Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

Jibu la Lady Jaydee kwa Shabiki Kuhusu Tuhuma za kujichubua

$
0
0

Jibu la Lady Jaydee kwa shabiki kuhusu tuhuma za kujichubua
Malkia wa muziki wa Bongo Fleva nchini Lady Jaydee amejikuta katika tuhuma nzito kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake.

Jide anatuhumiwa kuanza kujichubua na kupoteza muonekano wake wa zamani.

Sakata hilo limeibuka baada ya Jaydee kupost picha yake kwenye mtandao wa Instagram akiwa na muonekano kabambe wa kuvutiana na kuandika, "🖤 Black Woman 🖤."

Hapo aliibuka shabiki mmoja kwa kuandika comment inayosomeka, "Black Woman zamani Mama cku hizi unajichubua."

Aunt Ezekieli Afunguka Kuhusu Ndoa yake na Baba Cookie

$
0
0
Aunt Ezekieli Afunguka Kuhusu Ndoa yake na Baba Cookie
Aunt Ezekiel ni staa ambaye hivi sasa ana jina kubwa kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka 10 iliyopita.

Kama ulikuwa hufahamu, basi Aunt ni mtoto wa marehemu kiungo mahiri wa zamani wa Simba na Yanga, Ezekel Grayson ‘Jujuman’.

Ni binti fulani matata pindi ukimchokoza. Mfupi wastani mwenye shepu ya uchokozi na rangi nyeusi yenye mng’ao (kama bado hajajichubua.) Macho makubwa na mashavu ya kumwagika.

Kuna lingine pia, Aunt ameshawahi kushiriki shindano la Miss Tanzania. Kwa kifupi ni staa huyu amepitia mambo mengi magumu katika safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipo.

Ameshawahi kucheza baadhi ya filamu kama Mrembo Kikojozi, Miss Bongo, Yellow Banana, House Girl and House Boy, Nampenda mke Wangu, Usiku wa Maajabu na nyingine nyingi.

Staa huyu pia amewahi kuwa kwenye uhusiano mbalimbali na hata kufikia kufunga ndoa mara mbili.

Kwa sasa yuko kwenye uhusiano wa kimapenzi na dansa staa wa Bongo fleva Diamond, Moses Iyobo baada ya aliyekuwa mumewe, Sunday Demonte kutumikia kifungo kule Dubai.

Aunt na Iyobo wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Cookie.

Leo Aunt amepiga stori na Mwanaspoti na kuzungumza safari nzima ya maisha yake.

Hivi karibu Aunt alitoa filamu yake mpya baada ya kimya cha muda mrefu. Filamu hiyo inaitwa, Mama akiwa amemshirikisha mwanaye, Cookie.

“Cookie amecheza kama mhusika msaidizi katika filamu hiyo. Ni filamu ambayo imenigharimu Sh 12 milioni hadi inakamilika. Unajua mama ni muhimu katika maisha ya ndio maana nimeamua kutoa filamu hiyo.

“Binafsi sioni kitu kingine baada ya Mungu ni mama ndio anayefuatia,” Aunt anafunguka.

“Picha za filamu hiyo zimepigwa maeneo ya Kisarawe (Mkoa wa Pwani) na huko ndiko marehemu baba yangu alipokulia na nimeamua kufanyia kazi huko,” anaongeza.

Mwanaspoti lilimuuliza Aunt kwa nini soko la filamu limeshuka?

“Matendo machafu. Wasanii wa filamu ni sehemu ya watu waliochangia kushuka kwa soko la filamu nchini. “Inabidi tuwe wakweli tu ,maana hali ya sasa haifichiki kuhusu filamu. Kipindi hiki filamu zimepoteza mvuto na watu wamekuwa wakizungumza mengi ila ninachokiona ni matendo yetu machafu yanachangia.

“Mbona wasanii kama kina King Majuto bado wanafanya vizuri? Skendo zinayumbisha soko la filamu na siyo kitu kingine,” Aunt anafunguka.

Msanii huyo anafafanua skendo zinazotajwa zaidi kuwatikisa wasanii wa kike wa filamu ni kutoka na waumume wa watu.

Pia, kuolewa na kuachika pamoja na kubadilisha mabwana mara kwa mara.

Kwa upande wa wanaume kiki za kijinga, ulevi pamoja na kubadilisha wanawake.

“Hakuna kingine zaidi ya kuachana na skendo hizo za kijinga.”

Aunt anaamini bado filamu zina uhai ila kwa sasa zimedorora tu kwani Watanzania wanapenda filamu zao kuliko za nje ambazo haziwahusu kijamii wala kiutamaduni na nyingi hadi zitafasiriwe.

Kama kuna kitu ambacho Aunt hakipendi kukizungumzia ni kuhusu uhusiano wake na wanaume waliopita.

Lakini kitu ambacho watu wengi hawakifahamu Aunt aliwahi kufunga ndoa mara mbili na kuachana na ndoa hizo.

“Mwaka 2007 nilifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara maarufu, Jack Pemba, nilianza kuishi na Jack kama mke na mume huku akinisaidia katika mambo yangu ya sanaa.

“Baadaye alinizuia kwani alikuwa hapendi nitoke nyumbani na baada ya muda nilipata ujauzito kitu kilichomfurahisha sana na kunizawadia vito vya dhahabu vyenye uzito wa kilo moja.

“Lakini kwa bahati mbaya ilipofika miezi saba nilijifungua mtoto akafariki dunia,” anasema kwa majonzi.

“Ndoa ilikuwa nzuri, nilikuwa napata kila kitu nilichokitaka na kutembelea magari ya kifahari lakini kitu amba cho nilikish ind wa ni vipigo vikali nilivyokuwa nikivipata.

“Nakumbuka kuna siku alinipiga kiasi ambacho mashuka meupe yalikuwa kama yamepakwa rangi nyekundu. Bibi yangu alikuja kunichukua na nikaondoka moja kwa moja.”

“Baada ya kuondoka kwa Jack, nilianza kupigana katika maisha na niliingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine.

“Nikarudi kucheza filamu ambapo huko jina langu lilizidi kukua siku hadi siku, hivyo nikawa naendesha maisha yangu, mpaka nilipokutana na Sunday Demonte aliyekuwa anaishi Dubai.”

Baada ya kuwa na uhusiano wa muda na Demonte hatimaye Aunt na mwanaume huyo wakafunga ndoa.

Aunt alifunga ndoa ya Kiislamu na Demonte, Novemba 2012, ambapo alibadili dini na kuitwa Rahma.

“Unajua kazi yangu kipindi hicho ilikuwa ni uigizaji hapa Tanzania na kazi hiyo ndio ilikuwa kila kitu katika maisha yangu.

“Sasa watu walikuwa wanajiuliza mume Dubai miye Tanz ania, lakini nilikuwa nafanya kazi zangu kwa kutengeneza filamu kama tatu, kisha naenda Dubai kukaa na Sunday hata hivyo tulikuja kuachana,” anaeleza.

Aunt anasema mume wake alitiwa nguvuni na polisi wa Dubai akikabiliwa na makosa kadhaa, likiwemo la kuishi bila ya kuwa na kibali na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 mwaka 2014.

Lakini kwa sasa yuko uraiani tangu mwaka 2016 baada ya kuachiwa huru kwa msamaha maalumu unaotolewa kabla ya kuanza kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kila mwaka.

Aunt hataki kuingia kwa undani kuhusu ndoa yake hiyo kama alipewa talaka au la.

“Kila mmoja kwa sasa ana maisha yake. Miye nina yangu na Sunday ana yake full stop.”

KWANINI AMEDUMU NA IYOBO?

Mara nyingi uhusiano wa mastaa huwa unakuwa na drama nyingi sana na Aunt haikutarajiwa kama angeweza kuendesha maisha na Iyobo.

Awali, wengi walidai Aunt alikuwa akijificha tu kwa Iyobo lakini kulikuwa mwanaume mwingine aliyekuwa na uhusiano naye. Kadiri watu wanavyoamini kuwa uhusiano huo utakufa, Aunty na Iyobo kwa sasa wanakaribia kutimiza takribani miaka minne.

“Kikubwa ni kuzungumza na moyo wako. Je, umetua mahali sahihi? Unapata faraja unapokuwa hapo?

Mimi na Iyobo tunasikilizana na kuheshimiana na hatuleteani ustaa katika uhusiano wetu,” anasema Aunt.

Hata hivyo, staa huyo anasema katika mapenzi huwezi kuishi bila ya migongano kwani alishawahi kumfumania Iyobo na yeye alishawahi kubambwa na meseji kwenye simu yake ikionesha mtu alikuwa anampenda na yeye akampotezea.

ANA MPANGO WA KUOLEWA NA IYOBO?

“Mambo ya ndoa ni mwanaume ndiye anayeamua. Lakini pia kufunga ndoa ni makaratasi tu kikubwa ni jinsi gani unaishi na mwenzako na na maelewano kwa kiasi gani.

“Lakini kwenye suala la kuongeza mtoto niko tayari hata kesho,” anasema na kuachia tabasamu.

“Mara nyingi kazi zake ni za kusafiri na anakutana na watu mbalimbali, inasumbua sana mpaka kuna wakati huwa nahisi kutaka kushindwa.

“Lakini nikiangalia meseji anazotumiwa, nagundua wasichana wanampenda tu kwa sababu ni mtu fulani.”

“Unajua napenda sana mwanaume asiyekuwa na kero. asiyependa kuzungumza sana yaani kiufupi sipendi gubu,” anamaliza Aunty.

Aunt alizaliwa Dar es Salaam. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alimalizia darasa la saba katika Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Kisarawe, mkoani Pwani.

Lugola Awataka Wakimbizi Kurejea Kwao......Pia Katoa Maagizo Kuhusu Wafungwa Kujilisha, Simu Gerezani na Swala la Ajali Nchini

$
0
0

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametoa maagizo kadhaa kwa idara mbalimba zilizopo chini yake kuhakikisha wanayatekeleza kwa maslahi ya nchi.


Ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anatoa tathimini ya ziara yake aliyoifanya katika vyombo vya vyote vya ulinzi na usalama na idara zote za wizara hiyo.


Amefafanua katika ziara yake aliyoianza Julai 11 mwaka huu yako mambo ambayo ameyabaini na hivyo ameona haja ya kuyaeleza kwa mustakabali wa ustawi wa Taifa kwa ujumla.


“Miongoni mwa mambo ambayo nimeelekezwa na Rais Dk.John Magufuli ni kuhakikisha anasimamia suala la Magereza kujitosheleza kwa chakula.


“Hivyo nimeagiza Jeshi la Magereza nchini kuwasilisha mkakati madhubuti na unaotekelezeka wa kujitosheleza kwa chakula ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kulisha wafungwa,”amesema.


Akifafanua katika hilo amesema kuwa kama mkakati huo kutakuwa na kipengele kinachoweka vikwazo kwa wafungwa kutofanya kazi za kuzalisha basi katika Bunge la Septemba wataanza kwa kuweka kipengele ambacho kinaelekeza wafungwa kufanya shughuli za uzalishaji chakula.


“Mbona walioko majumbani wanalima kwa ajili ya kupata chakula kwanini waliko magerezani wasilime chakula kwa ajili yao na ikiwezekana kupata na ziada kwa ajili ya kulisha maeneo mengine,”amesema.


Wakati huo huo Lugola amesema ili kukomesha vitendo vya kuingiza vitu hatarishi magerezani ikiwemo simu za mkononi tayari ametoa maagizo kwa Kamishna Jenerali wa Magereza kusimamia kikamilifu nidhamu ya askari wake wenye wajibu mkubwa katika kukomesha vitendo hivyo vya kihalifu.


“Katika kikao changu na maofisa wa Magereza , nimezungumza na CGP kuwa gereza lolote ambalo linapatikana na matukio hayo Mkuu wa Gereza awatajibika.


Pia Waziri Lugola amesema katika utatuzi wa ajali za barabarani ambazo zimekuwa tatizo kubwa kwa kupoteza maisha ya Watanzania na kuacha majeruhi amesema tayari amevunja baraza la Taifa la Usalama barabarani na kamati zake za mikoa na wilaya ili kuanza upya.


“Kabla ya mwisho wa mwezi huu nitakuwa nimeshaunda baraza jipya.Aidha nimeagiza Jeshi la Polisi nchini kuongeza juhudi katika usimamizi wa Sheria ya usalama barabarani na ukaguzi wa magari ili kudhibiti ajali.


“Hatua kali zitachukuliwa kwa wote watakaobainika kutotii sheria za usalama barabarani na kuendesha magari mabovu yanayosababisha ajali na kusababisha vifo,”amesema.


Aidha amesema amesema kumekuwepo na kero ya muda mrefu ya askari na watumishi raia kutobalishiwa mishahara baada ya kupandishwa vyeo.


“Nimewaagiza wakuu wote wa vyombo vya ulinzi na usalama na idara zote ndani ya Wizara hii ifikapo mwisho wa Agosti kero zote ziwe zimetatuliwa na asiwepo askari wala raia ambaye analipwa mshahara tofauti na cheo chake au kutolipwa mashahara kabisa,”amesema.


Wakati huohuo Waziri Lugola amesema ametoa maagizo kwa Idara ya Huduma za Wakimbizi kuongeza kasi ya kurejesha wakimbizi wa Burundi kwani hali ya amani kwenye nchi hiyo imerejea.


Pia ametoa maagizo kuhakikisha wakimbizi wote wasioishi kambini warejeshwe kambini mara moja


Pia Waziri Lugola amesema kwa suala la usalama wa raia na mali zao ni jambo muhimu kwa Watanzania ambao wanahitaji kufanya kazi saa 24 ili kuendana na azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati.


Amesema tayari ametoa maelekezo kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini kuwalisha mkakati wa kuimarisha usalam ili watanzania waweze kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii kwa saa 24 wakiwa na uhakika na usalama wao na mali zao.


“Hatuwezi kupewa amri , maelekezo na ratiba za kazi zetu na wahalifu.Gari inatoka Kagera  na kasha inapita Mwanza eti ikifika Morogoro inaambiwa haitakiwi kusafiri usiku kwasababu ya kufohia usalama.Hii haiwezekani.Tutakaa na wadau wa usafiri ili nao utapate maoni yao na kasha tutaamua,”amesema.

Zahanati yateketea kwa moto, watano wadakwa akiwemo mtendaji

$
0
0

Watu watano akiwamo ofisa mtendaji wa kijiji cha Ulaya, wilayani Igunga mkoani Tabora,  Zablon Hussin wanashikiliwa polisi kwa mahojiano wakihusishwa na tukio la jengo la zahanati ya kijiji hicho kuungua moto. 

Jengo hilo liliungua moto usiku wa Julai 14, 2018 na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh85 milioni. 

Akizungumza na wanahabari leo Jumamosi Julai 21, 2018  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Emmanuel Nley amesema majina ya watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa yanahifadhiwa kuepuka kuharibu upelelezi. 

"Wakati moto huo unazuka, zahanati ile haikuwa na mlinzi na tayari tumetoa maelekezo kwa viongozi wa Serikali za mitaani kuhakikisha maeneo yote ya umma yanakuwa na ulinzi," amesema Kamanda Nley. 

Kaimu Mganga Mkuu wilaya ya Igunga, Dk Bonaventura Kalumbete amesema moto huo pia umeteketeza dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh25 milioni. 

Dk Kalumbete amesema juhudi zinaendelea kutafuta jengo jingine ili litumike kwa ajili ya huduma wakati mchakato wa ukarabati zahanati iliyoungua ukiendelea.

Kocha Yanga awataka viongozi wawaambie ukweli mashabiki

$
0
0

Wachezaji wote wa Yanga unaowajua wewe ambao usajili wao upo CAF jana Ijumaa waligoma kufanya mazoezi huku Kocha Mwinyi Zahera akiwasihi viongozi wawaambie mashabiki wa timu hiyo ukweli.

Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawajui. 

Wachezaji wote waliocheza mechi ya Gor Mahia hakuna hata mmoja aliyeonekana mazoezini na Zahera hakuwa na taarifa yoyote lakini Championi limejiridhisha kwamba wameambizana kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi mitatu na kushinikiza pia mashabiki wajitokeze kuokoa jahazi. 

Yanga Jumatano ya wiki hii ilipigwa mabao 4-0 na Gormahia kwenye mechi ya Shirikisho na timu hizo zitarudiana Dar es Salaam Ijumaa ijayo saa 1.00 usiku. 

SOMO: If you're Afraid to Lose Money NEVER INVEST, Baki na Hela zako.

$
0
0

Sikia....

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.
Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.

Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi amefilisika? No.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza.

Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.
Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Bora ukazinywee soda tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.

Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?

Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa. Kama haupo tayari kukosekana pesa basi kazinunulie nguo mpya sikukuu zikifika uvae.

Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU katika jamii huwa ni wachache tu.

If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upugufu wa Nguvu za Kiume, Busha, Kisukari na Vidonda vya Tumbo

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO? BUSHA BILA KUPASUA KISUKALI NA VIDONDA VYA TUMBO? asilimia kubwa ya wanaume wanaupungufu wa nguvu za kiume NA maumbile madogo NI NINI KINACHOSABABISHA UUME KUZIDI KUWA MDOGO NA WEMBAMBA 1 kuugua chango LA uzazi 2 unene kupita kiasi 3 kuvaa nguo au chupi za kubana 4 kupiga punyeto kwa mda mrfu ,NI NINI TIBA YAKE MAKAKANUA MIX nidawa ya mitishamba iliyochanganywa NA mizizi kumi NA mbili urfusha NA kunenepesha UUME saizi upendayo ich 5,6,7, NA 8 kwa urfu NA sentimita 3,4, na 5 ipo dawa ya kunywa na kupaka NI NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupungukiwa kwa homoni ya testerone 2 kuhudhurika kwa Neva au uti wa mgongo 3 utumiaji holela wa madawa ya kizungu 4 usongo wa mawazo na asira 5 utumiaji wa vyakula vya mafuta mengi NI NINI TIBA YAKE MAPRO POWER NO 2 NDIO tiba tosha kwa sasa kwani utibu matatizo matatu kwa pamoja 1 itakufanya uchelewe kufika kileleni dk 15 adi 20 ,2 itakufanya urudie tendo zaidi Mara tatu 3 uhimalisha uume uliolegea na kusinyaa OKOA NDOA YAKO SASA ujihepusha na lawama ndani ya ndoa yako au pale ukutanapo na mpezi dawa hii itamfanya mpenzi wako hakueshimu na hasitoke nnje ya ndoa na ata wazee wenye umri mkubwa wanapona zipo dawa za kupunguza kitambi,minyama uzembe, presha ,kisukar mvuto wa mpezi au biashara FIKA OFISINI KWETU MBAGALA ZAKHEMU na wateja wa kanda ya ziwa yupo wakala wetu mwanza mjini au piga simu 0752348593

DR MABULA na utaletewa popote ulipo uduma hizi

'Nabii' aliyeshindwa kumfufua mfu akamatwa na polisi Ethiopia

$
0
0
Maafisa wa polisi nchini Ethiopia wamemkamata kijana mmoja anayejiita 'nabii' kwa jina Getayawkal Ayele baada ya kushindwa kumfufua mfu aliyefariki siku nne zilizopita.

Tukio hilo lilifanyika katika mji wa Galilee huko Wollega magharibi mwa Ethiopia.

Kanda ya video ya 'nabii' huyo ikiita jina la mfu huyo kwa lengo la kumfufua ilisambazwa sana katika mtandao wa facebook.

Kanda hiyo ya video inaonyesha 'nabii' huyo akilala kando ya mwili huo na kuita jina la marehemu.

Kanisa linalotukuza unywaji pombe Afrika Kusini
Awali alikuwa amekwenda kwa familia ya mfu huyo kwa jina Belay Bifu na kuwahubiria kuhusu habari ya Lazurus, vile Yesu alivyomfufua, muhubiri kutoka mji wa Dhinsa Dabela aliambia BBC.

''Niliona watu wengi wakikimbia kuelekea kule kaburi hilo lilikokuwa wakisema Belay anakaribia kufufuka. Niliwashauri watu kutomuamini nabii huyo lakini walinifukuza wakisema sina imani'', muhubiri huyo alisema.

Nabii huyo baadaye aliwafanya watu kuchimba kaburi , na kuchukua kipande cha nguo kilichotumika kumfunga marehemu na kuanza kumwambia Belay amka tena na tena.


Baada ya majaribio kadhaa ambayo hayakufanikiwa nabiii huyo aliondoka katika kaburi hilo akisema haiwezekani.

Wanachama kadhaa wa familia walikuwa wagonjwa huku wengine karibia wazirai hapo hapo Dhinsa alisema.

Watu waliokuwa wakitazama kisa hicho walikasirika na kuanza kumpiga kabla ya polisi kuwasili na kumkamata.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo Tadese Amenu alithibitisha kwa BBC kwamba nabii huyo anazuiliwa na maafisa wa polisi.

Kulingana na kamanda huyo nabii huyo aliyegunduliwa kuwa mfanyikazi wa afisi ya idara ya afya na hakuwa mwanachama wa kanisa lolote.

Otile Brown Alalamika Baada ya Kushutumiwa Kutumia Uchawi Kumteka Mrembo Vera Sidika

$
0
0

- Otile Brown mwenye ghadhabu aliwakaripia wanawake wenye kijicho mitandaoni

- Mwimbaji huyo alilalamika kwamba alikuwa akishutumiwa dhidi ya kutumia uchawi kumweka Vera

- Aliropokwa cheche za maneno makali akiwaanika wanawake kwa kudai ilikuwa jambo lisilowezekana kwa Vera kumpenda mtu wa kawaida Unapomchumbia sosholaiti, ni sharti uwe tayari kukumbana na kila aina ya matokeo yanayoambatana na kitendo hicho, na Otile Brown anajifunza taratibu faida na hasara ya kuwa mpenziwe wa kuhusudiwa Vera Sidika.

Uhusiano huo usiotarajiwa kabisa yamkini unanawiri kila uchao lakini hili halijawakomesha wakosoaji kupima mapenzi haya kuhusu ni jinsi gani mwanamziki kutoka kijiji kidogo pwani angeweza kumnyakua mwanamke aliye mfano mwafaka Kenya wa umbo kamilifu.

Hapo awali, ni Otile Brown aliyenyeshewa na maoni ya husuda ambayo yalipakiwa kama huruma kutoka kwa mashabiki na hata watu maarufu, huku wakidai alikuwa amepotea njia kwa kuamua kujaribu mambo na mwanamke ambaye sifa yake ilimsaliti kabisa. 

Otile hakufa moyo na akaendelea na ndoto zake za kuwa mpenzi ikiwemo kutoa kibao kwa jina huku akijitahidi kumwonyesha sosholaiti huyo alimaanisha mambo.

Maadamu yamkini msimamo wa Otile hautatikiswa na aina yoyote ya shutma, yaonekana sasa mahasidi wamebadili na nakala na sasa wanahisi ni Vera anayeelekea kuvunjika moyo mno hatimaye.
Otile aliyepandwa na ghadhabu alijitosa katika mtandao wa kijamii katika hatua isiyotarajiwa kulalamikia jumbe ambazo amekuwa akipo 

Otile, ambaye kwa kawaida huwa jasiri mno mitandaoni, aliwasuta wanawake ambao alidai wamekuwa wakisema aligeukia uchawi ili kuhakikisha Vera mwenye umbo la kudondosha mate hakumponyoka. Katika malamishi hayo  mahasidi wa Otile, ambao kwa namna ya kushangaza ni wanawake,wanadai mwanamme wa hadhi yake kifedha hangemudu kumweka Vera kupitia tu vitendo vya mapenzi na maneno matamu.

“Hivyo wasichana wamekuwa wakimtumia mpenzi wangu jumbe wakisema amefeli vibaya kwa kunipenda. Sisi husoma tu hizo jumbe pamoja (na Vera) na kucheka. Hivyo mmoja alinitumia ujumbe na ukanikwaza kwa sababu ulisema nilikuwa natumia hirizi kwake na hakuna vile Vera angempenda mwanamme wa kawaida kama mimi,” kilisema kijisehemu cha ujumbe wake.  

 "Kwa vile tu mwanamme hana hela za kununua mwilio wako haimaanishi ni mjinga. Ni werevu mno kukushinda. Sina muda wa kukuthibitishia chochote. Ikiwa ni sharti ujinadi ili ujenge himaya sitowahi kamwe kukuhukumu hadi utakapoanza kuwavunjia watu heshima,” alisema.  

Download Hapa Application ya Udaku Special Kwenye Simu Yako Kushuhudia Vimbwanga Mtaani na Stori za Mapenzi

$
0
0
Usipitwe na Habari zetu za Mapenzi na Udaku,kuzisoma kirahisi kupitia Application ya Udaku Special ambayo ipo Play Store kwa watumiaji wa Simu za Android

Bonyeza Hapa Chini Kuinstall/Kudownload :




Note: Kama unayo tayari huna haja ya kudownload tena


Serikali Yatengua Katazo la Wananchi Kuzuiwa Kupanda Meli

$
0
0

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Atashasta Nditiye ametengua katazo la wananchi kuzuiwa kupanda meli ya serikali hadi wawe na vitambulisho vya uraia au cha mpiga kura jijini Mwanza.

Nditiye amesema kuwa utaratibu wa awali uendelee kutumika hadi pale watakapo kaa upya kujadili ni njia ipi sahihi itakayoweza kuwawezesha wananchi kupata huduma ya usafiri bila kikwazo.

Nditiye ameongeza kuwa suala hilo lilitokana na kutokuwa na maelewano mazuri baina ya Shirika la Meli pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama jijini humo.

“Wananchi wanamatatizo mengi, unapoanza kumchanganya na mambo ya vitambulisho tena unakuwa unawavuruga naomba utaratibu wa awali utumike na tuangalie utaratibu mwingine hapo baadaye”, amesema Nditiye.

Mamia ya abiria waliotakiwa kusafiri kwa meli ya Mv.Nyehunge kutoka jijini Mwanza kuelekea wilayani Ukerewe wamekwama kwa siku nne katika bandari ya Mwaloni Kirumba jijini humo baada ya kushindwa kutekeleza sharti linalomtaka kila msafiri kuwa na kitambulisho rasmi cha uraia au kupigia kura.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 22

$
0
0



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 22

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME DR SITTA NDO SULULISHO LAKO tatiza, hili limekuwa likiwaasili watu wengi,sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine, kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo zipo , sababu nyingi zinazosababisha, tatizo hilo baadhi ni (i) upungufu wa vichocheo vya HORMONES ZA CETROGEN ambazo mwanaume, anapobarehe vichocheo hivi, HORMONES hizo, husaidia ukuaji wa uume

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mlija iliysinyaa,

NSHOLA ni dawa bora, ya kurudisha nguvu, za, kiume bari inatibu ,kabisa kutoa tatizo hilo, na kukupa , hamu ya , kurudia tendo, la ndoa zaidi, ya mala nne 4 ,bila kuchoka atakama unaumli ,wa mika 80,! pia ana ,dawa za ,kutibu, presha ya kupanda ,na kushuka, kisukari kuondoa, mafuta , mwilini ,na maumivu ya, mgogo kiuno, dawa zipo, matazo, ya hedhi, kwa ,wanawake hedhi, zisizokuwa na, mpangilio, na kasonono, pia , vidonda ,vya, tumbo ,(STOMACHI UCLENS) IHUSHI ndoji lako.

NKANYA ni dwa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi ariyekuacha, mke mme, atakuludia kwa, mda, wa msaa3 tu , ukishaitumia atarudi ,mwenyewe bila ,ugovi tena, NKOMA ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada .

HERBON, ni, dawa, ya kuongeza, CD4, NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu ,miguu, kufaganzi, na ,kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! DR SITTA, amebobea, kwa tiba asilia

DAR ANAPATIKANA MBAGALA, ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI SHINYANGA, KAHAMA MJINI, KWA MAELEZO ZAIDI ,

PIGA SIMU 0763172670 au 0715172670

Hii ndo Simba Bwana! Yafikia Hoteri ya Kifahari Uturuki

$
0
0
Hii ndo Simba Bwana! Yafikia Hoteri ya Kifahari Uturuki
JUMLA ya wachezaji 26 wa kikosi cha Simba, wanatarajiwa kuondoka kesho Alfajiri kuelekea Uturuki kuweka kambi ya takribani wiki mbili kabla ya kurejea hapa nchini Agosti 5, mwaka huu.

Wachezaji wa Simba ambao watakuwa kwenye safari hiyo jana Ijumaa walikuwa na zoezi la upimwaji wa afya kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar. Katika nyota hao 26 watakaosafiri, kiungo mkongwe, Mwinyi Kazimoto, hatakuwepo kwenye msafara huo ambao utaongozwa na kocha mpya wa kikosi hicho, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji. Msafara mzima wa Simba unaotarajiwa kwenda Uturuki kwenye kambi hiyo, utakuwa na jumla ya watu 35.



Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Simba, kimelidokeza Championi kuwa, mbali na Kazimoto, pia Mosses Kitandu, Jamal Mwambeleko, Ally Shomary na Said Mohammed ‘Nduda’ nao watabaki hapa nchini.



“Kama ambavyo imepangwa, kikosi kitaondoka Jumapili alfajiri ambapo baada ya kocha mpya kutangazwa jana (juzi Alhamisi), yeye ndiye atakuwa anawaongoza vijana wake hao sambamba na msaidizi wake, Masoud Djuma.

“Lakini kabla ya kikosi hakijaondoka, kocha atatambulishwa mbele ya wachezaji wote,” kilisema chanzo hicho.



KUFIKIA KAMBI YA KISHUA

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Umoja wa Utalii wa Michezo wa Uturuki, Samil Yasacan sehemu inapokwenda kuweka kambi Simba wikiendi hii mwaka jana zilifurika timu za soka 1500 kutoka dunia nzima.



Antalya ni mji maarufu wa kitalii ulioko umbali wa saa moja na dakika 15 kwa ndege kutoka mji mkuu wa Uturuki, Istanbul. Umbali kutoka Dar es Salaam mpaka Istanbul ni kilomita 5420 kwa ndege sawa na saa 7. Ambako huko kunasifika kwa kuwa na hoteli zenye hadhi ya juu ‘kishua’ na Simba itafikia kwenye moja kati ya hoteli hizo.

Sasa Ninja Nimeingia Mawaziri Wote Waliopita Hawakuwa Maninja- Lugola

$
0
0
Waziri wa mambo ya ndani Kagi Lugola amesema kuwa mawaziri wote wa mambo ya ndani waliopita hawakuwa maninja na sasa ameingia Ninja ambaye ndio yeye.



Maneno hayo ameyaongea katika mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam wakati akitoa Tathimini ya ziara zake alizozifanya kuanzia Julai 11 2018 katika miongoni mwa taasisi zilizochini ya wizara yake ya Mambo ya ndani.

Wakari anaongea ameweza kuongea mambo kibao likiwemo la kumuagiza mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Vitambulisho vya taifa (NIDA) Andrew Massawe kufika ofisini kwake katika ofisi zake za Dodoma, afike pamoja na mtambo wa kutengenezea Vitambulisho vya taifa.



Lakini pia Waziri Lugola ameweza kutoa tamko la kumwagiza mkuu wa polisi nchini Saimon Siro kumpeleka Lugumi ofisini kwake Mnamo Julai 31 mwaka huu Jijini Dodoma haraka iwezekanavyo.



Waziri Lugola ameongeza kuwa angependa kuona Lugumi anafika ofisini kwake asubuhi pale anaposikia habari hizi “Ntapenda kuona anafika ofisini kwangu agonge mlango ninaposema karibu nikifungua mlango nimkute ni yeye sio lazima mpaka afuatwe na polisi kwa Lugumi ana  familia na anaishi Tanzania”

Rais Magufuli Amemteua Eliud Sanga Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF

$
0
0
Rais Magufuli Amemteua Eliud Sanga Kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF
Leo July 22, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Eliud Sanga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund – PSSSF).



Kabla ya Uteuzi huo Sanga alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pension wa LAPF. Uteuzi wake umeanza rasmi July 21, 2018.

'Nabii' Aliyeshindwa Kumfufua Mfu Akamatwa na Polisi

$
0
0
Maafisa wa polisi nchini Ethiopia wamemkamata kijana mmoja anayejiita 'nabii' kwa jina Getayawkal Ayele baada ya kushindwa kumfufua mfu aliyefariki siku nne zilizopita.

Tukio hilo lilifanyika katika mji wa Galilee huko Wollega magharibi mwa Ethiopia.

Kanda ya video ya 'nabii' huyo ikiita jina la mfu huyo kwa lengo la kumfufua ilisambazwa sana katika mtandao wa facebook.

Kanda hiyo ya video inaonyesha 'nabii' huyo akilala kando ya mwili huo na kuita jina la marehemu.


Awali alikuwa amekwenda kwa familia ya mfu huyo kwa jina Belay Bifu na kuwahubiria kuhusu habari ya Lazurus, vile Yesu alivyomfufua, muhubiri kutoka mji wa Dhinsa Dabela aliambia BBC.

''Niliona watu wengi wakikimbia kuelekea kule kaburi hilo lilikokuwa wakisema Belay anakaribia kufufuka. Niliwashauri watu kutomuamini nabii huyo lakini walinifukuza wakisema sina imani'', muhubiri huyo alisema.

Nabii huyo baadaye aliwafanya watu kuchimba kaburi , na kuchukua kipande cha nguo kilichotumika kumfunga marehemu na kuanza kumwambia Belay amka tena na tena.

Wanandoa Maarufu Kusoma Taarifa ya Habari Pamoja Kila Jmosi

$
0
0
Wanandoa Maarufu  Kusoma Taarifa ya Habari Pamoja Kila Jmosi
Chombo cha habari cha Citizen nchini Kenya kimewatangaza wanandoa maarufu, Rashid Abdalla na mkewe Lulu Hassan kuanza kusoma taarifa ya habari wakiwa pamoja kila ifikao siku ya Jumamosi na Jumapili.

Rashid ambaye ni mume wa mwana dada Lulu alikuwa mtangazaji wa kituo cha NTV kabla ya kujiunga na Citizen ambapo amekabidhiwa majukumu hayo mapya akiwa sanjari na mkewe kwenye kipindi cha Nipashe Wikendi kinachoruka hewani kila Jumamosi na Jumapili kuanzia tarehe 21 mwezi Julai 2018.

Tukio hili la wanandoa kusoma habari wakiwa pamoja ni kwa mara ya kwanza linatokea nchini Kenya. Rashid Abdalla anachukua nafasi ya Kanze Dena ambaye aliajiriwa na Ikulu ya rais kuwa msemaji mnamo mwezi Juni.

Wakenya wengi wakisubiri kuona ikiwa wapenzi hao wataweza kufanya kazi kwenye osifi moja, huku uongozi wa Nipashe Wikendi wakithibitisha wawili hao kuanza kufanya kazi pamoja Julai 22, 2018.

Soma Nafasi za Ajira Zilizotangazwa

$
0
0

Kiongozi Mwingine Mkubwa Yanga Aachia Ngazi

$
0
0
Hali ya klabu ya Yanga imeendelea kuwa si shwari ambapo taarifa zinaelezwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Khalfan Hamis ametangaza kujiuzulu wadhifa wake.

Taarifa inaeleza Hamis ameamua kuandika barua kwenda kwa Kaimu Mwenyekiti wa klabu, Clement Sanga akiomba kuachia ngazi kutokana na viongozi wa klabu hiyo kushindwa kufanya mambo kwa ueledi.

Barua hiyo imeeleza kuwa Yanga imekuwa na viongozi ambao wamekuwa hawaweki mambo sawa na badala yake kumekuwa na kificho bila kuweka kila kitu wazi kwa faida ya klabu.

Aidha imeelezwa kukosa ueledi kwa baadhi ya viongozi ni moja ya sababu tajwa ambazo zimeelezwa katika zilizoandikwa kwenye barua hiyo.

Sababu hizo ndizo zimepelekea kwa Hamis kuamua kuandika barua hiyo ya kuomba kujizulu ili kuwapa nafasi wengine.

Kuondoka kwa Hamis kumekuja baada ya siku kadhaa zilizopita kuelezwa kuwa Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa naye ameachia wadhifa huo ndani ya Yanga.
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images