Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

TFF Yaongeza Idadi ya Wachezaji wa Kimataifa

$
0
0
Image result for tffTFF Yaongeza Idadi ya Wachezaji wa Kimataifa
SHIRIKISHO la Soka Tan­zania (TFF), limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kwa klabu za Ligi Kuu Bara kutoka saba na kufi­kia kumi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.



Hiyo itakuwa nafasi pekee kwa klabu kongwe za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikilalamikia kubanwa usajili wa profesheno wachache hapo awali.



Simba tayari hadi hivi sasa ina wachezaji nane wa kimataifa ambao ni James Kotei, Emmanuel Okwi, Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Haruna Niyonzima, wengine wal­iowasajiliwa hivi karibuni ni Pascal Wawa, Meddie Kagere na Fabrice Kakule.



Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumatano, shirikisho hilo limepanga kuanza kutumia kanuni hizo katika msimu ujao wa ligi ili kuhakikisha wawak­ilishi wa michuano ya kimataifa wanakuwa na kikosi cha wachezaji wengi profesheno wenye uzoefu.



Mtoa taarifa huyo alisema, wakati shirikisho hilo likitangaza kuongeza idadi hiyo ya wachezaji tayari limetoa sharti la kutumia nyota saba pekee katika kila mchezo wa ligi huku mashindano ya kimataifa likiwaruhusu kutumia wowote watakaohitaji.



“TFF limepanga kuongeza idadi ya wachezaji wa kimataifa kutoka wachezaji saba hadi kumi katika kuelekea msimu ujao wa ligi.



“Tayari klabu zimeanza kupewa taarifa za usajili huo wa wache­zaji wa kimataifa, lengo kubwa ni baadhi za klabu kuziimarisha timu zao katika kuelekea michuano ya kimataifa.



“Kanuni hizo za wachezaji kumi ziliwahi kutumika misimu mitano iliyopita ya ligi kwa TFF kutoa na­fasi ya kusajili idadi hiyo ya wache­zaji ambayo tunaamini siyo ngeni,” alisema mtoa taarifa huyo.



Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao, kuzungumzia hilo simu yake ya mkononi iliita bila ya mafanikio ya kupokelewa, lakini Championi linafahamu tayari viongozi wa klabu wameshapewa taarifa.

Manchester City Yathibitisha Kumsajili Riyad Mahrez

$
0
0
Manchester City Yathibitisha Kumsajili Riyad Mahrez
Mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, Manchester City wamethibitisha kumsajili mchezaji, Riyad Mahrez kwa dau la pauni milioni 60 kutokea Leicester City.



Mahrez ambaye amesajiliwa kwa dau lililoweka rekodi ya klabu hiyo marakadhaa amekuwa akitakiwa na City lakini dili likigonga mwamba.

Miamba hiyo ya soka ya Uingereza imekamilisha kandarasi ya winga huyo wa Leicester ambaye amefanikiwa kufunga jumla ya mabao 13 kwenye michezo yake 41 aliyocheza akiwa na mbweha hao msimu uliyopita.

Winga huyo anaweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi katika historia ya Manchester City na kufuta rekodi iliyowekwa na beki wa Ufaransa, Aymeric Laporte aliyetua hapo kwa pauni milioni 57 mwezi Januari.

Mahrez alijiunga na Leicester mwezi Januari mwaka 2014 na kuiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa ligi ya Sky Bet Championship.

Beka Flavour Amuonya Aslay

$
0
0
Msanii wa Bongofleva Beka Flavour amefunguka na kumtaka mwanamuziki mwenzake Aslay kuongeza nguvu na maarifa kwenye muziki wake ili aweze kufika mbali zaidi huku akimsii kuachana na masuala ya kiki za mitandoni.


Beka ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Aslay kuachana na mama watoto wake na kuamua kuweka wazi 'penzi' lake jipya mitandaoni jambo ambalo wengi wameliona kama ni 'kiki' ili kusudi aendelee kuzungumziwa midomoni mwa watu.

"Kuna watu wakifanya 'kiki' ina wasaidia na muziki wao unaenda inawezekana Aslay ndiyo miongoni mwa hao lakini mimi sijui, ila ninachomshauri afanye muziki mzuri, najua ni mwanamuziki mkubwa ila siwezi kumwambia aache kufanya kiki kwenye mitandao za ku-post mpenzi wake mpya itakuwa haileti maana kwa kuwa mimi sio mzazi wake", amesema Beka.

Pamoja na hayo, Beka ameendelea kwa kusema "watanzania wamekaririshwa kuwa ili mtu aonekane amefanya muziki mzuri na kuwa maarufu zaidi ya wengine basi lazima utengeneze kiki ya mahusiano ya kutembea na staa mkubwa aidha bongo movie au bongo fleva. Ila kwa katika nafsi yangu mimi siwezi kuliamini hili", amesema Beka Fleva.

Mtazame hapa chini msanii Beka Flavour ambaye ni moja ya zao la Yamoto Band akimshauri swahiba wake Aslay juu ya muziki wake.

Serikali Yawataka Wananchi Kutoa Taarifa cha Utaratibu Mbaya wa Vituo vya Afya

$
0
0
Serikali Yawataka Wananchi Kutoa Taarifa cha Utaratibu Mbaya wa Vituo vya Afya
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewataka wananchi kutoa taarifa kwa hospitali, zahanati au kituo cha afya chochote kitakachokuwa kinatoa majibu ya kipimo cha typhoid ndani ya nusu saa kwa kuwa siyo utaratibu za kitabibu.



Tamko hilo limetolewa na Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizungumza na eatv.tv leo Julai 10, 2018 baada ya kupita siku kadhaa tokea alivyotoa kauli yake iliyozua taharuki na kuwaacha wengi njia panda kuwa 'asilimia 70 ya homa Tanzania siyo malaria wala siyo typhoid, hivyo unapokwenda kwenye vituo vya afya kupimwa halafu ukaambiwa una typhoid inabidi uhoji ni kigezo gani kilichotumika mpaka uambiwe unaumwa ugonjwa huo'.

"Mara nyingi sana katika vituo vyetu vya kutoa huduma ya afya kumekuwa na tatizo la kila mgonjwa kuwa na malaria au muda mwingine kusema ana typhoid. Utaratibu wa kupima kipimo cha Typhoid sio kama wanavyosema kuwa unaenda leo unapimwa halafu unapatiwa majibu ndani ya nusu saa. Mara nyingi kipimo hiki huwa kinatoa majibu ndani ya saa 48", amesema Dkt.Ndugulile.

Pamoja na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "siasa na afya ni vitu viwili tofauti hivyo nawaomba wananchi wasipuuzie suala hili la kuhoji endapo watapewa majibu ya typhoid ndani ya nusu saa maana hiyo ni haki yao ya msingi".

Kwa upande mwingine, Naibu wa Waziri Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa mtu yoyote ambaye atalalamika kutopewa haki za msingi anapokuwa amekwenda hospitalini, anayohaki ya kwenda kufungua mashitaka na mtoa huduma kuchukuliwa hatua stahiki.


Kelechi: Brown Hana Hadhi Ya Kutembea na Wema Sepetu

$
0
0
Kelechi: Brown Hana Hadhi Ya Kutembea na Wema Sepetu
Msanii wa muziki anayefanya kazi zake  Mombasa Kenya, Kelechi amefunguka na kudai msanii mwenzake Brown Mauzo hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu.

Brown Mauzo ameibuka  na kufunguka juu ya mapenzi yake kwa msanii wa filamu Tanzania Wema Sepetu na kudai anataka kumuoa jumla jumla.

Kwenye mahojiano na Enews ya East Africa Tv, Kelechi amefunguka na kudai Brown hawezi kumuoa Wema Sepetu wala hata kumuhudumia hawezi:

"Huyu Brown ni mtoto mdogo sana hawezi kumpata Wema Sepetu alafu isitoshe ni Dogo sana kwa Wema na pia hana hata hadhi ya kuwa  naye kimapenzi”.

Lakini pia Kelechi amedai Brown amekimbia Mombasa na kurudi Tanzania baada ya kutembea na mke wa Meneja wake.

Mbwa Hatari zaidi Huyu Ndiye Mbwa Mkali Duniani Anakamata Watu 6 kwa Mara Moja

$
0
0
Mbwa HATARI zaidi Huyu Ndiye Mbwa Mkali Duniani Anakamata Watu 6 kwa Mara Moja
Ufugaji wa mnyama aina ya Mbwa ambapo inaelezwa kuwa kuna Mbwa wanafikia uzito wa hadi Kilo 150 waliochanganywa na mbegu za Simba na Chui wakiwa na uwezo wa kukamata watu 6 kwa wakati mmoja.

Afisa Masoko wa Mkuki Dog Kennel, Sylvester Luena anasema Mbwa wenyewe uwezo wa namna hiyo wengi wanachanganya mbegu katika mataifa ya nje kwa Tanzania hakuna.

“Jamii ya hao wanapatina Marekani, Afrika Kusini, Uingereza na mataifa mengine ambapo sisi tunafanya kuagizia na wana uwezo mkubwa wa kukamata hata watu 6 kwa muda,”. amesema Luena

Luena amesema kuwa Mbwa wa namna hiyo wanafundishwa jinsi ya kulinda na kukabiliana na wahalifu hasa kwa nyakati za usiku.

Hii Ndio Idadi ya Wachezaji Anayoitaka Kocha wa Simba

$
0
0
Hii Ndio Idadi ya Wachezaji Anayoitaka Kocha wa Simba
Kocha Mkuu wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, amesema kuwa kikosi chake kinahitaji kuwa na wachezaji 27 pekee huku akiahidi kuwatoa kwa mkopo baadhi ya wachezaji wasiokuwa na kiwango katika timu huku jina la kipa Emmanuel Mseja likiwa la kwanza.

Kauli hiyo, aliitoa juzi jioni baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.

Simba tayari imefanikiwa kuwasajili wachezaji sita hadi sasa ambao ni Adam Salamba, Mohammed Rashid, Meddie Kagere, Abdul Mohammed, Marcel Boniventure na Pascal Wawa.

Akizungumza na Championi Jumatano, Djuma alisema katika usajili huo wa wachezaji 30, wanataka kubakisha nafasi tatu pekee kwa ajili ya kuongeza katika usajili wa dirisha dogo kama akihitajika mchezaji kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao.

Djuma alisema, wachezaji watakaobaki kuichezea Simba ni wale watakaoweza kupambana ndani ya uwanja katika kuipa matokeo mazuri huku akiahidi kuwaondoa baadhi ya wachezaji wenye mikataba kwenda kwenye klabu nyingine kwa ajili ya kulinda viwango vyao.

“Sidhani kama ni sawa kuendelea kukaa na mchezaji mwenye mkataba kwenye timu wakati hana nafasi ya kucheza katika kikosi changu, hivyo nimeona ni vema nikamuachia kwenda kwa mkopo kwingine kwa ajili ya kwenda kucheza kuliko aendelee kukaa benchi.

“Hivyo, hiyo inaweza kumsababishia mchezaji kuua kiwango chake kama mfano kipa wetu Mseja msimu uliopita wa ligi hakupata nafasi ya kucheza, hivyo kama kocha nimeshauri tumtoe kwa mkopo ili aende kwingine akacheze.

“Na hilo tayari nimelifanyia kazi na kuutarifu uongozi, hivyo Mseja hatakuwa katika sehemu ya kikosi chetu, pia wapo wengine ambao hivi karibuni nitawaweka wazi,” alisema Djuma.

Kim Kardashian Ataka Wafungwa Wakike Wakaguliwe na Askari Wa Jinsia Yao

$
0
0
Kim Kardashian Ataka Wafungwa Wakike Wakaguliwe na Askari Wa Jinsia Yao
MWANAMITINDO na mtangazaji wa televisheni nchini Marekani, Kim Kardashian West , ametaka ukaguzi magerezani ufanyiwe mabadiliko ili wafungwa wa kike wakaguliwe maungoni na askari wanawake wenzao, si pamoja na wanaume kama ilivyo sasa.

Aliyasema hayo wiki hii  alipotembelea gereza la wanawake alilofungwa maisha mwanamke Alice Marie Johnson kwa kujihusisha na madawa ya kulevya ambapo alibidi kutoa ombi hilo kwa Rais Trump wa Marekani ili amsamehe mwanamke huyo.

Ombi la mabadiliko hayo alilifikisha kwa Gavana Jerry Brown aliyesema wanalifanyia kazi.


Kim akiwa  na Trump alipokwenda kumwombea msamaha Alice Marie Johnson.


Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI ,

PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

WOTE MNAKALIBISHWA, KAMA, UTAKUWA NA TATIZOUTAHUDUMIWA

Lunch Time inavyotumiwa na Wafanyakazi Wanandoa Kuchepuka

$
0
0
Usije ukajidanganya kumuona mumeo au mkeo eti anarudi nyumbani mapema na weekend hatoki ukadhani uko salama.

Sasa hivi ile lunch time kuanzia saa saba mpaka nane huko maofisini ibilisi anakuwa ameshika usukani, ikizingatiwa sasa kuna mahotel mazuri pande kariakoo, manzese, magomeni zile zinakuwa zimejaa ikifika muda huo, wake za watu na waume za watu wanakuwa wanacheza mechi za kirafiki watch out.

Hili halina ubishi

Wanawake Wanataka Ndoa Lakini Hawapati, Ni Kweli Hamna Waoaji?

$
0
0

Kuna kitu kinanichanganya ni kweli hamna waoaji siku hizi au wanawake wanachagua sana?

Sasa hivi hili limekuwa kama janga la Taifa.
Single ladies wengi sana unakuta mwanamke mpaka miaka 33 hana hata mchumba wa kusingizia.

Na ni wengi mitaani tunawaona na wengi wao wakiona umri unazidi basi wanaamua kuzaa na kuwa single mums.

Nyie mnaonaje ni tabia hazikidhi mwanamke kuolewa?

Au ni gharama za harusi?

Wanaume please please muoe watoto wasio na baba wanazidi kuongezeka.

Na hamuwatendei haki wanawake.

Hii Hapa Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo ya Uume

$
0
0
Tatizo hili limekuwa likiwaadhiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baada ya kujiona wapo tofauti sana na wengine kwa kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi 6-8 kwanza upungufu wa vichocheo hivi huchochea ukuaji wa uume chongo ambalo hushambulia nerve ambayo uharibu kabisa ukuaji wa uume, ngiri, punyeto, ambayo huathili misuli ya uume, ngiri huleta maumivu, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, korodani moja kuvimba, kutopata choo vizuri, sababu hizi hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara nyingi hata nguvu za kiume ( hamu ya tendo la ndoa) hupungua na kwisha kabisa

GEMBE :Ni dawa inayozalisha na kukufanya uume kukua na kuongezeka
NGEMO : Ni dawa bora ya kuongeza nguvu za kiume

Hukutia hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi mara4 nne bila kukinai au kuchoka pia itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk30-45 kwa mtumiaji pia tunatibu kisukari, bp, ngiri, miguu kuwaka moto KAMA HUNAMDA WA KUFIKA OFISINI KWETU UTALETEWA POPOTE TUPO MBAGALA RANGI TATU

 0753471612/ 0715249530
0623 386 305

DR KUZENZA

Waziri Aagiza Polisi Wamkamate Mwalimu Aliyembaka Mwanafunzi

$
0
0
Waziri Aagiza Polisi Wamkamate Mwalimu Aliyembaka Mwanafunzi
NAIBU Waziri wa Elimu,  Sayansi na Teknolojia, William Olenasha, ameagiza kukamatwa kwa mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Loliondo,  Erick Kalaliche,  kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wake wa kidato cha tatu (jina limehifadhiwa) ambaye kwa sasa amehamia mkoa wa Lindi baada ya kutenda kosa hilo.



Akizungumza katika kikao cha dharura kilichofanyika  makao makuu ya Halmashauri ya Ngorongoro,  Olenasha amesema jambo hilo linasikitisha na kuidhalilisha sekta ya elimu na lazima hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe mara moja.



Amesema wizara yake haiwezi kuvumilia walimu ambao wanafundisha watoto ambao pia ni kama wazazi wanaofumbia macho vitendo vya vichafu ambavyo vinarudisha nyuma sekta ya elimu na juhudi za serikali ya kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.



Afisa elimu wa wilaya ya Ngorongoro, Emanuel Sukuma,  amekiri mwalimu huyo kutenda kosa la kumbaka mwanafunzi huyo ambapo kitendo hicho kilifanyika mwezi wa tatu na kujulikana mwezi wa sita ambapo hakuna hatua zozote za kinidhamu zilizochukuliwa.



Amesema kuwa mwalimu Erick alimchukua mwanafunzi huyo ambaye alikuwa anasoma kidato cha tatu katika shule hiyo ya Sekondari Loliondo na kumpeleka nyumba ya kulala wageni na kumbaka.



Tarehe 9 July 2018 naibu waziri wa Elimu sayansi na Teknolojia Mh William Olenasha alifanya ziara ya Kushtukiza shule ya sekondari Loliondo na kuhoji kuhusiana taarifa za mwalimu huyo ambapo mwalimu mkuu wa Shule hiyo Bi Neema Mchao alikosa majibu sahihi mbele ya Naibu waziri lakini baadae kukiri kwamba mwalimu alihama shuleni na alikuwa ametenda kosa hilo.



Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Loliondo Bi Neema Mchao amekiri kufuatilia jambo hilo lakini alipohojiwa kwanini hakuchukua hatua za kinidhamu alisema yeye aliachia mamlaka husika kwasababu hata yeye jambo hilo lilimsikitisha.



Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashidi Mfaume Taka amesema kuwa utaratibu unafanyika kurudishwa kwa mwalimu huyo kutoka mkoa aliyohamishiwa kuja Ngorongoro kwa kuwa kitendo alichokifanya ni Udhalilishaji katika wilaya hiyo.



Kufuatia kikao hicho mkuu wa Polisi wilayani Ngorongoro amemtaka Mkuu wa Shule ya Sekondari Loliondo pamoja na Afisa Elimu kufika kituoni  kwa ajili ya Uchunguzi zaidi wa tukio hilo.

Ambulance Yakamatwa Ikiwa Imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya Aina ya Mirungi

$
0
0
Ambulance Yakamatwa Ikiwa Imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya Aina ya Mirungi
Gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime yenye namba za DFPA 2955 imekamatwa ikiwa imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya aina ya Mirungi.

RPC wa Mara Juma Ndaki amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime.

Akiongea na AyoTV Kamanda Ndaki amesema “Tumewakamata na Mirungi Kilo 800, tunawashikilia watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime, ushauri wangu tuwe makini tunapoajiri Madereva serikalini,”





Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Waandamanaji Wanaopinga Kulipia Kodi Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Polisi Watumia Mabomu Kuwatawanya Waandamanaji Wanaopinga Kulipia Kodi Mitandao ya Kijamii
Polisi nchini Uganda imefyetua gesi ya kutoa machozi na risasi hewani kutawanya kundi la waandamanji wanaopinga kodi iliyoidhinishwa ya kutumia mitandao ya kijamii.

Mwandishi wa BBC anasema polisi wamejaribu kumkamata mbunge ambaye pia ni muimbaji mashuhuri Robert Kyagulany, anayefahamika kwa umaarufu Bobi Wine, aliyeongoza maandamano hayo, lakini amefanikiwa kutoroka.

Mpiga picha mmoja katika maandamano hayo amekuwa akituma picha katika mtandao wa kijamii Twitter kuhusu yanayoendelea:

Kodi hiyo iliyoidhinishwa mwanzoni mwa mweiz huu inahitaji watumiaji mitandao ya kijamii nchini kulipa shilingi 200 za Uganda [$0.05, £0.04] ili waweze kutumia mitandao kama Facebook, Twitter na WhatsApp.

Ni kwanini serikali inatoza kodi hii ?
Bunge liliidhinisha kodi hiyo mnamo Mei baada ya rais Yoweri Museveni kushinikiza mageuzi hayo.

Rais Museveni a anaoutaja kuwa maoni, upendeleo, matusi na hata chati kwa marafiki.

Katika barua aliyomuandikia waziri wa fedha mnamo Machi, rais Museveni amesema kodi kwa mitandao ya kijamii inaweza kuongeza kipato cha serikali, na kupunguza mikopo inayochukua serikali na pesa za ufadhili.

Ameongeza kwamba haungi mkono kodi iitozwe kwa matumizi jumla ya mtandao kwasababu hili litaathiri matumizi yake kwa misingi ya 'elimu, na utafiti '.

Waziri wa habari na mawasiliano Uganda Frank Tumwebaze pia ametetea kuidhinishwa kwa kodi hiyo, akisema kwamba fedha zitakazopatikana zitatumiwa 'kuwekeza katika rasilmali zaidi za kimitandao'.

Twaweza Yaangukia Mikono ya Serikali.... Yalimwa Barua Kujieleza Sababu ya Kutoa Utafiti Bila Kibali

$
0
0
Twaweza Yaangukia Mikono ya Serikali.... Yalimwa Barua Kujieleza Kutoa Utafiti Bila Kibali
Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imeitaka Taasisi ya Twaweza kujieleza ndani ya siku saba kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa.

Barua hiyo ya Costech imesema, Twaweza waliomba kibali cha tafiti nne ambazo mmoja umekamilika na nyingine tatu bado zinaendelea.

Kwa mujibu wa barua hiyo iliyosambaa mitandaoni ikionyesha imesainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Amos Nungu, tume hiyo ndiyo yenye mamlaka ya kusajili na kutoa kibali cha tafiti zote za muda mfupi na mrefu zinazofanywa nchini.

Barua hiyo imedai kuwa mwishoni mwa wiki, kulikuwa na taarifa za Twaweza kutoa utafiti uliopewa jina la ‘Sauti za Wananchi’  ambao, tume haina rekodi zilizoruhusu kuchapishwa kinyume cha sheria.

“Kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 7 cha mwaka 1986, tume hiyo ndiyo yenye mamlaka kusajili na kutoa kibali cha kufanyika tafiti nchini,” imesema barua hiyo.

Taarifa kutoka Twaweza zinathibitisha taasisi hiyo kupokea barua kutoka Costech na kwamba wanaifanyia kazi.

Hivi karibuni Twaweza walitoa ripoti ya utafiti wa ‘Sauti za Wananchi’ ukielezea maoni ya wananchi kuhusu siasa nchini.

Utafiti huo umeonyesha kuporomoka kwa ukaribu wa wananchi na vyama vya siasa, utekelezaji wa majukumu kwa viongozi walioko madarakani, Rais anavyotekeleza majukumu yake tangu alipoingia madarakani na uhuru wa kujieleza katika baadhi ya maeneo.

Nisha: Siwezi Tena Kudate na Mwanaume Asiye na Pesa Sababu Hawana Shukrani

$
0
0
Nisha: Siwezi Tena Kudate na Mwanaume Asiye na Pesa Sababu Hawana Shukrani
Msanii wa filamu, Salma Jabu aka Nisha Bebee amefunguka kwa kudai kwamba hawezi kudate na mwanaume ambaye hana pesa kwa madai hawana shukrani.


Muigizaji huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, amedai wanaume wengi waliopita kwake walikuwa wanampenda kwaajili ya pesa lakini sio mapenzi ya kweli.

“Nimeshadate tayari na watu ambao hawana mtonyo lakini mwisho wa siku hawana shukrani,” Nisha aliimbia Bongo5. “So kwa sasa hivi siwezi kudate na mtu ambaye nimempita kipato, lazima awe amenipita,”

Aliongeza, “Wanaume wengi ambao walikuwa wanakuja kwangu walikuwa wanataka mpaka kununuliwa nguo, kila wiki wanataka shopping ya nguo, baby sijui nimeona kitu fulani kizuri, sijui nataka kile halafu mwisho wa siku hawana mapenzi wa kweli,”


Muigizaji huyo amesema kwa sasa amempata mwanaume wa kizungu ambaye amedai anaona anaweza kufika naye mbali zaidi kimaisha.

Wakulima Mkoani Kagera : Bora Tulime Baangi Kuliko Kuuza Kahawa

$
0
0
Wakulima Mkoani Kagera : Bora Tulime Baangi Kuliko Kuuza Kahawa
Wananchi na wakulima wa kahawa mkoani Kagera wamelalamikia suala la kukamatwa wakati pindi wanapokuwa sokoni wakiuza zao hilo na kusema kuwa kuliko kuuza kahawa bora walime bangi kwani wakulima wa zao hilo hawako huru kwa sasa.



Wakulima hao wamefunguka hayo wakati wakizungumza na Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof. Anna Tibaijuka ambapo wamesema kuwa zao la kahawa halina uhuru kwani wafanyabishara hao wanahusishwa na biashara za magendo kwa kile walichodai kuwa hakuna magendo yanayofanyika kwa watu wa ndani.

“Tunaomba hili zao letu lipewe uhuru, ndani ya nchin hakuna biashara ya magendo huwa ni kubadilishana tu ninakupa mahindi unanipa kahawa, nakupa kahawa unanipa ndizi”, amesema mmoja wa wananchi.

Akizungumza na wananchi Prof. Tibaijuka, amesema kuwa amekuwa akizungumzia sana suala la kahawa bungeni, kwakuwa bila kahawa hakuna maendeleo mkoani humo.

“Mimi kama mbunge wa Muleba Kusini, nitawatetea wakulima na sikubaliani na kuzuia watu kuuza binafsi, kilio changu juu ya zao la Kahawa hata Rais Magufuli anafahamu”, amesema Prof. Tibaijuka

Hayo yanajiri baada ya  Serikali mkoani humo kutangaza kuwa  kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani, kwa mantiki hiyo hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika.

Hatimaye Watoto wa Wakimbizi Wakutanishwa na Wazazi Wao

$
0
0
Hatimaye Watoto wa Wakimbizi Wakutanishwa na Wazazi Wao
WAKATI wazazi kadhaa wakimbizi,  wengi wao kutoka Mexico wakiunganishwa na watoto wao waliotenganishwa nao kwenye mpaka wa Marekani na Mexico miezi kadhaa iliyopita kutokana na sera za Rais Trump wa Marekani, wengi wao wanasubiri kuwaona watoto wao.

Watoto kadhaa jana (Jumanne) waliungana na wazazi wao kwa chereko huko Michigan.

Hilo limetokea baada ya Idara ya Uhamiaji kusema wakimbizi hao watakuwa huru wakati matatizo yao yakishughulikiwa na mahakama ya uhamiaji.

Hizi Hapa Sababu za Madiwani Watatu Kuvuliwa Uanachama CUF

$
0
0
Hizi Hapa Sababu za Madiwani Watatu Kuvuliwa Uanachama
Chama cha Wananchi (CUF) kimewavua uanachama wa chama hicho Madiwani watatu mkoani Tanga kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Kuu za chama hicho kwa niaba ya vijana wa Jumuiya za Wilaya za DSM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ilala (JUVICUF), Canal Kitimai amesema Madiwani hao ni Rashid Hamza wa Kata ya Mwanzange na Madiwani wawili wa viti maalum wa Wilaya ya Tanga ambao ni Halima Mbwana na Fatuma Hamza.

“Kutokana na Katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la mwaka 2014 ibara ya 83 kifungu cha (4) nanukuu ‘Baraza Kuu l uongozi la taifa linaweza kuchukua hatua za kinidhamu zilizo zilizoainishwa katika kifungu cha (5) cha kifungu hiki dhidi ya viongozi watokanao na CUF.” -Kitimai

Hatua zinazoweza kuchukuliwa na Baraza la Uongozi la Taifa la CUF zilizoainishwa katika kifungu cha (5) dhidi ya kiongozi yoyote aliyetajwa kwenye kifungu cha (4) ni pamoja na kutoa onyo kwa maandishi, kutoa karipio kali kwa maandishi, kumsimamisha au kumfukuza uanachama.
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images