Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Maelfu Wajitokeza Kumsindikiza Freeman Mbowe Polisi Alipoitwa Kuhojiwa Kuhusu Kauli yake ya Maandamano

$
0
0
MAMIA ya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi hii wamejitokeza kumsindikiza Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa, Freeman Mbowe kuelekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi yaliyopo Posta jijini Dar es Salaam.

Mbowe amefika makao makuu hayo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu kauli yake aliyoitoa Jumapili iliyopita ya kuitisha maandamano nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge Maalumu la Katiba.

Katika tukio hilo, baadhi ya waandishi wa habari wamekimbizwa na polisi waliokuwa na mbwa wakitakiwa kukaa umbali wa mita 200 kutoka katika makao makuu hayo ya polisi.

Follow us:
Instagram:@udakuspecially

Jide na Gadner Sasa ni Kama Paka na Panya, Kila Mmoja Atinga Ukumbini na Kampani Yake

$
0
0
Stori: Richard Bukos
PAMOJA na kutumia nguvu nyingi kukanusha kwenye mitandao kwamba ndoa yao haijavunjika, mtangazaji mahiri Bongo, Gardner Gabriel Habash ‘G. Habash’ na ‘mtalaka’ wake, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’, Jumamosi iliyopita walifanya tukio lililowashangaza watu kufuatia kila mmoja kuingia ukumbini akiwa na kampani yake na kukwepana kama paka na panya, Amani liliwanasa kwa vile lilikuwepo.

Tukio hilo lililoamsha minong’ono kwa watu waliosoma mchezo mzima, liliibukia ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge (zamani Business Park) uliopo Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uzinduzi wa albamu ya Bongo Fleva.

WALIVYOKAA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Gardner alipoingia alikwenda kukaa kwenye meza na watu wengine watatu,  baadaye akafika Miss Mara 2000, Rashida Wanjara na kuunga ambapo walikuwa wakibadilishana mawazo na kufunguliana vinywaji kwa meno na kumiminiana kwenye glasi.

JIDE NAYE
Wakati Gardner ambaye pia hujulikana kwa jina la utani la Kapteni akiendelea kujipoza na Rashida na wengine, Jide yeye alikaa meza moja na kijana mmoja aliyevalia shati la kitenge la mtindo uliowahi kutamba miaka mitano nyuma, wengine huita Mackezie sanjari na wadada wawili.

WALICHOTAKA WATU
Baadhi ya watu walisikika wakishauri kwa sauti ushauri ambao haukuwafikia wawili hao ambapo walisema kama kweli ndoa hiyo haijavunjika, ni vyema Jide angeenda  kwenye meza aliyokaa Gardner na kusema chochote kisha kuondoka hali ambayo hakuwepo.
GPL

Makubwa:Mwanafunzi Aamua Kujinyonga kwa Kukosa Huduma Hospitalini

$
0
0
Mwanafunzi wa kidato cha 5 shule ya sekondari Ihungo(19) Ameamua kujinyonga kwa kutumia shuka lake katika hospital ya mkoa wa Kagera baada ya kulazwa hospitalini hapo bila kupata huduma ipasavyo, Kabla ya Kujinyonga aliacha ujumbe akisema si halali kwa mwanadamu kutibiwa kama mnyama.
Jamani Hasira Hasara.

Mishahara Hewa Kwa Watumishi wa Serekali Sasa Basi, Mwigulu Nchemba Noma Sana

$
0
0
Serikali imeagiza watumishi wote wa umma walipwe mishahara moja kwa moja kupitia akaunti zao sahihi za benki ambazo zitatumika kupitishia mihahara yao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari ofisi za Hazina leo jijini Dar es salaam.“Mishahara ya Watumishi wote wa Serikali, wakala na taasisi za umma italipwa moja kwa moja kupitia akaunti zao za banki” alisema Mwigulu.

Ili kufanikisha adhima hiyo ya Serikali, Mwigulu aliwaagiza waajiri wote wa sekta ya umma kuwa wawe na akaunti namba za benki za watumishi wao wote waliochini ya fungu husika ambazo zina taarifa sahihi na wakizingatia mfumo sahihi wa taarifa za kiutumishi.

Mwigulu alionya kuwa mtumishi asiye na akaunti benki asilipwe mshahara wake dirishani ambapo amewahimiza waajiri kuwasisitiza watumishi walio chini yao kufungua akaunti sahihi ya benki kwenye mfumo ambayo itatumika kulipa mshahara husika kupitia orodha ya malipo ya mshahara (payroll) inayotolewa na Hazina.

Aidha, Mwigulu amasema kuwa kila ifikapo tarehe 10 ya kila mwezi  waajiri wote wawe wamewasilisha maombi ya fedha za kulipa mishahara kwa mwezi unaohusika wakiambatisha orodha ya malipo ya  watumishi ya kuthibitisha kiasi kinachoombwa.

“Waajiri watakaoshindwa kutoa ‘Payroll’ watasababisha watumishi wanaowaongoza kushindwa kupata mishahara yao kwa mwezi husika jambo ambalo sio nia ya Serikali” alisisitiza Mwigulu.

Utaratibu huu wa kulipa mishahara utakuwa endelevu na umedhihirisha kuwa na tija kwa matumizi ya fedha za umma kwani umeonesha mafanikio ambayo kwa mwezi wa saba na wa nane hakuna mtumishi, Wakala za Serikali wala Taasisi iliyolalamika kukosa mishahara.

Mama wa Mtoto wa Maajabu Aliyepanda Ndege Bila Kugundulika Mpaka Zanzibar Aongea Makubwa

$
0
0
Stori: Richard Bukos
MTOTO Happiness (10) (pichani) ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita  alizua kizazaa mjini Zanzibar baada ya kuonekana akizungumza na viumbe wa ajabu na wanyama, ametua jijini Dar kufuatia kufika kisiwani humo kimaajabu.

Kwa mujibu wa mama huyo, aliambiwa na maofisa wa uwanja huo kuwa sehemu hizo zote mtoto wake alipita bila kuonekana na kamera za uwanjani hapo wala kuacha kumbukumbu yoyote hali iliyozidi kuwaumiza vichwa maofisa wa uwanja huo. 
Zefania alisema wakati maofisa hao wakitafakari hayo, ndipo msamaria mwema mmoja alijitokeza na kumchukua kwenda kumuhifadhi nyumbani kwake.
“Akiwa nyumbani kwa msamaria mwema huyo, nimeambiwa mwanangu alianza kumfanyia maajabu mbalimbali ikiwemo kuzungumza na wanyama na viumbe wengine wa ajabu au kutoka nje huku mlango umefungwa kwa ndani.
“Kuna muda alizungumza na viumbe wasioonekana ambapo aliwasiliana nao na kumletea vitu kadhaa alivyovitaka. Wakati mwingine alizungumza na wanyama wa mle ndani, kama kuku na paka ambao alikuwa akiwatuma kumfanyia yote aliyokuwa akiwaagiza.
“Hali hiyo ilimshtua yule msamaria mwema naye aliomba kupambazuke ili ampeleke mwanangu ustawi wa jamii. Yaani nahisi pengine angekuwa amemuokota sehemu bila kukabidhiwa mbele ya mashahidi pengine angemtupa usiku huohuo.

“Baada ya kushuhudia vituko hivyo, asubuhi iliyofuata alimkimbiza ustawi wa jamii ambako nako wameniambia alianza kuwafanyia vituko kama hivyo na kuwaambia kuwa angewatoroka muda wowote, kisha kuonekana akiparamia juu ya paa na kutaka kutoka.
“Yaani kwa muda mfupi waliokaa naye, maofisa wa ustawi wa jamii wanasema amewahenyesha vya kutosha ndipo walipofanya juhudi za kunitafuta na mimi nikaenda kumfuata,” alisema mama huyo muda mfupi baada ya kutua bandarini Dar.
Paparazi wetu alipomtaka mtoto huyo kuzungumza alikataa katakata na kujifanya bubu hali iliyomshangaza hata mama yake. “Nashangaa, sijui kwa nini hataki kuzungumza na wewe wakati ni mzungumzaji sana,” alisema mama Happiness. 
Akizungumzia historia ya mtoto huyo, mama huyo alisema alimzalia Musoma, Mara na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina la Juli ambaye walitengana na hawana mawasilino mazuri.

Mama huyo alisema alimpeleka mtoto wake shuleni lakini kila akifika harudi nyumbani na kutorokea anakokujua na kuonekana baada ya wiki mbili au tatu.
Kufuatia hali hiyo amewaomba wasamaria wema na viongozi wa dini kumwombea mtoto wake ili arudi katika hali ya kawaida kwani anajua kuna mkono wa mtu wa karibu uliyemharibu mtoto wake.

Kama Mbowe yuko huru basi na Sheikh Ponda aachiwe

$
0
0
Kutokana na kauli ali iyotoa mwenyekiti wa chadema mh.mbowe ya kuitisha maandamano nchi nzima tena yasiyo na kikomo.nilitegemea kwa kauli ile mbowe alitakiwa awe ameshakamatwa siku ile ile.lakini cha ajabu mpaka leo bado anatamba uraiani.lakini shekh ponda mpaka leo bado anateseka gerezani bila hatia.hivi kati ya ponda na mbowe nani anastahili kukaa rumande?

Huyu Jamaaa Ndio Ataiwakilisha Tanzania kwenye Nyumba ya Big Brother Afrika Mwaka Huu

$
0
0
Mpiga picha, Idris ni mmoja wa wawakilishi wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa mwaka huu.

“Idris is a photographer from Tanzania, filled with positive energy. He admits to having a strategy, hoping that his fellow housemates will turn to him “when they want to be inspired or when they feel down,” wameandika BBA kumwelezea Idris. 
Bonyeza >hapa< Kuangalia Video

Mambo Ambayo ni Diamond na Wema tu, Ndio Wanaoweza Kufanya Hapa Bongo!

$
0
0
Hivi ni vitu ambavyo inabidi tu tuwaachie Diamond na Wema waendelee kufanya yao, wengine wabaki watazamaji tu, afterall siyo kila mtu yuko kwenye movie yao ambayo bado inaendelea, hii ni moja ya celebrity couple inayopendwa na watu wengi zaidi nchini Tzee na nje, ila kwa haya wayafanyayo, hutakuja kuona couple wowote hapa tzee wakifanya haya wanaofanya yao, labda huko nchi za wengine ila kwa hapa Bongo, ni Wema Sepetu tu na Diamond Platnumz ndio wanayoweza.

Kudai kutengeneza movie ambayo haijatoka hadi leo”Temptation”

Kati ya vitu ambavyo si rahisi cople wengi kukuta wanafanya pamoja ni movie, ila kwa hili la wapendanao hawa ni noma zaidi, ndio moja ya celebrity couples ambao wamewahi kudai kucheza movie wakati walipokuwa wameachana, ili tu wawe karibu pamoja, ikiwa inasemekanailikwenda kufanyiwa shooting nchini China, na ikiwa nimwaka wapili huu sasa wamesharudiana, na movie hiyo haijakamilika bado,huku ikibakia msemo tu “Acha movie iendelee”.

Kuachana na kurudiana zaidi ya mara mbili.

Kama ni vituko basi hapa huwa haviishi, saa zingine unaweza kusema ni mapenzi kuzidi, ila kwa Diamond kuvalishwa wigi, kupigwa picha na mpenzie(Wema) na kupost kwenye mitandao ya kijamii, Only Diamond na Wema ndio kweli wanaweza kufanya hivi, katika miaka hata ya baadae, sidhani kama watatokea couple maarufu wenye vituko kama hivi, ni nadra sana ukute mtu maarufu wakiume kuvaa wigi la kike, kupiga picha na kupost kwenye mitandao.


Kurekodi video  wakiwa kitandani na kupost kwa mashabiki kuangalia.

Kama ni love ku-show love kwa mashabiki iko poa zaidi, kwa Diamond na Wema ndio inasemekana kuwa hata baada ya kudai hapo awali kuwa kwa sasa wanataka kuweka mambo yao yawe yao binafsi, ila ndio couple waliowazi zaidi ku-show mambo yao hadharani, si couple wote hapa bongo wenye uwezo wa kufanya hivi, zaidi ya kujipiga picha wakiwa kitandani na kupost kwenye media. Tumezoea kuona watu wengi hasa maarufu wakifanya mambo yao kwa siri zaidi, ila kwa couple hawa wako wazi sana wakifanya mambo yao.

credit : vibe

Global Publishers Yawaomba Radhi Zitto Kabwe na Diva Loveness

$
0
0
Kupitia gazeti la Amani la Septemba 11-17, 2014, kulichapishwa habari ukurasa wa mbele iliyosomeka: “DIVA: ZITTO NI MUME WANGU.” Ikikolezwa na dondoo ‘Adai ni mke anayetambulika kisheria’ na ‘Asema hayuko tayari kuachana naye kirahisi,’. Na sasa uongozi wa gazeti hilo umekusudia kwa nia njema kutoa ukweli juu ya habari hiyo.

Ufafanuzi huu unalenga kumaliza mkanganyiko uliojitokeza hasa baada ya kuwepo kwa madai kutoka kwa mhusika ambaye ni Loveness Malinzi (Diva) kuwa, hakuzungumza na gazeti kile kilichoandikwa na kwamba alikuwa anazushiwa; madai haya aliyawasilisha chumba cha habari kwa njia ya simu na sehemu kuyaweka kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.

Kama hilo halitoshi, Diva alikana kuzungumza na mwandishi wa habari hiyo ambapo alisema mazungumzo yao yalihusu mwaliko wa Kipindi cha Global TV Online ambacho kinarushwa na mtandao unaoendeshwa na Kampuni ya Global Publishers inayomiliki pia Gazeti la Amani na si vinginevyo.

Malalamiko haya ya Diva yalikuja muda mchache baada ya gazeti kutoka likiwa na habari hiyo ambapo jopo la wahariri wa Amani kabla ya kuchapisha habari hiyo walijiaminisha kuwa ni ya kweli kutokana na taarifa pamoja na vielelezo vya rekodi ya sauti ya mazungumzo alivyoviwasilisha mwandishi kwenye dawati kuthibitisha kuwa alifanya mazungumzo na mhusika kuhusiana na msingi wa habari nzima iliyoandikwa.

Kama tulivyoeleza, baada ya habari hiyo kutoka na kipande cha sauti kuingizwa kwenye Tovuti ya Global Publishers, ndipo yalipoibuka madai hayo huku baadhi ya wasomaji wakieleza kuwa ile siyo sauti ya Diva; hapo ndipo uongozi wa gazeti ulipoamua kufuatilia ukweli na kubaini yafuatayo.

Pamoja na ukweli kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Kaskazini) na Diva wana ukaribu, mazungumzo kati ya mwandishi na mwanadada huyo kuhusiana na kauli yake ya: “Zitto ni Mume Wangu,” hayakufanyika na kwamba mwandishi alipika habari na kutengeneza sauti ya Diva kwa lengo la kuwahadaa wahariri kwa nia mbaya!

Kwa msingi huo sisi kama chombo cha habari makini, kinachosimamia weledi, kulinda na kuheshimu haki za binadamu; tunachukuwa nafasi hii kumuomba radhi Diva, Mheshimiwa Zitto, sanjari na jamii kwa ujumla kwa usumbufu wowote uliosababishwa na habari hiyo. Aidha, uongozi unapenda kuutangazia umma kuwa, hatua kali za kinidhamu zimeshachukuliwa dhidi ya mwandishi husika sambamba na onyo kwa viongozi wote wa gazeti kwa udhaifu uliojitokeza katika habari hiyo.

Tunaomba jamii ielewe kwamba Global Publishers siku zote inasimamia UKWELI na kamwe hairuhusu kabisa habari za uongo kuandikwa katika magazeti yake.

Jamii iendelee kutuamini na kushirikiana nasi katika kusimamia weledi wa uandishi wa habari. Milango ya kukosolewa iko wazi, hivyo kwa mwenye malalamiko yoyote juu ya habari zetu, iwe ni uongo au kutotendewa haki, asisite kuwasiliana na viongozi kwa hatua zaidi. Ndimi, Mhariri Kiongozi, Magazeti Pendwa.

Global Publishers 

Anti Ezekiel na Kassim Mganga Wahusishwa Kuwa na Uhusiano wa Kimapenzi

$
0
0
Gazeti la Makorokocho ambalo mhariri wake ni Soudy Brown kutoka XXL ya Clouds Fm leo kwenye ukurasa wa mbele kabisa kuna stori inayomhusu Anti Ezekiel pamoja na Kassim Mganga.
Stori hii imeanzia wakati wapo pamoja Marekani kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo ambapo inasemekana walikua karibu zaidi na hata hotel kwa sasa wanalala hotel moja.
Soudy Brown amempata Kassim Mganga na kakubali kuongelea hiki kinachozungumzwa kwenye mitandao kuwa anatoka na Anti Ezekiel kwa sasa.

Bonyeza play kusikiliza.

Msichana Aelezea Jinsi Wasichana wa Bongo Wanavyodanganywa Kwenda Kufanya Kazi za Umalaya Dubai

$
0
0
Ushuhuda wa huyu dada inawezekana ukakufumbua macho na kujua wapi sehemu sahihi ya kuelekea na kujua nini unachotakiwa kukifanya kama umeshaanza kujiandaa safari ya kwenda Dubai.
Wimbi kubwa la ukosefu wa ajira nchini bado ni tatizo kubwa ambalo hupelekea wengine wanaposikia kuna kazi sehemu huamua kwenda moja kwa moja kufatilia kuhusu ajira hiyo.
Gea Habib ameongea na msichana huyu amabye kiasili yeye ni Mwenyeji wa Moshi na amesimulia stori yake nzima na vitu walivyokuwa wanafanyiwa wakati yupo huko Dubai.

Bonyeza play kusikiliza.

Baada ya Kufunga Ndoa, Lucy Komba "AWALIPUA" Wabaya Wake

$
0
0
Msanii maarufu wa filamu nchini, lucy komba, ambaye ivi karibuni alifunga ndoa na aliyekuwa mchumba wake wa siku nyingi, ambaye ni raia wa denmark. Msanii huyo amewatupia dongo la haja wabaya wake waliokuwa wakimwambia ataishia kuvaa shera kwenye movie tu na hawezi kuolewa kweli. Kupitia ukurasa wake wa instagram lucy alipost hii picha(chini) akiambatanisha na maneno yafuatayo:

"Ni kwale waliokuwa wakisema utaishia kuvaa shera kwenye filamu tu, hizo zilikuwa ni dua la kuku, mboga dagaa tu kuku nyama ya hamu".


Martin Kadinda Hivi Kweli Meneja Ndo Anatakiwa Awe Hivi Kwa Mteja Wake? Jisomee Alichoandika

$
0
0
Katika pitapita zangu instagram nikakutana na post aliyoiweka Martin Kadinda kuhusu mteja wake mpya Elizabeth michael aka Lulu.

Nilishangazwa sababu maneno haya hayakutakiwa kuwekwa na manager wake,labda kama ana mmanage kwenye biashara ya Ngono..
Picha hiyohapo niliyo screenshoot.

Binti Huyu Ametupanga Wanaume Kumi na Moja na Wote Anatupa Uroda Bila Kujijua..Kipaji au Umalaya?

$
0
0
Ukimuona kwa macho utasema huyu ndio mwanamke kumbe ni bonge la kimeo…ilikuwa mida ya jioni natoka zangu kazini mara ikaingia massage..baby uko wapi nimekumiss…nikamjibu ndo natoka kazini now..yeye..Basi naomba upitie nyumbani japo nikuone nimekumiss sana we mwanaume.

Nikaona isiwe shida ngoja nikamuone roho yake itulie nipo njiani wazo likanijia…Nikapitia duka moja maarufu Sinza na kumnunulia zawadi ya viatu kama suprize nimejikoki mwenyewe naenda kwa babybaby…mademu bwana..!

Kufika akanipokea kwa bashasha na mabusu motomoto dady’s home..Yeye.. najua umechoka baby wangu kaa kwa kochi upumzike nataka nikutengenezee juice fresh unayo ipendaga..nikamwambia ngoja kwanza nikupe zawadi yako nikatoa vile viatu na kumpatia akafurahi sana na kuvijaribisha..vilimtosha na kumpendeza..Nikapewa busu lingine la sekunde kazaa.,

Akatoka kwenda kuandaa juice..huku simu yake na vile viatu akiwa ameviacha jirani na kochi nililokaa..Nikamuuliza simu yako inabando..akanijibu ndio..Nikaichukua nakuingia sehemu ya kubrowse internent ..akili ikanituma nifanye udukuzi kidogo nikafungua application yake ya watsupp mbona nilichoka..

Nilikuta msururu wa wanaume anaochati nao nakuwatumiana picha akiwa amevaa pichu tu nakukaa kimitego…huku wakiambiana ni jinsi gani wamemisiana kupeana utamu..kijasho kikanitoka. .nikajikaza mwenyewe na kuendelea kuperuzi kwa wote idadi ikafikia wanaume kumi na moja na kwa mtiririko wa chating yao wote waonekana wameshapewa utamu..Napenda kusema kitu kimoja hapa tangu nimeanza mahusioano nae tumefikisha mwaka sasa sikuwahi hata siku moja kuishika simu yake.,

Nilishikwa na hasira sana yani huduma zote ninazo mpatia kumbe nahudumia kahaba..nikamwita na kumuuliza aniambie hao watu ni akina nani..utetezi alionipa anasema ni marafiki zake nisimfikirie vibaya..

Nilitamani nimkate kofi moja la nguvu yani ushahidi wote ninao hapa unanijibu rejareja hivyo..nikamuuliza huo urafiki pamoja nakugongana..!we kweli kiboko sasa unataka nikupe cheo gani huu ni umalaya au kipaji...Akaanza kulia huku akiomba nimsamehe..

Kwakweli nilichanganyikiwa nakujiuliza hivi huyu binti anawezaje kutupanga wengi hivi..nilichofanya nikuchukua viatu nilivyokuja navyo nikamwambia nimejitoa kwenye hiyo cheni na kama viatu atakuleta mwingine hivi naondoka navyo..

Nipo njiani kurudi home massage za kuomba asemehewe na kuto rudia tena zinamiminika kwenye simu yangu huku akijuta na kudai mimi ndo ananipenda kiukweli nikimwacha hatopata furaha ya maisha nakuomba nimpe last chance abadirike…nikamjibu nakumwambia huwa natoa msamaha kwa makosa mengine lakini sio kwa hilo la kuchapiwa naomba tuachane kwa amani tu mama…akanipigia simu sikupokea akarudia tena na tena nikapokea..

Nikamuuliza unasemaje..akanimbia ananipenda sana na hawezi kuishi bila mimi uku akilia..nilichomjibu ni kwamba siwezi kuendelea nae.,

Kitu kingine kinacho nichanganya hapa nikwamba ametishia kujiua na yupo chini ya uangalizi wa dada yake..jamani hata kama ni msamaha nikifiria idadi yake ya wanaume nachefuka kabisa..napigiwa simu kila mara kuombwa nirudishe moyo na ndugu zake ninachowajibu ni kwamba siwezi ajaribu kumchagua mwingine atakayempenda sana..mpaka nafikia hatua ya kuwaandikia hii habari huyu binti amelazwa hospital presha imeshuka..

Hapa nafanyaje wakuu kiukweli huyu mwanamke amenitoka kabisaa..hofu yangu ni hiyo ya kulazwa kisa mimi inamaana nikigoma hata kwenda hospital..si ndio majanga yataongezeka..msaada wenu wakuu kichwa changu kimevurugwa kabisa.,

KAJALA Akwama PESA ya Kumtoa Mumewe Jela

$
0
0
Licha ya mkwanja kumtembelea, msanii wa filamu Bongo, Kajala Masanja amekwama kupata pesa ya kumlipia faini mumewe Faraji Chambo ili aweze kutoka jela.

Akizungumzia ombi la mumewe huyo kumtaka kutofuja pesa badala yake amlipie faini ili aondokane na mateso ya gerezani, Kajala alisema ni kweli anampenda sana mumewe na angetamani kufanya hivyo lakini kiasi cha shilingi milioni 200 kinachotakiwa si kidogo hivyo hawezi kukipata.

“Nampenda sana mume wangu, hilo halina ubishi na pia najua anateseka sana kule gerezani kwani nakujua lakini milioni 200 siyo hela ndogo ujue. “Natamani hata leo niwe nayo nimlipie lakini ndiyo hivyo tena,” alisema Kajala kwa masikitiko.

Hata hivyo, licha ya Kajala kuwa na nia ya kumtoa jela mumewe, mmoja wa mawakili aliyekuwa akihusika na kesi yao aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:

“Kama Kajala anafikiria kumlipia mumewe faini simshauri afanye hivyo kwani hukumu iliyotolewa ni ya kesi moja na ile nyingine ya kuuza nyumba iliyokuwa imewekwa bondi na Takukuru, bado inaendelea na huwa Faraji anatoka gerezani kwenda mahakamani.

“Sasa Kajala anaweza kutoa pesa zake, mumewe akatoka lakini hukumu ya ile kesi nyingine ikatolewa na akarudi tena jela,” alisema wakili huyo. Hivi karibuni, mume wa Kajala alituma ujumbe kupitia watu wanaokwenda kumtembelea akimtaka mkewe kumuonea huruma na kumlipia faini ili atoke gerezani badala ya kuzitumia pesa kwa anasa.

Hatimaye Dada wa Mwanamuziki Diamond Platnumz Esma Afunga na Petit man

$
0
0


Ni habri mpya ya mjini kwa sasa,ndoa ya Dada wa Diamond na kipenzi wa Wema petiti man wakuache,amabapo uhusiano wao ulioanza kama utani hatimae  umezalisha kile amabcho wengi hawakukitgemea kama kingekuwa mapema hivi...Udakuspecially inawatakia maisha mema ya ndoa na baraka tele.

Msanii Mez B Aingia Katika Kashfa Nzito Baada ya Kuwalazimisha Warembo Kupiga Picha Huku Wakiwa Uchi

$
0
0
Msanii wa kitambo wa Bongo Fleva aliyewahi kutamba na Kundi la Chamber Squad na ngoma yake ya taifa ya Kama Vipi, Moses Bushagama ‘Mez B’ anadaiwa kuwaaibisha ma-miss kwa kuwalazimisha kupiga nao picha wakiwa watupu.

Tukio hilo la kidhalilishaji na lisilovumilika lilijiri juzikati kwenye Ufukwe wa Mikadi uliopo Kigamboni jijini Dar muda mfupi baada ya jamaa huyo ‘kushuti’ video ya ngoma yake mpya ya Shemeji.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, jamaa huyo aliwafuata warembo hao waliojitambulisha kwa majina ya Vicky na Rebecca waliokuwa kwenye swimming pool (bwawa la kuogelea) ambao ilisemekana kuwa siyo raia wa Bongo na huko wanakotokea ni ma-miss.

Ilidaiwa kwamba Mez B ndiye aliyewaomba kupiga nao picha lakini jamaa huyo ‘akaharibu’ baada ya kwenda mbele zaidi na kuanza kuwaminya ‘vifuu’ vyao kifuani vilivyoonekana ni vya saa sita vilivyokuwa wazi bila hata ‘braa’.

Ilisemekana kwamba baada ya kupiga picha hizo, yeye (Mez B) aliwafowadia washikaji zake ndipo zikazagaa kupitia mtandao wa WhatsApp.

“Hawa wasanii wetu kweli ni majanga. Ona Mez B alichokifanya na hawa mabinti. Yaani wapo kama walivyozaliwa lakini yeye yupo freshi na nguo zake. Kama siyo kudhalilishana ni nini! Amewaaibisha sana. Lakini na wao hawakuona?” alihoji mrembo mmoja aliyefowadiwa  picha hizo na rafiki yake kwenye WhatsApp.

Baada ya kuzitia picha hizo kibindoni, gazeti hili lilimtafuta Mez B kisha kumbana kuhusu tukio hilo ambapo alijitetea kwa ufupi:“Wale ma-miss walikuwa wanaogelea vifua wazi kwa muda mrefu. Wao ndiyo walioniomba kupiga nao picha.”

Kumekuwa na kasumba ya kupiga picha za utupu kisha kuziachia mtandaoni kwa kudhani kuwa ni kujiongezea umaarufu lakini ukweli ni kujiondolea utu na heshima mbele ya jamii.

Cathy:Kujiuzulu Kwa Steve Nyerere ni Pigo Kubwa Bongo Movie, Hakika Kundi Linakufa

$
0
0
Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.

Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.

“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.
GPL

Diamond Platnumz Aingizwa Mkenge na Promotor Huyu, Atoa Onyo kwa wa Bongo wa UK

$
0
0
 Mwanamuziki Diamond Platnumz Asubuhi hii Amepost Picha ya huyu jamaa juu akitoa onyo kwa Wabongo waishio UK Kwambo huyo Jamaa ni Tapeli kwa kusema, Mnaposikia Kaandaa Show ni Vyema Kuziepuka , Jisomee Hapo chini:

Diamond Azidi Kujiharibia Yamkuta Tena Huko London Usiku wa Kuamkia Leo Jumamosi

$
0
0
Haya promota VICTOR aliye Andaa Show ya Diamond London kashikiliwa na polisi, walionunua ticket kuona show yake wamegoma kuondoka hadi warudishiwe pesa na wamerudishiwa.

Diamond hakuonekana ukumbi wa La Face huko London ambapo alitangaza kutumbuiza, na kesho alidai usiku wa tar 20 atatumbuiza ujerumani bure. na hadi mida ile hakujulikana alipo au imekuwaje...tusubirie

Sasa huyu kijana amekuwa anapata bahati mbaya hivi..... Maana inakuwaje juzi iwe ujerumani leo london michezo ya ajabu inamtokea?

HAYA UKWELI TUUSUBIRIE KUUSIKIA AS NDIO BADO HAKUJAKUCHA SASA.... ukweli/uongo utakuja

ila mie nimechoka kumsikia eti show show inabidi management yake ijifunze kitu wasiburuzweeeeeee...tutasikia. inasikitisha sie tunaependa miziki yake na jitihada zake

*******
SIJUI NINI KINAENDELEA JAMANI ILA NAANZA KUMUONEA HURUMA AS EARLIER KWA FB PAGE YAKE ALIANDIKA HIVI

"Tafadhali, nikikuomba unipangie list ya nyimbo ambazo ungependa niziimbe usiku wa leo pale #LAFACE_CLUB London utanipangiaje???...
(if i ask you to arrange a playlist for my Performance tonight at #LAFACE_CLUB #LONDON how would it be.....?)"

ALIKUWA TAYARI KABISAKUTUMBUIZA...... HAYA TUTASIKIA

********
SASA CHA KUSHANGAZA ZAIDI NI KUWA

Masaa kama 7 yaliyopita niseme kama saa 5 usiku mida ya London, alirusha kideo kikionyesha ukumbi huko Ujerumani atakapo piga ile show yake siku ya jumamosi tar 20 Sept (BURE) kufidia yaliyotokea siku ambayo akufanya show. the huku iko hivi ameacha tena sohooo huko London la kutofanya show

Itabidi ajibu kuwa alikuwa wapi mida aliyotakiwa kuwa ukumbini London, nimeona ameanza kuitwa tapeli...

WEWE DIAMOND KAMA ULIKUWA UNAJUA UTAKUWA UJERUMANI KWANINI HAUKURUSHA UJUMBE KUOMBA MSAMAHA FANS WAKO WASISUMBUKE KWENDA?????

TUSUBIRIE STORY ZA KAPUNI....VIDEO TENA MNASIKIKA MNAONGEA KISWAHILI...HOW COME? TUFAFANULIE TUJUE MAANA IKIWA ULISAFIRI KWENDA KWA MWEST KUMFURAHISHA MMMHHHH...SEMA MAANA LAZIMA UTASEMA WA UK HAWAKUKUPA PESA MLIZOAHIDIANA AU???

****
OK DIAMOND KWA INSTA KAMRUSHA MKAKA PICHA NA KUANDIKA HAYA

Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!....kuweni makini sana na promoter huyu (Victor - Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au Hafla yoyote...ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli.... si unajua aisifiae mvua imemnyeshea... basi mie nimeloa kabisa!"

HIII NI KAMA SAA MOJA ILIYOPITA YAANI SAA 11:40 ASUBUHI MIDA YA LONDON


MAJIBU NAYO MOJAWAPO NI

"embu jieleze vizuri sasa maana wengi tukisikia show zako hatutakuja hata kwa kunusa mlango. kwanini unamuita tapeli? juzi ujerumani ulisema hivyohivyo yule kaka tapeli embu sema acha uswahili na kutapeli jina ni lako kamahaujifunzi shauri yako. sema elezea nini sio kukmchafua mwenzio bila proof"

"A piece of advice naomba uwe na mwanasheria wakuangalia hiyo mikataba sasa kuna vitu vimejificha nyuma ya kutaka kukuharibiaa kazi shemu letu kuwa makini na jitahidi uwe na mwanasheriaa binadamu sisi wabaya walaaahi nakuambia kuna kitu tuu hapa c bure"

"Kwanza kama wasemvyo wadau, hizo ni njama, shtukia chezo na ujipange kimataifa na kimaarifa zaidi. Set new terms and hire a professional lawyer kwa ajili ya kuingia mikataba ya kazi zako na kusimamia. Haya yasikuyumbishe wala kukurudisha nyuma bali yawe ngazi ya kufikia kule wasikotaka ufike. @diamondplatnumz"
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images