Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Sakaya Amkingia Kifua Maalim Seif bungeni

$
0
0

NA FATUMA MUNA
Mbunge wa Kaliua (CUF), Magdalena Sakaya ameweka wazai kuwa  yeye ndiye anayepaswa kuhojiwa kuhusu matumizi ya Chama cha Wananchi (CUF) na si Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad.

Sakaya ametoa kauli hiyo leo bungeni Juni 5, 2018 wakati akichangia hoja ya Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji aliyetaka Maalim Seif kuhojiwa kwa kutokupeleka taarifa za CUF kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Maalim Seif toka mwaka 2016 hayuko ofisini. Mimi ndiye najua matumizi ya CUF napaswa kuhojiwa. Suala la kusema Serikali imetoa fedha, ruzuku imetolewa kwa CUF kama taasisi na Takukuru ije kunihoji mimi na si Maalim Seif. "Huwezi kujua mambo ya ofisi kama hauko ofisini, hawezi kujua mambo ya ofisini kama yuko mitaani,” amesema.

Awali Mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kumhoji Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kwa kutokupeleka taarifa za matumizi za chama kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akichangia bajeti ya wizara ya fedha na mipango ya mwaka 2018/19 leo bungeni Juni 5, 2018, Khatibu alisema kwamba Seif  hajakitendea haki Chama kwa kuacha kupeleka hesebu kwa CAG.

“Kama chama changu kimeshindwa kupeleka taarifa zake kwa CAG kukaguliwa na kama hakijapeleka, Napata wapi ujasiri wa kuhoji  Sh1.5 trilioni?.

Serikali yafunguka Millioni 50 za JPM Kwa Kila Kijiji

$
0
0
Serikali yafunguka Millioni 50 za JPM Kwa Kila Kijiji
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema ahadi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji itaanza kutekelezwa mara baada ya mfumo wa kuanza kuzitoa utakapokamilika.

Dk Mpango ametoa kauli hiyo leo jioni bungeni wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Karagwe (CCM), Innocent Bashungwa aliyoitoa wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati kupitia vifungu kwa vifungu vya Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango ya mwaka 2018/19.

Bashungwa amesema, “Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020, tulitoa ahadi ya kutoa Sh50 milioni kila kijiji.” “Bajeti ya mwaka 2016/17 ilitengwa Sh60 bilioni na mwaka 2017/18 ilitenga Sh60 bilioni lakini mpaka sasa hazijaenda, nataka kujua kwa nini hazijaenda?” Amehoji.

Akijibu hoja hiyo, Dk Mpango amesema, “ni kweli jambo hili ni ahadi ya chama na ninaomba nikumbushe kwamba ni ahadi ya chama kwa kipindi cha miaka mitano.

Watu Watatu Wakamatwa kwa Kuwapa Simba Sumu

$
0
0
Jana June 5, 2018 stori kutoka Jeshi la Polisi mkoani Mara limewatia mbaroni watu watatu kwa tuhuma za kuwapa sumu simba tisa katika mbuga ya Serengeti.

Inaelezwa kuwa maafisa wa mbuga ya Serengeti  waligundua mizoga ya simba wikiendi iliyopita na walikuta watuhumiwa hao wamewakata mikia na miguu simba hao na kuondoka nayo.

Msemaji wa Hifadhi ya Taifa Pascal Shalutete amesema kuwa waligundua vifo vya simba hao baada ya kula mizoga ya ng’ombe waliokuwa wakifugwa kandokando ya hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbuga ya wanyama ya Serengeti ndio mbuga kubwa na mashuhuri nchini Tanzania ikiwa na kilomita zaidi ya elfu 14 huku kwa mwaka ikitajwa kutembelewa na watalii zaidi ya laki tatu na nusu.

Aidha watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani upelelezi ukikamilika.

Sababu ya Falz Kupewa siku 7 Kufuta Video ya “This is Nigeria”

$
0
0
Staa wa muziki kutokea Nigeria Falz ambaye anatamba na ngoma yake ya “This Is Nigeria” amepewa siku saba kufuta video hiyo kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kikundi cha kutetea haki za Waislamu cha Nigeria(MURIC).

Kikundi hicho cha MURIC kinadai kuwa wimbo huo umevunja sheria za Kiislamu kutokana na staa huyo kuwatumia wasichana waliovaa hijab kwenye video yake ya “This Is Nigeria” na hivyo Falz kujitetea kuwa aliwatumia wasichana hao kufikisha ujumbe kuhusu wasichana wanaoshikiliwa na Boko Haram.

Mkurungezi wa MURIC ameonekana kutovutiwa na jibu alilolitoa mwanamzuiki huyo na kumtaka afute video hiyo na kumtaka awaombe Wanigeria msamaha na kudai kuwa video hiyo imetia uchochezi wa kidini na ikishindikana kufanya hivyo basi atachukuliwa hatua za kisheria.

Floyd Mayweather Ashika Namba Moja Kwa Utajiri Zaidi Duniani

$
0
0
Floyd Mayweather Ashika Namba Moja Kwa Utajiri Zaidi Duniani
Bondia wa nchini Marekani, Floyd Mayweather ametwaa tena nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wanamichezo 100 matajiri zaidi duniani kwa mujibu wa Jarida la kibiashara la Forbes.

Bondia huyo alijipatia kitita cha Dola za kimarekani milioni 275 kufuatia ushindi wake katika pambano dhidi ya Conor McGregor, ambaye ameshika nafasi ya nne katika orodha hiyo.

Mwanasoka nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye aliongoza orodha hiyo kwa miaka miwili mfululizo ameshuka hadi nafasi ya tatu akipigwa kikumbo na mpinzani wake wa Barcelona, Lionel Messi ambaye ameshika nafasi ya pili.

Katika orodha hiyo hakuna mwanamichezo mwanamke, baada ya mwanamkee pekee aliyekuwepo mwaka jana Serena Williams kuondolewa.

Wanamichezo hao 100 kwa ujumla wao walijipatia Dola za Kimarekani bilioni 3.8 likiwa ni ongezko la 23% kutoka mwaka jana limeeleza Jarida la Forbes, ambapo dereva wa mashindano ya Langalanga kutoka nchini Uingereza Lewis Hamilton akishika nafasi ya 12 na mapato ya dola milioni 51.

Hata hivyo wachezaji wa mpira wa kikapu wamedhibiti orodha hiyo kutokana na kulipwa mishahara minono iliyochochewa na mikataba kati ya Ligi ya NBA na makampuni ya Televisheni hasa matangazo yanayofikia dola bilioni 34.

Nay wa Mitego Amshambulia Babu Tale Kisa Daimond na Zari

$
0
0
Nay wa Mitego Amshambulia Babu Tale Kisa Daimond na Zari
BAADA ya hivi karibuni Meneja wa Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’; aitwaye Hamis Taletale ‘Babu Tale’ kuibukia Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya kumuombea msamaha msanii wake huyo kwa mzazi mwenziye, Zarinah Hassan ‘Zari’, Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amemvaa meneja huyo kwa kuchelewa kwake kuchukua hatua.

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Nay alisema kitendo cha Babu Tale kwenda Sauz kumuombe msamaha Diamond ni kizuri lakini angekifanya tangu awali na kuhoji kwa nini amesubiri yeye (Nay) aoneshe nia ya kuwapatanisha wapenzi hao ndiyo akachukua wazo hilo na kulifanyia kazi.

“Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

“Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine.

“Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli,” alisema Nay.

ILIKUWA HIVI

Awali baada ya Diamond kuachia wimbo mpya wa Iyena, Nay alimpongeza kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka na maneno mengine makali ya kuwaita wanawake anaokuwa nao kwenye uhusiano hawana nyota ila Zari ndiye mwenye nyota.

Baada ya kuandika hivyo na maneno mengine makali yasiyoandikika gazetini watu mbalimbali mitandaoni wamekuwa wakimwita Hamisa Mobeto ambaye pia ni mzazi mwenza na Diamond jina baya. Nay alipoulizwa kuhusiana na jina hilo alisema hakumtaja mtu bali alijiandikia kwa watu wote na hajamtuma mtu kumwita Mobeto jina au maneno aliyoandika yeye.

Simba Yakanusha Kujiuzulu kwa Kocha Wake

$
0
0
Simba Yakanusha Kujiuzulu kwa Kocha Wake
Kocha msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Simba, Masoud Djuma, amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni mapema jana, kuwa amejiuzulu kuifundisha timu hiyo huku akisema yeye bado yupo sana.

Akifanya mahojiano maalum na msemaji wa klabu hiyo Haji Manara mjini Nakuru Kenya ambapo timu hiyo ipo, Masoud amesema hizo habari si za kweli ni uzushi tu wa watu hivyo mashabiki wazipuuze.

''Sijui haya maneno yametoka wapi, mimi bado nina mkataba na Simba, nimetoka nyumbani kuja kuitumikia Simba na kile kidogo Mungu amenipa nitakitoa kusaidia Simba mpaka mkataba wangu uishe, sina mawazo ya kujiuzulu leo wala kesho labda wanifukuze'', amesema.

Kwa upande mwingine mkataba wa kocha mkuu wa Simba Pierre Lechantre unamalizika June 18, lakini bado haijawekwa wazi kama ataongezewa mkataba au ataondoka. Lechantre alisaini mkataba wa miezi sita na klabu hiyo kukiwa na kipengele cha kuongezewa endapo watajiridhisha na kazi yake.

Timu ya Simba kwasasa ipo mjini Nakuru Mkoa wa Bonde la Ufa nchini Kenya kwenye michuano ya SportPesa Super Cup ambayo imefikia hatua ya nusu fainali baada ya kushinda robo fainali kwa penati dhidi ya Kariobangi Sharks.

Mafundi Waelezea Upekee wa Jeneza la Pacha Walioungana Maria na Consolata

$
0
0
Mafundi waelezea upekee wa jeneza la pacha walioungana Maria na Consolata
Kitabu cha maisha ya Maria na Consolata Mwakikuti kinafungwa leo watakapozikwa katika makaburi ya Tosamaganga, Iringa vijijini.

Jeneza litakalotumika kuhifadhi miili ya pacha hao walioungana ni la kipekee lililoandaliwa kwa siku nzima ya jana.

Mkurugenzi wa karakana ya Mandela iliyotengeneza jeneza itakamohifadhiwa miili ya pacha hao, Kihwelo Mandela alisema walitumia siku nzima kulikamilisha kutokana na namna lilivyohitaji ufundi wa kipekee.

Fundi mkuu wa karakana hiyo, Oscar Mfugale alisema tofauti ya jeneza hilo na mengine inatokana na vipimo vilivyotumika.

Alisema jeneza la kawaida huwa na upana wa futi 1.5, lakini la akina Maria na Consolata lina upana wa futi tatu.

Mfugale alisema jeneza hilo litakuwa na urefu wa futi tano na kina cha futi mbili, tofauti na la kawaida ambalo kina chake ni futi moja.Padri aliyesimamia ujenzi wa kaburi, Benedict Chavala alisema uamuzi wa pacha hao kwamba wazikwe kwenye makaburi ya Tosamaganga ambako huzikwa viongozi wa Kanisa Katoliki ni wa busara na utasaidia kuendelea kuwaenzi.

“Wakiwa karibu nasi tutawafanyia ibada kila siku, tutawakumbuka kwa sababu ni watoto wetu waliolelewa na masista, hivyo ni busara kuzikwa hapa,” alisema.

Aliwataka ndugu wa pacha hao kuungana na watawa katika kuwaombea kwa kuwa waliyofanya duniani ni ushuhuda.

Sista mkuu wa Shirika la Mtakatifu Teresa, Jimbo Katoliki la Iringa, Kalista Ludega alisema pacha hao watazikwa mahali wanapozikwa masista wa Shirika la Maria Consolata ambalo ndilo limewalea tangu wakiwa wadogo.

Msafara wa mazishi na ving’ora

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alisema kuwa msafara wa mazishi ya pacha hao utaongozwa na gari la polisi na ving’ora.

Alisema waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako ndiye ataongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa pacha hao.

Viongozi wengine watakaohudhuria, alisema ni naibu waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu wenye Ulemavu, Stella Ikupa, wakuu wa wilaya na mikoa walikowahi kusoma pacha hao.

Pacha hao walisoma Shule ya Msingi Ikonda wilayani Makete walikohitimu darasa la saba. Walijiunga na Sekondari ya Maria Consolata wilayani Kilolo walikomaliza kidato cha nne, na kidato cha sita walihitimu katika Sekondari Udzungwa.

“Tunatarajia viongozi wengine wengi wa kitaifa watakuwa pamoja nasi,” alisema Kasesela.

Kasesela ambaye ni kaimu mkuu wa Mkoa wa Iringa, alisema pacha hao waliofariki dunia Juni 2 katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa huo, miili yao itapelekwa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (Rucu), saa moja asubuhi kwa ajili ya misa na kuagwa.

Maria na Consolata walikuwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo wakisoma shahada ya elimu.

Kasesela alisema misa itaongozwa na Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa wa Jimbo Katoliki la Iringa na Askofu Alfred Maluma wa Jimbo la Njombe.

“Kutakuwa na salamu kutoka kwa viongozi kisha msafara wa kuelekea Tosamaganga utaanza saa saba mchana,” alisema.

Mkuu huyo wa wilaya alisema mazishi yanatarajiwa kufanyika saa nane na nusu mchana.

Kauli ya baba

Asukile Mwakikuti, baba mkubwa wa Maria na Consolata alisema kifo cha watoto hao kimeacha simanzi kubwa kwa familia yao.

Alisema kutokana na malezi bora ya Shirika la Maria Consolata wameridhia watoto wao wazikwe Tosamaganga.

Ishara za Ndege Iliotoweka na Abiria 10 Nchini Kenya Zapatikana

$
0
0
Ishara za ndege iliotoweka na abiria 10 nchini Kenya zapatikana
Ishara za simu kutoka kampuni ya ndege ya FlySax ambayo ilitoweka siku ya Jumanne jioni zimepatikana katika eneo la Aberdares katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya.

Naibu mkurugenzi wa shirika la wanyama pori nchini anayesimamia maeneo ya milima Simon Gitau siku ya Jumatano aliambia shirika la habari la Nation kwamba wataendelea usakaji wao wa ndege hiyo katika eneo la Kinangop ambapo ishara hizo zimeonekana.

Baadhi ya maafisa wa utafutaji na uokoaji walikuwa wakitarajiwa kusafirishwa kwa ndege kutoka katika uwanja wa Njambini ili kupelekwa katika eneo la utafutaji mwendo wa saa moja alfajiri.

Ndege hiyo nyepesi ya kubeba abiria aina ya Cesna C208 ilio na nambari ya usajili ya Y-CAC kutoka Kitale Magharibi mwa Kenya , ilipoteza mawasiliano na mnara wa kudhibiti ndege muda wa saa kumi na moja jioni siku ya Jumanne katika eneo la Aberdares, yapata kilomita 60 kabla ya kufika eneo ililokuwa ikielekea.

Ndege hiyo iliokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta , iliondoka Kitale, muda mfupi kabla ya saa kumi jioni ikiwa na abiria wanane na wafanyikazi wawili na ilitarajiwa kuwasili Nairobi saa moja baadaye.

Kulingana na taarifa taarifa iliotolewa na mkuu wa mamlaka ya usafiri wa angani nchini Kenya utafutaji wa ndege hiyo ambao ulikuwa ukiendelea ulisimamishwa kwa muda na utaendelea siku ya Jumatano alfajiri.

Hatua hiyo inatokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri uonekano wa anga na shughuli za maafisa wa uokoaji.

Ndege hiyo inasimamiwa na kampuni ya ndege ya East Africa Safari Air Express,

Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo zinasema kuwa ndege hiyo ilitoweka lakini juhudi za pamoja zinazoshirikisha mashirika ya wanyama pori KWAS na kitengo cha kuchunguza ajali za ndege zimekuwa zikiendelea kuisaka ndege hiyo.

Ndugu na jamaa wa abiria wametakiwa kusubiri katika hoteli ya Weston iliopo jijini Nairobi.

Mfungo wa Mwezi Ramadhani Wambadirisha Sanch

$
0
0
Mfungo wa Mwezi Ramadhani Wambadirisha Sanch
MFUNGO wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani umeonekana kumbadili mwanamitindo Jane Rimoy ‘Sanch’ kutoka kwenye kuvaa mavazi ya kihasarahasara ambayo amekuwa akiyavaa na sasa kutinga mavazi ya heshima kwa kuvaa mabaibui kuendana na wanaofunga.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Sanch amekuwa akitupia picha mbalimbali zinazomuonesha akiwa kwenye mavazi ya baibui na kuandika kuwa anapata baraka nyingi.

Hata hivyo, wapo waliodai kuwa mrembo huyo amebadilika kwa sasa lakini wapo wanaodai kuwa anavaa hivyo kwa sababu ya kutangaza maduka ya mabaibui ingawa yeye amekuwa akitaja nguo yake amenunua wapi lakini wakati mwingine anaishia tu kuandika kuwa ni baraka za Mwenyezi Mungu.

Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimpongeza na wengine kumshawishi kuendelea kuvaa mavazi hayo hata baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwani anapendeza na kujistiri pia.

“Nakushauri uvae mavazi haya yanakupendezesha sana na mbali na kuonekana umependeza lakini pia yanaustiri mwili wako,” aliandika shabiki mmoja anayeitwa Ali.

Mbali na shabiki huyo wengine walimwambia kuwa ana sura nzuri akijistiri anapendeza zaidi kwani mwili wake una mvuto wa kipekee akiwa katika mavazi ya kujistiri.

Alipotafutwa na Risasi Mchanganyiko ili kuzungumzia maoni hayo ya mashabiki wake, Sanch hakuweza kupatikana mara moja lakini mara kadhaa amekuwa akisema anapendelea kuvaa vile anavyojisikia na hakuna wa kumpangia maisha yake.

Ukiingia kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sanch ambaye ana umbo lenye mvuto wa kipekee, amekuwa kinara wa kutupia picha za nusu utupu akiwa katika nchi tofautitofauti na kusindikiza na jumbe mbalimbali.

Ajali ya Treni Yaua Saba na Kujeruhi Vibaya Watu 27

$
0
0
Ajali ya Treni Yaua Saba na Kujeruhi Vibaya Watu 27
WATU saba wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma, asubuhi ya leo Jumatano, Juni 6, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo linalofanya safari zake kutoka Kigoma kuelekea Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi hilo.

Aidha, dereva wa basi hilo ambaye hajajulikana jina ni miongoni mwa waliofariki dunia, huku idadi ya vifo ikitajwa huenda ikaongezeka kutokana na hali mbaya za majeruhi walio wengi.

Kamanda Otieno amesema kuwa, Jeshi hilo linaendelea kuokoa miili na majeruhi wengine, na taarifa zingine zitafuata mara baada ya zoezi kukamilika.

Rosa Ree Afunguka Siri ya Mafanikio Yake

$
0
0
Rosa Ree Afunguka Siri ya Mafanikio Yake
MWANADADA ambaye hivi sasa anakimbiza na wimbo wake wa Way Up, Rosary Robert ‘Rosa Ree’, ametoboa siri nyingine ya kuzidi kutusua kimuziki na kufika hapo alipo, kiasi hata cha kupata menejimenti nchini Afrika Kusini ‘Sauz’ kutoka Dimo Production.

Akichonga na Risasi Vibes, Rosa Ree alisema kuwa, siri hiyo ni namna ya uimbaji wake kwani haujakaa Kibongo sana na anajiweka ‘kimtoni’ zaidi ndiyo maana anafanikiwa.

“Ukiwasikiliza wanamuziki wa kike wa Bongo, wengi wanavyorap ni ‘local’ ndiyo maana hata hawatusui kama mimi, kikubwa aina yangu ya uimbaji inanifanya kupata mashabiki wengi zaidi nje ya Bango,” alisema Rosa Ree.

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0

Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa 

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka 
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume 

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU 

 0753471612/ 0715249530 
0623 386 305 

DR KUZENZA 

Mchungaji wa Kabisa Auawa kwa Kushambuliwa na Mamba

$
0
0

ETHIOPIA: Mchungaji wa Kanisa la Kiprotestanti, Docho Eshete ameuawa kwa kushambuliwa na Mamba

Mchungaji huyo amekumbwa na mauti wakati akiwabatiza waumini wapya wa kanisa lake

Mchungaji, Docho alikuwa ameanza kumbatiza muumini wa kwanza kati ya 80 waliokuwa wakisubiri ubatizo

Tukio hilo limetokea kando ya Ziwa Ayaba

Ishara za ndege iliotoweka na abiria 10 nchini Kenya zapatikana

$
0
0

Ishara za simu kutoka kampuni ya ndege ya FlySax ambayo ilitoweka siku ya Jumanne jioni zimepatikana katika eneo la Aberdares katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya.

Naibu mkurugenzi wa shirika la wanyama pori nchini anayesimamia maeneo ya milima Simon Gitau siku ya Jumatano aliambia shirika la habari la Nation kwamba wataendelea usakaji wao wa ndege hiyo katika eneo la Kinangop ambapo ishara hizo zimeonekana.

Baadhi ya maafisa wa utafutaji na uokoaji walikuwa wakitarajiwa kusafirishwa kwa ndege kutoka katika uwanja wa Njambini ili kupelekwa katika eneo la utafutaji mwendo wa saa moja alfajiri.

Ndege hiyo nyepesi ya kubeba abiria aina ya Cesna C208 ilio na nambari ya usajili ya Y-CAC kutoka Kitale Magharibi mwa Kenya , ilipoteza mawasiliano na mnara wa kudhibiti ndege muda wa saa kumi na moja jioni siku ya Jumanne katika eneo la Aberdares, yapata kilomita 60 kabla ya kufika eneo ililokuwa ikielekea.

Ndege hiyo iliokuwa ikielekea katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta , iliondoka Kitale, muda mfupi kabla ya saa kumi jioni ikiwa na abiria wanane na wafanyikazi wawili na ilitarajiwa kuwasili Nairobi saa moja baadaye.

Kulingana na taarifa taarifa iliotolewa na mkuu wa mamlaka ya usafiri wa angani nchini Kenya utafutaji wa ndege hiyo ambao ulikuwa ukiendelea ulisimamishwa kwa muda na utaendelea siku ya Jumatano alfajiri.

Hatua hiyo inatokana na hali mbaya ya hewa ambayo imeathiri uonekano wa anga na shughuli za maafisa wa uokoaji, Ndege hiyo inasimamiwa na kampuni ya ndege ya East Africa Safari Air Express,

Taarifa kutoka kwa kampuni hiyo zinasema kuwa ndege hiyo ilitoweka lakini juhudi za pamoja zinazoshirikisha mashirika ya wanyama pori KWAS na kitengo cha kuchunguza ajali za ndege zimekuwa zikiendelea kuisaka ndege hiyo.

Ndugu na jamaa wa abiria wametakiwa kusubiri katika hoteli ya Weston iliopo jijini Nairobi.

Nay wa Mitego Amfungukia Babu Tale Sakala la Kwenda Kuomba Msamaha Kwa Zari

$
0
0

BAADA ya hivi karibuni Meneja wa Staa wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’; aitwaye Hamis Taletale ‘Babu Tale’ kuibukia Afrika Kusini ‘Sauz’ kwa ajili ya kumuombea msamaha msanii wake huyo kwa mzazi mwenziye, Zarinah Hassan ‘Zari’, Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amemvaa meneja huyo kwa kuchelewa kwake kuchukua hatua. 

Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Nay alisema kitendo cha Babu Tale kwenda Sauz kumuombe msamaha Diamond ni kizuri lakini angekifanya tangu awali na kuhoji kwa nini amesubiri yeye (Nay) aoneshe nia ya kuwapatanisha wapenzi hao ndiyo akachukua wazo hilo na kulifanyia kazi. 

“Suala la Babu Tale kwenda kumuombea msamaha Diamond ni zuri lakini alitakiwa afanye hivyo muda mrefu na siyo asubiri mpaka nizungumze mimi kwamba nitawapatanisha. “Nashukuru wazo langu limekubalika na kila mtu na yeye mwenyewe kuliona linafaa na kufanyia kazi.

“Diamond ni mshikaji wangu wa muda mrefu sana, japo mapenzi hayaingiliwi lakini kwa upande wangu namkubali sana mama Tee (Zari) maana akiwa naye mambo yake yanakuwa kwenye mstari kwani anakuwa mtu wa kazi sana tofauti na akiwa na hawa wanawake wengine. 

“Kutokana na kuliona hilo ndiyo maana niliona nimpe ushauri kupitia ukurasa wangu wa Instagram na kuahidi kuwarudisha pamoja, lakini kabla sijafanya hivyo, Babu Tale akalifanyia kazi, siyo vibaya nimefurahi sana kwa kweli,” alisema Nay. 

ILIKUWA HIVI 
Awali baada ya Diamond kuachia wimbo mpya wa Iyena, Nay alimpongeza kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiweka na maneno mengine makali ya kuwaita wanawake anaokuwa nao kwenye uhusiano hawana nyota ila Zari ndiye mwenye nyota. 

Baada ya kuandika hivyo na maneno mengine makali yasiyoandikika gazetini watu mbalimbali mitandaoni wamekuwa wakimwita Hamisa Mobeto ambaye pia ni mzazi mwenza na Diamond jina baya. Nay alipoulizwa kuhusiana na jina hilo alisema hakumtaja mtu bali alijiandikia kwa watu wote na hajamtuma mtu kumwita Mobeto jina au maneno aliyoandika yeye. 

Gari Aina ya Land Rover Inauzwa Kwa bei Nafuu Kabisa

$
0
0

Gari Aina ya Land Rover Inauzwa Kwa bei Nafuu Kabisa
Imetembea KLM 87,000
Engine CC 2490
Automatic and Manual
Gari IPO Dar Tegeta
Piga simu namba 0713468299 au 0713302266 kwa maelewano zaidi

Rosa Ree Akanusha Kumiliki Mjengo Aliyopewa Kuishi, Aeleza Kwanini Kaamua Kurudi Kwenye Lebo

$
0
0
Week hii, Story zilizagaa kuwa Rosa Ree amekabidhiwa mjengo na record label inayo msimamia kwa sasa kutoka Afrika ya Kusini. Well kwenye Friday Night Live, Rosa Ree amekanusha kumiliki mjengo huo bali ni makazi yake ya sasa kwakuwa yupo kwenye label hiyo. Akimiliki mjengo wake basi watu watafahamu. VIDEO:

TAZAMA WIMBO MPYA WA ROSA REE:

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo

$
0
0

Gari Aina ya Land Rover Inauzwa Kwa bei Nafuu Kabisa

$
0
0

Gari Aina ya Land Rover Inauzwa Kwa bei Nafuu Kabisa
Imetembea KLM 87,000
Engine CC 2490
Gari IPO Dar Tegeta
Bei Mil 12 Maelewano yapo
Piga simu namba 0713468299 au 0713302266 kwa maelewano zaidi
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Latest Images