikisho la Manesi nchini humo limesema mpaka sasa manesi hao hawajapokea barua yoyote kuonyesha kuwa wamefukuzwa rasmi kazi.

Menesi hao walianza mgomo Jumatatu ya April  16, 2018 wakitaka serikali kuwaboreshea mazingira ya kazi, lakini serikali iliwafukuza kazi baada ya kugoma kurejea kazini licha ya kukubali kutatua changanoto zao na kuongeza kiasi cha pesa.

Cannavaro Aipa 'Salute' Simba SC

$
0
0
Cannavaro aipa 'salute' Simba SC
Nahodha wa Klabu ya Mabingwa Watetezi Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amefunguka na kudai kuwa bado hawajakata tamaa katika kuutetea ubingwa wao japo kuwa Simba SC wamewaacha kwa kiasi kikubwa katika msimamo wa ligi mpaka sasa.


Cannavaro amebainisha hayo baada ya kikosi chake kuwasili katika ardhi ya Tanzania na muda huo huo kikiunganisha kwenda jijini Mbeya kwa lengo la kujiweka sawa kuelekea mchezo wake wa kesho dhidi ya Mbeya City ikiwa ni muendelezo wa michuano ya ligi.

"Nawaheshimu Simba SC kwa kuwa ni timu ambayo nzuri nasi pia ni wazuri ila tu kwenye ligi lolote linawezekana. Nitaendelea kuwa-control vijana waendelee kupambana mpaka jasho la mwisho kwasababu bado tuna matumaini ya kuutetea ubingwa wetu. Najua bado itakuwa kazi ni ngumu ila hatujakata tamaa kwasababu kwenye mpira lolote linawezekana likatokea", amesema Cannavaro.

Mpaka dakika hii Simba bado wanaendelea kushikilia kilele msimamo wa ligi kuu kwa alama 58, Yanga akiwa nafasi ya pili kwa alama 47 huku Azam FC ikiwa ya tatu kwa alama 46.

Rais wa Korea Asitisha Majaribio ya Siraha za Nyuklia

$
0
0

Rais wa Korea Asitisha Majaribio ya Siraha za Nyuklia
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amefanya uamuzi kusitisha majaribio ya makombora na kufunga maeneo yote yaliyokuwa yakitengeneza silaha za Nuklia.

Shirika la habari la Korea Kaskazini lilitangaza kuwa “Kuanzi leo, Aprili 21, Korea Kaskazini inaachana na majaribio ya nuklia pamoja na uzinduzi wa makombora ya kisasa,”.

Kim amesema kuwa majaribio hayo sasa siyo ya muhimu sababu uwezo wa masuala ya Nuklia wa Korea Kaskazini “umeshathibitishwa”.

Tangazo hilo la kushtukiza limekuja wakati Korea Kaskazini ikijiandaa kufanya mazungumzo ya kihistoria na nchi ya Marekani na Korea Kusini.

Rais wa Marekani baada ya tangazo hilo ameandika katika ukurasa wake wa Twitter  “Hii ni hatua nzuru na habari njema kwa Korea Kaskazini na Dunia kwa ujumla!”.

Tanzia: Mwili wa Masogange Kuagwa Kesho Leaders Club na Kusafirishwa Kijini Kwao

$
0
0
Tanzia: Mwili wa Masogange Kuagwa Kesho Leaders Club na Kusafirishwa Kijini Kwao
BAADA ya wadau wa sanaa kukaa na familia kujadili ratiba ya mazishi ya Agnes Gerald (Masogange), wameamua mwili wa marehemu utaagwa kesho (Jumapili) katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam ambapo pia patafanyika misaa maalum.

Shughuli hiyo itaanza saa tatu asubuhi hadi saa saba mchana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, baada ya hapo mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Mbeya kwa ajili ya mazishi ambapo pia kutakuwa na mabasi maalum mawili kwa wale watakaopenda kumsindikiza marehemu mpaka Mbeya.

Alichokisema Beckham Baada ya Wenga Kujiengua Nafasi Yake

$
0
0
Alichokisema Beckham Baada ya Wenga Kujiengua Nafasi Yake
Wadau mabalimbali wa soka duniani wameendelea kutoa maoni yao tangu hapo jana (Ijumaa) Arsene Wenger alipotangaza kustaafu kuifundisha Arsenal mwishoni mwa msimu huu.

Mchezaji mwenye heshima kubwa Uingereza na duniani, David Beckham ametoa maoni yake kuhusu kocha huyo huku akidai kuwa Wenger alikuwa hapati heshima yake iliyokuwa inastahili kwenye soka japo amefanya makubwa.

Beckham amesema hayo kupitia mtandao wa Instagram huku akiongeza kuwa kocha huyo alisaidia kuleta ushindani mkubwa kwenye ligi kuu hasa kwa klabu ya Manchester United.

Kupitia mtandao huo, Beckham ameandika:

Labda mtu huyu sasa atapata heshima anayostahili kwa miaka 22 ya kuleta wachezaji wakubwa, soka kubwa na ushindani mkubwa kwa sisi @manchesterunited kwenye ligi kuu. Sasa ni wakati wa kusherehekea kila kitu ambacho Arsene alitoa kwa klabu ya soka ya Arsenal @arsenal

Huu Hapa Ushauri wa Mbasha kwa JokateBaada ya Alikiba Kuoa Mwanamke Mwingine

$
0
0
Huu Hapa Ushauri wa Mbasha kwa JokateBaada ya Alikiba Kuoa Mwanamke Mwingine
Siku ya April 19,2018 msanii wa Bongo Fleva Ali Kiba alifunga pingu za maisha na mpenzi wake Amina Khalef,  Mjini Mombasa nchini Kenya na mastaa mbalimbali walitoa pongezi zao kuhusiana na maamuzi hayo aliyoyafanya Ali Kiba

Kwa upande wa muimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha ameamua kumpa Jokate Mwegelo ushauri kuhusiana na Ali Kiba kufunga ndoa kutokana na tetesi zilizokuwa zikiwahusisha Ali Kiba na Jokate kuwa ni wapenzi lakini hawakuwahi kulithibitisha hilo popote.

>>>”Usihofu Mungu hajakuacha @jokatemwegelo yakwetu inakuja😀tv zote zitakuwa live ukumbini hadi wasafi tv😀😀”

Makonda Kupima Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba kwa Lazima

$
0
0
Makonda Kupima Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba kwa Lazima
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda, anatarajia kuanza mkakati maalum wa kupima tezi dume kwa lazima nyumba kwa nyumba mkoani Dar es salaam.


Taarifa hiyo imetolewa leo na mwenyewe Paul Makonda alipokuwa akizindua warsha ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana, ikihusisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa, na kusema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba, lakini hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo.

“Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu, kuhakikisha hii kasi ya vifo vya kina baba kwa tatizo la tezi dume inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu”, amesema Paul Makonda.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Dar es salaam amewataka viongozi wote wa serikali za mitaa na viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wafike kwenye vituo vya afya vinavyotoa chanjo hiyo kwa wingi kupata chanjo.

Mwili wa Mtanzania Aliyeuwawa Wingereza Wakabidhiwa kwa Familia Yake

$
0
0
Mwili wa Mtanzania Aliyeuwawa Wingereza Wakabidhiwa kwa Familia Yake
Mwili wa Mtanzania, Leyla Mtumwa, aliyeuawa Uingereza wiki chache zilizopita, umeachiwa huru leo na kukabidhiwa kwa ndugu zake ili kuusafirisha kuurudisha hapa nchini kwa ajili ya mazishi.

Mwili huo wa Leyla ambaye aliuawa baada ya kuchomwa visu na mumewe, Kema Salum, ulikuwa ukishikiliwa na jeshi la polisi nchini Uingereza kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya kujiridhisha ndipo wakaukabidhi kwa familia.

Kutana na Mtabibu Mongwa Mganga wa Waganga...Sasa Anapatikana Mikoa Yote...

$
0
0
KUTANA NA MTABIBU MONGWA MGANGA WA WAGANGA SASA WAKO MIKOANI KARIBU YOTE NCHINI...
.
HIVYO WATATOA TIBA MAENEO YOTE YA MBEYA ,DODOMA, IRINGA , MOROGORO, MWANZA,ZANZIBAR

==>KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA

➖Husafisha nyota na kutoa Pete za bahati na kwawale walio sumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa chochote sasa njoo ujionee miujiza hapo kwahapo bila malipo yoyote malipo baada yakazi napia humpa mtu jini la mali kwayule anaye taka kumiliki bila mashariti yoyote

➖ tunatibu magonjwa mbalimbali yaliyo shindikana mpenzi aliye kukimbia nakumrudisha kwa masaa 24 tu napia natoa dawa za nguvu za kiume kuurefusha uume paka pale unapotaka .

➖natoa dawa za biashara na mvuto ==tunatoa dawa zauzazi kwa wale kina mama wenye matatizoya uzazi walio angaika kwa muda mrefu bila kupata mafanikio yoyote njoo umalize tatizo lako sasa
➖natoa mazindiko yanyumba na mwili biashara na mvuto kazini

➖ kupandisha nyota ili kungaa kupandishwa cheo kazini kurudisha mali zilizo pote zilizo ibiwa kuzulumiwa

➖kesi zilizo shindikana uzimaliza mara moja namengine mengi ya siri

Piga simu
+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657
+255 764291657

Halima Mdee Afunguka ya Moyoni Kuhusu Ripoti ya CAG

$
0
0

Mbunge wa Jimbo la Kawe (CHADEMA), Halima Mdee ameendeleza hoja kuhusu matumizi ya fedha ambazo hazijulikani zimetumikaje, kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
-
Kupitia akaunti yake katika Mtandao wa JamiiForums, Mdee amemtaka Rais Magufuli na Serikali kwa ujumla kuacha kutumia vitisho na badala yake wajikite kwenye kutoa majibu sahihi kuhusiana na matumizi ya fedha hizo, ili kuondoa mkanganyiko uliopo kwa wananchi
-
Aidha, Mbunge huyo amehoji masuala mengine 8 yenye utata yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ya CAG na kuwataka wananchi waamke kutoka kwenye usingizi wa pono unaoligharimu Taifa
-
Mwisho, Halima Mdee amemueleza Rais Magufuli kupitia hayo mambo 8, ajipime kama amefanikiwa kuinyoosha nchi au nchi imemnyoosha
Viewing all 104789 articles
Browse latest View live




Latest Images