Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live

Mh.Mbatia: Jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake

$
0
0
Serikali imeshauriwa jeshi la polisi lifanyiwe marekebisho ya kimfumo ili kuboresha utendaji wake ambao kwa sasa unalalamikiwa kwa sehemu kubwa na wananchi kwa kukiuka haki za binadamu.



Akizungumza jana mjini Dodoma katika kuhitimisha hoja kuhusu kukamatwa kwa kiongozi wa wa chama cha CUF, Prof Ibrahim Lipumba na wanachama wake,Mbatia alisema kuwa kitendo hicho kilikiuka haki za binadamu ikiwemo wanawake kudhalilishwa kijinsia.

Mh. Mbatia emeongeza kuwa ili chaguzi zijazo ziwe za amani na utulivu ameishauri serikali kubadilisha sera za vyama vya siasa na utawala pamoja na mfumo wa jeshi la polisi kuendeleza amani na utulivu ambavyo kwa sasa vinaonekana kuanza kutoweka.

Mwimbaji Nazizi Afanya Maajabu, Ajikondesha na Kuwa Mrembo wa Haja Ukimuona Hutoamini

$
0
0

Mwanamuziki Nazizi Kutoka Kenya Ameshangazi Wengi Baada ya Kufanikiwa kupunguza mwili wake kwa kiasi cha wengi kuto amini kama ni yeye, Mwanamuziki huyo kabla ya hapo alivyo sasa alikuwa ni Bonge nyanya yaani mnene kupindukia , lakini siku za karibuni mwanamuziki huyo ameingia Gym na Kufanikiwa kupunguza mwili wake kwa kiasi kikubwa sana.



Artist and music sensation Nazizi has made all our jaws drop to the floor, as we get busy picking our jaws from the floor and getting reanimated from our shock, lets share the shock with you too, lets see if you handle the jaw-drop. Damn this is like an RKO from nowhere! She has literally stunned us.

 Now look at That!


Habari za Project Mpya ya Jack Wolper na Marco Chali wa Mj Records Kutoka Kimapenzi, Sikiliza You Heard Hapa

$
0
0
Kama ulikuwa na mbali na Radio yako ukapitwa na U Heard kwenye XXL ya leo January 30, Soudy Brown alikuwa na story kuhusu tetesi za uhusiano uliopo kati ya Producer wa MJ Records, Marco Chali na staa wa Bongo Movie, Jackline Wolper.



Gossip Cop alimtafuta Jackline Wolper lakini hakupatikana kwenye simu, alipomtafuta Marco Chali alikataa kujibu chochote kuhusu tetesi hizo ila alimjibu Soudy kwamba itabidi amtafute ili wafanye Interview kabisa kuhusu ishu hiyo.

Isikilize U Heard yote kwenye hii sauti hapa, bonyeza play.


Muuza Genge Achezea Kichapo kizito baada ya kunaswa na Mke wa Mtu

$
0
0
Muuza genge mmoja kwenye Soko la Mji Mpya mjini Morogoro ambaye jina halikupatikana mara moja, amejikuta akichezea kichapo kwa madai ya kunaswa na mke wa mtu kisha kutembezwa mtupu mtaani.



Fumanizi hilo lililojaza umati wa jinsi na rika zote wakiwemo watoto lilijiri katikati ya wiki hii, maeneo ya Mji Mpya ndani ya chumba na kitanda cha wanandoa hao.

Kwa  mujibu wa majirani, jamaa huyo anadaiwa kuwa na kasumba ya kumhonga vyakula mke huyo wa mtu ambaye naye kwa kukosa uaminifu kwenye ndoa alijikuta akiingia mkenge hasa mumewe anapokuwa safarini kwa kuwa ni mtu wa kusafiri katika biashara zake binafsi.

Ilidaiwa kwamba, mwanamke huyo hutumia mwanya huo kumwingiza mchepuko wake huyo kwenye chumba na kitanda anacholala na mumewe kisha ‘kufanya yao’.

Baada ya kukolea huku mahaba niue yakitajwa na sauti ‘tamutamu’ zikisikika chumbani, majirani walikerwa na kitendo hicho cha jirani yao kudhulumiwa ‘mali’ zake ndipo wakaamua kumpa  taarifa mumewe.

Ilisemekana kwamba, mume, akishirikiana na majirani aliowaomba ushirikiano, aliweka mtego ambapo alijifanya anasafiri kama kawaida.


Siku ya tukio, saa husika ilifika, kama kawaida jamaa alifika nyumbani kwa wanandoa hao kisha kuchoma chumbani kwa wanandoa tayari kwa kulicheza ‘segere’.

Mwenye mke, akiwa chimbo alitonywa na majirani kuwa mambo ‘yamekwiva’ chumbani ndipo akawaibukia na kumkuta jamaa laivu akiwa mtupu. Haikujulikana kama ilikuwa ‘tayari au bado’.

Akiwa na hasira, mwenye mke alidaiwa kumshushia kipigo mgoni kilichomfanya kuloa damu chapachapa na baadaye kumtoa nje akiwa mtupu kisha kumtembeza mtaani kwenda nyumbani kwake huku ‘kadamnasi’ ikipiga kelele ‘watu weweee...”

Katika hali ya kushangaza, mwenye mke aliomba mkewe asipigwe picha akidai bado anampenda na hayuko tayari kumuacha.

Credit: Gpl/Risasi

Chenge Ageuka Mbogo Bungeni baada ya kuitwa FISADI.......Amtaka Halima Mdee Atoe Ushahidi Kuthibitisha Kauli yake

$
0
0
MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM), kwa ufisadi.

Chenge alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za Bunge zilizowasilishwa juzi.



Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.

Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).

“Wabunge tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,” alisema Mdee na kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa (Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.

Kauli hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; “kwa heshima zote nimemvumilia sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.

Mimi ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.

 “Nina mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu, kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,” alisema Chenge.

Mwenyekiti wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata hivyo Mdee alijibu, “Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa kuleta nitaleta.

"Tunazungumza hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu haya ni mambo makubwa.

Kocha Mkuu wa Simba Kopunovic Agoma Kupangiwa Kikosi na Kiongozi wa Juu wa Timu Hiyo

$
0
0
Hali inayosemekana kuwa timu zetu kongwe za kariakoo jijini dar es salaam kuwa na tabia ya viongozi wa timu hizo kuwapangia makocha wachezaji wa kucheza match.



 leo hii kupitia kituo cha redio cha PRIDE FM YA MTWARA kwenye kipindi cha michezo kimetoa taarifa kuwa kocha mkuu wa simba Goran Kopunovic amempiga mkwara kiongozi wa juu wa timu hiyo ndugu GOERFREY NYANGE KABURU kuacha tabia ya kumpigia simu ya kumwambia asiwapange baadhi ya wachezaji kwenye wanazocheza wekundu hao wa msimbazi.

Baadhi ya wachezaji ambao KABURU amekuwa akiwataja ili wasipangwe ni Hassan Isiaka, Said Hamisi Ndemla na Tshabalala. Kwa style hii ya viongozi wa timu zetu za bongo kuwapangia makocha wachezaji wa kucheza kwenye match wala tusitarajie mabadiliko yoyote kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Hivi kweli kaburu ana sababu za msingi za kuwakataa hawa wachezaji wasipangwe kwenye match wanazocheza simba!!!!!

VIDEO: Halima Mdee Akiwalipua Andrew Chenge na Idd Simba Kwa Ufisadi Bungeni

$
0
0
Mara ya kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege (ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.



Licha ya kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni 200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT)

Angalia Hapa Chini Video Jinsi Halimaa Mdee Alivyokuwa anawalipua Bungeni:


Lulu:Sijawahi Kuwa Mweusi, Rangi ya Mtume Nimezaliwa Nayo

$
0
0
Urembo:Mrembo na mwigizaji wa filamu za kibongo, Diana Elizabeth Michael ‘Lulu’ hivi majuzi alitupia picha yake ya zamani mtandaoni (hiyo hapo juu) ikiwa kama ni “ThrowBackThursday” (TBT) yake, na kuiandikia mameno haya;





  • “Let me ThrowitBack ,Shikana Mama, Enzi ZaUjanaSijawahi kuwa mweusi lol..! Rangi Ya Mtume Nimezaliwa Nayo”


Wengi walimsifu na kumpongeza Lulu  kwa kuweza kuitunza ngozi yake kwakutupia “comments” na kugonga “likes” za kutosha kwenye picha hiyo, kwani anaonekana kuwa hatumii madawa/vipodozi ya kujichubua kama wadada wengi  wa siku hizi hutumia madawa/vipodozi ili kubadili rangi za ngozi zao.

Jiwe gizani, wewe je hautumii? Hata wa kaka nao nasikia wamo!!!!.

Jini Kabula Amtaka Mzazi Mwenzie Chuz Aoe, Umri Umeenda Anazidi Kuzeeka

$
0
0
Mwigizaji  wa filamu z kibongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amemtaka mzazi mwenziye, Tuesday Kihangala ‘Mr Chuz’ aoe ili kulinda heshima yake.



Akizungumzia maisha yake ya uhusiano mbele ya mwanahabari wa GPL, Kabula alisema anajivunia kuzaa na Chuz lakini kwa kuwa yeye hakupanga kuolewa na prodyuza huyo mkongwe, ni bora aoe kwani umri unamtupa mkono.


  • Chuz aoe tu sasa umri umeenda. Tena akioa  mimi nitacheza muziki balaa siku hiyo, si unajua mambo yangu. Mbaya zaidi sina kabisa wivu naye,” alisema Jini Kabula.

Diamond Amshukia King Lawrenc Amwita Mpuuzi AnayeTafuta Umaarufu Kwa Nguvu kwa Kupitia Yeye na Zari

$
0
0
Stori: Musa Mateja/Risasi
ICON wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’,  juzikati aliamua kumtolea uvivu, aliyewahi kuwa mpenzi wa mwandani wake wa sasa, Zarinah Hassani ‘Zari’, King lawrenc kwa kumuita mpuuzi anayetafuta kiki kwa vile kila kukicha kazi yake ni kumfuatafuata kwa maneno ya kejeli na kumtusi.



Akipiga stori mbili tatu na gazeti hili hivi karibuni, staa huyo alisema mara nyingi amejitahidi kumpuuza kwa kitendo chake cha kumkejeli katika mitandao ya kijamii, lakini kitu alichogundua ni kwamba mpenzi huyo wa zamani wa Zari anataka yeye amjibu ili aweze kulikuza jina lake, kitu ambacho  ni cha kijinga.

Nimejitahidi sana kukaa kimya kila anaponitusi huyu jamaa, lakini kumbuka mimi ni binadamu, najaribu kuliangalia jambo hili nagundua kwamba hana chochote cha msingi anachoongea zaidi ya matusi,  anatafuta nimjibu kitu ili apate kiki aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Diamond na kuongeza:

Nashukuru nimegundua hana mada ya kuzungumza katika mitandao zaidi ya mimi na Zari, ningemshauri aendelee na shughuli zake za kila siku, asihangaike na kitu asichokijua, kugombana na mimi ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa, mimi nawaza nifanyeje ili niweze kuitangaza nchi yangu, yeye anawaza afanyeje ili aweze kupandisha jina lake, siwezi kubishana na mpuuzi.”

Mwanaume huyo Mganda, kwa muda mwingi amekuwa akiweka picha zake, Zari na Diamond akisindikiza na maneno ya kejeli na dhihaka dhidi ya mkali huyo wa Bongo Fleva, katika kile kinachoonekana kuwa ni kushikwa na wivu.

TFF wakubali Coutinho kuichezea Taifa Stars Kwa Masharti Haya Hapa

$
0
0
Na Mohammed Mdose

BAADA ya kiungo wa Yanga, Andrey Coutinho, raia wa Brazil, kuonyesha nia yake ya kuichezea timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limemkubalia lakini limempa masharti ya kufuata.




Coutinho aliyetua Yanga mwanzoni mwa msimu huu, alitamka kuwa kutokana na nafasi finyu ya yeye kuichezea timu ya taifa ya nchini kwao, basi yupo tayari kuichezea Taifa Stars kama TFF itamhitaji afanye hivyo.

Katibu wa TFF, Selestine Mwesigwa, amesema kuwa hakuna kifungu chochote ndani ya shirikisho hilo kitakachomzuia kuichezea Stars, lakini anatakiwa kwanza kubadili uraia na siyo shirikisho kuhangaika kumbadilishia.

“Sisi hatumzuii ila kama anahitaji hivyo inatakiwa yeye mwenyewe abadili uraia na siyo sisi kumbadili, kingine pia kocha wa timu ya taifa, Martin Nooij ndiyo mwenye maamuzi ya mwisho kama akishabadili atutaarifu ili tufahamu, kama kocha akivutiwa na kiwango chake na akichaguliwa basi tumjumuishe kwenye kikosi,” alisema Mwesiga.

Kipigo cha Mbeya City Yasababisha Kocha wa Simba Kuomba Kuacha Kazi

$
0
0
Martha Mboma na Sweetbert Lukonge
KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, ameomba kuondoka klabuni hapo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo ilipofungwa na Mbeya City mabao 2-1 katika Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.



Matola ambaye alianza kuifundisha timu hiyo msimu uliopita akisaidiana na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo, Zdravko Logarusic, ameomba kuondoka baada ya kuwepo kwa maneno mengi juu ya uwepo wake katika benchi ya ufundi akiwa chini ya Goran Kopunovic.

Rais wa Simba, Evans Aveva ndiye ambaye ametoa kauli juu ya taarifa hiyo na kukiri kuwa wamepokea barua ya Matola akiomba kuachia ngazi juzi.Aveva amesema kuwa katika barua hiyo, Matola ameomba kupunguziwa majukumu na kupewa mengine au kuondoka kabisa klabuni hapo baada ya kukabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kifamilia ambayo yanamfanya ashindwe kufanya kazi yake kwa ufanisi mkubwa.

Aveva amesema kuwa uongozi wa Simba unamuamini Matola na amekuwa mtumishi mzuri klabuni hapo kwa muda mrefu na kusisitiza kuwa wao hawana tatizo naye.

“Matola alileta barua yake jana (juzi) jioni ya kuomba kupunguziwa majukumu kwa kupewa kazi nyingine au kuachana kabisa na klabu kutokana na kukabiliwa na masuala ya kifamilia.
“Hatujatoa tamko lolote, tutakutana na kamati ya utendaji kuweza kujadiliana kujua nini cha kufanya,” alisema Aveva.

Aidha, Aveva aliongeza kuwa, mkutano mkuu wa klabu hiyo, unatarajiwa kufanyika Machi Mosi, mwaka huu baada ya awali kutofanyika kutokana na kuingiliana na Kombe la Mapinduzi.Alipoulizwa Matola jana kuhusiana na ishu hiyo alisema: “Ni kweli lakini nipo njiani, naelekea mazoezini, kwa hiyo siwezi kuizungumzia kwa sasa.”

Agness Masogange Akana Tuhuma za Kutoka na King Lawrenc, Saa yamkononi yaleta Utata

$
0
0
 Baada ya Mrembo Agness Masogange Aishie Njia South Afrika kupost kwenye instagram Picha ya Mkono wa Mwanaume wenye saa nyeusi, watu na page mbali mbali walianza kumshambulia na kusema mkono huo ni wa King Lawrenc na wengine kuandika kuwa ni project mpya, Agness Masogane Amejitokeza na kuandika haya instagram:




"Mkono huo ni wa Boyfriend wangu na sio wa huyo mnaemsema na wala simjui hata sijawahi kumuona..muwe mnachunguza vitu kwanza sio kukurupuka tu na kuongea ongea ovyo"


Washabiki Msipende Kudandia Treni kwa Mbele Mtagongwa - Shilole

$
0
0
Kwenye Kipindi cha TV cha Friday Night Jana usiku Kituo cha EAT Shilole Amefungukia mashabiki wake kuwa Wasipende kudandia Treni kwa mbele Mtagongwa ,kawaambieni hivyo mashabiki wake kwakuwa mmeishupalia ishu ya kumpiga vibao 'mmewe' wakati hamjui kilichotokea

Lazaro Nyalandu na Aunt Ezekiel Wachanwa Bungeni Kuhusu Safari ya Kwenda Kutangaza Utalii

$
0
0
Jana wakati mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema , akichangia  hoja Bungeni nakudai kuwa mawaziri wengi  hawana ubunifu nakumrushia “bomu”  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kuwa anazunguka nje ya nchi na msichana kwa madai ya kutangaza utalii.

Lema alisema;



“Angalia Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alikwenda kutangaza utalii nje ya nchi akiwa ameongozana na (mwigizaji maarufu wa filamu wa Tanzania) Anti Ezekiel,” alisema na kuongeza kuwa waziri huyo hashindi ofisini kwa kisingizio cha kutangaza utalii.

Picha za wawili hawa wakiwa nchini Marekani  wakitangaza utalii zilisambaa sana mtandaoni mwaka jana na kizua stori nyingi juu kile kilichofanyika.

Picha : Waziri Nyalandu akiwana Aunty Ezekiel pamoja na DJ Luke (wakatikati) wakitangaza Utalii, New York, Marekani.

Lakini hivi kuna ubaya gani Staa wetu kushirikiana na waziri katika kutangaza UTALIIII?!!!!

Zari Atua ndani ya Dar, Athibitisha kwa Mara ya Kwanza kwa Kauli yake Kuwa Mpenzi wa Diamond

$
0
0
Katika mitoko yako ya weekend hii usije kushtuka utakapokutana na couple fulani ‘Ameizing’ ya TZ+UG, sababu Zari Tlale a.k.a The Boss Lady yupo ndani ya jiji la Dar au kama anavyopaita mrembo huyo D-City.

Kupitia Instagram mrembo huyo....



 wa Uganda ambaye makazi yake yako Afrika Kusini amepost picha kadhaa akiwa na mpenzi wake Diamond Platnumz kwenye gari ya staa huyo aina ya BMW.

Katika picha nyingine inayothibitisha uwepo wake ndani ya jiji la joto, ni picha aliyopiga na mpenzi wa dancer wa Diamond, dumyutamu anayejiita jujudumyz.

Kwenye moja ya picha hizo ameandika : “Another beautiful day in D-City”, na kwenye picha nyingine ameandika moja ya misemo inayovuma kwa sasa hapa mjini “Kishkwambiii”.

Licha ya kwamba Diamond na Zari kwa sasa wanajulikana kuwa ni wapenzi, lakini mara zote walipoulizwa juu ya uhusiano wao wamekuwa wakikanusha na kusisitiza kuwa wana project ya pamoja. Lakini safari hii Zari amethibitisha mwenye kwa kauli yake baada ya kumuita girlfriend wa dancer wa Diamond “wifi”.

Kwenye picha aliyopiga na msichana huyo Zari ameandika: “With wifi @jujudumyz out and about D-City

Hivi karibuni Diamond alithibitisha kuwa anategemea kupata mtoto na Zari baada ya kupost picha ya Ultra Sound ikithibitisha kuwa Zari ni mjamzito. Hivyo huenda Diamond atakuwa anafurahia kukishika kitumbo kinachokua cha Zari ambamo ndani yupo Chibu Junior.

Jide: Kazi ya muziki nzuri jamani, Nilitoka kwetu na elfu 6 nikarudi mkoba umejaa. Aringishia mkwanja alizotunzwa jukwaani

$
0
0
Msanii akishafanikiwa kuwashawishi mashabiki kulipa kiingilio na kuingia kwenye show yake, hana kazi ya ziada zaidi ya kufanya show nzuri ambayo huwafanya mashabiki wenyewe kuingia tena mifukoni na kuwatunza kwa misimbazi ya kutosha.

Lady Jaydee kupitia Instagram ametuonesha.....



noti za msimbazi ambazo alitunzwa jukwaani na mashabiki waliohudhuria show yake ya jana pale MOG.

Kwenye picha hiyo ameandika:

“Asanteni wote mlionitunza jukwaani Nilitoka kwetu na alfu 6 Nikarudi mkoba umejaa
Kazi ya muziki nzuri jamani Ila Haka ka mkoba jana @niitesonga alikuwa anataka kuka kwapua Mi mwenyewe nna madeni kibao Nawaza nianze lipi kulilipa “

~Bongo5

Picha Mbali Mbali za Sherehe ya THT Kusherehekea Miaka Kumi, Amini Alia Jukwaani na Mkewe Kwa Furaha

$
0
0
Amini Akilia jukwaani na Mkewe
 Jana Jumba la Vipaji Tanzania THT walisherehekea Miaka Kumi toka Kuanzishwa Kwake Pale Escape 1, Mambo yalikuwa matamu sana kwani wasanii wote walio.....



 pitia katika Jumba Hilo la Vipaji walitoa Burudani safi kabisa ya live na kufanikiwa kuwagonga nyoyo mashabiki waliofurika kushuhudia Tukio Hilo...Mpiga picha wa Udaku Specially Eli Ulomi Aliweza Kupata Matukio Mbali Mbali Likiwemo la Amini na Mkewe Kulia Kwa Furaha Jukwaani , Amini na Mkewe wote ni zao la THT , walikutana Hapo na Mwisho ikazaliwa Ndoa..








JWTZ yaapa Kupambana na Majambazi Wanao pora Silaha za Askari

$
0
0
Jeshi la wananchi nchini (JWTZ) kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama nchini limeahidi kukabiliana na makundi ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi sugu ambao wanapora silaha za ....



askari huku wengine wakiuawa hatua ambayo imeanza kutishia usalama wa nchi.

Akizungumza jijini Tanga kufuatia hivi karibuni makundi hayo kupora silaha na kisha kuua askari huko Rufiji mkoani Pwani na wengine wakipora askari wawili silaha nyakati za usiku jijini Tanga na kisha kuwadhuru hatua ambayo imesababisha kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga bombo,katibu mkuu wizara ya ulinzi na jeshi la kujenga taifa  JOB MASIMA amesema vyombo vya ulinzi vitakaa na kuhakikisha kuwa mtandao huu unapatikana ili kurejesha silaha hizo.

Hata hivyo katibu mkuu amekana vikali kuwa huenda makundi haya ya uhalifu yanayojihusisha na kupora silaha askari ni wahitimu waliopitia mafunzo ya jeshi la kujenga taifa JKT ambao baadhi yao hawakupata ajira baada ya kurudu uraiani na kuongeza kuwa hata wanaojihusisha na ugaidi sio wote ambao wamepitia mafunzo ya kijeshi.

Mwanamuziki Diamond Alipwa Millioni 50 Cash Kuwatumbuiza CCM Leo

$
0
0
Chama cha mapinduzi CCM kesho tarehe 1 Feb 2015 kinaadhimisha miaka 38 tangu kuanzishwa kwake mjini songea mkoani Ruvuma......



Kundi la TOT ambalo linamilikiwa na CCM litakuwepo mjini songea kutumbuiza na mwanamuziki Diamond Plutinumz amekubali kutumbuiza baada ya chama cha CCM kukubaliana naye kwa shingo upande kumlipa milioni hamsini (50 mil.) ili Diamond atumbuize kesho.
Viewing all 104808 articles
Browse latest View live


Latest Images