Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Madudu Lukuki Bodi ya Mikopo, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 14

$
0
0

Madudu Lukuki Bodi ya Mikopo, Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya June 14

Limbeli Ataja Sababu Zilizomfanya Kukumbia Chadema na Kurudi CCM

$
0
0
Mbunge wa zamani wa Kahama, James  Lembeli ametangaza kurejea CCM.

Ametangaza uamuzi huo leo Juni 13, 2018 muda mfupi baada ya kutangaza kuachana na siasa akidai ni kwa sababu ya kubanwa na utaratibu wa mashirika ya kimataifa anayofanyia kazi yasiyotaka mtu anayejihusisha na siasa.

Mbunge huyo wa zamani wa Kahama kwa miaka 10 amefikia uamuzi huku akilia baada ya mama yake mzazi, Maria Lembeli (80), kumshurutisha hadhari kurejea CCM.

Maria ameeleza kusononeshwa na uamuzi wa mwanaye kuhamia Chadema mwaka 2015.

Kauli hiyo ilipokewa kwa nderemo na vifijo na watu umati uliohudhuria shughuli hiyo

Awali, Lembeli alitangaza kuachana na siasa akitaja sababu kuu mbili; kwanza, mashirika na taasisi anazofanya nazo kazi zimemwambia achague moja kubaki kwenye siasa au kuendelea kushirikiana na taasisi hizo.

Akizungumza nyumbani kwake katika kKjiji cha Mseki, kata ya Bulungwa wilayani Ushetu, alisema sababu ya pili iliyomfanya aachane na siasa ni matatizo ambayo familia yake inayapitia baada ya yeye kujiunga na Chadema.

Dawa Bora za Nguvu za Kiume na Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa

$
0
0

Baada ya utafiti wa muda mrefu juu ya matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume na ukosaji wa hamu ya tendo la ndoa ama kushindwa kurudia tendo kwa haraka sasa

MWASELE HERBAL CLINIC. inakuletea suluhu juu ya matatizo haya kwa kutumia dawa za

FULL POWER .ni dawa asili ya vidonge inayotibu tatizo la upungufu au ukosefu wa nguvu zakiume. dawa hii ina mchanganyiko wa kutosha kuzalisha vichocheo vingi vya hormone za gestrogen ziwemo vitamin B6&B1, vitamini E pamoja madini aina ya zinc vitakufanya kuwa na nguvu na muzunguko mzuri wa damu na kuongeza hamu na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya hatua nne au zaidi na kuchelewa kufika kileleni zaidi ya dakika 20-30. ZAT 50 inarudisha maumbile ya uume yaani kurefusha na kunenepesha ulefu nchi 3-7, upana cm, 3-4 standard kiafya haijalishi umri wako hata kwa wazee ukitumia maumbile yatabaki kuwa hivyo siku zote . pia tunatibu matatizo mengine kama presha, kisukari , ngiri ,chango la tumbo,tumbo kujaa gesi, kutokupata choo vizuri,miguu kuwaka moto,matatizo ya uzazi, bawasili namagonjwa yazinaa kama kisonono nakaswende.

Tunapatikana DAR ES SALAAM. SHINYANGA NA ZANZIBAR. kwa wakazi wa dar es salaam utaletewa huduma hii popote ulipo . wa mikoani tunawatumia kwanjia ya mabasi .

Wasiliana nasi kwa sim no 0717702227 au 0754568767.DR . SAGUDA nyote mnakaribishwa

BAKWATA yapiga marufuku kutangaza Eid

$
0
0

Baraza Kuu la waislam Tanzania (BAKWATA) limepiga marufuku utangazaji wa sherehe za Iddi na sherehe zozote zile za dini ya Kiislam bila kupata vibali vya baraza hilo ambalo ndio chombo kikuu cha kusimamia dini hiyo nchini.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu Taifa BAKWATA na Msemaji Mkuu wa Mufti Mkuu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka mbapo amesema kumekuwa na mkanganyiko wa siku na tarehe za sikukuu za Iddi kutokana na baadhi ya watu kujiamulia kutangaza bila kuwa na vibali vya dini hiyo hali ambayo imekua inaleta shida kwa waumini wa dini hiyo.

"Kufuatilia na kutangaza mwezi mwandamo ni suala muhimu na lenye kupewa uzito mkubwa sana na dunia kote jambo hilo huwa kuna mamlaka maalum ambayo inautangaza huo mwezi baada ya  kuuthibitisha", amesema Mataka

Pamoja na hayo, Sheikh Mataka ameendelea kwa kusema "leo Alhamisi Juni 14 ndio tarehe 29 Ramadhani na magharibi yake mwezi ufuatiliwa ili kama umeandama inatangazwa Eid Al Fitr".

Kwa upande mwingine,  Sheikh Mataka amewaomba umma wa kiislamu endapo watafanikiwa kuuona mwezi muandamo basi watoe taarifa kwa sheikh wake au Imam wa msikiti  ili mamlaka zinazohusika na kuutangaza ziweze kuujuza umma.

“Dodoma inaweza kuitwa jiji lakini bado ni kijiji”-Mbunge Mtolea

$
0
0


Leo Bungeni Dodoma Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene amewasilisha azimio la kumpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi wa kuendeleza mji wa Dodoma na kuupa hadhi ya Jiji. Baada ya uwasilishaji wa azimio hilo mmoja wa wabunge waliopata nafasi ya kujadili azimio hilo ni mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea.


Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH mzee khamisi Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili

$
0
0


Kutana na Mtabibu Mwenye KUBRI kutoka kwa ALLAH mzee khamisi Mtabibu wa Nyota za Binadamu na Dawa za Asili ya Africa Mwenye UWEZO Kubaini tatizo lako Pindi tu Utakapo Fanya Mawasilino Kupitia Wasaa Husika..

JE UNASUMBULIWA NA Mapenzi? (Umeachwa na Umpendae,Awe Mume,Mke na Bado unampenda?Na Umejaribu Sehemu nyingi Bila Mafanikio?Wasilina na Mzee khamisi Ujione muujiza wa Papo kwa Papo.. anauwezo WA KURUDISHA MAHUSIANO NA KUIMARISHA NDOA YAKO NDANI YA SAA 12 TU.

Umekimbiwa na Mumeo,mkeo au Mpenzi na anaishi na mtu mwingine? Muone akutatulie Anauwezo wa Hali ya Juu wa Kusambalatisha Mahusiano yao Endapo utafata Atakacho kuelekeza.
Atamfanya Atimize Ahadi zote kwa Muda Mfupi.
Mzee khamisi Anatumia Jina la Muhusika au Picha Kumaliza Tatizo lako..

Anatibu kwa Kutumia Vitabu vya QUR-AN Dawa za Asili za Africa,Dawa za Kiarabu na Majini.Anatafsiri Ndoto. Kushinda BAHATI NASIBU, KUSAFISHA NYOTA. Mvuto wa Mwili na BIASHARA, Kinga ya Mwili,ZINDIKO za Nyumba.MIGUU Kufa GANZI.Kufungua KIZAZI kwa wale walio fungwa kwa njia za KISHIRIKINA. Anakupa Jini la Mali kwa yule anaehitaji Utajiri BILA MASHARTI. Nguvu za KIUME, Humaliza Kesi zilishindika ndani ya siku 14 tu..

Na mengi zaidi whatsapp +255 623448511 au 0783636592 au +255 622588038
NB: TIBA KWA DINI ZOTE NA IMANI ZOTE...

Mimi Ndiye Msanii bora wa Kike Hapa Nchini- Odama

$
0
0
Mimi Ndiye Msanii bora wa Kike Hapa Nchini- Odama
MSANII wa filamu Bongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya J-Film 4 Life, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amejitapa kuwa yeye ndio msanii bora wa kike hapa nchini.



Odama aliyasema hayo hivi karibuni katika mkutano na waandishi wa habari wa kutangaza uzinduzi wa sinema yake mpya ya Mr Kiongozi, uliofanyika katika Hoteli ya Hugo, Kinondoni jijini Dar.



“Unapoiongelea Bongo Movie kwa ujumla, unaniongelea mimi na baadhi ya wasanii wengine, kwa sababu mimi ndio msanii wa kwanza wa kike ambaye nimeanza kutengeneza muvi zangu kwa kampuni yangu,” alisema Odama.



Odama alisema kwenye uzinduzi huo wa filamu yake unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni jijini Tanga, kutakuwa na burudani kabambe kutoka kwa Wasafi Classic Baby ‘WCB’ wakiongozwa na Rayvanny.

Makamu wa Rais ZFA Atangaza Kujiuzulu Rasmi

$
0
0
Makamu wa Rais ZFA Atangaza Kujiuzulu Rasmi
MAKAMU wa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Pemba, Ali Mohammed Ali, ametangaza rasmi kujiuzulu wadhifa huo.

Makamu huyo ameungana na Rais wa chama hicho, Ravia Idarous Faina, Makamu wa Rais Unguja, Mzee Zamu Ali na Abdul Ghani Msoma.



Akizungumza na waandishi wa habari Kisiwani Pemba, makamu huyo alisema hatua hiyo imekuja baada ya kujitathmini kwa kina na kuona tayari viongozi wenzake wameshaachia nyadhifa zao.



“Baada ya kuona viongozi wenzangu wa juu wamejiuzulu nyadhifa zao, sina budi na mimi kujiuzulu kama walivyofanya wenzangu, kuanzia  tarehe 13/6/2018,” alisema.



Ingawa wamekuwa hawataki kuweka wazi kisa cha hali hiyo, inaelezwa kwamba suala la kikosi cha Zanzibar cha vijana kupeleka wachezaji wenye umri mkubwa katika michuano ya Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) ndicho chanzo kikubwa.





Michuano ya Kombe la Dunia Kuanza Leo Urusi

$
0
0
Michuano ya Kombe la Dunia Kuanza Leo Urusi
Michuano ya Kombe la Dunia ya Fifa ya mwaka 2018 inaanza leo nchini Urusi ambapo Urusi watacheza dhidi ya Saudi Arabia baada ya kufanyika kwa sherehe ya ufunguzi katika uwanja wa Luzhniki, mjini Moscow.

Mechi hiyo itaanza saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki.

Michuano hiyo itashirikisha mataifa 32, wakiwemo mabingwa watetezi Ujerumani, na itakuwa na mechi 64 zitakazochezwa katika kipindi cha siku 32.

Fainali itachezwa 15 Julai.

Fainali za sasa za Kombe la Dunia ambazo ni za 21 zitachezwa katika viwanja 12 katika miji 11 nchini Urusi, ambayo inapatikana eneo la upana wa maili zaidi 1,800.

Kutokana na hili, kutakuwa na tofauti kubwa katika wakati mechi zinachezwa.

Ujerumani, waliowashinda Argentina katika fainali ya Kombe la Dunia 2014, wanapania kuwa taifa la kwanza kushinda kombe hilo mtawalia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1962.

Monalisa Kukutana na Staa Bofeda Kutoka Nigeria

$
0
0
Monalisa Kukutana na Staa Bofeda Kutoka Nigeria
Msanii wa filamu Bongo, Monalisa atakutana na staa filamu kutoka Nigeria (Nollywood), Bofeda Moji nchini Marekani.

Wawili hao na wasanii wengine kutoka Afrika watakutana Dallas Marekani kuanzia June 29 hadi July 03, 2018 katika Tamasha la filamu ‘The African Film Festival’ ambalo Bofeda ndiye host.

Katika Tamasha hilo Monalisa atakutana na mastaa wengine kama Naomi Achu kutoka Cameroon, Kelechi Eke kutoka Nigeria na wengineo. Monalisa ndiye msanii pekee atakayeiwakilisha Tanzania katika tamasha hilo.

Utakumbuka April 14, 2016 Monalisa alishinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika. Tuzo hizo zilitolewa Accra nchini Ghana, Msani mwingine wa Tanzania aliyeshinda katika tuzo hizo ni Ray Kigosi.

EID OFA Punguzo 20%, Pata saa Hii ya Automatic Hapa

$
0
0
  • Bonyeza buy now kuagiza saa hii jaza detail zako tutaleta utalipa mzigo ukifika majiji yote TanzaniaSPECIFICATION
  • 1.automatic watch
  • 2.made with steel
  • 3.water proof 3atm
  • 4.full boxed

Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020

$
0
0
Marekani inaitaka Korea Kaskazini kuangamiza silaha ifikapo 2020
Marekani ina matumaini ya kuanza kuona shughuli ya kuangamizwa silaha nchini Korea Kaskazini ifikapo mwaka 2020, mwa mujibu wa waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Mike Pompeo.

Matamshi yake aliyoyatoa alipofanya ziara nchini Korea Kusini, yanafuataia mkutano kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un.

Trump na Kim Jong Un wakubaliana mambo manne makuu
Walisaini makubaliano ya kufanya kazi katika kuangamiza kabisa silaha za nyuklia katika rasi ya Korea.

Lakini nakala hiyo imekosolewa kwa kukosa taarifa za kina kuhusu ni lini na ni vipi Korea Kaskazini itaachana na silaha zake.

"Huwezi Kupambana na Ufisadi"- Dkt. Bashiru

$
0
0
"Huwezi kupambana na ufisadi"- Dkt. Bashiru
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Bashiru Ali amefunguka na kudai watanzania wanaitegemea Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa ndicho chombo imara kinachoweza kutoa huduma kwa wanyonge.


Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo leo Juni 13, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa Jiji la Dodoma waliofika kumlaki pamoja na wanachama wa CCM na viongozi na kusema amepewa dhamana kubwa na wana CCM ya kusimamia mageuzi makubwa ambayo yanakirejesha chama hicho kwa wanachama na katika misingi ambayo iliasisiwa na chama hicho.

"Kuna umuhimu wa kuimarisha Chama Cha Mapinduzi, kwa sababu mambo haya ya mageuzi yanahitaji chombo cha uongozi, huwezi ukajenga uchumi wa kitaifa bila chombo cha uongozi, huwezi ukapambana na ufisadi, ukaimarisha uwajibikaji na uwazi ukatoa huduma za kijamii kwa wanyonge bila ya kuwa na chombo imara na chombo imara", amesema Dkt. Bashiru.

Pamoja na hayo, Dkt. Bashiru ameendelea kwa kusema "kinachotegemewa na watanzania ni Chama Cha Mapinduzi na katika Ilani yetu ya uchaguzi kuna sura mahususi inayohusu uimarishaji wa chama chetu".

Kwa upande mwingine,  Dkt.  Bashiru amedai hali ya maslahi ya watumishi wa chama hicho sio wa  kuridhisha huku akiwataka watumishi wa CCM kuendelea kufanyakazi kwa moyo wa kujitolea.

Mtu na Mpenzi wake Wamefariki Wakipiga Selfie Juu Ghorofa

$
0
0
Mtu na Mpenzi wake Raia wa Australia wamefariki baada ya kudondoka kutoka kwenye ukuta mrefu wa fukwe maarufu ya Ericeira nchini Ureno walipokuwa wakipiga Selfie.

Taarifa zinasema kuwa Wapenzi hao walidondoka kutoka umbali wa mita 30, na Miili ya yao iliokotwa na msafishaji wa fukwe hiyo asubuhi ya June 11.

Polisi wamesema kuwa wanaamini Wapenzi hao walikosa usawa walipokuwa kwenye ukuta huo na kudondoka chini.

Timu ya waokoaji imeeleza kuwa walikuta simu ya mkononi katika eneo la tukio na kuamini kwamba Wapenzi hao walikuwa wanapiga Selfie na ndipo simu ikadondoka kisha wakajaribu kuiokoa na ndipo walipodondoka chini .

Mpaka sasa Wapenzi hao bado hawajatambuliwa majina yao lakini inakadiriwa kuwa Mwanamke anaweza kuwa na umri wa miaka 30 huku Mwanaume akitazamiwa kuwa na umri wa miaka 40.

Jamiii Forums Watoa Tahadhari "Hatujaanzisha JamiiForums Mpya’

$
0
0

‪TAHADHARI: Hatujaanzisha ‘JamiiForums Mpya’ kama ambavyo baadhi ya wateja wetu wanaaminishwa
-
Kama ukitumia jukwaa lolote tofauti na JF, epuka kuweka data zako ulizotumia katika jukwaa letu‬

Navy Kenzo kumwaga mkwanja kwa mashabiki wao

$
0
0

Kundi la muziki Bongo, Navy Kenzo limetangaza fursa kwa vijana au mashabiki wao. 

Guess what, fursa hii ni kwa wale wanaojua kucheza ambapo watatuma clip wakicheza wimbo mpya wa kundi hilo uitwao Fella. 

Ambaye ataibuka mshindi atajinyakulia dola za kimarekani 1,000 zaidi ya Tsh. 2,200,000.

Fella ni wimbo wa kwanza kwa Navy Kenzo kutoa mwaka huu tangu pale walipomshirikisha Patoranking katika wimbo wao unaokwenda kwa jina la Bajaj uliotoka June 19, 2017.

Hashimu Rungwe- Nitaungana na Mbowe, Zitto Ili Kuongeza Nguvu

$
0
0
Hashimu Rungwe- Nitaungana na Mbowe, Zitto Ili Kuongeza Nguvu
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe amesema kuwa yupo tayari kuungana na upinzani pale muda utakapofika na kujiridhisha kuwa mipango inatekelezeka.


Rungwe amesema hayo wakati akizungumza na eatv.tv ambapo amefunguka kuwa endapo ataridhishwa na muungano huo wa vyama vya upinzani atajiunga ili kuongeza nguvu.

“Bado sijajua wanatekeleza vipi sera zao lakini pindi nitakapopata muda na kueleweshwa zaidi nitaungana nao kwakuwa muda ni kila kitu”, amesema Rungwe.

Rungwe ameongeza kuwa kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa kunapunguza hamasa kwa wananchi katika masuala mbalimbali kwa kile alichodai kuwa mikutano ya kisiasa imekuwa ikiongeza hamasa kwa wananchi.

Hivi karibuni viongozi hao wa vyama vya upinzani nchini ACT-Wazalendo pamoja na Chama cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) walitangaza kuunda umoja utakaokuza na kuhamasisha demokrasia unaokwenda kwa jina la ‘United Democratic Front’ utakaohusisha asasi zingine pia na sio siasa pekee.



Tanzia: Mume wa Naibu Waziri Angelina Mabula Afariki Dunia

$
0
0
Tanzia: Mume wa Naibu Waziri Angelina Mabula Afariki Dunia
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula.  amepata pigo la kuondokewa na mumewe aliyefariki dunia jana Jumatano, Juni 13, 2018 majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.



Taarifa ya msiba huo imetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi,  na kusomwa na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge,  ambaye amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa Mwanza, keshokutwa Jumamosi.



Mwezi Aprili mwaka huu, Angelina Mabula alipata pigo kwa kufiwa na baba yake mzazi, Sylvester Lubala Shimba.

Dude Afichua Siri ya Kilichomfanya Adumu Miaka Mingi na Mkewe

$
0
0
Dude Afichua Siri ya Kilichomfanya Adumu Miaka Mingi na Mkewe
MKALI wa sinema za Kibongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ amefunguka kuwa, kitu kikubwa kilichomfanya adumu miaka mingi na mkewe Eva ni kutofichana mambo.



Akizungumza na Amani juzi, Dude alisema licha ya kupitia ‘mishale’ mingi kwenye uhusiano wake, wamefanikiwa kuikwepa sababu hawafichani mambo.



“Unajua mke wangu amekuwa akisikia mengi sana, mara sijui Ester Kiama, Irene Uwoya sijui nani lakini kwa kuwa nikirudi nyumbani simfichifichi wala sina makandokando, ananiamini kwamba sina mchepuko,” alisema Dude ambaye ana watoto takriban saba, wawili kati yao akiwa amezaa na mkewe anayeishi naye sasa, Eva.

Kocha Pierre Lechantre Aondoka ...... Awaachia Ujumbe Mzito Viongozi wa Simba

$
0
0
Kocha Pierre Lechantre Aondoka ...... Awaachia Ujumbe Mzito Viongozi wa Simba
Mfaransa Pierre Lechantre ameondoka, lakini amewaachia ujumbe mzito viongozi wa klabu ya Simba ambao utakuwa na manufaa endapo utafanyiwa kazi.

Lechantre ameondoka kwa mafanikio kwa kuipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kukosa kwa miaka mitano. Mara ya mwisho Simba ilitwaa ubingwa mwaka 2012.

Akizungumza Dar es Salaam jana muda mfupi kabla ya kuondoka jijini kwenda Ufaransa, kocha huyo alisema anaondoka kwa amani akiwa na rekodi nzuri Simba.

Lechantre, aliyekuwa ameingia mkataba wa miezi sita Simba, alisema kuwa ili klabu hiyo ipate mafanikio inatakiwa kujenga uwanja wa kisasa wa mazoezi na mechi.

“Simba inatakiwa kuwa na vifaa vyote vya kufanyia mazoezi, kama ‘MO’ (Mohammed Dewji) alivyosema kutakuwepo na hosteli, ‘gym’ na mambo mengine muhimu ili kupunguza gharama,” alisema Lechantre.

Hata hivyo, alisema haikuwa kazi rahisi kuinoa Simba kwa kuwa ilikuwa mara ya kwanza kufika Tanzania na aliwakuta wachezaji wakiwa kwenye morali ndogo.

“Niliikuta timu katika morali ya chini wachezaji wengi hawakuwa na fiti kushindana muda wote jambo ambalo nilirekebisha na timu kushindana muda wote,”aliongeza Lechantre.

Pia alidai alikuta baadhi ya wachezaji hawakuwa na nidhamu, hivyo alikemea vikali jambo hilo sanjari na kutoa adhabu ikiwemo ya kukatwa mshahara kwa mchezaji aliyekiuka utaratibu wa klabu.

Kocha huyo alimalizana na Simba Jumanne wiki hii, baada ya kukacha kukaa kwenye benchi la Simba katika mchezo wa michuano ya SportPesa ambao timu hiyo ilifungwa mabao 2-0 na Gor Mahia ya Kenya. Gor Mahia itacheza na Everton baada ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
Chanzo: Mwananchi
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live


Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>