Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Makalio ya Maimartha Jesse Yawa Gumzo, Wengine Wamnanga na Kusema Anatumia Mchina

$
0
0
Na Gladness Mallya
KUTOKANA na kubadilika kimuonekano na kila kukicha makalio kuzidi kuwa makubwa, mtangazaji maarufu Bongo, Maimartha Jesse amenangwa kwamba anatumia dawa za Kichina kuyaongeza ukubwa.

Tofauti na alivyokuwa zamani, Maimartha kwa sasa anaonekana kuwa na makalio makubwa hali ambayo imewashtua baadhi ya wadau wake wa karibu na kusema kwamba mwanadada huyo anatumia dawa za kuongeza makalio kwani yeye mwenyewe anaziuza dukani kwake.

“Yaani Maimartha anashangaza kweli kwani kila kukicha makalio yanaongezeka wakati zamani alikuwa mwembamba pia hivi sasa anaonekana kuwa ana shepu, kwanza kuna wakati hayampendezi,” alisema mdau mmoja pasipo kutaja jina.

Maimartha alipoulizwa kuhusu ishu hiyo alisema: “Jamani nimeridhika tu na maisha yangu situmii dawa za kuongeza makalio.

Picha za Mboni Mwasimba wa Mboni Show Kabla Hajawa Maarufu

$
0
0

Picha za Mboni Mwasimba wa Mboni Show Kabla Hajawa Maarufu Watu tumetoka Mbali sana Hiyo picha ya kwanza imeniacha hoi..Mboni Msela

Makalio Makubwa For Ladies Ndio HabariYa Mjini, Some are Real Blessed ! But Others Mh!

$
0
0



Ni shida Hapa Mjini kwa Wadada , Kila Mdada anataka Awe na Mkia as ndo kitu kina kiki hapa Town, Inafikia Wengine wanaamua kutafuta Makalio Fake kwa Njia yoyote ile Kama kumeza dawa za mchina ama kuvaa vigodoro..Wadada Jamani Taratibu Siku hizi Wanaume hata hatujui lipi Fake lipi Original...

Diamond Platnumz Platnumz Atajwa Kuwania Tuzo Zingine Kubwa Afrika

$
0
0
Channel O wametangaza majina ya wasanii watakaowania tuzo za
CHOAMVA mwaka huu. Diamond
ametajwa kuwania vipengele vinne
ambavyo ni pamoja na 
MOST GIFTED VIDEO OF THE YEAR, 
MOST GIFTED NEW COMER, 
MOST GIFTED AFRO POP
na MOST GIFTED EAST AFRICA

Mbunge John Mnyika Kumshtaki Pinda Mahakamani

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Ubungo Jijini Dar es Salaam Mh. John Mnyika anakusudia kumshtaki mahakamani Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda kwa kosa la ofisi yake kushindwa kutangaza tarehe pamoja na maadalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam huku akiwa ameambatana na mwanasheria wake, Mh. Mnyika amesema moja ya hoja zilizomo katika shauri watakalofungua kuwa ni kutaka mahakama imlazimishe waziri mkuu Mh. Pinda, atoe kanuni pamoja na kutangaza ni lini uchaguzi huo utafanyika baada ya kile alichodai kuwa ni kuwepo kwa kimya kirefu kuhusu kufanyika kwa uchaguzi huo.
Mh. Mnyika amesema kuwa kwa mujibu wa sheria, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa inatakiwa itangaze pamoja na kutoa kanuni za uchaguzi huo miezi miwili kabla ya mwezi Oktoba na kwamba kitendo cha ofisi hiyo kukaa kimya hakileti tafsiri sahihi juu ya hatma ya uchaguzi huo.
Mbali ya kutaka waziri mkuu atangaze kanuni na siku ya kufanyika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnyika amesema katika hoja zake ataiomba mahakama iitake serikali ibadilishe taratibu na sheria zinazosimamia uchaguzi huo ili uwe huru na wa haki.

'Kajala Nitoe Gerezani' Mume Wake Apaza Sauti Baada ya Mkwanja Kumtembelea Kajala

$
0
0
Stori: Sifael Paul
ANA hoja? Siku chache baada ya gazeti pacha la hili, Ijumaa Wikienda, toleo la Jumatatu iliyopita kuripoti juu ya utajiri mkubwa wa staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘K’, mumewe Faraji Agustino amempigia saluti na kumuomba amtoe gerezani.

KWANI ILIKUWAJE?
Machi mwaka jana, Faraji alihukumiwa kifungo cha miaka saba jela au faini ya zaidi ya Sh. milioni 200 baada ya kupatikana na hatia ya kutakatisha fedha haramu kwenye Benki ya NBC, Tawi la Dar ambapo jamaa huyo alishindwa kulipa kiasi hicho cha fedha na kujikuta ‘akiozea’ Segerea au Segedansi kama wanavyoita mastaa wa Kibongo.

UTAJIRI WA GHAFLA
Katika msala huo, Kajala alihukumiwa miaka mitano jela au faini ya Sh. milioni 13 kwa kukutwa na hatia ya kuuza nyumba yao iliyowekwa kizuizini na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ambapo alilipiwa shilingi Milioni 13 na Wema Isaac Sepetu na sasa anapeta mtaani na utajiri wa ghafla.

HOJA YA MSINGI
Baada ya kuokolewa jela na Wema, Kajala ametembelewa na utajiri ambapo amekuwa akitanua mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar, akisukuma magari ya kifahari, kupanga ghorofa maeneo ya Sinza-Madukani anayolipia Sh. milioni 3.2 kwa mwezi, akimiliki kampuni ya kuzalisha sinema ya Kay Entertainment huku akaunti yake ikiwa imenona kwa mamilioni kadhaa.

GEREZANI SEGEREA
Hivi karibuni, ‘mtu wetu’ alikwenda kumtembelea Faraji kwenye Gereza la Segerea, Dar ambapo alipata nafasi ya kutoa la moyoni juu ya mkewe Kajala ambaye alifunga naye ndoa kanisani miezi michache kabla ya kukutwa na msala huo.

Akizungumza kwa huruma, Faraji alisema habari za Kajala kuwa na utajiri wa kutupwa alianza kuzisikia kwa ndugu zake hivyo kumuomba staa huyo kumkumbuka kwenye ufalme wake.

Jamaa huyo alisema kila akikaa huwa anakumbuka good time (kipindi cha matanuzi) yao ambapo ilikuwa ni bata mwanzo mwisho hasa nyakati za wikiendi.

Kwa mujibu wa mtu wetu huyo, Faraji alimwambia: “Mwambieni K akumbuke yeye ni mke wangu. Nimemsaidia kwa mengi, asiniache nateseka huku yeye anachezea pesa ambazo anaweza kunilipia na nikatoka kifungoni. Pia akumbuke ahadi yetu ya ndoa kanisani na jinsi tulivyoishi kwa upendo.

“Bado ni mke wangu, bado nampenda sana. Nilisikia alishavua pete ya ndoa lakini ukweli ni kwamba bado mapenzi yetu yapo palepale. Kama kweli Kajala amepata utajiri naomba anitoe gerezani, sitamsahau maisha yangu yote. Kama nilivyoahidi kanisani, nitampenda na kumtunza hadi kifo kitutenganishe.”

Chanzo hicho kilidai kwamba Faraji alisema Kajala amuonee huruma, azungumze na wadau wake wote wamtoe gerezani halafu atajua jinsi ya kurejesha fedha hizo.Habari nyingine kuhusu suala hilo ilisemekana kwamba jamaa huyo ametengeneza netiweki akiwa gerezani kupitia kwa watu wake wanaomtembelea ambao wapo tayari kuungana na staa huyo ili kufanikisha jambo hilo.

INAWEZEKANA?
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanasheria wenye uzoefu na kesi za mastaa aliyeomba hifadhi ya jina alisema kwamba jambo hilo linawezekana endapo mteja (mume wa Kajala) ataomba kesi yake ifanyiwe ‘reference’ (mapitio).

“Unajua haya ni mambo ya kisheria, kwa mtu wa kawaida anaweza asiyaelewe kirahisi lakini uwezekano upo bila hata kukata rufaa.“Faraji alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (Dar). Kitakachofanyika ni kwamba kama akitaka kesi yake itafanyiwa reference kwenye mahakama ya juu.
“Baada ya hapo Faraji au wakili wake anaweza kuomba kulipa faini badala ya kifungo kwa sababu hukumu ilisema kifungo cha miaka saba au faini ya hiyo shilingi milioni 200.

“Kama kweli Kajala ana hiyo fedha si mbaya akafanya hizo process (taratibu), akamtoa mumewe,” alisema ‘loya’ huyo.

KAJALA ANASEMAJE?
Baada ya kujazwa data hizo, Jumatano iliyopita Ijumaa lilimtafuta Kajala ambaye simu yake haikuwa hewani kila ilipopigwa na hata alipofuatwa nyumbani kwake hakuwepo lakini kwenye makabrasha kulikuwa na maelezo yake juu ya mumewe alipohojiwa siku kadhaa zilizopita.

Kwa mujibu wa Kajala, Faraja bado ni mumewe na huwa anakwenda gerezani kumuona kila wikiendi na anatamani awe huru ili waendelee na maisha kwani hawakuwa wamefaidi penzi lao, hata mtoto walikuwa hawajapata.

MARAFIKI WANASEMAJE?
Marafiki wa wanandoa hao waliozungumza na Ijumaa walisema kwamba kama kweli Kajala ana nia hiyo, basi afanye hiv yo kwani itakuwa thawabu kubwa kwake kama alivyofanyiwa na Wema aliyemnusuru kifungo cha miaka mitano jela.


Mwanamuziki Diamond Platnumz Aeleza Jinsi Alivyodhalilishwa

$
0
0
Stori: Shakoor Jongo
SIKU chache baada ya kufanyiwa fujo katika shoo yake nchini Ujerumani, staa wa Mdogo Mdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameibuka na kueleza namna ambavyo alidhalilishwa nchini humo.
Diamond aliponea chupuchupu kupewa kipigo baada ya kuchelewa kwenye shoo iliyokuwa ifanyike katika Ukumbi wa Sindelfingen katika mji wa Stuttgart, Ujerumani.

Akizungumza na paparazi wetu baada ya kutua Bongo Jumanne iliyopita, Diamond alisema anasikitika kwani alidhalilishwa wakati alipokuwa akidai haki ya kumaliziwa malipo yake ya shoo euro 250 (zaidi ya sh 500,000).

“Inaniuma sana kwani mimi pale nilikuwa nasimamia haki yangu, kwani nilikuwa nawadai euro 250 sasa nikaona wananizungusha na nilipokomaa zaidi huku wakiona muda wa shoo unapita, ndipo walipoanza kunitukana bila sababu.

“Wamenitukana mimi, wamewatukana hadi ndugu zangu ambao hawakuhusika na chochote na wala hawakuwepo kule. Wamenidhalilisha bila kosa. Kimsingi sikutaka kupanda jukwaani pasipo kumaliziwa fedha zangu licha ya kuwa si nyingi kiivyo,” alisema mtoto huyo wa Tandale.

Kwenye maelezo menginena paparazi wetu, Diamond alisema baada ya kutokea vurugu hizo alilazimika kurejea nchini pasipo kumaliziwa fedha zake lakini promota wa shoo hiyo, Kamabritts aliahidi kuandaa shoo nyingine ya bure ili kujisahihisha kwani kosa lilikuwa la kwake.

Kwenye mvutano huo kati ya msanii na promota huyo, Diamond alitegemewa kupanda jukwaani saa nne usiku lakini ilishindikana hadi ilipofika saa 10 alfajiri kitendo ambacho kilisababisha mashabiki wafanye vurugu kwa kuvunja viti na thamani nyingine za ukumbi zinazokadiriwa kufikia Euro 128,222 (Sh. milioni 280).
GPL

Mwanamke Akikujibu SMS yako Hivi Acha Haraka Sana Kuchat Nae

$
0
0
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.

KWA MFANO: 
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'', usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela dear''

2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''

3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi'' usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''

4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa upo serious.

Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu ''pole wangu, mambo mengine vipi?''

Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao unakuja mbele yako. 

By Dr. MCHUNGUZI HURU


Bunge Lakataa Elimu ya Kidato cha Nne kwa Wabunge, Sasa We Jua Kusoma na Kuandika Tu Ubunge Unao

$
0
0
 Pendekezo la Rasimu ya Katiba kuwa wabunge walau wawe na elimu ya kidato cha nne limetupiliwa mbali na wajumbe wa Bunge Maalumu, baada ya Kamati karibu zote kulikataa.

Kamati hizo zimependekeza kigezo cha elimu kuanzia walau kidato cha nne kama sharti muhimu la mtu anayetaka kugombea Ubunge kiondolewe, badala yake mgombea ama ajue tu kusoma na kuandika, au ajue kusoma na kuandika Lugha ya Kiswahili au Kiingereza kama ilivyo kwenye Katiba ya sasa.Mbali na pendekezo hilo, kamati hizo zimegawanyika kuhusu Ibara ya 129 ya Rasimu ya Katiba inayowapa wananchi nguvu ya kumuondoa mbunge wao madarakani kabla ya miaka mitano kumalizika.

AY Apendekeza Kiwango Bora cha Show Wanachopaswa Kulipwa Wasanii Wakubwa Tanzania

$
0
0
Malipo ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya Tanzania katika shows ni sehemu ya kilio cha wasanii hao ingawa wapo wachache wanaotangaza kuneemeka na kipato hicho.

Akiwa katika Maskani ya 100.5 Times Fm na Gardner G Habash, msanii wa kimataifa Ambwene Yesaya amependekeza kuwa wasanii wakubwa wa Tanzania (A-List) walipwe wastani wa shilingi milioni kumi na tano (15,000,000) kwa show moja ili kukuza zaidi kiwanda cha muziki.

AY ameeleza kuwa endapo wasanii wakubwa watalipwa vizuri itakuwa nafasi nzuri ya wao kuongeza nguvu na kufanya show nzuri zaidi ili waongezewe kipato na wasishuke. Lakini pia kiwango hicho kitawahamasisha zaidi wasanii walio katika madaraja mengine ya chini kuongeza bidii ili kufikia kiwango hicho.

Ameongeza kuwa endapo wasanii watakuwa wanalipwa vizuri watatoa ajira zaidi kwa watu wengine wakiwemo dancers, wauzaji wa nguo za shows, watu wa back vocals, wasaidizi binafsi na wengine.

Hivi sasa msanii anaelipwa kiasi kikubwa zaidi kwa shows za ndani ni Diamond Platinumz. Kwa mujibu wa meneja wake, Babu Tale hawafanyi shows nchini bila Tsh. 15,000,000.

Hata hivyo kiwango hiki kina utofauti mkubwa na viwango vya wasanii wengine wakubwa nchini wanaofanya shows za nyumbani.
Udaku Special Inakubaliana na Pendekezo la AY ..Je Wewe?


Nick Cannon Akana Taarifa za Kuwa na Ugomvi na Mariah Carey, 'Nisingeweza Kusema Hivo'

$
0
0
Mchekeshaji Nick Cannon amekanusha taarifa zilizotolewa wiki kadhaa zilizopita kuwa yeye na mkewe Mariah Carey wana ugomvi mkubwa na kwamba hawaishi nyumba moja  kwa zaidi ya miezi mitatu.

Nick Cannon ameonesha kuwa maelezo hayo yalitengenezwa na hayakutolewa kwake na kwamba yeye asingeweza kusema hivyo.

“Trouble in Paradise” is the dumbest phrase I’ve ever heard! I would never say that s***” Ametweet kwa hasira katika moja ya tweet yake.

Unaweza kujiuliza alikuwa wapi muda wote huo kukanusha, lakini kwa kufahamu swali hili Nick Cannon amelitolea majibu.

“Binafsi nimekuwa nje ya mitandao ya kijamii miezi kadhaa iliyopita kwa sababu za kawaida lakini najisikia hitaji la kutaka kuzungumzia.
Nick amemsifu sana Mariah kwenye tweets zake akimuita mama bora aliyembariki kwa kumpatia watoto.

Gardner G Habash Azungumzia Tetesi za Kuachana na Lady Jay Dee na Chanzo Chake, 'Hatuna Tatizo'

$
0
0
Gardner G Habash amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kwenye mitandao kuwa yeye na mkewe Lady Jay Dee wako kwenye wakati mgumu wa ndoa yao.

Akizungumza katika Exclusive Friday ya 100.5 Times Fm, Gardner ameeleza kuwa hizo ni taarifa zisizo za kweli ambazo amekuwa akizisikia tu.

“Hakuna tatizo. Kusema ukweli nimekaa na Lady Jay Dee kwa miaka mingi sana na hii sio mara ya kwanza kuzungumzwa kwa mambo kama hayo. Na tumeshazoea. Hata kama kuna kitu kinazungumzwa, mimi hata sina habari kwa sababu nimeshazoea. Kwa hiyo na mimi pia nimesikia kama ulivyosikia wewe. Lakini tatizo hakuna.” Amesema Gadner.

Ameeleza kuwa chanzo cha tetesi hizo kinaweza kuwa siku ambayo yeye alionekana polisi  katika kesi ya usalama barabarani na Lady Jay Dee hakufika.

Amesema huenda watu walichukulia tofauti lakini ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyemshauri asiende ili kuepusha attention zaidi.

Na kwa watu kuzungumza…unajua Jay Dee ni mtu mashuhuri, ni mkubwa sana. Kiasi kwamba kitu kidogo tu kikitokea, hata akijikwaa kinazungumzwa kwa ukubwa huo. Kwa mfano mimi nimepata shida kidogo ya kesi ya traffic, kwa hiyo nikamshauri mwenzangu asije pale polisi kwa sababu ya kuogopa tu vitu kama mapicha na nini. Kumbe watu walinotice kwamba hakuja. Kuanzia hapo ndio ikaanza ‘aah kuna tatizo..kuna tatizo’.

Lakini kwa kweli kuzungumzwa kwa msanii mkubwa kama yule ni jambo la kawaida. Na ni jambo ambalo ameshalizoea na mimi nimeshalizoea pia.”

Hivo karibuni Jide alipost picha ya mkono inayoonesha pete yake ya ndoa kumaanisha uimara wa ndoa yao tofauti na kilichokuwa kikisemwa.

Amng'ata Midomo Mpenzi Wake Wakati Wanakiss kwa Kuhisi ana Mchepuko wa Facebook

$
0
0
Udaku Special Tumepata habari kutoka Uingereza ya kusikitisha ya kijana Rhys Culley kumng’ata vibaya midomo mpenzi wake Chanttelle Ward mwenye umri wa miaka 18 wakati anamkiss baada ya kuwa na ugomvi unaohusisha na wivu wa mapenzi.

Kijana huyo wa miaka 23 alikuwa na wasiwasi baada ya kuhisi kuwa mpenzi wake alikuwa anachat na mwanaume kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook akimsaliti.

Akisimulia mkasa huo mbele ya jopo la majaji, Chanttelle ameeleza kuwa baada ya kutoka kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mama yake msichana huyo walielekea nyumbani kwao ambapo Rhys alianzisha mzozo akimtuhumu kuwa anamsaliti kupitia Facebook.

Kijana huyo alichukua simu ya Chanttelle kwa makubaliano ya kuangalia jumbe alizokuwa anatuma Facebook lakini hakukuta mawasiliano kati ya msichana huyo na mwanaume aliyekuwa anamhisi. Moja kwa moja akaanza kupaza sauti kwa hasira akidai kuwa amezifuta.

Hasira za kijana huyo zilimuogopesha akaona ni bora ampigie simu mama yake lakini alinyang’anywa simu. Rhys alifunga mlango na kuendelea kumshambulia kwa maneno.

Chanttelle anaeleza kuwa mgogoro huo ulipofikia hatua ya kupoa hivi, kijana huyo alimkiss huku akimuuliza kama kweli ana mpenda na hapo ndipo kila kitu kilibadilika.

“Aliweka mdomo wake wote kuzungumguka lips zangu na kuvuta, nilidhani lips zote zimetoka. Damu zilisambaa kila sehemu.” Msichana huyo alieleza.

Show ya Fiesta Musoma Yaahirishwa Kufuatia Ajali ya Mabasi 2 iliyosababisha Vifo vya Zaidi ya Watu 45

$
0
0
 Ajali hiyo imehusisha basi la MWANZA COACH T736 AWJ lililogongana na gari lingine la J4 Express T677 CYC. Miili ya marehemu na majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya mkoa iliyopo Musoma mjini.

Akizungumza na Bongo5 leo, Mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba amesema uamuzi huo umeendana na majadiliano na wasanii jinsi ya kutoa msaada kwa wahanga.

“Tumefikia uamuzi wa kuahirisha tukio hili ambalo linahusu watanzania wengi, idadi ya watu 60 kwenda mbele, ni namba kubwa sana, hatuwezi kusema tuendelee na tamasha kwa leo. Kwahiyo pamoja na kwamba maandalizi yote yalikuwa tayari kabisa, watu walio =nunua tiketi zao tumekaa na uongozi pamoja wasanii wenyewe tumeona ni lazima tuwape heshima wale waliopoteza maisha yao, kuomboleza pamoja nao waliopotelewa na ndugu zao. Lakini pia tunawapa pole wale waliopatwa na majereha. Leo yenyewe sasa hivi wasanii, wanajitolea kila mtu anajitolea kiasi kidogo kununua mahitaji ya kupeleka hospitali. Kwahiyo hapa kuna kundi la wasanii ambalo wamekwenda kununua vifaa vya kuwasaidia wagonjwa na taratibu nyingine zinazoendelea,” amesema Ruge.

Baadhi ya wasanii walipata nafasi ya kuzungumza na Victoria FM na kutoa pole kwa wakazi wa Musoma pamoja na mkoa wa Mara kwa ajali iliyotokea.

Barnaba
Tumeguswa kama binadamu wenye kupenda wenzetu waendelee kuwepo, kwa sababu huwezi jua na wenzetu wana mchango gani kwenye hii sanaa tunayoifanya. Mungu hawalaze mahali pema peponi, tufanya maombolezo.

Christian Bella
Kwanza tunawapa pole wale wote ambao wamepata matatizo kwa siku ya leo, pia ninawapa pole wale wote waliokutwa na matatizo.

Edu Booy
Kitu ambacho ninaweza kusema mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, hii ni njia ya wote dunia ni daraja sote tunavuka.

Roma
Pole kwa watu wote waliofiwa na ndugu zao, tunajua tumepoteza mama zetu, baba zetu na ndugu zetu , sisi wasanii tumewapoteza mashabiki wetu na tunajua kabisa kuna watu walipanga kuhudhuria Serengeti fiesta ila leo hawapo tena. Kwahiyo ni jambo ambalo kweli limemgusa kila msanii na mdau ambaye alikuja kwenye Serengeti Fiesta. Tunawapa pole tena na tunawaombea wote waliotangulia mbele ya haki.

Shilole.
Kiukweli nimepoteza ile furaha yangu ambayo nilikuwa nayo kwa sababu ya kupata taarifa za msiba wa ajali ya gari kiukweli nikiwa kama mwanamke imeniuma sana ila siwezi kupishana na kazi ya mwenyezi Mungu.

Blog ya Jiachie imeeleza kisa cha ajali hiyo kuwa:

Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa

Hizi ni baadhi ya picha katika eneo la tukio hilo.



Nuhu Mziwanda: Uhusiano Wangu wa Kimapenzi na Shilole Umenipa Kick ya Kutoka Kimuziki

$
0
0
Mwaka 2013 ni watu wachache tu waliokuwa wakilifahamu jina la Nuh Mziwanda kwakuwa alikuwa msanii mchanga anayetafuta nafasi yake kwenye muziki wa Tanzania. Wimbo wake ulioanza kumtambulisha uliitwa ‘Otea Nani’ ambao ulipata nafasi kiasi kwenye vituo vya redio.

Lakini jina la muimbaji huyo lilikuja kuwa kubwa zaidi baada ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na Shilole, uhusiano ambao umekuwa wa wazi katika mitandao yao ya kijamii. Kuonesha kuwa ana mapenzi ya kweli kwa Shilole ambaye ni mama wa watoto wawili, Nuh alijichora tattoo mkononi yenye jina la Shilole.

Shilole pia aliamua kumpa shavu mpenzi wake kwa kuonekana kwenye video ya wimbo wake ‘Msondongoma’ na hivyo kumwongezea wigo zaidi. “Yeye ndo Mama watoto Mungu akijaalia,” aliandika Nuh kwenye picha ya Shilole aliyoiweka kwenye akaunti yake mtandao wa Instagram yenye followers zaidi ya 19,000.

“Ukichagua kitu roho yako inapenda raha sana.sasa kwa mfano mimi Mziwanda nna haja gani ya kucheat wakati mtoto ana kila kitu, kiukweli napenda mke wangu alivyojaa jaa mie hoooooi,” aliandika kwenye picha nyingi ya Shilole.

Naye Shilole kwenye picha aliyoiweka kwenye mtandao huo akiwa na Nuh Mziwanda aliandika, “Ilove my baby,” kudhihirisha upendo wake. Hakuna shaka kuwa uhusiano huo umemwezesha Nuh Mziwanda kukuza jina lake na ameutumia vizuri kujitambulisha zaidi.

Picha: Huyu Ndiye Girlfriend wa Mwanamuzi Ben Pol?

$
0
0
Ben Pol ni msanii ambaye amekuwa nadra kuingia kwenye headlines zinazohusu mapenzi ya mastaa wa bongo na pia ni miongoni mwa wasanii wasioweka hadharani mahusiano yao ya kimapenzi.

Lakini safari hii muimbaji huyo wa ‘Unanichora’ amepost picha iliyozua maswali mengi, lakini yote yakihitaji jibu moja tu, ‘Huyu ndiye ‘baby’ wa Ben Pol?

Katika picha Ben Pol anaonekana kifua wazi huku pembeni yake yupo mrembo aitwaye Latifah Mohamed aliyekuwa mshindi wa pili katika Miss Tanzania 2013.
Credits:Bongo5

Kivazi cha Kajala Kilichozua Tabu Mitandaoni, Upaje Nje Nje

$
0
0
Mwanadada Kajala anaye Make headlines nyingi kwa sasa akiwa katika pozi na Kivazi Kilichozua Tabu Mitandaoni, Upaje Nje Nje, Anazidi Kupendeza tu Shosti Wetu wa Ukweli..

Jipya Kuhusu Young Killer Kumbe Alishatoa Mahari Kimya Kimya Baada ya Kupewa Kitisho Hiki

$
0
0
Rappa kutoka 88.1 Mwanza ambaye msimu wa Serengeti Fiesta 2012 ulifanikiwa kumuwakia na kuwa mshindi wa kwanza kwenye mashindano ya Serengeti Super Nyota Young Killer leo amehusishwa tukio la kutoa mahari kimya kimya bila kumfahamisha mtu.
Mezani kwa Soudy Brown,Young Killer ameulizwa kuhusu madai hayo ambayo inasemekana mzazi wa msichana anayetajwa kuishi nae Halimaty alimwambia Young Killer kuwa kama asipotoa mahari atampiga ‘Allah Badili’
Young Killer alipopigiwa na Soudy Brown kadai yuko kwenye ndege anajiandaa kwenda Musoma kwenye Serengeti Fiesta hivyo ametakiwa kuzima simu na kuahidi atampigia baadae simu Soudy Brown. Sikiliza Hapa:

Wakati Mkiongea ya Germany,Diamond Anafanya Yake South Africa na MTV Base

$
0
0
Siku ya Jana mwanamuziki nguli wa Bongo fleva , Diamond Platnumz yupo nchini Africa Kusini akishoot kipindi na Televisheni ya MTVBase ya nchini humo. Bado haikuweza kujulikana kipindi hicho kinahusu nini lakini itaelekea kitakua si tu kuhusu Diamond bali Tanzania kwa ujumla baada ya Diamond kuanza kurekodia kipindi hicho kwenye balozi za Tanzania nchini Africa kusini

Lundenga na Miss Tanga Wazichapa Kisa Mchepuko, Lundenga Akamatwa

$
0
0

KW/RB/8441/2014 imemshikilia Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashimu Lundenga kwa madai ya kuzichapa na Miss Tanga 1997, Mona Faraja ambaye pia ni mke wake na kumsababishia majeraha, Risasi Jumamosi lina ‘full’ stori.

Ishu hiyo iliyonyakwa laivu na majirani ilijiri usiku wa Jumatano iliyopita maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar, nyumbani kwa Lundenga wakati wawili hao walipokuwa wamepumzika baada ya mihangaiko ya mchana kutwa.Kwa mujibu wa mtoa habari wetu, wakiwa wanabadilishana mawazo, mara simu ya Lundenga iliita na ndiyo chanzo cha mtafaruku, upi huo?

TUJINGE NA CHANZO
Mtoa habari wetu alisema kuwa, tatizo lilikolea mara baada ya simu hiyo kuita mfululizo kwa namba ngeni iliyodaiwa kuwa ni ya ‘kichenchede’ cha pembeni huku bosi huyo akiwa hana mpango wa kuipokea.

“Mke wa Lundenga alikuwa na shauku ya kujua nani anayepiga simu ya mumewe muda huo na kwa nini mumewe haipokei lakini wakati akiendelea kujiuliza ndipo ikaingia meseji ambapo inadaiwa Lundenga alikwenda ‘fasta’ kwenye inbox na kuifutilia kwa mbali.

“Kitendo cha kufuta SMS hiyo nacho  kilitibua kabisa hali ya hewa, Mona akataka kujua kwa nini mumewe alikuwa hataki kupokea simu na SMS iliyoingia ilitoka wapi? 
“Mona akawa mkali baada ya kuona haridhishwi na majibu ya mumewe ndipo alipoanza kutoa maneno yenye shutuma kwa mzee mzima ambapo naye uvumilivu ulimshinda kama binadamu wengine, wakaanza kutwangana,” kilisema chanzo hicho.

MKE AWAHI POLISI
Chanzo hakikuwa tayari kuweka ‘fullstop’, kiliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kuwa, baada ya mke kuona anazidiwa kwa kushushiwa makonde mazito yaliyomvimbisha uso, usiku huohuo  alikimbilia Kituo cha Polisi Kawe, Dar kumripoti mumewe.

POLISI WAMKAMATA LUNDENGA
Mara baada ya mke kumaliza malalamiko yake kituoni hapo, saa chache baadaye polisi walifika nyumbani wakiwa na difenda ambapo walimchukua mlalamikiwa huyo hadi kituoni kujibu madai hayo.
“Polisi hawakuwa na maneno mengi, walipofika nyumbani walimkamata Lundenga na kwenda kumlaza kituoni kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria,” kilisema chanzo.

MAJIRANI WANENA
Baadhi ya majirani waliolitambua sakata hilo walionesha kushangazwa huku wakimhurumia Mona ambaye alikuwa ameumia usoni, hususan mzunguko wote wa jicho la kushoto.

MKE AINGIWA NA HURUMA
Wakati gazeti hili likiwa katika hatua za mwisho kuelekea mitamboni, Mona alidaiwa kuingiwa na huruma kwa kitendo cha kumlaza mumewe kituoni hivyo alikwenda kwa lengo la kumfutia mashitaka.

“Mke alimuonea huruma mumewe licha ya kupewa kipondo maana wamedumu kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 10 sasa, si mchezo. Alikwenda Kawe kufuta kesi lakini polisi wakamkomalia kwamba ishu lazima ifike mahakamani,” kilisema chanzo.

Mwandishi wetu alifika kituoni hapo na kukuta polisi na Mona wakiendelea na mazungumzo lakini hadi tunakwenda mitamboni, Lundenga alikuwa bado anashikiliwa kituoni hapo.
GPL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images