Quantcast
Channel: UDAKU SPECIAL
Viewing all 104795 articles
Browse latest View live

FULL TEXT: Hotuba ya Upinzani Bungeni, Lema Abainisha Viashiria vya Vurugu

$
0
0
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. GODBLESS LEMA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MAONI YA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI, KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA SILAHA NA RISASI YA MWAKA 2014 (THE FIREARMS AND AMMUNITION CONTROL ACT, 2014)

Inatolewa chini ya Kanuni ya 86(6) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013

__________________________

UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, Ninamshukuru sana Mwenyezi Mungu, familia yangu na viongozi wangu wa chama na wananchi wa Jimbo langu. Nawashukuru pia maadui zangu kwa dhati kwani uadui wao, hila zao, na mbinu zao chafu dhidi yangu zimeendelea kuiimarisha imani yangu na tumaini langu siku hadi siku, katika vita hii muhimu tunayopigana ya kulikomboa taifa hili.

Mheshimiwa Spika,Muswada huu wa Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi unaletwa katika Bunge lako tukufu wakati ambapo nchi hii iko katika mtanziko mkubwa ambapo matukio ya ujambazi wa kutumia silaha yamekithiri; mauaji ya raia kwa kutumia silaha za moto yameongezeka; matukio yenye sura ya ugaidi ya utekaji na utesaji yameshuhudiwa hapa nchini, matukio ya uvamizi na uporaji wa silaha katika vituo vya polisi yanashamiri na uhamiaji haramu umekuwa ukiongezeka pia kwa kasi hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Ni ukweli usiopingika kwamba matukio yote haya yametokea huku kukiwa na sheria ya Usimamizi wa Silaha na Risasi ambayo itafutwa na muswada huu kama utapitishwa na Bunge. Hii ni dhahiri kwamba tatizo kubwa la nchi hii sio sheria na matumizi yake, bali ni uongozi uliokosa fikra chanya na utu katika kutawala.

Ndio maana leo, Serikali inafikiri kupambana na janga la Mauaji ya Albino ni kuwatenga Albino na jamii kutoka kwenye makazi yao ya kawaida wakati tatizo la msingi ni imani potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaamini kwamba; huwezi kuipinga imani kwa kutumia silaha isipokuwa kwa habari njema (imani inayojali utu) kuwafikia watu wote.

Mheshimiwa Spika,Pamoja na nia njema ya Serikali ya kuleta Muswada huu, Kambi Rasmi ya Upinzani inaamini kwamba, kama Serikali itajali utu, usawa, haki na demokrasia ya kweli pengine hakungekuwa na hofu ya matumizi mabaya ya silaha miongoni mwa wananchi na hivyo kusingekuwa na na haja ya kuleta sheria za kudhibiti silaha na kuweka masharti magumu kwa wananchi kumiliki silaha, hasa kipindi hiki ambacho kumekuwa na matukio mengi ya kigaidi, ya uvamizi, utekaji na utesaji ambapo kimsingi wananchi wanahitaji ulinzi wa Serikali na ulinzi binafsi zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

Mheshimiwa Spika,Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ifikapo Oktoba mwaka huu wa 2015. Matumizi bora ya sheria za kulinda amani nchini ni muhimu sana wakati huu. Lakini mambo muhimu na ya msingi yakipuuzwa amani inaweza kutoweka licha ya sheria ngumu za udhibiti ikiwemo ya udhibiti wa silaha kuwepo: Masuala hayo ni kama yafuatayo:

i. Kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza kwamba, mzaha katika jambo hili hautavumilika. Aidha, ijulikane kwamba wananchi watakapotambua kuwa hawawezi kuwapata viongozi wao wanaowataka kupitia sanduku la kura, basi wanaweza kutafuta haki yao kwa njia nyingine hali ambayo inaweza kuliingiza taifa katika machafuko kwani haki haiombwi ila inadaiwa.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatoa wito kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura ili waweze kuamua nani atakuwa kiongozi wao kwenye uchaguzi Mkuu unaokuja. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inamkumbusha kila mwananchi atambue kwamba “Kura yako ni Maisha yako, Nenda Kajiandikishe Sasa”

ii. Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi:

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaionya Serikali kutofanya Mzaha na jambo hili kwani linaweza kuiingiza nchi katika machafuko makubwa. Mheshimiwa Spika, Viongozi wa nchi hii wamekuwa wakifanya mizaha kuhusu maisha ya wananchi kwa mambo mengi, yakiwemo ufisadi uliokithiri. Kwa mfano wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, uliwahi kumwomba Mheshimiwa Andrew Chenge kutoa mwongozo wa kutengeneza maazimio ya Bunge kuhusu watuhumiwa wa wizi wa fedha za Escrow wakati yeye mwenyewe alikuwa ni mtuhumiwa.

Huu ni mzaha mkubwa ambao kwa tafsiri inaonyesha kwamba watawala wanawaona watanzania kuwa ni wajinga. Kambi Rasmi ya Upinzani inaonya kuwa mizaha kama hii ikiletwa kwenye suala la uwepo wa tume huru ya uchaguzi, taifa hili linaweza likasambaratika. Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inataka Tume Huru ya Uchaguzi, si kwa sababu inataka kushinda uchaguzi bali ni kwa sababu inataka kujenga na kulinda Imani ya Mpiga Kura ili kulinda amani ya nchi yetu”.

iii. Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi:

Mheshimiwa Spika, kwa vile imethibitika pasipo shaka yoyote kwamba Polisi mkatili na mkorofi dhidi ya Upinzani anapandishwa cheo, ni dhahiri kwamba kitendo hiki kimejenga msingi (precedence) wa polisi kuwaonea, kuwadhalilisha na kuwafedhehesha viongozi wa Upinzani kwa matarajio kwamba watapongezwa na kupandishwa vyeo na Serikali.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani imepigia kelele sana suala hili la matumizi mabaya ya Jeshi la Polisi ya kulinda maslahi ya kisiasa ya watawala kwa miaka yote. Viongozi, wanaharakati na wananchi wanaounga mkono mageuzi wamepita kwenye bonde la uvuli wa mauti kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, Hatukuonewa kwa sababu sisi ni wanyonge, ila ni kwa sababu tumeendelea kuwa wavumilivu. Nina mashaka kama uvumilivu huo utandelea kuwepo kama uonevu na ukandamizaji utaendelea.

Mheshimiwa Spika, Mwenyezi Mungu, pamoja na upole wake, ukarimu wake, upendo wake, rehema zake kwa watu wote lakini bado ametenga Jehanamu kwa watenda dhambi ambao amewaumba yeye mwenyewe. Tusisubiri wananchi wachoke kuvumilia, bali hekima ya Mungu ituongoze ili kuliepusha taifa letu na majanga ya uvunjifu wa amani pindi watu watakapokosa uvumilivu wa mateso.

iv. Ulinzi wa Raia na Mali zao:Mheshimiwa Spika,

Kukosekana kwa ulinzi na usalama wa raia na mali zao kunaweza kuliingiza taifa katika machafuko. Matukio ya kuuwawa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi – Albino, mauaji ya vikongwe na wanawake kutokana na imani za kishirikina yamekithiri sana katika nchi yetu licha ya kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Hali hii imefanya wananchi kukosa imani na Serikali kwa kuwa bado yanaendelea licha ya kampeni nyingi kutoka kwawanaharakati mbalimbali kupinga mauaji ya Albino. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitahadharisaha Serikali kutodharau kundi la Albino kuwa ni dogo na kutolipatia ulinzi wa kutosha.

Mheshimiwa Spika,Baada ya utangulizi huo, sasa naomba nijielekeze kwenye muswada wa Sheria uliopo mbele yetu unaohusu Usimamizi na Udhibiti wa Silaha na Risasi.

Mheshimiwa Spika,Matukio yote niliyoyataja hivi punde, ni matukio ambayo kwa kiasi kikubwa yamedhoofisha hali ya usalama hapa nchini. Hivyo, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba muswada huu umekuja wakati muafaka kwa kuwa matukio niliyoyataja hapo juu ambayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini, ni matukio ambayo utekelezaji wake unahitaji silaha. Na kwa kuwa matukio hayo ni ya kihalifu, ni dhahiri kwamba hata silaha zinazotumika, hazina uhalali.

Hivyo sheria bora itakayoweka udhibiti na usimamizi wa matumizi ya silaha hapa nchini inaweza kufanikiwa kupunguza matukio ya kihalifu ikiwa itatungwa kwa nia njema ya kulinda usalama wa raia wote na sio kwa lengo la kukandamiza kundi fulani la watu ili kukidhi matakwa ya kisisasa ya kundi la watu wachache.

MAONI NA MAPENDEKEZO YA JUMLA

Mheshimiwa Spika,Kabla sijaanza kuchambua vifungu vya muswada huu, naomba nitoe maoni ya jumla ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu utekelezaji bora wa muswada huu pindi utakapokuwa sheria kama ifuatavyo:

i. Serikali iimarishe ulinzi wa raia na viongozi sambamba na matumizi ya Sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi. Itakuwa haina maana sana kuweka sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha na risasi kama wananchi na viongozi watakuwa hawana ulinzi dhidi ya watu wanaotumia silaha kwa malengo ya kihalifu.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa ninapowasilisha maoni haya ya Kambi ya Upinzani kuhusu muswada huu, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawana ulinzi wa Serikali. Ni ajabu kwamba Mbunge ambaye kimsingi kazi zake zinamfanya awe na maadaui ambao ni wahalifu na mafisadi anakuwa hana ulinzi wowote wa serikali.

Kwa mfano maisha ya Mhe. David Kafulila aliyeibua sakata la wizi wa Escrow na kusababisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mawaziri kufukuzwa kazi yako hatarini kwa kuwa hana ulinzi wowote. Lakini wakuu wa Wilaya ambao kazi zao ni kupokea mwenge, kusoma taarifa za UKIMWI na njaa wilayani na kupokea wageni wa kitaifa wana ulinzi majumbani mwao.

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge mtakumbuka tukio la kuvamiwa na kuchomewa nyumba kwa wabunge wenzetu. Wabunge hawa wangekuwa wamepatiwa ulinzi wa polisi wenye silaha yamkini uvamizi ule ungeweza kuepukika.

Kwa mantiki hii Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kuanzia sasa kutoa ulinzi kwenye nyumba za wabunge na viongozi wengine wanaostahili huduma hiyo kama ambavyo Serikali ya Kenya imefanya kwa wabunge na viongozi wake. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali kutofanya ubaguzi wa ki-ulinzi kwa viongozi katika mihimili mitatu ya Dola (yani Serikali, Bunge na Mahakama).

ii. Wabunge wote na viongozi wote wenye hadhi ya kidiplomasia (Diplomats) wawe na sifa za moja kwa moja (direct entitlement) za kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda mara tu wanapopata hadhi hiyo ya kidiplomasia.

Utaratibu wa kuwatambulisha kwa msajili wa Silaha ili kupatiwa leseni ya umiliki wa silaha ufanywe na taasisi wanazozitumikia. Lengo hapa ni kuepusha mlolongo mrefu wa kuwajadili viongozi walioaminiwa na wananchi walio wengi (kama Rais na wabubunge) au viongozi walioaminiwa kwa kiwango cha juu na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadiliwa na ngazi za chini za uongozi katika vitongoji na mitaa kama ambavyo sheria ya sasa inavyoelekeza.

Kitendo cha kuruhusu viongozi wakuu walioaminika kujadiliwa na ngazi za chini kama wana sifa au hawana sifa za kumiliki silaha ni udhalilishaji wa itifaki (humiliation of protocol)

iii. Ulinzi na Usalama ni pamoja na kutambua hadhi na Itifaki.Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kutambua hadhi ya viongozi wakuu wa vyama vya siasa ambao si wabunge lakini vyama vyao vina uwakilishi Bungeni na kuwapa hadhi ya kidiplomasia. Mheshimiwa Spika haiingii akilini kuona kiongozi wa Kitaifa kama Profesa Ibrahim Lipumba ambaye chama chake kina wabunge wengi bungeni na kinaunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Zanzibar anakuwa hana hadhi ya ki-diplomasia.

Kwa upande mwingine inashangaza kuona kiongozi wa kitaifa kama Dkt. Wilbroad Slaa ambaye chama anachokiongoza kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni pia anakuwa hana hadhi ya kidipolmasia wakati wabunge walioko chini yake wana hadhi hiyo.Mheshimiwa Spika, viongozi wakuu wa vyama vya siasa vyenye uwakilishi mkubwa bungeni ni viongozi wa Serikali watarajiwa.

Hivyo kupuuza itifaki na ulinzi wao ni kuiweka nchi katika mtanziko na mashaka. Hili si jambo ambalo mnaweza kuliunga mkono kwa sasa lakini ni jambo muhimu kwenu kuelewa.

MAONI NA MAPENDEKEZO YA VIFUNGU MAHSUSI

Mamlaka ya Msajili wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Mamlaka na majukumu ya Msajili wa Silaha yametolewa chini ya kifungu cha 8(2) cha muswada huu wa sheria ya usimamizi na udhibiti wa silaha. Lakini kifungu hicho, hakijatoa mwongozo au mipaka ya utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa Silaha. Matokeo yake ni kwamba katika maeneo mbalimbali ya sheria hii, Msajili amepewa mwanya mkubwa wa kuamua anavyotaka (discretion).

Kwa mfano kifungu cha 17 (1) na (2) kinampa Msajili wa Silaha mamlaka ya kutoa kibali cha kumiliki silaha kwa mtu yeyote kwa kipindi ambacho ataamua yeye mwenyewe na kuweka masharti ya kibali hicho yeye mwenyewe. Aidha, Msajili anaweza katika muda wowote kufuta kibali cha umiliki wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inamtazamo kwamba, ni bora zaidi masharti ya utoaji kibali cha muda, masharti ya muda au kipindi ambacho kibali hicho kitakoma na masharti ya kufuta kibali yakawekwa na sheria na sio kutegemea utashi wa Msajili wa Silaha. Kwa kufanya hivyo, mianya ya rushwa au upendeleo au uonevu wa aina yoyote katika utekelezaji wa majukumu ya Msajili wa silaha inaweza kuzibwa na kuepukwa.

Watu wasio na Sifa ya Kumiliki Silaha

Mheshimiwa Spika,Katika kifungu cha 26(1) cha muswada huu ipo orodha ya mambo au tabia zinazoweza kumkosesha mtu sifa ya kumiliki silaha. Miongoni mwa tabia hizo ni pamoja na Ukorofi. Kwa kuwa tafsiri ya neno ukorofi ni subjective , na kwa kuwa kila mtu anaweza kutafsiri ukorofi kwa namna yake, hivyo msajili wa Silaha anaweza kuwa na tafsiri yake ya ukorofi kutokana na hisia zake na kumnyima mtu leseni ya kumiliki silaha kwa kisingizio kwamba mtu huyo ni mkorofi.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inashauri kwamba neno ukorofi litafsiriwe na sheria hii ili kuondoa mkanganyiko wa tafsiri pindi sheria hii itakapoanza kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Kifungu 26(2) cha muswada huu kinaeleza kwamba endapo msajili wa silaha ataridhika kwamba kuna sababu za msingi za kuamini kwamba mtu hana sifa ya kumiliki silaha, atatoa notisi ya maandishi akimtaka mtu huyo kufika mbele yake katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi hiyo ili kuonyesha ni kwa sababu gani asitangazwe kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, ikiwa mtu aliyepewa notisi hiyo atashindwa kuhudhuria katika muda na sehemu iliyotajwa katika notisi, Msajili wa silaha atamtangaza mtu huyo kuwa hana sifa ya kumiliki silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaona kwamba kifungi hiki kina mapungufu. Mapungufu hayo ni pamoja na muda wa kufika mbele ya msajili kutowekwa na sheria na badala yake kuachwa katika utashi (discretion) ya msajili wa silaha; na sharti la kufika mbele ya msajili wa silaha mwenyewe kujieleza kama mtu ana sifa ya kumiliki silaha iwapo kuna mashaka juu yake.

Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kwamba muda wa kufika mbele ya msajili uwekwe na sheria ili kuziba mwanya wa uonevu unaoweza kutumika kwa kuweka muda mfupi ili mtuhumiwa ashindwe kufika katika muda huo na kutangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha. Aidha, sharti la kufika mbele ya Msajili mwenyewe liondolewe na badala yake sheria iweke wasajili wasaidizi katika mikoa ili kupunguza adha na ghrama za kusafiri kumfuata msajili wa Silaha mmoja ambaye kwa vyovyote vile ofisi yake itakuwa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(3) kinasema kwamba cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kilichotolewa kwa mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha vitapoteza uhalali wake kuanzia tarehe ya kutangazwa huko. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inahoji, ni kwa nini Serikali itoe cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na kibali kwa mtu ambaye hana sifa?

Nasema hivi kwa sababu ikiwa Serikali itakuwa makini tangu mwanzo mtu anapoomba leseni au kibali cha kumiliki silaha basi uwezekano mtu huyo aliyekidhi vigezo tangu mwanzo vya kumiliki silaha kupoteza sifa na kutangazwa kuwa hana sifa utakuwa ni mdogo sana vinginevyo awe amekuwa kichaa ghafla.

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 26(4) kinasema kwa pia kwamba mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa ya kumiliki silaha, basi atasalimisha katika kituo cha Polisi haraka iwezekanavyo cheti cha kuonyesha uwezo, leseni na vibali vilivyotolewa kwake na silaha pamoja na risasi zilizo katika umiliki wake.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani inaona kwamba huu unaweza kuwa ni uporaji wa hila wa silaha za wananchi kwa kutumia sheria, kwa kuwa muswada huu haujatamka ni hatua gani zitafuata baada ya mtu aliyetangazwa kuwa hana sifa za kumiliki silaha atakaposalimisha silaha yake na nyaraka za umiliki katika kituo cha polisi. Sheria hii ikiachwa kama ilivyo inaweza kutumika kwa kulipiza visasi au kutekeleza maelekezo yenye nia mbaya.

Utoaji wa silaha na risasi kutoka katika ghala la umma au kituo cha Polisi

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 29(1) cha muswada huu kinaeleza kwamba silaha au risasi zilizohifadhiwa katika ghala la umma, kituo cha polisi au sehemu nyingine yoyote iliyoelezewa na Msajili hazitatolewa humo isipokuwa kwa kibali kilichosainiwa na msajili. Kambi Rasmi ya Upinzani inashauri kuwe na ugatuzi wa madaraka ili kibali cha kuondoa silaha katika ghala la umma au sehemu nyingine yoyote kiweze kusainiwa na Wakuu wa Polisi wa Mikoa hasa pale kunapotokea dharura mfano ujambazi, uasi, wanyama hatari nk.

Masharti kwa Wauzaji wa Silaha

Mheshimiwa Spika,Kifungu cha 33 cha muswada huu kinampa Waziri mamlaka makubwa ya kutunga kanuni zitakazoweka masharti ya utoaji wa kibali cha muuzaji wa silaha, masharti kuhusiana na eneo la biashara la muuzaji, masharti ya kutolewa upya kwa kibali cha muuzaji na masharti ya kusitishwa, kufutwa kwa muda kwa kibali cha muuzaji wa silaha.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza masharti hayo yatajwe na sheria ili kuziba mwanya wa Waziri kutumia madaraka yake vibaya kwa kuweka masharti kandamizi au ya upendeleo kwa baadhi ya makundi ya wauzaji wa silaha.

Upekuzi na Ukamataji wa Silaha

Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 54 cha muswada huu kinasema kwamba “Hakuna mashtaka au hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa dhidi ya Msajili au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa anayetekeleza majukumu yoyote chini ya sheria hii kwa lolote atakalolitenda wa nia njema”

Mheshimiwa Spika, Hakuna utendaji bora usiokuwa na mipaka. Kifungu hiki kinaweza kutumika vibaya kwa kuwa kinatoa mwanya mkubwa kwa Msajili au afisa yeyote aliyeidhinishwa kupekua au kukamata silaha kufanya jambo lolote hata kama ni ovu kwa kisingizio cha “nia njema. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kwamba sheria hii imtake msajili au afisa aliyeidhinishwa kuzingatia kanuni na taratibu za upekuzi na ukamataji, kwani kumiliki silaha kihalali sio kosa la jinai hivyo upekuzi na ukamataji uzingatie taratibu za kisheria hasa kwa wale wanaomiliki silaha kihalali.

Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya marekebisho ya baadhi ya vifungu yataletwa katika jedwali la marekebisho wakati wa Kamati ya Bunge zima.

HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, Imekuwa ni desturi kwa Serikali zilizoko madarakani kuleta miswada ya sheria kwa ajili ya kulinda maslahi yake yenyewe bila kujali maslahi mapana ya wananchi na taifa kwa jumla. Aidha, imekuwa ni desturi sheria nyingi kupitishwa haraka hara bila kupata maoni ya wadau wengi jambo ambalo husababisha sheria nyingi kupingwa kabla hata hazijaanza kutumika. Mfano halisi ni Muswada huu kutoshirikisha wadau ipasavyo. Wadau wengi walilalamika mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama kwamba hawakushirikishwa kabisa katika mchakato wa kuandaa muswada huu.

Kambi Rasmi ya Upinzani inaihoji Serikali ni kwa nini inapuuza wadau katika sheria muhimu kama hii? Je, Serikali haioni kuna athari kubwa kiulinzi na kiusalama kwa kutowashirikisha wadau wakubwa wa silaha na risasi kama vile makampuni ya ulinzi binafsi, na wafanyabiashara wakubwa wa silaha hapa nchini?

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasisitiza tena kwamba Amani na utulivu wa nchi hii hautategeme tu uwepo wa sheria ya udhibiti na usimamizi wa silaha na risasi bali uongozi unaozingatia misingi ya utawala bora, haki, usawa, ukweli na usitawi wa jamii nzima kwa jumla. Aidha, ugumu wa maisha unaosababishwa na umasikini uliokithiri kutokana na mfumuko wa bei, elimu duni, maradhi, ukosefu wa ajira, ukosefu wa maji safi na salama nk. ni viashiria vikubwa vya uvunjifu wa amani kuliko silaha na risasi ambazo Serikali inafanya bidii kubwa kutungia sheria.

Mheshimiwa Spika,Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni bado inaitaka Serikali kukumbuka na kuzingatia barabara masuwala manne muhimu iliyotahadharisha yasichezewe au kufanyiwa mzaha kwani yanaweza kuliingiza taifa katika machafuko.

Masuala hayo ni kuchezea haki ya mwananchi kujiandikisha kuwa mpiga kura, Kufanya Mzaha na uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi, Matumizi ya Kisiasa ya Jeshi la Polisi na Ulinzi wa Raia na Mali zao hususan ulinzi wa watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mheshimiwa Spika,Baada ya kusema hayo, kwaniaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, naomba kuwasilisha.


Godbless Jonathan Lema (Mb)


MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI


NA WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI


19 Machi, 2015

Bongo Movies Hili la Ukimwi Mlitazame Kwa Jicho la Tatu

$
0
0
Kwenu mastaa wa Bongo Movies, bila shaka mko poa na mnaendelea na majukumu yenu ya kila siku. Nawapongeza kwa hilo maana kazi nzuri tunaziona kila kukicha.Mkitaka kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya, kama kawaida naendeleza harakati zangu ndani ya mjengo wa Global Publishers.

Leo nimewakumbuka kupitia barua sababu wengi wenu huwa hatupati muda wa kuzungumza. Naamini kwa barua hii ujumbe utawafikia wengi kwa wakati mmoja.Dhumuni la barua hii ni kutaka kuwakumbusha kuhusu suala zima la ugonjwa wa Ukimwi (Ngoma). Hakuna asiyejua kwamba ugonjwa huu ni hatari na unaua.

Ndugu zangu, nimeguswa kuwaandikia barua hii sababu ukweli ni kwamba aina ya maisha yenu wengi wenu nayajua. Mara kwa mara tumekuwa tukisoma kuhusu nyinyi kushea mabwana na mabibi kwenye magazeti yetu.
Hiyo inaonesha ni jinsi gani mpo katika hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo. Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba, mastaa wengi wa kike wanaishi kwa kutegemea mabwana, hii ni hatari.

Kwa nini msifanye kazi zenu za kuigiza ambazo zimewapa umaarufu. Sanaa si ndiyo imewafanya muwe maarufu? Kwa nini mnaamua kuiweka kando?Hamtaki kufanya kazi, mnataka kugombea mabwana wenye nazo. Mbaya zaidi mabwana wenyewe mnaowagombea ndiyo walewale, fulani anamuona mwenzake anatembea na mtu fulani basi na yeye anamzunguka kwa tamaa ya fedha.

, Nasibu Abdul ‘Diamond’Hata huyo anayemzunguka mwenzake naye inafika wakati anapokonywa na mtu mwingine. Katika mzunguko huo mmoja akiwa muathirika basi wote mmekwenda na maji.

Baadaye msururu wa mabwana unahamia kwenda kwa mastaa wenzenu wa filamu, nao kila kukicha mnabadilishana. Leo utasikia fulani anatembea na fulani kesho amehamia kwa mwingine.Mastaa wa kiume wanatumia kigezo cha kudai watawachezesha sinema wasanii wachanga, ngono zembe inatawala, hakuna tena kuwapa hata hizo nafasi za kuigiza.

Jamani katika ulimwengu huu wa sasa si wa zama zile. Watu wanapaswa kubadilika, kuishi kisasa, kujitambua afya na kujikinga.Elimu imetolewa ya kutosha, hakuna mtu asiyejua. Kwa nini muendelee kufanya ngono zembe wakati mnatambua madhara yake? Kwa nini tunayahatarisha maisha yetu kiasi hiki? Tubadilike!

Mastaa wa kike badilikeni, fanyeni kazi msitegemee mabwana. Watanzania waliwajua kupitia sinema na michezo ambayo mlikuwa mkiigiza, komaeni kupitia kazi hizo za sanaa muweze kutengeneza kazi nzuri ambazo mtaziuza ndani na nje ya nchi.

Tumechoka kusikia habari za kukwapuliana mabwana. Tuseme inatosha kufanya ngono zembe.
Ni matumaini yangu mmenielewa, nawatakia kazi njema!

Barua Nzito By Erick Evarist, Global

Sangoma Akamatwa na Kichwa Cha Mtu

$
0
0

Wakati kamatakamata ya waganga wa kienyeji ikiendelea kupamba moto katika mikoa ya Kanda ya Ziwa, mmoja amenaswa akiwa na viungo vya binadamu, kikiwemo kichwa ambacho bado kilikuwa na nywele zake.

 

Mganga huyo, Nyamizi Makunga (70), mkazi wa Kijiji cha Igurubi wilayani Igunga, Tabora, alitiwa mbaroni juzi. Mbali na viungo hivyo, pia alikutwa na vifaa vingine, zikiwemo nyara za serikali.

 

Mwenyekiti wa Kijiji cha Igurubi, George Henry, alisema Makunga alikamatwa nyumbani kwake kutokana na msako mkali unaendelea kwa lengo la kuwabaini waganga wanaofanya ramli chonganishi.

 

Msako huo umetokana na kukithiri kwa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi, ambapo serikali katika kubaini chanzo, imekuwa ikisaka waganga wanaotuhumiwa kufanya ramli hizo.

 

Henry alisema polisi walifanikiwa kumnasa Makunga kutokana na taarifa kutoka kwa raia wema, ambapo walipofanya msako walikuta fuvu la kichwa la binadamu likiwa na nywele zake.

 

Mbali na fuvu hilo, polisi pia walikuta kipande cha mfupa wa binadamu, mkia wa nyumbu, gamba la kobe na ngozi za wanyama mbalimbali.

 

Wananchi wa Kijiji cha Igurubi, wamepongeza msako unaofanywa na polisi kuwatia mbaroni waganga ambao ndio chanzo cha kushamiri kwa mauaji ya albino.

 

Pia walisema kwa muda mrefu Makunga amekuwa kikwazo cha maendeleo kwenye eneo hilo kutokana na kufanya mambo kinyume na kwamba wananchi wamekuwa wakimwogopa.

 

Alipohojiwa, Makunga alikiri viungo hivyo ni vya binadamu na kuwa aliachiwa na baba yake ili kuendesha shughuli za uganga.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda, alithibitisha kukamatwa kwa mganga huyo akiwa na viungo vya binadamu.

Mke amfuma mumewe akijichua, Mke Azua Timbwili

$
0
0
Majira ya saa 6 usiku tukasikia purukushani kubwa nyumba ya jirani, mwana dada kachachamaa kwelikweli, tukaamua kujisogeza hapo maana unaweza shangaa kesho yake kuckia mmojawapo kachinjwa.

Kufika pale waungwana tukaanza jitihada za kushusha jazba za yule mdada na kumuomba atuelezee tatizo nini, ndipo dada wa watu akaanza kufunguka kwa hisia kali sana.

Huu sasa ni mwezi wa 3 mume wake hampi tendo la ndoa kwa kisingizio cha kwamba anaumwa UTI, akamvumilia tu lakini hajawahi hata siku moja kumuona anakunywa dawa za huo ugonjwa, pia walikuwa na utaratibu wa kuoga pamoja.

Lakini mwenzake akauvunja akawa anaoga peke yake tena anakaa muda mrefu sana bafuni, kama haitoshi akafanya na uzinduzi wa tabia nyingine mpya kabisa ya kuangalia hizi muvi za ngono hadi usiku wa manane,dada akaendelea kufunguka kuwa hilo wala halikumfanya amuhisi vibaya mwandani wake.

Za mwizi ni 40,Jana dada wa watu ameingia kulala, lakini akaja kustuka usiku mwingi anapapasa kitandani, hola mme wake hayupo.Mh! akashangaa akaamua atoke ili amuangalie labda pengine kapitiwa na usingizi pale sebuleni asije akaumwa na mbu akapata na Maralia maana anaamini eti anaumwa UTI.

Anafika sebuleni anamkuta jamaa yuko bize anautafuta mlima kitonga pembeni kuna kikopo cha mafuta yale mnayoyaita sijui k nini huko, jamani dada si ndio akalianza yowe hapo penye wengi hapaharibiki jambo, kulikuwa na wazee takribani watatu pale wakawachukua wale wana ndoa kuingia nao ndani kuanza utatuzi wa ile kesi.

Kilichonishangaza ni ule uzuri wa dada huyo, kama makalio anayo ya wastani huku pembeni zimechomoza hips za kiwango sura nzuri ya kuvutia na rangi yake ya weusi wa kung'aa, tabia njema kabisa sasa inakuwaje jamaa apige puli kwa kuvuta hisia za wazungu aliowaona kwenye mkanda.

Nuhu Mziwanda Amshukuru Shilole Kwa Kumpandisha Ndege Kwa Mara ya Kwanza..

$
0
0
"My best #Tbt kwa mara ya kwanza napanda ndege asee na Alienitoa ushamba ni baby wangu mwenyewe japo kazaliwa igunga na mimi mtoto wa dar lakini kanipandisha ndege ahahaha ...Usimdharau Mtu katika maisha #TBT" Nuhu Mziwanda

Wasira Atoa Mpya 'Staili Yangu ya Koti Imenipa Umaarufu Hadi Naweza Pata Umaarufu'

$
0
0
Wassira
Duh! Watu wanaona mbali sana asee...Mh. Stephen Wasira amesema ile picha aliyokosea kufunga kifungo, imempa umaarufu kiasi kwamba anaweza kupata Uraisi.

Ukute alifanya makusudi mjue.

Nyalandu: Urais Mwaka Huu ni Kivumbi ila Simuogopi Mtu Kati ya Wote Wanaotajwa

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu amesema uchaguzi wa Rais ajaye utakuwa na ushindani mkubwa ndani na nje ya CCM, huku akibainisha kuwa haogopi mtu kati ya wote wanaotajwa kwenye kinyang’anyiro hicho, bali anawaheshimu.

Lakini mbunge huyo wa Singida Kaskazini amesema mgombea pekee atakayemwogopa ni yule atakayekuwa anataka kulipiza kisasi dhidi ya wagombea wengine.

Waziri huyo alitoa kauli hiyo jana wakati alipofanya ziara kwenye makao makuu ya Ofisi za Mwananchi Communications inayozalisha magazeti ya The Citizen, Mwananchi na Mwanaspoti zilizoko Tabata Relini kando ya Barabara ya Mandela.

Ivo Mapunda : Mkiniiga Staili ya Kitaulo..Naingia na Blanketi Kabisa

$
0
0
KIPA wa Simba, Ivo Mapunda huwa haishiwi vituko jamani, eti kwa sababu idadi ya makipa wanaobeba mataulo Ligi Kuu Bara imekuwa ikiongezeka, amesema kama watakuwa wengi, atabadilisha staili hiyo na sasa ataingia na blanketi uwanjani.

Ivo amekuwa kivutio kwenye mechi kutokana na staili yake hiyo ya kuingia na taulo uwanjani. Ni staili ambayo ilimpa umaarufu tangu alipokuwa anaichezea Gor Mahia ya Kenya japo imekuwa ikihusishwa na imani za kishirikina.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ivo alisema: “Hii staili ya taulo naipenda, lakini kwa sasa naona wanaobeba wamekuwa wengi, kama wataendelea kuzidi nitaibadilisha.

“Na kama nitabadili, badala ya taulo, sasa nitakuwa naingia uwanjani na blanketi, nikiwa na mwonekano mwingine.”

Kutokana na taulo hilo, amekuwa akiingia kwenye migogoro na wachezaji wa timu pinzani pamoja na waamuzi.

Ugomvi wao ni pale anapokuwa anataka kulitundika kwenye nyavu za goli, jambo ambalo wenyewe wanaona siyo sahihi na kumtaka aliweke chini na wanafikiri kuwa upo uchawi ingawa mwenyewe huwa anapinga suala hilo.

Nay wa Mitego Amfumania Mchumba Wake Siwema Kitandani na Kiserengeti Boy..

$
0
0
KABAANG! Mkali wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, amedaiwa kumfumania ‘laivu’ mchumba wake Siwema akiwa kitandani na ‘serengeti boy’ wake ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, Ijumaa lina full stori.

NI MWANZA
Kwa mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mwanzo mwisho, tukio hilo lilichukua nafasi Machi 15, mwaka huu maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza ambako mrembo huyo alikuwa akiishi, baada ya Nay kupenyezewa ‘ubuyu’ kuwa mrembo huyo usiku wa Machi 14 alionekana akiponda raha ndani ya klabu moja iliyopo katika jengo la Hoteli ya Golden Crest.

“Wambeya walimpenyezea habari Nay, kesho yake asubuhi sana akatimba Mwanza kwa ndenge na kumkuta laivu Siwema akiwa na seregeti boy wake kitandani,” kilisema chanzo hicho kilichoomba hifadhi ya jina lake.

AMPOKONYA SIMU, AWAPIGA PICHA
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, Nay baada ya kuwakuta wawili hao wakiwa katika hali ya taharuki katika chumba cha nyumba hiyo ambayo alimpangishia Siwema, alimpokonya simu mpenzi wake huyo na kuwapiga picha za ushahidi wawili hao kisha akamchukua mwanaye kurudi Dar.

SIWEMA ATOKA NA KANGA MOJA
“Siwema baada ya kuona Nay amempokonya simu, alikurupuka akiwa na kanga moja kisha kumfuata ili arejeshewe simu yake, Nay aligoma na kukwea teksi akamuacha Siwema akilalama,” kilidai chanzo hicho.

NAY MSTARABU?
“Kiukweli Nay ni mstarabu sana maana hakuonyesha hasira za aina yoyote pamoja na kwamba aliwafuma laivu, alitoka taratibu, hakufanya ugomvi wowote kama watu wengine wanavyofanya pindi wanapofumania,” kilizidi kudai chanzo chetu.

NAY AKWEA PIPA, ARUDI DAR
Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya Nay kufanikiwa kumuacha Siwema na jamaa yake, alikwenda Uwanja wa Ndege wa Mwanza na kupanda ndege kurejea maskani kwake jijini Dar.
“Jamaa (Nay) hakutaka kuuweka usiku, alichokifanya ni kukwea pipa na kichanga chake hadi jijini Dar na kwenda kumkabidhi mama yake,” kilisema chanzo hicho.

Siwema.

NAY ANASEMAJE?
Mwanahabari wetu baada ya kuzinyaka habari hizo, alimvutia ‘waya’ Nay ambapo alipopatikana na kusomewa mashtaka ya kwenda kumfumania mchumba wake, alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa undani lakini akadai amemchukua mwanaye mikononi mwa Siwema kutokana na mchumba wake huyo kuzidiwa na mambo yake.

“Sitaki kuzungumzia chochote kwa sababu sitaki kuonekana mbaya, ila kiukweli nilienda Mwanza na kumchukua mwanangu na hapa ninapozungumza na wewe, mwanangu yupo chini ya uangalizi wa mama yangu mzazi,” alisema Nay.

SIWEMA KAFUATA SIMU YAKE
Wakati gazeti hili linakwenda mitamboni, chanzo kilicho karibu na wawili hao kilipenyeza ubuyu kuwa Siwema ameibuka jijini Dar kwa lengo la kufuata simu yake ikidaiwa kwamba eti ina siri zake nyingi.

SIWEMA HAPATIKANI
Jitihada za kumpata Siwema kupitia simu yake ili aweze kufunguka kwa upande wake hazikuzaa matunda kwani simu yake ilikuwa mikononi mwa Nay, jitihada zinaendelea ili na yeye afunguke ukweli wa tukio hilo.

TUJIKUMBUSHE
Nay na Siwema wamedumu kwenye uhusiano kwa takriban miaka mitatu ambapo wamefanikiwa kupata mtoto huyo mmoja. Awali, Nay aliwahi kuingia kwenye mgogoro na kigogo mmoja ambaye alikuwa akimtaka mrembo huyo lakini alifanikiwa kumuweka mikononi mwake kabla ya kumfumania na serengeti boy.

Diamond Platnumz...Ehee Mimba ya Zari Imetoka !!!

$
0
0
Mwanamuziki ambaye pia ni Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameshangazwa na madai kuwa eti mimba ya mpenzi wake Zarina Hassan ‘Zari’ imetoka na kuwataka Wabongo kuacha tabia ya uzushi.

Akizungumzia madai yaliyokuwa yamezagaa mtandaoni kuwa ile mimba yake aliyokuwa akiilea kama yai kwa Zari imechoropoka, Diamond alisema:

Hee! Eti mimba ya Zari imetoka! Wanaosema hivyo walaaniwe. Mbona Wabongo wazushi sana, itakuwaje hivyo halafu nisijue. Zari yuko fiti na mimba inaendelea vizuri, ona picha za kitumbo (anamuonesha paparazi picha za Zari kwenye simu yake).

Kuna wapuuzi wachache tu wanakaa na kujitungia mambo yao ili wajenge mada zao, niliona sana watu wakijibizana na kubishana juu ya hilo, lakini nikutoe wasiwasi kuwa hakuna taarifa kama hizo.”
GPL

Juma Nature: Nikitaka ubunge wa Temeke naupata kirahisi kabisa

$
0
0
Juma Nature anaamini kuwa akiamua kugombe ubunge wa Temeke ataupata kirahisi.

Nature ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa alishafuatwa na baadhi ya viongozi wamkita agombee nafasi hiyo.

“Walishanifuata watu, lakini kwa mwaka huu nimeona kwanza nikaushe,” amesema Nature. “Mimi mbona ubunge wa Temeke nakula, tena vizuri kabisa, bila hata matatizo. Kwa vyama mbalimbali siwezi kuvitaja, nimeacha kwanza akina Professor wachukue kwanza, lakini baadaye miaka mingapi usije ukashangaa nipo mjengoni, nimevaa suti kali,” aliongeza msanii huyo.

Nature alisema akiwa mbunge wa Temeke ataanza kushungulia miundo mbinu ya barabara pamoja na ujenzi holela ambao umekuwa ukisababisha mafuriko mara kwa mara.

Sugu: Wasanii hawakunisaidia kupata ubunge, walijipendekeza CCM

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, amesema hajaweza kufanya kitu chochote kuwasaidia wasanii kwakuwa wakati anagombea ubunge hakuna aliyekuwa nyuma yake.

Sugu amelazimika kusema hayo baada ya shabiki kutaka kujua ni kitu gani alichowafanyia wasanii tangu awe mbunge.

“Hao wanaozingua wakamuulize Kikwete studio aliyoitangazia dunia kawapa wasanii iko wapi na kamkabidhi nani,” amehoji Sugu kwenye Instagram. “Rais kashindwa kuwasaidia wanataka kumlaumu mbunge wa Mbeya mjini, wakati hata hao wasanii wenyewe kimsingi hawakutusapoti kwa namna yoyote wakati tunagombea huo ubunge, wote walikuwa wanajipendekeza kwenye kampeni za CCM.”

Sifa za Rose Mhando zaleta utata mtandaoni

$
0
0
Mwanamuziki wa Injili kutoka Tanzania Rose Muhando ameleta utata mtandaoni baada ya kutoa sifa za kuonyesha kumkubali Mwanamuziki wa Bongo Fleva H-Baba kwa kazi yake mpya Show Time,Rose Mhando alitoa sifa hizo baada

Msanii wa Bongo Fleva H Baba akiwa na Mwibaji wa nyimbo za injili Tanzania Rose Mhando.
ya kushuhudia show aliofanya H Baba na wimbo wake mpya wa Show Time.
Rose Mhando alinukuliwa akisema kuwa show aliyoiona kwa H Baba na huo wimbo wake mpya ni matata sana na kama akiendelea kutoa nyimbo kama hiyo hakika wasanii wenzake
wanatashidana sana lakini hawataweza kumfikia,lakini pia aliongeza kuwa H Baba ni msanii ambae anakuwa toka alipoanza kutoka na Mpenzi Bubu amekuwa anazidi kupanda
hata show zake ni matata sana ukilinganisha na show zingine za wasanii wa bongo fleva.
Baada ya watu kuonyesha hawajapendezwa na kitendo alichokifanya mwanamuziki huyo wa Injili kukubali nyimbo za kidunia H baba alisema kuwa Rose Mhando ni mwanamuziki
mwenzake hivyo haoni kama kuna ubaya yeye kumsifia kwani alichosifia amesifia sanaa yake na si kitu kingine hivyo hakuna tatizo lolote.

"Namkubali sana Mwanamuziki wa injili Rose Mhando kwakuongea ukweli kutoka moyoni.Naomba niulize Kwakuwa amesifiwa H.baba ndio kakosea mlitamani asifiwe nani sasa apo
ukweli utabakia Kuwa ukweli siku zote toka Mpenzi bubu,mpaka Leo nipo nijambo lakumshukuru muumba.sasa Rose ni mwanamuziki mwenzangu kunisifia nisawa tuu mbona disco
wanapiga nyimbo za Makoma kwani wale wanaimba mziki wakidunia?" Alihoji H-Baba.
"Hebu punguzeni kelele Rose Mhando amenisifia baada yakuona Show yangu wimbo nilioimba ukamvutia ni Show Time na upande wa Show pia jukwanii hilo linafahamika ila
linachengeshwa kila siku ila Mungu ananisimamia nipo mpaka leo,Mbona Alli Kiba amesifia show zangu hamjaongea kitu,hii imeingia kwenye historia ya nchi tayari.Ahsante
dada angu Rose Mhando nakukubali sanaa." Aliongeza H-Baba.

Kutokana na hili mwanamuziki wa Rap kutoka mwanza Fid Q kwa upande wake aliibuka na kusema kuwa hata yeye anaungana na mwanadada Rose Mhando kwani anamkubali sana H
Baba kwa show zake na nyimbo zake pia hali ambayo ilimfanya Fid aanze kutoa mwongozo kwa mashabiki wake ambao nao walionekana kupokea tofauti ujumbe wa Rose Mhando juu
ya kumkubali H baba na kuanza kumuhukumu kwa mambo mbalimbali na ufuatao ulikuwa ufafanuzi wa Fid Q kwa watu ambao wameweza kumjudge Rose Mhando juu ya kauli yake ya
kumkubali H baba.

"Nashukuru tumekubaliana katika suala la mwenye mamlaka ya hukumu..Joa lyimo sasa tubaki katika tafsiri ya UPENDO.. Sasa kama dada hatompenda ndugu yake anayemuona..
Atawezaje kumpenda Mungu asiyemuona? Ni ukweli tumeonywa kuhusu anasa za kidunia lakini pia tusisahau kama tunauhitaji msaada wa mwenye dhambi ili kumfukuza
shetani.Eliud Nyaulingo Lakini Kaisali ni kiumbe wa Mungu pia.. Huenda UPENDO huu alioonyeshwa ukamvutia kiasi cha yeye kurudi kundini.. Haudhani?"

Wema Sepetu na Millard Ayo wala shavu la tangazo la Mitsubishi

$
0
0
Makampuni mengi ya kimataifa yameanza kuamka na kutambua kuwa ili kufikisha ujumbe wao kwa wanunuzi, ni bora kuwatumia mastaa wa ndani.

Hivi karibuni, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo, wamepata shavu la kutangaza gari jipya la kampuni ya Mitsubishi aina ya ASX.

Kwenye tangazo la gari hilo, mastaa hao wenye ushawishi mkubwa wanaonekana wakisifia vitu mbalimbali vilivyomo kwenye gari hilo.

Zitto Kabwe 'Huu ni Mwanzo Mpya Sina Mpango wa Kuendelea Kupigania Uanachama Wangu wa CHADEMA'

$
0
0
"Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ninaomba kukutaarifu wewe na Bunge lako tukufu kwamba sina mpango wa kuendelea kupigania uanachama wangu wa CHADEMA katika viunga vya mahakama.
Kwa hiyo ninatangaza rasmi leo kwamba taratibu za kikatiba zitakapokamilika tu nitaachia uanachama wa CHADEMA, chama nilichokipenda sana kwa sababu ya kuendelea kukua kwa tofauti za kiitikadi, kimtazamo na hata kibinafsi kati yangu na viongozi katika chama changu.
Nimeona kuwa kuendelea kupigania uanachama kisheria ni kutatiza na kukwaza harakati za mabadiliko hapa nchini katika wakati ambapo mfumo wa kisiasa unatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa.
Kwa kuwa taratibu hizo sijui zitakamilika lini, natumia fursa hii kuwaaga wabunge wenzangu."

Tamko Rasmi la Zitto Kabwe Kwa Wabunge Kuhusu Kuachia Ubunge Hili Hapa

$
0
0
1) Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa fursa uliyonipa kutoa maelezo yangu binafsi katika Bunge lako Tukufu leo. Ninatoa maelezo haya kwa mujibu wa Kifungu cha 50 (1) cha Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Aprili, 2013 kinachosema kwamba,
“Mbunge yeyote anaweza, kwa idhini ya Spika, kutoa maelezo binafsi Bungeni yanayolenga kufafanua kuhusu jambo lolote linalomhusu na lililoifikia jamii”
2) Mheshimiwa Spika, Nilijiunga na Bunge lako Tukufu kwa mara ya kwanza Mwaka 2015 nikiwa na lengo kuu la kupaza sauti ya vijana kwenye masuala yanayohusu nchi yetu na kutetea maslahi ya Watanzania hususani Wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Mkoa wa Kigoma, na Watanzania kwa ujumla. Nilichaguliwa na wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Wananchi wa Kigoma Kaskazini walinichagua tena Mwaka 2010 kupitia tiketi ya CHADEMA.
3) Mheshimiwa Spika, kupitia fursa ya ubunge niliyopewa na wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa udhamini wa CHADEMA, nimejifunza mengi hapa Bungeni na nje ya Bunge hili. Nimeijua nchi yangu, nimejua siasa na nimejulikana ndani na nje ya Tanzania. Muhimu zaidi ni kwamba nimepata fursa adhimu ya kutoa mchango wangu katika kutunga sheria na sera mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Aidha, nilipata fursa ya kipekee kama Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati zako mbili ya kuisimamia, kuishauri na kuiajibisha serikali.
4) Mheshimiwa Spika, Ninawashukuru sana wanachama wa CHADEMA kwa dhamana mbalimbali walizonipa ndani ya CHADEMA. Ninawashukuru viongozi wangu na hasa Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Freeman Mbowe kwa kunilea na kuniamini kufanya naye kazi kwa kipindi chote tangu nilipokuwa mwanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, katika chama na hapa Bungeni. Kama ambavyo nimesema mara nyingi, CHADEMA imenilea na kunikuza tangu nikiwa na umri wa miaka 16 na tangu kipindi hicho nimejifunza mengi.
5) Mheshimiwa Spika, Nichukue nafasi hii kuwashukuru sana wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa mapenzi yao na imani waliyonipa na kuniwezesha kukalia KITI hiki ninachokalia ndani ya Bunge lako Tukufu. Nashukuru kwamba juzi nilipata fursa ya kipekee ya kuwashukuru kwa imani waliyonipa kuwatumikia kwa vipindi viwili mfululizo. Mola atawalipa wananchi wa Kigoma Kaskazini kwa imani kubwa walioionyesha kwangu na kuniwezesha kulitumikia Taifa langu kwa namna nilivyolitumikia.
6) Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa pamekuwa na msuguano wa kiuongozi kati yangu na viongozi wangu ndani ya CHADEMA uliosababishwa na tofauti za kimtazamo juu ya tafsiri pana ya demokrasia ndani ya chama chetu. Hatimaye tofauti hizi zilipelekea mwezi Novemba 2013 Kamati Kuu ya CHADEMA kunivua nafasi zangu zote za uongozi nilizokuwa nazo. Sikuridhika na maamuzi hayo na hivyo nikaonyesha kusudio la kukata rufaa katika Baraza Kuu la chama chetu kama taratibu za kikatiba za chama chetu zinavyotaka. Bahati mbaya ofisi ya Katibu Mkuu haikunipa fursa hiyo, na huo ndio ukawa msingi wa mimi kufungua kesi mahakamani kuweka pingamizi la Kikao cha Kamati Kuu kujadili hatima ya uanachama wangu hadi pale ofisi ya Katibu Mkuu itakaponipa fursa ya kukata rufaa katika vikao vya chama. Yaliyotokea baada ya hapo ni historia, lakini hatimaye Mahakama Kuu imetoa hukumu yake tarehe 10 Machi 2015. Katika hukumu hii, nimeshindwa kwa sababu za kiufundi kwa maelezo kwamba pingamizi letu liliwasilishwa kimakosa.
Pamoja na kwamba hatukuridhika na mwenendo wa jinsi kesi hii ilivyoamuliwa pamoja na maudhui ya hukumu yenyewe, ninaheshimu maamuzi ya mahakama na sina mpango wa kukata rufaa.
7) Mheshimiwa Spika, katika hali ya kawaida na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, ilitarajiwa kwamba baada ya maamuzi ya Mahakama Kuu, Kamati Kuu ingekaa na kunipa rasmi mashtaka yangu yanayohusu uanachama wangu, mimi kuitwa kujieleza na hatimaye Kamati Kuu kutoa uamuzi wake. Hata hivyo, mara baada ya hukumu ya Mahakama Kuu dunia nzima ilitangaziwa na Mwanasheria wetu Mkuu, kwa niaba ya chama, kwamba mimi nimeshafukuzwa na sio mwanachama tena wa CHADEMA. Baada ya hapo viongozi wangu wametoa matamko mbalimbali yote yakionyesha kwamba sitakiwi tena katika chama hiki, pamoja na kwamba hadi ninapoongea hapa leo sijawahi kukabidhiwa barua yeyote inayonitaarifu kufukuzwa kwangu katika chama.
8) Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ni wazi kwamba uanachama wangu wa kisiasa ndani ya CHADEMA umeshaondolewa. Ninaweza kuendelea kupigania uanachama wangu kisheria na kwa kweli nina sababu na misingi yote kubaki na uanachama wangu kisheria. Lakini mimi ni mwanasiasa. Sikuja hapa bungeni kwa sababu ya kushinda kesi mahakamani. Nilichaguliwa na wananchi wa Kigoma Kaskazini na ninatambua kwamba huwezi kuwa mbunge bila udhamini wa chama cha siasa. Huu ndio utaratibu wa kisheria tuliojiwekea. Kwa mujibu wa viongozi wangu katika chama ni kwamba udhamini wa chama changu umekwishaondolewa.
9) Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya hapo juu, ninaomba kukutaarifu wewe na Bunge lako tukufu kwamba sina mpango wa kuendelea kupigania uanachama wangu wa CHADEMA katika viunga vya mahakama. Kwa hiyo ninatangaza rasmi leo kwamba taratibu za kikatiba zitakapokamilika tu nitaachia uanachama wa CHADEMA, chama nilichokipenda sana kwa sababu ya kuendelea kukua kwa tofauti za kiitikadi, kimtazamo na hata kibinafsi kati yangu na viongozi katika chama changu. Nimeona kuwa kuendelea kupigania uanachama kisheria ni kutatiza na kukwaza harakati za mabadiliko hapa nchini katika wakati ambapo mfumo wa kisiasa unatambua uwepo wa vyama vingi vya siasa. Kwa kuwa taratibu hizo sijui zitakamilika lini, natumia fursa hii kuwaaga wabunge wenzangu.
10) Mheshimiwa Spika, vyama vya siasa ni jukwaa muhimu katika ujenzi wa demokrasia lakini havipaswi kamwe kuwa juu ya wananchi. Kwa hiyo ni maoni yangu kwamba wakati sasa umefika wa kukomesha udola na ufalme wa vyama vya siasa hapa nchini. Mfumo wa siasa ambao unavipa vyama vya siasa mamlaka ya kisheria ya kukanyaga mamlaka ya wananchi haupaswi kuendelea katika Karne ya 21 na katika nchi ambayo inaendeshwa kwa misingi ya demokrasia ya kuheshimu wananchi. Mimi ninaondoka bungeni sio kwa sababu wananchi wangu wa Kigoma Kaskazini walionichagua wametaka niondoke. Siondoki kwa sababu nimeshindwa kufanya kazi zangu za ubunge. Na kwa kweli siondoki kwa sababu wanachama wenzangu katika CHADEMA wametaka niondoke. Ninaondoka kwa sababu mfumo wetu wa kisheria unavipa vyama vya siasa mamlaka juu ya wananchi na wapiga kura. Ni matumaini yangu kwamba Bunge lako tukufu halitaruhusu mfumo huu unaoruhusu vyama vya siasa kupora mamlaka ya wananchi uendelee. Ni Bunge lako pekee lenye uwezo wa kukomesha mfumo ambao unatukuza Parties’ Power, badala ya People’s Power.
11) Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema awali kwamba vyama vya siasa ni jukwaa. Bahati nzuri nchi yetu inafuata mfumo wa vyama vingi vya siasa na sasa tuna vyama 22. Kwa hivyo, wananchi wanaoniunga mkono wasisikitike kwa maamuzi yangu ya leo. Bado ninayo fursa ya kuwatumikia kupitia jukwaa lingine ambalo nitaamua katika siku chache zijazo, na inshala Mungu akitujalia nitarudi tena hapa Bungeni katika Bunge la 11 kwa nguvu za wananchi.
12) Mheshimiwa Spika, kwa miaka kumi niliyotumikia hapa Bungeni, si yote niliyoyafanya yalikuwa sahihi, yapo ambayo niliyakosea kama mwanadamu katika kufanya kazi zangu, kwa namna yeyote ile naomba radhi Watanzania wote kwa yote ambayo sikuyafanya kwa usahihi. Mimi ni binadamu, kiumbe dhaifu, sijakamilika. Ni Mola peke yake aliyekamilika.
13) Mheshimiwa Spika, siwezi kuanza maisha yangu mapya kisiasa bila ya kulishukuru Bunge lako Tukufu. Kwanza, Bunge la Tisa chini ya Mzee Samwel Sitta, mzee wa kasi na viwango! Bado ninakumbuka vizuri jinsi hoja ya Buzwagi ilivyotikisa Bunge lake na hatimaye kupelekea nchi yetu kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa uendeshaji wa sekta ya madini (Sera mpya ya Madini na Sheria mpya ya Madini ) na hivyo kukuza mapato ya sekta ya madini kutoka Tshs. 32 bilioni kwa mwaka mpaka Tshs. 450 bilioni kwa mwaka.
14) Mheshimiwa Spika, ninajivunia kuwa sehemu ya Bunge la Kumi chini yako, Mama shupavu Anna Semamba Makinda. Katika Bunge hili nimekuzwa, nimejifunza, nimepambana, nimefurahi na nimelia ndani ya Bunge hili. Kwa pamoja tumepigania maslahi ya wananchi wetu kwa juhudi na maarifa na hivyo kuleta mabadiliko kadhaa. Ni katika kipindi hiki ambapo wabunge tumekuwa na sauti. Bunge la Tisa lilijijenga likawa ‘Bunge lenye Meno’ katika kupambana na ufisadi. Bunge la Kumi limejenga ‘Bunge lenye Nguvu’ katika mfumo wa Bajeti ya nchi yetu. Kupitia Bunge hili tumeweka misingi ya kujenga mfumo madhubuti wa uwajibikaji katika nchi yetu. Na katika siku za hivi karibuni Bunge la Kumi litakumbukwa kwa Hoja Maalumu ya Tegeta Escrow iliyopelekea mfumo wetu wa maadili ya Viongozi kupitia Baraza la Maadili kuanza kufanya kazi kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa katika miaka iliyopita.
15) Mheshimiwa Spika, wajumbe wa PAC ( ambao nimeishi nao kama familia ) tumekuwa nguzo kubwa ya kujenga uwajibikaji wa Serikali kwa Bunge na wananchi. Napenda kuwashukuru kwa dhati kabisa kwa kuniunga mkono na kwa kunipa ushirikiano kama Mwenyekiti wao. Changamoto na malezi mliyonipa kwa miaka yote hii yamejenga Mtanzania mmoja mwenye nia ya dhati ya kuitumikia nchi yake, muda wowote, wakati wowote na kwa namna yeyote ile bila woga wala upendeleo. Nawashukuru kwa kujitoa kwenu kwa nchi yetu na dhamira isiyo na mawaa ya kujenga Taifa imara zaidi. Pamoja na kwamba ninaondoka Bungeni leo, ninaahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa Kigoma Kaskazini na Taifa langu katika kusimamia ukweli, kutetea demokrasia ya kweli na kupigania maendeleo ya kweli kwa mwananchi wa kawaida bila ubaguzi wowote.
16) Mheshimiwa Spika, Kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA, najivunia kwa fursa mliyonipa kuwa sehemu ya Baraza hili la Taifa ambalo leo ninalihutubia kwa mara ya mwisho kama mbunge wa Kigoma Kaskazini. Inawezekana tusiweze kuelewana katika masuala ya uongozi, misingi na itikadi, lakini ninaamini tunapaswa kuelewana na kukubaliana katika dhamira kubwa ya kuijenga nchi yetu kuwa Taifa linalojitegemea na lisilo na aina yeyote ya ubaguzi. Taifa lenye uchumi shirikishi wenye kuzalisha ajira na kuondoa umasikini, ujinga na maradhi, yaani Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ni matumaini yangu kuwa tutakuwa bega kwa bega katika harakati hizi katika siku zijazo. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo. Nafasi hii ya kihistoria tuliyopewa haihitaji siasa za ubinafsi na unafsi! Uzalendo wetu utapimwa kwa uwezo wetu wa kuweka tofauti zetu binafsi pembeni kwa lengo lililo kubwa zaidi yetu.
17) Mheshimiwa Spika, Ninawashukuru tena na tena wana Kigoma na wananchi wote wa Tanzania ambao kwa ridhaa yao nimekaa katika viti hivi kwa miaka takribani kumi. Ninawahakikishia kuwa changamoto nilizokumbana nazo na ambazo zimenilazimisha leo niondoke bungeni zimechochea zaidi dhamira, nia na sababu yangu ya kuwatumikia kwa nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule. Huu ni mwanzo mpya.
Mheshimiwa Spika,
Asanteni sana na Kwa herini!

Masanja Awa Mbele ya Jaydee na Profesa Jay Kwa Utajiri Tanzania

$
0
0
Utajili wa komediani maarufu Bongo, Emmanuel Mgaya ‘Masanja Mkandamizaji’ ni kufuru! Tena unatisha na sasa anaonekana kuwa miongoni mwa wasanii wanaomiliki fedha na mali nyingi Bongo gazeti la Risasi Mchanganyiko limeripoti.

Awali, habari kuhusu utajiri wa Masanja ilitua mezani mwa gazeti hilo kama kidokezo, hapo mwandishi wao akaingia mzigoni na kuanza kuchunguza kwa kina mali anazomiliki msanii huyo na kugundua kuwa ni kati ya mastaa mabilionea Bongo.

“Masanja sio yule tena. Ana mpunga (fedha) mrefu sana. Hakuna msanii wa maigizo Bongo anayeweza kumfikia kwa sasa. Hao wengine ni mbwembwe tu, lakini pesa imelala kwa Masanja,” kilipasha chanzo chao.

Kikaongeza: “Kwanza ana ghorofa lipo Tabata, hapo ndipo anapoishi. Pia ana magari kibao ya kifahari, mashamba ya mpunga na Kampuni ya OK Security inayolinda sehemu mbalimbali zikiwemo taasisi nyeti nchini.

“Ni msanii gani mwenye kampuni kubwa kama ya Masanja? Wengi wanaishia kudai wanatayarisha filamu ambazo hata matunda yake hayaonekani.”

Uchunguzi wa gazeti hilo  ulibaini ukweli wa mali za msanii huyo na mambo mengine mengi yanayoingia kama vyanzo vya mapato yake.

Ilibainika kuwa, Masanja anamiliki magari sita, yakiwemo ya kifahari. Baadhi ya magari hayo ni Toyota Land Cruiser V8, Nissan Hardboad na Toyota Verossa. Pia, mkali huyo wa kuvunja mbavu, anamiliki nyumba tatu za maana jijini Dar es Salaam, moja ni ghorofa ipo Tabata, nyingine Kigamboni na nyingine haifahamiki eneo rasmi ilipo.

Hata hivyo, imebainika kuwa mbali na mijengo yake hiyo iliyopo jijini Dar, nyumbani kwao Mbarali, Mbeya ana mjengo wa maana.

Msanii huyo hayupo nyuma kwenye kilimo, ana mashamba kadhaa Kigamboni jijini Dar es Salaam lakini linalotia fora ni lile lililopo Mbarali lenye ukubwa wa hekari 50 ambalo analima mpunga.

Kwa utajiri huo, ipo minong’ono kuwa, nyota huyo anaweza kuwa kwenye namba za juu za wasanii wa maigizo wenye mkwanja mrefu.
Wengine wanaotajwa kwenye orodha ya waigizaji matajiri Bongo ni Husna Posh ‘Dotnata’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ na Amri Athumani ‘Mzee Majuto’.

Katika muziki wa Bongo Fleva, wasanii wanaoaminika wana utajiri mkubwa zaidi ni Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Joseph Haule ‘Profesa Jay’.
Wasanii hao wanamiliki mijengo ya maana, achilia mbali magari ya kifahari na miradi kadhaa.

Utajiri wa Masanja umeonekana kuibuka ghafla huku vyanzo vyake vya kumwingizia kipato vikijulikana ni sanaa ya uigizaji, muziki na huduma ya uchungaji.

Je, kwa uigizaji tu katika Kundi la Orijino Komedi ‘OK’ ndiko alikopata mkwanja huo na kuanzisha miradi hiyo mikubwa?

Kama ndiyo, kwa nini memba wenzake ndani ya kundi hilo hawana maendeleo makubwa kama yeye?

Kazi nyingine ya Masanja ni muziki wa Injili ambapo kwa sasa albamu yake ya Hakuna Jipya iko sokoni. Je, albamu hiyo na shoo anazofanya zinaweza kuwa chanzo cha utajiri huo?

Lakini pia Masanja ni mchungaji ambaye anahudumu katika Kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) ‘Mito ya Baraka’ lilicho chini ya Askofu Bruno Mwakiborwa. Je, mshahara anaoupata kutokana na huduma hiyo unaweza kuwa chanzo cha mapato yake?

Gazeti hilo  lilimsaka Masanja kwa simu na kumhoji juu ya mali zake ambapo kwanza alithibitisha kweli anamiliki mali hizo na nyingine ambazo hakupenda kuzitaja.

“Ni kweli nina nyumba tatu hapa mjini, kampuni ya ulinzi na mashamba ya mpunga eka 50 nyumbani Mbarali, Mbeya. Kuhusu magari pia ni kweli kabisa. Mimi ni mtumishi sitakiwi kusema uongo,” alisema Masanja.

Mwandishi: Lakini mbona utajiri wako umekuwa wa haraka sana mtumishi, vipi vyanzo vya mapato yako?

Masanja: Orijino Komedi ndiyo chanzo cha vyote... pale ndipo kwenye koki.

Mwandishi: Kuchekesha tu kaka? Au kwenye muziki wa Injili pia kunalipa?

Masanja: Injili na uchungaji ninaotumika kanisani ni huduma kaka, sitegemei mapato kutoka huko. Nipo kwa ajili ya kulisha kondoo wa Bwana.

Mwandishi: Wasanii wenzako wa Orijino Komedi wanachukuaje mafanikio yako?

Masanja Wanafurahia, wananiunga mkono maana ni sehemu ya mafanikio yao pia. Sisi tunaishi kama ndugu. Kwa hiyo kuna baadhi ya aidia ni zao, hivyo wanajivunia sana mafanikio yangu.

Hatua ya Tanzania kupunguza Safari za shirika la ndege la Kenya imeanza kuliumiza Shirika hilo kiuchumi

$
0
0
The effects of the drastic reduction of Kenya Airways (KQ) flights into the country have begun to bite, with the business community in particular questioning the timing and expected outcome of the move.

As Transport Minister Samuel Sitta told The Citizen yesterday in Dodoma that the reduction of the flights from 42 to 14 every week was a legal matter, critics argued that the government did not consider the economic consequences of the action. “We were just doing them (KQ) a favour but now TCAA (Tanzania Civil Aviation Authority) has acted in accordance with the Bilateral Air Services Agreement,” said Mr Sitta, who is the Acting Leader of Government Business in Parliament.

The Citizen established that Kenya Airways offices in Dar were not issuing any new travel tickets as all its flights were full for the next three weeks. Sources said the airline had called clients who had prior bookings to reschedule their flights.

There were fears that the high demand for travel and available seats would likely push ticket prices up to $1,000 from the current average of $700 on the Dar es Salaam-Nairobi route, which is dominated by Kenya Airways.

Tourism operators in Zanzibar yesterday expressed shock over the ban, with the Zanzibar Association of Tourism Investors (Zati) chairman, Mr Omar Shaaban, accusing TCAA of overlooking Zanzibar’s interests.

Mr Shaaban said the association was already reviewing tourist packages and products that had already been arranged based on the old flight schedules. He added: “The aviation industry does not stand alone. It involves many sectors like tourism, the hotel business, horticulture and other related activities, and this decision is affecting all these. The government should have involved us so we could take measures to mitigate the knock-down effect on our businesses.”

Former Zati Chairman Abdul Samad Said lamented that the KQ ban would spell doom for Zanzibar’s economy. “This is a decision that will add to the Union problems because our mainland colleagues did not care to organise how tourists coming to Zanzibar would be catered for now,” he said, noting that the Kenyan airline brought in more than 80 per cent of visitors to Zanzibar.

According to Mr Said, the decision was driven by business interests to protect Fastjet and settle political scores with Kenya. “In the absence of a national carrier, this smacks of a desperate and self-defeatist move.”

Mr Ali Mufuruki, Chairman and CEO of Infotech Investment Group, also questioned the timing and blamed the monopoly enjoyed by KQ in Tanzania and Uganda on the failure of the two governments to sustain their own national airlines. Mr Mufuruki added: “It is ironic that the government is taking that kind of drastic action on behalf of a foreign-owned airline (Fastjet) but refused to intervene when Air Tanzania needed it most. It is too little too late and a bit misguided too.”

Other players felt that international carriers would not automatically fly directly to Tanzania after the move because of prohibitive landing fees. “Many carriers skipped Tanzania not because we don’t have good hotels and tourist attractions but due to the high landing fees at our airports,” travel publisher Victor Mollel told The Citizen. “I consider this a wrong decision. The implications for the tourism industry will be big.”

The measure was another indication that member states of the East African Community (EAC) have deep-rooted differences despite constant pledges of co-operation. “When they meet, they shake hands and smile, but inside them they have deep-rooted animosity,” Mr Mollel said, urging the two countries to sort out the issue for the benefit of the air travel industry.

Mr Shoo Alibless Shoo, the CEO of the Arusha-based Sky Group, said the move would distort the economy. “Tanzania has no national airline. That in itself is a shame. Why then should we ban other carriers from bringing visitors to our country?” he asked.

Source: The Citizen

Dudu Baya Akwapua Simu Bar, Nusura Wananchi Wamchome Moto

$
0
0
Msanii Dudubaya Ameingia katika Skendo nyingine baada ya kushutumiwa kutaka kuiba simu ya mdau mkubwa wa Twanga pepeta ajulikanae kama Mapao ambae alikuwa amekaa naye meza moja pale Mango Garden huku Twanga Peteta wakiburudisha Tarehe 14 March..
Inasemekana Papa Mapao baada ya kutosheka na Burudani aliamka na kuondoka lakini baada ya kufika nje alishtuka kuwa ameacha simu mezani na kurudi lakini alikuta simu haipo na mtu aliyemwacha hapo ni Dudubaya ambae bado alikuwa hapa .Hali ilikuwa mbaya ukumbini kwani baadhi ya mashabiki walipendekeza Dudubaya Asachiwe lakini ghafla simu ilionekana miguuni kwa Dudubaya akiwa ameikanyagia na viatu..ilibaki kidogo jamaa wamchome Moto ..alisema mdau mmoja aliyekuwepo eneo la Tukio.....



Dansa wa Diamond Aonekana Mtaani na Nguo za Mume wa Aunty Ezekiel Ambae Yupo Jela

$
0
0
Gazeti la Kiu Limetoa Siri kuwa Dansa wa Diamond Moses Iyobo amedaiwa kuanza kurithi mali za mume wa Msanii Aunty Ezekiel, Sunday Demonte Ambaye yupo Gerezani nchini Abu Dhabi akitumikia kifungo cha Miaka Kumi .

Mali anazodaiwa kurithi Iyobo ni pamoja na nguo anazodaiwa kuonekana nazo mitaani na kwenye Show za Diamond..Chanzo cha ndani kinasema nguo hizo ni zile alizokwenda kuzichukua Aunty ezekiel nyumbani kwake nchini Dubai siku chache baada ya Demonte kusekwa Jela..

"Kuna uwezekano Iyobo hajui kama nguo hizo ni za Demonte lakini ukweli ndio huo, nguo hizo sisi tunazijua na Demonte alikuwa akizivaa sana Dubai sasa tunashangaa mtu hajafa nguo zake zimesharithishwa kwa mwanaume mwingine" Kililalamika Chanzo cha habari hii

Aunty Ezekile alipotafutwa kuzungumzia hilo Simu yake iliita bila Kupokelewa...

Je kama ni Kweli ni Sasa Anavyofanya?


Viewing all 104795 articles
Browse latest View live




Latest Images