Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live

Video:Mtanzame Idris Mshindi wa Big Brother Africa Akijibu Maswali ya Mashabiki wa Africa

$
0
0

Mtanzame Idris Mshindi wa Big Brother Africa Akijibu Maswali ya Mashabiki wa Africa 
Ameulizwa ni jinsi gani atazitumia Mil 500, Pia ameulizwa ni msichana gani kutoka Big Brother angependelea kuendeleza nae mahusiano..Mtazame hapa chini:


Shilole akanusha kupelekwa Ubelgiji na ‘Pedeshee’

$
0
0
Shilole amekanusha tetesi zilizoandikwa kwenye magazeti ya udaku kuwa hakwenda nchini Ubelgiji kutumbuiza, bali alipelekwa na mwanaume.

Shilole ameiambia Bongo5 kuwa anashangazwa mno na tabia ya wabongo ya kuzusha mambo yasiyo na kichwa wala miguu.

“Mimi wabongo nimeshawazoea kabisa hawaniumizi kichwa kwa sababu mimi nilienda kufanya kazi yangu halafu nina uhakika na kazi yangu,” amesema Shisi Baby mwenye uhusiano wa kimapenzi na Nuh Mziwanda.

“Mtu mwingine anasema sikwenda kwenye kazi sijui nilienda kwa mabwana! Japokuwa vitu hivyo vinawezekana lakini sio kwa mimi. Wasanii tunajiheshimu sana labda watu wengine na sio msanii kama mimi. Wangekuwa wanafuatilia kazi zangu zinazoonekana tu lakini sio kuongea tu. Sometimes jealous na wanaweza kuongea kitu hata bila uhakika kwa mimi nimeshawazoea.”

Kuhusu ngoma mpya, Shishi amesema: Kuna kazi nilifanya na Abdul Kiba ila nimesikia imevuja lakini sio ishu itakuwa Abdul Kiba ndo kaivujisha. Lakini haitanizuia kuachia ngoma, nitaachia ngoma mpya kabla mwaka haujaisha.”

Ikulu: JK hatawaadhibu vigogo wa escrow bila ya uchunguzi

$
0
0
Ikulu imesema pamoja na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekwishapokea maazimio ya Bunge kuhusu wanaotuhumiwa kuchota Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, hawezi kuwachukulia hatua mpaka hapo uchunguzi kuhusu suala hilo utakapokamilika.

“Rais lazima aagize vyombo vya uchunguzi kufanya kazi yake na baada ya hapo ndipo atapata mahali pa kuanzia. Watu wengi walitaka Rais Kikwete achukue hatua baada ya kupewa maazimio ya Bunge. Jambo hilo haliwezekani,” Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alisema jana na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa na makosa ya kimaadili au jinai baada ya uchunguzi.

Alisema uchunguzi kuhusu uchotwaji wa mabilioni hayo uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) pia utazingatiwa na Rais katika kutoa uamuzi.

“Maazimio ya Bunge ni mazuri ila inatakiwa muda kwanza ili Rais naye apate taarifa za uchunguzi zaidi. Maazimio hayo ni muhimu na si ya kupuuzwa hata kidogo,” alisema.

Alisema vyombo vinavyofanya uchunguzi kuhusu suala hilo ni vile ambavyo vilitajwa kufanya hivyo katika maazimio manane ya Bunge.

Bavicha wamtaka Kikwete achukue hatua

Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuacha kuhamisha wakuu wa mikoa na badala yake atoe uamuzi wa kuwashughulisha watuhumiwa wote waliohusika na kashfa ya escrow.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Bavicha, Mwita Julius alisema: “Wakati huu si mzuri wa kuanza kuhamisha wakuu wa mikoa kwa kuwa ni gharama, ni muda wa kuwachukulia hatua wahusika wote waliotajwa bungeni wakihusika na sakata la escrow.”

Alisema Rais anatakiwa kuwashughulikia wateule wake wote waliotajwa bungeni kwani wananchi wanasubiri kuona mabadiliko hayo kwa haraka.

Juzi, Rais Kikwete aliteua mkuu mmoja wa mkoa na kuwahamisha wengine sita.

Lulu Michael Ainadi Miguu Yake Mtandaoni..Soma Alichoandika Kuhusu Miguu Hiyo

$
0
0
“Nishawahi kusema naipenda miguu yangu!????
Wallah Naipenda kwa Moyo mmoja ,oky naendelea kuoga hela..kuoga Maji mwisho Dar Es Salaaam...kwa kina Mutashobya(BUKOBA) ni kuoga Hela tu...!oky bye” Lulu alimaliza.

Shilole Feki Aibuka na Kuchafua Hali ya Hewa Mtandaoni Kwa Kuandika Kingereza Kibovu

$
0
0
Lile wimbi la watu kutumia majina ya mastaa kwenye mitandao ya kijamii likiwa bado linaendelea  kwa kasi. Bongo movies imekutana  huyu anejiita SHILOLE CLASIC.

Akijifanya kuwa yeye ni  Shilole, ambae mwigizaji na mwanamziki maarufu hapa Bongo. Hebu tusaidiane kusoma hii NGELI alioitoa hapa.



Baada ya taarifa hizi kumfikia Shilole mwenye hiki ndicho alichokisema.

Nimetumiwa hii pic na kaka yangu  dully sykes kuhusu hii account fake ya Facebook na najisikia vibaya coz si Mimi na kama unatumia jina langu kama shabiki yangu sawa ila usiandike habari za uongo na zisizoeleweka .ila Nina fanpage tu ya Facebook inayoitwa shilole kiuno na nna account twitter pia inaitwa shilolekiuno.so msidanganyike nje ya majina hayo.nawapenda Sana na tusaidiane kuwaambia na wengine.”

Jamani tubadilike na tuitumie vizuri mitandao hii ya kijamii.Bongo movies.com inakemea tabia hii kwani ina athari kubwa kwa msanii na jamii kwa ujumla.

Mastaa wa Bongo Wamejaa Zambi na Kutumia Muda Mwingi Kupiga Majungu

$
0
0
WAKATI tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka 2014, msanii wa filamu Ruth Suka ‘Mainda’, amedai kuwa hakuna jambo ambalo mastaa wa Bongo wamelifanya zaidi ya kuchuma dhambi na kutumia muda mwingi kupigana majungu kuliko kumcha Mungu kwa matendo mema.

Akizungumza na gazeti la Uwazi, Mainda alisema kuwa ndani ya tasnia ya filamu bado mambo ni magumu kwani mastaa wengi wamekuwa nyuma na matendo ya Mungu kwa kufanya anasa kila kukicha huku wengine wakizidi kuchafuana kwa kupigana majungu.

Ni kweli mwaka umeisha lakini lazima tujue wapi tumekosea, lakini wasanii wetu hawana roho ya kuamini kuwa Mungu yupo ndiyo maana wanapigana majungu kila kukicha.

Tangu kifo cha kipenzi Kanumba kutokea nilisemwa sana na baadhi ya wasanii wakidai kuwa siwezi kuwika tena lakini wanasahau kuwa niko bize na kazi ya Mungu na si kupiga majungu au kukaa kijiweni kumsema mtu,” alisema Mainda.


KAZI MPYA:Wema Atua Nchini Ghana Kufanya Kazi na Van Vicker

$
0
0
Aliekuwa Miss Tanzania (2006), Mwigizaji na mkurugenzi wa kampuni ya  Endless Fame, inayojishughurisha na mambo ya filamu hapa nchini, Wema Sepetu aka Madame hivi sasa yupo nchini Ghana kwaajili ya kufanya kazi na msanii maarufu nchini humo na Afrika kwa ujumla aitwaye van vicker.

Leo hii kwenye mtandao wa kijamii Wema aliweka picha hiyo akiwa na msanii huyo na kuandika “In the Making” na kumtag Van.

Jina la project (MOVIE) hiyo mpya hadi sasa bado halijajulikana. Endelea kutufuatilia hapa tutakujuza.

ILA KWA SASA TUACHE PROJECT IENDELEE

Hauwezi Amini Mpunga Alioupata Mshindi wa Pili wa Big Brother Africa Kutoka Kwa Bilionea wa Kinigeria

$
0
0
Tajiri mmoja nchini nigeria aitwaye Ayiri Emani amempa tayo ambaye ni mshindi wa pili wa shindano la big brother africa hotshots dola za kimarekani laki 3 na nusu kiasi ambacho ni zaidi ya pesa aliyopewa mshindi wa shindano hilo Mtanzania Idris sultani aliyepata dola za kimarekani laki 3 kamili...Hiyo Imekuja Baada ya Wanageria Wengi Kulalamika Baada ya Tayo Kushindwa Kuchukua nafasi ya kwanza na wengine kusema Idris Alipendelewa

Aneth Kushaba Maneja wa Skylight Band Nusura Kupigwa Risasi

$
0
0
Kwenye XXL ya leo Gossip Cop ametoboa kuhusu Meneja wa Skylight Band  kutishiwa kupigwa Bastola.
Baada ya Soudy kumtafuta Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba amesema ni kweli walitishiwa bastola na Promota ambaye aliwatapeli hela baada ya kufanya naye makubaliano ya kufanya naye show kwa makubaliano kulipwa hela siku moja kabla ya show kama mkataba unavyosema lakini promota huyo hakutimiza.
Siku ya show walikubaliana kwamba Skylight wapate mtu mmoja ambaye atakuwa akipokea kiingilio lakini baadaye waliamua kumfuata promota huyo ili awaongezee pesa za malipo ya show hiyo lakini aligoma kuwapatia malipo hayo na kumtishia kumpiga risasi Meneja huyo wa Skylight huku akimtukana.
Nimekuwekea hapa unaweza kubonyeza play kuisikiliza

Team Wema Sepetu Yapata cha Kujisifia ..Wema Aanza Kufanya Projects Kubwa Kubwa Nje ya Nchi

$
0
0
Makundi ya mashabiki mitandaoni maarufu kama TEAMS yamekuwa ni sehemu ya maisha ya mtandaoni ya wasanii na watu maarufu wengi hapa nchini. Linapokuja swala ya ushabiki na mada nzito team hizi  huvutana kwa kutupiana maneno na wakati mwingine hadi maneno makali.
Siku za hivi karibuni baada ya mwigizaji Wema Sepetu alipoachana na mpenzi wake Diamond Platnum, na badaye Diamond kuamua kutoka na mwanamama Zari kutoka nchini Uganda, Mashabiki (TEAM) wa Diamond na wale wanaomponda Wema Sepetu wamekuwa kwakiasi kikubwa wakiwatupia maneno na vijembe wale mashabiki wa Wema (TEAM WEMA), kwa picha na maneno.kiasi ambacho TEAM WEMA kuonekana kama” LOSSERS”.

Lakini leo hii upepo umebadilika huko mitandaoni na  TEAM WEMA wanaonekana kuwa na nguvu zaidi, baada ya mwigizaji Wema Sepetu kuachia baadhi ya picha akiwa nchini Ghana akifanya  kazi na Van vicker ambae ni msanii mkubwa hapa Afrika.

Team Wema wamepongeza sana juhudi za mwigizaji huyo kutaka kuivusha tasnia ya filamu hapa nchini na kuipeleka kimataifa hivyo wanataka Le Projectii iemdelee
Bongomovies pia inampongeza na kunampa moyo  katika juhudi zake hizi za kukuza tasnia yetu.Hiyo ni moja ya picha za project hiyo mpya

Mabomu Yarindima Tanzania Siku ya Uhuru, Barabara Zafungwa na Matairi Kuchomwa na Wananchi

$
0
0
Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  wananchi wa dumila na  mbigiri wilayani kilosa mkoani Morogoro  baada ya kufunga barabara ya Morogoro Dodoma kwa kutumia mawe na kuchoma matairi barabarani katika eneo la dumila na  kusababisha abiria wanaotumia barabara ya Morogoro Dodoma kukosa mawasiliano kwa zaidi ya masaa sita.


ITV imeshuhudia wananchi hao wakifunga barabara kwa mawe na matairi huku wengine wakionekana na mapanga ambapo wamesema wanalalamikia viongozi wa serikali ya kuanzia ngazi ya kijiji hadi wilaya kufumbia macho mgogoro wa ardhi na kushindwa kuwachukulia hatua wafugaji wanaowazuia wakulima wasilime katika eneo la mbigiri.

Vurugu hizo zilidumu kwa muda mrefu na juhudi za kudhibiti wakulima hao zimechukua muda baada ya askari wachache wakituo cha dumila kuonekana kuzidiwa nguvu ambapo baadhi ya wakulima wengine  wameonekana wakivamia wakuvunja nyumba za wageni zinazomilikiwa na wafugaji na kupora magodoro na vitu mbalimbali ambapo baadae  vikosi vya jeshi la polisi viliongezwa na kufanikiwa kudhibiti  baadhi ya watuhumiwa na kufungua barabara.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Lenard Paul amesema chanzo cha vurugu hizo ni wazee zaidi ya kumi walizuiwa kulima katika mashamba yao mbigiri ambapo walipelekeka malalamiko yao kwa afisa tarafa ambapo wakiwa ofisini kundi la vijana walifika na kufunga ofisi wazee hao pamoja na afisa tarafa hadi walipofika na kukolewa na jeshi la polisi na katika tukio hilo watu 20 wanashikiliwa  na jeshi la polisi.

Afisa tarafa na wazee walifungiwa ndani wakizungumzia tukio hilo wamesema kunamgogoro wa siku nyingi kati ya wakulima na wafugaji na upo katika ngazi za juu huku wakieleza kusikitishwa na hatua za kufunga barabara na kuomba serikali kuingilia kati kutatua mgogoro wa ardhi uliopo.
 - See more at: http://mambomsetohuru.blogspot.com/2014/12/breaking-newsss-mabomu-yarindima.html#sthash.uBahkJ8X.dpuf

Mwigizaji Amanda Poshi Anaswa na Kibabu cha Kizungu

$
0
0
Stori: Gladness Mallya

MSANII nyota wa filamu Tanzania, Tamrina Poshi maarufu kama Amanda, amenaswa katika picha akiwa na mzungu anayeonekana kumzidi umri ambaye unaweza kumwita kijeba aliyemtambulisha kama rafiki yake.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema, picha hizo ziliibwa katika simu ya msanii huyo na mtu asiyefahamika, ambaye kwa lengo lisiloeleweka, alianza kuzitawanya kwa watu mbalimbali.

Inadaiwa kuwa Amanda amekuwa akionekana sehemu tofautitofauti jijini Dar akiwa na mzungu huyo ambaye anasemekana kuwa na makazi yake maeneo ya Masaki.Amanda alionekana kushtushwa baada ya kuulizwa kuhusu kuwepo kwa picha hizo na kukiri kuwa ni kweli mtu huyo anafahamiana naye.

“Duh! hizo picha zimefikaje kwenu? Jamani haya ni maisha yangu binafsi naombeni mniache na huyo jamaa ni rafiki yangu sana, kwanza siyo mtanzania ni raia wa Uturuki,” alisema muigizaji huyo.

Drake: Sijawahi kutembea na Karrueche, kwanza sio type yangu

$
0
0
Drake amemmind Chris Brown kwa kumtaja kama sababu ya kuachana kwake na Karrueche Tran.

Chris aliandika kwenye Instagram kuwa mpenzi wake huyo aliwahi kufunga safari kibao za Toronto kwenda kuonana na Drake. Hata hivyo ameomba radhi tayari.

Kauli hiyo ya Brown imeibua tena beef iliyokuwa imeisha kati yake na Drake.

Vyanzo vilivyo karibu na Drake, vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa hakuna ukweli kuhusiana na kauli hiyo na Drake anadai kuwa Karrueche si aina ya wanawake anaopenda.

Drake amesema msichana pekee wa Chris ambaye ni type yake ni Rihanna.

Drake amekubali aliwahi kukutana na Karrueche huko Toronto lakini kwasababu tu alikuwa ni rafiki wa msichana anayefahamiana naye.

Napenda na Kupendwa na Wanawake Wenzangu Kimapenzi

$
0
0
Naomba ushauri: Wengi wanadhani nimependa kuwa hivi au tunaopenda wenzetu wa jinsia moja tumetaka.La hasha!!!Mimi ni mrembo sana,kuanzia sura, umbo, nina akili lakini pia nimekuzwa familia ya dini sana. Nikiwa sekondari form 2 nilitokea kumpenda sana dada mmoja yeye alikuwa Advance. Alinipenda sana pia ,ila kuliishia kukumbatiana tu. 

Nikiwa Advance nilipendwa na binti mmoja,niliogopa sana maana alikuwa ananipa care kupita kiasi.Uhusiano ulifika mbali zaidi mpaka nikawa mtumwa wa mapenzi.Sikuweza kula wala kufanya chochote bila yeye.Nilikuja kugundua alianza uhusiano mpya hivyo tukaachana soon nilipomaliza A level.

Nikiwa chuo nilipata boyfriend kwa mara ya kwanza.Nilijaribu sana kuwa nae karibu maana alinipenda sana na alinipa kila kitu.Sikuwa najisikia mapenzi hata kidogo.Wengi waliniona nina bahati maana alikuwa mzuri sana, mchapa kazi na ana akili zaidi ila tu hajatulia. 

Nililigundua hilo nikiwa ndani ya uhusiano. Japo kila nikimkamata anasema wanawake ndio wanamtaka ila hana time nao. Pamoja na yote kwa kweli alinipenda. Maombi yangu kwa Mungu yalikuwa na mm niweze kuwa in love na mwanaume. Niliomba sana na kufunga.Nilijitenga na wanawake. Nilipomaliza chuo niligundua jamaa alikuwa bado hajatulia tukaachana japo mwenyewe mapenzi hayakuwa kihivyo. Mara nyingi nilikuwa namkumbuka my x,nilikuwa mnyonge sana. 
Nilijihisi kwa huyo bf mimi nilikuwa kama sex mashine. Nilikuwa mwaminifu sana ndani ya mahusiano.Baadae tukaachana, mm nikaamua kumdate mke wa mtu.Alinipenda mwenyewe. Sikuwahi kumwambia chochote juu yangu.Ila kila wakati aliniita mpenzi,honey darlin na kunikiss kila mara.Tulifall in love. Ila nilijilaumu kwa kuwa sikutamani niwe na mwanamke tena ila sasa uhusiano na wanaume ulikuwa mgumu ,napendwa ila kupenda hakukuwepo. Nikaona nitavunja ndoa ya watu nikawa namkimbia. Nikajikuta nafall tena kwa mke wa mtu ambae alikuwa rafiki yangu.
Kila wakati aliniletea zawadi na kuniambia ananifeel sana. Tulidate kwa muda kidogo nikaanza kumkwepa maana alianza kumchukia mumewe.Akiamka break ya kwanza kwangu. Ananipeleka hoteli za kifahari .Ila pia alikuwa kanizidi sana umri. Nilipata shida sana kujitoa kwenye penzi lake maana aliapa kuniua nikimuacha. Alinipenda kiasi cha kujitoa ufaham.Nilifanikiwa kumkwepa karibia miezi 8 hv.Namba ya simu nikabadili.Tangu wakati huo naendelea kupata shida maana nimekuwa heart breaker.
Nikiumizwa tu na boyfriend kidogo huwa sirudi tena. Nasali sana hii hali iniondoke lakini wapi. Naumia sana, Sijui nifanyeje.

Najua ni kinyume cha jamii na pia dini.Ila mimi sipendi pia hali hii. Mimi sio tom boy na hata mtu akiniona hawezi kudhani.Nimejikuta napendwa na wanawake wengi ,sijui kwa nini pia,huwa sijawahi kumtongoza mwanamke yeyote ila wao hunianza. Ninapokuwa na mwanamke kwenye mahusiano nasikia raha na moyo unarelax.Nifanyeje???

By Jemi

Mwigizaji Mlela Azipangua Tuhuma Zilizozagaa Kitaa Kuwa Anatumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
Stori: Gladness Mallya

MSANII anayefanya vizuri katika filamu Bongo, Yusuf Mlela ambaye amekuwa akidaiwa kutumia madawa ya kulevya maarufu kama unga, amesema utofauti wa muonekano wake kwa sasa siyo kwa sababu ya uteja, bali inatokana na umri wake kusogea.

“Unajua mtu unavyozidi kukua na muonekano nao unabadilika, lakini itafikia kipindi nitakuwa sawa tu hivyo naomba mashabiki wangu waelewe kwamba mimi siyo teja na sijawahi kutumia ‘unga’ hizo ni habari za kizushi tu,”alisema Mlela.

Hivi karibuni Mlela alitupia picha kwenye mtandao wa Instagram ambapo wadau mbalimbali walionekana kushangazwa na muonekano wake na kumfananisha na mateja.

Maajabu! Aliyezamishwa Sululu Kichwani Apona

$
0
0
HAKUNA neno jingine la kutumia zaidi ya kusema; KWELI MUNGU MKUBWA! Ni miezi mitano sasa imekatika tangu kusambaa kwa picha mitandaoni zilizomwonesha mwanaume mmoja akiwa ameshindiliwa sululu kichwani huku kisa kikiwa hakijulikani.

Mbali na mitandao ya kijamii, Gazeti la Risasi Jumamosi nalo lilijitoa kufuatilia tukio hilo na kuandika habari katika toleo lake la Julai 26, mwaka huu ikiwa na kichwa cha habari;TUKIO LA KUTISHA. YALIKUWA MANENOMANENO Baadhi ya mitandao iliandika kuwa, jamaa huyo apigwa sululu baada ya kufumaniwa na mke wa mtu gesti, mingine ikasema hapana, alipigwa sululu katika kugombea madini machimboni, wengine wakasema kwanza tukio lile halikuwa Tanzania.

SASA MAMBO HADHARANI

Ni kawaida kwa Magazeti Pendwa ya Global Publishers kufuatilia mambo kwa kina, hata ikipita miaka. Hivi karibuni, timu ya waandishi wa Global jijini Mwanza ilimchimba mwanaume huyo mpaka ikampata na kubaini kwamba anaitwa Oka Kaombe.

Oka ni mkazi wa Mtaa wa Nyakazuzu, Kata ya Nyamatogo wilayani Sengerema, Mwanza ambapo waandishi wetu walimtembelea nyumbani anakoishi na baba yake mzazi (mzee Kaombe) na kuzungumza naye ‘ei tu zedi’ kuhusu mkasa wake huo wa kuzamishwa sululu kichwani.

KUZAMISHWA SULULU KICHWANI

“Kwanza kabisa napenda kusema kweli Mungu ni mkubwa, nimepona! Ingawa mwili bado hauna nguvu sawasawa lakini naendelea vizuri. “Ilikuwa tarehe 19, Julai mwaka 2013  katika machimbo ya Mgodi wa Miombo- Rwamgasa  wilayani Geita, mimi ni fundi wa kuchimba maduara yanayotumika kuchimbia dhahabu.

“Baada ya kumaliza kazi zangu majira ya jioni, nikaenda kupumzika ili kujiandaa kwa siku iliyofuata. “Nilikuwa nimepumzika na wenzangu zaidi ya mia moja, unajua tena migodini. Kufika saa 3 hivi usiku nikiwa nimeanza kusinziasinzia, nilishtukia kitu kizito kinaingia kichwani mwangu upande  wa kushoto.” ALISHINDWA KUPIGA KELELE “Nilishindwa kupiga kelele nadhani kwa sababu ya kule kusinzia. Wenzangu ambao nao walianza kulala walishtuka kwa kusikia harufu ya damu, wakaamka na kuja wakanikuta sululu ikiwa imezama kichwani.

“Hii sululu kule machimbo ni maarufu kwa jina la Moko, hutumika kuchimbia madini katika migodi. Nilichukuliwa na sululu yangu kichwani na kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza  kwa ajili ya matibabu ya haraka.” SIKU NNE BILA FAHAMU Oka anazidi kusimulia: “Mengine ninayosimulia niliambiwa kwani nilipoteza fahamu kwa siku nne.

Nilianza kujitambua baada ya siku nne nikiwa palepale Bugando na kujikuta nipo hospitali lakini nilikuwa siwezi kuzungumza wala kusikia vizuri. Maumivu yalikuwa makali sana kutokana na sululu kuzama kichwani maana ilipoingia ilikwenda kutokea upande wa pili wa kichwa. “Nikiwa nimeshafanyiwa upasuaji kwa kuchomolewa sululu, niliendelea kukaa Bugando kwa siku 52.”

ATOROKA BUGANDO, AMSAKA MBAYA WAKE

Oka alisema kuwa, hiyo siku ya 52 aliamua kutoroka hospitalini hapo kwa sababu alishindwa kulipia gharama za matibabu ambazo ni shilingi laki tisa (900,000). “Kiasi hicho cha pesa kwangu kilikuwa kikubwa na hata sasa bado ni kikubwa ndiyo maana niliamua kutoroka,’’ alisema Oka.

ALIYEMZAMISHA SULULU AJULIKANA

Oka anaendelea kusimulia:

“Nilipotoka hospitalini kitu cha kwanza nilianza kumtafuta mtu aliyenifanyia kitendo kile cha kinyama, marafiki zangu wakanipa ushirikiano  na kuniambia unyama ule ulifanywa na jamaa mmoja anayeitwa  Masha. “Huyu Masha ni mchimbaji wa madini kwenye ule mgodi lakini alikimbia baada ya kufanya tukio na mpaka sasa hajulikani alipo.”

KISA CHA KUPIGWA SULULU PIA CHAJULIKANA

Oka alisema taarifa alizopata baadaye kutoka kwa wachimbaji mgodini hapo ni kwamba,  lengo la Masha kumpiga na sululu lilikuwa ni kumtoa kafara (ndagu) ili aweze kupata dhahabu nyingi na awe bilionea kwa siku za usoni. “Ila Mungu ni mkubwa alitupilia mbali wazo hilo mpaka sasa niko hai,” alisema Oka.

AFYA YAKE KWA SASA

Oka alisema kwa sasa anaamini amepona kabisa kidonda chake kichwani ila hawezi kufanya kazi yoyote kutokana na mwili kukosa nguvu za kutosha.

UPASUAJI MWINGINE

Aliendelea kusema kuwa, akiwa Bugando aliambiwa na madaktari kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji kwa mara nyingine na kuwekewa vyuma kichwani baada ya kuwekewa vyuma hivyo itabidi akae miaka mitatu bila kufanya kazi yoyote ndipo atapata nguvu za kufanya kazi kama zamani.

MAISHA YAKE KWA SASA

Oka alisema maisha yake kwa sasa ni magumu kwani ana watoto 5, lakini pia alitengana na mke wake hivyo yeye ndiye baba na mama wa familia kwani hata wazazi wake wamezeeka, hivyo wanamtegemea yeye. ANACHOWAOMBA WATANZANIA Alisema kwa sababu bado ana safari ya kujitibu na pia kutunza familia, amewaomba Watanzania wenye kuguswa na mkasa wake wamsaidie pesa kwa kiasi chochote atakachojaliwa mtu kwa kutumia simu yake ya mkononi ambayo ni 0682 013479.

Sakata la Tegeta Escrow: Rais Kikwete Kutoa Maamuzi Yanayosubiriwa na Wengi Week Ijayo

$
0
0
UAMUZI juu ya maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotaji fedha katika Akaunti ya Tegeta Escrow, utatolewa wiki ijayo na Rais Jakaya Kikwete.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Dar es Salaam jana, ilisema tayari Rais Kikwete amepokea Ripoti ya ukaguzi uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ilisema Rais Kikwete pia amepokea nyaraka na ushauri uliotolewa na Bunge la Jamhuri ya Muungano kuhusu sakata hilo.
“Rais Kikwete ameanza kupitia na kusoma nyaraka hizo, wiki ijayo atatoa maamuzi katika mambo yanayomhusu yeye na yale yanayoihusu Serikali, atayatolea maagizo na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.
“Baada ya kurudi nchini akitokea Marekani ambako alifanyiwa upasuaji wa tezi dume, Rais alianza kazi Desemba 8 mwaka huu,” ilifafanua taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, Rais Kikwete ameelekeza Ripoti ya CAG iwekwe hadharani ili umma uweze kuisoma na kujua nini kimesemwa, kupendekezwa na CAG.
Pia ameagiza ripoti hiyo itangazwe katika magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii.
Akutana na viongozi wa dini

Mapya kuhusu ESCROW, Shule ya Prof Tibaijuka yathibitisha kupokea pesa' in good faith'

$
0
0
TAARIFA YA BODI YA WADHAMINI WA JOHA TRUST KWA WAZAZI NA UMMA KUHUSU MCHANGO WA SHS BILIONI 1.617 KUTOKA KWA BW. JAMES RUGEMALIRA WA TAREHE 12 FEBRUARI, 2014

1. Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Barbro Johansson Girls’ Education Trust (JOHA TRUST au BARBRO) inatoa taarifa hii kutokana na utata uliojitokeza kuhusu mchango wa Shs bilioni moja milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,0000/- ) tulioupokea kutoka kwa Bw James Rugemalira wa VIP Engineering and Marketing Limited.

2. Mwanzilishi wa Shirika na Malengo yake: Bodi ya Wadhamini BARBRO inachukua nafasi hii kufafanua kwamba kiongozi wa Waanzilishi wa asasi yetu ni Mhe Profesa Anna Tibaijuka ambaye pia ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Malengo na madhumuni ya taasisi ya JOHA TRUST ni kuendeleza elimu kwa mtoto wa kike kwa kuwafadhili wasichana wenye vipaji lakini watokao katika familia za kipato kidogo kusoma katika shule bora inazoziendesha.

3. Jina la taasisi ya JOHA TRUST linatokana na uamuzi wa wanawake waanzilishi kumpa heshima Hayati Dr. Mama Barbro Johansson (1912-1999) aliyewasili kutoka Sweden mwaka 1946 kama mmisionari na kuanzisha shule ya wasichana ya kati hapo Kashasha Bukoba. Mwaka 1954 alijiunga na Mwalimu Nyerere kupigania uhuru na baadaye kuwa raia wa Tanzania na Mbunge. Mwaka 1964 aliombwa na Mwalimu Nyerere kujitolea kuwa Mwalimu Mkuu wa sekondari ya juu (High School) pekee ya wasichana ya Tabora Girls iliyokuwa imekumbwa na utovu wa nidhamu na kutaka kufungwa. Mama Barbro akafanikiwa sana kuigeuza shule hiyo kiasi kwamba ilipata nishani ya UNESCO mwaka 1967. Mama Barbro ndiye alianzisha elimu ya watu wazima nchini na pia ndiye alimuunganisha Mwalimu Nyerere na wahisani kutoka nchi za Nordic ambazo zilianza ufadhili wake katika Kituo cha Elimu Kibaha na Kituo cha Kilimo, Uyole, Mbeya.

4. Shule za JOHA TRUST na Sura yake: Shirika linamiliki na kuendesha Sekondari mbili nchini. Kwanza ni Sekondari Bingwa ya Barbro iliyopo jijini Dar es Salaam. Ilianzishwa mwaka 2000 ikiwa na wasichana 40 na hivi sasa wapo 632 wote wa bweni katika kidato cha 1 hadi 6. Pili ni Kajumulo Girls’ High School iliyopo Manispaa ya Bukoba. Ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wasichana 31 na hivi sasa wapo 151 katika kidato cha 1, 5 na 6. Jumla shule hizi zina wanafunzi 783 na waliomaliza ni 1,512. Wote isipokuwa 5 walifaulu mitihani na kujiunga na elimu ya juu katika vyuo vikuu mbali mbali ndani na nje ya nchi. Kwa kulingana na uwezo wa mfuko wa ufadhili, wasichana 453 sawa na asilimia 30% ya wanafunzi wamesaidiwa karo. Shule ya Barbro imekuwa miongoni mwa shule kumi bora Tanzania (2010) na kwa wastani inakuwa kati ya shule 50 bora katika mitihani ya taifa. Itambulike kwamba mafanikio haya yanapatikana pamoja na shule kuwa na sera ya kutowafukuza wanafunzi kwa misingi ya ufaulu wa mitihani ili mradi wawe na nidhamu. Falsafa yetu ni kuwahimiza wanafunzi kuweka bidii kadri ya uwezo wao, kujithamini na kujiamini katika maeneo wanayofanya vizuri. Kipa umbele chetu ni maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja kwanza na sifa kwa shule baadaye. Katika hali hii walimu hawana budi kufanya kazi ya ziada.

5. Gharama za Uendeshaji na vyanzo vyake: Tangu ianzishwe JOHA TRUST imetumia gharama ya Shs bilioni thelathini na mbili (Shs 32,267,000,000/-) ambazo zimetokana na karo na michango ya wazazi asilimia 37%; wafadhili wa nje asilimia 35%, wafadhili wa ndani asilimia 7% na mikopo asilimia 21%. Kama taasisi nyingi zinazotoa elimu, JOHA TRUST inakabiliwa na uhaba wa fedha na ujenzi bado kukamilika. Shule inatoa huduma ya elimu bora na haifanyi biashara kama wengi wasioelewa wanavyofikiri. Bila ruzuku na misaada viwango vyake vya juu haviwezekani. Shirika la misaada la Sweden (SIDA ) ambalo limekuwa mfadhili mkubwa limekamilisha ahadi yake ya ufadhili wa miaka 10 (2002-2012) lililopanga kwamba ingelitosha kusimika taasisi ya JOHA TRUST na kuitaka ijitegemee. Hata hivyo SIDA imeacha utekelezaji wa Master Plan ya BARBRO ya mwaka 2004 bado kukamilika. Jambo hili limekuwa changamoto kubwa kwa Bodi kwa sababu katika Master Plan SIDA ilipandisha viwango vya majengo kuwa juu kulingana na sifa na hadhi ya Mama Barbro. Ikihitimisha ufadhili huo, SIDA ilihimiza Bodi kuhamasisha michango ya ndani ili kujenga uendelevu na kukamilisha ujenzi wa Master Plan hiyo.

6. Maombi ya Ufadhili: Kwa kuzingatia ushauri huo wa SIDA, mwaka 2012 Bodi ilimtaka Mwanzilishi (ProfesaTibaijuka) ambaye pia ni Mtafuta Fedha (Fund Raiser) wa JOHA TRUST kuwaomba baadhi ya wafanyabiashara mashuhuri nchini kuunga mkono shughuli za asasi yetu kwa michango. Bwana na Bibi James Rugemalira ni miongoni mwa wafanyabiashara walioombwa mchango huo kwa barua ya tarehe 4 Aprili 2012 kupitia kampuni yao ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited. Hatimaye mapema Februari 2014, bila kutaja ni kiasi gani, Bw. Rugemalira alimjulisha Mwanzilishi kwamba yuko tayari kufanya mchango ulioombwa na kumwagiza kwamba sharti ni yeye Mwanzilishi kufungua account hapo Mkombozi Benki kuupokea mchango huo na kuchukua jukumu la kuufikisha shuleni na kuhakikisha unatumika kama ilivyokusudiwa. Bw Rugemalira alieleza hakutaka kuhangaika kuhamisha fedha kwenda benki nyingine ambapo tayari kulikuwa na akaunti za shule.

7. Mchango wa VIP ulivyopokelewa: Kama alivyotakiwa, Mwanzilishi alifungua account hiyo hapo Benki ya Mkombozi tarehe 3 Februari, 2014 na kuupokea mchango huo wa jumla ya bilioni moja, milioni mia sita kumi na saba na lhaki moja (Shs 1,617,100,000/=) kwa niaba ya shule tarehe 12 Februari, 2014 kutoka kwa kampuni ya VIP Engineering and Marketing.

8. Maamuzi ya Bodi: Bodi ya Wadhamini BARBRO ilikaa katika kikao maalum tarehe 13 Februari, 2014 kupokea taarifa ya mchango huo mkubwa kutoka kwa Bw. Rugemalira kupitia kampuni yake ya VIP Engineering. Bodi iliukubali na kuamua mchango huo utumike kulipa sehemu ya deni la shule hapo Bank M ambalo lilikuwa changamoto kubwa. Kwa hiyo Mwanzilishi aliagizwa na Bodi kuhamisha fedha hizo kutoka akaunti yake ya Mkombozi kwenda akaunti ya Bank M kulipia mkopo huo. Hii inafafanua kwa nini fedha zilihama kwa haraka kutoka Benki ya Mkombozi kwenda Bank M kwa wale wanaohoji suala hili.

9. Ulipaji wa Deni na Madai yaliyobakia: Ili kutekeleza Master Plan, Julai 2011 JOHA TRUST ilikuwa imechukua mkopo wa Shs bilioni mbili (Shs 2,000,000,000/-) hapo Bank M kwa ajili ya ujenzi wa bweni kubwa lenye uwezo wa vitanda 163. Hadi kufikia tarehe 19/04/2014 mkopo huo ulipolipwa wote, deni hilo lilikuwa limezaa riba na gharama nyingine na kuongezeka hadi kufikia takriban jumla ya Shs bilioni mbili, milioni mia saba arobaini na moja, lhaki tatu sabini na nne elfu, mia nne arobaini na nne (Shs 2,741,374,444/-). Kwa hiyo, pamoja na ukubwa wa mchango wa Bw Rugemalira bado umelipia sehemu ya deni hilo tu. Sehemu nyingine iliyobaki (Shs 1,124,274,444/-) imelipwa kutoka vyanzo vingine vya mapato ikiwemo mkopo wa milioni mia mbili tisini na moja, lhaki tatu sabini na nne, mia nne arobaini na nne (Shs 291,374,444/-) zilizotolewa na Mwanzilishi kulipa riba ya kila mwezi wakati wa uhai wa mkopo huo. Ilikuwa maamuzi ya Bodi kupunguza madai hayo ya Mwanzilishi kutoka takriban Shs milioni 291 na kubakia takriban Shs milioni 174 . Kwa hiyo fedha zote alizozitoa Bw Rugemalira za Shs 1.617,100,000/- zilitumika kulipa mkopo na wala hazikutosha. Katika hali hiyo, hisia na madai yanayotolewa kwamba Mwanzilishi alijinufaisha na fedha hizo SI KWELI. Isingewezekana.

10. Ufadhili Endelevu wa Shule: Itambulike kwamba hata kwa nafasi yake Mwanzilishi ni mfadhili na mdhamini mkubwa wa JOHA TRUST kwa fedha zake binafsi. Bodi ilimwomba awe analikopesha shirika letu na wafadhili wakipatikana tunamrejeshea fedha zake polepole. Kwa mfano SIDA iliwahi kuridhia kwamba sehemu ya msaada wake utumike kurejesha mkopo uliotolewa na Mwanzilishi wakati wa kuanzisha shule kati ya mwaka 2000 hadi 2003.

11. Mchango wa VIP ulipokelewa kwa nia Njema. Shirika halina utaratibu kuwahoji wafadhili wetu wa ndani au nje kwanza kuthibitisha chanzo cha fedha zao wanazotuchangia. Misaada na michango, iwe mikubwa au midogo, yote imekuwa ikipokelewa kwa nia njema tukiamini pia inatolewa kwa nia njema. Tunaamini hivi pia ndivyo ilivyo kwa asasi nyingine nchini na jamii kwa ujumla kwa mfano michango ya maendeleo na hata harusi na shughuli nyingine kama hizo. Kwa kuwa tulihakikishiwa na Benki ya Mkombozi kwamba fedha za Bw Rugemalira zilikuwa zimelipiwa kodi, tulipokea mchango wake kwa furaha bila wasi wasi wowote.

12. Michango ya kuendeleza shule siyo zawadi binafsi kwa viongozi wake: Tunatambua kuwa sheria ya Maadili ya viongozi huwataka kuwasilisha zawadi zote zinazozidi Shs elfu hamsini (Shs50,000/-) kwa mwajiri wao. Kuna wanaodai Mwanzilishi amekiuka maadili kwa kutouwasilisha mchango huo Serikalini. Pia kuna wanaohoji kwa nini mchango mkubwa huo haukwenda kwenye jimbo lake la uchaguzi (Muleba Kusini) ili kuendeleza shule za Kata. Wote wanakosea. Mchango ulitolewa kwa shule ya JOHA TRUST na Mwanzilishi alipoufikisha kwetu tuliupokea na kuutumia kama ilivyokusudiwa kwa shughuli za maendeleo ya shule na kumwendeleza mtoto wa kike. Kufanya vinginevyo ndiko kungelikuwa kukiuka maadili.

13. Umuhimu wa Uchunguzi: Kupitia luninga tulifuatilia mjadala Bungeni Dodoma jioni ya Ijumaa tarehe 28, Novemba, 2014 kabla ya kikao hicho kuvurugika. Tulishuhudia jinsi Bunge zima lilivyoazimia kwamba vyombo vya uchunguzi vifanye kazi yake kuhusu waliopata ͞mgao͟ ili kuondoa mashaka na taarifa kamili zipatikane ili pale penye makosa hatua stahiki kuchukuliwa. Kwa hiyo, katika kikao cha Bodi cha tarehe 2 Desemba, 2014, kilichoitishwa rasmi kujadili jambo hili, kwa kauli moja tunatamka kwamba hatuamini kabisa na tunashindwa kuelewa kwa nini Mwanzilishi wetu atakiwe kuwajibishwa nafasi yake Serikalini kwa kuwa tu alipokea mchango wa shule kwa niaba yetu. Jambo hili litatuchanganya na kutukatisha tama sisi wananchi wa kawaida tunaojitolea kutekeleza shughuli mbali mbali za maendeleo hususan elimu. Tunaamini hatua hiyo pia itafifisha juhudi za viongozi wengine wengi wanaohangaika kuhamasisha michango ya shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo elimu, afya, maji, vijana, walemavu, watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wazee, wajane, n.k. katika taifa letu changa. Tunaomba Mhe Rais alione jambo hili. Ikiwa michango ya maendeleo inayopokelewa na viongozi kwa niaba ya wadau wao itatafsiriwa kama zawadi zao binafsi kuna hatari kuzorotesha ͞harambee͟ za maendeleo. Tunaamini ufafanuzi huu utatosha kuondoa utata katika suala hili ili umma na viongozi wa ngazi za juu wapate ukweli juu ya jambo hili na ushiriki wetu. Bodi yetu iko tayari kujibu maswali yoyote yanayoweza kuulizwa ili kuondoa utata huu kabisa.

14. Shukrani kwa Wafadhili: Katika miaka 15 ya uwepo wa taasisi yetu (2000 -2014) , JOHA TRUST imepokea michango jumla ya Shs bilioni 13.59 kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Wafadhili wakubwa wa nje ni SIDA ambayo imetoa jumla ya Shs bilioni 8. 15 sawa na asilimia 60% na JOHA TRUST Sweden Shs bilioni 1.79 sawa na asilimia 13.11%. Mwaka 2000 Serikali ya Tanzania chini ya Mhe Rais mstaafu Benjamin Mkapa ilitoa ardhi ekari 50 kujenga shule ya Barbro jijini Dar es Salaam. Mwaka 2005 kabla ya kuondoka madarakani Rais Mkapa alikuja kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne kukagua maendeleo yetu, akaridhika na kuchangia Shs milioni tano (Shs 5,000,000/-). Kwa wahisani wa ndani ya nchi Dr. Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP amechangia jumla ya Shs milioni 278 mwaka 2013 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya kidato cha nne. Kwa hiyo alichofanya Bw James Rugemalira ni sawa sawa na wahisani wengine waliotuunga mkono. Tunawashukuru wafadhili wetu wote wa ndani na nje ya nchi kwa michango yao na tunawaahidi kuongeza juhudi zetu za kumwelimisha mtoto wa kike na kwa kufanya hivyo jamii nzima ya Watanzania.

15. Ujumbe kwa Wazazi: Kama ilivyofafanuliwa tarehe 25 Septemba, 2014 katika mahafali ya kidato cha nne, ni muhimu kwa wazazi na walezi kuyaelewa vizuri yaliyojiri katika suala hili kuepuka upotoshwaji unaotokana na sababu za kisiasa dhidi ya Mwanzilishi wetu. Pamoja na matatizo yaliyojitokeza hatujakata tamaa katika juhudi zetu kumjengea uwezo mtoto wa kike. Tunawaahidi wazazi ambao wamekuwa na wasiwasi kuhusu ufadhili wa watoto wao kwamba kazi inaendelea kama kawaida. Hivi sasa wasichana 83 katika shule ya BARBRO na wasichana 20 katika shule ya KAJUMULO wanasoma kwa ufadhili. Tunawahakikishia wasichana wote hawa 103 ambao ni asilimia 13% ya wanafunzi wote 783 tulionao wasiwe na wasiwasi bali kuendelea kusoma kwa bidii. Hakuna binti mwenye ufadhili tayari atakayepoteza nafasi yake katika shule zetu kwa sababu ya tukio hili. Tunachukua nafasi hii kuhimiza michango kutoka kwa wafadhili wengine watakaoguswa na juhudi zetu ili tuweze kuongeza uwezo wa kuwafadhili wahitaji wafikie asilimia 30% tuliyokusudia. Pamoja tuendelee kushirikiana katika kuendeleza elimu na ulezi bora kwa mtoto wa kike. Kama alivyosema Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere ͞Hasa wakati wa shida kukata tamaa ni dhambi

Picha Hii ya Kikwete na Lowassa Jana Yaongea Mengi na Kutoa Majibu Maswali ya Kuelekea 2015

$
0
0
Kwa picha hiyo jinsi inavyoonekana, inaonekana mzee wa EL na JK watakuwa 'wamecompromise' ili ampigie debe ili apeperushe tiketi ya CCM kwa nafasi ya Urais mwakani.

Hilo likitimia watanzania tutakuwa tunakumbushwa kauli iliyowahi kutolewa na EL wakati ule wa sakata ya Richmond, pale aliposema kuwa yeye na JK hawajakutana barabarani!

JK naye akamjibu mzee EL kuwa asiwe na wasiwasi kwani historia itamtendea haki na ipo siku yeye EL atakuwa 'huru' kutokana na skandali hiyo ya Richmond!

Bila shaka hii picha itakupa majibu ya maswali uliyo kua nayo kichwani mwako.....yetu macho na masikio kuelekea octoba 2015.

Singa Singa wa IPTL, Harbinder Singh Sethi atoweka Nchini

$
0
0
Mmiliki wa kampuni ya IPTL,Harbinder Seth, ametoweka na vyombo vya usalama vimejiandaa kumkamata ndapo atarejea nchini, Raia mwema limeelezwa.Singh ambayekampuni yake ya Pan african Power solution (PAP) inadaiwa kununua umiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL katika mazingira yaliyozua utata, anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya au Africa ya Kusini.

Gazeti hili limeelezwa kwamba Singh aliondoka nchini siku chache kabla ya bunge la Tanzania ya wahusika wote wa makosa ya kijinai katika suala hilo wakamatwe na hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.

Azimio namba moja la Bunge lilisema;....Takukuru, Jeshi la polisi na vyombo vingine husika vya Ulinzi na usalama viwachukule hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,watu wote waliotajwa na Taarifa maalumu ya kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya akaunti ya Escrow, kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalmbali unavyoendelea.

Raiamwema limeelezwa kwamba, singh ambaye katka siku za nyuma alikua akipenda kufika katika hotel mbalimbali ikiwemo Sea cliff ya Jijini dar es salaam, Sasa hayupo Dar es salaam lakini anafuatilia kea karibu yanayo endelea.

Naweza kukuthibitishia kwamba sethi hayupo nchini hivi sasa. Kwenye hili swala sitaki kuwa mzungumzaji wake lakini nafahamu kwamba aliondoka kabla ya Bunge kuazimia kwamba wahusika wakamatwe.

"Sasa kama alifanya akijua kwamba hayo hayo yanaweza kutokea mimi sijui. Siwezi pia kujibu swali lako la atakuja lini sabau sijaambiwa. Hata hili la kukuambia kwamba hayupo nimekwambia kwa sababu tunafahamiana na sitaki kukudanganya, Alisema mmoja wa watu wafanyakazi wa Sethi ambaye hata hivyo gazeti hili haliwezi kumtaja jina
Viewing all 104809 articles
Browse latest View live




Latest Images